NAHJULBALAGHAH Juzuu 1

NAHJULBALAGHAH0%

NAHJULBALAGHAH Mwandishi:
: Sheikh Haruna Pingili
Kundi: VITABU VYA HADITHI

NAHJULBALAGHAH

Mwandishi: SAYYIDI SHARIFU RADHIY
: Sheikh Haruna Pingili
Kundi:

Matembeleo: 5460
Pakua: 1997


Maelezo zaidi:

Juzuu 1 Juzuu 2
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 7 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 5460 / Pakua: 1997
Kiwango Kiwango Kiwango
NAHJULBALAGHAH

NAHJULBALAGHAH Juzuu 1

Mwandishi:
Swahili

NAHJUL-BALAGHAH

JUZUU YA KWANZA

2. MIONGONI MWA KHUTBA ZAKE(a.s) BAADA YA KUTOKA KWAKE SIFFIINI

أحْمَدُهُ اسْتِتْماماً لِنِعْمَتِهِ، وَاسْتِسْلاَماً لِعِزَّتِهِ، واسْتِعْصَاماً مِنْ مَعْصِيَتِهِ، وَأَسْتَعِينُهُ فَاقَةً إِلى كِفَايَتِهِ، إِنَّهُ لاَ يَضِلُّ مَنْ هَدَاهُ، وَلا يَئِلُ مَنْ عَادَاهُ، وَلا يَفْتَقِرُ مَنْ كَفَاهُ; فَإِنَّهُ أَرْجَحُ ما وُزِنَ، وَأَفْضَلُ مَا خُزِنَ

Namuhimidi yeye (s.w.t) nikiomba utimilifu wa neema Zake, na kusalimu amri kwa utukufu Wake, na kujihifadhi na maasi yake, Namwomba msaada nikiwa mwenye haja ya toshelezo Lake: Kwa hakika hapotei aliyemwongoza, wala hajinasui mwenye kumfanyia uadui. Wala hawi fukara mwenye kutoshelezwa na yeye. Kwani kumhimidi ni kuzito mno katika mizani na ni hazina bora.

وَأَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلهَ إِلاَّ اللهُ، شَهَادَةً مُمْتَحَناً إِخْلاَصُهَا، مُعْتَقَداً مُصَاصُهَا، نَتَمَسَّكُ بها أَبَداً ما أَبْقانَا، وَنَدَّخِرُهَا لاَهَاوِيلِ مَا يَلْقَانَا، فَإِنَّها عَزيمَةُ الاْيمَانِ، وَفَاتِحَةُ الاْحْسَانِ، وَمَرْضَاةُ الرَّحْمنِ، وَمَدْحَرَةُ الشَّيْطَانِ

Na ninashuhudia kuwa hapana mungu isipokuwa Allah, Peke yake hana mshirika, ushuhuda uliotihaniwa wenye ikhilasi hali ya kuitakidi uhalisi wake. Tunashikamana nayo shahada milele kwa kadiri atakavyotubakisha, na tunaihifadhi kwa ajili ya hofu itakayotupata, kwa sababu ni azma thabiti ya imani, na ni ufunguo wa mema na radhi ya Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, na ni sababu ya kuwa mbali na Shetani.

وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّداً عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، أرْسَلَهُ بِالدِّينِ المشْهُورِ، وَالعَلَمِ المأْثُورِ، وَالكِتَابِ المسْطُورِ، وَالنُّورِ السَّاطِعِ، وَالضِّيَاءِ اللاَّمِعِ، وَالاَمْرِ الصَّادِعِ، إزَاحَةً لِلشُّبُهَاتِ، وَاحْتِجَاجاً بِالبَيِّنَاتِ، وَتَحْذِيراً بِالايَاتِ، وَتَخْويفاً بِالمَثُلاَتِ، وَالنَّاسُ في فِتَن انْجَذَمَ فِيها حَبْلُ الدِّينِ، وَتَزَعْزَعَتْ سَوَارِي اليَقِينِ، وَاخْتَلَفَ النَّجْرُ، وَتَشَتَّتَ الاْمْرُ، وَضَاقَ الْـمَخْرَجُ، وَعَمِيَ المَصْدَرُ، فَالهُدَى خَامِلٌ، واَلعَمَى شَامِلٌ.

Na ninashuhudia kuwa Muhammad ni mja Wake na mjumbe Wake, amemtuma na dini mashuhuri, na sheria iliyonukuliwa, na Kitabu kilichoandikwa, na nuru yenye mwanga, mwanga wenye kuangaza, na amri iliyo wazi, ili kuondoa shaka, na kutoa hoja kwa ubainifu, na kutahadharisha kwa alama, na kuhofisha kwa adhabu. Na watu wapo katika fitna ya moja kwa moja. Kuna kamba ya dini, na nguzo ya yakini imetetereka, Misingi imetofautiana, mambo yalikuwa yamevurugika, njia ya kujinasua ilibana. Upenyo uliingia giza, mwongozo ulikuwa haujulikani, upofu ulienea.

عُصِيَ الرَّحْمنُ، وَنُصِرَ الشَّيْطَانُ، وَخُذِلَ الاْيمَانُ، فَانْهَارَتْ دَعَائِمُهُ، وَتَنكَّرَتْ مَعَالِمُهُ، وَدَرَسَتْ سُبُلُهُ، وَعَفَتْ شُرُكُهُ

Mungu mwingi wa rehema walimuasi, Shetani akanusuriwa, imani ilitelekezwa, kwa hiyo nguzo zake zikaporomoka. Mafunzo yake yakabadilika na njia mitaa yake iliharibika.

أَطَاعُوا الشَّيْطَانَ فَسَلَكُوا مَسَالِكَهُ، وَوَرَدُوا مَنَاهِلَهُ، بِهِمْ سَارَتْ أَعْلامُهُ، وَقَامَ لِوَاؤُهُ، في فِتَن دَاسَتْهُمْ بِأَخْفَافِهَا، وَوَطِئَتْهُمْ بأَظْلاَفِهَا، وَقَامَتْ عَلَى سَنَابِكِهَا، فَهُمْ فِيهَا تَائِهُونَ حَائِرونَ جَاهِلُونَ مَفْتُونُونَ، في خَيْرِ دَار، وَشَرِّ جِيرَان، نَوْمُهُمْ سُهُودٌ، وَكُحْلُهُمْ دُمُوعٌ، بأَرْض عَالِمُها مُلْجَمٌ، وَجَاهِلُها مُكْرَمٌ

Walimtii Shetani wakafuata mwenendo wake, wakapita mapito yake, kwao wao alama zake zilipita, bendera yake ikasimama katika fitina, iliyowakanyanga kwa kwato zake, hivyo wao wamepotea wanatangatanga, wajinga wamefitiniwa, wakiwa ndani ya nyumba bora na majirani waovu[19] . Usingizi wao ni kukesha, na wanja wao ni machozi[20] . Hali ya kuwa wako katika ardhi ambayo mwanachuo wake huzibwa kinywa[21] , na jahili wake huheshimiwa[22] .

NDANI YA KHUTBA HII PIA ALIASHIRIA KWA AALI ZAKE NABII(a.s.) :

هُمْ مَوْضِعُ سِرِّهِ، وَلَجَأُ أَمْرِهِ، وَعَيْبَةُ عِلْمِهِ، وَمَوْئِلُ حُكْمِهِ، وَكُهُوفُ كُتُبِهِ، وَجِبَالُ دِينِه، بِهِمْ أَقَامَ انْحِناءَ ظَهْرِهِ، وَأذْهَبَ ارْتِعَادَ فَرَائِصِهِ

Wao ni mahali pa kuweka siri yake, kimbilio la mambo yake, chombo cha ilimu yake. Marejeo ya hekima zake, pango la vitabu vyake, (mahali pa kuhifadhia vitabu) na milima ya dini yake, kupitia kwao Mungu amenyoosha mgongo[23] , mgongo wa dini yake, na aliondoa mtetemeko wa viungo vyake[24] .

NA AKAWAKUSUDIA WATU WENGINE (WANAFIKI):

زَرَعُوا الفُجُورَ، وَسَقَوْهُ الغُرُورَ، وَحَصَدُوا الثُّبُورَ، لا يُقَاسُ بِآلِ مُحَمَّد(عليهم السلام)مِنْ هذِهِ الاُمَّةِ أَحَدٌ، وَلا يُسَوَّى بِهِمْ مَنْ جَرَتْ نِعْمَتُهُمْ عَلَيْهِ أبَداً هُمْ أَسَاسُ الدِّينِ، وَعِمَادُ اليَقِينِ، إِلَيْهمْ يَفِيءُ الغَالي(6)، وَبِهِمْ يَلْحَقُ التَّالي، وَلَهُمْ خَصَائِصُ حَقِّ الوِلايَةِ، وَفِيهِمُ الوَصِيَّةُ وَالوِرَاثَةُ، الاْنَ إِذْ رَجَعَ الحَقُّ إِلَى أَهْلِهِ، وَنُقِلَ إِلَى مُنْتَقَلِهِ.

Waliupanda uovu na wakaunyweshea kwa hila na walivuna maangamizi[25] , Aali Muhammad(a.s) Hawalinganishwi na yeyote kutika Ummah huu, wala hawawi sawa kabisa nao ambao neema zao zimepitia kwao. Wao ndio msingi wa dini, na nguzo ya yakini. Kwao hurejeshwa mwenye kuvuka mpaka, na kwao huunganishwa aliyeachwa nyuma[26] . Haki ya uongozi ni mahususi kwao. Na kwao kuna wasia na urithi; hivi sasa wakati haki imerejea kwa wenyewe, na inahamishiwa mahala penyewe!

3. KATIKA JUMLA YA KHUTBA ZAKE(a.s) :

Nayo ni ile maarufu kuwa ni khutba ya Shaq’shaqiyah[27] .

أَمَا وَالله لَقَدْ تَقَمَّصَها فُلانٌ، وَإِنَّهُ لَيَعْلَمُ أَنَّ مَحَلِّيَ مِنهَا مَحَلُّ القُطْبِ مِنَ الرَّحَا، يَنْحَدِرُ عَنِّي السَّيْلُ، وَلا يَرْقَى إِلَيَّ الطَّيْرُ، فَسَدَلْتُ دُونَهَا ثَوْباً، وَطَوَيْتُ عَنْهَا كَشْحاً، وَطَفِقْتُ أَرْتَئِي بَيْنَ أَنْ أَصُولَ بِيَد جَذَّاءَ، أَوْ أَصْبِرَ عَلَى طَخْيَة عَمْيَاءَ، يَهْرَمُ فيهَا الكَبيرُ، وَيَشِيبُ فِيهَا الصَّغِيرُ، وَيَكْدَحُ فِيهَا مُؤْمِنٌ حَتَّى يَلْقَى رَبَّهُ

Amma! Wallahi fulani, ameuvaa (Ukhalifa)[28] hali akiwa yuajuwa kuwa nafasi yangu kuhusiana nao ni sawa na mahala pa muhimili wa jiwe la kusagia, maji ya mafuriko huniporomokea wala ndege hawezi kunirukia. Nilijikinga nao kwa nguo na nikajiweka kando nao. Nikajifikiria, je! Nishambulie na mkono butu, au nilivumilie giza la upofu[29] , mtu mkubwa humo huzeeka, na mdogo humo huwa kijana, muumini anataabika humo mpaka akutane na Mola wake.

فَرَأَيْتُ أَنَّ الصَّبْرَ عَلَى هَاتَا أَحْجَى، فَصَبَرتُ وَفي الْعَيْنِ قَذىً، وَفي الحَلْقِ شَجاً، أرى تُرَاثي نَهْباً، حَتَّى مَضَى الاْوَّلُ لِسَبِيلِهِ، فَأَدْلَى بِهَا إِلَى فلان بَعْدَهُ

Nikaona kuivumilia hali hii ni busara, basi nikasubiri hali jichoni mwangu muna utongotongo, na kooni kuna kitu kilichokwama. Naiona mirathi yangu imepokonywa[30] , wa kwanza akapita katika njia yake, - yaani alikufa - akampasia (ukhalifa) fulani baada yake.

ثم تمثل بقول الاعشى : شَتَّانَ مَا يَوْمِي عَلَى كُورِهَا وَيَوْمُ حَيَّانَ أَخِي جَابِرِ.

Kisha Alinakili ubeti wa kauli ya Al-A’asha - maana yake: kuna tofauti kubwa kati ya siku yangu nikiwa juu ya ngamia na siku ya Hayyani nduguye Jabir: (yaanni siku ya Hayyani ilikuwa ya raha).

فَيَا عَجَباً!! بَيْنَا هُوَ يَسْتَقِيلُها في حَيَاتِهِ إِذْ عَقَدَهَا لاخَرَ بَعْدَ وَفَاتِهِ ـ لَشَدَّ مَا تَشَطَّرَا ضَرْعَيْهَا ! ـ فَصَيَّرَهَا في حَوْزَة خَشْنَاءَ، يَغْلُظُ كَلْمُهَا، وَيَخْشُنُ مَسُّهَا، وَيَكْثُرُ العِثَارُ[فِيهَا] وَالاْعْتَذَارُ مِنْهَا، فَصَاحِبُهَا كَرَاكِبِ الصَّعْبَةِ، إِنْ أَشْنَقَ لَهَا خَرَمَ، وَإِنْ أَسْلَسَ لَهَا تَقَحَّمَ، فَمُنِيَ النَّاسُ ـ لَعَمْرُ اللهِ ـ بِخَبْط وَشِمَاس، وَتَلَوُّن وَاعْتِرَاض.

Ajabu ilioje! Alikuwa anaomba wamuuzulu wakati wa uhai wake, punde si punde akaagiza uende kwa mwingine baada ya kifo chake! Kwa hakika wameshirikiana viwele vyake viwili wao kwa wao tu, huyu mmoja ameuweka (ukhalifa) katika upande ulio mgumu, mguso wake wakwaruza, kujikwaa kunakithiri na kuomba udhuru, aliyekuwa nao ni kama aliyepanda ngamia machachari asiyepandika: akimvuta hatamu atamkaba na akimlegezea atamtupa kweye maangamizi, hapo wallahi watu watapatwa na myumbo, uovu na kupotoka.

فَصَبَرْتُ عَلَى طُولِ الْمُدَّةِ، وَشِدَّةِ الْمحْنَةِ، حَتَّى إِذا مَضَى لِسَبِيلِهِ جَعَلَهَا في جَمَاعَة زَعَمَ أَنَّي أَحَدُهُمْ. فَيَاللهِ وَلِلشُّورَى! مَتَى اعْتَرَضَ الرَّيْبُ فِيَّ مَعَ الاْوَّلِ مِنْهُمْ، حَتَّى صِرْتُ أُقْرَنُ إِلَى هذِهِ النَّظَائِرِ! لكِنِّي أَسفَفْتُ إِذْ أَسَفُّوا، وَطِرْتُ إِذْ طَارُوا، فَصَغَا رَجُلُ مِنْهُمْ لِضِغْنِه، وَمَالَ الاْخَرُ لِصِهْرهِ، مَعَ هَن وَهَن.

Nilivumilia kwa muda mrefu wote huo, ingawaje ulikuwa mtihani mgumu: Na alipofikia muda wake akauweka chini ya uchaguzi wa kundi la watu sita akadai akinidhania mimi ni mmoja kati yao. Eee Mungu! Nahusika nini mimi na Shuura![31] .

Lini ameingiwa na shaka na mimi wa kwanza katika wao kiasi niwe naambatanishwa na mfano wa hawa! Lakini nilitua walipotua, na niliruka waliporuka, mtu miongoni mwao alinigeuka kwa sababu ya kunichukia kwake[32] , na mwingine alielemea upande wa shemeji yake[33] . Pakiwa na hili na lile.

إِلَى أَنْ قَامَ ثَالِثُ القَوْمِ، نَافِجَاً حِضْنَيْهِ بَيْنَ نَثِيلهِ وَمُعْتَلَفِهِ، وَقَامَ مَعَهُ بَنُو أَبِيهِ يَخْضَمُونَ مَالَ اللهِ خَضْمَ الاْبِل نِبْتَةَ الرَّبِيعِ، إِلَى أَنِ انْتَكَثَ عَلَيْهِ فَتْلُهُ، وَأَجْهَزَ عَلَيْهِ عَمَلُهُ، وَكَبَتْ بِهِ بِطْنَتُهُ

Mpaka akasimama watatu wao hali ameinua kifua chake mbele kati ya kinyesi chake na chakula chake - chakula cha mifugo - walisimama pamoja naye watoto wa babu yake, wakawa wanazitafuna mali za Mungu kama anavyotafuna ngamia majani ya msimu wa kuchipua (spring season), mpaka kamba yake ikakatika, na matendo yake yakammaliza, na ulafi wake ukamtupa chini kifudifudi.

فَمَا رَاعَنِي إلاَّ وَالنَّاسُ إليَّ كَعُرْفِ الضَّبُعِ، يَنْثَالُونَ عَلَيَّ مِنْ كُلِّ جَانِب، حَتَّى لَقَدْ وُطِىءَ الحَسَنَانِ، وَشُقَّ عِطْفَايَ، مُجْتَمِعِينَ حَوْلي كَرَبِيضَةِ الغَنَمِ

Nilishitushwa na kundi la watu likimiminika kuja kwangu mfano wa manyoya ya shingoni mwa fisi toka kila upande, kiasi kwamba Hasan na Husayn walikanyagwa, na sehemu za ncha za mabega ya vazi langu zikararuriwa, wakiwa wamejikusanya kunizunguka kama kundi la kondoo na mbuzi.

فَلَمَّا نَهَضْتُ بِالاْمْرِ نَكَثَتْ طَائِفَةٌ، وَمَرَقَتْ أُخْرَى، وَفَسَقَ [وقسط ]آخَرُونَ كَأَنَّهُمْ لَمْ يَسْمَعُوا اللهَ سُبْحَانَهُ يَقُولُ: تِلْكَ الدَّارُ الاخِرَةُ نَجْعَلُهَاِ للَّذِينَ لاَ يُريدُونَ عُلُوّاً في الاَرْضِ وَلاَ فَسَاداً وَالعَاقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ

Nilipochukua hatamu za uongozi, kundi moja lilivunja ahadi na jingine liliasi, na lililobaki lilifanya uovu na dhulma[34] kana kwamba hawakusikia neno la Mungu aliposema: “Hayo ndiyo makazi ya akhera, tumewafanyia wale wasiotaka kujitukuza duniani wala ufisadi, na mwisho mwema ni wa wachamungu .” (28:83).

بَلَى! وَاللهِ لَقَدْ سَمِعُوهَا وَوَعَوْهَا، وَلكِنَّهُمْ حَلِيَتَ الدُّنْيَا في أَعْيُنِهمْ، وَرَاقَهُمْ زِبْرِجُهَا! أَمَا وَالَّذِي فَلَقَ الْحَبَّةَ، وَبَرَأَ النَّسَمَةَ، لَوْلاَ حُضُورُ الْحَاضِرِ، وَقِيَامُ الْحُجَّةِ بِوُجُودِ النَّاصِرِ، وَمَا أَخَذَ اللهُ عَلَى العُلَمَاءِ أَلاَّ يُقَارُّوا عَلَى كِظَّةِ ظَالِم، وَلا سَغَبِ مَظْلُوم، لاَلقَيْتُ حَبْلَهَا عَلَى غَارِبِهَا، وَلَسَقَيْتُ آخِرَهَا بِكَأْسِ أَوَّلِها، وَلاَلفَيْتُمْ دُنْيَاكُمْ هذِهِ أَزْهَدَ عِنْدِي مِنْ عَفْطَةِ عَنْز!

Ndio wallahi waliyasikia na waliyaelewa lakini machoni mwao dunia ilijipamba na kuliwapendeza kujiremba kwake. Angalia! naapa kwa yule ambaye ameatua mbegu na kumuumba binadamu, lau si kufika kwa watu na kulazimu hoja kwa kuwepo wasaidizi - yaani askari wa kumnusuru - na ahadi iliyochukuliwa na Mungu kwa wanachuoni, kuwa wasiridhike kimya kimya na ulafi wa madhalimu na kusagwa kwa haki ya mdhulumiwa, ningeitupa kamba ya ukhalifa kwenye bega lake - yaani ninge tupilia mbali suala la ukhalifa bila kujali - na ningemtendea wa mwisho kama wa kwanza. Na mungeona kwa maoni yangu huu ulimwengu wenu si bora kuliko chafya ya mbuzi”.

قالوا: وقام إِليه رجل من أهل السواد عند بلوغه إلى هذا الموضع من خطبته، فناوله كتاباً، فأقبل ينظر فيه، فلمّا فرغ من قراءته قال له ابن عباس: يا أميرالمؤمنين، لو اطَّرَدت مَقالتكَ من حيث أَفضيتَ.

Walisema kuwa: Amirul-Mu’minina alipofikia hapa katika KHUTBA hii, mtu mmoja katika watu wa Iraqi alisimama na kumkabidhi karatasi yenye maandishi, akawa anaiangalia, alipomaliza kuisoma, ibn Abbas alimwambia: Ewe Amirul-Mu’minina ungeendelea na KHUTBA yako ulipoachia!

فَقَالَ(عليه السلام) : هَيْهَاتَ يَابْنَ عَبَّاس! تِلْكَ شِقْشِقَةٌ هَدَرَتْ ثُمَّ قَرَّتْ !

Hivyo basi alijibu: “Ewe ibn Abbas hilo ni povu la ngamia, ameunguruma kisha akanyamaza”.

قال ابن عباس: فوالله ما أَسفت على كلام قطّ كأَسفي على ذلك الكلام أَلاَّ يكون أميرالمؤمنين(عليه السلام)بلغ منه حيث أراد

Ibn Abbas akasema: “Wallahi sikuwahi kuhuzunikia maneno kamwe, kama huzuni yangu juu ya maneno haya kwamba awe Amirul-Mu’minin hakufikia alipotaka”.

Amesema Sharifu (r.a), kauli yake(a.s) : “Ni kama mfano wa aliyepanda ngamia mkorofi”: Anakusudia kuwa, ikiwa atakaza kuvuta hatamu hali akimkinza kichwa chake atararua pua yake, na endapo atamlegezea kitu kidogo na ugumu wake atamuendesha mbio ovyo, na wala hatomdhibiti, husemwa: Ashnaka naakata akikivuta kichwa chake kwa hatamu na kukiinua, na Washanakahaa aidhwan, pia hutumika kwa maana hiyo, hilo limesemwa na ibn Sakiit katika kitabu Islahu al-Mantiq. Na sababu ya kusema(a.s) (Ashanaka laha) na wala hakusema Ashnaakaha kwa kuwa amelijaalia liwe mkabala wa kauli yake: (Aslasalaha) hivyo inakuwa kama kwamba amesema: In raf ’a laha ra’saha bizimami: yaani ameishika.

Na katika hadithi imekuja kuwa Mtume wa Mungu(s.a.w.w) alihutubia akiwa juu ya ngamia aliyemvuta hatamu kwa kuinua kichwa chake.

Na miongoni mwa ushahidi kuwa (ashnaka) maana yake (Shaanaka) ni kauli ya Adiyyu bin Zayd al-Abadiyy: Sa’a aha maa tabaiyyana fil aidi wa ish- nakuhaa ilal-a’anaaqi.

4. NA MIONGONI MWA KHUTBA ZAKE(a.s)

وفيها يعظ الناس ويهديهم من ضلالتهم، ويقال: إنه خطبها بعد قتل طلحة والزبير.

Hotuba hii ameitoa baada ya kuuliwa Talha na Zubair ili kuwaongoza watu na (kuwabainishia) ukamilifu wa yakini ya ustahiki wa uongozi wake:-

بِنَا اهْتَدَيْتُمْ في الظَّلْمَاءِ، وَتَسَنَّمْتُمُ العلْيَاءَ، وبِنَا انْفَجَرْتُم عَنِ السِّرَارِ، وُقِرَ سَمْعٌ لَمْ يَفْقَهِ الوَاعِيَةَ، كَيْفَ يُرَاعِي النَّبْأَةَ مَنْ أَصَمَّتْهُ الصَّيْحَةُ؟ رُبِطَ جَنَانٌ لَمْ يُفَارِقْهُ الخَفَقَانُ.

“Kupitia sisi mumeongoka kutoka gizani[35] na mumepanda daraja ya juu. Na kupitia sisi mumepambazukiwa na alfajiri mkiwa mbali na giza la usiku. Asiyenisikia, basi lizibe sikio lisilosikia mawaidha. Vipi ataisikia sauti dhaifu na aizingatie aliyefanywa kiziwi (hakuweza kusikia) na ukelele wa sauti kubwa? (Atasikia sauti yangu dhaifu?). Uimarike moyo ulioendelea kumwogopa Allah.

مَا زِلتُ أَنْتَظِرُ بِكُمْ عَوَاقِبَ الغَدْرِ، وَأَتَوَسَّمُكُمْ بِحِلْيَةِ الـمُغْتَرِّينَ، سَتَرَني عَنْكُمْ جِلْبَابُ الدِّينِ، وَبَصَّرَنِيكُمْ صِدْقُ النِّيَّةِ، أَقَمْتُ لَكُمْ عَلَى سَنَنِ الحَقِّ في جَوَادِّ الـمَضَلَّةِ، حيْثُ تَلْتَقُونَ وَلا دَلِيلَ، وَتَحْتَفِرُونَ وَلا تُميِهُونَ

Siku zote nilikuwa natazamia kutoka kwenu usaliti, na nimekuoneni ndani ya pambo la walioghurika, pazia ya dini imewaficheni mbali na mimi. Lakini nia yangu ya kweli imenionesha mlivyo. Nilizisimamisha kwa ajili yenu njia za haki kati ya njia za upotovu, hali ikiwa mlikuwa mnakutana lakini hapakuwa na kiongozi, na mlichimba bila ya kupatikana maji.

اليَوْمَ أُنْطِقُ لَكُمُ العَجْمَاءَ ذاتَ البَيَان! عَزَبَ رَأْيُ امْرِىء تَخَلَّفَ عَنِّي، مَا شَكَكْتُ في الحَقِّ مُذْ أُرِيتُهُ! لَمْ يُوجِسْ مُوسَى خِيفَةً عَلَى نَفْسِهِ، أَشْفَقَ مِنْ غَلَبَةِ الجُهَّالِ وَدُوَلِ الضَّلالِ! اليَوْمَ تَوَاقَفْنَا عَلَى سَبِيلِ الحَقِّ وَالباطِلِ، مَنْ وَثِقَ بِمَاء لَمْ يَظْمَأْ!

Leo navifanya hivi vitu bubu[36] vyenye ubainifu viwasemesheni. Hana rai mwenye kuwa kinyume na mimi. Sikuwa na shaka na haki toka nilipoonyeshwa! Musa(a.s) hakujihofia binafsi[37] , bali alihofia ushindi wa majahili na zamu ya upotovu! Leo tumesimama njia panda kati ya haki na batili[38] . Mwenye kuwa na hakika ya kupata maji hawezi kuhisi kiu[39] .

Maelezo: Maneno haya na mifano yamedondolewa kutoka KHUTBA ndefu iliyonasibishwa kwake(a.s) , kaumu ya watu fulani imezidisha humo vitu, kilichowafanya wafanye hivyo ni utashi wa nafsi zao.

Matamshi hayo hayaafikiani na utaratibu wake(a.s) katika KHUTBA, wala ufasaha wa hayo hauendani na ufasaha wake. Wala hapana haja ya kutaja kwa kuwa ni mashuhuri.

Na sisi tutafafanua matamko haya, kwa kuwa ni maneno yake(a.s) , hawi na shaka na hilo mwenye dhouqu na naqdu na kuwa na maarifa na mwenendo wa watoa khutba na wenye ufasaha katika khutba zao na risala zao. Na kwa sababu Ar-Radhiyy (r.a) ameidondoa na ameinasibisha kwake(a.s) na ameisahihisha na kuondoa yasiyo yake.