7
MAISHAYA ABU DHARR
"Sasa sikilizeni! Maisha yenu yamegawanyika katika hatua mbili. Mojawapo ya hatua hizo imepita na nyingine inakuja. Fanyeni amali njema na jiepusheni na kutenda dhambi wakati huu uliopo kwa ajili ya hatua ijayo. Sikilizeni! Kama hamtafuata ushauri huu, bila shaka mtaangamia na mtalaaniwa huko Peponi."
Mtu mmoja akamuuliza, "Vema! Tujulishe kwa nini hatupendi kifo?" akasema, "Kwa sababu mmeangamiza maisha yenu ya baada ya hapa duniani kwa sababu ya kupenda mambo ya kidunia. Mnajua kwamba hamkufanya lolote kwa ajili ya Pepo na mtapata matatizo huko. Kwa hiyo inawezekanaje mtu apende kuondoka kwenda mahali, ambapo anajua kwamba haitakuwa vizuri yeye kufanya hivyo."
Halafu akauliza, "Ni jinsi gani tutafikishwa mbele ya Mwenyezi Mungu?" Abu Dharr akajibu, "Wale waliofanya amali njema watakwenda Kwake kama msafiri ambaye amerudi nyumbani kwake, na wala waovu watafika huko kama mtoro aliyefikishwa hapo baada ya kukamatwa."
Halafu, akauliza tena, "Hali yetu itakuwaje mbele ya Mwenyezi Mungu?" Abu Dharr alijibu, "Unaweza kuamua wewe mwenyewe. Yafanyie hukumu matendo yako kwa kuzingatia Kitabu cha Dini. Mwenyezi Mungu anasema: "Watu waadilifu watakwenda Peponi na waovu watakwenda Jahanamu." Akauliza, "kama ndiyo hivyo, huruma Yake itatusaidiaje?" Abu Dharr alisema; "Mwenyezi Mungu tayari amekwisha sema kwamba, huruma Yake ni kwa ajili ya watu waadilifu."
Mtu mmoja alimwandikia Abu Dharr, "Andika vitu vya ujuzi kwa ajili yangu." Alijibu, "Mambo ya ujuzi ni mengi wala hayana mwisho. Ninaweza kukuandikia hadi wapi kuhusu ujuzi huo? Jambo moja tu la kuzingatia usimfanyie ubaya rafiki yako." Halafu aliandika, "Yupo mtu yeyote ambaye humfanyia ubaya rafiki
yake?" Abu Dharr akaandika, "Ujipende wewe zaidi na usiwe na mtu mwingine yeyote ambaye utampenda kuliko unavyojipenda wewe mwenyewe. Kwa hali yoyote ile, ukimkosea Mwenyezi Mungu kwa kutenda dhambi, hakika utakuwa umejifanyia ubaya wewe mwenyewe."
Pia, mahali pengine amesema, "Enyi watu! Mwenyezi Mungu amekuumbeni kama mwanadamu. Usijiteremshe daraja na kuwa hayawani na kuwa mnyama katili kwa kumkosea Yeye kwa kutenda dhambi."
Allamah Shaykh Mufid ameandika; "Siku moja Abu Dharr alisema katika hotuba: "Utalipwa kufuatana na matendo yako. Utavuna kile ulichokipanda, yaani utapata thawabu kulingana na amali zako.Ukifanya amali njema hapa duniani utapata thawabu nzuri Peponi na endapo unafanya matendo maovu utapata adhabu kulingana na hayo Ulimi wako ni ufunguo wa matendo mema na maovu. Unatakiwa kuuziba moyo wako kama unavyofunga pochi yako. Ni kwamba, kama unavyolinda utajiri wako, unatakiwa kuulinda moyo wako vivyo hivyo na jaribu kufanya kila uwezavyo usiruhusu uovu wowote usiingie humo.
Mawazo yanayojikusanya humo lazima yawe safi." (Amali, Shaykh Mufid)
Allamah Majlis ameandika: "Abu Dharr alikuwa na desturi ya kusema mihadhara yake na hotuba zake. Ewe mtafutaji wa ujuzi! Vitu vyote vya hapa duniani vinavyo hali moja katika hizi mbili. Uzuri wao unakunufaisha wewe au uovu wao unakudhuru wewe. Unatakiwa ukipende kitu chenye matarajio ya kukunufaisha. Ewe mtafutaji wa ujuzi! Upo uwezekano isije familia yako na utajiri wako vikufanye wewe usiwe mwangalifu wa maisha yako, kwa sababu ipo siku ambapo kwa hakika utatenganishwa na familia yako na rasilimali yako
na utakapokaribia kuondoka, utakuwa kama mgeni ambaye ameishi na kundi la watu kwa usiku moja na kuondoka kesho yake asubuhi. Sikiliza! Umbali uliopo baina ya kifo na Ufufuo ni kama kuwa katika hali ya ndoto na kuamka haraka sana."
"Ewe mtafutaji wa ujuzi! Peleka amali zako njema mapema kwa ajili ya siku hiyo ambapo utasimamishwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuhojiwa na kujieleza. Mnamo siku hiyo utapata thawabu za amali zako njema na utalipwa fidia kwa tendo lolote jema ambalo umelifanya hapa duniani."[13]
Masimulizi ya hadithi ni kitu chenye muhimu mkubwa. Wala si kila mtu anaruhusiwa kusimulia, ama kusikiliza simulizi zao. Ujuzi wa wahadithi ndio kipimo chake. Abu Dharr ni mmojawapo wa wasimulizi wa kuaminika, kutegemewa na wakweli ambao simulizi zao hazitiliwi shaka au kukataliwa. Amekuwa na Mtukufu Mtume kwa muda mrefu sana wa uhai wake. Kwa maelezo yake ni mengi sana miongoni mwa hayo, machache yameandikwa hapa.
Kuhusu Aya za Qurani Tukufu! Enyi mliamini! Mtiini Mwenyezi Mungu, Mjumbe wake na "Ulil amr-i minkum," Imamu Fakuddin Razi ametoa maelezo kwenye Tafsirul Kabir kwamba Aya hiyo inawazungumzia wale wasiokosea na Saiyid Ali Hamadani ameitaja katika Mawaddatul Kubra kwamba inawahusu wenye utakaso kumi na wawili.
Lakini inahitaji kuthibitishwa na masahaba wa Mtume wenye kuheshimika kwamba Mtume mwenyewe alisimulia hadithi hiyo. Abu Dharr anasimulia kutoka kwa Mtume kwamba aya iliyotajwa hapo juu ilipo funuliwa, alimwomba Mtukufu Mtume amwambie majina ya Waku wa mambo 'Ulil Amr. Aliwataja maimamu kumi na mbili. Baada ya kuwataja majina, Abu Dharr anatoa maelezo kwa ufupi kwamba mteule wa kwanza ni Ali na wa mwisho ni Imamu Mahdi. (Yanabiul Mawaddah, Shaykh Sulayman Qandozy al-Hanafi na Riuzatul Ahbab).
Abu Ishaq Thalabi ameandika kwenye maelezo yake: "Siku moja Bin Abbas alikuwa anasimulia hadithi za Mtukufu Mtume(s.a.w.w) alipokuwa ameketi karibu na kisima cha Zamzam ambapo mtu mmoja aliyefunika uso wake alikuja hapo. Bin Abbas alinyamaza kwa muda. Mtu huyo alianza kusimulia hadithi ya Mtume Bin Abbas akasema, "Ewe mtu! Nina kuuliza katika jina la Mwenyezi Mungu uniambie kwa kweli wewe ni nani?" Alifunua uso wake na akasema, "Enyi watu! Yule anaye nijua mimi ananijua mimi, lakini yule asiyenijua mimi, anatakiwa anitambue kwamba mimi ni Abu Dharr Ghifari. Nimesikia kutoka kwa Mtukufu Mtume kwa masikio haya mawili ambayo yanaweza kupata maradhi na kuwa kiziwi kama sikukosea, na nimeona kwa macho haya mawili ambayo yanaweza kupofuka endapo mtasema uwongo kwamba Mtume alisema kuhusu Ali kwamba ni kiongozi wa watu waadilifu na muuaji wa watenda maovu. Mtu aliye msaidia yeye alipata ushindi na yule aliye mtelekeza yeye naye alitupwa."
Kufuatana na simulizi ya Abu Dharr Ghifari, Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: "Ali ni lango la ujuzi wangu mwongozo wa wafuasi wangu wa lengo lililosababisha nitumwe. Kumpenda yeye ni imani na kumfanyia uadui yeye ni unafiki na kuwa rafiki yake ni ibada."[14]
Kwa mujibu wa simulizi ya Abu Dharr, Mtume alisema: "Mtu akiniheshimu mimi, anamheshimu Mwenyezi Mungu. Asiye iheshimu mimi, hamheshimu Mwenyezi mungu. Mtu anayemheshimu Ali, ananiheshimu mimi, na yule asiyemheshimu Ali haniheshimu Mimi."[15]
Abu Dharr anasema; "Tulikuwa tunawatambua wanafiki kwa vitu vitatu: Kwanza kwa kumkana Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, mbili kwa kuacha kusali, na tatu kwa chuki yake dhidi ya Ali." (Arjahul Matalib uk. 608 kwa mamlaka ya bin Shazan).
Ipo hadith ambayo imesimuliwa na Abu Dharr, kwamba Mtume alisema, "Ali ni lango la ujuzi wangu. Yeye ni msimulizi wa mambo hayo ambayo yamesababisha niteuliwe. Ku mpenda Ali ni imani na kumchukia ni unafiki, na kumwangalia yeye ni ibada." Bin Abd al-Barr ameandika kwenye Istiab kwamba masahaba wengi wamesimulia hadithi hii ya Mtume: "Ewe Ali! Hapana yeyote atakaye kuwa rafiki yako isipokuwa muumini, na hapana yeyote atakayekuwa adui yako isipokuwa mnafiki."[16]
Abu Dharr amemnukuu Ummu Salamah kwa kusema kwamba alimsikia Mtukufu anasema; "Ali yu mkweli na ukweli umo kwa Ali na Ali na ukweli hawatatengana hadi watakapofika kwenye Haudhi ya Neema.[17]
Allamah Subaiti ameandika: "Abu Dharr amesema kwamba Mtume alimwambia yeye "Mtu anaye kubali imani kwa uaminifu huuweka moyo wake katika hali safi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, husema ukweli, huwa makini, anakuwa na tabia njema, hutumia masikio yake kusikiliza mambo mazuri, na hutumia macho yake kuona vitu vinavyostahili, atapata ukombozi."
Abu Dharr anasema kwamba Mtume amesema: "Wafuasi wangu hawata neemeshwa endapo watafuturu kabla ya muda na kuchelewa kula daku kabla ya alfajiri (muda wa kuanza kufunga wakati wa mwezi wa ramadhani)."Abu Dharr anasema kwamba Mtukufu Mtume anasema: "Furaha yangu ni kwamba dhahabu igawiwe kama sadaka hata kama ingekuwa kubwa kama Mlima Uhud."[18]
Abu Dharr anasema kwamba Mtukufu Mtume amesema: "Ewe Ali! Mwenyezi Mungu ametufanya mimi na wewe kuwa mti mmoja. Mimi ni mizizi ya mti huo na wewe ni tawi lake. Mwenyezi Mungu atamtupa mtu Jahananu kwa kutanguliza uso wake, kama akikata Tawi Lake." Aliendelea kusema, "Ali ni kiongozi wa Waislamu na Imamu wa wacha Mungu. Atawaua watakaovunja ahadi ya utiiifu kwake (watu wa Jamal), walio tengwa na jamii (makhawariji) na wakanushaji."[19]
Abu Dharr anasema kwamba Mtukufu Mtume amesema; "Ali kwangu ni kama Harun alivyokuwa kwa Musa isipokuwa tofauti moja tu kwamba hapatakuwepo na Mtume badala yangu."
Hadithi hii imenukuliwa na masahaba wengine wengi, miongoni mwao wakiwemo Umar bin Khatab, Sa'd bin Abi Waqqas, Abu Hurayrah, Abdullah bin Mas'oud, Abdallah bin Abbas, Jabir bin Abdullah, Abu Said Khidri, Jabir bin Samrah, Malik bin Harith, Bara bin Azib, Zayd bin Arqam, Anas bin Malik, Abu Ayyub Al-Ansari, Aqil bin Abi Talib na kadhalika (Arjahul Matalib).
Allamah Abdul Mu'min Shablanji ameandika kwenye kitabu chake 'Nurul Absar' kwamba, Abu Dharr, ananukuu kutoka kwa Mtume ambaye alisema: "Kitendo kizuri kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni kumpenda yeye na kutofanya chochote kinyume na Ridhaa Yake.."
Abu Dharr anamnukuu Mtukufu Mtume(s.a.w.w) akisema: "Unapokuwa na urafiki na mtu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mfahamishe ."
Abu Dharr anasimulia kwamba Mtukufu Mtume anasema; "Mtu anapokasirika, kama amesImamua, ni vema aketi chini na endapo hasira haipungui, alale chini. "[20]
Abu Dharr ananukuu hadithi ya Mtume kwamba Mwenyezi Mungu humpenda mtu anaye vumilia anapotendewa mabaya na jirani yake. (Nurul Absar, uk. 32).
Abu Dharr anasema kwamba Mtume(s.a.w.w) ameagiza uchaji Mungu na kujinyima na alituomba tulinde dhamana, tusipite tunaomba kwa mtu yeyote, tusivunje uhusiano wa kimapenzi uliopo baina ya watu wawili, kumtendea wema mtu anayekutendea ubaya, na kumuogopa Mwenyezi Mungu kila mara katika jambo la wazi na siri (Nurul Absar, uk. 33).
Abu Dharr anasimulia hadith ya Mtume hivi: "Mwenyezi Mungu alifananisha Ahlul Bait na Safina ya Nuhu (Safinatu Nuh) kwa wafuasi wangu. Yeyote aliyepanda humo, aliokoka na yeyote ambaye hakupanda alikufa maji, yaani kwa usemi mwingine alikengeuka.
Pia Ahlul Bait wangu, wapo kama mlango wa kwendea toba (Hittab) kwa wafuasi wangu. Kuhusu wana wa Uyahudi ambao Mwenyezi Mungu aliwaambia kwamba mtu aliyeingia kupitia mlangoni, ataokoka kutokana na mateso ya dunia na Akhera. Vivyo hivyo,
yeyote yule kutoka miongoni mwa wafuasi wangu akifuata njia ya Ahlul-Bait wangu na anaendelea kuwa imara katika kuwafuata, ataokolewa katika Siku ya Hesabu."
(Ainul Hayat).
Ali bin Shahab Hamadani anamnukuu Abu Dharr ambaye anasema kwamba alimsikia Mtukufu Mtume anasema; "Ewe Abu Dharr! Ali ni yeye ndiye atakayezigawanya Pepo na Jahanamu. Ewe Abu Dharr! Hakuna hata malaika moja aliyeweza kupata heshima ya kugawa Pepo kutoka kwenye Jahamanu. Tazama! Pepo ipo pale kwa ajili ya wanao muunga mkono yeye na amepewa ndugu kama mimi ambapo hakuna ndugu ya mtu yeyote yupo kama mimi."
Abu Dharr anamnuku Mtukufu Mtume akisema; "Mwenyezi Mungu ameimarisha Uislamu kupitia kwa Ali Ali anatokana na mimi na mimi ninatokana na Ali, na Aya hii,
"Basi mtu aliye na dalili wazi itokayo kwa Mola wake Mlezi, inayofuatwa na shahidi anaye toka kwake na kabla yake kilikuwa Kitabu cha Musa kilicho kuwa mwongozi na rehema ......" (11:17).
Imeteremshwa kuhusu yeye (Ali) mimi ninao uthibitisho katika Aya hii na Ali ni shahidi yangu" (Muwaddatul Qurba, uk. 78)
Kwa mujibu wa Abu Dharr, Mtume alimwambia Ali, "Ewe Ali! Mtu anayenitii mimi, anamtii Mwenyezi Mungu na mtu anayekutii wewe,
ananitii mimi, na mtu asiyenitii mimi hamtii Mwenyezi na mtu asiyekutii wewe, hanitii mimi." (Muwaddatul Qurba uk. 78 na Yanabiul Mawaddah, Shaykh Sulayman Qandozy).