NINANI KHALIFA ( KIONGOZI ) WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI?

MAMBO YALIYO INJE YA ADA KATIKA KADHIA YA IMAMU MAHDI (A.F)

Mara nyingi baadhi ya wasiojua wamekuwa wakisema kuwa, itikadi ya Shia kuhusiana na Imamu Mahdi (a.f) ni itikadi isiyokubalika; kwa sababu imesimama juu ya misingi ya mambo ya kubuni na siyokuwa na uhakika, kwa sababu haingii akilini kwamba Mahdi awe ameishi miaka zaidi ya elfu moja, kama ambavyo ni jamo lisilokubalika Mahdi awe ni kiongozi na Imamu wa waislamu akiwa na umri wa miaka mitano!

Ama itikadi ya Ahli Sunna, ni itikadi ambayo imetokana na hadithi sahihi zisizopingana na akili na uhalisia wa mambo; kwani zimeepukana na yaliyo inje ya ada na yasiyokubalika. Ahli Sunna wanaamini kuwa Mahdi ni mtu atakaezaliwa katika zama za mwisho, ambae Mwenyezi Mungu atamwafikisha kuijaza ardhi usawa na uadilifu baada ya kujaa dhuluma na uovu, sio chini ya hayo wala zaidi.

Lakini ukweli ni kuwa maneno haya hayana uadifu hata kidogo; kwani Imani ya Ahli Sunna nayo juu Imamu Mahdi (a.f) imekusanya mambo yaliyo nje na ada. Mambo hayo ni mengi, miongoni mwayo ni:

IMAMU MAHDI(A.F) KUZITAWALA PANDE ZOTE ZA DUNIA

Kwa hakika atakalolifanya Imamu Mahdi (a.f) -yaani kutawala pande zote za Ardhi na kuijaza usawa na uadilifu- ni jambo lililo nje ya ada na kawaida; kwani jambo hilo halijafanywa na yeyote kati ya manabii, makhalifa na watu wema wengine, bali hakuna mtu mwenye uwezo wakulifanya hata kama atakuwa kapewa pawa na wasaidizi kiasi gani, kama matukio yanayojiri katika zama zote yanavyoshudilia hilo.

MWENYEZI MUNGU ATAMUANDALIA IMAMU MAHDI(A.F) MAZINGIRA YA USHINDI NDANI YA USIKU MMOJA

Ahmad Ibni Hanbal, Ibni Maajah, Abu Nuaim na Ibni Abu Shaibah wameandika kutoka kwa Ali(a.s) kuwa alisema: Alisema mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) :

( المهدي مِنَّا أهل البيت ، يصلحه الله في ليلة).

"Mahdi ni katika sisi Ahli Baiti, Mwenyezi Mungu atamuandaa ndani ya usiku mmoja"[184] . Yaani, Mwenyezi Mungu atamtengenezea jambo lake ndani ya usiku mmoja[185] , kwa kumwandalia sababu na mazingira ya ushindi.

Mshereheshaji wa Sunan Ibni Maajah Amedai kuwa, makusudio ya hadithi hiyo ni kumwandaa Imamu kwa ajili ya uongozi ndani ya usiku mmoja[186] . Haifichiki kuwa, sawa sawa kuandaa huko kuwe ni maana hii au ile, yote bado ni mambo ambayo yako nje ya ada.

HAKIKA MAHDI HATADHIHIRI MPAKA JUA LITAKAPO CHOMOZA NA ALAMA

Ameandika Abdurazaki katika kitabu cha 'Almuswannafu' kwa mapokezi sahihi kutoka kwa Ali Ibni Abdallah Ibni Abbaasi, alisema:

(لا يخرج المهدي حتى تطلع مع الشمس آية).

"Hatadhihiri Mahdi mpaka jua lichomoze na alama"[187] . Abdurazaki kaipokea kutoka kwa Muammar kutoka kwa Inbi Twawuusi kutoka kwa Ali Ibni Abdallah Ibni Abbaasi, na upokezi huu ni sahihi, na wapokezi wa hadithi hiyo ni waaminifu kwao.

Vilevile, Daaru Qutni ameandika katika Sunan yake kutoka kwa Jaabir kutoka kwa Muhammad Ibni Ali, alisema:

(إن لمهديِّنا آيتين لم تكونا منذ خلق السماوات والأرض، ينكسف القمر لأول ليلة من رمضان، وتنكسف الشمس في النصف منه، ولم تكونا منذ خلق الله السماوات والأرض).

"Kwa hakika Mahdi wetu ana alama mbili abazo hazijawahi kutokea tangu Mbingu na Ardhi vinaumbwa. Mwezi utapatwa usiku wa Ramadhani mosi, na Jua litapatwa katikati yake, na mambo haya hayajatokea tangu kuumbwa mbingu na Ardhi”[188] .

NABII ISSA(A.S) KUSHUKA ZAMA ZA ALMAHDI(A.F) NA KUSWALI AKIWA NYUMA YAKE

Ufafanuzi wa jambo hili umekwisha tangulia hapo kabla.

JESHI LITAKALOTOKA LIKIKUSUDIA KUMUUWA IMAMU ALMHDI(A.F) LITAANGAMIZIWA KATIKA ARDHI YA ALBAIDAU

Amesema Ibni Habbaan katika sahihi yake: "Katika kusimulia hadithi yenyekueleza wazi kuwa watu watakao angamizwa, hakika wao ni wenyekutoka wakimkusudia Mahdi kwa lengo la kumnyanganya utawala". Vilevile kanukuu kutoka kwa Ummu Salamah, kwamba alisema: Alisema mjume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) :

(يكون اختلاف عند موت خليفة، فيخرج رجل من قريش من أهل المدينة إلى مكة، فيأتيه ناس من أهل مكة فيُخرجونه وهو كاره، فيبايعونه بين الركن والمقام، فيبعثون إليه جيشاً من أهل الشام، فإذا كانوا بالبيداء خُسف بهم، فإذا بلغ الناس ذلك أتاه أبدال أهل الشام وعصابة أهل العراق فيبايعونه... فيقسم بين الناس فَيْأَهم، ويعمل فيهم بسُنَّة نبيِّهم (ص)، ويلقي الإسلام بجرانه إلى الأرض، يمكث سبع سنين )

"Kutakuwa na ikhtilafu wakati wa kifo cha kiongozi, basi mtu mmoja katika Makuraishi atatoka Madina kuelekea Makka, watu watamfuata kisha watamtoa akiwa simwenyekupenda, na watampa kiapo cha utii akiwa kati ya Rukuni na Maqaam. Watamtumia jeshi katika watu wa Shaam (ili kwenda kumuuwa), watakapokuwa katika ardhi ya tambarare (kati ya Makka na Madina) wataangaminzwa. Taarifa hiyo itakapowafikia watu, watamjia watu wema miongoni mwa watu wa Shaam na kundi katika watu wa Iraq, kisha watampa kiapo cha utii... Atazigawanya ngawira kwa watu, na atawatendea kwa mujibu wa Sunna ya mtume wao (s.a.w.w), atauimarisha Uislamu Ardhini, na atabakia kwa muda wa miaka saba"[189] .

Suala la kuangamizwa jeshi katika ardhi ya tambarare limetajwa katika hadithi nyingi sana walizozitaja wahifadhi wengi wa hadithi, kama vile: Muslim katika kitabu chake cha Sahihi, Alhaakem katika Mustadrak, Ahmad Ibn Hanbali katika Musnadi na wengineo[190] .

MAAJABU YALIYOTAJWA KUHUSIANA NA VITA VYAKE

Ametaja Muslim katika kitabu chake cha Sahihi kwa mapokezi yake kutoka kwa Abu Hurairah kwamba mtume(s.a.w.w) alisema:

(سمعتم بمدينة جانبٌ منها في البر وجانبٌ منها في البحر؟ قالوا: نعم يا رسول الله قال: لا تقوم الساعة حتى يغزوها سبعون ألفاً من بني إسحاق، فإذا جاؤوها نزلوا، فلم يقاتلوا بسلاح، ولم يرموا بسهم، قالوا: ( لا إله إلا الله والله أكبر ) فيسقط أحد جانبيها. قال ثور: لا أعلمه إلا قال: الذي في البحر، ثم يقولوا الثانية: (لا إله إلا الله والله أكبر) فيسقط جانبها الآخر ، ثم يقولوا الثالثة : ( لا إله إلا الله والله أكبر ) فيفرج لهم، فيدخلوها فيغنموا، فبينما هم يقتسمون المغانم إذ جاءهم الصريخ فقال: ( إن الدجال قد خرج ) فيتركون كل شيء ويرجعون)

"Je mmesikia mji ambao upande wake mmoja ni nchi kavu na mwingine ni bahari? wakasema: "Ndio, ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu". Akasema: "Hakitasimama Kiyama mpaka watakapo ufavamia mji huo watu sabini wanaotokana na kizazi cha nabii Is'haaka(a.s) . Watakapoufikia mji huo watapumzika, na hawatapigana kwa silaha wala hawatatupa mshale, bali watasema: "Laa ilaha ilallah wallahu akbaru", kisha upande wake mmoja utaanguka. Thouri Akasema: “Siujui upande huo, isipokuwa alisema: ni upande ambao upo baharini”. Kisha watasema kwa mara ya pili: "Laa ilaha ilallah wallahu akbaru" upande wake wa pili nao utaanguka, kisha watasema kwa mara ya tatu: "Laa ilaha ilallah wallahu akbaru", watapewa ushindi. Hapo wataungia mji huo na watapata ngawaira. Katika kipindi ambacho wao watakuwa wakigawana ngawira hizo, mara atawajia mtoa mnada na kusema: "Kwa hakika Dajjal ametoka", wataacha kila kitu na kurejea"[191] .

Ninasema kuwa: Kauli yake: "Kwa hakika Dajjal ametoka", ni dalili kuwa watu hawa waliofungua mji huo ni wafuasi na jeshi la Imamu Mahdi (a.f), kwani Dajjal atatoka baada ya kudhihiri kwa Imamu (a.f).

Qurtubi baada ya kuitaja hadithi hii katika kitabu chake cha ‘Akhbaarul Mahdi’ Alisema: "Huwenda ushindi wa Mahdi ukawa wa namna mbili: mara kwa kupingana na mara nyingine kwa takbira, yaani kwa kusema: " Laa ilaha ilallah wallahu akbaru"[192] .

KWAMBA MBINGU ITATEREMSHA MVUA YAKE NA ARDHI ITATOA BARAKA ZAKE

Alhaakem katika kitabu cha Mustadrak ametaja kutoka kwa Abu Saidi Alkhidri kwamba mtume alisema:

(فيبعث الله عزَّ وجل رجلاً من عترتي، فيملأ الأرض قسطاً وعدلاً كما مُلئت ظلماً وجوراً، يرضى عنه ساكن السماء وساكن الأرض، لا تدَّخر الأرض من بذرها شيئاً إلا أخرجتْه، ولا السماء من قطرها شيئاً إلا صبَّه الله عليهم مدراراً).

"Kisha Mwenyezi Mungu atamtuma mtu katika kizazi changu, ataijaza Ardhi asawa na uadilifu baaya kujazwa dhuluma na uovu, waishio mbinguni na ardhini watamridhia, Ardhi haitabakisha mbegu yoyote isipokuwa itaitoa, na mbingu haitabakisha mvua yake isipokuwa Mwenyezi Mungu ataimimina juu yao"[193] .

UMMA UTANEMEKA KWA NEEMA AMBAYO HAIJAWAHI KUTOKEA HAPO KABLA

Ibni Maajah, Alhaakem, Twabraani na wengineo wametaja katika misnadi zao kutoka kwa Abu Said Alkhidri kwamba Mtume(s.a.w.w) alisema:

(يكون في أمتي المهدي، إن قُصِرَ فَسَبْع وإلا فتِسْع، فتنعم فيه أمتي نعمة لم ينعموا مثلها قط، تؤتَى أُكُلها، ولا تدَّخر منهم شيئاً، والمال يومئذ كُدُوس، فيقوم الرجل فيقول: يا مهدي أعطني. فيقول: خذ).

"Mahdi atakuwa ni katika umma wangu, ikiwa atakukumu kwa muda mfupi basi itakuwa ni miaka saba, kama sihivyo basi ni miaka tisa. Umma wangu utanemeka kwa neema ambazo wahajapata kunemeka nazo kamwe, Ardhi itatoa mazao yake wala haitabakisha kitu, mali kipindi hicho zitakuwa rundo, hata itafikia hatua mtu kusema: "Ewe Mahdi, naomba (mali)". Imamu atamwambia: "Chukua"[194] .

CHUKI NA WIVU VITATOWEKA KATI YA WATU

Muslim na Ibni Habbaan katika sahihi zao wamepokea kutoka kwa Abu Hurairah kwamba alisema: Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) :

(والله ثم لينزلنَّ ابن مريم حكماً عادلاً، فليكسرنَّ الصليب، وليقتلنَّ الخنزير، وليضعنَّ الجزية،ولتُتركنَّ القِلاص فلا يُسعَى عليها، ولتذهبنَّ الشحناء والتباغض والتحاسد، وليَدْعُوَنَّ (وليُدعَوُنَّ) إلى المال فلا يقبله أحد)

"Ninaapa kwa jina Allah, kisha bila shaka atateremka mwana wa Mariam awe ni hakimu mwadilifu, kisha kwa yakini atauvunja masalaba, atauwa nguruwe, ataweka kodi (kwa makafiri), ndama wa ngamia wataachwa na hakuna ataeshughilika nao, chuki na wivu vitatoweka kwa watu, watu wataitwa kuchukua mali hakuna atakubali kuchukua"[195] .

MBWA MWITU ATASHIRIKIANA NA MBUZI NA KONDOO KATIKA MALISHO, NA SIMBA NA NGAMIA WATACHANGIA MALISHO, NA WATOTO WATACHEZEA NYOKA

Ameandika Haakim Nishabouri katika Mustadrak, Ibni Habbaan katika Sahihi na Ahmad katika Musnadi kutoka kwa Abu Hurairah (Allah awe radhi nae), kwamba alisema: Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) :

(إن روح الله عيسى بن مريم نازل فيكم... فيدق الصليب، ويقتل الخنزير، ويضع الجزية، ويدعو الناس إلى الإسلام، فيهلك الله في زمانه المسيح الدجال، وتقع الأمنة على أهل الأرض حتى ترعى الأسود مع الإبل والنمور مع البقر والذئاب مع الغنم، ويلعب الصبيان مع الحيَّات لا تضرُّهم )

"Hakika Ruhullah Issa mwana wa Mariam(a.s) ni atateremka kwenu... kisha atauvunja msalaba, na atauwa nguruwe, atawawekea kodi makafiri, na ataawalingania watu kwenye Uislamu, kisha Mwenyezi Mungu atamuangamiza Masihi Dajjal katika zama zake, na amani itaenea kwa watu ardhini kiasi cha simba na ngamia kulisha kwa pamoja, chui na ng'ombe, mbwa mwitu na mbuzi na kondoo nao watalisaha kwa pamoja, watoto watacheza na nyoka na hazitawadhuru..."[196] .

MASWAHABA WA MAHDI (A.F) MWENYEZI MUNGU NDIE ATAKAE WAKUSANYA NA KUZIUNGANISHA NYOYO ZAO

Ametaja Alhaakim Nishaaburi katika Mustadrak, na Thahabi akasahihisha na kuiafiki, kutoka kwa Ali(a.s) kwamba alisema:

(ذاك يخرج في آخر الزمان إذا قال الرجل: ( الله الله ) قُتل ، فيجمع الله تعالى له قوماً قزع كقزع السحاب، يؤلِّف الله بين قلوبهم، لا يستوحشون إلى أحد، ولا يفرحون بأحد، يدخل فيهم على عدة أصحاب بدر، لم يسبقهم الأولون ولا يدركهم الآخرون، وعلى عدد أصحاب طالوت الذين جاوزوا معه النهر)

"Huyo atatokea katika zama za mwisho, wakati mtu atakapokuwa akisema: "Allah Allah" anauwawa, wakati huo Mwenyezi Mungu atamkusanyia watu ambao watakaokuwa wamesambaa mfano wa mawingu ya msimu wa vuli yaliyosambaratika yanavyokusanyika, Mwenyezi Mungu ataziunganisha nyoyo zao, kiasi kuwa hawatamuogopa mtu yeyote, wala mtu kujiunga nao hakutawafanya wafurahie, ididi yao ni sawa na idadi ya watu wa Badri, hakuna aliewahi kufikia mfano wa daraja yao miongoni mwa waliotangulia, wala hakuna watakaolifikia, vilevile idadi yao ni sawa na idadi ya wafuasi wa Twalout waliovuka nae mto"[197] .

MAMBO MENGI YANAYOHUSIANA NA DAJJALI YAKO NJE YA ADA

MIONGONI MWA MAMBO YAHO: kwamba atakuwa na mito miwili, mmoja wa maji na mwingine wa moto.

Ameandika Muslim na Ibni Habbaani katika Sahih zao na wasiokuwa hao pia wameandika hadithi hii kutoka kwa Rab'ii Ibni Haraash, alisema: " Siku moja Hudhaifah na Abu Maso'ud walikusanyika, Hudhaifah akasema: Mimi ni mjuzi zaidi wa mambo atakayokuwa nayo Dajjali, kwa hakika atakuwa ana mto wa maji na mto wa moto, ule mtakao ona ni moto yatakuwa ni maji, na ule mtakao ona ni maji utakuwa ni moto, hivyo yeyote miongoni mwenu atakaekuwa kipindi hicho akataka kunywa maji, basi anjwe katika ule mto anaodhania kuwa ni moto; kwani atakuta ni maji"[198] .

MAMBO MENGINE : kwamba milima ya mikte na mito ya maji itakuwa ikitembea na Dajjali.

Kwa hakika Ahmad Ibni Hambali ameandika katika Musnadi wake, na wengine pia wameandika kwamba mjumbe Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alisema:

(أنذرتُكم المسيح، وهو ممسوح العين، قال: أحسبه قال اليسرى، يسير معه جبال الخبز وأنهار الماء).

"Ninakuhadharisheni na Masihi Dajjali, na yeye ni kipofu, kasema: nadhani alisema jicho la kushoto, milima ya mkate na mito ya maji vitatembea nae "[199] .

Jambo lingine: kwamba kati ya macho yake kuna maandishi ambao wataweza kuyasoma wasiojua kusoma na wanaojua.

Muslim ameandika katika Sahihi yake kwamba mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alisema:

(وإن الدجال ممسوح العين، عليها ظفرة غليظة، مكتوب بين عينيه: (كافر) يقرؤه كل مؤمن كاتب وغير كاتب).

"Hakika Dajjali ni kipofu, juu ya jicho lake kutakuwa ngozi[200] nzito, kati ya macho kutakuwa kumeandikwa neon: “kafiri” atakalolisoma kila muumini mwenye kujua kuandika na asiejua"[201] .

Jambo lingine: kwamba Dajjali atakapomuona nabii Issa(a.s) , atayeyuka kama inavyoyeyuka chumvi.

Hakika Muslim, Ibni Habbaan, na wengineo wameandika kutoka kwa Abu Hurairah katika hadithi kwamba alisema:

(فإذا جاؤوا ـ أي المؤمنون ـ الشام خرج، فبينما هم يُعِدُّون للقتال يُسوُّون الصفوف إذ أُقيمت الصلاة، فينزل عيسى بن مريم ( ع ) فأمَّهم، فإذا رآه عدو الله ذاب كما يذوب الملح في الماء، فلو تركه لانذاب حتى يهلك، ولكن يقتله الله بيده، فيُريهم دمه في حربته)

"(Waumini) watakapokuja Shamu atatoka, wakati wao wakijiandaa kwa ajili ya vita wanapanga mistari, mara itakimiwa Swala, hapo atateremka Issa mwana Mariam(a.s) kisha atawaswalisha, pindi adui wa Mungu atakapomuona tu, atayeyuka mfano wa chumvi iyeyukavyo katika maji, lau angalimuacha angaliyeyuka mpaka akaangamia, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamuuwa kwa mkono wa nabii Issa, kisha nabii Issa atawaonyesha damu yake ikiwa kwenye ncha ya kali"[202] .

Jambo lingine : kwamba Dajjali atawajia watu kisha atawataka waungane nae watamwamini na kuukubali wito wake, ataiamuru mbingu iteremshe mvua na mvua itanyesha, na ataiamuru Ardhi itatoa mimea... kisha atawatajia watu wengine na kuwataka waungane nae hawataukubali wito wake, Dajjaali atawaacha na kuondoka zake. Watapatwa na ukame, hawatabaki na kitu chochote wanachokimiliki miongoni mwa mali zao. Kisha atapita kwenye magofu ya zamani, atayaambia: "Toa hazina zako", hazina za eneo hilo zitamfuata mfano makundi ya nyuki yanavyomfuata malikia wao, kisha atamwita mtu kijana, atamkata kwa upanga vipande viwili. Kisha atamwita tena kijana yule (baada kurudi kuwa hai) atakuja hali yakuwa uso wake ukionyesha tabasamu na kucheka"[203] .

Jambo lingine: kwamba Dajjali ataponya ukoma na vibarango na atawafufu wafu.

Ameandika Ahmad katika kitabu chake cha Musnad, kutoka kwa Samrah Ibni Jundub kwamba mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alisema:

(إن الدجَّال خارج، وهو أعور عين الشمال، عليها ظفرة غليظة، وإنه يُبرئ الأكمه والأبرص ويحيي الموتى).

"Hakika Dajjaal atatokea, yeye ni kipofu jicho lake la kushoto, juu ya jicho hilo kuna ngozi nzito, na kwa hakika yeye anaponya magonjwa ya ukoma na vibarango na atawafufua wafu"[204] .

Jambo lingine: ni yaliyopokelewa kuhusiana na sifa za punda wa Dajjali.

Ahmad Ibni Hambal na Haakim wameandika katika vitabu vyao Musnad na Mustadrak, kutoka kwa Jaabir kutokakwa Mtume(s.a.w.w) kwamba alisema kuhusiana na sifa za punda Dajjaali:

(وله حمار يركبه، عَرْض ما بين أذنيه أربعون ذراعاً).

"Dajjali atakuwa na punda anaempanda, upana uliopo katika masikio yake ni dhiraa arobaini"[205] .

MATUKIO MENGINE YAKUSTAJABISHA KUHUSU MAUDHUI HAYA

Miongoni mwa matukio hayo: kwamba Ibni Sayyaad alichukia, kisha akavimba hata akajaa njia nzima.

Ameandika Muslim katika Sahihi yake kutoka kwa Naafi'i kuwa alisema: "Ibni Omar alikutana na Ibni Sayyaad katika baadhi ya njia za Madina, akamwambia kauli iliyomchukiza, basi Ibni Sayyaad akawa amevimba kiasi cha kujaa njia nzima. Ibni Omar akawa ameingia kwa Hafsa hali yakuwa taarifa hiyo ilishamfikia, Hafsa akamwambia Ibni Omar: Allah akurehemu, ulitaka nini kutoka kwa Ibni Sayyaad? Je haukujua kuwa mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alisema:

(إنما يخرج من غضبة يغضبها).

"Hakika yeye (Ibni Sayyaad) huwa anatoka katika hali yake ya kawaida anapo ghadhibishwa "[206] .

Niseme kuwa mimi binafsi nashindwa kuelewa kwamba wanaamini vipi kuwa mtu anaweza kuchukia kisha akavimba kiasi cha kujaa pande zote mbili za njia, kisha akarudi katika hali yake ya mwanzo?!

Jambo lingine: kwamba ndenge watambeba nabii Issa na wafuasi wake, na mambo mengine ya ajabu yanayo husiana na vyakula na vinywaji.

Ameandika Muslim na wengineo kutoka kwa Nawaasi Ibni Sam'aan katika hadithi ndefu, imekuja katika hadithi hiyo kuwa: "Na Mwenyezi Mungu atawatuma Yaajuju na Maajuju, nao watateremka kwa kasi katika kila mlima, wakwanza wao watapita juu ya bahari ya Galilaya kisha watakunywa kile kilichomo ndani yake, kisha wengine watapita nakusema: (awamu hii yatakuwa ni maji kweli). Nabii wa Mwenyezi Mungu Issa(a.s) na wafuasi wake watazingirwa vikali, hata itafikia hatua mmoja wao kuwa na kichwa cha ng'ombe ni bora kwake kuliko kuwa na Dinari mia moja siku hiyo. Kisha nabii Issa na wafuasi wake watamwomba Mwenyezi Mungu na kumkabidhi mambo yao yeye. Hapo ndipo Mwenyezi Mungu atakapo watuma wadudu wanaokuwa mapuani mwa ngamia, mbuzi na kondoo, wajulikanao kwa jina la: ( النَّغَف ), kwenye mashingo ya maaduwi, wote wataangamia kwa mpigo mfano wa kifo cha mtu mmoja. Kisha nabii Issa na wafuasi wake watafika nchi kavu. Hawatakuta katika Ardhi hiyo sehemu ya ukubwa wa shibri hata moja isipokuwa watakuta mafuta na harufu mbaya za maadui. Kisha nabii Issa(a.s) na wafuasi wake watamwomba Mwenyezi Mungu na kumkabidhi mambo yao yeye tu. Mwenyezi Mungu atawatumia ndenge mfano wa ngamia wa Khurasani, watawabeba na hatimae kuwashusha mahala atakapopataka Mwenyezi Mungu. Kisha Mwenyezi Mungu ataiteremsha mvua ambayo hakuna nyumba yoyote ya udogo wala ya manyoa itakayoweza kuizuwia. Mvua hiyo itaisafisha Ardhi na kuiacha kama kioo. Hapo ndipo Ardhi itakapo ambiwa: "Otesha mimea na matunda yako na rejesha kheri na baraka zako". Wakati huo kundi kubwa la watu litashiba kwa kula komamanga moja, na ganda lake wataweza kulifanya kuwa kivuli na nahala pakujinga na jua. Maziwa ya wanyama yataongezeka, hata kufikia kiasi maziwa ya ndama wa ngamia yatatosheleza kundi kubwa la watu, na maziwa ya ndama wa ng'ombe yatalitosheleza kabila nzima, na maziwa ya mtoto wa kondoo au mbuzi yataitosheleza familia kubwa"[207] .

Niseme kuwa bado nashindwa kuelewa kwamba Ahli Sunna, wanawezaje kivikubali visa hivi vya visivyo na uhalisia na vyakupuni ambavyo kiakili havikubaliki, na je inaingia akilini kwamba nabii moingoni manabii wakubwa (ulul-azm) akabebwa na ndege?! Je inewezekana komamanga likakuwa kiasi cha nganda lake kutumiwa na kundi kubwa la watu kama kivuli?! Na ikiwa maziwa ya ndama yanaweza kulitosheleza kundi kubwa la watu, basi ukubwa wa ndama huyo utakuwa ni kiasi gani?! Bila shaka atakapokuwa atakuwa ni sawa mlima wenye kilele kirefu!!

Jambo lingine: kwamba mawe na miti vitaongea katika vita na Mayahudi.

Wameandika Bukhari, Muslim -maneno ya hidhithi hii ni ya Muslim- na wengineo kutoka kwa Ibni Omar kutoka kwa bwana mtume(s.a.w.w) kuwa alisema:

(لتُقاتِلُنَّ اليهود فلتقتُلُنَّهم، حتى يقول الحجر: يا مسلم هذا يهودي، فتعال فاقتله)

"Bila shaka mtambana na Mayahudi, na bila shaka mtawauwa, hata jiwe litakuwa likisema: Ewe mwislamu, huyu ni yahudi njoo umuuwe"[208] .

Na kutoka kwa Abu Hurairah, kwamba mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alisema:

(لا تقوم الساعة حتى يقاتل المسلمون اليهود، فيقتلهم المسلمون، حتى يختبئ اليهودي من وراء الحجَر والشجر، فيقول الحجر أو الشجر: ( يا مسلم يا عبد الله هذا يهودي خلفي، فتعال فاقتله )، إلا الغَرْقَد فإنه من شجر اليهو).

"Kiyama hakitasimama mpaka waislamu wapigane na Mayahudi, kisha waislamu watawauwa Mayahudi, mpaka myahudi atakuwa akijificha nyuma ya jiwe na mti, kisha jiwe au mti utasema: "Ewe mwislamu, ewe mja wa Mwenyezi Mungu, huyu hapa myahudi kajificha nyuma yangu, hivyo njoo umuuwe", isipokuwa mti wa nitraria ( الغرقد ), hakika mti huo ni wa mayahudi"[209] .

Qurtubi amesema: "Mwawiji[210] unapokuwa huitwa nitraria, na katika hadithi: kwamba mti huo ni miongoni mwa miti ya mayahudi. Hivyo, atakapo teremka nabii Issa(a.s) na akawauwa mayahudi watakao kuwa na Dajjaal, hakuna yeyote miongoni mwao atakaejificha nyuma ya mti isipokuwa utatamka na kusema:" Ewe mwislamu, huyu hapa muyahudi nyuma yangu, njoo umuuwe". Isipokuwa mti wa Nitraria, kwani ni miongoni mwa miti ya mayahudi, hivyo hautatamka. Muslim kaisahihisha hadithi hii"[211] .

Jambo lingine: kuwa chakula cha watu katika zama za Dajjaal kitakuwa ni Takbiir, Tahlil na Tasbiih.

Wameandika Ahmad Ibni Hambal, Abu Ya'alaa na wengineo kutoka kwa Aisha, kwamba mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) alitaja uwezo atakaokuwa nao Dajjaal, wakasema: Ni mali gani itakuwa ni bora kipindi hicho? Akasema:

(أيُّ المال خير يومئذ؟ قال: غلام شديد يسقي أهله الماء، وأما الطعام فليس قالوا: فما طعام المؤمنين يومئذ ؟ قال: التسبيح والتكبير والتهليل. قالت عائشة: فأين العرب يومئذ ؟! قال: العرب يومئذ قليل).

"Kijana mwenye nguvu ataweza kuwapa maji watu wake, na sio chakula". Wakamuuliza: Hivyo basi, nini kitakuwa ni chakula cha waumini kipindi hicho? Akajibu kwa kusema: "Tasbiih (kusema: Sub'haanallah), Takbiir (kusema: Allahu Akbar) na Tahlil (kuesma: Laa ilaaha illa llah)". Bibi Aisha akasema: "Wakati huo warabu watakuwa wapi?". Akasema: "Warabu watakuwa wachache wakati huo"[212] .

Vilevile, Hakim Nisaaburi ameandika katika kitabu chake cha Mustarak kwa mapokezi kutoka kwa Ibni Omar kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) aliulizwa kuhusiana na chakula cha waumini katika zama za Dajjaal, akasema: "Chakula cha malaika". Wakasema: "Chakula cha malaika ni kipi?". Akawajibu kwakusema: "Chakula chao ni kufanya Tasbiih na Taqdiis (kumtakasa Mwenyezi Mungu) , hivyo yeyote ambae matamshi yake kipindi hicho yatakuwa ni Tasbiih na Taqdiis, Mwenyezi Mungu atamuondolea njaa, na hataokopa njaa"[213] .

Na jambo lingine: kwamba masiku katika zama za Dajjaal yatatofautiana na masiku mengine.

Wametaja Muslim katika Sahihi yake, Abu Daud katika Sunan yake na wengieo katika hadithi ndefu, kwamba mtume(s.a.w.w) aliulizwa kuhusu Dajjaal, akaambiwa:

(يا رسول الله وما لبثه في الأرض ؟ قال: أربعون يوماً، يوم كسنة، ويوم كشهر، ويوم كجمعة، وسائر أيامه كأيامكم. قلنا: يا رسول الله، فذلك اليوم الذي كسنة أتكفينا فيه صلاة يوم ؟ قال: لا، اقدروا له قدره).

Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu, atabakia ardhini kwa muda gani? Akasema: "Miaka arobaini, siku moja itakuwa ni sawa na mwaka, na siku nyingine itakuwa ni sawa na mwezi, na siku inayofuata itakuwa ni sawa na wiki moja, masiku yaliyosalia yakuwa kama masiku yenu". Tukasema: "Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, je siku hiyo itakayokuwa sawa na mwaka, sala ya siku moja itatutosha ndani ya siku hiyo? Akasema: Hapana, mtaikadiria kwa kiwango chake"[214] .

Vilevile Haakim amaeandika na Dhahabi akaisahihisha na kuikubali, kutoka kwa Kaahuli kutoka kwa mtume(s.a.w.w) kwamba alisema -katika hadithi ndefu ambayo ndani yake ametaja mambo yatakayo kuwa zama za Dajjaal: "... Hakika masiku ya Dajjaal yatakuwa arobaini, siku moja itakuwa sawa na mwaka mmoja, na siku nyingine itakuwa sawa na mwezi, na siku inayofuatia itakuwa ni sawa na wiki moja, masiku mengine yatakuwa sawa na masiku ya kawaida, ama siku ya mwisho itakuwa kama sarabi, mtu atakuwa akiamkia kwenye mlango wa Madina, mpaka jioni inaingia kabla hajaufikia mlango wake mwingine". Maswahaba wakamuuliza: "Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu, katika masiku hayo mafupi tutakuwa tukiswali vipi?". Akasema: "Mtakuwa mkikadiria katika masiku yaho, kisha mtaswali kama mnavyokadiria katika masiku marefu"[215] .

ANGALIZO

Haifichiki kuwa nasi hatuyakanushi mengi ya mabo haya yaliyo nje ya ada, bali ukweli ni kwamba waislamu katika baadhi ya mambo hayo wameafikiana, kama vile: Imamu Mahdi (a.f) kutawala pande zote za Dunia, kuijaza Ardhi usawa na uadilifu baada yakuwa imejaa dhuluma na uovu, kuteremka nabii Issa mwana wa Bi Mariam(a.s) na mfano wa hayo yanayojulikana na yaliyomashuhuri, isipokuwa nilichotaka kumbainshia msomaji mpendwa ni kuwa, sauala la Imamu Mahdi (a.f) limezungukwa na mambo mengi ya ghaibu na yaliyo nje ya ada na kawaida ya mwanadamu, na kwamba kuingia kwake ughaibuni kwa muda mrefu na umri wake mtukufu kuwa mrefu - hata kama ni mambo ya kawaida- ni sawa na mambo mengine yaliyothibiti kwa dalili na hoja sahihi, wala sio busara kuyapinga na kuyakanusha au kuyatumia kama kigezo cha kuhujumu na kuchafua jina la Ushia na Mashia.