Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

MAISHA YA BIBI FATIMA BAADA YA MTUME (S.A.W.W) 4

0 Voti 00.0 / 5

MAISHA YA BIBI FATIMA BAADA YA MTUME(S.A.W.W) KUFARIKI

Sehemu ya Nne

KISA CHA SHAHADA.

Tukio liumizalo ni tukio la watu watatu kati ya muhajirina ambao ni Omar,Abubakar,na Abu ubaida pele walipoelekea katika thaqifa ya bani aida ili kuwabana maanswari na kushughulikia suala la ukhalifa baada ya Mtume,ili ajivike cheo mmoja baada ya mwingine.

Omar alimtuma mtu akamtafute Abubakar na Abubakar alikuwa nyumbani kwa Mtume na baadhi ya muhajirina na ma nswari na Imam Ally watu ambao walimpa kiapo cha utii katika Ghadir khum.Twabari anasema omar alikuja nyumbani kwa mtume kumtafuta Abubakar,Abubakar alikuwepo na Ally alikuwa akishughulikia maiti ya mtume,Omar alimuita Abubakar naAbubakr akasema nina shughuli.

Omar akmtumia ujumbe kwa mara nyingine na kumjulisha ya kuwa kuna mmbo yametokea ni lazima uwepo.Abubakar akatoka na Omar akmwambia je unafahamu ya kuwa answar wamekusanyika katika thaqifa bani saida ili kumchagua wamchague saadi bin ubaada kuwa khalifa?basi wakashika njia kuelekea huko na walipo kuwa njiani walikutana na Abu ubaida na wote watatu wakaelekea katika Thaqifa.

Mambo yote hayo yalifnyika kwa siri na kwa uficho,billa kutoa habari kwa watu,hata kwa wakubwa wa rai na wenye vyeo,na wakati huo wakasema ya kuwa hayo yalikuwa ni makubaliano ya ummaau watu woote,je nikweli umma wa kiisalam ulishirikishwa?Enyi watu wenye inswafu(uadilifu) ij maa ya umma iko wapi?historia kamwe haituonyeshi ispokuwa watu watatu tu katika muhajirina.basi yakafanyika yaliyo fanyika na Abubakar akawa khalifa.

Abubakar akchukua uamuzi wa kwenda kwa Ally ili kuchukua kiapo cha utii (Baia) Abubakar na Omar walijua kwamba Ally hawezi kuwapa kiapo cha utii kwa sababu ndie aliestahili kuwa khalifa wa Mtume baada ya kufariki Mtume.

Lbda watu watajiuliza vipi Abubakar alithubutu kuchukua kiapo cha utii kutoka kwa Ally?wakati wanafahamu ya kuwa Ally ni shujaa na asie ogopa?

Jibu ni kuwa:Wo walijua ya kuwa ni moyo (kipenzi)cha mtume Mohammad (S.A.W.W).na vilevile walijua ya kuwa masuala ya utume,na masuala ya kiislam (Dini)na ulinzi aliyafikiria na kuyajli sana,na ilikuwa ni kawaida kwake na watu wake kujitolea muhnga katika Dini,haikuwa taabu kwake kuto jli ushujaa wake na manufaa yake kwa ajili ya Dini.kwake ilikuwa ni bora Dini isimame na mafnikio yake binafsi yakosekane. kwa hivyo basi kutokana na msimamo huu si ajabu Ally kutoa kiapo cha utii kwa Abubakar.

Ibnu kutaiba anasema katika kitabu chake:(Al imama was siyaasa)

(( Abuubakar aliwatuma watu wakamlete Ally ili aje kumpa kiapo cha utii.Na omar akwafuata watu wote.Omar alifika katyika mlango wa Ally na kuwatawanya watu na wote wakatoka nje, na aka amrisha uwashwe moto na akasema:(Nina apa kwa mila ambae moyo wa Omar upo mikononi mwake tokeni nje laasivyo ninaichioma nyumba motona kila alie ndani. Watu wakamwambia Ewe baba wa Hafswa,Fatima yuko ndani ya nyumba, Omar akasema:Hata kama akiwepo ndani Fatima.

Baada ya mazungumzo haya wote walitoka nje na kumpa kiapo ispokuwa Ally.

Na Omar akawa na yakini kwamba Ally amesema:Nina apa sinto toka nyumbani mpak nimalize kuandika Qur an.

Fatima alisimama nyuma ya mlango na kusema:sija ona ujaji wa watu wabaya kama ujaji wenu (yaani sijaona watu wabaya kama nyinyi)mme litelekeza jeneza la Mtume mkaenda kufanya kazi zenu na wala hamkuwa na fikra na sisi na pia hamkutupa haki zetu. Omar akenda kwa Abubakar na kumwambia je watu ambao hawaja kupa kiapo cha utii huchukui kiapo hicho kutoka kwao? Abubakar akamtuma mtumwa wake qunfush na kumwambia nenda ukamlete Ally.

Qunfudh alikwenda kwa Allyna Ally aka muuliza unataka nini?Qunfuhd akajibu:unaitwa na khalifa wa Mtume,Ally akasema:ajabu,inashangaza, kwa haraka wameanza kuzua uongo juu ya Mtume.

Qunfudh akarudi na kumueleza Abubakar kuhusiana na kisa hicho,Abubakar akalia.

Omar akasema usimpe muda mtu huyu ambae hataki kukupa kiapo cha utii.

Kwa mara nyingine Abubakar akamtuma mtumwa wake na kumwambia:kamwambie ya kuwa unaitwa na kiongozi wa waumini ili ukampe kiapo cha utii (Baia)Ally alinyanyua sauti yake na kusema:((Wanadai mdai ambayo hawastahili kuyadi))

Qunfudh akarudi na kufikisha ujumbe .Abubakar akalia.omar baada ya kusikia hivo alinyanyuka pamoja na badhi ya watu na kwenda hadi nyumbani kwa Fatima na kugonga mlango.Fatima baada ya kusikia sauti akapaza sautina kusema:Ewe baba ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu baada yako tuliwafanya nini watoto wa khatwab (Omar)na mtoto wa Quhafa (Abubakar )watu kisikia kilio cha Fatima wakarudi.

Muandishi mwisho aneleza kuwa Omar alimueleza Abubakar njoo twende kwa Fatima kwani sisi tume muudhi,wote wawili wakaelekea kwa Fatima na wakaomba ruhusa ya kuingia,Fatima hakuwaruhusu,bali Ally ndie aliekuja kwa Fatima kuwaombea ruhusa ya kuingia kwa Fatima,na walipofika hadhat zahraa aliridi ukutani na walimsalimia lakini zahraa hakujibu salam yao.Abubakar akasema:Ewe tabasamu la mtume watu wa Mtume (Falia yake)kwangu niwatukufu zaidi kuliko familia yangu,na ninakupenda wewe zaidi kilik mwanangu Aisha na nilipenda kwamba siku aliyo kufa Mtume nami nife baada yake na nisibakie nikiwa hai.Nina jua kwamba wewe unanijua vizuri sana mimi na nina jua utukufu wako na cheo chako,sasa ni vipi nimechukua haki yako na urithi wako ulio achwa kutoka kwa Mtume? Hdhraat zahraa akasema je ikiwa nitawambia hadithi kutoka kwa mtume mtaifanyia kazi?wakasma ndio.

Fatima akasema:Nina apa kwa Mwenyezi Mungu je nyinyi hamkusikia kutoka kwa mtume pale alipo sema,Radhi za fatima ndi radhi zangu,na ghadhabu za Fatima ndio ghadhabu zangu basi kila mwenye kumpenda mwanangu Fatima amenipenda mimi na kila mwenye kumridhisha Fatima ameniridhisha mimi na kila mwenye kumuudhi Fatima ameniudhi mimi?

Wakasema:Ndio tuliisikia hadithi hii kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Fatima akasma:Mwenyezi Mungu na malaika wanashuhudia kuwa nyinyi mmeniudhi mimi na hamkuniridhisha na wakati wowote nitakapo muona Mtume nita washitakia nyie juu yangu.Abubakar akasema:Ewe Fatima mimi baada ya kuku udhi wewe na yeye (Mtume)ninajuta kwa Mwenyezi Mungu na hapo Abubakar ak anza kulia hadi kukaribia kupasuka .

Fatima akasema:Nina apa kwa Mwenyezi Mungu kila baada ya sala nitakuwa nikikulaani wewe.Abubakar haki akilia akatoka nyumbani kwa Fatima na watu akakusanyika pembezoni mwake na aliwageukia na kuwambia:Kila mmoja wenu akalale usiku huu na mkewe hadi asubuhi,na afurahi na familia yake na mimi niacheni katika hali yangu hii,sitaki tena viapo vyenu na kiapo changu ninakichukua mwenyewe.

Watu wakamwambia:Ewe khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu haiwzekani kuachana na maswala haya,wewe ni mjuzi zaidi kuushinda sisi,ikiwa utafanya hivi Dini ya Mwenyezi Mungu itateketea.

Sikufanya hivi ispokuwa ni baada ya kuona na kusikia kile kilichoo kwa Fatima (A.S).

Imam Ally (A.S) wakati wa uhai wa Fatma hakutoa kiapo cha utii ispokuwa baada ya kifo cha Fatima.Na alitoa kiapo hicho kwa hekima na kw sababu maalumna na wala haikuwa ni kwa kuridhia ya kuwa Abubakar ni kiongozi. Fatima baada ya kifo cha baba yake hakuishi zaidi ya siku sabini na tano.

Fuatana nami katika makala ijayo kuhusu Maisha ya Mtukufu Huyu Baada ya Mtume (s.a.w.w) .

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini