UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYYAH

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYYAH0%

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYYAH Mwandishi:
: Abdul Kareem J. Nkusui
Kundi: Tarehe

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYYAH

Mwandishi: Dr. As'ad Waheed Alqasim
: Abdul Kareem J. Nkusui
Kundi:

Matembeleo: 8216
Pakua: 1618

Maelezo zaidi:

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYYAH
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 13 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 8216 / Pakua: 1618
Kiwango Kiwango Kiwango
UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYYAH

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYYAH

Mwandishi:
Swahili

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYA

KIMEANDIKWA NA: DR. ‘ASAD WAHID AL-QAASIM.

KIMEATAFSIRIWA NA: ABDUL KARIM J. NKUSUI

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu, kwa jina la: Haqiqat Shi’a Ithna-Asahariyyah kilichoandikwa na, Dr. ‘Asad Wahid Al-Qaasim.

Kitabu hiki ni utafiti wa kina uliofanywa na mwanachuoni huyu mahiri, kuhusu mitafaruku iliyotokea katika Uislamu na baina ya Waislamu, kuanzia wakati wa Mtukufu Mtume(s . a . w . w) , na mara tu baada ya kufariki kwake hadi sasa. Katika utafiti wake huu, ameiangalia sana historia ya Kiislamu kama ilivyohifadhiwa katika vitabu vya historia vilivyo andikwa na wanachuoni wa Kiislamu wa kuaminika wa madhehebu zote za Kiislamu zijulikanazo. Katika kujadili masuala mbali mbali yenye utata, huwa ametumia dalili, hoja, akili na elimu.

KUHUSU MTUNGAJI

Mtungaji ni mtafiti katika misingi ya ukweli, mwenye kujitahidi jitihada kubwa kabisa katika njia ya kuufikia, hadi Allah (s.w.t.) akamwongoa katika njia ya sawa, “Na wale ambao wamejitahidi katika njia yetu. tutawaongoa katika njia zetu.”

Amezaliwa katika kijiji cha Dairul-Ghusun katika ukingo wa Magharibi, katika nchi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Amehitimu masomo yake ya Sekondari, kisha akaenda Jordan Na akapata Diploma ya Uhandisi, kisha akaenda Ufilipino na akapata Shahada ya kwanza ya Uhandisi kisha akapata Shahada ya pili katika Idara ya ujenzi. Na hivi sasa amepata shahada ya Udaktari katika Idara ya utawala wa serikali baada ya kumaliza utafiti wake (wa “Islamic public Administration” “Mfumo wa utawala wa Kiislam”).

NENO LA MCHAPISHAJI

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu, kwa jina la: Haqiqat Shi’a Ithna-Asahariyyah kilichoandikwa na, Dr. ‘Asad Wahid Al-Qaasim.

Kitabu hiki ni utafiti wa kina uliofanywa na mwanachuoni huyu mahiri, kuhusu mitafaruku iliyotokea katika Uislamu na baina ya Waislamu, kuanzia wakati wa Mtukufu Mtume(s . a . w . w) , na mara tu baada ya kufariki kwake hadi sasa. Katika utafiti wake huu, ameiangalia sana historia ya Kiislamu kama ilivyohifadhiwa katika vitabu vya historia vilivyo andikwa na wanachuoni wa Kiislamu wa kuaminika wa madhehebu zote za Kiislamu zijulikanazo. Katika kujadili masuala mbali mbali yenye utata, huwa ametumia dalili, hoja, akili na elimu.

Pia katika jitihada yake hii, amejaribu kuelezea kwa urahisi kabisa njia za kupunguza (kama si kuondoa kabisa) misuguano iliyopo baina ya Waislamu na baina ya madhehebu.

Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo watu hawakubali kitu mpaka kwa hoja na dalili za wazi. Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya ‘Al-Itrah Foundation’ imeona ikitoe kitabu hiki kwa luhga ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yale yale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.

Tunamshukuru ndugu yetu, Sheikh Abdul Karim J. Nkusui kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vile vile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.

Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni mwanga kwa wasomaji wetu na kuzidisha upeo wao wa elimu katika dini.

Mchapishaji:

Al-Itrah Foundation

S. L. P. 1017

Dar-es-Salaam.

DIBAJI YA MTARJUM

Mtunzi wa kitabu hiki Haqiqat Shi’a Ithna-’Ashariyyah amejitahidi sana kutoa ushahidi wa hoja zake katika Kitabu cha Sahih Al-Bukhari na hiyo ni kutokana na uzito na umuhimu wa Kitabu hicho ambacho kinazingatiwa na ndugu zetu Ahl as-Sunnah wal Jama’a kuwa ni Kitabu Sahih zaidi baada ya Kitabu cha Allah (s.w.t.).

Na yaonyesha kuwa Mtunzi amenukuu ushahidi wake kutoka Sahih Al-Bukhari (Arabic- English) cha Dr. Muhammad Muhsin Khan-chapa ya Dar al-Arabia Beirut.

Ama kuhusu Sahih zingine kama vile Sahih Muslim na nyinginezo, Mtunzi ametaja ni mlango na maudhui gani amenukuu ushahidi wake jambo ambalo halitamwia vigumu msomaji kufuatilia pindi atakapopenda kufanya hivyo.

Ni matumaini yetu kuwa - wasomaji wetu watavutiwa na mtiririko wa Kitabu hiki; pili, watakuwa ni wadadisi, waadilifu na wapambanuao haki na batili. Hivyo hawatakanusha au kukubali jambo bila ya ushahidi wowote.

Tunamwomba Allah (s.w.t) atuonyeshe njia ya haki na atujaalie kuifuata na atuonyeshe njia ya mfarakano na atujaalie kuiepuka.

Wabillaahi Taufiq.

Abdul Karim J. Nkusui

27/11/2001

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYA

KIMEANDIKWA NA: DR. ‘ASAD WAHID AL-QAASIM.

KIMEATAFSIRIWA NA: ABDUL KARIM J. NKUSUI

NATOA ZAWADI YA KITABU HIKI

Ulimwengu wa Kiislamu siku hizi unashuhudia majaribio mengi ya kuchochea fitina na kuleta mparaganyiko baina ya Madhehebu ya Kiislamu na kuyachongea baadhi yake kwa mengine, na unashuhudia mashambulizi makali yanayo elekezwa kwa Shi’a Al-Imamiah Al-Ithna- ’Ashariyah kwa kuitukana itikadi yao ya Kiislamu na kuishambulia bila ya adabu au huruma.

Na ulimwengu wa Ki-Islamu umegharikishwa kwa mamilioni ya nakala za vitabu ambavyo vinatukana itikadi ya madhehebu hii. Na ambacho hakifichikani kwa yeyote ni kwamba vingi kati ya vitabu hivyo vinatungwa kwa msukumo unaotoka kwa Mawahhabi, na misaada kutoka kwao inaendelea kwa madai ya kutetea Ahl as-Sunnah wal- Jama’a.

Na majarabio yao haya si kingine isipokuwa ni kutaka kutimiza malengo ya wakubwa wao ambao wanaenda mbio kuwagonganisha Waislam wao kwa wao, na wanashutumu dhehebu la Shi’a kwa ukafiri, ushirikina, umajusi, kuritadi na tuhuma za mazushi mengine.

Na haikuwa kuandika kwetu maudhui haya isipokuwa ni kuuzindua ‘Ummah kuhusu ukweli wa dhehebu hili linalo singiziwa, ambalo mizizi ya itikadi yake na fikira zake ni kutoka ndani ya Kitabu Kitukufu na Sunnah Tukufu za Nabii, na utaona katika kurasa za utafiti huu, hoja na dalili zinazounga mkono hayo kutoka katika Qur’an Tukufu na vitabu Sahih vya Hadith kutoka kwa Ahl as-Sunnah, na hasa kitabu cha Al- Bukhari ambacho wanakizingatia kuwa ni kitabu Sahih baada ya Kitabu cha Allah (s.w.t.).

Na Mwandishi wa maudhui haya ni mmoja tu miongoni mwa wengi walioona haki na wakaifuata baada ya kuwa amekumbwa na fitina, lakini akakataa kujiingiza humo isipokuwa baada ya utafiti na uchunguzi kama alivyoamrisha Allah (s.w.t.):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا أَن تُصِيبُوا قَوْمًا بِجَهَالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلَىٰ مَا فَعَلْتُمْ نَادِمِينَ ﴿٦﴾

Enyi mlioamini kama Fasiq akikujieni na habari: (yeyote ile, msikubali tu) bali pelelezeni (kwanza) msije mkawadhuru watu kwa ujahili na mkawa wenye kujuta juu ya yale mlio yatenda. (49:6).

Mwanzo ulikuwa ni pale nilipopata vitabu vya Ihsan Ilahi Dhahiri, Musa Al-Musawi na wengineo katika Waandishi ambao wanadai kuwa Shi’a ni makafiri na wala hawaamini Sunnah za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) na kwamba wana Qur’an nyingine na wananasibisha kwenye misingi isiokuwa ya Ki-Islamu kabisa. Mwanzo sikuwa natilia maanani kauli zote hizo, na hiyo ni kwa sababu ya elimu yangu ya mwanzo kwa misingi ya vitabu hivyo vyenye sumu na ambavyo havina malengo isipokuwa kuchochea fitina na mparaganyiko, tukiachilia mbali kutia chumvi mno na kukuza mambo kupita kiasi.

Haikuwa rahisi kuviamini, hasa kwa kuwa sikuwa na shaka kabla ya hapo ya kwamba Shi’a ni Waislamu kama wengine miongoni mwa Ahl as-Sunnah, na hiyo ni pamoja na kuwa na elimu ya kuwepo baadhi ya hitilafu ambazo haziafikiani na fujo hilo la kutia shaka na kukufurishana.

Lakini kutokuwa kwangu na elimu ya uhakika wa itikadi ya Kishia kwa undani, na kutosheka kwangu kwa mwanzo, hakukuwa kunastahimili mbele ya mawimbi makubwa ya kuwa na shaka. Mawimbi ambayo yalikuwa yanaletwa na watu ambao wametumbukia na kuwa mateka wa baadhi ya vitabu vyenye sumu, baada ya kuamini kila kilichopo humo bila ya kudadisi wala kujaribu kujua rai ya Shi’a katika hilo kama kwamba watunzi wa vitabu hivyo ni ma’asum (wasio na madhambi), ambao haijuzu kufikiri juu ya kauli zao au kuzijadili au kuhakikisha upeo wa usahihi wake.

Na kwa masikitiko makubwa miongoni mwa hawa mateka kuna mwenye nia nzuri, na kwa mashambulizi yake dhidi ya Shi’a hataki chochote isipokuwa kutetea itikadi Sahih ya ki-Islamu kama anavyoona yeye.

Lakini Ta’assub ya upofu wenye kuchukiza na ujahili ni udhuru ambao haukubaliki baada ya kutimia njia za utafiti na uchunguzi. Mu’umin ni mwerevu na wala haamini kila kinachosikiwa na kusemwa, kwani kuna wapiga debe wa masultan na maulamaa waovu, jambo ambalo linatulazimu kuchukua kinga na tahadhari katika anga lenye kufunikwa na mawingu ya fitina na kugubikwa na giza lake.

Na mbele ya nyenzo hizi nilikuta nafsi yangu inasukumwa kwenye utafiti na uchunguzi ili kujua ukweli wa hawa Mashi’a, na nimetazama maoni ya pande mbili, na hoja zao kimaudhui na akili timamu. niliepusha nafsi yangu kutokana na Ta’assub ya kimadhehebu ya upofu ambayo haisaidii chochote katika haki, hasa katika utafiti wa masuala ya hitilafu baina ya Shi’a na Sunni unazingatiwa kwamba ni utafiti ambao uko katika duru la Uislamu kwa dalili zitokazo katika Qur’an Tukufu na Hadith tukufu za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w )

Hapa naleta mukhtasari wa utafiti wangu kwa msomaji mtukufu, ambaye namuomba afikirie katika yale anayoyasoma, kwa hakika katika utafiti huu tumetegemea sana Hadith kutoka katika vitabu Sahih vya Ahl as-Sunnah na hasa Sahih Bukhari ambayo wameizingatia kuwa Hadith zake ni sahih haziguswi na shaka wala haiwezekani kuwatuhumu wapokezi wake[1] mpaka ikawa daraja ya Sahih Bukhari kwao inafuatia Kitabu cha Allah (s.w.t.). Na katika uchunguzi huu tutaeleza nukta muhimu za Ikhtilafu baina ya Sunni na Shi’a, mfano; Uimamu, msimamo wa Mashi’a kwa Masahaba, Qur’an na Sunnah tukufu za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) tukiongezea baadhi ya maudhui ambayo ni mashuhuri kwa Mashi’a kama vile ndoa ya Muta’ (ndoa ya muda maalum) na Taqiyah …. Kwa dalili na hoja kutoka katika Kitabu Kitukufu cha Allah (s.w.t.) na Hadith sahih kutoka kwa Ahl as-Sunnah. Na hapa tunaashiria misingi tulioitegemea katika utafiti wetu na tunaitakidi kuwa ni salama zaidi katika kufikia ukweli.

Nayo ni kwamba, tumezingatia kwamba mwongozo wetu katika kutoa dalili uwe ni katika yale yote yanayoafikiana na mafuhumu ya Kitabu Kitukufu, na ambao utangulizi wake ni salama kwa sababu tunaweza kuitakidi dalili zinazoonekana kuwa ni Sahih lakini bila ya kuangalia utangulizi wake kiakili ambao huenda haukuafikiana na kinachotolewa ushahidi, na hili ni jambo ambalo limewatumbukiza wengi kwenye dimbwi la kuchanganyikiwa katika kujua ukweli na kuwapeleka mbali na ukweli.

Anayeamini tangu mwanzo kwamba Masahaba wote ni katika wale ambao hawaguswi na masharti ya kukosolewa na kurekebishwa, anaweza kukubali baadhi ya uwongo kuwa ni kweli, kwa matokeo ya nyendo za baadhi ya Masahaba ambao hawaendi sambamba na ubainifu wa Kitab na Hadith tukufu. Kisha hakuna budi tueleze baadhi ya nukta za makala ya daktari Muhammad Ar-Ramihi chini ya maudhui yenye anuani:

“Je, tunahitaji kujifunza namna ya kufikiria?” kutokana na faida inayopatikana humo, tumeonelea katika kumfumbua macho msomaji mtukufu kwa misingi ya fikira Sahih ya kielimu, na misingi yake huenda itamsaidia katika kusoma kwake utafiti huu katika upande mmoja bila ya mwingine.

Hii ni pamoja na kuongezea kwamba ushahidi wa Shi’a kwa Hadith zinazotoka katika vitabu Sahih vya Ahl as-Sunnah haimaanishi kwa hali yeyote ile kuamini kwao usahihi wa yote yaliopokelewa humo bali ni kwa kusimamisha hoja na dalili kwa wanao wapinga kwa yale yaliokuja kwa njia yao na kuwalazimisha kwa yale walio jilazimisha nafsi zao na huu ndiyo usawa na uadilifu halisi kwa watu wa mantiki na uadilifu.

Na kuhusu manhaji (njia) sahihi ya kufikiria au utafiti sahihi wa kielimu tumeonelea kwamba tuelezee baadhi ya nukta za makala ya daktari Muhammad Al-Ramihi Mhariri wa Jarida la Kiarabu la Kuwait:

Je, Tunahitaji Kujifunza Namna Ya Kufikiri?

“Moja ya mambo ambayo yamekuwa ni muhimu katika akili ya Mwarabu (binadamu) wa leo ni jambo la fikra sahihi au kufikiria kielimu - tukitaka ukweli halisi - nalo ni jambo ambalo lipo katika mifumo yetu ya malezi na katika jamii zetu kwa upana zaidi, na bila ya kuwepo mapito mema kwa mkabala wa kufahamu jambo hili tutabaki tunasikia, kusoma na kusema mambo ambayo Allah (s.w.t.) hakuyateremshia dalili, yanayoonekana mazuri kwa mandhari yake, lakini yana kila madhara kwa jamii yetu ya Kiarabu (Kiislamu) kwa sasa na kwa wakati ujao, na hatua za awali za fikra sahihi ni kutojisalimisha kwa kila kinachosemwa na kuandikwa na kukichukua kijuujuu, ikiwa hakina tegemeo la dhahiri la kiakili.

Mwanadamu ni kiumbe hai anapatwa na mambo, anapatia na kukosea, na sio lazima kila anachokisema ndiyo mwisho na kikomo kama ile kauli isemayo “kauli ya zamani tu ndio Sahihi kwa sababu waliotangulia wamekwishaisema,” haimanishi kikomo cha usahihi wake.

Rai ya zamani kuhusu jambo miongoni mwa mambo imekwisha semwa na kizazi kilichoishi katika wakati ambao binadamu walikuwa bado hawajapata maarifa waliyo nayo hivi sasa, na kwa kiasi vizazi vinavyokuja vitapata maarifa makubwa na mapana zaidi kuliko tuliyo nayo leo, kwa sababu elimu na maarifa ni kitu kipana na sio mazoea yanayobadilika kila siku kulingana na matamanio ya baadhi yetu au kutokana na ufinyo wa fahamu zao.

Hakika ubaya ambao unaenea baina yetu kwa wingi unatutishia kubaki mateka wa kutokuwa na maendeleo hali ya kuwa tunaghariki katika vita bila ya lengo, tunapigana na kuzozana kwa matamanio na kujisababishia matatizo ya kipuuzi, na tunazozana baina ya hitilafu bila ya kufikiria fikra ya kielimu ambayo ndiyo alama ya leo na ni kigezo cha kubaki hai”[2]

Dhana Nzuri Ya Moja Kwa Moja Kwa Maulamaa Walio Tangulia Mara Nyingine Inamwongoza Mtafiti Kwenye Upotovu

Na ushahidi ni kwamba, fikra potofu zimekuwa nyingi baina yetu. Ametoa Fatwa hata yule ambaye usahihi hana hata chembe ya kuweza kutoa Fatwa katika siasa, dini, utamaduni na uchumi, na tukashangilia (kuwa ni wenye kujitahidi). Upeo wa elimu yao ni ton lililodondoka kutoka kwenye maandishi ya waliotangulia, na waliokuja baada yao au kuyasoma katika zama na nyakati zinazo tofautiana sana na zama zetu na hali zetu, wao katika hali zote - ni wenye kujitahidi au kunukuu - hawafikirii kwa yale yalioandikwa au kusemwa katika wanayo yatolea Fatwa katika mambo ya dunia na dini.

Hakika ni kwa ajili ya kupenda kutoa fatwa bila ya elimu katika mambo kumewafanya watu wawe na wasiwasi katika mambo yao ya msingi, mambo ya dini na dunia yao. Ni kweli elimu mpya za kijamii zinatuambia: “Hakuna kisomo kisicho fungamana na dalili, kwani wewe unaposoma dalili unasoma kwa maarifa yako ya kielimu, kisiasa, kiutamaduni … lakini ni kweli vile vile kuna dalili ambazo kuna uwezekano wa kuwepo Ikhtilaf (tofauti) ndogo ndogo na kuna dalili zinazo gongana na akili kwa mara ya kwanza.

Na kabla hatujaingia katika maudhui ya Kitabu hiki ambacho msomaji atapata humo ukweli wenye kuathiri na hoja zenye nguvu, ni vema tuelezee baadhi ya kauli chache za maulamaa wa Ahl as-Sunnah ambazo zinathibitisha na kukiri Uislamu wa Mashi’a na ambazo bila shaka zinaweka wazi uongo wa kauli za wale ambao wanawakufurisha, na wana watuhumu kwa mengi yasiokuwa hayo na ambayo hawanayo.

Imam Shahid Hassan Al-Banna alikuwa ni mmoja wa wajumbe wa kamati ya kuleta uelewano kati ya pande mbili za Sunni na Shi’a. Na ustadh Saalim Al-Bahnasaawi anasema juu yake “Tangu ilipoanzishwa ‘Jamaatut-taqribi’ baina ya Madhehebu ya Kiislamu na ambayo Imam Hassan Al-Banna alitoa mchango wake na Al-Qummi, ushirikiano unaendelea baina ya Ikhwanul-Muslimin na Shi’a”.[3]

Na huyu Al-’Allamah Al-Sheikh Muhammad Al-Ghazaali anasema: “… hakika pande mbili zinasimamisha uhusiano wao kwa Uislamu kwa kuamini Kitabu cha Allah (s.w.t.) na Sunnah za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) na wanaafikiana maafikiano ya moja kwa moja juu ya misingi ya jumla katika dini hii,[4] vile vile anasema: “Hakika kila kilichobaki katika wakati wetu huu miongoni mwa Ikhtilaf ni fitina iliyozuliwa baina ya Sunni na Shi’a! Nayo ni fitina inayoenezwa na ukoloni na kwa uchache wanataka kuibakisha ili iwe ni utambi daima baina yao kisha watekeleze malengo yao kupitia utambi huo.[5]

Na ustadhi Anwar Al-Jundi anasema: “Ukweli ni kwamba tofauti kati ya Sunni na Shi’a haizidi tofauti zilizopo tofauti baina ya madhehebu manne”[6]

Na anasema Sheikh Hassan Ayyub katika maneno yake ya kusifu Shi’a al-Imamiah Al-Ithna-’Ashariyah: “Huenda kundi la Imamia kwa ujumla liko mbali sana na ghuluu (kusifu kupita kiasi) na lililo kubaliana na akili katika dini yake, na ni katika makundi ya Kishi’a yaliyo karibu sana na Ahl as-Sunnah …”, dhehebu lao ni ya Tawhid halisi katika sifa za Allah (s.w.t.) na kumtakasa Muumba kutokana na kufanana na viumbe …[7]

Sheikh wa Al-Azhar Muhammad Shaltut anatoa Fatwa ya kujuzu kufanya ‘ibada kulingana na madhehebu ya Shi’a Ithna- ‘Ashariyah. Na anayetaka ziada ya kauli za maulamaa wa Ahl as-Sunnah ambazo zinashuhudia Uislamu na itikadi ya Kishi’a basi arejee Kitabu cha As- sunnatu wa Shi’a dhajatu muftailah au Kitabu cha Araul-Ulamaai l- Muslimina Fi Shiati wa Thawrahtil-Islamiyah vya Dr. Izzudin Ibrahim.

Ikiwa Maulamaa watukufu mfano wa Al-Banna, Kishki, Al-Maududi, Anwar Al-Jundi Al-Ghazaali na Hawway, Hassan Ayyub, Fatihi Yakun, Atilimisani, Abu Zahra, Shaltut na wengineo wengi ambao nafasi haitoshi kuwataja - wanaona kuwa Shi’a ni Waislamu wenye kumpwekesha Allah (s.w.t.), je, ni mantiki na akili kuacha kauli zao na kuchukuliwa kauli za Dhahiriy, Al-Khatib Al-Jazairi, Al-Gharib, na wengineo miongoni mwa waandishi wanaowakufurisha Shi’a na ambao hawakumsikia yeyote isipokuwa kupitia katika vile vitabu vyao vyenye sumu?

Wako wapi wao kati ya Maulamaa wajuzi ambao wametoa Fatwa juu ya Uislamu mzuri wa Shi’a?

Na ni nani Musa Al-Musawi ambaye baadhi wanakitolea ushahidi Kitabu chake dhaifu, na kukizingatia kuwa ni msingi wa hukumu yao juu ya Shi’a isipokuwa ni kati ya watu waovu waajiriwa (mamluki) aliye tayarishwa na maadui wa Uislamu baada ya kufaulu mapinduzi ya Kiislamu ili kufanya mambo maovu wakamvalisha kilemba cha Maulamaa wa Kishi’a ili atukane itikadi yao kwa jina la Ushi’a baada ya kujazwa mifuko yake kwa kile kitakacho fikisha paji lake motoni siku ambayo haitofaa mali wala watoto isipokuwa yule atakayemwendea Allah (s.w.t.) kwa moyo safi, na watajua wale ambao wamedhulumu ni mwisho gani wataishilia.