TOFAUTI KUU ZA SHERIA 4

BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM

TOFAUTI KUU ZA SHERIA 4
SHERIA ZA KIISLAMU NA MUUMBA.
Mazingatio makuu ya Sheria ya Kiislamu ni kuweka uhusiano imara baina ya Muumba na kiumbe. Kwa mfano Swalah, Zakaah, kufunga Ramadhan ni kwa ajili ya Allah (Subhanahu Wataala) peke Yake tu na kumuabudu Yeye Allah (Subhanahu Wataala.) Yeye ndie Mtoa Sheria, Anaamrisha binaadamu kufanya au kujizuia kufanya kitu kwa minajili ya kuwa karibu na Muumba na wakati huo huo kulinda haki yake mwanaadamu na viumbe wengine. Kwa mfano tunazuiwa kuzini, kuiba, kuua, kuharibu mazingira n.k ili kulinda cheo cha binaadamu pamoja na kulinda haki za binaadamu na viumbe wengine. Tofauti na sheria za binaadamu ambapo mazingatio yake makuu ni kutofautisha dini na sheria. Ni kusema kuwa sheria za mwanaadamu haiweki kanuni na mahusiano baina ya watu au watu na Serikali yao. Lakini sheria ni sehemu ya dini ndani ya Uislamu. Uislamu unaweka kanuni baina ya binaadamu na Muumba wake na wakati huo huo ukiwekwa uhusiano mzuri baina yake na watu wengine, tofauti na sheria za binaadamu ambazo zinaweka mahusiano baina ya watu tu.
Hapa lazima tukumbushe kuwa mwanaadamu ametunga sheria za kulinda wanyama na mazingira. Sio kwa ajili ya hao wanyama au mazingira, bali kuharibiwa kwake kunaathiri maisha ya mwanaadamu na uhai wa dunia kwa ujumla. Uislamu umeenda mbali na kusema kila kiumbe (hata jua ni kiumbe) kina haki ya kuishi na kutumiwa kulingana na mafundisho sahihi ya dini.

MWISHO