UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYYAH

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYYAH0%

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYYAH Mwandishi:
: Abdul Kareem J. Nkusui
Kundi: Tarehe

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYYAH

Mwandishi: Dr. As'ad Waheed Alqasim
: Abdul Kareem J. Nkusui
Kundi:

Matembeleo: 8247
Pakua: 1632

Maelezo zaidi:

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYYAH
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 13 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 8247 / Pakua: 1632
Kiwango Kiwango Kiwango
UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYYAH

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYYAH

Mwandishi:
Swahili

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYA

KIMEANDIKWA NA: DR. ‘ASAD WAHID AL-QAASIM.

KIMEATAFSIRIWA NA: ABDUL KARIM J. NKUSUI

UTANGULIZI

NI NANI SHI’A ITHNA-’ASHARIYYAH?

Tunaeleza katika mwanzo wa utafiti huu nini makusudio ya neno Shi’ah, vipi limeanza, na kuenea kwa Ushi’a Tunakuta katika kamusi za lugha kuwa neno Shi’a lina maana ya “Kufuata na wafuasi, na aghlabu limetumika jina hili kwa wafuasi wa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) na watoto wake mpaka likawa ni maalum kwao”.

Na wa mwanzo aliepanda mbegu ya Ushi’a katika Uislamu ni Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) naye ni wa kwanza kutamka jina la Shi’a kwa wafuasi wa Ahlul Bayt(a.s ) kama alivyopokea hayo As-Suyuti katika tafsiri yake Durrul-Manthur katika Ayah tukufu (Hao ni viumbe bora). Amesema: Amepokea Ibn Asakir katika Sanad yake kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillah amesema: Tulikuwa kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) na akaingia Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) basi akasema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) : “Naapa kwa ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika huyu na wafuasi wake wao ni wenye kufaulu siku ya Qiyamah na kwake imeteremka! “Hakika walioamini na kufanya vitendo vyema hao ndiyo viumbe bora.[8]

Hivyo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) alilingania Manhaj (njia) hii na akawafanyia Ahlul-Bayt(a.s ) wapenzi na wafuasi. Na utapata juu ya hayo katika sehemu ya kwanza ya utafiti huu, dalili zinazothibitisha wosia wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) kwa Ahlul-Bayt(a.s ) wake kwa Uimamu katika ‘Ummah huu baada yake, kuanzia kwa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) na kuishia kwa Al Imam Muhammad Mahdi Sahibu-z- Zamaan(a.s ) ambaye atadhihiri mwisho wa zama ili kujaza dunia kwa haki na uadilifu kama ilivyojaa dhuluma na ujeuri.

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) alipoaga dunia, kundi katika Masahaba, walionelea ukhalifa usiende kwa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) , na Imam(a.s ) alikwishasema kwa kupinga kwake juu ya hilo kwa kukataa kwake kumbai Abubakr kwa kipindi cha miezi sita kama alivyopokea hayo Bukhari katika Sahih yake ambayo maelezo yake yatakuja katika sehemu ya kwanza kwa idhini ya Allah (s.w.t.). Na walikataa kumbai pamoja naye kundi la Masahaba wakubwa, mfano wa Zuber, ‘Ammar, Salman, Abudhar na wengineo.

Kisha Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) alipoona kukataa kwake kunasababisha mbomoko usiotengenezeka katika Uislamu, na sote tunajua kuwa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) hakuwa akitaka Ukhalifa wala hakutaka kutawala wala kupupia Ufalme na kushinda - alikubali na akayafumbia macho yale anayo yaona kuwa ni haki yake kwa kuunusuru Uislamu kutokana na kubomoka na kuparaganyika. Wafuasi wake walibaki chini ya uongozi wake, na Ushi’a haukuwa na nafasi ya kudhihiri katika zama za Makhalifa wa kwanza, kwa sababu Uislamu ulikuwa unapita katika manhaj yake iliyo sawa sawa.

Na alipopewa Bai’a Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) , Mu’awiyah bin Abi Sufian alikataa kumbai na akampiga vita katika sehemu ya Siffin, na alimtangulia kwa hilo ‘Aisha bint Abubakr as- Siddiq.

Alitoka akiongoza jeshi linalompiga vita Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) katika vita vinavyojulikana kama vita vya Jamal. Masahaba wengi walijiunga pamoja na Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) katika vita vya Siffin hadi wengi wao wakauliwa chini ya uongozi wake, kama vile ‘Ammar bin Yaasir, Khuzaimatu Dhi Shahadatain, Abu Ayyubil-Ansari na wengineo.

Na baada ya mambo kumnyookea Mu’awiyah bin Abi Sufian na kumalizika kwa duru ya Makhalifa, Mu’awiyah bin Abi Sufian alifuata sera ya madikteta, akawakandamiza Waislam na kuchukua Bai’a ya mwanae Yazid bin Mu’awiyah bin Abi Sufian kwa, ‘Ummah kwa mabavu, na akazikhalifu Ayah za Allah (s.w.t) zilizo wazi, kama vile kumnasibisha Ubaydullah bin Ziyad kwa baba yake na kupanua meza za vyakula, kujenga mahekalu makubwa na mengineyo katika israf na upuuzi, yote hayo kwa mali za ‘‘Ummah na pato la Waislamu.

Haya yote na watu bado wako karibu na zama za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) na makhalifa, na namna walivyokuwa wakiyapanyongo mambo ya dunia na matamanio yake.

Kisha akamtilia sumu Al Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) na akamuua baada ya kutengua ahadi na masharti yote aliyomuahidi, kisha akachukua bayi’a kwa mwanae Yazid bin Mu’awiyah bin Abi Sufian kwa mabavu na hali yake inajulikana kwa ‘Ummah bila ya kuwa na ikhtilafu - Waislamu walishamjua kuwa ni mtu wa dunia hana uhusiano na dini… mpaka yakatokea mapinduzi ya Al Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) Karbala, na kuuawa kwake Shahid pamoja na wafuasi wake wasiopungua sabini na mbili miongoni mwa Aali zake na wafuasi wake, baada ya kukataa kumbai Yazid bin Mu’awiyah bin Abi Sufian.

Vivyo hivyo ulikuwa ni mwendo wa watawala wa Bani Ummayyah na Bani Abbas, katika kuwakandamiza Ahlul-Bayt(a.s ) . Ukandamizaji kwa Ahlul Bayt(a.s ) , ulikuwa kwa muda wote huo, na waliyapata (matatizo) mengi, miongoni mwayo ni kuuliwa, kufungwa jela na kuadhibiwa.

Ukiuchunguza mwendo wa watoto wa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) na Ahlul Bayt wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) kwa ujumla, na ukaulinganisha na mwendo wa wafalme wa Bani Umayyah na Bani ‘Abbas, utagundua kuwa ndio umesababisha kuenea kwa Ushi’a ambao ndio Uislamu wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) na si vinginevyo, na wala si kama walivyosema wapumbavu ambao walikuwa wakikariri wanayo yaeneza watawala wa Bani Umayyah na Bani ‘Abbas kuwa Ushi’a ni upuuzi wa ‘Abdillah bin Saba’ au mengineyo yasiyokuwa hayo miongoni mwa uongo ambao unasambaratika mbele ya macho ya anayesoma Itikadi hata kwa uchache tu.

Katika kipindi cha kwanza cha Bani Abbas, Al Imam Ja’afar as-Sadiq(a.s ) ambaye ni Imam wa Sita wa Mashi’a - kutokana na siasa yake ya hekima, aliweza kushirikiana na watawala na watu.

Na kwa sababu ya watawala kushughulika na kuimarisha utawala wao - alianza kueneza hukumu na kusambaza Hadith ambazo alizichukua kwa baba yake Al Imam Muhammad Al-Baqir(a.s ) kutoka kwa baba yake Al Imam Zaynul ‘Abidiin(a.s ) kutoka kwa Al Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) , Bwana wa Mashahid (na Imamu Hasan as), kutoka kwa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib( a.s ) kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) .

Ushi’a ukadhihirika bila ya kuwa na mfano katika zama hizo, kupanuka Madrasah ya Al Imam Ja’afar as-Sadiq(a.s ) katika zama hizo na umashuhuri wake ndiyo sababu ya kuitwa madhehebu ya Ja’afariyyah katika manhaji (njia) ambayo Shi’a Imamiyyah Ithna-’Ashariyyah wanaiamini tangu wakati huo hadi leo hii, na ambayo si kingine isipokuwa ni madhehebu ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) na ambayo ndiyo dhehebu la ki-Islamu la asili.

Miongoni mwa waliokuwa wanafunzi wake wakubwa ni kama vile Hassan Al-Basriy na Abu Hanifa An-Nu’uman ambaye amesema katika kauli yake mashuhuri. “Kama sio miaka miwili angeangamia Nu’uman” alikuwa na maana ya miaka miwili ambayo alikuwa mwanafunzi katika darasa la Imam Jaafar bin Muhammad bin Ali bin Hussein bin Ali bin Abu Talib(a.s ) , na ambaye amepewa laqab ya As-Sadiq.

Abu Hanifa aliuawa kwa sumu katika jela ya Abu Ja’afar Al-Mansur kwa sababu ya mapenzi na ufuasi wake kwa Ahlul Bayt(a.s ) , na kumpinga kwake Mansur, na kwa sababu alikataa cheo cha Qadhi katika utawala wake. (rejea chochote ukitakacho katika vitabu vya historia juu ya hilo) Mansur alimkataza kutoa Fatwa hali yuko ndani ya jela.

Ama aliye eneza yanayojulikana kama madhehebu ya Hanafi ni Qadhi Abu Yusuf ambaye alikuwa mwanafunzi wa Abu Hanifa, Haruna Rashid alimpa uqadhi, jambo ambalo lilimsaidia katika kueneza madhehebu hayo.

Ni maarufu katika tarikh kuwa madhehebu manne yamechipukia kwa Al Imam Ja’afar as-Sadiq(a.s ) , Imam Malik amechukua elimu yake kutoka kwenye vitabu vya Abu Hanifa ambaye amesoma miaka miwili kwa Al Imam Ja’afar as-Sadiq(a.s ) kama tulivyo bainisha juu, kisha Shaf’i akachukua kutoka kwa Malik, kisha Imam Ahmad akasoma kwa Shaf’i. Hivyo kinacho patikana katika vitabu vya madhehebu manne na kikaafikiana na madhebu ya Al Imam Ja’afar as-Sadiq(a.s ) , basi kimetoka kwa Al Imam Ja’afar as-Sadiq(a.s ) ; na kinacho tofautiana ni Ijtihad yao.

Hakika Shi’a al-Imamiyyah Ithna-’Ashariyyah ni dhehebu ambalo limeepukana na Shub-ha na shaka, kwa sababu chini ya jina la Ushi’a yamechipuka makundi mengi sio katika Shi’a wala Shi’a sio miongoni mwa hayo na wala sio katika Uislamu hata chembe, Shi’a wako mbali nayo kama vile mbwa mwitu na damu ya Yusuf. Mfano wa baadhi ya madhehebu ambayo yamesema juu ya uungu wa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) , wakidai kuwa sehemu ya uungu ipo kwa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) na imeungana na mwili wake, na baadhi yake yanasema kuwa Maimam ni Manabii wakidai kuwa wao ni waungu. Al Imam Ja’afar as-Sadiq(a.s ) alipojua Itikadi yao akawa mbali nao akawalaani na akawaambia wafuasi wake wawe mbali nao, na akatoa kauli kali juu ya hilo.

Na sijui ni kwa nini tunaona baadhi wanAyahesabu makundi haya na mfano wake katika Ushi’a pamoja na kujulikana kwake kuwa yako nje ya Uislamu na Mashi’a wako mbali nayo.

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYA

SEHEMU YA KWANZA: UIMAMU

Kauli ya Uimamu sio bida’a iliyozuliwa na Shi’a kwani makundi yote ya Kiislamu yanasema kuwa Uimamu ni wajib, bali ni dharura ya kimaumbile kwa watu wote. Pamoja na kwamba Shi’a wana maoni maalumu, yaliyo muhimu zaidi ni kwamba, Uimamu ni maalumu kwa Maimamu kumi na mbili kutoka katika Ahlul-Bayt(a.s ) wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) , na utaona hoja zenye nguvu juu ya hili kutoka katika vitabu Sahih vya Hadith vya Ahl as-Sunnah.

Na kama Uimamu usingekuwa faradhi kwa Waislamu wote basi wasingekuwa chini ya uongozi wa Makhalifa na kuwafuata wafalme ambao walichukua utawala kwa jina la Ukhalifa kama vile Banu Umayyah, Banu Abbas na wengineo, na kukataza kuwakhalifu na kutoka katika utawala wao, kwa sababu wao ni Makhalifa na Ulul-’Amr. kwa hiyo Uimamu ni dharura ya kimaumbile, akili ina hukumu hivyo kwa ajili ya kulinda Shariah kutopuuzwa na kuchezewa. Hivyo ilikuwa ni dhuluma kuwatukana Shi’a kwa kauli yao juu ya Uimamu. Amma kuhusu itikadi yao ya kuwa Uimamu ni maalumu kwa Maimamu wa Ahlul Bayt(a.s ) kumi na mbili, kuna dhambi gani kwa hilo? Je siyo vyema kwetu kuwauliza Shi’a ni dalili gani waliyo nayo juu ya hilo? Tutafupisha hoja na dalili zetu katika majibu yetu juu ya swali hili kwa utaratibu ufuatao:-

Kwanza: Hoja Za Kuthibitisha Uimamu Wa Ahlul- Bayt (A.S.)

Dalili zilizopokelewa kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) juu ya Uimamu wa Ahlul-Bayt(a.s ) katika ‘Ummah baada yake ni nyingi. Tunaorodhesha zilizo mashuhuri kati ya hizo:

*Katika Sahih Muslim kwa Isnad yake kutoka kwa Zaid bin Arqam amesema: “Hakika Mtume alisimama akahutubia katika Ghadir Khum (baina ya Makkah na Madina), akasema: “Enyi watu hakika mimi ni binadamu, anaweza kunijia Mjumbe wa Mola wangu (Malaika wa Mauti) basi nikamwitikia, hakika mimi nawaachieni vizito viwili cha kwanza ni Kitabu cha Allah (s.w.t.) humo kuna uongofu na Nuru, basi chukueni (uongofu) katika Kitabu cha Allah (s.w.t.) na shikamaneni nacho, na Ahlul Bayt wangu ”.[9]

*Na katika Sahih At-Tirmidhi kwa isnad yake kutoka kwa Ja’bir bin ‘Abdullah amesema: “Nilimwona Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) katika Joho lake siku ya ‘Arafa naye yuko juu ya ngamia wake anahutubia, basi nilimsikia anasema: “Enyi watu hakika mimi nimekwisha kuachieni ambayo kama mtashikamana nayo hamtapotea kamwe, Kitabu cha Allah (s.w.t.) na kizazi changu, Ahlul Bayt wangu[10] .

Tanbihi

Pia imepokewa kwamba Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema: “Hakika mimi ninawaachieni ambacho kama mtashikamana nacho hamtapotea kamwe, Kitabu cha Allah (s.w.t.) na Sunnah zangu ”.

Tukikadiria usahihi wa Hadith hii basi haipingani na Hadith mbili zilizo Sahih hapo juu, kwa sababu Ahlul-Bayt(a.s) wao ndiyo njia zinazoaminika zaidi katika kupokea Sunnah za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Isipokuwa neno wa sunnatiy peke yake kama ilivyo katika Hadith ya mwisho halitoshelezi kujua (hiyo sunnah), kwa sababu madhehebu zote za Kiislamu zinadai kuwa zinafuata Sunnah za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) pamoja na kuwepo hitilafu nyingi baina ya madhehebu. Kwa kutazama hitilafu zao katika Hadith iliyopokelewa kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , basi ni Sunnah ipi tutafuata?

Bila shaka Sunnah ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ni moja lakini njia za kuipokea ni nyingi. Hivyo Sunnah imetofautiana kwa kutofautiana mapokezi ya wanaopokea, hivyo Sunnah ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ikawa ni nyingi, na matokeo ya hayo Waislamu wamekuwa madhehebu mengi. Imepokewa kwamba idadi yake ni makundi sabini na tatu, kila kundi linasema kuwa linafuata Sunnah Sahih ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , na kushikamana na kundi lolote kati ya haya hakuleti uongofu unaotakiwa kupatikana kama ilivyokuja katika Hadith.

Hivyo ikawa kuamini Hadith inayosema kushikamana na Kitabu cha Allah (s.w.t.) na Ahlul-Bayt(a.s) inakubalika zaidi katika akili na mantiki, kwa sababu kuna yanayotufanya tujue na yanaondosha shaka na Ikhtilaf kwa kujulikana kutakaswa kwa Ahlul Bayt(a.s) kutokana na uchafu kama utakavyoona katika yanayofuata. Katika Sahih Muslim hakika Mtume amebainisha kuwa Ahlul-Bayt(a.s) wake ni Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) , Bi.Fatimah az- Zahra(a.s) na watoto wao Al Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) na Al-Imam Hussain ibn Ali ibn Abi Talib na kwamba wao ndiyo ambao imeteremka kwao Ayah ya Tat-hiir (kutakaswa) kama anavyopokea Muslim kwa isnad yake.

“Kutoka kwa Swafiyyah bint Shaibah amesema: ‘Aisha amesema: “Alitoka Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ana Kisa’(amejifunika shuka), basi alikuja Al Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) akamuingiza pamoja naye (chini ya shuka), kisha alikuja Al Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) akamuingiza pamoja naye, kisha akaja Bi.Fatimah az-Zahra(a.s) akamuingiza pamoja naye, kisha akaja Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) akamwingiza, kisha akasema: “Hakika Allah (s.w.t) anataka kukuondoleeni uchafu nyinyi Ahlul Bayt na kukutakaseni kabisa kabisa”[11] .

Na katika Sahih At-Tirmidhi inabainika kwa hoja zilizo wazi kuwa wake wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) sio waliokusudiwa katika Ayah ya Tat-hiir kama baadhi ya watu wanavyodai ambapo At-Tirmidhi amepokea kwa isnad yake. Kutoka kwa ‘Amr bin Abi Salamah, mtoto wa kulelewa wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kwamba amesema: “Imeteremka Ayah hii ‘Hakika Allah (s.w.t) anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul Bayt na kukutakaseni kabisa kabisa” Katika nyumba ya ‘Umm Salamah, basi akamwita Bi.Fatimah az-Zahra(a.s) ,Al Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) na Al Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) na akawafunika kwa Kisa’ (shuka), na Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) yuko nyuma ya mgongo wake akawafunika kwa Kisa’ kisha akasema: ‘Ee Allah (s.w.t) hawa ni Ahlul Bayt wangu basi waondolee uchafu na watakase kabisa kabisa.’

‘Umm Salamah akasema: ‘Na mimi niko pamoja nao ewe Mtume wa Allah(s.a.w.w) ?’ Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akasema: ‘Wewe uko mahala pako na uko katika kheri .“[12]

Na katika Musnad ya Ahmad amepokea kwa Isnad yake kutoka kwa ‘Umm Salamah: “Hakika Mtume wa Allah(s.a.w.w) alimwambia Bi Fatimah az-Zahra(a.s) : ‘Niitie mume wako na watoto wako’, basi akaja nao, hivyo akawafunika kwa Kisa’, kisha akaweka mkono wake juu yao akasema: ‘Ewe Allah; hakika hawa ni Ahlul Bayt wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) basi jaalia rehema zako na baraka zako kwa Muhammad na Aali wa Muhammad, hakika wewe ni Mwenye kuhimidiwa mtukufu’. ‘Umm Salamah akasema basi nikanyanyua Kisa’ ili niingie pamoja nao akakivuta kutoka kwenye mkono wangu na akasema: ‘Hakika wewe uko katika kheri.“[13]

Hadith Ya ‘Ummu Salamah Katika Mapokezi Ya Bukhari

Katika Mustadrak As-Sahihain amepokea Al-Hakim kwa isnad yake kutoka kwa Hanashi Al-Kinaani, amesema: “Nilisikia Abu Dhar anasema akiwa ameshika mlango wa Ka’aba: Enyi watu anaenijua basi mimi ni yule mnaemjua na asienijua basi mimi ni Abu-Dhar, nimemsikia Mtume wa Allah(s.a.w.w) akiwa amesema; ‘mfano wa Ahlul Bayt wangu kwenu ni kama mfano wa Jahazi la Nabii Nuh(a.s) , atakayelipanda amenusurika na atakayeacha kulipanda ameghariki na kuteketea”[14]

Vilevile katika Mustadrak As-Sahihain kwa isnad yake kutoka kwa Ibn ‘Abbas: Amesema Mtume wa Allah(s.a.w.w) “Nyota ni tumaini kwa watu wa ardhini kutokana na kughariki, na Ahlul Bayt wangu ni tumaini kwa ‘Ummah wangu kutokana na ikhtilaf, kama kabila katika Waarabu litawakhalifu basi watakhitilafiana na kuwa kundi la Iblis“[15] .

Na kwa kufafanua zaidi na kuongezea katika yaliyopita miongoni mwa dalili katika kuthibitisha kuwa Ahlul Bayt(a.s) ndio wenye vyeo hivyo vitukufu kwa kutakaswa, wamefanywa kuwa ni maalumu kwa kupewa sifa ya tamshi la Alayhi Salaam (katika vitabu, kunatumika vifupisho vya hivyo kama(a.s) bila ya Masahaba wengine wote na wake wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , na hiyo ni kutokana na vyeo vyao vitukufu na kwa yale aliyo yafanya Allah (s.w.t.) kuwa ni maalumu kwao kwa kuwatakasa kutokana na uchafu na makosa madogo kwa makubwa kama yanavyo dhihirika katika sehemu nyingi katika Sahih Bukhari: “‘Ali alayhi-s-salaam amesema:’Nilikuwa na ngamia katika hisa yangu ya ngawira na Mtume(s.a.w.w) alikuwa amenipa sehemu katika (mali ya) Khums, basi nilipotaka kumwoa Fatimah alayha-s-salaam binti wa Mtume wa Allah(s.a.w.w) …“[16] .

Katika mlango wa kuhimiza Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Sala ya usiku na Sunnah bila ya kuifanya kuwa ni wajib, akasema “Mtume(s.a.w.w) aliwagongea mlango Fatimah na ‘Ali alayhima-s-salaam usiku kwa ajili ya Sala “[17]

Na katika riwaya nyingine: amesema: “Nilimwona Mtume(s.a.w.w) na Hasan ibn ‘Ali alayhima-s-salaam alikuwa anafanana naye…”[18] Na vilevile: kutoka kwa Ali ibn Hussein alayhima-s-salaam alimwambia[19] “Hakika Al Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) amemwambia kwamba Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) amemwambia kuwa Mtume wa Allah(s.a.w.w) alimgongea mlango usiku yeye na Bi.Fatimah az-Zahra(a.s) binti wa Mtume wa Allah(s.a.w.w) , akawaambia je, hamsali?”

Na ni mashuhuri kwamba sifa hii ya (Alayhi Salaam) hakupewa asiye kuwa Ahlul Bayt isipokuwa Manabii tu.

Na ameamrisha Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ya kwamba kuwasalia Ahli bayt wake kuambatane na kumsalia yeye, katika hadith ya Bukhari kupitia kwa Abdul-Rahman bin Abi Layla, amesema: “Alinikuta Kaab bin ‘Ujrah akasema: Je, nikupe zawadi? Hakika Mtume(s.a.w.w) alitujia (siku moja) basi tukasema: “Ewe Mtume wa Allah(s.a.w.w) , tumeshafahamu namna ya kukusalimia, basi ni namna gani tutakusalia?” akasema: “Semeni: Allahumma Salli ‘alaa Muhammadin wa Aali Muhammadin kamaa Sallayta ‘alaa Ibrahima wa aali Ibrahima Innaka Hamidum Majid”[20] .

Hiyo ni kwa sababu Ibrahim alikuwa ni mtume na ahlul-bayt wake walikuwa ni manabii na wenye kulinda Shariah baada yake, vivyo hivyo walikuwa Ahlul Bayt wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) lakini tofauti ni kwamba wao wamekuja ili wawe Maimamu na wala sio Manabii kama alivyobainisha hayo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alipomwambia Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s) “Nafasi yako kwangu ni kama nafasi ya Harun kwa Mtume Musa(a.s) isipokuwa hakuna Nabii baada yangu”[21] kama yatakavyokuja hayo baadaye. inafahamika katika yote yaliotangulia miongoni mwa Hadith kwamba Allah (s.w.t) Mtukufu kama alivyomfanya Mtume Wake kuwa ni maalumu anayeteremshiwa wahyi - Kwa Uma’asum na kutakaswa kwa kuwa sifa yake ni kufikisha ujumbe na dhamana ya usalama wa tablighi yake vinginevyo watu wasingeamini maneno yake na wala wasingekuwa na uhakika wa ujumbe wake. vile vile amewafanya Maimamu wa Ahlul Bayt(a.s) kuwa ni maalumu kwa Uma’asum na kutakaswa kwa dalili ya Ayah:

إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيُذْهِبَ عَنكُمُ الرِّجْسَ أَهْلَ الْبَيْتِ وَيُطَهِّرَكُمْ تَطْهِيرًا ﴿٣٣﴾

Hakika Allah anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul Bayt na kukutakaseni kabisa kabisa (Al-Azhab 33:33).

Na kwa sifa yao ya kujaza nafasi ambayo ameiacha Mtume. Na hiyo ni kwa kubeba Shariah ya Allah (s.w.t) kwa vizazi vijavyo kwa ajili ya kuihifadhi dini kutokana na upotovu wa wapotoshaji, uongo wa wadanganyifu na shaka za wenye shaka. Kwani kitu kibaya mno kilichokumba Shariah zilizotangulia ni kwamba wafuasi wake walikuwa wanachukua hukumu za Manabii wao baada ya kuondoka kwao kwa kila mtu. Basi upotovu ukawa kama ilivyosema Qur’an Tukufu basi wakapotoka na kupotea:

أَفَتَطْمَعُونَ أَن يُؤْمِنُوا لَكُمْ وَقَدْ كَانَ فَرِيقٌ مِّنْهُمْ يَسْمَعُونَ كَلَامَ اللَّـهِ ثُمَّ يُحَرِّفُونَهُ مِن بَعْدِ مَا عَقَلُوهُ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿٧٥﴾

Mnatumaini ya kwamba watakuaminini (hao WAyahudi) na hali baadhi yao walikuwa wanasikia maneno ya Allah kisha wanayabadilisha baada ya kuwa wameyafahamu, na hali wanajua ” (Surah Al-Baqarah 2:75).

Na kwa hiyo Uimamu unazingatiwa kuwa ni mlolongo wa Unabii katika jumla ya kazi zake isipokuwa kinachohusiana na Wahyi kwani huo ni maalumu kwa Manabii, na makusudio ya kuwa Uimamu ni mlolongo wa Unabii ni kule kuhifadhi Shariah kinadharia na kivitendo. Hivyo ikawa ni wajib Maimamu wawe Ma’asum kutokana na uwajib wa kunukuu Shariah ya Allah (s.w.t.) - ambayo alikuja nayo Mtume wa Allah(s.a.w.w) - Kwa vizazi vijavyo kupitia katika njia safi, na ya asili ambayo imepitia kwa Maimamu kumi na wawili wa Ahlul Bayt(a.s) .Na kuna dalili za Qur’an zinazoashiria kuwa Uimamu ni cheo kitukufu hakipati mtu, dhalimu au fasiki, amesema Allah (s.w.t):

قَالَ إِنِّي جَاعِلُكَ لِلنَّاسِ إِمَامًا ۖ قَالَ وَمِن ذُرِّيَّتِي ۖ قَالَ لَا يَنَالُ عَهْدِي الظَّالِمِينَ ﴿١ ٢٤﴾

Hakika mimi nitakufanya kuwa Imam kwa watu”; akasema (Ibrahim): “Je na katika kizazi changu?”; (Allah) akasema: “(ndiyo, lakini) ahadi yangu haitawafikia madhalimu ”.(Al Baqarah 2:124).

Hivyo makosa madogo na makubwa yanamfanya anayeyatenda kuwa ni dhalimu, hivyo ikawa hakuna budi ya Imam kuwa ni Ma’asum kutokana na makosa yeyote au dhambi kama ilivyoonyesha Ayah iliyotangulia.

Uchunguzi Juu Ya Ayah Ya “Tat-Hiir”

Hakuna shaka kwamba Ayah ya “Hakika Allah anataka kukuondoleeni Uchafu Ahlul-Bayt na kukutakaseni kabisa kabisa” inaonyesha Uma’asum wa wale iliyo teremshwa kwa ajili yao, kwa sababu rijsi katika lugha ina maana ya uchafu (na uchafu ni kinyume cha usafi), na tohara katika lugha ina maana ya utakaso na usafi.

Rijsi ni dalili ya dhambi na tohara ni dalili ya uchamungu, hivyo mradi wa Allah (s.w.t.) Mtukufu kuwaondolea rijisi (uchafu) ni kuwaepusha na kuwaweka mbali na mambo yanayo sababisha upungufu kwao, hii haina maana nyingine isipokuwa ni Uma’asum na utakaso ambao Ayah imeteremka kwa ajili yao nao ni Ahlul Bayt(a.s) “Muhammad, Ali, Fatwimah, Hassan na Hussein” kama zilivyo onyesha hayo kwa uwazi Hadith zilizotangulia.

Pamoja na hayo, kuna baadhi ya wanaosema kwamba Ayah hii siyo maalumu kwa Ahlul Bayt wa Nabii(s.a.w.w) , (Ali, Fatwimah, Hassan na Hussein) tu, bali inawahusu wake zake pia kwa hoja ya kuja Ayah ya Tat- hiir katikati ya Ayah nyingi (Katika sura ya Al-Ahzab) zinazohusu wake wa Nabii.

Lakini Ushahidi huu haukubaliwi, kwa kuongezea tuliyoyaeleza kuhusu Hadith ya ‘Umm Salamah kuwa Ayah hii ni maalumu kwa waliobainishwa majina yao miongoni mwa Ahlul Bayt(a.s) .

Hakika Ayah inaonyesha kwa dalili ya wazi juu ya Uma’asum wa ambao imeteremka kwa ajili yao kama tulivyotangulia kubainisha na wanawake wa Nabii sio Maasumu na hakusema yeyote juu ya hilo, na kutishiwa kwao talaka kama ilivyokuja katika Ayah zilizo tangulia Ayah ya Tat-hiir inatosha kuthibitisha ukweli huu, tukiachilia mbali kutoka kwa ‘Aisha bint Abubakr ibn Abu Quhafa na kuongoza jeshi lenye kumpiga vita Khalifa wa Waislamu na Imam wao ambaye ni wajib kumtii, na mengineyo mengi utakayoyaona kwa ufafanuzi zaidi huko mbele. Na yanayotilia nguvu pia, kutoingia wake wa Nabii katika makusudio ya Ayah ya Tat-hiir ni dhamira ya wenye kusemeshwa katika Ayah zilizotangulia Ayah hizo, ni dhamiri ya wingi wa wanawake zitazame Ayah:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ إِن كُنتُنَّ تُرِدْنَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا فَتَعَالَيْنَ أُمَتِّعْكُنَّ وَأُسَرِّحْكُنَّ سَرَاحًا جَمِيلًا ﴿٢٨﴾ وَإِن كُنتُنَّ تُرِدْنَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَالدَّارَ الْآخِرَةَ فَإِنَّ اللَّـهَ أَعَدَّ لِلْمُحْسِنَاتِ مِنكُنَّ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿٢٩﴾ يَا نِسَاءَ النَّبِيِّ مَن يَأْتِ مِنكُنَّ بِفَاحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍ يُضَاعَفْ لَهَا الْعَذَابُ ضِعْفَيْنِ ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرًا ﴿٣٠ ﴾ وَمَن يَقْنُتْ مِنكُنَّ لِلَّـهِ وَرَسُولِهِ وَتَعْمَلْ صَالِحًا نُّؤْتِهَا أَجْرَهَا مَرَّتَيْنِ وَأَعْتَدْنَا لَهَا رِزْقًا كَرِيمًا ﴿٣١﴾ يَا نِسَاءَ النَّبِيِّ لَسْتُنَّ كَأَحَدٍ مِّنَ النِّسَاءِ ۚ إِنِ اتَّقَيْتُنَّ فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ وَقُلْنَ قَوْلًا مَّعْرُوفًا ﴿٣٢﴾ وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَ بَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَىٰ ۖ وَأَقِمْنَ الصَّلَاةَ وَآتِينَ الزَّكَاةَ وَأَطِعْنَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيُذْهِبَ عَنكُمُ الرِّجْسَ أَهْلَ الْبَيْتِ وَيُطَهِّرَكُمْ تَطْهِيرًا ﴿٣٣ ﴾

Yaa ayyuha Nnabiyyu qul-liaz’waajika in kuntunna turidnal-hayata- d-dun’yaa waziynatahaa fataalayna....umatti’ikunna wa usarrihkunna saraahan jamilan wain kuntunna… minkunna … ya nisaa Nnabiyi man yya’ti minkunna bifaahishatin… lastunna… falaa takhdha’na... waqarna fiy buyuutikunna walaa tabarrajna.. .” (Al Azhab 33:28-33).

Na maneno yalipoanza kuhusu jambo la Tat-hiir, dhamiri ya mwenye kusemeshwa ikabadilika kwenda katika dhamiri ya wingi wa wanaume “Innamaa yuriydullahu liyudh’hiba ankumu-r-rijsa ahlal-bayti wa yutwahhirakum tat’hiyra”, na hakika kuteremka Ayah za Qur’an kwa kuwahofisha wanawake wa Nabii kwa talaka, na Allah (s.w.t) kutaka kuwataka Ahlul Bayt(a.s) kuja kwa kufutana, haina maana ya ulazima wa makusudio ya minasaba miwili kuwa ni wanawake wa Nabii, hiyo ni kwa sababu kuna Ayah nyingi za aina hii katika Qur’an zinazo zungumzia kuhusu mambo mawili tofauti, na huenda sababu ya kuja pamoja katika Ayah hiyo hiyo ni kuafikiana kwa kutokea minasaba miwili kama amabavyo Qur’an Tukufu haikupangwa kulingana na mfuatano wa Ayah kama zilivyoteremka, na hii inajulikana.

Hivyo basi hakuna ushahidi wowote kuwa sehemu ya Ayah ya Tat-hirr ni katika kipande ambacho kipo katika Qur’an iliyokusanywa.

Mwisho, katika yanayothibitisha kutoteremka Ayah ya Tat-hiir kwa wake wa Nabii ni Hadith ya Thaqalain (vizito viwili) ambayo inaamrisha kushikamana na Kitabu na Ahlul Bayt(a.s) . Kama makusudio ya Ahlul- Bayt(a.s) ni wake zake, je kunapatikana Hadith tukufu kwa Waislamu inayosema tufuate wanawake na kushikamana nao baada ya kufa kwa Nabii sambamba na kushikamana na Kitabu cha Allah (s.w.t)? Bila shaka hakuna. Namna gani itakuwa hivyo hali wamekwisha amrishwa kujilazimisha kubaki katika nyumba zao tukiachilia mbali kuwa wote walikuwa katika wakati mmoja, na kama itasemwa kwamba kushikamana nao ni kufuata walioyapokea, miongoni mwao katika Hadith za Nabii tunasema; kuna miongoni mwao ambaye hakupokea hata Hadith moja.

Pili -Dalili Za Kuthibitisha Idadi Ya Maimamu Wa Ahlul Bayt (A.S.) Ni Kumi Na Mbili

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ameeleza kwamba Idadi ya Maimamu wa Ahlul Bayt(a.s) ambao wanafuata baada yake ni kumi na mbili. Imekuja katika Kitabul-Ahkam katika Sahih Bukhari: “Amesema: nimemsikia Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) anasema: ‘Watakuwa Maimamu kumi na mbili’, akasema neno sikulisikia, baba yangu akasema amesema kwamba wote ni kutoka katika Maquraish .”[22]

Na katika Sahih Muslim: “Dini haitaacha kuwa imesimama hadi siku ya Qiyamah na watakuwepo kwenu Makhalifa kumi na mbili wote ni katika Maquraish ”.[23]

Na “mambo ya watu hayataacha kutengemaa maadam wataongozwa na Maimamu kumi na mbili.”[24]

Na katika Musnad ya Ahmad kwa isnad yake kutoka kwa Abdallah bin Mas’ud kwamba amesema “Aliulizwa Mtume wa Allah(s.a.w.w) kuhusu jambo la Makhalifa, akasema ni kumi na mbili kama vile idadi ya viongozi wa Bani Israil.”[25]

Na katika Taurati ya Ahlul-Kitab (kuna aya) ambayo madhumuni yake ni: “Hakika Allah (s.w.t.) Mtukufu alimbashiria Mtume Ibrahim kuhusu Ismail kwamba atamkuza, atampa kizazi na atamjaalia katika kizazi chake viongozi kumi na wawili na ‘‘Ummah mkubwa. Na tamko la neno kwa neno kama ilivyokuja katika (Taurati) kutoka katika Kitabu kitakatifu: “Na kwa habari za Ishmaeli nimekusikia, nimembariki, nitamzidisha, nami nitamwongeza sana sana. Atazaa maseyidi kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kuu”.[26]

Hakika Hadith za hapo juu baadhi yake zinabainisha kwamba utukufu wa Uislamu umejaaliwa katika Makhalifa kumi na mbili, na baadhi yake zinaonyesha kuwa uhai wa dini na kubaki kwake hadi siku ya Qiyamah umeegemezwa kwao na kwamba wao wote ni katika Maquraish. Na katika mapokezi mengine wote ni katika Bani Hashim, mapokezi haya hayaafikiani na madhehebu yeyote isipokuwa madhehebu ya Ahlul Bayt(a.s) - Madhehebu ya Shi’a Al-Imamiah Al-Ithna ‘Ashariyyah - na hiyo ni kwa kuafikiana idadi hii pamoja na idadi ya Maimamu wa Ahlul Bayt(a.s) kumi na mbili, wakati ambapo Maulamaa wa Ahl as-Sunnah katika kufasiri Hadith hii wamefikia katika njia yenye kikomo. Je makusudio yake ni Makhalifa wanne kwa kuongezea na makhalifa wa Bani Umayyah na Bani ‘Abbas?

Sisi tunajua kwamba Makhalifa wa mwanzo hawakuwa kumi na mbili, na wala kuwajumuisha kwao Bani Umayyah na Bani Abbas idadi hii haipatikani kwao na wala maulamaa wa Kisunni hawatatofautiana katika jambo kama walivyo tofautiana katika kufasiri kwao Hadith hii. Tunatoa mfano mmoja ili uone mgongano wao katika tafsiri ya Hadith hii, nayo ni rai ya As-Suyuti, anataja katika Kitabu chake cha tarekhe:

“Na walishapatikana Makhalifa kumi na mbili, Makhalifa wanne, Al Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) , Mu’awiyah bin Abi Sufian, Zuber na ‘Umar bin ‘Abdul-Azizi, hawa ni nane, na inakisiwa anaweza kuunganishwa nao Al-Mahdi Al-Abbas kwa sababu yeye katika Bani ‘Abbas ni kama vile Abdul-azizi katika Bani Umayyah, na Tahir Al-’Abbas vile vile, kwa kile alichopewa miongoni mwa uadilifu, wanabaki wawili wanaosubiriwa mmoja wao ni Al-Mahdi kwa sababu yeye ni katika Ahlul Bayt(a.s) .”[27]

Na idadi ya kumi na mbili haitopatikana katika kundi lolote isipokuwa katika Maimamu wa Shi’a Ithna-’Ashariyyah. Na Hadith zilizo pokelewa maalumu kwa jambo hili katika njia za Kishi’a ni nyingi zinapita mpaka wa Tawatur ambapo humo kumetajwa majina ya Maimamu kumi na mbili kwa ufafanuzi zaidi kiasi ambacho haikubaliki shaka wala Ikhtilaf.

Basi ni kipi kinachotufanya tuache tafsiri ya Hadith iliyo wazi inayoafikiana na mfuatano wa Maimamu kumi na mbili wa Kishi’a na tunatupia nafsi zetu wenyewe katika matatizo ambayo hakuna pa kutokea.

Ni mashuhuri kwamba bwana wetu Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na Ahlul- Bayt(a.s) na kizazi chao kimetokana na Mtume Ismail(a.s) na viongozi kumi na mbili ni maimamu wa Ahlul Bayt(a.s) na ‘Ummah mkubwa ni ‘Ummah wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na hii inafaa kuwa hoja kwa Ahlul-Kitab kuhusu ukweli wa bwana wetu Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) .

Tatu-Hoja Za Kuthibitisha Kupewa Ukhalifa Al Imam ‘Ali Ibn Abi Talib (A.S.)

Tumekwisha tanguliza hoja za Uimamu wa Ahlul Bayt(a.s) na kwamba Maimamu wao kumi na mbili ndiyo Makhalifa wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Na katika yafuatayo tunabainisha Hadith zinazoonyesha Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kumfanya Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) kuwa Khalifa katika ‘Ummah baada yake, na Imam wa kwanza (katika Maimamu kumi na mbili). Hadith hizi ni Mutawattir katika pande mbili isipokuwa Ikhtilaf baina yao imepatikana katika ushahidi wake, Hadith zilizo muhimu zaidi kuhusu hili ni ile inayojulikana kama hotuba ya Ghadiir, tunaitaja kwa muhtasari.

Katika Sahih Tirmidhi katika sanad yake kutoka kwa Zaidi bin Arqam kwamba Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:” (yeyote) ambaye Mimi ni kiongozi wake, basi ‘Ali (pia) ni Kiongozi wake.”[28] .

Na katika Sunan Ibn-Maajah kwa isnad yake kutoka kwa Al-baraa’ bin ‘Aazib amesema: “Tulirejea pamoja na Mtume wa Allah(s.a.w.w) kutoka kwenye Hijja ambayo alihiji akateremka katika baadhi ya njia akaamuru Sala ya Jama’a, basi akashika mkono wa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) akasema: “Je, mimi si bora zaidi kwa waumini kuliko nafsi zao?” Wakasema: “Ndiyo!! Wewe ni bora”, Akasema: “Je, mimi si bora zaidi kuliko kila mumini kwa nafsi yake?” Wakasema: “Ndiyo”, Akasema: “Basi huyu ni kiongozi wa (yule) ambaye mimi ni kiongozi wake; Ewe Allah, mpende atakayemfanya kuwa kiongozi, Ewe Allah mfanye adui atakaye mfanyia uadui.”[29] .

Na katika Musnad Ahmad bin Hambal kwa isnad yake kutoka kwa Al-Barra’ bin Aazib amesema “ Tulikuwa pamoja na Mtume kutoka kwa Al-Barra’ bin Aazib amesema “Tulikuwa pamoja na Mtume wa Allah(s.a.w.w) katika safari tukateremka Ghadir Khum, tukalinganiwa Sala ya Jama’a, pakasafishwa kwa ajili ya Mtume wa Allah(s.a.w.w) chini ya miti miwili basi akasali Adhuhuri na akamshika Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) mkono akasema: “Je, si mnajua kuwa mimi ni bora zaidi kwa waumini kuliko nafsi zao?” Wakasema: “Ndiyo.” Akasema: “Je, si mnajua kuwa mimi ni bora zaidi kwa kila Muumin kuliko nafsi yake?” Wakasema: “Ndiyo.” Basi akashika mkono wa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) na akasema: “Ambaye nilikuwa kiongozi wake basi ‘Ali ni kiongozi wake! Ee Allah, mpende atakayempenda na mfanyie uadui atakayemfanyia uadui .”

Baada ya hapo ‘Umar bin Al-Khattab akasema: “Pongezi ewe mtoto wa Abu Talib, umekuwa kiongozi wa kila Muumin mwanamume na mwanamke.”[30]

Hadith hii imekuwa ni Mashuhuri kwa jina la Al-Ghadir kwa kutokea katika sehemu ya Ghadir al-Khum, nayo ni miongoni mwa dalili za Shariah zenye nguvu na iliyo wazi zaidi juu ya Ukhalifa wa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) na Uimamu wake baada ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w).

Na Hadith hii inazingatiwa ni katika daraja la juu la usahihi na yenye nguvu kwa sababu ni Mutawatir kwa Waislamu wote Sunni na Shi’a.

Baadhi katika wale ambao hawakuweza kuutilia shaka usahihi wa sanad ya Hadith hii wamejaribu kutilia shaka ushahidi wake juu ya Uimamu na Ukhalifa kwa kuchukulia kuwa neno mawla: lina maana ya Urafiki au Mpenzi na sio kiongozi, lakini neno Maula kama lilivyo katika Hadith ifuatayo kwa mfano limekuja kwa maana ya kiongozi au M-bora zaidi kwa uongozi au uwakala.

Kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema: “Hakuna Muumini (yeyote) isipokuwa mimi ni bora kwake zaidi kuliko watu (wote) katika dunia na akhera ”.

Mkipenda someni: “Annabiy awla bil-mu’minina min anfusihim, Fa ayyumaa Muumin taraka maalan falyarithuhu as-habuhu man kanuu, fa in taraka dainan au dhiyaa’n falyaatini wa anaa mawlaahu.”[31]

Tukiangalia mazingira ya Hadith ya Ghadir, wakati wake na sehemu ambayo imeizunguka na vielelezo vingine, vyote hivyo vinaonyesha kweli kwamba makusudio hayakuwa isipokuwa Uimamu na utawala ambao una maana ya uongozi kwa maana zake zote na kati ya vielelezo hivyo ni: -

1. Hakika Ayatu-t-Tablighi “(Ewe Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) fikisha uliyo teremshiwa kutoka kwa Mola wako na kama hutofikisha basi utakuwa hujafikisha Ujumbe wake, na Allah (s.w.t.) atakulinda na watu),”[32] ambayo ilishuka kabla ya tukio la Ghadiri kwa tamko lake kali na vielelezo vilivyopo, inaonyesha kuwa mazungumzo hayakuwa ni juu ya urafiki wa kawaida, kwa sababu haya hayawajibishi umuhimu wote huo na mkazo, kwani Allah (s.w.t.) amefanya jambo la kufikisha kuwa ni lenye kutegemea kuthibiti kwa Ukhalifa baada yake kwa sababu ni kwa Ukhalifa tu na wala sio jambo lingine Allah (s.w.t.) na Mtume wake watausalimisha ‘Ummah huu na dini yao kwa wale waliorithi elimu ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) baada kufariki kwake.

Kama ilivyo Ayah maalumu kwa kukamilisha dini: (“Leo nimekukamilishieni dini yenu na nimekutimizieni neema zangu na nimekuridhieni Uislamu kuwa ni dini yenu”)[33] ambayo iliteremka baada tu ya kumalizika hotuba ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , ambapo alimtawaza Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) kuwa Khalifa na Imam kwa ‘Ummah. Inaonyesha kwa dalili ya wazi kwamba maudhui yalikuwa ni muhimu mno kama vile maudhui ya uongozi na Ukhalifa baada ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , na kwamba alikuwa katika mnasaba wa kumteua Imam baada yake. Huyu atakayekuwa Imam baada yake si mwingine ila ni Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) , na makusudio ya Hadith sio (“Ambaye nilikuwa kipenzi chake na msaidizi wake basi Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) ni kipenzi chake na msaidizi wake).

2. Njia ambayo Hadith imeelezwa kwa hali zake zote, jangwa lenye joto kali, ambapo hotuba ilitolewa hapo na kuchukua muafaka wa watu katika hali hiyo na sehemu hiyo yote, haya yanaonyesha usahihi wa mwelekeo tulio uchukua wa kumtawalisha Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) katika nafasi ya Uimamu na wala sio jambo lingine, kwa sababu ni jambo muhimu na ni wajibu lijulikane kabla ya kufika mauti ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , ambayo yeye mwenyewe hakuwa anajua itakuwa ni lini kwani yanaweza yakamfika kabla ya kufika kwake Madina. Hivyo ni wajibu wake kutangaza jina la kiongozi baada yake wakati huu, kwani kutangaza jina la kiongozi kuna athari za kivitendo kwa Waislamu baada yake na kwa dunia yao.

Ama kujua kwao kwamba Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) ni kipenzi cha waumini - kwa mfano - ni jambo ambalo halina athari katika maisha ya watu na kutojua kwao hakubadilishi kitu katika maisha yao na taratibu zao.

3. Na katika Sahih Tirmidhi kwa isnad yake kutoka kwa Imran bin Huswayn amesema: “Mtume wa Allah(s.a.w.w) alituma jeshi na akampa uongozi wake Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) wakaenda katika sariya (kikosi) akampata msichana akamchukua, wakamkataza, na wanne katika Masahaba wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) wakakubaliana wakasema tutakapokutana na Mtume wa Allah(s.a.w.w) tutamweleza aliyo yafanya Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) , basi Mtume wa Allah(s.a.w.w) alikuja na ghadhabu inaonekana katika uso wake na akasema: “Mnataka nini kwa ‘Ali? Hakika ‘Ali ametokana na mimi na mimi nimetokana na yeye, naye ni kiongozi wa kila muumini baada yangu.”[34] .

Na kauli ya Allah (s.w.t.):

إِنَّمَا وَلِيُّكُمُ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُمْ رَاكِعُونَ ﴿٥٥﴾

Hakika kiongozi wenu ni Allah, Mtume wake na walioamini ambao wanasimamisha sala na wanatoa zaka hali wakirukuu”. (Al Maidah 5:55)

Imeshuka kwa ajili ya Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) , kama inavyofafanuliwa katika tafsiri za wafasiri wengi[35] alipotoa sadaka pete yake kwa maskini aliyemjia akiwa katika sala hali akirukuu.

Na katika Hadith zingine ambazo zinaashiria Ukhalifa wa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) ni Hadith ya Manzilah (Cheo), kutoka kwa Mus’ab bin Sa’ad kutoka kwa baba yake: ‘Hakika Mtume wa Allah(s.a.w.w) alitoka kwenda Tabuk, na akamwacha ‘Ali(a.s) .

Ambaye alisema: “Unaniacha pamoja na watoto na wanawake?” Mtume akasema: “Je, huridhii kuwa cheo chako kwangu ni kama cheo cha Harun kwa Musa, isipokuwa hakuna Nabii baada yangu?”[36]

Hadith hii inaonyesha kuwa vyeo vyote alivyokuwa navyo Harun kwa Bani Israil katika upande wa Mtume Musa(a.s) kwa kuondoa Unabii. - Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) alikuwa navyo, kwa sababu Hadith haina kizuizi chochote au sharti, na kwa hivyo yanafahamika kutoka ndani ya hadith hiyo yafuatayo:-

1. Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) alikuwa ni waziri wa Mtume na msaidizi wake maalumu na mshirika wake katika uongozi wa ‘Ummah kwa sababu vielelezo vimethibitsha vyeo hivyo kwa Haruna. Qur’an Tukufu inasema:

وَاجْعَل لِّي وَزِيرًا مِّنْ أَهْلِي ﴿٢٩﴾ هَارُونَ أَخِي ﴿٣٠﴾ اشْدُدْ بِهِ أَزْرِي ﴿٣١﴾ وَأَشْرِكْهُ فِي أَمْرِي ﴿٣٢﴾ كَيْ نُسَبِّحَكَ كَثِيرًا ﴿٣٣﴾ وَنَذْكُرَكَ كَثِيرًا ﴿٣٤﴾ إِنَّكَ كُنتَ بِنَا بَصِيرًا ﴿٣٥﴾ قَالَ قَدْ أُوتِيتَ سُؤْلَكَ يَا مُوسَىٰ ﴿٣٦﴾

Na nijaalie waziri katika jamaa zangu, Ndugu yangu Haruna (mfanye awe ndiye waziri wangu), nitie nguvu kwa (ndugu yangu) huyu, na umshirikishe katika kazi yangu (hii)…” (Allah) Akasema: “Hakika umepewa maombi yako (yote haya uliyoyataka)., ewe Musa! (Twaha 20:29-36).

2. Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) , alikuwa ni bora zaidi katika ‘Ummah baada ya Mtume kama alivyokuwa Harun katika Bani Israil.

Na yanayotilia nguvu kustahiki Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) katika cheo hiki kitukufu na kuwa kwake Khalifa wa ‘Ummah baada ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ni kwamba yeye alikuwa ni mjuzi kati ya Masahaba wote. Katika kutambua hili walio mashuhuri kati yao ni hawa wafuatao:-

Kutoka kwa Said Bin Jubeir kutoka kwa Ibn ‘Abbas: “Amesema ‘Umar:’ Msomaji wetu mzuri ni Ubay na hakimu wetu ni Ali’.”[37] Hiyo ni kwa sababu mwenye kuhukumu zaidi ndiyo mjuzi zaidi wa hukumu na kanuni, na hilo liko wazi,na inatosha kuthibitisha ujuzi wake mkubwa kule kuwa kwake mlango wa mji wa elimu ya Mtume wa Allah(s.a.w.w) , na hekima yake, kama ilivyo katika Sahih Tirmidhi kwa isnad yake kutoka kwa Ibn ‘Abbas amesema: ‘Amesema Mtume(s.a.w.w) : “Mimi ni mji wa hekima na ‘Ali ni mlango wake.”[38]

Na katika Mustadrak As-Sahihain kwa sanadi yake kutoka kwa Ibn ‘Abbas (r.a) amesema: “Mimi ni mji wa elimu na ‘Ali ni mlango wake, basi anayetaka elimu apitie mlangoni.”[39] Al-Hakim amesema isnad ya Hadith hii ni Sahih. Na katika Mustadrak As-Sahihain vilevile Mtume wa Allah(s.a.w.w) alimwambia ‘Ali: “Wewe utaubainishia ‘Ummah wangu yale waliyo hitilafiana baada yangu.”[40]

Tujaalie kwamba Nabii wa Uislamu hakutaka yeyote kushika nafasi ya Ukhalifa baada yake; na tujaalie kwamba uchaguzi wa ukhalifa ulikuwa ni jukumu la ‘Ummah. Je, inajuzu katika uchaguzi kumwacha mjuzi zaidi na mchamungu zaidi na mwenye sifa nyingi zaidi katika pande zote kama tulivyobainisha? Kwani Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) alikuwa ni mjuzi zaidi kati ya Masahaba wote na walikuwa wakirejea kwake wanapopatwa na mushkeli mgumu wa kidini.

Ama kuhusu juhudi yake na uchaMungu wake, amekwisha julikana kwamba ni Imam wa wenye juhudi. Na kuhusu ushujaa wake na ujasiri wake wa kipekee, alikuwa ni wa kwanza kujitolea muhanga katika Uislamu na alikuwa na nafasi muhimu katika kila tukio, katika vita vya Badr ameua kwa upanga wake Dhul-fiqar mashujaa thelathini katika mashujaa wa Kiquraish, na katika Uhud na Hunain alisimama msimamo wa kihistoria wa kufa na kupona akimtetea Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) baada ya wengi katika Masahaba kukimbia. Na katika Khandaq alijitokeza kupambana na shujaa mkubwa wa washirikina ‘Amr bin ‘Abdiwud Al-’Amiri, wakati ambapo hakujaribu yeyote kujitokeza miongoni mwa Masahaba waliobaki.

Na katika Khaibar Allah (s.w.t) kupitia kwake alifungua mlango wa ngome baada ya kuwashinda, na lilishindwa kufungua kundi kubwa la Masahaba wakiwa pamoja. Vilevile ametafautiana na Masahaba wengine kwa kutomgusa ukafiri hata chembe, alipata malezi yake ya kipekee chini ya mwalimu wa kwanza wa binadamu, Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ambapo hakumwacha hata punde moja katika uhai wake wote mpaka alipoaga dunia akiwa mikononi mwake.

Katika uhai wake wote alikuwa anachukua elimu na hekima kutoka kwa Mtume wa Allah(s.a.w.w) , hivyo akastahiki kwa jitihada yake kuwa ni mlango wa mji wa elimu ya Mtume wa Allah(s.a.w.w) , na mlango wa hekima yake na ndugu yake.

Na katika Sahih Tirmidhi kwa isnad yake kutoka kwa ‘Umar amesema: ‘Mtume wa Allah(s.a.w.w) alifanya udugu baina ya Masahaba wake, basi alikuja Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) akilia, akasema: ‘Ewe Mtume wa Allah(s.a.w.w) umefanya udugu baina ya Masahaba wako na hukufanya udugu baina yangu na yeyote, Mtume wa Allah(s.a.w.w) akasema: ‘Wewe ni ndugu yangu duniani na akhera[41]

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimwambia Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) : ‘Wewe umetokana na mimi na mimi nimetokana na wewe’[42] Pia ametofautiana na Masahaba wengine kwa kuwa ana fadhail nyingi zaidi. Imekuja katika Mustadrak As-Sahihain kutoka kwa Ahmad bin Hanbal, amepokea kwamba: “Haikupokewa kwa yeyote katika Masahaba wa Mtume wa Allah(s.a.w.w) katika fadhail kama ilivyopokewa kwa ‘Ali”[43] Na katika Kanzul-’Ummal: Amesema Mtume wa Allah(s.a.w.w) ‘Hakika Allah ameniamrisha kumwozesha Fatimah kwa ‘Ali’[44]

Na hiyo ni baada ya kukataa kumwozesha kwa baadhi ya Masahaba waliokwenda kumposa kwa kujaribu kupata utukufu huu mkubwa kwa kuoa mtoto wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ,bibi wa wanawake waumini wa watu wa peponi, ambaye Allah (s.w.t) anaghadhibika kwa ghadhabu yake; Na ni mkweli aliyesema: ‘kama ‘Ali asingeumbwa Bi.Fatimah asingepata mtu anayemfaa’.[45]

Na baada ya hayo yote kama tukijaalia kuwa uchaguzi wa ukhalifa uliachiwa watu wenyewe basi kwa hakika Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) alikuwa ni bora wa waliokuwepo na anayefaa zaidi kwa ukhalifa.

Kukhalifu Kwa Jamhuri Ya Waislamu Nasi (Pokezi) Za Uimamu

Baada ya kueleza hoja na dalili zilizotangulia juu ya Nabii kumteua Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) kwa amri ya Allah (s.w.t), kuwa Imam wa Waislamu baada yake kwa kuanzia na Maimamu wa Ahlul-Bayt(a.s) kumi na mbili kwa ujumla, baadhi ya watu wanaweza kuuliza kwa kusema: Ikiwa ni kweli nasi (pokezi) zote hizo ni za Uimamu wa Ahlul Bayt(a.s) basi kwa nini na vipi ukhalifa umeenda kwa wengine?

Kwa kujibu swali hili tutaeleza baadhi ya matukio muhimu ya kihistoria ambayo yalikuwa na athari kubwa katika kubadilisha mwelekeo wa historia ya ki-Islamu tukianzia na ijtihad ya makhalifa wa mwanzo katika ukhalifa na mengineyo mbele ya Hadith zilizo thabiti za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na kumalizia kwa Bani Umayyah kuuteka ukhalifa kwa nguvu na kutishia kwa upanga, kwa yanayopatikana humo miongoni mwa neema za kidunia na ukubwa, ambao ndiyo ndoto waliyokuwa wakiiota mara nyingi. Miongoni mwa matukio hayo ni: -

1. Baadhi ya Masahaba kumzuia Mtume wa Allah(s.a.w.w) kuandika wosia.

2. Baadhi ya Masahaba kukhalifu jeshi la Usamah na kukosoa kupewa kwake uongozi.

3. Matukio ya Saqifah na Bai’a ya Abubakr.

4. Ukhalifa wa ‘Umar na Bai’a yake.

5. Shura na Bai’a ya Uthman.

6. Tukio la Jamal na kutoka ‘Aishah.

7. Tukio la Siffin na uasi wa Mu’awiyah bin Abi Sufian.

8. Kufa Shahidi Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) .

9. Kufa shahidi kwa Al Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) .

10 Mapinduzi ya Karbala na kuawa shahidi kwa Al Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) .

Na katika yafuatayo tutayaelezea matukio haya kila moja kwa kirefu:-

Kwanza- Baadhi Ya Masahaba Kumkataza Mtume Wa Allah(s.a.w.w) Kuandika Wosia.

Mtume alipotaka kuandika wosia mbele ya Masahaba wakubwa akiwa katika hali ya mwisho ya uhai wake, na kuzidiwa na maradhi, baadhi yao walimtuhumu kwa neno ambalo lilizua zogo kubwa, na Mtume akakasirika kwa athari yake, hivyo akawafukuza katika majilisi yake na akaacha kuandika wosia. Tukio hili lilitokea siku ya Alhamisi, kabla ya kufa kwake kwa siku chache, na tukio hili limejulikana kama; ‘Huzuni ya siku ya Al-hamisi’. Kama yanavyo dhihirika hayo katika Hadith zifuatazo:-

Amesema Ibn ‘Abbas: “Siku ya Al-khamisi, ni ipi siku ya Al-khamisi, Mtume wa Allah(s.a.w.w) alizidiwa na maumivu akasema: ‘Njooni nikuandikieni wosia, hamtapotea kamwe baada yangu’, wakazozana, na haifai kuzozona mbele ya Nabii, wakasema: “Ana nini? Anaweweseka?” Wakataka kumwuliza, basi wakampinga: Akasema: “Niacheni kwani ambayo niko nayo ni bora kuliko hayo mnayoniitia”[46]

Ibn ‘Abbas amesema: ‘Alipozidiwa Mtume wa Allah(s.a.w.w) na katika nyumba (yake) kuna wanaume, Nabii akasema: “Njooni nikuandikieni wosia hamtapotea kamwe baada yake”; Baadhi yao wakasema: “Hakika Mtume wa Allah(s.a.w.w) amezidiwa na maumivu, na mnayo Qur’an, na kinatutosha Kitabu cha Allah (s.w.t). Walio kuwepo walikhitalafiana na kuzozana, baadhi yao wakasema karibieni akuandikieni, na baadhi yao wakasema yasiokuwa hayo. Walipozidi kukhitalifiana, Mtume wa Allah(s.a.w.w) Akasema: “Ondokeni.” ‘Ubaidullah akasema: Ibn ‘Abbas alikuwa akisema, “Hakika huzuni iliyo kubwa kabisa ni ile ambayo ilitokea baina ya Mtume wa Allah(s.a.w.w) na kuwaandikia wosia huo kwa kule kuhitalifiana kwao na kupaza kwao sauti zao’. [47]

Kutoka kwa Ibn ‘Abbas Amesema: ‘Alipozidiwa Mtume wa Allah(s.a.w.w) na katika nyumba kuna wanaume kati yao ni ‘Umar bin Al-Khattab, Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akasema njooni nikuandikieni maandiko hamtapotea baada yake,” ‘Umar akasema, “Hakika Nabii amezidiwa na mnayo Qur’an.

Kinatutosha Kitabu cha Allah (s.w.t); walio kuwepo wakakhitalifiana na kuzozana kati yao, kuna wanao sema sogeeni Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) awaandikie maandiko hamtapotea baada yake na kati yao kuna wanaosema aliyo sema ‘Umar, walipozidi kuzozana na kukhitalafiana mbele ya Nabii, Mtume wa Allah(s.a.w.w) akasema: “Ondokeeni.”

‘Ubaidullah akasema: Na Ibn ‘Abbas alikuwa akisema: “Hakika huzuni kubwa kabisa ni ile iliyotokea baina ya Mtume wa Allah(s.a.w.w) na baina ya kuwaandikia maandiko hayo kutokana na Ikhtilaf yao na mzozo wao.”[48] .

Na katika Sahih Muslim majibu yao yalikuwa: ‘Wakasema: “Hakika Mtume wa Allah(s.a.w.w) anaweweseka.”[49] Ibara hii ya mwisho ambayo inamtuhumu Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kwa sifa ambayo inagusa Uma’asum wake na utukufu wake, inafahamika wazi kwamba wasemaji wake wanataka kuwazuia Waislamu wasiandikiwe mandiko na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na kutaja jina la khalifa wake wazi wazi, isije ikazuia wenye tamaa kufanya mikakati na kubadilisha mwelekeo wa ukhalifa wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ili upitie wanakotaka wao. Abubakr Ahmad bin Abdul-azizi Al-Jauhari amejaribu katika Kitabu chake As-Saqifah kuficha jambo hili akasema: “Basi ‘Umar akasema neno ambalo maana yake ni kwamba maumivu yamemzidia Mtume wa Allah(s.a.w.w) kisha akasema tuna Qur’an Kitabu cha Allah (s.w.t)’[50] .

Ni wazi neno “Yahjur”, (anaweweseka) halina maana ya “Yatawajaa” (anaumwa) ambalo ametaka huyu aliyechelewa kulibadilisha, ili kuficha ubaya wa neno la kwanza kwa Nabii.

Na kila anayefikiria katika Hadith hizi anapata yakini kuwa wa kwanza kusema: “Yahjuru Rasulu Ilahi” siku hiyo ni ‘Umar bin Al-Khattab kisha likasambaa kwa waliokuwepo ambao walikuwa na rai kama yake, na kwa sababu hiyo Mtume wa Allah(s.a.w.w) akakasirika na kuwafukuza kwa kuwaambia: “Niondokeeni”.

Na ukifikiria katika kauli ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : ‘Njooni nikuandikieni maandiko hamtapotea kamwe baada yake,’ na kauli yake katika Hadith ya Thaqalain- ‘Hakika mimi nimekuachieni vitu viwili vilivyo vizito miongoni mwenu ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea,- Kitabu cha Allah (s.w.t) na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu,[51] unajua kuwa lengo la Hadith mbili hizi ni moja, ambapo Mtume katika maradhi yake alitaka kuwaandikia ufafanuzi wa aliyoyafanya kuwa ni wajibu kwao katika Hadith ya Thaqalain.

Lakini akaacha kuandika baada ya neno lao hilo ambalo walimshtusha kwalo na ambalo lilimlazimisha kuacha ili baadhi yao wasifungue mlango katika kumtuhumu Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) – ambapo haikubakia athari ya kuandika maandiko isipokuwa fitina na Ikhtilaf baada yake, ya kwamba je, aliweweseka katika aliyoyaandika? Allah (s.w.t) atuepushe mbali - au hakuweweseka, kama walivyo khitalifiana katika hilo mbele yake, kama ilivyodhihirika katika Hadith zilizotangulia, ambapo wao walitosheka kwa waliyo nayo miongoni mwa Qur’an na wakajawazisha wenyewe kuacha maneno ya Nabii naye yuko katika hali ya maradhi, kana kwamba wamesahau aliyoyasema Allah (s.w.t) juu ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) .

وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٣﴾ إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ ﴿٤﴾ عَلَّمَهُ شَدِيدُ الْقُوَىٰ ﴿٥﴾

Hasemi kwa matamanio yake isipokuwa wahyi unaofunuliwa, amemfundisha Mwenye nguvu sana , (An-Najm 53:3-5).

وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿٧ ﴾

Aliyo kuleteeni Mtume yachukueni na aliyokukatazeni yaacheni ” (Al-Hashr 59:7).

إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ { 19 } إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ ﴿١٩﴾ ذِي قُوَّةٍ عِندَ ذِي الْعَرْشِ مَكِينٍ ﴿٢٠﴾ مُّطَاعٍ ثَمَّ أَمِينٍ ﴿٢١﴾ وَمَا صَاحِبُكُم بِمَجْنُونٍ ﴿٢٢﴾.

Hakika hiyo ni kauli ya Mjumbe Mtukufu mwenye nguvu, mwenye cheo cha heshima kwa Allah (s.w.t.), anayetiiwa huko (mbinguni na malaika wenzake). Kisha mwaminifu na Mtume wenu sio kichaa ” (At-Tak’wiyr; 81:19:22)

Ibn ‘Abbas ameueleza msimamo huo kwa maelezo mazuri aliposema: “Hakika ni huzuni kubwa kabisa iliyo tokea baina ya Mtume wa Allah(s.a.w.w) na baina ya kuandika usia kwa sababu ya khitilafu yao na sauti zao,” yote hayo yalitokea mbele ya Mtume, sasa ni mangapi yatatokea kwa kuondoka kwake na baada ya kufa kwake?

Pili- Baadhi Ya Masahaba Kukhalifu Jeshi La Usamah Na Kukosoa Kupewa Kwake Uongozi

Ni maarufu kwa Waislamu wote kwamba Mtume aliandaa sariya (kikosi) kwenda kupigana Roma na akampa uongozi Usamah bin Zaid, naye ni kijana wa miaka kumi na saba, na hiyo ni sariya ya mwisho katika zama za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , na hakubaki yeyote katika wakuu wa Muharjirin na Ansar, kama vile Abubakr, ‘Umar, Abu ‘Ubaidah, Sa’ad na mfano wao isipokuwa aliwaingiza katika jeshi”[52] Na kuna ijma’ juu ya uhakika huu, na kwa watu wa sira na historia ni jambo la kawaida.

Akamwamuru ‘Usamah kuondoka lakini waliona uzito kwa hilo na baadhi yao wakatuhumu kufanywa kwake kiongozi mpaka Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akakasirika sana kwa kutuhumu kwao, akatoka akiwa amefunga kitambaa kichwani (kwa maumivu), na hiyo ilikuwa ni wakati wa maradhi yake, na kabla ya kufariki kwake kwa muda wa siku mbili, akapanda mimbar na akasema; kama alivyopokea Bukhari kwa isnad yake kutoka kwa ‘Umar.

Kutoka kwa Ibn ‘Umar amesema: “Mtume wa Allah(s.a.w.w) alimwamuru ‘Usamah kuongoza watu basi wakatuhumu katika uongozi wake. Mtume akasema: ‘Kama mtatuhumu katika uongozi wake, basi mlikwisha tuhumu katika uongozi baba yake, naapa Wallahi hakika alikuwa ni katika watu wanaopendeza sana kwangu, na hakika huyu ni katika watu ninaowapenda sana baada yake”[53] Kisha akawahimiza kuondoka naye na kufanya haraka, isipokuwa walizembea kwa mara nyingine na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alifariki kabla hawajaanza kuondoka. Katika tukio hili tunajifunza yafuatayo:-

1. Ijtihadi ya baadhi ya Masahaba katika kauli ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ambapo walipinga uteuzi wa Usamah kuwa kiongozi wao kutokana na umri wake mdogo, pamoja na kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alikabidhi bendera yake kwake. Tukilifahamu hili basi haitakuwa vigumu kwetu kufahamu namna na sababu katika ijtihadi yao mbele ya kauli ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) katika mambo makubwa zaidi, kama vile kumteua Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib (a.s) kuwa Khalifa na Uimamu wake.

2. Hakika Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kumfanya Usamah kuwa kiongozi wao naye ni kijana wa miaka kumi na saba tu, amelifanya hilo ili iwe funzo la kivitendo katika kukubali uongozi wa ambaye ni mdogo kuliko wao kiumri na hivyo Mtume alidhihirisha ghadhabu yake walipo tuhumu huo uongozi wa Usamah.

3. Mtume alipompa Usamah bendera alikuwa anajua kwamba wakati wa kwenda kwa Mola wake umeshakaribia, na bila shaka alikuwa anafikiria yale yatakayotokea baada yake katika kugombania ukhalifa. Hekima yake kubwa ya kuwaweka wakuu wa Muhajirin na Ansar katika sariya hiyo ambayo aliiamuru kuondoka kabla ya kufa kwa siku chache, ni ili pasiwe na nafasi ya kugombania uongozi, tukiachilia mbali kufanyika kwa ijtihadi.

Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) alikuwa anaandamana na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) muda wote huo, na wala hakuachana naye hata mara moja wakati wa maradhi yake, na baada ya kufariki kwake alishughulika na kumwosha, na Muhajirin na Ansar wakaenda kugombania uongozi katika Saqifah ya Bani Sa’ada baada ya kuona uzito wa kwenda katika jeshi la Usamah ambalo wao walikuwa ni askari wake, na hivyo ndivyo ilivyokuwa ijtihadi yao kwa kuogopa yatakayotokea baada ya kufariki Mtume wa Allah(s.a.w.w) katika hali ya kutokuwepo kwao.

Tatu -Matukio Ya Saqifah Na Bay’ia Ya Abubakr

Katika wakati ambao Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) pamoja na aliokuwa nao wanashughulika na mazishi ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , ‘Umar alikuwa anatangaza kupinga kwake kufariki kwa Mtume wa Allah(s.a.w.w) na anatishia kumuua kila anayesema hilo, na wala hakuwa anaamini kufariki kwa Mtume mpaka aliporejea Abubakr kutoka sehemu iliyo nje ya Madina inayoitwa Al-Sunh, kama ilivyo pokewa kutoka kwa ‘Aisha (r.a):

“Hakika Mtume wa Allah(s.a.w.w) alifariki na Abubakr yuko (sehemu iitwayo) Sun’hi.” Isma’il akasema: ‘Akimaanisha (Aisha sehemu iitwayo) Aliyah.’

Basi ‘Umar alisimama na akasema: “Naapa Wallahi kuwa Mtume wa Allah(s.a.w.w) hakufariki. Wallahi sikuwa nawaza moyoni mwangu isipokuwa hilo na Allah (s.w.t) atamfufua, na atakata mikono na miguu ya wanaume.”

Akaja Abubakr akamfunua Mtume wa Allah(s.a.w.w) akambusu na akasema: “Kwa Baba yangu na mama yangu, ulikuwa mwema wakati ulipokuwa hai na ukiwa maiti, naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake, Allah (s.w.t) hatakufisha mara mbili, kisha akatoka na akasema: ‘Ewe mwenye kuapa tulizana.’[54] .

Lakini Ansar walikwisha jikusanya katika Saqifah ya Bani Sa’ada na wakampendekeza Sa’ad bin ‘Ubadah ili awe khalifa wa Mtume wa Allah(s.a.w.w) na wakuu wa Muhajirin (Abubakr, ‘Umar na Abu ‘Ubaidah) walipojua hilo waliwaendea haraka, na wakatangaza kuwa wao wana haki zaidi katika jambo hilo.

Pakatokea mjadala baina ya Muhajirin na Ansar, mjadala na mzozo ukazidi, akasimama kiongozi wa Ansar Sa’ad bin ‘Ubadah kisha akasema: ‘Amma baad, sisi ni Ansar wa Allah (s.w.t) na Jeshi la Kiislamu na nyinyi Muhajirin ni kundi, na lilikuja kundi katika kaumu yenu, hivyo wakawa wanataka kutung’oa katika asili yetu na kutupakata katika jambo (hili)[55] .

Abubakr akasimama na akatoa hutoba, akataja humo fadhail za Muhajirin na akatoa hoja ya Uquraish wao katika kustahiki kwao ukhalifa. Abubakr, ‘Umar Al-Khattab na Abu ‘Ubaidah bin Al-Jarah wakawaendea. ‘Umar akawa anazungumza, Abubakr akamnyamazisha[56] Abubakr akasema: ‘Hapana, lakini sisi ni viongozi na nyinyi ni mawaziri, wao (Maquraish) ni Waarabu wa nyumba ya kati na ni ukoo bora.[57] Nimewaridhia mmoja kati ya hawa wanaume wawili[58] mpeni bay’ia ‘Umar Al-Khattab au Abu ‘Ubaidah bin Al-Jarah.’[59]

Mmoja wa wakuu wa Ansar akajibu, naye ni Habab bin Al-Mundhar, akasema: ‘Hapana hatufanyi kwetu kuwe na kiongozi na kwenu kuwe na kiongozi.’[60]

Na jibu la Ansar lilikuwa katika Hadith nyingine: “akasema msemaji wa Ansar: ‘Mimi ni asili yake isiyo tingishika na tawi lake lenye nguvu, kwetu kuwe na kiongozi na kwenu kuwe na kiongozi enyi Maquraish.’ Fujo ikazidi na kelele zikawa nyingi mpaka nikaudhika kutokana na Ikhtilaf’[61] .

Hali ilipokuwa mbaya kiasi hiki, ikaja duru ya ‘Umar Al-Khatib akasema: ‘Haiwezekani kuingia panga mbili katika ala moja, Wallahi Waarabu hawaridhii kuwafanya nyinyi viongozi na Nabii wake hajatoka kwenu na sisi tuna hoja juu ya hilo kwa anayekataa.’ Habab bin Al-Mudhir akamjibu kwa kusema:’

Enyi Ansar shikamaneni na jambo lenu na wala msisikie maneno ya huyu na wenzake, kwani ninyi mna haki zaidi na jambo hili kuliko wao’.

Lakini safari hii Ansar waligawanyika, ‘Usaid bin Hudhair kiongozi wa Aus ambaye alikuwa mpinzani wa Sa’ad bin ‘‘Ubadah, kiongozi wa Khazraji akatangaza kuwaunga kwake mkono Muhajirin na akaahidi kuwapa bay’ia. Basi ‘Umar alisimama akamwambia Abubakr: ‘Nyoosha mkono nikupe bay’ia’. ‘Umar akamba’yi na baadhi ya Muhajirin’.

Ansar, kama alivyopokea Bukhari kwa isnad yake kutoka kwa ‘Aisha kwamba ‘Umar alichukua bay’ia kwa Abubakr kwa kuwatishia na kuwaogopesha.

‘Aisha amesema: ‘basi haikuwa hotuba yao miongoni mwa hutoba isipokuwa Allah (s.w.t.) aliwanufaisha kwayo, kwani ‘Umar aliwatisha watu na kulikuwa na unafiki kwao, basi Allah (s.w.t.) akawajibu kwa hilo’[62] .

‘Umar alimwambia kiongozi wa Ansar Sa’ad bin ‘Ubadah ambaye alikataa kubay’i: “Tulimrukia Sa’ad bin ‘Ubadah”, basi akasema msemaji miongoni mwao:’ Mnamuua Sa’ad bin ‘Ubaadah’ ‘Umar akasema:’Allah (s.w.t) amuue’[63] .

Mpaka hapa tunafunga pazia la maigizo ya matukio ya Saqifah ambayo yalimalizika kwa kumbay’i Abubakr baada ya ugomvi ulio shuhudiwa baina ya Muhajirin na Ansar juu ya ukhalifa, na ‘Umar Al-Khattab amekiri kwamba bay’a ya Abubakr ilikuwa ya ghafla, lakini - kwa rai yake - Allah (s.w.t) ameepusha shari. “Basi asidanganyike mtu kusema kwamba bay’ia ya Abubakr ilikuwa ghafla na ikatimia, ndiyo ilikuwa hivyo kweli, lakini Allah (s.w.t) ameepusha shari yake.[64]

Na wote wanajua kwamba Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) na wengine katika Bani Hashim na wengineo katika Masahaba mfano Zuber, Twalha, ‘Ammar, Salman, Miqdad, Abu Dhar, Khuzaima dhi-Shahadatain, Khalid bin Sa’ad, ‘Ubay bin Ka’ab, Abu Ayyub Ansari na wengineo - hawakushuhudia bay’ia hiyo, wala hawakuingia Saqifah siku hiyo kwa sababu wao walikuwa wanashughulika na tukio kubwa la kifo cha Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , na kufanya wajibu wa kuandaa mazishi yake na kuzika mwili wake mtukufu kwenye kaburi lake.

Watu wa Saqifah walimpa Abubakr bay’ia, hivyo hapakuwa na njia kwa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) pamoja na aliokuwa nao isipokuwa kukataa kumbay’i kama yanavyo dhihirika hayo katika maneno ya ‘Umar: “Allah (s.w.t) alipomfisha Nabii wake tulikuwa tuna habari, isipokuwa Ansar walikhalifu na wakakusanyika katika Saqifah ya Bani Sa’adah, na akatukhalifu sisi ‘Ali, Zubeir na waliokuwa pamoja nao”[65] .

Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) hakuona athari ya kujadiliana isipokuwa ni fitina ambayo aliona ni bora kupoteza haki yake kuliko kuipata katika hali hiyo, kwa sababu ya fitina mbaya ambayo iliuzunguka Uislamu kwa kila upande.

Hatari ya wanafiki na wale walio pembezoni mwake miongoni mwa mabedui waliobobea katika unafiki - kama zilivyosema Ayah za Qur’an - na nguvu zao ziliongezeka kwa kuondoka Mtume, ukiongozea hatari ya Musailamah al-Kadh-dhaab, Twaliyhat bin khuwailid mwongo, Sajaah Ad-Dajalah, Warumi, Kisra, Qaisar na wengineo miongoni mwa wanao watakia shari Waislamu. Na hatari nyingine zisizokuwa hizo zilizokuwa zinautishia Uislamu na kubaki kwake, hivyo ilikuwa ni jambo la kawaida kwa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) kutoa muhanga haki yake, lakini bila ya kufuta hoja zake katika ukhalifa.

Alitaka kuhifadhi haki yake katika ukhalifa na kumjadili aliyefanya jitihadi humo kwa njia ambayo haitaleta fitina itakayowapa mwanya maadui wa Uislamu. Alibaki nyumbani kwake na akakataa kumbay’i yeye pamoja na aliokuwa nao kwa muda wa miezi sita, na alipoona kumbay’i ni kuepukana na fitina alituma ujumbe kwa Abubakr[66] . “Njoo na wala asije yeyote pamoja nawe” kwa kuchukia asije akahudhuria ‘Umar.

Na kama angefanya haraka kumbay’i isingetimia hoja yake wala wafuasi wake wasingepata hoja, lakini kwa aliyoyafanya alikusanya baina ya kuhifadhi dini na kuhifadhi haki yake ya Ukhalifa kwa Waislamu; wakati huo hali haikuruhusu kupigana kwa upanga wala kushinda kwa hoja, na ukweli unadhihirika wazi alipojaribu Abu Sufian kumwendea Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) zaidi ya mara moja alimhimiza kushikilia haki yake ya ukhalifa kwa kusema: “Ukitaka, tutakupa farasi na watu wa kupigana nao na nitawanyima wao katika sehemu yao”[67] .

Lakini Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) alikataa aina hii ya msaada mara zote kwa sababu alikuwa anajua kuwa makusudio ya Abu Sufian ni kuchochea cheche ya fitina na kuanzisha vita ambavyo Uislamu hautasimama tena baada ya hapo.

Hasira (Ghadhabu) Ya Bibi Fatimah Az-Zahra(A.S)

Bi Fatimah az-Zahra(a.s) alifariki akiwa na hasira juu ya Abubakr, kwa sababu ya kumkataza mirathi yake kutoka kwa Mtume. “Hakika Bi Fatimah az-Zahra(a.s) binti wa Mtume wa Allah(s.a.w.w) alimtaka Abubakr baada ya kufariki Mtume wa Allah(s.a.w.w) , amgawie mirathi yake katika alioyaacha Mtume wa Allah(s.a.w.w) katika aliyo mpa Allah (s.w.t). Abubakr akamwambia: ‘Hakika Mtume wa Allah(s.a.w.w) amesema: “Haturithiwi, bali tuliyoyaacha ni sadaka”.

Binti wa Mtume wa Allah(s.a.w.w) akakasirika na akamhama Abubakr na hakuacha kufanya hivyo mpaka akafariki, na aliishi miezi sita baada ya kufariki Mtume wa Allah(s.a.w.w) . Alikuwa anamwomba Abubakr fungu lake kati ya aliyo yaacha Mtume wa Allah(s.a.w.w) miongoni mwa mali ya Khaibar, Fadak na sadaka zake za Madina, Abubakr akamkatalia na akasema, si kuwa ni mwenye kuacha kitu alicho kifanya Mtume wa Allah(s.a.w.w) [68] .

Na hasira yake kwa Abubakr ilikuwa kubwa kiasi ilimfanya amuusie Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) kuwa Abubakr asimsalie wala kusindikiza jeneza lake, na Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) alizika mwili wake kwa siri usiku. Bukhari amesema katika Kitabul-Maghazi “Abubakr alikataa kumpa kitu chochote, basi akamkasirikia Abubakr kwa ajili hiyo na akamhama na hakumsemesha mpaka akafariki, na ameishi miezi sita baada ya kufariki Nabii, na alipofariki, mume wake Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) alimsalia na akamzika usiku na hakumruhusu Abubakr kumsalia”[69] .

Ardhi hiyo ya Fadak ni kijiji katika Hijaz walikuwa wakiishi humo wAyahudi, na Mtume(s.a.w.w) alipoiteka Khaibar, Allah (s.w.t) alitia hofu katika nyoyo zao wakafanya suluhu na Mtume kwa kumpa Fadak. Ikawa ni miliki ya Mtume wa Allah(s.a.w.w) kwa sababu ni katika vitu ambavyo havikupatikana kwa vita si kwa wapanda farasi wala kwa wanaokwenda kwa miguu, kisha akampa binti yake Bi.Fatimah az-Zahra (a.s) Tukiongezea yale aliyo miliki Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) katika mali ya khums ya Khaibar na sadaka za Nabii haya yote yalikuwa ni milki ya Mtume wa Allah(s.a.w.w) khasa, na hakuna yeyote mwenye haki isipokuwa yeye.

Bi.Fatimah az-Zahra(a.s) alikuwa - kulingana na rai ya Abubakr - ametaka asiyokuwa na haki nayo, hivyo ni moja kati ya mambo mawili wala hakuna la tatu, ima alikuwa ni jahili hajui hukumu ya mirathi ya Nabii au alikuwa mwongo ana tamaa ya kuchukua kisichokuwa haki yake. Mambo yote mawili ni mustahili kwa Bi.Fatimah az-Zahra(a.s) ambaye Allah (s.w.t) alikuwa akikasirika kwa hasira yake, naye ni bibi wa wanawake waumini wa peponi, na Allah (s.w.t) amemtakasa kutokana na kila dhambi na uchafu kama ilivyotangulia, na ambaye Mtume wa Allah(s.a.w.w) amesema juu yake ni “Kipande (cha nyama) kinachotokana na mimi basi atakaemkasirisha amenikasirisha.[70] ”.

Na amemwambia: “Ewe Fatmah je, huridhii kuwa ni bora wa wanawake wa ‘Ummah huu?”[71] Vile vile amesema “Ni bibi wa wanawake wa watu wa peponi”[72] . Na hata kama tukisema Bi.Fatimah az-Zahra(a.s) alikuwa ni kama wanawake wengine na wala hana sifa zote hizo kama ilivyo katika Hadith hapo juu - basi kuwa kwake binti wa mwalimu wa binadamu na mke wa Amirul-Mu’uminiina Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) ambaye wameshuhudia kuwa ni hakimu wao yaani mjuzi wao, zinapinga dhana yeyote ya kuwa mjinga, hiyo ni kwa sababu kama Bi.Fatimah az-Zahra(a.s) alikuwa ametaka haki isiyokuwa yake - kama alivyoona Abubakr na kwamba Mitume(a.s) hawarithiwi, basi yeyote kati ya baba yake na mume wake angekuwa ni bora zaidi kumfahamisha hayo, ilihali mume wake Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) ndiyo hakimu wao kwa kutambua hayo, angemkataza kutaka mirathi hiyo kama isingekuwa ni haki yake.

Lakini tusijaalie hivyo na tunajilinda kwa Allah (s.w.t) kuwa hivyo, kwani ilipomfikia habari ya kuwa Abubakr amekataza haki yake katika Fadak, na mali nyingine aliompa Allah (s.w.t) baba yake Madina, na khums ya Khaibar, alimwendea akiwa na kundi la Muhajirin na Ansar na akawahutubia hotuba iliyo waliza watu. Na katika jumla ya aliyo yasema (bi. Fatimah) ni haya: “...na ninyi sasa mnadai kwamba hatuna mirathi wala cheo, je wanataka hukumu ya kijahili, je nani ni mbora wa kuhukumu kuliko Allah (s.w.t) kwa watu wenye yakini.

Ole wenu enyi Waislamu, katika Kitabu cha Allah (s.w.t) unamrithi baba yako na mimi simrithi baba yangu? Hakika umeleta kitu kibaya kabisa, kisha akawasomea Ayah “Muhammad hakuwa isipokuwa ni mtume na walishapita kabla yake mitume, je, akifa au akiuliwa mtarudi kwenye ukafiri? na atakae rudi kwenye ukafiri basi hamdhuru Allah (s.w.t) chochote na Allah (s.w.t) atawalipa wenye kushukuru”. Enyi watu! Nadhulumiwa mirathi ya baba yangu na ninyi mnaniona na kunisikia...? Hadi mwisho wa hotuba hiyo[73] .

Hakika maana ya kauli ya Mtume wa Allah(s.a.w.w) “Haturithiwi” haina maana ya kuzuia hukumu ya mirathi katika mali ya Manabii na milki zao za kidunia kama alivyofanya ijtihad Abubakr - kwani Nabii Suleiman alimrithi Daud kama inavyosema Qur’an juu ya hilo katika kauli yake Allah (s.w.t) Mtukufu:

وَوَرِثَ سُلَيْمَانُ دَاوُودَ ﴿١٦﴾

Na akamrithi Suleiman Daud .”(An-Naml 27:16).

يَرِثُنِي وَيَرِثُ مِنْ آلِ يَعْقُوبَ وَاجْعَلْهُ رَبِّ رَضِيًّا ﴿٦﴾ يَا زَكَرِيَّا إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَامٍ اسْمُهُ يَحْيَىٰ لَمْ نَجْعَل لَّهُ مِن قَبْلُ سَمِيًّا ﴿٧﴾

Anirithi mimi na arithi watu wa Yaaqubu na mjaalie ewe Mola awe ni mwenye kuridhiwa,ewe Zakaria, hakika sisi tunakubashiria mtoto jina lake ni Yahya . (Maryam 19: 6-7).

Na maana ya anirithi katika Ayah iliyotangulia haina maana ya kurithi Unabii kwa Sababu Unabii sio wa kurithiana hivyo maana ya kauli ya Mtume-haturithiwi - tukifaradhisha kuwepo kwake ni kwamba Manabii hawatakusanya au kulimbikiza dhahabu na fedha ili iwe ni mirathi baada yao kama wanavyofanya wale wanaotaka dunia.

Tanbih

Hakuna budi kueleza jambo muhimu nalo ni kwamba Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) kuacha kumbay’i Abubakr ilikuwa ni kwa sababu ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kumuusia Uimamu na Ukhalifa na sio kwa sababu ya Abubakr kumkataza Bi.Fatimah az-Zahra(a.s) mirathi yake, kama ambavyo wengine wanavyosingizia kuacha kwake hilo, vinginevyo ni sababu ipi iliyofanya kundi la Masahaba wakubwa kukataa kumbay’i vile vile, na hali walisha mfuata Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) , na nini maana ya kauli ya ‘Aisha - kama ilivyo tangulia hapo mwanzo.

Ni kuchukia kuhudhuria kwa ‘Umar? ‘Umar hakuingilia chochote katika hitilafu ya mas’ala ya mirathi ya Bi.Fatimah az-Zahra(a.s) wakati ambapo tumeona namna gani alikuwa na nafasi muhimu katika maslahi ya Abubakr tukiachilia mbali kuwa mas’ala ya mirathi hayawezi kuchukuliwa kuwa ni kipingamizi cha Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) kutompa bai’a Abubakr isipokuwa kama ataona kwamba yeye sio Khalifa wa kisheria, na kama si hivyo ingekuwa ni wajibu kwa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) kubay’i mara moja bila ya kuacha hata kwa siku moja, sasa itakuwaje kama ataacha kwa muda wa miezi sita?

Je, Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w) Alidokeza Juu Ya Abubakr Kupewa Ukhalifa?

Baadhi ya watu wanatoa hoja juu ya haki ya Abubakr kuwa Khalifa, na kudokezewa na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) juu ya suala hilo, katika Hadith aliyopokea Ibnul-Jauzi kwa Isnad yake kutoka kwa ‘Al- Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema: “Alipofariki Mtume wa Allah(s.a.w.w) na alikwisha mtanguliza Abubakr katika sala basi tukaridhia kwa dunia yetu kwa aliyeridhiwa na Mtume wa Allah(s.a.w.w) kwa ajili ya dini yetu, hivyo tukamtanguliza Abubakr. [74]

Hadith hii ina uongo uliowazi ‘Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) ambaye wanadai amepokea Hadith hii ndiye aliye mkhalifu Abubakr, na hakumbay’i isipokuwa baada ya miezi sita, na walishamfuata katika kukhalifu Masahaba wakubwa - kama ilivyotangulia - na tukikadiria usahihi wa Hadith hii basi inalazimu Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) awe ndiyo wa kwanza kubay’i.

Lakini riwayah inapingana kabisa na hotuba maarufu za ‘Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) ambazo ziko wazi juu ya malalamiko ya Ukhalifu wa Abubakr na kuunyakua kwake. Kwa kuongezea kukhalifu kwa ‘Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) kumbay’i Abubakr ambako peke yake kunatosha kutengua Hadith hiyo, hapa kuna dalili nyingine zinazotilia mkazo uongo wa Hadith hiyo:-

a.) Jeshi la ‘Usamah bin Zaid ambalo Mtume wa Allah(s.a.w.w) alimkabidhi bendera mikononi mwake na akawahimiza Masahaba kuondoka naye yuko katika pumzi za mwisho katika umri wake mtukufu, na walikuwepo katika sariya hiyo wakubwa wa Muhajirin mfano, Abubakr, ‘Umar na Abu ‘Ubaidah - kama Mtume angetaka kumfanya Abubakr kuwa Khalifa asingemweka katika sariya hiyo.

b.) Kama Hadith ya juu ingekuwa sahihi basi Abubakr angeitolea hoja mwenyewe siku ya Saqifa kwa walio mkhalifu, wakati ambapo alikuwa na haja sana ya hoja ili kumaliza ugomvi, lakini siku hiyo tulimwona anatoa hoja kwamba kabila la Maquraish ni bora zaidi kama ilivyo tangulia.

c.) Na juu ya yote hayo riwayah hii inatenguliwa na riwayah zenye nguvu zilizo thabiti katika Ukhalifa wa ‘Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) hivyo rejea tuliyonukuu juu ya hilo katika kurasa zilizo tangulia.

Je, Bi.Fatimah Az-Zahra (A.S.) Alikufa Kifo Cha Kijahiliyyah (Kikafiri)?

Hakika Bi.Fatimah az-Zahra(a.s) alifariki dunia hali ya kuwa ni mwenye kukasirika juu ya Abubakr, na wala hakumbay’i na aliusia kuwa asimsalie wala asisindikize jeneza lake - tazama Hadith inayokuja chini inayoonyesha ushahidi wenye nguvu juu ya aina ya Uimamu (au amiri) ambaye ni wajibu kumtii na iliyo kusudiwa katika Hadith zinazofuata chini yake.

Binti wa Mtume wa Allah(s.a.w.w) alikasirika akamhama Abubakr na hakuacha kuwa ni mwenye kumhama mpaka akafariki, na aliishi miezi sita baada ya Mtume wa Allah(s.a.w.w) kufariki dunia [75] . Alipokufa mume wake alimsalia na alimzika usiku na hakumruhusu Abubakr kumsalia[76] .

Kutoka kwa Ibn ‘Abbas kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema: “Atakayechukia jambo kwa kiongozi wake basi asubiri, kwani atakayetoka kwa kiongozi shubiri moja atakufa kifo cha kikafiri .[77]

Na katika Sahih Muslim “Atakaye kufa na hana Bay’ia katika shingo yake atakufa kifo cha kikafiri”[78] . Na katika Musnad Ahmad: “Atakaye kufa bila ya Imam atakufa mauti ya kikafiri”[79] .

Hivyo Imam (au amiri) aliyekusudiwa katika Hadith tatu za juu - Hadith hizo ambazo zinabainisha wajibu wa kumtii Imam na kwamba anayekufa bila ya kumbay’i mauti yake yatakuwa ya kikafiri bila shaka sio Abubakr. Kwa nini? kwa sababu kama Abubakr angekuwa ni khalifa na kufa kwa kumkhalifu maana yake ni mauti ya kikafiri, basi lisingetokea hilo kwa ambaye Waislamu wote wanaafikiana kuwa yeye ni bibi wa wanawake wa Jannat, na ambaye Nabii anakasirika kwa hasira yake ambayo bila shaka ina maana ya ghadhabu ya Allah (s.w.t) kwa anaye mkasirikia kwa sababu Bi, Fatimah az-Zahra(a.s) yeyeni katika Ahlul-Bayt(a.s) ambao Allah (s.w.t) amewaondolea uchafu na akawatakasa kabisa.

Na ambapo Mtume wa Allah(s.a.w.w) amesema juu yake: “Ni pande langu atakaye mkasirisha amenikasirisha mimi[80] .” Bali amesema juu yake vile vile “Ni bibi wa wanawake wa watu wa peponi.[81]

Tunasema Bi.Fatimah az-Zahra(a.s) mwenye vyeo hivi kwa Mtume na Waislamu hakufa - (Allah (s.w.t) aepushe mbali) - mauti ya kikafiri, kwa sababu kwa kuchukia kwake msimamo wa Abubakr na muamala wake kwake, kwa kutoka kwake katika utawala wake sio shibiri moja tu bali maili nyingi, kwa kukataa kwake kumbay’i na kumkasirikia na akafariki akiwa katika hali hiyo na kuusia kwake kwamba asimsalie; (yote hayo) ni dalili tosha ya kuonyesha kuwa Abu bakr si miongoni mwa wale viongozi ambao kuwakhalifu kunamsababishia mtu kufa kifo cha kijahiliyyah.

Matokeo

Kwa hiyo Maimamu (viongozi) walio kusudiwa katika Hadith zilizotangulia ambao ni wajibu kuwatii sio aliowakhalifu kamwe Bi.Fatimah az-Zahra(a.s) . Ni nani basi hawa Maimamu (viongozi) ambao ni wajib kuwatii na kutowaba’i ni kuangamia?

Mtume wa Allah(s.a.w.w) alikwisha jibu swali hili kwa kusema: Amesema: “…kutakuwa na viongozi kumi na wawili’[82] .” Na nyinginezo zilizo tangulia katika Hadith za Uimamu.

Nne: ‘Umar Kupewa Ukhalifa Na Bay’ia Yake

Abubakr aliposhikwa na maradhi alimwita ‘Uthman bin ‘Affan na akamwambia: “Andika kwa jina la Allah (s.w.t) Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu, haya ni aliyoamua Abubakr bin Quhafah kwa Waislamu, ‘amma baad…”, Abubakr akazimia. ‘Uthman bin ‘Affan akaandika, ‘amma baad, mimi nimemfanya ‘Umar bin Al-Khattab kuwa Khalifa wenu na sikuwatawalisheni mtu mwema’, kisha Abubakr akazinduka, ‘Uthman akamsomea alivyoandika. Abubakar akasema: “Na kuona uliogopa watu kukhitalifiana kama ningekufa katika kuzimia kwangu.” akasema: ‘Ndiyo’, akasema: “Mungu akulipe kheri kwa ajili ya Uislamu na watu wake.” Abubakr akaafiki haya[83] .

Kama ilivyopokelewa kwamba ‘Umar alikuwa na karatasi ambayo humo Abubakr alimteua kuwa khalifa na alikuwa anawaambia watu sikilizeni na tiini kauli ya khalifa wa Mtume wa Allah(s.a.w.w) , anasema kwamba: “Hakika mimi sikuwatawalishieni mtu mwema[84] .”

Na inabainika kwamba Abubakr alikuwa anaogopa hitilafu na watu kugombania ukhalifa baada yake na hivyo akauusia uwe kwa ‘Umar na akaandika katika karatasi ili iwe ni hoja kwa watu, na ili kusiwepo na nafasi ya kugombania.

Swali ambalo linajitokeza hapa ni, je, Mtume hakufikiria kama alivyofikiria Abubakr? Au hakuogopa Ikhtilaf na ugomvi katika ‘Ummah juu ya uongozi kama alivyoogopa Abubakr?

Na tofauti ilikuwa kiasi gani baina ya hali ya Waislamu wakati alipofariki Mtume wa Allah(s.a.w.w) , na hali yao wakati wa kufariki Abubakr? Je, dhana ya kukhitilafiana na kufarakana baada ya kufariki kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) haikuwa ni kubwa zaidi wakati huo kuliko ule wa Abubakar? (na hiyo ni kwa sababu tulizozitaja mwanzo: hatari ya kuritadi wanafiki, Warumi waliokuwa wanasubiri kuwabadilisha Waislamu wakati watakapo pata fursa, tukiachilia mbali ugomvi wa kikabila baina ya Mabedui) Au Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) hakufahamu hatari zote hizi zinazosubiri Uislamu na watu wake kama alivyo fahamu Abubakr?

Hakika ni ajabu ya maajabu, pamoja na Hadith zote zilizothibiti za Mtume kumfanya Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) kuwa Khalifa - kama ilivyo tangulia - wote walipinga kwa hoja ya kuwa Mtume alifanya jambo la Ukhalifa liwe Shura baina ya Waislamu - rejea matukio ya Saqifa utaona ni kwa aina gani ya Shura ilitimia Bai’a ya Abubakr- na Abubakr anamfanya ‘Umar kuwa Khalifa wa Waislamu kwa kauli yake bila ya kumshauri yeyote katika Waislamu, iko wapi Shura wanayoidai?

Bila shaka watasingizia msimamo huu kuwa Abubakr ana haki ya kumteua yeyote amtakae kati ya Waislamu anayeona kuwa anafaa kubeba jukumu la Ukhalifa, pamoja na kwamba alikuwa anaumwa sana wakati wa kuchukua uamuzi huo ambapo alizimia wakati wa kuandika kwake, halafu ‘Uthman akakamilisha badala yake. ‘Uthman ambaye alikuwa anajua kuaminiana kati ya makhalifa wawili, kwa sababu ‘Umar bin Al-Khattab alisimama msimamo mkali ulioshuhudiwa siku ya Saqifa katika kumsaidia Abubakr kupata ukhalifa. La ajabu na la kushangaza ni kwamba hakusema yeyote kati ya Masahaba kuwa Abubakr alikuwa anaweweseka wakati alipoandika wosia, kama ambavyo walimwambia Mtume wa Allah(s.a.w.w) neno hilo wakati alipowaamuru wamletee karatasi awaandikie ili wasipotee baada yake, na wakamkataza kuandika wosia wake katika karatasi ambapo ilikuwa inawezekana kumpa Ukhalifa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) na kuwaonyesha ushahidi kama alivyoonyesha ‘Umar karatasi hiyo ambayo Abubakr alimwandikia kuwa khalifa.

Tano-Shura Na Bayi’a Ya ‘Uthman Bin ‘Affan.

‘Umar alipochomwa jambia, akaambiwa ungeteua khalifa, akasema: “kama Abu ‘Ubaidatil Jaraha angekuwa hai ningemteua kuwa khalifa na kama Salim mtumwa wa Abi Hudhaifah angekuwa hai ningemteua kuwa Khalifa, kisha akawaambia “Hakika watu wanasema kwamba Bai’a ya Abubakr ilikuwa ghafla, Allah (s.w.t) ameepusha shari yake na Bai’a ya ‘Umar haikuwa Shura na Ukhalifa baada yangu ni Shura”[85] .

Kisha akasema nimefanya jambo lenu liwe Shura baina ya watu sita miongoni mwa Muhajirin wa mwanzo, ambapo aliwataja kwa kusema “Niitieni Al- Imam’Ali ibn Abi Talib(a.s) , ‘Uthman, Talha, Zubeir, ‘Abdurahman bin ‘Auf na Sa’ad bin Abi Waqqasi, kama wataafikiana wanne basi wawili wafuate rai ya wanne na kama wataafikiana watatu basi fuateni rai ya ‘‘Abdurahman bin Auf, sikilizeni na tiini...[86]

Kutokana na riwayah ya hapo juu inadhihirika kwamba ‘Umar alijaalia jambo la kuteua mikononi mwa ‘Abdurahman bin Auf na hii ni aina ya tatu katika aina za Shura ambayo wanaisema ‘Umar alimwamuru ‘Abdurahman bin ‘Auf aweke sharti la kufuata mwendo wa Masheikh wawili Abubakr na ‘Umar katika bayi’a, tukiongeza kufuata Kitabu cha Allah (s.w.t) na Sunnah za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) .

Kama alivyotarajia watu sita waligawanyika sehemu mbili na waliopendekezwa ni Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) na ‘Uthman bin ‘‘Affan, na Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) alikataa kufuata mwendo wa masheikh wawili kwa kusema:

“Nitafuata Kitabu cha Allah (s.w.t), Sunnah za Nabii wake na ijtihadi yangu,[87] ambapo ‘Uthman aliafiki sharti hilo, hivyo ukhalifa ukamwendea kwa sababu hiyo.

Bukhari ametoa katika Kitabu chake sehemu ya tukio hili kama inavyodhihirika katika Hadith ifuatayo: Akasema (Abdrahman): “Niitieni Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) akamwita, akamnong’oneza mpaka usiku ukaingia. Kisha Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) akatoka kwake akiwa ana matarajio, na ‘Abdurahman alikuwa anaogopa kitu (fulani) kwa Al- Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) kisha akasema: Niitieni ‘Uthman akamwita akamnong’oneza mpaka muadhini wa asubuhi aliwatenganisha, aliposalisha watu sala ya asubuhi na kundi hilo likakusanyika, walipokusanyika ‘Abdurahman akatoa shahada kisha akasema: Ama baad ewe ‘Ali ibn Abi Talib nimetazama jambo la watu sikuwaona kuwa wanamtaka mwingine isipokuwa ‘Uthman bin ‘Affan hivyo usiipe nafsi yako mwanya.

Akasema kumwambia ‘Uthman bin ‘Affan: Nakubay’i kwa kufuata Kitabu cha Allah (s.w.t.), Sunnah za Mtume na mwendo wa makhalifa wawili baada yake, Aburahman akambayii na watu wakambayii[88] .”

Kuuliwa Kwa ‘Uthman Bin ‘Affan

Maneno mengi yamesemwa kuhusu kuuliwa kwa ‘Uthman, na kauli na mapokezi yamegongana juu ya hilo, hasa kuhusu kundi ambalo lilikuwa linahimiza kuuliwa kwake na sababu ambazo zilikuwa zinawasukuma juu ya jambo hilo na matukio hayo kufikia malengo yake.

Lakini vyovyote mambo yatakavyokuwa, hakika ilikuwa ni kutokana na vitendo vinavyohusiana na utawala na kuteua magavana katika jamaa zake na kuwagawia mali kutoka kwenye hazina ya dola ndiko kulikozua lawama za wenye kufanya Thawrah (mapinduzi).

Na hapa tunanukuu rai ya Khalid bin Muhammad Khalid neno kwa neno, katika yanayohusiana na masuala haya. “Bali tunakaribia kushuku kuwa ‘Uthman alikuwa anafahamu kwamba wengi wa waliofurahi kuchaguliwa kwake kuwa Khalifa badala ya Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) karamallahu wajhahu... hakika walifanya hivyo kwa kutaka kuondokana na ugumu na ukata wa maisha ambavyo watu wamekuwa wakikabiliwa navyo kwa muda mrefu, na ambavyo vingeleta taabu upya kama Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) angechukua uongozi kwa msimamo wake madhubuti na uadilifu wake ulio makini[89] .

Hivyo matamanio ya kundi la jamaa zake katika Bani Umayyah yalichezea mwelekeo wa dola, pato lake na mali zake kwa ujumla. Abu Sufian aliingia kwake baada ya Bai’a na kumwambia: “Enyi Banu Umayyah udakeni kama mnavyo daka mpira, kwa yule ambaye Abu Sufian anaapa kwaye sikuacha kuwa natamani liwe kwenu, basi na liwe ni lenye kurithiwa na watoto wenu[90] . Na katika mapokezi mengine “udakeni kama mnavyodaka mpira kwani hakuna pepo wala moto[91] .”

Yote hayo yamesababisha masahaba watukufu kupinga na kutofautiana kwao na ‘Uthman, kati ya hao ni Abudhar Al-Ghafaariy, ‘Abdallah bin Mas’ud na ‘Ammar bin Yasir ambao Khalifa aliwachukulia msimamo mkali kabisa.

Ama Abudhar alifukuzwa na kwenda katika jangwa la Rabadhah kwa kuadhibiwa na ‘Uthman, kwa Sababu ya kumpinga kwake Mu’awiyah bin Abi Sufian-gavana wa ‘Uthman huko Sham-kwa kulimbikiza kwake dhahabu na ufujaji wake katika hazina ya mali ya Waislamu.

“Nilipitia Rabadhah basi nikamkuta Abudhar nikamwambia: Nani aliyekuleta huku?” Akasema: “Nilikuwa Sham nikakhitalifiana na Mu’awiyah bin Abi Sufian katika wale wanao limbikiza dhahabu na fedha na wala hawazitoi katika njia ya Allah (s.w.t) - Mu’awiyah bin Abi Sufian akasema: ‘Imeteremka kwa Ahlul-Kitab’, na nikasema: Imeteremka kwetu na kwao, hivyo ndivyo ilivyokuwa baina yangu na yeye, na akamwandikia ‘Uthman akimlalamikia juu yangu.

‘Uthman akaniandikia: ‘Njoo Madina’, basi nikaja, watu wakanikusanyikia kama kwamba hawajawahi kuniona kabla ya hapo, nikamweleza hayo ‘Uthman, akaniambia ukitaka nyamaza kimya utakuwa karibu yangu. Hayo ndiyo yaliyonileta hapa, na kama wangeamrisha jeshi kwangu ningetii na kusikiliza”[92] .

Ama ‘‘Abdallah bin Masu’ud mtunza hazina wa Kufah alishavunjwa mbavu zake[93] , baada ya kupigwa na kijana wa ‘Uthman, kama adhabu yake kwa kumpinga kwake Al-Walid bin ‘Uqbah bin Abi Muit - ndugu wa ‘Uthman kwa upande wa mama na gavana wake wa Kufah, aloiyechukua nafasi hiyo baada ya kuuzuliwa Sa’ad bin Abi Waqaas - kwa sababu ya kuchukua kwake mali katika Baitul-Maal bila ya kurudisha.

Ama ‘Ammar Yasir alipata mpasuko kutokana na pigo kali kutoka kwa kijana wa ‘Uthman kama adhabu yake kwa sababu ya kufanya kulingana na wosia wa Ibn Mas’ud ya kuwa amsalie na amzike bila ya khalifa kujua ili asimsalie[94] .

Na mengine mengi yasio kuwa hayo kati ya misimamo ambayo sababu yake ilikuwa ni vitendo vya jamaa wa ‘Uthman katika Bani Umayyah na kufuja kwao mali ya dola, na hasa Marwan bin Al-Hakam ambaye peke yake alichukua khums ya kutoka Afrika, na wala hakuna ajabu kwa hilo, kwani ngawira na mali zilikuwa zinabubujika katika hazina ya dola kama maji yanavyo bubujika, na hiyo ni kwa sababu ushindi ulifikia mbali sana wakati wa ‘Uthman.

Na ghadhabu ya ‘Aisha kwa ‘Uthman ilichangia kuzidi kwa Thawrah (mapinduzi) ya wenye kufanya Thawrah, na kunyanyuka sauti za wapinzani kutokana na kuhimiza kwake juu ya kuuliwa khalifa na kumtuhumu kwa kubadilisha Sunnah ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kwa kusema “Muuweni Naathala (sanamu) hakika ameshakufuru[95] ” na neno hili lilitoka katika kinywa cha ‘Aisha na kusambaa kwa watu kama vile unavyo sambaa moto katika nyasi kavu, wakakusanyika kwake watu wengi miongoni mwao ni watu wa Madina pamoja na watu ambao waliwasili kutoka Misri, Sham na Kufah na wakamwua.

Bai’a Ya Al-Imam ‘Ali Ibn Abi Talib(A.S)

Baada ya kuuliwa ‘Uthman watu walimiminika kwa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) wakitaka kumbay’i wakamwambia: “Hakika huyu mtu ameshauliwa na ni lazima watu wawe na kiongozi na leo hatuoni anayestahiki jambo hili kuliko wewe na Bai’a ikatimia.”

Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) alipotaka kusimamisha uadilifu baina ya watu; kumfanya mnyonge awe sawa na mwenye nguvu, na wala kusiwe na tofauti baina yao, na kutekeleza adhabu alizo ziteremsha Allah (s.w.t) katika Kitabu chake, baadhi yao wakampinga na wakawa wakaidi kwake. Wakaeneza fitina na wakaandaa jeshi, huku wakitangaza uasi na ukaidi kwa Khalifa wa Waislamu na Imam wao ambaye ni wajib kumtii na hiyo ilikuwa ni katika matukio mawili mabaya nayo ni Vita vya Jamal na Siffin.

Sita- Tukio La Jamal Na Kutoka Kwa ‘Aisha

‘Aisha alipojua kuuliwa kwa ‘Uthman na watu kumbay’i Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) , alimwambia yule aliyempa habari; naye ni ‘Ubaidullah bin Kilab: “Wallahi natamani ningekufa, kama jambo litakuwa kwa sahibu yako, ole wako tazama unayoyasema!” ‘Ubaidullah akamwambia: “Nilivyokuambia ndivyo, Wallahi simjui yeyote aliye bora zaidi yake, basi ni kwa nini unachukia uongozi wake?” ‘Aisha akapiga kelele: “Nirejesheni, nirejesheni”, akaondoka kuelekea Madina huku akiwa anasema: “Wallahi ‘Uthman ameuliwa kwa dhulma, Wallahi nitalipiza kisasi kwa damu yake!” ‘Ubaidullah akamwambia: “Kwa nini? Wallahi wa kwanza kusema auliwe ni wewe, ulikuwa ukisema: muuweni sanamu ameshakufuru.” Akasema: “Wao walimwambia atubu kisha wakamuuwa, nilisema na wao walisema, na kauli yangu ya mwisho ni bora kuliko kauli ya mwanzo.”

Akaondoka kuelekea Makkah akateremka kwenye mlango wa Msikiti, watu wakakusanyika, akasema: “Enyi watu! Hakika ‘Uthman ameuliwa kwa dhulma Wallahi nitalipiza kisasi kwa ajili ya damu yake[96] .”

Ghadhabu za ‘Aisha ziliafikiana na ghadhabu za Talha na Zubeir. Baada ya Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) kuwaondolea ugavana wa nchi za Yemen na Bahrain, basi wakatengua Bai’a yao kwa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) , na wakaenda Makkah wakimhimiza ‘Aisha kwenda kumpiga vita Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) , wakatoka na likaondoka pamoja nao jeshi kubwa chini ya uongozi wa ‘Aisha kuelekea Basra ambapo vilitokea vita vinavyo julikana kwa jina la Vita vya Jamal; na ushindi mkubwa ulikuwa upande wa jeshi la Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) na humo akauliwa Talha na Zubeir na Waislamu elfu kumi na tatu, yote hayo ni kwa sababu ‘Aisha anataka kulipiza kisasi kwa waliomwuwa ‘Uthman kama alivyosingizia katika kutoka kwake, na ambao alidai kuwa waliingia katika jeshi la Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) .

Vyovyote mambo yatakavyokuwa je, isingekuwa ni bora kwake kuacha jambo hili kwa kiongozi? Yeye hilo la mhusu nini? ‘Uthman ni mtu katika Bani Umayyah na ‘Aisha ni katika Bani Tamim, isipokuwa kama kutoka kwake kuna sababu nyingine isiyokuwa hiyo! Mtume alishatoa habari juu ya fitina hii ambayo ilitokea kwa sababu ya kutoka ‘Aisha kwake:

Na bakieni katika nyumba zenu na wala ....”(Al-Ahzaab 33:32)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alisema alipohutubia akaashiria kwenye nyumba ya ‘Aisha akasema: “Hapa kutatokea fitina, akakariri mara tatu; kutatokea upembe wa Shetani[97] .

Na aliyoyapokea ‘Ammar Yaasir yanaonyesha kuwa aliyemtii ‘Aisha kwa kutoka kwake dhidi ya Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) hayo yanahesabiwa kuwa ni katika kutomtii Allah (s.w.t).

“Nilimsikia ‘Ammar anasema: “Hakika ‘Aisha alienda Basra Wallahi hakika yeye ni mke wa Mtume wenu katika dunia na akhera, lakini Allah (s.w.t) amewapatia mtihani ili ajue mtamtii Allah (s.w.t) au yeye (Aisha)[98] .”

Na imeshajulikana kwa ‘Aisha gherah yake kubwa kwa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) , kwani alikuwa hawezi hata kutaja jina lake. Amesema ‘Ubaidullah bin ‘‘Abdallah bin ‘Utbah kwamba ‘Aisha amesema: “Alipougua Mtume(s.a.w.w) na akazidiwa na maradhi yake alitaka ruhusa kwa wake zake augulie katika nyumba yangu basi wakamruhusu Nabii akatoka akiwa baina ya wanaume wawili akikokota miguu yake ardhini, baina ya ‘Abbas na mwanamume mwingine.” ‘Ubaidullahi akasema:”Basi nikamweleza ‘‘Abdallah bin ‘Abbas akasema: “Je, unajua mwanamume mwingine ni nani?” Nikasema: “Hapana.” Akasema: “Ni Al- Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s)[99] .

Na huenda aliyo yasikia katika kauli ya Al- Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) kwa Mtume wa Allah(s.a.w.w) kuhusu yeye katika tukio la ‘Ifki’ yalikuwa ni sababu ya chuki na gherah hii[100] .

Kiongozi wa washairi Ahmad Shauqi ameelezea gherah ya ‘Aisha katika beti zifuatazo akimhutubia kwayo Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) :

“Ewe jabali, majabali yanashindwa uliyoyabeba, lawama ngapi amekutupia bibi wa Jamal, ni kulipiza kisasi kwa damu ya ‘Uthman kumemhuzunisha au ni wivu ambao huzuni yake bado haijakwisha?

Hiyo ni hila ambayo haikuwa akilini, hila za wanawake zinafanya majabali kuwa mepesi, hakika ‘Aisha ni mwanamke hata kama ametakaswa na kuepushwa na makosa, ameyatoa katika jinsia yake na umri wake ambao yatabaki milele miongoni mwa chuki yake”.

Uzushi Wa ‘‘Abdallah Bin Saba’

Tumetegemea katika tulioyanukuu miongoni mwa Hadith katika “kuuliwa kwa ‘Uthman” na Vita vya Jamal” Hadith zinazoaminiwa na zinazoafikiana na tukio na nyakati ambazo zimezunguka matukio haya mawili. Lakini pamoja na Hadith hizi, kuna Hadith za uongo amabazo ameziweka mpokezi mmoja, na kwake wamechukua waandishi na wana historia wote, aliezua Hadith zote hizo ni “SEIF BIN ‘AMRU AT- TAMIMIY AL-BARJAMI AL-KUUFI”. Aliyefariki mwaka 170 Hijriyyah. Huyu mpokezi ameweka uzushi wa uongo, shujaa wake ni ‘Abdallah bin Saba myahudi ambaye nasaba yake ni kutoka Sana’a Yemen, na muhtasari wa uongo huo ni:

Hakika mtu huyu mwongo ‘‘Abdallah bin Saba alidhihirisha Uislamu wake wakati wa ‘Uthman ili kuwahadaa Waislamu, basi akatembea katika miji ya Kiislamu Misri, Sham, Basra na Kufah akibashiri kurejea kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na kwamba Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) ndiye wasii wake na kwamba ‘Uthman amenyang’anya haki ya wasii. Basi wakamwamini na likamfuata kundi miongoni mwa Masahaba wakubwa na Tabi’in mfano ‘Ammar bin Yaasir, Abu Dhar, Muhammad bin Hudhaifah na wengineo, na akaweza kuandaa jeshi kwa ajili ya kumwuwa ‘Uthman hadi wakamwua ndani ya nyumba yake.” hivi ndivyo anavyoorodhesha “SEIF BIN ‘AMRU” matukio katika uzushi wake wa uongo mpaka anaishia katika Vita vya Jamal ambapo anaamuru na kuchochea vita, hivi ndivyo ilivyotokea Vita ya Jamal (kwa mujibu wa mzushi huyu).

Uzushi huu wa uongo ameuzua “SEIF BIN ‘AMRU” na kutoka kwake wamechukua wanahistoria wote, kisha kisa kikawa mashuhuri na kuenea katika vitabu vya tarekh tangu karne zote hadi leo, mpaka ikawa ni katika matukio mashuhuri ambayo hayaguswi na shaka. Na wamepita (na kukubaliana) waandishi wengi na wana historia wa mashariki na mustashiriqina, kwamba uongo huu ameuzua mpokezi mmoja peke yake, hana mshirika na kwamba mpokezi huyu ni mashuhuri kwa maulamaa wa Hadith waliotangulia kwa uongo anatuhumiwa kwa uzaindiki, Abu Daud amesema juu yake:

“Si chochote, mwongo.”

Na amesema Ibn ‘Abdil-Barri: “Seif ni mwenye kuachwa lakini tumetaja Hadith yake kwa ajili ya kujua”. Na Nisai amesema: “Ni dhaifu, Hadith zake ni zenye kuachwa sio mkweli wala sio mwaminifu”.

Na wamechukua (pokea) kutoka kwa huyu mpokezi: Tabari, Asaakir, na Ibn Abi Bakr na kutoka kwa Tabari wamechukua waandishi na wana historia wengine hadi leo hii, hivi ndivyo ulivyo enea uongo katika vitabu vya tarekh baada ya kupokea Tabari kutoka kwa Seif bin ‘Amru peke yake.

Ni maarufu kuwa Hadith za Ahad hazimaanishi isipokuwa dhana ya kielimu na wala hazimaanishi yakini, sasa itakuwaje ikiwa Hadith hii moja sio ya kweli bali ni mashuhuri kwa uongo wake na uzindiki wake, je Hadith yake itakubaliwa?

Namna gani itakubaliwa kuhukumiwa ‘Ummah mkubwa katika Waislamu kwa kuzingatia Hadith moja ya pweke (Ahad), na kuachwa Hadith mutawatir zilizo thibiti kutoka kwa Mtume wa Allah(s.a.w.w) kinyume cha aliyo yasema yule mwongo Seif bin ‘Amru At-Tamimiy?

Hakika ni katika upuuzi wa kihistoria Ushi’a kunasibishwa na mtu mwongo naye ni ‘‘Abdallah bin Saba’ na kwamba yeye ndiye aliyesema juu ya wosia wa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) , pamoja na kuwepo Hadith zote hizo za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ambazo zimethibitisha kwamba Ushi’a haukuwa isipokuwa ni wa Muhammad wala si vinginevyo, rejea Hadith za Uimamu katika kurasa zilizo tangulia ili uone iko wapi nafasi ya ‘‘Abdallah bin Saba’. Je ‘‘Abdallah bin Saba’ ndiye aliyesema: “Nimewaachia Kitabu cha Allah (s.w.t) na kizazi changu Ahlul-Bayt(a.s )?”

Je, ‘‘Abdallah bin Saba’ ndiye aliyesema: “Baada yangu kutakuwa na Maimamu kumi na wawili?”

Je, ‘‘Abdallah bin Saba’ ndiye aliyesema: “Ambaye nilikuwa kiongozi wake basi Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) ni kiongozi wake?”

Na ni upuuzi wa namna gani tunakubali kwamba mwanamume wa kiyahudi amekuja kutoka Yemen na kutangaza Uislamu wake kwa unafiki kisha anafanya kazi zote hizo ambazo zinafikia kuongoza jeshi la Kiislamu dhidi ya baadhi ya Waislsmu bila ya yeyote kumjua? Je, uongozi wa Waislamu na Maimamu walikuwa katika ghafla ya kiasi hiki?

Hakuna shaka kuwa anayesema haya amepotea upotovu ulio wazi na orodha ifuatayo inabainisha msururu wa wapokezi ya uongo wa ‘Abdallah bin Saba’ kutoka kwa mzushi wake wa kwanza “Seif bin ‘Amru At-Tamimiy” hadi kwa wapokezi wake katika wale waliokuja baada yake.