Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

KUMTEGEMEA ALLA

1 Voti 01.0 / 5

BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM

KUMTEGEMEA ALLA

Wengi katika waliomtegemea M/MUNGU katika ulinzi wake ni wenye kufaulu kwani M/MUNGU hashindwi na viumbe vyake kwa kuwa ndiye aliyeumba uhai na mauti basi hapana aliye na nguvu kumshinda. M/MUNGU ni mpururiaji na yanapowafika Binaadamu warudi na watafakari lakini wasipotoke kwa kudhani M/MUNGU kawasahau.
Bali aliloandika limfike Mwanaadamu hapana wakudhuwiya ,ni vyema sote tuwe nafikira moja kuu nayo nikurudii kwake baada ya muda alotuandikia kuishi,mwenyewe MWENYEZI MUNGU anasema katika kitabu chake kitukufu ayya ya 51 Suraaat AT-TAWBA “Sema halitatusibu ila katuandikia M/MUNGU yeye ni mola wetu basi Waislam wamtegemee M/MUNGU tuu”
Wengi walipewa nguvu na wakazitumia nguvu hizo vibaya ,wengi wakaneemeshwa mali na mali hizo zikawatia kiburi na jeuri .Bila shaka hivi ndivyo dunia ilivyotawaliwa na fikra potofu ya Mwanaadamu kumdharau Mwanaadamu mwenziwe .Mwenye nguvu humkandamiza mwengine ,na mwenye husda na fisadi kwa jamii nyengine hutafuta sababu na vipenyo kutimiza ndoto ya Ufisadi wake kwa lengo na madhumuni maovu zidi ya mwenziwe.
Kwenye ayya 116 ya Al-TAWBA ALLAH (S.W) Anasema . “M/Mungu anao Ufalme wa mbingu na ardhi huhuwisha na hufisha nanyi hamna walinzi wala wasaidizi isipokuwa M/mungu” .Dunia imeanza kwa miaka ,karne na dahari waliondoka Watawala wa dola zilizovuma walipururiwa wakajiona wakajisahau kwa kuona nguvu na majigambo yao kwa watu ,neema ya mali na ujuzi ilitosha kuwaenguwa miongoni Mwawanaadamu waliomtegemea M/Mungu .
Lakini bila shaka walivaa kofia ya ujahili,koti la ukatili na viatu vya ufedhuli vyote hivyo ni vyepesi kuondolewa tena kwa wepesi sana !!Lakini jee hatupewi mtihani ilituamini kikweli? Maanawapo ambao mara mazito yanapo wakabili hubabaika na huamini duwa ni nyepesi mbele ya matendo, ndivyo ambavyo Firauni alitenda na kujiamini lakini alinaswa kwa wepesi silaha yake ni asili yake ,yaani maji kama ni asilii ya uhai basi maji yalimmaliza pia na kuwekwa bayana ufukweni . Basi Ufirauni unaendelea kwa maana ya watu wenye matendo ya fiarauni kujiona wana nguvu nawakaamuwa kudhili ulimwengu huchukuwa hukumu nzito na wakazichekelea lakini wasisahau historia na maandiko matakatifu wajikumbushe humo.M/Mungu huwatia ujasiri viumbe wake na katika ujasiri huo pakawepo siri ya ukweli kwa wale wanaoamini na wale wanao kufuru .
M/Mungu katika ayya 111 ya surat AL-TAWBA anawambia waumini “ Mwenyezi mungu amenunuwa kwa Waislam nafsi zao mali zao ili na yeye awape pepo wanapigana katika njia ya M/Mungu wanauwa na wanauwawa hii ni ahadi aliyojilazimisha katika Taurati,Injili na Qura’n ,Na ninani atekelezaye ahadi yake kuliko M/Mungu ?” Hadi mwisho wa ayya hiyo .
Ni tabia ya wanaadamu wanapoonyana basi hupatikana wenye kusikia na wapo wenye kukadhibisha wapo wenye subra na fikra na wapo wenye haraka na upumbavu hupatikana kipimo hapo iwe kwa mtu, kikundi au hata Dola iliyo na nguvu jinsi MOLA alivyo na nguvu ya kusambaratisha Dola hiyo au msimamo wake , na pia hutia msukosuko na mtihani kwa sehemu hizo hukosa uwezo au kutokuwa na msimamo au kuvumilia mtihani uliyojitokeza . Anayepewa zile nguvu baadhi ya wakati humdharau yule asiye na nguvu lakini nguvu ya moyo yenye kumtuma mtu huwa na nguvu zaid kuliko dhana au majigambo hiii ni mitihani yake MOLA ndiyo apimae mwenye kuamini na wasiyo amini.
kwenye Surrat Fatri ayya 43 na 44 .Anatwambia M/Munngu "Kwaajili ya kutakabari kwao katika ardhi na kufanya vitimbi vibaya vibaya na vitimbi vibaya vibaya havimteremkii ila yule aliyevifanya basi hawangoji ila desturi iliyokuwa kwa watu wa zamani watu hutapata mabadiliko katika kawaida ya M/Mungu wala hutakuta mageuko katika kawaida ya M/Mungu ,Jee hawakusafiri katika aridhi wakaona mwisho wa wale walokuwa kabla yao ? Na walikuwa wenye nguvu zaid kuliko wao na hakuna kitu kinachoweza kumshinda M/Mungu mbinguni na aridhini bila shaka yeye ni mwenye kujuwa mwenye uweza ” Hadi mwisho wa tafsiri .

Mifano ni mingi wapo walioangamizwa kwa harika ya maji , wapo walo mwagiwa changarawe za motoni ,wapo walodondoshewa vijiwe na ndege wadogo na wakabwagwa chini na ndovu wao wakubwa , nawapo walopelekewa tufanii.Basi na watambee na waangamize lakini watafurahi kidogo bali watalia sana hiyo ni ahadi ya MOLA kwa kila aliyemuovu fisadi katika ardhi.

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini