Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

MAISHA YA BIBI FATIMA BAADA YA MTUME (S.A.W.W)1

0 Voti 00.0 / 5

MAISHA YA BIBI FATIMA BAADA YA MTUME (S.A.W.W) KUFARIKI

Sehemu ya Kwanza

FATIMA KAUTHAR

Ewe fatima, ewe menye kushangaza zama.Ewe dalili ya mwenyezimungu.Ewe moyo wa mohammad ambae umefunikwa chini ya kisaa.

Ewe kauthar mwenye huruma kwa mayatima,mateka (wafungwa) na masikini,na kwa ajili yako ikateremka kuoka mbinguni sura kamili ya Al insaan.Siku ya kiama malaika atanadi ((fumbeni macho na inamisheni vichwa chini mpaka fatima avuke siraat (njia).Hii ni katika khususia (sifa)zak pekee.

Ewe ua la moyo wa mtume mohammad, wakati wote uko hai na wakati wote ni wa milele ewe shahiid.

FATIMA (A.S) KABLA YA KUOLEWA.

Fatima kabla ya kuolewa alikuwa ni mwenye ku jitihada na mwenye kujituma katika kuutumikia uislaam.Kupewa utume baba yake kulimfanya awe na furaha na uchangamfu katika moyo wake,na kulimfanya awe na hisia za uhakika na utukufu,hisia ambazo zilimpelekea kufanya jitihada za kupambana na jamii ya waabudu masanam,kuondoa ujahili na ujinga.

Fatima ni mtu ambae kutokana na ukubwa wa kima anawia ,ukamilifu wa kimaumbile,na kutokana na sifa hizi aliweza kuupa uchangamfu moyo wa baba yake.Mtime (S.A.W.W.)kabla ya kisa cha kauthar cha Fatima (A.S)alifarijika kutokana na kizazi chake ambacho kilitokana na mama mwenye mapendo yaani Bibi Khadija (A.S)ambae ni mama wa Fatima,na sifa hii aliyonayo Bibi Khadija ndio iliyo muonyesha na kumfanya aonekane kuwa ni sawa na chombo chenye ua ndani yake na ua hilo ni mwana Fatima (A.S),na vilevile sifa moja wapo ya Bibi huyu ni kuwa mama wa Fatima (A.S).

HARUSI YA FATIMA

Harusi yake iliandaliwa mbinguni ,aliolewa na mtu ambae jina lake linatajwa mbinguni,na kuwepo kwake Fatima ni nguzo yake,na vitu vyote baada ya kutajwa kwa jina lake vina pata utulivu,nae si mwingine bali ni sayyidina Ally (A.S)na asingelikuwa yeye katika ulimwengu huu basi asinge patikana wa kumuoa Fatima(A.S),kwani Ally(A.S)ni mfan wa Fatima (A.S)

Katika cheo cha kimaanawiya,kwa hivyo basi tunaikuta ndoa ya Bibi Fatima

(A.S)na Imam Ally (A.S)ni nuru juu ya nuru.

Fatima (A.S) ni moyo wa mtime (S.A.W.W)na kwa ajili hiyo haikuwa n vigumu kwake kuanza maisha ya zuhud (kuipa nyongo dunia),tuki zingatia

Kwamba Fatima (A.S) na Imam Ally (A.S)waliwahi kuishi pamoja

katika nyumba ya mtume mohammad (S.A.W.W),kwa hivyo anastahiki

Fatima (A.S) au Imam Ally (A.S) kuwa na maisha ya zuhud,tabia njema n.k.kwani waliweza kuya chyma hayo kwenye nyumba hiyo ya utume.

Harusi ya Bibi Fatima ilikuwa ni yenye mafunzo makubwa na mazuri kwa waislaam na waumini ,kwani tunakuta kwa mfano vitu vilivyo andaliwa kwa matumizi ya nyumbani vilikuwa ni Godro,sufuria,n.k,vitu ambavyo ni vya kawaida na vitoavyo picha kamili ya kuwa Harusi si lazima ifanyike kifakhari

Bali jambo la muhimu ni kutimiza kile kinacho hitajiwa na Mwenyezi Mungu kutoka kwa waja wake yaani ndoa.

 Fuatana nami katika makala ijayo kuhusu Maisha ya Mtukufu Huyu Baada ya Mtume (s.a.w.w) .

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini