Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

MAMZAZI YA IMAMU MAHDY (A.J) 1

0 Voti 00.0 / 5

Kuzaliwà KWA IMAMU MAHDY 15 SHAABANI 255 HIJIRIA

Imamu MÀHDI a.s alizaliwa SAMARRA nchini Iraq na alighibu kupitia ghorofa ya chini iliyoungana na jengo la maziara ya Maimamu wa kumi na kumi na moja. Uwingi wa umati wa Samarra ni Ahlisuna/Sunni (90-95%) ambao wanaamini juu ya uhai wa Imamu MÀHDI a.s kwa sababu MIUJIZA mingi hutokea huko.

Zaidi ya hayo Imamu MÀHDI a.s anapokuja kuzuru makaburi ya baba na babu yake (Maimamu wa kumi na kumi na moja) jiji zima hujaa Nuru. Waarabu wa huko hufurahia kwa msisimko na wanawake hupanda juu maghorofani kufurahia kuja kwa Imamu MÀHDI a.s

Hata katika usiku wa giza, Imamu MÀHDI a.s anapozuru, hilo jiji hung'aa kwa Nuru. Ikiwa mtu yeyote akionyesha kidole au akitoa ufunguo na kuuning'iniza hutoa mwanga kama mshumaa. Hata baada ya MIUJIZA mingi kutokea SAMARRA, hao waarabu hawaachi kuwasumbua Mashia wanaokuja kwa ajili ya ziara.

Mwenyezi Mungu hukamilisha mathibitisho yake. Miujiza mingi na dalili nyingi hutokea kuthibitisha ukweli wa UWEPO wa Imamu MÀHDI a.s na kuwa yuko hai ili imani ya waumini iimarike na uwe uthibitisho kwa wabishi. Hata hivyo, bado kuna maswali machache yanayoulizwa na majibu yake ni kama yafuatayo:

Swali 1: Ikiwa Imamu MÀHDI a.s atajitokeza sasa, bila shaka uovu na ukandamizaji na kufuru vitakoma duniani, Amani, usalama na utii kwa Mwenyezi Mungu utadhihirika, na waumini hawatakuwa na shaka yoyote ?

Jibu: Dunia hii ni pahala pa majaribio kwa binadamu. Mwenyezi Mungu amekamilisha mathibitisho yake juu ya kila mtu. Kujitokezà kwa Imamu MÀHDI a.s hutegemea amri ya Mwenyezi Mungu. Mtu yeyote hana haki ya kuharakisha au kudadisidadisi. Licha ya hayo, hata baada ya kuja kwa Imamu MÀHDI a.s waliopotoshwa watapotoka tu.

Wengi walimuona Mtume s.a.w.w na Maimamu wetu, kushuhudia miujiza na kusikia maagizo yao, lakini walipotoshwa kwa tamaa ya dunia na wakabakia bila Imani hata waliweza kuwasaidia madhalimu ( Bani Umayyah na Bani Abbas) na kusababisha upinzani na uadui dhidi ya Maimamu wetu na hatimaye kuwaua. Kwa hivyo, ni jambo dhahiri kwamba Mwenyezi Mungu hutenda kila jambo kwa kupenda yeye Mwenyewe.

Swali 2: Waislamu wengi huishi katika hali ya vitisho kutoka kwa maadui wao na Uislamu, hudharauliwa na kuteswa hata kuuwawa. Huomba msaada kutoka kwa Imamu MÀHDI a.s lakini matatizo yao hubaki pale pale. Kwa hiyo shaka na wasiwasi huingia moyoni mwao ambalo siyo jambo jema.

Jibu: Siku moja mwana mmoja wa mama mmoja akawa mgonjwa mahututi sana na hapakuwa na tamaa yoyote ya huyo mwana kupona.

Huyo mama alisema kwamba ikiwa Mwenyezi Mungu yupo naye ndiye Mwenye kila uwezo na Mwenye Rehema bila shaka huyu mwana atapona tu au la sivyo Imani yake juu ya Mwenyezi Mungu haina maana. Haya mtoto akafariki. Je, uwezo wa Mwenyezi Mungu na rehema ya Mwenyezi Mungu hubatilika kwa hayo ?

Ikiwa huyo mtu anayeomba msaada kutoka kwa Imamu MÀHDI a.s ni mkandamizaji na asiye na imani thabiti na haswali au kutenda maovu mengine basi hastahili msaada wowote. Kwa hiyo, huyo mtu akipata au asipate msaada haitaathiri ukweli wa UWEPO wa Imamu MÀHDI a.s. Haina umuhim wowote kwa Imamu a.s ikiwa mtu anaamini Uimam au dalili, alama, aya za Qur'an na hadithi za kuthibitisha Uimam wa Imamu MÀHDI a.s. Kuukubali Uimam wake humletea manufaa Muumini Mwenyewe na kwa ajili ya wokovu wake binafsi. Katika jambo la dini hakuna mtu anayelazimishwa.

Baada ya Mtume s.a.w.w, Mwenyezi Mungu ameteua warithi kumi na moja, moja baada ya moja, huku duniani kwa ajili ya mwongozo wa binadamu na wote wameuliwa kwa upanga au kwa sumu na madhalimu kama Muawiyah, Yazeed, watawala wa Bani Umayyah na Bani Abbas.

Zaidi ya hayo, hao Maimamu walikuwa wanaonekana na kuishi pamoja na watu na vile vile kuonyesha miujiza mingi. Wao (Maimamu) wameongoza waislamu, wachache tu waliwaamini na wengi wao (Waislamu ) wakawaacha hao Maimamu a.s. Hata kama huyo Imamu wa kumi na mbili (MÀHDI a.s) angekuwa anaonekana angalikabiliwa na mambo hayo hayo. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu amemhifadhi kwa muda maalum.

Mtukufu Mtume s.a.w.w Amesema: "Katika siku za mwisho za dunia watu watakuwa na sura za binadamu kwa maumbile tu watakuwa waovu moyoni, wapendao kumwaga damu, wakatili walioghariki katika maasi na kugeuza kilichoharamishwa kukifanya ni halali na kilichohalalishwa kukifanya haram. Waumini watafikiriwa ni wadhoofu na siyo wàaminifu, lakini waovu na wasiokuwa na dini kufikiriwa kuwa ni watu wema. Hakuna mtu yeyote atakayetaka kushirikiana na wenzie katika kutenda mema. Nyakati hizo zitakabiliwa na njaa, maafa na watawala dhalimu.

Rejea: Sahihi Muslim

Mtukufu Mtume akaongezea kusema: Katika siku za mwisho wa dunia mali itaabudiwa ( Mwenyezi Mungu atakumbukwa wakati wa njaa na shida) watu watatukuza mno wanawake, utajiri ndio utakuwa kipimo cha heshima na utukufu wa dini ( Imani) itakuwa ni wa jina tu. Watu wataukubali Uislamu kwa maneno tu. Qur'an itasomwa kwa wakati maalum tu lakini haitafuatwa kwa vitendo. Misikiti itajaa wafanya ibada lakini nyoyo zao zitakuwa zimejaa chuki, bugudha na Husuda kwa wenzie. Wengi wa wanazuoni watakuwa waovu mno na wenye tamaa ya utajiri duniani. Nyakati hizo zitakabiliwa na njaa, maafa na ukandamizaji.

Rejea Sahihi Muslim.

Fuatana nami sehemu ya kumi na nane historia ya Imamu MÀHDI a.s

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini