NINANI KHALIFA ( KIONGOZI ) WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI?
BAADHI YA SIFA ZA KIONGOZI WA WAISLAMU
Nilazima kwa anaye taka kuwa kiongozi wa waislamu, awe na vigezo vitakavyo muwezezsha kuwa kiongozi wa wengine, hivyo wanazuoni wa kisuni wametaja baadhi ya vigezo hivyo, ambavyo anatakiwa kuwa navyo kiongizi wa waislamu, vigezo hivyo ni vifuatavyo:
1- Awe mkurayshi
Hautasihi uongozi wa yeyote asiye kuwa mkurayshi, hiyo imetokana na maneno ya Mtume(s.a.w.w) kuwa:
(الأئمة من قريش)
Viongozi (Maimamu) watatoka katika ukoo wa Kuraishi [20] .
Alisema Annawawi: jamuhuri ya wanazuoni waliifanyia kazi hadithi hii, hivyo waka weka sharti kwamba; kiongozi ni lazima awe katika makuraishi.
Pia akasema: hadithi hii ndio iliyo kuwa hoja ya mashekhe wa wili (Abubakari na Omari) siku ya saqifah, na ikakubalika kwa Maswahaba wote bila kipingamizi[21] .
Na alisema Ibuni Hajari, akinukuu kutoka kwa Ayyadhi kuwa: wanazuoni wote, wamekubaliana kuwa; kiongozi ni katika makuraishi, wala haikuwahi nukuliwa pingamizi, kutoka kwa yeyote katika hilo, pia akasema: kauli ya Makhawariji na walio waafiki katika muutazila, hazita zinagatiwa, kutokana na kwamba zina pinzana na jamuhuri ya waislamu[22] .
Na akasema Almaawardi kuwa: kiongozi kuwa katika ukoo wa makuraishi, imetokana na hadithi ya Mtume, pia ijmau, hivyo hauta zingatiwa ukeukaji wa Bin Amru, palea alipo ruhusu uongozi kwa watu wote, kwa sababu hoja ya Abubakari siku ya saqifa kwa Answari, ya kukataa uteuzi wao kwa Saadi Bin Ubadah, ilisimamia maneno ya Mtume(s.a.w.w) yasemayo: Viongozi(Maimamu) ni katika kuraishi, hivyo hayata zingatiwa maneno ya yeyote atakaye pinga[23] .
Ibun Hazmi pia alisema: hauta sihi uongozi wa asiye toka katika kizazi cha kuraishi, hivyo utakuwa batili uongozi wa yeyote asiye kuwa katika ukoo huo, wala hata kuwa na amri yoyote, bali atakuwa fasiki na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu mtukufu, yeye na kila mwenye kumsaidia, au kuridhia uongozi wake, kwa sababu watakuwa wamevuka mipaka ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake(s.a.w.w) [24] .
Abdulqaahir Albaghdadi, katika (Alfarqu baina Alfiraqu)[25] . Na Ibun Hazmu, katika: (Alfaswilu Filmilali wal Ahawaa wa Annihali). Na Taftazani, katika: (Sharhilmaqaswidi)[26] . Na Alghazali, katika: (Qawaidul-aqaidi)[27] . Na Alqurtubi, katika: Tafsiri yake[28] . Na wengineo, walilitaja sharti hili, la kuwa kiongozi ni katika makuraish.
2- Awe mwenye elimu na mujitahidi
Alisema Al-ijey: Jamuhuri ya wanazuoni ina amini kuwa; kiongozi inabidi awe na uwezo wa kuifahamu itikadi na sheria, ili aweze kuisimamia dini ipaswavyo[29] .
Na akasema Abdulqahir Albaghdadi: wanazuoni wa kisuni, wali wajibisha kuwa kiwango cha Elimu, anacho paswa kuwa nacho kiongozi, kiwe kimefikia ijitihadi katika sheria[30] .
Akasema pia Alqurtubi: kiongozi anatakiwa awe ni katika wasomi waliofikia kiwango cha kuwa kadhi, mwenye ijitihadi, asiye wahitajie wengine katika kutoa hukumu (fat’wa) ya matukio, na hili lime kubaliwa na wote[31] .
Sharti hili la kuwa kiongozi wa waislamu, ni lazima awe mujitahidi, pia lime tajwa na: Almaawardi, katika: (Al-ahkamu Asultwaniyah)[32] . Na Tafatazani, katika: (Sharhi Almaqaswidi)[33] . Na Baaqilani, katika: (Altamuhidi)[34] . Na wengineo.
3- Awe muadilifu, asiwe fasiki
Alisema Albaghdadi, baada ya kuwa ametaja sharti la uadilifu: wanazuoni wa kisuni wali wajibisha kwa kiongizi, awe muadifu, katika dini yake, mwenye kujihifadhi katika mali na hali yake, asiwe mwenye kufanya madhambi makubwa, wala kuendelea kufanya madhambi madogo[35] .
Na akasema Al-ijey: Nilazima kiongozi awe muadilifu, asiye fanya maovu. Akaongeza kuwa: sharti hili lime kubaliwa na wote[36] .
Qurtubi pia akasema: Kiongozi anatakiwa awe muadilifu, kwa sababu hakuna tofauti baina ya wanazuoni kuwa; hairuhusiwi kumpa uongozi fasiki.
Kisha Jmamuhuri ya wanazuoni, ikasema: hakika utabatilika uongozi wa kiongozi yeyote atakae fanya maovu dhahiri, au kujulikana, kwa sababu imethibiti kuwa; uongozi uliwekwa kwa ajili ya kusimia sheria, kurejesha haki za wanyonge, kuhifadhi mali za mayatima, na mengineyo yaliyo tajwa huko nyuma, hivyo kama tutamruhusi fasiki kuwa kiongozi, itakuwa ni kinyume na malengo ya uongozi huo[37] .
Sharti hili la kuwa kiongozi wa waislamu, ni lazima awe muadilifu, pia lime tajwa na: Almaawardi, katika: (Al-ahkamu Asultwaniyah)[38] . Na Alghazali katika: (Qawaidul-aqaidi)[39] . Na Tafatazani, katika: (Sharhi Almaqaswidi)[40] . Na wengineo.
Na sifa zingine mfano wa hizo, ambazo hawakuwa nazo viongozi wao wengi, kwani uongozi baada ya kubadilika na kuwa ufalme, unaothiriwa na watoto kutoka kwa baba zao, masharti hayo hayakuzingatiwa, hivyo waislamu wakatawaliwa na mafasiki, ambao hawakuwa na maarifa ya hukumu za dini, ukiachia mbali kuwa hawakuwa na Elimu yoyote.
Yote hayo yalifanywa mbele ya wanazuoni wa kisuni, ambao wali usahihisha uongo wa viongozi hao, na wakahukumu kuwa ni uongozi wa kisheria, na kwamba ni lazima kutoa kiapo cha utii kwa uongozi huo, na kuwa hairuhusiwi kusimama dhidi yake.
Wanazuoni wa kisuni, wameeleza kuwa; hairuhusiwi kutoa kiapo cha utii kwa viongozi wa wili, wakati mmoja, hata kama watakuwa katika maeneo tofauti.
Alisema Annawawi: Wame kubaliana wanazuoni kuwa; hairuhusiwi kutoa kiapo cha utii, kwa viongozi wa wili katika wakati mmoja, hata kama miji ya kiislamu itakuwa mingi.
Kisha akanukuu maneno ya Imamu wa Makkah na Madini kuwa: kuna uwezekano ikaruhusiwa, kama miji ya kiislamu ita panuka. Akasema kujibu kauli hiyo kuwa; ni kauli fasidi, inayo pingana na kauli ya wanazuoni, pia dhahiri ya hadithi[41] .
Akasema pia Ibun Kathiri, katika tafsiri yake: Ama kuwateua viongozi wa wili, au zadi ya wawili katika wakati mmoja, hairuhusiwi, hiyo inatokana na maneno ya Mtume(s.a.w.w) pale aliposema: yeyote atakaye kujieni na ilihali mna uongozi mmoja, na akataka kukufarakisheni, basi muuweni. Na hii ndio kauli ya jamuhuri. Na imenukuliwa na wengi, ijmau juu ya hilo, miongoni mwao ni Imamu wa Makka na Madina[42] .
Na akasema Ibun Hazmi, katika kitabu chake; Almuhalaa: Hairuhusiwi katika Dunia kuwa na kiongozi zaidi ya mmoja, bali uongozi utakuwa ni wa mwanzo kupewa baiyah[43] .
Akasema pia Qirtubi: Hairuhusiwi kuteuliwa viongizi wawili au watatu wakati mmoja. Alisema Imamu Abulmaali: wamekataa wanazuoni wetu kuteuliwa viongozi wawili wakati mmoja. Kisha akasema: kama itatokea kuteuliwa viongozi wawili wakati mmoja, basi itakuwa ni sawa na mawali wawili kumuozea binti mmoja kwa wanamume wawili, bila ya mmoja wao kujua kuwa kasha ozeshwa na mwengine[44] .
Kuna hadithi nyingi zilizo zungumzia hali itakayo wakumba waislamu, ya kukithiri wanao dai uimamu, na watakao pora ukhalifa, na kwamba watakuwa wengi, katika wakati mmoja.
Amepokea Bokhari na Muslimu, katika sahihi zao, na wengineo, kutoka kwa Abu Huraira kuwa; alipokea kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) kuwa alisema:
(كانت بنو إسرائيل تسوسهم الأنبياء، كلما هلك نبي خلفه نبي، وإنّه لانبي بعدي، وسيكون خلفاء فيكثرون. قالوا: فما تأمرنا؟ قال: فوا ببيعة الأوّل فالأوّل، أعطوهم حقّهم فإنّ الله سائلهم عمّا استرعاهم.)
Wana wa israeli walikuwa wakiongozwa na Manabii, ilikuwa kila anapo kufa Nabii, hufuatia Nabii mwengine, lakini baada yangu hakuta kuwa na Nabii, hivyo wata kithiri Makhalifa. Wakasema maswahaba: katika mazingira hayo, ni upi wadhifa wetu? Akawajibu; Toeni baiyah kwa mmoja baada ya mwengine, wapeni haki zao, kwani Mwenyezi Mungu atawasaili juu ya walicho simamia[45] .
Na hadithi zingine zikaeleza wadhifa wa wajibu juu ya hali hiyo, kwa kusema kuwa: wajibu wa waislamu juu ya hali hiyo, ni kushikamana na na khalifa wa kwanza, na kuuliwa khalifa mwengine, kama hata kubali.
Amepokea Muslimu katika Swahihi yake, kutoka kwa Abi Saidi Alkhidri kuwa; Mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) , alisema kuwa:
(إذا بويع لخليفتين فاقتلوا الآخر منهما)
Iwapo watachaguliwa viongozi wa wili, basi muuweni mmoja wao [46] .
Alisema Annawawi, katika Sharhi ya Swahihi Muslimu: Maana ya hadithi hii ni kwamba: atakapo chaguliwa Khalifa baada ya kuchaguliwa mwengine, basi uchaguzi wa kwanza utakuwa Sahihi, na inatakiwa utiiwe, na uchaguzi wa pili utakuwa batili, na hairuhusiwi kuutii, sawa sawa awe amechaguliwa bila kujua kuwa kuna mwengine kasha chaguliwa au la, na sawa sawa iwe katika nchi moja au nchi mbili, hii ndiyo inayo kubaliwa na jamuhuri ya wanazuoni[47] .
Na akasema Qurtubi, katika tafsiri yake: watakapo chaguliwa Makhalifa wa wili, basi ukhalifa utakuwa ni wamwanzo, na mwengine atauliwa, lakini wanazuoni walikhtilafiana kuhusu kinacho kusudiwa katika kumuuwa, je inakusudiwa kumuenguwa katika uongozi, au kumuuwa? Lakini maana ya kwanza ndio yenye mashiko zaidi; Alisema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) : Watakapo chaguliwa viongozi wa wili, basi auliwe mmoja wao. Hadithi hii imepokelewa na Muslimu kutoka kwa: Abu Saidi Alkhidri.
Hiyo ndio dalili kubwa inayo kataza kuwepo viongozi wa wili, kwa sababu kuwepo viongozi wa wili kutazidisha unafiki, mifarakano, fitina na kutoweka Nema[48] .
Na akasema Sharbini: Wala hairuhusiwi kuteliwa viongozi wa wili, au zadi, hata kama itakuwa katika mataifa tofauti yaliyopo mbali mbali, kutokana na kwamba swala hilo lina sababisha kutofautiana rai, na kufarikiana, hivyo kama watateuliwa viongozi wa wili kwa wakati mmoja, uongozi huo uta batilika, na kama mmoja wao ata tangulia, basi yeye ndiye atakuwa kiongozi, kama ilivyo katika ndoa, na wapili ata adhibiwa, yeye na walio muunga mkono, kwa sababu wame fanya haramu.
Inasemekana kuwa: imepokewa katika Muslimu: watakapo chaguliwa makhalifa wa wili, basi muuweni mmoja wao, hivyo inakuwaje aadhibiwe tu? Jibu lake ni kwamba, maana ya Hadithi hiyo ni kwamba: Msimtii, hivyo basi kuwa sawa na aliye uliwa[49] .
Tunapo angalia uhalisia wa Ahlu sunnah, katika zama hizi, na kabla yake, tunawakuta kuwa walizikhalifu Hadithi zilizo sahihi kwao, ambazo tumezinukuu baadhi yake hapo kabla, lakini pia wakayaacha maneno ya wanazuoni wao, kama tulivyo nukuu maneno yao.
Hakika wao hawa kumteua kiongozi mmoja, pamoja na kuwa ni wajibu kwao kufanya hivo, hivyo waka ridhia kutawaliwa na wafalme tofauti tofauti ambao si makhalifa, bali ni wafalme, maraisi na maamiri.
Kama Ahlu sunnah wanaamini kuwa wafalme hao na wengineo, si viongozi wa kisheria, basi ni wajibu kwao kuwaenguwa madarakani, na kumteua kiongozi mmoja wa waislamu, kinyume na hivyo, watakuwa wanafanya takiya ambayo wao hawaiamini.
Na kama watakuwa wana amini kuwa wao ni viongozi wa kisheria, basi watakuwa wamekhalifu makubaliano ya maswahaba na wanazuoni wao, ambao walisema kuwa: hairuhusuwi kuteua viongozi wa wili wakati mmoja. Na hawa kuzifanyia kazi hadithi sahihi zinazo eleza ulaziama wa kumpa baiyah kiongozi mmoja, na kumuua kiongozi mwengine.
Ukiongezea kuwa hawakuzingatia sharti la kwamba; kiongzi anatakiwa awe mkuraishi, na kwamba natakiwa awe muadilifu na mwenye Elimu.
Hivyo Uongozi ukawa ni wakila mwenye kuwashinda wengine kwa nguvu.
Mjumuisha wa hayo ni kwamba: Ahlu sunnah wote, wametumbukia katika madhambi, sawa sawa wawe wametoa baiyah ya utii kwa wafalme hao au la, hiyo ni kwa sababu hawakumteua awe ni kiongozi wa waislamu wote, kwa minajili hiyo, wanakuwa wameacha wajibu na wadhifa wao wa kisheria.
Wanaweza kusema kuwa: kila kikundi cha Ahlu sunnah, katika kila taifa, kilimteua kiongozi wake wa kisheria, hivyo kutekeleza wadhifa wao wa kisheria walio faradhishiwa na Mwenyezi Mungu, wa kumbayei kiongozi wao wa zama hizi.
1- Hatakama tutakubaliana na hilo, ukweli ni kwamba; kila kikundi cha Ahlu sunnah, kitakuwa kimemteua kiongozi wake tu, na wala hakitakuwa kimewateua vingozi wa mataifa mengine.
Na hapa twaweza kusema kuwa: uteuzi huo, ima utakuwa sahihi, hivyo basi kulazimika wengine kuwafuta katika hilo, kiasi kwamba ikiwa wataacha kufanya hivio, watakuwa wameacha wajibu. Au uteuzi huo usiwe sahihi, hivyo kuto kuwa na thamani (mazingatio) yoyote.
2- Uteuzi wao kwa viongozi wao unapingana na uteuzi wa wengine katika miji mingine ya kiislamu, na hairuhusiwi kuwateua viongozi wa wili katika wakati mmoja, hivyo uchaguzi wowote utakao fanyika utakuwa batili, kwa minajili hiyo, ishkali itabakia kwa Ahlusunnah walio wengi.
3- Watu hao waliotoa baiya, walitoa baiyah hiyo kwa kiongozi wao ili awe kiongozi wa taifa lao, na si awe kiongozi wa waislamu wote, kwasababu hiyo, ndio mana hatujawahi sikia kuwa kunakiongozi yeyote katika zama hizi, aliye dai uongozi kwa waislamu wote, na uongozi unaokuwa wa wajibu, ni huu wapili na sio ule wa mwanzo.
4- Ukhalifa wa haki, kwa mujibu wa Ahlusunnah, hauwi isipokuwa kwa Amri ya Mwenyezi Mungu, au ya mjumbe wake, au kwa kuteuliwa na kiongozi wa kabla yake, au kwa mashauriano (shura) baina waislamu wote, au kwa kufanya mapinduzi katika miji mingine ya kiislamu. Na tunapowaangalia viongozi wa sasa, hakuna yeyote aliyeteuliwa kwa kutuliwa kwa kutumia njia hizo.
Lakini pia kwa mujibu wao, uongozi unaweza kuwa, kwa kuteuliwa na wanazuoni, hivyo basi kama waliotoa baiyah, watakuwa ni katika wanazuoni, basi uteuzi wao utakuwa sahihi, na kama haitakuwa hivyo, basi uteuzi wao hauta kuwa sahihi.
Na hakuna kikundi cha kisunni katika zama hizi, chenye sifa hizo, kwa minajili hiyo, uteuzi wa watu hao hautakuwa sahihi, na wala uteuzi huo hautawalazimu wengine, bali uteuzi huo utakuwa chini ya maneno ya Omari Ibunl-khatwabi ya kuwa:
(فمن بايع رجلاً على غيرمشورة من المسلمين فلايتابع هو ولا الّذي بايعه تعِزَّة() [50] ) أن يقتلا)
Atakaye mpa baiyah mtu, bila ya mashauriano (shura) baina ya waislamu, basi hatofuatwa yeye na aliyemachagua, kwa kuhofia kuuliwa[51] .
Pia kwa mujibu wao, uteuzi hauwi sahihi isipukuwa kiongozi anapokuwa ni katika ukoo wa Quraishi, muadilifu na mwenye elimu, kama ilivyo tajwa huko nyuma, lakini viongozi wao wote hana sifa hizo, hivyo uteuzi wao utakuwaje lazima kwa waislamu wote?!.
Inawezekana wakasema kuwa: Hakika kila mmoja katika Ahlusunnah, anamfuata kiongozi (Imamu) katika viongozi wa waislamu, na kama ilivyo wazi kuwa Ahlusunnah wana maimamu wanne; miongoni mwao kuna wanaomfuata Abuhanifa Annuumani, na kuna wengine wanaomfuata Maliki Ibun Anasi, na wengine humfuata Ahmadi bin Hambali, kama ambavyo kuna wengine kati yao humfuata Muhammadi Ibun Idrisa Alshafi’i, hivyo basi kila mmoja kati yao anapo kufa, hufa akiwa na baiyah shingoni mwake ya mmoja kati ya maimamu hawa, na hivyo kuto kuwa na ishkali.
1 – Mazungumzo yetu ni kuhusu kutoa baiyah kwa kiongozi atakaye wasimamia waislamu, na kuwa na utawala wa muda kwa watu wote, hii ndio baiyah waliyoiwajibisha Ahlusunah katika ibara zao zilizo tangulia, na pia hadithi zilizo tangulia. Na wala mazungumzo yetu si kuhusu Imamu wa wanazuoni ambao watu hufuata fat’wa zao, na kuzifanyia kazi, kwani hao si wajibu kuwabayi’i kwa itifaki ya wanazuoni wote, bali ni wajibu kuwauliza ilikujua hukumu ya kisheria, kama alivyo sema Mwenyezi Mungu mtukufu kuwa:
فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٧﴾
Basi waulizeni wenye elimu ikiwa nyinyi hamjui [52] .
2 – hakuna yeyote kati ya maimamu wanne, aliyewahi kutoa fat’wa juu ya uwajibu wa kuwapa baiyah wao au wanazuoni wengine, kama ambavyo haijanukuliwa kutoka kwa yeyote katika wanazuoni wa kisunni, kuwa waliwahi kupewa baiyah, si katika zama zao au katika zama za baada yao, hivyo kama kuwapa baiyah ingekuwa ni wajibu wangewaambia watu, na kuwasisitiza juu ya kutoa baiyah hiyo.
3 – tulisema huko nyuma kuwa: kutoa baiyah, maana yake ni kuahidi, na ahadi hiyo haiwezi kuthibiti isipokuwa kwa imamu aliye hai, kwa minajili hiyo haiwezekani kumpa baiyah yeyote kati ya maimamu tulio wataja hapo nyuma, kutokana na kwamba walisha kufa, hilo lipo wazi na halihitaji ufafanuzi zaidi.
Wanaweza kusema: hakika imam wa waislamu ni mmoja kati ya wanazuoni wa waislamu wasasa, nasisi wadhifa wetu ni kuwafuata katika fat’wa zao.
1 - Tuliyo yasema hapo nyuma, hapa pia yanakuja, kwani tulisema kuwa; maongezi yetu ni kuhusu kumteua kiongozi atakaye simamia mambo ya waislamu, na kuwa kiongozi wao, na si kuhusu maimamu wa wanazuioni, hakika maimamu wa wanazuoni, si wajibu kuwapa Baiyah kwa mujibu wa Ahlusunnah.
2 - Tulisema hapo mwanzo kuwa: ni sharti kwa kiongozi awe mujtahidi, na kwakuwa mlango wa ijtihadi ulifungwa, na ukabakia kwa maimamu wanne tu, hivyo basi wanazuoni wa ahlusunnah wasasa watabakia kuwa wamuasi tu, na yeyote miongoni mwao atakae dai ijitihadi, hato kubaliwa, na hivyo yeyote kati yao kukosa sifa ya kuwa kiongozi.
3 – Hata kama tutakubaliana kuwa katika wanazuoni hao wasasa kuna mwenye sifa ya kuwa kiongozi, hawezi kuwa kiongozi kwa kupata sifa tu, bali ili awe kiongozi anabidi achaguliwe, na awe na nguvu katika miji yote ya kiislamu, kama ilivyo itifaki ya Ahlisunnah, kwa sababu hiyo, walimuhesabu Muawiya kuwa ni katika maimamu kumi na mbili.
Pia wanaweza kusema kuwa: tukubaliane kuwa Ahlusunnah waliacha faradhi hii ya kumteua kiongozi wao, sawa sawa katika zama hizi, au zama zilizo fuatia zama za makhalifa, lakini hilo, hali maanishi kuwa wao walifanya maasi, hivyo kufa kifo cha kijahili, kwa sababu hilo linge walazimu kama wangeacha kwa makusudi na si kwadharura[53] .
1 - Sisi hatukubali kuwa: Ahlusunna wameshindwa kumteua kingozi wao katika zama hizi, kwa sababu baiyah, niagano la kuusilikiliza na kuutii uongozi, na hili linawezekana, kwani wanazuono wao wanaweza kutoa muongozo kwa wafuasi wao watoe baiyah kwa kiongozi mmoja wanaomuona kuwa anasifa ya kuwa kiongozi.
Ama kuhusu kuogopa hasira za wafalme wao katika miji yao, si sababu ya kuwafanya waache faradhi hii muhimu, na kuacha wadhifa adhimu kama huu, kwa sababu wao hawaamini kufanya taqiyah kwa wafame wao, kwa minajili hiyo, ilikuwa katika ubora wa Maliki bin Anasi, na Ahmadi bin Hambali, pia wengineo ni kuwa kwao wa wazi katika itikadi zao, pamoja na wafalme wa zama zao kuto kuwa radhi nao, Hivyo kuingia matatizoni.
Hayo ni mbali na kwamba; kunasehemu za kimataifa zinazo wawezesha kuongea, na kutangaza itikadi yako bila wasi wasi, hivyo hilo nijambo linalo wezekana kwa wote, au wengi wao, lakini pamoja na yote hayo kati yao aliyeongea juu ya hilo.
2 – Tukubaliane kwamba Ahlusunnah walishindwa kumteua kiongozi wao, kwa sababu ya dharura, jambo ambalo linawatoa katika madhambi, kutokana na kwamba Mwenyezi Mungu mtukufu hawakalifishi watu kwa lile wasiloliweza.
Ama kuhusu kuto kufa kifo cha kijahili, kwa sababu ya udharura huo, hatuwezi kukubalina nao, kwa sababu hata wale walioishi zama za kijahili, ambao hawakuwa wanajua chochote kuhusu dini au maisha zaidi ya chakula, na wakaashi maisha ya kudhoofishwa katika ardhi, wao twaweza kusema hawata adhibiwa kwamijubu wa maneno ya Mwenyezi Mungu mtukufu, pale aliposema:
وَمَا كُنَّا مُعَذِّبِينَ حَتَّىٰ نَبْعَثَ رَسُولًا ﴿١٥﴾
Wala Sisi hatuadhibu mpaka tumpeleke Mtume. [54]
Lakini pamoja na hayo watabakia kuwa katika wapotovu, kwa sababu kila mwenye kuiacha haki, atakuwa mpotevu, hatakama atakuwa na udhuru.
Nasi pia tunalolizungumzia ni mafano wa hilo, kwa sababu hadithi ya Muslimu ilisema kuwa; yeyote hatakuwa na baiyah shingoni mwake, basi atakufa kifo cha kijahili, hivyo hadithi hii inamshamili hata aliye na udhuru au kushindwa.
Kutokana na yaliyo tangulia, tunaweza kusema kuwa: hakika masunni, katika miji yote ya kiislamu, ima watakuwa na mtu mwenye vigezo vya kuwa kiongozi wa waislamu, hivyo kupaswa kumpa baiyah ili awe kiongozi wao.
Au hawatakuwa na mtu mwenye vigezo hivyo, na kutakiwa kutoa baiyah kwa kiongozi mmoja wa waislamu wote, mwenye vigezo vilivyo tajwa, na hairuhusiwi kuwaacha waislamu bila kuwa na kiongozi, kama ilivyothibiti katika hadithi na maneno ya wanazuoni.
Ahlusunah katika miji yote, hawakumteua kiongozi wao, hivyo wao wapo kinyume na fat’wa za wanazuoni wao, na wamezipuuza hadithi sahihi za mtume(s.a.wa.w) , hivyo kifo chao kitakuwa cha kijahili, kwa mujibu wa hadithi iliyo pokewa na Muslimu.