NAHJULBALAGHAH Juzuu 1

NAHJULBALAGHAH60%

NAHJULBALAGHAH Mwandishi:
: Sheikh Haruna Pingili
Kundi: VITABU VYA HADITHI

Juzuu 1 Juzuu 2
  • Anza
  • Iliyopita
  • 7 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 6612 / Pakua: 4030
Kiwango Kiwango Kiwango
NAHJULBALAGHAH

NAHJULBALAGHAH Juzuu 1

Mwandishi:
Swahili

NAHJUL-BALAGHAH

MAJMUA YA KHUTBA, AMRI, BARUA, RISALA, MAWAIDHA NA SEMI ZA

AMIRUL-MUUMININ ALI BIN ABU TALIB(a.s)

Mkusanyaji: Al-Sharif Al-Radhii

Kimetarjumiwa na: Sheikh Haroon Pingili

NENO LA MCHAPISHAJI

Kitabu kilichoko mkononi mwako ni tarjumi kutoka lugha ya Kiarabu ya kitabu maarufu katika ulimwengu wa Kiislamu, Nahju 'l-Balaghah. Kitabu hiki kitachapishwa katika majalada mbali mbali, na hili ulilo nalo mkononi ni jalada la kwanza.

Nahju 'l-Balaghah ni mkusanyiko wa khutba, barua na maelekezo ya Imam Ali(a.s) . Mengi yamesemwa kuhusu ubora na ufasaha wa maneno yaliyomo katika khutba na harua hizo. Kwa ufupi, Nahju 'l-Balaghah ni kilele cha ufasaha.

Mbali na mawaidha yaliyomo humo, msomaji atafaidika na lugha iliyomo katika khutba na barua hizo, hususan kwa wasomaji wa Kiarabu.

Inasemekana kwamba baada ya Qur'ani Tukufu na maneno ya Mtukufu Mtume(s.a.w.w) , Nahju 'l-Balaghah ndiyo inayofuatia kwa ufasaha na ubora wa maneno.

Si rahisi kwa msomaji wa Kiswahili kupata ladha ileile aipatayo msomaji wa Kiarabu kutokana na ukweli kwamba lugha ya Kiarabu ni pana mno na msamiati wake ni mkubwa. Pamoja na hayo, mtarjumi wetu amejitahidi sana kuleta maana ya maneno ya Kiarabu kwenye lugha ya Kiswahili bila kupoteza maana yake.

Kwa vile kitabu hiki ni muhimu sana, tumeona ni bora tukichapishe katika lugha ya Kiswahili ili Waislamu na wasomaji wetu wazungumzao Kiswahili wapate kunufaika na yaliyomo humo. Hivyo, ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakkuwa ni chenye manufaa sana kwao na katika jamii yetu.

Tunamshukuru ndugu yetu, Sheikh Harun Pingili kwa kukubali jukumu hili kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.

Mchapishaji

Al-Itrah Foundation

S. L. P. 19701

Dar-es-Salaam, Tanzania

DIBAJI

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu. Kwanza yanipasa nimshukuru Mwenyezi Mungu Jalali, asiye kuwa na mithali, kwa neema zake za kila hali na kila mahali, hata nikaweza mimi mja mpungufu, kutimiza kazi hii tukufu ya kuipitia tarjuma hii ya Kiswahili ya Nahju 'l-Balaghah.

Nahju 'l-Balaghah ni jina la diwani mashuhuri yenye khutba, uweza wa kusema, na barua za Imam Alî bin Abu Talib(a.s) . Haya yote yamekusanywa na Sharîf Ar-Radhi. Diwani hii yenye khutba takriban 237, baru 79 na mithali 480 ilikamilika mwezi wa Rajab 400 A.H./1009 A.D. Maana ya NAHJ ni njia iliyo wazi, au barabara kuu; na maana ya Balaghah ni ufasaha (wa lugha) au ilimu ya usemaji, n.k. Kwa hivyo Nahju 'l-Balaghah yaani Barabara kuu ya ufasaha.

"Huyu Imam 'Ali ni nani? Ni vigumu mno kuzitaja sifa zake kwa ukamilifu. Yeye alikuwa mtaalamu, shujaa na khatibu kuliko wote. Uchamungu wake, mapenzi yake ya Mwenyezi Mungu, uaminifu wake na ushupavu wake wa kufuata dini ulikuwa wa darja ya juu kuliko mtu yeyote akichukia diplomasia (ujanja), na akipenda haki na insafu. Sera zake ni kama zilivyoamrishwa na Mwenyezi Mungu. Wataalamu wa Kiyahudi na wa Kikristo wakijaaliwa kujua daraja ya ilimu yake huisujudia ilimu hiyo isioweza kufananishwa.

Wafalme wa Ki-Rumi wangependa kuzitundika picha zake katika kasri zao, na maaskari wakubwa wa vita wangependelea kulichonga jina lake kwenye panga zao.

لآ فثي إ لاَّ عَلِيَّ وَ لآ سَيْفَ اِلاَّ ذُو الْفقار

"Hayuko kijana shujaa mfano wa 'Ali! wala hakuna upanga mfano wa Dh-ul-Faqar (upanga wa Imam 'Alî (a.s) aliorithi kwa Mtume) ."

Allama Mustafa Beck Najeeb wa al-Azhar, Cairo amesema:

خَرَجَ اِلَي الدُّ نْيَا وَ الثَّهَادَةُ مَكْتُوْبَهَّ عَلي جَبَيْنِهِ وَ خَرجَ مِنْهَا وَ الثَّهَادَةُ مَكْتُوْبَهَّ عَلي دَ لِكَ الجَبَيْنِ بضَرْبَهِ حُسَّا مٍ لَقدْ كَمَا عَلِمْنَا فِي الْكَعْبَهِ وَ ضُربَ كَمَ عَلِمْنَا فِي الْمَسْجِدِ قأَيَّه بَدَايَهٍ وَ نِهَايَهٍ اَثْْبَهَ بالْحَيَاةِ الّتي بَيْنَهُمَا مِنْ تِلْكَ الْبدَايَهٍ وَ تِلْكَ النَّهَايَهِ؟

"Imam 'Alî amekuja duniani na shahada imeandikwa kwenye kipaji chake; na ameondoka duniani na shahada vile vile imeandikwa kwenye hicho kipaji kwa dharba ya upanga. Kama tunavyojua amezaliwa ndani ya Ka'bah, na kama tujuavyo amepigwa dharba (ya upanga) msikitini. Ilioje ajabu? Mwanzo wake na mwisho wake kupata darja ya kifo cha kishahidi ."

Sheikh Abbas Mahmud al-Aqqad - mwandishi maarufu wa Ki-masri amesema:

"Mtu yeyote ambaye amebobea katika lugha ya Ki-arabu atakubali tu kwamba Nahju 'l-Balaghah inafuata kwa ubora wake baada ya maneno ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Maneno ya 'Alî ni yenye maana na fikra nzito. Kwa hivyo Nahju 'l-Balaghah lazima isomwe kwa makini, na irejewe na idondolewe na wanafunzi na walimu. Ninapenda kutilia mkazo kwamba Nahju 'l-Balaghah iingizwe kwenye mukhtasar wa masomo na mafundisho (syllabi) ya vyuo vikuu vyote vya Masri na Beirut kwenye masomo ya kiwango cha juu ya lugha na falsafa."

Sheikh Muhammad 'Abdo - Mufti wa Masri na Profesa wa lugha ya Kiarabu na falsafa amesema:

تَحْتَ كَلاَمِ الْخَالِق وَ فَوْقَ كَلاَ مِ الْمَخْلُوق.

"Mtu yeyote hawezi kukataa kwamba 'Alî alikuwa Imamu wa makhatibu, mwalimu na kiongozi wa waandishi na wanafalsafa. Bila ya shaka khutba zake na maneno yake ni yenye kiwango cha juu kabisa kushinda maneno ya mtu ye yote isipokuwa maneno ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake:"

'Abd-ul-Masîh al-Antaqi - Mhariri wa Kikristo wa gazeti la Ki-masri Al- Ahram amesema:

'Alî alikuwa Imamu kwenye nyanja za vita, Imamu wa siasa, Imamu wa dini, Imamu wa falsafa, Imamu wa maadili, Imamu wa maandiko mbali mbali, na Imamu wa ilmu na hikma."

Profesa Muhammad Kamil, Cairo amesema:

فاِ دَا لَمْ يَكُنْ عَلِيّ نَبِيًّا فلَقدْ كَانَ خُلُقُهَ نَبَوتًّا.

"Ijapokuwa Imam 'Alî alikuwa si nabii, lakini khulqa yake ilikuwa ya kinabii ."

Shaykh Nasif al-Yazidi alipokuwa akimwaidhi mwanawe alimwambia: “Kama unataka mamlaka ya juu kabisa dhidi ya wenzako katika masomo, hikma, maandiko, inshaa n.k. basi hifadhi Qur'ani Tukufu na Nahju 'l- Balaghah”.

Amîn Nakhlah anasema: “Mtu yeyote anayetamani kuikata kiu yake (ya kiroho) kwa maneno ya 'Ali(a.s) lazima ausome kila ukurasa wa Nahju 'l- Balaghah kwa uangalifu.

Nahju 'l-Balaghah ni diwani ambayo humfanya kila mtu kuukubali ubingwa wa Imam 'Ali(a.s) . Hakuna kitabu kinachoweza kuishinda Nahju 'l- Balaghah isipokuwa Qur'ani Tukufu. Humo ndani ya Nahju 'l-Balaghah utazikuta lulu za maarifa zilizotungwa kwenye mikufu mizuri, utayakuta maua ya lugha ambayo huifanya akili ya binadamu inukie kwa harufu nzuri ya ushujaa na uungwana; vile vile humo utaikuta mito ya lugha safi ambayo ni mitamu na baridi zaidi kuliko mto wa al-Kauthar.

Imam 'Alî(a.s) anawaidhi juu ya maudhui mbali mbali, k.m. Kuumbwa kwa ardhi na mbingu, tawhîd, taqwa, malaika, zuhd, Qiyamah, kiburi, tamaa, vita vya Jamal, Siffin, Nahrawan, ibada, maarifa, tamaa, imani, insafu, n. k.

Katika mithali yake mashuhuri Imam 'Alî(a.s) anatuwaidhi sisi wanaadamu kutobaguwana kwa makabila.

"Watu kwa makamu ni sawa sawa

Baba ni Adamu na mama Hawa

Ukijia'dhimu kwa kuzaliwa

Maji na kinamu uliumbiwa

Fahamu na jua mwana Adamu"

Maneno haya ya Sayyidna 'Alî yamo katika msingi wa Qur'ani Tukufu. (Sh. 'Alî Muhsin al-Barwani).

Tunatumai wasomaji wetu watastafidi sana na tarjama hii ya Nahju 'l-Balaghah (kwa lugha ya Kiswahili) ambayo imefanywa kwa kifundi na ujuzi mkubwa. Mwenyezi Mungu atujaalie tawfiq ya Kutenda Kheri na atuepushe na kila shari.

Wa Billahi Tawfîq,

KUKHUSU NASABA YA AMIRUL-MU’MININA ALI(A.S) NA KUTAJA SEHEMU KIDOGO YA FADHAILI ZAKE

Yeye ni Abul’Hasan Ali bin Abi Taalibina jina lake Abdu Manaf bin Abdulmuttalib - na jina lake ni: Shaybatul’hamd bin Hashim-na jina lake ni Amr bin Abdu Manaf bin Qusayyi. Kuniya ambayo aghlabu hutumika kumuita ilikuwa: Abul’hasan.

Na mwanawe Hasan(a.s) katika zama za uhai wa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alikuwa akimwita Abulhusayn, na Husayn(a.s) alikuwa akimwita Abulhasan, na wawili hao walikuwa wakimwita Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) baba yao, na alipokufa Nabii(s.a.w.w) ndipo walimwita baba yao baba.

Na Mtume wa Mwenyezi Mungu alimpa kunia ya: Abu Turab, hivyo ni kwa sababu siku moja alimkuta amelala usingizi kwenye mchanga, hali ikiwa ridaa-nguo-yake imemdondoka, na mchanga ukawa umemtapakaa mwilini mwake. Akamjia na akaketi karibu ya kichwa chake, na alimwamsha na akawa yuampangusa mchanga toka mgongoni huku akimwambia: “Kaa; kwa hakika wewe ni Abu Turab” na tokea hapo ikawa miongoni mwa kunia aipendayo mno katika kunia zake(a.s) . Alikuwa ana- furahi kuitwa kunia hii (Abuturab).

Na Bani Umayyah walikuwa wakiwaraghibisha makhatibu wao wamtukane kwa kunia hii wakiwa juu ya mimbari, na waliifanya kuwa ni upungufu fulani na ni dosari kwake; Basi ikawa kwake kama wamemvika pambo, kulingana na alivyosema Hasan Albasri (r.a). Jina lake la kwanza ambalo mama yake alimwita ni: Haidara, ikiwa ni jina la baba yake Asad bin Hashim - na Alhaidara ni: Simba, baba yake (yaani Abutalib) alimbadilisha jina hilo na akamwita Ali. Na kuna kauli isemayo kuwa: Haidara ni jina ambalo Makurayshi walikuwa wana mwita. Kauli ya kwanza ndio sahihi; kwa kuwa kuna habari yajulisha hivyo kutokana na yeye mwenyewe, siku alipomkabili Marhab ambaye alikuwa anajigamba kutafakhari akisema: “Ana lladhi sammatni ummi Marhaba” ndipo hapo Imam Ali(a.s) alimjibu na kumkabili: “Ana lladhi sammatni Haidara”.

Jina la mama yake ni Faatima binti Asad bin Hashim bin Abdi Manaf bin Qusayyi, ni (mwana mama wa kwanza Hashimiya amezaa kwa Bwana wa kihashimii; Ali(a.s) alikuwa mdogo katika watoto wake (huyu mama), na Ja’far alikuwa mkubwa kuliko yeye kwa miaka kumi, na Aqiil alikuwa mkubwa kuliko yeye kwa miaka kumi, na Talib ni mkubwa kuliko Aqiil kwa miaka kumi, na Fatima binti Asad mama wa hao wote.

NAHJUL-BALAGHAH

JUZUU YA KWANZA

1. NA KATIKA KHUTBA ZAKE(a.s)

Ndani ya khutba hii anaelezea kuumbwa kwa ardhi, mbingu, na kuumbwa kwa Adam(a.s)

الحَمْدُ للهِ الَّذَي لاَ يَبْلُغُ مِدْحَتَهُ القَائِلُونَ، وَلاِ يُحْصِي نَعْمَاءَهُ العَادُّونَ، ولاَ يُؤَدِّي حَقَّهُ الُمجْتَهِدُونَ، الَّذِي لاَ يُدْركُهُ بُعْدُ الهِمَمِ، وَلاَ يَنَالُهُ غَوْصُ الفِطَنِ، الَّذِي لَيْسَ لِصِفَتِهِ حَدٌّ مَحْدُودٌ، وَلاَ نَعْتٌ مَوْجُودٌ، وَلا وَقْتٌ مَعْدُودٌ، وَلا أَجَلٌ مَمْدُودٌ فَطَرَ الخَلائِقَ بِقُدْرَتِهَ، وَنَشَرَ الرِّيَاحَ بِرَحْمَتِهِ، وَوَتَّدَ بِالصُّخُورِ مَيَدَانَ أَرْضِهِ.

Sifa zote njema zinamstahikia Mwenyezi Mungu ambaye ubora wa sifa zake hawa ufikii wasemaji. Ambaye neema zake wahasibu hawawezi kuzihisabu. Wenye juhudi hawawezi kutekeleza haki ya utii wake.Ambaye fahamu ya hali ya juu ya wenye akili haiwezi kumfikia kumtambua[1] , wala, utambuzi wa kina hauwezi kumuelewa[2] ambaye sifa zake hazina mpaka wenye kikomo[3] , wala hana sifa. Wala wakati uhisabiwao, wala muda uliowekwa[4] . Ameumba viumbe kwa uwezo wake, na ameutawanya upepo kwa rehema zake; kwa milima ameimarisha ardhi yake ili isiyumbe.

أَوَّلُ الدِّينِ مَعْرِفَتُهُ، وَكَمَالُ مَعْرِفَتِهِ التَّصْديقُ بِهِ، وَكَمَالُ التَّصْدِيقِ بِهِ تَوْحِيدُهُ، وَكَمَالُ تَوْحِيدِهِ الاخْلاصُ لَهُ، وَكَمَالُ الاخْلاصِ لَهُ نَفْيُ الصِّفَاتِ عَنْهُ، لِشَهَادَةِ كُلِّ صِفَة أَنَّها غَيْرُ المَوْصُوفِ، وَشَهَادَةِ كُلِّ مَوْصُوف أَنَّهُ غَيْرُ الصِّفَةِ، فَمَنْ وَصَفَ اللهَ سُبْحَانَهُ فَقَدْ قَرَنَهُ، وَمَنْ قَرَنَهُ فَقَدْ ثَنَّاهُ،وَمَنْ ثَنَّاهُ فَقَد جَزَّأَهُ، وَمَنْ جَزَّأَهُ فَقَدْ جَهِلَهُ، [وَمَنْ جَهِلَهُ فَقَدْ أشَارَ إِلَيْهِ]، وَمَنْ أشَارَ إِلَيْهِ فَقَدْ حَدَّهُ، وَمَنْ حَدَّهُ فَقَدْ عَدَّهُ.

La kwanza katika dini ni kumtambua yeye[5] , na ukamilifu wa kumtambua ni kumsadiki, na ukamilifu wa kumsadiki ni kumpwekesha[6] . Na ukamilifu wa kumpwekesha ni kumtakasa na ukamilifu wa kumtakasa ni kumuepusha mbali na sifa. Na mwenye kumsifu Mwenyezi Mungu swt. Atakuwa amemuambatanisha[7] , na mwenye kumuambatanisha amemfanya kuwa wawili[8] , na mwenye kumfanya kuwa wawili atakuwa amemfanya kuwa mwenye sehemu sehemu, na mwenye kumfanya kuwa mwenye sehemu sehemu atakuwa hamjui (s.w.t), na asiyemjua atakuwa amemuonyesha, na mwenye kumuonyesha atakuwa amemwekea mipaka [9] , na mwenye kumuwekea mipaka atakuwa amemuhesabu [10] .

وَمَنْ أشَارَ إِلَيْهِ فَقَدْ حَدَّهُ، وَمَنْ حَدَّهُ فَقَدْ عَدَّهُ، وَمَنْ قَالَ: «فِيمَ» فَقَدْ ضَمَّنَهُ، وَمَنْ قَالَ: «عَلاَمَ؟» فَقَدْ أَخْلَى مِنُهُ كائِنٌ لاَ عَنْ حَدَث، مَوْجُودٌ لاَ عَنْ عَدَم، مَعَ كُلِّ شَيْء لاَ بِمُقَارَنَة، وَغَيْرُ كُلِّ شيء لا بِمُزَايَلَة، فَاعِلٌ لا بِمَعْنَى الْحَرَكَاتِ وَالاْلةِ، بَصِيرٌ إذْ لاَ مَنْظُورَ إلَيْهِ مِنْ خَلْقِهِ، مُتَوَحِّدٌ إذْ لاَ سَكَنَ يَسْتَأْنِسُ بهِ وَلاَ يَسْتوْحِشُ لِفَقْدِهِ

Na mwenye kusema yuko ndani ya nini? Anakuwa amemwingiza (s.w.t) ndani ya kitu[11] . Na mwenye kusema yuko juu ya nini? Atakuwa amemtoa humo[12] . Amekuwa yupo sio kwa kutukia, yupo lakini sio kwa maana ya hakuwapo hapo kabla. Yuko pamoja na kila kitu si kwa mwambatano wa kimwili[13] . Yutafauti na kila kitu si utafauti wa kimwili, mtendaji sio kwa maana ya harakati za kimwili na vyombo, mwenye kuona pindi hakuna wakuonwa kati ya viumbe wake. Yu pweke pindi hakuna mkazi analiwazika naye wala haoni ukiwa kwa kukosekana kwake.

KUUMBWA KWA ULIMWENGU:

أَنْشَأَ الخَلْقَ إنْشَاءً، وَابْتَدَأَهُ ابْتِدَاءً، بِلاَ رَوِيَّة أَجَالَهَا، وَلاَ تَجْرِبَة اسْتَفَادَهَا، وَلاَ حَرَكَة أَحْدَثَهَا، وَلاَ هَمَامَةِ نَفْس اظْطَرَبَ فِيهَا أَحَالَ الاْشياءَ لأوْقَاتِهَا، وَلاَمَ بَيْنَ مُخْتَلِفَاتِهَا، وَغَرَّزَ غَرائِزَهَا، وَأَلزَمَهَا أشْبَاحَهَا، عَالِماً بِهَا قَبْلَ ابْتِدَائِهَا، مُحِيطاً بِحُدُودِها وَانْتِهَائِهَا، عَارفاً بِقَرَائِنِها وَأَحْنَائِهَا

Alianza kuumba viumbe mwanzo, na kuvibuni kwa ubunifu, bila ya kupitisha fikra, wala kufaidika na uzoefu wowote, wala hakufanya harakati yeyote, wala kusumbuliwa na azma ya ndani ya nafsi, amevitoa viumbe (kutoka hakuna kitu na kuviingiza) kwenye ulimwengu wa kuwepo kwa wakati wake.

Akaviunganisha viumbe pamoja na tofauti zao. Akaweka silika zao, na akaziambatanisha hizo silika na wenyewe. Akiwa mjuzi (s.w.t) kabla hajabuni (viumbe) akiwa mwenye kuelewa kwa ukamilifu, mipaka yao na mwisho wao, akiwa mwenye kutambua utashi wao na sehemu zao nyingi.

ثُمَّ أَنْشَأَ ـ سُبْحَانَهُ ـ فَتْقَ الاْجْوَاءِ، وَشَقَّ الاْرْجَاءِ، وَسَكَائِكَ الَهوَاءِ، فأَجازَ فِيهَا مَاءً مُتَلاطِماً تَيَّارُهُ، مُتَراكِماً زَخَّارُهُ، حَمَلَهُ عَلَى مَتْنِ الرِّيحِ الْعَاصِفَةِ، وَالزَّعْزَعِ الْقَاصِفَةِ، فَأَمَرَها بِرَدِّهِ، وَسَلَّطَهَا عَلَى شَدِّهِ، وَقَرنَهَا إِلَى حَدِّهِ، الهَوَاءُ مِنْ تَحْتِها فَتِيقٌ، وَالمَاءُ مِنْ فَوْقِهَا دَفِيقٌ

Kisha aliumba (s.w.t) mwanya wa anga na eneo la mbingu na utando wa upepo, alimimina humo maji ambayo mawimbi yake yalikuwa makali na mawimbi yalilundikana moja juu ya jingine, aliyabebesha kwenye upepo uendao kwa kasi, na mtikisiko mkali, na kimbunga kinachovunja. Aliyaamrisha yamwage (mvua) aliufanya upepo uwe na uwezo wa kuzuia nguvu za mvua na kuijulisha mipaka yake. Upepo ulivuma chini hali maji yalibubujika kwa kasi kwa upande wa juu.

ثُمَّ أَنْشَأَ سُبْحَانَهُ رِيحاً اعْتَقَمَ مَهَبَّهَا، وَأَدَامَ مُرَبَّهَا، وَأَعْصَفَ مَجْرَاها، وَأَبْعَدَ مَنْشَاهَا، فَأَمَرَها بِتَصْفِيقِ المَاءِ الزَّخَّارِ، وَإِثَارَةِ مَوْجِ البِحَارِ، فَمَخَضَتْهُ مَخْضَ السِّقَاءِ، وَعَصَفَتْ بهِ عَصْفَهَا بِالفَضَاءِ.

Kisha (s.w.t) aliumba upepo ambao ulifanya mvumo wake uwe tasa. Yaani mvumo wa hewa ulifanywa usioweza kurutubisha kizazi, kwa kuwa kuna upepo urutubishao mimea na kuifanya itoe mazao. Na upepo huu uli- umbwa ili kuyatikisa maji tu. Na akadumisha kubaki kwake, mwendo wake ulishika kasi na akayatawanya kwa umbali na kwa upana.

تَرُدُّ أَوَّلَهُ عَلَى آخِرِهِ، وَسَاجِيَهُ عَلَى مَائِرِهِ، حَتَّى عَبَّ عُبَابُهُ، وَرَمَى بِالزَّبَدِ رُكَامُهُ، فَرَفَعَهُ فِي هَوَاء مُنْفَتِق، وَجَوٍّ مُنْفَهِق، فَسَوَّى مِنْهُ سَبْعَ سَموَات، جَعَلَ سُفْلاَهُنَّ مَوْجاً مَكْفُوفاً، وَعُلْيَاهُنَّ سَقْفاً مَحْفُوظاً، وَسَمْكاً مَرْفُوعاً، بِغَيْر عَمَد يَدْعَمُهَا، وَلا دِسَار يَنْظِمُها ثُمَّ زَيَّنَهَا بِزينَةِ الكَوَاكِبِ، وَضِياءِ الثَّوَاقِبِ، وَأَجْرَى فِيها سِرَاجاً مُسْتَطِيراً، وَقَمَراً مُنِيراً: في فَلَك دَائِر، وَسَقْف سَائِر، وَرَقِيم مَائِر.

Kisha aliuamrisha upepo kuyanyanyua maji yalio kwenye kina, na kuongeza kasi ya mawimbi ya bahari. Yakatikisa mtikiso kama ule ufanywao kwa kinywaji cha maziwa. Na kuvuma nayo angani. (Anakusudia kueleza kuwa upepo ukivuma angani anga ambazo ziko tupu huwa mvumo wake mkali kwa sababu ya kutozuilika na kitu chochote, na upepo huu ulivuma na maji mengi mvumo mkali sana). Wayarudisha ya mwanzo nyuma na yaliyotulia kuyapeleka kwa yaliyo kwenye mtikisiko, mpaka yakainuka mwinuko. Na sehemu ya chini ilijaa povu. Baadaye Mungu (s.w.t) aliinua povu lile juu ya upepo ulio wazi kutoka humo aliumba mbingu Saba. Na sehemu ya mawimbi ya chini aliyazuia na kuwa kituo, na ya juu kuwa kama dari inayo zuia na jumba lililoinuka bila ya nguzo zenye kulikinga, wala misumari inayo imarisha, kisha alizipamba (mbingu) kwa mapambo ya nyota na mianga yenye nuru. Na alipitisha humo jua lenye taa yenye kuenea mwanga wake. Na mwezi wenye nuru katika sayari zinazozunguka. Na dari inayokwenda, na ubao uendao[14] .

KUUMBA MALAIKA

ثُمَّ فَتَقَ مَا بَيْنَ السَّمواتِ العُلاَ، فَمَلاَهُنَّ أَطْواراً مِنْ مَلائِكَتِهِ : مِنْهُمْ سُجُودٌ لاَيَرْكَعُونَ، وَرُكُوعٌ لاَ يَنْتَصِبُونَ، وَصَافُّونَ لاَ يَتَزَايَلُونَ، وَمُسَبِّحُونَ لاَ يَسْأَمُونَ، لاَ يَغْشَاهُمْ نَوْمُ العُيُونِ، وَلاَ سَهْوُ العُقُولِ، وَلاَ فَتْرَةُ الاَبْدَانِ، ولاَ غَفْلَةُ النِّسْيَانِ.

Kisha aliumba mwanya kati ya mbingu za juu na kuzijaza malaika wake wenye daraja tofauti[15] .Mabingwa wa ibada, miongoni mwao kuna ambao wamesujudu na wala hawarukuu, na kuna waliorukuu na wala hawasimami, kuna waliosimama katika safu na wala hawatawanyiki kuna wanaosabihi na wala hawachoki, hawasinzii, wala hapitiwi, wala hawanyong’onyei, wala kughafilika kwa kusahau.

وَمِنْهُمْ أُمَنَاءُ عَلَى وَحْيِهِ، وأَلسِنَةٌ إِلَى رُسُلِهِ، وَمُخْتَلِفُونَ بِقَضَائِهِ وَأَمْرهِ وَمِنْهُمُ الحَفَظَةُ لِعِبَادِهِ، وَالسَّدَنَةُ لاِبْوَابِ جِنَانِهِ

b. Miongoni mwao kuna waaminifu wa wahyi wa Mungu, na ni ndimi zitamkazo ndani ya vinywa vya mitume Wake, na wanaopokezana kwa hukumu na amri zake (kupitia wao Mungu hupitisha hukumu kwa amtakae kwa apendacho).

وَمِنْهُمُ الثَّابِتَةُ في الاْرَضِينَ السُّفْلَى أَقْدَامُهُمْ، وَالمَارِقَةُ مِنَ السَّماءِ العُلْيَا أَعْنَاقُهُمْ، والخَارجَةُ مِنَ الاَقْطَارِ أَرْكَانُهُمْ، وَالمُنَاسِبَةُ لِقَوَائِمِ العَرْشِ أَكْتَافُهُمْ، نَاكِسَةٌ دُونَهُ أَبْصارُهُمْ، مُتَلَفِّعُونَ تَحْتَهُ بِأَجْنِحَتِهِمْ، مَضْرُوبَةٌ بَيْنَهُمْ وَبَيْنَ مِنْ دُونَهُمْ حُجُبُ العِزَّةِ، وَأسْتَارُ القُدْرَةِ، لاَ يَتَوَهَّمُونَ رَبَّهُمْ بالتَّصْوِيرِ، وَلاَ يُجْرُونَ عَلَيْهِ صِفَاتِ المَصْنُوعِينَ، وَلاَ يَحُدُّونَهُ بِالاْماكِنِ، وَلاَ يُشِيرُونَ إِلَيْهِ بِالنَّظَائِرِ

c. Malaika wahifadhi wa waja Wake (s.w.t), kana kwamba wao ni nguvu iliyowekwa ndani ya miili ya wanadamu na nafsini mwao. Na miongoni mwao wamo ambao miguu yao imeimarika katika ardhi ya chini, na shingo zao zimechomoza kwenye mbingu ya juu, na nguzo zao zimezidi kwenye peo (horizon), na mabega yamelingana na nguzo za Arshi, wenye kuinamisha macho yao mbali na Arshi, wenye kuizingira kwa mbawa zao, imepigwa pazia ya utukufu kati yao na wasiokuwa wao na stara ya uwezo, hawamfanyii taswira Mola wao, wala hawampitishii sifa za viumbe, wala hawamuwekei mipaka ya mahali, wala hawamuashirii kwa mifano.

KUUMBWA KWA ADAM(A.S)

ثُمَّ جَمَعَ سُبْحَانَهُ مِنْ حَزْنِ الاْرْضِ وَسَهْلِهَا، وَعَذْبِهَا وَسَبَخِهَا، تُرْبَةً سَنَّهَا بالمَاءِ حَتَّى خَلَصَتْ، وَلاَطَهَا بِالبَلَّةِ حَتَّى لَزَبَتْ، فَجَبَلَ مِنْها صُورَةً ذَاتَ أَحْنَاء وَوُصُول، وَأَعْضَاء وَفُصُول: أَجْمَدَهَا حَتَّى اسْتَمْسَكَتْ، وَأَصْلَدَهَا حَتَّى صَلْصَلَتْ، لِوَقْت مَعْدُود، وَأجَل مَعْلُوم.

Kisha (s.w.t) alikusanya aina za udongo: Ngumu, laini, tamu, chachu, udongo ambao aliumwagia maji mpaka ukalowana, na aliukanda kwa unyevunyevu mpaka ukaganda, kutoka humo aliumba sura yenye pande tofauti, na viungo tanzu, sehemu ya pingili aliigandisha na ikashikamana, akaifanya kuwa ngumu mpaka ikawa ngumu, kiasi cha kusikika sauti, kwa wakati uliowekwa kwa muda ujulikanao.

ثُمَّ نَفَخَ فِيها مِنْ رُوحِهِ فَمَثُلَتْ إِنْساناً ذَا أَذْهَان يُجيلُهَا، وَفِكَر يَتَصَرَّفُ بِهَا، وَجَوَارِحَ يَخْتَدِمُهَا، وَأَدَوَات يُقَلِّبُهَا، وَمَعْرِفَة يَفْرُقُ بِهَا بَيْنَ الحَقِّ وَالبَاطِلِ، والاَذْوَاقِ والَمشَامِّ، وَالاْلوَانِ وَالاْجْنَاس، مَعْجُوناً بطِينَةِ الاْلوَانِ الُمخْتَلِفَةِ، وَالاَشْبَاهِ المُؤْتَلِفَةِ، وَالاْضْدَادِ المُتَعَادِيَةِ، والاَخْلاطِ المُتَبَايِنَةِ، مِنَ الحَرِّ والبَرْدِ، وَالبَلَّةِ وَالْجُمُودِ، وَالْمَساءَةِ وَالسُّرُورِ.

Baadaye alipulizia humo roho, akawa mtu mwenye akili imsukumayo, na fikra aitumikishayo, na viungo vya mwili avitumiavyo, na ala zimsaidiazo kubadilisha hali yake, na maarifa ambayo kwayo anatofautisha kati ya haki na batili, akiwa na uwezo wa kuonja, na kunusa, kupambanua rangi, na jinsi yenye mchanganyiko wa udongo wa rangi tofauti, na vitu vyenye kufanana na kuafikiana, vitu vilivyo kinyume na visivyoafikiana. Aina tofauti za mchanganyiko: kama vile joto, baridi, hali ya chepe, ugumu, chuki, furaha.

وَاسْتَأْدَى اللهُ سُبْحَانَهُ المَلائكَةَ وَدِيعَتَهُ لَدَيْهِمْ، وَعَهْدَ وَصِيَّتِهِ إِلَيْهمْ، في الاْذْعَانِ بالسُّجُودِ لَهُ، وَالخُنُوعِ لِتَكْرِمَتِهِ، فَقَالَ عزَّمِن قائِل: (اسْجُدُوا لاِدَمَ فَسَجَدُوا إِلاَّ إِبْلِيسَ) وَقَبِيلَهُ، اعْتَرَتْهُمُ الحَمِيَّةُ، وَغَلَبَتْ عَلَيْهِمُ الشِّقْوَةُ، وَتَعَزَّزُوا بِخِلْقَةِ النَّارِ، وَاسْتَوْهَنُوا خَلْقَ الصَّلْصَالِ، فَأَعْطَاهُ اللهُ تَعالَى النَّظِرَةَ اسْتِحْقَاقاً لِلسُّخْطَةِ، وَاسْتِتْماماً لِلْبَلِيَّةِ، وَإِنْجَازاً لِلْعِدَةِ، فَقَالَ: (إنَّكَ مِنَ المُنْظَرِينَ إِلَى يَوْمِ الْوَقْتِ الْمَعْلُومِ)

Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwataka malaika watekeleze ahadi aliyowekeana nao, na kutimiza agizo lake la kuwataka wamsujudie Adamu, na kunyenyekea ili kumpa heshima, akasema (s.w.t): “Msujudiyeni Adamu, wote walisujudu isipokuwa iblisi ”. Quran 2:34. Yeye alijiona, akazidiwa na uovu, akajitukuza na kufanya kibri kwa sababu ya kuumbwa kutokana na moto. Alikebehi asili ya umbo la Adamu, yaani udongo. Mwenyezi Mungu Mtukufu alimpa (Ibilisi) muda ili ghadhabu ithibiti kwake. Na kukamilisha mtihani ( kwa mwanadamu) na kutekeleza ahadi, akasema: “Basi kwa hakika umekwisha kuwa mingoni mwa waliopewa muhula mpaka ya siku ya wakati maalum ” (15:38, 38:81).

ثُمَّ أَسْكَنَ سُبْحَانَهُ آدَمَ دَاراً أرْغَدَ فِيهَاعَيْشَهُ، وَآمَنَ فِيهَا مَحَلَّتَهُ، وَحَذَّرَهُ إِبْلِيسَ وَعَدَاوَتَهُ، فَاغْتَرَّهُ عَدُوُّهُ نَفَاسَةً عَلَيْهِ بِدَارِ الْمُقَامِ، وَمُرَافَقَةِ الاْبْرَارِ، فَبَاعَ الْيَقِينَ بِشَكِّهِ، وَالعَزِيمَةَ بِوَهْنِهِ، وَاسْتَبْدَلَ بِالْجَذَلِ وَجَلاً، وَبِالاْغْتِرَارِ نَدَماً ثُمَّ بَسَطَ اللهُ سُبْحَانَهُ لَهُ في تَوْبَتِهِ، وَلَقَّاهُ كَلِمَةَ رَحْمَتِهِ، وَوَعَدَهُ المَرَدَّ إِلَى جَنَّتِهِ، فَأَهْبَطَهُ إِلَى دَارِ الَبَلِيَّةِ، وَتَنَاسُلِ الذُّرِّيَّةِ

Baadaye Mwezi Mungu Mtukufu alimuweka Adamu peponi ambapo aliyafanya maisha yake yakuridhisha, na kubaki kwa amani. Alimtahadharisha na Ibilisi na uadui wake. Adui yake (ambae ni Ibilisi) alimghuri. Akimwonea wivu kubaki kwake milele Peponi akiwa na watendao mema. Akauza yakini kwa shaka yake, na azma kwa unyonge wake, na furaha aliibadilisha kwa woga. Na kuhadaika ikawa ni majuto. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu alimpa Adamu fursa ya kutubia. Alimfundisha neno la rehema Zake. Na alimuahidi kumrudisha kwenye Pepo yake. Alimteremsha duniani kwenye makazi ya mtihani, nyumba ya majaribu, na kuzaa watoto.

KUTEULIWA KWA MANABII(A.S)

وَاصْطَفى سُبْحَانَهُ مِنْ وَلَدَهِ أَنْبيَاءَ أَخَذَ عَلَى الْوَحْيِ مِيثَاقَهُمْ، وَعَلَى تَبْليغِ الرِّسَالَةِ أَمَانَتَهُمْ، لَمَّا بَدَّلَ أَكْثَرُ خَلْقِهِ عَهْدَ اللهِ إِلَيْهِمْ، فَجَهِلُوا حَقَّهُ، واتَّخَذُوا الاْنْدَادَ مَعَهُ، وَاجْتَالَتْهُمُ الشَّيَاطِينُ عَنْ مَعْرفَتِهِ، وَاقتَطَعَتْهُمْ عَنْ عِبَادَتِهِ.

Mwezi Mungu Mtukufu aliwateua manabii katika kizazi chake - watoto wa Adamu(a.s) - akachukuwa kwao ahadi kwa ajili ya wahyi, na kuchukuwa dhamana kwao kwa ajili ya kuifikisha risala - Ujumbe - lakini wengi katika viumbe Wake walivyobadili ahadi ya Mungu walipotosha agizo lake (s.w.t) kwao wakapuuza haki yake wakamfanyia washirika pamoja naye. Shetani aliwapotosha mbali na kumtambua Yeye. Na aliwaweka mbali na ibada yake.

فَبَعَثَ فِيهمْ رُسُلَهُ، وَوَاتَرَ إِلَيْهِمْ أَنْبِياءَهُ، لِيَسْتَأْدُوهُمْ مِيثَاقَ فِطْرَتِهِ، وَيُذَكِّرُوهُمْ مَنْسِيَّ نِعْمَتِهِ، وَيَحْتَجُّوا عَلَيْهِمْ بَالتَّبْلِيغِ، وَيُثِيرُوا لَهُمْ دَفَائِنَ الْعُقُولِ، وَيُرُوهُمْ آيَاتِ الْمَقْدِرَةِ: مِنْ سَقْف فَوْقَهُمْ مَرْفُوع، وَمِهَاد تَحْتَهُمْ مَوْضُوع، وَمَعَايِشَ تُحْيِيهِمْ، وَآجَال تُفْنِيهمْ، وَأَوْصَاب تُهْرِمُهُمْ، وَأَحْدَاث تَتَابَعُ عَلَيْهِمْ.

Aliwatuma kwao Mitume wake, aliwapeleka manabii wake kwao kwa vipindi: Ili watekeleze ahadi ya kuumba kwao, na wakumbushe neema zake zilizosahauliwa, na ili watoe hoja kwao kwa kufikisha ujumbe. Ili kuamsha vipaji vya hikima vilivyofichikana. Na kuwaonesha alama za uwezo wake wa kila kitu kama vile mbingu zilizoinuliwa na ardhi iliotandikwa chini yao, na sababu za maisha zinazowapa uhai, na ajali zinazowamaliza, na taabu zinazowazeesha na matukio yanayofululiza kwao.

وَلَمْ يُخْلِ اللهُ سُبْحَانَهُ خَلْقَهُ مِنْ نَبِيٍّ مُرْسَل، أَوْ كِتَاب مُنْزَل، أَوْ حُجَّة لاَزِمَة، أَوْ مَحَجَّة قَائِمَة، رُسُلٌ لا تُقَصِّرُ بِهِمْ قِلَّةُ عَدَدِهِمْ، وَلاَ كَثْرَةُ المُكَذِّبِينَ لَهُمْ: مِنْ سَابِق سُمِّيَ لَهُ مَنْ بَعْدَهُ، أَوْ غَابِر عَرَّفَهُ مَنْ قَبْلَهُ عَلَى ذْلِكَ نَسَلَتِ القُرُونُ، وَمَضَتِ الدُّهُورُ، وَسَلَفَتِ الاْباءُ، وَخَلَفَتِ الاْبْنَاءُ.

Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuwaacha viumbe wake bila ya nabii mwenye kutumwa, au bila ya Kitabu kilichoteremshwa, au bila ya hoja ya lazima, au bila ya njia iliyonyooka. Hawa wajumbe, hawakujihisi kuwa wachache kwa udogo wa idadi yao wala kwa ukubwa wa idadi ya wanaowakadhibisha. Miongoni mwao aliyetangulia humtaja anayefuata baada yake au mfuasi aliyetambulishwa na mtangulizi wake. Kwa utaratibu huo karne baada ya karne zilipita, vilizaliwa vizazi. Miaka ikapita, mababa walipita na watoto walichukua nafasi.

KUTUMWA KWA MUHAMMAD (s.a.w.w)

إِلَى أَنْ بَعَثَ اللهُ سُبْحَانَهُ مُحَمَّداً(صلى الله عليه وآله) لاِنْجَازِ عِدَتِهِ وَتَمامِ نُبُوَّتِهِ، مَأْخُوذاً عَلَى النَّبِيِّينَ مِيثَاقُهُ، مَشْهُورَةً سِمَاتُهُ، كَرِيماً مِيلادُهُ

Hali iliendelea hivyo mpaka Allah (s.w.t) alipomtuma Muhammad(s.a.w.w) , mjumbe Wake ili kutimiza idadi Yake, na kukamilisha unabii Wake. Akiwa mwenye kuchukua ahadi Yake kutoka kwa manabii, alama zake(s.a.w.w) zilikuwa mashuhuri, uzao wake ni wa heshima.

وَأهْلُ الاْرْضِ يَوْمَئِذ مِلَلٌ مُتَفَرِّقَةٌ، وَأَهْوَاءٌ مُنْتَشِرَةٌ، وَطَرَائِقُ مُتَشَتِّتَةٌ، بَيْنَ مُشَبِّه للهِ بِخَلْقِهِ، أَوْ مُلْحِد في اسْمِهِ، أَوْ مُشِير إِلَى غَيْرهِ

Watu wa dunia hii wakati huo walikuwa kwenye itikadi zinazotofautiana, tamaa za nafsi zimeenea, na njia zikiwa tofauti, wakiwemo waliomshabihisha Mungu (s.w.t.) na viumbe Wake au wenye kupotosha jina lake (s.w.t) au wenye kumshirikisha na viumbe.

فَهَدَاهُمْ بهِ مِنَ الضَّلاَلَةِ، وَأَنْقَذَهُمْ بمَكانِهِ مِنَ الجَهَالَةِ ثُمَّ اخْتَارَ سُبْحَانَهُ لِمحَمَّد صلى الله عليه لِقَاءَهُ، وَرَضِيَ لَهُ مَا عِنْدَهُ، فَأَكْرَمَهُ عَنْ دَارِالدُّنْيَا، وَرَغِبَ بِهَ عَنْ مُقَارَنَةِ البَلْوَى، فَقَبَضَهُ إِلَيْهِ كَرِيماً.

Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaongoza kupitia kwake kutokana na upotovu, na kwa nafasi yake(s.a.w.w) aliwaokoa mbali na ujahili. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu alimhitari Muhamamd(s.a.w.w) kukutana naye na alimridhia ili awe karibu Yake (s.w.t), na alimzidishia heshima kwa kumwondoa duniani mahali pa majaribu, kwa hiyo alimchukuwa Kwake(s.a.w.w) kwa heshima.

وَخَلَّفَ فِيكُمْ مَا خَلَّفَتِ الاْنْبيَاءُ في أُمَمِها، إذْ لَم يَتْرُكُوهُمْ هَمَلاً، بِغَيْر طَريق واضِح، ولاَعَلَم قَائِم

Na aliacha kwenu ambayo manabii waliacha katika Umma zao[16] . Kwani hawakuwaacha wamepuuzwa, bila ya kuwaeleza njia iliyowazi, wala watakayoongoka kwayo.

KITABU CHA MWENYEZI MUNGU NA SUNNAH

كِتَابَ رَبِّكُمْ [فِيكُمْ:] مُبَيِّناً حَلاَلَهُ وَحَرامَهُ، وَفَرَائِضَهُ وَفَضَائِلَهُ، وَنَاسِخَهُ وَمَنْسُوخَهُ، وَرُخَصَهُ وَعَزَائِمَهُ، وَخَاصَّهُ وَعَامَّهُ، وَعِبَرَهُ وَأَمْثَالَهُ، وَمُرْسَلَهُ وَمَحْدُودَهُ، وَمُحْكَمَهُ وَمُتَشَابِهَهُ، مُفَسِّراً جُمَلَهُ، وَمُبَيِّناً غَوَامِضَهُ

Amekuachieni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, Mola wenu: kibainishacho halali yake na haramu yake[17] . Faradhi zake na fadhila zake. Batilisho (nasikh) zake na zilizobatilishwa (mansukh) zake, ruhusa zake na azma zake, hukumu ambazo ni makhsusi, na ambazo zipo katika sura ya jumla, na ambazo zina mafunzo ndani yake na mithali, ndefu na fupi, thabiti zake na mutashabih zake: zilizo wazi na ambazo ni ngumu kueleweka maana yake, zenye kufasiri aya zilizokuja kwa maana ya jumla, na zenye kubainisha maana zake ngumu.

بَيْنَ مَأْخُوذ مِيثَاقُ عِلْمِهِ، وَمُوَسَّع عَلَى العِبَادِ في جَهْلِهِ، وَبَيْنَ مُثْبَت في الكِتابِ فَرْضُهُ، وَمَعْلُوم في السُّنَّهِ نَسْخُهُ، وَوَاجب في السُّنَّةِ أَخْذُهُ، وَمُرَخَّص في الكِتابِ تَرْكُهُ.

Humo kuna aya ambazo kuzijua ni lazima, na kuna ambazo watu wanaruhusiwa kutozijua. Na ambazo imethibiti Kitabuni faradhi yake, na zajulikana kutenguliwa katika sunnah, na ambazo ni wajibu katika sunnah kuzitekeleza, na ambazo katika kitabu zaruhusiwa kuziacha.

وَبَيْنَ وَاجِب بِوَقْتِهِ، وَزَائِل في مُسْتَقْبَلِهِ، وَمُبَايَنٌ بَيْنَ مَحَارِمِهِ، مِنْ كَبير أَوْعَدَ عَلَيْهِ نِيرَانَهُ، أَوْ صَغِير أَرْصَدَ لَهُ غُفْرَانَهُ، وَبَيْنَ مَقْبُول في أَدْنَاهُ، ومُوَسَّع في أَقْصَاهُ

Na kuna ambazo ni wajibu kwa wakati wake, na wenye kuondoka wakati ujao, uharamu wake pia watofautiana, kuna ambazo ni kubwa ametishia kwa (kosa hilo) moto wake, au ndogo zenye ghofrani yake, na kati ya yanayokubalika uchache wake na yenye wasaa katika umbali wake. Kuna ambazo uchache wake wakubaliwa (kwa Mungu) na zenye uwezekano wa kutanuliwa (hukumu yake)[18] .

NDANI YA KHUTBA HII AELEZEA HIJJA

وَفَرَضَ عَلَيْكُمْ حَجَّ بَيْتِهِ الحَرَامِ، الَّذِي جَعَلَهُ قِبْلَةً لِلاْنَامِ، يَرِدُونَهُ وُرُودَ الاَنْعَامِ، وَيأْلَهُونَ إِلَيْهِ وُلُوهَ الحَمَامِ

Na amewajibisha juu yenu kuhiji nyumba yake tukufu, ambayo ameifanya Qibla kwa wanadamu, wanaiendea kama wanyama walazimikapo kuyaendea manyweo ya maji wanayahamanikia uhamanikaji wa njiwa.

جَعَلَهُ سُبْحَانَهُ عَلاَمَةً لِتَوَاضُعِهمْ لِعَظَمَتِهِ، وَإِذْعَانِهِمْ لِعِزَّتِهِ، وَاخْتَارَ مِنْ خَلْقِهِ سُمَّاعاً أَجَابُوا إِلَيْهِ دَعْوَتَهُ، وَصَدَّقُوا كَلِمَتِهُ، وَوَقَفُوا مَوَاقِفَ أَنْبِيَائِهِ، وَتَشَبَّهُوا بمَلاَئِكَتِهِ المُطِيفِينَ بِعَرْشِهِ، يُحْرِزُونَ الاْرْبَاحَ فِي مَتْجَرِ عِبَادَتِهِ، وَيَتَبَادَرُونَ عِنْدَهُ مَوْعِدَ مَغْفِرَتِهِ

Mwenyezi Mungu Mtukufu ameifanya (Kaaba) iwe ndio alama ya unyenyekevu wao kuunyenyekea utukufu Wake, na utii wao kwa enzi Yake. Amechagua kutoka kwa viumbe Wake watiifu walioitikia wito wake. Na wamesadikisha neno Lake. Na wakasimama msimamo wa manabii Wake. Wakashabihiana na malaika wake wazungukao Arshi Yake. Wanafaidika na biashara ya ibada yake. Wakiharakia kwenye ahadi ya msamaha Wake.

جَعَلَهُ سُبْحَانَهُ لِلاِسْلامِ عَلَماً، وَلِلْعَائِذِينَ حَرَماً، فَرَضَ حَجَّهُ، وَأَوْجَبَ حَقَّهُ، وَكَتَبَ عَلَيْكُمْ وِفَادَتَهُ، فَقَالَ سُبْحَانَهُ: (وَللهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلاً وَمَنْ كَفَرَ فَإِنَّ اللهَ غَنِيٌّ عَنِ العَالَمينَ.

Mungu (s.w.t.) ameifanya (nyumba hii) kuwa ni alama ya Uislamu na ni lengo la heshima kwa wanaojikinga nayo.

Amefaradhisha haki yake, na kulazimisha kuihiji. Na amefanya faradhi juu yenu kuiendea aliposema (s.w.t.): “Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awazae njia ya kwendea. Na atakayekanusha basi Mwenyezi Mungu si mhitaji kwa walimwengu. (3:97).

2

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU

I- UISLAMU NA MAISHA YA KISASA

Suala la dini na maisha ya kisasa ni moja ya mambo ambayo hayawagusi Waislamu peke yao. Dini nyingine pia zilikumbana na tatizo hili. Watu wengi wenye kupendelea mabadiliko duniani, wameikana dini kwa sababu wanaamini kuwa dini na maisha ya sasa haviendi pamoja. Wanafikiri kuwa kudumaa, kutuama na kutobadilika ni sifa za lazima za mtu mshika dini. Kwa maneno mengine, wanafikiri kuwa kudumaa na ukinaifu unatokana na kutokuwepo kwa mabadiliko na kwamba kudumisha hali ya kizamani ndio tabia za dini.

Marehemu Bwana Nehru aliyekuwa waziri Mkuu wa India alikuwa na mawazo ya kisekula na hakuwa akiamini dini yoyote. Inaoinekana kutokana na kauli zake kuwa kilichomfanya asipende dini ni kutobadilika kwake na ukinaifu unaotokana na kutokuwepo kwa mabadiliko. Kuelekea kipindi cha mwisho cha maisha yake Nehru alihisi kuwa na uwazi moyoni mwake na aliamini kuwa uwazi ule ungezibwa na nguvu ya kiroho tu.

Lakini hakuelekea kuiamini dini yoyote kwa sababu aliamini kuwa hali ya ukinaifu na kutokuwepo kwa mabadiliko ilikuwepo katika dini zote. Mwandishi wa habari wa Kihindi, aitwaye Karanjia, alimhoji Nehru katika kipindi chake cha mwisho mwisho cha uhai wake (Nehru) na alivyoonekana haya yalikuwa ni mahojiano ya mwisho ambapo Nehru alitoa maoni yake juu ya matatizo ya jumla ya ulimwengu.

Alipokuwa akimzungumzia Gandhi, Karanjia alisema, "Baadhi ya wanaopendelea mabadiliko (liberals) na maendeleo wanaamini kuwa Gandhiji, kwa kupitia na kwa kutokana na utatuzi wake wa matatizo kwa hisia kali, unyofu na njia za kiroho, zimedhoofisha na kuitia ubaridi imani yako ya asili ya ujamaa wa kisayansi." Katika kulijibu hili, Nehru alisema; "Ni muhimu na vizuri kutumia fursa ya njia za kimaadili na kiroho.

Mara zote nimekubaliana na Gandhiji juu ya hili. Ninaamini kuwa ni muhimu zaidi kutumia fursa ya njia hizi, kwani sasa, kwa kiasi kikubwa kuliko ilivyokuwa huko nyuma, tunahitaji majibu ya kiroho na kimaadili juu ya maswali yanayotokana na pengo la kimaadili linalosababishwa na tamaduni za kisasa, ambazo zinazidi kuwa maarufu." Kisha Kiranjia aliuliza swali juu ya Ukomunisti.

Nehru alikiri mapungufu yake na katika majibu yake alionyesha baadhi ya mapungufu na ubovu wake (wa ukomunisti). Kwa mara nyingine tena alipendekeza suluhisho la kiroho juu ya matatizo ya dunia. Alipofika hapa Karanjia akasema; "Bwana Nehru, je dhana yako ya utatuzi wa matatizo ya kimaadili na kiroho haikufanyi uwe tofauti na Jawahanal wa jana? (Nehru mwenyewe enzi za ujana wake).

Ulichokisema kinaonyesha kuwa Bwana Nehru, katika kuelekea mwisho wa uhai wake, ameanza kumtafuta Mungu." Nehru alisema; "Ndiyo, nimebadilika. Msisitizo wangu juu ya unyofu na maadili ya kiroho na utatuzi wa matatizo sio wa bahati mbaya." Akaongeza kuwa; "Swali sasa ni jinsi ya kukuza maadili na imani ya kiroho katika daraja la juu zaidi.

Hapana shaka kwamba kwa ajili ya hili, dini zipo, lakini kwa bahati mbaya zimechukua mtazamo finyu na matendo yasiyobadilika na zimebaki kuwa taratibu rasmi lakini duni. Ni umbo lake la nje tu lililobaki, lakini ari na dhana yake ya kweli imetoweka." Uislamu na mahitaji ya wakati. Katika dini zote ni Uislamu tu unaojihusisha zaidi na vipengele vyote vya maisha ya mwanadamu.

Mafundisho yake hayajajikita katika matendo ya ibada na sala na mfumo wa ushauri wa maadili peke yake. Uislamu, kama ulivyoshughulikia uhusiano wa watu na Mwenyezi Mungu, ndivyo hivyohivyo ulivyoshughulikia mahusiano baina ya watu. Katika sura mbali mbali Uislamu umeshughulikia haki za watu binafsi na majukumu yao pia.

Hii ndio sababu swali kwamba mafundisho yake yanafaa kutumika au la katika mazingira yanayozidi kubadilika ni thabiti zaidi katika suala la Uislamu kuliko dini nyingine yoyote. Kwa bahati imetokea kwamba, wasomi wengi na waandishi wasiokuwa Waislamu wamezisoma sheria za kijamii na kiraia (za madai na za jinai) na wamezisifu kuwa ni chombo cha kisheria cha kimaendeleo na endelevu.

Wameusifu Uislamu kwa mapana na marefu, kuwa ni dini hai na itakayodumu milele, na wameuelezea uwezo na sifa za sheria hizi za Kiislamu wa kuweza kutumika nyakati zote na katika hali zote. Mwandishi maarufu sana wa Kiingereza aliyekuwa akipendelea msimamo wa wastani (liberal), Bernard Shaw amesema; "Mara zote nimekuwa nikiipa dini ya Muhammad heshima kubwa (daraja kubwa), kutokana na uhai wake wa ajabu.

Ni dini pekee inayoonekana kwangu kuwa na uwezo wa kunyumbulika na hivyo kuweza kutumika katika dunia inayobadilika na katika zama zote. Nimetabiri kuwa imani ya Muhammad itakubaliwa na Ulaya ya kesho, na dalili za hili zinajionyesha hata sasa. Makasisi wa zama za kati aidha kwa sababu ya ujinga au kwa sababu ya kung'ang'ania bila hoja imani zao waliupaka Uislamu rangi mbaya kabisa. Kwa kusema kweli walifundishwa kumchukia mtu huyu, Muhammad na dini yake. Kwao Muhammad alikuwa mpinga Kristo.

Mimi nimemsoma, mtu huyu wa ajabu, na kwa maoni yangu hakuwa mpinga Kristo kabisa na lazima aitwe mkombozi wa wanaadamu. Ninaamini kuwa kama mtu kama yeye angetwaa madaraka /uongozi wa dunia ya sasa angefanikiwa kutatua matatizo katika namna ambayo ingeleta amani na furaha, vitu ambavyo vinahitajika sana kwa sasa. Dr. Shibli Shama'il ni myakinifu wa Kiarabu wa Lebanoni. Kwa mara ya kwanza alitafsiri kitabu cha 'Darwin Kiitwacho 'Origin of Species' kwenda katika lugha ya Kiarabu, pamoja na sharhe ya mwanasayansi wa kijerumani aitwaye Boucher katika kitabu hicho akakipa jina la 'A weapon against religious belief.' ('Silaha dhidi ya imani za kidini.') Ingawa hamwamini Mwenyezi Mungu, haoni aibu kuusifu Uislamu na muasisi wake mtukuka. Ameusifu Uislamu kwa kusema kuwa ni dini hai inayoweza kutumika katika zama zote.

Mtu huyu, katika juzuu ya pili ya kitabu chake kiitwacho, 'Philosophy of Evolution' ambacho amekichapisha kwa Kiarabu, ameandika makala yenye kichwa cha cha habari 'Uislamu na Ustaarabu'. Ameandika makala hii kukanusha madai ya wasio Waislamu kwa kutoa madai kuwa Uislamu ndio uliosababisha kuporomoka kwa hali ya Waislamu. Shibli Shama'il amejaribu kuthibitisha kuwa jambo hasa lililosababisha kuporomoka kwa hali za Waislamu ni wao Waislamu kuyaacha (kuacha kutekeleza) mafundisho ya kijamii ya Uislamu.

Wale wazungu wanaoushambulia Uislamu aidha hawajui au wanafanya hivyo kwa nia mbaya ya kuwafanya watu wa Mashariki (Asia) wazitilie shaka sheria zao na mfumo wao ili kuwafanya wafuate mfumo wa Kimagharibi. Wakati wa zama zetu, suala la iwapo Uislamu unaafikiana na hali halisi ya maisha ya sasa au la limekuwa likiulizwa sana. Tunapata picha ya ndani ya watu hasa wale wanaotoka katika tabaka la wasomi na tunakuta kuwa swali hili linaulizwa zaidi kuliko maswali mengine.

PINGAMIZI

Wakati fulani watu hawa wanatoa hoja za kifalsafa juu ya suala hili kuwa vitu vyote hapa duniani lazima vibadilike. Hakuna kinachobaki vile vile bila kubadilika, na halikadhalika binadamu wanabadilika. Sasa inawezekanaje sheria za Kiislamu zibaki hivyo bila kubadilika kwa zama nenda rudi? Kama tukilitazama swala hili kwa mtazamo wa kifalsafa kabisa, jibu ni rahisi.

Ni vitu (maada) vinavyobadilika kila mara, ambavyo hukua na kuporomoka na ambavyo hupasika katika kugeuka na kuoza. Lakini sheria za ulimwengu hazibadiliki. Kwa mfano, viumbe vyote hai vimegeuka na vimeendelea kugeuka kwa mujibu wa utaratibu na kanuni fulani zilizoelezwa na wanasayansi. Hapana shaka kwamba viumbe hivi vinageuka na kubadilika lakini kanuni zinazotawala mabadiliko haya hazibadiliki. Na sasa tunazungumzia kanuni (sheria) hizi.

Katika hili, hakuna tofauti yoyote iwapo sheria hizi ni za asili au zimetungwa na kukusanywa, kwani inawezekana kwamba sheria ambazo zimetungwa zinaweza kuwa na asili kama chanzo chao na kuafikiana na mchakato wa mabadiliko ya mtu mmoja mmoja na halikadhalika jamii ya wanadamu kwa ujumla.

Hata hivyo, swali kuhusiana na kuafikina au kutoafikiana kwa Uislamu na mahitaji ya muda halina sura ya kiujumla na kifalsafa peke yake. Swali ambalo huulizwa zaidi ni kuwa kwa vile sheria huundwa kukidhi mahitaji ya wanaadamu na mahitaji yenyewe yanabadilika kila mara inawezekanaje sheria hizo za kijamii zibaki hivyo hivyo bila kubadilika? Ni swali zuri.

Na imetokea kuwa tabia za kimiujiza za Uislamu zimewezesha sheria zisizohitaji kubadilishwa kukidhi mahitaji yasiyobadilika ya mtu mmoja na jamii na sheria zinazobadilika badilika kwa mahitaji ya muda mfupi na yanayobadilika. Hii ni sifa ya kipekee ambayo Waislamu wote wajuzi wa mambo ya sheria za kiislamu na waliozisoma sheria zake wanajivunia. Tutalielezea hili vizuri zaidi baadaye. Je mabadiliko ya kijamii yanakwenda na wakati? Kabla ya kuliendea swali hili tungependa kuibua nukta mbili. Nukta ya kwanza ni kuwa watu wengi wanaoongelea maendeleo na mabadiliko ya hali wanadhani kuwa mabadiliko yoyote ya kijamii, hasa kama yametokea nchi za Kimagharibi, basi ni matokeo ya maendeleo.

Hili ni moja ya mawazo potofu liliyoendekezwa na kizazi hiki. Watu wanadhani kuwa kwa vile njia za maisha hubadilika siku hadi siku, zilizo duni hubadilishwa kwa zilizo bora zaidi na sayansi na viwanda vinaboreka kila siku, mabadiliko yote katika maisha ya binadamu ni aina ya maendeleo na kwa hiyo yanafaa kukaribishwa na kupokelewa kwa mikono miwili. Wanafikiri pia kuwa mabadiliko haya hayaepukiki na huja baada ya muda fulani.

Kwa kusema kweli sio kwamba mabadiliko yote ni matokeo ya maendeleo ya sayansi na viwanda wala sio kwamba hayaepukiki. Huku sayansi ikiendelea kukua, asili ya ubinafsi na unyama wa mwanadamu nayo hubaki bila kubadilika. Ujuzi (elimu) na busara humpeleka mtu katika ukamilifu na asili ya unyama wa mwanadamu humsukumia kwenye ufisadi na upotofu.

Asili ya unyama wa mwanadamu mara zote hujaribu kutumia ujuzi kama njia ya kupatia matamanio yake. Kwa kadiri muda unavyokwenda, kwa kadiri maendeleo na mabadiliko yanavyotokea, ufisadi na upotofu ndivyo unavyozidi kukua na kukomaa. Tunapaswa kwenda na wakati lakini wakati huo huo lazima tupige vita ufisadi pia. Mleta mabadiliko (mema) na mpinga mabadiliko (mema) wote wanapigana dhidi ya muda, tofauti yake ni kuwa mleta mabadiliko mema hupigana dhidi ya upotofu unaoletwa na mabadiliko ya muda na mpinga maendeleo (mabadiliko) hupigana dhidi ya mabadiliko (maendeleo halisi) yanayoletwa na mabadiliko ya muda.

Kama tunauchukulia muda na mabadiliiko yake kama kigezo cha mema yoyote na maovu yote, sasa ni kigezo gani cha kuupimia muda wenyewe? Kama kila kitu kitakwenda na wakati sasa je wakati wenyewe unapaswa kwenda na nini? Kama mwanadamu ataufuata muda na mabadiliko yake kwa utii mkubwa, sasa nini kitafanyika juu ya majukumu na nafasi ya utashi wa mwanadamu? Mwanadamu anaendesha gari la wakati, ambalo liko kwenye mwendo.

Lazima awe mwangalifu na aliongoze vyema gari lake. Vinginevyo atakuwa kama mtu aliyepanda farasi na akamwachia farasi wake aende popote atakapo. marekebisho au kuondoa kabisa? Nukta ya pili inayofaa kutajwa hapa ni kwamba baadhi ya watu wamelitatua tatizo gumu la Uislamu na mahitaji ya wakati kwa namna rahisi sana.

Wanasema kuwa Uislamu ni dini ya milele, na inaweza kurekebishwa ili kuafikiana na mahitaji ya kila zama na wakati. Lakini wanapoulizwa marekebisho haya yanafanyikaje na kanuni yake ni nini, mara moja wanasema kuwa hali ya maisha inapobadilika, sheria zilizopo hubatilishwa na kuwekwa nyingine. Wanatoa hoja kuwa sheria za msimu (muda mfupi) za kidini lazima ziwe na uwezo wa kurekebishwa na ziafikiane na maendeleo ya elimu na sayansi pamoja na kupanuka kwa utamaduni na ustaarabu. Kwa mujibu wao, uwezo huo wa sheria wa kuweza kurekebishwa ili kuafikiana na mahitaji ya wakati haupingani na Uislamu na sio kinyume na mafundisho yake.

Wanadai kuwa, kwa vile mahitaji ya wakati yanabadilika kila mara, basi kila zama huhitaji sheria mpya. Wanaendelea kudai kuwa sheria za kiraia na kijamii za Uislamu zinaafikiana na maisha rahisi ya Waarabu waliokuwa wakiishi kabla ya Uislamu, na ambazo kwa kiasi kikubwa zilikuwa ni kwa mujibu wa mila na desturi zao.

Sasa kwa kuwa haziafikiani na maisha ya zama hizi zinatakiwa ziondolewe na ziwekwe nyingine mpya za kisasa. Watu hawa wanapaswa kuulizwa: Kama uwezo wa sheria kuweza kurekebishwa maana yake ni uwezo wa kubatilishwa na kufutwa, basi ni sheria gani ambayo haina sifa hii? Kuna sheria basi yeyote ambayo haiendi na wakati kwa mtazamo huu?

Tafsiri hii ya uwezo wa sheria kurekebishwa na kuweza kutumika katika zama zote ni sawa na kusema kuwa vitabu vyote na maktaba ndio njia bora kabisa za kufurahia maisha kwa sababu muda wowote mtu atakapotaka starehe, anaweza kuviuza na kutumia fedha zitakazopatikana kwa ajili ya kukidhi matamanio yake. Mwandishi wa Kiirani anasema kuwa mafundisho ya Uislamu yamegawanyika katika sehemu tatu.

Sehemu ya kwanza ina imani za msingi kama vile tauhidi (imani kuwa Mungu ni mmoja tu), Utume, Ufufuo n.k. Sehemu ya pili inahusiana na matendo ya ibada kama vile sala, saumu, udhu, tohara, hija n.k sehemu ya tatu ina sheria zinazohusiana na maisha ya watu. Kwa mujibu wake yeye ni sehemu mbili tu za mwanzo ambazo ni za lazima katika dini na ambazo zinafaa kuhifadhiwa milele.

Lakini sehemu ya tatu sio sehemu ya lazima ya dini kwa kuwa dini haihusiani na maisha ya kila siku ya watu. Mtukufu Mtume mwenyewe hakuamuru kuwa sheria hizi ziwe sehemu ya dini kwa vile hazikuhusiana na ujumbe wake yeye kama Mtume. Ilitokea tu kwamba akawa ni mkuu wa Dola, kwa hiyo akalazimika kuweka sheria pia. Vinginevyo dini haina lolote la kulazimisha katika maisha ya kidunia ya watu. Ni vigumu kuamini kuwa mtu anayeishi katika nchi ya Kiislamu anaweza kuwa mjinga wa mafundisho ya Uislamu kiasi hiki. Je, Qur'ani haijaelezea lengo la kuleta Mitume na Manabii? Je, Qur'ani haisemi wazi wazi kuwa:'Tumewaletea Mitume wetu na dalili za wazi na tumewaleta pamoja nao kitabu na vipimo, ili watu wahukumiane kwa haki. (Suratul Hadidi; 57:25). 35 Qur'ani imeuelezea uadilifu katika jamii kama lengo kuu la Mitume wote.

Kama unataka unaweza usiyafuate mafundisho ya Qur'ani, lakini kwa nini unatenda dhambi kubwa zaidi kwa kuusingizia na kuuzushia Uislamu na Qur'ani? Bahati yetu mbaya zaidi inatokana na ukweli kwamba maadili yetu na sheria vimepoteza chanzo pekee cha nguvu yake, yaani dini. Ni katika nusu karne tu tulipoanza kusikia watu wakipiga kelele kuwa Uislamu ni mzuri, ili muradi tu ubakie ndani ya majumba ya ibada, na usishughulike na jamii.

Kelele hii imepigwa kutoka ndani ya mipaka ya nchi za Waislamu na imeenezwa katika ulimwengu wote wa Kiislamu. Ili kuliweka lengo la kelele hizi wazi tunaweza kusema kuwa nia ni kuufanya Uislamu ubaki kuwa ni kikwazo cha kuzuia kuenea kwa ukomunisti lakini kama huu huu Uislamu utagongana na maslahi ya Magharibi basi upingwe vikali.

Kwa mtazamo wa watu wa Magharibi, matendo ya Uislamu lazima yaendelee, ili pindi ikitokea haja, Waislamu wahamasishwe kuupinga mfumo wa kikomunisti ambao hauamini mambo ya dini na Mungu, lakini sheria za kijamii za Uislamu ambazo zinatoa falsafa ya maisha ya Uislamu lazima ziondoshwe, kwa vile sheria hizi huwapa Waislamu uhuru fulani na kuwafanya wawe watu tofauti wanaojitegemea katika mfumo wao, jambo ambalo litawazuia kumezwa na nchi za Magharibi zenye tamaa kali. Kwa bahati mbaya, watetezi wa hoja kuwa Uislamu haujihusishi na maisha ya kila siku ya watu, wamesahau baadhi ya ukweli wa msingi. Awali miaka 1400 iliyopita, Uislamu ulipinga kanuni kuwa tunaamini baadhi ya mambo (baadhi ya mafundisho ya Uislamu) na tunayakataa mengine, na ukatamka kuwa kanuni na sheria za Uislamu hazibadiliki.

Pili tunaamini kuwa muda umefika ambapo Waislamu hawapaswi kupotoshwa na mbiu za uongo. Watu sasa pole pole wameanza kuamka na wameanza kutofautisha kati ya maendeleo ambayo ni matokeo ya kuchanua kwa vipaji vya kisayansi na kiakili, na kudhihiri kwa ufisadi na upotofu, kutoka nchi za Magharibi. Watu wa ulimwengu wa Kiislamu hivi sasa, kuliko kipindi kingine chochote, wameanza kufahamu thamani ya mafundisho ya Uislamu na wametambua kuwa wanaweza tu kuishi maisha huru kwa kuyafuata. Hawatayaacha, kwa gharama yoyote.

Waislamu makini wanafahamu kuwa propaganda dhidi ya sheria za kiislamu si chochote bali udanganyifu wa mabepari. Tatu, watetezi wa hoja hii wanapaswa kujua kuwa Uislamu unapokuwa na nguvu, hushinda mifumo mingine yote, iwe ya kikafiri au vinginevyo. Uislamu unataka kutawala maisha ya jamii kama falsafa ya maisha, na hautaki kubakia misikitini tu na sehemu nyingine za ibada. Uislamu ambao utabakia kwenye nyumba za ibada, utaacha nafasi kwa ajili ya mawazo ya Kimagharibi na halikadhalika mawazo yanayopingana na umagharibi na itikadi zake. Adhabu ambazo nchi za magharini zinatumikia, katika baadhi ya nchi za Waislamu ni matokeo ya kutoujua ukweli huu.

3

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU

- II UISLAMU NA MAISHA YA KISASA

Mwanadamu sio kiumbe pekee anayeishi maisha ya kijamii. Wanyama wengi, na hususan wadudu hupenda kuishi pamoja na kushirikiana. Wanafuata kanuni za mgawanyo wa kazi, uzalishaji na ugavi na kutoa na kupokea amri. Nyuki, na baadhi ya wadudu jamii ya mchwa wana mfumo huu bora wa maisha, mfumo ambao utamchukua mwanadamu, anayejiona kuwa ni mfalme wa viumbe vyote, miaka au hata karne ili kufikia kiwango hicho cha ufanisi.

Ustaarabu wao (wadudu hawa) haujapitia vipindi kama vile zama za mwituni, zama za mawe na zama za nyuklia. Toka mwanzo wamekuwa na ustaarabu na mfumo wa namna moja kama tu walivyo leo. Ni mwanadamu aliyeanzia sifuri. Tazama : "Mwanadamu aliumbwa dhaifu ."Suratul Nisaa 4:28 Kwa upande wa wanyama, mahitaji yao ya maisha hayabadiliki. Kwao usasa na fasheni mpya havina maana. Ulimwengu wa kale na ulimwengu wa sasa kwao hauna tofauti yoyote.

Kwao sayansi haifanyi ugunduzi wowote ule. Bidhaa mpya kabisa nyepesi na nzito za viwanda hazikuingia katika soko lao; kwa nini? Kwa sababu wanaishi kwa silika na sio kwa akili (mantiki). Maisha ya kijamii ya mwanadamu mara zote yanabadilika. Kila karne ulimwengu unabadilika. Hapo ndio kuna siri ya mwanadamu kuwa mfalme wa viumbe vyote.

Mwanadamu ni mtoto wa maumbile aliyekomaa na kustahili heshima. Amefikia hatua ambayo hahitaji muongozo wa moja kwa moja wa ile nguvu ya ajabu iitwayo silika. Maumbile yanafahamu kuwa mwanadamu ni kiumbe aliyekomaa, na ndio maana yamemuacha huru. Yale ambayo wanyama wanayatekeleza kwa silika na kwa kufuata kanuni za maumbile ambazo hawawezi kuzivunja/kukiuka, wanaadamu wanatakiwa kuyatekeleza kwa kutumia akili na elimu na kwa kufuata sheria zilizopitishwa na zinazoonekana. Mwanadamu akiwa ni mwamuzi wa mwisho wa majaaliwa yake mara zote anaweza kupotoka na kuiacha njia ya maendeleo, na hapa ndio kuna siri ya kuteleza kwake, vipingamizi vyake (anavyokumbana navyo) kupotoka na kushindwa kwake.

Kama tu ilivyo kuwa maendeleo yapo wazi kwake, halikadhalika njia ya kuelekea upotofu, ufisadi na kushindwa haijafungwa. Wanaadamu wamefikia hatua ambayo kwa mujibu wa maneno ya Qur'ani wanaweza kubeba dhamana ambayo mbingu, ardhi na milima haviwezi kubeba; kwa maneno mengine, wanaweza kuishi maisha huru na wanaweza kuchukua majukumu ya kisheria, kitaalamu na mengineyo. Hii ndio sababu hawana kinga ya makosa, ubinafsi, ujinga na dhulma. Pale Qur'ani inapouelezea uwezo huu wa ajabu wa binadamu, mara moja unamtaja kuwa ni 'dhalimu na mjinga'.

Uwezo na sifa hizi mbili za mwanadamu, uwezo wa kuboreka (kuwa bora zaidi) na uwezo wa kupotoka havitenganishiki. Mwanadamu sio kama mnyama ambaye katika maisha yake ya kijamii, huwa haendi mbele wala nyuma, hageukii kulia wala kushoto. Lakini mwanadamu kwa upande wake, katika maisha yake wakati fulani huenda mbele na wakati fulani nyuma. Katika maisha ya wanadamu kama kuna mwendo na kasi, basi kuna kusimama na kupumzika pia. Kama kuna maendeleo na kubadilika kwenda katika hali bora zaidi basi kuna ufisadi na upotofu pia. Kama kuna haki na wema, basi kuna udhalimu na ushari pia.

Kama elimu na busara vimedhihiri basi ujinga na matamanio duni yamedhihiri pia. Inawezekana kwamba mabadiliko yanayotokea na hali mpya zinazoonekana vikawa ni vya kundi la pili (la mabaya). Wasiotaka kubadilishwa na waliopotoshwa. Ni moja ya tabia za mwanadamu kwamba wakati fulani hufanya jambo kupita kiasi na wakati fulani hufanya jambo kwa kiasi kidogo zaidi kuliko inavyohitajika. Kama akichagua kundi la kati na kati hufanya jitihada kutofautisha kati ya mabadiliko ya aina sahihi na mabadiliko ya aina potofu.

Hujaribu na hufanya jitihada kuusukuma muda mbele kwa msaada wa elimu na ubunifu wake na kujinasibisha na maendeleo huku akijaribu kuudhibiti upotofu na kuepuka kutangamana nao. Lakini kwa bahati mbaya, si mara zote mwanadamu huchagua njia hii. Anaandamwa na magonjwa mawili ya hatari, ugonjwa wa kutotaka kubadilika na ugonjwa wa ujinga. Ugonjwa wa kwanza matokeo yake ni kubaki bila mabadiliko na kujiepusha na maendeleo na matokeo ya ugonjwa wa pili ni upotofu wa kuangamia. Asiyetaka kubadilika huchukia kila jambo jipya na hawezi kuafikiana na kitu chochote isipokuwa cha zamani.

Kwa upande wa pili, limbukeni huona kila kitu kipya kuwa ni cha kisasa na maendeleo na hukiaona kuwa ndio hitajio la wakati. Kwa yule asiyetaka mabadiliko (rigid) kila maendeleo mapya kwake anaona ni ufisadi na upotofu wakati limbukeni anaona mambo yote mapya bila kubagua yote yana maana kupanuka kwa utamaduni na elimu. Asiyetaka mabadiliko hatofautishi kati ya pumba na kiini safi na kati ya njia na malengo. Kwa maoni yake kazi ya dini ni kuhifadhi yale yote ya kale na kuukuu hata kama hayatumiki.

Anafikiri kuwa Qur'ani iliteremshwa ili kudhibiti mwendo wa wakati na kuibakiza hali ya dunia iwe vile vile siku zote. Kwa mujibu wa mtazamo huu, mila za zamani na zilizopitwa na wakati, kama vile kuanza kusoma Qur'ani kuanzia mwisho, kuandikia kalamu za matete na wino wa kuchovya kunawia kwenye beseni la kituruki; kula kwa mikono, kutumia taa ya mafuta ya taa na kubakia bila ya kujua kusoma na kuandika ni mambo ya kidini ambayo lazima yahifadhiwe na kudumishwa. Kwa upande mwingine limbukeni huelekeza macho yake yote nchi za Magharibi ili aweze kuiga mtindo wowote mpya utakaotokea na kila mila mpya. Huiita hali hii kuwa ni kisasa na jambo la lazima kufuatwa lililoletwa na wakati. Wote wawili, wasiotaka mabadiliko na waliopotoka (wajinga) wanaamini kuwa mila na desturi zote za zamani ni kanuni/matendo ya kidini, tofauti ni kuwa asiyetaka mabadiliko anataka kuzihifadhi wakati mjinga anaona kuwa dini ni sawa na kudorora (bila mabadiliko yoyote).

Katika karne chache zilizopita suala la migongano kati ya dini na sayansi limekuwa likibishaniwa sana miongini mwa watu wa nchi za Magharibi. Wazo la migongano liliibuka kutokana na mambo mawili. Kwanza kanisa lilikuwa limezikubali baadhi ya dhana za kisayansi na kifalfasa kuwa ni imani za kidini, lakini maendeleo ya sayansi yakathibitisha uongo wa dhana hizo. Pili, sayansi imebadilisha muundo na hali za maisha. Wale wasiotaka mabadiliko, ambao wana muonekano wa kushika dini, wanataka kuufanya muonekano wa nje wa maisha ya kimaada kuwa sehemu ya dini, kama tu, bila ulazima wowote walivyoyapa sura ya kidini baadhi ya masuala ya kifalsafa.

Limbukeni nao wanaamini kuwa dini imeamuru muundo fulani wa maisha ya kimaada, na kwa vile sayansi imeamuru kuwepo kwa mabadiliko katika muundo huu, dini inapaswa kutupiliwa mbali. Kupinga mabadiliko kwa kundi moja, na ujinga wa kundi jingine, kumezua wazo la kubuni la mgogoro kati ya sayansi na dini. Hadith ya mafumbo katika Qur'ani Uislamu ni dini ya kimaendeleo na inataka wafuasi wake waendelee. Qur'ani imetumia hadith ya mafumbo (yenye mafundisho) kuwashawishi Waislamu wasonge mbele, chini ya nuru ya Qur'ani. Inasema kuwa wafuasi wa Mtume Muhammad(s.a.w.w) ni kama mbegu iliyopandwa katika ardhi. Kwanza matawi yake hutokeza kama majani laini ya mbegu. Kisha hukua na kuimarika sana kiasi cha kuweza kusimama katika kikonyo chake. Hakua haraka mno kiasi cha kuwashangaza sana wakulima.

Huu ni mfano wa jamii ambayo Qur'ani inaukusudia. Qur'ani inachokikusudia ni kukua. Qur'ani inataka kuweka msingi wa jamii ambayo mara zote itakuwa ikikua, ikiendelea na kupanuka. Will Durant anasema hakuna dini iliyowataka wafuasi wake kuwa na nguvu kama Uislamu ulivyofanya. Historia ya Uislamu wa awali inaonyesha ni kiasi gani Uislamu ulivyo na nguvu ya kuijenga upya jamii na kuisukuma mbele kimaendeleo. Uislamu unapingana na vyote viwili kutaka mabadiliko na ulimbukeni (ujinga) na unaviona vyote hivi viwili kuwa ni hatari. Uchakavu wa kiakili wa wasiotaka mabadiliko na kung'ang'ania kwao mila za zamani ambazo hazina uhusiano wowote na Uislamu, kumetoa kisingizio kwa limbukeni kuuona Uislamu kuwa unapingana na maisha ya kisasa (usasa).

Kwa upande mwingine kufuatana na kuiga mitindo mipya zaidi na namna za maisha za Magharibi kunakofanywa na limbukeni, imani yao kwamba kufuata utaratibu wa Kimagharibi kimwili na kiroho, kukubali kwao tabia, adabu na desturi za Magharibi, na kuiga kibubusa sheria za kiraia na kijamii kutoka katika nchi za Magharibi, kumetoa kisingizio kwa wasiotaka mabadiliko kukitazama kila kitu kipya kwa mashaka na kukiona kama tishio kwa dini yao, uhuru wao na kwa haiba ya kijamii ya jumuiya yao. Kwa sasa, Uislamu unagharamikia makosa ya makundi yote mawili.

Ung'ang'anizi wa wasiotaka mabadiliko umeacha uwanja wazi kwa limbukeni kufanya uharibifu na ujinga wa limbukeni umewafanya wasiotaka mabadiliko kuwa ving'ang'anizi zaidi katika imani zao. Inashangaza kuona kuwa hawa wanaojiita wameelimika na kustaarabika ingawa kiuhalisia ni watu wajinga, wanafikiri kuwa muda ni maasumu (haubebi dhambi). Ukweli ni kuwa mabadiliko yote yanaletwa na watu, na mwanadamu sio maasumu hata kidogo (hajaepukana na madhambi). Sasa vipi inaweza kufikirika kuwa mabadiliko ya muda mara zote huwa hayana makosa na matatizo. Kama ilivyo tu kuwa mwanadamu ana matakwa ya kupenda sayansi, maadili, sanaa na dini, na mara zote huchukua hatua mpya kwa maslahi ya wanadamu, pia ana baadhi ya tabia mbaya.

Ni mbinafsi, mwenye uchu wa madaraka na mwenye kupenda raha. Anapenda fedha na unyonyaji kama tu alivyo na uwezo wa kugundua mambo mapya na kutafuta njia bora zaidi za kufanya mambo pia ana dhamana ya kutenda makosa. Lakini limbukeni na waliopotoka hawajui mambo hayo. Wanarudia mahadhi yale yale kuwa ulimwengu wa kisasa upo hivi na vile. Kinachoshangaza zaidi ni kuwa wanalinganisha kanuni za maisha na vitu; kama vile viatu, kofia na gauni. Kwa vile vitu hivi hutafutwa na kuhitajika vinapokuwa vipya na kutupwa vinapochakaa, halikadhalika kwa mujibu wao, hali iwe hivyo hivyo kwa ukweli usiobadilika. Kwao, kizuri na kibaya havina maana zaidi ya kipya na cha zamani.

Ukabaila ni mbaya kwa sababu tu ni mfumo wa zamani na umepitwa na wakati. Vinginevyo ulikuwa mzuri kabisa wakati unaanzishwa duniani kwa mara ya kwanza. Halikadhalika unyonyaji wa wanawake ni mbaya tu kwa vile haupendwi na ulimwengu wa kisasa; vinginevyo hadi hivi majuzi, watu hawa hawa walikuwa hawampi mgao wa urithi. Walikuwa hawajaitambua haki yake ya kumiliki mali na walikuwa hawaheshimu ridhaa na maoni yake.

Kwa mujibu wa watu hawa, katika zama hizi, zikiwa ni zama za anga (kuruka na ndege n.k), kama ilivyokuwa tu haiwezekani kusafiri kwa punda na kuacha ndege, kuwasha kibatari na kuacha umeme, kushona nguo kwa mkono na kuandika kwa mkono huku ukiacha mashine kubwa za kisasa za kuchapishia, halikadhalika haiwezekani kuacha kwenda kwenye sherehe za muziki, sherehe ambazo watu wanavaa mavazi ya kuogelea, mialiko ya chakula cha usiku chenye nyama za kubanikwa, kutoshiriki katika vicheko vya ovyo, kutocheza karata, kutovaa visketi vifupu kwani vitu vyote hivi ni mitindo ya karne hii. Wanahofu kuwa wasiposhiriki katika mambo haya watarudi nyuma katika zama za kuendesha farasi. Wanadai kuwa hizi ni zama za nyukilia, zama za sayansi, zama za miezi ya kubuni na zama za makombora ya masafa marefu.

Hili ni jambo zuri! Sisi pia tunamshukuru Mungu kuwa tunaishi katika zama hizi na tunaomba kwamba tufurahie na kufaidika na sayansi na viwanda kwa kiwango cha juu kabisa. Lakini je, mambo yote haya yanasababishwa na sayansi tu? Je, hali zote za karne hii ni matokeo ya maendeleo ya kisasa ya sayansi? Je, sayansi inadai kuwa imedhibiti mambo yote hapa duniani? Sayansi haijawahi kudai hivyo hata siku moja.

Balaa la karne yetu ni kuwa kundi la wanasayansi kwa nia njema kabisa, huitumia sayansi kufanya ugunduzi mpya, lakini kundi jingine la wabinafsi na wenye uchu wa madaraka na wanaoabudu fedha huyatumia vibaya matunda ya jasho la wanasayansi ili kuyafikia malengo yao ya kiovu. Sayansi inalalamika kuwa inatumiwa vibaya na wanaadamu wakorofi na hii ndio bahati mbaya ya kizazi chetu. Sayansi inasonga mbele katika fani za fizikia na inagundua sheria za mwanga na kuakisi na kundi la wakorofi na wabinafsi wanaitumia kutengenezea filamu za bluu (ngono) za uharibifu na uovu. Kemia inaendelea na kugundua tabia za vitu mbali mbali na michanganyiko yake.

Baadhi ya watu wanaamua kutumia ugunduzi huu kutengeneza madawa ya kulevya, heroin ambayo ni laana kwa wanaadamu. Sayansi iligundua chanzo kizuri cha nishati ndani ya atom, lakini kabla ya ugunduzi haujatumika kwa manufaa ya wanaadamu, wenye tamaa ya madaraka walifanya haraka kutengeneza bomu la atomiki, na kuwadondoshea watu wasio na hatia. Mapokezi yalipoandaliwa, kwa ajili ya heshima ya Einstein, mwanasayansi mkubwa wa karne ya 20, yeye mwenyewe alipanda juu ya jukwaa na kusema, "Mnampa heshima mtu ambaye amechangia kwa namna fulani kutengenezwa kwa bomu la atomiki?"

Einsten mwenyewe hakutumia elimu yake kutengeneza bomu. Ni wengine waliotumia ugunduzi wake kwa lengo hili. Matumizi ya heroin, mabomu ya atomiki na filamu za matusi (bluu) haviwezi kuhalalishwa eti kwa madai kuwa ni mambo ya karne hii. Ikiwa ndege za kisasa kabisa za mabomu zinatumika kurushia mambomu bora kabisa kwa watu wa nchi nyingine, na watu walioelimika sana wanaajiriwa kufanya kazi hii, je, usasa huu unaweza kupuguza ushenzi wa kurithi wa tendo hili?

4

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU

- III UISLAMU NA USASA

Hoja kuu ya wale ambao wanasema kuwa katika masuala ya haki za kifamilia tunapaswa kufuata mfumo wa Kimagharibi, ni kuwa muda umebadilika na mahitaji ya karne hii yanatutaka tufanye hivyo. Tunaonelea kuwa ni vizuri tuyaweke maoni yetu wazi juu ya nukta hii, kwa sababu bila kufanya hivyo, mjadala juu ya nukta yoyote hautakuwa kamili, ingawa kwa sababu ya uchache wa nafasi haiwezekani kulijadili suala hili kwa mitazamo yake yote, kifalsafa, kisheria, kijamii na kimaadili. Itatosheleza hapa kujadili nukta mbili tu. Nukta ya kwanza ni kwamba kuafikiana kwayo na kukubaliana na mabadiliko ya wakati sio suala rahisi sana kama baadhi ya watu wasiojua wanavyofikiri. Mabadiliko yanayoletwa na wakati, wakati fulani huwa ni ya kurudisha maendeleo nyuma.

Tunapaswa kwenda na mabadiliko ya wakati ya kimaendeleo na tunapaswa kuyapiga vita mabadiliko yanayoletwa na wakati ambayo ni ya kiharibifu. Ili kutofautisha aina hizi mbili za mabadiliko na kujua asili yake, tunapaswa kujua chanzo cha maendeleo (ugunduzi au mabadiliko) haya mapya na yameelekezwa katika mwelekeo gani. Tunapaswa kuangalia ni tabia gani za kibinadamu zimeyaleta (njema au mbaya) na ni matabaka gani ya watu yanatetea mambo haya mapya?

Tunapaswa kuangalia je yameletwa na tabia tukufu za mwanadamu au matamanio duni yanayofanana na wanyama, na kama yamekuja kama matokeo ya uchunguzi usio wa kibinafsi wa wanazuoni na wasomi, au yameletwa na matamanio duni ya wanaotumikia nafsi zao na tabia za kifisadi za jamii.

MNYAMBULIKO WA SHERIA ZA KIISLAMU

Nukta ya pili inayofaa kuwekwa wazi ni kuwa baadhi ya wasomi wa kiislamu wanaamini kuwa Uislamu una uwezo na sifa ambazo zinaupa uwezo wa kutumika zama zote. Kwa mujibu wa wasomi hawa, mafundisho ya Uislamu yanaafikiana na maendeleo ya wakati, kupanuka kwa utamaduni na matokeo ya mabadiliko haya. Hebu tuangalie asili, sifa na uwezo huu ambao Uislamu unao. Kwa maneno mengine hebu tuangalie ni vifaa gani vimewekwa katika jengo hili la dini, na ikiwa vimeipa sifa ya kuafikiana na hali zote zinazobadilika, bila kuwa na haja ya kuacha baadhi ya mafundisho yake na bila mgogoro wowote kati ya mafundisho yake na hali yoyote inayojitokeza ya kupanuka kwa elimu na ustaarabu.

Ingawa suala hili lina sura ya kiufundi, ili kuondoa shaka shaka ya wale wanaotilia shaka ukweli huu kuwa Uislamu una sifa hii, tunalielezea kwa kifupi hapa. Kwa undani zaidi juu ya suala hili, wasomaji wanaweza kusoma kitabu kiitwacho 'Tanbihul Ummah' cha hayati Ayatullah Naini au kitabu kingine kiitacho 'Marjaiyyat Wal Imamat cha mwanazuoni mkubwa wa zama hizi Allamah Tabatabai. Lakini vitabu vyote hivi vipo katika lugha ya kifursi. Kuna nukta nyingi, ambazo zinaunda siri ya Uislamu kuwa na uwezo wa kuafikiana na kupanuka kwa elimu na ustaarabu, na uwezo wa kutumika kwa sheria zake thabiti na imara katika hali mbali mbali za maisha. Hapa tutataja baadhi yake.

Msisitizo katika roho na kutojali sana kiwiliwili. Uislamu haujashughulikia maisha ya nje (kimwili) tu ambayo hutegemea kiwango cha maendeleo ya elimu ya mwanadamu. Mafundisho ya Uislamu hushughulikia roho pia na malengo ya maisha na hutoa njia bora kabisa ya kuyafikia malengo haya. Sayansi haijabadilisha roho na malengo ya maisha wala haijapendekeza njia yoyote nzuri zaidi, fupi zaidi na salama zaidi ya kuyafikia malengo haya. Imetoa tu njia bora zaidi na vifaa vya kukwamisha njia ya kuyafikia malengo haya. Uislamu, kwa kuhifadhi malengo tu katika himaya yake na kuacha muundo na mbinu kwenye himaya ya sayansi na teknolojia, umeepuka migongano dhidi ya utamaduni na ustaarabu.

Sio hivyo tu lakini pia kwa kuhimiza mambo yanayosaidia kupanuka kwa ustaarabu, yaani elimu, kazi, uchamungu, ridhaa, ujasiri na uvumilivu bila kukata tamaa, umejitolea kuwa kigezo kikuu cha kupanua ustaarabu. Uislamu umeweka alama za barabarani katika njia yote ya maendeleo ya mwanadamu. Alama hizi kwa upande mmoja zinaonyesha njia na kituo cha mwisho na kwa upande wa pili zinaonyesha makorongo na sehemu za hatari. Sheria zote za Kiislamu ni alama za barabara, aidha za aina ya kwanza au ya pili. Njia za maisha katika zama hutegemea juu ya kiwango cha elimu ya wanaadamu.

Kwa kadri elimu ya watu inavyopanuka, ndivyo njia bora zaidi za kujipatia kipato zinavyotokea na moja kwa moja zinachukua nafasi ya zile njia duni (za zamani). Mifumo ya nje na ya kimaada ya njia hizi (za kupatia riziki) haina utakatifu katika Uislamu, na Waislamu hawalazimiki kuzidumisha. Uislamu haujasema kifaa hiki na kile kitumike kwa ushonaji, ususi, kilimo, usafiri, vita au kazi nyingine. Hivyo hapawezi kuwa mgogoro wowote kati ya sayansi na Uislamu, pindi kifaa kinapopitiwa na wakati, cha kisasa zaidi kinaweza kutumika badala yake.

Uislamu haujaagiza kutumika kwa mtindo maalum ya viatu au nguo, wala haujapendekeza aina fulani ya ujenzi wa majengo. Halikadhalika hauhimizi juu ya mbinu fulani fulani za uzalishaji na ugavi. Hii ni moja ya sifa hizo za Uislamu, ambazo zimeuwezesha kuweza kutumika katika maendeleo yote ya wakati. Sheria madhubuti kwa mahitaji madhubuti na sheria zinazobadilika kwa mahitaji yanayobadilika. Sifa nyingine ya Uislamu, ambayo ina umuhimu mkubwa ni kuwa umeweka sheria madhubuti (zisizobadilika) kwa ajili ya mahitaji madhubuti (yasiyobadilika) na sheria zinazobadilika kwa mahitaji yanayobadilika. Mbali na mahitaji ya wanaadamu, mahitaji ya mtu mmoja mmoja na vikundi, yote yana asili ya kudumu.

Hayabadiliki kwa mujibu wa wakati. Kanuni za mifumo inayotawala silika za binadamu na mahusiano ya kijamii hazibadiliki. Tunazijua nadharia za 'Maadili husianishi' na 'Uadilifu husianishi' ambazo zina wafuasi wake, na tutatoa maoni yetu kuhusiana nao baadaye. Sehemu nyingine ya mahitaji ya mwanadamu ni ile ya mahitaji yanayobadilika, na hii huhitaji sheria zinazobadilika. Uislamu ulishayaona mahitaji hayo na umeyaunganisha na kanuni fulani ambazo zina sheria ndogo zinazobadilika kila hali inapobadilika. Kufafanua nukta hii hebu tuangalie mifano hii;'Andaeni majeshi kwa ajili yao (maadui)' (Suratul Anfal 8:60.) Wakati huo huo tunasoma hadith kadhaa za Mtume katika vitabu vya sheria za Kiislamu chini ya kichwa cha habari 'Kuendesha farasi na kurusha mishale.' Mtume aliwaelekeza Waislamu wajifunze kuendesha farasi na kurusha mishale na wawafundishe watoto wao pia. Haya yalikuwa ni sehemu ya mafunzo ya Kiislamu katika zama hizo.

Ni dhahiri kabisa hapa kuwa amri ya msingi ni 'Kuandaa majeshi.' Upinde na mshale, jambia na mkuki na farasi sio vya muhimu. Kilicho cha muhimu ni kuwa imara kijeshi dhidi ya maadui. Kuandaa majeshi ni amri ya kudumu ambayo imetokana na hitajio la kudumu. Hata hivyo ulazima wa kupata ujuzi katika kuendesha farasi na kurusha mishale sio wa kudumu, na hubadilika kutokana na wakati.

Kutokana na kubadilika kwa hali, ujuzi wa kufyatua risasi umechukua nafasi ya kurusha mishale. Mfano mwingine ni sheria ya kijamii inayohusu kubadilishana mali, iliyotajwa katika Qur'ani. Uislamu umetambua kanuni ya umiliki wa mali wa mtu binafsi. Hata hivyo umiliki huu unaotambuliwa na Uislamu ni tofauti na ule uliopo katika nchi za kibepari. Tabia ya umiliki wa mali wa watu binafsi katika Uislamu ni kanuni ya kubadilishana. Kwa utaratibu huu Uislamu umeweka sheria fulani.

Mojawapo imeelezwa na Qur'ani Tukufu katika maneno haya'Na msile mali zenu (kila mmoja kula za mwenzake) kwa batili' (Suratul Baqarah, 2:188).

Kwa maneno mengine katika mauzo ya biashara, fedha isitoke mkono mmoja kwenda mwingine isipokuwa kwa kubadilishana na kitu kingine cha halali chenye kuwa na mamlaka ya mwisho juu ya mali hiyo. Imelezwa na kufafanuliwa katika sheria ya Kiislamu mauzo na manunuzi ya vitu fulani yamekatazwa. Vitu hivyo ni pamoja na damu na kinyesi cha binadamu. Sababu ni kuwa vitu hivi havina thamani inayoviwezesha kuhesabika kuwa sehemu ya mali ya mwanadamu. Kanuni hii ni sawa ya mali ya mwanadamu. Kanuni hii ni sawa na ile iliyo katika Aya iliyonukuliwa hapo juu.

Ubatili wa mauzo na manunuzi ya damu na kinyesi cha binaadamu ni sehemu au mfano tu wa matumizi ya kanuni hiyo. Hata kama hakuna ubadilishaji uliofanyika, (wa bidhaa au bidhaa kwa fedha) fedha au mali inayomilikiwa na mtu fulani haiwezi kufujwa au kuliwa bure. Sheria inayokataza kula mali ya mtu mwingine bure (bila kufanya kazi) au kiwizi ni kanuni madhubuti na inatumika zama zote, na imetokana na hitajio la kudumu la jamii.

Lakini kanuni kuwa damu na kinyesi cha binadamu havihesabiki kama mali na haviruhusiwi kuuzwa, inahuisiana na wakati na kiwango cha ustaarabu. Kanuni hii inaweza kubadilishwa kutokana na mabadiliko ya hali, maendeleo ya sayansi na viwanda na uwezekano wa kuzitumia bidhaa hizi katika namna sahihi na yenye manufaa. Mfano mwingine; "Imam Ali(a.s) hakuwahi kuweka dawa kwenye nywele zake hata siku moja, ingawa zilikuwa zimekuwa za mvi katika miaka ya mwisho ya uhai wake.

Siku moja mtu mmoja alimwambia, 'Je Mtume hakuamrisha nywele za mvi ziwekwe dawa?" Ali alijibu 'Ndiyo aliamrisha' Sasa kwa nini huweki dawa kwenye nywele zako? Yule mtu aliuliza. Ali akasema; "Katika wakati ule ambao Mtume alitoa maelekezo haya, idadi ya Waislamu ilikuwa ndogo na kulikuwa wazee wengi waliokuwa wakishiriki vitani. Mtume aliwaamrisha wazipake dawa ili kuficha umri wao halisi, kwani kama adui angeona kuwa anapambana na kundi la wazee tu, hamasa yake ingeongezeka. Kwa kuwa Uislamu umeenea dunia yote, hali imebadilika. Kila mtu yupo huru kupaka dawa nywele zake au kuacha." Kwa maoni ya Imamu Ali, maelekezo ya Mtume hayakuwa ya kudumu wala haikuwa sheria ya kudumu.

Uislamu unajali muonekano wa nje na roho ya ndani pia. Lakini unataka pumba kwa ajili ya punje yenyewe na unataka nguo kwa ajili ya mwili. Suala la kubadilisha herufi Katika siku za hivi karibuni hapa Iran kumekuwa na ubishani juu ya kubadlisha herufi. Suala hili linaweza kuangaliwa katika pande mbili kwa mtazamo wa kanuni za Kiislamu, na kwa sura mbili. Kwanza ni iwapo Uislamu unapendelea herufi fulani na kuzibagua nyingine.

Je Uislamu unaziona herufi za sasa, ambazo ni za Kiarabu, kama zake, na herufi nyinginezo kama zile za kilatini zinazoonekana ni za kigeni? Uislamu ambao ni dini ya ulimwengu mzima unaziona herufi zote duniani kuwa ni sawa. Sura ya pili ni kuwa kiasi gani kubadilika kwa herufi kutachanganya utamaduni wa Taifa la Kiislamu na watu wengine na kutakuwa na madhara gani kwa utamaduni wa taifa hili. Na zaidi ya hayo, katika karne 14 zilizopita, vitabu vya Kiislamu na kisayansi vilivyozalishwa na Irani vimeandikwa katika herufi za sasa (za kiarabu), je kubadilisha herufi si kutazifuta (haribu) kazi zote hizi?

Swali jingine ni, 'Ni akina nani wanaopendekeza mabadiliko haya, na ni akina nani watakaoyatekeleza? Maswali yote haya ni thabiti.' Kuwategemea wengine ndio kumekatazwa, sio kofia ya kizungu Watu kama mimi mara nyingi wanakumbana na maswali, yanayoulizwa kwa dharau au kejeli. "Sheria ya Kiislamu inasemaje kuhusu kula ukiwa umesimama?' Ni vipi kuhusu kula kwa kijiko au uma?' Je kuvaa kofia ya kizungu kumekatazwa?' Je kutumia lugha za kigeni kumekatazwa?'" Katika kujibu maswali haya, tunasema kuwa Uislamu haujatoa maelekezo yoyote mahsusi juu ya hili. Uislamu haujawaelekeza wafuasi wake kula kwa mkono au kijiko. Ulichowaelekeza ni kuzingatia usafi.

Uislamu haujaelekeza matumizi ya mitindo ya aina fulani ya viatu, kofia au nguo. Kwa mtazamo wa Uislamu lugha zote Kiingereza, Kijapani, Kifursi, zina hadhi sawa. Hata hivyo, Uislamu unasema kitu fulani zaidi. Umesema kuwa imekatazwa mtu kupoteza utambulisho wake. Kuwaogopa wengine bila ulazima kumekatazwa, Kuwaiga wengine kumekatazwa, kuchekeshwa na kuvutiwa na wengine kama sungura anavyovutiwa na nyoka, kumekatazwa.

Kumchukulia punda mgeni aliyekufa kuwa ni farasi kumekatazwa. Kuingiza nchini upotofu na ukosefu wa maadili kutoka nje, kwa madai ni mambo ya kisasa ya karne hii, kumekatazwa. Kuamini kuwa Waislamu wanapaswa kufuata mila na utamaduni wa Kimagharibi ndani na nje, kimwili na kiroho, kumekatazwa. Kwenda nchi ya Kimagharibi kwa siku chache na baada ya kurudi, unaanza kutamka maneno yetu kama wao (wazungu) kumekatazwa. Muhimu na muhimu zaidi. Sura nyingine ya Uislamu inayoufanya uende na mahitaji ya wakati ni kukubaliana kwa mafundisho yake na akili/mantiki.

Uislamu umetangaza kuwa sheria zake zimezingatia maslahi makubwa zaidi. Na wakati huo huo, Uislamu wenyewe umetoa madaraja mbali mbali ya umuhimu wa maslahi haya. Hii inarahisisha kazi ya wataalamu wa sheria za Kiislamu katika fani hizo ambapo maslahi tofauti yanaonekana kugongana. Katika hali hizo, Uislamu umewaruhusu wataalamu wa sheria za Kiislamu kupima uzito wa maslahi tofauti, na kuzingatia mwongozo ambao Uislamu wenyewe umetoa, katika kuangalia ni maslahi gani hilo ni muhimu zaidi. Katika fani ya sheria za Kiislamu, hii huitwa suala la "muhimu na muhimu zaidi." Kuna mifano mingi ambapo kanuni hii ya maslahi ya juu na ya juu zaidi imepata kutumika.

Hata hivyo kwa sababu ya uchache wa nafasi, tunairuka sehemu hii Sheria yenye haki ya Turufu. Sifa nyingine ya Uislamu ambayo imeipa dini hii uwezo wa kuhamishika na kutumika katika hali mbali mbali na imeifanya kuwa dini inayoishi na ya kudumu milele ni kuwa ndani yake kuna chombo cha sheria ambacho kazi yake ni kudhibiti na kurekebisha sheria nyingine.

Mafakihi wanaziita kanuni hizi kuwa ni " kanuni za kuongozea." Kanuni ya 'Hakuna madhara' na 'Hakuna hasara' kwamba sheria haitatumika pale ambapo inaweza kusababisha ugumu au madhara kwa maslahi ya mtu asiye na hatia, imeuenea (imeutawala) mfumo mzima wa kisheria. Lengo la kanuni hizi ni kudhibiti na kurekebisha sheria nyingine. Kwa kusema kweli Uislamu umezipa nguvu ya turufu kanuni hizi ambazo hubadilisha kanuni nyingine.

Madaraka ya mtawala Kwa nyongeza kuna mfululizo mwingine wa kanuni za kuweka mambo katika mizania ambazo Mwenyezi Mungu ameipa dini hii ya mwisho. Ayatullah Na'ini na Allamah Tabatabai, juu ya hili, wametegemea madaraka ambayo Uislamu umeipa serikali ongofu ya Kiislamu. Kanuni ya ijtihadi Mshairi na mwanafalsafa wa Kipakistani anasema kuwa Ijtihadi (kuzalisha sheria kutoka vyanzo vyake vya asili) ni nguvu ya hamasa ya Uislamu. Yuko sawa kusema hivyo. Lakini kilicho muhimu zaidi ni kuwa Uislamu una sifa maalum ya kuruhusu Ijtihadi. Hakuna dini nyingine yenye sifa hii katika namna hii hii. Jengo la ndani la Uislamu limejengwa katika namna ambayo kwa msaada wa Ijtihadi, unaweza mara zote kwenda na mahitaji yanayobadilika katika maisha.

Abu Ali Ibn Sina (Avicenna) katika kitabu chake Al-Shifa, ameelezea haja ya Ijtihadi kuwa inatokana na kubadilika kila mara kwa mahitaji. Anasema kuwa hali za maisha mara zote zinabadilika. Matatizo mapya yanaibuka kila mara, lakini misingi ya Uislamu haibadiliki. Hivyo katika hali hii, lazima wawepo watu wanaojua sheria za kiislamu vizuri na mafundisho ya Kiislamu vizuri ili waweze kujibu maswali yote yanayoibuka katika kila zama na hivyo kukidhi mahitaji ya wakati. Katiba ya Iran inaamuru kuwa pawepo chombo cha mujtahidi wasiopungua watano (wanazuoni wakubwa wa Theolojia wanaoweza kufanya ijtihadi) kitakachokuwa kikichunguza sheria zinazopitishwa na serikali kila wakati.

Lengo hapa ni kuwa watu hawa (mujtahidi) kwa vile sio wapinga mabadiliko wala hawapingi maendeleo ya kisasa, wala sio limbukeni wala hawawafuati wengine kibubusa, waangalie na kudhibiti mfumo wa sheria wa nchi. Inapaswa kueleza kuwa ijtihad kwa namna halisi ina maana kubobea na inahitaji uelewa wa ndani sana wa misingi ya Uislamu na nguzo zake na elimu kubwa kabisa ya kanuni za fikihi ya Kiislamu, ambayo si kila mtu aliyesoma Uislamu kwa muda fulani anaweza kudai kuwa mujtahid.

Hapana shaka kuwa hii ni kazi ya umri mzima wa mtu ili kubobea katika kanuni na mafundisho ya Uislamu, na mbali na kipaji, nia na akili, inahitaji pia msaada wa Mungu. Mbali na kubobea (kwenye mchepuo maalum) na Ijtihad, baadhi ya watu wanaweza kupata elimu na kufikia kiasi kwamba maoni yao yanaweza kuchukuliwa kuwa ni fatwa. Historia ya Uislamu inawataja watu hao ambao licha ya elimu yao kubwa na maadili yao ya hali ya juu walikuwa na hadhari kubwa, walipokuwa wakitoa maoni yao, juu ya masuala ya kisheria.

5