5
ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE
SURA 5
HADITHL KUHUSU KUWEPO KWA IMAM WA ZAMA HIZI
Hadhrat Mahdi(a.s) wanazuoni wengi mashuhuri wa madhehebu ya kisunni wameandika kuhusu kuwapo kwa hadhrat mehdi(a.s) katika vitabu vyao. kati ya hao tunaorodhesha majina ya wanazuoni 14:
1) Shaikh Kamil Abdul Wahab Sharam.
2) Mulla Ali Asadullah Akbar bin Mawdudi.
3) Mulla Nurdin bin Abdulrahman bin Ahmad jamii.
4) Khaja muhammad parsa, Ahmad bin Mahmoud Al hafizi.
5) Sheikh Abdul Haqi Muhadith Dehlawi,
6) Allama Sheikh Nuruddin bin Sabag Maliki.
7) Shah Waliyullah Muhaddis Dehlawi.
8) Allam Hamwayn Shafi'i mwandishi wa Faraidu Simtayn.
9) Sheikh ata Naishapuri.
10) Sheikh Kabir Shamshudin Tabrizi.
11) Sheikh Neimkillah Al Walli.
12) Sheikh Kamil Arif Matuk Misri.
13) Sheikh Saad bin Hamawi.
14) Shaik Suleiman bin Ibrahim Balkhi Kunduzi sheikhul islam wa Istambul (uturuki) na mwandishi wa wa kitabu kinacho julikana sana katika madhehebu ya sunni Yanabiu Al-Mawaddah.
Waandishi hao wote wameandika katika vitabu vyao kuwa mwana wa hadhrat Imam hassan askari(a.s) , hadhrat Mahdi(a.s) yu hai na ameghibu.
Licha ya hayo wanazuoni wengi wengine wamenakili taarifa kama hizo katika vitabu vifutavyo:
1. Kitabu cha Jaamiul- Usul, kikitumia ushuhuda uliopo katika Bukhari, Muslim. Abu Dawood na Tirmidhi wamenakili matamshi ya Abu Hureira kwamba: Mtume(s.a.w.w) alisema:"Miongoni mwa wafuasi wangu kikundi kimoja kitatangaza jihadi ya kushinda vita vyote. hapo nabii Issa atateremka kutoka mbin guni na kiongozi wa hicho kikundi hadhrat mehdi (a.s) atamkaribisha nabii Issa kuongoza swala ya jamaa lakini nabii Issa atajibu "wewe ndiye mwenye mamlaka (madaraka) juu ya viumbe wa Mungu na kutokana na dhuria ya mtume Muhammad (s.a.w.w) Mwenyezi Mungu amekutunukia heshima na ubora kuliko waumini wote wa wakati huu". kanji, mfuasi wa ushafi'i, vile vile amenakili hadithi hii na ametilia mkazo kwamba hadithi hiyo ni sahihi.
2. Hafidh Abu Nairn na Tabarani katika kitabu chao Muazamu -akber wamenakili kwamba mtume muhammad(s.a.w.w) amesema: "Baada yangu watakuja makhalifa ambao baadhi yao watakuwa watawala na baadhi yao watakuwa wafalme dhalimu.
Baada ya hapo atakuja mehdi kutokana na kizazi changu kama mungu alivyoahidi na atatokeza na kueneza unyoofu na uadilifu katika dunia hii.
3. mwanazuoni anaye aminiwa sana katika madhehebu ya sunni huko india obeidullah amratsari, amenakili katika kitabu chake arjahul ma talib, ukurasa 472, kwamba sheikh abu abdullah na muhammad bin yusufu kanji shafi katika kitabu chao al bayan fi akhbare-sahibuz-zaman ameandika kwamba hadhrat mehdi(a.s) yu hai na ameghibu na kuna sababu nyingi za kuthibitisha hayo. Kwa mfano nabii issa, nabii idris na nabii ilyas ni mitume ambao wamekuwa hai kwa miaka maelfu na vile vile katika maadui wa mungu, dajjal na iblis watakuwa hai mpaka muda maalum; kwa hivyo hakuna cha kustaajabisha kwamba hadhrat mehdi(a.s) yuna umri wa miaka 1100.
4. Ibnu hajar hanafi makki katika kitabu chake sawaikul muhrika, ukurasa 481, ameandika kwamba jina la hadhrat mehdi(a.s) ni muhammad na majina mengine yake maarufu yanayo julikana ni: abul qasim na lakabu ni mehdi, saleh, qaaim, muntadhar, na sahibuz-zaman. wakati alipofariki baba yake hadhrat imam hassan askari(a.s) , imam mehdi(a.s) alikuwa na umri wa miaka mitano tu. mwenyezi mungu alimjaalia elimu hekima katika utoto wake. sababu ya kupatiwa lakabu ya qaaim ni kuwa yupo hai lakini ameghibu na maskani yake hayajulikani.
5. Katika kitabu hicho hicho, ukurasa 102, imeandikwa kwamba hadhrat mehdi(a.s) atajitokeza kabla kurudi (kuteremka kutoka mbinguni) nabii issa. katika hadithi nyingi mtume mtukufu(s.a.w.w) amesisitiza kwamba hadhrat Mahdi(a.s) atatokana na kizazi chake na baada ya kujitokeza atatawala kwa muda wa miaka saba na kustawisha insafu duniani na baada ya muda mfupi tu nabii issa atateremka kutoka mbinguni na hadhrat mehdi(a.s) atamwua dajjal.
Kuna hadithi nyingi kuhusu hadhrat mehdi katika vitabu vinavyojulikana sana katika madhehebu ya sunni lakini bado baadhi ya wanavyuo wa kisunni wanaamini kwamba hadhrat medhi hajazaliwa bado na baadaye ndiyo ataeneza insafu duniani. ijapokuwa hiyo ni baadhi ya imani ya maulamaa wa kisunni, lakini kutokana na wingi wa hadithi na ushahidi wa kihistoria ni dhahiri kwamba hadhrat mehdi(a.s) alikwisha zaliwa tarehe 15 shaban 255 a.h. kwa hiyo, si jambo la kubishana tena juu ya kuzaliwa kwake. mwanazuoni wa kuaminika mno wa kisunni, muhammad yazeed hafiz bin maajah (aliyefariki dunia 273 a.h.) katika kitabu chake sunan ibni maajah ameandika (kurasa 518/519) kwamba zipo hadithi nyingi za mtume muhammad(s.a.w.w) kuhusu hadhrat mehdi(a.s) kuwa atatokana na dhuria yake na kizazi cha binti wake fatima(a.s) . atakuwa ameteuliwa kwa amri ya allah na atakuwa mrithi wake. Mtume mtukufu(s.a.w.w) tena amewataradhia waislamu wote kwamba wakipata bahati ya kuonana naye (kuwa hai katika karne ya hadhrat mehdi(a.s) basi wamtii yeye. vile vile ameeleza kwamba hamza, jaffar, ali, hassan, hussein na mehdi watakuwa viongozi huko peponi.
Imam Ahmad bin Hambal (aliyefariki 240 a.h.) mwandishi maarufu wa vitabu vya kisunni amearidhia katika sehemu ya kwanza ya kitabu chake musnad, ukurasa 99, kwamba imesimuliwa kuwa "mwenyezi mungu atamleta mehdi(a.s) aliyetokana na dhuria yangu kutoka mafichoni kabla ya siku ya kiyama, japokuwa ikibakia hata siku moja kabla mwisho wa dunia, naye ataeneza haki, usawa na usalama duniani na kutokomeza dhuluma na ukandamizaji." sheikh-ul-islam wa istanbul, sheikh suleiman nakshbandi hanafi, katika kitabu cha yanabeeul-mawaddah, katika ukurasa wa 494, amenakili masimulizi kutoka kwa jabir bin abdullah ansari kuwa Mtume(s. a.w.w) amesema: "Baada yangu watakuwa maimam 12; wa kwanza ni Ali, na watakaofuata baada ya Ali ni Hassan, Hussein, Ali bin Hussein, Muhammad bin Ali(a.s) (Baqir). Eh! Jabir wewe utabahatika kuonana na huyo Baqir(a.s) , tafadhali mpe salam zangu. Na baada yake, Jaffar bin Muhammad. Mussa bin Ali bin Muhammad, Hassan bin Ali na Baada yao atakuja msubiriwa Mahdi(a.s) . Mahdi atakuwa mrithi wa kumi na mbili na wa mwisho. yeye atakuwa na jina langu na lakabu ya kassim. atakuwa mwana wa Hassan bin Ali, Al-Askari.
ahmad bin hajar makki katika kitabu chake sawaikulmuh-rika, ukurasa wa 116, na vile vile tirmidhi katika kitabu chake jame-a, ukurasa wa 33, wamenakili kwamba mtumemtukufu(s.a.w.w) amesema, "baada yangu watakuwa warithi wangu kumi na wawili ambao watakuwa makhalifa wangu na hao wote watatokana na mbari ya quraishi".
Sheikhul-kamil, Abdul Wahab, amearidhia katika kitabu chake yawakit wa jawahir kuwa, "wakati dunia itapojaa ukandamizaji na ukafiri ndipo hadhrat mehdi(a.s) atatokeza. yeye (hadhrat mehdi(a.s) ni mwana wa hadhrat hassan al- askari(a.s) , alizaliwa tarehe 15 shaaban 255 a,h. na yupo hai duniani. wakati nabii issa atapoteremka kutoka mbinguni yeye (mehdi a.s.) atatokeza na kuishi naye; wakati wa kuandika kitabu hiki umri wake (hadhrat mehdi a.s.) ulikuwa umekwisha timia miaka 1146."
Abu Abdullah muhammad bin muhammad bin yusuf muhammad bin kanji shafii amenakili katika kitabu chake "kifayya tut-talib" kuwa: "haiwezi kupingwa kwamba hadhrat mehdi(a.s) yu hai hadi leo. Dalili kwamba yeye anaweza kuwa hai kwa muda mrefu inatokana na uhakika kwamba manabii issa, khidhr na elias wapo hai duniani kwa miaka elfu kwa maelfu. Hao ni manabii wa mungu, lakini maadui wake (mungu) pia kama dajjal mwenye jicho moja na lblis aliye laaniwa wapo hai hadi leo kama ilivyo thibitishwa katika qur'an.