Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

HISTORIYA YA IMAMU HUSSEIN (A.S) 12

0 Voti 00.0 / 5

IMAMU HUSSEIN A.S

Sehemu ya kumi na mbili

Jihadi ya Imamu Hussein bin Aliy a.s

HUSSEIN a.s ATAFUTA MAJI HUKO SHARAF

Alitembea kutoka Batnul Aqabah hadi alipoteremka Sehemu ya Sharaf, na wakati wa kupambazuka aliamuru vijana wake watafute maji kwa wingi, na katikati ya mchana alimsikia mwanaume mmoja miongoni mwa wafuasi wake akisema:  "Mungu mkuu الله اكبر" . Hussein a.s akasema: "Kwa nini unasema الله اكبر Mungu mkuu?" Akasema: "Nimeona mitende." Waliokuwa pamoja naye wakapinga kuwepo kwa mitende Sehemu hiyo, lakini hizo ni ncha za mikuki na masikio ya farasi,  Hussein a.s akasema na mimi naona hivyo, kisha akawauliza mahala watakapojihifadhi. Wakasema hii hapa Dhuul Hasim kushoto kwako nayo ni kama ulivyotaka, Hussein akawawahi na akapiga hema lake.

Aliwatokea Hurr Bin Yazid Riyahi pamoja na askari elfu moja 1000 aliowatuma Ibn Ziyad kumzuia Imamu Hussein a.s asirejee Madina popote atakapomkuta au amlete Kufah. Imamu Hussein a.s alipowaona watu jinsi walivyo na kiu akawaamuru wafuasi wake wawanyweshe maji wao na farasi zao, wakanyweshwa wote wao na farasi zao, Ally bin Taam Al Muharibiy alikuwa pamoja na Hurr, alikuja akiwa wa mwisho huku akiwa amepatwa na kiu kali sana, Hussein a.s akamwambia: "Muinamishe ar Rawayah, naye ni Ngamia kwa lahaja ya watu wa Hijaz, lakini hakufahamu makusudio yake, akamwambia Muinamishe Ngamia, na alipotaka kunywa maji yakawa yamemwagika kwenye kiriba, Imamu Hussein as akamwambia inamisha kiriba, akawa hajui la kufanya kutokana na kiu kali, akasimama yeye mwenyewe a.s akamshikilia kiriba mpaka akanywa na kukata kiu, na akamnywesha farasi wake.

Kisha Hussein as akawakaribisha akamshukuru Mwenyezi Mungu na kumhimidi, akasema: "Hakika ni udhuru kwa Mwenyezi Mungu na kwenu, hakika mimi sikuwajia mpaka ziliponijia barua zenu, na zimenifikia kupitia wajumbe wenu kwamba njoo kwetu kwani sisi hatuna Kiongozi na huenda Mwenyezi Mungu atatukusanya kwako katika uongofu. Kama mko hivyo basi nimeshawajia na nipeni yanayonipa matumaini miongoni mwa ahadi zenu. Na kama mnachukia kuja kwangu nitaondoka kwenu kwenda Sehemu ambayo nimetokea." Wote wakanyamaza kimya.

Al Hajjaj Bin Masruq Al ja'fiy akaadhini kwa ajili ya swala ya Adhuhuri, Hussein as akamwambia Hurr: "Utawasalisha wafuasi wako?"" Akasema: "Hapana bali wote tutaswali kwa swala yako." Hussein as akawaswalisha na baada ya kumaliza swala akawaelekea, akamshukuru Mwenyezi Mungu na kumhimidi na kumtakia amani Nabii Muhammad s.a.w.w na akasema:

               Enyi Watu hakika nyinyi kama mtamuogopa Mwenyezi Mungu na kujua haki ya watu wake, Itakuwa inamridhisha Mwenyezi Mungu. Na sisi Ahlubaiti wa Muhammad ni bora zaidi katika uongozi wa jambo hili kuliko wale wanaodai lisilokuwa lao, wale wenye kwenda mwendo wa ujeuri na uadui. Na kama mtakataa isipokuwa kutuchukia sisi na kuchukua haki yetu, na uamuzi wenu hivi sasa ukawa ni kinyume na zilivyonijia barua zenu, basi nitaondoka kwenu."

Hurr akasema sijui ni barua zipi unazozisema: Hussein as akamuamuru Uqbah Bin Sam'an akatoa kapu mbili zilizojaa barua. Hurr akasema: "Mimi sio miongoni mwa hawa na mimi nimeamriwa nisikuache nitakapokukuta mpaka nikupeleke Kufah kwa Ibn Ziyad. "Hussein as akasema: "Mauti yako karibu mno kwako kuliko hilo." Akaamuru wafuasi wake kupanda farasi, wanawake wakapanda Ngamia. Wakawazingira kuwazuia wasiondoke kuelekea Madina, ndipo Hussein as akamwambia Hurr. "Mama yako ana hasara, unataka nini kwetu? "

Hurr akasema: "Kama mwingine asiyekuwa wewe miongoni mwa waaraba angeniambia haya, naye yuko katika hali hii, nisingeacha kumsema mama yake kwa ubaya wowote ule, Wallaahi sina njia ya mimi kumtaja mama yako isipokuwa kwa wema kadiri tuwezavyo, lakini fuata njia ambayo haikupeleki Kufah wala kukurejesha Madina hadi nimwandikie barua Ibn Ziyad, huenda Mwenyezi Mungu ataniruzuku afya na asinipe mtihani wowote katika jambo lako." Kisha akamwambia mimi nashuhudia kuwa kama utapigana bila shaka utauliwa. Hussein as akasema: "Utanitishia Mauti, je ni rahisi kwenu kuzungumza kuwa utaniuwa? Nitasema kama alivyosema ndugu wa Ausi kwa mtoto wa Ami yake pindi alipotaka kumnusuru Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w

                "Nitakwenda Mauti sio aibu kwa kijana

                anaponuia haki na akapigana jihadi hali ni Mwislamu.

              Na akashirikiana na wanaume wema kwa nafsi yake,

              akaaga kwa kuuliwa na akawahalifu waovu.

    Kama nitaishi sintajuta na nikifa sintaona uchungu, ni udhalili tosha, kuishi kwa kukandamizwa."

      Hurr aliposikia haya kutoka kwake akasogea mbali naye, basi Hussein as akawa anakwenda na wafuasi wake katika upande mmoja, na Hurr na waliokuwa pamoja naye wanakwenda katika upande mwingine.

          Na katika Sehemu ya Al Baidhatu Hussein as aliwahutubia wafuasi wa Hurr, akasema baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumhimidi:

                 "Enyi Watu, hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w.  alisema:" "atakaye mwona Kiongozi muovu mwenye kuhalalisha haramu ya Mwenyezi Mungu, mwenye kutengua ahadi yake, mwenye kukhalifu Sunnah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w , anawafanyia waja wa Mwenyezi Mungu Uovu na uadui, na hakumkataza kwa kitendo wala kwa kauli, ni haki kwa Mwenyezi Mungu kumuingiza motoni."

Ee na hakika hawa wamejilazimisha kumtii shetani na wameacha kumtii Mwenyezi Mungu, wamedhihirisha ufisadi, wamevuka mipaka wamepora mali, wamehalalisha haramu ya Mwenyezi Mungu na wakaharamisha halali yake, na mimi nina haki zaidi kuliko aliyebadilisha. Na zimeshanijia barua zenu na nimekuja kupitia wajumbe wenu na kiapo cha utii wenu, kwamba nyinyi hamtanidhalilisha wala kunifedhehesha, basi kama mtatimiza kiapo cha utii wenu mtapata uongofu wenu.

"Mimi ni Hussein Bin Ally na mtoto wa Fatimah binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w , nafsi yangu iko pamoja na nafsi zenu, watu wangu wako pamoja na watu wenu, na mnacho kwangu kigezo na kama hamtafanya basi mtakuwa mmetengua ahadi yenu, na mmevua kiapo cha utii wenu katika shingo zenu, hakika hamuwezi mkakataa, kwani mmekwishafanya hayo kwa baba yangu na ndugu yangu na kwa mtoto wa Ami yangu Muslim bin Aqili a.s . Amedanganyika aliyewadanganya, utu wenu mmeukosa na nafasi zenu mmezipoteza, na mwenye kutengua basi hakika anatengua kwa ajili ya nafsi yake, Mwenyezi Mungu atawatosheleza, na amani na rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yenu

والسلام عليكم ورحمه الله وبركاته

       Na katika Sehemu ya ar Rahiymah alikutana na mwanaume kutoka katika watu wa Kufah anayeitwa Abu Haram, akasema: "Ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu ni kipi ambacho kimekutoa katika haram ya babu yako? " Akasema: "Ewe Abu haram! Hakika Bani Umayyah wametukana utu wangu nikasubiri, wamechukua mali yangu nikasubiri, wakataka damu yangu nikakimbia, na Wallaahi wataniuwa na hapo Mwenyezi atawaletea udhalili wa jumla na upanga wenye kukata, na atawatawalishia atakaye wadhalilisha mpaka wawe dhalili kuliko kaumu ya Sabaa(ipo Yemen), pale alipowatawala mwanamke(Balkaysi) ambaye alikuwa anahukumu katika mali zao na damu zao."

Fuatana nami sehemu ya kumi na tatu historia ya Maasum Hussein a.s

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini