25%

2

MOTO NA PEPO

3. ADHABU ZA KABURINI

Sisi sote tunatambua kuwa kutakuwa na adhabu katika makaburi kwa ajili ya kila mmoja ikiwa ni Mwislamu au asiye Mwislamu. Lakini kunatofauti katika adhabu hizo baina ya makundi hayo mawili ya watu kwani makafiri, wanafiki na wasio wasio Waislamu itakuwa zaidi kuliko Waislamu. Lakini kuna baadhi ya Waislamu ambao wao wenyewe humu duniani wanapuuzia baadhi ya mambo na hivyo katika kituo cha kwanza cha safari ya Aakhera na ambacho ndicho baada ya dunia, watakumbana na magumu na mazito.

1. SABABU ZA ADHABU ZA KABURINI

Ninapenda kuwaleteeni Hadith ya kwanza inayomnakili Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) [3]

1. Kuchonganisha na kufitinisha

"Kwa hakika adhabu ya kaburi ni kali mno kwa yule mtu ambaye ni mchonganishi (mambo na maneno ya hapa anayapeleka huko na ya kule anayaleta huku na kufitinisha)

2. Kutojiepusha na vilivyo Najis

Sisi tunapuuzia mno na hatutilii muhimu Najis iwe katika katika hali yoyote ile kwa mafano mkojo, mavi, damu na vitu vingi mno vinajulikana.

3. Kutowawia wema wananyumba yake

Mara nyingi tunaona kuwa mtu anakuwa mchungu na mkali kwa familia yake na hata wengine huwadhulumu wake na watoto wake na kuwaonea na kuwanyanyasa. Na hii ndiyo sababu moja kubwa ya adhabu kali za kaburini. Hivyo inambidi mtu awe mwema na mpole na mwenye mapenzi kwa mke na watoto wake na inambidi kuwalinda na kuwatimizia mahitaji yao na kuwalinda.

Sa'ad ibn Ma'adh alikuwa ni Sahabah wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na alikuwa mwzuri sana na kwamba sanda na mazishi yake yalikuwa yamesimamiwa na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) mwenyewe na hata kuteremka katika kaburi lake aliteremka Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na vile Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema kuwa Malaika wengi mno walikuwa wameshiriki katika mazishi yake.

Mama yake alipopata habari hizo, alisema kuwa Allah swt amjaalie Pepo na kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alijibu, "Bila shaka! Lakini atakuwa na adhabu kali mno kaburini! "Kwa kusikia hayo Masahaba waliuliza, "Je itawezekanaje hivyo wakati bwana Sa'ad alikuwa ni mja na Sahaba mwema?" Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) aliwajibu, "Naam, alikuwa ni mtu mwema lakini alikuwa mkali kwa mke wake, na hivyo atapata adhabu kali humo kaburini."