TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA TATU Juzuu 13

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA TATU33%

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA TATU Mwandishi:
: HASANI MWALUPA
Kundi: Qurani tukufu

Juzuu 1 Juzuu 2 Juzuu 3 Juzuu 4 Juzuu 5 Juzuu 6 Juzuu 7 Juzuu 8 Juzuu 12 Juzuu 13 Juzuu 14 Juzuu 15 Juzuu 16 Juzuu 17 Juzuu 18 Juzuu 19 Juzuu 20 Juzuu 21 Juzuu 22 Juzuu 23 Juzuu 24
  • Anza
  • Iliyopita
  • 17 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 14524 / Pakua: 3628
Kiwango Kiwango Kiwango
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA TATU

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA TATU Juzuu 13

Mwandishi:
Swahili

1

2

5

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA TATU

Sura Ya Kumi Na Tatu: Surat Ar-Ra’d

Imeshuka Madina, ina Aya 43

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu

المر تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ وَالَّذِي أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ الْحَقُّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١﴾

1. Alif Laam Raa. Hizo ni Aya za Kitabu. Na uliyoteremshiwa kutoka Mola wako ni haki lakini watu wengi hawaamini.

HIZO NI AYA ZA KITAB

Aya 1

MAANA

Alif Laam Raa.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 1 mwanzo wa Sura Baqara.

Hizo ni Aya za Kitabu.

Yaani Aya za Sura hii ni katika Qur’an Tukufu. Lengo la kutoa habari hii ni kubainisha kuwa sura hii ni haki kwa sababu ni katika Qur’an. Kwa vile Qur’an ni haki basi nayo ni haki. Haya ndiyo makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

Na uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako ni haki.

Hapa linakuja swali : Kuna dalili gani kuwa Qur’an ni haki?

Jibu : utalipata Juz. 1 (2:23-25) Imam Ali(a.s) anasema:“Hakika Qur’an dhahiri yake ni safi na undani wake ni wa kina, maajabu yake hayaishi wala giza haliondoki ila kwayo.”

Lakini watu wengi hawaamini Qur’an wala kauli nyingine ya haki na uadilifu ila yule anayeona heri yake ni heri ya watu na shari yake ni shari yao pia.

Mtu mmoja katika watu wa Mungu aliambiwa kuwa soko limeungua lakini duka lako halikuungua, akasema: Alhamdullilah. Kisha akatanabahi kuwa ameasi kwa kujitakia yeye binafsi heri kuliko watu wengine, akatubia dhambi yake na akaomba msamaha.

Mfano wa watu hawa ni wachache ambao wanawafikiria wengine, ndio aliowakudia Mwenyezi Mungu kwa kusema: ‘Lakini watu wengi hawaamini”.

اللَّـهُ الَّذِي رَفَعَ السَّمَاوَاتِ بِغَيْرِ عَمَدٍ تَرَوْنَهَا ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ كُلٌّ يَجْرِي لِأَجَلٍ مُّسَمًّى يُدَبِّرُ الْأَمْرَ يُفَصِّلُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُم بِلِقَاءِ رَبِّكُمْ تُوقِنُونَ ﴿٢﴾

2. Mwenyezi Mungu ndiye aliyeziinua mbingu bila ya nguzo mnazoziona; kisha akatawala kwenye Arshi na amelitiisha Jua na Mwezi, kila kimoja kinaendelea mpaka muda uliotajwa. Anayapanga mambo Anazipambanua ishara, ili mpate kuwa na yakini ya kukutana na Mola wenu.

وَهُوَ الَّذِي مَدَّ الْأَرْضَ وَجَعَلَ فِيهَا رَوَاسِيَ وَأَنْهَارًا وَمِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ جَعَلَ فِيهَا زَوْجَيْنِ اثْنَيْنِ يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ ﴿٣﴾

3. Na yeye ndiye aliyeitandaza ardhi. Na akaweka humo milima na mito. Na katika kila matunda akafanya humo viwili viwilidume na jike. Huufunika usiku kwa mchana. Hakika katika hayo zimo ishara kwa watu wanaofikiri.

وَفِي الْأَرْضِ قِطَعٌ مُّتَجَاوِرَاتٌ وَجَنَّاتٌ مِّنْ أَعْنَابٍ وَزَرْعٌ وَنَخِيلٌ صِنْوَانٌ وَغَيْرُ صِنْوَانٍ يُسْقَىٰ بِمَاءٍ وَاحِدٍ وَنُفَضِّلُ بَعْضَهَا عَلَىٰ بَعْضٍ فِي الْأُكُلِ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ ﴿٤﴾

4. Na katika ardhi mna vipande vilivyokaribiana. na zipo bustani za mizabibu na mimea mingine na mitende ichipuayo kwenye shina na isiyochipua kwenye shina moja inayonyweshwelezwa maji yale yale Na tunaifanya bora baadhi yake kuliko mingine katika kula. Hakika katika hayo kuna ishara kwa watu wanotia akilini (mambo).

AMEINUA MBINGU BILA YA NGUZO

Aya 2-4

MAANA

Mwenyezi Mungu ndiye aliyeziinua mbingu bila ya nguzo mnazoziona.

Yaani mnaziona hizo mbingu, Maana ni kuwa hakika Mwenyezi Mungu ameziinua mbingu kwa amri yake nazo zimeinuliwa hasa kama mnavyoziona bila ya nguzo.

Katika Mustadrak Nahjul-balagha imeelezwa kuwa Imam Ali(a.s) alizisifu mbingu kwa kusema:“Ameinua mbingu bila ya nguzo – yaani kihalisi na kidhahiri – na akaitandika ardhi hewani bila ya nguzo”.

Kisha akatawala kwenye arshi.

Hili ni fumbo kuwa yeye anamiliki ulimwengu na kupangilia mambo yake kwa elimu yake na hekima yake, kama alivyosema: ‘Anayepanga mambo.’ Jumla hii imekwishapita katika Juz. 8 (7:54) na katika Juz. 11 (10:3).

Na amelitiisha Jua na Mwezi, kila kimoja kinaendelea mpaka muda uliotajwa.

Kwa nidhamu, kama yaonavyo macho yetu na kwa lengo maalum kama zinavyotambua akili zetu.

Jua linapita kwenye falaki yake katika mwaka, na mwezi nao unapita kwenye falaki yake kwa muda wa mwezi mmoja. Vilikuwa hivyo tangu mamilioni ya miaka iliyopita na vitaendelea hivyo mpaka atakapotaka Mwenyezi Mungu.

Hakuna mwaka unaotofautiana na mwingine wala muda unaotofautiana na muda mwingine. Hii ni dalili mkataa ya kuweko mjuzi mwenye hekima. Ama sadfa inabatilishwa na nidhamu na kukaririka mambo.

Anayapanga mambo yote bila ya kubakisha, yakiwemo kulitiisha jua na mwezi, kutuma mitume kuteremsha vitabu n.k.

Anazipambanua ishara, Anabainisha dalili za kupatikana kwake, Kwa nini anafanya hivyo?

Ili mpate kuwa na yakini ya kukutana na Mola wenu.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameumba ulimwengu na akaupanga kwa ukamilifu katika njia zote. Akili iliyosalama inatambua mipangilio hii na kupata dalili kwayo ya kupatikana mzingatiaji mwenye hekima na uweza wake wa kurudisha viumbe.

Kwa sababu mwenye kuweza kuuleta ulimwengu uliokuwa hauko na akaupangilia pamoja na vilivyomo ndani yake, zikiwemo nyota na sayari nk, kwa mpangilio wa kiuhakika, basi bila shaka atakuwa na uwezo zaidi wa kuukusanya pamoja baada ya kutawanyika.

Ukithibiti kwa akili uwezo wa kuurudisha, na mkweli mwaminifu akautolea habari kwa wahyi, basi kutokea kwake ni kwa lazima.

Baada Mwenyezi Mungu (s.w.t) kutaja mbingu ametaja ardhi na lengo ni moja - kuwatanabaisha walioghafilika kwenye dalili za kiulimwengu za kupatikana Mwenyezi Mungu na utukufu wake.

Na kwamba mwenye kuumba ulimwengu huu mkubwa pamoja na ardhi yake na mbingu yake anaweza kutuma mitume na kuteremsha vitabu, kufufua wafu.

Dalili hizo miongoni mwake ziko za mbinguni; kama vile kuinua mbingu bila ya nguzo, kulitiisha jua na mwezi n.k. Na nyingine ni za ardhini; kama zile alizoziashiria Mwenyezi Mungu kwa kauli zifuatazo:

1.Na yeye ndiye aliyeitandaza ardhi yaani aliyeitandika.

Mahali pengine Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

وَاللَّـهُ جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ بِسَاطًا ﴿١٩﴾

“Na Mwenyezi Mungu ndiye aliye wafanyia ardhi kuwa busati” (71:19)

وَالْأَرْضَ بَعْدَ ذَٰلِكَ دَحَاهَا ﴿٣٠﴾

“Na ardhi baada ya hayo akaitandika” (79:30)

Inavyoonyesha ni kwamba kutandazwa ardhi na kutandikwa pamoja na upana wake, hakuna uhusiano wowote na kuwa ardhi ni mviringo au ni bapa. Kwa sababu kitu kikiwa kikubwa sana, kama ardhi, kila upande wake unakuwa umeenea kwa upana na urefu, hata kama kiko mviringo.

Kwa hiyo basi Aya haizuii kuwa ardhi ni mviringo, jambo ambalo halina shaka. Razi anasema katika kufasiri Aya hii: “Hakika imethibiti, kwa dalili kwamba, ardhi ni tufe na ardhi ni kitu kikubwa na tufe likiwa ni kubwa sana basi kila sehemu yake inaonekana kama bapa.”

Wataalamu wa Kiyunani (kigiriki) katika enzi za Aristatle, waliafikiana kuwa ardhi ni mduara, lakini wakasema kuwa imetulia.

2.Na akaweka humo milima.

Neno milima limefasiriwa kutoka na neno Rawasi lenye maana ya kila kitu kilichothibiti mahali, lakini neno hili limetumika zaidi kwa milima, kiasi ambacho likitajwa tu bila ya nyongeza, inafahamika kuwa ni milima.

Hekima ya kupatikana hiyo milima ni utulivu wa ardhi na uthabiti wake, Mwenyezi Mungu anasema: “Je, hatukuifanya ardhi kuwa ni tandiko na milima kuwa ni vigingi?” (78:7).

3.Na mito.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) amekutanisha kutaja milima na mito kwa sababu mito inachimbuka kutoka humo milimani. Anasema:

وَجَعَلْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ شَامِخَاتٍ وَأَسْقَيْنَاكُم مَّاءً فُرَاتًا ﴿٢٧﴾

“Na tukaweka humo milima mirefu na tukawanywesha maji tamu” (77:27)

4.Na katika kila matunda akafanya humo viwili viwili–dume na jike.

Kila aina ya matunda ina dume na jike katika aina zake kwa dhahiri, kama vile mtende dume mtende jike, au kwa undani, kama mimea mingine.

Sheikh Al-Maraghi, katika tafsiri yake, anasema: “Imethibitisha elimu hivi sasa kwamba mti na mmea wowote hauzai matunda isipokuwa kwa ushirikiano baina ya wa kike na wa kiume. Aghlabu mbegu zinakuwa katika mti mmoja kama ilivyo miti mingi, au katika miti miwili tofauti, kama ilivyo kwa mtende.”

Katika jarida la Al-ulum la Lebanon toleo la Juni 1967 kwenye kichwa cha maneno “Vipi uhai unakuwa katika vitu”, imeelezwa kuwa vidudu vinachukua mbegu za uzazi kwenye mwili wake kupeleka kwenye makole ya maua bila ya kukosea, na kwamba ndege wanachukua mbegu za uzazi za yungi yungi kwenye midomo yao. Hakika ni muujiza.

Katika vita kuu vya ulimwengu vya pili walifika wapiganaji huko Corse, zaituni ikapata magonjwa na matunda yakapungua. Amerika ikataka kusaidia kutatua tatizo hilo, Kwa hiyo wakanyunyizia miti dawa ya DDT. Vidudu vya maradhi vikafa, lakini vikafa na vidudu vingine. Katika mwaka uliofuatia natija ikawa ni kutopatikana chochote! Si zaituni si limao wala lozi.

Kwa hiyo inatubainikia kuwa mimea haiwezi kuzaa matunda isipokuwa kwa kukutana mbengu za kike na za kiume.

5.Huufunika usiku kwa mchana.

Imepita tafsiri yake katika Juz. 8 (7:54).

Hakika katika hayo zimo ishara kwa watu wanaofikiri.

Katika ulimwengu huu ambao unakwenda kulingana na kanuni thabiti zisizotetereka kwa hali yoyote ile. Lau si uthabiti wake, isingeliwezekana kwa wataalamu kuuchunguza na kuuelewa. Ilivyo ni kwamba linalodumu linapinga sadfa. Na kwa ajili hii wataalamu wengi wa maumbile wameamini kuweko Mungu.

Na katika ardhi mna vipande vilivyokaribiana.

Ardhi imeungana, lakini kuna sehemu kadhaa zinazotofautiana, kuna tambarare, milima na mabonde. Pia kuna udongo mgumu na mchangatifu, changarawe na utelezi, weusi na weupe n.k. Siri ya hilo ni amri ya Mwenyezi Mungu na upangiliaji wake katika kuumba.

Na zipo bustani za mizabibu na mimea mingine na mitende ichipuayo kwenye shina, Ni mitende ya aina moja.

Na isiyochipua kwenye shina moja ni ile mitende inayotokana na mashina tofauti. Amehusisha kutaja mizabibu na mitende kwa sababu ndiyo matunda yanayopatikana sehemu nyingi au ndio yenye chumo na pengine ndiyo iliyokuwa muhimu wakati huo. Hilo linafahamika kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

وَاضْرِبْ لَهُم مَّثَلًا رَّجُلَيْنِ جَعَلْنَا لِأَحَدِهِمَا جَنَّتَيْنِ مِنْ أَعْنَابٍ وَحَفَفْنَاهُمَا بِنَخْلٍ وَجَعَلْنَا بَيْنَهُمَا زَرْعًا ﴿٣٢﴾

“Na wapigie mfano wa watu wawili: Mmoja wao tulimjalia vitalu viwili vya mizabibu na tukavizungushia mitende na kati yake tukatia mimea ya nafaka” (18:32)

Inanyweshwelezwa maji yale yale ; kama vile mvua, kisima au mto. Pia sehemu ni moja kwa kukarubiana, lakini matunda yanatofautiana kirangi, ukubwa, harufu na hata ladhaa. Siri ya hilo ni upangiliaji wake Mwenyezi Mungu na hekima yake.

Na tunaifanya bora baadhi yake kuliko mingine katika kula pamoja na kuwa nyezo za kumea kwake ni aina moja.

Hakika katika hayo kuna ishara kwa watu wanaotia akilini (mambo).

Yaani tofauti hii inayopatikana katika nyezo za aina moja, yakiwemo maji na hewa, ni dalili wazi ya kuweko mpangiliaji mambo vizuri, kwa yule ambaye haamini kitu ila baada ya kufikiri na kutia akilini.

Miongoni mwa kauli ya Imam Ali(a.s) :“Hakuna elimu kama kufikiri wala hakuna fahari kuliko kunyeyekea” .

SAYYID AFGHANI NA WANAOMKANA MUNGU

Ufafanuzi mzuri wa Aya hii kwa ujumla ni majibu ya Sayyid, Jamaluddin Al-Afghani, kwa wale wanaokana kuweko Mwenyezi Mungu anasema: “Akiulizwa Darwin kuhusu miti iliyoko katika misitu wa India na mimea inayozaliana humo tangu zama za kale sana ambazo historia haijui muda wake, isipokuwa kudhania tu.

Mashina yake yote yako katika uwanja mmoja matawi yake yote yanakwenda kwenye anga moja, Sasa ni kitu gani kinachofanyika mpaka mmoja ukatofautiana na mwingine katika umbile lake, majani yake, kimo chake na ukubwa.

Vile vile maua yake, matunda yake na hata ladha yake? Ni, kitu gani cha nje kilichoathiri mpaka ikapatikana tofauti katika makuzi ya aina moja, maji na hewa ya aina moja? Nadhani hawezi kupata jibu la hayo

Akiulizwa kuhusu hawa samaki wa mto Oural na wa bahari ya Qazwini (Caspian sea) wanashirikiana katika vyakula, lakini wanatofautiana kabisa kimaumbile, je kuna sababu gani ya kutofautiana huku? Sioni kama ataweza kuwa na majibu isipokuwa kushindwa”

Unaweza kuuliza kuwa : Darwin anaweza kumjibu Sayyid Afghani kwamba wataalamu wa mimea wanajua sababu ya kutofautiana huku na wanaweza kuifichua kwa kila anayetaka na kupendelea; Kwa hiyo basi, hakuna dharura, katika hali hii, kulazimika kuweko mpangiliaji?

Jibu : Tuchukulie kuwa wataalamu wa mimea wanajua sababu ya hilo, lakini ujuzi wao utakuwa na kiwango cha kujua sababu ya karibu ya hilo.

Na kama wakiulizwa sababu ya mbali iliyosababisha hii ya karibu hawatapata isipokuwa moja ya sababu mbili: Ama sadfa au kuweko mpangiliaji mwenye hekima. Sababu ya kwanza itakuwa batili kwa sababuu sadfa haikaririki wala kudumu, Kwa hiyo itabaki sababu ya pili.

Mara kadhaa tumebainisha kuwa ni desturi ya Qur’an kutegemeza matukio yote ya kimaumbile kwenye sababu yake ya kilimwengu.

Hilo ni katika kukitegemeza kitu kwa mtendaji wake wa kwanza, kwa lengo la kukumbusha kuweko Mwenyezi Mungu na kwamba yeye ndiye muumba wa ulimwengu wote pamoja na ardhi yote na mbingu yake.

Unaweza kusema tena : Wakana Mungu nao wanaweza kuuliza: Kuna sababu gani ya kuweko mpangiliaji mambo?

Jibu : Hakika swali hili sio la msingi kwa sababu kuweko mpangiliaji hakuna sababu na kwamba yeye ndiye msabibishaji sababu. Kuuliza sababu ya kuweko msababishaji ni sawa na kuuliza: Nina ni aliye muumba Mungu baada ya kufaradhia kuwa yeye ni muumba sio muumbwa.

Au kuuliza sababu ya kusadikisha jicho lilichokiona na sikio lilichokisikia na huku tunaamini kuwa hiyo ni hoja mkataa ya kila shaka na kila shubha.

وَإِن تَعْجَبْ فَعَجَبٌ قَوْلُهُمْ أَإِذَا كُنَّا تُرَابًا أَإِنَّا لَفِي خَلْقٍ جَدِيدٍ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ وَأُولَـٰئِكَ الْأَغْلَالُ فِي أَعْنَاقِهِمْ وَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٥﴾

5. Na kama ukistaajabu basi cha ajabu ni usemi wao: ‘Ati tutakapokuwa mchanga, kweli tutakuwa katika umbo jipya?’ Hao ndio waliomkufuru Mola wao na hao ndio watakokuwa na minyororo shingoni mwao na hao ndio watu wa motoni, Humo watadumu.

وَيَسْتَعْجِلُونَكَ بِالسَّيِّئَةِ قَبْلَ الْحَسَنَةِ وَقَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِمُ الْمَثُلَاتُ وَإِنَّ رَبَّكَ لَذُو مَغْفِرَةٍ لِّلنَّاسِ عَلَىٰ ظُلْمِهِمْ وَإِنَّ رَبَّكَ لَشَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿٦﴾

6. Wanakuhimiza ulete maovu kabla ya mema, hali ya kuwa imepita kabla yao mifano. Na hakika Mola wako ni mwenye maghufira kwa watu juu ya udhalimu wao. Na hakika Mola wako ni mkali wa kuadhibu.

وَيَقُولُ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ آيَةٌ مِّن رَّبِّهِ إِنَّمَا أَنتَ مُنذِرٌ وَلِكُلِّ قَوْمٍ هَادٍ ﴿٧﴾

7. Na husema wale ambao wamekufuru: ‘Mbona hakuteremshiwa ishara kutoka kwa Mola wake.’ Hakika wewe ni mwunyaji tu. Na kila kaumu ina wa kuwaongoza.

KWELI TUTAKUA KATIKA UMBO JIPYA?

Aya 5-7

MAANA

Na kama ukistaajabu basi cha ajabu ni usemi wao: ‘Ati tutakapokuwa mchanga, kweli tutakuwa katika umbo jipya?’

Maneno yanaelekezwa kwa Muhammad(s.a.w.w) wasemaji ni washirikina waliokana utume wake. Maana ni kuwa ikiwa ewe Muhammad utashangazwa na ibada ya masanamu ya washirikina na kukanusha kwao utume wako, basi la kushangaza zaidi ni kukadhibisha kwao ufufuo.

Kwa sababu wao wanakubali kuwa yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Muumba wa ulimwengu, na mwenye kuweza hilo si anakuwa na uwezo zaidi wa kumrudisha mtu baada ya kufa kwake?

Hao ndio waliomkufuru Mola wao na hao ndio watakokuwa na minyororo shingoni mwao na hao ndio watu wa motoni, Humo watadumu.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametaja neo ‘hao’ mara tatu kuelezea kwa ufasaha zaidi hasira zake na kuchukia kwake. Kauli yake: Hao ndio waliomkufuru Mola wao, inafahamisha kuwa Mwenye kuamini kuwa Mwenyezi Mungu ni muumba wa ulimwengu inamlazimu yeye, kwa hali yoyote, kuamini kuwa yeye ni muweza wa kuwafufua walio makaburini. Atakayepinga hilo atakuwa moja kwa moja amemkufuru Mwenyezi Mungu atake asitake.

Mwenye kuchanganya imani ya Mungu na kushindwa kufufua watu, atakuwa amechanganya mambo mawili yanayopingana. Washirikina wamepinga ufufuo, kwa vile, kulingana na madai yao, Mwenyezi Mungu hawezi; kama inavyojulisha kauli yao “Ati tutakapokuwa…” Kwa hiyo, ilivyo hasa, ni kuwa wao wanampinga Mwenyezi Mungu kwa ndimi zao.

WANAOAMINI MAADA NA MAISHA BAADA YA MAUTI

Wanaoamini maada wanakana kuweko Mwenyezi Mungu, sana sana wanapinga maisha baada ya mauti. Dalili yao ni moja tu haibadiliki wala haigeuki. Nayo ni kuwa kila linaloweza kuhisiwa na kushuhudiwa inapasa kuliamini na kila lisiloweza kuhisiwa inapasa kulikana na kulipinga.

Kwa hiyo, kwao, hisia ya dhahiri peke yake ndiyo dhahiri na ndiyo batini, ndiyo ya mwanzo na ya mwisho; kama wanavyosema. Vipi wataamini Bustani (Pepo) nao hawajala matunda yake, vipi wakubali kuwa kuna Jahannam na moto wake haujawafikia?

Sisi nasi, kwa upande wetu, tunauliza hivi: Mmepata wapi elimu au imani ya kuwa hisia za dhahiri pekee ndiyo njia ya haki na hali halisi, na kwamba mengineyo ni upuuzi? Mkisema hayo mmeyajua kupitia hisia, tutasema:

Sisi pia tunazo hisia na hatujamuona mwingine zaidi yenu akisema kuwa msiamini isipokuwa hisia. Ikiwa mtasema mmejua hilo kwa njia nyingine isiyokuwa hisia, basi mtakuwa mmejipinga wenye kwa kuamini kisichoshuhudiwa na hisia.

Mnamo mwaka 1962 nilitunga kitabu kuwajibu wanaoamini maada, kwa jina Falsafatul-Mabda’ (falsafa ya misingi), Kisha baadae nikasoma mambo mengi kuhusu wanavyoamini wa maada na majibu yao; miongoni mwayo ni:

1. Kwa mujibu wa wanaoamini maada ni lazima kutokuweko tofauti yoyote baina ya mtu aliye na miujiza na vidudu duni vinavyotokana na uchafu kwa vile wote hao ni watoto wa sharia ya sadfa na maumbile pofu yasiyokuwa na mipangilio yoyote

2. Wataalamu wamepata katika ubongo wa binadamu nyuzi milioni elfu 14 zimefumwa na kupangiliwa vizuri sana kwa namna ambayo wahandisi wakuu wote hawawezi; kiasi ambacho unyuzi mmoja tu ukienda kombo basi mtu hatakuwa na utambuzi au atachanganyikiwa, sawa na umeme ukiharibika moja ya nyaya zake. Hakuna tafsiri ya hayo, kwa mwenye akili, isipokuwa kuweko mpangiliaji mwenye hekima asiyeweza kuonwa kwa jicho, kusikiwa na sikio, kuguswa kwa mkono, kunuswa na pua au kuonjwa kwa ulimi.

Kwa namna yoyote itakavyokuwa sadfa na muujiza, lakini haiwezi kufanya umeme; sikwambii kuunganisha nyuzi milioni elfu 14 zilizopangiliwa, kiufundi na kuwekwa kwenye chombo kimoja kwa idadi ya vichwa na bongo za binadamu wote; tena waweze kuhisi na kutambua.

3. Waamini maada wanasema kuwa ubongo wa binadamu ni sawa na akili ya mashine. Zote mbili zimetokana na vitu vilivyosukwa na kupangwa kuweza kuleta athari.

Mtaalamu wa kifaransa, aitwaye Caussine, aliwajibu kwa kusema: Iwapo gari yangu ya zamani ikianza kutoa sauti mbovu kama mtu aliyepatwa na ugonjwa wa baridi yabisi, inawezekana niseme kuwa gari yangu ina baridi yabisi? Na kabureta inapotatarika wakati ninapokanyaga mafuta, je, itafaa niseme kuwa gari yangu imepatwa na pumu?

Nasi tunaongezea juu ya kauli ya mtaalamu huyu kwa kusema: mpangilio na utaratibu kwenye akili ya mashine umetokana na kitendo cha mtu, hilo halina shaka. Lakini ni nani aliyepangilia na akaweka mfumo kwenye ubongo wa binadamu?

Ikiwa binadamu amevumbua akili ya mashine, je akili hii ya mashine inaweza kuvumbua akili nyingine mfano wake au kitu duni kama pini? Katika kitabu Al-amal wal – Mukh (kazi na ubongo), kilichofasiriwa na Shakri Azir cha Mtaalamu wa Kirusi Yuri Bakhlov, anasema: Wale wanaodhani kuwa kuna uwezekano wa mashine kuchukua nafasi ya akili ya binadamu wamekosea kosa kubwa sana… ubongo wa binadamu unatofautiana kabisa na chombo chochote katika utendaji kazi wake, uwelekevu na ustadi wake usio na kikomo. Ama akili ya mashine ina kikomo - kile alicho kiweka binadamu.

4. Kuna ugunduzi mkubwa wa nyuki kuhusu vifaa vya kupunguza joto (viyoyozi), Kwamba nyuki aligundua kifaa hiki kabla ya binadamu. Joto linapozidi kwenye Masega ya nyuki kundi moja linaondoka kuleta maji kwa kutumia visiku vyao na kuyaweka kwenye tanki. Kikipatikana kiasi cha kutosha husimama kundi jengine kunyunyiza maji na kundi jingine la tatu linatengeneza tiyara ya hewa na maji yanayayuka kwa haraka; kwa myeyuko huo kiwango cha joto kinashuka.

Ni nani aliyempa nyuki akili hii? Ni sadfa? Au kuna nguvu ya hakika inayojitokeza kwenye maumbile na nidhamu yake? Nyuki na sisimizi wana masimulizi ambayo hayana tafsiri wala picha yoyote isipokuwa kuweko mpangiliaji mwenye hekima.

Turudie kauli ya Voltare ambaye huko nyuma tumewahi kumdokeza mara kwa mara, anasema: Mbele ya fikra ya kuweko Mwenyezi Mungu kuna vikwazo lakini katika fikra ya kupinga kuna upumbavu …Namna hii binadamu anahama kutoka kwenye shaka hadi shaka nyingine mpaka anafikia kusadikisha kuwa kuweko Mwenyezi Mungu ndio jambo la karibu zaidi na kwaye zinafungamana kanuni za dharura ya ulimwengu.

Wanakuhimiza ulete maovu kabla ya mema, hali ya kuwa imepita kabla yao mifano.

Makusudio ya maovu hapa ni adhabu na mema ni thawabu na mifano ni mifano ya adhabu.

Mtume(s.a.w.w) aliwalingania washirikina kwenye Tawhid, na akawaahidi thawabu wakiitikia mwito na kuwapa kiaga cha adhabu wakitoitikia.

Wao badala ya kuitikia mwito na kutubia shirk, waliendelea kuasi na wakajifanya jeuri, huku wakisema: Harakisha unayotuahidi ukiwa ni mkweli waliyasema haya bila ya kuzingatia umma zilizopita ziliyoyapata baada ya kuwaasi Mitume wao.

Kwa hakika mghafala huu wa kutopata funzo, hauhusiki na washirikina peke yao, Watu wengi hawazingatii yaliyowapata wenzao wala hawapati funzo; hata wenyewe wanaotoa mawaidha. Siri ya hilo ni kuwa wengi wanashindwa na tamaa na masilahi sio kwa akili wala dini.

Kuna mfano maarufu wa kimagharibi unaosema: Mwanamke kumwongoza mwana- mume kwa tumbo si kwa akili.

Na hakika Mola wako ni mwenye maghufira kwa watu juu ya udhalimu wao. Na hakika Mola wako ni mkali wa kuadhibu.

Makusudio ya maghufira hapa ni kupuuza na kutoharakisha adhabu kwa dhambi. Hilo linafahamika kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu: “Na hakika Mola wako ni mkali wa kuadhibu. Kwa sababu maghufira hayawi pamoja na adhabu ya akhera sikwambii iliyo kali.

Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) hamwadhibu mja mara tu anapo- fanya dhambi isipokuwa anamngojea na kumfungulia mlango wa toba ili aweze kurejea kutokana na upotevu wake, aweze kupata thawabu kwenye uwongofu wake.

Kuna tafsiri nyingine isemayo kuwa Mwenyezi Mungu husamehe dhambi za walioasi katika waislamu na anakuwa mkali wa kuadhibu kwa makafiri. Lakini tafsiri hii iko kinyume na dhahiri, tena inahimiza uasi. Usawa hasa ni yale tuliyoyasema kuongezea Aya nyingine isemayo:

وَلَوْ يُؤَاخِذُ اللَّـهُ النَّاسَ بِظُلْمِهِم مَّا تَرَكَ عَلَيْهَا مِن دَابَّةٍ ﴿٦١﴾

“Lau Mwenyezi Mungu angeliwachukulia watu kwa sababu ya dhulma yao, asingelimwacha hata mnyama mmoja juu yake” (16:61).

Na husema wale ambao wamekufuru: ‘Mbona hakuteremshiwa ishara kutoka kwa Mola wake?’ Hakika wewe ni mwonyaji tu. Na kila kaumu ina wa kuwaongoza.

Imepita mifano yake katika Juz.7 (6:37), Na tumefafanua kuhusu muujiza wa Mtume Muhammad(s.a.w.w) na matakwa ya wenye kiburi katika Juz 1 (2:118).

2

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA NNE

﴿وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ تَفَرَّقُوا وَاخْتَلَفُوا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ وَأُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴾

105.Wala msiwe kama wale waliofarakana wakahitalifiana baada ya kuwajia wao dalili zilizo wazi; na hao ndio wenye adhabu kubwa.

﴿يَوْمَ تَبْيَضُّ وُجُوهٌ وَتَسْوَدُّ وُجُوهٌ فَأَمَّا الَّذِينَ اسْوَدَّتْ وُجُوهُهُمْ أَكَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ﴾

106.Siku ambayo nyuso zitang'aa na nyuso (nyingine) zitasawijika. Na ama ambao nyuso zao zitasawijika, (wataambiwa): Je mlikufuru baada ya kuamini kwenu? Basi onjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyakanusha.

﴿وَأَمَّا الَّذِينَ ابْيَضَّتْ وُجُوهُهُمْ فَفِي رَحْمَةِ اللَّـهِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴾

107.Na ama ambao nyuso zao zitang'aa, watakuwa katika rehema ya Mwenyezi Mungu, Wao humo watadumu.

﴿تِلْكَ آيَاتُ اللَّـهِ نَتْلُوهَا عَلَيْكَ بِالْحَقِّ وَمَا اللَّـهُ يُرِيدُ ظُلْمًا لِّلْعَالَمِينَ ﴾

108.Hizo ni Aya za Mwenyezi Mungu, tunakusomea wewe kwa haki; na Mwenyezi Mungu hataki kuwadhulumu viumbe.

﴿وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَإِلَى اللَّـهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ ﴾

109.Ni vya Mwenyezi Mungu vilivyomo ardhini na vilivyomo mbinguni; na kwa Mwenyezi Mungu hurejezwa mambo yote.

KUHITALIFIANA BAADA YA MTUME

Aya 105 - 109

MAANA

Wala msiwe kama wale waliofarakana wakahitalifiana baada ya kuwajia wao dalili zilizo wazi.

Aya hii inamalizia kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu nyote" Makusudio ya wale waliofarakana ni watu wa Kitabu, Ambapo mayahudi walichangukana vikundi sabini na moja baada ya Mtume wao Musa, wakristo wakawa vikundi sabini na mbili baada ya Mtume wao Isa, Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu."Baada ya kuwajia hoja iliyo wazi" inafahamisha kwamba mtu haadhibiwi kwa kuiacha haki na kufuata batili, ila baada ya kubainishiwa hoja. Ama siri ya mkazo huu na kuupa kipaumbele muungano wa umma, ni kuwa utengano ndio kiini cha ufisadi na kwamba umma uliotengana hauwezi kuwa na maisha mazuri, wachilia mbali kuuita umma mwingine kwenye kheri. Pamoja na kuwapo Riwaya nyingi, na Hadith zinazohimiza muungano wa waislamu, lakini bado wamefarakana na kuwa vikundi mbali mbali, wamewazidi mayahudi kwa vikundi viwili zaidi na wakristo kikundi kimoja; kama ilivyoelezwa katika Hadith mashuhuri.

Kuna Hadithi nyingine isemayo: "Mtakuwa na desturi ile ile ya waliokuwa nayo kabla yenu." Akaulizwa: "Unakusudia mayahudi na manaswara ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?" Akasema: "Kumbe ninawakusudia kina nani? Utachanguka uthabiti wa waislamu" Katika kitabu Al-Jam'u Bainas-Sahihayni cha Hamid, kwenye Hadith Na. 131, anasema: Katika yaliyoafikianwa kutoka Musnad ya Anas bin Malik, amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) :"Watanijia watu miongoni mwa sahaba zangu kwenye hodhi, nitakapowaona na watakapokuwa wanaletwa kwangu watazuiwa ili wasinifikie. Hapo nitasema: 'Ewe Mola! Sahaba zangu, sahaba zangu! Nami nitaambiwa: 'Wewe hujui walizua nini baada yako" Katika kitabu hicho hicho Hadith Na. 267 anasema: "Katika yaliyaofikianwa kutoka Musnad ya Abu Huraira kutoka katika njia mbali mbali, ni kwamba Mtume amesema: "Wakati nikiwa nimesimama - siku ya Kiyama - litatokea kundi la watu mpaka nitakapowatambua, atatokea mtu baina yangu na yao na awambie: 'Haya twendeni.' Mimi nitauliza: Mpaka wapi? Naye aseme: 'Mpaka motoni' Nami niulize wana nini? Naye ajibu: 'Hakika wao walirtadi baada yako"

Siku ambayo nyuso zitang'aa na nyuso (nyingine) zitasawijika.

Makusudio ya Siku, ni Siku ya Kiyama. Kung'aa uso, ni fumbo la kuonyesha furaha ya mumin kufurahia radhi za Mwenyezi Mungu na fadhila Zake. Kusawijika uso ni huzuni ya kafiri na fasiki kwa ghadhabu na adhabu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Na ama ambao nyuso zao zitasawijika,(wataambiwa), je, mlikufuru baada ya kuamini kwenu?

Arrazi, Tabari na wafasiri wengine wengi wamenukuu kutoka kwa baadhi ya waliopita, kwamba makusudio ya watakaoambiwa hivyo ni Khawariji. Kwa sababu Mtume alisema kuwahusu:"Hakika wao watachomoka kutoka katika dini, kama unavyochomoka mshale kutoka katika uta (upinde)." Lakini dhahiri ya Aya inamkusanya kila mwenye kukufuru baada ya imani, wakiwemo Khawariji, watu wa bid'a na wenye maoni potofu. Kwa vile adhabu haihusiki tu na aliyekufuru baada ya imani bali inamuhusu kafiri yeyote, kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

Onjeni adhabu, kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyakanusha, Na ama ambao nyuso zao zitang'aa, watakuwa katika rehema ya Mwenyezi Mungu, wao humo watadumu.

Rehma ya Mwenyezi Mungu ni Pepo. Kwa ufupi ni kwamba wale ambao wameshikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu, na kufanya mambo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na wakasaidiana kwenye mambo ya kheri na ya masilahi ya umma, basi watafufuliwa kesho wakiwa watukufu, wenye furaha na wenye kuridhia. Ama wale ambao wamehitalifiana kwa kuipupia dunia, wasiojishughulisha na dini wala umma au nchi, na ambao hawajishughulishi na lolote isipokuwa masilahi yao na ya watoto wao tu, basi wao watafufuliwa Siku ya Kiyama wakiwa madhalili, wenye hasara na makazi yao ni Jahanam, nayo ni marejeo mabaya kabisa. Ajabu ya maajabu ni kwamba baadhi ya wenye nyuso zilizosawijika wanadai kuwa wanamzungumzia Mungu na kutumia Jina lake, lakini mtu akiwaambia "Muogopeni Mungu" wao husema: "Umemkufuru Mwenyezi Mungu." Aliyewatangulia katika hilo ni Abdul Malik bin Marwan aliposema pale alipochukua Ukhalifa: "Kuanzia leo atakayeniambia muogope Mwenyezi Mungu nitamkata kichwa chake."

Hizo ni Aya za Mwenyezi Mungu, tunakusomea wewe kwa haki.

Hizi, ni ishara ya Aya zinazoelekezea kuneemeshwa watu wema na kuadhibiwa makafiri. Msemo unamwelekea Muhammad(s.a.w.w) , muulizaji anaweza kuuliza: "Kuna faida gani katika habari hii, ikiwa Muhammad anajua kwa yakini kwamba Aya hizi ni haki na ni kweli?" Jibu: Ni kawaida ya Qur'an kulikariri hilo katika Aya kadhaa. Na makusudio sio kwa Muhammad hasa, bali ni kwa yule anayetia shaka na kudhani kwamba Aya hizi na mfano wake zinatoka kwa Muhammad, si kwa Mwenyezi Mungu.

﴿وَمَا كُنتَ تَتْلُو مِن قَبْلِهِ مِن كِتَابٍ وَلَا تَخُطُّهُ بِيَمِينِكَ إِذًا لَّارْتَابَ الْمُبْطِلُونَ﴾

"Na hukuwa mwenye kusoma kitabu chochote kabla ya hiki wala hukukiandika kwa mkono wako wa kuume, ingekuwa hivyo wangefanya shaka wabatilifu" (29:48)

Na Mwenyezi Mungu hataki kuwadhulumu viumbe, Kwa sababu dhuluma ni mbaya na Mwenyezi Mungu ameepukana nayo.

Aya hii ni dalili ya mkato kwamba Mwenyezi Mungu hakalifishi mja asiloliweza.

﴿كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُم مِّنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ﴾

110.Mmekuwa ni umma bora mliotolewa kwa watu, mnaamrisha mema na kukataza maovu na mnamwamini Mwenyezi Mungu. Na lau watu wa Kitabu wangeliamini ingekuwa heri kwao. Katika wao kuna wanaoamini na wengi wao ni wafasiki .

﴿لَن يَضُرُّوكُمْ إِلَّا أَذًى وَإِن يُقَاتِلُوكُمْ يُوَلُّوكُمُ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنصَرُونَ ﴾

111.Hawatawadhuru isipokuwa kuwaudhi tu, na wakipigana nanyi watawakimbia, kisha hawatasaidiwa.

UMMA WA MUHAMMAD

Aya 110 - 111

MAANA

Mmekuwa ni umma bora mliotolewa kwa watu, mnaaamrisha mema na kukataza maovu na mnamwamini Mwenyezi Mungu

Kuna njia kadhaa kuhusu Aya hii, kama ifuatavyo:

1) Katika makusudio ya umma, hakuna mwenye shaka kuwa makusudio ya umma hapa ni Umma wa Muhammad(s.a.w.w) , kwa dalili ya mfumo wenyewe wa maneno ulivyo na mtiririko wa misemo inayoelekezwa kwa waumini; kama vile; "Enyi ambao mmeamini mcheni Mwenyezi Mungu. Na shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu kwenu…" Mpaka kufikia kauli yake Mwenyezi Mungu:"Mmekuwa ni umma bora."

2). Je, makusudio ni waislamu wote katika wakati wote, au ni kuwahusu wale walio kuwa katika siku za kwanza za uislamu kama vile Masahaba na waliofuatia (tabiina)?

Jibu : Kuainisha makusudio ya umma hapa, kunahitaji kujua makusudio ya herufi kana (kuwa) ambayo ilivyo ni kuwa inahitaji isimu na habari yake. Pia hiyo kana inafahamisha kufanyika kitendo wakati uliopita, lakini haielezi ni wakati gani kimefanyika hicho kitendo wala kuwa kinaendelea au la.

Isipokuwa hilo linaweza kufahamika kutokana na vitu vingine vilivyo pamoja nayo kimaneno au hali ilivyo. Kwa mfano kusema, Zaid alikuwa ni mwenye kusimama. Hapo inachukuliwa kutendeka tendo la kusimama na kuisha bila kuendelea. Yaani Zaid, hakuwa ni mwenye kusimama, basi akasimama kipindi fulani bila ya kuendelea kusimama maisha. Lililofahamisha hilo ni neno mwenye kusimama, yaani hawezi kusimama maisha. Lakini kama tukisema Mwenyezi Mungu amekuwa ni Mwingi wa maghufira Mwenye kurehemu, hapo hali inafahamisha kudumu kwa tendo lenyewe, kwa sababu rehema na maghufira haviepukani na dhati yake Mwenyezi Mungu, na dhati yake Mwenyezi Mungu Mtukufu ni ya milele na milele. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameufungamanisha ubora wa umma na kumwamini kwake, na kuamrisha mema na kukataza maovu, basi maana ya Aya yanakuwa ni: Enyi waislamu! Msiseme tu sisi ni umma bora mpaka muamrishe na kukataza maovu; na kwamba sifa hii ya ubora itawaondokea mara tu mnapopuuza hilo.

Kwa hivyo basi kana hapa inakuwa ni kamilifu, sio pungufu; yaani haihitaji khabar. Kwa maana hayo makusudio ni waislamu wote([2] ) .

3).Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu 'mliotolewa kwa Watu' inafahamisha kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemleta Muhammad na umma wake(s.a.w.w) ushinde umma zote za mwanzo ukiwa umechukua Kitabu cha Mwenyezi Mungu mkono mmoja na Hadith za Mtume kwenye mkono mwingine, huku ukiwalingania vizazi vishikamane na vitu viwili hivyo na kuvitegemea kwa itikadi, sharia na maadili. Kwa sababu ndio marejeo pekee yanayoweza kuhakikisha ufanisi wa mambo yote, kudhamini maisha ya kila mtu na kufungua uwanja wa wenye uwezo wa kufanya ijitihadi kwa misingi ya usawa, amani na uhuru wa watu wote([3] ) .

Aya hii katika madhumuni yake inaafikiana na Aya isemayo:

﴿وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِّتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا﴾

"Tumewafanya ni umma wa wastani, ili muwe mashahidi juu ya watu na Mtume awe shahidi juu yenu." (2:143)

Ikiwa waislamu hawatafanya harakati zozote za kulingania kwenye kheri au kuamrisha mema na kukataza mabaya, basi sifa za uongozi zitawaondokea na watakuwa na haja ya kiongozi atakayewaamrisha mema na kuwakataza maovu. Ulikuwepo wakati ambapo waislamu walikuwa na harakati hizi. Wakati huo walikuwa wakistahili kuwa viongozi wa umma zingine; kisha wakapuuza; wakaendelea hivyo mpaka wakawa wanakataza mema na kuamrisha maovu; kama tuonavyo sasa. Leo vijana wamekuwa wanajivua kabisa na dini na hulka njema. Wakimwona mtu anaswali au kufunga husema kwa dharau: "Bado kuna Swala na Saumu katika karne ya ishirini?" Mwenye Tafsir Al-Manar, katika kufasiri Aya hii, anasema: "Kwa kweli hasa ninasema, haukuzimika ubora wa umma uliotolewa kwa watu, mpaka pale ulipoacha kuamrisha mema na kukataza mabaya. Na haukuacha hivyo kwa kupenda au kupuuza amri ya Mwenyezi Mungu, bali ni kwa kulazimishwa na ufedhuli wa Wafalme wa bani Umayya na waliofuata nyayo zao."

Kwa msingi vitu hutajwa kwa kinyume chake; kama ambavyo hutajwa kwa kifani chake, basi tutaleta Hadith tukufu aliyoitaja Hafidh Muhibbudin Attabari, amesema: "Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) 'Mfano wa Ahlu bait wangu, ni kama safina ya Nuh mwenye kuipanda ataokoka, na mwenye kushikamana nayo ataokoka, na mwenye kuachana nayo ataghariki'". Ama Hadith ya "Mimi nawaachia vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Kizazi changu - Ahlul bait wangu," imepokewa na wapokezi 35 katika Masahaba.

Na lau wangeliamini watu wa Kitabu, ingelikuwa heri kwao.

Yaani lau watu waliopewa Tawrat na Injil, wangelimwamini Muhammad(s.a.w.w) ingelikuwa imani yao hiyo ni heri yao katika muda wa sasa na ujao.

Katika wao kuna wanaoamini na wengi wao ni wafasiki.

Yaani katika watu wa Kitabu kuna waliomwamini Muhammad(s.a.w.w) ; kama vile Abdullah bin Salam na watu wake, na wengineo katika wanaswara, na wengi wao walibaki katika ukafiri.

Neno Fasiq na Kafir yanapokezana maana, hutumiwa Fasiq kwa maana ya Kafiri na Kafir kwa maana ya Fasiq. Na Fasiq hapa ina maana ya kafiri. Hawatawadhuru, isipokuwa kuwaudhi tu, na wakipigana nanyi watawakimbia Madhara yako aina mbili:

Kwanza : ni kiasi cha huzuni na kusikia uchungu tu, ambako kadiri siku zinavyokwenda nayo yanafutika; kama vile inavyotokea katika nafsi kwa kusikia habari mbaya.

Pili : ni yale yanayogusa maisha na kuyumbisha; kama vile madhara yaletwayo na dola ya Israil ndani ya nchi ya Waarabu. Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewabashiria maswahaba wa Mtume(s.a.w.w) kwamba watu wa Kitabu:

Hawatawadhuru isipokuwa kwa maneno tu, kama vile uzushi na mabezo. Ama katika uwanja wa vita, nyinyi ndio washindi.

Amesema kweli Mwenyezi Mungu katika kiaga chake, Aliwapa ushindi waislamu wa mwanzo kwa wakristo na wengineo.

﴿ضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ أَيْنَ مَا ثُقِفُوا إِلَّا بِحَبْلٍ مِّنَ اللَّـهِ وَحَبْلٍ مِّنَ النَّاسِ وَبَاءُوا بِغَضَبٍ مِّنَ اللَّـهِ وَضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الْمَسْكَنَةُ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَانُوا يَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَيَقْتُلُونَ الْأَنبِيَاءَ بِغَيْرِ حَقٍّ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ﴾

112.Wamepigwa na udhalili popote wanapokutanikana, isipokuwa ni kwa kamba ya Mwenyezi Mungu na kamba ya watu, Na wamestahili ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na wamepigwa na unyonge na udhalili. Hayo ni kwa sababu walikuwa wakizikanusha ishara za Mwenyezi Mungu na kuwaua Manabii pasi na haki, hayo ni kwa sababu ya kuasi kwao na kupetuka mipaka.

WAMEPIGWA CHAPA YA UDHALILI

Aya 112

MAANA

Wamepigwa na udhalili popote wanapokutanikana isipokuwa ni kwa kamba ya Mwenyezi Mungu na kamba ya watu, Na wamestahili ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na wamepigwa na unyonge na udhalili.

Wafasiri wameafikiana kuwa, Aya hii imeshuka kwa ajili ya mayahudi; kama ambavyo wameafikiana kuwa makusudio yake ni kuwa Mwenyezi Mungu amewanyima utukufu na takrima, na akawaandikia udhalili tangu ulipoanza uislamu hadi siku ya mwisho. Kwa sababu wao katika ufisadi na kupetuka mipaka wamefikilia hatua ambayo hakuifikia na hataifikia yeyote. Baada ya wafasiri kuafikiana juu ya hilo, wametofautiana kuhusu aina ya udhalili na unyonge walio nao (Mayahudi ambayo iko kwa kila kizazi). Tofauti hiyo hasa inatokana na tofauti ya hali ya mayahudi wakati wa kufasiri, ambapo walikuwa wakitoa kodi kwa waislamu, yaani kauli ya mfasiri imekuja kuakisi na walivyokuwa wayahudi. Hiyo si ajabu maadam mtu anaathirikia kwa anachokisikia na kukiona, Na tafsiri yangu ya Aya hii inafuata desturi hii.

Vyovyote iwavyo, ninavyofahamu ni kwamba udhalili wa mayahudi uliokusudiwa na Aya ni huku kutawanyika kwao duniani, Mashariki na Magharibi, wakiwa wako kwenye nchi mbali mbali. Wao daima ni wafuasi na wala sio wanaofuatwa na kuhukumiwa katika dola yao. Wako peke yao katika mambo yao. Ama Israeli iliyoko Tel Aviv ni Dola ya jina tu, ilivyo hasa ni kambi tu ya kikoloni na ni kituo cha jeshi cha uchokozi. Hakika hii imedhihiri wazi wazi baada uchokozi wa Israel katika ardhi za Waarabu mnamo tarehe 5 Juni 1967. Ni uchokozi ambao wanaufanya waisrail ili kutekeleza mahitaji yao. Lau watauacha siku moja tu watanyang'anywa na waarabu.

Huo ndio udhalili hasa, kwa sababu mwenye heshima zake hutegemea nguvu zake mwenyewe na kujihami kwa mikono yake sio mikono ya wengine. Kwa hali hii, inatubainikia kuwa makusudio ya kamba ya watu, ni msaada wa kihali na mali utolewao na mataifa ya kikoloni kwa ajili ya kambi ya kikoloni ya Israel. Kwa hivyo basi tunaamini bila ya tashwish yoyote kwamba Dola ya Israil itaondoka tu kwa kuondoka ukoloni. Na ukoloni uko njiani kuisha iwe ni sasa au baadae. Wala maneno hayo sio ndoto, isipokuwa ni natija hasa itakayotokea, kama ilivyoeleza Hadith ya Mtume:"Hakitasimama Kiyama mpaka muwapige vita mayahudi na kwamba jiwe litasema: Ewe Mwislamu! Huyu hapa Yahudi nyuma yangu muue"([4] )

Ama Kamba ya Mwenyezi Mungu ni fumbo la matakwa yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: yaani kwamba mayahudi wataendelea kuwa na udhalili mpaka atakapotaka Mwenyezi Mungu: ni sawa na kauli yake Mwenyezi Mungu pia isemayo:

﴿قَالَ النَّارُ مَثْوَاكُمْ خَالِدِينَ فِيهَا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُ﴾

"Moto ndio makazi yenu mtadumu humo milele ila apende Mwenyezi Mungu" (6:128)

Kisha baada ya hapo, Mwenyezi Mungu amebainisha sababu iliyowajibisha udhalili wao na ghadhabu yake kwao, kwa kusema:

Hayo ni kwa sababu walikuwa wakizikanusha ishara za Mwenyezi Mungu na kuwaua Manabii pasi na haki; hayo ni kwa sababu ya kuasi kwao na kupetuka mipaka.

Umetangulia mfano wa Aya hii katika Sura ya Baqara Aya 61.

Unaweza kuuliza : Kuna wasiokuwa Mayahudi katika mataifa mengine waliokanusha dalili za Mwenyezi Mungu, kuwaua watu wema, kuasi na kupetuka mipaka; pamoja na hayo Mwenyezi Mungu hakuwapiga chapa ya udhalili na uduni. Je,kuna siri gani katika kuwahusisha Mayahudi?

Jibu : Mtu anaweza kupetuka mpaka kwa msukumo fulani unaotokana na masilahi yake na manufaa yake. Ama kupetuka mpaka si kwa lolote isipokuwa kwa kupendelea tu kufanya dhambi, hakujatokea kwa yeyote isipokuwa mayahudi tu, na pupa hii ya kupenda dhuluma na uovu iko ndani ya dini ya mayahudi. Wao wanaitakidi kwamba Mwenyezi Mungu yuko na wao tu, sio wengineo; bali pia yuko dhidi ya maadui zao; na kwamba watu wote wameumbwa kwa ajili yao tu ili wawafanye vile watakavyo, sawa na mtu amfanyiavyo mnyama. Jambo linalofahamisha zaidi sera yao hiyo, zamani na sasa, ni fedheha yao katika Palestina, hasa waliyo yafanya huko Dayr Yasin, kuwachinja wanawake na watoto.

Mwanzo walikuwa wakiwaua Mitume wakati dunia ilipokuwa na Mitume. Ama leo, ambapo hakuna Mitume wanawaua wasuluhishaji; kama vile Bernadotte([5] ) , na wanawake na watoto. Kwa sababu, la muhimu katika itikadi yao na maumbile yao ni kuwaua watu wasiokuwa na hatia; wawe Mitume au wasuluhishi au watoto.

Tawrat yao imeandika uhalali wa kumwaga damu ya wanawake na watoto, na imelihimiza hilo. Kwa ujumla ni kwamba kuzikanusha dalili za Mwenyezi Mungu, kuwaua wasuluhishi na watu wema wasio na hatia, na kufanya dhuluma na uchokozi, yote hayo ni dini na itikadi ya Mayahudi. Myahudi akimfanyia kosa mwengine asiyekuwa Myahudi basi anafanya kwa kujiburudisha tu, sio kwa haja fulani. Na kama akiacha kufanya hivyo, basi anaacha kwa kuogopa sio kwa kujistahi.

Hii ndiyo tofauti kati ya mayahudi na wasiokuwa mayahudi. Kwa hiyo hakuna ajabu kwa Mwenyezi Mungu kuwawekea udhalili popote walipo.

Ama serikali habithi ya Israel ya sasa itaondoka tu, hakuna budi, Ushahidi mkubwa wa kwisha kwake ni kwamba imefungamana na ukoloni, ukoloni ukiondoka nayo inaondoka. Na ukoloni lazima uondoke tu, hata kama ni baada ya miaka. Maadam maumbile ya kibinadamu yanaukataa ukoloni na kuupinga kwa damu yake, basi utaondoka tu.

Yote haya tuliyoayataja yanakamilisha kifungu cha 'Mayahudi hawana mfano' katika tafsiri ya Sura Baqara (2) Aya63 na 66.

﴿لَيْسُوا سَوَاءً مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ أُمَّةٌ قَائِمَةٌ يَتْلُونَ آيَاتِ اللَّـهِ آنَاءَ اللَّيْلِ وَهُمْ يَسْجُدُونَ﴾

113.Wote si sawa Katika watu wa Kitabu wamo walio na msimamo, wakasoma Aya za Mwenyezi Mungu nyakati za usiku huku wakinyenyekea.

﴿يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَأُولَـٰئِكَ مِنَ الصَّالِحِينَ ﴾

114. Wanamwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na wanaamrisha mema na wanakataza mabaya na wanaharakia mambo mema na hao ndio miongoni mwa watu wema.

﴿وَمَا يَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَلَن يُكْفَرُوهُ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالْمُتَّقِينَ ﴾

115.Heri yoyote watakayoifayahaitakataliwa, Na Mwenyezi Mungu anawajua wamchao.

WOTE SI SAWA

Aya 113 -115

LUGHA

Mwenye Majmaul-bayan anasema: Tofauti kati ya neno Sura na Ajala ni kwamba Sura ni kufanya haraka linalojuzu kufanywa, Nako kunasifiwa. Na Ajala ni kufanya haraka jambo lisilofaa kufanywa, nako kunashutumiwa.

MAANA

Aya hizi tatu ziko wazi hazihitaji tafsir, Maana yake kwa ujumla ni kwamba watu wa Kitabu hawako sawa kwamba wote wamepotea, bali wako watu wema miongoni mwao. Wafasiri wengi wamechukulia sifa hii kwa aliyesilimu miongoni mwa watu wa Kitabu, na uzuri wa uislamu wake kimatendo na kiitikadi.

HUKUMU YA MWENYE KUACHA UISLAMU

Mwito wa kumwamini Muhammad kama Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa watu wa ulimwenguni bado upo mpaka Siku ya Mwisho. Nao unaelekezwa kwa watu wote, wa Mashariki na Magharibi. Mwenyezi Mungu anasema:

﴿قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُمْ جَمِيعًا ﴾

"Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu nyote" (7:158).

Dalili ya ukweli wake ni mantiki ya kiakili, kuthibiti muujiza na kufaa dini kwa maisha. Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) anasema: "Msingi wa dini yangu ni akili" Na Mwenyezi Mungu anasema katika Kitabu chake Kitukufu:

﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّـهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ﴾

"Enyi ambao mmeamini muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume (wake) anapowaitia katika yale yatakayowapa maisha (8:24)

Lengo letu sio kutoa dalili za Utume wa Muhammad(s.a.w.w), ([6] ) isipokuwa lengo ni kubainisha kuwa je, asiyeamini Utume wa Muhammad anastahili adhabu: au hapana budi ya ufafanuzi? Kabla ya kumtofautisha mjuzi na asiye mjuzi na asiyemudu na mzembe, tutaonyesha msingi na vipimo vya kwanza vya kustahili adhabu au kutostahili; kutokana na hivyo, uhakika utafumbuka na kuwapambanua watu. Wote wameafikiana kwamba mtu, vyovyote awavyo, dini yoyote aliyo nayo, hastahili adhabu ila baada ya kusimamishiwa hoja. Na hoja haisimami ila baada ya kuweza yeye kufikia kwenye dalili ya haki na kuweza kwake kuitumia. Hapo akiacha hatakuwa na kisingizio. Ikiwa hakupata dalili ya haki yenye msingi au aliipata akashindwa kuifikia au aliifikia na akatekeleza mtazamo wake wa haki mpaka akafikia mwisho, lakini pamoja na hayo haki haikumdhihirikia, basi yeye atakuwa na udhuru, kwa sababu ya kutokamilika hoja juu yake. Kwa sababu, asiyethibitikiwa na haki haadhibiwi kwa kuiacha, ila ikiwa amezembea katika utafiti.

Vile vile miongoni mwa kawaida za msingi ambazo zinaambatana na utafiti huu ni ile ya "Adhabu kuepukwa na mambo yenye kutatiza." Kwa hiyo haijuzu kumhukumu mwenye kuiacha haki kuwa ni mwenye makosa anayestahili adhabu, maadamu tunaona kuwa kuna uwezekano kuwa anao udhuru katika kuacha kwake. Na kawaida hii inafungamana na watu wote, sio waislamu tu, Pia inakusanya aina zote za mipaka, Mfano kawaida ya 'Mwenye kukosea katika ijtihadi, basi kosa lake linasamehewa', Kawaida hii ni ya kiakili, haiwezekani kuihusisha na dini fulani tu, madhehebu, shina au tawi. Baada ya maelezo hayo hebu tuangalie hali hizi zifuatazo:

1) Kuishi binadamu mji ulio mbali na uislamu na waislamu; wala hakufikiliwa na mwito au hata kusikia jina la Muhammad(s.a.w.w) katika maisha yake yote. Pia awe hajawaza kwa karibu au mbali kwamba duniani kuna dini yenye jina la kiislamu na Mtume aitwaye Muhammad(s.a.w.w) . Hapana mwenye shaka kwamba huyu atasamehewa kwa kuwa hastahili adhabu. Maana akili ina hukumu ubaya wa adhabu bila ya ubainifu na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

"Na sisi si wenye kuadhibu mpaka tupeleke Mitume" (17:15) Bila shaka akili ni Mtume wa ndani kwa ndani, ila tu yenyewe ni dalili ya kupatikana Mwenyezi Mungu tu. Ama dalili ya kuthibiti Utume wa Mtume, hapana budi kuwako na muujiza na udhihirishwe na yeye mwenyewe pamoja na akili kuhukumu kutowezekana kudhihiri kwa wasiokuwa Mitume.

2) Kuusikia mtu uislamu na Muhammad, lakini akawa hawezi kupambanua haki na batili, kwa sababu ya kushindwa kwake na kutoweza kufahamu dalili za haki na maarifa yake. Huyu pia anasamehewa, Kwa sababu yeye ni sawa na mtoto au mwenda wazimu. Mfano ni akitomwamini Muhammad(s.a.w.w) tangu udogo kwa kuwafuata wazazi wake na akajisahau alipokuwa mkubwa, akaendelea na itikadi yake bila ya kuitilia shaka yoyote, huyu atasamehewa. Kwa sababu kumkalifisha aliyejisahau asiye na uwezo ni sawa na kumkalifisha aliyelala. Amesema Muhaqqiq Al-Qummi: "Kujikomboa kutokana na kuiga wazazi ni jambo lisilofikiriwa na wengi, bali hata linakuwa zito aghlabu kwa wanavyuoni waliotosheka ambao wanadhani kuwa wamejivua kutokana na kuiga huko." Amesema tena: "Asiyeweza kung'amua wajibu wa kujua misingi, ni sawa na mnyama na mwedawazimu ambao hawana taklifa yoyote." Sheikh Tusi anasema: "Mwenye kushindwa kupata uthibitisho yuko katika daraja ya mnyama."

Hata hivyo, ikiwa aliyejisahau atakumbushwa wajibu wa maarifa, au kuambiwa na mtu: "Wewe uko au hauko sawa katika itikadi yako", lakini pamoja na hayo akang'ang'ania na wala asifanye utafiti na kuuliza, basi huyo atakuwa ni mwenye dhambi, kwa sababu atakuwa ni mzembe, na kutojua kwa mzembe si kisingizio.

3) Kutomwamini Muhammad(s.a.w.w) pamoja na kuwa anao uwezo wa kutosha wa kufahamu haki, lakini yeye alipuuza wala asijali kabisa: au alifanya utafiti pungufu na akauacha bila ya kuangalia mwisho wake; kama wafanyavyo wengi, hasa vijana wa kisasa. Basi huyu hatasameheka kwa sababu amekosea bila ya kujitahidi na alikuwa na uwezo wa kujua haki, lakini akapuuza. Ni wazi kuwa pia ataadhibiwa ambaye amefanya utafiti na akakinai, lakini pamoja na hayo akakataa kumwamini Muhammad(s.a.w.w) kwa ubaguzi na mali.

4).Kuangalia dalili na kuwa na mwelekeo wa kufuata haki kwa ikhlasi, lakini pamoja na hayo akakosa kuelekea kwenye njia ambayo itamwajibishia kumwamini Muhammad(s.a.w.w) ama kwa kushikamana kwake na mambo yenye kutatiza ya ubatilifu bila ya kuangalia ubatilifu wake, au kuchanganyikiwa na mengineyo ambayo yanazuia kuona haki. Huyu ataangaliwa hali yake, ikiwa atakanusha Utume wa Muhammad(s.a.w.w) kwa kauli ya mkato, basi yeye ataadhibiwa na kustahili adhabu. Kwa sababu yule ambaye imefichika kwake haki, haifai kwake kukataa moja kwa moja kukanusha haki. Inawezekana kuwa haki ipo lakini akazuiliwa, kuifika, na aghlabu huwa hivyo, kwa sababu mambo ya ulimwenguni yapo lakini tuyajuayo ni machache tu. Hali ni hivyo hivyo kuhusu kuwajua Mitume na wasuluhishi, Ni nani awezaye kujua kila kitu?

Watu wa mantiki wamelielezea hilo kwa ibara mbali mbali, miongoni mwazo ni: Kutokujua hakumaanishi kutokuwepo, kutopatikana hakumaanishi kuacha kupatikana, kuthibitisha na kukanusha kunahitaji dalili. Tumewaona wanavyuoni wengi wakiungana na hakika hii. Wanazituhumu rai zao na kujichunga katika kauli zao; wala hawajifanyi kuwa wao ndio kipimo cha ukweli. Hawawezi kusema: "Rai hii ni takatifu isiyo na shaka, na nyinginezo si chochote." Bali wao huipa mtazamo wa kujiuliza kila rai. Dalili kubwa zaidi ya kuwa mtu hana elimu, ni kule kujidanganya mwenyewe, kuiona safi elimu yake, na kudharau rai na itikadi za wengine.

Zaidi ya hayo kuacha kukinai mtu mmoja miongoni mwa watu kuhusu Utume wa Muhammad(s.a.w.w) hakumruhusu kukanusha Utume wa Mtume Mtukufu(s.a.w.w) moja kwa moja. Na kama akifanya hivyo, basi atakuwa na jukumu. Hasa baada ya kuona idadi ya mabingwa ambao hawakuathiriwa na kurithi au mazingira, wakimwamini Muhammad na risala yake; si kwa lolote isipokuwa kuiheshimu haki na kuikubali hali halisi ilivyo([7] ) . Hayo ni ikiwa atapinga. Ama akiangalia dalili wala asikinai na pia asipinge; wakati huo huo akawa amenuia kwa moyo safi kuiamini haki wakati wowote itakapomdhihirikia; kama vile mwanafiqh mwadilifu ambaye hufutu jambo kwa nia ya kubadilisha mara tu ikimbainikia kuwa amekosea, basi huyu hatakuwa na jukumu, kwa sababu mwenye kukosea katika ijtihadi yake bila ya kufanya uzembe, hataadhibiwa kwa kukosea kwake; kama inavyohukumu akili na maandishi pia. Imepokewa kutoka kwa Imam Jafar Sadiq(a.s) , amesema:"Lau kama watu wasipofahamu (jambo) wakasimama na wala wasipinge, basi hawakukufuru" Katika Riwaya nyingine: "Hakika anakufuru tu akipinga"

Sheikh Ansari katika kitabu chake maarufu Arrasil mlango wa Dhana katika Usul, anasema: "Hadith nyingi zimefahamisha kuthibiti ukati na kati baina ya kufuru na imani" Ya kwamba mpingaji ni kafiri, mwenye kuitakidi ni Mumin, na mwenye shaka si kafiri wala Mumin. Katika Hadith zinazowezekana kuzitolea dalili ya kutoadhibiwa mwenye kufanya ijitihadi bila ya uzembe kama akikosea katika mambo ya itikadi, ni Hadith hii mashuhuri kwa sunni na shia:"Akijitahidi hakimu na akapata basi atalipwa mara mbili. Na akijitahidi akakosea, basi atalipwa mara moja" Kama mtu akisema kuwa Hadith hii inahusu mwenye kujitahidi katika matawi si katika masuala ya itikadi, kama walivyodai baadhi ya wanavyuoni, basi tutamjibu hivi: Linalomlinda, mwenye kujitahidi katika hukumu, asiadhibiwe ni kule kujichunga kwake na kutofanya uzembe katika utafiti, Na kinga hii inapatikana hasa katika masuala ya kiitikadi.

Zaidi ya hayo Mafaqihi wote wameafikiana kwa kauli moja kwamba mwenye kushindwa kuifikia itikadi ya kweli, anasamehewa. Miongoni mwao ni wale waliohusisha Hadith hii na matawi. Nasi hatuoni tofauti yoyote kati yake na yule mwenye kujitahidi, aliyetoa juhudi zake. Kwa sababu,wote wawili wameshindwa kujua maadam hawakuufikia uhakika. Kwa ufupi ni kwamba mwenye kuipinga, haki yoyote, basi ataadhibiwa, ni sawa awe amejitahidi au la, isipokuwa kama hana maarifa, kama mnyama. Kama akibakia kwenye msimamo wa kutopinga wala kuthibiti sawa, kujitahidi na kuangalia dalili au alifanya ijtihadi pungufu, basi ataadhibiwa. Ikiwa ameangalia dalili akajitahidi mpaka akafikia mwisho wake, basi yeye atasamehewa kwa sharti ya kubakia na mwelekeo wa haki kwa kuazimia kubadili msimamo wake wakati wowote itakapomdhihirikia haki.

Unaweza kuuliza : Umesema kuwa mwenye kushindwa kujua itikadi ya kweli - kama vile Utume wa Muhammad – atasamehewa, Vile vile mwenye kujitahidi ambaye hakuzembea katika jitihadi. Je, maana yake ni kuwa inajuzu kwetu kufanya naye muamala wa kiislamu, kama kuoa, kurithi n.k.

Jibu : Msamaha tunaoukusudia hapa ni kutostahiki adhabu akhera; ama kuoa na kurithi hapa duniani ni jambo jengine. Na kila asiyeamini utume wa Mtume Muhammad(s.a.w.w) kwa hali yoyote atakayokuwa, haifai kuwa na muamala naye wa kiislam k.v. ndoa, urithi n.k. Ni sawa awe kesho atapona au ataangamia; kama ambavyo mwenye kusema "Laila ilaha illa llah Muhammad Rasulullah" anastahiki ya waislamu, ni juu yake yaliyo juu yao, hata kama alikuwa ni fasiki, bali hata mnafiki vile vile.

6

7

8

9