Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

KUFUNGUA SAFARINI KWA MUJIBU WA KITABU NA SUNNA 1

0 Voti 00.0 / 5

KUFUNGA SAFARINI KWA MUJIBU WA KITABU NA SUNNAH/ HADITHI SAHIHI

Sehemu ya kwanza

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema mwenye Kurehemu.

بسم الله الرحمن الرحيم

Kila sifa njema ni za Mwenyezi Mungu mlezi wa Ulimwengu.

الحمد لله رب العالمين

Rehema na Amani zimfikiea Mbora wa viumbe na hitimisho la Mitume wake, pia kizazi chake kitakatifu ambacho ndiyo kasha la elimu yake na hazina ya mafunzo yake.

Hakika Uislamu ni imani na Sheriah. Imani ni kuamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake na siku ya Mwisho. Na Sheriah ni hukumu za Mwenyezi Mungu Mtukufu ambazo zina jukumu la kumpa mwanadamu maisha bora nakumhakikishia wema wa dunia na Akhera.

Sheriah ya Kiislamu ni ya kipekee kwa Kuwa inahusika na kila jambo huku ikiweka wazi utatuzi wa matatizo yote yanayompata mwanadamu katika sekta zote za maisha yake, hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema:

Leo (18 Dul Hijja, 10H, karibu na kisima cha Ghadir khom) nimewakamilishieni dini yenu na kuwatimizieni neema yangu na nimewapendeleeni Uislamu uwe dini yenu." 5:3.

اليوم أكملت لكم دينكم وأتممت عليكم نعمتي ورضيت لكم الإسلام دينا

Isipokuwa kuna masuala madogo madogo ambayo wanavyuoni wa Sheriah wametofautiana kwa sababu ya kutofautiana kwao kuhusu riwaya (za kubuni) ambazo zimenasibishwa kwa Mtukufu Mtume saww, jambo lililosababisha kutofautiana kuhusu masuala madogo madogo ya Sheriah.

Kwa kuwa ukweli hutokana na uchunguzi/utafiti basi hakika katika mtiririko wa makala haya tumejaribu kuliweka swala hili juu ya meza ya uchunguzi/utafiti, kwani huenda ikawa ndiyo njia ya kuunganisha mtazamo na kusogeza hatua katika uwanja huu, kwani tofauti iliyopo si katika asili na misingi ya dini hata ipelekee kuwa na uadui na chuki, bali tofauti iliyopo ni kuhusu riwaya (za kubuni) zilizonasibishwa na Mtume saww, nalo ni jambo dogo ukilinganisha na mambo mengi tunayoafikiana kati ya madhehebu za Kiislamu.

Na muongozo wetu katika njia hii ni Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

"Na Shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu nyote wala msifarakane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu, mlipokuwa maadui na akaziunganisha nyoyo zenu kwa neema zake mkawa ndugu." 3:103.

واعتصموا بحبل الله جميعا ولا تفرقوا واذكروا نعمت الله عليكم إذ كنتم أعدآء فألف بين قلوبكم فأصبحتم بنعمته إخوانا

Fuatana nami Sehemu ya pili kuchunguza kuhusu kufunga safarini ni wajibu au ni hiari kwa mujibu wa Qur-ani Tukufu na hadithi Sahihi.

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini