Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

SIRI ZA MAFANIKIO II

0 Voti 00.0 / 5

BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM

SIRI ZA MAFANIKIO II

Pendeleo na shauku

Moja katika sababu za mafanikio ni kufanya kazi unayoipenda na ambayo inalingana na akili au uwezo wako wa kiakili.

Mwenyezi Mungu hajatuumba sisi katika namna moja. Sisi wote hatukupewa uwezo wa kufanya kila kitu. Bali, ili kuendesha jamii kwa yakini, amempa kila mtu ladha na mwelekeo wa aina yake. Imekuwa hivyo, ili mtu aweze kuchukua utaalamu anaoupenda au unaolingana na kipaji cha akili yake, na unaomvutia; na hivyo kuzalisha faida kutokana na ustadi wa kiasili.
Kwa ujumla, moja kati ya sababu za vijana kushindwa na hata kuanguka ni kutofuata kanuni hii imara. Na kutokana na propaganda mbaya na mafunzo ya kimakosa huziendea kazi ambazo haziendani na vipaji vyao.Huchukua shughuli zisizofaa.
Husahau kanuni inayokubalika isemayo: “kila akili ina mwelekeo maalumu. Bahati nzuri ni kwa yule anayeupata”.

Maendeleo na mafanikio ya mwanafunzi hupata pigo kali pale anapoingia katika uwanja ambao haupo katika safu ya kipaji chake asilia. Kwa mfano, ikiwa kijana anavutiwa na fasihi, kama ulimi na kalamu yake vinatawanya lulu za fasihi na akawa moja kwa moja hana mapenzi na masomo ya hisabati, kwa hakika hatoweza kufanikiwa isipokuwa katika uwanja wa fasihi.
Ukurasa katika historia ya mchoraji mashuhuri:

Sasa, tusome mfano kutoka kwenye kumbukumbu za mchoraji mashuhuri: Alikuwa ni kijana mzembe kipindi cha masomo yake. Hakusoma vizuri na wala hakuwaruhusu washirika wake kufanya hivyo. Alikuwa ni mwiba katika njia yake mwenyewe na ile ya wenzake. Bado muonekano wake ulionyesha kuwa alikuwa ni kijana mwenye kipawa.
Profesa mmoja ambaye alikuwa ni mtaalamu wa mambo ya saikolojia, alimuita, akampa ushauri na kumounya kuwa alikuwa na mtiririko mbaya wa aina ya maisha yake. Alishauri kuwa: hakuna yeyote mwenye bahati ya kutosha ya kuwa katika ulinzi wa wazazi wake milele. Maisha yamejaa masaibu. Namna uishivyo itakufanya uathirike vibaya huko mbeleni…Hata hivyo, profesa huyo aligundua kuwa wakati alipokuwa akimshauri huyo kijana, yeye alikuwa akishughulishwa na kuchora picha sakafuni kwa kutumia kipande cha mkaa.

Mara moja, profesa huyo mwerevu, alitambua kuwa kijana huyu alizaliwa kuwa msanii na hakuwa na habari yoyote na matatizo ya hesabu za aljebra. Juhudi yoyote ambayo angeifanya katika uwanja wa hisabati isingemfaa chochote.
Kwa kutambua jukumu lake juu ya jambo hili, alimtaarifu mlezi wa kijana huyu kuhusu ugunduzi wake. Alimweleza baba wa kijana huyo kuwa: “mtoto wako anapendezewa na uchoraji. Kama ukibadilisha kitivo chake, atapata umaarufu mkubwa katika uwanja wa sanaa”.

Siku zilipita na maneno ya profesa yakawa kweli, kwani kijana huyo alikuja kuwa mchoraji mahiri.
Edison aliulizwa na baadhi ya watu: “kwanini vijana hawawezi kuishi maisha yenye mafanikio?” Akajibu: “kwa sababu hawaijui njia yao na hivyo wanasafiri kupitia njia nyingine”.

Watu wa namna hiyo huwa na madhara kwa jamii katika namna mbili: Hawachukui utaalamu ambao wana uwezo nao na unaoweza kuwapatia mafanikio. Na madhara mengine ni kwamba, wanajibebesha majukumu ambayo hawawezi kuyatekeleza.

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini