TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA TATU Juzuu 23

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA TATU0%

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA TATU Mwandishi:
: HASANI MWALUPA
Kundi: Qurani tukufu

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA TATU

Mwandishi: Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya
: HASANI MWALUPA
Kundi:

Matembeleo: 26471
Pakua: 2627


Maelezo zaidi:

Juzuu 1 Juzuu 2 Juzuu 3 Juzuu 4 Juzuu 5 Juzuu 6 Juzuu 7 Juzuu 8 Juzuu 12 Juzuu 13 Juzuu 14 Juzuu 15 Juzuu 16 Juzuu 17 Juzuu 18 Juzuu 19 Juzuu 20 Juzuu 21 Juzuu 22 Juzuu 23 Juzuu 24
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 30 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 26471 / Pakua: 2627
Kiwango Kiwango Kiwango
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA TATU

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA TATU Juzuu 23

Mwandishi:
Swahili

5

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA TATU

مَّثَلُ الْجَنَّةِ الَّتِي وُعِدَ الْمُتَّقُونَ فِيهَا أَنْهَارٌ مِّن مَّاءٍ غَيْرِ آسِنٍ وَأَنْهَارٌ مِّن لَّبَنٍ لَّمْ يَتَغَيَّرْ طَعْمُهُ وَأَنْهَارٌ مِّنْ خَمْرٍ لَّذَّةٍ لِّلشَّارِبِينَ وَأَنْهَارٌ مِّنْ عَسَلٍ مُّصَفًّى وَلَهُمْ فِيهَا مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ وَمَغْفِرَةٌ مِّن رَّبِّهِمْ كَمَنْ هُوَ خَالِدٌ فِي النَّارِ وَسُقُوا مَاءً حَمِيمًا فَقَطَّعَ أَمْعَاءَهُمْ ﴿١٥﴾

15. Mfano wa Pepo waliyoahidiwa wenye takuwa ina mito ya maji yasiyoharibika, Na mito ya maziwa. Na mito ya mvinyo yenye utamu. Na mito ya asali iliyosafishwa. Na wao humo watakuwa na kila namna ya matunda, na maghufira kutoka kwa Mola wao. Basi je, hao ni kama watakaodumu Motoni? Na wakinyweshwa maji yanayochemka yatakayokata matumbo yao.

وَمِنْهُم مَّن يَسْتَمِعُ إِلَيْكَ حَتَّىٰ إِذَا خَرَجُوا مِنْ عِندِكَ قَالُوا لِلَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ مَاذَا قَالَ آنِفًا أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ طَبَعَ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَاتَّبَعُوا أَهْوَاءَهُمْ ﴿١٦﴾

16. Na wapo miongoni mwao wanaokusikiliza, mpaka wakiondoka kwako huwauliza waliopewa ilimu: Amesema nini sasa hivi? Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao, na wakafuata hawaa zao.

وَالَّذِينَ اهْتَدَوْا زَادَهُمْ هُدًى وَآتَاهُمْ تَقْوَاهُمْ ﴿١٧﴾

17. Na ambao wameongoka anawazidishia uongofu.

فَهَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا السَّاعَةَ أَن تَأْتِيَهُم بَغْتَةً فَقَدْ جَاءَ أَشْرَاطُهَا فَأَنَّىٰ لَهُمْ إِذَا جَاءَتْهُمْ ذِكْرَاهُمْ ﴿١٨﴾

18. Kwani wanangojea jengine isipokuwa iwafikie Saa kwa ghafla? Basi sharti zake zimekwisha kuja. Na itapowajia kutawafaa wapi kukumbuka kwao?

فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مُتَقَلَّبَكُمْ وَمَثْوَاكُمْ ﴿١٩﴾

19. Basi jua ya kwamba hapana mola ila Mwenyezi Mungu. Na omba maghufira kwa dhambi zako na za waumini wanaume na waumini wanawake. Na Mwenyezi Mungu anajua mahali penu pa kwenda na kurudi na mahali penu pa kukaa.

SIFA ZA PEPO

Aya 15 – 19

MAANA

Mfano wa Pepo waliyoahidiwa wenye takuwa ina mito ya maji yasiyoharibika.

Makusudio ya mfano wa pepo ni sifa zake. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu anawapa habari waja wake kwamba miongoni mwa sifa za pepo ni kuwa ndani yake mna mito ya maji yanayobaki na asili yake bila ya kubadilishwa na chochote.

Na mito ya maziwa isiyoharibika ladha yake wala rangi au harufu yake.Na mito ya mvinyo yenye utamu kwa wanywao . Ni tamu mdomoni wala hauleweshi.Na mito ya asali iliyosafishwa kutokana na masega na mengineyo.Na wao humo watakuwa na kila namna ya matunda yakiwemo yale ambayo hayana mfano wake duniani.

Katika baadhi ya vitabu vya kisufi imeandikwa kuwa Makusudio ya maji hapa ni ilimu, maziwa ni matendo, mvinyo ni mahaba na asali ni utamu wa maarifa na kuwa karibu na Mwenyezi Mungu.

Tumekwishatangulia kusema mara nyingi kwamba kila kinachokuja katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu inapasa kukichukulia kwa dhahiri yake mpaka ithibitike kinyume kutokana na nakili au akili. Hapa akili haikatai chochote katika sifa za pepo zilizotajwa. Kwa hiyo basi ni wajibu kuchukulia dhahiri yake na kubaki hivyo hivyo.

Unaweza kuuliza : Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametaja mara kadhaa katika Kitabu chake kuwa watu wa Peponi watastarehe kwa ladha za kimaana, sio za kihisia; kama vile Kupendwa na kuridhiwa na Mwenyezi Mungu na kuinuliwa daraja zao kwake. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

فِي مَقْعَدِ صِدْقٍ عِندَ مَلِيكٍ مُّقْتَدِرٍ ﴿٥٥﴾

“Katika makao mazuri karibu na Mfalme Mwenye uwezo.” (54:55)

Na kauli yake:

سَيَجْعَلُ لَهُمُ الرَّحْمَـٰنُ وُدًّا ﴿٩٦﴾

“Mwingi wa rehema atawajaalia mapenzi.” Juz. 16 (19:96).

Sasa je, kuna wajihi gani wa kuchanganya Aya zile zinazofahamisha neema ya Peponi inayokuwa kwa ladha za kihisia na zile zinazofahamisha ladha ya kimaana?

Jibu : hakuna kizuizi cha kuzuia kuchanganya zote mbili na kutumia ufahamisho wote. Kwa hiyo watu wa Peponi watastarehe kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kuinuliwa daraja zao mbele yake; vile vile watastarehe na vitu vizuri katika vyakula na vinywaji.

Mula Sadra anasema katika Asfar: “Ama Pepo iko kama ilivyojulishwa na Kitabu na sunna kwa kufuatana na dalili. Ndani yake hamtakuwa na mauti wala uzee, ghamu au maradhi. Hakuna kuisha wala kuondoka.

Ni nyumba ya cheo na utukufu. Wakazi wake hawatapata tabu wala kuchoka. Humo watapata kila kinachotamaniwa na nafsi na kuburudisha macho na watadumu humo.

“Wakazi wake watakua karibu na Mwenyezi Mungu, ni mawalii wake ni wapenzi wake na ni watu wa karama yake. Na kwamba wao watakuwa na daraja bora; miongoni mwao kuna watakaostarehe kwa tasbih na takbir, na wengine watastarehe kwa ladha za hisia; kama vile aina ya vyakula, vinywaji na matunda. Pia makochi, mahurilaini na kutumikiwa na vijana. Vile vile kukaa kwenye mito na mazulia na kuvaa hariri nyepesi na nzito. Kila mmoja ataburudika kulingana na hamu yake.”

Na maghufira kutoka kwa Mola wao.

Wale wanaostarehe na anasa za dunia huko watahisabiwa hisabu nzito: Ama watu wa Peponi wao watakuwa kwenye neema wakiwa kwenye amani ya hisabu ya Mwenyezi Mungu na adhabu yake.

Basi je hao ni kama watakaodumu Motoni?

Hapa kuna maneno ya kukadiriwa yanayofahamika kutokana na mfumo wa maneno; kukadiriwa kwake ni je, atakayedumu Peponi ni sawa na atakayedumu Motoni? Hapana hawalingani sawa.

Na wakinyweshwa maji yanayochemka yatakayokata matumbo yao.

Vipi watakuwa sawa na hali watu wa Peponi watakunywa maji matamu, maziwa, mvinyo na asali safi; na watu wa motoni watakunywa usaha na maji moto yanayotokota matumboni?

Na wapo miongoni mwao wanaokusikiliza, mpaka wakiondoka kwako huwauliza waliopewa ilimu: Amesema nini sasa hivi?

Yaani miongoni mwa watu wanaokusikiliza wewe Muhammad wako makafiri au wanafiki na wanapotoka wanasema kwa dharau kuwaambia wale waliohudhuria katika maulama wa watu wa kitabu: ati amesemaje huyo sasa hivi? Sisi hatukufahamu. Je nyinyi mmefahamu kitu? Hii ndio tabia ya yule asiyeona chochote isipokuwa matamanio yake tu.

Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao, na wakafuata hawa zao.

Kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t): ‘Na wakafuata matamanio yao,’ inaashiria jawabu la swali; Kwanini Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao? Ndio majibu yakawa, kwa vile hawa zao zimememea kwenye nyoyo zao mpaka ikawa kama kwamba Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu yake au amewaumba bila ya nyoyo; kama anavyosema Mwenyezi Mungu:

فَلَمَّا زَاغُوا أَزَاغَ اللَّـهُ قُلُوبَهُمْ ﴿٥﴾

“Walipopotoka Mwenyezi Mungu alizipotoa nyoyo zao” (61:5).

Na ambao wameongoka anawazidishia uongofu.

Waumini waliutafuta uongofu kwa ukweli na ikhlas, kwa hiyo Mwenyezi Mungu amekuwa ndio muongozi na mlezi wao; akawazidishia elimu ya heri na akawapa ulinzi wake na tawfiki yake kwenye yale yaliyo na heri ya dunia yao na Akhera yao. Haya ndiyo Makusudio yana anawapa takua yao.

Kwani wanangojea jengine isipokuwa iwafikie Saa ya Kiyamakwa ghafla?

Wanaambiwa wale waliosema kwa dharau: Ati amsema nini sasa hivi? Walisema hivi wakiwa wameghafilika kabisa na siku ambayo itawanyakuwa ghafla na wasimame mbele ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya hisabu.

Basi sharti zake zimekwisha kuja.

Makusudio ya sharti hapa ni dalili na hoja mkataa za ufufuo. Zimekuja katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na mdomoni mwa Muhammad(s.a.w. w ) kwa mifumo mbalimbali wala hazikuacha udhuru wowote kwa mkanushaji.

Na itapowajia kutawafaa wapi kukumbuka kwao?

Maana ni kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu aliwakumbusha duniani, lakini wakakataa, na watakapofufuliwa na kuona adhabu watakumbuka na kujuta, lakini wakati huo hakutafaa chochote kukumbuka kwao.

Basi jua ya kwamba hapana Mola ila Mwenyezi Mungu Yeye anahuisha na kufisha na kuadhibu na kutoa adhabu. Sio mbali kuwa maana ya hapana mola isipokuwa Mwenyezi Mungu hapa, ni lingania Mwenyezi Mungu na umoja wake.

Na omba maghufira kwa dhambi zako na za waumini wanaume na waumini wanawake.

Kuomba maghufira kwa dhambi ni jambo linalopendeza kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na ni jambo linalotakina hasa; ni sawa kuweko na dhambi au la.

Na Mwenyezi Mungu anajua mahali penu pa kwenda na kurudi matendo ya dunianina mahali penu pa kukaa mtakapoacha matendo yenu au kwenda zenu Akhera; kama ilivyosemekana.

Vyovyote iwavyo ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) anajua hali ya waja wake duniani na Akhera na pale wanapokuwa katika harakati na wanapotulia.

وَيَقُولُ الَّذِينَ آمَنُوا لَوْلَا نُزِّلَتْ سُورَةٌ فَإِذَا أُنزِلَتْ سُورَةٌ مُّحْكَمَةٌ وَذُكِرَ فِيهَا الْقِتَالُ رَأَيْتَ الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ يَنظُرُونَ إِلَيْكَ نَظَرَ الْمَغْشِيِّ عَلَيْهِ مِنَ الْمَوْتِ فَأَوْلَىٰ لَهُمْ ﴿٢٠﴾

20. Na wanasema wale ambao wameamini: Kwa nini haiteremshwi Sura? Na inapoteremshwa Sura iliyo waziwazi na vikatajwa ndani yake vita, utawaona wenye maradhi katika nyoyo zao. wanakutazama mtazamo wa anayezimia kwa mauti. Basi ole wao.

طَاعَةٌ وَقَوْلٌ مَّعْرُوفٌ فَإِذَا عَزَمَ الْأَمْرُ فَلَوْ صَدَقُوا اللَّـهَ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ ﴿٢١﴾

Utiifu na kauli njema. Na jambo likishaazimiwa, basi wakiwa ni wakweli kwa Mwenyezi Mungu, bila ya shaka itakuwa ni heri kwao.

فَهَلْ عَسَيْتُمْ إِن تَوَلَّيْتُمْ أَن تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَتُقَطِّعُوا أَرْحَامَكُمْ ﴿٢٢﴾

22. Basi yanayotarajiwa kwenu mkitawala ndio mtafanya ufisadi katika nchi na mtaukata udugu wenu?

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّـهُ فَأَصَمَّهُمْ وَأَعْمَىٰ أَبْصَارَهُمْ ﴿٢٣﴾

23. Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewalaani, na akawatia uziwi, na akawapofoa macho yao.

UTIIFU NA KAULI NJEMA

Aya 20 – 23

MAANA

Na wanasema wale ambao wameamini: Kwa nini haiteremshwi Sura?’’ Na inapoteremshwa Sura iliyo waziwazi na vikatajwa ndani yake vita, utawaona wenye maradhi katika nyoyo zao wanakutazama mtazamo wa anayezimia kwa mauti.

Hapa kuna kukadiria maneno kuwa: Kwa nini haiteremshwi sura ya vita? Dalili ya kukadiria huku ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Na vikatajwa ndani yake vita.’ Hali hii watu wa nahw wanaiita ufahamisho unaofahamishwa na wa pili. Iliyo waziwazi ni kutaja vita waziwazi. Maradhi hapa ni shaka na unafiki.

Maana ni kuwa waumini wenye ikhlasi walikuwa wakitamani Qur’an iwaamrishe jihadi ya kupigana na makafiri na waovu. Wanapoitwa walikuwa wakienda haraka kujitolea nafsi zao katika njia ya Mwenyezi Mungu, huku wakiwa na furaha ya kukutana na Mwenyezi Mungu na thawabu zake.

Ama wale walio na maradhi nyoyoni mwao ambao ni wanafiki, walikuwa wakichukia sana jihadi na vita, na inapoteremshwa Aya ya vita basi mishipa inawasimama kwa hofu wakimwangalia Mtume kwa mtazamo wa hofu, kama anayeangalia mauti yakimjia.

Basi ole wao.

Wafasiri wengi wamesema maana ya neno Awla hapa ni ‘ole wao’ ambalo pia lina maana ya bora. Mfumo wa maneno unakubaliana na maana hii ya ole wao.

Utiifu na kauli njema.

Haya ni maneno yanayoanza tena. Maana yake ni kuwa kumtii Mwenyezi Mungu na kauli njema atakayoikubali Mtume ni bora kwao kuliko kukijaza kifua na unafiki na kumtazama Mtume kwa jicho la chuki na hofu.

Na jambo likishaazimiwa, basi wakiwa ni wakweli kwa Mwenyezi Mungu, bila ya shaka itakuwa ni heri kwao.

Lau wanafiki wangelimfanyia ikhlasi Mwenyezi Mungu na wakaitikia mwito wa Mtume inapokuja amri ya vita na ikawa ni lazima, ingelikuwa ni heri ya dunia yao na Akhera yao. Lakini walikataa isipokuwa ufisadi.

Basi yanayotarajiwa kwenu mkitawala ndio mtafanya ufisadi katika nchi na mtaukata udugu wenu?

Nyinyi wanafiki mmedhihirisha Uislamu kwa kujilazimisha na kuogopa nguvu yake. Huenda mkipata nguvu na utawala mtaijaza ardhi ufisadi kwa ibada ya masanamu na kumwaga damu, kupora mali na kuvunja udugu.

Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewalaani kwa kuwaweka mbali na rehema, na akawatia uziwi, na akawapofoa macho yao.

Walipoutilia uziwi mwito wa haki na kuufumbia macho ndio Mwenyezi Mungu naye akawatia uziwi na kuwapofua. Kwa maneno mengine ni kuwa walifuata njia ya maangamizi kwa hiyari yao ndio Mwenyezi Mungu akawaangamiza:

وَمَا ظَلَمْنَاهُمْ وَلَـٰكِن ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ﴿١٠١﴾

“Na hatukuwadhulumu, lakini wamejidhulumu wenyewe” Juz. 12 (11:101).

6

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA TATU

أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ الْقُرْآنَ أَمْ عَلَىٰ قُلُوبٍ أَقْفَالُهَا ﴿٢٤﴾

24. Je, Hawaizingatii hii Qur’an? Au kwenye nyoyo zipo kufuli?

إِنَّ الَّذِينَ ارْتَدُّوا عَلَىٰ أَدْبَارِهِم مِّن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ الْهُدَى الشَّيْطَانُ سَوَّلَ لَهُمْ وَأَمْلَىٰ لَهُمْ ﴿٢٥﴾

25. Kwa hakika ambao wanarudi kwa migongo yao baada ya kuawabainikia uwongofu, Shetani huyo amewashawishi na amewachelewesha.

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا لِلَّذِينَ كَرِهُوا مَا نَزَّلَ اللَّـهُ سَنُطِيعُكُمْ فِي بَعْضِ الْأَمْرِ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ إِسْرَارَهُمْ ﴿٢٦﴾

26. Hayo ni kwa sababu waliwaambia waliochukia aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu: Tutawatii katika baadhi ya mambo. Na Mwenyezi Mungu anajua siri zao.

فَكَيْفَ إِذَا تَوَفَّتْهُمُ الْمَلَائِكَةُ يَضْرِبُونَ وُجُوهَهُمْ وَأَدْبَارَهُمْ ﴿٢٧﴾

27. Basi itakuwaje Malaika watakapowafisha wakawa wanawapiga nyuso zao na migongo yao!

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ اتَّبَعُوا مَا أَسْخَطَ اللَّـهَ وَكَرِهُوا رِضْوَانَهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ ﴿٢٨﴾

28. Hayo ni kwa sababu wao waliyafuata yaliyomchukiza Mwenyezi Mungu na wakachukia yanayomridhisha. Basi akaviangusha vitendo vyao.

أَمْ حَسِبَ الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ أَن لَّن يُخْرِجَ اللَّـهُ أَضْغَانَهُمْ ﴿٢٩﴾

29. Je, ambao wana maradhi nyoyoni mwao wanadhani kwamba Mwenyezi Mungu hatazidhihirisha chuki zao?

وَلَوْ نَشَاءُ لَأَرَيْنَاكَهُمْ فَلَعَرَفْتَهُم بِسِيمَاهُمْ وَلَتَعْرِفَنَّهُمْ فِي لَحْنِ الْقَوْلِ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ أَعْمَالَكُمْ ﴿٣٠﴾

30. Na lau tungelipenda, tungelikuonyesha hao na ungeliwatambua kwa alama zao. Na bila ya shaka utawajua kwa namna ya usemi Na Mwenyezi Mungu anavijua vitendo vyenu.

وَلَنَبْلُوَنَّكُمْ حَتَّىٰ نَعْلَمَ الْمُجَاهِدِينَ مِنكُمْ وَالصَّابِرِينَ وَنَبْلُوَ أَخْبَارَكُمْ ﴿٣١﴾

31. Na bila ya shaka tutawajribu mpaka tuwajue wapignao jihadi katika nyinyi na wanaosubiri. Nasi tutazijaribu habari zenu.

JE HAWAIZINGATI QUR’AN?

Aya 24 – 31

MAANA

Je, Hawaizingatii hii Qur’an? Au kwenye nyoyo zipo kufuli?

Wanaambiwa wanafiki. Kwa sababu Aya hii na ilie iliyo kabla yake inawazungumzia wao. Dalili zote zilizokuja katika Qur’an, za kuweko Mwenyezi Mungu katika kuumbwa mbingu na ardhi, hoja wazi za utume wa Muhammad(s.a.w. w ) .

Ubaya wa shirki, dhulma na ufisadi katika ardhi, yote hayo yako wazi hayakufumbwafumbwa; kuongezea athari ya mfumo wa Qur’an katika moyo wa msomaji na msikilizaji anavyopata hisia. Basi makafiri wananini hawaathiriki na muujiza huu? Je, wamekosa usikizi na macho au nyoyo zao zimefungwa na kufuli na kutu.

Kwa hakika ambao wanarudi kwa migongo yao baada ya kuawabainikia uwongofu, Shetani huyo amewashawishi na amewachelewesha.

Neno kurudi tumelifasiri kutokana na neno la kiarabu Irtaddu (kuritadi) lenye maana ya kuamini haki kisha kuikanusha. Pia kuijua haki kwa dalili mkataa kisha kuikanusha kwa matamanio ya nafsi, kunaingia katika hukumu ya kuritadi, kwa sababu kuijua haki ni sawa na kuiamini na kuichukia ni sawa na kuiritadi.

Ama mwenye kuficha ukafiri na akadhihirisha imani huyo ni mnafiki na murtadi vile vile. Ni mnafiki kwa vile amedhihirisha kinyume na yaliyo moyoni mwake na ni murtadi kwa kuwa duniani anakuwa kama mumin na Akhera anakuwa kafiri; kama kwamba yeye ni mumin na wakati huo huo ni murtadi.

Tamko la Aya limegusia aina zote tatu. Kwa sababu dalili za dhahiri zilizosimaia kwenye Tawhid, ufufuo na utume wa Muhammad(s.a.w.w) ndio hoja aliyoikusuduia Mwenyezi Mungu kwa kusema: ‘Baada ya kuwabainikia uongofu,’ lakini shetani aliwadanganya kwa unafiki na kuiritadi haki na kuipinga. Akawaahidi ahadi ya uwongo na kuwatia wasiwasi wa tamaa na matamanio.

Hayo ni kwa sababu waliwaambia waliochukia aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu: Tutawatii katika baadhi ya mambo.

Waliosema ni wanafiki na waliochukia ni mayahudi waliokuwa majirani wa Mtume. Kwa sababu mayahudi ndio watu wanaochukia zaidi kila kilichoteremshwa na Mwenyezi Mungu; hasa Qur’an. Maana ni kuwa wanafiki waliwambia mayahudi: sisi tuko pamoja na nyinyi kuhusu Muhammad na tunashirikiana nanyi katika kumpiga vita; isipokuwa hali haituruhusu kutangaza uadui wetu kwake. Kwa hiyo tuacheni tujionyeshe kuwa ni waislamu na tutakuwa pamoja nanyi kwenye njama dhidi yake.

Na Mwenyezi Mungu anajua siri zao.

Yaani siri za mayahudi na za wanafiki, kwa sababu kwake hakifichiki chochote katika ardhi wala mbinguni.

Basi itakuwaje Malaika watakapowafisha wakawa wanawapiga nyuso zao na migongo yao!

Wamekimbia jihadi kwa kuogopa mauti, je wataweza kuyakimbia mauti na mapigo yake? Na ufufuo na vituko vyake.

Hayo ni kwa sababu wao waliyafuata yaliyomchukiza Mwenyezi Mungu na wakachukia yanayomridhisha.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) atawaadhibu wakati wa mauti na baada yake vile vile, kwa vile waliathirika na yale yanayomchukiza Mwenyezi Mungu kuliko yale yanayomridhisha.

Basi akaviangusha vitendo vyao, havitawafaa kitu.

Je, ambao wana maradhi nyoyoni mwao wanadhani kwamba Mwenyezi Mungu hatazidhihirisha chuki zao?

Wanafiki walificha chuki na uadui kwa Mtume na maswahaba; wakawadhihirishia upendo na utii; wakadhani kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) hatadhihirisha wanayoyaficha vifuani mwao.

Na lau tungelipenda tungelikuonyesha hao na ungeliwatambua kwa alama zao.

Kukuonyesha ni kukutambulisha na kutambua ni kuwatambua kwa alama zao. Lengo la kugawanya huku kunakofanana na kukaririka ni kusisitiza kuwa Mtume hapitwi na kitu anachofahamishwa na Mwenyezi Mungu. Lakini asiyekuwa Mtume anaweza kukosea katika kufahamu kwake.

Dhahiri ya Aya inafahamisha kuwa ilishuka kabla ya Mtume kuwafahamu wanafiki, kutokana na neno ‘lau,’ lakini Mtume(s.a.w.w) aliwatambua baadae kutoka na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

Na bila ya shaka utawajua kwa namna ya usemi wao.

Namna ya usemi ni kule kumaanisha kwake; kama vile udhuru wa uwongo waliokuwa wakiutoa wanafiki na jinsi wanavyowalaumu watu wema na kuwasifu washari na mengineyo yanayojiachia mdomoni yanayaofahamisha ria na unafiki.

Imepokewa Hadith kutoka kwa Anas: “Hakufichika mnafiki kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) , baada ya Aya hii.” Vile vile Nabii(s.a.w.w) alikuwa akiwajuwa wanafiki kwa vitendo vyao. Walikuwa wakiikimbia jihadi na wakiona uzito kujitolea kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Na Mwenyezi Mungu anavijua vitendo vyenu.

Hili ni kemeo kwa kila anayedhihirisha heri na kuficha shari.

Na bila ya shaka tutawajaribu mpaka tuwajue wapignao jihadi katika nyinyi na wanaosubiri. Nasi tutazijaribu habari zenu.

Mwenyezi Mungu anawajua wanaopigana jihadi na walio na subira kabla ya kuwafanyia majaribio, lakini anafanya hivi kwa kuamrisha na kukataza ili amdhihirishe na amtambulishe muovu na mwema kwa vitendo ambavyo vinastahiki adhabu au thawabu.

Imeelezwa katika Nahjul-balagha: “Mwenyezi Mungu anataka mumnusuru na hali yeye ana majeshi ya mbinguni na ardhini na Yeye ni Mwenye nguvu Mwenye hekima. Na anataka mukopeshe na Yeye ana hazina za mbingu na ardhi na Mwenye kujitosha Mwenye kusifiwa…Anataka kuwajaribu ninani wenu mwenye matendo mema zaidi.

Basi harakisheni matendo yenu mtakuwa jirani na Mwenyezi Mungu.”

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ وَشَاقُّوا الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ الْهُدَىٰ لَن يَضُرُّوا اللَّـهَ شَيْئًا وَسَيُحْبِطُ أَعْمَالَهُمْ ﴿٣٢﴾

32. Hakika ambao wamekufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu na wakakinzana na Mtume baada ya kuwabainikia uwongofu, hawatamdhuru Mwenyezi Mungu kwa lolote, na ataviangusha vitendo vyao.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَلَا تُبْطِلُوا أَعْمَالَكُمْ ﴿٣٣﴾

33. Enyi ambao mmeamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake! Mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume; wala msiviharibu vitendo vyenu.

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ثُمَّ مَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ فَلَن يَغْفِرَ اللَّـهُ لَهُمْ ﴿٣٤﴾

34. Hakika ambao wamekufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu, kisha wakafa na hali ni makafiri, Mwenyezi Mungu hatawaghufiria.

فَلَا تَهِنُوا وَتَدْعُوا إِلَى السَّلْمِ وَأَنتُمُ الْأَعْلَوْنَ وَاللَّـهُ مَعَكُمْ وَلَن يَتِرَكُمْ أَعْمَالَكُمْ ﴿٣٥﴾

35. Basi msilegee na kuita kwenye suluhu. Na hali nyinyi ndio mko juu; Na Mwenyezi Mungu yuko pamoja nanyi, Wala hatawanyima malipo ya vitendo vyenu.

إِنَّمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا لَعِبٌ وَلَهْوٌ وَإِن تُؤْمِنُوا وَتَتَّقُوا يُؤْتِكُمْ أُجُورَكُمْ وَلَا يَسْأَلْكُمْ أَمْوَالَكُمْ ﴿٣٦﴾

36. Hakika uhai wa duniani ni mchezo na upuzi. Na mkiamini na mkawa na takua, atawapa ujira wenu, Wala hawaombi mali zenu.

إِن يَسْأَلْكُمُوهَا فَيُحْفِكُمْ تَبْخَلُوا وَيُخْرِجْ أَضْغَانَكُمْ ﴿٣٧﴾

37. Akiwaomba hizo na akiwashikilia mtafanya ubakhili, na atatoa chuki zenu.

هَا أَنتُمْ هَـٰؤُلَاءِ تُدْعَوْنَ لِتُنفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَمِنكُم مَّن يَبْخَلُ وَمَن يَبْخَلْ فَإِنَّمَا يَبْخَلُ عَن نَّفْسِهِ وَاللَّـهُ الْغَنِيُّ وَأَنتُمُ الْفُقَرَاءُ وَإِن تَتَوَلَّوْا يَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُونُوا أَمْثَالَكُم ﴿٣٨﴾

38. Ehee! Nyinyi mnaitwa mtumie katika njia ya Mwenyezi Mungu, Na wapo katika nyinyi wanaofanya ubakhili. Na anayefanya ubakhili basi anajifanyia ubakhili mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, na nyinyi ndio wahitaji. Na mkigeuka atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi.

MSIBATILISHE AMALI ZENU

Aya 32 – 38

MAANA

Hakika ambao wamekufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu na wakakinzana na Mtume baada ya kuwabainikia uwongofu, hawatamdhuru Mwenyezi Mungu kwa lolote, na ataviangusha vitendo vyao.

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w. w ) alilingania kwenye Uislamu kwa dalili na ubainifu; wakakaukataa watu wa masilahi na wakawazuia watu wasiukubali Uislamu kwa kutumia nguvu, mali na propaganda za uwongo.

Lakini Mwenyezi Mungu alimpa nguvu Mtume wake, akaidhihirisha dini yake na akaviangusha vitendo vya wahaini.

Hadi leo Uislamu na waislamu wanakabiliana sana na nguvu za shari. Zilizo hatari zaidi ni baadhi ya dola zinazobeba jina la Uislamu huku zikishirikiana na adui mkubwa zaidi, mkoloni wa kizayuni. Umefika wakati, sasa, waislamu waondoe vumbi la chuki na mfarakano ili waweze kuungana pamoja dhidi ya adui yao mwenye ushirikiano na wenzake.

Enyi ambao mmeamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake!Mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume; yaani fanyeni mambo kwa imani yenu.

Kwa hiyo kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Mtiini Mwenyezi Mungu,’ baada ya kusema: ‘Enyi ambao mmeamini,’ ni sawa na kauli yake:

فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا ﴿١١٠﴾

“Mwenye kutaraji kukutana na Mola wake basi naatende matendo mema.” Juz. 16: (18:110).

Wala msiviharibu vitendo vyenu kwa shirki na unafiki wala kwa masimbulizi na udhia au kwa maovu ambayo huondoa mema. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

إِنَّمَا يَتَقَبَّلُ اللَّـهُ مِنَ الْمُتَّقِينَ ﴿٢٧﴾

“Hakika Mwenyezi Mungu huwapokelea wamchao tu.” Juz. 6 (5:27).

Kuna Hadith isemayo: “Mwenyezi Mungu hakubali matendo ila kwatakua.” Imam Ali(a . s) anasema:“Kwenye matendo, kuweni ni wenye kujishughulisha zaidi na kukubaliwa matendo.”

Hakika ambao wamekufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu, kisha wakafa na hali ni makafiri, Mwenyezi Mungu hatawaghufiria huko Akhera. Kwa sababu Mwenyezi Mungu (s.w.t.) atawafufua watu kulingana na walioyofia na atawahisabu kulingana na walivyomaliza uhai wao kwenye ukafiri au imani.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 2 (2:161) na Juz. 3 (3:91).

QUR’AN NA SIASA YA VITA

Basi msilegee na kuita kwenye suluhu.

Matukio yamethibitisha kwamba mwenye kulegea mbele ya adui yake na akaogopa kumkabili basi ndio amempa silaha atayompigia na kujifanya mnyonge kwake. Imam Ali(a.s ) anasema:“Kuogopa ni kuvunjika moyo na kuona haya ni kusumbuka.”

Tazama Juz. 22 (33: 59-62) kifungu ‘Vita vya nafsi.’

Siasa nzuri ya vita ni kuwa mkakamavu mtu mbele ya adui yake, vile vile asipuuze nguvu za adui, bali ajiandae vizuri na amkabili kwa uimara kabisa bila ya kujali mashaka na tabu atakayoipata.

Qur’an imeandika siasa hii kwa kusema: “Basi msilegee na kuita kwenye suluhu.” Yaani msilegee mbele ya adui mkasalimu amri kwenye nguvu zao na utaghuti wao.

Pia kauli yake: “Na waandalieni nguvu vile muwezavyo.” Juz. 10 (8:60). Yaani msidharau nguvu zao; mjifunge kibwebwe kwa kila nguvu mliyo nayo ya watu na ya kiuchumi.

Na hali nyinyi ndio mko juu; yaani mtashinda, lakini mpaka muungune na kuwa safu moja kumkabili adui wenu na adui wa Mwenyezi Mungu; vinginevyo mtashindwa na haitabakia hata harufu yenu; kama inavyosema Qur’an katika Juz. 10 (8:46).

Na Mwenyezi Mungu yuko pamoja nanyi, mkiitikia mwito wake wa jihadi kwa hali na mali, ili tamko la Mwenyezi Mungu liwe juu ili neno la haki liwe juu na neno la batili liwe chini. Ama yule mwenye kupenda raha na akasalimu amri kwenye nguvu ya upotevu na ufisadi, basi Mwenyezi Mungu ataachana naye na kumwachia aliyejisalimisha naye

Wala hatawanyima malipo yavitendo vyenu kuanzia nafsi, watu au mali iliyotoka kwa ajili ya dini, nchi au haki yoyote. Muhanga huu hauwezi kwenda burebure; bali ni heshima ya dini na nchi katika maisha ya duniani na ni akiba Akhera mbele ya Mwenyezi Mungu.

Unaweza kuuliza : Kauli yake Mwenyezi Mungu: “Basi msilegee na kuita kwenye suluhu na hali nyinyi ndio mko juu,” si inajulisha waziwazi kwamba mwenye nguvu anafaa kumdhibiti mnyonge bila ya kuwa na huruma naye wala kuwa na suluhu naye? Bila shaka hili linapingana na ubinadamu na uadilifu, wala haliafikiani na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً ﴿٢٠٨﴾

“Enyi ambao mmeamini! Ingieni kwenye usalama nyote” Juz. 2 (2:208)?

Jibu : kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Basi msilegee na kuita kwenye suluhu na hali nyinyi ndio mko juu,” maana yake ni ikiwa mtapata balaa ya adui aliye mnyama asiyekuwa na kipimo cha haki wala uadilifu wala hajilazimishi na kanuni wala ahadi na pia hafahamu lugha yoyote isipokuwa nguvu. Mkifikiwa na adui wa aina hii basi nilazima mkabiliane; msimwogope wala msiwe na huruma katika haki. Kummaliza adui huyu ni kuimaliza shari na kuleta heri ya wote.

Ajabu ya sadfa! Imetokea wakati nikiandika maneno haya leo hii 8 April 1970, Israil, ikitumia ndege aina Phantoum ya Amerika na makombora yake, imeshambulia shule ya msingi ya Bahrul-baqar katika Jamhuri ya Umoja wa Kiarabu [3] 1, na kuua watoto 47, na kujeruhi kadhaa, wenye umri wa kati ya miaka 6 hadi 12.

Bila shaka U.S.A. ndiyo inayobeba majukumu ya kuuliwa watoto wadogo wasiokuwa na hatia yoyote. Na pia majukumu ya mashambulizi ya mfano huo yaliyotokea katika kiwanda cha Aba Za’abal yaliyowaacha wahanga 33 majeruhi na waliouawa.

Amerika ndio yenye majukumu, kwa vile ndiyo iliyoisheheni Israil kwa silaha na mali na ikaamrisha iwafanyie waarabu; kama hiyo yenyewe inavyoifanyia Vietnam. Vyombo vya habari vimenukuu kuwa jeshi la Amerika limesambaratisha mji mzima katika Vietnam. Hakuokoka katika mji huo mtoto wala mwanamke. Mji huu na mashule yake unahusiana vipi na vita?!

Je, usalama utakuweko na wanyama hawa? Jamani! Pengine labda maana ya usalama yawe ni kusalimu amri kwa madhalimu na waasi!

Hakika uhai wa duniani ni mchezo na upuzi kwa mwenye kuipondokea na akahadaika na ubatilifu wake; bali ni shari hasa kwa mwenye kuanzisha vita kwa ajili ya dunia. Na ni nyumba ya heri kwa mwenye kuwaidhika nayo na akaifanya ni maandalizi ya Akhera yake.

Na mkiamini na mkawa na takua atawapa ujira wenu.

Kuunganisha takua na imani kunafahamisha kuwa kuamini tu na kusadikisha hakuna malipo mbele ya Mwenyezi Mungu; bali hapana budi kuweko na vitendo pamoja na imani. Ufafanuzi zaidi wa Aya hii ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجْرَ مَنْ أَحْسَنَ عَمَلًا ﴿٣٠﴾

“Hakika wale ambao wameamini na wakatenda mema, hakika sisi hatupotezi ujira wa anayefanya mazuri.”Juz. 15 (18:30)

Wala hawaombi mali zenu. Na akiwaomba hizo na akiwashikilia mtafanya ubakhili, na atatoa chuki zenu.

Makusudio ya hawaombi ni hawataki mtoe mali yote wala kutoa mali nyingi ya kuwadhuru. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) amejaalia fungu la mafukara katika mali ya matajiri na akachunga kiwango cha kutosheleza mahitaji na vile vile masilahi ya watowaji wasidhurike.

Lau kuwa Mwenyezi Mungu, ambaye imetukuka hekima yake, angeliwataka matajiri zaidi kiwango hiki na akawahimiza kutoa, basi wangelizuia na wangekua na chuki na Uislamu na Nabii.

Ehee! Nyinyi mnaitwa mtumie katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Kundi la wafasiri wamesema kuwa Makusudio ya njia ya Mwenyezi Mungu ni jihadi. Usahihi ni kuwa inakusanya kila lililo na radhi ya Mwenyezi Mungu na masilahi ya watu kwa namna moja au nyingine.

Na wapo katika nyinyi wanaofanya ubakhili. Na anayefanya ubakhili basi anajifanyia ubakhili mwenyewe.

Bakhili anamnyima Mwenyezi Mungu na kujilimbikizia mwenyewe, lakini natija inakuwa kinyume na anavyotaka; pale anapoiweka nafsi yake kwenye ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na kuinyima radhi zake na thawabu zake. Tazama kifungu; ‘Mali ndio sababu ya ugomvi’ mwanzo wa Juz. 4 (3:92).

Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, na nyinyi ndio wahitaji wa fadhila zake na rehma zake. Hakupata ukwasi mja yeyote ila kwa sababu inayotoka kwake. Ama Yeye Mwenyezi Mungu ni mkwasi kwa dhati yake sio kwa kufaidika, ni mtendaji sio kwa kutumia ala, na ni mkadiriaji sio kwa kufikiria.

Na mkigeuka atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi.

Kama mkiupinga mwito wa Mwenyezi Mungu na mkang’ang’ania uasi na ujeuri basi atawaondoa na awalete wengine watakaomsabihi na kumsifu bila ya kumuasi na lolote. Umetangulia mfano wake katika Juz. 13 (14:19) na Juz. 22 (35:16).

MWISHO WA SURA YA ARUBAINI NA SABA: SURAT MUHAMMAD