3
MWENYEZI MUNGU NA SIFA ZAKE
SOMO LA TATU
MWENYEZI MUNGU NA MANTIKI YA JARIBIO (JARABA)
Bila shaka, hali ya kijamii, mambo ya kihistoria na kielimu, na aina mbali mbali za kazi za binadamu ni mambo ambayo haviwezi kuwa bila mvuto juu ya uonyeshaji kwa vitendo wa mwelekeo wa ndani wa mtu na tabia zake za kiroho na kihisia. Ingawa hali hizi mbali mbali hazisababishi ulazima wowote au umuhimu katika uchaguzi wa mwelekeo wa mtu, zinaweza kusababisha kuwepo kwa mazingira yanayofaa zaidi kwa ajili ya uchaguzi wa aina fulani, kwa hiyo kutoa mchango muhimu kuhusu jinsi binadamu anavyoviona vitu. Hali hizi wakati mwingine zinaweza hata kujionesha katika umbo la kikwazo kwenye uhuru wa mtu na uwezo wa kuchagua. Kama matokeo ya uzoefu zaidi wa maamuzi ya kisayansi na ya kimajaribio, akili ya binadamu kwa kawaida huelekea kuonea haya kwa kiasi fulani maamuzi halisi ya kiakili kabisa, hususan kama jambo linalofanyiwa uchunguzi sio yakinifu na halina maana.
Kwa ujumla, uwezo wa kiakili za mtu hupata nguvu na ustadi kwenye eneo ambamo zinatumiwa sana. Mambo yaliyoko nje ya eneo hilo, kwake (binadamu) huonekana kuwa si ya kweli au si halisi au vizuri zaidi ni jambo la hatua ya pili au linalohusika kidogo sana na jambo analolishughulikia maalum hasa. Kwa hiyo, mwanadamu huelekea kuhukumu kila kitu kwa namna ya kipekee. Mojawapo ya vipengele viharibifu na vinavyo potosha sana katika fikra zihusuzo Mwenyezi Mungu ni kuziwekea mipaka fikra ndani ya mantiki ya elimu za kimajaribio na kushindwa kutambua viwango na mipaka ya mantiki hiyo. Kwa kuwa wataalamu wa sayansi za majaribio kutumia nguvu zao zote za kiakili kwenye elimu za kihisia, wanakuwa wageni kwa mambo yaliyoko nje ya utambuzi wa hisia.
Ugeni huu, umbali huu kutoka kwenye mambo yasiyohusiana na hisia, imani hii isiyo ya kawaida juu ya data zinazotokana na sayansi za majaribio, hufikia kiwango kiasi kwamba kupima na kufanya majaribio huunda muundo wote wa akili na mtazamo wa dunia wa wataalamu kama hao. Wanaona majaribio kama ndio nyenzo pekee inayokubalika na njia ya utambuzi, kama kigezo pekee Wanakitegemea hicho kutatua matatizo yote. Kazi ya sayansi hizo ni kufafanua uhusiano baina ya mambo; lengo lao ni kuthibitisha uwiano baina ya matukio, si baina ya Mwenyezi Mungu na matukio. Katika sayansi za majaribio, mwanadamu hahusiki kabisa na Mwenyezi Mungu. Mtu asiwe na matumaini ya kuweza kutambua ukweli wa hisia za juu kwa kutumia kigezo cha hisia, au kamuona Mwenyezi Mungu ndani ya maabara.
Sayansi hizo haziwezi kufanya majaribio ya maabara juu kuwepo kwa Mwenyezi Mungu na halafu wafikie uamuzi kwamba endapo kitu hakionekani kimwili na hakiwezi kuthibitishwa kwa njia ya majaribio ya maabara na ukokotozi wa kimahesabu, kwa hiyo, kitu hicho hakina ukweli. Kwa kweli hakuna jaribio lolote linaloweza kufanywa na kupambanua kama kitu kisicho cha ki-maada kipo au hakipo, kwa sababu ni kitu hicho tu ambacho kinaweza kukanushwa kwa njia ya majaribio kinachoweza kuthibitishwa kwa njia ya majaribio. Sayansi na metafizikia ni aina mbili za elimu ambazo zina kiwango sawa cha uhalali na usahihi. Kanuni ya metafizikia haitokani na majaribio wala haiwezi kukanushwa na majaribio.
Maelfu ya majaribio ya kisayansi yanabuniwa ili yathibitishe kwamba vitu vyote ni vya ki-maada, yote yatashindwa kufikia malengo yao. Mwanasayansi wa majaribio anayo haki ya kusema, "Nimevumbua hiki na hiki," au "Sijagundua hiki na hiki." Hana haki ya kusema, "Kitu hiki na kile havipo." Mbinu za maabara, pamoja na utata wao na hali ya juu ya maendeleo, haziwezi kupata njia kupitia yasiyojulikana, giza na dunia iliyopanuka ya vitu vya asili, ambavyo ndio kiini cha majaribio, haziwezi kufahamu ukweli wote uliojificha katika kiini cha chembe zisizo na kikomo na haziwezi kuvumbua hata asili halisi ya kitu.
Mbinu inayotegemea majaribio imekuwa na manufaa sana katika kuendeleza utambuzi wa mwanadamu wa mpangilio sahihi wa maumbile, na inaweza kutoa msingi ulio dhahiri na mpya kwa ajili ya kumwamini Mola Mlezi kupita kwenye uchunguzi wake wa utaratibu wa uumbaji, kwani inaashiria kuwepo kwa Muumba mtambuzi na mwenye uwezo. Hata hivyo, nia na madhumuni ya wana sayansi katika utafiti na uchunguzi katika masuala ya maumbile na siri za dunia kwa ujumla si kwa sababu ya kumtambua Muumbaji wa uhai. Ikiwa katika mkondo wa kuendelea kukua kwake katika mikono ya watafiti, sayansi wakati wote imekuwa inagundua siri za kuwepo kwa maumbile bila ya wanasayansi kujitokeza, kwa njia ya sayansi yao, kutoka kwenye ujuzi mfinyu na wenye mipaka ambao wameupata kutoka kwenye hatua yao ya utafiti wa sasa.
Endapo wangelikuwa wafanye hivyo, wangelifahamu uunganishwaji wa mambo na kujiweka chini kwa vitu vyote kwenye utaratibu uliowekwa, na kwa hiyo, kupata hatua nyingine mbili za ziada za ujuzi na utambuzi. Kwanza wangeweza kuwianisha data zao zote za kihisia na majaribio, na halafu wangeweza kutoa uamuzi wa busara na kufanya tafsiri. Bila kukubali kuwepo kwa Muumba mwenye busara, haiwezekani kutoa tafsiri kwa kusadikisha ukamilifu wa data zenye tofauti zinazotokana na elimu mbalimbali na uhusiano uliopo baina yao.
Kwa matendo, hata hivyo, kazi na mbinu za fikra ya kisayansi ni kuunda kanuni na kufanya utafiti bila marejeo kwa Mwenyezi Mungu, hivyo kwamba mfumo wa fikra ambamo Mwenyezi Mungu hahusishwi unakuwa mhimili ambao juu yake kazi ya kisayansi huugeukia, na kusababisha mwanadamu kuwa mgeni na chochote kilichopo nje ya upeo wa fikra hiyo. Wakati huo huo, maisha ya kivitendo ya mwanadamu yanasihusiana na elimu bila kuepukika. Matokeo yanayotokana na ujuzi unaotegemea majaribio yanajumuisha mielekeo yote ya ki-maada ya maisha, kuwafunga wanadamu kwenye kuta zao nne zisizopenyeka, na ni vigumu sana kupata nyenzo yoyote ya kawaida miongoni mwa njia za maisha ya mwanadamu.
Hali hii kwa ulazima huongeza kuamini kwa binadamu katika sayansi na huathiri tabia yake, kumdukizia nafsini mwake hali ya mashaka na wasiwasi. Juu ya hayo, manufaa ya hali ya asili ya kitu kilichofanyiwa uchunguzi kwa kutumia sayansi ya majaribio kinagusika na kiko dhahiri kwa kila mtu, kwa tofauti kubwa sana ikilinganishwa na masuala ya metafizikia. Vivyo hivyo, vitu vya kimaada ambavyo vimechunguzwa kwa kutumia sayansi ya majaribio vinaeleweka sana, ambapo kinyume chake ni kweli katika masuala ya metafizikia.
Kuwasilisha masuala ya kidini kwa kutumia mbinu isiyo sahihi iliyofuatwa na kanisa la zama za kati (1100-1500A.D), ikichanganywa na uadui kwenye udhihirikaji wote wa sayansi, ilikuwa ndio jambo muhimu sana katika kuifanya sayansi ya majaribio kuonekana yenye kupendelewa zaidi kuliko yale ya mambo kifalsafa na ya kimaada. Kwa ufupi, sayansi ilionekana kupingana cha dini, si kwenda sambamba nayo. Mara mantiki ya majaribio ilipofuzu katika kumwaga fikra zote ndani ya umbo lake, ilibadili sura ya mtazamo wa wanadamu juu ya dunia kwa kiwango ambacho kwamba walisadiki kwamba huo tu ndio ulikuwa msingi kwa ajili ya kukubali ukweli wa kitu. Waliiteua kuwa ndio mamlaka ya mwisho na wakaona kwamba haiwezekani kuthibitisha kuwepo kwa kitu chochote ambacho hakitambuliki kwenye akili.
Hivyo, mwana sayansi anayetegemea majaribio, ambaye hafahamu utaratibu wa watu wanaomjua Mwenyezi Mungu, anakubali na kuona kuwa ni sawa katika maisha yake, kila kinacholingana na mantiki na fikra ya kisayansi. Hujichukulia mwenyewe haki ya kukanusha chochote kisichochukuana na desturi yake ya kisayansi. Utaratibu wake ni imani kamili katika majaribio na kuiona kuwa ni ndio uthibitisho pekee wa usahihi wa maamuzi yoyote. Katika hali kama hii, ambapo msingi wote wa fikra za kidini unapuuzwa, mwanasayansi anajikuta hana kanuni zozote za kumwezesha kutafsiri yale masuala madogo madogo ya kidini ambayo hujitokeza katika namna ya amri na makatazo. Akiwa amezoea kabisa lugha ya kisayansi na kutegemea kanuni, anakuwa amejifunga kabisa kwenye desturi yake na kudhani amri za dini zinazoshurutisha, zilizo rahisi na zinazoeleweka, kuwa hazina maudhui au thamani.
Njia hii ya fikira ina dosari na si sahihi. Ingawa sayansi zina fomula (kanuni) changamani za ajabu na sahihi, ambazo kuzielewa kwake huhitaji uchunguzi wa kina na mgumu, fomula hizo hizo huondoka kwenye nyanja ya sayansi mara ziingiapo katika maisha yetu ya kawaida, hujitenga na lugha ya kifundi ya wana sayansi. Kama isingekuwa hivi, zingedhibitiwa kutumika kwenye vituo vya kisayansi na viwanda, maktaba na vituo vya utafiti.
Kila mtu anaweza kutumia vifaa kama simu na radio. Hali ni hiyo hiyo kwa nyenzo na zana za kisayansi. Juu ya usahihi na uchangamano wao, maelekezo kidogo yenye utaalamu yatamwezesha mtu yeyote kuzitumia. Mtu aliyebobea na mtaalam huwa hawatoi maarifa ya umakenika na ya ufundi kwa wanunuzi wa kifaa, badala yake, hufupisha maelezo yao katika sentensi fupi fupi yale matokeo ya kazi ngumu zilizovumiliwa na wavumbuzi. Kwa hiyo, si haki na ni kinyume cha mantiki ya kisayansi kujaribu kulazimisha amri za dini (ambazo haziwezi kufupishwa kuwa fomula za kisayansi, ambapo zikiwa rahisi na za kila mahali) kwenye tabia ya dhana na maoni ya mtu, na halafu zitangazwe kwamba hazina thamani na si za maana, huku wakipuuza wajibu wao wa kimaamuzi na athari zao za maana sana katika maisha yetu. Maelezo ya kivitendo huzaa matunda yao wakati yanapotamkwa katika lugha inayoeleweka kwa ujumla na kuwa na mguso kwa kila mtu na maisha ya kijamii.
Zaidi ya hayo, endapo ingedhaniwa kwamba amri na maelekezo ya dini yangeamuliwa na ufahamu, uelewa na muonjo wetu hapangekuwepo na haja ya wahyi na Mitume; tungeweza kuanzisha dini zetu wenyewe! Mara nyingi mwanadamu huwa hazioni dosari zake, akishughulishwa kama alivyo na nguvu zake. Mwenye kuabudu sayansi wa dunia ya leo anajivunia sana pia ujuzi wake kama matokeo na maendeleo ambayo yameyapatikana kutoka kwenye sayansi za majaribio kiasi kwamba anajidhania yeye mwenyewe kwamba ameshinda na kwa ushindi huo amechukua umiliki wa dunia ya ukweli. Lakini, hapana mtu ambaye wakati wowote ameweza kudai kwamba amepata ujuzi wa siri zote za ulimwengu na kuondosha mapazia yote kutoka kwenye dunia ya maumbile ya asili.
Mtu lazima achukuwe mtazamo mpana zaidi juu ya hali halisi na atambue ni jinsi gani tone la elimu yake lilivyo dogo likilinganishwa na bahari ya siri zilizofichika ambazo zinatukabili sisi. Baada ya kila ugunduzi wa kisayansi, msururu zaidi wa mambo yasiyojulikana hujitokeza. Katika karne zote ambapo mwanadamu amekuwa akifanya kazi bila kupumzika pamoja na rasilimali zake zote ili aweze kuijua dunia kwa kadiri iwezekanavyo, matokeo pekee ya jitihadi zake yamekuwa ugunduzi wa mambo machache miongoni kwa siri nyingi za ulimwengu. Ni hatua chache tu zimechukuliwa katika njia hii, na kuna lundo kubwa la yasiyojulikana yaliyoizunguka elimu ya mwanadamu kama wingu.
Kwa hiyo, mtu lazima atathimini kwa uhakika zaidi upeo wa utambuzi wa sayansi za hisia na sehemu zao zinazofaa kwa shughuli na athari. Mawazo yote yaliyokuwepo hapo kabla ambayo ni kama vizuizi kwenye njia ya kwenye ukweli lazima yaachwe kwa ajili ya uchambuzi sahihi.
Bila shaka, sayansi za majaribio zinaweza kutujulisha vipengele vya nje tu vya jambo; ni vitu vya ki-maada na mambo yakinifu ambavyo vinakuja kwenye upeo wa uchunguzi wao na vinaweza kuathirika kwenye majaribio ya maabara. Utaratibu wa sayansi katika kufanikisha malengo yao, wakiwa wanatafuta kupata faida kutoka kwenye kila ongezeko dogo katika ujuzi, ni uchunguzi na majaribio. Kwa kuwa shughuli ya msingi wa sayansi ya majaribio ni uchunguzi wa dunia ya nje, ili kuweza kuwa na uhakika kwamba nadharia fulani ya kisayansi ni sahihi, lazima tuilinganishe na ulimwengu wa nje ili kuijaribu. Endapo dunia ya nje inathibitisha kwa kufaa zaidi, sisi tunaikubali; laa kama sivyo, basi hatuikubali.
Kwa hiyo, kuzingatia lengo na utaratibu wa sayansi ya majaribio, lazima tuhoji endapo kama ukweli wa metafizikia unategemea kwenye kipimo cha hisia na kufanyiwa majaribio? Hivi hoja yoyote ya majaribioya kisayansi lazima ina haki ya kuingilia kati masuala ya imani na itikadi? Je, kuna sehemu yoyote ya sayansi ya majaribio inayohusika na Mwenyezi Mungu? Ili kuweza kugundua usahihi na kutokuwa sahihi kwa jambo katika sayansi za majaribio, ni muhimu kufanya matumizi ya mabadiliko na ya kuondoa vipengele tulivyopewa, pamoja na mazingira yake. Utaratibu huu hautumiki kwenye uhai wa ki-mungu, wa milele, usiobadilika na wa vitu vingi.
Ujuzi yakinifu ni taa ambayo inaweza kumulika baadhi vitu visivyojulikana kwa miale yake lakini si taa ambayo inaweza kuondosha giza lote. Kwani elimu ya mfumo hutegemea kuufahamu ujumla wake wote kabisa na namna ya ufahamu ambayo inaweza kuunganisha wenyewe sehemu zote za utambuzi, na kusababisha mtazamo wa mbali mtimilifu kabisa. Sasa kuifungia elimu ya mwanadamu kwenye kikomo cha sayansi za hisia hauwezi kumfikisha mtu kwenye mtazamo wa mbali kamili, bali kwenye ufahamu wa eneo la ndani zaidi la nafsi.
Kama tunamwamini Mwenyezi Mungu au laa, kwa kweli haina uhusiano na sayansi za majaribio, kwa sababu kwa kuwa kiini cha uchunguzi wao ni maada, sayansi zinazojihusisha na mambo yanayoonekana hayana haki ya kujieleza yenyewe kwa kukubali au kukataa kuhusu jambo lolote lisilokuwa la ki-maada. Kwa mujibu wa imani ya kidini ya madhehebu mbali mbali, Mwenyezi Mungu sio mtu - hana mwili. Hawezi kufahamika kwa kutumia milango ya fahamu. Yeye ameupindukia muda na nafasi (havihitajii). Yeye ni Ambaye kuwepo kwake hakutawaliwi na mipaka ya kidunia na nafasi haiwezi kumbana. Kwa hiyo, Yeye ameepukana na kuhitaji na ametukuka katika dhati yake juu ya upungufu wa aina yoyote.
Anavijua vipengele vya ndani sana na vya nje vya ulimwengu. Dunia ipo wazi mbele Yake. Mwisho kabisa, Anacho kiwango cha juu kabisa cha ukamilifu na ametukuka zaidi kuliko chochote kinachomhusu Yeye kinachoweza kuingia kwenye akili ya mwanadamu. Hatuwezi kabisa kuujua msingi wa dhati Yake, tukiwa tuna upungufu wetu wenyewe na wa uwezo wetu, akili na nyenzo za upambanuzi. Kwa sababu hii; endapo ukivichunguza vitabu vyote vya sayansi ya majaribio, hutakuta utajo hata kidogo wa majaribio kuhusu Mwenyezi Mungu au uamuzi wowote umetolewa kuhusu Mwenyezi Mungu.
Hata kama tutachukulia utambuzi wa hisia kuwa ndio njia pekee ya kugundua ukweli, hatuwezi kuthibitisha kwa kutegemea utambuzi wa hisia, kwamba hakuna kitu chochote kinachokuwepo nje ya ulimwengu wa hisia. Madai kama hayo, yenyewe yatakuwa si ya kutegemea majaribio, yakiegama kwenye ushahidi usiokuwa wa hisia au majaribio. Hata kama wafuasi wa madhehebu ya kidini walikuwa hawana uthibitisho wa kutetea madai yao, kuhitimisha kwa uthabiti na kwa nguvu kwamba visivyokuwana uhai, vimeenea nje ya upeo wa hisia, ungekuwa ni uchaguzi usio wa kisayansi, ulio tegemea kwenye dhana na minong'ong'oni.
Watu wengine hujaribu kutangaza njozi hizi kwa kuisingizia sayansi na kuonyesha uchaguzi wao kuwa umetokana na fikra ya kisayansi. Hata hivyo, katika mchanganuo wa mwisho, ukanushaji unaohusishwa kwenye madai kama hayo hayana thamani ya sayansi na falsafa, na vilevile yanapingana na mantiki ya majaribio. Kwenye kitabu kiitwacho 'The Elementary Principles of Philosophy'. George Pulitzer anasema, "kukidhania kitu ambacho hakikalii muda na nafasi na hakiathiriwi na mabadiliko wala maendeleo, ni jambo lisilowezekana."
Ni wazi ya kwamba maneno haya yanaakisi njia fulani ya fikra ambayo haijui inatafuta nini. Kama ingejua inachokitafuta, pia ingeelewa namna ya kukitafuta. Kwa kuwa shughuli ya aina hii ya fikra inazunguka kwenye maumbile na himaya ya hisia, ni kawaida kwamba itachukulia kama ni kitu ambacho hakiwezekani, kila kile kilichopo nje ya eneo la shughuli yake na kuwepo kwake ambako hakuwezi kuthibitishwa kwa njia ya majaribio ya hisia. Itaiona imani katika ukamilifu wake hasa kama ni kinyume na muundo wa fikara ya kisayansi. Hata hivyo, wasomi wanaojishughulisha na elimu asilia wanakabiliwa na lundo kubwa la vitu visivyojulikana kuhusu dunia hii hasa, na vya dhahiri, visivyo na uhai ingawaje wakati wote vina mawasiliano nayo (mbali na ulimwengu wa maada, wenye miujiza na siri nyingi zisizo na idadi, haihusishi hili tufe la dunia tunayoishi tu). Wasomi kama hao, kwa hiyo, wanayo haki yakusema tu, "Kwa vile nyanja za kimiujiza zipo nje ya upeo wa zana zangu za kitaalamu, ninanyamaza kimya na sitakanusha. Wangewezaje kujiruhusu kutoa madai ambayo yangesababisha elimu pana kiasi cha kama mpango wa ulimwengu wote, ambapo ujuzi wao wa mpango wote wa uhai unakaribia sufuri?
Kuna uthibitisho gani wa kuhakikisha madai kwamba uhai ni sawa na kitu cha ki-maada na kwamba dunia yote ya uhai imejaa vitu vya kimaada? Ni mwanasayansi gani anayeikataa metafizikia ambaye ameweza kusimamisha kanusho lake juu ya mantiki au ushahidi, au kutoa ushahidi kwamba nje ya kutokuwepo uhai, hakuna kitu kilichopo nje ya uwanja wa hisia? Ingawa sayansi haikatai kwa uwazi na uhakika kabisa kila kitu kisichojulikana kwa sababu tu kwamba haina uwezo wa kukifikia kwa kutumia nyenzo na vifaa vyake, badala yake inangojea kwa uvumilivu siku ambapo kitu hicho kitavumbuliwa, wapenda anasa za dunia wala hawaliendei suala la kuwepo kwa Mwenyezi Mungu kwa shaka na wasi wasi, kwa misingi ya maoni yao ya kimakosa na haraka, wanatangaza uamuzi wao kwamba hakuna Muumbaji!
Watu kama hawa huanzisha vigezo na viwango fulani kwa ajili ya matumizi yao; na hawapo tayari kutumia kigezo kingine kilichoanzishwa kwa makusudi fulani katika eneo lililokusudiwa. Mathalan, kamwe hawatatumia kigezo ambacho kinatumika kwenye uso wa kitu kupimia mwili, lakini inapokuja kwenye kupima dunia ya hisia nyingi wanajaribu kumpima Mwenyezi Mungu, roho na msukumo, kwa kutumia nyenzo hizo hizo wanazotumia kupima dunia yakinifu. Wanapojikuta hawawezi kupata ujuzi wowote wa viumbe kamili husika, wanaendelea kukana kuwepo kwa vitu hivyo.
Sasa kama mtu aliyefungwa kwenye mantiki ya majaribio atapenda kukubali ukweli wa ulimwengu kwa kadiri tu alivyoruhusiwa na uzoefu wa hisia na kukanusha chochote kilichopo nje ya hilo, lazima atambue kwamba hii ni njia ambayo amejichagulia mwenyewe, si matokeo ya uchambuzi wa majaribio ya kisayansi. Aina hii ya itikadi bandia ya usomi na uwezo wa kiakili hutokana na uasi wa kisomi na mtu kuacha asili yake halisi.
Huyo Mwenyezi Mungu ambaye mwanasayansi wa kawaida, anataka "kuthibitisha" kwa kutumia nyenzo zake na vifaa vyake, kwa hali yoyote ile, sio mungu asilani kwa mtazamo wa wale wanaomcha Mwenyezi Mungu.