TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE Juzuu 24

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE18%

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE Mwandishi:
: HASANI MWALUPA
Kundi: Qurani tukufu

Juzuu 1 Juzuu 2 Juzuu 3 Juzuu 4 Juzuu 5 Juzuu 6 Juzuu 7 Juzuu 8 Juzuu 12 Juzuu 13 Juzuu 14 Juzuu 15 Juzuu 16 Juzuu 17 Juzuu 18 Juzuu 19 Juzuu 20 Juzuu 21 Juzuu 22 Juzuu 23 Juzuu 24
  • Anza
  • Iliyopita
  • 30 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 28958 / Pakua: 5123
Kiwango Kiwango Kiwango
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE Juzuu 24

Mwandishi:
Swahili

1

2

3

4

5

6

23

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

Sura Ya Sabini Na Nne: Surat Al- Muddathir. Imeshuka Makka Ina Aya 56.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ ﴿١﴾

1. Ewe uliyejigubika!

قُمْ فَأَنذِرْ ﴿٢﴾

2. Simama uonye!

وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ ﴿٣﴾

3. Na Mola wako mfanyie takbira!

وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ ﴿٤﴾

4. Na nguo zako zitwaharishe.

وَالرُّجْزَ فَاهْجُرْ ﴿٥﴾

5. Na mabaya yaambae!

وَلَا تَمْنُن تَسْتَكْثِرُ ﴿٦﴾

6. Wala usitoe kwa kutaka kingi.

وَلِرَبِّكَ فَاصْبِرْ ﴿٧﴾

7. Na kwa ajili ya Mola wako, fanya subira!

فَإِذَا نُقِرَ فِي النَّاقُورِ ﴿٨﴾

8. Basi litapopulizwa barugumu.

فَذَٰلِكَ يَوْمَئِذٍ يَوْمٌ عَسِيرٌ ﴿٩﴾

9. Siku hiyo, basi, itakuwa siku ngumu.

عَلَى الْكَافِرِينَ غَيْرُ يَسِيرٍ ﴿١٠﴾

10. Kwa makafiri haitakuwa nyepesi.

EWE ULIYEJIGUBIKA

Aya 1 - 10

MAANA

Aya hizi zinaashiria wadhifa wa Muhammad(s.a.w.w) kama mjumbe wa haki kwa viumbe. Pia kuna ishara kuwa watu wote mbele ya Mwenyezi Mungu wako sawa; ufafanuzi ni kama ufufatavyo:­

Ewe uliyejigubika!

Huyo ni Mtume mtukufu(s.a.w.w) . Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemwita kwa sifa hii kwa sababu wakati huo alikuwa katika hali hiyo kutokana na sababu fulani; kama tulivyosema mwanzo wa Sura iliyopita.

Simama uonye!

Neno linaweza kuwa na maana moja ya kilugha, lakini maana hayo, mara nyingi, yanatofautiana kulingana na msemaji na anayeambiwa. Mfano neno ‘onya,’ maana yake katika kamusi za lugha lina maana ya kuhofisha na kuhadharisha.

Kwa mfano ukimuona mtu anachimba shimo njiani na kumwambia toa onyo, utakuwa unamaanisha atangaze na kuwaonya wapita njia wasiingie shimoni. Ukimwambia mwana fakihi katika kijiji: ‘onya.’ Utakuwa unamaanisha awafundishe watu wa hapo hukumu za dini na kuwahofisha kuzihalifu.

Ama kauli ya Mtukufu kwa Nabii wake; ‘simama uonye,’ Maana yake ni pambana na waasi wenye nguvu na kiburi kwa neno la haki na uwambie: nyinyi ni wapotevu wafisadi na mtajua kesho hizaya na udhalili utakaowapata, kama hamtarudi kuuacha upotevu wenu. Ukiwambia hivi uvumilie yatakayokupata kutoka kwao na umsabihi Mola wako na kumshukuru.

Tukiona jinsi Muhammad(s.a.w.w) alivyopambana na makuraishi wakiwa na nguvu na kauli na yeye hana chochote zaidi ya ikhlasi na imani, hapo ndio tunabainikiwa na yaliyomsibu kutoka kwao: walimpa sifa ya uchawi, uwongo, ushairi na hata wendawazimu. Walimshakizia watoto wamfanyie masikhara na kumtupia mawe; wakawaambia wanawake waweke miba kwenye njia atakayopita na wasafihi wamwekee uchafu na najisi njiani; hata kuna mmoja wao aliyewahi kumvua kilemba Mtume na kukifunga shingoni mwake. Fauka ya yote hayo makuraishi waliweka azimio la kumwekea vikwazo Mtume na watu wake na kumzuia asiwe na mahusiano na jamii.

Pamoja na yote hayo Nabii(s.a.w.w) alivumilia na kuendelea na mwito wake bila ya kujali hali ngumu waliyompa makuraishi, wakaunda vikosi na majeshi. Akavumilia, akawa imara na subira na kuitikia kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Ewe uliyejigubika! Simama uonye.”

Haya yanatuwekea wazi kuwa wadhifa wa Mtume ni kuonya pamoja na uvumilivu wa tabu na mashaka. Hili ndilo jambo la kwanza. Ama la pili, ni usawa baina ya watu, linalofa­hamika kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

Na Mola wako mfanyie takbira!

Ukimwambia mtu wa kawaida: Mfanyie takbira Mwenyezi Mungu, tutafa­hamu kuwa unataka asema Allahf akbar; kama vile ukisema: mswalie Mtume.

Lakini kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kumwambia Nabii wake: ‘Na Mola wako mfanyie takbira, ina maana kubwa na nzito zaidi, ambayo ni: Ewe Muhammad(s.a.w.w) waambie usoni mwao wale wanoji­fanya majabari wenye kiburi kuwa enzi ni ya Mwenyezi Mungu na Yeye pekee ndiye mkubwa aliye juu, na kwamba nguvu, utukufu na utawala ni wa mmoja aliye pekee asiyekuwa na mshirika kutoka kwenye miungu wenu au nyinyi wenyewe au kutoka kwa wengine; na kwamba watu wote wako sawa katika kumwabudu Mwenyezi Mungu; hakuna tofauti baina ya mweusi na mweupe wala baina ya tajiri na fukara.

Muhammad aliitikia mwito wa Mola na kuwaambia mataghuti mengi tu; miongoni mwayo ni: “Hakika nyinyi na hayo mnayoyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni kuni za Jahannam, mtaifikia.” Juz. 17 (21:98).

Na nguo zako zitwaharishe.

Vile vile hii inafungamana na kulingania na kuonya. Hakuna anayetia shaka kuwa usafi wa mwili na nguo ni katika imani, lakini makusudio hapa ni zaidi ya hivyo; kwamba Mtume(s.a.w.w) atoe mwito wa usafi wa nje, kama vile uchafu, na usafi wa ndani, kama vile udanganyifu na hiyana, ria na unafiki, ujinga na kuhadaika na madhambi mengineyo.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) hayo ameyatolea ibara ya usafi wa nguo, kwa kutumia des­turi ya waarabu; wanaposema: Fulani ni msafi wa mapindo ya nguo yake, wakimaanisha kuwa ni msafi wa moyo na dhati.

Na mabaya yaambae!

Hii inakuwa ni tafsiri na ufafanuzi wa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Na nguo zako zitwaharishe,’ kama ilivyosemekana. Pia imese­mekana makusudio ni ushirikina na kuabudu masanamu.

Wala usitoe kwa kutaka kingi.

Makusudio ya kutaka kingi hapa ni kujiona umefanya mengi. Maana ni kuwa Ewe Muhammad! umewafanyia watu mema mengi na fadhila nyin­gi, lakini usimsimbulie yeyote kwa hilo ukajiona kuwa umefanya mengi, ukasema mimi nimefanya hili ni kawafadhili lile. Kwani kila ulilojitolea ni fadhila yako kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kuna fadhila gani na tukufu zaidi kuliko kuafikiwa kufanya kheri?

Mara nyingi huko nyuma tumeeleza kuwa makatazo yanafaa hata ikiwa anayeambiwa hana azma ya kufanya hilo linalokatazwa, mbali ya kuwa amri za Mwenyezi Mungu na makatazo yake yanawahusu waja wake wote, hata wale wenye takua.

Imesemwa katika Nahjul-balagha: “Kutekeleza haja hakuwezi kuendelea ila kwa mambo matatu: Kwa kuifanya ndogo itakuwa kubwa, kwa kuificha itajitokeza na kwa kuiharakisha itasifika.”

Na kwa ajili ya Mola wako, fanya subira!

Mwenyezi Mungu hakumwamrisha Nabii wake mtukufu jambo lolote la taklifa ya kufikisha na utume ila analikutanisha na subira, kama ilivyose­mekana, kwa sababu ya kujua kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu maudhi atakayopambana nayo kutoka kwa wenye inadi.

Basi litapopulizwa barugumu; siku hiyo, basi, itakuwa siku ngumu; kwa makafiri haitakuwa nyepesi.

Ni kama mfano wa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

فَإِذَا نُفِخَ فِي الصُّورِ ﴿١٠١﴾

“Basi itakapopuziwa parapanda, Juz. 18 (23:101).

Baada ya Mwenyezi Mungu kumwamuru Mtume wake kuwa na uvumilivu kutokana na adha ya wakadhibishaji, sasa anawahadharisha na Siku ya Kiyama ambayo itakuwa ngumu na kali sana kwao; itakuwa nzito isiyofu­atiwa na wepesi. Yametangulia makumi ya Aya kuhusiana na aliyoyaandaa Mwenyezi Mungu kwa wakosefu; yakiwemo chakula, kinywaji na adhabu kali.

ذَرْنِي وَمَنْ خَلَقْتُ وَحِيدًا ﴿١١﴾

11. Niache peke yangu na niliye­ muumba.

وَجَعَلْتُ لَهُ مَالًا مَّمْدُودًا ﴿١٢﴾

12. Na nikamjaalia kuwa na mali mengi.

وَبَنِينَ شُهُودًا ﴿١٣﴾

13. Na wana wanaoonekana.

وَمَهَّدتُّ لَهُ تَمْهِيدًا ﴿١٤﴾

14. Na nikamtengenezea mipan­go.

ثُمَّ يَطْمَعُ أَنْ أَزِيدَ ﴿١٥﴾

15. Kisha anatumai nimzidishie!

كَلَّا إِنَّهُ كَانَ لِآيَاتِنَا عَنِيدًا ﴿١٦﴾

16. Sivyo! Kwani hakika yeye alikuwa akizifanyia inadi Aya zetu!

سَأُرْهِقُهُ صَعُودًا ﴿١٧﴾

17. Nitamtesa kwa mateso ya hali ya juu.

إِنَّهُ فَكَّرَ وَقَدَّرَ ﴿١٨﴾

18. Hakika yeye alifikiri na akapima.

فَقُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ ﴿١٩﴾

19. Basi amelaaniiwa! Vipi alivyopima!

ثُمَّ قُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ ﴿٢٠﴾

20. Tena amelaaniiwa! Vipi alivyo pima!

ثُمَّ نَظَرَ ﴿٢١﴾

21. Kisha akatazama.

ثُمَّ عَبَسَ وَبَسَرَ ﴿٢٢﴾

22. Kisha akakunja uso na aka­nuna.

ثُمَّ أَدْبَرَ وَاسْتَكْبَرَ ﴿٢٣﴾

23. Kisha akageuka, na akatak­abari.

فَقَالَ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ يُؤْثَرُ ﴿٢٤﴾

24. Akasema: Haya si chochote ila ni uchawi ulionukuliwa.

إِنْ هَـٰذَا إِلَّا قَوْلُ الْبَشَرِ ﴿٢٥﴾

25. Haya si chochote ila ni kauli ya binadamu.

سَأُصْلِيهِ سَقَرَ ﴿٢٦﴾

26. Nitamtia kwenye Saqar.

وَمَا أَدْرَاكَ مَا سَقَرُ ﴿٢٧﴾

27. Na nini kitakujulisha ni nini Saqar?

لَا تُبْقِي وَلَا تَذَرُ ﴿٢٨﴾

28. Haubakishi wala hauachi.

لَوَّاحَةٌ لِّلْبَشَرِ ﴿٢٩﴾

29. Unababua ngozi.

عَلَيْهَا تِسْعَةَ عَشَرَ ﴿٣٠﴾

30. Juu yake wapo kumi na tisa.

وَمَا جَعَلْنَا أَصْحَابَ النَّارِ إِلَّا مَلَائِكَةً وَمَا جَعَلْنَا عِدَّتَهُمْ إِلَّا فِتْنَةً لِّلَّذِينَ كَفَرُوا لِيَسْتَيْقِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَيَزْدَادَ الَّذِينَ آمَنُوا إِيمَانًا وَلَا يَرْتَابَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَالْمُؤْمِنُونَ وَلِيَقُولَ الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ وَالْكَافِرُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّـهُ بِهَـٰذَا مَثَلًا كَذَٰلِكَ يُضِلُّ اللَّـهُ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ وَمَا يَعْلَمُ جُنُودَ رَبِّكَ إِلَّا هُوَ وَمَا هِيَ إِلَّا ذِكْرَىٰ لِلْبَشَرِ ﴿٣١﴾

31. Na hatukuwafanya walinzi wa Moto ila Malaika, Wala hatukufanya idadi yao ila kuwa jaribio kwa wale waliokufuru. Ili wawe na yakini waliopewa Kitabu na wazidi imani wale walioamini, wala wasiwe na shaka wale waliopewa Kitabu na waumi­ni, na wapate kusema walio na maradhi katika nyoyo zao na makafiri: Mwenyezi Mungu amekusudia nini kwa mfano huu? Ndio kama hivyo Mwenyezi Mungu humpoteza amtakaye na humwongoza amtakaye. Na hapana ajuae majeshi ya Mola wako ila Yeye. Na huo si chochote ila ni ukumbusho kwa watu.

NIACHE PEKE YANGU NA NILIYEMUUMBA

Aya 11 - 31

KISA KWA UFUPI

Walid bin Al-Mughira Al-Makhzumi, alikuwa ni miongoni mwa vigogo wa kikuraishi, akiwa na mali nyingi na watoto. Siku moja akamsikia Mtume akisoma Aya mojawapo ya Qur’an, akasema: “Hii sio maneno ya binadamu wala jinni. Wallah, hakika kauli yake ‧ yaani Qur’an ‧ ina utamu na ina mvuto na kwamba juu yake kuna matunda na chini yake kumejaa. Hakika iko juu na haishindwi.”

Basi makuraishi waliposikia hivi waka­hofia maneno ya Walid kama yakienea kwa watu, watamwamini Muhammad(s.a.w.w) . Wakamtaka Walid ampinge Mtume. Akasema nisemeje sasa? Niseme ni mwendawazimu, nani ataamini? Au niseme ni kuhani, naye hakuwahi kuwa kuhani kabisa.

Nikisema ni mshairi, yeye hajawahi kutamka shairi na nikisema ni mwongo, hakuna yeyote aliyewahi kusikia uwongo kwake. Kisha akafiria akaona ampe sifa ya uchawi na kwamba yeye ameichukua Qur’an kutoka kwa wachawi.

MAANA

Niache peke yangu na niliyemuumba.

Maneno yanaelekezwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) . Makusudio yake ni kumkemea na kumhadharisha Walid bin Mughira kwa maafikiano ya wafasiri. Maana ni kuwa niachie mimi huyo ewe Muhammad, usijishughulishe naye, wala na yale anayokuzulia. Mimi peke yangu ndiye nitakayempiga vita na kumpa adhabu.

Mwenyezi Mungu alifikia ghadhabu hii kwa Walid, kwa sababu yeye alip­ituka mipaka na uovu; akakufuru neema ya Mwenyezi Mungu na akaipin­ga haki na kuifanyia kiburi haki na watu wake. Kila mwenye kuipinga haki basi ni mlengwa wa ghadhabu hii na makemeo haya; kama vile Walid Bin Mughira, kwa vile sababu ya kushuka Aya haihusiki na aliyeteremshiwa tu, bali inaenea, kama tulivyosema mara nyingi.

Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:Na nikamjaalia kuwa na mali mengi, inaashiria kuwa linasobabisha na kuleta msukumo wa kufanya uovu ni utajiri na wingi wa mali. Aya kadhaa zianaashria hakika hii, ikiwemo Aya 11 ya sura iliyopita na pia kauli yake Mwenyezi Mungu akimsimulia muasi aliyojifaharisha kwa mtu mwema:

أَنَا أَكْثَرُ مِنكَ مَالًا ﴿٣٤﴾

“Mimi nimekushinda kwa mali” Juz. 15 (18:34).

Inatosha kuwa ni ushahidi wa hayo kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

كَلَّا إِنَّ الْإِنسَانَ لَيَطْغَىٰ ﴿٦﴾ أَن رَّآهُ اسْتَغْنَىٰ ﴿٧﴾

“Hakika mtu hupituka mipaka, kwa kujiona amejitosheleza.” (96:6-7).

Kwa kutegemea Aya hizi na nyingine zilizo mfano wake, inawezekana kusema, ijapokuwa ni kwa kubuni, kwamba asili ni kuwa kila tajiri ni muasi, mpaka ithibitike kinyume. Imelezwa kwenye Nahjul-balagha: “Ni uzuri ulioje wa matajiri kuwanyenyekea mafukara kwa kutaka yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu! Na uzuri zaidi kuliko huo ni maringo ya mafukara kwa matajiri kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu.”

Kuna Hadith isemayo: “Heri zote ni za aliyesilimu na ikawa maisha yake ni kutosheka.. ewe Mwenyezi Mungu mruzuku Muhammad na kizazi cha Muhammad kujichunga na kutosheka.”

Na wana wanaoonekana , wakiwa pamoja naye wakishindana kumhudu­mia.Na nikamtengenezea mipango . Nimemsahilishia njia ya jaha na mali akiogelea kwenye neema atakavyo.

Kwa mnasaba huu tunaashiria kwamba neema za dunia hazifahamishi kuridhiwa na Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: “Hakika maisha ya dunia ni mchezo na upuzi tu.” Juz. 26 (47:36). Kwenye Hadith amesema: “ Lau dunia mbele ya Mwenyezi Mungu italinganishwa na kheri kwa ubawa wa mbu, basi kafiri asingekunywa hata tama moja la maji.”

Ilijitokeza dunia kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, mbora wa viumbe wa Mwenyezi Mungu, akaikataa, lakini Walid, muovu wa viumbe wa Mwenyezi Mungu, ilikithiri mali yake,kisha anatumai nimzidishie ! Yaani ana tamaa ya kuzidishiwa mali yake ili azidi uovu na uadui.

Haiwezekani kuchanganyika wema na tamaa katika moyo mmoja. Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) anasema: “Tamaa ni ufunguo wa kila maasi na ni msingi wa kila hatia na ni sababu ya kuanguka mambo mema.”

Sivyo! Kwani hakika yeye alikuwa akizifanyia inadi Aya zetu!

Tokomea mbali ewe mpinzani mwenye hiyana! Hivi una tamaa kwa Mungu na wewe unaifanyia inadi haki na kuizuia kwa kutangaza vita kwa watu wa haki? Wapokezi wanasema kuwa iliposhuka tu Aya hii Walid alibadilika kutoka kwenye enzi na kuwa dhalili, utajiri kuwa fukara, na akafa na hali mbaya.

Amesema kweli aliyoesema: “Hawakusema watu kwa jambo lolote kuwa lina heri ila kuna shari iliyofichwa na nyakati.” Hii ni duniani, ama malipo yake huko Akhera yanaelezwa na Aya hii:

Nitamtesa kwa mateso ya hali ya juu.

Hali ya juu inaweza kuwa ni ukali na mashaka na inaweza kuwa ni zaidi. Mfumo wa maneno unajulisha maana zote mbili na kwamba adhabu siku hiyo itazidi kiwango na kiaina, muda baada ya muda.

Hakika yeye alifikiri na akapima.

alifikiria kuhusu Qur’an na akaandaa kauli ya uzushi kwamba Qur’an ni uchawi ulionukuliwa, kama itakavyokuja mbele.

Basi amelaaniwa! Vipi alivyopima! Tena amelaaniwa! Vipi alivyopima!

Amelaaaniwa kisha akalaaniwa katika kufikiria kwake na kupanga kwake kauli, vitendo na makusudio yake yote. Hakuna kitu kinachofahamisha ufasaha zaidi kuliko kukaririka laana kwa waovu.

Kisha akatazama . Baadaa ya kufikiria aliinua jicho lake kwa vigogo wa kikuraishi,kisha akakunja uso , kwa kukunja nyusi zakena akanuna ; uso ukamuiva.

Kisha akageuka, na akatakabari.

Alihakikisha alipofikiria kuwa Qur’an ni haki isiyokuwa na shaka, lakini pamoja na hayo aliipinga na akaitukukiaakasema: “Haya si chochote ila ni uchawi ulionukuliwa. Haya si chochote ila kauli ya binaadamu ,” aliyoichukua Muhammad kutoka kwa makuhani wa kichawi.

Picha hii ya Walid iliyopigwa na Qur’an, ya kufikiri, kupima, kukunja uso na kununa, inatujulisha kuwa yeye alikuwa hana la kufanya katika kupanga uwongo kwenye jambo analoliamini kuwa ni haki na kweli.

Nitamtia kwenye Moto waSaqar . Atakayetiwa ni huyo huyo Walid. Saqar ni miongoni mwa majina ya Jahannam.Na nini kitakujuulisha ni nini huo Moto waSaqar ? Kwani umefika kikomo cha kutisha; miongoni mwayo ni kwamba huohaubakishi yeyote katika wakosefuwala hauachi aina yoyote ya adhabu ila inawashushia naunababua ngozi .

Makusudio ya kubabua hapa ni kuiva, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

كُلَّمَا نَضِجَتْ جُلُودُهُم بَدَّلْنَاهُمْ جُلُودًا غَيْرَهَا ﴿٥٦﴾

“Kila zitakapoiva ngozi zao, tutawabadilisha ngozi nyingine.” Juz. 5 (4:56).

Juu yake wapo kumi na tisa.

Yaani juu ya hiyo Saqar. Kumi na tisa ni walinzi wa Jahannam. Je, kumi na tisa ni idadi, au aina au ni viongozi? Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi.

Kuna riwaya isemayo kuwa Abu Jahl, aliwaambia makuraishi: ‘’Hamna maana ninyi! Hivi watu kumi katika nyinyi wanashindwa kumshika mmoja katika hao 19?”

Mmoja alieyitwa Abul-Mushid alisema: “Mimi peke yangu nitawatoshea na 17, nyinyi shikeni wawili tu.” Huyu alisema kwa madharau kama alivyosema Abu Jahl.

Na hatukuwafanya walinzi wa Moto ila Malaika.

Walinzi wa moto si katika aina ya binadamu; bali ni malaika wakali wenye nguvu; hakuna anayewazidi nguvu isipokuwa aliye pekee, Mwenye nguvu ambaye ameumba kila kitu.

Kama kwamba muulizaji ameuliza: Nini makusudio ya kutajwa idadi, jambo ambalo linafungua mlango wa madharau kwa wapinzani? Ndio aka­jibu Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwamba kutaja kwake kuna faida tatu:

1.Wala hatukufanya idadi yao ila kuwa jaribio kwa wale waliokufuru.

Ndio! Mwenyezi Mungu anajua kwamba washirikina watakaposikia idadi watacheka na kufanya stihizai, lakini pamoja na hayo ametaja, kwa sababu haki inapaswa itangazwe, hata kama natija yake ni madharau ya wanaod­harau. Kwa maneno mengine ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) anawa­jaribu waja, naye ni mjuzi zaidi kuliko nafsi zao. Anawajaribu kwa raha na dhiki. Vile vile anasema haki ili vijitokeze vitendo vyao vinavyostahiki thawabu na adhabu.

Kutajwa idadi kumedhihirisha hakika ya washirikina ya kudharau ghaibu, hivyo wakastahiki ghadhabu na adhabu ya Mwenyezi Mungu; kama kulivyodhihirisha hakika ya waumini wakastahiki radhi za Mwenyezi Mungu na thawabu zake, kama yatakavyokuja maelezo. Zaidi ya hayo ni kuwa kutangaza Mtume neno la haki bila ya kuangalia yatakayompata kwa ajili yake, ni dalili mkataa kwamba hana jingine analolitaka isipokuwa kui­hakikisha haki na kuibatilisha batili.

2.Ili wawe na yakini waliopewa Kitabu.

Ulama wa kiyahudi na wa kinaswara wakati huo walishuhudia kwa imani na yakini kwamba walinzi idadi yao ni 19, kwa sababu hilo linaafikiana na waliyoyasoma katika Tawrat na Injil.

3.Na wazidi imani wale walioamini.

Wahyi wa mambo ya ghaibu unawazidisha makafiri upinzani na jeuri na waumini wanazidi imani. Imesemekana kuwa waumini huzidi yakini waki­ambiwa na watu wa Kitabu kuwa idadi imo kwenye vitabu vyao. Usawa ni kuwa kila Aya katika Aya zake Mwenyezi Mungu Mtukufu inawazidisha waumini yakini kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake; ni sawa watu wa Kitabu wakubali au wapinge. Ni kweli kwamba kukubali kwao ni hoja kwa wapinzani.

Wala wasiwe na shaka wale waliopewa Kitabu na waumini.

Huu ni ufafanuzi na msisitizo wa yaliyokuwa kabla yake, kwa sababu kutokuweko shaka ni kuwa na yakini na kuzidi imani.

Na wapate kusema walio na maradhi katika nyoyo zao na makafiri: Mwenyezi Mungu amekusudia nini kwa mfano huu?

Vile vile huu ni ufafanuzi na msisitizo wa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Wala hatukufanya idadi yao ila kuwa jaribio kwa wale walioku­furu,” pamoja na kufafanua aina ya makafiri ambao ni wanafiki walio na maradhi katika nyoyo zao. Umetangulia mfano wake katika Juz. 1 (2:26).

Ndio kama hivyo Mwenyezi Mungu humpoteza amtakaye na humwongoza amtakaye.

Mwenye kufuata njia ya upotevu Mwenyezi Mungu humpoteza:

فَلَمَّا زَاغُوا أَزَاغَ اللَّـهُ قُلُوبَهُمْ ﴿٥﴾

“Walipopotoka, Mwenyezi Mungu alizipotoa nyoyo zao.” Juz. 28 (61:5).

فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَهُمُ اللَّـهُ مَرَضًا ﴿١٠﴾

“Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi.” Juz. 1 (2:10).

Na mwenye kufuata njia ya uongofu Mwenyezi Mungu humuongoza: “Na ambao wameongoka anawazidishia uongofu.” Juz. 26: (47:17).

Umetangulia mfano wake katika Juz. 22 (35:8).

Na hapana ajuae majeshi ya Mola wako ila Yeye.

Askari wa Mwenyezi Mungu sio wale 19 tu, viumbe wote wanatii matak­wa hata wanyama, wadudu, ndege, upepo, matetemeko, matufani na men­gineyo ambayo hakuna anayejua isipokuwa mwanzishaji wa viumbe na mrudishaji.

Na huo si chochote ila ni ukumbusho kwa watu.

Huo ni huo moto wa Saqar. aliyoumba Mwenyezi Mungu (s.w.t) na kuwa­hadharisha nao ili wayaogope maasi kwa ndani na nje.

24

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

كَلَّا وَالْقَمَرِ ﴿٣٢﴾

32. Sivyo! Naapa kwa mwezi!

وَاللَّيْلِ إِذْ أَدْبَرَ ﴿٣٣﴾

33. Na kwa usiku unapokucha!

وَالصُّبْحِ إِذَا أَسْفَرَ ﴿٣٤﴾

34. Na kwa asubuhi inapopam­bazuka!

إِنَّهَا لَإِحْدَى الْكُبَرِ ﴿٣٥﴾

35. Hakika huo ni mojawapo ya mambo makubwa!

نَذِيرًا لِّلْبَشَرِ ﴿٣٦﴾

36. Ni onyo kwa watu.

لِمَن شَاءَ مِنكُمْ أَن يَتَقَدَّمَ أَوْ يَتَأَخَّرَ ﴿٣٧﴾

37. Kwa anayetaka miongoni mwenu kwenda mbele au kurudi nyuma.

كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ رَهِينَةٌ ﴿٣٨﴾

38. Kila nafsi iko kwenye rahani kwa iliyoyachuma.

إِلَّا أَصْحَابَ الْيَمِينِ ﴿٣٩﴾

39. Isipokuwa watu wa kuliani.

فِي جَنَّاتٍ يَتَسَاءَلُونَ ﴿٤٠﴾

40. Watakua katika mabustani wakiulizana.

عَنِ الْمُجْرِمِينَ ﴿٤١﴾

41. Kuhusiana na wakosefu.

مَا سَلَكَكُمْ فِي سَقَرَ ﴿٤٢﴾

42. Ni kipi kilichowapeleka Motoni?

قَالُوا لَمْ نَكُ مِنَ الْمُصَلِّينَ ﴿٤٣﴾

43. Watasema: Hatukuwa mion­goni mwa waliokuwa wak­iswali.

وَلَمْ نَكُ نُطْعِمُ الْمِسْكِينَ ﴿٤٤﴾

44. Wala hatukuwa tukiwalisha masikini.

وَكُنَّا نَخُوضُ مَعَ الْخَائِضِينَ ﴿٤٥﴾

45. Na tulikuwa tukijiingiza pamoja na wanaojiingiza.

وَكُنَّا نُكَذِّبُ بِيَوْمِ الدِّينِ ﴿٤٦﴾

46. Na tulikuwa tukikadhibisha siku ya hukumu.

حَتَّىٰ أَتَانَا الْيَقِينُ ﴿٤٧﴾

47. Mpaka ikatujia yakini.

وَكُنَّا نُكَذِّبُ بِيَوْمِ الدِّينِ ﴿٤٦﴾

46. Basi hautawafaa uombezi wa waombezi.

حَتَّىٰ أَتَانَا الْيَقِينُ ﴿٤٧﴾

47. Basi wana nini wanapuuza ukumbusho huu?

فَمَا تَنفَعُهُمْ شَفَاعَةُ الشَّافِعِينَ ﴿٤٨﴾

48. Kama kwamba wao ni punda waliotimuliwa.

فَمَا لَهُمْ عَنِ التَّذْكِرَةِ مُعْرِضِينَ ﴿٤٩﴾

49. Basi wana nini hata wanapuuza onyo hili?

كَأَنَّهُمْ حُمُرٌ مُّسْتَنفِرَةٌ ﴿٥٠﴾

50. Kama kwamba wao ni mapunda walio timuliwa,

فَرَّتْ مِن قَسْوَرَةٍ ﴿٥١﴾

51. Wanaomkimbia simba!

بَلْ يُرِيدُ كُلُّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ أَن يُؤْتَىٰ صُحُفًا مُّنَشَّرَةً ﴿٥٢﴾

52. Bali kila mmoja katika wao anataka apewe nyaraka zilizo­funuliwa.

كَلَّا بَل لَّا يَخَافُونَ الْآخِرَةَ ﴿٥٣﴾

53. Sivyo! Bali hawaiogopi Akhera.

كَلَّا إِنَّهُ تَذْكِرَةٌ ﴿٥٤﴾

54. Sivyo! Kwa hakika hiyo ni ukumbusho.

فَمَن شَاءَ ذَكَرَهُ ﴿٥٥﴾

55. Basi atakaye ataukumbuka.

وَمَا يَذْكُرُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ هُوَ أَهْلُ التَّقْوَىٰ وَأَهْلُ الْمَغْفِرَةِ ﴿٥٦﴾

56. Na hawatakumbuka isipokuwa atake Mwenyezi Mungu.

TUKIJIINGIZA PAMOJA NA WANAOJIINGIZA

Aya 32 – 56

MAANA

Na hawatakumbuka isipokuwa atake Mwenyezi Mungu.

Sivyo! Komeni enyi washirikina kucheza na moto na kuwadharau walinzi wake.

Naapa kwa mwezi na kwa usiku unapokucha na kwa asubuhi inapopambazuka. Hakika huo ni mojawapo ya mambo makubwa.

Baada ya Mwenyezi Mungu kuwakemea wapinzani, sasa anaapa kwa mwezi, usiku na mchana kwamba Moto ni kweli isiyokuwa na shaka na ni adhabu ambayo haina mfano na hakuna adhabu nyingine inayoishinda hiyo. Kuapa kwa maumbile haya ni kuashiria kuwa wenye busara wanap­ata dalili ya mtengenezaji kutokana na ubunifu wa utengenezaji, na kwam­ba mwenye kufanya kitu bila ya chochote, anaweza kuipa uhai mifupa iliyochakaa.

Ni onyo kwa watu, kwa anayetaka miongoni mwenu kwenda mbele au kurudi nyuma.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewahadharisha waja na moto na akawafa­hamisha njia yake na kuwambia jichagulieni wenyewe kuundea au kuwa mbali nao. amejitoa lawamani Mwenye kuonya.

Kila nafsi iko kwenye rahani kwa iliyoyachuma.

Hii ni sababu ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kwa anayetaka kwenda mbele au kurudi nyuma. Maana ni kuwa jichagulieni wenyewe, nyinyi mmefungika kwenye rahani ya mliyoyafanya na mna deni la mliyoyatanguliza; ikiwa ni heri basi mtalipwa heri na ikiwa ni shari basi ni shari. Umetangulia mfano wake katika Juz. 21 (30:44).

Isipokuwa watu wa kuliani.

Qur’an inawaita watu wa upande wa kulia wale wanaomcha Mungu na wakosefu inawaita watu wa upande wa kushoto, Tazama Juz. 27 (56: 8-9, 38-41).

Maana ni kuwa hakuna mtu yeyote ila nafsi yake inakuwa ni mateka wa matendo yake; isipokuwa wenye takua, wao wamelipa madeni yao na wamezifungua nafasi zao kwa matendo yao mema, na malipo yao ni Bustani za milele zinazopitiwa na mito.

Watakua katika mabustani wakiulizana kuhusiana na wakosefu: Ni kipi kilichowapeleka Motoni.

Baada ya kutulia watu wa Peponi wataulizana wenyewe kwa wenyewe: Wako wapi wakosefu waliokuwa wakitupa tabu?

Mwenyezi Mungu (s.w.t) atawaonyesha walipo katika Jahannam, ili wazi­di furaha, kama yalivyoeleza baadhi ya mapokezi.

Atawauliza kwa kuwatahayariza: ni jambo gani lililowapeleka kwenye makazi haya?Watasema kwa lugha ya hali au ya maneno:Hatukuwa miongoni mwa waliokuwa wakiswali . Yaani hatukuacha machafu na maovu duniani. Tafsiri hii tumeichukua katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

إِنَّ الصَّلَاةَ تَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ ﴿٤٥﴾

“Hakika Swala inakataza machafu na maovu.” Juz. 21 (29:45)

Wala hatukuwa tukiwalisha masikini, bali tulilimbikiza mali bila ya kuyatoa katika njia ya Mwenyezi Mungu.Na tulikuwa tukijiingiza pamoja na wanaojiingiza.

Makusudio ya kujiingiza hapa ni kupiga porojo. Maana ni kuwa tukidha­rau kila jambo isipokuwa upuzi na mchezo na tukijiingiza kila mahali isipokuwa kwenye haki na kheri.

Na tulikuwa tukikadhibisha siku ya hukumu, mpaka ikatujia yakini, yaani mauti.

Neno hukumu tumelifasiri kutokana neno Din. Sheikh Abdul-Qadir Al-Maghribi anasema: “Siku ya Kiyama imeitwa hivyo kwa sababu ndani yake mna malipo, hisabu na hukumu. Yote haya ni katika maana ya neno din. Vile vile inaitwa siku ya ufufuo, kuhukumiwa watu, mlipaji na hakimu.

Wamesema Ali bin Abi Twalib ni hakimu wa umma huu baada ya Nabii; yaani baada ya Nabii(s.a.w.w) yeye alikuwa na aina ya pekee ya kuhukumu baina ya mahasimu. ( kwa kutumia neno din kwa maana ya hukumu)”

Basi hautawafaa uombezi wa waombezi

Hakuna muombezi atakayefaa wala udhuru utakaokubalika, isipokuwa toba na matendo mema.

Basi wana nini wanapuuza ukumbusho huu; kama kwamba wao ni punda waliotimuliwa, wanaomkimbia simba.

Wanaambiwa washirikina, makusudio ya ukumbusho ni Qur’an na punda ni wa mwituni. Maana ni kuwa wananini hawa wanakimbia uongofu na haki kama wanaokimbia mauti?

Bali kila mmoja katika wao anataka apewe nyaraka zilizofunuliwa.

Kuna riwaya isemayo kuwa washirikina walimwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu: “Hatutakuamini mpaka umteremshie kila mmoja wetu waraka usemao fulani bin fulani mfuate Muhammad(s.a.w.w) .”

Iwe sawa riwaya hii au la, lakini inafasiri dhahiri ya Aya. Hilo linatiliwa nguvu na Aya isemayo:

وَلَن نُّؤْمِنَ لِرُقِيِّكَ حَتَّىٰ تُنَزِّلَ عَلَيْنَا كِتَابًا نَّقْرَؤُهُ ﴿٩٣﴾

“Na hatutaamini kupaa kwako mpaka ututeremshie Kitabu tukisome.” Juz. 15 (17:93).

Lakini wao hawawezi kuamini hata kama wangeliitikiwa matakwa yao, kama ilivyoliweka wazi hilo kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

وَلَوْ نَزَّلْنَا عَلَيْكَ كِتَابًا فِي قِرْطَاسٍ فَلَمَسُوهُ بِأَيْدِيهِمْ لَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿٧﴾

“Na lau tungelikuteremshia maandishi katika karatasi na wakayagusa kwa mikono yao, bila shaka wale waliokufuru wangelisema: Haya si chochote ila ni uchawi dhahiri.” Juz. 7 (6:7).

Siri katika hilo ni kupupia kwao masilahi yao na mambo yao na wala sio hasadi, kama walivyosema baadhi ya wafasiri. Dalili ya hayo tuliyoyasema ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu iliyokuja moja kwa moja:Sivyo! Bali hawaiogopi Akhera . kwa sababu wao hawajui isipokuwa maisha ya dunia wala hawategemei isipokuwa anasa zake na starehe. Ama ubinadamu, haki na heri kwao ni maneno yasiyokuwa na maana.

Sivyo! Kwa hakika hiyo ni ukumbusho.

Mara nyingine tena Mwenyezi Mungu (s.w.t) anawakemea wakadhibisha­ji na kuwabainishia kuwa hii Qur’an ni mawaidha kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwenda kwa waja wake na wala sio kauli ya mchawi wala mshairi.

Basi atakaye ataukumbuka.

Yaani atanufaika na hukumu zake na mawaidha yake.

Na hawatakumbuka isipokuwa atake Mwenyezi Mungu.

Unaweza kuuliza : Kauli yake Mwenyezi Mungu: ‘atakaye ataukumbuka,’ inaonyesha kuwa mtu ana hiyari ya uhuru wake na utashi wake. Na kauli hii ‘Hawatakumbuka isipokuwa atake Mwenyezi Mungu,’ inaonyesha kuwa mtu hana hiyari, anaendeshwa na hana uhuru wala utashi; sasa ni vipi mgongano huu?

Jibu : Makusudio ya matakwa ya kwanza, ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemwachia mtu hiyari ya kujichagulia imani au ukafiri. Na makusudio ya ya matakwa ya pili ni kuwa mpinzani anayekana hawezi kuamini mpaka Mwenyezi Mungu amlazimishe kwa nguvu. Kwa hiyo maana ya kauli mbili ni kuwa Mwenyezi Mungu amemwamchia mtu hiyari ya kuamini au kukufuru; kama isemwavyo kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

وَقُلِ الْحَقُّ مِن رَّبِّكُمْ فَمَن شَاءَ فَلْيُؤْمِن وَمَن شَاءَ فَلْيَكْفُرْ ﴿٢٩﴾

“Sema hii ni kweli itokayo kwa Mola wenu, basi atakaye aamini na atakaye akufuru.”

Juz. 15 (18:29).

Lakini mpinzani mwenye inadi hawezi, kwa hali yoyote ile, ila akifany­ishwa kwa nguvu na Mwenyezi Mungu; na hili haliwezi kuwa kabisa, kwa vile linapingana na uadilifu wa Mwenyezi Mungu na hikima yake. Kwa sababu uadilifu wake Mwenyezi Mungu Mtukufu na desturi yake kwa waja wake, ni kuwabainishia njia ya heri na kuwahimiza na kuwabinishia njia ya shari na kuwahadharisha nayo.

Kwa hiyo kila mmoja anakuwa na hiyari yeye mwenyewe ya mwishilio wake; vinginevyo thawabu na adhabu zitakua hazina maana yoyote.

Hili linaungwa mkono na kauli yake Mwenyezi Mungu iliyokuja moja kwa moja:

Takua ni kwake na maghufira ni yake.

Yaani yeye Mwenyezi Mungu ambaye imetukuka hikima yake, ndiye anayestahiki kutiiwa katika maamrisho yake na makatazo yake, na kuogopewa kwa ghadhabu yake na adhabu yake. Vile vile yeye ndiye mwenye kuwahurumia waja na kuwasamehe wanao­tubia na kurejea.

Kwa mnaeno machache na ya uwazi zaidi ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemuumba mtu akiwa na hiyari, mwenye akili na utashi, akamto­fautisha na mnyama kwa hilo; kwa hiyo akamkalifisha utiifu na msimamo. Kama angelitaka Mwenyezi Mungu angelimuondolea utashi wa akili na kumfanya kama mnyama au chini yake zaidi.

MWISHO WA SURA YA SABINI NA NNE: SURAT AL- MUDDATHIR

2

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU

I- UISLAMU NA MAISHA YA KISASA

Suala la dini na maisha ya kisasa ni moja ya mambo ambayo hayawagusi Waislamu peke yao. Dini nyingine pia zilikumbana na tatizo hili. Watu wengi wenye kupendelea mabadiliko duniani, wameikana dini kwa sababu wanaamini kuwa dini na maisha ya sasa haviendi pamoja. Wanafikiri kuwa kudumaa, kutuama na kutobadilika ni sifa za lazima za mtu mshika dini. Kwa maneno mengine, wanafikiri kuwa kudumaa na ukinaifu unatokana na kutokuwepo kwa mabadiliko na kwamba kudumisha hali ya kizamani ndio tabia za dini.

Marehemu Bwana Nehru aliyekuwa waziri Mkuu wa India alikuwa na mawazo ya kisekula na hakuwa akiamini dini yoyote. Inaoinekana kutokana na kauli zake kuwa kilichomfanya asipende dini ni kutobadilika kwake na ukinaifu unaotokana na kutokuwepo kwa mabadiliko. Kuelekea kipindi cha mwisho cha maisha yake Nehru alihisi kuwa na uwazi moyoni mwake na aliamini kuwa uwazi ule ungezibwa na nguvu ya kiroho tu.

Lakini hakuelekea kuiamini dini yoyote kwa sababu aliamini kuwa hali ya ukinaifu na kutokuwepo kwa mabadiliko ilikuwepo katika dini zote. Mwandishi wa habari wa Kihindi, aitwaye Karanjia, alimhoji Nehru katika kipindi chake cha mwisho mwisho cha uhai wake (Nehru) na alivyoonekana haya yalikuwa ni mahojiano ya mwisho ambapo Nehru alitoa maoni yake juu ya matatizo ya jumla ya ulimwengu.

Alipokuwa akimzungumzia Gandhi, Karanjia alisema, "Baadhi ya wanaopendelea mabadiliko (liberals) na maendeleo wanaamini kuwa Gandhiji, kwa kupitia na kwa kutokana na utatuzi wake wa matatizo kwa hisia kali, unyofu na njia za kiroho, zimedhoofisha na kuitia ubaridi imani yako ya asili ya ujamaa wa kisayansi." Katika kulijibu hili, Nehru alisema; "Ni muhimu na vizuri kutumia fursa ya njia za kimaadili na kiroho.

Mara zote nimekubaliana na Gandhiji juu ya hili. Ninaamini kuwa ni muhimu zaidi kutumia fursa ya njia hizi, kwani sasa, kwa kiasi kikubwa kuliko ilivyokuwa huko nyuma, tunahitaji majibu ya kiroho na kimaadili juu ya maswali yanayotokana na pengo la kimaadili linalosababishwa na tamaduni za kisasa, ambazo zinazidi kuwa maarufu." Kisha Kiranjia aliuliza swali juu ya Ukomunisti.

Nehru alikiri mapungufu yake na katika majibu yake alionyesha baadhi ya mapungufu na ubovu wake (wa ukomunisti). Kwa mara nyingine tena alipendekeza suluhisho la kiroho juu ya matatizo ya dunia. Alipofika hapa Karanjia akasema; "Bwana Nehru, je dhana yako ya utatuzi wa matatizo ya kimaadili na kiroho haikufanyi uwe tofauti na Jawahanal wa jana? (Nehru mwenyewe enzi za ujana wake).

Ulichokisema kinaonyesha kuwa Bwana Nehru, katika kuelekea mwisho wa uhai wake, ameanza kumtafuta Mungu." Nehru alisema; "Ndiyo, nimebadilika. Msisitizo wangu juu ya unyofu na maadili ya kiroho na utatuzi wa matatizo sio wa bahati mbaya." Akaongeza kuwa; "Swali sasa ni jinsi ya kukuza maadili na imani ya kiroho katika daraja la juu zaidi.

Hapana shaka kwamba kwa ajili ya hili, dini zipo, lakini kwa bahati mbaya zimechukua mtazamo finyu na matendo yasiyobadilika na zimebaki kuwa taratibu rasmi lakini duni. Ni umbo lake la nje tu lililobaki, lakini ari na dhana yake ya kweli imetoweka." Uislamu na mahitaji ya wakati. Katika dini zote ni Uislamu tu unaojihusisha zaidi na vipengele vyote vya maisha ya mwanadamu.

Mafundisho yake hayajajikita katika matendo ya ibada na sala na mfumo wa ushauri wa maadili peke yake. Uislamu, kama ulivyoshughulikia uhusiano wa watu na Mwenyezi Mungu, ndivyo hivyohivyo ulivyoshughulikia mahusiano baina ya watu. Katika sura mbali mbali Uislamu umeshughulikia haki za watu binafsi na majukumu yao pia.

Hii ndio sababu swali kwamba mafundisho yake yanafaa kutumika au la katika mazingira yanayozidi kubadilika ni thabiti zaidi katika suala la Uislamu kuliko dini nyingine yoyote. Kwa bahati imetokea kwamba, wasomi wengi na waandishi wasiokuwa Waislamu wamezisoma sheria za kijamii na kiraia (za madai na za jinai) na wamezisifu kuwa ni chombo cha kisheria cha kimaendeleo na endelevu.

Wameusifu Uislamu kwa mapana na marefu, kuwa ni dini hai na itakayodumu milele, na wameuelezea uwezo na sifa za sheria hizi za Kiislamu wa kuweza kutumika nyakati zote na katika hali zote. Mwandishi maarufu sana wa Kiingereza aliyekuwa akipendelea msimamo wa wastani (liberal), Bernard Shaw amesema; "Mara zote nimekuwa nikiipa dini ya Muhammad heshima kubwa (daraja kubwa), kutokana na uhai wake wa ajabu.

Ni dini pekee inayoonekana kwangu kuwa na uwezo wa kunyumbulika na hivyo kuweza kutumika katika dunia inayobadilika na katika zama zote. Nimetabiri kuwa imani ya Muhammad itakubaliwa na Ulaya ya kesho, na dalili za hili zinajionyesha hata sasa. Makasisi wa zama za kati aidha kwa sababu ya ujinga au kwa sababu ya kung'ang'ania bila hoja imani zao waliupaka Uislamu rangi mbaya kabisa. Kwa kusema kweli walifundishwa kumchukia mtu huyu, Muhammad na dini yake. Kwao Muhammad alikuwa mpinga Kristo.

Mimi nimemsoma, mtu huyu wa ajabu, na kwa maoni yangu hakuwa mpinga Kristo kabisa na lazima aitwe mkombozi wa wanaadamu. Ninaamini kuwa kama mtu kama yeye angetwaa madaraka /uongozi wa dunia ya sasa angefanikiwa kutatua matatizo katika namna ambayo ingeleta amani na furaha, vitu ambavyo vinahitajika sana kwa sasa. Dr. Shibli Shama'il ni myakinifu wa Kiarabu wa Lebanoni. Kwa mara ya kwanza alitafsiri kitabu cha 'Darwin Kiitwacho 'Origin of Species' kwenda katika lugha ya Kiarabu, pamoja na sharhe ya mwanasayansi wa kijerumani aitwaye Boucher katika kitabu hicho akakipa jina la 'A weapon against religious belief.' ('Silaha dhidi ya imani za kidini.') Ingawa hamwamini Mwenyezi Mungu, haoni aibu kuusifu Uislamu na muasisi wake mtukuka. Ameusifu Uislamu kwa kusema kuwa ni dini hai inayoweza kutumika katika zama zote.

Mtu huyu, katika juzuu ya pili ya kitabu chake kiitwacho, 'Philosophy of Evolution' ambacho amekichapisha kwa Kiarabu, ameandika makala yenye kichwa cha cha habari 'Uislamu na Ustaarabu'. Ameandika makala hii kukanusha madai ya wasio Waislamu kwa kutoa madai kuwa Uislamu ndio uliosababisha kuporomoka kwa hali ya Waislamu. Shibli Shama'il amejaribu kuthibitisha kuwa jambo hasa lililosababisha kuporomoka kwa hali za Waislamu ni wao Waislamu kuyaacha (kuacha kutekeleza) mafundisho ya kijamii ya Uislamu.

Wale wazungu wanaoushambulia Uislamu aidha hawajui au wanafanya hivyo kwa nia mbaya ya kuwafanya watu wa Mashariki (Asia) wazitilie shaka sheria zao na mfumo wao ili kuwafanya wafuate mfumo wa Kimagharibi. Wakati wa zama zetu, suala la iwapo Uislamu unaafikiana na hali halisi ya maisha ya sasa au la limekuwa likiulizwa sana. Tunapata picha ya ndani ya watu hasa wale wanaotoka katika tabaka la wasomi na tunakuta kuwa swali hili linaulizwa zaidi kuliko maswali mengine.

PINGAMIZI

Wakati fulani watu hawa wanatoa hoja za kifalsafa juu ya suala hili kuwa vitu vyote hapa duniani lazima vibadilike. Hakuna kinachobaki vile vile bila kubadilika, na halikadhalika binadamu wanabadilika. Sasa inawezekanaje sheria za Kiislamu zibaki hivyo bila kubadilika kwa zama nenda rudi? Kama tukilitazama swala hili kwa mtazamo wa kifalsafa kabisa, jibu ni rahisi.

Ni vitu (maada) vinavyobadilika kila mara, ambavyo hukua na kuporomoka na ambavyo hupasika katika kugeuka na kuoza. Lakini sheria za ulimwengu hazibadiliki. Kwa mfano, viumbe vyote hai vimegeuka na vimeendelea kugeuka kwa mujibu wa utaratibu na kanuni fulani zilizoelezwa na wanasayansi. Hapana shaka kwamba viumbe hivi vinageuka na kubadilika lakini kanuni zinazotawala mabadiliko haya hazibadiliki. Na sasa tunazungumzia kanuni (sheria) hizi.

Katika hili, hakuna tofauti yoyote iwapo sheria hizi ni za asili au zimetungwa na kukusanywa, kwani inawezekana kwamba sheria ambazo zimetungwa zinaweza kuwa na asili kama chanzo chao na kuafikiana na mchakato wa mabadiliko ya mtu mmoja mmoja na halikadhalika jamii ya wanadamu kwa ujumla.

Hata hivyo, swali kuhusiana na kuafikina au kutoafikiana kwa Uislamu na mahitaji ya muda halina sura ya kiujumla na kifalsafa peke yake. Swali ambalo huulizwa zaidi ni kuwa kwa vile sheria huundwa kukidhi mahitaji ya wanaadamu na mahitaji yenyewe yanabadilika kila mara inawezekanaje sheria hizo za kijamii zibaki hivyo hivyo bila kubadilika? Ni swali zuri.

Na imetokea kuwa tabia za kimiujiza za Uislamu zimewezesha sheria zisizohitaji kubadilishwa kukidhi mahitaji yasiyobadilika ya mtu mmoja na jamii na sheria zinazobadilika badilika kwa mahitaji ya muda mfupi na yanayobadilika. Hii ni sifa ya kipekee ambayo Waislamu wote wajuzi wa mambo ya sheria za kiislamu na waliozisoma sheria zake wanajivunia. Tutalielezea hili vizuri zaidi baadaye. Je mabadiliko ya kijamii yanakwenda na wakati? Kabla ya kuliendea swali hili tungependa kuibua nukta mbili. Nukta ya kwanza ni kuwa watu wengi wanaoongelea maendeleo na mabadiliko ya hali wanadhani kuwa mabadiliko yoyote ya kijamii, hasa kama yametokea nchi za Kimagharibi, basi ni matokeo ya maendeleo.

Hili ni moja ya mawazo potofu liliyoendekezwa na kizazi hiki. Watu wanadhani kuwa kwa vile njia za maisha hubadilika siku hadi siku, zilizo duni hubadilishwa kwa zilizo bora zaidi na sayansi na viwanda vinaboreka kila siku, mabadiliko yote katika maisha ya binadamu ni aina ya maendeleo na kwa hiyo yanafaa kukaribishwa na kupokelewa kwa mikono miwili. Wanafikiri pia kuwa mabadiliko haya hayaepukiki na huja baada ya muda fulani.

Kwa kusema kweli sio kwamba mabadiliko yote ni matokeo ya maendeleo ya sayansi na viwanda wala sio kwamba hayaepukiki. Huku sayansi ikiendelea kukua, asili ya ubinafsi na unyama wa mwanadamu nayo hubaki bila kubadilika. Ujuzi (elimu) na busara humpeleka mtu katika ukamilifu na asili ya unyama wa mwanadamu humsukumia kwenye ufisadi na upotofu.

Asili ya unyama wa mwanadamu mara zote hujaribu kutumia ujuzi kama njia ya kupatia matamanio yake. Kwa kadiri muda unavyokwenda, kwa kadiri maendeleo na mabadiliko yanavyotokea, ufisadi na upotofu ndivyo unavyozidi kukua na kukomaa. Tunapaswa kwenda na wakati lakini wakati huo huo lazima tupige vita ufisadi pia. Mleta mabadiliko (mema) na mpinga mabadiliko (mema) wote wanapigana dhidi ya muda, tofauti yake ni kuwa mleta mabadiliko mema hupigana dhidi ya upotofu unaoletwa na mabadiliko ya muda na mpinga maendeleo (mabadiliko) hupigana dhidi ya mabadiliko (maendeleo halisi) yanayoletwa na mabadiliko ya muda.

Kama tunauchukulia muda na mabadiliiko yake kama kigezo cha mema yoyote na maovu yote, sasa ni kigezo gani cha kuupimia muda wenyewe? Kama kila kitu kitakwenda na wakati sasa je wakati wenyewe unapaswa kwenda na nini? Kama mwanadamu ataufuata muda na mabadiliko yake kwa utii mkubwa, sasa nini kitafanyika juu ya majukumu na nafasi ya utashi wa mwanadamu? Mwanadamu anaendesha gari la wakati, ambalo liko kwenye mwendo.

Lazima awe mwangalifu na aliongoze vyema gari lake. Vinginevyo atakuwa kama mtu aliyepanda farasi na akamwachia farasi wake aende popote atakapo. marekebisho au kuondoa kabisa? Nukta ya pili inayofaa kutajwa hapa ni kwamba baadhi ya watu wamelitatua tatizo gumu la Uislamu na mahitaji ya wakati kwa namna rahisi sana.

Wanasema kuwa Uislamu ni dini ya milele, na inaweza kurekebishwa ili kuafikiana na mahitaji ya kila zama na wakati. Lakini wanapoulizwa marekebisho haya yanafanyikaje na kanuni yake ni nini, mara moja wanasema kuwa hali ya maisha inapobadilika, sheria zilizopo hubatilishwa na kuwekwa nyingine. Wanatoa hoja kuwa sheria za msimu (muda mfupi) za kidini lazima ziwe na uwezo wa kurekebishwa na ziafikiane na maendeleo ya elimu na sayansi pamoja na kupanuka kwa utamaduni na ustaarabu. Kwa mujibu wao, uwezo huo wa sheria wa kuweza kurekebishwa ili kuafikiana na mahitaji ya wakati haupingani na Uislamu na sio kinyume na mafundisho yake.

Wanadai kuwa, kwa vile mahitaji ya wakati yanabadilika kila mara, basi kila zama huhitaji sheria mpya. Wanaendelea kudai kuwa sheria za kiraia na kijamii za Uislamu zinaafikiana na maisha rahisi ya Waarabu waliokuwa wakiishi kabla ya Uislamu, na ambazo kwa kiasi kikubwa zilikuwa ni kwa mujibu wa mila na desturi zao.

Sasa kwa kuwa haziafikiani na maisha ya zama hizi zinatakiwa ziondolewe na ziwekwe nyingine mpya za kisasa. Watu hawa wanapaswa kuulizwa: Kama uwezo wa sheria kuweza kurekebishwa maana yake ni uwezo wa kubatilishwa na kufutwa, basi ni sheria gani ambayo haina sifa hii? Kuna sheria basi yeyote ambayo haiendi na wakati kwa mtazamo huu?

Tafsiri hii ya uwezo wa sheria kurekebishwa na kuweza kutumika katika zama zote ni sawa na kusema kuwa vitabu vyote na maktaba ndio njia bora kabisa za kufurahia maisha kwa sababu muda wowote mtu atakapotaka starehe, anaweza kuviuza na kutumia fedha zitakazopatikana kwa ajili ya kukidhi matamanio yake. Mwandishi wa Kiirani anasema kuwa mafundisho ya Uislamu yamegawanyika katika sehemu tatu.

Sehemu ya kwanza ina imani za msingi kama vile tauhidi (imani kuwa Mungu ni mmoja tu), Utume, Ufufuo n.k. Sehemu ya pili inahusiana na matendo ya ibada kama vile sala, saumu, udhu, tohara, hija n.k sehemu ya tatu ina sheria zinazohusiana na maisha ya watu. Kwa mujibu wake yeye ni sehemu mbili tu za mwanzo ambazo ni za lazima katika dini na ambazo zinafaa kuhifadhiwa milele.

Lakini sehemu ya tatu sio sehemu ya lazima ya dini kwa kuwa dini haihusiani na maisha ya kila siku ya watu. Mtukufu Mtume mwenyewe hakuamuru kuwa sheria hizi ziwe sehemu ya dini kwa vile hazikuhusiana na ujumbe wake yeye kama Mtume. Ilitokea tu kwamba akawa ni mkuu wa Dola, kwa hiyo akalazimika kuweka sheria pia. Vinginevyo dini haina lolote la kulazimisha katika maisha ya kidunia ya watu. Ni vigumu kuamini kuwa mtu anayeishi katika nchi ya Kiislamu anaweza kuwa mjinga wa mafundisho ya Uislamu kiasi hiki. Je, Qur'ani haijaelezea lengo la kuleta Mitume na Manabii? Je, Qur'ani haisemi wazi wazi kuwa:'Tumewaletea Mitume wetu na dalili za wazi na tumewaleta pamoja nao kitabu na vipimo, ili watu wahukumiane kwa haki. (Suratul Hadidi; 57:25). 35 Qur'ani imeuelezea uadilifu katika jamii kama lengo kuu la Mitume wote.

Kama unataka unaweza usiyafuate mafundisho ya Qur'ani, lakini kwa nini unatenda dhambi kubwa zaidi kwa kuusingizia na kuuzushia Uislamu na Qur'ani? Bahati yetu mbaya zaidi inatokana na ukweli kwamba maadili yetu na sheria vimepoteza chanzo pekee cha nguvu yake, yaani dini. Ni katika nusu karne tu tulipoanza kusikia watu wakipiga kelele kuwa Uislamu ni mzuri, ili muradi tu ubakie ndani ya majumba ya ibada, na usishughulike na jamii.

Kelele hii imepigwa kutoka ndani ya mipaka ya nchi za Waislamu na imeenezwa katika ulimwengu wote wa Kiislamu. Ili kuliweka lengo la kelele hizi wazi tunaweza kusema kuwa nia ni kuufanya Uislamu ubaki kuwa ni kikwazo cha kuzuia kuenea kwa ukomunisti lakini kama huu huu Uislamu utagongana na maslahi ya Magharibi basi upingwe vikali.

Kwa mtazamo wa watu wa Magharibi, matendo ya Uislamu lazima yaendelee, ili pindi ikitokea haja, Waislamu wahamasishwe kuupinga mfumo wa kikomunisti ambao hauamini mambo ya dini na Mungu, lakini sheria za kijamii za Uislamu ambazo zinatoa falsafa ya maisha ya Uislamu lazima ziondoshwe, kwa vile sheria hizi huwapa Waislamu uhuru fulani na kuwafanya wawe watu tofauti wanaojitegemea katika mfumo wao, jambo ambalo litawazuia kumezwa na nchi za Magharibi zenye tamaa kali. Kwa bahati mbaya, watetezi wa hoja kuwa Uislamu haujihusishi na maisha ya kila siku ya watu, wamesahau baadhi ya ukweli wa msingi. Awali miaka 1400 iliyopita, Uislamu ulipinga kanuni kuwa tunaamini baadhi ya mambo (baadhi ya mafundisho ya Uislamu) na tunayakataa mengine, na ukatamka kuwa kanuni na sheria za Uislamu hazibadiliki.

Pili tunaamini kuwa muda umefika ambapo Waislamu hawapaswi kupotoshwa na mbiu za uongo. Watu sasa pole pole wameanza kuamka na wameanza kutofautisha kati ya maendeleo ambayo ni matokeo ya kuchanua kwa vipaji vya kisayansi na kiakili, na kudhihiri kwa ufisadi na upotofu, kutoka nchi za Magharibi. Watu wa ulimwengu wa Kiislamu hivi sasa, kuliko kipindi kingine chochote, wameanza kufahamu thamani ya mafundisho ya Uislamu na wametambua kuwa wanaweza tu kuishi maisha huru kwa kuyafuata. Hawatayaacha, kwa gharama yoyote.

Waislamu makini wanafahamu kuwa propaganda dhidi ya sheria za kiislamu si chochote bali udanganyifu wa mabepari. Tatu, watetezi wa hoja hii wanapaswa kujua kuwa Uislamu unapokuwa na nguvu, hushinda mifumo mingine yote, iwe ya kikafiri au vinginevyo. Uislamu unataka kutawala maisha ya jamii kama falsafa ya maisha, na hautaki kubakia misikitini tu na sehemu nyingine za ibada. Uislamu ambao utabakia kwenye nyumba za ibada, utaacha nafasi kwa ajili ya mawazo ya Kimagharibi na halikadhalika mawazo yanayopingana na umagharibi na itikadi zake. Adhabu ambazo nchi za magharini zinatumikia, katika baadhi ya nchi za Waislamu ni matokeo ya kutoujua ukweli huu.

3

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU

- II UISLAMU NA MAISHA YA KISASA

Mwanadamu sio kiumbe pekee anayeishi maisha ya kijamii. Wanyama wengi, na hususan wadudu hupenda kuishi pamoja na kushirikiana. Wanafuata kanuni za mgawanyo wa kazi, uzalishaji na ugavi na kutoa na kupokea amri. Nyuki, na baadhi ya wadudu jamii ya mchwa wana mfumo huu bora wa maisha, mfumo ambao utamchukua mwanadamu, anayejiona kuwa ni mfalme wa viumbe vyote, miaka au hata karne ili kufikia kiwango hicho cha ufanisi.

Ustaarabu wao (wadudu hawa) haujapitia vipindi kama vile zama za mwituni, zama za mawe na zama za nyuklia. Toka mwanzo wamekuwa na ustaarabu na mfumo wa namna moja kama tu walivyo leo. Ni mwanadamu aliyeanzia sifuri. Tazama : "Mwanadamu aliumbwa dhaifu ."Suratul Nisaa 4:28 Kwa upande wa wanyama, mahitaji yao ya maisha hayabadiliki. Kwao usasa na fasheni mpya havina maana. Ulimwengu wa kale na ulimwengu wa sasa kwao hauna tofauti yoyote.

Kwao sayansi haifanyi ugunduzi wowote ule. Bidhaa mpya kabisa nyepesi na nzito za viwanda hazikuingia katika soko lao; kwa nini? Kwa sababu wanaishi kwa silika na sio kwa akili (mantiki). Maisha ya kijamii ya mwanadamu mara zote yanabadilika. Kila karne ulimwengu unabadilika. Hapo ndio kuna siri ya mwanadamu kuwa mfalme wa viumbe vyote.

Mwanadamu ni mtoto wa maumbile aliyekomaa na kustahili heshima. Amefikia hatua ambayo hahitaji muongozo wa moja kwa moja wa ile nguvu ya ajabu iitwayo silika. Maumbile yanafahamu kuwa mwanadamu ni kiumbe aliyekomaa, na ndio maana yamemuacha huru. Yale ambayo wanyama wanayatekeleza kwa silika na kwa kufuata kanuni za maumbile ambazo hawawezi kuzivunja/kukiuka, wanaadamu wanatakiwa kuyatekeleza kwa kutumia akili na elimu na kwa kufuata sheria zilizopitishwa na zinazoonekana. Mwanadamu akiwa ni mwamuzi wa mwisho wa majaaliwa yake mara zote anaweza kupotoka na kuiacha njia ya maendeleo, na hapa ndio kuna siri ya kuteleza kwake, vipingamizi vyake (anavyokumbana navyo) kupotoka na kushindwa kwake.

Kama tu ilivyo kuwa maendeleo yapo wazi kwake, halikadhalika njia ya kuelekea upotofu, ufisadi na kushindwa haijafungwa. Wanaadamu wamefikia hatua ambayo kwa mujibu wa maneno ya Qur'ani wanaweza kubeba dhamana ambayo mbingu, ardhi na milima haviwezi kubeba; kwa maneno mengine, wanaweza kuishi maisha huru na wanaweza kuchukua majukumu ya kisheria, kitaalamu na mengineyo. Hii ndio sababu hawana kinga ya makosa, ubinafsi, ujinga na dhulma. Pale Qur'ani inapouelezea uwezo huu wa ajabu wa binadamu, mara moja unamtaja kuwa ni 'dhalimu na mjinga'.

Uwezo na sifa hizi mbili za mwanadamu, uwezo wa kuboreka (kuwa bora zaidi) na uwezo wa kupotoka havitenganishiki. Mwanadamu sio kama mnyama ambaye katika maisha yake ya kijamii, huwa haendi mbele wala nyuma, hageukii kulia wala kushoto. Lakini mwanadamu kwa upande wake, katika maisha yake wakati fulani huenda mbele na wakati fulani nyuma. Katika maisha ya wanadamu kama kuna mwendo na kasi, basi kuna kusimama na kupumzika pia. Kama kuna maendeleo na kubadilika kwenda katika hali bora zaidi basi kuna ufisadi na upotofu pia. Kama kuna haki na wema, basi kuna udhalimu na ushari pia.

Kama elimu na busara vimedhihiri basi ujinga na matamanio duni yamedhihiri pia. Inawezekana kwamba mabadiliko yanayotokea na hali mpya zinazoonekana vikawa ni vya kundi la pili (la mabaya). Wasiotaka kubadilishwa na waliopotoshwa. Ni moja ya tabia za mwanadamu kwamba wakati fulani hufanya jambo kupita kiasi na wakati fulani hufanya jambo kwa kiasi kidogo zaidi kuliko inavyohitajika. Kama akichagua kundi la kati na kati hufanya jitihada kutofautisha kati ya mabadiliko ya aina sahihi na mabadiliko ya aina potofu.

Hujaribu na hufanya jitihada kuusukuma muda mbele kwa msaada wa elimu na ubunifu wake na kujinasibisha na maendeleo huku akijaribu kuudhibiti upotofu na kuepuka kutangamana nao. Lakini kwa bahati mbaya, si mara zote mwanadamu huchagua njia hii. Anaandamwa na magonjwa mawili ya hatari, ugonjwa wa kutotaka kubadilika na ugonjwa wa ujinga. Ugonjwa wa kwanza matokeo yake ni kubaki bila mabadiliko na kujiepusha na maendeleo na matokeo ya ugonjwa wa pili ni upotofu wa kuangamia. Asiyetaka kubadilika huchukia kila jambo jipya na hawezi kuafikiana na kitu chochote isipokuwa cha zamani.

Kwa upande wa pili, limbukeni huona kila kitu kipya kuwa ni cha kisasa na maendeleo na hukiaona kuwa ndio hitajio la wakati. Kwa yule asiyetaka mabadiliko (rigid) kila maendeleo mapya kwake anaona ni ufisadi na upotofu wakati limbukeni anaona mambo yote mapya bila kubagua yote yana maana kupanuka kwa utamaduni na elimu. Asiyetaka mabadiliko hatofautishi kati ya pumba na kiini safi na kati ya njia na malengo. Kwa maoni yake kazi ya dini ni kuhifadhi yale yote ya kale na kuukuu hata kama hayatumiki.

Anafikiri kuwa Qur'ani iliteremshwa ili kudhibiti mwendo wa wakati na kuibakiza hali ya dunia iwe vile vile siku zote. Kwa mujibu wa mtazamo huu, mila za zamani na zilizopitwa na wakati, kama vile kuanza kusoma Qur'ani kuanzia mwisho, kuandikia kalamu za matete na wino wa kuchovya kunawia kwenye beseni la kituruki; kula kwa mikono, kutumia taa ya mafuta ya taa na kubakia bila ya kujua kusoma na kuandika ni mambo ya kidini ambayo lazima yahifadhiwe na kudumishwa. Kwa upande mwingine limbukeni huelekeza macho yake yote nchi za Magharibi ili aweze kuiga mtindo wowote mpya utakaotokea na kila mila mpya. Huiita hali hii kuwa ni kisasa na jambo la lazima kufuatwa lililoletwa na wakati. Wote wawili, wasiotaka mabadiliko na waliopotoka (wajinga) wanaamini kuwa mila na desturi zote za zamani ni kanuni/matendo ya kidini, tofauti ni kuwa asiyetaka mabadiliko anataka kuzihifadhi wakati mjinga anaona kuwa dini ni sawa na kudorora (bila mabadiliko yoyote).

Katika karne chache zilizopita suala la migongano kati ya dini na sayansi limekuwa likibishaniwa sana miongini mwa watu wa nchi za Magharibi. Wazo la migongano liliibuka kutokana na mambo mawili. Kwanza kanisa lilikuwa limezikubali baadhi ya dhana za kisayansi na kifalfasa kuwa ni imani za kidini, lakini maendeleo ya sayansi yakathibitisha uongo wa dhana hizo. Pili, sayansi imebadilisha muundo na hali za maisha. Wale wasiotaka mabadiliko, ambao wana muonekano wa kushika dini, wanataka kuufanya muonekano wa nje wa maisha ya kimaada kuwa sehemu ya dini, kama tu, bila ulazima wowote walivyoyapa sura ya kidini baadhi ya masuala ya kifalsafa.

Limbukeni nao wanaamini kuwa dini imeamuru muundo fulani wa maisha ya kimaada, na kwa vile sayansi imeamuru kuwepo kwa mabadiliko katika muundo huu, dini inapaswa kutupiliwa mbali. Kupinga mabadiliko kwa kundi moja, na ujinga wa kundi jingine, kumezua wazo la kubuni la mgogoro kati ya sayansi na dini. Hadith ya mafumbo katika Qur'ani Uislamu ni dini ya kimaendeleo na inataka wafuasi wake waendelee. Qur'ani imetumia hadith ya mafumbo (yenye mafundisho) kuwashawishi Waislamu wasonge mbele, chini ya nuru ya Qur'ani. Inasema kuwa wafuasi wa Mtume Muhammad(s.a.w.w) ni kama mbegu iliyopandwa katika ardhi. Kwanza matawi yake hutokeza kama majani laini ya mbegu. Kisha hukua na kuimarika sana kiasi cha kuweza kusimama katika kikonyo chake. Hakua haraka mno kiasi cha kuwashangaza sana wakulima.

Huu ni mfano wa jamii ambayo Qur'ani inaukusudia. Qur'ani inachokikusudia ni kukua. Qur'ani inataka kuweka msingi wa jamii ambayo mara zote itakuwa ikikua, ikiendelea na kupanuka. Will Durant anasema hakuna dini iliyowataka wafuasi wake kuwa na nguvu kama Uislamu ulivyofanya. Historia ya Uislamu wa awali inaonyesha ni kiasi gani Uislamu ulivyo na nguvu ya kuijenga upya jamii na kuisukuma mbele kimaendeleo. Uislamu unapingana na vyote viwili kutaka mabadiliko na ulimbukeni (ujinga) na unaviona vyote hivi viwili kuwa ni hatari. Uchakavu wa kiakili wa wasiotaka mabadiliko na kung'ang'ania kwao mila za zamani ambazo hazina uhusiano wowote na Uislamu, kumetoa kisingizio kwa limbukeni kuuona Uislamu kuwa unapingana na maisha ya kisasa (usasa).

Kwa upande mwingine kufuatana na kuiga mitindo mipya zaidi na namna za maisha za Magharibi kunakofanywa na limbukeni, imani yao kwamba kufuata utaratibu wa Kimagharibi kimwili na kiroho, kukubali kwao tabia, adabu na desturi za Magharibi, na kuiga kibubusa sheria za kiraia na kijamii kutoka katika nchi za Magharibi, kumetoa kisingizio kwa wasiotaka mabadiliko kukitazama kila kitu kipya kwa mashaka na kukiona kama tishio kwa dini yao, uhuru wao na kwa haiba ya kijamii ya jumuiya yao. Kwa sasa, Uislamu unagharamikia makosa ya makundi yote mawili.

Ung'ang'anizi wa wasiotaka mabadiliko umeacha uwanja wazi kwa limbukeni kufanya uharibifu na ujinga wa limbukeni umewafanya wasiotaka mabadiliko kuwa ving'ang'anizi zaidi katika imani zao. Inashangaza kuona kuwa hawa wanaojiita wameelimika na kustaarabika ingawa kiuhalisia ni watu wajinga, wanafikiri kuwa muda ni maasumu (haubebi dhambi). Ukweli ni kuwa mabadiliko yote yanaletwa na watu, na mwanadamu sio maasumu hata kidogo (hajaepukana na madhambi). Sasa vipi inaweza kufikirika kuwa mabadiliko ya muda mara zote huwa hayana makosa na matatizo. Kama ilivyo tu kuwa mwanadamu ana matakwa ya kupenda sayansi, maadili, sanaa na dini, na mara zote huchukua hatua mpya kwa maslahi ya wanadamu, pia ana baadhi ya tabia mbaya.

Ni mbinafsi, mwenye uchu wa madaraka na mwenye kupenda raha. Anapenda fedha na unyonyaji kama tu alivyo na uwezo wa kugundua mambo mapya na kutafuta njia bora zaidi za kufanya mambo pia ana dhamana ya kutenda makosa. Lakini limbukeni na waliopotoka hawajui mambo hayo. Wanarudia mahadhi yale yale kuwa ulimwengu wa kisasa upo hivi na vile. Kinachoshangaza zaidi ni kuwa wanalinganisha kanuni za maisha na vitu; kama vile viatu, kofia na gauni. Kwa vile vitu hivi hutafutwa na kuhitajika vinapokuwa vipya na kutupwa vinapochakaa, halikadhalika kwa mujibu wao, hali iwe hivyo hivyo kwa ukweli usiobadilika. Kwao, kizuri na kibaya havina maana zaidi ya kipya na cha zamani.

Ukabaila ni mbaya kwa sababu tu ni mfumo wa zamani na umepitwa na wakati. Vinginevyo ulikuwa mzuri kabisa wakati unaanzishwa duniani kwa mara ya kwanza. Halikadhalika unyonyaji wa wanawake ni mbaya tu kwa vile haupendwi na ulimwengu wa kisasa; vinginevyo hadi hivi majuzi, watu hawa hawa walikuwa hawampi mgao wa urithi. Walikuwa hawajaitambua haki yake ya kumiliki mali na walikuwa hawaheshimu ridhaa na maoni yake.

Kwa mujibu wa watu hawa, katika zama hizi, zikiwa ni zama za anga (kuruka na ndege n.k), kama ilivyokuwa tu haiwezekani kusafiri kwa punda na kuacha ndege, kuwasha kibatari na kuacha umeme, kushona nguo kwa mkono na kuandika kwa mkono huku ukiacha mashine kubwa za kisasa za kuchapishia, halikadhalika haiwezekani kuacha kwenda kwenye sherehe za muziki, sherehe ambazo watu wanavaa mavazi ya kuogelea, mialiko ya chakula cha usiku chenye nyama za kubanikwa, kutoshiriki katika vicheko vya ovyo, kutocheza karata, kutovaa visketi vifupu kwani vitu vyote hivi ni mitindo ya karne hii. Wanahofu kuwa wasiposhiriki katika mambo haya watarudi nyuma katika zama za kuendesha farasi. Wanadai kuwa hizi ni zama za nyukilia, zama za sayansi, zama za miezi ya kubuni na zama za makombora ya masafa marefu.

Hili ni jambo zuri! Sisi pia tunamshukuru Mungu kuwa tunaishi katika zama hizi na tunaomba kwamba tufurahie na kufaidika na sayansi na viwanda kwa kiwango cha juu kabisa. Lakini je, mambo yote haya yanasababishwa na sayansi tu? Je, hali zote za karne hii ni matokeo ya maendeleo ya kisasa ya sayansi? Je, sayansi inadai kuwa imedhibiti mambo yote hapa duniani? Sayansi haijawahi kudai hivyo hata siku moja.

Balaa la karne yetu ni kuwa kundi la wanasayansi kwa nia njema kabisa, huitumia sayansi kufanya ugunduzi mpya, lakini kundi jingine la wabinafsi na wenye uchu wa madaraka na wanaoabudu fedha huyatumia vibaya matunda ya jasho la wanasayansi ili kuyafikia malengo yao ya kiovu. Sayansi inalalamika kuwa inatumiwa vibaya na wanaadamu wakorofi na hii ndio bahati mbaya ya kizazi chetu. Sayansi inasonga mbele katika fani za fizikia na inagundua sheria za mwanga na kuakisi na kundi la wakorofi na wabinafsi wanaitumia kutengenezea filamu za bluu (ngono) za uharibifu na uovu. Kemia inaendelea na kugundua tabia za vitu mbali mbali na michanganyiko yake.

Baadhi ya watu wanaamua kutumia ugunduzi huu kutengeneza madawa ya kulevya, heroin ambayo ni laana kwa wanaadamu. Sayansi iligundua chanzo kizuri cha nishati ndani ya atom, lakini kabla ya ugunduzi haujatumika kwa manufaa ya wanaadamu, wenye tamaa ya madaraka walifanya haraka kutengeneza bomu la atomiki, na kuwadondoshea watu wasio na hatia. Mapokezi yalipoandaliwa, kwa ajili ya heshima ya Einstein, mwanasayansi mkubwa wa karne ya 20, yeye mwenyewe alipanda juu ya jukwaa na kusema, "Mnampa heshima mtu ambaye amechangia kwa namna fulani kutengenezwa kwa bomu la atomiki?"

Einsten mwenyewe hakutumia elimu yake kutengeneza bomu. Ni wengine waliotumia ugunduzi wake kwa lengo hili. Matumizi ya heroin, mabomu ya atomiki na filamu za matusi (bluu) haviwezi kuhalalishwa eti kwa madai kuwa ni mambo ya karne hii. Ikiwa ndege za kisasa kabisa za mabomu zinatumika kurushia mambomu bora kabisa kwa watu wa nchi nyingine, na watu walioelimika sana wanaajiriwa kufanya kazi hii, je, usasa huu unaweza kupuguza ushenzi wa kurithi wa tendo hili?

4

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU

- III UISLAMU NA USASA

Hoja kuu ya wale ambao wanasema kuwa katika masuala ya haki za kifamilia tunapaswa kufuata mfumo wa Kimagharibi, ni kuwa muda umebadilika na mahitaji ya karne hii yanatutaka tufanye hivyo. Tunaonelea kuwa ni vizuri tuyaweke maoni yetu wazi juu ya nukta hii, kwa sababu bila kufanya hivyo, mjadala juu ya nukta yoyote hautakuwa kamili, ingawa kwa sababu ya uchache wa nafasi haiwezekani kulijadili suala hili kwa mitazamo yake yote, kifalsafa, kisheria, kijamii na kimaadili. Itatosheleza hapa kujadili nukta mbili tu. Nukta ya kwanza ni kwamba kuafikiana kwayo na kukubaliana na mabadiliko ya wakati sio suala rahisi sana kama baadhi ya watu wasiojua wanavyofikiri. Mabadiliko yanayoletwa na wakati, wakati fulani huwa ni ya kurudisha maendeleo nyuma.

Tunapaswa kwenda na mabadiliko ya wakati ya kimaendeleo na tunapaswa kuyapiga vita mabadiliko yanayoletwa na wakati ambayo ni ya kiharibifu. Ili kutofautisha aina hizi mbili za mabadiliko na kujua asili yake, tunapaswa kujua chanzo cha maendeleo (ugunduzi au mabadiliko) haya mapya na yameelekezwa katika mwelekeo gani. Tunapaswa kuangalia ni tabia gani za kibinadamu zimeyaleta (njema au mbaya) na ni matabaka gani ya watu yanatetea mambo haya mapya?

Tunapaswa kuangalia je yameletwa na tabia tukufu za mwanadamu au matamanio duni yanayofanana na wanyama, na kama yamekuja kama matokeo ya uchunguzi usio wa kibinafsi wa wanazuoni na wasomi, au yameletwa na matamanio duni ya wanaotumikia nafsi zao na tabia za kifisadi za jamii.

MNYAMBULIKO WA SHERIA ZA KIISLAMU

Nukta ya pili inayofaa kuwekwa wazi ni kuwa baadhi ya wasomi wa kiislamu wanaamini kuwa Uislamu una uwezo na sifa ambazo zinaupa uwezo wa kutumika zama zote. Kwa mujibu wa wasomi hawa, mafundisho ya Uislamu yanaafikiana na maendeleo ya wakati, kupanuka kwa utamaduni na matokeo ya mabadiliko haya. Hebu tuangalie asili, sifa na uwezo huu ambao Uislamu unao. Kwa maneno mengine hebu tuangalie ni vifaa gani vimewekwa katika jengo hili la dini, na ikiwa vimeipa sifa ya kuafikiana na hali zote zinazobadilika, bila kuwa na haja ya kuacha baadhi ya mafundisho yake na bila mgogoro wowote kati ya mafundisho yake na hali yoyote inayojitokeza ya kupanuka kwa elimu na ustaarabu.

Ingawa suala hili lina sura ya kiufundi, ili kuondoa shaka shaka ya wale wanaotilia shaka ukweli huu kuwa Uislamu una sifa hii, tunalielezea kwa kifupi hapa. Kwa undani zaidi juu ya suala hili, wasomaji wanaweza kusoma kitabu kiitwacho 'Tanbihul Ummah' cha hayati Ayatullah Naini au kitabu kingine kiitacho 'Marjaiyyat Wal Imamat cha mwanazuoni mkubwa wa zama hizi Allamah Tabatabai. Lakini vitabu vyote hivi vipo katika lugha ya kifursi. Kuna nukta nyingi, ambazo zinaunda siri ya Uislamu kuwa na uwezo wa kuafikiana na kupanuka kwa elimu na ustaarabu, na uwezo wa kutumika kwa sheria zake thabiti na imara katika hali mbali mbali za maisha. Hapa tutataja baadhi yake.

Msisitizo katika roho na kutojali sana kiwiliwili. Uislamu haujashughulikia maisha ya nje (kimwili) tu ambayo hutegemea kiwango cha maendeleo ya elimu ya mwanadamu. Mafundisho ya Uislamu hushughulikia roho pia na malengo ya maisha na hutoa njia bora kabisa ya kuyafikia malengo haya. Sayansi haijabadilisha roho na malengo ya maisha wala haijapendekeza njia yoyote nzuri zaidi, fupi zaidi na salama zaidi ya kuyafikia malengo haya. Imetoa tu njia bora zaidi na vifaa vya kukwamisha njia ya kuyafikia malengo haya. Uislamu, kwa kuhifadhi malengo tu katika himaya yake na kuacha muundo na mbinu kwenye himaya ya sayansi na teknolojia, umeepuka migongano dhidi ya utamaduni na ustaarabu.

Sio hivyo tu lakini pia kwa kuhimiza mambo yanayosaidia kupanuka kwa ustaarabu, yaani elimu, kazi, uchamungu, ridhaa, ujasiri na uvumilivu bila kukata tamaa, umejitolea kuwa kigezo kikuu cha kupanua ustaarabu. Uislamu umeweka alama za barabarani katika njia yote ya maendeleo ya mwanadamu. Alama hizi kwa upande mmoja zinaonyesha njia na kituo cha mwisho na kwa upande wa pili zinaonyesha makorongo na sehemu za hatari. Sheria zote za Kiislamu ni alama za barabara, aidha za aina ya kwanza au ya pili. Njia za maisha katika zama hutegemea juu ya kiwango cha elimu ya wanaadamu.

Kwa kadri elimu ya watu inavyopanuka, ndivyo njia bora zaidi za kujipatia kipato zinavyotokea na moja kwa moja zinachukua nafasi ya zile njia duni (za zamani). Mifumo ya nje na ya kimaada ya njia hizi (za kupatia riziki) haina utakatifu katika Uislamu, na Waislamu hawalazimiki kuzidumisha. Uislamu haujasema kifaa hiki na kile kitumike kwa ushonaji, ususi, kilimo, usafiri, vita au kazi nyingine. Hivyo hapawezi kuwa mgogoro wowote kati ya sayansi na Uislamu, pindi kifaa kinapopitiwa na wakati, cha kisasa zaidi kinaweza kutumika badala yake.

Uislamu haujaagiza kutumika kwa mtindo maalum ya viatu au nguo, wala haujapendekeza aina fulani ya ujenzi wa majengo. Halikadhalika hauhimizi juu ya mbinu fulani fulani za uzalishaji na ugavi. Hii ni moja ya sifa hizo za Uislamu, ambazo zimeuwezesha kuweza kutumika katika maendeleo yote ya wakati. Sheria madhubuti kwa mahitaji madhubuti na sheria zinazobadilika kwa mahitaji yanayobadilika. Sifa nyingine ya Uislamu, ambayo ina umuhimu mkubwa ni kuwa umeweka sheria madhubuti (zisizobadilika) kwa ajili ya mahitaji madhubuti (yasiyobadilika) na sheria zinazobadilika kwa mahitaji yanayobadilika. Mbali na mahitaji ya wanaadamu, mahitaji ya mtu mmoja mmoja na vikundi, yote yana asili ya kudumu.

Hayabadiliki kwa mujibu wa wakati. Kanuni za mifumo inayotawala silika za binadamu na mahusiano ya kijamii hazibadiliki. Tunazijua nadharia za 'Maadili husianishi' na 'Uadilifu husianishi' ambazo zina wafuasi wake, na tutatoa maoni yetu kuhusiana nao baadaye. Sehemu nyingine ya mahitaji ya mwanadamu ni ile ya mahitaji yanayobadilika, na hii huhitaji sheria zinazobadilika. Uislamu ulishayaona mahitaji hayo na umeyaunganisha na kanuni fulani ambazo zina sheria ndogo zinazobadilika kila hali inapobadilika. Kufafanua nukta hii hebu tuangalie mifano hii;'Andaeni majeshi kwa ajili yao (maadui)' (Suratul Anfal 8:60.) Wakati huo huo tunasoma hadith kadhaa za Mtume katika vitabu vya sheria za Kiislamu chini ya kichwa cha habari 'Kuendesha farasi na kurusha mishale.' Mtume aliwaelekeza Waislamu wajifunze kuendesha farasi na kurusha mishale na wawafundishe watoto wao pia. Haya yalikuwa ni sehemu ya mafunzo ya Kiislamu katika zama hizo.

Ni dhahiri kabisa hapa kuwa amri ya msingi ni 'Kuandaa majeshi.' Upinde na mshale, jambia na mkuki na farasi sio vya muhimu. Kilicho cha muhimu ni kuwa imara kijeshi dhidi ya maadui. Kuandaa majeshi ni amri ya kudumu ambayo imetokana na hitajio la kudumu. Hata hivyo ulazima wa kupata ujuzi katika kuendesha farasi na kurusha mishale sio wa kudumu, na hubadilika kutokana na wakati.

Kutokana na kubadilika kwa hali, ujuzi wa kufyatua risasi umechukua nafasi ya kurusha mishale. Mfano mwingine ni sheria ya kijamii inayohusu kubadilishana mali, iliyotajwa katika Qur'ani. Uislamu umetambua kanuni ya umiliki wa mali wa mtu binafsi. Hata hivyo umiliki huu unaotambuliwa na Uislamu ni tofauti na ule uliopo katika nchi za kibepari. Tabia ya umiliki wa mali wa watu binafsi katika Uislamu ni kanuni ya kubadilishana. Kwa utaratibu huu Uislamu umeweka sheria fulani.

Mojawapo imeelezwa na Qur'ani Tukufu katika maneno haya'Na msile mali zenu (kila mmoja kula za mwenzake) kwa batili' (Suratul Baqarah, 2:188).

Kwa maneno mengine katika mauzo ya biashara, fedha isitoke mkono mmoja kwenda mwingine isipokuwa kwa kubadilishana na kitu kingine cha halali chenye kuwa na mamlaka ya mwisho juu ya mali hiyo. Imelezwa na kufafanuliwa katika sheria ya Kiislamu mauzo na manunuzi ya vitu fulani yamekatazwa. Vitu hivyo ni pamoja na damu na kinyesi cha binadamu. Sababu ni kuwa vitu hivi havina thamani inayoviwezesha kuhesabika kuwa sehemu ya mali ya mwanadamu. Kanuni hii ni sawa ya mali ya mwanadamu. Kanuni hii ni sawa na ile iliyo katika Aya iliyonukuliwa hapo juu.

Ubatili wa mauzo na manunuzi ya damu na kinyesi cha binaadamu ni sehemu au mfano tu wa matumizi ya kanuni hiyo. Hata kama hakuna ubadilishaji uliofanyika, (wa bidhaa au bidhaa kwa fedha) fedha au mali inayomilikiwa na mtu fulani haiwezi kufujwa au kuliwa bure. Sheria inayokataza kula mali ya mtu mwingine bure (bila kufanya kazi) au kiwizi ni kanuni madhubuti na inatumika zama zote, na imetokana na hitajio la kudumu la jamii.

Lakini kanuni kuwa damu na kinyesi cha binadamu havihesabiki kama mali na haviruhusiwi kuuzwa, inahuisiana na wakati na kiwango cha ustaarabu. Kanuni hii inaweza kubadilishwa kutokana na mabadiliko ya hali, maendeleo ya sayansi na viwanda na uwezekano wa kuzitumia bidhaa hizi katika namna sahihi na yenye manufaa. Mfano mwingine; "Imam Ali(a.s) hakuwahi kuweka dawa kwenye nywele zake hata siku moja, ingawa zilikuwa zimekuwa za mvi katika miaka ya mwisho ya uhai wake.

Siku moja mtu mmoja alimwambia, 'Je Mtume hakuamrisha nywele za mvi ziwekwe dawa?" Ali alijibu 'Ndiyo aliamrisha' Sasa kwa nini huweki dawa kwenye nywele zako? Yule mtu aliuliza. Ali akasema; "Katika wakati ule ambao Mtume alitoa maelekezo haya, idadi ya Waislamu ilikuwa ndogo na kulikuwa wazee wengi waliokuwa wakishiriki vitani. Mtume aliwaamrisha wazipake dawa ili kuficha umri wao halisi, kwani kama adui angeona kuwa anapambana na kundi la wazee tu, hamasa yake ingeongezeka. Kwa kuwa Uislamu umeenea dunia yote, hali imebadilika. Kila mtu yupo huru kupaka dawa nywele zake au kuacha." Kwa maoni ya Imamu Ali, maelekezo ya Mtume hayakuwa ya kudumu wala haikuwa sheria ya kudumu.

Uislamu unajali muonekano wa nje na roho ya ndani pia. Lakini unataka pumba kwa ajili ya punje yenyewe na unataka nguo kwa ajili ya mwili. Suala la kubadilisha herufi Katika siku za hivi karibuni hapa Iran kumekuwa na ubishani juu ya kubadlisha herufi. Suala hili linaweza kuangaliwa katika pande mbili kwa mtazamo wa kanuni za Kiislamu, na kwa sura mbili. Kwanza ni iwapo Uislamu unapendelea herufi fulani na kuzibagua nyingine.

Je Uislamu unaziona herufi za sasa, ambazo ni za Kiarabu, kama zake, na herufi nyinginezo kama zile za kilatini zinazoonekana ni za kigeni? Uislamu ambao ni dini ya ulimwengu mzima unaziona herufi zote duniani kuwa ni sawa. Sura ya pili ni kuwa kiasi gani kubadilika kwa herufi kutachanganya utamaduni wa Taifa la Kiislamu na watu wengine na kutakuwa na madhara gani kwa utamaduni wa taifa hili. Na zaidi ya hayo, katika karne 14 zilizopita, vitabu vya Kiislamu na kisayansi vilivyozalishwa na Irani vimeandikwa katika herufi za sasa (za kiarabu), je kubadilisha herufi si kutazifuta (haribu) kazi zote hizi?

Swali jingine ni, 'Ni akina nani wanaopendekeza mabadiliko haya, na ni akina nani watakaoyatekeleza? Maswali yote haya ni thabiti.' Kuwategemea wengine ndio kumekatazwa, sio kofia ya kizungu Watu kama mimi mara nyingi wanakumbana na maswali, yanayoulizwa kwa dharau au kejeli. "Sheria ya Kiislamu inasemaje kuhusu kula ukiwa umesimama?' Ni vipi kuhusu kula kwa kijiko au uma?' Je kuvaa kofia ya kizungu kumekatazwa?' Je kutumia lugha za kigeni kumekatazwa?'" Katika kujibu maswali haya, tunasema kuwa Uislamu haujatoa maelekezo yoyote mahsusi juu ya hili. Uislamu haujawaelekeza wafuasi wake kula kwa mkono au kijiko. Ulichowaelekeza ni kuzingatia usafi.

Uislamu haujaelekeza matumizi ya mitindo ya aina fulani ya viatu, kofia au nguo. Kwa mtazamo wa Uislamu lugha zote Kiingereza, Kijapani, Kifursi, zina hadhi sawa. Hata hivyo, Uislamu unasema kitu fulani zaidi. Umesema kuwa imekatazwa mtu kupoteza utambulisho wake. Kuwaogopa wengine bila ulazima kumekatazwa, Kuwaiga wengine kumekatazwa, kuchekeshwa na kuvutiwa na wengine kama sungura anavyovutiwa na nyoka, kumekatazwa.

Kumchukulia punda mgeni aliyekufa kuwa ni farasi kumekatazwa. Kuingiza nchini upotofu na ukosefu wa maadili kutoka nje, kwa madai ni mambo ya kisasa ya karne hii, kumekatazwa. Kuamini kuwa Waislamu wanapaswa kufuata mila na utamaduni wa Kimagharibi ndani na nje, kimwili na kiroho, kumekatazwa. Kwenda nchi ya Kimagharibi kwa siku chache na baada ya kurudi, unaanza kutamka maneno yetu kama wao (wazungu) kumekatazwa. Muhimu na muhimu zaidi. Sura nyingine ya Uislamu inayoufanya uende na mahitaji ya wakati ni kukubaliana kwa mafundisho yake na akili/mantiki.

Uislamu umetangaza kuwa sheria zake zimezingatia maslahi makubwa zaidi. Na wakati huo huo, Uislamu wenyewe umetoa madaraja mbali mbali ya umuhimu wa maslahi haya. Hii inarahisisha kazi ya wataalamu wa sheria za Kiislamu katika fani hizo ambapo maslahi tofauti yanaonekana kugongana. Katika hali hizo, Uislamu umewaruhusu wataalamu wa sheria za Kiislamu kupima uzito wa maslahi tofauti, na kuzingatia mwongozo ambao Uislamu wenyewe umetoa, katika kuangalia ni maslahi gani hilo ni muhimu zaidi. Katika fani ya sheria za Kiislamu, hii huitwa suala la "muhimu na muhimu zaidi." Kuna mifano mingi ambapo kanuni hii ya maslahi ya juu na ya juu zaidi imepata kutumika.

Hata hivyo kwa sababu ya uchache wa nafasi, tunairuka sehemu hii Sheria yenye haki ya Turufu. Sifa nyingine ya Uislamu ambayo imeipa dini hii uwezo wa kuhamishika na kutumika katika hali mbali mbali na imeifanya kuwa dini inayoishi na ya kudumu milele ni kuwa ndani yake kuna chombo cha sheria ambacho kazi yake ni kudhibiti na kurekebisha sheria nyingine.

Mafakihi wanaziita kanuni hizi kuwa ni " kanuni za kuongozea." Kanuni ya 'Hakuna madhara' na 'Hakuna hasara' kwamba sheria haitatumika pale ambapo inaweza kusababisha ugumu au madhara kwa maslahi ya mtu asiye na hatia, imeuenea (imeutawala) mfumo mzima wa kisheria. Lengo la kanuni hizi ni kudhibiti na kurekebisha sheria nyingine. Kwa kusema kweli Uislamu umezipa nguvu ya turufu kanuni hizi ambazo hubadilisha kanuni nyingine.

Madaraka ya mtawala Kwa nyongeza kuna mfululizo mwingine wa kanuni za kuweka mambo katika mizania ambazo Mwenyezi Mungu ameipa dini hii ya mwisho. Ayatullah Na'ini na Allamah Tabatabai, juu ya hili, wametegemea madaraka ambayo Uislamu umeipa serikali ongofu ya Kiislamu. Kanuni ya ijtihadi Mshairi na mwanafalsafa wa Kipakistani anasema kuwa Ijtihadi (kuzalisha sheria kutoka vyanzo vyake vya asili) ni nguvu ya hamasa ya Uislamu. Yuko sawa kusema hivyo. Lakini kilicho muhimu zaidi ni kuwa Uislamu una sifa maalum ya kuruhusu Ijtihadi. Hakuna dini nyingine yenye sifa hii katika namna hii hii. Jengo la ndani la Uislamu limejengwa katika namna ambayo kwa msaada wa Ijtihadi, unaweza mara zote kwenda na mahitaji yanayobadilika katika maisha.

Abu Ali Ibn Sina (Avicenna) katika kitabu chake Al-Shifa, ameelezea haja ya Ijtihadi kuwa inatokana na kubadilika kila mara kwa mahitaji. Anasema kuwa hali za maisha mara zote zinabadilika. Matatizo mapya yanaibuka kila mara, lakini misingi ya Uislamu haibadiliki. Hivyo katika hali hii, lazima wawepo watu wanaojua sheria za kiislamu vizuri na mafundisho ya Kiislamu vizuri ili waweze kujibu maswali yote yanayoibuka katika kila zama na hivyo kukidhi mahitaji ya wakati. Katiba ya Iran inaamuru kuwa pawepo chombo cha mujtahidi wasiopungua watano (wanazuoni wakubwa wa Theolojia wanaoweza kufanya ijtihadi) kitakachokuwa kikichunguza sheria zinazopitishwa na serikali kila wakati.

Lengo hapa ni kuwa watu hawa (mujtahidi) kwa vile sio wapinga mabadiliko wala hawapingi maendeleo ya kisasa, wala sio limbukeni wala hawawafuati wengine kibubusa, waangalie na kudhibiti mfumo wa sheria wa nchi. Inapaswa kueleza kuwa ijtihad kwa namna halisi ina maana kubobea na inahitaji uelewa wa ndani sana wa misingi ya Uislamu na nguzo zake na elimu kubwa kabisa ya kanuni za fikihi ya Kiislamu, ambayo si kila mtu aliyesoma Uislamu kwa muda fulani anaweza kudai kuwa mujtahid.

Hapana shaka kuwa hii ni kazi ya umri mzima wa mtu ili kubobea katika kanuni na mafundisho ya Uislamu, na mbali na kipaji, nia na akili, inahitaji pia msaada wa Mungu. Mbali na kubobea (kwenye mchepuo maalum) na Ijtihad, baadhi ya watu wanaweza kupata elimu na kufikia kiasi kwamba maoni yao yanaweza kuchukuliwa kuwa ni fatwa. Historia ya Uislamu inawataja watu hao ambao licha ya elimu yao kubwa na maadili yao ya hali ya juu walikuwa na hadhari kubwa, walipokuwa wakitoa maoni yao, juu ya masuala ya kisheria.

10

11

12

13

14

15

16