50%

BIBLIA NENO LA MUNGU

KIMETUNGWA NA: SEYYID MUHAMMAD MAHDI HUSAINI SHIRAZI

KIMEFASIRIWA NA: SEYYID MUHAMMAD MAHDI MUSAWY SHUSHTANI

KIMETOLEWA NA: BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA

P.O. BOX 20033

DAR ES SALAAM

Tanzania

DIBAJI

Hii ni tafsiri ya Kijitabu Kilichoandikwa kwa lugha ya Kiarabu, Kilichoandikwa na Ayaatullah Seeyyid Muhammed Mahdi Shirazi wa Karbala. Tafsiri yenyewe ilifanywa na Seyyid Muhammed Mahdi Shushtari wa Unguja. Sura nyingi Zilichapishwa kwa mfulizo katika gazeti letu. Sauti ya Bilal na zilipendeza sana. Sasa kijitabu hiki kimechapishwa ili Kuwarithisha zaidi wasomaji wetu. Hatuna budi kutamka hapa kuwa mujibu wa imani yetu, Mitume wote waalikuwa wametumwa na Mwenyezi Mungu Kuwaongiza watu katika njia iliyo sawa. Waalifanya hivyo kwa kuhubiri wema wao mkuu na kwa matendo yao maadilifu.

Kufanya hivyo iliwapasa wawe waongofu zaidi, waadilifu na kuwa wakamilifu katika uchaji wao kwa Mwenyezi Mungu. Wasingeweza kusema uwongo iwapo wao walifundisha watu kusema kweli.Wasingeweza kumwomba Miungu, iwapo wao waliwataka watu kumwomba Mungu Aliye Mmoja tu, na kadhalika. Hata hivyo, Biblia inasingizia zote za maovu na madhambi kwa Mitume hao. Ama viongozi wa Kiyahudi na Wakristo walikuwa na madhambi makubwa kabisa, la sivyo, basi ni makosa ya Biblia yenyewe (inayoaminiwa kuwa si maandishi ya Musa wala Isa a.s) Kwa hiyo, ni juu ya msomaji mwenyewe kuteua yapi yanayomfaa na yapi yasiyomfaa.

Syed saeed Akhtar Rizvi