NAHJULBALAGHAH Juzuu 1

NAHJULBALAGHAH0%

NAHJULBALAGHAH Mwandishi:
: Sheikh Haruna Pingili
Kundi: VITABU VYA HADITHI

NAHJULBALAGHAH

Mwandishi: SAYYIDI SHARIFU RADHIY
: Sheikh Haruna Pingili
Kundi:

Matembeleo: 5489
Pakua: 2025


Maelezo zaidi:

Juzuu 1 Juzuu 2
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 7 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 5489 / Pakua: 2025
Kiwango Kiwango Kiwango
NAHJULBALAGHAH

NAHJULBALAGHAH Juzuu 1

Mwandishi:
Swahili

NAHJUL-BALAGHAH

JUZUU YA KWANZA

5. MIONGONI MWA KHUTBA ZAKE(a.s)

لمّا قبض رسول الله (صلى الله عليه وآله) وخاطبه العباس وأبوسفيان في أن يبايعا له بالخلافة:

Alipofishwa Mtume wa Mungu(s.a.w.w) , Abbas na Abu Sufyan bin Harb walimsemesha Ali(a.s) kuwa wamfanyie bai’a ya ukhalifa, ndipo aliposema(a.s) :

أَيُّها النَّاسُ، شُقُّوا أَمْوَاجَ الفِتَنِ بِسُفُنِ النَّجَاةِ، وَعَرِّجُوا عَنْ طَريقِ الـمُنَافَرَةِ، وَضَعُوا تِيجَانَ الـمُفَاخَرَةِ أَفْلَحَ مَنْ نَهَضَ بِجَنَاح، أوِ اسْتَسْلَمَ فَأَراحَ.

Enyi watu! yapasueni mawimbi ya fitna kwa merikebu za uokovu, na jiepusheni na njia za chuki, vueni taji za fahari, atakuwa amefanikiwa mwenye kuinuka na bawa[40] , au asalimu amri akapumzisha (akapumzisha nafsi yake au wengine wakabaki salama).

مَاءٌ آجِنٌ(3)، وَلُقْمَةٌ يَغَصُّ بِهَا آكِلُهَا، وَمُجْتَنِي الَّثمَرَةِ لِغَيْرِ وَقْتِ إِينَاعِهَا(4) كالزَّارعِ بِغَيْرِ أَرْضِهِ

Ni maji machafu[41] , na ni tonge limkwamalo mlaji wake, na ni sawa na mchuma matunda kabla ya wakati wa kupevuka kwake[42] , na ni sawa na mkulima wa ardhi isiyo yake.

فَإِنْ أقُلْ يَقُولُوا: حَرَصَ عَلَى الـمُلْكِ، وَإنْ أَسْكُتْ يَقُولُوا: جَزعَ مِنَ المَوْتِ! هَيْهَاتَ بَعْدَ اللَّتَيَّا وَالَّتِي! وَاللهِ لاَبْنُ أَبي طَالِب آنَسُ بالمَوْتِ مِنَ الطِّفْلِ بِثَدْي أُمِّهِ، بَلِ انْدَمَجْتُ عَلَى مَكْنُونِ عِلْم لَوْ بُحْتُ بِهِ لاَضْطَرَبْتُمُ اضْطِرَابَ الاْرْشِيَةِ في الطَّوِيِّ البَعِيدَةِ !

Nikisema mimi watasema: Amepupia ufalme, na nikinyamaza watasema: Amekuwa si mvumilivu wa umauti! haiwi baada ya kale (kafupi) na huyu (mrefu)![43] Wallahi mwana wa Abi Talib ni mchangamfu mno wa mauti kuliko mtoto mchanga anavyochangamkia ziwa la mama yake, isipokuwa nimezingirwa ndani ya ilimu iliyositiriwa, lau ningeifichua mngetetemeka mtetemo wa kamba ya kisima cha ndoo katika kisima kirefu.

6. MIONGONI MWA KHUTBA ZAKE(a.s)

ومن كلام له (عليه السلام) لمّا أشير عليه بألاّ يتبع طلحةَ والزبيرَ ولا يُرصدَ لهما القتال:

Aliposhauriwa kuwa asimfuatilie Talha na Zubair wala kwa lengo la kupambana dhidi ya Alisema:

وَاللهِ لاَ أَكُونُ كالضَّبُعِ: تَنَامُ عَلى طُولِ اللَّدْمِ، حَتَّى يَصِلَ إِلَيْهَا طَالِبُهَا،وَيَخْتِلَهَا رَاصِدُها، وَلكِنِّي أَضْرِبُ بِالمُقْبِلِ إِلَى الحَقِّ المُدْبِرَ عَنْهُ، وَبِالسَّامِعِ المُطِيعِ العَاصِيَ المُريبَ أَبَداً، حَتَّى يَأْتِيَ عَلَيَّ يَوْمِي فَوَاللهِ مَا زِلتُ مَدْفُوعاً عَنْ حَقِّي، مُسْتَأْثَراً عَلَيَّ، مُنْذُ قَبَضَ اللهُ تعالى نَبِيَّهُ(صلى الله عليه وآله)حَتَّى يَوْمِ النَّاسِ هذَا.

Wallahi siwi kama fisi anayelala muda wote wa mdundo mpaka amfike anayemtafuta, na amhadae muwindaji wake. Lakini mimi nitampiga aigeuziaye mgongo haki kwa msaada wa anayeikubali, na kwa msaada wa msikivu mtii nitampiga, nitampiga muasi mwenye shaka daima, mpaka nijiwe na siku yangu (ya mauti); Wallahi ningali nasukumwa mbali na haki yangu, imetwaliwa kinyume nami toka siku Mwenyezi Mungu Mtukufu alipomfisha Nabii wake(s.a.w.w) mpaka siku hii ya leo[44] .

7. MIONGONI MWA KHUTBA ZAKE(a.s)

ومن خطبة له (عليه السلام)، يذم فيها أتباع الشيطان

Katika kuwalaumu wafuasi wa Shetani:

اتَّخَذُوا الشَّيْطَانَ لاِمْرِهِمْ مِلاَكاً، وَاتَّخَذَهُمْ لَهُ أَشْرَاكاً، فَبَاضَ وَفَرَّخَ في صُدُورِهِمْ، وَدَبَّ وَدَرَجَ في حُجُورِهِمْ، فَنَظَرَ بِأَعْيُنِهِمْ، وَنَطَقَبِ أَلسِنَتِهِمْ، فَرَكِبَ بِهِمُ الزَّلَلَ، وَزَيَّنَ لَهُمُ الخَطَلَ، فِعْلَ مَنْ قَدْ شَرِكَهُ الشَّيْطَانُ في سُلْطَانِهِ، وَنَطَقَ بِالبَاطِلِ عَلى لِسَانِهِ!

Wamemfanya shetani kuwa ndio kiini cha mambo yao, na yeye amewafanya washirika wake. Hivyo basi ametaga na kutotoa vifuani mwao,1 na ametambaa na kujiburuza mapajani mwao,2kwa hiyo aliangalia kwa macho yao, na alitamka kwa ndimi zao, hivyo basi aliwapotosha, na kuwapambia kauli ovu, na makosa mabaya ni kitendo cha ambaye shetani ameshirikiana naye katika mamlaka yake na akatamka ya batili ulimini mwake.”

8. NA MIONGONI MWA MANENO YAKE(A.S)

ومن كلام له (عليه السلام)

يعني به الزبير في حال اقتضت ذلك ] ويدعوه للدخول في البيعة ثانية [

Kwayo anamkusudia Zubair katika hali ambayo ilibidi iwe hivyo:

يَزْعُمُ أَنَّهُ قَدْ بَايَعَ بِيَدِهِ، وَلَمْ يُبَايعْ بِقَلْبِهِ، فَقَدْ أَقَرَّ بِالبَيْعَةِ، وَادَّعَى الوَلِيجَةَ(4)، فَلْيَأْتِ عَلَيْهَا بِأَمْر يُعْرَفُ، وَإِلاَّ فَلْيَدخُلْ فِيَما خَرَجَ مِنْهُ

Anadhani kuwa amekula kiapo cha utii kwa mkono wake, wala hakula kiapo kwa moyo wake, kwa hiyo amekiri kula kiapo cha utii, na anadai yaliyojificha ndani ya dhamira yake, basi na alete hoja ya kuthibitisha hilo, kama sivyo yampasa aingie alikotoka[45] .

9. MIONGONI MWA MANENO YAKE(A.S)

ومن كلام له (عليه السلام)

في صفته وصفة خصومه ويقال إنّها في أصحاب الجمل

Miongoni mwa maneno yake(a.s). Maelezo yanayomhusu(a.s) na maelezo ya mahasimu wake, na pengine husemwa kuwa: yanawahusu watu wa Vita vya Jamal (Ngamia):

وقَدْ أَرْعَدُوا وَأبْرَقُوا، وَمَعَ هذَيْنِ الاْمْرَيْنِ الفَشَلُ، وَلَسْنَا نُرْعِدُ حَتَّى نُوقِعَ، وَلا نُسِيلُ حَتَّى نُمْطِرَ.

“Kwa kweli waliunguruma na kumulika[46] , pamoja na mambo mawili haya ni woga. Sisi hatuungurumi mpaka tushambulie adui na hatutiririki mpaka tunyeshe[47] .

10. MIONGONI MWA MANENO YAKE(A.S)

ومن خطبة له (عليه السلام)

يريد الشيطان أويكني به عن قوم

Miongoni mwa maneno yake(a.s) - Al wahihiy ameieleza hii ndani ya Kitabu chake (Al jamaalu).

Katika khutba hii huenda anamkusudia shetani wa kweli, na inawezekana awe anamkusudia Mu’awiya. Au kinaya - mfano wa maneno, anawakusudia watu fulani wafanyao yanayofanana na yafanywayo na shetani:

أَلاَ وإنَّ الشَّيْطَانَ قَدْ جَمَعَ حِزْبَهُ وَاسْتَجْلَبَ خَيْلَهُ وَرَجِلَهُ، وإِنَّ مَعِي لَبَصِيرَتي .مَا لَبَّسْتُ عَلَى نَفْسِي، وَلاَ لُبِّسَ عَلَيَّ. وَايْمُ اللهِ لاَفْرِطَنَّ لَهُمْ حَوْضاً أَنَا مَاتِحُهُ! لاَ يَصْدِرُونَ عَنْهُ، وَلاَ يَعُودُونَ إِلَيْهِ

Angalia! Kwa hakika shetani amekusanya kundi lake, na amewaleta wapanda farasi wake na askari waendao kwa miguu. Nami nina busara yangu. Sijajidanganya wala sijadanganywa. Nitawajazia hodhi la maji ambalo mimi ndiye mfutaji wake, hawarudi baada ya kunywa wala hawatolirudia[48] .

11. NA KATIKA MANENO YAKE(A.S)

ومن كلام له (عليه السلام)

لابنه محمّد بن الحنفية لمّا أعطاه الراية يوم الجمل

Kwa mwanawe Muhammad ibnul-Hanafiyya alipokuwa akimpa bendera siku ya Jamal:

تَزُولُ الجِبَالُ وَلاَ تَزُلْ! عَضَّ عَلَى نَاجِذِكَ، أَعِرِ اللهَ جُمجُمَتَكَ، تِدْفي الاْرْضِ قَدَمَكَ، ارْمِ بِبَصَرِكَ أَقْصَى القَوْمِ، وَغُضَّ بَصَرَكَ، وَاعْلَمْ أَنَّ النَّصْرَ مِنْ عِنْدِ اللهِ سُبْحَانَهُ

Milima huenda ikaondoka na ikatoweka (mahali pake) wewe usiondoke! Uma meno yako[49] . Mwazime Mungu fuvu lako la kichwa chako. Imarisha nyayo zako ardhini, mtazame adui wa mbali, fumba macho yako[50] . (Yaani usiogope adui kwa kujali wingi wao na kutishika), jua kuwa ushindi ni kutoka mwa Mwenyezi Mungu (s.w.t).

12. MIONGONI MWA MANENO YAKE(A.S)

ومن كلام له (عليه السلام)

لمّا أظفره الله تعالى بأصحاب الجمل

Mwenyezi Mungu alipompa ushindi dhidi ya watu wa Jamal (Ngamia).

وقد قال له بعض أصحابه:وددت أن أخي فلاناًمعك شاهداًليرى ما نصرك الله به علىأعدائك، فقال له عليه السلام :

Mmoja kati ya Sahaba wake alisema: “Natamani lau ndugu yangu fulani angekuwa yupo, ili aone ushindi Mungu aliokusaidia kuupata dhidi ya maadui zako.” Hapo akasema(a.s) :

أَهَوَى أَخِيكَ مَعَنَا؟ قال: نَعَم قالَ: فَقَدْ شَهِدنَا، وَلَقَدْ شَهِدَنَا في عَسْكَرِنَا هذَا أَقْوَامٌ في أَصْلاَبِ الرِّجَالِ، وَأَرْحَامِ النِّسَاءِ، سَيَرْعُفُ بِهِمُ الزَّمَانُ، ويَقْوَى بِهِمُ الاْيمَانُ

Je, mwelemeo na upendo wa ndugu yako u pamoja nasi?” Akasema: “Ndiyo,” akasema(a.s) : “Basi itakuwa kwamba alikuwa pamoja nasi katika kikosi cha askari wetu hawa, kwa hakika walikuwa wapo hata wale ambao bado wapo viunoni mwa wanaume na mifuko ya uzazi ya wanawake, punde tu wakati utawatoa, na kwa wao imani itakuwa na nguvu.

13. NA MIONGONI MWA MANENO YAKE(A.S)

ومن كلام له (عليه السلام)

في ذم البصرة وأهلها بعد وقعة الجمل

Kuwalaumu watu wa Basra baada ya vita vya Jamal (Ngamia):

كُنْتُمْ جُنْدَ الْمَرْأَةِ، وَأَتْبَاعَ البَهِيمَةِ، رَغَا فَأَجَبْتُم، وَعُقِرَ فَهَرَبْتُمْ أَخْلاَقُكُمْ دِقَاقٌ، وَعَهْدُكُمْ شِقَاقٌ، وَدِيْنُكُمْ نِفَاقٌ، وَمَاؤُكُمْ زُعَاقٌ المُقِيمُ بَيْنَ أَظْهُرِكُمْ مُرْتَهَنٌ بِذَنْبِهِ، وَالشَّاخِصُ عَنْكُمْ مُتَدَارَكٌ بِرَحْمة مِنْ رَبِّهِ كَأَنِّي بِمَسْجِدكُمْ كَجُؤْجُؤِ سَفِينَة، قَدْ بَعَثَ اللهُ عَلَيْها العَذَابَ مِنْ فَوْقِها وَمِنْ تَحتِها، وَغَرِقَ مَنْ في ضِمْنِها.

Mlikuwa askari wa mwanamke, na wafuasi wa mnyama[51] ; amepiga kelele mkamwitika, na akajeruhiwa mkakimbia. Tabia zenu ni mbaya na ahadi zenu ni khiyana na dini yenu ni unafiki, maji yenu ya chumvi[52] . Mwenye kuishi kati yenu yuko rehani kwa dhambi zake, mwenye kuondoka kwenu atapata amani ya rehema kutoka kwa Mola wake Mlezi. Kama nauona msikiti wenu wafanana na sehemu ya mbele ya Safina (boti), Mungu ameipeleka adhabu kutoka juu na kutoka chini yake, na waliomo humo wamezama.

وفي رواية: وَأيْمُ اللهِ لَتَغْرَقَنَّ بَلْدَتُكُمْ حَتَّى كَأَنِّي أَنْظُرُ إِلى مَسْجِدِهَا كَجُؤْجُؤِ سَفِينَة، أَوْ نَعَامَة جَاثِمَة.

Na katika riwaya nyingine: “Wallahi mji wenu utazama, kana kwamba nauona msikiti wenu ukiwa kama sehemu ya mbele ya boti au mbuni aliyeanguka kwa kifua chake.

وفي رواية أخرى: كَجُؤْجُؤِ طَيْر في لُجَّةِ بَحْر.

Na katika usemi wake mwingine: Kama kifua cha ndege katika kilindi cha bahari.

14. NA MIONGONI MWA USEMI WAKE(A.S)

ومن كلام له (عليه السلام)

في مثل ذلك

Katika mfano kama huo:

أرْضُكُمْ قَرِيبَةٌ مِنَ المَاءِ، بَعِيدَةٌ مِنَ السَّماءِ، خَفَّتْ عُقُولُكُمْ، وَسَفِهَتْ حُلُومُكُمْ، فَأَنْتُمْ غَرَضٌ لِنَابِل، وَأُكْلَةٌ لاِكِل، وَفَرِيسَةٌ لِصائِد

Ardhi yenu ipo karibu na maji. Iko mbali na mbingu [53] . Akili zenu ziko nyepesi, pia zimejaa upuuzi. Kwa hiyo nyinyi ni kilengwa cha mtupa mshale, na cha mlaji, na ni windo la mwindaji.

15. MIONGONI MWA MANENO YAKE(A.S)

ومن كلام له (عليه السلام)

فيما ردّه على المسلمين من قطائع عثمان

Kuhusiana na ardhi alizozirudisha kwa Waislamu kutoka Qata’iu za Uthman: [54]

وَاللهِ لَوْ وَجَدْتُهُ قَدْ تُزُوِّجَ بِهِ النِّسَاءُ، وَمُلِكَ بِهِ الاْمَاءُ، لَرَدَدْتُهُ; فَإِنَّ في العَدْلِ سَعَةً، وَمَنْ ضَاقَ عَلَيْهِ العَدْلُ، فَالجَوْرُ عَلَيْهِ أَضيَقُ !

“Wallahi hata ningezikuta (mali) zimetumika zikiwa mahari kwa kuolea wake, na vijakazi wamemilikiwa kwazo, ningezirudisha, kwa sababu kuwa katika uadilifu kuna wasaa.

Na ambaye umemuwia dhiki uadilifu, udhalimu kwake utakuwa dhiki mno. [55] .

16. MIONGONI MWA MANENO YAKE(A.S)

من كلام له (عليه السلام) لمّا بويع بالمدينة

[وفيها يخبر الناس بعلمه بما تؤول إليه أحوالهم وفيها يقسمهم إلى أقسام]

Baada ya kufanyiwa Bai’a huko Madina, na katika khutba hii anawapa watu habari juu ya ilimu yake ya yale yatakayojiri.

ذِمَّتي بِمَا أَقُولُ رَهِينَةٌ وَأَنَا بِهِ زَعِيمٌ: إِنَّ مَنْ صَرَّحَتْ لَهُ العِبَرُ عَمَّا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ المَثُلاتِ، حَجَزَهُ التَّقْوَى عَنْ تَقَحُّمِ الشُّبُهَاتِ أَلاَ وَإِنَّ بَلِيَّتَكُمْ قَدْ عَادَتْ كَهَيْئَتِهَا(1) يَوْمَ بَعَثَ اللهُ نَبِيَّهُ(صلى الله عليه وآله).

“Mimi ni dhamana wa niyasemayo, nayo yapo juu yangu. Kwa kweli mwenye kudhihirikiwa na mazingatio ya adhabu ya waliopita[56] iliyoko mbele yake taqwa itamzuia kujiingiza kwenye mambo yanayoshukiwa. Juweni kuwa balaa lenu limerudi katika sura yake ilivyo kuwa siku ambayo Mungu alimtuma Nabii wake(s.a.w.w) .[57]

وَالَّذِي بَعَثَهُ بِالحَقِّ لَتُبَلْبَلُنَّ(2) بَلْبَلَةً، وَلَتُغَرْبَلُنَّ غَرْبَلَةً(3)، وَلَتُسَاطُنَّ(4) سَوْطَ)القِدْرِ(5)، حَتَّى يَعُودَ أَسْفَلُكُمْ أَعْلاَكُمْ، وَأَعْلاَكُمْ أَسْفَلَكُمْ، وَلَيَسْبِقَنَّ سَابِقُونَ كَانُوا قَصَّرُوا، وَلَيُقَصِّرَنَّ سَبَّاقُونَ كَانُوا سَبَقُوا

Naapa kwa ambaye alimtuma (Muhammad{s.a.w.w} ) kwa ukweli mtachanganyikiwa vikali kabisa, na kutikiswa sana, na mtapigwa mfano wa mpigo wa chungu[58] mpaka aje juu aliyekuwa chini kati yenu, na aliyekuwa juu kati yenu aende chini, na Wallahi watatangulia waliokuwa nyuma, watachelewa nyuma waliokuwa wametangulia.”[59]

وَاللهِ مَا كَتَمْتُ وَشْمَةً، وَلا كَذَبْتُ كِذْبَةً، وَلَقَدْ نُبِّئْتُ بِهذا المَقامِ وَهذَا اليَوْمِ أَلاَ وَإِنَّ الخَطَايَا خَيْلٌ شُمُسٌ حُمِلَ عَلَيْهَا أَهْلُها، وَخُلِعَتْ لُجُمُهَا فَتَقَحَّمَتْ بِهِمْ في النَّارِ.

“Wallahi sikuwahi kuficha neno,[60] na mimi sikuwahi kusema uwongo na nilikwishapewa habari kuhusu hali hii na siku hii. Juweni kuwa makosa ni kama farasi aliyeasi (asiyepandika), wahusikao naye wamebebeshwa juu yake na akaondolewa hatamu zake na akawaingiza motoni.

أَلاَ وَإِنَّ التَّقْوَى مَطَايَا ذُلُلٌ، حُمِلَ عَلَيْهَا أَهْلُهَا، وَأُعْطُوا أَزِمَّتَها، فَأَوْرَدَتْهُمُ الجَنَّةَ حَقٌّ وَبَاطِلٌ، وَلِكُلٍّ أَهْلٌ، فَلَئِنْ أَمِرَ البَاطِلُ لَقَدِيماً فَعَلَ، وَلَئِنْ قَلَّ الحقُّ لَرُبَّما وَلَعَلَّ، وَلَقَلَّمَا أَدْبَرَ شَيءٌ فَأَقْبَلَ !

Ala! Juweni kuwa taqwa ni mfano wa farasi aliyefundishwa, wamebebeshwa wahusikao naye juu yake na wakakabidhiwa hatamu yake na akawafikisha Peponi. Kuna haki na kuna batili, na kila moja ina watu wake,[61] endapo batili ikishika hatamu, na toka zamani imefanya hivyo,[62] haki itaghilibiwa. Na haki inapokuwa ndogo, na imepata kuwa hivyo, ni mara chache kilichochelewa nyuma kuja mbele.[63]

وأقول: إنّ في هذا الكلام الادنى من مواقع الاحسان ملا تبلغه مواقع الاستحسان، وإنّ حظ العجب منه أكثر من حظ العُجب به، وفيه ـ مع الحال التي وصفنا ـ زوائد من الفصاحة لا يقوم بها لسان، ولا يَطَّلع فَجها إنسان، ولا يعرف ما أقوله إلاّ من ضرب في هذه الصناعة بحق، وجرى فيها على عرق، { وَمَا يَعْقِلُهَا إلاّ العَالمِونَ }.

Maelezo: Sayed Sharif alisema: kwa kweli ndani ya maneno haya machache kuna uzuri kuliko iwezavyo kutambuliwa, na kiwango cha kustaajabisha kilichochochewa nayo, ni zaidi kuliko utambuzi. Pamoja na hali tuliyoieleza muna ufasaha wa hali ya juu usiowezakufikiwa na mwingine. Na hawezi kuyatambua nisemayo isipokuwa mwenye kuwa na uelewa wa fani hii na kujuwa ilivyo. (Na hawaifahamu ila wenye ilimu; 29:43)

NA MIONGONI MWA YALIYO KATIKA KHUTBA HII

شُغِلَ مَنِ الجَنَّةُ وَالنَّارُ أَمَامَهُ! سَاع سَرِيعٌ نَجَا، وَطَالِبٌ بَطِيءٌ رَجَا، وَمُقَصِّرٌ في النَّارِ هَوَى الَيمِينُ وَالشِّمالُ مَضَلَّةٌ، وَالطَّرِيقُ الوُسْطَى هِيَ الجَادَّةُ(1)، عَلَيْهَا بَاقي الكِتَابِ وَآثَارُ النُّبُوَّةِ، وَمِنْهَا مَنْفَذُ السُّنَّةِ، وَإلَيْهَا مَصِيرُ العَاقِبَةِ

“Ameshughulishwa ambaye pepo na moto vi mbele yake! Mwenye juhudi na kuharakia atafaulu, na mtafutaji goigoi atakuwa na matumaini, mwenye kuzembea ataangamia motoni. Kulia na kushoto ni njia za upotofu, na njia ya kati ndio njia ya sawa, juu yake kuna Kitabu cha Milele na athari ya Nabii, na humo ndio mapitio ya Sunna na kwayo ndiyo hitimisho la matokeo.”

هَلَكَ مَنِ ادَّعى، وَخَابَ مَنِ افْتَرَى، مَنْ أَبْدَى صَفْحَتَهُ لِلْحَقِّ هَلَكَ، وَكَفَى بِالْمَرْءِ جَهْلاً أَلاَّ يَعْرِفَ قَدْرَهُ، لاَيَهْلِكُ عَلَى التَّقْوَى سِنْخُ(2) أَصْل، وَلاَ يَظْمَأُ عَلَيْهَا زَرْعُ قَوْم فَاسْتَتِرُوا بِبُيُوتِكُمْ، وَأَصْلِحُوا ذَاتَ بَيْنِكُمْ، وَالتَّوْبَةُ مِنْ وَرَائِكُمْ، وَلاَ يَحْمَدْ حَامِدٌ إِلاَّ رَبَّهُ، وَلاَ يَلُمْ لاَئِمٌ إِلاَّ نَفْسَهُ.

Mwenye kudai kinyume ameangamia na mwenye kuzua amepata hasara. Mwenye kukengeuka kwa uso wake ameangamia. Na yatosha mtu kuwa mjinga kwa kutojua hadhi yake. Hatoangamia aliyethibiti katika maoteo ya Uchamungu, wala mimea ya watu iliyo kwenye maoteo ya uchamungu haitokosa maji. Hivyo basi jisi- tirini majumbani mwenu, jirekibesheni wenyewe. Toba iko nyuma yenu, yampasa mtu kuhimidi asimhimidi ila Mola wake tu. Na mwenye kulaumu asilaumu ila nafsi yake.

17. MIONGONI MWA USEMI WAKE(A.S)

ومن كلام له (عليه السلام)

في صفة من يتصدّى للحكم بين الاْمة وليس لذلك بأَهل

Maelezo kuhusu wanaotoa hukumu kati ya watu hali wakiwa hawastahiki:

إِنَّ أَبْغَضَ الخَلائِقِ إِلَى اللهِ تعالى رَجُلانِ: رَجُلٌ وَكَلَهُ اللهُ إِلَى نَفْسِهِ، فَهُوَ جَائِرٌ عَنْ قَصْدِ السَّبِيلِ، مَشْغُوفٌ بِكَلاَمِ بِدْعَة، وَدُعَاءِ ضَلاَلَة، فَهُو فِتْنَةٌ لَمِنِ افْتَتَنَ بِهِ، ضَالٌّ عَنْ هَدْي مَنْ كَانَ قَبْلَهُ، مُضِلُّ لِمَنِ اقْتَدَى بِهِ في حَيَاتِهِ وَبَعْدَ وَفَاتِهِ، حَمَّالٌ خَطَايَا غَيْرِهِ، رَهْنٌ بِخَطِيئَتِهِ وَرَجُلٌ قَمَشَ جَهْلاً، مُوضِعٌ في جُهَّالِ الاْمَّةِ، غادر في أَغْبَاشِ الفِتْنَةِ، عِم بِمَا في عَقْدِ الهُدْنَةِ، قَدْ سَمَّاهُ أَشْبَاهُ النَّاسِ عَالمِاً وَلَيْسَ بِهِ

Kwahakika viumbe vyenye kuchukiza mno kwa Mwenyezi Mungu ni watu wa aina mbili: Aina ya kwanza: ni mtu ambaye Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemtelekeza yeye na nafsi yake. Huyu amepotoka mbali na njia ya kweli[64] ,anapenda sana kusema maneno ya bida’a na kuwaitia kwenye upotovu, kwa hiyo huyu ni fitna kwa wenye kudanganyika naye. Amepotea mbali na mwongozo wa waliokuwa wa kabla yake. Mwenye kuwapotosha wamfuatao maishani mwake na baada ya kufa kwake, mwenye kubeba makosa ya wengine, amekuwa rehani wa makosa yake. Aina ya pili: “Mtu aliyekusanya ujinga, yu aharakisha kati ya umma wak- ijahili kuwaghushi na kuwadanganya. Haraka haraka afaidika na giza la fitna. Haoni faida iliyo katika utulivu. Walio mfano wa watu wamemwita mjuzi wala hayuko hivyo.

بَكَّرَ فَاسْتَكْثَرَ مِنْ جَمْع، مَا قَلَّ مِنْهُ خَيْرٌ مِمَّا كَثُرَ، حَتَّى إِذَا ارْتَوَى مِنْ مَاء آجِن، وَأكْثَر مِن غَيْرِ طَائِل، جَلَسَ بَيْنَ النَّاسِ قَاضِياً ضَامِناً لِتَخْلِيصِ مَا التَبَسَ عَلَى غيْرِهِ، فَإِنْ نَزَلَتْ بِهِ إِحْدَى المُبْهَمَاتِ هَيَّأَ لَهَا حَشْواً رَثّاً مِنْ رَأْيِهِ، ثُمَّ قَطَعَ بِهِ، فَهُوَ مِنْ لَبْسِ الشُّبُهَاتِ في مِثْلِ نَسْجِ العَنْكَبُوتِ: لاَ يَدْرِي أَصَابَ أَمْ أَخْطَأَ، إنْ أَصَابَ خَافَ أَنْ يَكُونَ قَدْ أَخْطَأَ، وَإِنْ أَخْطَأَ رَجَا أَنْ يَكُونَ قَدْ أَصَابَ جَاهِلٌ خَبَّاطُ جَهلات، عَاش رَكَّابُ عَشَوَات.

Amefanya juhudi mapema asubuhi, na amekithirisha kukusanya vitu ambavyo uchache wake ni bora kuliko wingi wake, mpaka aondoapo kiu kwa maji machafu, na kukithirisha yasiyokuwa na maana, akaketi kati ya watu kama hakimu akichukua jukumu la kutatua yaliyowatatiza watu wengine, na endapo atafikwa na suala lenye maana isiyo dhahiri; ataliongelea kwa maneno mengi yasiyo kuwa na maana na kwa rai yake chakavu, kisha atalitolea maamuzi, kwa hiyo yeye katika kupanga mambo yenye utata ni kama utando wa buibui, hatambui amefanya sawa au amekosea; akifanya sawa yuahofia huenda amekosea, na akikosea huwa na matumaini ya kuwa amefanya sawa. Yu mjinga, anatangatanga bila ya mwongozo, haoni vizuri, mwenye kuyazamia mambo bila ya mwongozo.

لَمْ يَعَضَّ عَلَى العِلْمِ بِضِرْس قَاطِع، يُذرِي الرِّوَايَاتِ إذْراءَ الرِّيحِ الهَشِيمَ(6)، لاَ مَلِيٌ(7) ـ وَاللهِ ـ بِإِصْدَارِ مَا وَرَدَ عَلَيْهِ، وَلاَ هُوَ أَهْلٌ لِما فُوّضَ إليه، لاَ يَحْسَبُ العِلْمَ في شيْء مِمَّا أَنْكَرَهُ، وَلاَ يَرَى أَنَّ مِنْ وَرَاءِ مَا بَلَغَ منه مَذْهَباً لِغَيْرهِ، وَإِنْ أَظْلَمَ عَلَيْهِ أَمْرٌ اكْتَتَمَ بِهِ(8) لِمَا يَعْلَمُ مِنْ جَهْلِ نَفْسِهِ، تَصْرُخُ مِنْ جَوْرِ قَضَائِهِ الدِّمَاءُ، وَتَعَجُّ مِنْهُ المَوَارِيثُ.

Hakuishika ilimu kwa jino lenye makali, Riwaya anazipeperusha kama upepo upeperushavyo majani makavu[65] . Wallahi hawezi kuyatatua vyema matatizo yaliyoletwa kwake, wala hafai kwa jukumu alilopewa. Hajali kutojuwa asiyoyajuwa. Hatambui kuwa asilolijua yeye kuna ambao wanalijua. Na jambo lisipokuwa wazi kwake hulificha, kwa kuwa anajua kuwa mwenyewe ni mjinga. Damu zapiga kelele kutokana na hukumu zake zisizo za uadilifu, na mali zilizorithishwa vibaya zinamnung’unikia.

إِلَى اللهِ أَشْكُو مِنْ مَعْشَر يَعِيشُونَ جُهَّالاً، وَيَمُوتُونَ ضُلاَّلاً، لَيْسَ فِيهمْ سِلْعَةٌ أَبْوَرُ(2) مِنَ الكِتَابِ إِذَا تُلِيَ حَقَّ تِلاَوَتِهِ، وَلاَ سِلْعَةٌ أَنْفَقُ(3) بَيْعاً وَلاَ أَغْلَى ثَمَناً مِنَ الكِتَابِ إِذَا حُرِّفَ عَنْ مَوَاضِعِهِ، وَلاَ عِنْدَهُمْ أَنْكَرُ مِنَ المَعْرُوفِ، وَلاَ أَعْرَفُ مِنَ المُنكَرِ !

Ninalalamika kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuwahusu watu wanaoishi ujingani na wanakufa katika hali ya upotovu, kwao wao hakuna kisicho na thamani zaidi kuliko Kitabu (Qur’ani) endapo kitasomwa ipasavyo,[66] na wala hapana biashara yenye thamani zaidi kwa mauzo kuliko Kitabu (Qur’ani) endapo kitapotoshwa mbali na maeneo yake. Wala hapana kiovu zaidi kwao kuliko mema, na hapana mema zaidi kuliko maovu!”

18. NA MIONGONI MWA MANENO YAKE(A.S)

ومن كلام له (عليه السلام) في ذمّ اختلاف العلماء في الفتيا

Katika kulaumu tofauti za wanachuoni kwenye utoaji fatwa:

تَرِدُ عَلَى أحَدِهِمُ القَضِيَّةُ في حُكْم مِنَ الاْحْكَامِ فَيَحْكُمُ فِيهَا بِرَأْيِهِ، ثُمَّ تَرِدُ تِلْكَ القَضِيَّةُ بِعَيْنِهَا عَلَى غَيْرِهِ فَيَحْكُمُ فِيها بِخِلافِ قَوْلِهِ، ثُمَّ يَجْتَمِعُ القُضَاةُ بِذلِكَ عِنْدَ إمامِهِم الَّذِي اسْتَقْضَاهُم(4)، فَيُصَوِّبُ آرَاءَهُمْ جَمِيعاً، وَإِلهُهُمْ وَاحِدٌ! وَنَبِيُّهُمْ وَاحِدٌ! وَكِتَابُهُمْ وَاحِدٌ ! أَفَأَمَرَهُمُ اللهُ ـ سُبْحَانَهُ ـ بِالاخْتلاَفِ فَأَطَاعُوهُ! أَمْ نَهَاهُمْ عَنْهُ فَعَصَوْهُ! أَمْ أَنْزَلَ اللهُ سُبْحَانَهُ دِيناً نَاقِصاً فَاسْتَعَانَ بِهِمْ عَلَى إِتْمَامِهِ!

“Lamfikia mmojawao suala kuhusu hukumu mojawapo miongoni mwa hukumu, yeye analitolea hukumu kwa rai yake, kisha lamfikia tatizo lile lile mwanachuoni mwingine, yeye naye hulitolea hukumu tofauti na yule wa kwanza, kisha huwa makadhi au mahakimu wanakusanyika kwa Khalifa aliyewatawaza ukadhi na hukumu zile, naye anazipitisha kuwa ziko sahihi rai zao zote, hali Mungu wao ni mmoja! Nabii wao ni mmoja! na Kitabu chao ni kimoja! Je Mungu (s.w.t) aliwaamuru watofautiane na wao wakamtii!? Au aliwakataza kutofautiana wakamuasi! Au Mungu (s.w.t) aliteremsha dini yenye upungufu akaomba msaada kwao ili kuikamilisha!? Au walikuwa washirika Wake, kwa hiyo wao waseme watakalo na Yeye (s.w.t) apaswe kuridhika!?

أَمْ كَانُوا شُرَكَاءَ لَهُ فَلَهُمْ أَنْ يَقُولُوا وَعَلَيْهِ أَنْ يَرْضِى؟ أَمْ أَنْزَلَ اللهُ سُبْحَانَهُ دِيناً تَامّاً فَقَصَّرَ الرَّسُولُ(صلى الله عليه وآله) عَنْ تَبْلِيغِهِ وَأَدَائِهِ؟ وَاللهُ سُبْحَانَهُ يَقُولُ: (مَا فَرَّطْنَا في الكِتَابِ مِنْ شَيْء) وَفِيهِ تِبْيَانٌ لِكُلِّ شَيْء، وَذَكَرَ أَنَّ الكِتَابَ يُصَدِّقُ بَعْضاً، وَأَنَّهُ لاَ اخْتِلافَ فِيهِ، فَقَالَ سُبْحَانَهُ: { وَلَوْ كَانَ مِنْ عِنْدِ غَيرِ اللهِ لَوَجَدُوا فِيهِ اخْتِلافاً كَثِيراً } وَإِنَّ القُرآنَ ظَاهِرُهُ أَنِيقٌ(1)، وَبَاطِنُهُ عَمِيقٌ، لاَ تَفْنَى عَجَائِبُهُ، وَلاَتَنْقَضِي غَرَائِبُهُ، وَلاَ تُكْشَفُ الظُّلُمَاتُ إلاَّ بِهِ.

Au Mungu (s.w.t) aliteremsha dini iliyo kamili na Mtume(s.a.w.w) alizembea kuifikisha na kuitekeleza!, hali Mungu (s.w.t) anasema: “Hatujapuuza kitabuni kitu chochote” (6:38) “Ndani yake muna ubainifu wa kila kitu” na amesema kuwa Kitabu baadhi yake kinaisadikisha baadhi nyingine na yakuwa hakuna hitilafu humo kama alivyosema (s.w.t): “Lau ingekuwa imetoka kwa asiye Mwenyezi Mungu, bila shaka wangelikuta ndani yake khitilafu nyingi”. (An-Nisaa:82). Na yakuwa Qur’ani dhahiri yake nzuri yastaajabisha na sehemu yake ya ndani imekwenda kwa kina sana. Maajabu yake hayaishi wala mageni yake hayamaliziki wala mafum- bo yake hayatofumbuliwa isipokuwa kwayo.

19. MIONGONI MWA SEMI ZAKE(A.S)

ومن كلام له (عليه السلام)

قاله للاشعث بن قيس وهو على منبر الكوفة يخطب ، فمضى في بعض كلامه شيء اعترضه الاشعث، فقال: يا أميرالمؤمنين، هذه عليك لا لك، فخفض(عليه السلام) إليه بصره ثم قال:

Alimwambia Al-Ash’ath bin Qays, naye(a.s) akiwa juu ya mimbari ya al-Kufa akitoa hutba, kulipita jambo katika baadhi ya usemi wake ambalo Al-Ash’ath alilipinga. Akasema al-Ash’ath: “Yaa Amiral-Mu’minin, hili liko dhidi yako haliko kwa upande wako.”[67] Aliinamisha macho yake(a.s) na kutikisa kichwa na kumwangalia, kisha akasema:

ومَا يُدْرِيكَ مَا عَلَيَّ مِمَّا لِي؟ عَلَيْكَ لَعْنَةُ اللهِ وَلَعْنَةُ اللاَّعِنِينَ! حَائِكٌ ابْنُ حَائِك! مُنَافِقٌ ابْنُ كُافِر! وَاللهِ لَقَدْ أَسَرَكَ الكُفْرُ مَرَّةً وَالاسْلامُ أُخْرَى! فَمَا فَداكَ مِنْ وَاحِدَة مِنْهُمَا مَالُكَ وَلاَ حَسَبُكَ! وَإِنَّ امْرَأً دَلَّ عَلَى قَوْمِهِ السَّيْفَ، وَسَاقَ إِلَيْهِمُ الحَتْفَ، لَحَرِيٌّ أَنْ يَمقُتَهُ الاْقْرَبُ، وَلاَ يَأْمَنَهُ الاْبْعَدُ !

“Ni jambo gani linalokujulisha lililo dhidi yangu na ambalo ni langu! Laana ya Mungu iwe juu yako, na laana ya wenye kulaani, umfumaji, mtoto wa mfumaji,[68] wewe ni mnafiki mtoto wa kafiri. Wallahi ukafiri ulikuteka mara moja na uislamu mara nyingine.[69] Hukufidiwa kutoka mojawapo, si kwa mali yako wala kwa ukoo wako. Mtu huyu aliwafanyia hila watu wake wakapigwa kwa upanga na aliwasukumia kifo na maangamizi, anastahili kuchukiwa na watu wa karibu na haaminiwi na watu wa mbali.

قال الشريف الرضي: يريد(عليه السلام): أنه أُسر في الكفر مرة وفي الاِسلام مرة وأما قوله: «دل على قومه السيف»، فأراد به: حديثاً كان للاشعث مع خالد بن الوليد باليمامة، غرّ فيه قومه ومكر بهم حتى أوقع بهم خالد، وكان قومه بعد ذلك يسمونه «عُرْفَ النار»، وهو اسم للغادر عندهم.

Maelezo: ar-Radhiyu (r.a) amesema: “Amirul-Mu’minin(a.s) anakusudia kwamba huyu Ash’ath alitekwa akiwa mfungwa wa vita katika vita zama za ukafiri mara moja na katika Uislamu mara moja. Ama usemi wake(a.s) : (Dalla alaa Qaumihi saifa) alikusudia tukio lilikuwa kati ya Ash’ath na Khalid bin Al’Waliid huko Yamamah, aliwaghuri watu wake na kuwafanyia hila mpaka akasababisha Khalid awapige vita kwa upanga. Na baada ya hapo watu wa kaumu yake walikuwa wanamwita: “urfu nnari” nalo ni jina la mtu mdanganyifu kwao.”

20. KATIKA USEMI WAKE(A.S)

ومن خطبة له (عليه السلام)

فَإِنَّكُمْ لَوْ عَايَنْتُمْ مَا قَدْ عَايَنَ مَنْ مَاتَ مِنْكُمْ لَجَزِعْتُمْ وَوَهِلْتُمْ، وَسَمِعْتُمْ وَأَطَعْتُمْ، وَلكِنْ مَحْجُوبٌ عَنْكُمْ مَا عَايَنُوا، وَقَرِيبٌ مَا يُطْرَحُ الحِجَابُ! وَلَقَدْ بُصِّرْتُمْ إِنْ أَبْصَرْتُمْ، وَأُسْمِعْتُمْ إِنْ سَمِعْتُمْ، وَهُدِيتُمْ إِنِ اهْتَدَيْتُمْ، وَبِحَقٍّ أَقَولُ لَكُمْ: لَقَدْ جَاهَرَتْكُمُ العِبَرُ، وَزُجِرْتُمْ بِمَا فِيهِ مُزْدَجَرٌ، وَمَا يُبَلِّغُ عَنِ اللهِ بَعْدَ رُسُلِ السَّماءِ إِلاَّ البَشَرُ.

“Kwa hakika ninyi lau mungeyaona waliyoyaona waliokufa katika ninyi, mngefadhaishwa na kutishika, na mngesikiliza na kutii. Lakini yamefichika kwenu yale waliyoyaona, hivi punde pazia litaondolewa.[70] Mmeoneshwa isipokuwa kama hamkuona, na mmesikilizishwa, isipokuwa kama hamkusikia, na mumeongozwa isipokuwa kama hamkuongoka. Kwa haki nakuambieni mazingatio yamekudhihirikieni, na mumeonywa na ambayo (mtu) anaweza kuonyeka. Baada ya wajumbe wa mbingu (malaika) ni mwanadamu tu ndiye awezaye kufikisha ujumbe kutoka kwa Mungu.[71]

21. NA KATIKA JUMLA YA SEMI ZAKE(A.S)

ومن خطبة له (عليه السلام)

] وهي كلمة جامعة للعظة والحكمة [

Ili kuwawaidhi watu:-

فإِنَّ الغَايَةَ أَمَامَكُمْ، وَإِنَّ وَرَاءَكُمُ السَّاعَةَ تَحْدُوكُمْ، تَخَفَّفُوا تَلْحَقوا، فَإنَّمَا يُنْتَظَرُ بِأوَّلِكُمْ آخِرُكُمْ

Kwa kweli lengo liko mbele yenu[72] . Na kwa kweli nyuma yenu kuna (saa) kiyama kinakupelekeni munakoelekea. Jifanyeni wepesi mutawakuta[73] , bali tu, wa kwanza wenu wanawangoja wa mwisho wenu[74] .

قال الشريف الرضي: وأقول: إنّ هذا الكلام لو وزن بعد كلام الله سبحانه وكلام رسوله(صلى الله عليه وآله) بكل كلام لمال به راجحاً، وبرّز عليه سابقاً فأما قوله (عليه السلام): «تخففوا تلحقوا»، فما سمع كلام أقل منه مسموعاً ولا أكثر منه محصولاً، وما أبعد غورها من كلمة! وأنقع نطفتها من حكمة! وقد نبهنا في كتاب «الخصائص» على عظم قدرها وشرف جوهرها.

Maelezo: Sharif Ar-Radii (r.a) alisema: “Nasema kwa kweli maneno haya ya Ali lau yangewekwa kwenye mizani upande mmoja na maneno mengine upande mwingine mbali na maneno ya Mungu na maneno ya Mtume wake Mizani ingekuja chini kwa uzito wa maneno ya Ali, na yangethibiti kuwa na ushindi katika nyanja zote. Na usemi wake: “Takhaffafu tal’haqu” Kuweni wepesi mtashinda’ ni ibara fupi sana kupata kusikika iliyo na maana kubwa mno! Ina maana pana iliyoje! Bubujiko la hikima. Tumeishiria ukubwa wa maana yake katika Kitabu “Al-Khasa’is.”

22. MIONGONI MWA KHUTBA ZAKE(A.S)

ومن خطبة له (عليه السلام)

] حين بلغه خبر الناكثين ببيعته [

] وفيها يذم عملهم ويلزمهم دم عثمان ويتهدّدهم بالحرب [

] ذم الناكثين [

Walipomtuhumu kumuuwa Uthman (r.a):

أَلاَ وإِنَّ الشَّيْطَانَ قَدْ ذَمَّرَ حِزْبَهُ، وَاسْتَجْلَبَ جَلَبَهُ، لِيَعُودَ الجَوْرُ إِلَى أَوْطَانِهِ، وَيَرْجِعَ البِاطِلُ إِلَى نِصَابِهِ، وَاللهِ مَا أَنْكَرُوا عَلَيَّ مُنْكَراً، وَلاَ جَعَلُوا بَيْنِي وَبَيْنَهُمْ نَصِفاً (

“Jihadhari! Kwa kweli shetani ameanza kuwahimiza watu wake, na amekusanya wenzake ili udhalimu urejee kwenye nafasi yake, na irejee batili kwenye kiwango chake. Wallahi hawajaniona na jambo ovu waka- likanusha, wala hawajafanya insafu kati yangu na wao.

وَإِنَّهُمْ لَيَطْلُبُونَ حَقّاً هُمْ تَرَكُوهُ، وَدَماً هُمْ سَفَكُوهُ، فَلَئِنْ كُنْتُ شَرِيكَهُمْ فِيهِ فَإِنَّ لَهُمْ لَنَصِيبَهُمْ مِنْهُ، وَلَئِنْ كَانُوا وَلُوهُ دُوني، فَمَا التَّبِعَةُ إِلاَّ عِنْدَهُمْ، وَإِنَّ أَعْظَمَ حُجَّتِهِمْ لَعَلَى أَنْفُسِهِمْ، يَرْتَضِعُونَ أُمّاً قَدْ فَطَمَتْ، وَيُحْيُونَ بِدْعَةً قَدْ أُمِيتَتْ يا خَيْبَةَ الدَّاعِي! مَنْ دَعَا! وَإِلاَمَ أُجِيبَ! وَإِنِّي لَرَاض بِحُجَّةِ اللهِ عَلَيْهِمْ وَعِلْمِهِ فِيهمْ.

Kwa kweli wao wanaidai haki ambayo wameitelekeza, na damu ambayo wameimwaga, ikiwa nilikuwa mshirika wao basi bila shaka wana hisa humo, na ikiwa wao ndio waliotenda bila ya mimi, kisasi kitakuwa juu yao tu. Kwa kweli hoja yao kubwa dhidi yangu iko dhidi yao wenyewe. Wananyonyesha kwa mama alieacha kunyonyesha. Wanaihuisha bidaa iliyokwishauawa.

Oh! wee mdai usiyefanikiwa, njoo! Huu ndio wakati wako [75] .1 Nani mdai? Na kwa lipi ameitikiwa? Mimi naridhika na hoja ya Mungu dhidi yao na ujuzi Wake kwao.”

] التهديد بالحرب [

فَإِنْ أَبَوْا أَعْطَيْتُهُمْ حَدَّ السَّيْفِ، وَكَفَى بِهِ شَافِياً مِنَ البَاطِلِ، وَنَاصَراً لِلْحَقِّ ! وَمِنَ العَجَبِ بَعْثُهُمْ إِلَيَّ أَنْ أَبْرُزَ لِلطِّعَانِ! وَأَنْ أصْبِرَ لِلْجِلادِ! هَبِلَتْهُمُ الهَبُولُ! لَقَدْ كُنْتُ وَمَا أُهَدَّدُ بِالحَرْبِ، وَلاَ أُرَهَّبُ بِالضَّرْبِ! وَإِنِّي لَعَلَى يَقِين مِنْ رَبِّي، وَغَيْرِ شُبْهَة مِنْ دِيني.

TISHIO LA VITA!

“Endapo watakataa nitawakabili kwa makali ya upanga, ambao ni mponya- ji wa matendo batili na ni mnusuru wa haki. Yashangaza eti wamenitumia khabari ya kuwa nitoke kujiandaa na mapambano ya kuchomana mikuki na niwe tayari kwa vita vya upanga! Akina mama waombolezaji wawalilie.

Nilikuwa na ningali sihofishwi na vita wala kutishika na kupigwa. Nina yakini kwa Mola Wangu Mlezi na sina shaka na dini yangu”.

23. MIONGONI MWA KHUTBA ZAKE(A.S)

KUHUSU MGAO WA RIZIKI:

ومن خطبة له (عليه السلام)

[ وتشتمل على تهذيب الفقراء بالزهد وتأديب الاغنياء بالشفقة ]

أمَّا بَعْدُ، فَإِنَّ الاْمْرَ يَنْزِلُ مِنَ السَّماءِ إِلَى الاْرْضِ كَقَطر المَطَرِ إِلَى كُلِّ نَفْس بِمَا قُسِمَ لَهَا مِنْ زِيَادَة أَوْ نُقْصَان، فإذا رَأَى أَحَدُكُمْ لاِخِيهِ غَفِيرَةً في أَهْل أَوْ مَال أَوْ نَفْس فَلاَ تَكُونَنَّ لَهُ فِتْنَةً، فَإِنَّ المَرْءَ المُسْلِمَ مَا لَمْ يَغْشَ دَنَاءَةً تَظْهَرُ فَيَخْشَعُ لَهَا إِذَا ذُكِرَتْ، وَيُغْرَى بهَا لِئَامُ النَّاسِ، كانَ كَالفَالِجِ اليَاسِرِ الَّذِي يَنْتَظِرُ أَوَّلَ فَوْزَة مِنْ قِدَاحِهِ تُوجِبُ لَهُ المَغْنَمَ، وَيُرْفَعُ عَنْه بها المَغْرَمُ. وَكَذْلِكَ المَرْءُ المُسْلِمُ البَرِيءُ مِنَ الخِيَانَةِ يَنْتَظِرُ مِنَ اللهِ إِحْدَى الحُسْنَيَيْنِ: إِمَّا دَاعِيَ اللهِ فَمَا عِنْدَ اللهِ خَيْرٌ لَهُ، وَإِمَّا رِزْقَ اللهِ فَإِذَا هُوَ ذُوأَهْل وَمَال، وَمَعَهُ دِينُهُ وَحَسَبُهُ.ُ

“Hivyo, kwa kweli amri yateremka kutoka mbinguni mpaka ardhini kama matone ya mvua na kuifikia kila nafsi kiwango ilichogawiwa, ikiwa ni zaidi au pungufu, kwa hiyo endapo mmoja wenu anapoona kwa nduguye wingi wa ahli au mali au binafsi hilo lisimkere, kwa kuwa Muislamu hatendi kitendo ambacho lau kitafichuka atainamisha macho yake (kuona haya) na ambacho watu wasio na mashiko watashawishika, yeye ni mfano wa mcheza kamari anayetumainia mchezo wake wa kwanza utamhakikishia kipato na yakuwa utamfidia michezo ya nyuma aliyopata hasara.

Ni sawa na Mwislamu asiye na hiyana, anatazamia kwa Mungu mojawapo ya mazuri mawili: Ima wito kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na yaliyo kwa Mungu ni bora kwake. Au riziki ya Mungu, tayari ana watoto na mali, pia atakuwa na dini yake na hishma yake.

إِنَّ المَالَ وَالبَنِينَ حَرْثُ الدُّنْيَا، والعَمَلَ الصَّالِحَ حَرْثُ الاْخِرَةِ، وَقَدْ يَجْمَعُهُمَا اللهُ لاِقْوَام، فَاحْذَرُوا مِنَ اللهِ مَا حَذَّرَكُمْ مِنْ نَفْسِهِ، وَاخْشَوْهُ خَشْيَةً لَيْسَتُ بَتَعْذِير، وَاعْمَلُوا في غَيْرِ رِيَاء وَلاَ سُمْعَة; فَإِنَّهُ مَنْ يَعْمَلْ لِغَيْرِ اللهِ يَكِلْهُ اللهُ إِلَى مَنْ عَمِلَ لَهُ نَسْأَلُ اللهَ مَنَازِلَ الشُّهَدَاءِ، وَمُعَايَشَةَ السُّعَدَاءِ، وَمُرَافَقَةَ الاْنْبِيَاءِ

Na kweli mali na watoto ni matunda ya dunia tu, na matendo mema ni matunda ya akhera. Na Mungu (s.w.t) huenda akayakusanya mawili hayo kwa baadhi ya kaumu ya watu. Jihadharini na yale Mungu Aliyo wahadharisheni, na mwogopeni kwa kiasi kwamba haitohitajika kuomba msamaha. Na fanyeni (wema) bila ya kutaka kujionesha au kusikika, kwa kuwa atendaye kwa ajili ya mwingine ambaye si Mungu, Mungu atamuwakilisha kwa yule aliyetenda kwa ajili yake.Tunamuomba Mungu (s.w.t) mafikio ya mashahidi na tuishi maisha ya walio na maisha ya furaha, na kuwa pamoja na manabii.

أَيُّهَا النّاسُ، إِنَّهُ لاَ يَسْتَغْنِي الرَّجُلُ ـ وَإِنْ كَانَ ذَا مَال ـ عَنْ عَشِيرَتِهِ، وَدِفَاعِهِمْ عَنْهُ بِأَيْدِيهِمْ وَأَلسِنَتِهمْ، وَهُمْ أَعْظَمُ النَّاسِ حَيْطَةً مِنْ وَرَائِهِ وَأَلَمُّهُمْ لِشَعَثِهِ، وَأَعْطَفُهُمْ عَلَيْهِ عِنْدَ نَازِلَة إنْ نَزَلَتْ بِهِ. وَلِسَانُ الصِّدْقِ يَجْعَلُهُ اللهُ لِلْمَرْءِ في النَّاسِ خَيْرٌ لَهُ مِنَ المَالِ: يُورِثُهُ غيرَهُ

Enyi watu! mtu hawezi kujitosha - japo awe na mali - bila ya jamaa wa ukoo wake, na ulinzi wao juu yake kwa mikono yao na ndimi zao. Nao ni watu muhimu sana kwa uangalizi nyuma yake, nao ni kiunganishi mno cha mfarakano na ndugu zake, ni wenye huruma mno kwake anapokumbwa na shida. Utajo mwema Mungu amjaaliao mtu miongoni mwa watu ni bora kwake kuliko mali ambayo atawarithisha watu wengine.

منها : أَلاَ لاَيَعْدِلَنَّ أَحَدُكُمْ عَنِ القَرَابِةِ يَرَى بِهَا الخَصَاصَةَ أنْ يَسُدَّهَا بِالَّذِي لايَزِيدُهُ إِنْ أَمْسَكَهُ وَلاَ يَنْقُصُهُ إِنْ أَهْلَكَهُ، وَمَنْ يَقْبِضْ يَدَهُ عَنْ عَشِيرَتِهِ، فَإِنَّمَا تُقْبَضُ مِنْهُ عَنْهُمْ يَدٌ وَاحِدَةٌ، وَتُقْبَضُ مِنْهُمْ عَنْهُ أَيْد كَثِيرَةٌ; وَمَنْ تَلِنْ حَاشِيَتُهُ يَسْتَدِمْ مِنْ قَوْمِهِ المَوَدَّةَ

Na miongoni mwa sehemu ya khutba hii : “Ala! Mtu asiache kusaidia haja aionayo kwa ndugu wa karibu, awaonapo katika shida azitatue, kwa kile ambacho hakitomzidishia au kumsaidia chochote akiacha, na wala hakitompunguzia chochote endapo atakitumia. Na ambaye anauzuia mkono wake kuwasaidia ndugu zake wa karibu, ukweli ni kwamba unazuilika kutoka kwake kuwaendea wao mkono mmoja tu, na itazuilika kwake kutoka kwao mikono mingi. Mwenye tabia nzuri, mapenzi yake kwa ndugu yatadumu.

Maelezo : Amesema Sharif ar-Raadhiy; “Nasema Alghafiratu hapa ina maana ya kuzidi na uwingi, kutokana na usemi wao (Waarabu) kuhusu kundi la watu” Aljammau Alghafiru, yaani kundi kubwa la watu, na Aljam’u-Alghafiiru, ikiwa na maana hiyo hiyo. Na yaelezwa (If ’watun min Ahlin au mali) na Al’If ’watu; ni kitu bora, husema; Akaltu af ’wata ta’ami - nimekula chakula kilicho bora. Maana nzuri iliyoje aliyoikusudia (amani imfikie) kwa usemi wake mwenye kuuzuia mkono wake kwa kutowasaidia jamaa zake… mpaka mwisho wa usemi wake huo, kwa kweli mzuiaji kwa nduguye anazuia manufaa ya kheri ya mkono mmoja. Naye atakapohitaji nusura yao, na atakapodharurika na usaidizi wao, wao wata- jizuia kumnusuru, na watakuwa wazito kumpa sauti, kwa hiyo itakuwa umezuilika msaada wa mikono mingi, na kusimama nyayo nyingi.

24. NA MIONGONI MWA KHUTBA ZAKE(A.S)

Katika kuhimiza kuwapiga vita Khawarij:

ومن خطبة له (عليه السلام)

وَلَعَمْرِي مَا عَلَيَّ مِنْ قِتَالِ مَنْ خَالَفَ الحَقَّ، وَخَابَطَ الغَيَّ، مِنْ إِدْهَان وَلاَ إِيهَان. فَاتَّقُوا اللهَ عِبَادَ اللهِ، وَفِرُّوا إِلَى اللهِ مِنَ اللهِ، وَامْضُوا في الَّذِي نَهَجَهُ)لَكُمْ، وَقُومُوا بِمَا عَصَبَهُ بِكُمْ، فَعَلِيٌّ ضَامِنٌ لِفَلْجِكُمْ آجِلاً، إِنْ لَمْ تُمنَحُوهُ عَاجِلاً

“Naapa kwa umri wangu siko legelege wala dhaifu katika kupigana na mwenye kuhalifu ukweli na kuyumbayumba ndani ya upotovu. Hivyo basi waja wa Mungu mcheni Mungu kimbilieni kwa Mungu kutoka kwa Mungu[76] .

Nendeni katika njia ya wazi aliyokufanyieni. Tekelezeni yale aliyowaambatanisha nayo. Kwa kuwa Ali ni mwenye kuchukua dhamana ya kufuzu kwenu hapo baadaye endapo hamtatunukiwa hivi punde.

25. NA MIONGONI MWA KHUTBA ZAKE(A.S)

ومن خطبة له (عليه السلام)

وقد تواترت عليه الاَخبار باستيلاءِ أصحاب معاوية على البلاد، وقدم عليه عاملاه على اليمن ـ وهما عبيدالله بن العباس وسعيد بن نمران ـ لمّا غلب عليها بُسْرُ بن أبي أَرْطَاة، فقام(عليه السلام) إلى المنبر ضجراً بتثاقل أَصحابه عن الجهاد، ومخالفتهم له في الرأْي، وقال:

Habari zimeenea na kumfikia kuwa watu wa Muawiyah wameteka nchi (Yemen) na wafanyakazi wake wawili wa Yemen walimjia, nao ni Ubaidullahi bin Abbas na Saeed bin Namran alipowashinda nguvu Busru bin Abii Artaat. Hapo (amani imfikie), alisimama juu ya mimbari akiwa ameudhika na watu wake kuwa wazito kwenye jihadi na kuwa kwao kinyume na yeye katika rai, akasema:

مَا هِيَ إِلاَّ الكُوفَةُ، أقْبِضُهَا وَأَبْسُطُهَا(2)، إنْ لَمْ تَكُوني إِلاَّ أَنْتِ، تَهُبُّ أَعَاصِيرُك، فَقَبَّحَكِ اللهُ ! وتمثّل بقول الشاعر: لَعَمْرُ أَبِيكَ الخَيْرِ يَا عَمْرُوإِنَّني عَلَى وَضَر(4) ـ مِنْ ذَا الاْنَاءِ قَلِيلِ.

“Hakuna kilichobakia isipokuwa (mji wa) Kufah, naweza kuukunja na kuukunjua[77] ,1 kama haukuwa ila ni wewe [78] 2 kimbunga chako kinavuma Mungu akuweke katika hali mbaya!”

Kisha alitolea mfano ubeti wa shairi:

Oh! ewe Amr uzuri wa maisha mema ya babako,Nimeambulia makombo kidogo mchuzi wa kile chombo.

ثم قال (عليه السلام) : أُنْبِئْتُ بُسْراً قَدِ اطَّلَعَ الَيمنَ، وَإِنِّي وَاللهِ لاَظُنُّ هؤُلاءِ القَوْمَ سَيُدَالُونَ مِنْكُمْ بِاجْتِماعِهمْ عَلَى بَاطِلِهمْ، وَتَفَرُّقِكُمْ عَنْ حَقِّكُمْ، وَبِمَعْصِيَتِكُمْ، إِمَامَكُمْ في الحَقِّ، وَطَاعَتِهِمْ إِمَامَهُمْ في البَاطِلِ، وَبِأَدَائِهِمُ الاْمَانَةَ إِلَى صَاحِبِهِمْ وَخِيَانَتِكُمْ، وَبِصَلاَحِهمْ في بِلاَدِهِمْ وَفَسَادِكُمْ، فَلَو ائْتَمَنْتُ أَحَدَكُمْ عَلَى قَعْب لَخَشِيتُ أَنْ يَذْهَبَ بِعِلاَقَتِهِ.

Hatimaye Imamu Ali (s.a) alisema (a.s):

Nimepata habari kuwa Busra amehujumu na kuitwaa Yemen, nami namuapa Mungu nina yakini watu hawa watawashindeni na watakuwa na dola juu yenu kwa sababu ya kushikamana katika batili yao, na kwa sababu ya kufarikiana kwenu katika haki yenu, na kwa kumuasi kwenu Imam wenu akiwa katika haki, na kwa kumtii kiongozi wao akiwa katika batili, na kwa kutekeleza amana kwa kiongozi wao na kwa hiyana yenu, na kuwa kwao wema katika nchi yao, na kwa kuwa kwenu waovu.

Kama mmoja wenu ningemwamini na bilauri ya kunywea maji, ningeogopa huenda akaondoka na mkono wake.

اللَّهُمَّ إِنِّي قَدْ مَلِلْتُهُمْ وَمَلُّوني، وَسَئِمْتُهُمْ وَسَئِمُوني، فَأَبْدِلنِي بِهِمْ خَيْراً مِنْهُمْ، وأَبْدِلُهمْ بِي شَرَّاً مِنِّى، اللَّهُمَّ مِثْ قُلُوبَهُمْ(3) كَمَا يُمَاثُ الْمِلْحُ فِي الْمَاءِ، أَمَاوَاللهِ لَوَدِدْتُ أَنَّ لِي بِكُمْ أَلفَ فَارِس مِنْ بَنِي فِرَاسِ بْنِ غَنْم هُنَالِكَ، لَوْ دَعَوْتَ، أَتَاكَ مِنْهُمْ * فَوَارِسُ مِثْلُ أَرْمِيَةِ الحَمِيم.

Oh! ewe Allah, kwa kweli wamenichafua moyo na nimewachafu mioyo, nimewachoka nao wamenichoka.

Basi nibadilishie walio bora kuliko wao nami nibadilishe kwao na mwingine ambaye ni mshari zaidi kuliko mimi!

Oh! ewe Allah, ziyayushe nyoyo zao kama iyayukavyo chumvi ndani ya maji. Wallahi natamani lau ningekuwa na askari wapanda farasi elfu moja kutoka kwa Bani Firasi ibni Ghanmin kama asemavyo mshairi: Lau utawaita watakujia miongoni mwao Wapanda farasi kama wingu la kiangazi”.

ثم نزل(عليه السلام) من المنبر.

قلتُ أنا: والارمية جمع رَميٍّ وهو: السحاب، والحميم في هذا الموضع: وقت الصيف، وإنما خصّ الشاعر سحاب الصيف بالذكر لانه أشد جفولاً، وَأسرع خُفوفاً(4)، لانه لا ماء فيه، وإنما يكون السحاب ثقيل السير لامتلائه بالماء، وذلك لا يكون في الاكثر إلا زمان الشتاء، وإنما أراد الشاعر وصفهم بالسرعة إذا دُعوا، والاغاثة إذا استغيثوا، والدليل على ذلك قوله: «هنالك، لو دعوت، أتاك منهم

Kisha Imamu(a.s) aliteremka kutoka mimbari.

Sharifu Ar-Radhwiyu amesema: “Nasema Al’armiyatu ni wingi wa neno Ramiy, ni mawingu. Na Hamimu hapa: ni wakati wa kiangazi. Na mshairi ameyataja khususan mawingu ya wakati wa kiangazi, kwa sababu yanakwenda haraka mno kwa kuwa hayana maji, na mawingu huenda kwa uzito kwa kujawa na maji. Hali hiyo haiwi aghalabu ila wakati wa masika. Na mshairi alikusudia kuwasifu kuja kwao haraka waitwapo na kutoa msaada waombwapo msaada. Na dalili ni usemi wake: hunalika lau daauta ataaka min hum - hapo endapo utawaita watakujia miongoni mwao.

26. MIONGONI MWA KHUTBA ZAKE(A.S)

Katika kuwalaumu waliomfanyia bai’a kwa sharti:

ومن خطبة له (عليه السلام)

وفيها يصف العرب قبل البعثة ثم يصف حاله قبل البيعة له

العرب قبل البعثه

إِنَّ اللهَ سُبحانَه بَعَثَ مُحَمَّداً نَذِيراً لِلْعَالَمِينَ، وَأَمِيناً عَلَى التَّنْزِيلِ، وَأَنْتُمْ مَعْشَرَ العَرَبِ عَلَى شَرِّ دِين، وَفِي شَرِّ دَار، مُنِيخُونَ بَيْنَ حِجارَة خُشْن، وَحَيَّات صُمٍّ، تشْرَبُونَ الكَدِرَ، وَتَأْكُلُونَ الجَشِبَ، وَتَسْفِكُونَ دِمَاءَكُمْ، وَتَقْطَعُونَ أَرْحَامَكُمْ، الاَصْنَامُ فِيكُمْ مَنْصُوبَةٌ، وَالاْثَامُ بِكُمْ مَعْصُوبَةٌ.

Kwa kweli Mungu (s.w.t) alimtuma Muhammad(s.a.w.w) akiwa muonyaji kwa walimwengu na mwaminifu wa uteremsho (Qur’ani) na ninyi Waarabu mkiwa wafuasi wa dini ovu mno, na mkiwa mukiishi katika nchi yenye maisha magumu mno, kwenye mawe ya kwaruzayo na nyoka wenye sumu, mlikuwa mkinywa maji machafu sana na mnakula chakula cha ovyoovyo, mlikuwa mkimwaga damu zenu, mnakata mawasiliano na jamaa zenu. Sanamu zimesimamishwa mbele yenu, na dhambi zimekuambateni.

منها : فَنَظَرْتُ فَإِذَا لَيْسَ لِي مُعِينٌ إِلاَّ أَهْلُ بَيْتِي، فَضَنِنْتُ بِهمْ عَنِ المَوْتِ، وَأَغْضَيْتُ عَلَى القَذَى، وَشَرِبْتُ عَلَى الشَّجَا، وَصَبَرْتُ عَلَى أَخْذِ الكَظَمِ،وَعَلىْ أَمَرَّ مِنْ طَعْمِ العَلْقَمِ.

Na sehemu nyingine ya khutba hii : Niliangalia na kuona sina msaidizi isipokuwa watu wa nyumba yangu, hivyo nilijiepusha kuwatumbukiza kwenye mauti, nilifumba macho yakiwa na chembe ya vumbi[79] , na nilikunywa hali ya kwamba kooni kuna kilichokwama[80] , na nilivuta subira katika kuvuta pumzi, na kwa uchungu mno kuliko ladha ya shubiri.”

ومنها : وَلَمْ يُبَايعْ حَتَّى شَرَطَ أَنْ يُؤْتِيَهِ عَلَى البَيْعَةِ ثَمَناً، فَلاَ ظَفِرَتْ يَدُ المبايِعِ، وخَزِيَتْ أَمَانَةُ المُبْتَاعِ، فَخُذُوا لِلْحَرْبِ أُهْبَتَهَا، وَأعِدُّوا لَهَا عُدَّتَهَا، فَقَدْ شَبَّ لَظَاهَا، وَعَلاَ سَنَاهَا، وَاسْتَشْعِرُوا الصَّبْرَ، فَإِنَّهُ أحْزَمُ لِلنَّصْرِ

Na sehemu ya khutba hii : Hakufanya baia[81] hivyo basi haukufanikiwa mkono wa muuzaji na kutwezwa uaminifu wa mnunuzi[82] , hivyo basi kuweni tayari kwa vita na mtayarishe zana zake, mwale wake umepanda na mwanga wake umepaa na mjiambatanishe na subira, kwa kuwa subira yaita kuelekea ushindi.

27. MIONGONI MWA KHUTBA ZAKE(A.S)

ومن خطبة له (عليه السلام)

وفيها يذكر فضل الجهاد، ويستنهض الناس، ويذكر علمه بالحرب، ويلقي عليهم التبعة لعدم طاعته

Katika kuhimiza jihadi na kuwalaumu wanao kaa nyuma:

أَمَّا بَعْدُ، فَإِنَّ الجِهَادَ بَابٌ مِنْ أَبْوَابِ الجَنَّةِ، فَتَحَهُ اللهُ لِخَاصَّةِ أَوْلِيَائِهِ، وَهُوَ لِباسُ التَّقْوَى، وَدِرْعُ اللهِ الحَصِينَةُ، وَجُنَّتُهُ الوَثِيقَةُ، فَمَنْ تَرَكَهُ رَغْبَةً عَنْهُ أَلبَسَهُ اللهُ ثَوْبَ الذُّلِّ، وَشَمِلَهُ البَلاَءُ، وَدُيِّثَ بِالصَّغَارِ وَالقَمَاءَةِ، وَضُرِبَ عَلَى قَلْبِهِ بِالاْسْهَابِ، وَأُدِيلَ الحَقُّ مِنْهُ بِتَضْيِيعِ الجِهَادِ، وَسِيمَ الخَسْفَ، وَمُنِعَ النَّصَفَ.

Kwa hiyo kwa kweli jihadi ni mlango katika jumla ya milango ya Jannah (peponi), Mwenyezi Mungu ameufunguwa kwa ajili ya wapenzi Wake makhsusi. Nayo ndio vazi la taqwa (uchamungu), na ni ngao ya Mungu yenye kuhifadhi, na stara yake thabiti. Hivyo basi, mwenye kuiacha kwa kutoipenda, Mungu atamvisha nguo ya udhalili na balaa litamuenea na atadhalilishwa kwa kutwezwa, na kudharaulika, na moyoni mwake kuondolewa akili na fahamu. Ukweli umeondolewa kutoka kwake kwa sababu ya kuipoteza jihadi. Atakumbwa na aibu na kunyimwa insafu[83] .

أَلاَ وَإِنِّي قَدْ دَعَوْتُكُمْ إِلَى قِتَالِ هؤُلاَءِ القَوْمِ لَيْلاً وَنَهَاراً، وَسِرّاً وَإِعْلاَناً، وَقُلْتُ لَكُمُ: اغْزُوهُمْ قَبْلَ أَنْ يَغْزُوكُمْ، فَوَاللهِ مَا غُزِيَ قَوْمٌ قَطُّ في عُقْرِ دَارِهِمْ إِلاَّ ذَلُّوا، فَتَوَاكَلْتُمْ وَتَخَاذَلتُمْ حَتَّى شُنَّتْ عَلَيْكُمُ الغَارَاتُ، وَمُلِكَتْ عَلَيْكُمُ الاْوْطَانُ وَهذَا أَخُو غَامِد قَدْ وَرَدَتْ خَيْلُهُ الاْنْبَارَ، وَقَدْ قَتَلَ حَسَّانَ بْنَ حَسَّانَ البَكْرِيَّ، وَأَزَالَ خَيْلَكُمْ عَنْ مَسَالِحِهَا.

Angalieni mimi nimekuwa nikikuiteni kupambana na watu hawa usiku na mchana, kwa siri na kwa tangazo la wazi, na nilikuambieni (washambulieni kabla hawajakushambulieni, wallahi watu hawajapata kushambuliwa katu katika kitovu cha nyumba yao ila watadhalilishwa) mkategeana na mkadhoofu, mpaka mliposhambuliwa na miji yenu ikatekwa; basi huyu nduguye Ghamid farasi wake wameingia Anbaar[84] , na amemuua Hasan bin Hasan Al’Bakriy, na wamewaondoa farasi wenu kwenye ngome yao.

وَلَقَدْ بَلَغَنِي أَنَّ الرَّجُلَ مِنْهُمْ كَانَ يَدْخُلُ عَلَى المَرْأَةِ المُسْلِمَةِ، وَالاْخْرَى المُعَاهَدَةِ، فيَنْتَزِعُ حِجْلَهَا وَقُلْبَهَا وَقَلاَئِدَهَا، وَرِعَاثَهَا، ما تَمْتَنِعُ مِنْهُ إِلاَّ بِالاسْتِرْجَاعِ وَالاِسْتِرْحَامِ، ثُمَّ انْصَرَفُوا وَافِرِينَ، مَا نَالَ رَجُلاً مِنْهُمْ كَلْمٌ، وَلاَ أُرِيقَ لَهُمْ دَمٌ،

Na habari zimenifikia kuwa mtu miongoni mwao huingia kwa mwanamke Mwislamu na mwanamke dhimiy na anampora pambo la mguuni, bangili, kidani chake, na shanga na huwezi kumziwia ila kwa kusema; (Innaa lil lahi wain naa ilayhi raajiuna 2:156) na istir’haam – kupiga kelele ili kuomba rehema kisha wakaondoka bila ya kupunguwa mtu kati yao. Hakupata mtu kati yao jeraha, wala kumwagika damu yao.

فَلَوْ أَنَّ امْرَأً مُسْلِماً مَاتَ مِن بَعْدِ هَذا أَسَفاً مَا كَانَ بِهِ مَلُوماً، بَلْ كَانَ بِهِ عِنْدِي جَدِيراً فَيَا عَجَباً! عَجَباًـ وَاللهِ ـ يُمِيتُ القَلْبَ وَيَجْلِبُ الهَمَّ مِن اجْتِماعِ هؤُلاَءِ القَوْمِ عَلَى بَاطِلِهمْ، وَتَفَرُّقِكُمْ عَنْ حَقِّكُمْ! فَقُبْحاً لَكُمْ وَتَرَحاً، حِينَ صِرْتُمْ غَرَضاً يُرمَى: يُغَارُ عَلَيْكُمْ وَلاَ تُغِيرُونَ، وَتُغْزَوْنَ وَلاَ تَغْرُونَ، وَيُعْصَى اللهُ وَتَرْضَوْن! فَإِذَا أَمَرْتُكُمْ بِالسَّيْرِ إِلَيْهِم فِي أَيَّامِ الحَرِّ قُلْتُمْ: هذِهِ حَمَارَّةُ القَيْظِ أَمْهِلْنَا يُسَبَّخُ عَنَّا الحَرُّ، وَإِذَا أَمَرْتُكُمْ بِالسَّيْرِ إِلَيْهِمْ فِي الشِّتَاءِ قُلْتُمْ: هذِهِ صَبَارَّةُ القُرِّ، أَمْهِلْنَا يَنْسَلِخْ عَنَّا البَرْدُ، كُلُّ هذا فِرَاراً مِنَ الحَرِّ وَالقُرِّ; فَإِذَا كُنْتُمْ مِنَ الحَرِّ وَالقُرِّ تَفِرُّونَ فَأَنْتُمْ وَاللهِ مِنَ السَّيْفِ أَفَرُّ!

Lau mtu Mwislamu akifa baada ya hali hii, majonzini hangepaswa kulaumiwa, bali kwa mtazamo wangu angekuwa amestahiki! Oh! Ajabu ilioje inavunja moyo na inahuzunisha, kuona hawa watu walivyokuwa na mshikamano katika matendo yao batili, na kusambaratika kwenu mbali na haki yenu! Ubaya na huzuni ilikufikeni, mlipokuwa lengo la kutupiwa mishale. Mnashambuliwa wala hamshambulii, mnahujumiwa wala hamhujumu. Mungu anafanyiwa maasi mmebaki mmeridhika.

Nikiwaamuruni kuwaendea siku za joto mnasema hili ni joto kali, tungojee joto lipungue, na nikikuamuruni kuwaendea wakati wa baridi mnasema hii ni baridi kali, tungojee baridi iondoke. Hivyo yote ni kukimbia joto na baridi; na mkiwa mwalikimbia joto na baridi, basi ninyi wallahi upanga mtakuwa ni wenye kuukimbia zaidi!”

يَا أَشْبَاهَ الرِّجَالِ وَلاَ رِجَالَ! حُلُومُ الاْطْفَالِ، وَعُقُولُ رَبّاتِ الحِجَالِ، لَوَدِدْتُ أَنِّي لَمْ أَرَكُمْ وَلَمْ أَعْرِفْكمْ مَعْرِفَةً ـ وَاللهِ ـ جَرَّتْ نَدَماً، وَأَعقَبَتْ سَدَماً قَاتَلَكُمُ اللهُ! لَقَدْ مَلاَتُمْ قَلْبِي قَيْحاً، وَشَحَنْتُمْ صَدْرِي غَيْظاً، وَجَرَّعْتُمُونِي نُغَبَ التَّهْمَامِ أَنْفَاساً، وَأَفْسَدْتُمْ عَلَيَّ رَأْيِي بِالعِصْيَانِ وَالخذْلاَن، حَتَّى قَالَتْ قُريْشٌ: إِنَّ ابْنَ أَبِي طَالِب رَجُلٌ شُجَاعٌ، وَلْكِنْ لاَ عِلْمَ لَهُ بِالحَرْبِ.

Enyi mlio mfano wa wanaume wala si wanaume, fikra za kitoto, na mna akili mfano wa akili za wanawake watunza “nyumba ya mapambo.” Natamani nisingewaona wala nisingewatambua kabisa - wallahi kuwajua huku kumeleta aibu na kumalizikia huzuni na hasara. Mungu awalaani, mmeujaza moyo wangu usaha na kuusheheni hasira, na mmeninywesha konga la huzuni konga baada ya konga, mmeichafua rai yangu kwa kuasi na kunitelekeza, kiasi cha kufikia makuraishi kusema; ‘hakika mwana wa Abi Talib ni mtu shujaa lakini hana maarifa ya vita.

للهِ أَبُوهُمْ! وَهَلْ أَحدٌ مِنْهُمْ أَشَدُّ لَهَا مِرَاساً، وَأَقْدَمُ فِيهَا مَقَاماً مِنِّي؟! لَقَدْ نَهَضْتُ فِيهَا وَمَا بَلَغْتُ العِشْرِينَ، وها أناذا قَدْ ذَرَّفْتُ عَلَى السِّتِّينَ! وَلكِنْ لا رَأْيَ لَمِنْ لاَ يُطَاعُ !

Mungu awahurumie, hivi kuna yeyote miongoni mwao mkali na mwenye uzoefu zaidi na wa tangu zaidi kuliko mimi. Nimeinukia nayo nikiwa sijafikia umri wa miaka ishirini, na bado, mimi huyo niko humo nikiwa nimevuka miaka sitini, lakini hana rai muwafaka asiyetiiwa.

28. NA MIONGONI MWA KHUTBA ZAKE(A.S)

ومن خطبة له (عليه السلام)

أَمَّا بَعْدُ، فَإِنَّ الدُّنْيَا قَدْ أَدْبَرَتْ، وَآذَ نَتْ بِوَدَاع، وَإِنَّ الاْخِرَةَ قَدْ أَقْبَلَتْ، وَأَشْرَفَتْ بِاطِّلاَع، أَلاَ وَإِنَّ اليَوْمَ المِضْمارَ، وَغَداً السِّبَاقَ، وَالسَّبَقَةُ الجَنَّةُ، وَالغَايَةُ النَّارُ; أَفَلاَ تَائِبٌ مِنْ خَطِيئَتِهِ قَبْلَ مَنِيَّتِهِ! أَلاَ عَامِلٌ لِنَفْسِهِ قَبْلَ يَوْمِ بُؤْسِهِ! أَلاَ وَإِنَّكُمْ في أَيَّامِ أَمَل مِنْ وَرَائِهِ أَجَلٌ، فَمَنْ عَمِلَ في أَيَّامِ أَمَلهِ قَبْلَ حُضُورِ أَجَلِهِ فَقَدْ نَفَعَهُ عَمَلُهُ، وَلَمْ يَضرُرْهُ أَجَلُهُ; وَمَنْ قَصَّرَ في أَيَّامِ أَمَلِهِ قَبْلَ حُضُورِ أَجَلِهِ، فَقَدْ خَسِرَ عَمَلَهُ، وَضَرَّهُ أَجَلُهُ،

Hivyo sasa kwa kweli dunia imetupa mgongo na kutangaza msafara kuaga kwake. Na kwa kweli akhera imewadia na kupiga mbiu ya kuja kwake ghafla. Lo! Kwa kweli leo ni siku hasa ya maandalizi, na kesho ndio mashindano ya mbio, na nishani ni (Jannah) Pepo, na mwisho wake ni moto; je hakuna mwenye kutubu kwa makosa yake kabla ya mauti yake? Je hakuna wakutenda mema kwa ajili yake kabla ya siku atakayokuwa na haja kubwa.

Angalia! ninyi mpo katika siku za matumaini, ambazo nyuma yake kuna mauti. Hivyo mwenye kutenda mema katika siku zake za matumaini kabla ya kufikiwa na ajali yake, atakuwa amenufaishwa na matendo yake, na kifo chake hakitomdhuru, na mwenye kufanya uzembe katika siku zake za matumaini kabla ya kufikiwa na ajali yake, atakuwa amepata hasara kazi yake, na ajali yake itamdhuru.

أَلاَ فَاعْمَلُوا فِي الرَّغْبَةِ كَمَا تَعْمَلُونَ فِي الرَّهْبَةِ، أَلاَوَإِنِّي لَمْ أَرَ كَالجَنَّةِ نَامَ طَالِبُهَا، وَلاَ كَالنَّارِ نَامَ هَارِبُهَا، أَلاَ وَإنَّهُ مَنْ لاَيَنْفَعُهُ الحقُّ يَضْرُرهُ البَاطِلُ، وَمَنْ لا يستقم بِهِ الهُدَى يَجُرُّ بِهِ الضَّلاَلُ إِلَى الرَّدَىْ، أَلاَ وَإِنَّكُمْ قَد أُمِرْتُمْ بِالظَّعْنِ، وَدُلِلْتُمْ عَلى الزَّادَ وَإِنَّ أَخْوَفَ مَا أَخافُ عَلَيْكُمُ: اتِّبَاعُ الهَوَى، وَطُولُ الاْمَلِ، تَزَوَّدُوا فِي الدُّنْيَا مِنَ الدُّنْيَا مَا تَحُوزُونَ بِهِ أَنْفُسَكُمْ غَداً.

Angalia! fanyeni wema wakati wa upendo wenu kama mfanyavyo wakati wa hofu. Angalia! kwa hakika mimi sijaona kilichotelekezwa kama jannah (Pepo) kwani amelala mwenye kuitafuta, wala kuona kitu kilichopuuzwa kama moto amelala aukimbiaye[85] .Angalia, asiyenufaika na ukweli bila shaka batili itamdhuru[86] , na ambaye hawi mnyofu kwa mwongozo, upotovu utamkokota na kumzamisha kwenye maangamizi. Alaa! kwa kweli ninyi mmeamriwa kufanya msafara[87] , na mmeoneshwa masurufu; na kwa kweli ninalohofia mno kwenu ni kufuata utashi mbaya wa nafsi na kurefusha matumanini, basi chukueni masurufu kutoka hapa duniani ambayo kwayo mutakayojihifadhi nayo kesho nafsi zenu.

29. NA MIONGONI MWA KHUTBA ZAKE(A.S)

ومن خطبة له (عليه السلام)

أَيُّهَا النَّاسُ، الْمجْتَمِعَةُ أبْدَانُهُمْ، الُمخْتَلِفَةُ أهْوَاؤُهُمْ، كَلامُكُم يُوهِي الصُّمَّ الصِّلابَ، وَفِعْلُكُمْ يُطْمِعُ فِيكُمُ الاْعْدَاءَ! تَقُولُونَ فِي الَمجَالِسِ: كَيْتَ وَكَيْتَ، فَإذَا جَاءَ الْقِتَالُ قُلْتُمْ: حِيدِي حَيَادِ! مَا عَزَّتْ دَعْوَةُ مَنْ دَعَاكُمْ، وَلاَ اسْتَرَاحَ قَلْبُ مَنْ قَاسَاكُمْ، أَعَالِيلُ بِأَضَالِيلَ، دِفَاعَ ذِي الدَّيْنِ المَطُولِ، لاَ يَمنَعُ الضَّيْمَ الذَّلِيلُ! وَلاَ يُدْرَكُ الْحَقُّ إِلاَ بِالْجِدِّ! أَيَّ دَار بَعْدَ دَارِكُمْ تَمْنَعُونَ، وَمَعَ أَىِّ إِمَام بَعْدِي تُقَاتِلُونَ؟

Enyi watu (mlio kama wale ambao) miili yao iko pamoja, wenye kutofautiana matakwa yao, maneno yenu yalainisha mawe magumu kabisa, na vitendo vyenu vyawatumainisha kwenu maadui! Kwenye vikao mwasema hili na lile, vita vikija mwasema tokomea mbali. Wito wa mwenye kuwaiteni haupewi sikio wala moyo wa mwenye kuwachukulieni kwa nguvu hauwi na utulivu. Nyudhuru zisizo na maana. Mliniomba kurefusha muda, ni ulipaji wa mwenye deni msogeza muda, dhaifu hawezi kuizuia dhulma, na haki haipatikani ila kwa juhudi. Ni nyumba gani mtailinda baada ya nyumba yenu hii! Na kiongozi (imam) gani baada yangu mtaweza kupigana pamoja naye?

المَغْرُورُ وَاللهِ مَنْ غَرَرْتُمُوهُ، وَمْنْ فَازَبِكُمْ فَازَ بَالسَّهْمِ الاْخْيَبِ، وَمَنْ رَمَى بِكُمْ فَقَدْ رَمَى بِأَفْوَقَ نَاصِل أَصْبَحْتُ وَاللهِ لا أُصَدِّقُ قَوْلَكُمْ، وَلاَ أَطْمَعُ فِي نَصْرِكُمْ، وَلاَ أُوعِدُ العَدُوَّ بِكُم مَا بَالُكُم؟ مَا دَوَاؤُكُمْ؟ مَا طِبُّكُمْ؟ القَوْمُ رِجَالٌ أَمْثَالُكُمْ، أَقَوْلاً بَغَيْرِ عِلْم! وَغَفْلَةً مِنْ غَيْرِ وَرَع! وَطَمَعاً في غَيْرِ حَقٍّ؟ !

Wallahi aliyedanganyika ni yule mliyemdanganya, na mwenye kufaulu nanyi atakuwa amefaulu - Wallahi - na mshale usiofanikisha[88] . Na mwenye kutupa na ninyi atakuwa ametupa kwa mshale uliovunjika maingiliyo ya kamba, Wallahi nimekuwa sisadiki kauli yenu, na wala situ- mainii nusra yenu, wala simkamii adui kwa kuwatumainia ninyi. Mmekuwaje? Dawa yenu nini? Nini tiba yenu? Hao watu ni wanamume kama ninyi. Ni kauli tupu bila ya ilmu, na mghafiliko bila ya kujiepusha, na tamaa katika ambalo si haki!.

30. NA MIONGONI MWA SEMI ZAKE(A.S)

ومن كلام له (عليه السلام): في معنى قتل عثمان

Kuhusu maana ya kumuuwa Uthman:

لَوْ أَمَرْتُ بِهِ لَكُنْتُ قَاتِلاً، أَوْ نَهَيْتُ عَنْهُ لَكُنْتُ نَاصِراً، غَيْرَ أَنَّ مَنْ نَصَرَهُ لاَ يَسْتَطِيعُ أَنْ يَقُولَ: خَذَلَهُ مَنْ أَنَا خَيْرٌ مِنْهُ، وَمَنْ خَذَلَهُ لاَ يَسْتَطِيعُ أَنْ يَقُولَ : وَأَنَا جَامِعٌ لَكُمْ أَمْرَهُ، اسْتَأْثَرَ فَأَسَاءَ الاْثَرَةَ، وَجَزِعْتُمْ فَأَسَأْتُمُ الجَزَعَ، وَللهِ حُكْمٌ وَاقِعٌ في المُسْتَأْثِرِ وَالجَازعِ.

Lau ningeamuru hilo ningekuwa muuwaji, na lau ningekataza ningekuwa mwenye kunusuru[89] , ila ni ukweli kuwa aliyemnusuru hawezi kusema kuwa: Ametelekezwa na ambaye mimi ni bora kuliko yeye, na aliyemtelekeza hawezi kusema: Amemnusuru ambaye ni bora kuliko mimi[90] . Na mimi nayajumlisha mambo yake kwenu. Amejitwalia na kuyatumia vibaya aliyoyatwaa. Na mmekosa uvumilivu, mkafanya vibaya kutovumilia kwenu[91] . Na Mungu anayo hukumu muwafaka kwa mwenye kujitwalia na mtovu wa uvumilivu.

31. NA MIONGONI MWA SEMI ZAKE(A.S)

ومن كلام له (عليه السلام)

لمّا أنفذ عبدالله بن العباس(رحمه الله) إلى الزبير قبل وقوع الحرب يوم الجمل ليستفيئه إلى طاعته

Kwa ibni Abbas, Alipomtuma kwa Zubairi akimtaka arejee kwenye utii wake kabla ya vita vya Jamal:

لاتَلْقَيَنَّ طَلْحَةَ، فَإِنَّكَ إِنْ تَلْقَهُ تَجِدْهُ كَالثَّوْرِ عَاقِصاً قَرْنَهُ، يَرْكَبُ الصَّعْبَ وَيَقُولُ: هُوَ الذَّلُولُ، وَلكِنِ القَ الزُّبَيْرَ، فَإِنَّهُ أَليَنُ عَرِيكَةً، فَقُلْ لَهُ: يَقُولُ لَكَ ابْنُ خَالِكَ: عَرَفْتَني بَالحِجَازِ وَأَنْكَرْتَنِي بِالعِرَاقِ، فَمَا عَدَا مِمَّا بَدَا.

Usikutane na Talha, kwa kuwa wewe endapo utakutana naye utamkuta yuko kama ng’ombe maksai amezipindisha pembe zake, anayaparamia magumu huku akisema: ‘Ni mepesi hayo,’ lakini kutana na Zubair, kwa kuwa yeye ana tabia laini, na umwambie: ‘Mtoto wa mjomba wako anasema: Ulinitambua toka Hijazi[92] , na hunitambui Iraq, ni jambo gani limebadilisha yaliokudhihirikia?!.

قال الشريف الرضي: وهو (عليه السلام) أوّل من سمعت منه هذه الكلمة، أعني: «فَمَا عَدَا مِمَّا بَدَا».

Maelezo: Amesema Sharifu Ar-Radhiy (r.a.): Yeye(a.s) ni wa kwanza ambaye limesikika neno hili kutoka kwake, nakusudia: (Famaa ada mimmaa badaa) - nini kimemtoa mbali na lililomdhirihikia.

32. NA MIONGONI MWA KHUTBA ZAKE(A.S)

ومن خطبة له (عليه السلام): معنى جور الزمان

Kuhusu dhulma ya zama:

أَيُّهَا النَّاسُ، إِنَّا قَدْ أَصْبَحْنَا في دَهْر عَنُود، وَزَمَن كَنُود، يُعَدُّ فِيهِ الُمحْسِنُ مُسِيئاً، وَيَزْدَادُ الظَّالِمُ فِيهِ عُتُوّاً، لاَ نَنْتَفِعُ بِمَا عَلِمْنَا، وَلاَ نَسْأَلُ عَمَّا جَهِلْنَا، وَلاَ نَتَخَوَّفُ قَارِعَةً حَتَّى تَحُلَّ بِنَا فَالنَّاسُ عَلَى أَرْبَعَةِ أَصْنَاف : مِنْهُمْ مَنْ لاَ يَمْنَعُهُ الفَسَادَ في الاْرْضِ إِلاَّ مَهَانَةُ نَفْسِهِ، وَكَلاَلَةُ حَدِّهِ، وَمِنْهُمُ المُصْلِتُ لِسَيْفِهِ، وَالمُعْلِنُ بِشَرِّهِ، وَالُمجْلِبُ بِخَيْلِهِ وَرَجِلِهِ، قَدْ أَشْرَطَ نَفْسَهُ، وَأَوْبَقَ دِينَهُ لِحُطَام يَنْتَهِزُهُ، أَوْ مِقْنَب يَقُودُهُ، أَوْ مِنْبَر يَفْرَعُهُ.

“Enyi watu, kwa kweli sisi tupo katika muda wa dhulma na zama za kufuru[93] , mwema humo ahesabika muovu, na dhalimu huzidi humo kiburi, hatunufaiki na tulilojua, wala hatuulizi tusilolijua wala hatuogopi msiba mpaka utufike, na watu wako aina nne: Miongoni mwao kuna ambaye hakuna kinachomzuia kufanya ufisadi katika ardhi isipokuwa unyonge wa nafsi yake na ubutu wa silaha zake na uchache wa mali yake.

Na miongoni mwao kuna mwenye kujitokeza na upanga wake na kuitangaza shari yake, na ambaye ameleta askari wake wapanda farasi na askari wake waendao kwa miguu, ameiandaa nafsi yake kwa shari na ufisadi, ameiangamiza dini yake kwa ajili ya mali yenye kuvunjika afaidikayo nayo haraka, au kundi la farasi analolichunga au mimbari aipandayo[94] .

وَلَبِئْسَ المَتْجَرُ أَنْ تَرَى الدُّنْيَا لِنَفْسِكَ ثَمَناً، وَمِمَّا لَكَ عِنْدَ اللهِ عِوَضاً ! وَمِنْهُمْ مَنْ يَطلُبُ الدُّنْيَا بِعَمَلِ الاْخِرَةِ، وَلاَ يَطْلُبُ الاْخِرَةَ بِعَمَلِ الدُّنْيَا، قَدْ وَمِنْهُمْ مَنْ أقْعَدَهُ عَنْ طَلَبِ المُلْكِ ضُؤولَةُ نَفْسِهِ، وَانقِطاعُ سَبَبِهِ، فَقَصَرَتْهُ الحالُ عَلَى حَالِهِ، فَتَحَلَّى بِاسْمِ القَنَاعَةِ، وَتَزَيَّنَ بِلِبَاسِ أَهْلِ الزَّهَادَةِ، وَلَيْسَ مِنْ ذلِكَ في مَرَاح وَلاَ مَغْدىً.

Biashara mbaya ni kuiona dunia kuwa ina thamani kwa ajili yako, na uliy- onayo yatakuwa fidia kwa Mungu! Na miongoni mwao kuna ambaye aitaka dunia kwa kazi ya akhera, wala haitafuti akhera kwa kazi ya dunia, ameishusha chini haiba yake, na kuzifanya hatua zake karibu, na kupania nguo yake, na amejipamba nafsi yake ili aaminike, na ameifanya sitara ya Mungu kuwa ni kichaka cha kufanyia maasi[95] .

Na miongoni mwao kuna ambaye unyonge wa nafsi yake umemuweka mbali na kuutaka ufalme,4 na kukatika kwa sababu zake, hali hii imemzuia kuifikia nafasi yake, kutokana na hali hiyo akajipamba kwa jina la kutosheka, na kujipamba na vazi la walioipa nyongo dunia, na katika hilo hana safari ya matembezi ya jioni wala asubuhi.

وَبَقِيَ رِجَالٌ غَضَّ أَبْصَارَهُمْ ذِكْرُ الْمَرْجِعِ، وَأَرَاقَ دُمُوعَهُمْ خَوْفُ الْـمَحْشَرِ، فَهُمْ بَيْنَ شَرِيد نَادٍّ، وَخَائِف مَقْمُوع، وَسَاكِت مَكْعُوم، وَدَاع مُخْلِص، وَثَكْلاَنَ مُوجَع، قَدْ أَخْمَلَتْهُمُ التَّقِيَّةُ، وَشَمِلَتْهُمُ الذِّلَّةُ، فَهُمْ في بَحْر أُجَاج، أَفْوَاهُهُمْ ضَامِزَةٌ، وَقُلُوبُهُمْ قَرِحَةٌ، قَدْ وَعَظُوا حَتَّى مَلُّوا، وَقُهِرُوا حَتَّى ذَلُّوا، وَقُتِلُوا حَتَّى قَلُّوا.

Na wamebakia watu ambao kumbukumbu ya marejeo imeyafumba macho yao[96] , na woga wa kukusanywa umebubujisha machozi yao, (kukusanywa baada ya kufufuliwa watu Siku ya Kiyama), kwa hiyo wao wapo kati ya mwenye kukimbia kiasi cha kujitenga, na mwenye kuogopa aliyekandamizwa, na aliye kimya aliyefumbwa mdomo, na mlinganiaji aliye na ikhlasi, na mwenye kuhuzunika na anayeumia.

Taqiiya imewazimisha[97] , wamekumbwa na udhalili, hivyo wao wako ndani ya bahari ya chumvi[98] , vinywa vyao vimenyamaza, na nyoyo zao zimejeruhiwa. Wamewaidhi mpaka wamechoka, wamekandamizwa mpaka wamekuwa dhalili, na wameuliwa mpaka wamebaki wachache.

Dunia iwe kitu kidogo machoni mwenu kuliko majani ya mti yaliyopukutika, na mabaki ya manyoya ya ngamia yaliyotindwa[99] . Waidhikeni na waliokuwa kabla yenu, kabla hawajawaidhika na ninyi wale watakao kuwa baada yenu, ikataeni dunia ikiwa ni ya kulaumiwa, kwa kuwa hiyo imewakataa walioipenda zaidi kuliko ninyi.

Maelezo : Amesema Ar-Radhiy: Hutba hii huenda asiyejua akainasibisha na Muawiya; hali ikiwa ni miongoni mwa manemo ya Amirul-Mu’uminina(a.s) yasiyo na shaka. Basi wapi na wapi dhahabu na udongo! Na wapi na wapi maji baridi na ya chumvi! Na hilo limethibitishwa na dalili yenye umahiri. Na mkosoaji mwerevu Amr bin Bahri Al’Jahidh, amekosoa hilo kwa kuwa yeye ameitaja hutba hii ndani ya kitabu Al-Bayan wat-Tabyiin na amemtaja aliyeinasibisha na Muawiyah, kisha aliongea baada yake maneno kuhusu maana yake, kwa ujumla wake ni kuwa yeye alisema: “Maneno haya yashabihiyana mno na maneno ya Ali(a.s) na madhehebu yake katika kuzigawa aina za watu, na katika kutoa habari ya walivyo miongoni mwa makandamizo na udhalili, na miongoni mwa Taqiiyah na hofu yalingana mno.” Amesema: “Basi lini tumemkuta Muawiyah katika hali miongoni mwa hali, na katika usemi wake akienda mwenendo wa watu wenye zuhdi mwenendo wa wachamungu!.

33. NA MIONGONI MWA KHUTBA ZAKE(A.S)

Alipokuwa akitoka ili kupigana na watu wa Basra:

Abdullah bin Abbas alisema: “Niliingia kwa Amirul’Mu’minina(a.s) alipokuwa Dhuqaar,[100] naye akiwa yuashona ndara zake, akaniambia: “Nini thamani ya ndara hizi?” Nikamwambia: “Hazina thamani yoyote.” Akasema(a.s) : “Wallahi hizi nazipenda mno kuliko uamiri wenu (ukhalifa) ila tu endapo nitatenda haki au kuzuia batili” Hatimae alitoka na kuwahutubia watu akisema: Kwa kweli Mwenyezi Mungu swt. alimtuma Muhammad(s.a.w .w ) hapakuwa na mmoja yeyote katika waarabu asoma Kitabu, wala kudai unabii, basi yeye akawaongoza watu mpaka aliwafanya wakae mahali mwao[101] , na kuwafikisha kwenye uokovu wao, hivyo wakawa katika istiqama ndani ya Uislamu na kuimarika nyayo zao[102] .

Wallahi nilikuwa miongoni mwa waliokuwa wakiongoza, nikiwafurusha mpaka walitokomea wote, sikudhoofu wala sikuwa mwoga.

Kwa kweli mwendo wangu ni ule ule, Wallahi nitaitoboa batili mpaka haki ijitokeze pembezoni mwake[103] . Wana nini makuraishi na mimi!

Wallahi niliwapiga vita wakiwa makafiri, na nitawapiga vita wakiwa wamedanganyika, kwa kweli mimi ni mwenzao wa hapo jana na ni mwenzao hii leo. Wallahi hawatuadhibu makuraishi ila ni kwa sababu Mungu ametuchagua juu yao, na tumewaingiza ndani ya mamlaka yetu, kwa hiyo wamekuwa kama alivyosema wa kwanza (mshairi): Kwa maisha yangu, ungali wanywa maziwa mapya asubuhi,Na kula kwako tende kwa jibini. “Sisi ndio tuliokupa daraja, wala hukuwa wa juu,na kukuzungushia ulinzi (kwa farasi) na mikuki.

34. NA MIONGONI MWA KHUTBA ZAKE

Katika kuwaandaa watu ili kuwakabili watu wa Sham:

Ole wenu! Kwa kweli nimechoka kuwakemea! Je mmeridhika na maisha ya dunia yawe badala ya akhera na unyonge mahali pa utukufu? Endapo nikiwaita kumpiga vita adui yenu, macho yenu huzunguka kana kwamba mmefunikwa na mauti na kutokwa na fahamu kwa (kufunikwa na mauti).

Hufungika kwenu hutba yangu, kwa hiyo mnakanganyikiwa kana kwamba nyoyo zenu zimepagawa kwa hiyo hamuitii akilini. Ninyi kwangu hamuaminiki kamwe. Ninyi si nguzo itegemewayo, ninyi sio jamaa wa kuhitajiwa. Ninyi mko mfano wa ngamia ambao wachungaji wake wamepotea, kila wakusanywapo upande mmoja wanatawanyika upande mwingine, Wallahi wachochezi wabaya wa vita ni ninyi! Mnachokozwa wala hampigani, ncha zenu zinapunguzwa wala hamghadhibiki; adui halali na akawaacha na hali ninyi mpo katika mghafala mmesahau. Wallahi wamezidiwa wenye kutelekezana.

Wallahi mimi nakudhanieni endapo vita vitakuwa vikali, na mauti ikawa imeshika kasi mtakuwa mmejitenga na ibn Abi Talib kama kinavyojitenga kichwa.

Wallahi kwa kweli mtu anatoa mwanya kwa adui yake; anakuwa yu aila nyama yake, na anavunja mfupa wake na anachana ngozi yake, (huyu) kushindwa kwake ni kukubwa mno, kilichokusanya pande za kifua chake ni dhaifu (yaani yeye ni dhaifu). Wewe kuwa yeye ukipenda; ama mimi Wallahi simwezeshi binafsi adui yangu… viganja na nyayo zitadondoka na baada ya hivyo Mungu atafanya apendavyo.

Enyi watu, kwa hakika mimi nina haki juu yenu na ninyi mna haki juu yangu: Na haki yenu juu yangu ni kuwapeni nasaha, na kuwarahisishia ruzuku zenu, na kuwaelimisheni ili msiwe wajinga, na kuwaadabisheni ili mjue. Ama haki yangu juu yenu ni kuitekeleza bai’a, na nasaha mbele ya macho yangu na mbali nayo, na kuniitika niwaitapo, na kutii ninapowaamrisha”.

35. NA MIONGONI MWA KHUTBA ZAKE(A.S)

Baada ya hukumu (tah’kiim):

Shukrani ni za Mwenyezi Mungu japo zama zilete misiba mizito na tukio zito na kubwa[104] .

Na ninashuhudia kuwa hapana mungu isipokuwa Allah Mungu Mmoja peke Yake hana mshirika, hayuko mungu mwingine pamoja na Yeye, na kuwa Muhammad(s.a.w.w) ni mja Wake na mjumbe Wake.

Ama ba’ad, kwa kweli kumuasi mtoa nasaha mwenye huruma alie mjuzi mwenye uzoefu kunarithisha hasara, na matokeo ya majuto. Nami nilikuwa nimewaamrisheni amri yangu kuhusiana na hukumu hii[105] , na nilikuwa mnyofu kwenu, kwa kuwapa rai yangu iliyohifadhiwa, lau ingetiiwa amri ya Qasiir![106]

Mlinikatalia ukataaji wa wapinzani wakakamavu, na waasi wasio watiifu, mpaka mtoaji wa nasaha akaishakia nasaha yake[107] na kijiwe (kigumu kama cha kiberiti) kilishindwa kutoa cheche zake[108] , hivyo nikawa mimi na nyinyi ni kama alivyosema yule mshairi Hawaazin[109] . Nilikuamrisheni amri yangu huko Mun’arajil-Liwa Nasaha haikubainika isipokuwa baadae asubuhi ya kesho yake”.

36. NA MIONGONI MWA KHUTBA ZAKE(A.S)

Katika kuwahofisha watu wa An-Nah’rawan:[110]

Mimi ni mwonyaji kwenu, nakutahadharisheni msije kuwa waliotupwa chini wafu katika mto huu, na ardhi tulivu ya chini bila ya ubainifu wowote kutoka kwa Mola wenu Mlezi, wala hoja ya nguvu mliyonayo, mmekuwa katika myumbo na kudra imewatieni kamba.

Na nilikuwa nimewakatazeni hukumu hii - maamuzi mliyoyafanya - mkanikatalia ukataaji wa wapinzani wanaotupilia mbali, kiasi cha kunifanya niichukue rai yangu na kuitia kwenye utashi (potovu) wa nafsi zenu, na hali ninyi mkiwa wapumbavu wa akili - hamna baba - Mungu awaangamize! katika kuwakatazeni hukumu ile, sijawatakieni madhara yeyote.

37. NA MIONGONI MWA SEMI ZAKE(A.S)

Usemi huu waenda mwendo wa khutba:[111]

Na humo(a.s) anataja fadhaili zake aliisema baada ya tukio la An-Nah’rawan:

Nilitekeleza amri walipokuwa wameshindwa[112] na nilijitokeza walipofichama, na nilitamka waliponyamaza, nilipita kwa nuru ya Mungu waliposimama. Nilikuwa wa sauti ya chini mno kati yao, na wajuu mno kwa kwenda mbele, na niliruka na hatamu zake, na nilikuwa wapekee kuikabili khatari iliyokuwa ikiepukwa. Na nilikuwa kama jabali halitikiswi na upepo mkali wala haimuondoi dhoruba. Yeyote hakuwa na la kuniaibisha nalo, wala msemaji hakuwa na la kunikebehi (yaani sikuwa na aibu mtu awezayo kuniaibisha nayo)[113] .

Mnyonge kwangu ni mwenye hadhi mpaka nimrudishie haki yake, na mwenye nguvu kwangu ni dhaifu nitaichukuwa haki aliyodhulumu kutoka kwake.

Tumeyaridhia maamuzi yake Mungu[114] , na tumesalimu amri yake Mungu. Je, mwaona mimi nimsemee uwongo Mjumbe wa Mungu(s.a.w.w) ? Wallahi mimi ndimi wa kwanza kumsadiki, sitokuwa wa kwanza kumsemea uwongo. Niliangalia suala langu, na kuona utii wangu yapasa uitangulie ba’iah yangu, hali ikiwa ahadi yangu imekuwa mzigo shingoni mwangu[115] .

38. NA MIONGONI MWA KHUTBA ZAKE(A.S)

Akielezea maana ya shub’hah (kushabihiana):

Shub’ha imeitwa hivyo kwa sababu inashabihiana na ukweli, ama wapenzi wa Mungu, mwanga wao humo ni yakini, na dalili yao humo ni nji ya mwongozo. Ama maadui wa Mungu wito wao humo ni upotovu, na dalili yao ni upofu. Hatoepuka umauti mwenye kuuogopa[116] .

39. NA MIONGONI MWA KHUTBA ZAKE(A.S)

Kuwalaumu wanaobaki bila ya kwenda vitani:

Nimekumbwa na balaa la wasiotii nitoapo amri, wala hawaitikii nikiita. Hamna baba! Mnangoja nini kwa kumnusuru Mola wenu?

Hapana dini iwezayo kuwakusanya, wala hisia ya aibu kuwaghadhibisheni! Nasimama kati yenu nikiomba nusra, na nakuiteni nikiomba usaidizi, wala hamnisikilizi usemi wowote, wala kunitii amri, mpaka yafichuke matokeo mabaya! Kisasi hakilipwi pamoja na ninyi, wala lengo halifikiwi pamoja na ninyi. Niliwaita ili muwanusuru ndugu zenu mkakoroma mkoromo wa ngamia aliyepatwa na maradhi … na mkawa wazito kama uzito wa ngamia aliyekonda mwenye kujeruhiwa kisha nikajiwa na kikosi kutoka kwenu, dhaifu kikinepanepa; (Kana kwamba wanasukumwa kwenye mauti nao wanaona; 8:6)

Maelezo : Ar-Radhiy (r.a) amesema: Usemi wake (a.s): (mutadhai-bun) yaani yenye kuyumbayumba; kutokana na kauli yao: (tad- ha’abati riihu) yaani upepo umeyumbayumba, uvumapo ukiyumba, kutokana nalo hilo mbwa mwitu amepewa jina hilo kwa sababu ya kuyumbayumba mwendo wake.

40. NA MIONGONI MWA MANENO YAKE(A.S)

Kuhusu Khawariji alipoisikia kauli yao: “Hakuna hukumu ila ya Allah”

Na neno ni la kweli lakini linakusudiwa batili! Naam ni kweli kuwa hapana hukumu ila ni ya Mungu, lakini hao wanasema: Hapana uamiri ila wa Mungu. Na kwa kweli watu hapana budi wawe na mtawala mwema au muovu[117] , mu'umin atenda (mema) katika utawala wake[118] , na kafiri anastarehe humo, na Mungu aufikisha humo muda[119] , na hukusanywa (kwa utawala wake) kodi, pamoja na yeye hupigwa vita adui, pamoja naye njia zabakia na amani, pamoja naye huchukuliwa (haki zilizodhulumiwa) kutoka kwa mwenye nguvu kwa ajili ya mnyonge; Ili mwema apumzike na ili muovu apumzishwe

Na katika riwaya nyigine ni kuwa yeye(a.s) aliposikia hukumu yao akasema: “Hukumu ya Mungu naingoja iwe kwenu.” Na akasema: “Ama utawala mwema mchamungu humo hutenda mema, ama utawala muovu hustarehe humo mwenye mashaka (shaqiy); mpaka muda wake ukatike na mauti yake imkute”.

41. NA MIONGONI MWA KHUTBA ZAKE(A.S)

Na miongoni mwa Khutba yake(a.s) - Ameitaja ibn Talha katika kitabu Matalibus-Su’ul, Jz. 1, uk. 170

Kuhusu utekelezaji na ukweli:

“Enyi watu! Kwa kweli kutekeleza ahadi ni pacha wa ukweli[120] , siijui kinga yenye kuhifadhi mno kuliko hiyo (kwa shambulio la dhambi) wala hafanyi uhaini mwenye kujua marejeo yalivyo[121] .

Kwa kweli tumeingia katika wakati ambao walio wengi miongoni mwa watu wake wameufanya uhaini kuwa ni uwerevu, na wajinga wamewanasibisha watu kama hao kuwa huo ni ujanja mzuri. Wamekuwaje (watu hawa)! Mungu awaangamize!

Na mwenye uzoefu na uelewa wa mambo ya maisha anao udhuru wa kumzuia asitekeleze amri na makatazo yake Mungu, lakini hautilii maanani ingawaje anao uwezo, akawa yu ajua hila, na pembeni mwake kuna kizuizi miongoni mwa amri ya Mungu na katazo lake lakini anaacha baada ya kuwa alikuwa na uwezo wa kutenda hayo, na huitumia fursa hiyo asiye na kizuizi cha kidini.

42. NA KATIKA JUMLA YA USEMI WAKE(A.S)

Katika kuyafuata matamanio na kuwa na matumaini marefu:

Enyi watu! Kwa kweli niliogopalo zaidi juu yenu ni vitu viwili:

1. Kuyafuata matamanio

2. Na kuwa na matumaini ya muda mrefu[122]

Ama kuyafuata matamanio kunazuia haki, na kuwa na matumaini ya muda mrefu kunasahaulisha akhera. Oh, jueni kuwa dunia imepita haraka sana; hakuna kilichobaki humo ila mabaki mfano wa mabaki ya maji katika chombo ambacho maji yake yamemwagwa na mmwagaji wake.

Oh! jueni kuwa akhera imewadia, na kila mmoja wao anao watoto, basi ni bora muwe miongoni mwa wana wa akhera, na wala msiwe miongoni mwa wana wa dunia; kwa kuwa kila mwana atakutanishwa na mama yake Siku ya Kiyama, kwa kweli leo ni siku ya matendo na wala hapana hesabu na kesho ni hesabu tu hakutokuwa na matendo”.

43. NA MIONGONI MWA MANENO YAKE(A.S)

Walimshauri Sahaba zake kujiandaa kwa vita baada ya kuwa alikwisha mtuma Jarir bin Abdillah Al’Bajaliyi kwa Muawiyah:

“Kwa kweli kujiandaa kwangu kuwapiga vita watu wa Sham hali Jarir akiwa kwao ni kuifunga Sham, na kuwatowa watu wake mbali na kheri endapo wataitaka[123] .

Lakini nimemuwekea Jarir wakati ambao hatobaki baada ya wakati huo, ila endapo atakuwa amehadaiwa au ameasi. Rai sahihi iko pamwe na utulivu, basi kuweni watulivu, wala sichukii kujiandaa kwenu[124] .

Kwa kweli nimelichunguza suala hili kwa undani kupitia pande zote sikuona njia nyingine ila ni vita au kuyakufuru aliyoyaleta Muhammad(s.a.w.w ) . Kwa hakika umma huu ulikuwa na mtawala aliyezusha uzushi - alizua bid’a - aliwafanya watu wamkasirikie, na walisema, kisha walichemka na kubadilisha kila kitu.

44. NA MIONGONI MWA SEMI ZAKE(A.S)

Tabariy ameyataja ndani ya tarehe yake, Jz.6, uk. 65, na Ath- Thaqafiy ndani ya Al-Gharatu, na Al-Baladhuriy ndani ya Ansabul’ash’rafi, uk. 411. Masqalat bin Hubairat Ash-Shaibaniy alipokimbilia kwa Muawiyah, na alikuwa amekwishawanunua mateka wa Bani Naajiyata kutoka kwa mfanyikazi wa Amirul’Mu’minina(a.s) na kuwaacha huru, na alipomdai mali ya malipo alimfanyia udanganyifu na akakimbilia Sham[125] .

Mungu amuweke mbali na rehema Masqalah! Amefanya kitendo cha mabwana, na amekimbia ukimbiaji wa kitwana, kwa hiyo msifiaji wake hakutamka kwani amemnyamazisha, na wala mfanya wasifu wake hajaeleza kitu bali amemkemea, lau angebaki tungechukua kutoka kwake kile ambacho ni chepesi kwake kukilipa, na tungengoja kuzidi mali yake.

45. NA MIONGONI MWA KHUTBA ZAKE(A.S)

Nayo ni miongoni mwa khutba ndefu alihutubia siku ya Eid al’Fitri, akiilaumu humo dunia:

Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu ambaye rehema Yake haikatishi tamaa, wala hakuna anayeepukana na neema Yake, wala haukatishi tamaa msamaha wake, wala hafanyiwi kiburi kwenye ibada yake, ambaye kwake haikosekani rehema, wala haachi kuwa na neema.

Dunia ni nyumba iliyokadiriwa kuisha, na watu wake kutoweka humo, nayo ni tamu, ya (rangi) kijani[126] . Na kwa kweli imemharakia mwenye kuitaka, na imejiangika moyoni mwa mwenye kuitamani. Ondokeni humo mkiwa na masurufu yaliyo bora[127] , wala msiombe humo zaidi ya linalotosha [128] ,3 Wala msiombe kutoka humo zaidi ya mlo.

46. NA KATIKA MANENO YAKE(A.S)

Alipoazimia safari ya Sham:

Oh, Ewe Allah! kwa hakika mimi ninajilinda kwako na mashaka ya safari, na huzuni ya marejeo, na ubaya wa mandhari katika watu wa ndani na mali na mtoto.

Oh Ewe Allah! Wewe ni mwenzi safarini, na wewe ndio wa kuachwa nyuma na familia, wala havikusanyi viwili hivi asiyekuwa wewe[129] , kwa kuwa mwenye kuachwa nyuma hawezi kuwa mwenzi safarini, na ambaye ni mwenzi safarini hawi muachwa nyuma[130] .

Sayyid ar-Radhiy (r.a): “Na mwanzo wa maneno haya imeelezwa kutoka kwa Mjumbe wa Mungu(s.a.w. w) na Amirul-Mu’mini(a.s ) ameyafuatilia kwa balagha zaidi, na kuyahitimishia kihitimisho kizuri, kwa usemi wake (walaa yaj’mau’huma ghairuka) mpaka mwisho wa mlango.”

47. NA MIONGONI MWA MANENO YAKE(A.S)

Katika kuuelezea mji wa al-Kufa

Ewe al-Kufa! nakuona kana kwamba unawambwa mfano wa ngozi iliyotiwa rangi (iliyodibaghiwa) katika soko la Ukaadhu [131] 1 unapambana na shida, na wakumbana na misukosuko, nami najua fika kuwa mjeuri anapo kukusudia kwa uovu Mungu humshughulisha na balaa au humtupia muuwaji.

48. NA MIONGONI MWA KHUTBA ZAKE(A.S)

Alipokuwa akienda Sham:

Shukrani ni zake Mungu kila usiku uingiapo na giza linapokithiri, na shukrani ni za Mungu kila nyota inapojitokeza na kila inapozama. (Mungu amesema: Na shari ya giza la usiku liingiapo; 113:3). Na himidi ni ya Mungu hakosi kuneemesha, wala halipwi fadhila.

Kwa kweli nimekwisha tuma kikosi cha mbele cha jeshi, na nimewaamuru wabakie kwenye ukingo wa mto wa Dajlah (Tigris), mpaka wajiwe na amri yangu, nimeonelea niyavuke maji haya mpaka makazi madogo ya watu miongoni mwenu wanaokaa ukingo wa mto wa Dajlah (Tigris), ili niwasimamishe pamwe na ninyi mumwelekee adui yenu, na niwafanye wawe nyongeza ya nguvu kwenu.

Sharifu Ar-Radhiy anasema: ‘Anakusudia(a.s) kwa neno Miltaat hapa, upande aliowaamuru wabakie; nao ni ukingo wa mto wa Furaat, nalo latumika pia kwa ukingo wa bahari. Na asili ya neno ni ardhi iliyo tambarare. Na yu akusudia kwa neno nut’fah: maji ya Furaati, na hiyo ni miongoni mwa ibara ya aina yake na ya ajabu.’

49. NA MIONGONI MWA MANENO YAKE(A.S)

Kuhusu sifa ya Rububiya umola ulezi na ilimu ya Kiungu:

Mwenye kustahiki sifa ni Allah (swt) ambaye ameficha mambo yaliyofichikana, na yamejulishwa na dalili zilizo dhahiri, na amezuilika na jicho lenye kuona[132] ; hivyo basi hapana jicho la asiyemuona linalomkanusha[133] wala moyo wa aliyemthibitisha unaomuona[134] . Ametangulia katika kuwa juu hapana kitu kipo juu zaidi yake, na amesogea kwa ukaribu hapana kitu kilicho karibu mno kuliko Yeye[135] . Hivyo basi si kuwa juu mno kwake kumemuweka mbali na kitu katika viumbe Vyake, wala si ukaribu wake umewafanya viumbe wawe sawa naye katika mahali[136] .

Hajazijulisha akili mipaka ya sifa Zake, wala hakuzizuia kiasi cha kuwa mbali na wajibu wa kumtambua kwake, hivyo basi Yeye ndiye ambaye alama za kuwepo zamshuhudia, kwa kukiri moyo wa mwenye kupinga[137] , Mungu yu aepuekana na wayasemayo wamshabihishao na wanaompinga, yu juu juu juu kabisa!.

50. MIONGONI MWA MANENO YAKE(A.S)

Miongono mwa maneno yake (a.s)- Hotuba hii Al’Barqii ameielzea katika kitabu “Al’Mahasin” katika

kitabu cha ‘Masabiihu dhulmi’. Na at-Tawhidii ndani ya “Al’Basairu wa Dhakhairu” uk. 32. Na ibn

Waadhihu ndani ya “At-Tari’ikh”: Jz. 2, uk. 136. Na Al’Kaulayni ndani ya “Al’Kaafii” katika mlango wa Al’bid’au war’ra’ayu

Kuhusu chanzo cha fitna:

Hakika chanzo cha kutokea fitina ni kuendekeza na kufuata matamanio, na hukumu huzushwa, humo Kitabu cha Mungu huendwa kinyume, kwa hilo watu wanasaidiana wao kwa wao[138] kinyume na dini ya Mungu. Lau batili ingekuwa tupu bila ya kuchanganyika na haki isingefichika kwa wenye kuitafuta; Na lau haki ingekuwa imeepukana na kuvikwa na batili, ndimi za wapinzani zingekatika.

Lakini huchukuliwa kutoka huku fumba[139] na huku fumba na huchanganywa, hapo shetani huwashinda rafiki zake, wataokoka wale waliotunukiwa wema kutoka kwa Mungu hapo kabla.

51. NA MIONGONI MWA KHUTBA ZAKE(A.S)

Na miongoni mwa khutba zake(a.s) - Ameieleza hotuba hii ibn Muzahim ndani ya kitabu chake,‘Swifiin.’

Watu wa Muawiyah walipowazidi nguvu watu wake(a.s) kwa kuzingira njia ya maji na kuwaziwia wasiteke maji kutoka mto wa Furati huko Siffin:

Wamekuombeni vita, basi bakieni katika madhila na kubaki nyuma kwa daraja, au zikozeni kiu panga kwa damu mtakoza kiu zenu kwa maji: Mauti hasa ni maisha ya kuburuzwa, na uhai hasa ni kufa ndani ya kutenzwa nguvu. Lo! kwa hakika Muawiyah ameongoza kikundi cha watu waasi na amewafichia kheri kiasi cha kuwa wamezifanya shingo zao ziwe shabahio la mauti.

52. MIONGONI MWA KHUTBA ZAKE(A.S)

Miongoni mwa khutba zake(a.s) - Hotuba hii inaifuata hotuba iliyotangulia katika nakala ya ibn Abil-Hadid.

Kuhusu kujinyima:

Lo! Kwa kweli dunia imekwisha na imetoa ilani kwisha kwake. Mema yake, yameondoka yametokomea haraka, inawasukumia mwisho wakazi wake, inawasukuma kwenye umauti majirani zake. Vilivyokuwa vitamu imevifanya kuwa vichungu, na kuvichafua vilivyo kuwa safi, hakikubakia humo ila mabaki kidogo kama mabaki ya maji katika chombo au mfano wa funda la mgao, lau wenye kiu wawili wafyonze hawangekata kiu. asi enyi waja wa Mungu azimieni msafara wa kuitoka nyumba hii ambayo wakazi wake wamepangiwa kutoweka, wala yasikushindeni nguvu humo matumaini, wala muda msiufanye kuwa mrefu humo.

Wallahi hata mlie mfano wa ngamia walio huzunika kwa kuwakosa watoto wao au muite kwa mnung’uniko wa huzuni wa njiwa, au mnyanyue sauti kwa unyenyekevu mfano wa watawa (waliojitenga na dunia wakimuelekea Mungu,) na muwe mmejitowa mbali na mali na watoto mkimuelekea Mungu; kutaka ukaribu na yeye, ili kuinyanyua daraja kwake au kughufiriwa ovu lililohesabika na vitabu Vyake, na kuhifadhiwa na malaika Wake, ingekuwa thawabu kidogo kulinganisha na ninavyowatarajia thawabu Zake, na ninavyo wahofia adhabu Zake.

Namuapa Mungu hata nyoyo zenu ziyayuke kabisa na macho yenu yatiririshe machozi ya damu aidha mkimtarajia au kumhofia, kisha mbakishwe kuishi duniani muda wake wa kudumu, matendo yenu hayangetoa malipo ya neema Zake kubwa - hata kama msingebakisha kitu katika juhudi zenu - zisingelipia chochote katika fadhila Zake nyingi juu yenu - na kuwaongozeni kwake kwenye imani.

53. NA MIONGONI MWA KHUTBA ZAKE(A.S)

Katika kuielezea siku ya kuchinja na hali ya mnyama atakiwaye kuchinjwa:

Na miongoni mwa ukamilifu wa mnyama achinjwaye ni kunyooka na kuinuka masikio yake na usalama wa macho yake. Endapo masikio na macho yatakuwa salama, mnyama wa kuchinjwa atakuwa amekamilika na ametimia. Japo awe mweye kuvunjika pembe na yu auvuta mguu wake kwenda machinjioni[140] .

Sayyid Ar-Radhiy amesema: “Na mansaku hapa ni mahali pa kuchinjia.”

54. NA MIONGONI MWA KHUTBA ZAKE(A.S)

Na miongoni mwa khutba zake(a.s) - Ameitaja hii Ibn al-Athir katika kitabu an-Nihaya kwenye mada

ya Dakaka, jalada la pili, uk. 128. Rejea mwanzo wa hotuba ya 26.

Pindi waliposongamana watu ili kumfanyia bai’a:

Walisongamana kwangu msongamano wa ngamia wenye kiu, siku ya kunyweshwa kwao, pale mchunga wao akiwa amewapeleka, na wameondolewa kamba; ilifika hali nidhanie wataniua, au baadhi yao watawauwa baadhi mbele yangu. Na nimeliangalia jambo hili kwa kuligeuza nje ndani kiasi cha kunizuia usingizi, sikuwa na njia ila kupigana nao, au kuyakanusha aliyoyaleta Muhammad(s.a.w .w ) : Nikaona kuikabili vita [141] 1 ni wepesi kwangu kuliko kuikabili adhabu, na mauti ya dunia ni mepesi kwangu kuliko mauti ya akhera.

55. MIONGONI MWA MANENO YAKE(A.S)

Swahaba zake waliona kwamba ameichelewesha idhini ya kupigana huko Siffiin:

Ama kauli yenu kuwa: ‘yote haya yanatokana na kuuchukia umauti?’ Namuapa Mungu sijali iwe nimeingia kwenye umauti au umauti umenijia[142] .

Ama kauli yenu kuwa amekuwa na shaka ya kuwapiga watu wa Shamu! Wallahi sikuacha vita hata siku moja ila nikiwa na matumaini kuwa kundi la watu likutane na mimi na liongoke na mimi, liangaze kwa mwanga wangu japo kwa mtazamo finyu[143] na hilo lanipendeza mno kuliko niliuwe (kundi la watu) hali likiwa ndani ya upotovu; japokuwa linarejea na dhambi zake.

56 - NA MIONGONI MWA MANENO YAKE(A.S)

Na miongoni mwa maneno yake(a.s) - Zamakhshari ameieleza hotuba hii katika Rabiul-Abraar, mlango wa Al-qatil wa shaha- da. Na ibn Muzahim katika kitabu Swifiin, uk. 520.

Siku Ya Siffiin Alipowaamuru Watu Kufanya Suluhu

“Kwa hakika tulikuwa na Mtume wa Mungu(s.a.w.w ) ; tunawaua baba zetu na watoto wetu na ndugu zetu na ammi zetu. Hilo lilikuwa halituzidishii kitu isipokuwa imani na kusalimu amri, na kuendelea ndani ya njia ya sawa na kuvuta subira kwa machungu yake na umakini katika kumpiga vita adui. Alikuwa mtu kutoka upande wetu na mwingine kutoka kwa adui yetu wanashambuliana kama wanavyoshambuliana maksai wawili kwa pembe wakitoana nafsi zao, yupi miongoni mwao atawahi kumnywesha mwenzake kikombe cha umauti, basi mara ilikuwa sisi twafanikiwa dhidi ya adui yetu na mara nyingine anafanikiwa adui yetu dhidi yetu, Mungu alipoona ukweli wetu aliwateremshia adui zetu udhalili na kutelekezwa, na aliteremsha kwetu nusura, kiasi cha Uislamu kuimarika na kumakinika na kukaa mahali pake.

“Namuapa Mungu lau tungekuwa tunayafanya mliyoyafanya, dini haingekuwa na nguzo[144] , ya kutuwama wala imani tawi lake halingesitawi. Wallahi mtamkamua damu[145] na mtamfuatilia na majuto[146] .

57 - NA MIONGONI MWA MANENO YAKE(A.S)

Na miongoni mwa maneno yake(a.s) - Khutba hii ameieleza Al-Baladhuriy ndani ya Ansabul-Ashraafi) katika tarjuma ya Ali(a.s) , na Al’Haakim ndani ya Al’Mustadrak, Jz. 2, uk. 385, na At-Tuusi ndani ya Al-Amaali uk. 214 na 347, na wengine.

Akiwapa Habari Kuhusu Mtu Atakayeamrisha Atukanwe Imam(a.s)

“Punde baada yangu atapata ushindi juu yenu mtu mwenye koo pana, tumbo kubwa, ala akionacho, na huomba asichoweza kukipata, basi muuweni, na hamtomuuwa[147] . Lo! Kwa hakika yeye atawaamrisheni mnitukane, na kujiepusha na mimi; ama kuhusu kutukana nitukaneni, kwa kuwa hiyo kwangu ni utakaso na kwenu ni uwokovu; ama kuhusu kujiepusha na mimi; wala msijiepushe na mimi; kwa kuwa mimi nimezaliwa ndani ya fitra na kutangulia katika imani na hijra[148] .

58 - NA MIONGONI MWA USEMI WAKE (A.S)

Na miongoni mwa usemi wake(a.s) - Ibn Qutaybah ameieleza ndani ya Al’Imama was-siasa Jz. 1, uk.124. Na Sibtu Ibnul’Jauziy katika Tadhkiratul’khawasi uk.100.

Aliwasemesha Khawarij

“Tufani iwakumbeni, wala asibakie miongoni mwenu chakubimbi. Hivi baada ya imani yangu kwa Mungu, na jihadi yangu pamwe na Mtume wa Mungu(s.a.w.w ) nijishuhudie binafsi kuwa ni kafiri! “Hivyo basi nitakuwa nimepotea wala sitokuwa miongoni mwa walio ongoka.” (6:56)

Rejeeni marejeo ya shari, rejeeni mkifuata athari ya nyayo. Angalieni! kwa hakika mtapata udhalili baada yangu wa sura ya jumla, na upanga mkali wenye kukata, na hilo litachukuliwa na wadhalimu hao kwenu kuwa ni sunnah[149] .

Maelezo: Sharifu Ar-Radhiy (r.a) amesema: Usemi wake(a.s) huelezwa katika njia tatu: Iwe kama tulivyosema: kwa raa, kutokana na kauli yao kwa mtu ambaye anapandikiza mtende, yaani yuautengeneza vizuri. Na yaelezwa kwa na yakusudiwa kwalo yule aelezaye Hadithi, na kuizungumzia na hii ndiyo njia sahihi kwa maoni yangu. Kama kwamba(a.s) amesema: Habakii kati yenu msimuliaji. Na huelezwa kwa tamko kwa nayo hukusudiwa mwenye kuchupa na mwenye kuhiliki pia huambiwa.

59 - NA ALISEMA(A.S)

Alipoazimia Kuwapiga Vita Khawarij, Na Aliambiwa: Kwa Hakika Hawa Watu Wamekwishavuka Daraja La An-Nahrawaan

Hapo alisema: “Maangukio yao ni chini ya nutfa, Wallahi hawaponyoki kumi miongoni mwao,[150] na wala hawatokufa isipokuwa kumi miongoni mwetu.” Sharifu Ar-Radii (r.a) amesema: nutfa anakusudia maji ya mto wa Furaat na hili ni jina mbadala zuri mno kwa maji japo maji yawe mengi. Na hilo tuliliashiria hapo nyuma wakati wa kulipita linaloshabihiana nalo.

60 - NA AMESEMA (A.S)

Na Alisema(a.s) - Ameieleza al-Mubaridu katika al-Kamil Jz. 2, uk. 120, na al-Baihaqiy katika al- Mahasin wal Masawi uk. 380, katika mlango Mahasinus-Swidiqi, na Mas’ud katika Muruj al-Dhahab, Juz. 2, uk. 416.

Walipouliwa Khawarij Aliambiwa: “Ewe Amirul-Mu’minina, Hawa Jamaa Wameangamia Wote!” Ndipo Aliposema: Lahasha wallahi: wao ni nut’fah ndani ya migongo ya wanaume na mifuko ya uzazi ya wanawake, na kila kiongozi akijitokeza[151] kati yao hukatwa mpaka wa mwisho wao wawe wevi vibaka.

61 - NA ALISEMA(A.S)

Kuhusu Khawarij

Msiwapige vita Khawarij baada yangu; kwa kuwa sisawa kati ya mwenye kuutafuta ukweli na akakosea na ambaye ameitafuta batili na kuipata (amkusudia Muawiya na sahaba zake)[152] .

62 - NA KATIKA MANENO YAKE (A.S)

Na Katika Maneno Yake(a.s) - As-Saduq ameinakili katika Man laa Yahdhuruhu al-Faqih, jalada la kwanza, uk. 329, na Abu Na’im katika al-Hiliyatu, jalada la kwanza, uk. 77, na at-Tusi katika al-Misbahu, uk. 461, na al-Mufid katika al-Amaal, uk. 87.

Pindi Alipohofishwa Kuuliwa Ghafla (Akasema): Kwa hakika mimi nina ngao madhubuti kutoka kwa Mungu, siku yangu itakapokuja itajitoa mbali na mimi na kuniachia; wakati huo mshale hautokosea wala jeraha halitopona.

63 - NA MIONGONI MWA SEMI ZAKE(A.S)

Na Miongoni Mwa Semi Zake(a.s) - Ameieleza Zamakhshari katika Rabiul-Abrar, na ameieleza mwanzoni mwake Ibn Kathir katika al-Bidaya wan-Nihaya: Jz. 8, uk. 12.

Ahadharisha fitna za dunia

Lo! Kwa kweli dunia hii ni mahali ambapo usalama haupatikani ila mtu akiwa yumo humo,[153] tendo lililofanywa kwa ajili ya dunia tu haliokoi[154] .

Watu wamekabiliwa na mtihani wa maafa, walivyovichuma humo kwa ajili yake (ya dunia) watatolewa nje yake (kwa kifo) na kuhesabiwa dhidi yao [155] ,3 na walivyovichuma kutoka humo (kwa kutenda mema) si kwa ajili ya dunia - kwa ajili ya ya akhera - watavipata, na kubaki navyo humo; kwa kuwa hiyo – dunia - kwa wenye akili ni kama kivuli mara chajitanuwa na kujieneza punde chajikunja na kupungua.” Ameitaja al-Amidi katika kitabu Ghurarul-Hikami, chini ya herufi ‘inna.’

64 - NA MIONGONI MWA KHUTBA ZAKE(A.S)

Na Miongoni Mwa Khutba Zake(a.s) - Ameieleza ibnul-Jauz katika Tadhkira yake, uk. 145, na ameitaja al-Aamidi katika al- Ghuraru wal-Duraru.

Kuhusu Kujiandaa Kwa Ajili Ya Mauti:

Mcheni Mungu enyi waja wa Mungu, zitanguliyeni ajali zenu kwa matendo yenu (mema), na mnunuwe kinachobaki kwa ajili yenu kwa kinachowatokeni[156] , tokeni kwani mmehimizwa[157] , na jiandaeni kwa ajili ya umauti kwani hakika umewakurubia, na muwe kaumu ya watu waliopigwa kelele wakaamka[158] , na wakajua kuwa dunia kwao sio nyumba ya kubaki na wakaibadili; kwa kuwa Mungu (swt) hakuwaumbeni kwa mchezo bila ya lengo[159] , na wala hakuwaacheni bure[160] , na hakuna kitu (kinachozuia) kuingia mmoja wenu jannah au moto ila ni mauti[161] .

Na kwa kweli ni lengo linalopunguzwa na muda mfupi mno, na kubomolewa na saa, kadiri[162] inayopunguzwa na punde na kuharibiwa na saa yabidi izingatiwe kuwa ni fupi mno.

Na hakika ghaibu inayosukumwa na mabadiliko mawili mapya, yaani usiku na mchana, ni ya haraka mno kurejea. Msafiri anayerudi ama amefaulu au kutofaulu yu astahiki kuandaliwa masurufu bora.

Hivyo basi jiandalieni masurufu duniani kutoka duniani,8 kwa ambayo mtazihifadhi nafsi zenu kesho, kwa hiyo mja akimcha Mola wake Mlezi atakuwa ameinasihi nafsi yake, na atakuwa ameitanguliza toba yake, na atakuwa ameyashinda matamanio yake, kwa kuwa kifo chake kimefichwa, na matumaini yake yanamhadaa, na Shetani amefanywa kwake wakala, yuampambia maasi ili ayatende, na yuamshawishi kuchelewesha toba kwa kujifanya nitatubu baadae, kifo kitakapomhujumu kitamsahaulisha aliyonayo.

Lo! Hasara iliyoje kwa mwenye kughafilika ambaye umri wake utakuwa hoja dhidi yake, na siku zake zimfikishe kwenye maafa! Tunamuomba Mungu (swt) atujaalie na ninyi tuwe miongoni mwa ambao neema hai- wafanyi wajivune wala lengo haliwafanyi wazembee kumtii Mola Wao, wala baada ya umauti hafikwi na majuto wala huzuni.

SHARTI YA KUCHAPA

Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s) Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.

MWISHO WA KITABU