IBADA YA MASANAMU

BSMILAHI AR-RAHMANI AR-RAHIIMI

IBADA YA MASANAMU

Kwa jina la Allah, Mwingi wa rehema, mwenye kurehemu Ibada ya masanamu Miongoni mwa maajabu ya dunia, eti mtu atengeneza sanamu kutokana na jiwe, au chuma, au shaba, au kitu kingine chochote na kisha alielekea sanamu hilo kuliabudu, kuomba dua na kuwa muwakilishi (wa mambo yake) - akilitolea dhabihu na kujikurubisha kwalo kwa kila namna ambayo kiumbe hujikurubisha kwa Muumba wake. Na ajabu ni kwamba, kwenye jamii (hiyo) wapo washairi, wasomi na wengineo. Kwa hakika akili haiwezi kuamini mfumo huu wa mawazo, pamoja na upungufu huu ambao binadamu huupupia. Na pengine mastaajbu kutokana na hayo yataondoka iwapo tu utajua kwamba, zama hizi wapo mamilioni ya Wahindi wanaabudu ngo'mbe - kwa kujipaka mkojo wake na kutabaruku (kutaka baraka) kwa kinyesi chake - wakati huu wa elimu na maendeleo (ustaarabu) na zama za watu kwenda mwezini (space ages).

Na mvuto huu unaotokana na upungufu wa binadamu wa tangu kale kwenye ibada ya masanamu, na huu wa leo - kama tunavyoshuhudia kwenye ibada ya ngo'mbe - sio kingine isipokuwa ni nguvu ya kishetani! Je, humsikii Mtukufu (Mwenyezi Mungu) Aliyetakasika Utukufu wake: "Akasema: (Ibilisi) naapa kwa haki ya utukufu wako, bila shaka nitawapoteza wote. Isipokuwa wale waja wako miongoni mwao waliosafishwa." (38:83)

Na utukufu ni wake wa mtakasifu anasimulia neno lake: "Akasema (Iblisi): Kwa kuwa umenihukumia upotovu (kupotea), nitawakalia kwenye njia yako iliyonyoka, kisha nitawatokea kwa mbele yao, na kwa nyuma yao, na kuumeni kwao na kushotoni kwao. Na hutawaona wengi wao wakushukuru." (7:18) Na (pia) anasema Mtukufu Aliyetakasika: "Na bila shaka Ibilisi alisadikisha dhana yake juu yao nao wakamfuata isipokuwa kundi la waaminio." (34:20) Na la ajabu zaidi kutokana na hili na lile, ni unywaji wa pombe! Kwani dini pamoja na sharia zote zimekubaliana juu ya uharamu wake. Tiba za zamani na za sasa, zinataja maradhi mengi yanayotokana na unywaji wake; kwamba daima mnywaji wake humpelekea kupatwa na maradhi ya moyo, kukuwaa kwa mishipa ya fahamu, moyo kwenda mbio na.... Na nyongeza ya hayo ni ukosefu wa hamu ya chakula, kupotea bure kwa mali na akili pia. Lakini pamoja na hayo, binadamu bado wanaendelea kuinywa tu - wakiwemo Waislamu. Amesema Imam Abu Jaafar - Baqir (a.s.): "Mnywaji pombe ni sawa na muabudia sanamu."1

Kwani wote hawo wawili (muabudia sanamu na mnywaji pombe) wamepoteza kipawa kitukufu zaidi cha Mwenyezi Mungu Mtukufu alichopewa; nacho ni 'akili' akawa anapapasa kwenye ujinga (giza) pamoja na upungufu! Kwa hakika miongoni mwa matatizo makubwa yaliyowakabili Mitume (a.s.) ni tatizo la ibada za masanamu. Je, humsikii Ibrahim (a.s.) - kipenzi (cha Mwenyezi Mungu) asemavyo kwenye dua yake?: "Na niepushe mimi pamoja na wanangu tusiyaabudie masanamu, Mola wangu, hakika wao (masanamu) wamewapoteza wengi miongoni mwa watu, mwenye kunifuata mimi, basi huyo yu miongoni mwangu, na mwenye kuniasi mimi hakika wewe u Mwingi wa kusamehe, Mwenye rehema." (14:36)

Na Nabii Ilyas (a.s.) anawakemea watu wake: "Mnamwabudia Baali? na mnamwacha aliye mbora wa waumbaji?" (37:125) Nabii wa Mwenyezi Mungu Saleh (a.s.) naye aliwakabili watu wake kutokana na ibada ya masanamu - kwa karipio kali na thabiti. Kwa yakini alikaa nawo huku akiwa lingania kwenye ibada ya Mwenyezi Mungu S.W.T. zaidi ya miaka mia moja, nao wakawa hawakuzidisha chochote isipokuwa kujitenga na haki. Wakaendelea Waarabu pamoja na wengine miongoni mwa mataifa kwenye ibada ya masanamu hadi ulipokuja uislamu na wakati huo Waarabu walikuwa na masanamu 360 yaliyotundikwa kwenye kuta za Al-Ka'aba tukufu ikiongezwa pamoja na masanamu yao mengine yaliyokuwa nje ya Al-Ka'aba.

Na siku ile ya kuiteka Makkah tukufu, Mtume (saw) alimuamrisha Ali (Amirul Muumini (a.s.)) ayavunja: "Na yametimia maneno ya Mola wako kwa ukweli na uadilifu, hakuna mwenye kuyabadilisha maneno yake, naye ni mwenye kusikia; Mjuzi" (6:115) Muujiza Mkuu Na miongoni mwa upole wa Mwenyezi Mungu S.W.T. kwa binadamu, amewatumia Mitume (a.s.) na akawapa uwezo wa kuonyesha muujiza ili kubainisha ukweli kutokana na uongo, na ili kutoa hoja (dalili) kwa viumbe: "Na Mwenyezi Mungu ni hoja (dalili) ya kutosha."

Na miongoni mwa maajabu ya duniani, eti watu wanamtaka Mtume wao muujiza, kisha awaonyeshe, na pamoja na yote hayo wasiamini! Hata yalimtokea Mtume wetu Muhammad (saw), kwani Makureishi walimtaka auamrishe mwezi mchanga ujigawe sehemu mbili - nusu yake iende upande wa kulia, na sehemu iliyo baki ielekee upande wa kushoto. Mtume (saw) akauashiria, nao ukagawika. Kisha walimtaka yeye auashirie ili uunganike - naye akatekeleza hayo, na pamoja na yote hayo hayakuwazidishia kitu isipokuwa ujeuri. Nao watu wa Nabii Saleh (a.s.) walimtaka Mtume wao muujiza wa kutobolewa (kwa jabali) nao (huo muujiza) eti awatolee kutoka jabalini ngamia jike, mwekundu, mwenye manyonya meupe, asiyefanana na mwingine, na mwenye matege.

Imam Baqir (a.s.) anasema: "Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alimwuliza Jibril (a.s.) namna walivyo angamizwa watu wa Saleh" Akajibu: "Ewe Muhammad, hakika ya Saleh alitumilizwa kwa watu wake akiwa kijana wa miaka kumi na sita, akaishi nao hadi alipofikisha miaka 120 bila ya kumkubali heri, nao walikuwa na masanamu sabini wakiyaabudia kinyume na mwenyezi Mungu Mtukufu. Na alipowaona wako hivyo, akawaambia: Enyi watu, nimetumilizwa kwenu nami ni kiwa wakati huo kijana wa miaka sita, na kwa hakika (sasa) nimefikisha umri wa miaka 120. Sasa nawatoleeni kwenu mambo mawili: Mkipenda niombeni ili nimwombe Mola wangu apate kuwajibu kwa hayo mtakayoomba sasa hivi, na mkipenda nitawauliza Miungu wenu, nao wakinijibu kwa yale nitakuwa nimewatosheleza, nanyi mtakuwa mumenitosheleza.

Wakamwambia: Kwa hakika umefanya insafu (usawa) ewe Saleh. Wakatayarisha siku watakayotoka, nao wakatoka na masanamu yao kwenye migongo yao, kisha wakaleta vyakula pamoja na vinywaji vyao - wakala na kunywa. Walipomaliza, walimwita na kumwambia: Ewe Saleh, uliza. Akamwuliza yule mkubwa wao: Nani jina la hili (yaani sanamu) Wakamjibu: Fulani. Saleh akaliuliza: Ewe fulani, nijibu. Na kamwe halikumjibu. Saleh akauliza: Lina nini halijibu? Wakamwambia: Uliza (sanamu) lingine. Akayataja yote tena kwa majina yao, lakini kamwe hayakumjibu. Wakamwambia: Tuachie, na utuache pamoja na Waungu wetu sasa.

Kisha wakayafuata mabusati yao na kuyakunjua, wakazichukua nguo zao na kuzitia mchanga kisha mchanga huo wakaumwaga juu ya vichwa vyao na kuyaambia masanamu yao: Kama leo hamtamjibu Saleh, basi mtatia fedheha. Kisha wakamwita na kumwambia: Ewe Saleh, yaite. Naye akayaita, nayo kamwe hayakumjibu. Akamwambia: Enyi watu, kwa yakini nusu ya usiku imeishapita, nami siwaoni Waungu wenu wakinijibu, hivyo niulizeni ili nimwombe Mola wangu awajibuni sasa hivi. Wakamteulia miongoni mwao wanaume sabini kati ya wakubwa wao na wenye busara miongoni mwao; wakamwambia: Ewe Saleh, ikiwa Mola wako atatujibu, basi tutakufuata na kukubalia, na watu wote wa kijiji chetu watakuunga mkono. Saleh (a.s.) akawaambia: Niulizeni mpendalo. Wakamwambia: Twende pamoja nasi kwenye jabali lile.

Nalo jabali hilo lilikuwa karibu nao. Saleh akiwa pamoja nao wakaondoka, na mara walipolifikia lile jabali wakamwambia: Ewe Saleh, tuombee kwa Mola wako sasa hivi atutolee kutoka kwenye jabali hili ngamia (jike) mwekundu, mwenye manyoya meupe, asiyefanana na yeyote, na mwenye matege. Saleh akawaambia: Kwa hakika mumeniomba jambo kubwa mno kwangu, na litakuwa jepesi mno kwa Mola wangu Mtukufu. Akamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa hilo, ndipo jabali lile likapasuka mpasuko uliokaribia kuwafanya warukwe na akili zao walipousikia! Kisha jabali lile likatingishika kama mwanamke alipatwa na uchungu wa uzazi kichwa chake (huyo ngamia) mara kikajitokeza tayari mbele yao kutoka kwenye mpasuko (ufa) ule.

Mara tu baada ya (ngamia huyo) kumalizika kujitokeza shingo yake hadi ikajivuta - kisha sehemu yake ya mwili iliyobakia ikajitokeza, na kusimama kwenye ardhi. Walipoona vile wakasema: Ewe Saleh, haraka iliyoje ya aliyokujibu Mola wako! Tuombee kwa Mola wako atutolee ndama (mtoto) wake. Naye akamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu hilo, naye (yule ngamia) akamto (mtoto) akawa anatembea mbele yake. Akawauliza: Enyi watu je kumebakia kitu? Wakamjibu: Hapana, twende sote kwa watu wetu ili tuwafahamishe tuliyoyaona wapate kukuamini. Wakarejea na kamwe hawakutumia wale watu sabini mara tu baada ya kufika huko kwa watu wao - bali watu sitini na wanne kati yao waliritadi (walikanusha tena baada ya kuwa hapo mwanzoni walikiri) huku wakisema: Ni uchawi na uongo! Wakafika kwa wale wengine, na wale sita wakasema kuwa ni haki, na wale wote wakasema kuwa ni uongo na uchawi, nawo wakatawanyika, kisha mmoja wapo kati ya wale sita akajitoa (naye), na akawa ni miongoni mwa wale ambao baadaye walimchinja (ngamia huyo)."2 Kuangamia kwa madhalimu Hufuatiliza Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutumilizia Mitume - amani juu yao - pamoja na dalili (aya), na kutoa hoja za kuwaokoa waja wake, na kuwalingania wao kwenye njia ya ushindi, na hawaharakishii, kwani kamwe hafanyi haraka kwa yale ya kuwaumiza, na Daima huwafanyia majaribio kwa baadhi ya mabaa ili angalau warejee kwenye haki, na ili iwe hiyo balaa ni sehemu ya kinga yao.

Na mara tu muda unapotimia na bila ya kurejea kwenye njia ya haki pamoja na maongozi adili, hapo watastahiki tamshi la adhabu juu yao. Hivyo huwapatilizia kwa kamio la nguvu, la mwenye uwezo, na kuwazuilia uwezo wao wa kimaisha - ikiongezea na wanavyopewa hizaya ya muda mrefu pamoja na unyonge wa daima katika akhera. Kuhiliki kwa kuangamia Jihadhari ewe ndugu yangu; Mwenyezi Mungu akuhifadhi na kukulinda kutokana na maasi, kwani wewe hujui ni wakati gani utakapopatiliziwa kwayo, na kupatwa na mikasa yake. Kwa hakika Qur'an tukufu imetuhadithia visa vya umma ambao Mwenyewe Aliye Takasika aliwakamia kutokana na maasi yao ili wayazingatie hayo. Hivyo mtu mwema ni yule anayepokea (na kukubali) maonyo kwa kuona mfano kwa mwengine, na mkosaji ni yule anayekuwa mfano mbaya kwa watu. Nawe lau utasalimika kuadhibiwa kutokana na maovu yako, kwa hakika huwezi kusalimika kutokana na baadhi yatakatofuatia (miongoni mwa adhabu). Imam Jaafar Sadiq (a.s.) anamwambia Mufadhila bin Omar: "Tahadhari na madhambi, na wahadharishe wafuasi wetu. Na wallahi hayawi kwa mtu eti awe na haraka zaidi kuliko (athari ya) matokeo yake kwenu."

Hakika ya mmoja wenu yatamsibu matatizo kutokana kwa Mtawala (kiongozi), na hayo hayawi isipokuwa ni kutokan na madhambi yake, na kwa hakika yeye atatatizwa na maradhi, na hayo hayawi isipokuwa ni kutokana na madhambi yake, na kwamba yeye riziki yake itazuiliwa (itakuwa ya kumhangaisha), na hayo hayaji isipokuwa ni kwa ajili ya madhambi yake, na kwa hakika atapatishwa taabu wakati wa kufa, na hayo hayawi isipokuwa ni kwa ajili ya madhambi yake."3 Na lau utafikiria kwamba wewe umesalimika kutokana na hayo vile vile, huwezi kusalimika kutokana na moto alioukalifisha Muumbaji wake - jabari kutokana na ghadhabu zake, hivyo kujihadhari ni kujihadhari! Na ole wako usije ukakutwa na hasira za Mola wako Mtukufu Aliyetukuka, na lililo mbele ya macho yako ni (kukumbuka) yale yaliyowapata umma uliopita kutokana na adhabu wa kwanza wao wakiwa watu wa Saleh (a.s.).

Naye Imam Abu Abdillahi - Sadiq (a.s.) anatuhadithia yaliyowapata kutokana adhabu: "Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu Aliyetakasika alimfunulia (wahyi) kwamba: Ewe Saleh, waambie wao kuwa hakika Mwenyezi Mungu amempangia ngamia huyu anywe maji ya kisima chao siku (maalum), nanyi mtakunywa siku yenu. Akawa yule ngamia ilipofika siku yake ya kunywa, hunywa maji siku ile na kisha wao humkama maziwa na akawa habakii - sio mdogo wala mkubwa isipokuwa hunywa maziwa ya ngamia huyo siku hiyo. Unapoingia usiku, asubuhi huyaendea maji yao; nawo wakanywa humo siku hiyo na akawa ngamia huyo hanywi siku hiyo. Wakaendelea kufanya hivyo - kiasi alivyopenda Mwenyezi Mungu, kisha wao wakamfanyia Mwenyezi Mungu jeuri! Wakaendesha wao kwa wao; na kuambiana: "Mchinjeni ngamia huyu ili mustarehe kutokana naye, kwani kamwe haturidhiki eti tuwe na siku maalum ya kunywa, naye (huyo ngamia) awe na siku yake ya kunywa!"

Kisha wakaulizana: "Nani atakayesimamia suala la kumwua, nasi tutampatia kitu akipendacho?" Akawajia mtu mmoja mwekundu, mwenye nywele zenye mchanganyiko wa nyeupe na nyeusi, yu mwana haramu hajulikani baba yake; jina lake aliitwa Qakaar. Alikuwa mwovu wa waovu, na mkatili mkubwa, hivyo wakampatia hicho kitu. Mara tu ngamia yule alipoelekea kwenye maji aliyoyakusudia, alimwacha hadi alipokunywa yale maji aliyoyakusudia, alimwacha hadi alipokunywa yale, akawa sasa anarejea, ndipo alipomzuilia njia yake na kumkata kwa upanga - pigo ambalo halikumdhuru chochote (ngamia yule), ndipo akampiga pigo la pili lililomwua na kumwangusha chini kwa kulalia ubavu wake! Mtoto (ndama) wake akakimbia na kupanda juu yaa jabali huku akilia - mara tatu akiashiria mbiguni. Wakaja watu wa Saleh, na hakubakia yeyote miongoni mwao isipokuwa alishiriki kumpiga ngamia huyo.

Wakagawana nyama yake kati yao, na hakubakia mdogo wala mkubwa isipokuwa alikula nyama hiyo. Saleh alipoona hayo aliwajia na kuwauliza: "Nini kilichowapelekeeni kufanya mliyofanya, je mmemwasi Mola wenu?" Mwenyezi Mungu Mtukufu akampa Wahyi Nabii Saleh (a.s.): "Hakika ya watu wako wamevuka mpaka na kupotoka, wakamwua ngamia niliyewatumia kwao - kama hoja (dalili) juu yao, wala hakuwaletea madhara, kwani walipata manufaa makubwa kutoka kwake, hivyo waambie: "Mimi nitawatumieni adhabu yangu kwa muda wa siku tatu, ikiwa wao watatubia na kurejea, nitawakubali toba yao na kuwazuilia wao (adhabu), la kama ikiwa wao hawatatubia wala kurejea, basi nitawatumia adhabu yangu juu yao siku ya tatu."

Saleh (a.s.) aliwajia na kuwaambia: "Enyi watu, hakika mimi ni Mjumbe wa Mola wenu kwenu nyinyi, naye anawaambieni: Ikiwa nyinyi mtatubia, kurejea, pamoja na kuomba maghufira basi nitawasameheni na kuwakubalieni toba yenu." Alipowaambia hayo, wakawa wakali kuliko walivyokuwa, na waovu zaidi. Wakasema: "Ewe Saleh, tuletee hayo unayotuahidi ikiwa wewe u miongoni mwa wakweli." Akawambia: "Enyi watu, kesho mtaamka hali nyuso zenu zitakuwa rangi ya manjano, siku ya pili zitakuwa rangi nyekundu, na siku ya tatu zitakuwa nyeusi." Ilipofika siku ya kwanza nyuso zao zikawa ni za manjano, wakaendelea wao kwa wao na kuambizana: "Hakika yamekufikeni yale aliyowaambieni Saleh."

Wale wakaidi miongoni mwao wakasema: "Hatutasikiliza maneno ya Saleh, na kamwe hatutayakubali japo yawe ya kutishia!" Ilipofika siku ya pili, nyuso zao zikawa nyekundu, ndipo baadhi yao wakawaendea wenzao na kuwaambia: "Enyi watu, hakika yamekufikeni yale aliyowaaambieni Saleh." Wale waovu kati yao wakasema: "Lau tutaangamia sote, hatutasikia maneno ya Saleh, na wala hatutawaacha waungu wetu ambao walikuwa wakiabudiwa na mchang wetu."

Nawo hawakutubia wala kurejea. Na ilipotomia siku ya tatu, zikawa nyuso zao ni nyeusi. Ndipo baadhi yao wakaendeana na kuambizan kwamba: "Enyi watu, hakika yametimia kwenu yale aliyowaambieni Saleh." Na ilipofika usiku wa manane, Jibril (a.s.) aliwajia na kuwapigia ukelele uliopenya kwenyemasikio yao, ukazipasua nyoyo zao na kuyakata machango yao. Walikuwa katika siku ziletatu tayari wamejikusanya kujifunika - wakijua fika kuwa adhabu itawafika na watu wakafariki mara moja - wadogo kwa wakubwa, na hawakubakia na kondoo wala ngamia, na wala kitu chochote isipokuwa Mwenyezi Mungu alikiangamiza. Wakawa wote maiti majumbani mwao na kwenye sehemu zao za kulalia. Kisha Mwenyezi Mungu akawatumia moto ulioambatana na ukelele toka mbiguni uliowaunguza wote! Na hili ndicho kisa chao4 Kuridhia

Fahamu Mwenyezi Mungu akulinde - kwamba kuridhika na amali (vitendo) - sawa iwe nzuri au mbaya ni kushiriki katika asili yenyewe ya kitendo, na yule mwenye kuridhika kwa amali hiyo hupata ujira (malipo) mazuri iwapo amali hiyo ni ya kuridhisha, na (pia atapata) makosa yake iwapo itakuwa ni yenye kukasirisha. Ni kama kwamba kuridhika na kitendo ni sehemu ya utekelezaji na ukamilifu wake, kwani lau kama mwenye kuridhika angepewa uwezo na kutoa mchango wake kwenye amali, basi angeshiriki. Kwani husikii maneno ya sahaba mtukufu - Jabir bin Abdillahi Al-Ansariy (r.a.) wakati akiwahutubia mashahidi wa Karbala - (a.s.): "Naapa kwa yule aliyempelekea Muhammad kwa haki kuwa ni Nabii, kwa hakika tumewashirikisheni kwa yale ambayo mumeyaingia."

Atiya akamwuliza: "Ewe Jabir, itakuwaje hali sisi bado hatujaingia kwenye uwanja (wa mapambano), na bado hatujapanda mlima, wala hatujapigana kwa upanga na watu tayari wameshatenganishwa vichwa vyao mbali na miili yao, miili yao imekuwa na kiu, na wake zao wamekuwa wajane?" Akamjibu: "Ewe Atiyah, nimesikia kipenzi changu - mjumbe wa Mwenyezi Mungu (saw) akisema: "Mwenye kuwapenda watu (fulani), hufufuliwa pamoja nao, na anayeipenda amali ya watu, atakuwa mshirika wa kazi yao. Na naapa kwa yule aliyemtumilizia Muhammad kwa hakika kuwa ni Mtume - hakika ya nia yangu na nia za Masahaba zangu ziko juu ya yale yaliyowapata Husein (a.s.) pamoja na wafuasi wake." Naye Amirul Muumin Ali (a.s.) kuhusu suala la watu wa Saleh (a.s.) anasema: "Enyi watu, hakika ya watu hujikusanyia ridhaa na machukizo, na kwa hakika alilyemwua ngamia wa Thamuud alikuwa ni mtu mmoja tu, na Mwenyezi Mungu akaieneza adhabu kwa wote kwa sababu waliridhishwa na kitendo hicho."

Mwenyezi Mungu S.W.T. asema: "Wakamchinja (ngamia) na wakawa wenye kujuta." (26:157) Na halikuwa lingine isipokuwa kumezwa na ardhi kwa kuzama; myeyuko wa chuma chenye moto - kwenye ardhi yenye matope. Enyi watu, anayefuata njia ya wazi hupita maji, na anayekaidi hupotea."5

MWISHO