TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE Juzuu 24

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE18%

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE Mwandishi:
: HASANI MWALUPA
Kundi: Qurani tukufu

Juzuu 1 Juzuu 2 Juzuu 3 Juzuu 4 Juzuu 5 Juzuu 6 Juzuu 7 Juzuu 8 Juzuu 12 Juzuu 13 Juzuu 14 Juzuu 15 Juzuu 16 Juzuu 17 Juzuu 18 Juzuu 19 Juzuu 20 Juzuu 21 Juzuu 22 Juzuu 23 Juzuu 24
  • Anza
  • Iliyopita
  • 30 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 28952 / Pakua: 5121
Kiwango Kiwango Kiwango
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE Juzuu 24

Mwandishi:
Swahili

1

2

3

15

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

Sura Ya Sitini Na Nane: Surat Al- Qalam. Imeshuka Makka. Imesemekana kuwa baadhi imeshuka Madina. Ina Aya 52.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

ن وَالْقَلَمِ وَمَا يَسْطُرُونَ ﴿١﴾

1. Nun. Naapa kwa kalamu na yale wanayoandika.

مَا أَنتَ بِنِعْمَةِ رَبِّكَ بِمَجْنُونٍ ﴿٢﴾

2. Kwa neema ya Mola wako wewe si mwendawazimu.

وَإِنَّ لَكَ لَأَجْرًا غَيْرَ مَمْنُونٍ ﴿٣﴾

3. Na kwa hakika wewe una ujira usiokatika.

وَإِنَّكَ لَعَلَىٰ خُلُقٍ عَظِيمٍ ﴿٤﴾

4. Na hakika wewe una tabia tukufu.

فَسَتُبْصِرُ وَيُبْصِرُونَ ﴿٥﴾

5. Karibu utaona, na wao wataona.

بِأَييِّكُمُ الْمَفْتُونُ ﴿٦﴾

6. Ni nani kati yenu aliyepandwa na wazimu.

إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ ﴿٧﴾

7. Hakika Mola wako ndiye anayemjua zaidi aliyepotea njia yake na Yeye ndiye anaye­wajua zaidi walioongoka.

فَلَا تُطِعِ الْمُكَذِّبِينَ ﴿٨﴾

8. Basi usiwatii wanaokadhibisha.

وَدُّوا لَوْ تُدْهِنُ فَيُدْهِنُونَ ﴿٩﴾

9. Wanatamani lau ungelainisha ili nao wakulainishie.

وَلَا تُطِعْ كُلَّ حَلَّافٍ مَّهِينٍ ﴿١٠﴾

10. Wala usimtii kila mwingi wa kuapa aliye dhalili.

هَمَّازٍ مَّشَّاءٍ بِنَمِيمٍ ﴿١١﴾

11. Msingiziaji, apitae akifitini.

مَّنَّاعٍ لِّلْخَيْرِ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ ﴿١٢﴾

12. Mwenye kuzuia heri, mwenye kudhulumu, mwingi wa mad­hambi.

عُتُلٍّ بَعْدَ ذَٰلِكَ زَنِيمٍ ﴿١٣﴾

13. Mwenye roho ngumu, juu ya hayo, ni mwanaharamu.

أَن كَانَ ذَا مَالٍ وَبَنِينَ ﴿١٤﴾

14. Ati kwa kuwa ana mali na watoto!

إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ آيَاتُنَا قَالَ أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ ﴿١٥﴾

15. Anaposomewa Aya zetu, husema: Hizi ni ngano za watu wa kale!

سَنَسِمُهُ عَلَى الْخُرْطُومِ ﴿١٦﴾

16. Tutamtia doa juu ya pua.

WEWE SI MWENDAWAZIMU

Aya 1- 16

MAANA

Nun . kwa kukadiria maneno ya kuwa hii ni sura ya Nun. Hii sio kama mianzo mingineyo ya herufi zinazoanziwa sura, tulizozizungumzia katika Juz. 1 (2:1).

Kuna aliyesema kuwa ni samaki, mwingine akasema ni chombo cha wino, watatu akasema ni wino, wa nne akasema ni nun ya neno rahman, na jamaa wa kisufi wakasema kuwa ni nafsi. Kauli zote hizi zinahitajia dalili.

Naapa kwa kalamu na yale wanayoandika.

Wametofautiana kuhusu kalamu: Kuna waliosema ni kalamu iliyotumika kwenye lawh mahfud[ (ubao maalum uliohifadhiwa). Mwingne akasema ni kila kalamu, na kwamba herufi aliY na la` kwenye neno hili ni ya jinsi, ambayo inamaanisha kuenea.

Hii ndio kauli iliyo dhahiri; kwamba makusudio sio kalamu hasa, bali ni nyenzo yoyote ya kuandikia; kama inavyoashiria kauli inayofuatia inayosema: “Na yale wanayoyaandika.”

Kwa hiyo basi kalamu itakuwa ni kinaya cha chombo cha kuandikia, vyovyote kitakavyokuwa, kilichopo au kitakachogunduliwa karibuni au baadaye. Tumedokeza faida za ubainifu katika Juz. 27 (55:4), kwamba manufaa ya ubainifu ni sawa na manufaa ya maji na hewa.

Kwa neema ya Mola wako wewe si mwendawazimu.

Maneno yanaelekezwa kwa Muhammad(s.a.w.w) . Hakuna yeyote anayed­hania kuwa Muhammad(s.a.w.w) ni mwenda wazimu. Wale waliompa sifa hiyo walikusudia kuwa ana jinni linalompa wahyi; kama wanavyodai kwamba kila mshairi ana jinni linalomfundisha ushairi.

Hilo linaashiriwa na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu akiwasimulia:

وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُو آلِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَّجْنُونٍ ﴿٣٦﴾

“Na wakisema: Hivi tuiache miungu miungu yetu kwa ajili ya huyu mshairi mwendawazimu?” Juz. 23 (37:36).

Na kwa hakika wewe una ujira usiokatika.

Neno ‘usiokatika’ tumelifasiri kutokana na neno mamnun, ambalo pia lina maana ya kusimbuliwa au maana zote mbili pamoja (kukatika na kusimbuliwa).

Kimsingi ni kuwa malipo yanapimwa kwa natija ya kazi na athari yake. Bado athari za Muhammad(s.a.w.w) , mwito wake na ukuu wake unaendela hadi leo, kuanzia mashariki mwa ardhi hadi magharibi yake na utaendelea hadi siku ya mwisho. Kwa hiyo si kioja kupata karama ya milele kutoka kwa Mola wake.

Na hakika wewe una tabia tukufu.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) hakumsifu yeyote katika mitume wake na wasi­fa huu isipokuwa Muhammad.

Maana yake yanafupilizwa na kauli yake Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) : “Mola wangu amenifunza maadili akayafanya mazuri mafunzo yangu,” yaani Mwenyezi Mungu ameelekeza kwa Muhammad(s.a.w.w) maadili yale yale aliyoumba kwa ajli ya nafsi.

Vile vile Mwenyezi Mungu (s.w.t) hakuwahi kuapa kwa maisha ya mtu isipokuwa kwa maisha ya Muhammad(s.a.w.w) ; pale aliposema:

لَعَمْرُكَ إِنَّهُمْ لَفِي سَكْرَتِهِمْ يَعْمَهُونَ ﴿٧٢﴾

“Naapa kwa umri wako! Hakika hao walikuwa katika ulevi wao wakiman­gamanga.”

Juz. 14 (15:72).

Ama wasifu wa Muhammad(s.a.w.w) kuwa ni mwisho wa manabii, Maana yake ni kuwa Muhammad alifikia ukomo wa sifa za mtu zisizofikiwa na yeyote kwa ukamilifu. Ni muhali kuja baada yake atakayekuwa bora zaidi kuliko yeye au kuja na sharia bora zaidi ya sharia zake; bali hakuna kium­be yeyote kuanzia wa mwanzo hadi wa mwisho anayefanana naye. Hilo linaashiriwa na kauli yake Mtume(s.a.w.w) : “Mimi ni bwana wa watu wote, wala sisemi kwa kujifaharisha.”

Hii ni kwa kuwa sharia na utume umeishilizwa kwake. Ibn Al-arabiy anasema, katika Futuhat: kuwa Mwenyezi Mungu ameumba viumbe aina kwa aina, akafanya walio bora. Walio bora katika viumbe ni mitume, na katika mitume kuna wateule ambao ni ulul-az` na katika wao kuna mteule zaidi naye ni Muhammad(s.a.w.w) .

Karibu utaona, na wao wataona, ni nani kati yenu aliyepandwa na wazimu.

Hili ni onyo na kiaga, kwamba hivi karibuni itakubainikia wewe na maadui zako kwamba wao ndio wajinga, wapotevu na wendawazimu zaidi katika watu, na kwamba wewe ndiwe ulie juu, mwenye akili na mtukufu wa maadili zaidi ya watu wengine na kwamba ndiwe mtukufu wao zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu.

Hakika Mola wako ndiye anayemjua zaidi aliyepotea njia yake na Yeye ndiye anayewajua zaidi walioongoka.

Mwenyezi Mungu anajua cheo chako ewe Muhammad(s.a.w.w) na uongo­fu na anajua nafasi ya wahasimu wake ya upotevu na mbele yao kuna hisabu na malipo. Imetangulia kwa herufi zake katika Juz. 14 (16:125).

Basi usiwatii wanaokadhibisha.

Washirikina walijaribu kila njia kumzuia Mtume(s.a.w.w) na mwito wake, wakajaribu kumbembeleza kwa cheo na mali, akakataa. Wakatamani lau watakubaliana naye kufanya vile watakavyo, Mwenyezi Mungu akamkataza hilo. Lengo la kumkataza ni kuwakatisha tamaa na wajue kuwa hakuna mjadala wala makubaliano katika twaa ya Mwenyezi Mungu na amri yake. Katazo hili linafanana na anayekutaka mkubaliane naye kwenye dini yako, ukiwa unataka kumkatisha tamaa kabisa, na kumwambia: Mwenyezi Mungu amenikataza hilo.

Wanatamani lau ungelainisha ili nao wakulainishie.

Washirikina walitamani Mtume(s.a.w.w) apunguze baadhi ya yale anayowalingania na wao waache baadhi ya yale aliyowakataza, ijapokuwa ni kwa njia ya kupakaka mafuta kwa mgongo wa chupa ili kusiwe na mvu­tano baina ya pande mbili.

Mfumo wa maneno unafahamisha kuwa aliyetoa maoni hayo anasifika na sifa aliyoiashiria Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa kusema:Wala usimtii kila mwingi wa kuapa aliye dhalili . Anakithirisha viapo bila ya sababu jambo linalomsababisha kuwa dhalili anayedharauliwa.Msingiziaji anawatia ila sana watu.Apitaye akifitini . Anajaribu kuwavuruga watu kwa kunukuuu ya huku akiyapeleka kule.

Mwenye kuzuia heri , yeye haifanyi na anazuia wengine wasiifanye.Mwenye kudhulumu , haki za watu.Mwingi wa madhambi na makosa.Mwenye roho ngumu, juu ya hayo, ni mwanaharamu, asiyejua nasaba yake. Hii ni sifa mbaya zaidi ya zote zinazofikiriwa na akili.

Wafasiri wengi wamesema kuwa aliyekusudiwa na ushenzi huu ni Walid bin Al-mughira, aliyekuwa ni miongoni mwa vigogo wa kikuraishi, mwenye mali nyingi na watoto; kama alivyosema Mwenyezi Mungu:Ati kwa kuwa ana mali na watoto! Anaposomewa Aya zetu, husema: Hizi ni ngano za uwongoza watu wa kale!

Wafasiri wamesema kuwa Aya hii ni ya kukataza kumtii mshenzi huyu. Lakini lililo karibu zaidi na usawa ni kuwa huko kuwa na mali na watoto kumemfanya athubutu kusema Qur’an ni simulizi za watu wa zamani; kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

إِنَّ الْإِنسَانَ لَيَطْغَىٰ ﴿٦﴾ أَن رَّآهُ اسْتَغْنَىٰ ﴿٧﴾

“Hakika mtu hupituka mipaka kwa kujiona ametajirika.” (96:6-7).

Sikwambii tena akiwa na nguvu na watu.Tutamtia doa juu ya pua yake. Waarabu wanatumia kutaja pua kwa ajili ya utukufu na udhalii. Wanasema kwa utukufu: ana pua ya kunusa. Kwenye udhalili wanasema: pua yake ikio mchangani.

Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) atamfedhehesha mjeuri huyu ambaye amejitukuza kwa mali na watoto, atamdhalilisha muda wote, atam laani kwa lugha iliyosajiliwa kwenye Kitabu chake na atamfedhehesha Akhera mbele ya ushuhuda, kwa kusawijika uso na alama nyinginezo za kuakisi madhambi yake.

إِنَّا بَلَوْنَاهُمْ كَمَا بَلَوْنَا أَصْحَابَ الْجَنَّةِ إِذْ أَقْسَمُوا لَيَصْرِمُنَّهَا مُصْبِحِينَ ﴿١٧﴾

17. Hakika tumewajaribu kama tulivyowajaribu wenye sham­ba, walipoapa kwamba watal­ivuna itakapokuwa asubuhi.

وَلَا يَسْتَثْنُونَ ﴿١٨﴾

18. Wala hawakusema: Inshaallah!

فَطَافَ عَلَيْهَا طَائِفٌ مِّن رَّبِّكَ وَهُمْ نَائِمُونَ ﴿١٩﴾

19. Basi lilitokea tukio juu yake kutoka kwa Mola wako, nao wamelala!

فَأَصْبَحَتْ كَالصَّرِيمِ ﴿٢٠﴾

20. Likawa kama limefyekwa.

فَتَنَادَوْا مُصْبِحِينَ ﴿٢١﴾

21. Wakaitana asubuhi.

أَنِ اغْدُوا عَلَىٰ حَرْثِكُمْ إِن كُنتُمْ صَارِمِينَ ﴿٢٢﴾

22. Ya kwamba raukeni kondeni mwenu ikiwa mnataka kuvuna.

فَانطَلَقُوا وَهُمْ يَتَخَافَتُونَ ﴿٢٣﴾

23. Basi walikwenda na huku wakinong’onezana.

أَن لَّا يَدْخُلَنَّهَا الْيَوْمَ عَلَيْكُم مِّسْكِينٌ ﴿٢٤﴾

24. Ya kuwa leo asiliingie hata maskini mmoja.

وَغَدَوْا عَلَىٰ حَرْدٍ قَادِرِينَ ﴿٢٥﴾

25. Na walirauka, nao wana nguvu za kunyima.

فَلَمَّا رَأَوْهَا قَالُوا إِنَّا لَضَالُّونَ ﴿٢٦﴾

26. Basi walipoliona, wakasema: Hakika tumepotea!

بَلْ نَحْنُ مَحْرُومُونَ ﴿٢٧﴾

27. Bali tumenyimwa!

قَالَ أَوْسَطُهُمْ أَلَمْ أَقُل لَّكُمْ لَوْلَا تُسَبِّحُونَ ﴿٢٨﴾

28. Akasema Mbora wao: Je, Sikuwambia, kwa nini hamumsabihi Mwenyezi Mungu?

قَالُوا سُبْحَانَ رَبِّنَا إِنَّا كُنَّا ظَالِمِينَ ﴿٢٩﴾

29. Wakasema: Ametakasika Mola wetu! Hakika tulikuwa madhalimu.

فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَلَاوَمُونَ ﴿٣٠﴾

30. Basi wakakabiliana kulau­miana wao kwa wao.

قَالُوا يَا وَيْلَنَا إِنَّا كُنَّا طَاغِينَ ﴿٣١﴾

31. Wakasema: Ole wetu! Tulikuwa tumeikiuka mipaka!

عَسَىٰ رَبُّنَا أَن يُبْدِلَنَا خَيْرًا مِّنْهَا إِنَّا إِلَىٰ رَبِّنَا رَاغِبُونَ ﴿٣٢﴾

32. Asaa Mola wetu akatubadil­ishia lilio bora kuliko hili. Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu.

كَذَٰلِكَ الْعَذَابُ وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَكْبَرُ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿٣٣﴾

Kama hivyo inakuwa adhabu, na bila ya shaka adhabu ya Akhera ni kubwa zaidi, laiti wangelijua!

LIKAWA KAMA LIMEFYEKWA

Aya 17 – 33

MAANA

Hakika tumewajaribu kama tulivyowajaribu wenye shamba.

Waliojaribiwa ‧ katika neno tumewajaribu - ni washirikina wa kikuraishi waliomkadhibisha Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) ambao Mwenyezi Mungu amewaashiria katika Aya ya nane ya surua hii. ‘Basi usiwatii wanaokadhibisha.’ Akiwemo yule mwenye kupituka mipaka mwenye dhambi ambaye, kama walivyosema wafasri, ni Walid bin Almughira, kigogo wa makuraishi msemaji wa wakadhibishaji akielezea ufidhuli na jeuri yao juu ya haki.

Aya hizi tulizo nazo zinampigia mfano yeye na wao, kwamba kulikuwa na watu waliokuwa na shamba lililojaa mazao, lakini wao walikuwa mabahili kwa mafukara na masikini.

Mazao yalipokomaa na kukurubia kuvunwa walipanga njama na kuapa kuwa wavune shamba asubuhi na mapema, mafukara wakiwa hawana habari. Waliazimia hivyo bila ya kuyaunganisha maazimio yao na matakwa ya Mwenyezi Mungu. Waliambiana kuwa wawanyime wahitaji kile walichopewa na Mwenyezi Mungu, wakiwa wamesahau mipangilio ya Mwenyezi Mungu na uweza wake.

Usiku huo huo walioazimia kuvuna, Mwenyezi Mungu alilitermshia shamba janga la mbinguni lilioharibu mazao yote kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Walipoamka asubuhi na kwenda shambani walipigwa na butwaa, wakaan­za kulaumiana wenyewe kwa wenyewe, kila mmoja akimwambia mwen­zake: “Wewe ndiye sababu ya haya.” Miongoni mwao alikuwako mtu mwema aliyewapa nasaha kabla, lakini hawakumsikiliza, ndio akawaambia: Kwani sikuwaaambia, lakini mkakataa. Basi tubieni kwa Mola ili mpate kufaulu. Wakatubia kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na wakam­womba msamaha na kutaka wahurumiwe na kuneemeshwa kutoka shambani mwao.

Lengo la kupiga mfano huu, ni kupata funzo kila aliyeneemeshwa na Mwenyezi Mungu; hasa watu wa Makka akiwemo yule mshenzi. Wapokezi wa Hadith wanasema watu wa Makka walipatwa na kahati na njaa kwa vile walimkadhibisha Muhammad(s.a.w.w) , ndipo akawaombea majanga na Mwenyezi Mungu akaitikia maombi yake. Kahati iliendelea kiasi cha miaka saba mpaka wakawa wanakula mizoga na mifupa. Pia wapokezi wanasema Mwenyezi Mungu aliingamiza mali ya Walid.

Haya ndio makusudio ya Aya kwa ujumla wake. Ufuatao ni ufufanuzi wa Aya moja moja:-

Walipoapa kwamba watalivuna itakapokuwa asubuhi.

Wenye shamba waliapa kuwa watalivuna mafukara wakiwa hawana habari.

Wala hawakusema: Inshaallah!

Yaani hawakusema tutavuna asubuhi Mungu akipenda.

Tumefasiri wala hawakusema inshaallah! Kutokana na maneno ya kiarabu yastathnuua ambayo tafsiri yake ya moja kwa moja ni ‘hawakutenga au hawakutoa.’ Kwa hiyo baadhi ya wafasiri wakasema maana ni hawakutenga kitu kwa ajili ya masikini. Kila moja kati ya tafsiri mbili hizi inafaa. Vile vile zinaweza kwenda kwa pamoja.

Basi lilitokea tukio juu yake kutoka kwa Mola wako, nao wamelala! Likawa kama limefyekwa.

Wenye shamba walilala raha mustarehe wakiwa na imani ya kulivuna shamba lao asubuhi na mapema, lakini usiku huo likafikwa na janga.

Neno kufyekwa, tumelifasiri kutokana na neno Asswarim, ambalo maana yake nyingine ni weusi, kwa maana ya kuungua na kuwa jeusi kama usiku wa giza

Wakaitana asubuhi, ya kwamba raukeni kondeni mwenu ikiwa mnataka kuvuna.

Ilipofika asubuhi waliitana ili wawahi kwenda shamba bila ya masikini kujua.

Basi walikwenda na huku wakinong’onezana. Ya kuwa leo asiliingie hata masikini mmoja.

Walifanya haraka wakidhamiria kwa siri kuwa masikini asionje hata chembe ya mazao.

Hakuna mwenye shaka kuwa huu ni uchoyo. Ikiwa hawa shamba lilikuwa lao na mazao ni yao hawakuiba, lakini pamoja na hayo Mwenyezi Mungu aliwaghadhabikia na kuwaandalia adhabu; je, itakuwaje kwa yule aliyepituka mipaka kwenye maisha ya watu akawanyang’anya vyakula vyao, akawaua na kuwafukuza kwenye miji, kama wanavyofanya wakoloni hivi sasa katika mashariki ya dunia na magharibi yake?

Na walirauka, nao wana nguvu za kunyima.

Waliingia shambani mwao wakiwa na dhamira kabisa ya kuwanyima mafukara, wakiwa na mawazo kwamba shamba na mazao yake yako mikononi mwao. Hawakujua kuwa mkono wa Mwenyezi Mungu uko juu ya mikono yao.

Basi walipoliona, wakasema: Hakika tumepotea! Bali tumenyimwa!

Walipofika shamba yaliwashangaza waliyoyaona na wakakubali kuwa wamepotea na kusema: sisi ndio tuliokosa fadhila za Mwenyezi Mungu na thawabu zake, na tunastahili ghadhabu za Mwenyezi Mungu na adhabu yake na sio mafukara na masikini.

Miongoni mwao alikuwa mtu mwema aliyekuwa akiaamrisha mema na kuwakataza maovu, lakini hawakusikiliza nasaha zake. alipoona yaliyowafika:

Akasema Mbora wao: Je, Sikuwambia, kwa nini hamumsabi­hi Mwenyezi Mungu?

Yaani hamumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kauli wala kwa vitendo kwa kutoa. alisema hivi kwa kuwahurumia. Kisha akawaamuru kutubia:Wakasema: Ametakasika Mola wetu! Hakika tulikuwa madhalimu wa nafsi zetu kwa kumuasi Mwenyezi Mungu.

Basi wakakabiliana kulaumiana wao kwa wao.

Kila mmoja anamtupia lawama mwinziwe; kama ilivyo hali ya washiriki­na, wanapofikwa na yale yaliyofanywa na mikono yao.

Wakasema: Ole wetu! Tulikuwa tumeikiuka mipaka!

Walirudia akili zao na wakacha kulaumiana, wakakiri dhambi zao kwam­ba wao walikuwa katika upotevu, wakijiombea kufa kwa kusema ‘Ole wetu’ na kumwomba msamaha Mwenyezi Mungu, wakasema:Asaa Mola wetu akatubadilishia lilio bora kuliko hili. Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu.

Hii ni dua na matarajio yao kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) awasamehe yaliyopita na awabadilishie yaliyo bora kuliko yaliyopita. Na Mwenyezi Mungu anakubali toba kutoka kwa waja wake, anawasamehe mengi na anaitikia maombi ya anayemuomba kwa ukweli na ikhlasi.

Kama hivyo inakuwa adhabu, na bila ya shaka adhabu ya Akhera ni kubwa zaidi, laiti wangelijua!

Razi anasema hii iko wazi haihitaji tafsir, lakini sheikh Maraghi amekataa isipokuwa kuifasiri kwa kusema: “Yaani adhabu ya Akhera ni kali na inau­miza zaidi kuliko adhabu ya duniani.”

16

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّاتِ النَّعِيمِ ﴿٣٤﴾

34. Hakika wenye takua watakuwa na Bustani za neema kwa Mola wao.

أَفَنَجْعَلُ الْمُسْلِمِينَ كَالْمُجْرِمِينَ ﴿٣٥﴾

35. Kwani tutawafanya Waislamu kama wakosefu?

مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ ﴿٣٦﴾

36. Mna nini? Mnahukumu vipi?

أَمْ لَكُمْ كِتَابٌ فِيهِ تَدْرُسُونَ ﴿٣٧﴾

37. Au mnacho kitabu ambacho ndani yake mnasoma?

إِنَّ لَكُمْ فِيهِ لَمَا تَخَيَّرُونَ ﴿٣٨﴾

38. Kuwa mtapata humo mnayo yachagua?

أَمْ لَكُمْ أَيْمَانٌ عَلَيْنَا بَالِغَةٌ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ إِنَّ لَكُمْ لَمَا تَحْكُمُونَ ﴿٣٩﴾

39. Au mna viapo juu yetu vinavyofika Siku ya Kiyama ya kuwa mtapata mnayo­jihukumia?

سَلْهُمْ أَيُّهُم بِذَٰلِكَ زَعِيمٌ ﴿٤٠﴾

40. Waulize: Ni nani miongoni mwao mdhamini wa hayo?

أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ فَلْيَأْتُوا بِشُرَكَائِهِمْ إِن كَانُوا صَادِقِينَ ﴿٤١﴾

41. Au wanao washirika? Basi wawalete washirika wao waki­wa wanasema kweli.

يَوْمَ يُكْشَفُ عَن سَاقٍ وَيُدْعَوْنَ إِلَى السُّجُودِ فَلَا يَسْتَطِيعُونَ ﴿٤٢﴾

42. Siku utakapowekwa wazi muundi, na wataitwa kusu­judu, lakini hawataweza.

خَاشِعَةً أَبْصَارُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ وَقَدْ كَانُوا يُدْعَوْنَ إِلَى السُّجُودِ وَهُمْ سَالِمُونَ ﴿٤٣﴾

43. Macho yao yatanyenyekea fedheha itawafunika. Na hakika walikuwa wakiitwa wasujudu walipokuwa salama.

KWANI TUTAWAFANYA WAISLAMU KAMA WAKOSEFU?

Aya 34 – 43

MAANA

Hakika wenye takua watakuwa na Bustani za neema kwa Mola wao.

Katika Aya zilizotangulia Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwaahidi wakosefu adhabu kubwa, na katika Aya hii anawaahidi wanaomcha Mwenyezi Mungu kuwa na milki ya daima na neema ya kudumu. Namna hii Mwenyezi Mungu analinganisha mwisho wa wakosefu na wa wenye takua; kwa kuvutia na kuhadharisha.

Kwani tutawafanya Waislamu kama wakosefu? Mna nini? Mnahukumu vipi?

Makusudio ya waislamu hapa sio kila mwenye kusema: Lailaha ilallah muhammadur-rasulullah[ (Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu); bali makusudio ni wanaom­cha Mwenyezi Mungu. Kwa sababu mazungumzo hapa yanahusiana na wao na yale waliyo nayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu ya Pepo yenye neema.

Unaweza kuuliza : hatudhani kama kuna yeyote anayehukumu kuwa wenye takua wako sawa na wakosefu; sasa kuna haja gani ya Mwenyezi Mungu kusema: mnahukumu vipi?

Jibu : Ni kweli kuwa hakuna anayehukumu kuwa wakosefu na wenye takua wako sawa, lakini mara nyingi wakosefu wanajiona kuwa ni wacha Mungu na kwamba wao wanastahiki malipo na tahawabu wanazostahiki wenye takua.

Basi ndio Mwenyezi Mungu akalipinga hilo na kuwaambia, vipi mnajifanya mko sawa na wenye takua na kati yenu na wao kuna umbali wa mashriki na magharibi? Linalofahamisha maana haya kuwa ndio makusudio ni maswali haya yafuatayo:

Au mnacho kitabu ambacho ndani yake mnasoma? Kuwa mtapata humo mnayoyachagua?

Je, mna Kitabu kutoka mbinguni au ardhini mnachokisoma kwamba nyi­nyi duniani mtapata mnachokipenda na Akhera mpate mnachokitamani? Wasifu uko sawa na ule wa mayahudi na wanaswara: “Na Mayahudi na Manaswara wanasema: Sisi ni wana wa Mwenyezi Mungu na vipenzi vyake.” Juz. 6 (5:18).

Makusudio ya Aya tunayoifasiri ni ya vigogo wa kikuraishi. Ingawaje wao hawakudai kuwa na Kitabu, lakini lengo ni kuwanyamazisha, kwamba hakuna dalili wa mfano wa dalili kuwa wako sawa na wenye takua na kwamba wao watapata wanayoyataka.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 22 (35:30) na Juz. 25 (43:21)

Au mna viapo juu yetu vinavyofika Siku ya Kiyama ya kuwa mtapata mnayojihukumia?

Je, Mwenyezi Mungu amewaapia kiapo kizito na kuwapa ahadi msisitizo kuwa atawaingiza Peponi pamoja na wanaomcha Mungu? Kwamba hatabadilisha ahadi mpaka siku ya Kiyama?

Waulize: Ni nani miongoni mwao mdhamini wa hayo?

Yaani waulize wewe Muhammad! Ni nani aliyeahidiana nao kutekelezewa madai yao?

Au wanao washirika? Basi wawalete washirika wao wakiwa wanase­ma kweli.

Makusudio ya washirika hapa ni masanamu; kama alivyosema Mwenyezi Mungu: “Sema: nionyesheni wale mliowaunganisha naye kuwa washirika.” Juz. 22 (34:27).

Maana ni kuwa haya nawalete hao washrikina waungu wanaowaabudu ili washuhudie kwamba wao watapata Pepo pamoja na wenye takua.

Msawali yote aliyoyaelekeza Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa washirikina ni kuwa hakuna kitu kinachofahamisha kwa karibu wala mbali kwamba washirikina wana chochote. Aina hii ya hoja ni katika nyenzo nzuri sana ya kumnyamazisha hasimu, wakati huo ikielimisha na kuleta uhakika.

Siku utakapowekwa wazi muundi, na wataitwa kusujudu, lakini hawataweza.

Waarabu wanaiita siku ngumu na yenye shida kuwa siku ya kufunuka muundi. Ndio maana siku ya Kiyama imeitwa hivyo. hakuna atakayetaki­wa kusujudi siku hiyo wala kufanya ibada nyingineyo, kwa sababu hiyo ni siku ya hisabu na malipo sio siku ya taklifa na matendo. Kwa hiyo basi kutakiwa kusujudi ni kwa njia ya kutahayariza, sio kwa sharia na taklifa.

Kwa hiyo makusudio ya kutoweza kusujudi siku hiyo ni kwamba hakutawafaa kitu kwa sababu siku hiyo ni ya malipo sio ya kufanya amali. Maana ni kuwa wale ambao wamepituka mipaka au wakafanya uzembe duniani walipokuwa na uwezo wa kufanya, watatahayarizwa na kuadhibi­wa siku ya Kiyama ambayo hakuna hila wala njia ya kuwakurubisha kwa Mwenyezi Mungu.

Macho yao yatanyenyekea.

Kunyenyekea ni sifa ya moyo, lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu ameileta kwa kinaya cha udhalili wao na utwevu wao uliodhahiri machoni mwao. Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:fedheha itawafunika , ni tafsiri na ubainifu wa hilo.

Na hakika walikuwa dunianiwakiitwa wasujudu, lakini walikataa kwa kiburi.walipokuwa salama, bila ya kizuizi chochote. Baada ya kuiona adhabu sasa ndio wanataka kusujudi, lakini wakati umekwishapita.

فَذَرْنِي وَمَن يُكَذِّبُ بِهَـٰذَا الْحَدِيثِ سَنَسْتَدْرِجُهُم مِّنْ حَيْثُ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٤٤﴾

44. Basi niache na wanaokad­hibisha maneno haya! Tutawavuta kidogo kidogo kwa mahali wasipopajua.

وَأُمْلِي لَهُمْ إِنَّ كَيْدِي مَتِينٌ ﴿٤٥﴾

45. Na ninawapa muda; hakika hila zangu ni imara.

أَمْ تَسْأَلُهُمْ أَجْرًا فَهُم مِّن مَّغْرَمٍ مُّثْقَلُونَ ﴿٤٦﴾

46. Au wewe unawaomba ujira, kwa hiyo wanalemewa na gharama?

أَمْ عِندَهُمُ الْغَيْبُ فَهُمْ يَكْتُبُونَ ﴿٤٧﴾

47. Au wanayo ilimu ya ghaibu, nao wanaandika?

فَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ وَلَا تَكُن كَصَاحِبِ الْحُوتِ إِذْ نَادَىٰ وَهُوَ مَكْظُومٌ ﴿٤٨﴾

48. Basi ingojee hukumu ya Mola wako, wala usiwe kama sahibu wa samaki, aliponadi naye amezongwa.

لَّوْلَا أَن تَدَارَكَهُ نِعْمَةٌ مِّن رَّبِّهِ لَنُبِذَ بِالْعَرَاءِ وَهُوَ مَذْمُومٌ ﴿٤٩﴾

49. Kama isingelimfikia neema kutoka kwa Mola wake, bila ya shaka angeli tupwa ufuk­weni naye ni mwenye kulau­miwa.

فَاجْتَبَاهُ رَبُّهُ فَجَعَلَهُ مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿٥٠﴾

50. Lakini Mola wake alimteua na akamfanya miongoni mwa watu wema.

وَإِن يَكَادُ الَّذِينَ كَفَرُوا لَيُزْلِقُونَكَ بِأَبْصَارِهِمْ لَمَّا سَمِعُوا الذِّكْرَ وَيَقُولُونَ إِنَّهُ لَمَجْنُونٌ ﴿٥١﴾

51. Na waliokufuru hukaribia kukutelezesha kwa macho yao, wanaposikia mawaidha, na wanasema: Hakika yeye ni mwendawazimu.

وَمَا هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَالَمِينَ ﴿٥٢﴾

52. Na hayakuwa haya, ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote.

NIACHENI NA WANAOKADHIBISHA

Aya 44 - 52

MAANA

Basi niache na wanaokadhibisha maneno haya!

Wanaokadhibisha ni washirikina wa kiarabu. Maneno ni Qur’an. Neno ‘niache na’ ni lakutangaza vita nao kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kwam­ba Mwenyezi Mungu Yeye mwenyewe atatekeleza kuwaadhibu; apumue Nabii na wale walio pamoja naye kutokana nao na shari yao, kisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) akabainisha, vipi na kwa njia gani atawatesa pale aliposema:

Tutawavuta kidogo kidogo kwa mahali wasipopajua. Na ninawapa muda; hakika hila zangu ni imara.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anawapa muda wala hawafanyii haraka. Vile vile anawapa mali na watoto na kuwatoa kwenye hali nzuri hadi kwenye hali nzuri zaidi katika dhahiri ya maisha ya dunia, lakini wao kwa undani, wanagurishwa kutoka kwenye hali mbaya hadi kwenye hali mbaya zaidi; mpaka wakifikia kujiona kuwa wako katika ngome madhubuti, ndipo Mwenyezi Mungu huwapatiliza kwa mpatilizo wa mwenye nguvu mwenye uweza. Ili hilo liwe ni la kuumiza zaidi na kutia uchungu moyoni.

Mwenyezi Mungu amekuita huku kuvuta kidogo kidogo kuwa ni hila kwa sababu kunafanana na hila kwa dhahiri; vinginevyo ni kuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kutakata na hila na vitimbi. Vipi isiwe hivyo na hali hakimbilii kwake ila mwenye kushindwa, na Mwenyezi Mungu husema kukiambia kitu ‘kuwa kikawa.’ Zaidi ya haya lengo la kutajwa vitimbi ni asihadaike mtu na dunia ikimkabili na kumpa tabasamu. Anatakikana awe na hadhari na yanayojificha.

Au wewe unawaomba ujira, kwa hiyo wanalemewa na gharama? Au wanayo ilimu ya ghaibu, nao wanaandika?

Je, unawataka mali inayokuwa na uzito kwao kuitoa, au wamejua ilimu ya siri kwa hiyo wakafuta yale wanayotakiwa kuamini. Imetangulia kwa herufi zake katika Juz. 27 (40-41).

Basi ingojee hukumu ya Mola wako, wala usiwe kama sahibu wa samaki, aliponadi naye amezongwa.

Sahibu wa samaki ni Nabii Yunus ambaye alipata dhiki na watu wake na akawaacha kwa hasira. Umetangulia mfano wake katika Juz. 11 (10:97), Juz. 17 (21:87) na.Juz. 23 (37:140). Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemuusia Nabii wake mtukufu(s.a.w.w) kuwa na subira na adha ya watu wake, wala asifanye haraka, kama alivyofanya Yunus, aliyemezwa na samaki, akanadi akiwa tumboni mwa samaki:

أَن لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنتُ مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٨٧﴾

“Hapana Mola isipokuwa wewe, umetakasika. Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa madhalimu.” Juz. 17 (21:87).

Kama isingelimfikia neema kutoka kwa Mola wake, bila ya shaka angeli tupwa ufukweni naye ni mwenye kulaumiwa.

Yunus alimwomba Mola wake akiwa tumboni mwa samaki, akamwitikia dua yake kwa kumuhurumia, akatemwa na samaki akiwa si mwenye kulau­miwa. Lau si dua yake na kuhurumiwa na Mola wake angelikuwa katika wenye kulaumiwa; bali angelibakia tumboni mwa samaki hadi siku ya ufu­fuo. Ilivyo hasa nikuwa kulaumiwa hapa ni kwa sababu ya kuacha lilo bora sio kwa sababu ya dhambi na uasi.

Lakini Mola wake alimteua na akamfanya miongoni mwa watu wema.

Miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu kwa Yunus ni kwamba Yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu alimtoa tumboni mwa samaki, akiwa radhi naye, na akamrudisha kwa watu wake akiwa Nabii; kama alivyokuwa hapo mwanzo; wakanufaika naye na kwa mawaidha yake.

Lau angelibakia kati­ka tumbo la samaki hadi siku ya ufufuo, unabii wake usingelikuwa na athari yoyote. Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “akamfanya mion­goni mwa watu wema,” ni kuwa atamfufua kesho pamoja na manabii.

Na waliokufuru hukaribia kukutelezesha kwa macho yao, wana­posikia mawaidha

Maneno yanaelekezwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) . Maana ni kuwa washirikina wanaposikia Qur’an kutoka kwa Muhammad(s.a.w.w) wanamtazama kwa mtazamo wa kiuadui na chuki, na miguu ya Mtume(s.a.w.w) inakurubia kuteleza kutokana na mtazamo wao mkali kama mshale. Razi anasema: “Waarabu wanasema: Amenitazama kwa kwa mtazamo unaokaribia kuniangusha na kunila. Mshairi anasema: wakikutana macho huyazungusha, mtazamo wa nyoyo kuziangusha

Na wanasema: Hakika yeye ni mwendawazimu.

Walimtazama Mtume kwa mtazamo mkali, vile vile wakamtupia maneno makali, kama kusema kwao: Yeye ni mwendawazimu mwenyezi Mungu (s.w.t) amewarudi, mwanzo mwanzo mwa sura hii tuliyo nayo, kwa kuse­ma: “Kwa neema ya Mola wako wewe si mwendawazimu.”

Na hayakuwa haya, ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote.

Makusudio ya ukumbusho ni ukumbusho wa heri na mwongozo wa njia yake. Maana ni kuwa Qur’an ni wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu aliouteremsha kwa Muhammad(s.a.w.w) ili awaongoze watu wote, kila mahali na kila wakati.

MWISHO WA SURA YA SITINI NA NANE: SURAT AL- QALAM

9

HADITH ZA MTUME (s.a.w.w) NA MA-IMAMU (a.s)

KUSEMA UONGO

498. Anas Ibn Maliki Khisal-i-Sadduq, Uk. 321: Anaelezea kutoka Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema: "Chukueni mambo sita kutoka kwangu, na mimi nakubalia, na kutoa dhamana (Ya wewe kuingizwa Jannat)

1. Usiseme uongo

2.Unapo toa ahadi, usivunje

3. Unapo pewa amana na wengine, basi uwemuaminifu

4. Tazama chini ( usitende dhambi ).

5. Chunga heshima yako

6. Idhibiti mikono yako na ulimi wako.

499. Amesema Imam Al Hassan al-'Askari(a.s) : "Iwapo maovu yote yatawekwa katika nyunba moja, basi ufunguo ( wa milango yake ) itakuwa ni uongo ."[213] .

500. Amesema Al Imam Zaynul 'Abediin(a.s) : "Jiepusheni na kusema uongo hata kama ni uongo mgogo au mkubwa, kama kwa wadilifu au unasema kwa kdhihaki, kwasababu mtu anapo sema uongo mdogo basi anaweza kudiriki kusema uongo mkubwa pia.[214] .

501. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : Wakati mmoja Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . aliulizwa kuhusu umbali baina ya ukweli na uongo naye akiwa akionyesha umbali huo baina ya macho yake na maskio yake kwa vidole vinne katika kutoa jibu hilo, "Kile majo yako yanayooonani ukweli na mengi na yale yanayo sikilizwa na maskio yako ni sehemu kubwa ni uongo."[215] .

502. Amesema Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) : "Kwa hakika Allah swt ameyawekea maufuli maovu fulani, na ufunguo wake Allah swt ameweka katika pombe, lakinimaovu yatokanayo na kusema uongo ni zaidi hata kuliko pombe yenyewe ."[216]

503. Amesema Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) : "Muwe wasema ukweli na mujiepushe na usemaji uongo ."[217]

504. Amesema Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) : "Kwa hakika Allah swt ameya wekea maufuli maovu fulani, na ufunguo wake Allah swt ameweka katika pombe, lakinimaovu yatokanayo na kusema uongo ni zaidi hata kuliko pombe yenyewe ."[218] .

505. Amesema Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) : "Muwe wa sema ukweli na mujiepushe na usemaji uongo ."[219] .

MARAFIKI NA URAFIKI

506. Mtume Muhammad(s.a.w.w) Amesema: "Mtu anaathirika kwa imani ya marafiki zake. Kwa hivyo, muwe waangalifu kabisa katika urafiki wenu pamoja nao . " [220]

507. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) , Amesema: "Uwe rafiki wa yule ambaye atakuwa ndio heshima yako, si wewe uwe heshima yake. (Ufanye urafiki na wale walio juu yako ili wewe uweze kupata maendeleo kutokana na urafiki huo).[221] .

508. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . Amesema: "Ndugu yangu mpenzi ni yule (anayenitambulisha) makosa na kasoro zangu.[222]

509. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . Amesema: "Kwa hakika kuna marafiki wa aina tatu kwa ajili ya Muislam:

1. Rafiki anayesema mimi niko pamoja nawe iwapo upo hai au umekufa: Na hili ndio matendo yake.

2. Rafiki anayesema mimi nipo rafiki wako hadi ukingoni mwa kaburi na nitakuacha:hawa ni watoto wake.

3. Rafiki anayesema mimi nitakuwa nawe hadi pale utakapo kufa:hii ni mali ambayo ataiacha humu duniani kwa warithi wake baada ya kifo chake.[223]

Tanbih Kutokana na riwaya hii, na kama hizi sisi tunaelewa kuwa kitu ambacho kitakuwa pamoja na huyo mtu aliye kufa na kuaga dunia hii katika siku ya Qiyamah imani na matendo yake mema. Na suala hili limezungumziwa katika ahadithi nyingi sana za Kiislam na vile vile katika ayah za Qur'an tukufu, kwa mfano:

510. Allah swt anatuambia: Wale walio amini na wakatenda mema watakuwa na raha na marejeo mazuri. (Qur'an, 13:29).

511. Allah swt anatuambia: Hakika wale walio amini na wakatenda mema - hakika Sisi hatupotezi ujira wa anaye tenda mema. (Qur'an,18: 30).

512. Allah swt anatuambi: Hakika wale walio amini na wakatenda mema mashukio yao yatakuwa kwenye Pepo za Firdausi. (Qur'an, 18: 107).

513. Allah swt anatuambia:" Hakika walio amini na wakatenda mema Arrahmani Mwingi wa Rehema atawajaalia mapenzi. (Qur'an,19: 96).

514. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Muwe waangalifu katika kutafuta marafiki wa kweli na mujaribu kuwafanyia majaribio, kwa sababu wao watakuwa ndio msaada wenu pale mnapokuwa katika hali nzuri na watetezi wenu pale mtapokuwa katika shida na matatizo."[224]

515. Amesema Al Imam Zaynul 'Abediin(a.s) : "Kukutana pamoja na wacha Mungut kunawaleteeni mema ."[225]

516. Al Imam Zaynul 'Abediin(a.s) . Amesema: "Jitahadharisheni na urafiki wa watendao madhambi, na kuwasaidia madhalimu ."[226]

MARAFIKI WASIO WEMA

517. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Anayetafuta uhusiano na marafiki wa wale wanao wadhalilisha wapenzi wa Allah swt basi watambue kuwa wao wamemuasi Allah swt ."[227]

518. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . Amesema: "Mnapojulishwa kuhusu marafiki zenu wanapotenda maovu, nendeni mumwambie: Ewe fulani bin fulani ! Ama acha kutenda madhambi au ukae mbali nasi: Na hapo utengane naye hadi atakapo acha kutenda maovu.[228]

519. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amenakili kutoka baba yake Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) . ambaye Amesema kuwa baba yake Al Imam Hussein ibn Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . Amesema: "Ewe mwanangu! Jichunge na makundi matano na kamwe usifanye urafiki nao, wala usiongee nao na wala usifanye urafiki pamoja nao. Kwa hayo Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) . alimuuliza baba yake Je ni makundi gani hayo matano. Imam(a.s) . alimujibu: Jitahadharishe na wala usifanye urafiki pamoja na yule msema uongo kwa sababu yeye ni kama mazua mazua anaye kufanyia vitu vya mbali vikawa karibu, na anakifanya kiwe mbali kile ambacho kiko karibu nawe.[229]

Jihadhari na usifanye uhusiano pamoja na mtu ambaye hana tabia njema, kwa sababu atakuuza kwa thamani kwa tonge moja au hata chini ya hiyo. Jihadhari na wala usifanye uhusiano na bahili kwa sababu yeye atakunyima kutoka mali yake pale wewe utakapo hitaji hasa. Jihadhari na usifanye urafiki pamoja na mpumbavu, kwa sababu yeye atataka kukufaidisha wewe lakini kwa uhakika anakudhuru zaidi. Jihadhari na usifanye uhusiano pamoja na yule ambaye hawajali ndugu na maJama'a zake, kwa sababu mimi nimemona mtu kama huyo akilaaniwa katika kitabu cha Allah swt (yaani Qur'an Tukufu) katika sehemu tatu.

Nayo ni: Sura Al Baqarah, 2, Ayah ya 27; Wanao vunja ahadi ya Allah swt baada ya kwisha ifunga, na wakayakata aliyo amrisha Allah swt kuungwa, na wakafanya uharibifu katika nchi; hao ndio wenye Khasara. Sura Al-Raa'd, 13, ayah ya 25 Na wale wano vunja ahadi ya Allah swt baada ya kuzifunga, na wanakata aliy amrisha Allah swt yaungwe, na wanafanya fisadi katika nchi: Hao ndio watakao pata laana, na watapata Nyumba mbaya. Sura Muh'ammad, 47, ayah 22 Basi yanayo tarajiwa kwenu mkitawala ndio mfisidi katika nchi na mwatupe Jama'a zenu ?

520. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Ewe Kumail ! sema kile kilichopo katika hali yoyote ile. Uwe marafiki pamoja na wacha Allah swt na jiepushe na watendao maovu, jiweke mbali na wanafiki na usiwe pamoja na wadanganyifu na wahalifu na wahaini ."[230]

KUWAHUDUMIA WATU

521. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) : "Yeyote yule atakaye mpuuzia ndugu yake Muislam mwenzake matatizo na shida za dunia hizi, basi Allah swt atampunguzia shida na matatizo yake huko Akhera ." [231]

522. Amesema Al Imam Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Kwa hakika, maombi ya shida za watu zinazokuijia wewe ni miongoni mwa neema na baraka za Allah swt juu yako. Hivyo usisikitike kwa sababu ya neema na baraka hizi ."[232]

523. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Popote pale utakapoona ndugu yako Muislam ana shida, jaribu kuangalia kama utaweza kumusaidia. (Usimpuuze mpaka akutamkie shida zake.) "[233]

524. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . kuwa amenakili kutoka mababu zake(a.s) . ambao wamemnakili Mtume Muhammad(s.a.w.w) akisema: "Yeyote yule anayemlisha muumin aliye na njaa akashiba basi Allah swt atamlisha mpaka ashibe kutoka matunda ya Jannah; Na yeyote yule atakaye mvisha nguo yule aliye na shida za nguo, Allah swt atamvisha nguo zilizofumwa na za hariri, na yeyote yule atakaye mumalizia kiu muumin basi Allah swt atamjaalia kinywaji kilichopigwa lakiri; Na yeyote atakaye msaidia muumin kupunguza shida yake, basi Allah swt atamweka chini ya Arshi yake siku ya Qiyama siku ambayo hakutakuwa na kivuli chochote isipokuwa kivuli cha Arshi yake."[234]

525. Mtume Muhammad(s.a.w.w) Amesema: "Watu wanamtegemea Allah swt kwa ajili ya riziki, kwa hiyo mpenzi miongoni mwa watu kwake Allah swt ni yule ambaye anawasaidia wale watu wanaomtegemea Allah swt na kuwafanya watu wa familia ya nyumbani wakawa na furaha."[235] .

526. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) : "Yeyote yule atakaye wasaidia Waislam ndugu zake wakati wa shida, Allah swt atamwondolea shida na matatizo sabini na tatu, moja ambayo ni ambayo iko humu duniani na sabini na mbili zingine zitakazo kuwa wakati wa shida kubwa, ambapo watu watakuwa mashughuli katika mambo yao ya binafsi (katika Akhera) ." [236]

KUTOA MIKOPO

527. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) : "Yeyote yule anayeijiwa na ndugu yake Muislam kwa ajili ya kukopa na kama yeye hampi mkopo, basi Allah swt atamharamishia kuingia Jannat siku ambayo waja mema watakuwa wakilipwa na kufidiwa ." [237]

528. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) : "Yeyote yule anayetakiwa na ndugu yake Muislam kwa kukopeshwa na kama yeye hamkopeshi mkopo, Allah swt atamzuia kuingia Jannat siku ambayo waja wema watakuwa wakilipwa mema yao ." [238]

KUWASAIDIA WENYE SHIDA

529. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) : "Waulizeni maswali walio elimika, muongee pamoja na wale wenye hekima, na mujihusishe pamoja na masikini."[239]

530. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Sababu mojawapo ya kuteketea na kupotea kwa mali na utajiri wa mtu ni kule kutowajali na kutowasaidia wale wenye shida."[240]

531. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Mtume Muhammad (s.a.w.w) amemnakili Allah swt kwa kuameambiwa usiku wa Mi'raj: Ewe Ahamad! Mapenzi yangu ni kule kuwapenda masikini. Wafanye masikini wawe karibu nawe na uwaweke karibu nawe ili mimi niweze kukufikia wewe .."[241]

532. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Yeyote yule anayemmalizia muumin njaa yake kiasi kwamba akaridhika kikamilifu, basi hakuna binadamu yeyote miongoni mwetu au miongoni mwa Malaika wanaojua kiasi cha thawabu yake siku ya Qiyamah isipokuwa Allah swt mmiliki wa Malimwengu yote. Na aliongezea: Kumlisha Muislam aliye na njaa ni njia moja kubwa sana ya kuomba Tawba( usamehevu)."[242]

Baada ya hapo alisoma ayah ya Qur'an Tukufu Sura Al-Balad, 90, ayah 14 - 16. Au kumlisha siku ya njaa Yatima aliye Jama'a, Au masikini aliye vumbini.

ZAWADI NA KUWAFURAHISHA MUUMIN

533. Mtume Muhammad(s.a.w.w) Amesema: "Wakati sadaka inapotolewa na mtu kutoka mikononi mwake, basi hiyo sadaka inasema: Mimi nilikuwa kitu cha kwisha, lakini wewe umenipa maisha; Mimi nilikuwa sina thamani sasa wewe umenifanya niwe na thamani kubwa; mimi nilikuwa ni adui nawe umenifanya mie kuwa rafiki; Wewe ulikuwa daima ukinilinda na kunihifadhi lakini sasa mimi nitakulinda na kukuhifadhi hadi siku ya Qiyamah ." [243]

534. Amesema Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) : "Yeyote yule atakaye mfurahisha Muumin, basi kwa hakika kwanza kabisa amemfurahisha Allah swt, na pili amemfurahisha Mtume Muhammad (s.a.w.w) na tatu ametufurahisha sisi Ahlul Bayt (a.s) "[244]

535. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Allah swt ameweka mahitaji ya wale wasio na uwezo katika mali ya matajiri. Kwa hivyo atakapokuwa mtu asiye na uwezo akabakia katika hali ya njaa basi ni kwa sababu matajiri wamemnyima haki yake ."[245] .

536. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . Amesema: "Kwa kiapo cha Allah swt! Yeyote yule anayeizuia mali yake isiwasaidie Mumin wenye shida basi siku ya Qiyamah kamwe hawataonja chakula cha Jannat wala Kinywaji kilichopigwa Lakiri."[246]

SADAKA NA MISAADA

537. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Sadaka inalipia madeni na inaongezea katika barakah ."

538. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amenakili riwayah kutoka Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kuwa: "Sadaka inamwepusha mtu na ajali mbaya ."

539. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . anasema kuwa: "Mtu yeyote yule aliye mja wa Allah swt akiwa Mumin akatoa Sadaka, basi Allah swt baada ya kifo chake huyo mtu huwaweka vyema na kuwasaidia wananyumba yake katika hali njema." Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akaendelea kusema: "Faida ya kutoa Sadaka ni kwamba inamsaidia kulipia madeni na viile vile kuongezea katika barak a."

540. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Kusaidia na kutoa sadaka vyote hivyo vinaondoa umasikini na hurefusha umri wa mtu. Na yule anayetoa huweza kuepukana na aina sabini za ajali mbaya .

541. Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) . katika kuelezea tafsiri ya aya, ya Qur'an Tukufu, Sura Al-Layl, 92, Ayah ya 5 na 6: Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali Ama mwenye kutoa na akamcha Mungu. Ndipo amesema kuwa; Allah swt ndivyo anavyo walipa wale watendao mema, kwa mema yao mara kumi, au hata mara laki moja na hata zaidi ya hapo. Na vile vile amesema kuwa: anayetoa katika njia ya Allah swt basi Allah swt humjaalia kila aina ya tawfiqi katika kazi hiyo ya khairi."

542. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amemnakili Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kuwa "Mtu yeyote yule ambaye anamwamimi Allah swt kuwa atamlipa na atamwongezea zaidi ya kile anacho kitoa basi huyo mtu kwa moyo mkunjufu na bila aina ya ubakhili wowote atatoa sadaka na misaada kwa wingi kabisa."

543. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amemnakili Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kuwa: "Siku ya Qiyama ardhi itakuwa imepata moto kupita kiasi na mumin watakuwa katika kivuli na kivuli hicho itakuwa ni kile alicho kuwa akitoa Sadaka ."

544. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amenakili riwayah moja kutoka Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akisema kuwa: "Enyi watu! Toeni sadaka bila shaka sadaka inaongezea katika mali yenu, na hivyo mtoe sadaka na Allah swt atawarehemu ."

545. Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) . amesema kuwa: "Toeni sadaka mjipatie riziki ."

546. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Toeni sadaka mjiongezee riziki yenu. Bila shaka anayeamini kuwa Allah swt hulipa mambo yote. Basi yeye huwapa sadaka masikini kwa kupita kiasi. Allah swt humjaalia riziki kwa njia mbalimbali kwa kile huyu mtu akitoacho katika mali yake ."

547. Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) . amenakili riwayah kutoka Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akisema kuwa: "Kuwa na akida ya Tawhid ni nusu ya sehemu ya dini, enyi watu! Toeni Sadaka ili mpate riziki zaidi ".

548. Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) . ametoa riwayah kutoka Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kuwa: "Kuwa mali halisi ya mtu ni ile ambayo yeye ametolea sadaka ."

549. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema kuwa: "Toeni Sadaka asubuhi na mapema ili balaa zisiwafikieni katika siku nzima ."

550. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amenakili riwayah kutoka Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . kuwa: "Sadaka ni kinga dhidi ya moto wa Jahannam ."

551. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alikuwa akisema: "Enyi watu muwatibu wagonjwa wenu kwa kutoa Sadaka ."

552. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . katika Nahjul Balagha amesema kuwa: "Mnapoona riziki yenu inapungua na kuwa finyo basi muwe mkitoa sadaka ndivyo mtakuwa mkifanya biashara na Allah swt ."

553. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Imani ya muumini inakuwa na sifa nne za lazima, "Awe na tabia njema, "Awe mkarimu na mwepesi wa kutoa "Asizungumze zaidi ya yale yanayo takikana (hazungumzi mambo ovyo ovyo) " Hutumia kile kiasi kinacho takiwa ,siyo mfujaji (anaotoa katika njia ya Allah swt ).

554. Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) . amesema kuwa: "Iwapo mimi nitakwenda Hijja moja basi afadhali niwafanye huru watumwa kumi, lakini iwapo mimi nitajichukulia jukumu la kuwalisha familia ya Waislamu ambao wanashida ya chakula na ambao wanaishi kwa njaa nikawamalizia shida zao, nikawavalisha nguo wale ambao hawana nguo, na nikawarudishia heshima yao miongoni mwa watu, basi mimi ninaona jambo hili ni afadhali na bora zaidi kuliko hata kwenda kuhiji Hijja sabini. "

555. Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) . aliijiwa na mtu mmoja na aliyeuliza, "Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w)! Mimi ninazo pesa na utajiri je ni jambo gani afadhali nitoe sadaka au nimnunue mtumwa na kumfanya huru ?"

556. Kwa hayo Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) . alimjibu kuwa: "Kuwa mimi ninaonelea kuwa kutoa Sadaka ni afadhali zaidi."

557. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Siku moja Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimwuliza Maimuna binti Harun, Je Kijakazi wako amekuwaje? Akasema Maimuna kwa hayo alimjibu Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , 'Ewe Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ! Mimi nimemfanya huru.' Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimwambia "Iwapo kama wewe ungelichukua jukumu la kumlisha, kumtunza, kumsaidia na kumwonea huruma basi ingekuwa afadhali zaidi."

558. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Muwatibu wagonjwa wenu kwa Sadaka, na muzuie maafa kwa kuomba dua na kutoa sadaka muongezee riziki zenu zipanuke, na kwamba Sadaka inawaepusheni na mitego ya mashetani sabini ."

559. Siku moja walikuja wagonjwa wakilalamikia magonjwa yao mbele ya Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) ., naye akawaambia; "Nendeni mtoe Sadaka kwa ajili ya magonjwa yenu na mtapona, iwapo mtu atatoa Sadaka kwa kile akitumiacho kwa siku dharura wake, basi Allah swt huahirisha hata kifo chake na vile vile humwepusha na ajali mbaya ."

560. Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) . aliulizwa na Sahaba mmoja: "Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ! Mimi watoto wangu wawili wamefariki na amebakia mtoto wangu mdogo." Kwa hayo Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) . kamwambia: "Basi toa Sadaka kwa niaba ya mtoto wako huyo." Na siku moja Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) . alipomtembelea huyo mtu akamwambia, "Mwambie mtoto wako huyo atoe Sadaka kwa mkono wake walau kiasi kidogo chochote kile au hata kama kitakuwa ni kipande kidogo tu. Utambue wazi kuwa kiasi chochote kile hata kikiwa kiasi gani kama kitatolewa kwa roho safi basi mbele ya Allah huwa ni kipenzi, kwani Allah swt ameelezea kuwa: Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona! Na anaye tenda chembe ya uovu atauona! (Qur'an,99: 7 – 8).

561. Vile viel Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) . alimwelezea kuwa: "Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu, Surah Al-Balad,90, Ayah11 - 16 Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani. Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani? Kumkomboa mtumwa; Au kumlisha siku ya njaa Yatima aliye jamaa, Au masikini aliye vumbini

"Hivyo ewe Sahabi uelewe kuwa Allah swt anaelewa wazi wazi kuwa si watu wote wenye uwezo wa kuwanunua na wenye kufanya huru watumwa hivyo yeye ameweka thawabu hizo hizo kwa wale watakao toa Sadaka au watakao walisha yatima na masikini."

562. Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) . alijiwa mtu mmoja mbele yake na kuelezea habari za mtoto wake, na kwa hayo Al Imam akamjibu: "Toa Sadaka kwa niaba yake." Na mtu huyo akajibu kuwa "Sasa mtoto wake amekuwa na umri yaani amekuwa kijana." Basi Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) . alimwambia kuwa "Mtoto wako atoe Sadaka kwa mkono wake, hata kama itakuwa ni kipande cha mkate, na hapo ndipo Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) . alisema riwayah ya Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) . kuwa: "Katika Israil alikuwa mtu mmoja aliyekuwa akimpenda mno mtoto wake, na akaona katika ndoto yake anaanmbiwa kuwa, mtoto wako huyo umpendaye mno atakufa usiku wa ndoa yake. Kulipowadia usiku wa arusi baba mzazi wa mtoto huyo, usiku kucha akawa katika wasiwasi na hakupata usingizi na kamwe hakupata raha usiku huo. Na kulipo pambazuka asubuhi na mtoto alipotoka chumbani mwake akiwa hai basi baba yeke alimwuliza 'Ewe mwanangu! Je katika usiku huu wako wa kuamukia leo umefanya mema yoyote?' Kwa hayo mtoto akajibu "Ewe baba yangu! hakuna jambo la maana sana lililotendeka, bali alitokezea masikini mmoja akaja mlangoni kuomba chakula, alikuwa na njaa na kile chakula walichokuwa wameniwekea, mimi nikampa chakula chote huyo mtu aliyekuja kuomba.' Kwa hayo baba yake akasema "Kwa sababu hii tu ndiyo Allah swt amekuondoshea balaa kubwa iliyokuwa ikupate wewe usiku huo."

563. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . anasema kuwa: "Kwa kutoa Sadaka kwa mkono wako mwenyewe basi unajiepusha na ajali mbaya, unajiepusha na balaa na maafa sabini na mitego ya mashetani sabini na ambamo kila shetani yuko anakwambia 'ewe fulani! Usitoe Sadaka kamwe."

564. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Mgonjwa atoe Sadaka kwa mkono wake mwenyewe na anayempa amwambie amwombee dua ".

565. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) katika hadith zake amesema kuwa: "Mkono uliye juu yaani mtoaji ni afahali kuliko mkono ule ulio chini yake, yaani mpokeaji ."

566. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema kuwa: "Kuna aina tatu ya mikono wa " kwanza ni mkono ule wa Allah swt ambao uko juu kabisa na kwa hakika neema zote ni za Allah swt, " mkono wa pili ni ule mkono wa yule mtu anaye toa, ambaye anatoa katika njia ya Allah swt na " mkono wa tatu ni wa yule anaye pokea ambao mkono uliochini wa yule anayetoa. Kwa hivyo enyi watu chochote kile kinachobakia miongoni mwenu mtoe katika njia ya Allah swt na musikalifishe nafisi zenu".

567. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alikuwa amemfanyia usia Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) ; Ewe Ali! Ninakufanyia usia wa mambo mema machache na uyakumbuke vyema.

Ewe Allah swt umsaidie Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . Baada ya hapo wakati akifanya usia, Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alisema: Ama kuhusiana na sadaka tafadhali usiwe na mnunguniko wowote. Utoe kiasi kwamba mpaka uhisi kwamba wewe umefuja mali yako, lakini utambue wazi kuwa hiyo sio ufujaji bali hiyo umetoa katika njia ya Allah swt."

568. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . anasema kuwa kuna riwayah kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kuwa "Toeni Sadaka, angalau hata kwa sa' ya tende, na kama sa' moja hiyo hamnayo basi mtoe tende kwa kiganja kimoja na hata kama hivyo haitawezekana basi mtoe tende kiasi chochote kile na kama hivyo haitawezekana basi mtoe angalau kokwa moja ya tende, na kama hivyo pia haitawezekana basi yule masikini aliyekuja kuwaomba mumwambie maneno mazuri na matamu na maneno matakatifu katika kumwelezea kuwa hakuna chochote, na hayo pia ni sadaka. Kwa sababu isitokee Siku ya Qiyama kwamba Allah swt atakapo kuuliza hesabu ya neema alizokujaalia akakuambia 'Ewe mja! Mimi nilikupa mambo chungu nzima, sasa hebu angalia nafsini mwako je kwa kutumia neema hizo wewe umejiandalia nini?' Na hapo wewe utaangalia sehemu zote nne za dunia na utajawa na masikitiko, na utakuta hakuna jambo lolote lile litakalo kuokoa dhidi ya adhabu za Allah swt."

569. Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) . amesema kuwa: "Mtoe tende kiasi fulani kwani itawaokoa na moto wa Jahannam , mpanue riziki zenu na mteremshiwe riziki nyingi kwa kutoa Sadaka na kupitia dua mziondoe balaa na shida zenu." Mkumbuke kuwa kwa kutoa Sadaka hamtapungukiwa katika mali yenu. Na miongoni mwa jamaa zenu wanapokuwa na shida muwasaidiapo hiyo siyo Sadaka bali hiyo ni wajibu wenu."

570. Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) . amesema kuwa: "Kulikuwa na mja mmoja aliyekuwa akifanya ibada ya Allah swt kwa umri wake wa miaka themanini. Siku moja alimwona mwanamuke mmoja mzuri aliyekuwa akipendeza naye akawa ameingia katika mtego wake. Yeye alitimiza matamanio yake visivyo halali na mara akatokezea Malakul mauti (malaika anayetoa roho). Ulimi wake ulifunga kuongea na jasho lilianza kumtoka na kutokwa kwa roho na mara hapo alipita masikini akiomba. Basi mtu huyu ambaye alikuwa katika hali ya kukata roho alimwambia yule masikini kwa ishara kuwa mahala fulani kuna mkate hivyo auchukue hivyo aweze kula huyo masikini, na masikini huyo alivyoelekezwa akauchukua mkate akaondoka zake. Kwa hiyo ikatokea kwamba Allah swt aliibatilisha ibada zake za miaka themanini kwa sababu ya kuzini na ikatokea kwamba Allah swt akamsamehe madhambi yake yote kwa sababu ya kutoa Sadaka kwa moyo mkunjufu."

571. Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) . amesema kuwa; " Katika zama za Bani Israil kuliwahi kutokea baa la njaa ambao uliendelea kwa muda wa miaka mingi. Katika wakati huo ikatokezea kwamba bibi kizee mmoja akiwa amekabwa na njaa hali ya juu alikuwa ameketi akiwa na kipande kidogo cha mkate huku akitaka kukila kipande hicho, mara akasikia mlangoni sauti ikisema ya masikini aliyekuwa amekuja kuomba: 'Ewe mja wa Allah swt! Mimi nakufa kwa njaa naomba unisaidie, bibi kizee huyo akajiambia kwa hakika Sadaka ndiyo wakati huu muafaka wa kutoa, na kile alichokuwa akila akakitoa haraka akampa huyo aliyekuwa akiomba.

Bibi kizee huyo alikuwa na mtoto mmoja aliyekuwa amekwenda porini na ghafla kule alishambuliwa na mnyama. Kwa kusikia sauti ya mtoto wake huyo bibi kizee ikimwita, alikimbia kumfukuza mnyama huyo na kwa muujiza wa Allah swt ni kwamba, Allah swt alimtuma Malaika Jibrail(a.s) kwenda kumwokoa mtoto huyo katika mdomo na mabano ya mnyama wa huyo muuwaji, na Malaika Jibraili(a.s) . akamwambia 'Ewe bibi kizee! Je umefurahi sasa? Kwa kile ulichokitoa sadaka basi Allah swt naye amekulipa mema yake."

572. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema kuwa: " Mfanye mema katika hali ya shida na ufakiri, na wema huo ni Sadaka. Toeni Sadaka kama itakuwa ni kiasi gani kwa udogo wake. Mnaweza kutoa kiasi cha tende mkajiokoa na Jahannam. Kwa hakika udogo huo siyo hoja na Allah swt ataulea udogo huo kama kwamba nyie mnavyo walea watoto wadogo wanaonyonya maziwa, na siku ya Qiyama wakati mema yenu hayo (mliyokuwa mkisema ni madogo) yatakapoletwa mbele yenu mtaona kuwa ni sawasawa na ukubwa wa milima mikubwa sana."

573. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . ameseama kuwa Allah swt anasema kuwa : "Hakuna kitu kingine mbali na Sadaka ambacho mtu anaweza kumpatia mtu mwingine kidhahiri, na kwa hakika mimi ndiye wakili wake musitahiki, na mimi ninayepokea kwa mikono Sadaka hiyo halafu hata ikiwa kama ni tende kidogo haidhuru mimi ndiye ninaitunza, kama vile mwanadamu anavyowatunza watoto wake.

Siku ya Qiyama huyo mtoa Sadaka atastaajabishwa mno kwa Sadaka zake ndogo alizokuwa akitoa zimekuwa kubwa kama milima ya Uhud, milima mikubwa sana."

574. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amenakili riwayah kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kuwa: "Toeni Sadaka asubuhi na mapema kwa sababu kunaondoa balaa kwa siku nzima ."

575. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Kwa kutoa Sadaka asubuhi na mapema basi mtoa Sadaka huepukana na kila aina ya matatizo na mabaya yote kwa siku nzima ."

576. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Toeni Sadaka asubuhi, na kwa mapenzi kabisa, mwenyewe kutoa Sadaka amebahatika. Basi humwomba Allah swt amani kutokana na balaa zote zilizoko ardhini na mbinguni, na kwa hakika Allah swt humjaalia hivyo kwa sababu ya kutoa Sadaka ."

577. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . anaelezea kuwa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w) alimwusia Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . kuwa: "Ewe Al Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s).! Sadaka huondoa balaa ambazo lazima zitatokezea, na kwa kutenda mema pamoja na ndugu na majamaa kunarefusha umri .

Ya Ali! Iwapo jamaa na ndugu ni watu wenye shida, basi kuwapa Sadaka hao haitakuwa ni Sadaka. Ya Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) .!Kusema maneno bila vitendo ni ya bure hayana maana, na Sadaka bila kuwa na nia nayo haiwi Sadaka ."

578. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . anasema kuwa: Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimwuliza mtu mmoja "Je leo umefunga Saumu?" Mtu huyo alijibu "La hapana! Ewe Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) " Tena Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimwuliza: "Je leo umeshawahi kumtembelea aliye mgonjwa?" Naye akajibu: "Hapana! Ewe Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) " Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) aliendelea kumwuliza naye aliendelea kumjibu hapana hakufanya hivyo.

579. Mwishoni Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) aliendelea kumwuliza: "Je umemlisha masikini yeyote?" Naye akajibu: "Hapana Ewe Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) !" Na hapo ndipo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alipomwambia huyo mtu: "Nenda kwa wananyumba wako, nenda ukawatendee na uwe nao kwa mema na uwawie wema, basi hayo ndiyo yatakuwa Sadaka yako kwao."

580. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . ameripoti riwayah kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ambaye ameseama: "kwa baraka za Sadaka Allah swt humwondolea mwenye kutoa Sadaka balaa sabini, ambamo kuna magonjwa, madhara yatokanayo na moto, kuzama maji, kufunikwa na majumba mpaka kufa na atamwepusha ili asiwehuke au asiwe mwehu."

581. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . ameripoti riwayah kutoka Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . kuwa: "Ili kutaka kuepukana na shari za madhalimu basi toeni Sadaka ."

582. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . anaelezea kuwa: Siku moja Myaudi mmoja likuwa akienda kukata miti porini na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimwangalia na kuwaambia Ma-Sahaba wake : "Myahudi huyu leo ataumwa na nyoka na kifo chake kitasababishwa na sumu ya nyoka. Myahudi huyo kama kawaida yake alikata kuni na alijitwisha kichwani mwake na akarud akiwa salama. Na tena Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alipomwona Myahudi huyo akamwambia ateremshe mzigo wa kuni huo na auweke chini. Na Myahudi akafanya hivyo alivyoambiwa, na katika mzigo huo wa kuni wakaona kuna nyoka mweusi mwenye sumu kali sana huku akiuma kuni. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimwuliza Myahudi yule,'Je wewe leo umefanya jambo gani?' Myaudi huyo akasema: Mimi nimekata kuni na kuzifunga tu, lakini wakati nilivyokuwa nikirudi nilibakiwa na vipande viwili vya mkate na kipande kimoja mimi nikala na kipande kimoja nikampa masikini Sadaka. Hapo ndipo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akasema kwa kiapo cha Allah swt ni kwa sababu ya Sadaka ndiko balaa hii imekuondokea, kwa hakika Sadaka humwepusha mtu na ajali mbaya."

583. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . siku moja alikuwa pamoja na Ma-sahaba wake katika Masjid Nabawi, na upande mmoja wa ukuta ukaanguka chini. Kulikuwa na mtu mmoja hapo ambaye aliponea chupu chupu tu, kulianguka kizingiti kizito karibu na muguu wake. Lakini yeye bahati nzuri hakupata udhuru wowote. Hapo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . aliwaambia Ma-sahaba wake, hebu mwulizeni huyu mtu leo amefanya matendo gani? Na wakati alipoulizwa huyo mtu akasema: "Mimi nilipotoka nyumbani mwangu leo nilikuwa na kokwa chache za tende. Na kukatokezea na masikini mmoja akaniomba basi mimi nikampa kama Sadaka Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . akajibu "Basi kwa sababu hiyo tu leo, Allah swt amekuepusha na balaa hii ambayo ingekumaliza."

584. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . siku mmoja alimwambia Sahabi wake Mayassari kuwa: "Ewe Mayassari je wajua kuwa wewe umeisha fikiwa na mauti mara nyingi, lakini Allah swt amekuongezea umri wako zaidi kwa sababu ya wewe kuwa mkarimu na kuwajali jamaa na ndugu zako umewawia wema ndio maanake umri wako umezidi."

585. Al Imam Hasan al-'Askary(a.s) . anasema kuwa: " Wakati mmoja Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akiwa pamoja na wenzake walikuwa safari na wenzake hao walikuwa na mali nyingi sana. Na njiani wakapata habari kuwa wako majambazi wanaowapora matajiri mali zao. Kwa kusikia hayo hao matajiri walianza kutetemeka na wakaingiwa na hofu na wakaanza kumwuuliza Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . je tufanyeje sasa? Na kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akawajibu: 'Mkabidhini mali yenu yule ambaye ataweza kuifadhi mali yenu, na kwa kweli ataitunza sana na baada la kupungua hata itazidi pia, sio hayo tu na pale mutakapokuingiwa na shida ya mali yenu basi yeye kila siku atawarudishia pamoja na nyongeza yake. ' Kwa kusikia hayo hao wenzake aliokuwa nao katika safari wakamwuliza : "Je ni nani huyo?" Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akawajibu: "Yeye ni miliki wa malimwengu zote Allah swt." Basi hao wenzake wakamwuliza je tunaweza kumkabidhi vipi mali zetu hizi? Hapo Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akawaambia: Toeni Sadaka muwape wale wanaostahiki. Kwa kusikia hayo wakauliza ewe mjukuu wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ! Hapa tulipo tutawatoa wapi hawa masikini na mafakiri tutawatafuta wapi? Basi Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . aliwajibu: munuie kuwa sehemu moja ya mali yenu mtatoa Sadaka basi na msiwe na wasiwasi Allah swt atailinda mali yenu yote.

"Wale waliokuwa naye pamoja safarini walinuia hivyo kama vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . alivyowaambi,a na Imam(a.s) . akawaambia sasa nyie mko katika amani ya Allah swt, na wakiwa wanaendelea na safari majambazi hao walikumbana nao na kwa kudura za Allah swt wao wakawapita salama usalimini bila ya kudhurika na kusumbuliwa, hadi wakafika mwisho wa safari yao. Waliopofika tu mwisho wa safari yao wao wakatoa sehemu moja walizokuwa wamenuia kama Sadaka na sehemu iliyo bakia walifanyia biashara yao, na Allah swt akawajaalia baraka kiasi kwamba wakapata faida hata zaidi ya mara kumi."

586. Siku moja Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . alikuwa Mina pamoja na Ma-sahaba wake wakila zabibu. Mara akatokezea mtu mmoja na akaomba. Basi Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . kwa mkono wake akachukua fungu moja la zabibu akampa basi huyo akakataa kupokea, akisema "mimi sitaki zabibu hizi bali ninataka pesa tasilimu kama zipo ndio nichukue". Basi kwa kusikia hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akamwambia "Allah swt atakuzidishia" na Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . hakumpa chochote, baada ya muda si muda huyo mwombaji tena akarudi kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . na akamwambia Imam(a.s) . "Nipe zile zabibu ulizokuwa ukitaka kunipa." Na Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akamwambia Allah swt atakutafutia njia yake, pamoja na hayo Imam(a.s) . hakumpa chochote.

Wakati bado wakiwa wamekaa akatokezea mtu mwingine kuja kuomba, na Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . alitoa mbegu tatu tu za zabibu akampa huyo mwombaji. Mwombaji huyo alianza kumshukuru Allah swt kwa kumjaalia riziki hiyo na akaonyesha shukurani kwa ujumla. Kwa kusikia hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . alichota mikono ya zabibu miwili akampa na hapo tena huyo mwombaji akaendelea kumshukuru Allah swt zaidi na zaidi. Kwa kusikia hayo tena Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akamwambia mtumwa wake kama tuna pesa zozote zile tulizo nazo kwetu mpe huyo. Na huyo mfanyakazi wa Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . kwa amri yake alimpa Dirham Ishirini alizokuwa nazo. Mwombaji akiwa anachukua Dirham akasema: 'Ewe Allah swt! Nakushukuru mno sana na hakuna mwingine wa kushirkishwa nawe. Kwa kusikia hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . nguo aliyokuwa amejifunika akampa huyo mwombaji na huyo mwombaji baada ya kuivaa na kujifunika na hiyo nguo akamshukuru Allah swt ambaye amemjaalia nguo ya kujifunika. 'Ewe Aba 'Abdillah! Allah swt akulipe kila la heri. Na baada ya kusema hayo akaondoka zake. Kwa kuona haya Ma-sahaba wakamwambia Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . kuwa kila alivyoendelea yeye kumsifu Allah swt ndivyo wewe ulivyoendelea kumpa na kama asinge omba kwa kutaja jina la Al Imam(a.s) . lazima angeendelea kumpa chochote zaidi ya hayo."

7

8

9

10

11

12

13

14

15

16