Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

UFAFANUZI WA DINI NO.6

0 Voti 00.0 / 5

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

UFAFANUZI WA DINI NO.6

Ufafanuzi wa dini:-

Dini ni udadisi na utafutaji wa mwanaadamu kwa ajili ya kumfikia na kumtambua Mola wake, siku zote, hatima ya udadisi na utafutaji huo humalizikia kwa Mola Mtakatifu, kwa hiyo udadisi na utafutaji huo ni lazima ufanywe kwa mujibu wa mapendekezo ya mwanaadamu mwenyewe.

Ufafanuzi huo wa dini ulioelezewa hapo juu hautoshelezi, kwa sababu, (ingawa) Mwenyeezi Mungu anayekusudiwa ni yule Mwenyeezi Mungu aliye katika nyoyo za wanaadamu, na hii inaonyesha nafasi ya mwanaadamu katika dini, hali ya kwamba maudhui ya dini ni mwanaadamu, na nafasi ya dini kwa mwanaadamu sio Mwenyeezi Mungu tu, bali kuna mambo mbali mbali yaliyo muhimu kwa mwanaadamu.

Katika makala iliyopita tulielezea kuhusu ufafanuzi wa dini , na tukaashiria baadhi ya vidokezo ambavyo vinahusiana na mada hiyo ya dini katika makala hii vile vile tutaendelea kuelezea vidokezo hivyo vinavyohusiana na umuhimu wa dini katika jamii ya wanaadamu.

Ili kutambua umuhimu wa dini ni vyema tukaashiria baadhi ya vidokezo vinavyohusiana na ufafanuzi na umuhimu wa dini kwa walimwengu na jamii kwa ujumla.

Vidokezo kuhusiana na ufafanuzi wa dini.

Vidokezo vya mwisho:

Kidokezo ni habari au jambo linalosaidia kutoa fununu au njia ya kufumbua tatizo fulani.

Kidokezo cha kumi na tatu:

Dini ina nafasi muhimu katika uhusiano wa mambo mbali mbali ya mwanaadamu, na dini ni mpango uliopangwa katika nidhamu maalumu, basi dini sio kuakisika kwa uhusiano wa watu na jamii,(yaani, dini haiashirii (hairejeshi nyuma mahusiano ya wanaadamu). Ni dini pekee ndiyo iliyo na nafasi katika utendaji wa mambo mbali mbali, yakiwemo mahusiano ya wanaadamu, kwa maelezo zaidi, kwa ufupi tunaweza kusema hivi:-

(dini ina nafasi muhimu katika mahusiano mbali mbali ya wanaadamu). Kwa hiyo ni jambo lisilokubalika kusema kuwa; dini imekuja kuashiria mahusiano ya wanaadamu tu, bali dini imekuja na imeteremshwa kwa sababu mbali mbali, na uashiriaji wa mahusiano ya mwanaadamu ni miongoni mwa sababu hizo. Kwa hiyo ufafanuzi alioutoa Marks kuhusiana na dini sio sahihi na wala haukubaliki. Yeye anasema:-

“Dini (inaakisi) inaashiria mahusiano ya jamii, maashirio ambayo ni kama pazia linalozuia kuona kwa undani (kuona sawa sawa) maashirio hayo . Ufafanuzi huo sio sahihi, kwa sababu:-

Moja: Kwa ufafanuzi huo wa dini, inatubidi tukubali kuwa; kila uhusiano uliokwisha akisiwa ni dini, hali ya kwamba kuna tofauti baina uhusiano na uhusiano mwengine, basi kutakuwa kuna mapingano baina ya dini na dini. (dini zitakuwa zinapingana).

Mbili: kama itakuwa kila uakiswaji wa mahusiano ya jamii ni dini, basi mahusiano ya kijamii ya wale wasiokuwa na dini yako wapi? Au Marks anataka kusema kuwa watu wasio na dini hawana mahusiano yoyote na jamii?

Tatu: Haiwezekani kuifunga dini katika mambo ya mahusiano na jamii tu, kwa sababu mahusiano yenyewe yanajitokeza kulingana na mahitajio ya wanaadamu, au kutokana na dhati ya nafsi ya wanaadamu ilivyo.

Nne: Kukubalika kwa ufafanuzi huo wa Marks, yaani ni kukubalika kuwa katika dini hakuna maamrisho wala sheria zozote.

Tano: Kuna dalili gani zinazothibitisha kuwa, dini ni uakisi wa mahusiano ya jamii, na kuna uthibitisho gani unaothibitisha kuwa kuna malazimiano baina ya uakisi huo wa mahusiano na kutokuona uwiano uliopo katika jamii?.(yaani uakisi ndio unaosababisha kutokuona uwiano uliopo ndani ya jamii). Hivi kuna dalili gani inayothibitisha kuwa; mtazamo wa wale wasio na dini wanauona uakisi na mahusiano hayo kwa jicho la uhakika? (yaani; wasio na dini wana mtazamo gani kuhusu uhusiano wa jamii, hivi kweli watu hao wanauona uhusiano wa jamii kwa jicho la uhakika)?

Sita: Hivi dini imteremshwa kwa ajili ya kuthibitisha uhakika wa mahusiano ya jamii? Ikiwa dini imeteremshwa kwa ajili ya kubainisha mahusiano tu, basi wale wasio na dini wana mabainisho gani kuhusiana na mahusiano ya jamii? Wasio na dini wanatumia vigezo gani (vilivyo sahihi) katika kuthibitisha mtazamo wao. (kuhusiana na uhusiano wa jamii) na kupinga mtizamo wa wenye dini? (dini ya Mwenyeezi Mungu).

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini