5
JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA
MADHARA YA KIELIMU NA KISIASA
WAJIBU WA KUJIKINGA DHIDI YA MADHARA YA KIELIMU
Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Wahadharisheni watoto wenu na maghu- lati ili wasiwaharibu, kwani hakika maghulati ni viumbe wabaya mno kati ya viunbe vya Mwenyezi Mungu. Wanadharau utukufu wa Mwenyezi Mungu na wanadai uungu kwa waja wa Mwenyezi Mungu ."[411]
Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Harakisheni kuwafunza wanenu hadithi kabla murjiina hawajawatangulia kwao ."[412]
Tahadhari dhidi ya kuwafuata mbumbumbu: Mwenyezi Mungu amesema: "Wala usifuate usiyo na elimu nayo, hakika masikio na macho na moyo, hivyo vyote vitaulizwa ." (Surat Banii Israil: 36).
Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Msiwe mabubusa, mnasema: 'Watu wakifanya wema nasi tunafanya, wakidhulumu nasi tunadhulumu. Lakini zipeni mamlaka nafsi zenu, watu wakifanya wema nanyi fanyeni wema, wakifanya ubaya basi nyinyi msidhulumu ." [413]
Kumayl bin Ziyad amesema: "Jemedari wa waumini Ali bin Abu Talib alinishika mkono akanitoa hadi jangwani, basi alipoligusa tu jangwa alivuta pumzi kidogo na kisha akasema:'Ewe Kumayl bin Ziyad! Hizi nyoyo ni vyombo na kilicho bora zaidi ni kile chenye kuzingatia. Basi hifadhi kutoka kwangu yale nikwambiayo: Watu ni wa aina tatu: Yupo alimu mtiifu kwa Mola, mwenye kujifunza katika njia ya uokovu. Na mawimbi wafuata upepo wenye kumfuata kila mpiga kelele, wanafuata kila upepo, hawajaangaziwa kwa nuru ya elimu na wala hawajakimbilia kwenye nguzo imara. "[414]
Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Msiwe mabubusa, mnasema: Mimi niko pamoja na watu nami ni kama mmoja kati ya watu ."[415]
Abu Hamza Thumali amesema: Abu Abdillah(a.s) aliniambia: 'Jiepushe na uraisi na jiepushe usiwe mfuata nyayo za watu." Nikamwambia: 'Mimi ni fidia kwako. Ama urais tunaujua, ama kufuata nyayo za watu ni kuwa theluthi ya niliyonayo ni kutokana na kufuata nyayo za watu.' Akaniambia:'Si kama unavyodhani, ni kuwa jiepushe kumpa mtu utawala bila kuwa na hoja, ukaja kumsadikisha kwa kila alisemalo ."[416]
Imam Al-Kadhim(a.s) alimwambia Fadhlu bin Yunus: "Fikisha kheri na sema kheri na wala usiwe bubusa." Nikamwambia: 'Bubusa ni nani?' akasema: 'Usiseme: Mimi ni kama mmoja miongoni mwa watu, kwani hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: 'Enyi watu! Hakika njia ni mbili: Njia ya kheri na njia ya shari. Hivyo njia ya shari isiwe ipendwayo kwenu kuliko njia ya kheri ." [417]
Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Enyi kundi la vijana mcheni Mwenyezi Mungu na wala msiwafuate viongozi, waacheni mpaka wawe wafuasi. Msiwafanye watu marafiki wa moyo mkamwacha [418] Mwenyezi Mungu. Hakika sisi wallahi ni bora kwenu kuliko wao.' Kisha akapiga mkono wake juu ya kifua chake ."[419]
Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Lau kama Mwenyezi Mungu angefahamu kilicho chini zaidi ya (kusema kumwambia mzazi) Akh! katika kutotimiza haki za wazazi wawili basi angekiharamisha. Mwenye kushindwa kutimiza haki za wazazi afanye afanyavyo hatoingia Peponi ." [420]
Imam Al-Baqir(a.s) amesema: "Baba yangu alimwona mwanaume akiwa na mwanaye akitembea kwa miguu huku mtoto akiwa kaegemea kwenye dhiraa ya baba. Akasema: Basi baba yangu hakumsemesha kwa ajili ya kuchukizwa naye mpaka anaiacha dunia ."[421]
Imam Al-Baqir(a.s) amesema: "Baba mbaya ni yule ambaye wema unam- peleka kwenye uvukaji mipaka. Na mtoto mbaya ni yule ambaye kupuuzia humpelekea kutotimiza haki za wazazi ."[422]
Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Kiwango cha chini kabisa cha kutotimiza haki za wazazi ni neno Akh. Na lau kama Mwenyezi Mungu angejua kitu chepesi zaidi ya hilo basi angekikataza ."[423]
Imam Al-Askar(a.s) amesema: "Ujasiri wa mtoto dhidi ya baba yake utotoni mwake hupelekea kumnyima haki zake ukubwani mwake ."[424]
Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Tabia mbaya ni dham- bi isiyoghufiriwa ." [425]
Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alipoambiwa: "Fulani anafunga mchana na kuswali usiku lakini yeye ana tabia mbaya anamuudhi jirani yake kwa ulimi wake.'Akasema: 'Hana kheri, naye ni miongoni mwa watu wa motoni ." [426]
Imam Ali(a.s) amesema: "Ambaye tabia zake zitakuwa mbaya basi riziki yake itabana ."[427]
Imam Ali(a.s) amesema: "Ambaye tabia yake itakuwa mbaya atatengwa na rafiki ."[428]
Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Ambaye tabia yake itakuwa mbaya basi ameiadhibu nafsi yake ."[429]
Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Luqman(a.s) alisema:'Ewe mwanangu mpendwa! Jiepushe na ghadhabu, tabia mbaya na uchache wa subira, haku- na mtu anayekuwa sawa juu ya sifa hizi. Ilazimishe nafsi yako ridhaa kati- ka mambo yako, na ivumilishe nafsi yako katika matumizi ya jamaa na wafanyie watu wote tabia njema ."[430]
Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Ambaye ulimi wake utaogopwa na watu basi huyo ni mtu wa motoni ."[431]
Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Maafa ya uzuri ni mawazo hewa (yatokanayo na kiburi) ." [432]
Imam Ali(a.s) amesema: "Lililo baya mno kati ya mambo ni mtu kujikweza mwenyewe ."[433]
Imam Ali(a.s) amesema: "Atakayejiona adhimu ndani ya nafsi yake basi mbele ya Mwenyezi Mungu atakuwa duni ."[434]
Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Mcheni Mwenyezi Mungu wala msihusudiane nyinyi kwa nyinyi, hakika miongoni mwa sheria za Isa bin Maryam ilikuwa ni kutembea mjini, ndipo siku moja akatoka katika
matembezi yake akiwa na mwanaume mbilikimo miongoni mwa sahaba zake, naye alikuwa ni mwandama mno wa Isa bin Maryam(a.s) .
Isa(a.s) alipofika baharini alisema: 'Bismillahi' kwa usahihi akiwa na yakini nayo, akatembea juu ya maji. Basi mtu yule mbilikimo alipomtazama Isa(a.s) alimuiga kwa usahihi akiwa na yakini nayo, naye akapita juu ya maji na kuungana na Isa(a.s) . Hilo likamfanya ajikweze, akasema: 'Huyu Isa(a.s) Ruhullah anatembea juu ya maji nami pia natembea juu ya maji, basi ana ubora gani juu yangu.' Hapo hapo akazamishwa ndani ya maji na ndipo akaanza kuomba msaada toka kwa Isa(a.s) , akamshika mkono na kumwopoa toka ndani ya maji, kisha akamwambia: 'Ulisema nini ewe mbilikimo?' Akasema: 'Nilisema: Anatembea juu ya maji nami natembea juu ya maji, basi hilo likanifanya nijione.' Isa(a.s) akamwambia: 'Umeiweka nafsi yako sehemu isiyokuwa ile aliyokuweka Mwenyezi Mungu, ndipo Mwenyezi Mungu akakuchukia kwa uliyosema, hivyo tubu kwa Mwenyezi Mungu kutokana na uliyose- ma.' Basi mbilikimo yule akatubu na akarejea kwenye daraja lake ambalo Mwenyezi Mungu alimweka. Mcheni Mwenyezi Mungu msihusudiane nyinyi kwa nyinyi."[435]
Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Jiepusheni na kiburi, kwani hakika kiburi huwa kwa mtu hata kama ana joho ." [436]
Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Hakika mwanaadamu ni mwenye pupa juu ya yale aliyonyimwa ." [437]
Imam Ali(a.s) amesema: "Mwenye pupa ni fakiri hata kama ataimiliki dunia kwa mikono yake ."[438]
Imam Ali(a.s) amesema: "Husuda ni matokeo ya kuchoka ."[439]
Imam Ali(a.s) amesema: "Husuda huzuia raha ."[440]
Imam Ali(a.s) amesema: "Husuda haileti ila madhara na hasira. Hudhoofisha moyo wako na kuuguza mwili wako. Na shari ambayo inayohisiwa na moyo wa mtu ni husuda ."[441]
Imam Ali(a.s) amesema: "Hasidi milele ni mgonjwa (alilu) ."[442]
Imam Ali(a.s) amesema: "Hasidi daima ni mgonjwa hata kama ni mwenye mwili wenye siha ."[443]
Imam Ali(a.s) amesema: "Hasidi hafanikiwi ."[444]
Imam Ali(a.s) amesema: "La ajabu ni mghafiliko wa mahasidi kunako usalama wa miili ."[445]
Imam Ali(a.s) amesema: "Hasidi hudhihirisha mapenzi yake kwenye kauli zake na huficha chuki yake kwenye vitendo vyake. Ana jina la rafiki na sifa ya adui ."[446]
Imam Ali(a.s) amesema: "Matunda ya husuda ni mahangaiko ya dunia na akhera. "[447]
Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Luqman(a.s) alimwambia mwanae:'Hasidi ana alama tatu: Anasengenya anapokuwa hayupo. Huonesha mapenzi ya uongo anaposhuhudia na hufurahia msiba ."[448]
Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Hasidi ni mwenye kujidhuru yeye mwenyewe kabla hajamdhuru mhusudiwa, kama ambavyo Ibilisi kwa husuda yake alirithisha laana ndani ya nafsi yake, na akarithisha kwa Adam (a.s) kujielekeza (kwa Mola wake) ."[449]
Imam Ali(a.s) amesema: "Hikdi huumiza nafsi na huongeza maumivu ya moyo ."[450]
Imam Ali(a.s) amesema: "Atakayetoa chuki basi moyo wake na akili yake hustarehe .''[451]
Imam Ali(a.s) amesema: "Hasira ni sehemu ya uwendawazimu kwa sababu mwenye nayo hujuta, na ikiwa hajuti basi uwendawazimu wake huendelea ."[452]
Imam Ali(a.s) amesema: "Ubishi hunyakua rai ."[453]
Imam Ali(a.s) amesema: "Ubishi huharibu rai ."[454]
Imam Ali(a.s) amesema: "Matunda ya ubishi ni kuangamia ."[455]
Imam Ali(a.s) amesema: "Mbishi hukumbana na balaa. "[456]
Imam Zainul-Abidiin(a.s) amesema: "Ubishi huambatana na ujinga, na ushabiki huletwa na msiba, na sababu ya heshima ni unyenyekevu. "[457]
Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alimwambia Ali(a.s) : "Jiepushe na sifa mbili: Hasira na uvivu, kwani hakika wewe ukikasirika hutosubiri juu ya haki, na ukifanya uvivu hutotekeleza haki ."[458]
Imam Al-Baqir(a.s) amesema: "Hakika mimi nachukia sana mtu kufanya uvivu kunako jambo la dunia yake. Na atakayefanya uvivu juu ya jambo la dunia yake basi ni mvivu kunako jambo la akhera yake ."[459]
Imam Ali(a.s) amesema: "Hakika mambo yalipochanganyikana, uvivu na kushindwa vilijichanganya pamoja na hatimaye vikazaa ufakiri ."[460]
Imam Ali(a.s) amesema katika sifa za muumini: "Utamuona uvivu wake uko mbali; na uchangamfu wake ni wa daima ."[461]
Imam Zainul-Abidiin(a.s) amesema katika dua zake: "Ewe Mola wetu Mlezi tupe neema ya uchangamfu na utukinge na kufeli na uvivu ."[462]
Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Jiepusheni kuifanya nzito dini, kwani hakika Mwenyezi Mungu ameifanya nyepesi, ichukueni kadri muwezavyo, kwani hakika Mwenyezi Mungu hupenda maadamu tu ni katika amali njema hata kama ni ndogo. " [463]
Imam Ali(a.s) amesema: "Atakayeifanya nzito dini basi hatafika kwenye haki ."[464]
Imam Ali(a.s) amesema: "Hutomuona mjinga ila ni mwenye kupuuza au mwenye kupituka ."[465]
Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Si miongoni mwetu wale wanawake wenye kujishabihisha na wanaume. Na wala wanaume wenye kujishabihisha na wanawake ." [466]
Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Makundi ya aina mbili ni ya motoni na sitoyaona: Kaumu wenye mijeledi kama mikia ya ng'ombe wanaitumia kuwapiga watu. Na wanawake wenye kujiachia wenye kubaki uchi, wenye kushawishi wenye kuringa.hawatoingia peponi na wala hawatoipata harufu yake ."[467]
Imam Ali(a.s) amesema: "Mwenye kushabihiana na kaumu hukaribia kuwa miongoni mwao ."[468]
Imam Ali(a.s) amesema: "Ambaye fikara zake zitazama kwenye starehe basi zitamshinda ."[469]
Imam Ali(a.s) amesema: "Ambaye fikara zake zitazama kwenye maasi yatamwita ayaendee ."[470]
Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Wanafunzi wa Isa(a.s) walijikusanya kwake na kumwambia: 'Ewe mwalimu wa kheri tuongoze.' Akawaambia: 'Hakika Musa Kalimullah aliwaamuru msiape kwa Mwenyezi Mungu ilihali ni waongo. Na mimi nawaamuru kuwa msiape kwa Mwenyezi Mungu ilihali ni waongo na si wakweli.' Wakasema: 'Ewe Ruhullah tuzidishie.' Akasema:'Musa Nabii wa Mwenyezi Mungu aliwaamuru msizini nami nawaamuru msizisimulie nafsi zenu zinaa achia mbali kuitekeleza. Kwani hakika mwenye kuisimulia nafsi yake zinaa anakuwa kama mtu aliyewasha moto ndani ya nyumba iliyorembwa, na hatimaye moshi ukaharibu marembo hata kama nyumba haikuungua ."[471]
Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Pombe ni mama wa maovu na maasi ." [472]
Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Pombe ni mama wa mabaya. " [473]
Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Shari yote imekusany- wa ndani ya nyumba, na kunywa pombe kukafanywa ndio ufunguo wake ." [474]
Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Atakaelala amelewa basi huwa amelala akiwa biharusi wa shetani ." [475]
Imam Ali(a.s) amesema: "Mwenyezi Mungu alifaradhisha kuacha pombe ili kuilinda akili ."[476]
Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Hakika maasi akiyatenda mja kwa siri hayamdhuru ila mtendaji wake. Na akiyatenda waziwazi bila kukemewa hudhuru jamii nzima ." [477]