SIRI ZA MAFANIKIO I

BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM

SIRI ZA MAFANIKIO I

Kipindi cha matarajio na hamu ya kupata mafanikio

Kipindi cha ujana ni kipindi cha hamu ya kupata na matarajio. Ni kipindi cha kuwa na furaha. Ni wakati ambao mustakbali wa kila kijana huja mbele ya macho yake katika sura ya ndoto tamu. Huanza kufikiria. Hufanya mipango na kuzipima raghba kuu katika moyo wake.

Hata hivyo, wakati fulani hutokea mtu akashindwa katika kipindi cha ujana. Mtu huyo, hata baada ya kuwa mtu mzima. akawa hawezi kufikia hata moja katika matarajio yake.

Wakati fulani pia hutokea, bila mategemeo, kwamba mtu akapata zaidi ya matarajio yake na ndoto zake tamu zikawa kweli.

Kwa kweli, mtu mmoja kufanikiwa na mwingine kushindwa sio majaaliwa au bila sababu iliyo nyuma yake. Sababu za yote mawili lazima zitatokana na maisha ya wahusika.

Tunaweza kuwa na hakika kuwa yule anayefanikiwa alianza maisha katika namna ambayo humpa uhakika wa mafanikio, na yule anayeshindwa, kwa kiasi kikubwa, hufanya hivyo kutokana na makosa yake mwenyewe. Ni kwa sababu amepita katika njia ambayo haikumpeleka kwenye makusudio yake.

Katika mfululizo wa makala haya, malengo yetu ni kuelezea sababu za mafanikio ya watu waliofanikiwa ulimwenguni, ili kizazi kichanga kiweze kufaidika nayo na kupita njia ya moja kwa moja na hatimaye kuepuka vichochoro visivyojulikana vilivyojaa kila aina ya viunzi.

Siri za mafanikio sio moja au mbili tu. Ingawa mafanikio hupatikana kutokana na yale walioyarithi kutoka kwa wazazi wao katika namna ya sifa za ndani, tabia za kiasili na akili. Kwa hakika sifa hizo haziwezi kupatikana kwa kufanya juhudi, kwa kuwa ni hiba itokayo kwa Mungu, ambayo Mwenyezi Mungu amewajaalia kwa ajili ya kusimamia mambo yao ya kiulimwengu.

Kitabu hiki pia kitathibitisha kuwa, hata kama misingi hii ya kurithi huandaa maendeleo ya vijana, sio viamuzi pekee vya maisha ya mafanikio. Sababu za kweli za maendeleo ni tofauti kabisa, bali ni zile ambazo yeyote apendeleaye kufanikiwa anaweza kuzitafuta kwa urahisi na kuzitumia katika fursa yake. Kwa kutumia mbinu hizo anaweza kuwa mwanajamii wa aina yake na hata kuwa mtu aliyefanikiwa zaidi ulimwenguni. Mafanikio hayo pia ni ya thamani na yenye kusifika, kwa sababu, kuna vijana wengi ambao wanakosa njia ya mafanikio na hatimaye kushindwa katika maisha.

Maendeleo ya mtu, Kwa kiasi kikubwa, hutegemea, mafunzo, bidii, juhudi na mipangilio sahihi.Wasomaji watayaona mambo haya katika kurasa za sehemu hii.Taathira ya urithi Ni kidogo Sana ikilinganishwa na sababu hizo.

Sasa tutafafanua kwa ufupi siri za mafanikio huku tukitoa vielelezo vya mifano kutoka katika maisha ya watu wakubwa.

MWISHO