TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA TANO Juzuu 15

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA TANO22%

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA TANO Mwandishi:
: HASANI MWALUPA
Kundi: Qurani tukufu

Juzuu 1 Juzuu 2 Juzuu 3 Juzuu 4 Juzuu 5 Juzuu 6 Juzuu 7 Juzuu 8 Juzuu 12 Juzuu 13 Juzuu 14 Juzuu 15 Juzuu 16 Juzuu 17 Juzuu 18 Juzuu 19 Juzuu 20 Juzuu 21 Juzuu 22 Juzuu 23 Juzuu 24
  • Anza
  • Iliyopita
  • 19 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 17095 / Pakua: 4166
Kiwango Kiwango Kiwango
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA TANO

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA TANO Juzuu 15

Mwandishi:
Swahili

1

2

3

15

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA TANO

وَاضْرِبْ لَهُم مَّثَلَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَاءٍ أَنزَلْنَاهُ مِنَ السَّمَاءِ فَاخْتَلَطَ بِهِ نَبَاتُ الْأَرْضِ فَأَصْبَحَ هَشِيمًا تَذْرُوهُ الرِّيَاحُ وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ مُّقْتَدِرًا ﴿٤٥﴾

45. Na wapigie mfano wa maisha ya dunia ni kama maji tuliyoyateremsha kutoka mbinguni yakachanganyika na mimea ya ardhi ikawa majani makavu yaliyokatikakatika yanayopepeprushwa na upepo, Na Mwenyezi Mungu ana uwezo juu ya kila kitu.

الْمَالُ وَالْبَنُونَ زِينَةُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ خَيْرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ أَمَلًا ﴿٤٦﴾

46. Mali na watoto ni pambo la maisha ya dunia. Na vibakiavyo vizuri ndivyo bora mbele ya Mola wako na kwa malipo na tumaini bora.

PAMBO LA MAISHA YA DUNIA

Aya 45 – 46

MAANA

Na wapigie mfano wa maisha ya dunia ni kama maji tuliyoyateremsha kutoka mbinguni yakachanganyika na mimea ya ardhi ikawa majani makavu yaliyokatikakatika yanayopepeprushwa na upepo.

Dunia ni nzuri yenye mandhari ya kijani ya kupendeza, lakini ina ghururi na madhara. Haina kheri katika akiba yake isipokuwa takua; kama alivyosema Imam Ali(a.s) .

Haya ndiyo maana ya Aya; ambapo Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameifananisha dunia, katika uzuri wake, na mvua iliyonyesha kwenye ardhi ikairutubisha na ikaota miti ya kila aina, lakini mara inageuka na kuwa kame, majani yakawa makavu yanayopukusika yakirushwa na upepo. Hivi ndivyo yalivyo maisha ya dunia, ni mazuri lakini yameficha ubaya.

Na Mwenyezi Mungu ana uwezo juu ya kila kitu.

Anaweza kuuondoa ulimwengu na kuumaliza kabisa; kama alivyoweza kuumba na kuuleta. Anasema Ibnul Arabi katika kitabu Futahitl-Makkiyya “Mwenyezi Mungu ni muweza wa mambo na ana uwezo wa kuumba” Anakusudia kuwa Mwenyezi Mungu anasifika kuwa ni muweza pale anapotaka kitu kuwa kikawa, ni sawa aseme au asieme na anasifika kuwa ana uweza pale anaposema na kitu kikawa vilevile.

MALI NA WATOTO NI PAMBO LA MAISHA YA DUNIA

Mali na watoto ni pambo la maisha ya dunia.

Pambo la maisha liko aina mbili: La umma na la kibinafsi. La umma ni kama vile kujenga njia za mawasiliano; mfano barabara n.k. Au taasisi; mfano kujenga vyuo vikuu, vituo vya malezi ya watoto viwanda n.k.

Na la kibinafsi ni kama nyumba, gari, mtoto mtiifu aliyefaulu, viwanda, umaarufu katika jamii n.k. Vipambo hivi sio haramu. Vitakuwaje haramu na hali Yeye ndiye aliyesema:

قُلْ مَنْ حَرَّمَ زِينَةَ اللَّـهِ الَّتِي أَخْرَجَ لِعِبَادِهِ وَالطَّيِّبَاتِ مِنَ الرِّزْقِ ﴿٣٢﴾

“Sema: Ni nani aliyeharamisha pambo la Mwenyezi Mungu ambalo amewatolea waja wake, na vilivyo vizuri katika riziki?” Juz. 8 (7:32).

Lakini pambo binafsi halistahili mtu kujitukuza na kujifaharisha nalo. Kwa sababu kipimo cha kutukuzwa pambo ni kwa manufaa ya umma na kubakia vizazi na vizazi. Hili ndilo alilolikusudia Mwenyezi Mungu pale aliposema:

Na vibakiavyo vizuri ndivyo bora mbele ya Mola wako na kwa malipo na tumaini bora.

Kwa sababu mwenye kutekeleza atapata huko Akhera yale aliyoyatumai, mbali ya kupata heshima na kuendelea kutajika katika maisha haya ya dunia.

Kwa ufupi ni kuwa mali ni nyenzo sio lengo. Inapimwa na kukadiriwa kwa natija yake na athari yake. Ikiwa ni kheri itakuwa kheri na ikiwa ni shari basi itakuwa shari. Ikitumika kwa njia ya shari na ufisadi, kama vile mashindano ya silaha, basi itakuwa mali ni shari na ikitumika katika kutekeleza mahitaji, basi mali itkuwa ni kheri.

Na kheri hiyo iko aina mbili: Ikiwa itamletea manufaa mwenye nayo au kumkinga na madhara basi itakuwa ya binafsi na itaisha kwa kuisha. Lakini ikiwa manufaa yake ni kwa umma basi itakuwa ni katika vibakiavyo vizuri.

وَيَوْمَ نُسَيِّرُ الْجِبَالَ وَتَرَى الْأَرْضَ بَارِزَةً وَحَشَرْنَاهُمْ فَلَمْ نُغَادِرْ مِنْهُمْ أَحَدًا ﴿٤٧﴾

47. Na siku tutakayoipitisha milima na utaiona ardhi iwazi. tutawafufua wala hatuta- muacha yeyote katika wao.

وَعُرِضُوا عَلَىٰ رَبِّكَ صَفًّا لَّقَدْ جِئْتُمُونَا كَمَا خَلَقْنَاكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ بَلْ زَعَمْتُمْ أَلَّن نَّجْعَلَ لَكُم مَّوْعِدًا ﴿٤٨﴾

48. Na watahudhurishwa mbele ya Mola wako kwa safu. Hakika mmetufikia kama tulivyowaumba mara ya kwanza; bali mlidai kuwa hatutawawekea miadi.

وَوُضِعَ الْكِتَابُ فَتَرَى الْمُجْرِمِينَ مُشْفِقِينَ مِمَّا فِيهِ وَيَقُولُونَ يَا وَيْلَتَنَا مَالِ هَـٰذَا الْكِتَابِ لَا يُغَادِرُ صَغِيرَةً وَلَا كَبِيرَةً إِلَّا أَحْصَاهَا وَوَجَدُوا مَا عَمِلُوا حَاضِرًا وَلَا يَظْلِمُ رَبُّكَ أَحَدًا ﴿٤٩﴾

49. Na kitabu kitawekwa ndipo utawaona waovu wakiogopa kwa sababu ya yale yaliyomo. Na watasema: “Ole wetu! Kina nini kitabu hiki hakiachi dogo wala kubwa ila kinalihesabu? Na watakuta waliyoyafanya yamehudhurishwa, Na Mola wako hadhulumu yoyote.

TUTAWAFUFUA WALA HATUTAMUACHA YEYOTE

Aya 47 -49

MAANA

Na siku tutakayoipitisha milima na utaiona ardhi i wazi.

Ardhi hii tunayoishi leo, Mwenyezi Mungu ameitaja katika Aya nyingi, miongoni mwazo ni hii tuliyo nayo. Hapa Mwenyezi Mungu ameisifu kwa sifa mbili:

Kwanza, kuwa Mwenyezi Mungu ataing’oa milima mahali ilipo na aipeleke kama mawingu, Sifa ya pili, kwamba ardhi yote kuanzia pembe hadi pembe itakuwa wazi bila ya kuweko kizuizi chochote. Hapo ndio itakuwa ufufuo ambao Mungu ameuashiria kwa kusema:

Na tutawafufua wala hatutamuacha yeyote katika wao.

Mwenyezi Mungu atawafufua wote, kuanzia wa kwanza hadi wa mwisho, kwa ajili ya hisabu.

Na watahudhurishwa mbele ya Mola wako kwa safu.

Huko nyuma tumetaja kuwa hisabu na malipo ni kweli isiyokuwa na shaka. Tumelithibitisha hilo kwa dalili mkataa, katika kufasiri Aya zinazoonyesha hivyo; miogoni mwazo ni, Juz; 11 (10:4) kifungu cha ‘Hisabu na malipo ni lazima’.

Aya tuliyo nayo inasema kuwa viumbe watahudhurishwa kwa Mungu kesho wakiwa wamepiga safu. Makusudio ya kuhudhurishwa hapa ni kusimama kwa Mungu kwa ajili ya hisabu.

Ama kuhusu neno safu, wafasiri wametofautiana; wengine wameliacha neno na dhahiri yake, wengine wakaleta sarufi na kulichukulia tamko yale yasiyowezekana. Tuonavyo sisi ni kuwa safu ni fumbo la utaratibu na nidhamu, kwamba viumbe watahudhurishwa kwa mola wao kwa mpangilio madhubuti.

Hakika mmetufikia kama tulivyowaumba mara ya kwanza; bali mlidai kuwa hatutawawekea miadi.

Hivi ndivyo atakavyoanza Mwenyezi Mungu kuwahukumu wale waliokuwa wakipinga ufufuo: Tuliwatoa matumboni mwa mama zetu mkiwa uchi hamna chochote; vilevile leo tumewatoa makaburini mwenu. Hakuna tofauti isipokuwa pale mwanzo mlikuwa hamuulizwi chochote na leo mmetolewa ili muulizwe yale mliyokuwa mkiyafanya, kuyaamini na kuyasema. Miongoni mwayo ni kusema kwenu kuwa ufufuo ni uzushi na vigano. Je, mmeona leo?

Na kitabu kitawekwa ndipo utawaona waovu wakiogopa kwa sababu ya yale yaliyomo.

Hii ndiyo Siku ya Ufufuo mliyokuwa mkiikadhibisha, Kila mmoja atapewa daftari la matendo yake na aambiwe:

اقْرَأْ كِتَابَكَ كَفَىٰ بِنَفْسِكَ الْيَوْمَ عَلَيْكَ حَسِيبًا ﴿١٤﴾

“Soma kitabu chako! Nafsi yako leo inakutosha kukuhisabu” (17:14)

Yaani soma daftari la matendo yako na ujipigie mahisabu wewe mwenyewe. Atasoma huku akitetemeka kwa hofu isiyokuwa na matumini yoyote wala matarajio ya kuokoka. Lau angeliogopa adhabu tangu mwanzo na kajiepusha na njia yake, angelikuwa leo yuko kwenye amani na sala- ma. Lakini alijiaminisha huko na anahofu hapa.

Na watasema: ole wetu! Kina nini kitabu hiki hakiachi dogo wala kubwa ila kinalihesabu?

Hapo mwanzo walikuwa wakisema hakuna kitabu wala hisabu.

Na watakuta waliyoyafanya yamehudhurishwa, bila ya kuzidi wala kupungua; Kwanini isiwe hivyona Mola wako hadhulumu yoyote ? Si kwenye thawabu wala adhabu; bali huwa zikaongezwa thawabu kwa mwenye kufanya wema na kusamehewa mwenye kufanya uovu.

وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ كَانَ مِنَ الْجِنِّ فَفَسَقَ عَنْ أَمْرِ رَبِّهِ أَفَتَتَّخِذُونَهُ وَذُرِّيَّتَهُ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِي وَهُمْ لَكُمْ عَدُوٌّ بِئْسَ لِلظَّالِمِينَ بَدَلًا ﴿٥٠﴾

50. Na tulipowaambia Malaika: Msujudieni Adam! Walimsujudia isipokuwa Iblis. Alikuwa miongni mwa majini akatoka kwenye amri ya Mola wake. Je, mnamfanya yeye na dhuria zake kuwa mawalii badala yangu, hali wao ni adui zenu? Ni uovu mno badala hii kwa wenye kudhulumu.

مَّا أَشْهَدتُّهُمْ خَلْقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَا خَلْقَ أَنفُسِهِمْ وَمَا كُنتُ مُتَّخِذَ الْمُضِلِّينَ عَضُدًا ﴿٥١﴾

51. Si kuwashuhudisha kuumbwa kwa mbingu na ardhi wala kuumbwa kwa nafsi zao. Wala sikuwafanya wapotezao kuwa ni mkono.

وَيَوْمَ يَقُولُ نَادُوا شُرَكَائِيَ الَّذِينَ زَعَمْتُمْ فَدَعَوْهُمْ فَلَمْ يَسْتَجِيبُوا لَهُمْ وَجَعَلْنَا بَيْنَهُم مَّوْبِقًا ﴿٥٢﴾

52. Na siku atakaposema waiteni hao mliodai kuwa ni washirika wangu, Basi watawaita nao hawatawaitikia. Nasi tutaweka baina yao maangamizi.

وَرَأَى الْمُجْرِمُونَ النَّارَ فَظَنُّوا أَنَّهُم مُّوَاقِعُوهَا وَلَمْ يَجِدُوا عَنْهَا مَصْرِفًا ﴿٥٣﴾

53. Na wahalifu wataona moto na watadhani kuwa wao watauingia wala hawatapata pa kuepukia.

WALISUJUDI ISIPOKUWA IBLISI

Aya 50 – 53

MAANA

Na tulipowaambia Malaika: Msujudieni Adam! Walimsujudia isipokuwa Iblis;

Umetangulia mfano wake katika Juz. 1(2:11), Juz. 8 (7:11) na Juzuu hii ya 15 (17: 61).

Alikuwa miongoni mwa majini akatoka kwenye amri ya Mola wake.

Yaani alitoka kwenye twaa ya mola wake. Mara nyingi tumesema kuwa sisi tunaamini kuweko majini, kwa sababu wahyi unathibitisha hilo na akili haipingi hilo; na kwamba ufafanuzi wake tunamwachia Mjuzi wa ghaibu.

Je, mnamfanya yeye na dhuria zake kuwa mawalii badala yangu?

Qur’an huwa inajifasiri yenyewe na sehemu moja inaitolea ushahidi sehemu nyingine. Katika Aya nyingi imeleta ibara ya kuwa wale wanaoichanganya haki na batili kuwa ni askari wa Iblisi na mawalii wake.

Kwa hiyo hapa inafaa kufasiri kuwa dhuria za Iblisi ni askari wake na wazaidizi wake na kwamba kizazi cha Ibilisi, askari wake na mawalii wake, ni wale wanaoichanganya batili na uongo na kuzulia haki. Sio mbali kwamba ibara ya kuwa hao ni dhuria za Ibilisi, ni kufanana vitendo vyao na vyake.

La kushangaza ni kauli ya asemaye kuwa Ibilisi ana tupu ya kiume katika paja lake la kuume na tupu ya kike katika paja lake la kushoto. Kwa hiyo aniingiza ya kiume kwenye hiyo ya kike na anapata kizazi na dhuria

Hali wao ni adui zenu?

Kila anayekupambapamba na kukudanganya na mambo ya batili au kukusifia mambo usiyokuwa nayo, basi huyo ni adui yako, ujue hilo au usijue.

Ama yule anayezua vigano juu ya Ibilisi na wengineo, basi huyo ni adui wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na pia wa ubinadamu.

Ni uovu mno badala hii kwa wenye kudhulumu.

Madhalimu ni wale wanaobadilsha twaa ya Mwenyezi Mungu kuwa twaa ya shetani; miongoni mwao ni wale wanaowachagua wafisadi kwenye vyeo na kuwafidhilisha kuliko watu wema.

Si kuwashuhudisha kuumbwa kwa mbingu na ardhi wala kuumbwa kwa nafsi zao. Wala sikuwafanya wapotezao kuwa ni mkono.

Ambao hawakushuhudishwa ni ibilisi na dhuria zake. Makusudio ya mkono hapa ni usaidizi. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) akilitaka jambo ni kuliambia kuwa kisha likawa, hamshauri wala hamtaki msaada yeyote, kwa sababu yeye hawahitajii walimwengu.

Na wakati alipoumba vitu hakumuhudhurisha yeyote katika wao, hata kama ni mwenye takua zaidi ya wote; sikwambii tena akiwa ni mpotezaji; kama vile Ibiisi na askari wake. Madamu mambo yako hivyo, imekuwaje kuasiwa muumbaji na kutiiwa yule ambaye hawezi kujisaidia hata yeye mwenyewe au kujikinga na madhara?

Na siku atakaposema waiteni hao mliodai kuwa ni washirika wangu, Basi watawaita nao hawatawaitikia. Nasi tutaweka baina yao maangamizi.

Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu kesho atawaambia wale waliokuwa wakimfanyia washirika katika twaa yake: wako wapi wale ambao mliwatii na mkadai kuwa wao watawapa manufaa siku hii ya lo ngumu? Hebu waiteni tuone kama watawaitikia. Hapana! Wenyewe wana shughuli inayowashughulisha; wako katika adhabu ya moto, Kauli yake Mwenyezi Mungu kuwa watawaita na wasiwasikie ni fumbo la kukata kwao tamaa kwa matarajio waliyokuwa wakiyatarajia.

Na wahalifu wataona moto na watadhani kuwa wao watauingia wala hawatapata pa kuepukia.

Makusudio ya kudhani hapa ni kujua na kuwa na yakini. Pia kuepukia ni kuepuka na moto. Kukimbia kesho ni sawa na kujaribu kuyakimbia mauti leo hapa duniani.

وَلَقَدْ صَرَّفْنَا فِي هَـٰذَا الْقُرْآنِ لِلنَّاسِ مِن كُلِّ مَثَلٍ وَكَانَ الْإِنسَانُ أَكْثَرَ شَيْءٍ جَدَلًا ﴿٥٤﴾

54. Na hakika tumewaeleza watu katika hii Qur’an kila aina ya mifano. Lakini mtu amezidi kila kitu kwa ubishi.

وَمَا مَنَعَ النَّاسَ أَن يُؤْمِنُوا إِذْ جَاءَهُمُ الْهُدَىٰ وَيَسْتَغْفِرُوا رَبَّهُمْ إِلَّا أَن تَأْتِيَهُمْ سُنَّةُ الْأَوَّلِينَ أَوْ يَأْتِيَهُمُ الْعَذَابُ قُبُلًا ﴿٥٥﴾

55. Na hapana kilichowazuia watu kuamini ulipowajia uongofu na kuomba maghu- fira kwa Mola wao; isipokuwa yawafikie ya wale wa zamani au iwajie adhabu waziwazi.

وَمَا نُرْسِلُ الْمُرْسَلِينَ إِلَّا مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ وَيُجَادِلُ الَّذِينَ كَفَرُوا بِالْبَاطِلِ لِيُدْحِضُوا بِهِ الْحَقَّ وَاتَّخَذُوا آيَاتِي وَمَا أُنذِرُوا هُزُوًا ﴿٥٦﴾

56. Na hatuwatumi Mitume ila wawe wabashiri na waonyaji. Na waliokufuru wanabishana kwa batili, ili waivunje haki kwayo, na wanazifanya ishara zangu na yale waliyoonywa, kuwa ni mzaha.

MTU NI MBISHI SANA

Aya 54 – 56

MAANA

Na hakika tumewaeleza watu katika hii Qur’an kila aina ya mifano, Lakini mtu amezidi kila kitu kwa ubishi.

Makusudio ya mtu hapa sio kila mtu bali ni watu wengi zaidi, kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu kwenye Aya kadhaa: “Watu wengi hawana akili” “watu wengi hawajui” watu wengi hawaamini” n.k. Qur’an ni kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa waja wake, kinachowaongoza kwa dalili zake na mawaidha yake na kuhimiza kushikamana na hukumu zake na mafundisho yake.

Mwenyezi Mungu amefafanua mawaidha na dalilil hizi kwa mifumo mbalimbali na akazipigia mifano mbalimbali; ikiwemo ile ya watu wawili waliotajwa katika Aya ya 32 ya Sura hii na kufananisha maisha na maji katika Aya ya 54. lakini watu hawatii akilini na wanabishana katika mambo yaliyo wazi, wakijaribu kubatishilisha haki kwa mambo ya uongo na ya kupambamba.

Na hapana kilichowazuia watu kuamini ulipowajia uongofu na kuomba maghufira kwa Mola wao; isipokuwa yawafikie ya wale wa zamani au iwajie adhabu waziwazi.

Makusudio ya uongofu ni Qur’an na ubanifu wake ulio wazi. kuomba maghufira ni kutubia na yaliyowafikia wa zamani ni maangamivu; kama yaliyowafikia kaumu ya Nuh, Lut, A’d na Thamud.

Maana ni kuwa washirikina hawajaribu kuamni au kufikiria kuamni mpaka wapatikane na moja wapo ya mambo mawili: Kwanza ni kushukiwa na adhabu ya kuwafyeka; kama ilivyowashukia waliokuwa kabla yao; ndipo wataamni; ambapo imani, wakati huo, haifai kitu; kama Firauni ambaye aliamini alipoona maangamizi na kufa maji kunafika. Jambo la pili ni kuiona adhabu ana kwa ana.

Kwa maneno mengine ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) alipobainisha, katika aya zilizotangulia, kuwa Yeye ameleta dalii zilizo waziwazi na watu wengi wakakataa isipokuwa ubishi, sasa anasema kuwa dalili hizi hazifai kitu kwa watu wasioamini isipokuwa wakati wa kukata roho au wanapotishika na adhabu wanapoiona kwa macho yao au wanapoamini kuwa itawafikia tu.

Na hatuwatumi Mitume ila wawe wabashiri na waonyaji.

Huu ndio umuhimu wa Mtume kumpa habari njema ya neema yule mwenye kutii na kumuonya na adhabu yule mwenye kuasi, Maana haya yamekaririka mara nyingi. Tazama Juz. 6 (4:165).

Na waliokufuru wanabishana kwa batili, ili waivunje haki kwayo na wanazifanya ishara zangu na yale waliyoonywa, kuwa ni mzaha.

Ameziweka wazi ishara na akazithibitisha kwa ubainifu na dalili, lakini waliokufuru wakabishana na wakajaribu kuzibatilisha kwa uongo na mizaha. Makusudio ya kuzifanyia mizaha ishara za Mwenyezi Mungu hapa sio mizaha ya kusema tu; bali ni kuwa kila mweye kuijua hukumu, miogoni mwa hukumu za Mwenyezi Mungu, na asiitumie, basi yeye ni katika walioifanya Qur’an na dini ya Mwenyezi Mungu kuwa ni mchezo.

Imam Ali(a.s) anasema:“Mwenye kuisoma Qur’an, kisha akafa akaingia motoni – kwa kutoitumia Qur’an – basi huyo ni katika waliozifanyia mzaha ishara za Mwenyezi Mungu.

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن ذُكِّرَ بِآيَاتِ رَبِّهِ فَأَعْرَضَ عَنْهَا وَنَسِيَ مَا قَدَّمَتْ يَدَاهُ إِنَّا جَعَلْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ أَكِنَّةً أَن يَفْقَهُوهُ وَفِي آذَانِهِمْ وَقْرًا وَإِن تَدْعُهُمْ إِلَى الْهُدَىٰ فَلَن يَهْتَدُوا إِذًا أَبَدًا ﴿٥٧﴾

57. Na ni nani dhalimu zaidi kuliko yule anayekumbushwa ishara za Mola wake na akazipuuza na akasahau yaliyotangulizwa na mikono yake? Hakika tumeweka vifuniko juu ya nyoyo zao wasije wakaifahamu, na tumeweka kwenye masikio yao uziwi, Na ukiwaita kwenye uongofu hawataongoka kabisa.

وَرَبُّكَ الْغَفُورُ ذُو الرَّحْمَةِ لَوْ يُؤَاخِذُهُم بِمَا كَسَبُوا لَعَجَّلَ لَهُمُ الْعَذَابَ بَل لَّهُم مَّوْعِدٌ لَّن يَجِدُوا مِن دُونِهِ مَوْئِلًا ﴿٥٨﴾

58. Na Mola wako ni mwenye maghufira na mwenye rehema, lau angeliwachukulia kwa walioyachuma, bila shaka angeliwafanyia haraka kuwaadhibu, Lakini wana miadi ambayo hawatapata kimbilio la kuepukana nayo.

وَتِلْكَ الْقُرَىٰ أَهْلَكْنَاهُمْ لَمَّا ظَلَمُوا وَجَعَلْنَا لِمَهْلِكِهِم مَّوْعِدًا ﴿٥٩﴾

59. Na miji hiyo tuliwaangamiza walipodhulumu na tukawawekea miadi ya maangamizo yao.

ALIYEKUMBUSHWA ISHARA ZA MOLA WAKE AKAZIKATAA

Aya 57 – 59

MAANA

Na ni nani dhalimu zaidi kuliko yule anayekumbushwa ishara za Mola wake na akazipuuza na akasahau yaliyotangulizwa na mikono yake?

Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameziweka wazi dalili za kuweko kwake na wajibu wa kumtii Yeye kwa mifumo mbali mbali; kisha akapiga mifano mingi ya hayo. Akamwamrisha mtu kufanya kheri na kutubia dhambi zake zilizopita, akamkataza shari na akamuhadharisha kukhalifu amri na makatazo na kuendelea na dhambi. Lakini mtu ameyapuuza yote hayo na akaitia nafsi yake kwenye maangamivu.

Hakika tumeweka vifuniko juu ya nyoyo zao wasije wakaifahamu na tumeweka kwenye masikio yao uziwi.

Umetangula mfano wake pamoja na tafsiri katika Juz. 7 (6:25) na Juz. hii ya 15 (17: 46).

Na ukiwaita kwenye uongofu hawataongoka kabisa.

Wataongoka vipi na hali kwenye nyoyo zao kuna vifuniko na kwenye masikio yao kuna uziwi. Kila asiyenufaika na mawaidha mazuri, basi huyo ni sawa na kipofu wa moyo na macho na ni kiziwi.

Na Mola wako ni mwenye maghufira na mwenye rehema, lau angeliwachukulia kwa walioyachuma, bila shaka angeliwafanyia haraka kuwaadhibu.

Umetangula mfano wake pamoja na tafsiri katika Juz. 14 (16:61).

Lakini wana miadi ambayo hawatapata kimbilio la kuepukana nayo.

Mausudio ya miadi hapa ni wakati wa kufika mbele ya Mwenyezi Mungu, Ni miadi isiyovunjwa wala kukimbiwa.

Imam Ali (a.s) anasema kumwambia Mola wake:“Wewe ni wa milele huna muda na wewe ni mwishilio usioepukwa na wewe ni ahadi isiyokimbiwa. Uko mikononi mwako utosi wa kila mnyama na kwako ni marejeo ya kila nafsi.”

Na miji hiyo tuliwaangamiza walipodhulumu na tukawawekea miadi ya maangamizo yao.

Makusudio ya miji hapa ni ya kina A’d,Thamud na wengineo katika umma zilizopita. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu alijaalia wakati maalum wa kuaangamia madhalimu, ukifika hawatachelewa hata saa moja wala hawatatangulizwa.

16

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA TANO

وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِفَتَاهُ لَا أَبْرَحُ حَتَّىٰ أَبْلُغَ مَجْمَعَ الْبَحْرَيْنِ أَوْ أَمْضِيَ حُقُبًا ﴿٦٠﴾

60. Na pale Musa alipomwambia kijana wake: Sitaacha kuendelea mpaka nifike makutano ya bahari mbili au nitaendelea kwa muda mrefu.

فَلَمَّا بَلَغَا مَجْمَعَ بَيْنِهِمَا نَسِيَا حُوتَهُمَا فَاتَّخَذَ سَبِيلَهُ فِي الْبَحْرِ سَرَبًا ﴿٦١﴾

61. Basi wawili hao walipofika makutano ya bahari mbili, walimsahau samaki wao, naye akashika njia yake kuponyokea baharini.

فَلَمَّا جَاوَزَا قَالَ لِفَتَاهُ آتِنَا غَدَاءَنَا لَقَدْ لَقِينَا مِن سَفَرِنَا هَـٰذَا نَصَبًا ﴿٦٢﴾

62. Waliopokwishapita alimwambia kijana wake: Tupe chakula chetu cha mchana. Kwa hakika tumepata machovu sana kwa hii safari yetu.

قَالَ أَرَأَيْتَ إِذْ أَوَيْنَا إِلَى الصَّخْرَةِ فَإِنِّي نَسِيتُ الْحُوتَ وَمَا أَنسَانِيهُ إِلَّا الشَّيْطَانُ أَنْ أَذْكُرَهُ وَاتَّخَذَ سَبِيلَهُ فِي الْبَحْرِ عَجَبًا ﴿٦٣﴾

63. Akasema: Waona! Pale tulipopumzika penye jabali basi mimi nilimsahau samaki, na hapana aliyenisahaulisha nisimkumbuke ila shetani tu. Naye akashika njia yake baharini kwa ajabu

قَالَ ذَٰلِكَ مَا كُنَّا نَبْغِ فَارْتَدَّا عَلَىٰ آثَارِهِمَا قَصَصًا ﴿٦٤﴾

64. Akasema: Hayo ndiyo tuliyokuwa tunayataka. Basi wakarudi kwa kufuata nyayo zao.

MUSA NA MAKUTANO YA BAHARI MBILI

Aya 60 – 64

LUGHA

Kijana wake, anaweza kuwa mwenzake au mtumishi wae, Makutano ya bahari mbili ni mahali zinapokutana bahari mbili na kuwa moja. Inasemekana hapo palikuwa ni makutano ya bahari nyeupe na bahari nyekundu. Kama ningekuwa mtalamu wa jografia, ningelichanganya kauli zote kisha nikachagua iliyo sahihi zaidi.

MAANA

Na pale Musa alipomwambia kijana wake: Sitacha kuendelea mpaka nifike makutano ya bahari mbili au nitaendelea kwa muda mrefu, Basi wawili hao walipofika makutano ya bahari mbili, walimsahau samaki wao, naye akashika njia yake kuponyokea baharini.

Wametofautiana kuhusu Musa, mhusika mkuu wa kisa hiki; kuwa je, ni Musa bin Imran au ni mwenginewe. Amenukuu Razi kutoka kwa Mayahudi kwamba ni Musa bin Misha bin Yusuf bin Ya’qub. Huyo ni wa mbele kuliko Musa bin Imran. Wafasiri wengi wamesema kuwa ni yule mashuhuri, Musa bin Imran, Hiyo ndiyo kauli iliyo dhahiri.

Kuhusu kijana wake, kauli iliyo maarufu ni Yoshua bin Nun, mtoto wa dada yake Musa bin Imran, mwanaafunzi wake wa karibu na khalifa wake kwa wana wa Israil. Ama yule aliyeambiwa na Musa kuwa nikufuate, kauli maarufu ni Khidhr. Lakini Mwenyezi Mungu amelinyamazia jina la kijana na la aliyemfuata. Kwa hiyo sisi tutajumlisha kwa kusema huyu ni kijana wake na yule ni swahibu wake.

Imesemekana kuwa Khidhr sio jina lake hasa bali ni msimbo. Jina lake hasa ni Fabiliya bin Malkan, Wametofautiana kuhusu kuwa je, yeye alikuwa Mtume au walii? Pia imesemekana kuwa yeye ni katika waliope- wa umri mrefu na kwamba yuko hai hadi siku ya ufufuo.

Ama sisi tunalazimika kunyamaza kuhusu utume wake na uhai wake, kwa vile hakuna dalili ya kukata shaka kutoka katika Qur’an wala Hadithi inayohusiana na mojawapo ya hayo mawili. Wala hayo hayahusiki na itikadi yetu au maisha yetu. Wengine wamesema kuwa ni Malaika. Hiyo ni kauli ya mbali sana.

Kuna riwaya inayosema kuwa mtu mmoja alimuuliza Musa: “Ni nani mwenye elimu zaidi?” Musa akasema ni mimi.

Ndipo Mwenyezi Mungu (s.w.t) akataka kumfundisha kuwa juu ya kila mjuzi kuna mjuzi zidi; Kwa hiyo akampa wahyi kwamba katika makutano ya bahari mbili kuna mtu anajua ambayo huyajui, Musa akasema nitaku- tana naye vipi? Mungu akasema, chukua samaki asiyekuwa na uhai na utakapomkosa samaki huyo, basi hapo ndio kuna huyo mjuzi.

Basi Musa akamchukua samaki na akongozana na kijana wake. Akaenda mpaka Musa akachoka, akapumzika na akapata lepe la usingizi. Wakati akiwa amelala yule samaki akapata uhai na akaingia baharini. Hii ni katika miujiza ya Mwenyezi Mungu kwa Musa.

Ikiwa riwaya hii imetegema hali halisi au imetolewa kwenye maelezo ya Aya, lakini inatoa mwanga wa Aya za kisa hiki.

Walipokwishapita alimwambia kijana wake: Tupe chakula chetu cha machana. Kwa hakika tumepata machovu sana kwa hii safari yetu.

Baada ya Musa na kijana wake kupumzika kidogo kwenye makutano ya bahari mbili, walianza upya safari yao. Mpaka wakachoka na kuhisi njaa. Musa akataka chakula kutoka kwa kijana wake. Yule kijana alishuhudia miujiza ya samaki kupata uhai na kuingia baharini, lakini akasahau kumwambia Musa. Musa alipomtaka chakula ndio akakumbuka na akasema:

Waona! Pale tulipopumzika penye jabali basi mimi nilimsahau samaki, na hapana aliyenisahaulisha nisimkumbuke ila shetani tu. Naye akashika njia yake baharini kwa ajabu.

Musa aliposikia maneno hayo akaona dalili za kupata yale aliyoyataka na akasema: Hayo ndiyo tuliyokuwa tunayataka. Basi wakarudi kwa kufuata nyayo zao. Yaani Musa na kijana wake wakarudi nyuma pale alipoingia baharini kwa kufuata ile njia yao ya kwanza.

فَوَجَدَا عَبْدًا مِّنْ عِبَادِنَا آتَيْنَاهُ رَحْمَةً مِّنْ عِندِنَا وَعَلَّمْنَاهُ مِن لَّدُنَّا عِلْمًا ﴿٦٥﴾

65. Basi wakamkuta mja miongoni mwa waja wetu tuliyempa rehema kutoka kwetu na tukamfunza elimu kutoka kwetu.

قَالَ لَهُ مُوسَىٰ هَلْ أَتَّبِعُكَ عَلَىٰ أَن تُعَلِّمَنِ مِمَّا عُلِّمْتَ رُشْدًا ﴿٦٦﴾

66. Musa akamwambia: Je, nikufuate ili unifunze katika ule uongofu uliofunzwa?

قَالَ إِنَّكَ لَن تَسْتَطِيعَ مَعِيَ صَبْرًا ﴿٦٧﴾

67. Akasema: Hakika wewe hutaweza kuvumilia kuwa pamoja nami.

وَكَيْفَ تَصْبِرُ عَلَىٰ مَا لَمْ تُحِطْ بِهِ خُبْرًا ﴿٦٨﴾

68. Na utawezaje kuvumilia yale usiyokuwa na habari nayo?

قَالَ سَتَجِدُنِي إِن شَاءَ اللَّـهُ صَابِرًا وَلَا أَعْصِي لَكَ أَمْرًا ﴿٦٩﴾

69. Akasema: Inshallah utaniona ni mvumilivu wala sitoasi amri yako.

قَالَ فَإِنِ اتَّبَعْتَنِي فَلَا تَسْأَلْنِي عَن شَيْءٍ حَتَّىٰ أُحْدِثَ لَكَ مِنْهُ ذِكْرًا ﴿٧٠﴾

70. Akasema: Basi ukinifuata, usiniulize kitu mpaka nianze kukutajia.

MUSA ANAKUTANA NA SWAHIBU YAKE

Aya 65 – 70

MAANA

Basi wakamkuta mja miongoni mwa waja wetu tuliyempa rehema kutoka kwetu na tukamfunza elimu kutoka kwetu. Musa akamwambia: Je, nikufuate ili unifunze katika ule uongofu uliofun- zwa?

Makusudio ya ‘elimu kutoka kwetu’ ni baadhi ya elimu. Na makusudio ya elimu ni elimu ya ghaibu; yaani tulimpa kitu katika elimu ya ghaibu, akiishiria hilo kwa kuitoboa safina, na kumuua kijana. Masufi wanategemea Aya hii kusahihisha madhehebu yao wanaposema elimu ya kupewa; yaani kuwa na elimu bila ya kusoma.

Maana ni kuwa Musa na kijana wake waliporudi mpaka mahali walipop- umzika mwanzo, walimkuta mtu mingoni mwa waja wema wa Mwenyezi Mungu, aliyepewa rehema na Mwenyezi Mungu na akamneemesha elimu ya kutosha yenye kunufaisha, Musa akamwamkia, naye akamrudishia salam. Musa akamuambia wewe ndiye niliyekuwa nakutaka je, utaniruhusu niandamane nawe na unifundishe uongofu uliofunzwa ninufaike nao?

Wanodai kuwa mtu huyo alikuwa Mtume, wanatoa dalii kwa kauli hii ya Mwenyezi Mungu: ‘tuliyempa rehema kutoka kwetu’ kwa sababu rehema ni utume.

Lakini wamesahau kuwa rehema inaenea kwenye mambo mengine zaidi ya utume; na kupatikana inayoenea zaidi haifahamishi kupatikana mahsusi. Ukisema nimekula tunda, haifahamishi kuwa lazima uwe umekula zabibu, inawezekana ni aina nyingine ya tunda.

Akasema: Hakika wewe hutaweza kuvumilia kuwa pamoja nami. Na utawezaje kuvumilia yale usiyokuwa na habari nayo?

Yule mtu mwema alimwambia Musa kuwa lau utafuatana nami utaonamaajabu yatakayokufanya ushindwe kunyamaza, kwa sababu, kwa dhahiri yake yataonekana kuwa ni mambo mabaya na undani wake utakuwa huujui, nawe utakuwa huwezi kuyanyamazia mambo yanayonekana kuwa ni mabaya.

Akasema Musainshallah utaniona ni mvumilivu wala sitoasi amri yako.

Musa alijitoa kwa kusema inshaalah, kuhofia asije akashindwa kujizuia; kama ilivyotokea.

Akasema: Basi ukinifuata, usiniulize kitu mpaka nianze kukutajia.

Yule mtu mwema alimpa sharti Musa kuwa asimuulize kitu kwa yale atakayoyafanya, kwa hali yoyote itakayokuwa. Musa alikubali lile sharti, kwa sababu aliondoka naye; kama unavyoonyesha ufafanuzi ufuatao:

فَانطَلَقَا حَتَّىٰ إِذَا رَكِبَا فِي السَّفِينَةِ خَرَقَهَا قَالَ أَخَرَقْتَهَا لِتُغْرِقَ أَهْلَهَا لَقَدْ جِئْتَ شَيْئًا إِمْرًا ﴿٧١﴾

71. Basi wawili hao wakaondoka, mpaka walipopanda jahazi akailtoboa, Akasema: Unalitoboa ili uwazamishe watu wake? Hakika umefanya jambo baya.

قَالَ أَلَمْ أَقُلْ إِنَّكَ لَن تَسْتَطِيعَ مَعِيَ صَبْرًا ﴿٧٢﴾

72. Akasema: Sikukuambia kuwa wewe hutaweza kuvumilia kuwa pamoja nami?

قَالَ لَا تُؤَاخِذْنِي بِمَا نَسِيتُ وَلَا تُرْهِقْنِي مِنْ أَمْرِي عُسْرًا ﴿٧٣﴾

73. Akasema: Usinichukulie kwa niliyosahau, wala usinipe uzito kwa jambo langu.

فَانطَلَقَا حَتَّىٰ إِذَا لَقِيَا غُلَامًا فَقَتَلَهُ قَالَ أَقَتَلْتَ نَفْسًا زَكِيَّةً بِغَيْرِ نَفْسٍ لَّقَدْ جِئْتَ شَيْئًا نُّكْرًا ﴿٧٤﴾

74. Basi wawili hao wakaondoka, mpaka wakamkuta kijana; akamuua. Akasema: Umemuua mtu asiye na kosa na hakuua! Hakikia umefanya jambo baya kabisa!

WAKAONDOKA

Aya 71 – 74

KUJIZUIA NA YANAYOTATIZA

Aya hizi zinafahamisha kuwa kuna mambo amabayo dhahiri ni rehema na undani wake ni adhabu na mengine ni kinyume. Na kwamba hukumu kwenye mambo ya namna hiyo ni kungoja kuyaamulia mpaka upatikane uhakika.

Imepokewa Hadithi mutawwatir, Kutoka kwa Mtume mtukufu(s.a.w.w) kuwa yeye amasema: “Halali iko wazi na haramu iko wazi na baina ya halali na haramu kuna mambo yenye kutatiza.”

Watu wengi hawajui ni halali au ni haramu. Mwenye kuyaaacha kwa kuilinda dini yake na heshima yake, atakuwa amesalimika, Na mwenye kuijingiza kwenye kitu chochote katika hivyo, basi atakuwa anakurubia kuingia katika haramu” Hadithi nyingine inasema: “Kujizuia na yenye kutatiza ni bora kuliko kujiingiza kwenye maangamizi.”

Kuna mapokezi yanayosema kwamba Luqman, mwenye hekima, aliingia kwa Daud akamkuta anatengeneza deraya, naye alikuwa hajapata kuiona. Akataka kumuuliza, lakini akaona bora angoje, Daud alipomaliza kuitengeza, aliivaa huku akisema: nguo nzuri sana hii ya vita. Akafahamu Luqman kuwa ile nguo ni ya vita. Akasema: “Kunyamaza ni hekima.”

Ni wachache sana wanoweza kuvumilia hivyo. Yule mtu mwema ameleta mambo matatu ya ushahidi wa hakika hii, kama ifuatavyo:

1.Basi wawili hao wakaondoka, mpaka walipopanda jahazi akalitoboa.

Musa alikwenda na yule mwenzake kwenye ufuo wa bahari, Walipokuta jahazi, wakamwomba mwenyewe awachukue, akakubali.

Walipofika katikati ya bahari, yule mja mwema alilitoboa, kiasi ambacho wangeweza kuzama na kufa maji. Musa akashtuka na jambo hili baya naakasema: Unalitoboa ili uwazamishe watu wake? Hakika umefanya jambo baya kabisa, Musa akachukua nguo yake akaziba ile tundu; kama wanavyodai wafasiri.

Akasema: Sikukuambia kuwa wewe hutaweza kuvumilia kuwa pamoja nami?

Hapo anamkumbusha lile sharti la kutomuuliza kitu, Musa akaomba msamaha na akasema:Usinichukulie kwa niliyosahau. Kwa sababu kusahau hakuna nenowala usinipe uzito kwa jambo langu. Yaani usinid- hikishe kwa kusuhubiana na wewe.

2.Basi wawili hao wakaondoka, mpaka wakamkuta kijana; akamuua.

Moyo wa Musa ukafazaika kutokana na mauaji,akasema: Umemuua mtu asiye na kosa na hakuua! Hakikia umefanya jambo baya. Huyu maskini amefanya nini? Unamuua bure tu. Huu ni ubaya wa wazi.

SHARTI YA KUCHAPA

Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.

MWISHO WA WA JUZUU YA KUMI NA TANO

9

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA TANO

وَإِن كَادُوا لَيَفْتِنُونَكَ عَنِ الَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ لِتَفْتَرِيَ عَلَيْنَا غَيْرَهُ وَإِذًا لَّاتَّخَذُوكَ خَلِيلًا ﴿٧٣﴾

73. Na hakika walikaribia kukufitini uache tuliyokupa wahyi ili utuzulie mengine, Na hapo wangelikufanya rafiki.

وَلَوْلَا أَن ثَبَّتْنَاكَ لَقَدْ كِدتَّ تَرْكَنُ إِلَيْهِمْ شَيْئًا قَلِيلًا ﴿٧٤﴾

74. Lau sikukuweka imara ungelikurubia kuwaelekea kidogo.

إِذًا لَّأَذَقْنَاكَ ضِعْفَ الْحَيَاةِ وَضِعْفَ الْمَمَاتِ ثُمَّ لَا تَجِدُ لَكَ عَلَيْنَا نَصِيرًا ﴿٧٥﴾

75. Hapo basi, tungelikuonjesha maradufu ya uhai na maradufu ya mauti; kisha usingelipata wa kukunusuru nasi.

وَإِن كَادُوا لَيَسْتَفِزُّونَكَ مِنَ الْأَرْضِ لِيُخْرِجُوكَ مِنْهَا وَإِذًا لَّا يَلْبَثُونَ خِلَافَكَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٧٦﴾

76. Na kwa hakika walikaribia kukukera katika nchi ili wakutoe humo; na hapo wasingelibakia nyuma yako ila muda mchache.

سُنَّةَ مَن قَدْ أَرْسَلْنَا قَبْلَكَ مِن رُّسُلِنَا وَلَا تَجِدُ لِسُنَّتِنَا تَحْوِيلًا ﴿٧٧﴾

77. Ndio desturi ya wale tuliowatuma kabla yako wala hutapata mabadiliko katika desturi yetu.

JE MTUME ANAHADAIKA NA DINI YAKE

Aya 73 -77

MAANA

Na hakika walikaribia kukufitini uache tuliyokupa wahyi ili utuzulie mengine, Na hapo wangelikufanya rafiki.

Waliokaribia ni washirikina. Walijaribu washirikiane na Mtume(s.a.w.w) kwa kumtaka awakubalie matakwa yao na wamfanye kuwa ni kiongozi na rafiki. Miongoni mwa hayo ni kuigusa miungu yao au angalau aache kuikashifu, lakini Mtume hakuwakubalia matakwa yao washirikina, kwa sababu yeye ni maasum na maasum hawezi kuchangia dini yake na risala yake na mambo mengine.

Unaweza kuuliza : Kauli yake Mwenyezi Mungu: ‘walikaribia kukufitini’ inafahamisha kuwa yeye Mtume alikaribia kuwakubalia matakwa yao?

Jibu : Aya hii inafungamana moja kwa moja na Aya inayofuatia.

Lau sikukuweka imara ungelikurubia kuwaelekea kidogo.

Kwa hiyo maana ni kuwa, hakika wewe Muhammad lau si ulinzi wetu kwako kwa kukupa isma (kuhifadhika) ya dhambi, basi ungelikaribia kuwaelekea washirikina na kuwatikia maombi yao, Isma ndiyo iliyokuzuia kuwakubalia. Ni sawa na kusema: ‘Lau si fulani ungeliangamia’ Umetangulia mfano wake katika Juz; 12 (12: 24).

Zaidi ya hayo, kufikiria kufanya kitu ni jambo jingine na kukifanya ni jambo jingine. Kuna Hadith mutawatir kutoka kwa Mtume kwamba yeye amesema: “Umeondolewa umma wangu yale yanayozungumzwa na nafsi zao madamu hawakufanya au kuzungumza,” yaani kujizungumzia mtu mwenyewe nafsini mwake, hakuna athari, Kuna mapokezi yanayosema, kuwa washirikina walipomwambia Mtume alinyamaza, hakuwajibu.

Hapo basi, tungelikuonjesha maradufu ya uhai na maradufu ya mauti.

Maana ni kuwa, ewe Muhammad! Lau ungeliwaelekea washirikina tungelikuadhibu mara mbili zaidi ya mwengine, duniani na Akhera. Kwa sababu adhabu ya wakuuu inakua kulingana na ukuu wao na cheo chao. Hii ni kiasi cha kukadiria tu, na ‘kukadiria muhali sio muhali.’

Kisha usingelipata wa kukunusuru nasi, kukukinga na adhabu.

Katika Nahju-lbalagha imeelezwa: “Siku ya Kiyama ataletwa kiongozi mkandamizaji, akiwa hana wa kumsaidi wala wa kumtolea udhuru, atatupwa katika Jahannam, azunguke humo kama pia, kisha afungwe kwenye shimo lake.”

Na kwa hakika walikaribia kukukera katika nchi ili wakutoe humo; na hapo wasingelibakia nyuma yako ila muda mchache.

Waliposhindwa washirikina na Mtume walijaribu kumkera kwa kila njia ili atoke Makka, Lau wangelimtoa, basi Mwenyezi Mungu angeliwangamiza muda kidogo baada ya kutoka kwake.

Unaweza kuuliza kuwa : si walifanya hivyo washirikina pale walipoafikiana kumuua Mtume, mpaka akalazimika kutoka kwenda Makka kwa kuhofia, kama ilivyoelezwa katika Juz. 9 (8:30).

Jibu : makusudio ni kuwa lau washirikina wangelimtoa wao kwa nguvu na kua ni mkimbizi aliyefukuzwa asiyejua pa kwenda, basi Mwenyezi Mungu angeliwangamiza haraka sana. Lakini Mtume alitoka Makka kwa amri ya Mwenyezi Mungu kwenda kwa watu ambao walijitolea kwake kwa hali na mali na familia.

Ndio desturi ya wale tuliowatuma kabla yako wala hutapata mabadiliko katika desturi yetu.

Yametangulia maelezo kuhusu hukumu ya Mwenyezi Mungu na kadha yake, kwamba kaumu yoyote itakayomtoa Mtume wao kwa nguvu, Mwenyezi Mungu anaiangamiza haraka. Na hii ndio desturi katika viumbe vyake, haibadiliki wala haigeuki, inaendela wakati wote na mahali kote.

أَقِمِ الصَّلَاةَ لِدُلُوكِ الشَّمْسِ إِلَىٰ غَسَقِ اللَّيْلِ وَقُرْآنَ الْفَجْرِ إِنَّ قُرْآنَ الْفَجْرِ كَانَ مَشْهُودًا ﴿٧٨﴾

78. Simamisha Swala linapopinduka jua mpaka giza la usiku, na Qur'an ya alfajiri; hakika Qur'an ya alfajiri imekuwa ni yenye kushuhudiwa.

وَمِنَ اللَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِ نَافِلَةً لَّكَ عَسَىٰ أَن يَبْعَثَكَ رَبُّكَ مَقَامًا مَّحْمُودًا ﴿٧٩﴾

79. Na katika usiku amka kwayo ni ziada kwa ajili yako; huenda Mola wako akakuinua cheo kinachosifika.

وَقُل رَّبِّ أَدْخِلْنِي مُدْخَلَ صِدْقٍ وَأَخْرِجْنِي مُخْرَجَ صِدْقٍ وَاجْعَل لِّي مِن لَّدُنكَ سُلْطَانًا نَّصِيرًا ﴿٨٠﴾

80. Na sema: Mola wangu! Niingize muuingizo mwema na nitoe kutoka kwema, na unipe madaraka kutoka kwako ya ushindi.

وَقُلْ جَاءَ الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقًا ﴿٨١﴾

81. Na sema, haki imefika na batili imetoweka. Hakika batili ni yenye kutoweka.

SIMAMISHA SWALA LINAPOPINDUKA JUA

Aya 78-81

MAANA

Aya ya kwanza na ya pili ni miongoni mwa Aya za hukumu, zilizoshuka kwa ajili ya kubainisha nyakati za Swala. Wana-Fiqh wana kauli kadhaa, kama zifuatavyo:

1.Simamisha Swala linpopinduka jua mpaka giza la usiku.

Wametofautiana katika makusudio ya kupinduka jua, Imesemekana ni wakati wa kutua jua na ikasemkena ni kupinduka nusu ya mzingo wa mbingu (meridian), na hiyo ndiyo kauli ya wengi.

Imepokewa kutoka kwa Imam Ja’far As-swadiq(a.s) kwamba giza la usiku ni nusu ya usiku.

Katika tafsiri za kisunni na kishia imeelezwa kuwa Aya hii imekusanya nyakati zote za Swala tano: Adhuhuri na Alasiri zinaingia katika kupinduka jua. Magharibi na Isha zinaingia katika giza la usiku na Asubuhi katika Qur’an ya alfajiri.

Katika Shia amesema Tabrasi kwenye Majmau-bayan: “Aya hii imeku- sanya Swala tano: Swala ya adhuhuri na alasiri zinaingia katika kupinduka jua, swala ya magharibi na isha zinaingia katika giza la usiku na makusudio ya Qur’an ya alfajiri ni swala ya alfajiri; Hizi ndizo Swala tano.”

Katika sunni amesema Razi: “Simamisha Swala, yaani idumishe kuanzia wakati wa kupinduka jua mpaka giza la usiku, inaingia swala ya adhuhuri, alasiri magharibi na isha” Kisha akaendela kusema: “wamekongamana kuwa makusudio ya Qur’an ya alfajiri ni Swala ya asubuhi.”

Ilivyo ni kwamba mafaqihi, katika vitabu vyao, wanaanza maneno kwa Swala ya adhuhuri kutokana na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘linapopinduka jua’ ambapo ameanzia Mwenyezi Mungu (s.a.w.) kwa kutaja wakati wake.

Kuongezea mapokezi ya Hadith zinazoelezea kuwa adhuhuri ndiyo ya kwanza kufaradhishwa, kisha zikafuatia nyingine kwa utaratibu ulivyo. Hilo lilikuwa Makka usiku wa Israi, mwaka mmoja kabla ya Hijra (kuhamia Madina).

Madhehebu za kiislamu zimeafikiana kuwa haifai Swala kabla ya kuingia wakati wake na kwamba jua likipinduka ndio umeingia wakati wa Adhuhri, lakini wametofautiana kwenye kiwango cha muda huu, unaisha wakati gani?

Shia Imamiya wamesema kuwa mara tu bada ya kupinduka jua unahusika wakati wa Swala ya adhuhuri kwa kiasi cha kuswaliwa kwake na kiasi cha kuweza kuswaliwa swala ya alsiri mwisho wa mchana kinahusika na Swala ya alasiri. Baina ya wakati wa kwanza na wa mwisho ni wa ushirikano wa Swala mbili; yaani inaweza kuswalia adhuhuri na alasiri.

Dhahiri ya Aya iko pamoja nao: ‘linpopinduka jua mpaka giza la usiku’ wala Mwenyezi Mungu hakutenganisha; kama ilivyo kwenye madhehebu nyingine.

Wengineo wamesema kuwa wakati wa adhuhuri unaanza linapopinduka jua mpaka kuwa kivuli cha kila kitu mfano wake, ikizidi hapo wakati wa adhuhuri utakuwa umekwisha na utakuwa wakati wa alasiri umeingia. Ufafanuzi uko katika kitabu chetu: Al-fiqh ala madhahib al-khamsa (Fiqh kwenye madhehebu matano).

2.Na Qur’an ya alfajiri. Hakika Qur’an ya alfajiri imekuwa ni yenye kushuhudiwa.

Wameafikiana kwamba makusudio ya Qur’an ya alfajiri ni ile inayosomwa katika Swala ya alfajiri, yaani ya asubuhi. Vil vile wameafikiana kwamba wakati wake unaanzia kutokeza alfajiri ya kweli mpaka kutoka jua (mawiyo); isipokuwa Maliki anasema kuwa asubuhi ina nyakati mbili: Ya hiyari, inaanzia alfajiri hadi kujuana nyuso. Na wakati wa dharura unaoanzia kujuana nyuso hadi kutoka jua. Kauli ya kushangaza ni ile ya masufi wanaosema kuwa makusudio ya alfajiri ni kupasuka moyo.

Wamekongamana mafaqihi, kwa ushahidi wa Tabrasi na Razi, kwamba makusudio ya yenye kushuhudiwa, ni kwamba Malaika wa usiku na mchana wanakusanyika ili washuhudie Swala. Wametegemea riwaya aliyoipokea Bukhari kutoka kwa Abu Hurayra, katika Sahih Bukhari Juzuu ya 6 mlango wa sura Bani Israil, Sisi tunaishuku riwaya hii. Na tunafasiri yenye kushuhudiwa, kuwa ni kuhudhuria hisiya. Kwa sababu mtu wakati wa asubuhi hisia zake zinakuwa zipo baada ya kupumzika na usingizi. Ndio maana ikasemwa ‘usingizi unabeba maazimio ya siku’

3.Na katika usiku amka kwayo ni ziada kwa ajili yako.

Kwayo ni hiyo Qur’an. Kwa ajili yako ni kumuhusisha yeye tu. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu amekufaradhishia wewe Muhammad swala nyingine, zaidi ya zile tano ambazo ni zako na wengine, uiswali usiku. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

يَا أَيُّهَا الْمُزَّمِّلُ ﴿١﴾ قُمِ اللَّيْلَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٢﴾

“Ewe mwenye kujifunika nguo! Simama usiku isipokuwa kidogo” (73:1-2)

وَمِنَ اللَّيْلِ فَاسْجُدْ لَهُ وَسَبِّحْهُ لَيْلًا طَوِيلًا ﴿٢٦﴾

“ Na usiku umsujudie Yeye na umtakase usiku mrefu.” (76:26).

Swala hii inaitwa Swala ya usiku (swalatu-llayl); wakati wake ni kuanzia nusu ya usiku hadi alfajiri. Ni wajibu kwa Mtume(s.a.w.w) , kama tulivyoeleza mwanzo na ni sunna kwa mwenginewe.

Huenda Mola wako akakuinua cheo kinachosifika.

Huenda ni neno la kutarajia ikiwa linatoka kwa kiumbe na ni la mkato ikiwa linatoka kwa muumbaji, Hapa anaambiwa Muhammad(s.a.w.w) .

Hakuna kitu zaidi ya Muhammad wala cheo zaidi ya Muhammad na kizazi zaidi ya kizazi cha Muhammad; isipokuwa yule ambaye hakuna mfano wake kitu chochote. Kuna Hadithi isemayo kuwa Mtume(s.a.w.w) alifasiri cheo chenye kusifika katika Aya hii kuwa ni cheo atakachowaombea umma wake kesho.

Na sema: Mola wangu! Niingize muuingizo mwema na nitoe kutoka kwema.

Mwenyezi Mungu alimwamrisha Mtume wake mtukufu kuomba dua hii. Kuingia kwema na kutoka kwema ni fumbo la haki na ikhlsi katika itikadi, makusudio, vitendo, harakati zote na kupumzika. Hakuna shaka kuwa mwenye kuwa na silaha ya haki na akamfanyia ikhlasi Mwenyezi Mungu peke yake, basi atamuimarisha kwa kauli thabiti, atampa hoja imara na umakini wa moyo ulio mwema na safi.

Na unipe madaraka kutoka kwako ya ushindi.

Kuna ushindi na madaraka yanayozidi kutajwa Mtume mtukufu pamoja na jina la Mwenyezi Mungu mara tano kwa siku, katika adhana na katika swala za wajibu na sunna? Kuna nguvu gani na heshima adhimu kuliko ile aliyompa Muhammad, aliposema:

وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا ﴿٧﴾

“Anachowapa Mtume kichukueni na anachowakataza kiacheni,” (59:7).

Na sema haki imefika na batili imetoweka. Hakika batili ni yenye kutoweka.

Haki ni risala ya Muhammad, itikadi na sharia. Vinginevyo ni batili, kiuhalisi na mbele ya Mwenyezi Mungu; hata kama vitaaminiwa na watu wa ardhini wote. Wafasiri wamesema kuwa makusudio ya batili hapa ni ushirikina na kwamba Mtume(s.a.w.w) alipoikomboa Makka aliingia Al- ka’ba na mlikuwa na masanamu 360, akawa anazisukuma huku akisema: “Haki imefika na batili imetoweka, Hakika batili ni yenye kutoweka.”

NGUVU YA HAKI NA NGUVU YA BATILI

Unaweza kuuliza : Mara nyingi tunaona na kushuhudia watu wa batili wakishinda na watu wa haki wakishindwa. Hii si inapingana na kauli ya Mwenyezi Mungu ‘Hakika batili ni yenye kutoweka’?

Jibu : Hakika haki ina nguvu za dhati zisizoepukana nazo kwa hali yoyote; nazo zinatenda kazi na kuathiri kwenye nyoyo safi zilizo takatifu. Mara nyingi athari hii inafikia kiwango ambacho hakuna nguvu yote yote inayoweza kuisimamisha; si mapanga ya wachinjaji wala unyongaji wa mataghuti.

Historia inatusimilia jinsi mashahidi wa itikadi walivyojitolea kuwa mashahidi kwa nyuso za kutabasamu na nafsi zilizo radhi; bali hayo yametokea wakati wetu huu huko Vietnam, Korea, Palestina na kwengineko.

Ndio! Ni kweli hawa ni wachache; kama ilivyo kawaida ya kila jambo tukufu lenye thamani. Lakini wangelikuwa wengi kwa idadi au wengi kwa viwango vya asilimia, basi dunia ingelijaa uadilifu, na dhulma na jeuri isengelikuwa na athari yoyote. Sisi hatuna shaka ubinadamu utakwenda na njia hii; hata kama muda utakuwa mrefu.

Ama batili, haina nguvu wala urefu, isipokuwa kuweko kwake kunategema rushwa, dhulma, ukandamizaji, kuwafukuza watu njama n.k.

Haya yote yataondoka kadiri siku zinavyokwenda na hali kubadilika. Ama nguvu ya haki huwa inakwenda na wakati, inabakia hivyo hivyo tu wakati wote. Kwa sababu inategema hiyo haki yenyewe, kama ilivyo. Kwa ajili hii ndio tunasema tena: Sisi tuna imani isiyokuwa na shaka kwamba mwisho ni wa haki na neno la juu litakuwa la haki peke yake.

وَنُنَزِّلُ مِنَ الْقُرْآنِ مَا هُوَ شِفَاءٌ وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ وَلَا يَزِيدُ الظَّالِمِينَ إِلَّا خَسَارًا ﴿٨٢﴾

82. Na tunateremsha katika Qur’an ambayo ni ponyo na rehema; Wala haiwazidishii madhalimu isipokuwa hasara.

وَإِذَا أَنْعَمْنَا عَلَى الْإِنسَانِ أَعْرَضَ وَنَأَىٰ بِجَانِبِهِ وَإِذَا مَسَّهُ الشَّرُّ كَانَ يَئُوسًا ﴿٨٣﴾

83. Na tunapomneemesha mtu hugeuka na kujitenga kando na inapomgusa shari hukata tamaa.

قُلْ كُلٌّ يَعْمَلُ عَلَىٰ شَاكِلَتِهِ فَرَبُّكُمْ أَعْلَمُ بِمَنْ هُوَ أَهْدَىٰ سَبِيلًا ﴿٨٤﴾

84. Sema: kila mmoja anafanya kwa namna yake, Na Mola wenu anajua aliyeongoka katika njia.

وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الرُّوحِ قُلِ الرُّوحُ مِنْ أَمْرِ رَبِّي وَمَا أُوتِيتُم مِّنَ الْعِلْمِ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٨٥﴾

85. Wanakuuliza kuhusu roho, Sema: roho inatokana na amri ya Mola wangu. Nanyi hamkupewa katika elimu ila kidogo tu.

QUR’ANI NI PONYO

Aya 82-85

MAANA

Na tunateremsha katika Qur’an ambayo ni ponyo na rehema.

Qur’an ni rehema kwa yule anayeitakia nafsi yake rehema na ni ponyo la ukafiri, ulahidi, ujinga, ufisadi na kila uchafu, kwa yule mwenye kumfanyia ikhlasi Mwenyezi Mungu na haki.

Imam Ali(a.s) katika kuisifu Qur’an ansema:“Hakika hiyo ni kamba imara, nuru inayobainisha, ni dawa yenye kuleta nafuu, ni kichujio cha takataka, ni hifadhi kwa mwenye kushikamana nayo na ni uokovu kwa mwenye kufungamana nayo.” Mwenye kuhalifu hukumu miongoni mwa hukumu za Qur’an atakuwa miongoni mwa madhalimu na waliohasirika.

Wala haiwazidishii madhalimu isipokuwa hasara.

Qur’an ni rehema kwa waumini na nakama kwa madhalimu na wafisadi, kwa sababu kila wanapoasi hukumu miongoni mwa hukumu zake, wanazidi dhambi na adhabu.

Na tunapomneemesha mtu hugeuka na kujitenga kando na inapomgusa shari hukata tamaa.

Maana ya Aya hii yanafupilizwa na kauli ya Imam Ali(a.s) katika wasifu wa mtu: “Akijitosheleza huchangamka na kushawishika na anapofukarika hukata tamaa na kubweteka. Umepita mfano wake katika Juz; 11 (10:12) na Juz. 12 (11: 9).

Sema: kila mmoja anafanya kwa namna yake, Na Mola wenu anajua aliyeongoka katika njia.

Wafasiri wamesema: “Namna, ni njia. Na maana ya Aya ni kuwa kila mmoja kati ya mumin na kafiri anafanya kwa njia yake na maumbile yake” lakini sisi tutaifafanua, kama tulivyoifahamu, katika hali zifuatazo:

1. Neno kila mmoja linafahamisha kuenea kwa mtu mmoja mmoja; kwa mfano ukisema: kila mtu analifahamu hili, ni kama umesema: Zayd analifahamu na Bakari, Hindu n.k. (yaani kila mmoja ana namna yake ya kulifahamu) Lakini ukisema: watu wote wanalifahamu, itakuwa kadhia ni moja na hukumu itakuwa imewaenea kwa ujumla sio kwa mtu mmoja mmoja. Kwa hiyo maana ya Aya ni kuwa kila mmoja katika watu ana namna yake inayomuhusu yeye peke yake; kama vile alama za vidole, kila mmoja ana zake.

2. Imepokewa Hadith kutoka kwa Ja’far As-swadiq(a.s) kwamba yeye amefasiri namna kwa maana ya nia. Usahihi wa tafsiri hii unafahamika kutoka na kauli yake Mwenyezi Mungu: “Na Mola wenu anajua aliyeongoka katika njia’ iliyokuja moja kwa moja bila ya kuweko kiunganishi kingine.” Yaani Mwenyezi Mungu anamjua anayetaka kuongoka na kufu- ata njia yake bila ya makusudio mengine yoyote isipokuwa dhati yake Aliye Mtukufu.

Kwa hiyo maana ya Aya yatakuwa: Kila mtu anafanya kulingana na nia yake na kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) atapambana naye kulingana na nia yake; ikiwa kheri basi ni kheri na ikiwa ni shari basi itakuwa ni shari.

Mwenye kudhihirisha kheri mbele ya watu ili awahadae watu na kumbe ana malengo ya shari, basi huyo mbele ya Mwenyezi Mungu ni mshari. Na mwenye kuiba mkate ili ajisitiri njaa baada ya kukosa budi, akiwa hana njia nyingine, basi huyo mbele ya Mwenyezi Mungu hastahiki adhabu.

ROHO INATOKANA NA AMRI YA MOLA WANGU

Wanakuuliza kuhusu roho, Sema: roho inatokana na amri ya Mola wangu. Nanyi hamkupewa katika elimu ila kidogo tu.

Roho ina maana nyingi. Makusudio yake hapa ni uhai. Mtume(s.a.w.w) aliulizwa kuhusu roho, Mwenyezi Mungu akamwamrisha amwambie muulizaji kuwa roho ni katika vitu vinavyopatikana kwa amri ya Mungu ambayo ni kusema ‘Kuwa na ikawa.’

Kwa ufafanuzi zaidi ni kuwa vitu viko aina mbili: Aina ya kwanza, Mwenyezi Mungu anavileta kupitia sababu za kimaumbile kutokana na maada; kama mwili wa binadamu.

Aina ya pili ni ile inayopatikana kwa kiasi cha amri tu; ambayo ni neno ‘kuwa’ Na roho ni katika aina hiyo. Aya imeliweka wazi hilo, Kwa sababu neno: ‘roho inatokana na amri ya Mola wangu,’ ni ishara ya neno ‘amri’ lilioko katika kauli yake nyingine Mwenyezi Mungu:

إِنَّمَا أَمْرُهُ إِذَا أَرَادَ شَيْئًا أَن يَقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٨٢﴾

“Hakika amri yake anapotaka kitu ni kukiambia kuwa! Na kikawa,” (36:82).

Majaribio yamethibitisha hakika hii na wakaiamini wale waliobobea na kumaliza miaka mingi kwenye utafiti wa asili ya uhai. Waliamni hakika hii baada ya kubainika kwamba sababu ya moja kwa moja ya uhai haina muungano wowote wa kuishia kwenye maada. Lau ingelikuwa inaishia kwenye maada, wangeliweza kumtengeneza binadamu kwenye viwanda vyao na maabara yao.

Wamejaribu wakashindwa: “Nanyi hamkupewa katika elimu ila kidogo tu.” Yaani kadiri viwanda vyenu vinavyotengeneza vitu vya ajabu, lakini si chochote kulingana na chembe hai za nzi, sikwambii nzi mwenyewe: “Enyi watu! Umepigwa mfano, basi usikilizeni, Hakika wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu, hawataumba hata nzi, wajapojumuika kwa hilo, Na nzi akiwapokonya kitu hawawezi kukipata kutoka kwake.

ضَعُفَ الطَّالِبُ وَالْمَطْلُوبُ ﴿٧٣﴾

Amedhoofika huyo mwenye kutaka na mwenye kutakiwa,”(22:73)

Umepita mfano wake katika Juz; 9 ( 6:95).

MWENYEZI MUNGU NA ELIMU YA CHEMBE HAI

Imetokea sadfa, wakati nikifasiri Aya hii, nikasoma makala katika gazeti Ruzil Yusuf la Misri[9] toleo la April 1969 likiwa na maelzo haya:

“Mwili wa mtu una mamilioni ya chembe hai ambazo haziwezi kuonekana isipokuwa kwa darubini. Katika miaka ya karibuni ilikuwa ni vigumu kuweka elimu ya chembe kwa sababu wataalamu walikuwa hawawezi kuz- ifungua hizo chembe au kuzidunga sindano. Kwa vile kazi ilikuwa inahi- taji chombo kidogo kuliko milimita elfu moja, basi sindano nayo ingelihi- tajika iwe na ncha ndogo kuliko milimita milioni moja.

Hatimae walifanikiwa wataalamu kuzifungua chembe hizo kupitia mwanga, sawa na tunavyowasha sigara kutokana na mwanga wa jua kupitia kioo. Ni njia pekee iliyowawezesha wataalamu kuzifungua chembe hai na kugundua kuwa ni mkusanyiko uliosheheni makumi ya viumbe mbalimbali, kila kimoja kikiwa na sifa yake maalum na kazi yake na mfungamano ulionacho pamoja na wakazi wengine wa chembe hizo.

Kuweza kufahamu kazi hizo na mifungamano hiyo, kutahitajia miaka ya utafiti kama sio vizazi. Ndio ikaanza elimu ya chembe hai na tukawa sasa tunajua kwamba chembe hai zina mwili na viungo, utando, nyuzi na mengineyo ya kushangaza akili.

Imedhihirika kwamba chembe hai za damu ni mkusanyiko wa chembe zinazoelea. Idadi yake ni mara kumi zaidi ya watu wote. Mkusanyiko huo unatengeneza chembe nyingine kila baada ya miezi mine na kuhifadhi idadi ya chembe nyingine, kiasi ambacho zile zinazokuja hazipungui wala kuzidi zile zilizoondoka. Wala hazina matatizo ya makazi kwa sababu ya wingi, kama ilivyo kwa watu.

Hapa ndio kuna maajabu! Ubongo wa mifupa uzalishe mikondo ya damu ya aina na iliyo na kazi tofauti tofauti yenye chembe nyekundu na nyeupe zinazoua na zinazokinga, Vipi basi jinsi moja ilete jinsi nyingi tofauti tofauti? Kwani ngamia anaweza kuzaa ndovu, tena azae mamba, kisha azae kicheche? Lakini kwenye damu linapatikana hilo. Haya ni maajabu kweli! Kwa ufupi kabisa ni kwamba chembe hai hivi sasa zimekuwa ndio gumzo kubwa la utafiti wa kisayansi na njia yake mpya; pengine ni njia pekee ya kufahamu siri za uhai.”

Umeona maajabu haya! Kiumbe kidogo ambacho hakiwezi kuonekana isipokuwa kwa kukuzwa mara elfu, tena hakiwezi kupasuliwa ila kwa mwangaza, unywele kwake ni kama ndovu aliye kwenye chungu chungu.

Pamoja na yote haya, kiumbe hiki kina viungo, mishipa, utando na mengineyo; kama mwanadamu. Kisha viumbe hivi, vya ajabu, vinafanya maskani yake ndani ya mwili wa mtu, vikiwa ni mamilioni, kwa kiasi cha miezi mine kisha vinakuja vingine kwa idadi ile ile ya vile vilivyoondoka bila ya kuzidi wala kupungua; kisha vingine na vingine na kuendelea.

Je, hii yote ni sadfa? Je, sadfa inaweza kukaririka mara bilioni. Je, viungo vyote hivyo, utando na nyuzi zilizofumwa kwa nidhamu na mpangilio ni sadfa?

Je sadfa inaweza kuzalisha vitu vya aina mbali mbali kutoka katika aina moja? Maswali yote haya na mengineyo yanataka jawabu.

Hapana! Tena hapana kabisa! Hakuna tafsiri ila kuweko Mjuzi mwenye uweza wa kuumba ulimwengu na uhai kwa neno ‘Kuwa’ na ikawa.

Baada ya hayo, kila sayansi inavyozidi kupiga hatua, ndio dalili na ushahi- di wa kuweko Muumba mwenye amri, unazidi. Ametukuka Mwenyezi Mungu Mola wa ulimwengu, aliyesema: “Nanyi hamkupewa katika elimu ila kidogo tu”.

10

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA TANO

وَلَئِن شِئْنَا لَنَذْهَبَنَّ بِالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ ثُمَّ لَا تَجِدُ لَكَ بِهِ عَلَيْنَا وَكِيلًا ﴿٨٦﴾

86. Na tungelipenda, tungeliyaondoa tuliyokupa wahyi; kisha usingelipata wakili wa haya juu yetu.

إِلَّا رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ إِنَّ فَضْلَهُ كَانَ عَلَيْكَ كَبِيرًا ﴿٨٧﴾

87. Isipokuwa rehema itokayo kwa Mola wako. Hakika fadhila yake kwako ni kubwa.

قُل لَّئِنِ اجْتَمَعَتِ الْإِنسُ وَالْجِنُّ عَلَىٰ أَن يَأْتُوا بِمِثْلِ هَـٰذَا الْقُرْآنِ لَا يَأْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيرًا ﴿٨٨﴾

88. Sema: Lau wangelikusanyika watu na majini ili walete mfano wa hii Qur’an, basi hawaleti mfano wake, hata wakisaidiana wao kwa wao.

وَلَقَدْ صَرَّفْنَا لِلنَّاسِ فِي هَـٰذَا الْقُرْآنِ مِن كُلِّ مَثَلٍ فَأَبَىٰ أَكْثَرُ النَّاسِ إِلَّا كُفُورًا ﴿٨٩﴾

89. Na hakika tumewaeleza watu katika hii Qur’an kwa kila mfano, lakini watu wengi wamekataa isipokuwa kukanusha tu.

TUNGELIPENDA TUNGELIONDOA

Aya 86- 89

MAANA

Na tungelipenda, tungeliyaondoa tuliyokupa wahyi.

Razi anasema, katika kufasiri Aya hii, kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) baada ya kubainisha, katika Aya iliyotangulia, kuwa yeye amewapa elimu kidogo tu, hapa anabainisha kwamba yeye lau angelitaka kuwaondolea hiki kidogo, angeliweza, Na hilo ni kwa kufuta kuhifadhika kwake moyoni na maandishi yake ya vitabuni.

Kisha usingelipata wakili wa haya juu yetu, utakayemtegemea akutetee kukurudishia tulichokichukua kwako.Isipokuwa rehema itokayo kwa Mola wako ; Hiyo pekee ndiyo inayoweza kukurudishia ambacho tungekichukua kwako.

Hakika fadhila yake kwako ni kubwa kutokana na elimu aliyokupa na ubwana juu ya watu wote.

Sema: lau wangelikusanyika watu na majini ili walete mfano wa hii Qur’an, basi hawaleti mfano wake, hata wakisaidiana wao kwa wao.

Umepita mfano wake katika Juz 1 (2: 23).

Hakika tumewaeleza watu katika hii Qur’an kwa kila mfano, katika yanayohusiana na itikadi, sharia na maadili. Na tukaweka hoja mkataa na dalili wazi, lakini watu wengi wamekataa isipokuwa kukanusha tu, na kuwa mbali na haki. Kwa sababu iko chungu na ni nzito, hawawezi kuivumilia isipokuwa wenye takua.

وَقَالُوا لَن نُّؤْمِنَ لَكَ حَتَّىٰ تَفْجُرَ لَنَا مِنَ الْأَرْضِ يَنبُوعًا ﴿٩٠﴾

90. Na walisema: hatutakuamini mpaka utuchimbulie katika ardhi hii chemchemi.

أَوْ تَكُونَ لَكَ جَنَّةٌ مِّن نَّخِيلٍ وَعِنَبٍ فَتُفَجِّرَ الْأَنْهَارَ خِلَالَهَا تَفْجِيرًا ﴿٩١﴾

91. Au uwe na kitalu cha mitende na mizabibu na utupitishie mito kati yake ikimiminika.

أَوْ تُسْقِطَ السَّمَاءَ كَمَا زَعَمْتَ عَلَيْنَا كِسَفًا أَوْ تَأْتِيَ بِاللَّـهِ وَالْمَلَائِكَةِ قَبِيلًا ﴿٩٢﴾

92. Au utuangushie mbingu vipande vipande, kama ulivyodai, au utuletee Mwenyezi Mungu na Malaika ana kwa ana.

أَوْ يَكُونَ لَكَ بَيْتٌ مِّن زُخْرُفٍ أَوْ تَرْقَىٰ فِي السَّمَاءِ وَلَن نُّؤْمِنَ لِرُقِيِّكَ حَتَّىٰ تُنَزِّلَ عَلَيْنَا كِتَابًا نَّقْرَؤُهُ قُلْ سُبْحَانَ رَبِّي هَلْ كُنتُ إِلَّا بَشَرًا رَّسُولًا ﴿٩٣﴾

93. Au uwe na nyumba ya dhahabu au upae mbinguni, Na hatutaamini kupaa kwako mpaka ututeremshie Kitabu tukisome. Sema: ametakasika Mola wangu! Kwani mimi ni nani, isipokuwa ni mwanadamu Mtume?

وَمَا مَنَعَ النَّاسَ أَن يُؤْمِنُوا إِذْ جَاءَهُمُ الْهُدَىٰ إِلَّا أَن قَالُوا أَبَعَثَ اللَّـهُ بَشَرًا رَّسُولًا ﴿٩٤﴾

94. Na nini kilichowazuia watu kuamini ulipowajia utume, isipokuwa walisema: je, Mwenyezi Mungu hupeleka mwanadamu kuwa Mtume?

قُل لَّوْ كَانَ فِي الْأَرْضِ مَلَائِكَةٌ يَمْشُونَ مُطْمَئِنِّينَ لَنَزَّلْنَا عَلَيْهِم مِّنَ السَّمَاءِ مَلَكًا رَّسُولًا ﴿٩٥﴾

95. Sema: Lau ingelikuwa duniani kuna Malaika wanaotembea kwa utulivu, basi bila ya shaka tungeliwateremshia Malaika kuwa Mtume wao.

قُلْ كَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ إِنَّهُ كَانَ بِعِبَادِهِ خَبِيرًا بَصِيرًا ﴿٩٦﴾

96. Sema: Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi baina yangu na nyinyi. Hakika Yeye anawajua vyema waja wake na anawaona.

KUFIKIRIA MALI

Aya 90-96

KUJIPENDA

Kila mmoja wetu anajipenda; awe mwana mume au mwanamke, mzee au mtoto, mwenye takua au muovu n.k. Ni binadamu gani asiyekuwa na shauku na maisha yake na kutetea heshima yake na uhalisi wake? Lau si hivyo uhai usingeendelea kuwako wala tusingeendelea, Hakuna tofauti katika kujipenda huko baina ya watu; isipokuwa tofauti iko katika aina zifutazo:-

Kuna yule anayekuwa kwenye msingi wa maumbile na akili. Hili linafa- hamika kutokana na jinsi mtu anavyoheshimu haki za wengine, kutosheka na alichoandikiwa kilichotokana na jasho lake na kusaidiana na kila mwenye kutumai kheri na manufaa ya watu kwa namna moja au nyingine; bali hata kujitolea juu ya hilo.

Kwani mwenye kutoa na kujitolea kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, atakuwa amejipenda, atake asitake, kwa sababu Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa mwenye kufanya wema, vile vile jamii inamsifu na kumtukuza yule mwenye kujitolea kwa ajili ya hiyo jamii.

Na kuna yule anayejipenda kwa kutumia yale yanayopituka akili, dini na uhalisi. Hili linafahamika kutokana na tamaa ya mtu ambaye haioni umuhimu wala manufaa ya mwingine isipokuwa wake.

Hili halikubaliki na mantiki yoyote; hata ya yahisia na ya kuonekana; sawa na alivyosema Mwenyezi Mungu: “Wana nyonyo, lakini hawafahamu kwazo, na wana macho, lakini hawaoni kwayo, na wanayo masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama wanyama bali wao ni wapotevu zaidi, Hao ndio walioghafilika.” Juz; 9 (7: 179). Hawa wako kila mahali na kila wakati; miongoni mwao ni wale aliowaashira Mwenyezi Mungu kwa kuli zake zifuatazo:-

1. Na walisema: hatutakuamini mpaka utuchimbulie katika ardhi hii chemchem.

wapenda raha katika washirikina walitoa pendekezo kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kuwa awachimbulie chemchem au mto, wao sio watu wengine, kwa ajili ya chumo na faida. Kuna mapokezi yanayosema kuwa vijoho na wapenda anasa walisema: Ewe Muhammad! Hii ardhi ya Makka ni finyu, basi yaondoe majabali yake na utuchimbulie chemchem ili tunufaike na ardhi.

2.Au uwe na kitalu cha mitende na mizabibu na utupitishie mito kati yake ikimiminika.

Yaani kama hutatuchimbulia chemchem, basi angalu jichimbulie wewe, ili uwe unafanana na hadhi ya juu, Lakini ukiwa huna kitu basi wewe unatakikana uwasikilize walio nacho. Kwamba mali peke yake ndiyo itakayomfanya aliye nayo awe anafaa kuwa kiongozi na bwana mkubwa. Hawakujua kuwa risala ya Muhammad(s.a.w.w) ni utajiri mkubwa wa mtu, uhai wake, na kwamba Muhammad ni rehema kwa watu wa ardhini itakayowaokoa na ufukara, ujinga, dhulma na utaghuti. Wapi na wapi wanaoabudu mali na kupigana vikumbo na tamaa waweze kujua rehema na kheri?

3.Au utuangushie mbingu vipande vipande, kama ulivyodai, au utuletee Mwenyezi Mungu na Malaika ana kwa ana.

Walitaka wachimbuliwe chemchem yao au yake; kam sio hivyo au vile, basi awalete adhabu kutoka mbinguni au Mwenyezi Mungu mwenyewe aje na malaika kushuhudia kuwa Yeye ni Mtume.

Hii vile vile inatokana na fikra yao kwamba anayestahiki uongozi ni tajiri, sio fukara. Dalili ya hilo ni kule kuweka sharti la kumwamini Muhammad na jambo wanaloliona kuwa haliwezekani. Ni wazi kuwa kulazimisha jambo lisilowezekana maana yake ni kung’ang’ania matakwa yao ya kuchimbuliwa chemchem ardhini; sawa na kusema: Sifanyi hivi mpaka ngamia apite kwenye tundu ya sindano.

4.Au uwe na nyumba ya dhahabu.

Yaani iliyojengwa kwa dhahabu au iliyopambwa nayo. Hii vile vile inatokana na fikra ya mali.

Au upae mbinguni.

Nalo hili linafungamana na jambo lisilowezekana. Maana yake ni kung’ang’ania kuwa mali ndio kitu pekee cha kumweka mtu kwenye cheo.

Na hatutaamini kupaa kwako mpaka ututeremshie Kitabu tukisome.

Baadhi ya wafasiri wapya wanasema: “Unadhihiri utoto wa kuhafamu na kufikria; kama unavyodhihiri ukaidi wa kipumbavu.” Lakini hapana huo si utoto wala si upumbavu; isipokuwa hilo linatokana na ufisadi, kujibagua, uporaji, unyang’anyi na kuabudu mali. Kitu kinachofahamisha hilo zaidi ni kule kupendekeza na kuweka sharti la kumfuata Mtume awe na nyumba ya dhahabu kuwa ndio muabudiwa wao wa kwanza na ndio mfano wao mkuu.

Sema: Ametakasika Mola wangu! Kwani mimi ni nani, isipokuwa ni mwanadamu Mtume?

Anayefuata amri ya yule aliyemtuma na kukatazika kwa makatazo yake:

وَمَا كَانَ لِرَسُولٍ أَن يَأْتِيَ بِآيَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ﴿٣٨﴾

“Haiwi kwa Mtume kuleta muujiza isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.” Juz; 13 (13:38).

Na nini kilichowazuia watu kuamini ulipowajia utume, isipokuwa walisema: je, Mwenyezi Mungu hupeleka mwanadamu kuwa Mtume?

Wafasiri, akiwemo Tabrasi na Razi, wameiangalia Aya hii kuwa haiungani na Aya zilizotangulia na wakasema katika kuifasiri: Hakika washirikina wa Makka hawakumwamini Muhammad(s.a.w.w) kwa sababu wao walikuwa wakiitakidi kuwa mjumbe ni lazima awe ni katika jinsia ya malaika, si katika jinsia ya watu. Lakini tafsiri hiyo iko mbali sana kutokana na njia zifuatazo:-

Washirikina wa kikuraishi walikuwa wakiamini utume wa Ibrahim na kwamba wao wanatokana na kizazi chake.

Kauli ya washirikina: ‘Hatutakuamini mpaka utuchimbulie,’ inafahamisha kuwa wanaamini risala ya binadamu; isipokuwa walitoa sharti la kuwa Mtume awe tajiri: “Na walisema: kwanini hii Qur’an haikuteremshwa kwa mtu mkubwa katika miji miwili hii” (43:31) Makusudio ya mtu mkubwa ni Walidi bin Mughira, katika viongozi wa Makka au Urwa bin Masud katika viongozi wa Taif.

Lau ingelikuwa tafsiri kama wanavyosema, basi washirikina wangelikuwa na udhuru katika kupinga kwao utume wa Muhammad (s.a.w.), kwa sababu watakuwa wanafanya lile wanaloliitakidi, na Mwenyezi Mungu amewasifu kwenye Aya nyingi kuwa wanadhihirisha yale waliyoyaficha:

بَلْ بَدَا لَهُم مَّا كَانُوا يُخْفُونَ مِن قَبْلُ ﴿٢٨﴾

“Bali yamewadhihirikia waliyokuwa wakiyaficha zamani,” Juz, 7 (6:28)

“Na wakazikataa kwa dhulma na kujitia uluwa na hali ya kuwa nafsi zao zina yakini nazo.” (27:19).

Kwa ufupi ni kuwa maana sahihi ya Aya ni kwamba washirikina wali- poshindwa na hoja ya utume wa Muhammad, walikimbilia ubabaishaji na kujaribu kuwapoteza wajinga wasiokuwa na akili.

Ndio wakasema kama mbinu tu za kuhadaa, kuwa Mwenyezi Mungu hamtumi Mtume binadamu, isipokuwa Malaika tu. Walisema haya wakiwa wanajua kwamba wao ni waongo. Ndio maana Mwenyezi Mungu akasema ‘Ispokuwa walisema’ na wala hakusema walidhani n.k. Hii inafahamisha kuwa kupinga kwao ni kiasi cha inadi tu ya kauli si ya itikadi.

Sema: Lau ingelikuwa duniani kuna Malaika wanaotembea kwa utulivu, Yaani wanaotembea kama wanadamubasi bila ya shaka tun- geliwateremshia Malaika kuwa Mtume wao.

Hekima ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) inataka apeleke Mtume kwa viumbe wake kutokana na jinsi yao. Wakiwa ni watu basi mtume wao atatokana na wao na wakiwa ni Malaika basi watakuwa hivyo hivyo. Kwa sababu jinsia inapendelea zaidi kwenye jinsia yake:

لَقَدْ مَنَّ اللَّـهُ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ إِذْ بَعَثَ فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْ أَنفُسِهِمْ ﴿١٦٤﴾

“Hakika Mwenyezi Mungu amewaneemesha waumini kwa kuwaletea Mtume miongoni mwao” Juz. 4 (3:164).

Washirikina wanajua hilo, lakini wanafanya vitimbi na hadaa. Umetangulia mfano wake katika Juz.7 (6:9).

Unaweza kuuliza: Jibril ni Malaika naye alikuwa mjumbe wa Mungu kwa Muhammad ambaye ni mtu, imekuwaje? Jibu: baina ya hawa wawili kuna aina fulani ya kukurubiana katika jinsi; kwamba kila mmoja wao ni mjumbe kutoka kwa Mungu.

Sema: Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi baina yangu na nyinyi. Hakika Yeye anawajua vyema waja wake na anawaona.

Mwenyezi Mungu ni shahidi wa Muhammad kwa miujiza aliyoidhihirisha mikononi mwake, historia inashuhudia heri ya utu iliyopatikana kutokana naye na risala yake inashuhudia kwamba yeye ni rehema kwa viumbe na lolote katika sera ya Muhammad ni hoja tosha ya ukweli wake na utukufu wake.

وَمَن يَهْدِ اللَّـهُ فَهُوَ الْمُهْتَدِ وَمَن يُضْلِلْ فَلَن تَجِدَ لَهُمْ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِهِ وَنَحْشُرُهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَلَىٰ وُجُوهِهِمْ عُمْيًا وَبُكْمًا وَصُمًّا مَّأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ كُلَّمَا خَبَتْ زِدْنَاهُمْ سَعِيرًا ﴿٩٧﴾

97. Na anayeongozwa na Mwenyezi Mungu ndiye aliyeongoka na anayempotoa, basi, hutawapatia walinzi wasiokuwa Yeye. Na tutawakusanya Siku ya Kiyama hali ya kukokotwa juu ya nyuso zao wakiwa ni vipofu na mabubu na viziwi. Makazi yao ni Jahannam. Kila moto ukifanya kuzimika tutazidi kuuchochea uwake kwa nguvu.

ذَٰلِكَ جَزَاؤُهُم بِأَنَّهُمْ كَفَرُوا بِآيَاتِنَا وَقَالُوا أَإِذَا كُنَّا عِظَامًا وَرُفَاتًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ خَلْقًا جَدِيدًا ﴿٩٨﴾

98. Hayo ni malipo yao kwamba wao walizikataa ishara zetu na wakasema: je, tutakapokuwa mifupa na mapande yaliyosagika, je tutafufuliwa kuwa viumbe wapya?

أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللَّـهَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ قَادِرٌ عَلَىٰ أَن يَخْلُقَ مِثْلَهُمْ وَجَعَلَ لَهُمْ أَجَلًا لَّا رَيْبَ فِيهِ فَأَبَى الظَّالِمُونَ إِلَّا كُفُورًا ﴿٩٩﴾

99. Kwani hawaoni kwamba Mwenyezi Mungu aliyeumba mbingu na ardhi ni Mwenye kuweza kuumba mbingu mfano wao? Na yeye amewawekea muda usio na shaka yoyote, lakini madhalimu hawataki isipokuwa ukafiri.

قُل لَّوْ أَنتُمْ تَمْلِكُونَ خَزَائِنَ رَحْمَةِ رَبِّي إِذًا لَّأَمْسَكْتُمْ خَشْيَةَ الْإِنفَاقِ وَكَانَ الْإِنسَانُ قَتُورًا ﴿١٠٠﴾

100. Sema, lau mngelikuwa mnamiliki hazina ya rehema ya Mola wangu, basi mngeliizuia kwa kuchelea kuisha. Na mtu ni mchoyo sana.

ALIYEONGOZWA NA MUNGU

Aya 97-100

MAANA

Na anayeongozwa na Mwenyezi Mungu ndiye aliyeongoka na anayem- potoa, basi, hutawapatia walinzi wasiokuwa Yeye.

Hii ni kumwelezea aliye mwema; yaani anayekuwa hivyo mbele ya Mwenyezi Mungu; na wala sio yule watu wanayesema kuwa ni mwema. Kuna Hadith isemayo: “Dhahiri ni ya watu na batini ni ya Mungu.” Katika Nahjulbalagha imeelezwa: ”Utajiri na ufukara ni baada ya kuonekana kwa Mungu.”

Wafisadi na wapotevu hawana wa kuwanusuru wala kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu. Umetangulia mfano wake katika Juz. 9 (7: 178). Ama adhabu ya wapotevu wanaopoteza, ameiashiria Mwenyezi Mungu kwa kusema:

Na tutawakusanya Siku ya Kiyama hali ya kukokotwa juu ya nyuso zao wakiwa ni vipofu na mabubu na viziwi. Makazi yao ni Jahannam. Kila moto ukifanya kuzimika tutazidi kuuchochea uwake kwa nguvu.

Hili ni fumbo la uchungu wa adhabu na ukali wake kwa yule Mwenye kupinga hisabu na adhabu yake mpaka ajue aliyoyapinga:

كُلَّمَا أَرَادُوا أَن يَخْرُجُوا مِنْهَا أُعِيدُوا فِيهَا وَقِيلَ لَهُمْ ذُوقُوا عَذَابَ النَّارِ الَّذِي كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ ﴿٢٠﴾

“Na wataambiwa: onjeni adhabu ya moto ambayo mlikuwa mkiikadhibisha” (32:20).

Na hayo ni malipo yao kwamba wao walizikataa ishara zetu pamoja na ufafanuzi wa kutokea ufufuo. Walikanusha na wakapinga si kwa chochote ila ni kwa kuona ni mbali hilo.

Na wakasema: je, tutakapokuwa mifupa na mapande yaliyosagika, je tutafufuliwa kuwa viumbe wapya?

Imekwishatangulia Aya hii neno kwa neno katika Aya ya 49 ya Sura hii.

Kwani hawaoni kwamba Mwenyezi Mungu aliyeumba mbingu na ardhi ni Mwenye kuweza kuumba mbingu mfano wao? Na yeye amewawekea muda usio na shaka yoyote, lakini makafiri hawataki isipokuwa ukafiri.

Makusudio ya muda hapa ni muda wa ufufuo na kwamba huo utakuwa tu. Wameukana na hali wanaona kuumbwa kwa mbingu na ardhi huku wakikubali kuwa Mwenyezi Mungu ndiye aliyeziumba na akazipangilia vizuri kwa uweza wake, lakini wakasema kuwa Mwenyezi Mungu hawezi kuwarudisha tena baada ya kutoweka, kwa vile hilo ni jambo zito.

Ndio Mwenyezi Mungu akawaambia kuwa mwenye kuweza kukifanya kitu bila ya kitu basi ana uweza zaidi kukikusanya kitu hicho baada ya kutawanyika.

Maana ya Aya hii yamekwisha tangulia kwenye Aya nyingi, Angalia Juz.13 (13:5).

Hebu tusome kwa pamoja hoja hizi za kufunga mdomo wa mpinzani wa ufufuo, kwa mfumo usiokuwa na ushabiki; kisha useme: Ole wao wenye kukadhibisha:

“Walisema: Je, tutakapokufa na tukawa mchanga na mifupa ndio tutafu- fuliwa? Tuliahidiwa haya sisi na baba zetu zamani. Hayakuwa haya ila ni ngano za watu wa kale.”

“Sema: Ni ya nani ardhi na mbingu na vilivyomo ndani yake, kama nyinyi mnajua?”

“Watasema ni ya Mwenyezi Mungu.”

“Sema: Basi je, hamkumbuki?”

“Sema ni nani Mola wa mbingu saba na Mola wa Arshi kuu?”

“Watasema ni Mwenyezi Mungu.”

“Sema: Basi Je, hamuogopi?”

“Sema: ni nani ambaye ufalme wa kila kitu umo mikononi mwake, naye ndiye alindaye na halindwi, ikiwa mnajua?”

“Watasema ni vya Mwenyezi Mungu”

“Sema: basi vipi mnadanganywa?” 23: (82 – 89).

Huu ni ushahidi wazi kwamba itikadi ya kiislamu iko kwenye misingi ya elimu na uhuru wa akili na rai, Tazama: Juz; 7 (6:4) “Kifungu hakuna udikteta katika ardhi wala mbingu.”

Sema lau mngelikuwa mnamiliki hazina ya rehema ya Mola wangu, basi mngeliizuia kwa kuchelea kuisha.

Rehema ya Mwenyezi Mungu inaenea kwenye kila jambo, kama vile afya, ufahamu, mali na neema nyinginezo, lakini makusudio yake hapa ni kuhusu mali, kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t): “Kuhofia kuisha” na ile Aya ya 90 ya Sura hii.

Ubainifu wake ni kuwa Mwenyezi Mungu alimwamrisha Mtume wake awaambie wapenda anasa kuwa nyinyi mlitaka Mwenyezi Mungu awazidishie mali zenu na utajiri wenu kwa kuchimbua mito ardhini, huku akiwa anajua kwamba nyinyi lau mtamiliki hazina ya mbingu na ardhi ambayo haishi, basi mngeendelea na ubahili wenu na uchoyo kwa kuhofia kuisha. Hili linatilia mkazo tuliyosema kwamba wapenda anasa hawafikirii isipokuwa mali.

Na mtu ni mchoyo sana

Katika Juz. 12 (11: 9) tumesema kuwa Qur’an, haikusudii, kwa wasifu huu, kumueleza binadamu alivyo; isipokuwa ni kutafsiri tabia ya binadamu katika badhi ya hali zake. kwa maelezo zaidi rudia huko.


6

7

8

9