NINANI KHALIFA ( KIONGOZI ) WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI?

MTUNZI: SHEKH ALY AALI MUHSINI

MTARJUMI: SHEKH REHANI YASINI

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

UTANGULIZI

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na sala na salamu zimwendee Nabii wetu Muhammadi na Aali zake watoharifu.

Hakika swala la ukhalifa, na ninani aliyepaswa kuwa khalifa, ni katika mambo yaliyo kithiri ndani yake majadiliano, na ikhtilafu baina ya makundi ya kiislamu, hususani baina ya Shia na Sunni.

Ikhtilafu hizo zilianza punde tu baada ya mjumbe wa Mwenyezi Mungu kufariki dunia, hivyo kutokea marumbano na mabishano baina ya maswahaba katika mgahawa (saqifa) wa bani Saaidah, kuhusu nani anaye paswa kuwa kiongozo na khalifa baada ya mtume(s.a.w.w) , ikiwa ni katiaka jaribio lao la kwanza la kumteua kiongozo.

Hali hiyo haukuishia hapo, bali iliendelea katika kipindi chote cha mtiriko wa uongo (ukhalifa) wa waislamu, kuanzia za maswahaba mpaka leo hii. Hivyo kutokea makunduzi, na vita mbali mbali, viliyo pelekea kumwagika damu za waislamu bila hatia yoyote.

Kutokana na mazingira hayo, masunni waliwakubali viongozi waliokuwa wakitawala kwa mabavu, na kutoa kiapo cha utii kwa viongozi hao, pia kuhukumu kuwa: ukhalifa wa viongozi hao ni wakisheria, hivyo haipaswi kuupinga na kusimama dhidi yake.

Ingawaje baada ya utala wa Amamu Ali Ibni Abi Twalibi(a.s) , ukhalifa ulibadilika na kuwa ufalme, unaorithiwa na watoto kutoka kwa baba zao, pasipo na mashauriono baina ya waislamu, Isipokuwa tu ili kuuhalalisha ufalme huo ulibakia na jina la uislamu.

Baada ya kudhoofika hali ya kidini na yakisiyasa ya waislamu na kuzidi kuwa mbaya, miji ya kiislamu iligawika na kuwa vinchi vidogo vidogo, vyenye kugombewa na wafalme mbali mbali, wasio na sifa za kuwa viongozi wa waislamu, kama ilivyokuwa katika utawa wa bani Umayyah na bani Abbasi.

Hali hiyo iliendelea katika mfomo huo mpaka leo hii.

Kwa minajili hiyo, yalianza mazingira mapya katika miji ya kiislamu, yanayo pingana na maamuzi ya wanazuoni wa kisunni, ambayo ni: ulazima wa kutoa kiapo cha utii kwa kiongozi mmoja wa waislamu katika kila zama, na kuto kubali mfumo wa viongozi wengi, kama tutakavyo kuja kufafanuwa huko mbeleni.

Baada ya mazingira hayo, usahihi wa ishkali ya Mashia juu ya itikadi ya Masunni kuhusu ukhalifa na Makhalifa kwa ujumla, ulibainika zaidi.

Itikadi ya Mashia kuhusu ukhalifa ni kwamba: khalifa nilazima awe maasum na awe amaeteuliwa na Mwenyezi Mungu kupitia mtume wake, lakini pia awe ni katika kizani toharifu cha Mtume. Kwa sababu kama hiyo hawakukubali ukhalifa wa watu wasiokuwa na sifa hizo, kwani ukhalifa si haki ya yeyote yule, bali ni uteuzi utokao kwa Mwenyezi Mungu.

Ingawaje mgogoro mkubwa ulikithiri juu ya itikadi ya Mashia kuhusu Imamu Mahdi, Muhamadi Ibni Hasani Alaskari(a.s) , aliye zaliwa mnamo mwaka 255 hijiriya, na kwamba bado yupo hai mpaka sasa. Kwani Ahlisunnah wana amini kuwa itikadi hiyo, ni dalili tosha ya ufahamu dhaifu, kwani haiwezekani kumsadiki kiongozi aliyezaliwa kabla ya miaka mia moja tisini na sita, na kisha kudai kuwa bado yupo hai mpaka sasa. Madai hayo yalitokana na kuamini kuwa umri wa mtu wa kawaida, hauwezi kufikia miaka yote hiyo kwa vyovyote iwavyo.

Ahlisunnah waliwashambulia Mashia kwa madai hayo, bila kutoa majibu kuhusu nani kiongozi wa waislamu katika zama hizi. Wao waliinyamazia Haki, pamoja na umuhimu wake, na wala hawakutaka kulizungumzia swala hilo, kiasi ambacho hakuna Msunni yoyote mwenye majibu sahihi juu ya swala hilo.

Ninatarajia; kutokana na Utafiti huu, niwe nimetoa ufafanuzi kuhusiana na swala hili, na kuyafichua yaliyofichika.

Ninamuomba Mwenyzi Mungu mtukufu, aifanye kazi hii iwe kwaajili ya kutaka radhi zake, na aipokee kutoka kwangu kwa mapokezi mazuri, hakika yeye ni msikivu na mwenye kujibu maombi, na Sala na Salamu zimwendee Muhammadi na Aali zake watoharifu.

Tarehe 20 mwezi ramadhani 1424 hijiriya.

ALY AALI MUHSINI.