TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE Juzuu 24

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE0%

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE Mwandishi:
: HASANI MWALUPA
Kundi: Qurani tukufu

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

Mwandishi: Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya
: HASANI MWALUPA
Kundi:

Matembeleo: 25966
Pakua: 3227


Maelezo zaidi:

Juzuu 1 Juzuu 2 Juzuu 3 Juzuu 4 Juzuu 5 Juzuu 6 Juzuu 7 Juzuu 8 Juzuu 12 Juzuu 13 Juzuu 14 Juzuu 15 Juzuu 16 Juzuu 17 Juzuu 18 Juzuu 19 Juzuu 20 Juzuu 21 Juzuu 22 Juzuu 23 Juzuu 24
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 30 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 25966 / Pakua: 3227
Kiwango Kiwango Kiwango
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE Juzuu 24

Mwandishi:
Swahili

19

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

Sura Ya Sabini Na Mmoja: Surat Nuh. Imeshuka Makka Ina Aya 28.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

إِنَّا أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ أَنْ أَنذِرْ قَوْمَكَ مِن قَبْلِ أَن يَأْتِيَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١﴾

1. Hakika Sisi tulimtuma Nuhu kwa watu wake: Uwaonye kaumu yako kabla ya kuwafikia adhabu chungu.

قَالَ يَا قَوْمِ إِنِّي لَكُمْ نَذِيرٌ مُّبِينٌ ﴿٢﴾

2. Akasema: Enyi watu wangu! Kwa hakika mimi ni mwonyaji wa dhahiri kwenu,

أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاتَّقُوهُ وَأَطِيعُونِ ﴿٣﴾

3. Ya kwamba mumuabudu Mwenyezi Mungu, na mumche, na munitii.

يَغْفِرْ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمْ وَيُؤَخِّرْكُمْ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى إِنَّ أَجَلَ اللَّـهِ إِذَا جَاءَ لَا يُؤَخَّرُ لَوْ كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٤﴾

4. Atawaghufiria miongoni mwa madhambi yenu, na atawaakhirisha mpaka muda uliowekwa. Hakika muda wa Mwenyezi Mungu utapofika haucheleweshwi. Laiti mnge­jua!

قَالَ رَبِّ إِنِّي دَعَوْتُ قَوْمِي لَيْلًا وَنَهَارًا ﴿٥﴾

5. Akasema: Ee Mola wangu! Hakika mimi nimewalingania watu wangu usiku na mchana.

فَلَمْ يَزِدْهُمْ دُعَائِي إِلَّا فِرَارًا ﴿٦﴾

6. Lakini mlingano wangu haukuwazidisha ila kukimbia.

وَإِنِّي كُلَّمَا دَعَوْتُهُمْ لِتَغْفِرَ لَهُمْ جَعَلُوا أَصَابِعَهُمْ فِي آذَانِهِمْ وَاسْتَغْشَوْا ثِيَابَهُمْ وَأَصَرُّوا وَاسْتَكْبَرُوا اسْتِكْبَارًا ﴿٧﴾

7. Na hakika mimi kila nilipowai­ta ili upate kuwaghufiria, wali­jiziba masikio yao kwa vidole vyao, na wakajigubika nguo zao, na wakakamia, na wakafanya kiburi kingi!

ثُمَّ إِنِّي دَعَوْتُهُمْ جِهَارًا ﴿٨﴾

8. Tena niliwalingania kwa uwazi,

ثُمَّ إِنِّي أَعْلَنتُ لَهُمْ وَأَسْرَرْتُ لَهُمْ إِسْرَارًا ﴿٩﴾

9. Kisha nikawatangazia, tena nikasema nao kwa siri.

فَقُلْتُ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ إِنَّهُ كَانَ غَفَّارًا ﴿١٠﴾

10. Nikasema: Ombeni maghufira kwa Mola wenu; hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe.

يُرْسِلِ السَّمَاءَ عَلَيْكُم مِّدْرَارًا ﴿١١﴾

11. Atawaletea mvua nyingi.

وَيُمْدِدْكُم بِأَمْوَالٍ وَبَنِينَ وَيَجْعَل لَّكُمْ جَنَّاتٍ وَيَجْعَل لَّكُمْ أَنْهَارًا ﴿١٢﴾

Na atawapa mali na wana, na atawapa mabustani na atawafanyia mito.

NILIWALINGANIA WATU WANGU

Aya 1 - 12

MAANA

Hakika Sisi tulimtuma Nuhu kwa watu wake: Uwaonye kaumu yako kabla ya kuwafikia adhabu chungu.

Sheikh Abdul-qadir Al-Maghrib, akifasiri Aya hizi alinukuu vitabu vya mwanzo mwanzo kwamba Historia ya kuabudu masanamu inaanzia zama za Anush bin Shith bin Adam, na kwamba wakati wa Nuh shirki ilifikia ukomo, ndio akachaguliwa na Mwenyezi Mungu kupambana na shiriki hii na kuwaonya washirikina na maangamizi kama watanga’ang’ania upotevu.

Jina halisi la Nuh ni Raha, na baina ya Nuh na babu yake mkubwa Adam, kuna miaka 1056. Ilipotokea tufani umri wake ulikuwa ni miaka 600, na aliishi miaka 350 baada ya hapo. alimuwahi mjukuu wake Ibrahim na akaishi naye zaidi ya nusu karne. Baada ya Nuh kuokoka na tufani alilima na kupanda kwenye ardhi.

Huu ni muhtasari wa aliyoyanukuu Al-Maghribi kutoka kwenye vitabu hivyo, Mwenyezi Mungu ndiye mjuzi zaidi.

Akasema: Enyi watu wangu! Kwa hakika mimi ni mwonyaji wa dhahiri kwenu. Ya kwamba mumuabudu Mwenyezi Mungu, na mum­che, na munitii.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimtuma Nuhu kwa watu kwa mambo matatu: Kwanza, Waache kuabudu masanamu na kumwabudu Mungu mmoja. Pili, wafanye kheri na wajiepushe na shari. Tatu, wamtii katika yale aliy­owaamrisha na kuwakataza. Akawadhaminia mambo mawili kwa Mwenyezi Mungu, kama wataitikia:

La kwanza:Atawaghufiria miongoni mwa madhambi yenu, mliyoy­afanya kabla ya imani, kwa sababu imani inafuta yaliyo kabla yake, lakini yale madhambi mtakayoyafanya baada ya imani mtakua na majukumu nayo. Haya yanashiriwa na neno ‘miongoni mwa dhambi yenu.’

La pili:Na atawaakhirisha mpaka muda uliowekwa. Hakika muda wa Mwenyezi Mungu utapofika haucheleweshwi.

Mkimwamini Mwenyezi Mungu peke yake atawaondolea adhabu ya kuangamizwa na tufani nk, atawapa muda wa kumaliza umri wa kawaida na mwenye dhambi atampa muda hadi siku ya Kiyama; vinginevyo atawa­harakishia adhabu ya kuangamia duniani.

Laiti mngejua , kuwa Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na wanay­oyafanya madhalimu.Akasema: Ee Mola wangu! Hakika mimi nimewalingania watu wangu usiku na mchana, Lakini mlingano wangu haukuwazidisha ila kukimbia.

Maana ya usiku na mchana ni daima. Nuhu aliwaita kwenye haki na akawasisitiza, mpaka: “Wakasema: Ewe Nuh! Umejadiliana nasi na ume­zidishi kutujadili.” Juz. 12 (11:32), lakini yeye aliendelea na mwito wake na wao wakaendelea na inadi yao.

Na hakika mimi kila nilipowaita ili upate kuwaghufiria, walijiziba masikio yao kwa vidole vyao, na wakajigubika nguo zao, na wakaka­mia, na wakafanya kiburi kingi!

Walijiziba masikio kwa vidole ili wasisikie mwito wa haki, na walijifuni­ka nguo ili wasiuone uso wa mwenye kulingania. Hii inaweza kuwa ni hakika hasa, na pia inaweza kuwa ni kwa majazi ya inadi yao. Vyovyote iwavyo, maana ni moja tu, nayo ni kuikataa haki kwa kiburi. Nuh wal­imuona ana daraja ya chini kuliko wao, kwa hiyo wakaona vipi wanaweza kuwa wafuasi wake? Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwasimulia wao:

وَمَا نَرَاكَ اتَّبَعَكَ إِلَّا الَّذِينَ هُمْ أَرَاذِلُنَا بَادِيَ الرَّأْيِ وَمَا نَرَىٰ لَكُمْ عَلَيْنَا مِن فَضْلٍ ﴿٢٧﴾

“Wala hatukuoni wamekufuata ila wale wanaonekana dhahiri kwetu kuwa ni watu duni, wala hatuwaoni kuwa mnayo ziada juu yetu.” Juz. 12 (11:27).

Tena niliwalingania kwa uwazi, Kisha nikawatangazia, tena nikasema nao kwa siri.

Kundi la wafasiri wamesema kauli ya Nuh ya kwanza: Nimewalingia watu wangu usiku na mchana, na kauli ya pili: Tena niliwalingania kwa uwazi na kauli ya tatu: kisha nikawatangazia na nikasema nao kwa siri, zinajul­isha kuwa mwito wake ulikuwa na daraja tatu: aliuanza kwa siri, kisha aka­ufanya wazi, tena mara ya tatu akautangaza na kuufanya siri pamoja.

Kauli hii haiko mbali na dhahiri ya Aya, lakini inawezekana pia kuwa makusudio ya maunganishi haya na kukaririka huku ni kuwa yeye aliwalingania kwa kila mfumo bila ya kuchoka, lakini pia haikufaa kitu.

Nikasema: Ombeni maghufira kwa Mola wenu; hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe. Atawaletea mvua nyingi. Na atawapa mali na wana, na atawapa mabustani na atawafanyia mito.

Ikiwa watamwamini Mwenyezi Mungu peke yake na wakamfanyia ikhlasi kwa kauli na vitendo, basi Nuhu atawadhaminia kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) awasamehe maovu yao yaliyoopita na awatoshelezee katika fadhi­la zake kwa mali na watoto; mbingu zimimine heri zake na ardhi nayo itoe mazao yake na wawe na siha, amani, raha pamoja na kuzidi kizazi.

IMANI NA RAHA

Aya hizi zimeifunga raha na amani kuwa lazima ziwe pamoja na imani na takua, lakini inavyoonekana ni kinyume na hivyo. hai ni Marekani (U.S.A.). Inajulikana kuwa hiyo ndio dola iliyo na ubabe kuliko yoyote duniani, ndiyo yenye ufisadi na uadui zaidi; mpaka ikajiwekea msingi kuwa asiyekuwa mtumwa wake basi huyo ni adui yake. Sote tunajua siasa yao hiyo jinsi ilivyoleta majanga - hakuna damu inayomwagika au ufisadi unajitokeza mashariki mwa dunia na magharibi ila Marekani ina mkono wake, kwa namna moja au nyingine. Hakuna mhaini yeyote wa nchi yake ila wanamtukuza.

Pamoja na haya yote hiyo ndio dola tajiri na yenye nguvu zaidi ulimwen­guni. Ushahidi wa hilo ni kuwa pato lake ni asilimia 43 ya pato lote la ulimwengu na hali wakazi wake ni asilimia 6 tu ya wakazi wote waulimwengu[8] .

Sasa kuna wajihi wa kuunganisha haya na dhahiri ya Aya inayoifunga raha na imani?

Jibu :kwanza , Aya hizi zilihusiana na watu wa Nuh, na hakuna dalili ya kuwa zinaenea, ili zihusaiane na wengine. Kuongezea kuwa Mwenyezi Mungu ana muamala maalum na umma unaoonywa na mitume wake moja kwa moja.

Pili , utajiri wa U.S.A. unatokana na shetani sio na Mwenyezi Mungu, kwa sababu zaidi sana umetokana na uporaji na unyang’anyi.

Tatu , Aya hizi zimeunganisha baina ya imani na raha ya dunia na Akhera kwa pamoja. Sio imani na raha ya dunia peke yake: “Wala wasidhanie kabisa wale waliokufuru kwamba muda tunaowapa, ni heri kwa nafsi zao. Hakika tunawapa muda na wanazidi tu katika (kufanya) dhambi na wana wao adhabu idhalilishayo.” Juz. 4 (3:178).

Nne , umejuaje kuwa Amerika na dola nyingine dhalimu ziko kwenye amani? Ni nani mwenye akili anayejiaminisha na majanga? Je, himaya ya Roma ilidumu? Au ya uingereza na himaya nyinginezo zilidumu mpaka udumu ufidhuli wa USA?

Hizi hapa dalili za kuanguka zinaanza kujitokeza, kuanzia mawimbi ya ukombozi ulimwenguni kote hadi kwenye mapinduzi ya watu weusi wap­atao milioni thalathini ndani ya USA. Na kuanzia utawala wa ujasusi wakuua na kuanzisha vita hadi kwenye bangi na madawa ya kulevya, na kuanzia ugomvi na uadui pamoja na watu wa mabara yote matano hadi kwa raisi anayewalinda wezi na wamwagaji damu na mengine yasiyokuwa na kikomo.

Ni muhali kudumu amani na raha kwa mfumo huu wa kushangaza.

Ajabu ni sadfa iliyotokea wakati nikandika maneno haya nikasoma gazeti la Aljumhuriya la Misr la tarehe 10 ‧ 7- 1970, likinukuu magazeti ya New York, kwamba mashoga wapatao elfu tano wazee kwa vijana wamean­damana kwenye barabara za New York, wakibeba mabango wakitaka serikali ihalalishe ulawiti, kwa kuiga wanawake waaliohalalishiwa kujiuza miili yao (umalaya).

Kwenye gazeti la News wee^ la tarehe 12 -7-1970, kuna maelezo kuwa kasisi Barry ambaye ni mashuhuri kwa ulawiti alitoa mwito wa kueneza ulawiti na usagaji, kwa sababu mambo hayo mawili ni katika upendo wa Mungu. Mwito wake huu umeenea na kuwa na wafuasi wengi katika pembe zote za USA.

Hakuna mwenye shaka kwamba katika mashoga na mabasha hawa wata­tokea viongozi watakaotawala siasa za usalama na vita, mambo ya elimu na kazi katika jamii ya Marekani. Hapo ndio itakuwa USA ni duni kuliko nyumba ya buibui.

مَّا لَكُمْ لَا تَرْجُونَ لِلَّـهِ وَقَارًا ﴿١٣﴾

13. Mna nini hamumwekei heshi­ma Mwenyezi Mungu?

وَقَدْ خَلَقَكُمْ أَطْوَارًا ﴿١٤﴾

14. Na hali Yeye amewaumba katika hali mbalimbali?

أَلَمْ تَرَوْا كَيْفَ خَلَقَ اللَّـهُ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ طِبَاقًا ﴿١٥﴾

15. Kwani hamwoni jinsi Mwenyezi Mungu alivyoziumba mbingu saba kwa matabaka?

وَجَعَلَ الْقَمَرَ فِيهِنَّ نُورًا وَجَعَلَ الشَّمْسَ سِرَاجًا ﴿١٦﴾

16. Na akaufanya mwezi ndani yake uwe nuru, na akalifanya jua kuwa taa?

وَاللَّـهُ أَنبَتَكُم مِّنَ الْأَرْضِ نَبَاتًا ﴿١٧﴾

17. Na Mwenyezi Mungu ame­waotesha katika ardhi kama mimea.

ثُمَّ يُعِيدُكُمْ فِيهَا وَيُخْرِجُكُمْ إِخْرَاجًا ﴿١٨﴾

18. Kisha atawarudisha humo na atawatoa tena.

وَاللَّـهُ جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ بِسَاطًا ﴿١٩﴾

19. Na Mwenyezi Mungu ame­wafanyia ardhi kuwa busati.

لِّتَسْلُكُوا مِنْهَا سُبُلًا فِجَاجًا ﴿٢٠﴾

Ili mtembee humo katika njia zilizo pana.

AMEWAUMBA KATIKA HALI MBALIMBALI

Aya 13 - 20

MAANA

Mna nini hamumwekei heshima Mwenyezi Mungu? Na hali Yeye ame waumba katika hali mbalimbali?

Nuhu anawakana watu wake huku akiwashangaa, vipi hawamwogopi Mwenyezi Mungu pamoja na utukufu wake, na hali wanajua kwamba Yeye amewaumba kwa mchanga, kisha kwa tone la manii, kisha kwa pande la damu. Anaendela hivi hadi kuwa mkongwe.

Vile vile anawaelekeza kuuangalia uwezo wa Mwenyezi Mungu katika kuumba mbingu na ardhi na sayari, akasema:

Kwani hamwoni jinsi Mwenyezi Mungu alivyoziumba mbingu saba kwa matabaka?

Chunguzeni na mzingatie umbile la mbingu na nidhamu yake inayojulisha kupatikana mtengenezaji mwenye hikima. Umetangulia mfano wake kati­ka Juzuu hii tuliyo nayo kwenye sura (67:3). Pia tumeifafanua kidogo kati­ka Juz. 28 (66:12).

Kauli ya Nuh inafahamisha kuwa watu wake walikuwa pia wakiamini kuwa mbingu ni saba na kwamba itikadi hii ilianzia zamani za kale.

Na akaufanya mwezi ndani yake uwe nuru, na akalifanya jua kuwa taa?

Ndani yake ni ndani ya mkusanyiko wake. Mwenyezi Mungu (s.w.t) amelipa Jua sifa ya taa na mwezi kuwa ni nuru, kwa sababu taa ndio chim­buko la nuru na Jua nalo ni chimbuko la mwezi na mwanga wake unaenea na una manufaa zaidi kuliko wa mwezi. Umetangulia mfano wake katika Juz. 11(10:5).

Na Mwenyezi Mungu amewaotesha katika ardhi kama mimea. Kisha atawarudisha humo na atawatoa tena.

Huyu ndiye mwanadamu. Ameumbwa kutokana na ardhi, kisha arudishwe humo, tena atolewe humo. Umetangulia mfano wake katika Juz. 16 (20:55).

Na Mwenyezi Mungu amewafanyia ardhi kuwa busati ili mtembee humo katika njia zilizo pana.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) amefanya njia pana katika ardhi ili watu wayaendee makusudio yao. Umetangulia mfano wake katika Juz. 17 (21:32).

قَالَ نُوحٌ رَّبِّ إِنَّهُمْ عَصَوْنِي وَاتَّبَعُوا مَن لَّمْ يَزِدْهُ مَالُهُ وَوَلَدُهُ إِلَّا خَسَارًا ﴿٢١﴾

21. Nuh akasema: Mola wangu! Hakika hao wameniasi, na wamemfuata yule ambaye mali yake na wanawe hawakumzidishia ila hasara.

وَمَكَرُوا مَكْرًا كُبَّارًا ﴿٢٢﴾

22. Na wakapanga vitimbi vikub­wa.

وَقَالُوا لَا تَذَرُنَّ آلِهَتَكُمْ وَلَا تَذَرُنَّ وَدًّا وَلَا سُوَاعًا وَلَا يَغُوثَ وَيَعُوقَ وَنَسْرًا ﴿٢٣﴾

23. Na wakasema: Msiwaache miungu yenu; msimwache Wadda wala Suwaa wala Yaghutha, wala Yau’qa, wala Nasra.

وَقَدْ أَضَلُّوا كَثِيرًا وَلَا تَزِدِ الظَّالِمِينَ إِلَّا ضَلَالًا ﴿٢٤﴾

24. Na hao walikwisha wapoteza wengi, wala usiwazidishie waliodhulumu ila kupotea.

مِّمَّا خَطِيئَاتِهِمْ أُغْرِقُوا فَأُدْخِلُوا نَارًا فَلَمْ يَجِدُوا لَهُم مِّن دُونِ اللَّـهِ أَنصَارًا ﴿٢٥﴾

25. Basi kwa ajili ya makosa yao kuwanusuru badala ya Mwenyezi Mungu.

وَقَالَ نُوحٌ رَّبِّ لَا تَذَرْ عَلَى الْأَرْضِ مِنَ الْكَافِرِينَ دَيَّارًا ﴿٢٦﴾

26. Na Nuh akasema: Mola wangu! Usimwache juu ya ardhi mkaazi wake yeyote katika makafiri!

إِنَّكَ إِن تَذَرْهُمْ يُضِلُّوا عِبَادَكَ وَلَا يَلِدُوا إِلَّا فَاجِرًا كَفَّارًا ﴿٢٧﴾

27. Hakika ukiwaacha wata­wapoteza waja wako, wala wao hawatazaa ila waovu makafiri.

رَّبِّ اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِمَن دَخَلَ بَيْتِيَ مُؤْمِنًا وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَلَا تَزِدِ الظَّالِمِينَ إِلَّا تَبَارًا ﴿٢٨﴾

28. Mola wangu! Nighufirie mimi na wazazi wangu, na kila aliyeingia nyumbani mwangu kuwa ni mumin, na waumini wanaume, na waumini wanawake; na wala usi­wazidishie waliodhulumu

ila kuangamia.

WALA MSIMWACHE WADDA WALA SUWAA

Aya 21 - 28

MAANA

Nuhu akasema: Mola wangu! Hakika hao wameniasi, na wamemfua­ta yule ambaye mali yake na wanawe hawakumzidishia ila hasara.

Hii ni ripoti au mashtaka kutoka kwa Nuh kwenda kwa Mola wake, akimwambia Mola wangu na Bwana wangu! Umenituma kuwaongoza waja wako washirikina, nimetekeleza ujumbe kwa njia yake, lakini wao wamenipinga, wakawaitikia viongozi walioingiwa na kiburi kutokana na mali na watoto. Kila wanavyozidi mali na watoto, basi wanazidi kufuru, inadi na kuwa na nguvu ya kupiga vita haki na watu wake, kwa kupupia jaha na chumo lao.

Na wakapanga vitimbi vikubwa.

Yaani hao viongozi waliopituka mipaka. Makusudio ya vitimbi vyao, ni mifumo waliyookuwa wakiitumia kuwazuia wanyonge kuwa na imani; miongoni mwayo ni kusema kwao:Na wakasema: Msiwaache miungu yenu; yaani msiache kuabudu masanamu kwa ibada ya Mungu mmoja.

Walikuwa na masanamu mengi; yaliyokuwa muhimu na shani kwao ni matano, ndio maana wakayahusisha kuyataja na wakasema:msimwache Wadda wala Suwaa wala Yaghutha, wala Yau’qa, wala Nasra.

Nuh alikuwa akitilia mkazo sana kukataza ibada ya haya masanamu matano, kwa sababu ndiyo yaliyokuwa makubwa.

Jamaa katika wafasiri wamesema kuwa haya matano yaliabudiwa wakati wa jahilia hadi wakati wa Mtume Mtukufu(s.a.w.w) , na Wadda alikuwa wa kabila la Kalb, Suwaa ni wa Hudhayl, Yaghutha ni wa Ghatwif, Yau’qa ni wa Hamadan na Nasra ni wa Himyar. Pia kuna masanamu mengine ya watu wengine; kama vile Lata, Uzza, Hubal na Manat.

Na hao walikwishawapoteza wengi, wala usiwazidishie waliodhulumu ila kupotea.

Viongozi waliopituka mipaka wamewapoteza. Makusudio ya kupotea ni kuangamia; mfano kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

إِنَّ الْمُجْرِمِينَ فِي ضَلَالٍ وَسُعُرٍ ﴿٤٧﴾

“Hakika wakosefu wamo katika upotofu na mioto.” Juz. 27 (54:47).

Basi kwa ajili ya makosa yao waligharikishwa wakaingizwa Motoni, wala hawakuwapata wa kuwanusuru badala ya Mwenyezi Mungu.

Aya hii ni maneno yaliyooingilia kati maneno ya Nuh na dua yake, lakini yameyakamilisha. Maana yake ni kuwa watu wa Nuh waling’ang’ania ukafiri na upotevu, ndio Mwenyezi Mungu akawapatiliza kwa tufani, na adhabu ya Akhera ni kali na yenye kubaki, wala hakuna yoyote atakayeokoka nayo.

Na Nuh akasema: Mola wangu! Usimwache juu ya ardhi mkaazi wake yeyote katika makafiri!

Yaani usimbakishe yeyote. Nuh hakuomba dua hii ila baada ya kupata wahyi usemao:

وَأُوحِيَ إِلَىٰ نُوحٍ أَنَّهُ لَن يُؤْمِنَ مِن قَوْمِكَ إِلَّا مَن قَدْ آمَنَ فَلَا تَبْتَئِسْ بِمَا كَانُوا يَفْعَلُونَ ﴿٣٦﴾

“Akaletewa wahyi Nuh kuwa hataamini katika watu wako isipokuwa yule aliyoekwishaamini.

Basi usisikitike kwa waliyokuwa wakiyatenda.” Juz. 12 (11:36).

Hakika ukiwaacha watawapoteza waja wako, wala wao hawatazaa ila waovu makafiri.

Hii inafahamisha kwamba ukafiri na uovu umepituka mipaka kwenye jamii ya watu wa Nuh, kiasi ambacho kila anayeinukia anakuwa ni kafiri muovu. Inajulikana kwamba nafsi ya mtoto ni kama kioo, inaakisi kila linalomzunguka.

Kuna riwaya inayosema kuwa mtu alikuwa anamchukua mtoto wake hadi kwa Nuh na kumwambia jihadhari na huyu - yaani Nuh - kwa sababu ni muongo, na baba yangu aliniusia kama ninavyokuusia wewe. Basi mkubwa anakufa akiwa na hilo na mtoto naye anainukia nalo.

Mola wangu! Nighufirie mimi na wazazi wangu, na kila aliyoeingia nyumbani mwangu kuwa ni mumin, na waumini wanaume, na wau­mini wanawake.

Baada ya kuwaduilia makafiri, alimuomba Mwenyezi Mungu maghufira yeye na wazazi wake wawili, na kila aliyeamani katika watu wake na wato­to wake aliowakusudia katika kauli yake: ‘aliyeingia nyumbani mwangu.’ Vile vile alimuombea kila mumin mwanamume na mwanamke kuanzia Adam hadi siku ya ufufuo Na wala usiwazidishie waliodhulumu ila kuangamia, kwa yule aliyekataa maangamizi na Moto.

Katika Kamusi ya Kitabu kitakatifu imeelezwa: “Athari zilizofukuliwa zimedhihirisha kuwa tukio la gharika lilikuwa tukio halisi, na kwamba kisa hiki kilianza kuandikwa baina ya miaka 1590 ‧ 1595 BC (kabla ya kuzalia Nabii Isa). Tazama Juz. 12 (11:45-49) kifungu cha “Tufani imethibiti kwa umma nyinginezo.”

Hapa kuna swali linajitokeza: Je, tufani iliyofahamishwa na athari zilizofukuliwa na ikaelezwa kwenye vitabu vya kale ni ya Nuh au ni nyingine?

Jibu : vyovyote iwavyo, ni kuwa Tufani ya Nuh haiwezi kuzuia tufani nyingine kutokea. Kila wakati kunatokea tufani moja au zaidi katika sehemu yoyote katika ardhi. Inawezekena kuwa Tufani ya Nuh ilienea, au ilihusu sehemu fulani katika ardhi. Hakuna nukuu wazi katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu inayofahamisha kuwa ilikuwa hiyo tu.

MWISHO WA SURA YA SABINI NA MMOJA: SURAT NUH

20

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

Sura Ya Sabini Na Mbili: Surat Al-Jinn. Imeshuka Makka Ina Aya 28.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِّنَ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا ﴿١﴾

1. Sema: Nimepewa wahyi ya kuwa kundi moja la majini lilisikiliza, na likasema: Hakika sisi tumeisikia Qur’an ya ajabu!

يَهْدِي إِلَى الرُّشْدِ فَآمَنَّا بِهِ وَلَن نُّشْرِكَ بِرَبِّنَا أَحَدًا ﴿٢﴾

2. Inaongoza kwenye uwongofu, kwa hivyo tumeiamini, wala hatutamshirikisha yeyote na Mola wetu.

وَأَنَّهُ تَعَالَىٰ جَدُّ رَبِّنَا مَا اتَّخَذَ صَاحِبَةً وَلَا وَلَدًا ﴿٣﴾

3. Na kwa hakika utukufu wa Mola wetu umetukuka; hakuji­fanyia mke wala mwana.

وَأَنَّهُ كَانَ يَقُولُ سَفِيهُنَا عَلَى اللَّـهِ شَطَطًا ﴿٤﴾

4. Na kwa hakika mpumbavu miongoni mwetu alikuwa akise­ma juu ya Mwenyezi Mungu ya kupituka mipaka.

وَأَنَّا ظَنَنَّا أَن لَّن تَقُولَ الْإِنسُ وَالْجِنُّ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا ﴿٥﴾

5. Nasi tulidhani kuwa watu na majini hawatasema uwongo juu ya Mwenyezi Mungu.

وَأَنَّهُ كَانَ رِجَالٌ مِّنَ الْإِنسِ يَعُوذُونَ بِرِجَالٍ مِّنَ الْجِنِّ فَزَادُوهُمْ رَهَقًا ﴿٦﴾

6. Na hakika walikuwako wanaume katika watu walio kuwa wakitafuta kujikinga kwa wanaume katika majini; kwa hivyo wakawazidisha mzigo.

وَأَنَّهُمْ ظَنُّوا كَمَا ظَنَنتُمْ أَن لَّن يَبْعَثَ اللَّـهُ أَحَدًا ﴿٧﴾

7. Na hakika wao walidhani, kama mlivyodhani nyinyi, kuwa Mwenyezi Mungu hatam­tuma Mtume.

KUNDI MOJA LA MAJINI

Aya 1 – 7

MAANA

Sema: Nimepewa wahyi ya kuwa kundi moja la majini lilisikiliza, na likasema: Hakika sisi tumeisikia Qur’an ya ajabu!

Jinni ni uhakika na uhalisia, hatii shaka juu hilo mumin, kwa sababu Aya za Qur’an yenye hikima, zimethibitisha hilo, kwa njia isiyokubali shaka wala taawili (tafsiri nyingine). Tutazifanyia vipi taawili kauli zake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Wakimfanyia alipendalo, kama mihrabu na masanamu na sinia kubwa kama mahodhi, na masufuria makubwa yasiy­oondoka mahali pake.” Juz. 22 (34:13). “Akasema Afriti katika majini: mimi nitakuletea” Juz. 19 (27:39). “Sisi tumesikia Kitabu kilichoteremshwa baada ya Musa.” Juz. 26 (46:30). Pia Aya zilizo katika sura hii tuliyo nayo.

Je, tuziletee taawili ya virusi vya magonjwa, au redio na vinginevyo katika vifaa vya elektroni?

Ukisema: Sayansi haikuthibitisha kuweko majini, nasi tutasema: Je, katika sayansi kuna linalopinga kuweko majini? Je, sayansi imemaliza kugundua vilivyomo ulimwenguni vyote, vya dhahiri na batini? Ni mtaalamu gani wa zamani au wa sasa anayejijua uhakika wake na akili yake? Au hata kuujua mwili wake wa hisia na wa dhahiri, ikiwemo mishipa na nywele?

Asiyejijua yeye mwenyewe hawezi kumjua mwenginewe; hasa yaliyo katika ulimwengu wa ghaibu.

Wahyi umethibitisha kuweko majini na Malaika, kwa hiyo ni wajibu kuamini kuweko; atakayekanusha, basi ni lazima athibitishe ukanusho wake kwa akili au wahyi; sawa na ilivyothibitishwa.

Baada ya hayo, ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimjulisha Nabii wake mtukufu kuwa kundi la majini walimsikiliza akisoma Kitabu cha Mwenyezi Mungu, wakakifahamu na kuzingatia maana yake; wakapigwa na mshangao kutokana na mpangilio na maana yake makuu; wakaambiana: jamani mnaionaje hii Qur’an? Je, mmeshawahi kusikia kitu mfano wake? Hakika ni muujiza na kwambaInaongoza kwenye uwongofu , inaelekeza, kutoa mwongozo, kuaamrisha na kupendekeza kwenye kila heri. Pia inafahamisha, kukataza na kuonya kila shari.

Kwa hivyo tumeiamini, wala hatutamshirikisha yeyote na Mola wetu.

kwa sababu Yeye ni Muweza wa kila kitu. Na mwenye uweza wa kila kitu basi hahitajii washirika, na kama atataka msaada maana yake ni kuwa anashindwa, na mwenye kushindwa hawezi kuwa Mungu.

Na kwa hakika utukufu wa Mola wetu umetukuka; hakujifanyia mke wala mwana.

Ametakata Mola wetu na kujifanyia watoto na ametakata kuwagusa wanawake. Vipi awe hivyo na hali Yeye ni mwenye kujitosha mwenye kusifika.

Na kwa hakika mpumbavu miongoni mwetu alikuwa akisema juu ya Mwenyezi Mungu ya kupituka mipaka.

Makusudio ya mpumbavu hapa ni mjinga asiyejua. Hapa kuna ishara kwamba katika majini kuna kikundi kikiamini utatu: Mungu, mwana na mkewe. Hakuna mwenye shaka kwamba hii ni kupituka mipaka na ni upumbavu.

Nasi tulidhani kuwa watu na majini hawatasema uwongo juu ya Mwenyezi Mungu.

Viongozi wa dini katika majini walikuwa wakiwaambia wafuasi wao ubatilifu na upotevu; miongoni mwayo ni kuwa Mwenyezi Mungu ana mke na watoto. Basi wafuasi wao wenye akili za juu wakawa wanawaamini kwa kuona kuwa hakuna yeyote anayeweza kujasiri kumzulia Mwenyezi Mungu uwongo na kumsifia kwa sifa zisizokuwa zake. Lakini waliposikia Qur’an wakaamini kwamba viongozi wao wanamzulia Mwenyezi Mungu na kumsifu kwa sifa zisizoafikiana naye.

Jambo la kuangalia hapa ni kuwa majini walisikia hikima ya Qur’an kwa mara ya kwanza, wakaielewa na kuwaidhikia nayo. Na sisi tunasikia Qur’an na kuisoma mara kwa mara na hakuna nyumba yoyote ya mwisla­mu isiyokuwa na msahafu, lakini hatunufaiki na mawaidha yake wala kuongoka kwa mwongozo wake. Je, majini wana nafsi safi au wana akili timamu zaidi au ni kuwa katika maisha yao hawana matamanio na vishaw­ishi? [9] 1

Na hakika walikuwako wanaume katika watu walio kuwa wakitafuta kujikinga kwa wanaume katika majini; kwa hivyo wakawazidisha mzigo.

Wametofutiana katika kufasiri Aya hii. Lillo karibu zaidi na ufahamu‧ tofauti na walivyosema wafasiri wengi. ni kuwa makusudio ya wanaume katika watu ni wale wenye akili za juu juu, na wanaume katika majini ni wale watu wanaowavunga wenzao kuwa wana mawaasiliano na majini na wanaweza kuwaita wakati wowote wanapotaka na kuwatumia watakavyo.

Kwa hiyo maana ni kuwa watu wasiokuwa na akili walikuwa wakitaka hifadhi kwa watu waliokuwa wakidai kuwa na mawasiliano na majini ili wajikinge na hatari ya majini, au wawafahamishe yatakayotokea au wawakurubishie yaliyo mbali au kulipeleka mbali lililo karibu. Ama kuwazidishia mzigo ni kuwa wavungaji walikuwa wakiwataka malipo wasiyoyaweza.

Na hakika wao walidhani, kama mlivyodhani nyinyi, kuwa Mwenyezi Mungu hatamtuma Mtume.

Wao ni makafiri katika watu na nyinyi ni nyinyi majini. Maana ni kuwa waumini wa kijini waliwaambia makafiri katika kaumu yao kuwa nyinyi mna wanaofanana nanyi katika watu wasioamini ufufuo na hisabu.

وَأَنَّا لَمَسْنَا السَّمَاءَ فَوَجَدْنَاهَا مُلِئَتْ حَرَسًا شَدِيدًا وَشُهُبًا ﴿٨﴾

8. Nasi tuliigusa mbingu, tukaiona imejaa walinzi wenye nguvu na vimondo.

وَأَنَّا كُنَّا نَقْعُدُ مِنْهَا مَقَاعِدَ لِلسَّمْعِ فَمَن يَسْتَمِعِ الْآنَ يَجِدْ لَهُ شِهَابًا رَّصَدًا ﴿٩﴾

9. Na hakika tulikuwa tukikaa humo katika baadhi ya makao ili kusikiliza, lakini sasa anayetaka kusikiliza atakuta kimondo kinamvizia!

وَأَنَّا لَا نَدْرِي أَشَرٌّ أُرِيدَ بِمَن فِي الْأَرْضِ أَمْ أَرَادَ بِهِمْ رَبُّهُمْ رَشَدًا ﴿١٠﴾

10. Nasi hatujui kama wanataki­wa shari wale wanaokaa kwenye ardhi au Mola wao anawatakia uwongofu.

وَأَنَّا مِنَّا الصَّالِحُونَ وَمِنَّا دُونَ ذَٰلِكَ كُنَّا طَرَائِقَ قِدَدًا ﴿١١﴾

11. Na hakika katika sisi wamo walio wema, na wengine kati­ka sisi ni kinyume na hivyo. Tumekuwa njia mbali mbali.

وَأَنَّا ظَنَنَّا أَن لَّن نُّعْجِزَ اللَّـهَ فِي الْأَرْضِ وَلَن نُّعْجِزَهُ هَرَبًا ﴿١٢﴾

12. Nasi tulijua kuwa hatu­tomshinda Mwenyezi Mungu duniani, wala hatuwezi kumshinda kwa kukimbia.

وَأَنَّا لَمَّا سَمِعْنَا الْهُدَىٰ آمَنَّا بِهِ فَمَن يُؤْمِن بِرَبِّهِ فَلَا يَخَافُ بَخْسًا وَلَا رَهَقًا ﴿١٣﴾

13. Nasi tulipousikia uwongofu tuliuamini. Basi mwenye kumuamini Mola wake hao­gopi kupunjwa wala kudhulu­miwa.

وَأَنَّا مِنَّا الْمُسْلِمُونَ وَمِنَّا الْقَاسِطُونَ فَمَنْ أَسْلَمَ فَأُولَـٰئِكَ تَحَرَّوْا رَشَدًا ﴿١٤﴾

14. Na hakika wamo katika sisi Waislamu, na wamo katika

وَأَمَّا الْقَاسِطُونَ فَكَانُوا لِجَهَنَّمَ حَطَبًا ﴿١٥﴾

15. Na ama walioacha haki, hao wamekuwa kuni za Jahannamu.

وَأَن لَّوِ اسْتَقَامُوا عَلَى الطَّرِيقَةِ لَأَسْقَيْنَاهُم مَّاءً غَدَقًا ﴿١٦﴾

16. Na lau kama wangelisimama sawasawa juu ya njia tungeli­wanywesha maji kwa wingi.

لِّنَفْتِنَهُمْ فِيهِ وَمَن يُعْرِضْ عَن ذِكْرِ رَبِّهِ يَسْلُكْهُ عَذَابًا صَعَدًا ﴿١٧﴾

17. Ili tuwajaribu kwa hayo, na anayepuuza kumkumbuka Mola wake atamsukuma kwenye

adhabu ngumu

TULIZIGUSA MBINGU

Aya 8 – 17

MAANA

Nasi tuliigusa mbingu, tukaiona imejaa walinzi wenye nguvu na vimondo.

Neno kugusa tumelitarjumu kutokana na neno la kiarabu lamd ambalo asili yake ni kugusa kwa mkono, lakini mara nyingi linatumika kwa kutaka; hasa likinyumbuliwa na kuwa iltimas.

Aya hii inarudi madai ya makuhani na wanaodai kuwa na mawasiliano na majini yaliyooelezwa kwenye Aya zilizotangulia hii. Inavunja madai yao kwa kukiri majini wenyewe kuwa hawana uwezo wa kufika mbinguni kusikiliza, kwa sababu ina ulinzi mkali na vimondo.

Ni sawa liwe hili ni uhakika au ni kinaya cha kutojua majini ghaibu, lakini lengo la kwanza ni kutanabaisha kuwa makuhani na wanaodai kuwasiliana na majini wanamzulia Mwenyezi Mungu na majini, kwa sababu ilimu ya ghaibu ni ya Mwenyezi Mungu peke yake:

وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُطْلِعَكُمْ عَلَى الْغَيْبِ ﴿١٧٩﴾

“Na hakuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwafunulia mambo ya ghaibu,” Juz. 4 (3:179)

وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ ﴿٥٩﴾

“Na ziko kwake funguo za ghaibu; hakuna azijuaye ila Yeye.” Juz. 7 (6:59).

Umetangulia mfano wake katika Juz. 14 (15:17-18), Juz. 12 (37: 6-7) na Juzuu hii tuliyo nayo (67:5).

Na hakika tulikuwa tukikaa humo katika baadhi ya makao ili kusik­iliza, lakini sasa anayetaka kusikiliza atakuta kimondo kinamvizia!

Dhahiri ya Aya hii inafahamisha kuwa majini, kabla ya kuja Mtume(s.a.w.w) , waliwahi kupanda sehemu fulani mbinguni, na kwamba walikuwa wakisikia sauti au maneno, kisha wakazuliwa zama za Mtume Muhammad(s.a.w.w) .

Hii haimaanishi kwamba wao walikuwa wakifichua habari za ghaibu mbinguni, hapana! Isipokuwa walisikia kitu tu mbinguni, na si lazima kitu hicho kiwe ni ghaibu; bali haiwezekani kabisa kuwa ni katika aina za ghaibu, kwa sababu ghaibu ni ya Mwenyezi Mungu tu peke yake kwa nukuu ya Qur’an.

Mbinguni ni makazi ya Malaika lakini pamoja na hivyo:

قَالُوا سُبْحَانَكَ لَا عِلْمَ لَنَا إِلَّا مَا عَلَّمْتَنَا إِنَّكَ أَنتَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ ﴿٣٢﴾

“Wakasema: Utakatifu ni wako hatuna elimu isipokuwa ile uliyotufundis­ha.” Juz. 1 (2:32).

Je, yuko aliye mtukufu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu katika mbingu na ardhi kuliko Muhammad(s.a.w.w) , lakini pamoja na hayo alisema:

وَلَوْ كُنتُ أَعْلَمُ الْغَيْبَ لَاسْتَكْثَرْتُ مِنَ الْخَيْرِ وَمَا مَسَّنِيَ السُّوءُ ﴿١٨٨﴾

“Na lau kama ningelijua ghaibu ningejizidishia kheri nyingi, wala isinge­nigusa dhara.”

Juz. 9 (7:188).

Ikiwa mtukufu wa viumbe wa Mwenyezi Mungu hajui ghaibu hata katika mambo yanayomuhusu yeye mwenyewe, vipi majini watajua heri au shari itakayowatokea watu baadae?

Nasi hatujui kama wanatakiwa shari wale wanaokaa kwenye ardhi au Mola wao anawatakia uwongofu.

Hii ni kauli ya majini; maana yake ni kuwa vipi anadhania mpumbavu kwamba sisi tuna ilimu ya ghaibu na kujua heri au shari itakayotokea mbele; na kwamba sisi tunawapa hayo makuhani, na hali sisi hatujui aliyoyakadiria Mwenyezi Mungu kwa yeyote katika watu wa ardhi wala kwa watu wetu?

Na hakika katika sisi wamo walio wema, na wengine katika sisi ni kinyume na hivyo. Tumekuwa njia mbali mbali.

Majini wanajisimulia wao wenyewe kuwa miongoni mwao wamo wema na waovu, na kwamba wao wamegawanyika mataifa na madhehebu mbali mbali, sawa na walivyo watu.

Nasi tulijua kuwa hatutomshinda Mwenyezi Mungu duniani, wala hatuwezi kumshinda kwa kukimbia.

Baada ya majini kuisikia Qur’an waliamini kuwa Mwenyezi Mungu ambaye imetukuka hikima yake, hashindwi na atakayemtaka wala ham­ponyoki atakayemkimbia.

Nasi tulipousikia uwongofu tuliuamini. Basi mwenye kumuamini Mola wake haogopi kupunjwa wala kudhulumiwa.

Makusudio ya mwongozo ni Qur’an. Maana ni kuwa majini waliisikia Qur’an wakaiamini kwa ujumla na kwa ufafanuzi, wakiwa na yakini na uadilifu wa Mwenyezi Mungu, kwamba mwenye kufanya mema akiwa na imani basi hahofii kudhulumiwa wala kupunjwa.

Na hakika wamo katika sisi Waislamu, na wamo katika sisi wanaoacha haki.

Hili ni fungu la pili la majini baada ya uislamu. Ama fungu la kwanza lil­ioelezwa kwenye Aya 11 ya sura hii tuliyo nayo, wema na walio kinyume, hilo ni kwa mtazamo wa kabla ya kusilimu. Hakuna tofauti katika hilo isipokuwa namna ya kuita tu, wema waliitwa hivyo kabla ya uislamu na wakaitwa waislmu baada ya uislamu.

Basi waliosilimu, hao ndio waliotafuta uwongofu.

Waliosilimu waliutafuta uwongofu wakaupata na wakajichagulia heri wakawa wazuri kwayo.

Na ama walioacha haki, hao wamekuwa kuni za Jahannamu.

Sheikh Ismail Haqi, katika tafsiri yake: uhulbayaa anasema: “Alqasie ni yule aliyoiacha haki na uqsie ni yule anayeiendea haki. Jina qasie limetu­mika sana kuitwa kundi la Muawiya, kutokana Hadith ya Mtume alipokuwa akimwambia Ali bin Abi Twalib: Utapigana na nakithin, na qasitia na mariqiia (wavunja ahadi, walioiacha haki na waliochomoka). Kwa hiyo waliovunja ahadi ni watu wa Aisha waliovunja baia, walioiacha haki ni watu wa Muawiya, kwa vile waliiacha haki pale walipopigana na Imam wa haki na waliochomoka ni makhawariji, kwa sababu walitoka kwenye dini ya Mwenyezi Mungu, wakahalalisha kupigana na khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.w.t).

Na lau kama wangelisimama sawasawa juu ya njia tungeliwanywesha maji kwa wingi.

Haya ni maneno mengine wakikusudiwa majini na watu. Makusudio ya njia hapa ni sharia ya haki na uadilifu. Maji mengi ni kinaya cha raha na ukunjufu wa riziki, kwa sababu maji ni asili ya uhai. Maana ni kuwa lau watu wangelimwamini Mwenyezi Mungu kwa ukweli, wakatumia sharia kwa uadilifu na wakajiepusha na dhulma na uadui, basi wangeliishi katika ukunjufu, raha na amani.

Ili tuwajaribu kwa hayo.

Yaani hayo ya raha. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) anawapa neema kisha aangalie, wakizidi imani na ikhlasi kwayo basi watakuwa wema duniani na Akhera na wakiibadilisha basi atakuwa anawangoja.

Na anayepuuza kumkumbuka Mola wake atamsukuma kwenye adhabu ngumu.

Kila anayekumbushwa haki akaidharau, Mwenyezi Mungu atamwadhibu adhabu chungu.