NAHJUL-BALAGHAH
JUZUU YA KWANZA
1. NA KATIKA KHUTBA ZAKE
Ndani ya khutba hii anaelezea kuumbwa kwa ardhi, mbingu, na kuumbwa kwa Adam
الحَمْدُ للهِ الَّذَي لاَ يَبْلُغُ مِدْحَتَهُ القَائِلُونَ، وَلاِ يُحْصِي نَعْمَاءَهُ العَادُّونَ، ولاَ يُؤَدِّي حَقَّهُ الُمجْتَهِدُونَ، الَّذِي لاَ يُدْركُهُ بُعْدُ الهِمَمِ، وَلاَ يَنَالُهُ غَوْصُ الفِطَنِ، الَّذِي لَيْسَ لِصِفَتِهِ حَدٌّ مَحْدُودٌ، وَلاَ نَعْتٌ مَوْجُودٌ، وَلا وَقْتٌ مَعْدُودٌ، وَلا أَجَلٌ مَمْدُودٌ فَطَرَ الخَلائِقَ بِقُدْرَتِهَ، وَنَشَرَ الرِّيَاحَ بِرَحْمَتِهِ، وَوَتَّدَ بِالصُّخُورِ مَيَدَانَ أَرْضِهِ.
Sifa zote njema zinamstahikia Mwenyezi Mungu ambaye ubora wa sifa zake hawa ufikii wasemaji. Ambaye neema zake wahasibu hawawezi kuzihisabu. Wenye juhudi hawawezi kutekeleza haki ya utii wake.Ambaye fahamu ya hali ya juu ya wenye akili haiwezi kumfikia kumtambua
, wala, utambuzi wa kina hauwezi kumuelewa
ambaye sifa zake hazina mpaka wenye kikomo
, wala hana sifa. Wala wakati uhisabiwao, wala muda uliowekwa
. Ameumba viumbe kwa uwezo wake, na ameutawanya upepo kwa rehema zake; kwa milima ameimarisha ardhi yake ili isiyumbe.
أَوَّلُ الدِّينِ مَعْرِفَتُهُ، وَكَمَالُ مَعْرِفَتِهِ التَّصْديقُ بِهِ، وَكَمَالُ التَّصْدِيقِ بِهِ تَوْحِيدُهُ، وَكَمَالُ تَوْحِيدِهِ الاخْلاصُ لَهُ، وَكَمَالُ الاخْلاصِ لَهُ نَفْيُ الصِّفَاتِ عَنْهُ، لِشَهَادَةِ كُلِّ صِفَة أَنَّها غَيْرُ المَوْصُوفِ، وَشَهَادَةِ كُلِّ مَوْصُوف أَنَّهُ غَيْرُ الصِّفَةِ، فَمَنْ وَصَفَ اللهَ سُبْحَانَهُ فَقَدْ قَرَنَهُ، وَمَنْ قَرَنَهُ فَقَدْ ثَنَّاهُ،وَمَنْ ثَنَّاهُ فَقَد جَزَّأَهُ، وَمَنْ جَزَّأَهُ فَقَدْ جَهِلَهُ، [وَمَنْ جَهِلَهُ فَقَدْ أشَارَ إِلَيْهِ]، وَمَنْ أشَارَ إِلَيْهِ فَقَدْ حَدَّهُ، وَمَنْ حَدَّهُ فَقَدْ عَدَّهُ.
La kwanza katika dini ni kumtambua yeye
, na ukamilifu wa kumtambua ni kumsadiki, na ukamilifu wa kumsadiki ni kumpwekesha
. Na ukamilifu wa kumpwekesha ni kumtakasa na ukamilifu wa kumtakasa ni kumuepusha mbali na sifa. Na mwenye kumsifu Mwenyezi Mungu swt. Atakuwa amemuambatanisha
, na mwenye kumuambatanisha amemfanya kuwa wawili
, na mwenye kumfanya kuwa wawili atakuwa amemfanya kuwa mwenye sehemu sehemu, na mwenye kumfanya kuwa mwenye sehemu sehemu atakuwa hamjui (s.w.t), na asiyemjua atakuwa amemuonyesha, na mwenye kumuonyesha atakuwa amemwekea mipaka [9]
, na mwenye kumuwekea mipaka atakuwa amemuhesabu
.
وَمَنْ أشَارَ إِلَيْهِ فَقَدْ حَدَّهُ، وَمَنْ حَدَّهُ فَقَدْ عَدَّهُ، وَمَنْ قَالَ: «فِيمَ» فَقَدْ ضَمَّنَهُ، وَمَنْ قَالَ: «عَلاَمَ؟» فَقَدْ أَخْلَى مِنُهُ كائِنٌ لاَ عَنْ حَدَث، مَوْجُودٌ لاَ عَنْ عَدَم، مَعَ كُلِّ شَيْء لاَ بِمُقَارَنَة، وَغَيْرُ كُلِّ شيء لا بِمُزَايَلَة، فَاعِلٌ لا بِمَعْنَى الْحَرَكَاتِ وَالاْلةِ، بَصِيرٌ إذْ لاَ مَنْظُورَ إلَيْهِ مِنْ خَلْقِهِ، مُتَوَحِّدٌ إذْ لاَ سَكَنَ يَسْتَأْنِسُ بهِ وَلاَ يَسْتوْحِشُ لِفَقْدِهِ
Na mwenye kusema yuko ndani ya nini? Anakuwa amemwingiza (s.w.t) ndani ya kitu
. Na mwenye kusema yuko juu ya nini? Atakuwa amemtoa humo
. Amekuwa yupo sio kwa kutukia, yupo lakini sio kwa maana ya hakuwapo hapo kabla. Yuko pamoja na kila kitu si kwa mwambatano wa kimwili
. Yutafauti na kila kitu si utafauti wa kimwili, mtendaji sio kwa maana ya harakati za kimwili na vyombo, mwenye kuona pindi hakuna wakuonwa kati ya viumbe wake. Yu pweke pindi hakuna mkazi analiwazika naye wala haoni ukiwa kwa kukosekana kwake.
KUUMBWA KWA ULIMWENGU:
أَنْشَأَ الخَلْقَ إنْشَاءً، وَابْتَدَأَهُ ابْتِدَاءً، بِلاَ رَوِيَّة أَجَالَهَا، وَلاَ تَجْرِبَة اسْتَفَادَهَا، وَلاَ حَرَكَة أَحْدَثَهَا، وَلاَ هَمَامَةِ نَفْس اظْطَرَبَ فِيهَا أَحَالَ الاْشياءَ لأوْقَاتِهَا، وَلاَمَ بَيْنَ مُخْتَلِفَاتِهَا، وَغَرَّزَ غَرائِزَهَا، وَأَلزَمَهَا أشْبَاحَهَا، عَالِماً بِهَا قَبْلَ ابْتِدَائِهَا، مُحِيطاً بِحُدُودِها وَانْتِهَائِهَا، عَارفاً بِقَرَائِنِها وَأَحْنَائِهَا
Alianza kuumba viumbe mwanzo, na kuvibuni kwa ubunifu, bila ya kupitisha fikra, wala kufaidika na uzoefu wowote, wala hakufanya harakati yeyote, wala kusumbuliwa na azma ya ndani ya nafsi, amevitoa viumbe (kutoka hakuna kitu na kuviingiza) kwenye ulimwengu wa kuwepo kwa wakati wake.
Akaviunganisha viumbe pamoja na tofauti zao. Akaweka silika zao, na akaziambatanisha hizo silika na wenyewe. Akiwa mjuzi (s.w.t) kabla hajabuni (viumbe) akiwa mwenye kuelewa kwa ukamilifu, mipaka yao na mwisho wao, akiwa mwenye kutambua utashi wao na sehemu zao nyingi.
ثُمَّ أَنْشَأَ ـ سُبْحَانَهُ ـ فَتْقَ الاْجْوَاءِ، وَشَقَّ الاْرْجَاءِ، وَسَكَائِكَ الَهوَاءِ، فأَجازَ فِيهَا مَاءً مُتَلاطِماً تَيَّارُهُ، مُتَراكِماً زَخَّارُهُ، حَمَلَهُ عَلَى مَتْنِ الرِّيحِ الْعَاصِفَةِ، وَالزَّعْزَعِ الْقَاصِفَةِ، فَأَمَرَها بِرَدِّهِ، وَسَلَّطَهَا عَلَى شَدِّهِ، وَقَرنَهَا إِلَى حَدِّهِ، الهَوَاءُ مِنْ تَحْتِها فَتِيقٌ، وَالمَاءُ مِنْ فَوْقِهَا دَفِيقٌ
Kisha aliumba (s.w.t) mwanya wa anga na eneo la mbingu na utando wa upepo, alimimina humo maji ambayo mawimbi yake yalikuwa makali na mawimbi yalilundikana moja juu ya jingine, aliyabebesha kwenye upepo uendao kwa kasi, na mtikisiko mkali, na kimbunga kinachovunja. Aliyaamrisha yamwage (mvua) aliufanya upepo uwe na uwezo wa kuzuia nguvu za mvua na kuijulisha mipaka yake. Upepo ulivuma chini hali maji yalibubujika kwa kasi kwa upande wa juu.
ثُمَّ أَنْشَأَ سُبْحَانَهُ رِيحاً اعْتَقَمَ مَهَبَّهَا، وَأَدَامَ مُرَبَّهَا، وَأَعْصَفَ مَجْرَاها، وَأَبْعَدَ مَنْشَاهَا، فَأَمَرَها بِتَصْفِيقِ المَاءِ الزَّخَّارِ، وَإِثَارَةِ مَوْجِ البِحَارِ، فَمَخَضَتْهُ مَخْضَ السِّقَاءِ، وَعَصَفَتْ بهِ عَصْفَهَا بِالفَضَاءِ.
Kisha (s.w.t) aliumba upepo ambao ulifanya mvumo wake uwe tasa. Yaani mvumo wa hewa ulifanywa usioweza kurutubisha kizazi, kwa kuwa kuna upepo urutubishao mimea na kuifanya itoe mazao. Na upepo huu uli- umbwa ili kuyatikisa maji tu. Na akadumisha kubaki kwake, mwendo wake ulishika kasi na akayatawanya kwa umbali na kwa upana.
تَرُدُّ أَوَّلَهُ عَلَى آخِرِهِ، وَسَاجِيَهُ عَلَى مَائِرِهِ، حَتَّى عَبَّ عُبَابُهُ، وَرَمَى بِالزَّبَدِ رُكَامُهُ، فَرَفَعَهُ فِي هَوَاء مُنْفَتِق، وَجَوٍّ مُنْفَهِق، فَسَوَّى مِنْهُ سَبْعَ سَموَات، جَعَلَ سُفْلاَهُنَّ مَوْجاً مَكْفُوفاً، وَعُلْيَاهُنَّ سَقْفاً مَحْفُوظاً، وَسَمْكاً مَرْفُوعاً، بِغَيْر عَمَد يَدْعَمُهَا، وَلا دِسَار يَنْظِمُها ثُمَّ زَيَّنَهَا بِزينَةِ الكَوَاكِبِ، وَضِياءِ الثَّوَاقِبِ، وَأَجْرَى فِيها سِرَاجاً مُسْتَطِيراً، وَقَمَراً مُنِيراً: في فَلَك دَائِر، وَسَقْف سَائِر، وَرَقِيم مَائِر.
Kisha aliuamrisha upepo kuyanyanyua maji yalio kwenye kina, na kuongeza kasi ya mawimbi ya bahari. Yakatikisa mtikiso kama ule ufanywao kwa kinywaji cha maziwa. Na kuvuma nayo angani. (Anakusudia kueleza kuwa upepo ukivuma angani anga ambazo ziko tupu huwa mvumo wake mkali kwa sababu ya kutozuilika na kitu chochote, na upepo huu ulivuma na maji mengi mvumo mkali sana). Wayarudisha ya mwanzo nyuma na yaliyotulia kuyapeleka kwa yaliyo kwenye mtikisiko, mpaka yakainuka mwinuko. Na sehemu ya chini ilijaa povu. Baadaye Mungu (s.w.t) aliinua povu lile juu ya upepo ulio wazi kutoka humo aliumba mbingu Saba. Na sehemu ya mawimbi ya chini aliyazuia na kuwa kituo, na ya juu kuwa kama dari inayo zuia na jumba lililoinuka bila ya nguzo zenye kulikinga, wala misumari inayo imarisha, kisha alizipamba (mbingu) kwa mapambo ya nyota na mianga yenye nuru. Na alipitisha humo jua lenye taa yenye kuenea mwanga wake. Na mwezi wenye nuru katika sayari zinazozunguka. Na dari inayokwenda, na ubao uendao
.
KUUMBA MALAIKA
ثُمَّ فَتَقَ مَا بَيْنَ السَّمواتِ العُلاَ، فَمَلاَهُنَّ أَطْواراً مِنْ مَلائِكَتِهِ : مِنْهُمْ سُجُودٌ لاَيَرْكَعُونَ، وَرُكُوعٌ لاَ يَنْتَصِبُونَ، وَصَافُّونَ لاَ يَتَزَايَلُونَ، وَمُسَبِّحُونَ لاَ يَسْأَمُونَ، لاَ يَغْشَاهُمْ نَوْمُ العُيُونِ، وَلاَ سَهْوُ العُقُولِ، وَلاَ فَتْرَةُ الاَبْدَانِ، ولاَ غَفْلَةُ النِّسْيَانِ.
Kisha aliumba mwanya kati ya mbingu za juu na kuzijaza malaika wake wenye daraja tofauti
.Mabingwa wa ibada, miongoni mwao kuna ambao wamesujudu na wala hawarukuu, na kuna waliorukuu na wala hawasimami, kuna waliosimama katika safu na wala hawatawanyiki kuna wanaosabihi na wala hawachoki, hawasinzii, wala hapitiwi, wala hawanyong’onyei, wala kughafilika kwa kusahau.
وَمِنْهُمْ أُمَنَاءُ عَلَى وَحْيِهِ، وأَلسِنَةٌ إِلَى رُسُلِهِ، وَمُخْتَلِفُونَ بِقَضَائِهِ وَأَمْرهِ وَمِنْهُمُ الحَفَظَةُ لِعِبَادِهِ، وَالسَّدَنَةُ لاِبْوَابِ جِنَانِهِ
b. Miongoni mwao kuna waaminifu wa wahyi wa Mungu, na ni ndimi zitamkazo ndani ya vinywa vya mitume Wake, na wanaopokezana kwa hukumu na amri zake (kupitia wao Mungu hupitisha hukumu kwa amtakae kwa apendacho).
وَمِنْهُمُ الثَّابِتَةُ في الاْرَضِينَ السُّفْلَى أَقْدَامُهُمْ، وَالمَارِقَةُ مِنَ السَّماءِ العُلْيَا أَعْنَاقُهُمْ، والخَارجَةُ مِنَ الاَقْطَارِ أَرْكَانُهُمْ، وَالمُنَاسِبَةُ لِقَوَائِمِ العَرْشِ أَكْتَافُهُمْ، نَاكِسَةٌ دُونَهُ أَبْصارُهُمْ، مُتَلَفِّعُونَ تَحْتَهُ بِأَجْنِحَتِهِمْ، مَضْرُوبَةٌ بَيْنَهُمْ وَبَيْنَ مِنْ دُونَهُمْ حُجُبُ العِزَّةِ، وَأسْتَارُ القُدْرَةِ، لاَ يَتَوَهَّمُونَ رَبَّهُمْ بالتَّصْوِيرِ، وَلاَ يُجْرُونَ عَلَيْهِ صِفَاتِ المَصْنُوعِينَ، وَلاَ يَحُدُّونَهُ بِالاْماكِنِ، وَلاَ يُشِيرُونَ إِلَيْهِ بِالنَّظَائِرِ
c. Malaika wahifadhi wa waja Wake (s.w.t), kana kwamba wao ni nguvu iliyowekwa ndani ya miili ya wanadamu na nafsini mwao. Na miongoni mwao wamo ambao miguu yao imeimarika katika ardhi ya chini, na shingo zao zimechomoza kwenye mbingu ya juu, na nguzo zao zimezidi kwenye peo (horizon), na mabega yamelingana na nguzo za Arshi, wenye kuinamisha macho yao mbali na Arshi, wenye kuizingira kwa mbawa zao, imepigwa pazia ya utukufu kati yao na wasiokuwa wao na stara ya uwezo, hawamfanyii taswira Mola wao, wala hawampitishii sifa za viumbe, wala hawamuwekei mipaka ya mahali, wala hawamuashirii kwa mifano.
KUUMBWA KWA ADAM
ثُمَّ جَمَعَ سُبْحَانَهُ مِنْ حَزْنِ الاْرْضِ وَسَهْلِهَا، وَعَذْبِهَا وَسَبَخِهَا، تُرْبَةً سَنَّهَا بالمَاءِ حَتَّى خَلَصَتْ، وَلاَطَهَا بِالبَلَّةِ حَتَّى لَزَبَتْ، فَجَبَلَ مِنْها صُورَةً ذَاتَ أَحْنَاء وَوُصُول، وَأَعْضَاء وَفُصُول: أَجْمَدَهَا حَتَّى اسْتَمْسَكَتْ، وَأَصْلَدَهَا حَتَّى صَلْصَلَتْ، لِوَقْت مَعْدُود، وَأجَل مَعْلُوم.
Kisha (s.w.t) alikusanya aina za udongo: Ngumu, laini, tamu, chachu, udongo ambao aliumwagia maji mpaka ukalowana, na aliukanda kwa unyevunyevu mpaka ukaganda, kutoka humo aliumba sura yenye pande tofauti, na viungo tanzu, sehemu ya pingili aliigandisha na ikashikamana, akaifanya kuwa ngumu mpaka ikawa ngumu, kiasi cha kusikika sauti, kwa wakati uliowekwa kwa muda ujulikanao.
ثُمَّ نَفَخَ فِيها مِنْ رُوحِهِ فَمَثُلَتْ إِنْساناً ذَا أَذْهَان يُجيلُهَا، وَفِكَر يَتَصَرَّفُ بِهَا، وَجَوَارِحَ يَخْتَدِمُهَا، وَأَدَوَات يُقَلِّبُهَا، وَمَعْرِفَة يَفْرُقُ بِهَا بَيْنَ الحَقِّ وَالبَاطِلِ، والاَذْوَاقِ والَمشَامِّ، وَالاْلوَانِ وَالاْجْنَاس، مَعْجُوناً بطِينَةِ الاْلوَانِ الُمخْتَلِفَةِ، وَالاَشْبَاهِ المُؤْتَلِفَةِ، وَالاْضْدَادِ المُتَعَادِيَةِ، والاَخْلاطِ المُتَبَايِنَةِ، مِنَ الحَرِّ والبَرْدِ، وَالبَلَّةِ وَالْجُمُودِ، وَالْمَساءَةِ وَالسُّرُورِ.
Baadaye alipulizia humo roho, akawa mtu mwenye akili imsukumayo, na fikra aitumikishayo, na viungo vya mwili avitumiavyo, na ala zimsaidiazo kubadilisha hali yake, na maarifa ambayo kwayo anatofautisha kati ya haki na batili, akiwa na uwezo wa kuonja, na kunusa, kupambanua rangi, na jinsi yenye mchanganyiko wa udongo wa rangi tofauti, na vitu vyenye kufanana na kuafikiana, vitu vilivyo kinyume na visivyoafikiana. Aina tofauti za mchanganyiko: kama vile joto, baridi, hali ya chepe, ugumu, chuki, furaha.
وَاسْتَأْدَى اللهُ سُبْحَانَهُ المَلائكَةَ وَدِيعَتَهُ لَدَيْهِمْ، وَعَهْدَ وَصِيَّتِهِ إِلَيْهمْ، في الاْذْعَانِ بالسُّجُودِ لَهُ، وَالخُنُوعِ لِتَكْرِمَتِهِ، فَقَالَ عزَّمِن قائِل: (اسْجُدُوا لاِدَمَ فَسَجَدُوا إِلاَّ إِبْلِيسَ) وَقَبِيلَهُ، اعْتَرَتْهُمُ الحَمِيَّةُ، وَغَلَبَتْ عَلَيْهِمُ الشِّقْوَةُ، وَتَعَزَّزُوا بِخِلْقَةِ النَّارِ، وَاسْتَوْهَنُوا خَلْقَ الصَّلْصَالِ، فَأَعْطَاهُ اللهُ تَعالَى النَّظِرَةَ اسْتِحْقَاقاً لِلسُّخْطَةِ، وَاسْتِتْماماً لِلْبَلِيَّةِ، وَإِنْجَازاً لِلْعِدَةِ، فَقَالَ: (إنَّكَ مِنَ المُنْظَرِينَ إِلَى يَوْمِ الْوَقْتِ الْمَعْلُومِ)
Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwataka malaika watekeleze ahadi aliyowekeana nao, na kutimiza agizo lake la kuwataka wamsujudie Adamu, na kunyenyekea ili kumpa heshima, akasema (s.w.t): “Msujudiyeni Adamu, wote walisujudu isipokuwa iblisi
”. Quran 2:34. Yeye alijiona, akazidiwa na uovu, akajitukuza na kufanya kibri kwa sababu ya kuumbwa kutokana na moto. Alikebehi asili ya umbo la Adamu, yaani udongo. Mwenyezi Mungu Mtukufu alimpa (Ibilisi) muda ili ghadhabu ithibiti kwake. Na kukamilisha mtihani ( kwa mwanadamu) na kutekeleza ahadi, akasema: “Basi kwa hakika umekwisha kuwa mingoni mwa waliopewa muhula mpaka ya siku ya wakati maalum
” (15:38, 38:81).
ثُمَّ أَسْكَنَ سُبْحَانَهُ آدَمَ دَاراً أرْغَدَ فِيهَاعَيْشَهُ، وَآمَنَ فِيهَا مَحَلَّتَهُ، وَحَذَّرَهُ إِبْلِيسَ وَعَدَاوَتَهُ، فَاغْتَرَّهُ عَدُوُّهُ نَفَاسَةً عَلَيْهِ بِدَارِ الْمُقَامِ، وَمُرَافَقَةِ الاْبْرَارِ، فَبَاعَ الْيَقِينَ بِشَكِّهِ، وَالعَزِيمَةَ بِوَهْنِهِ، وَاسْتَبْدَلَ بِالْجَذَلِ وَجَلاً، وَبِالاْغْتِرَارِ نَدَماً ثُمَّ بَسَطَ اللهُ سُبْحَانَهُ لَهُ في تَوْبَتِهِ، وَلَقَّاهُ كَلِمَةَ رَحْمَتِهِ، وَوَعَدَهُ المَرَدَّ إِلَى جَنَّتِهِ، فَأَهْبَطَهُ إِلَى دَارِ الَبَلِيَّةِ، وَتَنَاسُلِ الذُّرِّيَّةِ
Baadaye Mwezi Mungu Mtukufu alimuweka Adamu peponi ambapo aliyafanya maisha yake yakuridhisha, na kubaki kwa amani. Alimtahadharisha na Ibilisi na uadui wake. Adui yake (ambae ni Ibilisi) alimghuri. Akimwonea wivu kubaki kwake milele Peponi akiwa na watendao mema. Akauza yakini kwa shaka yake, na azma kwa unyonge wake, na furaha aliibadilisha kwa woga. Na kuhadaika ikawa ni majuto. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu alimpa Adamu fursa ya kutubia. Alimfundisha neno la rehema Zake. Na alimuahidi kumrudisha kwenye Pepo yake. Alimteremsha duniani kwenye makazi ya mtihani, nyumba ya majaribu, na kuzaa watoto.
KUTEULIWA KWA MANABII
وَاصْطَفى سُبْحَانَهُ مِنْ وَلَدَهِ أَنْبيَاءَ أَخَذَ عَلَى الْوَحْيِ مِيثَاقَهُمْ، وَعَلَى تَبْليغِ الرِّسَالَةِ أَمَانَتَهُمْ، لَمَّا بَدَّلَ أَكْثَرُ خَلْقِهِ عَهْدَ اللهِ إِلَيْهِمْ، فَجَهِلُوا حَقَّهُ، واتَّخَذُوا الاْنْدَادَ مَعَهُ، وَاجْتَالَتْهُمُ الشَّيَاطِينُ عَنْ مَعْرفَتِهِ، وَاقتَطَعَتْهُمْ عَنْ عِبَادَتِهِ.
Mwezi Mungu Mtukufu aliwateua manabii katika kizazi chake - watoto wa Adamu
- akachukuwa kwao ahadi kwa ajili ya wahyi, na kuchukuwa dhamana kwao kwa ajili ya kuifikisha risala - Ujumbe - lakini wengi katika viumbe Wake walivyobadili ahadi ya Mungu walipotosha agizo lake (s.w.t) kwao wakapuuza haki yake wakamfanyia washirika pamoja naye. Shetani aliwapotosha mbali na kumtambua Yeye. Na aliwaweka mbali na ibada yake.
فَبَعَثَ فِيهمْ رُسُلَهُ، وَوَاتَرَ إِلَيْهِمْ أَنْبِياءَهُ، لِيَسْتَأْدُوهُمْ مِيثَاقَ فِطْرَتِهِ، وَيُذَكِّرُوهُمْ مَنْسِيَّ نِعْمَتِهِ، وَيَحْتَجُّوا عَلَيْهِمْ بَالتَّبْلِيغِ، وَيُثِيرُوا لَهُمْ دَفَائِنَ الْعُقُولِ، وَيُرُوهُمْ آيَاتِ الْمَقْدِرَةِ: مِنْ سَقْف فَوْقَهُمْ مَرْفُوع، وَمِهَاد تَحْتَهُمْ مَوْضُوع، وَمَعَايِشَ تُحْيِيهِمْ، وَآجَال تُفْنِيهمْ، وَأَوْصَاب تُهْرِمُهُمْ، وَأَحْدَاث تَتَابَعُ عَلَيْهِمْ.
Aliwatuma kwao Mitume wake, aliwapeleka manabii wake kwao kwa vipindi: Ili watekeleze ahadi ya kuumba kwao, na wakumbushe neema zake zilizosahauliwa, na ili watoe hoja kwao kwa kufikisha ujumbe. Ili kuamsha vipaji vya hikima vilivyofichikana. Na kuwaonesha alama za uwezo wake wa kila kitu kama vile mbingu zilizoinuliwa na ardhi iliotandikwa chini yao, na sababu za maisha zinazowapa uhai, na ajali zinazowamaliza, na taabu zinazowazeesha na matukio yanayofululiza kwao.
وَلَمْ يُخْلِ اللهُ سُبْحَانَهُ خَلْقَهُ مِنْ نَبِيٍّ مُرْسَل، أَوْ كِتَاب مُنْزَل، أَوْ حُجَّة لاَزِمَة، أَوْ مَحَجَّة قَائِمَة، رُسُلٌ لا تُقَصِّرُ بِهِمْ قِلَّةُ عَدَدِهِمْ، وَلاَ كَثْرَةُ المُكَذِّبِينَ لَهُمْ: مِنْ سَابِق سُمِّيَ لَهُ مَنْ بَعْدَهُ، أَوْ غَابِر عَرَّفَهُ مَنْ قَبْلَهُ عَلَى ذْلِكَ نَسَلَتِ القُرُونُ، وَمَضَتِ الدُّهُورُ، وَسَلَفَتِ الاْباءُ، وَخَلَفَتِ الاْبْنَاءُ.
Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuwaacha viumbe wake bila ya nabii mwenye kutumwa, au bila ya Kitabu kilichoteremshwa, au bila ya hoja ya lazima, au bila ya njia iliyonyooka. Hawa wajumbe, hawakujihisi kuwa wachache kwa udogo wa idadi yao wala kwa ukubwa wa idadi ya wanaowakadhibisha. Miongoni mwao aliyetangulia humtaja anayefuata baada yake au mfuasi aliyetambulishwa na mtangulizi wake. Kwa utaratibu huo karne baada ya karne zilipita, vilizaliwa vizazi. Miaka ikapita, mababa walipita na watoto walichukua nafasi.
KUTUMWA KWA MUHAMMAD (s.a.w.w)
إِلَى أَنْ بَعَثَ اللهُ سُبْحَانَهُ مُحَمَّداً(صلى الله عليه وآله) لاِنْجَازِ عِدَتِهِ وَتَمامِ نُبُوَّتِهِ، مَأْخُوذاً عَلَى النَّبِيِّينَ مِيثَاقُهُ، مَشْهُورَةً سِمَاتُهُ، كَرِيماً مِيلادُهُ
Hali iliendelea hivyo mpaka Allah (s.w.t) alipomtuma Muhammad(s.a.w.w)
, mjumbe Wake ili kutimiza idadi Yake, na kukamilisha unabii Wake. Akiwa mwenye kuchukua ahadi Yake kutoka kwa manabii, alama zake(s.a.w.w)
zilikuwa mashuhuri, uzao wake ni wa heshima.
وَأهْلُ الاْرْضِ يَوْمَئِذ مِلَلٌ مُتَفَرِّقَةٌ، وَأَهْوَاءٌ مُنْتَشِرَةٌ، وَطَرَائِقُ مُتَشَتِّتَةٌ، بَيْنَ مُشَبِّه للهِ بِخَلْقِهِ، أَوْ مُلْحِد في اسْمِهِ، أَوْ مُشِير إِلَى غَيْرهِ
Watu wa dunia hii wakati huo walikuwa kwenye itikadi zinazotofautiana, tamaa za nafsi zimeenea, na njia zikiwa tofauti, wakiwemo waliomshabihisha Mungu (s.w.t.) na viumbe Wake au wenye kupotosha jina lake (s.w.t) au wenye kumshirikisha na viumbe.
فَهَدَاهُمْ بهِ مِنَ الضَّلاَلَةِ، وَأَنْقَذَهُمْ بمَكانِهِ مِنَ الجَهَالَةِ ثُمَّ اخْتَارَ سُبْحَانَهُ لِمحَمَّد صلى الله عليه لِقَاءَهُ، وَرَضِيَ لَهُ مَا عِنْدَهُ، فَأَكْرَمَهُ عَنْ دَارِالدُّنْيَا، وَرَغِبَ بِهَ عَنْ مُقَارَنَةِ البَلْوَى، فَقَبَضَهُ إِلَيْهِ كَرِيماً.
Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaongoza kupitia kwake kutokana na upotovu, na kwa nafasi yake(s.a.w.w)
aliwaokoa mbali na ujahili. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu alimhitari Muhamamd(s.a.w.w)
kukutana naye na alimridhia ili awe karibu Yake (s.w.t), na alimzidishia heshima kwa kumwondoa duniani mahali pa majaribu, kwa hiyo alimchukuwa Kwake(s.a.w.w)
kwa heshima.
وَخَلَّفَ فِيكُمْ مَا خَلَّفَتِ الاْنْبيَاءُ في أُمَمِها، إذْ لَم يَتْرُكُوهُمْ هَمَلاً، بِغَيْر طَريق واضِح، ولاَعَلَم قَائِم
Na aliacha kwenu ambayo manabii waliacha katika Umma zao
. Kwani hawakuwaacha wamepuuzwa, bila ya kuwaeleza njia iliyowazi, wala watakayoongoka kwayo.
KITABU CHA MWENYEZI MUNGU NA SUNNAH
كِتَابَ رَبِّكُمْ [فِيكُمْ:] مُبَيِّناً حَلاَلَهُ وَحَرامَهُ، وَفَرَائِضَهُ وَفَضَائِلَهُ، وَنَاسِخَهُ وَمَنْسُوخَهُ، وَرُخَصَهُ وَعَزَائِمَهُ، وَخَاصَّهُ وَعَامَّهُ، وَعِبَرَهُ وَأَمْثَالَهُ، وَمُرْسَلَهُ وَمَحْدُودَهُ، وَمُحْكَمَهُ وَمُتَشَابِهَهُ، مُفَسِّراً جُمَلَهُ، وَمُبَيِّناً غَوَامِضَهُ
Amekuachieni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, Mola wenu: kibainishacho halali yake na haramu yake
. Faradhi zake na fadhila zake. Batilisho (nasikh) zake na zilizobatilishwa (mansukh) zake, ruhusa zake na azma zake, hukumu ambazo ni makhsusi, na ambazo zipo katika sura ya jumla, na ambazo zina mafunzo ndani yake na mithali, ndefu na fupi, thabiti zake na mutashabih zake: zilizo wazi na ambazo ni ngumu kueleweka maana yake, zenye kufasiri aya zilizokuja kwa maana ya jumla, na zenye kubainisha maana zake ngumu.
بَيْنَ مَأْخُوذ مِيثَاقُ عِلْمِهِ، وَمُوَسَّع عَلَى العِبَادِ في جَهْلِهِ، وَبَيْنَ مُثْبَت في الكِتابِ فَرْضُهُ، وَمَعْلُوم في السُّنَّهِ نَسْخُهُ، وَوَاجب في السُّنَّةِ أَخْذُهُ، وَمُرَخَّص في الكِتابِ تَرْكُهُ.
Humo kuna aya ambazo kuzijua ni lazima, na kuna ambazo watu wanaruhusiwa kutozijua. Na ambazo imethibiti Kitabuni faradhi yake, na zajulikana kutenguliwa katika sunnah, na ambazo ni wajibu katika sunnah kuzitekeleza, na ambazo katika kitabu zaruhusiwa kuziacha.
وَبَيْنَ وَاجِب بِوَقْتِهِ، وَزَائِل في مُسْتَقْبَلِهِ، وَمُبَايَنٌ بَيْنَ مَحَارِمِهِ، مِنْ كَبير أَوْعَدَ عَلَيْهِ نِيرَانَهُ، أَوْ صَغِير أَرْصَدَ لَهُ غُفْرَانَهُ، وَبَيْنَ مَقْبُول في أَدْنَاهُ، ومُوَسَّع في أَقْصَاهُ
Na kuna ambazo ni wajibu kwa wakati wake, na wenye kuondoka wakati ujao, uharamu wake pia watofautiana, kuna ambazo ni kubwa ametishia kwa (kosa hilo) moto wake, au ndogo zenye ghofrani yake, na kati ya yanayokubalika uchache wake na yenye wasaa katika umbali wake. Kuna ambazo uchache wake wakubaliwa (kwa Mungu) na zenye uwezekano wa kutanuliwa (hukumu yake)
.
NDANI YA KHUTBA HII AELEZEA HIJJA
وَفَرَضَ عَلَيْكُمْ حَجَّ بَيْتِهِ الحَرَامِ، الَّذِي جَعَلَهُ قِبْلَةً لِلاْنَامِ، يَرِدُونَهُ وُرُودَ الاَنْعَامِ، وَيأْلَهُونَ إِلَيْهِ وُلُوهَ الحَمَامِ
Na amewajibisha juu yenu kuhiji nyumba yake tukufu, ambayo ameifanya Qibla kwa wanadamu, wanaiendea kama wanyama walazimikapo kuyaendea manyweo ya maji wanayahamanikia uhamanikaji wa njiwa.
جَعَلَهُ سُبْحَانَهُ عَلاَمَةً لِتَوَاضُعِهمْ لِعَظَمَتِهِ، وَإِذْعَانِهِمْ لِعِزَّتِهِ، وَاخْتَارَ مِنْ خَلْقِهِ سُمَّاعاً أَجَابُوا إِلَيْهِ دَعْوَتَهُ، وَصَدَّقُوا كَلِمَتِهُ، وَوَقَفُوا مَوَاقِفَ أَنْبِيَائِهِ، وَتَشَبَّهُوا بمَلاَئِكَتِهِ المُطِيفِينَ بِعَرْشِهِ، يُحْرِزُونَ الاْرْبَاحَ فِي مَتْجَرِ عِبَادَتِهِ، وَيَتَبَادَرُونَ عِنْدَهُ مَوْعِدَ مَغْفِرَتِهِ
Mwenyezi Mungu Mtukufu ameifanya (Kaaba) iwe ndio alama ya unyenyekevu wao kuunyenyekea utukufu Wake, na utii wao kwa enzi Yake. Amechagua kutoka kwa viumbe Wake watiifu walioitikia wito wake. Na wamesadikisha neno Lake. Na wakasimama msimamo wa manabii Wake. Wakashabihiana na malaika wake wazungukao Arshi Yake. Wanafaidika na biashara ya ibada yake. Wakiharakia kwenye ahadi ya msamaha Wake.
جَعَلَهُ سُبْحَانَهُ لِلاِسْلامِ عَلَماً، وَلِلْعَائِذِينَ حَرَماً، فَرَضَ حَجَّهُ، وَأَوْجَبَ حَقَّهُ، وَكَتَبَ عَلَيْكُمْ وِفَادَتَهُ، فَقَالَ سُبْحَانَهُ: (وَللهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلاً وَمَنْ كَفَرَ فَإِنَّ اللهَ غَنِيٌّ عَنِ العَالَمينَ.
Mungu (s.w.t.) ameifanya (nyumba hii) kuwa ni alama ya Uislamu na ni lengo la heshima kwa wanaojikinga nayo.
Amefaradhisha haki yake, na kulazimisha kuihiji. Na amefanya faradhi juu yenu kuiendea aliposema (s.w.t.): “Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awazae njia ya kwendea. Na atakayekanusha basi Mwenyezi Mungu si mhitaji kwa walimwengu. (3:97).