11%

ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE

MUANDISHI: MAREHEMU MULLA MUHAMMAD JAAFAR SHERIF DEWJI

DIBAJI

kitabu hiki kinatoa ufafanuzi wa hadithi maarufu ya mtume muhammad(s.a.w.w) ambaye amesema:

"Yeyote atakayekufa pasina kumtambua imamu wake atakufa mauti ya mpagani." kila mwislamu mwenye kuamini kauli ya bwana mtume(s.a.w.w) hana budi kufanya kila juhudi ya kumtambua imamu wake wa wakati huu maana dunia hii haiwezi kubaki hata sekunde moja bila ya hujjah ya mwenyezi mungu (s.w.t) kuwapo. ama kwa hakika, kuwa na imani katika imami ni mzizi mmoja wapo wa dini, maana kazi ya kuiongoza na kuihifadhi dini ni wajibu wa imamu baada ya kuondoka duniani bwana mtume(s.a.w.w) .

Ndipo kitabu hiki kinafaa kisomwe na kila mwislamu! na kutafakari aya za kurani, hadithi za bwana mtume(s.a.w.w) za maimamu waliotajwa na mtume(s.a.w.w) na maelezo ya kihistoria yaliyomo ndani yake. kila neno lina maana na maarifa yake.

Mwalifu wa kitabu hiki, marehemu mulla muhammad jaafar sherif dewji, amefanikiwa kueleza kwa uwazi dhana ya uimamu ambaye ni usuli unaofafanuliwa kwa masimulizi kuhusu kuzaliwa, na kughibu na maisha yake marefu, ungojaji wa waumini kutokeza kwake, mahala aishipo, na ishara na dalili za kujitokeza kwa imam mehdi. vilevile ameeleza faradhi za waumin miongoni mwa mambo mengine mengi ya msingi na muhimu. mtarjumi wa kitabu hiki kwa lugha ya kiingereza kutoka lugha ya kigujarati ni alhajj murtaza a. lakha na alhaj z; m. s. lakha amekitarjumi kwa kiswahili chepesi na chenye ufasaha.

Maulana seyyid sabir husein musawi, qibla, ametilia shime kitabu hiki kichapishwe kwa kiswahili na mkarimu mmoja amejitolea kugharimia uchapishaji wa hiki kitabu.

Alla subhanahu wa taala kwa wasita wa mtume muhammad(s.a.w.w) na mwanae imam mehdi(a.s) atawajazi kila lililo jema mchapishaji huyo na wengine waliosaidia kwa dhati dhamira , hali na mali kueneza habari hizi muhimu zinazohusu imani na amali za waumini wa dini ua uislaam. miye, al-hakiri, ninashukuru kupewa fursa hii ya kuandika dibaji na ninaamini kuwa nami pia nitakubaliwa na imamu wangu kuwa mmojawapo wa mfuasi wake na kupata shifaa yake siku ya kiyama na pia hadhi ya kukutana naye hapa duniani.

alhaji muhsin m.r.alidina

Dare -es-Salaam

25 shawwal, 1409.