UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYYAH

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYYAH28%

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYYAH Mwandishi:
: Abdul Kareem J. Nkusui
Kundi: Tarehe

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYYAH
  • Anza
  • Iliyopita
  • 13 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 9982 / Pakua: 3367
Kiwango Kiwango Kiwango
UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYYAH

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYYAH

Mwandishi:
Swahili

1

2

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYA

SEHEMU YA TANO

NDOA YA MUDA

Ndoa ya muda ambayo inajulikama vile vile kama ndoa ya "Mut'a," nayo ni mwanamke kuozesha nafsi yake kwa mwanamme kwa mahari maalumu na kwa muda maalumu, kwa kufunga ndoa iliyotimiza masharti Sahih ya kishariah. Tamko lake ni mwanamke kumwambia mwanaume baada ya maafikiano na maridhiano juu ya mahari na muda: "Zawwajtuka nafsi bimahri qadruhu kadha ilal-ajalil-maalum" (Nimekuoza nafsi yangu kwa mahari kadha kwa muda maalumu), na muda unabainishwa wazi. Na jibu la mwanaume linakuwa haraka "Qabiltu" (Nimekubali).

Na wakala unajuzu katika ndoa hii kama ilivyo katika mikataba mingine. Na kwa kukamilika masharti ya ndoa, mwanamke anakuwa ni mke wa mwanaume na mwanaume anakuwa ni mume wake hadi mwisho wa muda uliopangwa katika ndoa. Na wanaweza kuongeza muda mwingine, na ni wajibu kwa mke akae 'Iddah baada ya kumalizika muda kwa tohara mbili (hedhi mbili) kama anapatwa na hedhi, vinginevyo ni kwa muda wa siku arobaini na tano. Na mtoto wa mut'a awe ni mvulana au binti ananasibishwa kwa baba yake.

Na Waislamu pamoja na khitilafu za madhehebu yao wanaafikiana na aina hii ya ndoa, ndoa hii ni katika mambo yalioanza tangu mwanzo wa Uislamu na kwayo imeteremka Ayah:

فَمَا اسْتَمْتَعْتُم بِهِ مِنْهُنَّ فَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ فَرِيضَةً ﴿٢٤﴾

"Kwa mlio jifurahisha nao miongoni mwao basi wapeni mahari yao .” (An-Nisaa 04:24)

Na wamefasiri wengi wa wafasiri wa Ahl as-Sunnah Al-Istimtai katika Ayah hii kwa ndoa ya Mut'a na Ibn 'Abbas na 'Ubay bin Kaab na Sa'id bin Jubair walikuwa wanasoma Ayah hii "Fama-stamta'atum bihii minhunna ilaa ajalim-musammaa fa'tuuhunna ujuurahunna."[226]

Amesema Ibn Kathir katika tafsiri yake akielezea hilo "na jambo ambalo liko mbali sana, ni hawa kuamini kupotoshwa kwa Qur'an, hivyo ni lazima kwa lililokusudiwa na wala sio kusoma"[227] na kuteremka Ayah hii katika ndoa ya Mut'a ni katika ambayo hayapasi kuwa ni maudhui ya mjadala, bali mjadala ni kuwa Ayah hii ni Mansukh au sio Mansukh? yaani imeharamishwa baada ya kuhalalishwa kwake au imebakia katika hali yake?

Mwanzo tunaeleza baadhi ya yaliopokewa katika Hadith zinazothibitisha ndoa ya Mut'a, kuwa ni ya kisheria katika Uislamu miongoni mwa aliyopokea Bukhari katika Sahih yake.

Kutoka kwa 'Abdillah amesema tulikuwa tukipigana vita pamoja na Nabii(s.a.w.w) na hatukuwa na wanawake basi tukasema Je tufanye ponyeto (tujichue wenyewe)? Akatukataza hilo, akaturuhusu baada ya hapo kuoa mke kwa kumpa nguo - kisha akasema: "Enyi mlioamini msiharamishe mazuri aliyo wahalalishia Allah (s.w.t)."[228]

Na Hadith ifuatayo inathibitisha bila ya shaka yoyote kwamba Mtume amefariki bila ya kuharamisha ndoa ya Mut'a na kwamba aliyekataza ni mtu mwingine baada ya kufariki kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Amesema Ayah ya Mut'a imeteremka katika Kitabu cha Allah (s.w.t) na haikuteremka Ayah ya Qur'an ya kuiharamisha na kuikataza mpaka akafariki, Mtu (fulani) akasema kwa maoni yake aliyoyataka.[229]

Na 'mtu' anaye ashiriwa katika Hadith iliyotangulia, si mwingine isipokuwa ni 'Umar al-Khattab, ambaye imethibitika kuwa yeye ndiye aliyeharamisha ndoa hii kama ilivyokuja katika Sharh ya Al-Baari katika Sahih Bukhari - angalia maelezo yake chini kwa tarjuma ya Kiingereza.

Na imekuja katika Sahih Bukhari vile vile katika Babu al-Tamattu' 'alaa ‘ahdi rasulilah(s.a.w.w) : ametusimulia Musa bin Isma’il, ametusimulia Hamaam kutoka kwa Qatadah amesema, amesimulia Mutarifu kutoka kwa Imran amesema: Tulifanya Mut'a wakati wa Mtume wa Allah(s.a.w.w) na Qur'ani ilishuka (juu ya hilo), na mtu (fulani) akasema kwa maoni yake anayoyataka.[230]

Ni uwazi ulioje wa vipi mtarjum alivyopiga chenga kwa kuifanya kwake kuwa ni mahsusi kwa Tamattu iliyopokewa katika riwayah ya Imran kuwa ni Haji-Tamattu na wala sio Mut'a ya wanawake. Vyovyote iwavyo kilicho muhimu kwetu ni kile kilichopokewa katika Sahih Bukhari tu, na kuashiria kwetu katika tarjuma haikuwa isipokuwa ni kudhihirisha alicho kinukuu mtarjum kutoka sharh ya Al-Baary katika Sahih Bukhari, na hasa kwa mwanamme asiyejulikana katika riwayah. Na yanatiwa nguvu kwa aliyo mwanamme asiyejulikana katika riwayah. Na yanatiwa nguvu kwa aliyo yapokea Muslim katika Sahih yake kwa Isnad ya Ibnun-Nadhar amesema: “Ibn ‘Abbas alikuwa anaamrisha Mut’a na Ibn Zubeir alikuwa anaikataza basi nikaeleza hilo kwa Jabir.”

Akasema:”Tulifanya Mut’a pamoja na Mtume wa Allah(s.aw.w) na alipotawala ‘Umar akasema: “Hakika Allah (s.w.t) anahalaisha kwa Mtume wake anayoyataka, basi timizeni Hijja na Umra na acheni kuoa hawa wanawake, sitoletewa mwanamme aliyeoza mwanamke kwa mwanamme isipokuwa nitampiga kwa mawe.”[231]

Na katika Sahih Tirmidhi kutoka kwa 'Abdallah bin 'Umar aliulizwa na mtu kutoka katika watu wa Sham juu ya Mut'a ya wanawake, akasema: "Ni halali", akasema: "Hakika baba yako alikwishaikataza." Ibn 'Umar akasema: "Unaonaje kama baba yangu amekataza na Mtume(s.a.w.w) ameifanya, utaacha Sunnah na kufuata kauli ya baba yangu?"[232]

Vile vile katika Sahih Muslim kumepokewa: "Kisha wakataja Mut'a, akasema kweli tulifanya Mut'a wakati wa Mtume wa Allah(s.a.w.w) , Abubakr na 'Umar."[233]

Na imekuwa mashuhuri kwa hibril-ummah 'Abdallah bin 'Abbas (r.a.) kwa rai yake kuwa Mut'a haikufutwa kama anavyopokea hayo Al- Zamakh'shariy katika Tafsiri yake Al-Kashaaf, ambapo ananukuu kutoka kwa Ibni 'Abbas kwamba Ayah ya Mut'a ni katika Muhkamaati, na vile vile katika Sahih Bukhari kuna yanayotilia mkazo hayo.

Amesema: "Nilimsikia Ibn 'Abbas anaulizwa kuhusu mtumwa wake akamwambia: 'hakika hiyo ni katika hali ngumu na wanawake wakiwa ni wachache au mfano wa hayo?’. Ibn Abbas akasema: “Ndiyo.” [234] 9 Pamoja na uwazi wa dalili hizo ni kama vile uwazi wa jua katikati ya mchana kuhusu kuendelea uhalali wa ndoa ya Mut’a.

Watu wengi katika Ahl as-Sunnah wako kinyume na hayo, lakini Ayah ambayo ni maalumu katika ndoa hii wanadai kuwa imefutwa na wamehitilafiana kuhusu Ayah iliyo ifuta, kati yao wanasema imefutwa na Ayah iliyopo katika Qur'an, na kati yao wanasema iliyofuta ni riwayah zilizopo kati ya Hadith. Tunajibu rai zote mbili kwa Hadith zilizothibiti ambazo zimetangulia, na ambazo zinaonyesha kufariki kwa Mtume(s.a.w.w) bila ya kukataza, na wale waliosema iliyofuta ni Ayah katika Qur'an nayo ni:

وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ ﴿٥﴾ إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ ﴿٦﴾

"Na wale ambao wanahifadhi tupu zao isipokuwa kwa wake zao au iliyowamiliki mikono yao ya kuume .”(Al-Mu’minun 23:5-6).

Inatosha kujibu rai yao hii kwa kutazama katika Ayah hii ambayo wanadai kuwa imefuta Ayah ya Mut'a, Ayah hii ni Makki (yaani imeshuka Makkah) na Ayah ya Mut'a ni Madani (yaani imeshuka Madina) na hukumu ya kisheria ya ndoa ya Mut'a ni madani (yaani imeshuka baada ya Ayah ya (na ambao wanahifadhi tupu zao...) na Ayah iliyotangulia haifuti inayokuja baada yake.

Ama aliyesema iliyofuta ni Hadith zilizopokewa kwa Mtume(s.a.w.w) , hakika Hadith hizo wanazozidai kuwa zimefuta, zinapingana zenyewe kwa zenyewe, baadhi yake zinasema imefutwa katika Khaibar na nyingine katika Autasi, ya tatu inasema ni katika siku ya Fath Makkah, na ya nne katika vita vya Tabuk na ya tano ni katika Umrah ya Qadhaa, ya sita ni katika Hajjat tul-Wida'a.

Kugongana na kupingana kwa riwayah hizo sio kwengine ila ni kuonyesha dalili ya kutokuwa ni Sahih, hayo ni pamoja na kuongezea kuwa riwayah hizo. Haziepukani na kuwa kwake ni Hadith za Ahaad, ambazo hazifai kuwa ni zenye kufuta hukumu ambayo imeletwa na Qur'an, na Shariah yake imethibiti kwa kongamano la Waislamu wote, kwa sababu Naasikhi haipatikani kwa habari ya mtu mmoja kwa ijmai, na Ayah haifutwi isipokuwa na Ayah kwa dalili ya kauli ya Allah (s.w.t):

مَا نَنسَخْ مِنْ آيَةٍ أَوْ نُنسِهَا نَأْتِ بِخَيْرٍ مِّنْهَا أَوْ مِثْلِهَا ﴿١٠٦﴾

"Hatufuti Ayah au kuisahaulisha isipokuwa tutaleta iliyo bora zaidi au mfano wake .”(Al-Baqarah 02:106)

Na ambacho kinaweza kuwa ni kisingizio cha ijtihad ya 'Umar katika kuharamisha ndoa ya Mut'a ni kwamba, mmoja wa Waislamu jina lake ni 'Amr bin Harith alitumia vibaya Shariah hii, hivyo akachokoza hasira za 'Umar na ikampelekea kuharamisha huku. Na dalili kuhusu haya ni riwayah ambayo ameipokea Muslim katika Sahih yake kutoka kwa Ja'abir: "Tulikuwa tunafanya mut'a kwa kutoa kiasi cha tende na unga wakati wa Mtume(s.a.w.w) na Abubakr na Umar, mpaka alipokataza kutokana na jambo la 'Amr bin Hurayth.[235]

Na ameitoa Tabarani na Tha'alabi katika tafsiri zao kwa isnad ya Al- Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema: "Kama asingekataza 'Umar Mut’a, basi asingezini isipokuwa mwovu.”[236]

Na katika riwayah nyingine isipokuwa wachache.

Baada ya riwayah zote hizi ambazo zinathibitisha hukumu ya ndoa ya Mut'a, na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kutoikataza, na kubaki kwake halali hadi alipoharamisha 'Umar wakati wa ukhalifa wake, hatupati ufumbuzi wa tatizo hili, isipokuwa 'Umar amefanya ijtihad kwa rai yake kwa ajili ya maslahi aliyoyaona - kwa mtazamo wake - kwa Waislamu katika wakati wake na siku zake, yaliyo sababisha kuzuia kufanya Mut'a.

Kuzuia huko ni kwa kijamii na wala sio kwa kidini kwa ajili ya maslahi ya muda, kwa sababu 'Umar ana cheo kikubwa na alikuwa na daraja kitawala, hawezi kuharamisha alichokihalalisha Allah (s.w.t) au kuingiza kitu katika dini naye anajua kuwa halali ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ni halali hadi siku ya Qiyamah, na haramu ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ni haramu hadi siku ya Qiyamah.

Hivyo ni lazima makusudio yake ya kukataza yawe ya muda na ni kuharamisha kwa kijamii na wala siyo kwa kidini. Na msimamo wake huu mkali katika jambo la ndoa ya Mut'a sio wa kwanza katika aina yake kwani amejulikana kwa ukali na ugumu katika mambo yake yote. Anafanya ijtihad katika hilo kwa kutaka kupata maslahi bora zaidi - kwa mtazamo wake - kwa ajili ya Uislamu na kusimamisha Shariah. Na miongoni mwa mifano katika ijtihad ya 'Umar katika hukumu na ukali wake, ni amri yake kwa Waislamu kusali Sala ya Ramadhani (tarawih) katika jamaa baada ya kuwa inasaliwa furada (mmoja mmoja) wakati wa Mtume wa Allah(s.a.w.w) .

Kutoka kwa Abu Huraira: "Hakika Mtume wa Allah (s.a.w.w.) amesema mwenye kusali Sunnah ya Ramadhani kwa imani na kutaka thawabu anasamehewa yaliyo tangulia katika dhambi zake." Ibnu Shihab amesema: "Mtume wa Allah(s.a.w.w) amefariki na watu wanafanya hivyo, kisha mambo yalikuwa vivyo hivyo katika zama za Abubakr na mwanzo wa zama za 'Umar (r.a.)."

Akasema (Ibn Shihab): "Nilitoka pamoja na 'Umar Al-Khattab usiku wa mwezi wa Ramadhani kwenda msikitini basi tukakuta watu wametapakaa na wametawanyika, kila mtu anasali peke yake na mtu anasali na kundi linasali nyuma yake, 'Umar akasema mimi naona kama nitawakusanya hawa kwa msomaji mmoja ingekuwa ni bora.

Kisha akaazimia, akawakusanya kwa 'Ubay bin Ka'ab, kisha nilitoka pamoja naye usiku mwingine na watu wanasali kwa sala ya msomaji wao, 'Umar akasema: "Bida'a nzuri ni hii na wale wanaolala (wakasali usiku) ni bora kuliko wanaoisali (sasa), amekusudia mwisho wa usiku na watu walikuwa wanasali mwanzo wa usiku.”[237]

Vile vile amefanya ijtihadi katika Sunnah hiyo ambayo imeitwa sala ya tarawih kwa kuongeza idadi ya raka'a zake hadi kufikia ishirini. Kutoka kwa 'Abdurahman kwamba amempa habari kwamba yeye alimwuliza 'Aisha Sala ya Mtume wa Allah(s.a.w.w) ilikuwaje katika mwezi wa Ramadhani?" Akasema: "Mtume wa Allah(s.a.w.w) hakuwa anazidisha katika Ramadhani wala katika mwezi mwingine zaidi ya raka'a kumi na moja."[238]

Lakini baadhi ya walioishi wakati wa khalifa na walio kuja baada yake baadhi ya muhadithin wajinga, waliona ni jambo kubwa mno kuwa ameharamisha alichokihalalisha Allah (s.w.t) na wakalazimika kutoa kisingizio kwa ajili ya hilo. Hivyo hawakupata isipokuwa madai ya nasikh kutoka kwa Nabii baada ya kuhalalishwa, basi wakagongana mgongano huo na kauli zao zikapingana mpingano huo.

Tazama riwayah ifuatayo ili uone upeo wa mgongano na mgawanyiko ambao tunauzungumzia, na mshangao ni kwamba wazushi wa riwayah hiyo wameinasibisha kwa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) na watoto wake.

Kutoka kwa Zuhri kutoka kwa Hassan na 'Abdillah watoto wa Muhammad bin 'Ali kutoka kwa baba yao: Hakika Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) aliambiwa kuwa Ibn 'Abbas haoni ubaya wa Mut'a ya wanawake, akasema: 'Hakika Mtume wa Allah(s.a.w.w) ameikataza siku ya Khaibar, pamoja na nyama ya punda wa nyumbani', na baadhi ya watu wakasema na kama atafanya hila hadi akafanya Mut'a basi ndoa itakuwa ni batil na baadhi yao wamesema: "Ndoa inajuzu na sharti litakuwa batili."[239]

Kama hawa wangefahamu sababu ya khalifa kukataza Mut'a hilo lingewatosha kutokana na mgawanyiko na kutokuendelea.

Hakika mtazamo wa ndoa ya Mut'a uliotangulia ulikuwa ni kwa pande mbili; kidini na kihistoria. Ama mtazamo katika upande wa tabia ya kijamii kuhalalishwa kwake kumekuja kuwa ni rehema kwa wanaadamu na ruhusa kwa walio wengi, na hasa wanaosafiri kwa kutafuta elimu au biashara au wanaopigana jihadi au wanajeshi pamoja na kushindwa kwao kuoa ndoa ya daima, kwa vile mara nyingi kuna vipengele na vitu ambavyo haviendani na hali ya wasafiri, hasa ambao wako katika umri wa ujana na mchemko wa shahawa.

Kwani hali yao haiepukani na mambo mawili, ima subira na kubana nafsi ambako kunasababisha matatizo ambayo yanaleta maradhi ya kudumu na magonjwa ya kinafsi yenye kuangamiza, na mengineyo katika madhara ambayo hayafichikani kwa yeyote, na ima kutumbukia katika zinaa ambayo imejaza dunia kwa ufisadi na madhara. Na imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbas kuhusu suala hilo; " Mut'a haikuwa isipokuwa ni rehema ya Allah (s.w.t) ameuhurumia ‘Ummah wa Muhammed na kama sio kukataza kwake (yaani ‘Umar) asingezini isipokuwa mwovu.”[240]

Na katika yanayotia mkazo dharura ya kitabia na kijamii kwa kuhalalisha aina hii ya ndoa ya muda, ni ambayo baadhi ya Waislamu wametoa Fatwa katika wakati ambao tunao kwa kuruhusu ndoa ya aina nyingine inayomrahisishia msafiri peke yake kutatua matatizo yake katika hali ya kutoweza kuoa ndoa ya daima, na sifa ya ndoa hii ni ya muda kwa upande wa wanaume na ni ya daima kwa upande wa wanawake. Na aliyo kusudia mume katika nafsi yake bila ya yeyote kujua unapomalizika muda, anamshitusha mke wake masikini kwa kumpa talaka.

Hivyo aina hii ya ndoa wameipa jina la "Ndoa kwa nia ya talaka (kuachika)," pamoja na kutambua wale waliozua kuwa huo ni uongo kwa mke na ni udanganyifu na hakuna dalili juu ya hilo katika Kitabu wala Sunnah ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) lakini wao wanafanya kwa hoja ya kuwa madhara yake yatabaki yamefichikana kuliko ufisadi wa zinaa. Yote ni kwa kuwa wao wameamini kubatilika kwa ndoa ya Mut'a ambao uhalali wake umekuja katika Kitabu kitukufu na Sunnah za Mtume na kwa kufanya hivyo watakuwa wamebadilisha bida'a walioizua na hukumu ya Allah (s.w.t). "Je mnabadilisha ambacho ni duni kwa kile kilicho bora." Fala haula wala Quwata illa billahi.

Mut'atul Hajj

Mtume amekwisha ifundisha na akaamuru kutokana na kauli ya Allah (s.w.t) Mtukufu: “Basi atakayefanya umrah ya hijja, hiyo ni kwa ambaye familia yake haiko karibu na Msikiti Mtakatifu wa Makkah.” (Al-Baqarah 02:196)

Na makusudio ya hayo ni 'Umrah katika miezi ya hijja kabla ya hijja, nayo ni faradhi kwa ambaye familia yake iko mbali na Makkah. Na imeitwa Tamattu ya hijja kwa yale yaliyomo humo katika kujifurahisha, (yaani raha ya kuhalalishiwa makatazo ya Ihraam katika muda uliopo baina ya Ihraam mbili - Ihraam ya umrah Tamattu na Ihraam ya hijja. Na hayo ni ambayo 'Umar aliyachukia pia, na akayakataza pamoja na kuwa Mtume(s.a.w.w) alifariki bila ya kukataza.

Kutoka kwa Sa'id bin Mussayib amesema: "Ali(a.s) alikhitilafiana na 'Uthman na wao wako katika kuhirimia 'Umrah Tamattu. 'Ali(a.s) akasema: 'Hataki isipokuwa kukataza jambo alilolifanya Nabii(s.a.w.w) .' 'Ali(a.s) alipoona hivyo akahirimia zote mbili."[241]

Kutoka kwa Al-Hakim amesema: "Niliwaona 'Ali(a.s) na 'Uthman , na (huku) 'Uthman anakataza Mut'a na kuunganisha baina yake, 'Ali(a.s) alipoona akapaza sauti kwa vyote viwili: " Labayka bi umrati wa hajjati. " Akasema: 'Sikuwa ni mwenye kuacha Sunnah ya Nabii kwa kauli ya yeyote.”[242]

Ama udhr wa 'Uthman katika rai yake hiyo ni kwa kuwa yeye alikubali sharti kabla ya kupewa bay'a ya kuwa khalifa, Abdulrahman bin 'Auf alitoa sharti kwa wosia kutoka kwa 'Umar, ahukumu kwa Kitabu cha Allah (s.w.t)

Sunnah za Nabii wake na kwa mwenendo wa masheikh wawili kama ilivyo tangulia katika sehemu iliyo tangulia. Na imepokewa kwa tawatur kauli ya 'Umar: "Mut'a mbili zilizo kuwepo wakati wa Mtume wa Allah(s.a.w.w) mimi nazikataza” [243] 18 na anakusudia kwa kauli yako hiyo Mut’a ya wanawake na Mu’ta ya Hijja.

Na maneno ya 'Umar yanadhihirisha uamuzi wa hukumu hizo ni wake,na wala sio wa mwengine, kwani yeye anakiri kuwa Mut'a mbili zilizokuwa katika wakati wa Nabii(s.a.w.w) .

Na hakunasibisha kukataza kwake kwa Mtume bali amekataza yeye mwenyewe kwa kauli yake "na mimi nakataza" na Allah (s.w.t) amrehemu aliyesema kuhusu Hadith ya mwisho kuhusu 'Umar "Tumekubali ushahidi wake lakini hatujakubali kuharamisha kwake."

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYA

SEHEMU YA SITA

TAQIYYAH

Taqiyyah ni mwanadamu kuficha ukweli wa imani yake, ili kujihifadhi katika sehemu za hatari anapohisi kuwa kuna hatari kwa nafsi yake au mali yake, kwa sababu ya kutangaza itikadi (imani) yake au kujidhihirisha nayo. Na kumepatikana baadhi ya watu wanaotuhumu Shi'a kwa itikadi (imani) yao ya Taqiyyah kwa ujahili wao wa kutojua maana yake, nafasi yake na makusudio yake. Na kama wangefanya uchunguzi katika jambo (hili) na kufahamu hukumu, wangejua kuwa Taqiyyah ambayo wanaisema Shi'a haiwahusu wao tu, wala sio wao peke yao wanaosema hivyo, bali ni jambo la dharura la kiakili.

Matakwa ya binadamu na Shariah ya Kiislamu na kila mwanadamu analazimika kutetea nafsi yake na kuhifadhi maisha yake, navyo ni vitu vitukufu mno kwake na anavyo vipenda zaidi. Ni kweli wakati mwingine inakuwa rahisi kuvitoa katika njia ya utukufu na kuhifadhi heshima na kulinda haki.

Lakini katika yasiyokuwa makusudio haya na malengo matukufu, kufanya israf kwayo na kujitumbukiza katika sehemu za hatari ni ujinga na upumbavu, akili hairidhii wala Shariah. Na Uislamu umemruhusu Mwislamu katika sehemu za hofu, kuficha haki na kuifanyia kazi kwa siri mpaka dola ya haki inusurike katika dola ya batili. Kulingana na kauli yake Allah (s.w.t):

"isipokuwa mkiogopa kwao madhara .”(Ali-Imran 03:28)

Na kauli yake:

"isipokuwa aliye lazimishwa na moyo wake umetulizana kwa imani ". (An-Nahl 16:106).

Na kisa cha 'Ammar na wazazi wake na mateso ya washirikina kwao na baadhi ya Masahaba kwa kuwataka wakubali ushirikina na kudhihirisha kwao ukafiri ni mashuhuri. Na katika kufanya Taqiyyah kuna hukumu tatu:-

1. Wajibu: na hiyo ni ikiwa kuiacha kunasababisha kuangamia nafsi bila ya faida.

2. Ruhusa: ikiwa kuiacha kwake na kudhihirisha haki ni kuipa haki nguvu basi ana hiari kuitoa mhanga nafsi yake.

3. Haramu: na hiyo ni ikiwa kufanya Taqiyyah kunasababisha kueneza batili na kudhalilisha haki na kuihuisha dhulma na ujeuri.

Na ni maarufu kwa wafuasi wa madhehebu ya Shi'a Ithna-'Ashariyyah, na Maimamu wao wamepata balaa na kila aina ya dhiki katika uhuru wao katika zama zote ambazo madhehebu yoyote au 'Ummah wowote ule haujapata. Hivyo walilazimika katika wakati mwingi wa zama zao kutumia Taqiyyah kwa kuwaficha wanao wakhalifu kwa yale ambayo yangeleta madhara katika dini na dunia, na kwa sababu hii wamejulikana sana kwa Taqiyyah kuliko wasiokuwa wao.

Mwisho

Tumekwisha bainisha katika sehemu za utafiti huu yaliyo muhimu zaidi, ambayo kumetokea hitilafu baina ya Sunni na Shi'a, na tukabainisha njia ya sawa humo kwa kueleza dalili nyingi na hoja ambazo nyingine zimechukuliwa katika Sahih Bukhari.

Nayo ni ambayo inazingatiwa kuwa ni Kitabu muhimu cha marejeo na kinachoaminika kwa Ahl as-Sunnah baada ya Kitabu cha Allah (s.w.t), na haikuwa kuandika kwetu kurasa hizi kwa njia hii ambayo pengine inawaumiza baadhi ya watu, isipokuwa ni wasila (njia).

Tumelazimika kuitumia baada ya waongo kuvuka mpaka kwa upeo wa uongo na upotovu; wamekwisha turushia (sisi Mashi'a) tuhuma, na uongo mbaya zaidi miongoni mwa tuhuma hizo ni ushirikina, umajusi, unasara na uyahudi; mpaka wametoa Fatwa juu ya ukafiri wetu.

Na Mawahhabi wamechukua jukumu la mwelekeo huu mwovu ambao umesababisha kuzuka fitina hii kubwa baina ya Waislamu, na kuwapoteza wasiojua miongoni mwao kwa kutumia kila njia isiyokuwa ya kisheria miongoni mwa uongo na udanganyifu katika mambo ili kufikia malengo yao ya kutenganisha 'Ummah na kuwaridhisha mabwana zao ambao kumewakasirisha kuona Uislamu unameremeta na kuamka tena kutoka katika usingizi wake wa upotofu.

Vinginevyo kwa nini hatukuona aina hii ya fitina inakua na kumea isipokuwa baada ya kufaulu kwa mapinduzi matukufu ya Kiislamu nchini Iran? Mapinduzi hayo ambayo yametikisa utawala wa madhalimu na madikteta na ambayo Waislamu wote walipata matumaini, pamoja na tofauti zao za madhehebu. Baada ya kheri na matumaini ya kuchukua hatamu za haraka, katika njia ya kuwarejesha Waislamu katika nguvu na utukufu wao baada ya kuwa dhalili, 'Ummah zinageuzwa geuzwa kama chakula kinavyogeuzwa geuzwa juu ya sahani.

Maadui wa Uislamu walipokosa njia yenye mafanikio katika kuwaweka mbali Waislamu na mapinduzi haya, wamejaribu kutia shaka katika itikadi ya watu wake baada ya kushindwa vibaya sana kuvunjika hayo kwa Helikopta zao ambazo Allah (s.w.t) aliuwezesha mchanga wa jangwani kuziharibu na kuzisambaratisha, na kuharibu mbinu zao katika vita vyao ambavyo walipanga kupitia mamluki wao mtiifu ambaye walimvalisha vazi la utaifa hakuvuna isipokuwa hasara na fedheha katika mwito wake mwovu wa utaifa.

Amesema Sheikh mwanajihadi Abdulhamid Kishki, katika mazungumzo yake ya kujibu kauli ya mwovu huyo mwenye kuajiriwa: "Kwamba watu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wao ni Wafursi tu, hawajui Uislam wala Qur'an ambayo imeteremka kwa Waarabu na lugha yao, hivyo wao wanajua zaidi kuliko watu wengine wasio kuwa Waarabu kwa kusema kuwa Shi'a wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni Waislamu wenye kumpwekesha Allah (s.w.t) na Uislamu wao umekuwa mzuri tangu walipoingia katika Uislamu katika zama za 'Umar."[244]

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alishabashiri tangu karne ya kumi na nne, watu hawa ambao walipokea Uislamu na kuupeleka katika taifa hili la Kiislamu lililopo sasa, katika Hadith ambayo ameitoa Bukhari katika Sahih yake.

Kutoka kwa Thaur kutoka kwa Abu Huraira amesema: "Tulikuwa tumekaa kwa Mtume(s.a.w.w) , basi akateremshiwa Surah al-Jumuah (na wengine miongoni mwao bado hawajajiunga nao) akasema: 'Nilisema nani hawa ewe Mtume wa Allah(s.a.w.w) hakumjibu hadi akauliza mara tatu na alikuwepo pamoja nasi Salman Al-Farsi akaweka mkono wake juu ya Salman, kisha akasema kama imani ingekuwa kwenye sayari basi wangeifikia wanaume au mwanamume katika hawa."[245]

Na Allah (s.w.t) ameashiria katika Kitabu chake kitukufu juu ya watu hawa kwa kauli Yake: "Ninyi ndiyo mnalinganiwa ili mtoe katika njia ya Allah (s.w.t) miongoni mwenu kuna wanaofanya ubakhili na anaefanya ubakhili hakika anafanya ubakhili kwa nafsi yake na Allah (s.w.t) ni tajiri na nyinyi ni mafakiri na kama mtakataa ataleta watu wengine, kisha hawatakuwa mfano wenu."[246]

Kutoka kwa Abu Huraira: "Hakika Mtume(s.a.w.w) alisoma Ayah hii (na kama mtakataa ataleta watu wengine kisha hawatakuwa mfano wenu)." Wakasema: "Ewe Mtume wa Allah(s.a.w.w) nani hao ambao kama tutakataa wataletwa baada yetu kisha hawatakuwa mfano wetu?" Basi akapiga juu ya paja la Salman kisha akasema: "Huyu na watu wake na kama dini ingekuwa katika sayari basi wangeifikia wanaume kutoka Farsi (Jamhuri ya Kiislamu ya Iran)."[247]

Lakini maadui wa Uislamu hawakukata tamaa baada ya kushindwa kwao katika uwanja wa mapambano na bado wanazo nafasi nyingine wanazopigana na huu ndiyo Uwahhabi umeshika nafasi ile ile.

Lakini kwa mara hii ni kwa silaha tofauti, wameshawavalisha askari wao vazi la Uislamu huenda ukawa unang'ara zaidi kuliko vazi la utaifa ambao umegeuka kuwa majivu katika upande wao wa mashariki.

Hila mpya kwa masikitiko makubwa imewakumba baadhi ya watu wasiojua, na wengi wametumbukia katika mtego wa fitina hii, ambayo hawajui itawapeleka wapi! "siku ambayo haitafaa mali wala watoto isipokuwa yule atakaye mwendea Allah kwa moyo safi."

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alishatahadharisha hadhari kubwa kutokutumbukia kwenye moto wa fitina hii, kama wangekuwa wanajua Sunnah zake katika Hadith nyingi ambazo amebainisha humo hata wale watakao isababisha kama ilivyo katika Hadith aliyoitoa Bukhari katika Sahih kutoka kwa Naf'i kutoka kwa Ibn 'Umar amesema:”

Mtume(s.a.w.w) alisema: "Ewe Allah! Tubariki sisi katika Sham. Ewe Allah! Tubariki sisi katika Yemen." Wakasema: "Na katika Najd?" Akasema: "Ewe Allah! Tubariki sisi katika Sham. Ewe Allah! Tubariki sisi katika Yemen." Wakasema: "Ewe Mtume wa Allah! Na katika Najd?" Alisema mara tatu: "Huko kuna tetemeko na fitina na huko kutachomoza upembe wa Shetani.”[248]

Na kundi lililokusudiwa katika Hadith iliyotangulia hatuoni isipokuwa linaafikiana na kundi la Mawahhabi ambalo muasisi wake ni Muhammad bin Abdul-Wahhab amezaliwa katika moja ya vijiji vya Najd kinachoitwa Uyainah. Kundi hili ambalo limekuwa ni tezi la kansa katika jamii ya Kiislamu na kukua kwake na kuendelea kwa juhudi zake za kubomoa katika njia ya kurejea Uislamu mtukufu; kwa hakika si lingine isipokuwa ni fitina nyuma yake umesimama ukoloni mwovu kama ambavyo historia yake inaonyesha hivyo na unalenga kwenye:-

1. Kubomoa shakhsiyyati (watu muhimu) za kidini kwa kuzuia watu kuwa karibu yao na kuwa karibu na athari na misingi yao.

2. Kutoa Uislamu kwa sura ya dini kavu isiyo na maendeleo ambayo haikubali kutekelezeka katika zama mbali mbali.

3. Kutengeneza vikundi na hitilafu katika safu za Waislamu kwa kuzuia umoja na udugu wao.

Na wameichukulia Tawhid kuwa ni uwanja wa malengo yao maovu kwa kutuhumu madhebu mengine kwa ushirikina kwa kudai kwamba tawassul kwa Manabii na watu wema ni chanzo cha ushirikina, wakapinga kwa hilo yaliyo pokewa kutoka kwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) kwa tawatur kwa kuruhusu hilo.

Na yanatutosha aliyoyatoa Bukhari katika Sahih yake juu Tawassul ya 'Umar kwa 'Abbas. Kutoka kwa Anas: "Hakika 'Umar al-Khattab alikuwa wakipatwa na ukame akimwomba 'Abbas bin 'Abdul-Muttalib awaombee mvua akasema: "

Ewe Allah (s.w.t) hakika sisi tulikuwa tuna-tawasali kwako kupitia kwa Nabii(s.a.w.w) wetu na unatunyesheleza, na hakika sisi tuna-tawasali kwako kupitia kwa Ami wa Nabii wetu basi tunyesheleze akasema: 'Basi wanateremshiwa mvua.'"[249]

Bali inatosha kwa kuwajibu Mawahhabi kwa kauli yake alama zao[250] ni kunyoa (wanawake vipara). Kama alivyopokea hayo Bukhari katika Sahih yake, hakika hakufanya hayo yeyote miongoni mwa wazushi isipokuwa wao kama ilivyo julikana hivyo katika historia yao.[251]

Na katika Hadith nyingine Nabii alibainisha maelekezo yake ya kinabii kwa watu katika yaliyo " wajib kuyafanya wakati zinapotokea fitna " kama hizi; anasema watu walikuwa wanamwuliza Mtume wa Allah(s.a.w.w) kuhusu kheri na nilikuwa namwuliza kuhusu shari kwa kuogopa isije ikanifika.

Nikasema:"Ewe Mtume wa Allah(s.a.w.w) ! Hakika sisi tulikuwa katika ujahili (ujinga) na shari, Allah (s.w.t) akatuletea kheri hii je baada ya kheri hii kuna shari?"

Akasema: "Ndiyo!"

Nikasema:"Je baada ya shari hiyo kuna kheri?"

Akasema: "Ndiyo na kuna dakhani (wanaoongoza bila ya uongofu)."

Nikasema:"Je dakhani ni nini?"

Akasema: "Ni watu wanaoongoza bila ya uongofu, baadhi yao utawajua na baadhi yao hutawajua."

Nikasema:"Je! baada ya kheri hiyo kuna shari?"

Akasema: "Ndiyo, wenye kulingania katika milango ya Jahannam atakaye waitikia watamtupia humo."

Nikasema:"Ewe Mtume wa Allah (s.a.w.w.)! Tupe sifa zao."

Akasema: "Wao ni katika kabila letu, wanazungumza lugha yetu."

Nikasema:"Unaniamuru nini kama hayo yatanifikia?"

Akasema: "Jilazimishe na jamaa ya Waislamu na Imam wao.

Nikasema:"Na kama hawatakuwa na jamaa wala Imam?"

Akasema: "Basi jitenge na kundi hilo lote hata kama ni kung'ang'ania shina la mti hadi mauti yakufikie na wewe uko hapo."[252]

Na Hadith ya hapo juu inabainisha wazi wajibu wa kujilazimisha kushikamana na jamaa ya Kiislamu na Imam wao, na kwamba katika hali ya mkanganyiko wa mambo kutofahamika na kutowezekana kujua uhakika wake.

Basi maelezo ya Nabii yanatuamuru kunyamaza na vile vile Hadith inabainisha kuwa walinganiaji katika milango ya Jahannam atakaye waitikia watamtupia humo sio katika Waajemi bali ni katika Waarabu, na haya yanatilia mkazo yaliokuja katika Hadith iliyotangulia (kutoka Najd).

Jambo hili lazima limfanye Mwislamu awe katika hali ya uangalifu sana na tahadhari kwa kufuata mwendo unao mpelekea kwenye usalama katika Sunnah ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , na hasa pamoja na kuwepo makundi mengi ambayo idadi yake ni sabini na tatu, kila moja linadai kuwa kunukuu kwake Sunnah za Nabii(s.a.w.w) ni sahih na amekwishatupa habari ambaye hatamki kwa matamanio yake kuwa kundi moja tu ndilo Sahihi na mengine sio Sahih.

Hivi ndivyo zilivyo patikana tofauti na Ikhtilaf hadi Waislamu wakawa wanatahayari na wenye kushangaa kwa yote yanayotendeka pembezoni mwao, miongoni mwa zogo hili kubwa na fitina kubwa.

Na mimi sishangai tahayari hii na mshangao huu, kwani Nabii wa Uislam amekwisha ashiria kuhusu jambo hili kwa kauli yake: "Uislamu umeanza katika hali ya ugeni na utarejea kuwa mgeni kama ulivyoanza." Je, ugeni hauko katika Waislamu kumpiga vita yule ambaye ni Mwislamu halisi? Je, sio ugeni! Na mshangao zaidi kwa watoa mawaidha kusimama na vilemba vyao juu ya mimbar na kupaaza sauti na hali wakiwakufurisha ambao ni Waislamu halisi?

Ewe Mtume wa Allah(s.a.w.w) umesema kweli na hawa ndio Waislamu wanawapiga vita na kuwakufurisha Mashi'a (wafuasi wako) ambao wameshikamana na Sunnah zako kupitia katika njia ya viumbe watoharifu zaidi (Ahlul Bayt(a.s) baada yako. Hakika wao wanampiga vita huyu mwenye kurejea na watu wake wamekuwa wageni katika kundi la Waislamu na wamepotoshwa na kupelekwa katika njia ya wale ulio tahadharisha kuwa ndiyo machomozo ya upembe wa Shetani, tetemeko na fitina. Na ulishasema kuwa kundi katika 'Ummah wangu halitaacha kudhihirisha haki, hata wadhuru atakaye wakhalifu mpaka itakapokuja amri ya Allah (s.w.t.) kulingana na kauli ya Allah (s.w.t.):

لَقَدْ جِئْنَاكُم بِالْحَقِّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَكُمْ لِلْحَقِّ كَارِهُونَ ﴿٧٨﴾

"Tumekwisha wajieni kwa haki, lakini wengi wenu wanaichukia haki.”(Az-Zukhruf 43:78)

Na umekwisha mbashiri Mahdi wa Aali Muhammad mjukuu wako na wasii wako, Imam wa kumi na mbili (Al Imam Muhammad Mahdi Sahib az-Zamaan(a.s) ambaye atajaza dunia haki na uadilifu, baada ya kujazwa dhulma na jawr (ujeuri) na umetuamuru kuelekea kwake hata kama ni kwa kutembea juu ya theluji kwa kauli yako: "Hakika sisi ni Ahlul-Bayt; Allah (s.w.t) ametuchagulia akhera dhidi ya dunia, na hakika watu wa nyumba yangu watapata baada yangu tabu, shida na kufukuzwa katika nchi, mpaka watakuja watu, (kutoka hapa akaashiria kwa mkono wake upande wa mashariki) watu wenye bendera nyeusi, wataombwa haki, lakini hawataitoa watapigana, basi watanusurika na watapewa wayatakayo hawatakubal,i hadi wampe mwanamme katika watu wangu. Basi ataijaza dunia uadilifu kama ilivyojazwa dhuluma, basi atakaye fikiwa na huyo amwendee, hata kama ni kwa kutembea juu ya theluji.[253]

Mwisho wa ulingano wetu tunamwomba Allah (s.w.t), atuja'alie kuwa miongoni mwa ambao wanasikiliza kauli, wakafuata mazuri yake. Na shukurani njema ni za Allah (s.w.t) Mola wa viumbe, sala na salamu zimwendee Bwana wetu Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na Ahlul Bayt zake watoharifu.

Wassalamu ‘alaykum wa Rahmatullahi wa Barakatuh

SHARTI YA KUCHAPA

Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.

MWISHO WA KITABU

YALIYOMO

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYA 1

KIMEANDIKWA NA: DR. ‘ASAD WAHID AL-QAASIM 1

KIMEATAFSIRIWA NA: ABDUL KARIM J. NKUSUI 1

KUHUSU MTUNGAJI 1

NENO LA MCHAPISHAJI 2

DIBAJI YA MTARJUM 3

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYA 4

KIMEANDIKWA NA: DR. ‘ASAD WAHID AL-QAASIM 4

KIMEATAFSIRIWA NA: ABDUL KARIM J. NKUSUI 4

NATOA ZAWADI YA KITABU HIKI 4

Je, Tunahitaji Kujifunza Namna Ya Kufikiri? 6

Dhana Nzuri Ya Moja Kwa Moja Kwa Maulamaa Walio Tangulia Mara Nyingine Inamwongoza Mtafiti Kwenye Upotovu 7

Wako wapi wao kati ya Maulamaa wajuzi ambao wametoa Fatwa juu ya Uislamu mzuri wa Shi’a? 8

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYA 9

KIMEANDIKWA NA: DR. ‘ASAD WAHID AL-QAASIM 9

KIMEATAFSIRIWA NA: ABDUL KARIM J. NKUSUI 9

UTANGULIZI 9

NI NANI SHI’A ITHNA-’ASHARIYYAH? 9

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYA 12

SEHEMU YA KWANZA: UIMAMU 12

Kwanza: Hoja Za Kuthibitisha Uimamu Wa Ahlul- Bayt (A.S.) 12

Hadith Ya ‘Ummu Salamah Katika Mapokezi Ya Bukhari 14

Uchunguzi Juu Ya Ayah Ya “Tat-Hiir” 16

Pili -Dalili Za Kuthibitisha Idadi Ya Maimamu Wa Ahlul Bayt (A.S.) Ni Kumi Na Mbili 18

Tatu-Hoja Za Kuthibitisha Kupewa Ukhalifa Al Imam ‘Ali Ibn Abi Talib (A.S.) 19

Kukhalifu Kwa Jamhuri Ya Waislamu Nasi (Pokezi) Za Uimamu 24

Kwanza- Baadhi Ya Masahaba Kumkataza Mtume Wa Allah (s.a.w.w) Kuandika Wosia 25

Pili- Baadhi Ya Masahaba Kukhalifu Jeshi La Usamah Na Kukosoa Kupewa Kwake Uongozi 28

Tatu -Matukio Ya Saqifah Na Bay’ia Ya Abubakr 29

Hasira (Ghadhabu) Ya Bibi Fatimah Az-Zahra(A.S) 32

Je, Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w) Alidokeza Juu Ya Abubakr Kupewa Ukhalifa? 35

Je, Bi.Fatimah Az-Zahra (A.S.) Alikufa Kifo Cha Kijahiliyyah (Kikafiri)? 35

Nne: ‘Umar Kupewa Ukhalifa Na Bay’ia Yake 37

Tano-Shura Na Bayi’a Ya ‘Uthman Bin ‘Affan 38

Kuuliwa Kwa ‘Uthman Bin ‘Affan 39

Bai’a Ya Al-Imam ‘Ali Ibn Abi Talib(A.S) 41

Sita- Tukio La Jamal Na Kutoka Kwa ‘Aisha 41

Uzushi Wa ‘‘Abdallah Bin Saba’ 43

ORODHA YA WAPOKEZI WA UONGO WA SABA’100 45

MZUSHI WAKE NI SEIF BIN ‘AMRU AT-TAMIMIY ALIYEFARIKI MWAKA WA 170 HIJRIYYAH. WAPOKEZI WAKE:- 45

Saba: Vita Vya Siffin Na Uasi Wa Mu’awiyah Bin Abi Sufian 45

Nane-Kufa Shahid Kwa Al-Imam ‘Ali Ibn Abi Talib(A.S ) 48

Al Imam Hasan Ibn ‘Ali Ibn Abi Talib(a.s) Na Suluhu Ya Mu’awiyah Bin Abi Sufian 48

Tisa: Kufa Shahid Kwa Al-Imam Hasan Ibn ‘Ali Ibn Abi Talib(a.s) 49

Kumi: Thawrah (Mapambano) Ya Karbala Na Kufa Shahid Kwa Al Imam Hussein Ibn ‘Ali Ibn Abi Talib(a.s) 50

Shura Baina Ya Misingi Na Utekelezaji 53

1. Ukhalifa Wa Abubakr Ibn Abu Quhafa 54

2. Zama Za ‘Umar 54

3. Zama Za ‘Uthman Bin ‘‘Affan 54

4. Zama Za Mu’awiyah Bin Abi Sufian 54

5. Zama Za Yazid Bin Mu’awiyah Bin Abi Sufian 54

Mwisho Wa Utafiti Wa Uimamu 55

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYA 57

SEHEMU YA PILI 57

UADILIFU WA MASAHABA 57

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYA 66

SEHEMU YA TATU 66

SHI'A NA QUR'AN TUKUFU 66

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYA 71

SEHEMU YA NNE 71

SHI'A NA SUNNAH TUKUFU ZA NABII (S.A.W.W) 71

Kuondoa Shaka Kuhusu Uma'asum Wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w) 72

Abu Huraira Na Wingi Wa Riwayah Zake Katika Hadith 79

Kisimamo Pamoja Na Bukhari Katika Sahih Yake 85

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYA 89

SEHEMU YA TANO 89

NDOA YA MUDA 89

Mut'atul Hajj 94

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYA 96

SEHEMU YA SITA 96

TAQIYYAH 96

Mwisho 96

SHARTI YA KUCHAPA 101

MWISHO WA KITABU 101

YALIYOMO 102

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYA

SEHEMU YA PILI

UADILIFU WA MASAHABA

Maneno yamekuwa mengi kuhusu uadilifu wa Masahaba, na watu katika hilo wamekhitalafiana Ikhtilaf kubwa. Ahl as-Sunnah wanaona kuwa Masahaba wote ni waadilifu hawatuhumiwi wala haijuzu kwa yeyote kuwakosoa, au kushuku katika mapokezi yao katika Hadith za Mtume wa Allah(s.a.w.w ) . Na anayefanya hivyo wanatoa Fatwa juu ya ufasiki wake na wanazingatia kuwa ni zandiki, na wao kwa hilo wanajilazimisha kwa kila alicho kipokea Sahaba, kwa mfano inatosha kwao kukubali Hadith iliyopokelewa kwa Sahaba yeyote yule, na Sahaba kwao ni kama alivyoeleza Al-Bukhari: “Ni ambaye alifuatana na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) au aliye mwona miongoni mwa Waislamu.”

Na wala sioni katika hukumu yao hiyo katika ufasiki wa kila anaye mkosoa yeyote miongoni mwa Masahaba, isipokuwa ni israf katika kuamini na ni kupinga Kitabu cha Allah (s.w.t), Sunnah za Nabii wake na tabia ya binadamu kama tutakavyo thibitisha hayo katika kurasa zinazofuata.

Hakika wanayo singiziwa Shi’a kwamba wao wanakufurisha Masahaba wote, kwa kuongeza kuwatukana kwao na kuwalaani, hayo si kingine isipokuwa ni uongo ulio wazi na wala hauna usahihi wowote. Shi’a hawawakufurishi Masahaba lakini wanaona kuwa wao wanaweza kukosolewa na kurekebishwa na kwamba wote hawakuwa katika daraja moja ya uadilifu, na kumkosoa kwao Sahaba huyu au yule haina maana ya kuwakufurisha, kama wanavyoeneza baadhi ya wapumbavu, na kama ukosoaji wao umesimama juu ya dalili, sasa hasira ni ya nini? Na kelele yote hii ni ya nini?

Katika Masahaba kuna waumini walio wema, Allah (s.w.t) amewasifu katika Qur’an tukufu kwa kauli yake:

لَّقَدْ رَضِيَ اللَّـهُ عَنِ الْمُؤْمِنِينَ إِذْ يُبَايِعُونَكَ تَحْتَ الشَّجَرَةِ فَعَلِمَ مَا فِي قُلُوبِهِمْ فَأَنزَلَ السَّكِينَةَ عَلَيْهِمْ وَأَثَابَهُمْ فَتْحًا قَرِيبًا ﴿١٨﴾

Kwa hakika Mwenyezi Mungu amewapa radhi Waumini walipo fungamana nawe chini ya mti, na alijua yaliyomo nyoyoni mwao. Basi akateremsha utulivu juu yao, na akawalipa kwa Ushindi wa karibu . (Al-Fath 48:18)

Hivyo Allah (s.w.t) amewasifu tu waumini mahsusi, kati ya waliohudhuria tukio la Bay’atus-Shajarah na hakuwahusisha wanafiki ambao walihudhuria mfano ‘Abdallah bin ‘Ubay na Aus bin Khauli. Na hakuna dalili katika Ayah juu ya Allah (s.w.t) kuridhia Masahaba wote waliobay’i - pamoja na kuwa wao wanawahesabia kuwa ni katika Masahaba kwa madai ya Bukhari na mfano wake - bali haionyeshi juu ya mwisho mwema kwa waumini wote walio bay’i.

Ayah haionyeshi zaidi ya kwamba Allah (s.w.t) ameridhia Bai’a yao hii - yaani ameikubali kutoka kwao - na amewapa thawabu, ridhaa ya Allah (s.w.t) juu ya watu wa Bai’a hii hailazimu ridhaa yake hii kuwa ni daima, na dalili katika hilo ni kauli ya Allah (s.w.t) katika jambo lao

إِنَّ الَّذِينَ يُبَايِعُونَكَ إِنَّمَا يُبَايِعُونَ اللَّـهَ يَدُ اللَّـهِ فَوْقَ أَيْدِيهِمْ ۚ فَمَن نَّكَثَ فَإِنَّمَا يَنكُثُ عَلَىٰ نَفْسِهِ ۖ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِمَا عَاهَدَ عَلَيْهُ اللَّـهَ فَسَيُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿١٠ ﴾

Hakika wale wanaokubay’i wanambay’i Allah (s.w.t) mkono wa Allah (s.w.t) uko juu ya mikono yao na atakaye tengua (Bai’a yake) basi hakika anatengua kwa ajili ya nafsi yake, na atakaye tekeleza aliyomwahidi Allah (s.w.t) basi atampa malipo makubwa”. (Al-Fath 48:10).

Na miongoni mwa Masahaba kuna ambaye Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) ameeleza kuritadi kwake baada ya kufa kwake na kisha kuangamia kwao siku ya Qiyamah kama yanavyo dhihirika wazi hayo katika Hadith mbili zifuatazo chini:-

Sa’ad amesema nimemsikia Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) amesema: “Mimi nitawatangulia katika Hawdh atakaye nifikia atakunywa kwayo na atakaye kunywa hata pata kiu kamwe baada yake, watanijia watu na wajua na wananijua kisha kutawekwa kizuizi baina yangu na wao.”

Akasema nilimsikia akiongezea: Akasema: “Hakika wao ni katika watu wangu, itasemwa: Hakika wewe hujui waliyo yabadilisha baada yako, basi nitasema, awe mbali aliye badilisha baada yangu[113] .”

Amesema ‘Abdillah kwamba amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) : “Mimi nitawatangulia katika Hawdh, hakika wataletwa wanaume mionngoni mwenu mpaka nitakapo karibia ili niwapatie (maji) watazuiwa dhidhi yangu, basi nitasema: Ewe Allah (s.w.t), Masahaba wangu.’ Atasema: ‘Hujui waliyoyazua baado yako[114] .

Na mkazo wa Hadith mbili zilizo tangulia ambazo zinaonyesha kuzua na kubadilisha – yaani kuritaddi - hakika Hadith ifuatayo inawalinganisha na ‘Ummah za Kiyahudi na Kinasara ambao walipotosha maneno katika makusudio yake. (Kutoka kwa Nabii amesema: “Hakika mtafuata nyendo za waliokuwa kabla yenu shibr kwa shibr, dhiraa kwa dhiraa hata kama wataingia katika shimo la kenge mtawafuata.” Nikasema: “Ewe Mtume wa Allah(s.a.w.w ) : “MAyahudi na Manasara?” Akasema: “Ni nani basi?”[115]

Katika Masahaba kuna miongoni mwa aliowaelezea Allah (s.w.t.) katika Kitabu chake kitukufu:

وَإِذَا رَأَوْا تِجَارَةً أَوْ لَهْوًا انفَضُّوا إِلَيْهَا وَتَرَكُوكَ قَائِمًا قُلْ مَا عِندَ اللَّـهِ خَيْرٌ مِّنَ اللَّـهْوِ وَمِنَ التِّجَارَةِ وَاللّ َـهُ خَيْرُ الرَّازِقِينَ ﴿١١﴾

Na wanapoona biashara au upuuzi wanakimbilia huko na wanakuacha umesimama …”(Al-Juma’a 62:11).

Ayah hii imeteremka kwa Masahaba walioondoka msikitini wakati Mtume(s.a.w.w ) amesimama anawahutubia siku ya Ijumaa ulipowasili msafara kutoka Sham na hawakubaki pamoja na Mtume(s.a. w.w ) isipokuwa wanaume kumi na mbili kama inavyodhihirika katika Hadith mbili hapa chini.

Amesema Jaabir ibn Abdillahi: Uliwasili msafara wa ngamia siku ya Ijumaa na sisi tuko pamoja na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) basi watu walitoka isipokuwa wanaume kumi na mbili, basi Allah (s.w.t) akateremsha Ayah; “Na wanapoona biashara au upuuzi wanaenda huko”[116]

Amesema:”Tulipokuwa tunasali pamoja na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) basi ukawasili msafara wa ngamia umebeba chakula wakauendea na hawakubaki pamoja na Nabii isipokuwa wanaume kumi na wawili basi ikateremka Ayah hii (Na wanapoona biashara au upuuzi wanauendea na wanakuacha umesimama)[117] .

Idadi hiyo hiyo - katika mamia yote hayo miongoni mwa Masahaba - walibaki pamoja na Mtume wakati walipokimbia katika vita vya Uhud kiasi kwamba Mtume(s.a.w.w ) alijiweka mbali nao kutokana na kitendo chao.

Amesema: Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) alimpanga ‘Abdallah bin Jubayr katika wapiganaji wanao kwenda kwa miguu siku ya Uhud na wakakimbia waliposhindwa, hivyo Mtume akawa anawaita kwenye Akhera yao, na hawakubaki pamoja na Nabii isipokuwa wanaume kumi na wawili)[118] .

(Kutoka kwa Anas (r.a) amesema: Alitoweka ami yangu Anasi bin Nadhir katika vita vya Badr akasema: Ewe Mtume wa Allah(s.a.w.w) : Nilighibu katika vita vya mwanzo ulivyowapiga washirikina, naapa kama Allah (s.w.t) atanijaalia kupigana vita na washirikina basi Allah (s.w.t) ataona nitakavyofanya.

Siku ya Uhud ilipofika na Waislamu wakashindwa na kukimbia, akasema: “Ewe Allah mimi naomba samahani kwako kwa waliofanya hawa watu, yaani Masahaba wake[119] .”

Na siku ya Hunain kukimbia kwao kulikuwa ni jambo la kushangaza wakati ambapo walikuwa maelfu.

وَيَوْمَ حُنَيْنٍ إِذْ أَعْجَبَتْكُم ْ كَثْرَتُكُمْ فَلَمْ تُغْنِ عَنكُمْ شَيْئًا وَضَاقَتْ عَلَيْكُمُ الْأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ ثُمَّ وَلَّيْتُم مُّدْبِرِينَ ﴿٢٥﴾

Na siku ya Hunain ulipowashangaza wingi wenu na haukuwasaidia kitu chochote na ardhi ikawa finyu kwenu kutokana na mlivyoshambuliwa kisha mkakimbia kurejea nyuma, halafu Allah akateremsha utulivu wake kwa Mtume wake na waumini. ”(At-Taubah 9:25-26).

Na katika masahaba kuna ambao wameteremkiwa na Ayah:

مَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَكُونَ لَهُ أَسْرَىٰ حَتَّىٰ يُثْخِنَ فِي الْأَرْضِ ۚ تُرِيدُونَ عَرَضَ الدُّنْيَا وَاللَّـهُ يُرِيدُ الْ آخِرَةَ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٦٧﴾ لَّوْلَا كِتَابٌ مِّنَ اللَّـهِ سَبَقَ لَمَسَّكُمْ فِيمَا أَخَذْتُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿٦٨ ﴾

Haikuwa kwa Nabii awe na mateka hadi apate dhiki katika ardhi, mnataka utajiri wa kidunia na Allah anataka akhera. Allah ni Mtukufu na ni Mwenye nguvu. Kama si Kitabu kitokacho kwa Allah basi ingekufikieni adhabu kubwa kwa yale mliyoyafanya .(Al-Anfaal 8:67-68).

Ayah hii imeteremka siku ya Badr, au baada yake katika kundi miongoni mwa masahaba. Nabii alikuwa amewataka ushauri ili kuona upeo wa kuwa kwao tayari kwa ajili ya vita-basi maoni yao yakawa ni kuteka ngamia na kilichobebwa na msafara wa Abu Sufian na wala wasipigane kama yanavyo dhihirika hayo katika Hadith ifuatayo ambapo inadhihiri ta’assub yao ya kikabila-na wao ni katika masahaba…hata mbele ya Mtume?

‘Amru amesema: “Nilimsikia Jaabir bin ‘Abdillah (r.a) akisema: ‘Tulikuwa katika vita, Sufian akasema (maneno fulani) katika jeshi, basi mtu mmoja katika Muhajirin akampiga mtu (mwengine) miongoni mwa Ansar, yule mu-Ansar akasema: Enyi Ansar (wenzangu) na (yule mwengine katika) Muhajirin akasema: Enyi Muhajirin (wenzangu), Mtume wa Allah(s.a.w.w ) akasikia hayo akasema: Huu mwito wa kijahili ni wa nini[120] .”

Sa’ad bin Ma’adh akasimama na kusema: “Ewe Mtume wa Allah(s.a.w.w ) nakuomba msamaha kwa hayo kama ni katika Aus tutamkata shingo lake na kama ni katika ndugu zetu wa Khazraj utatuamuru amri yako.” Akasimama Sa’ad bin ‘Ubadah naye ni bwana wa Khazraji na kabla ya hapo alikuwa ni mtu mwema, na alikuwa ameshikwa na ta’assub akasema: “Uongo hutamwua wala hilo huliwezi, akasimama Usiad bin Hadhiri akasema: “Umesema uongo Wallahi tutamuuwa, hakika wewe ni mnafiki unajadili juu ya wanafiki.

Basi ikazuka fujo kati ya Aus na Khazraj mpaka wakataka kupigana na Mtume yuko juu ya mimbar, alishuka akawatuliza hadi wakanyamaza naye akanyamaza[121] .

Na katika Masahaba kuna baadhi yao walikuwa wanamchukia Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) , ambaye kumchukia ni alama ya unafiki kama ilivyoelezwa:

Kutoka kwa Buraydah amesema: Nabii alimtuma ‘Ali kwa Khalidi kuchukua Khums, na nilikuwa namchukia ‘Ali na alikuwa ameshaoga, nikamwambia Khalid, je humwoni huyu? Tulipofika kwa Nabii nikamweleza akasema: “Ewe Buraydah unamchukia ‘Ali?” Nikasema: “Ndiyo,” akasema usimchukie hakika yeye katika Khums ana zaidi ya hayo[122] .

Na miongoni mwao kuna walio mkosoa Mtume katika kumpa uongozi Usama bin Zaid juu yao: - Kutoka kwa ‘Abdillah bin ‘Umar amesema Mtume alituma kikosi na akampa Usama bin Zaid uongozi baadhi ya watu wakakosoa katika kumpa uongozi, Nabii akasema kama mnakosoa katika uongozi wake basi mlikwishakosoa katika uongozi wa baba yake kabla yake[123] .

Na katika Masahaba kuna aliowatoa Nabii katika majilisi yake walipomtuhumu kwa neno baya, naye yuko katika maradhi yake ya mwisho kabla ya kuyaaga maisha ya dunia. Sa’id bin Jubayr alimsikia Ibn ‘Abbas anasema siku ya Alhamisi, ni ipi siku ya Alhamisi, kisha akalia mpaka machozi yake yakaloanisha changarawe nikasema:

“Ewe Ibn ‘‘Abbas ni ipi siku ya Alhamisi?” Akasema: “Mtume alizidiwa na maradhi yake akasema: ‘Nileteeni karatasi niwaandikie maandiko hamtapotea kamwe baada yake’, basi wakazozana na haifai kuzozana mbele ya Mtume, wakasema, ‘ana nini, anaweweseka? Muulizeni’, akasema: ‘Niacheni kwani niliyo nayo ni bora kuliko hayo mnayo niitia[124] .”

Na katika Masahaba kuna waliogombania uongozi baada ya kufariki Mtume mpaka ikafikia kutaka kuchaguliwe viongozi wawili mmoja wa Muhajirin na mwingine wa Ansar.

Kisha akasema; ‘amma ba’ad, sisi ni Ansar wa Allah (s.w.t) na kikosi cha Kiislamu na nyinyi Muhajirin ni kundi na limenyemelea kundi katika kaumu yenu basi wakawa wanataka kututoa katika msingi wetu na kutupokonya uongozi[125] .

Msemaji wa Ansar akasema: Mimi ni shina lake lenye nguvu na tawi lake lenye matunda akasema: Mimi ni shina lake lenye nguvu na tawi lake lenye matunda kwetu kuwe na kiongozi na kwenu kuwe na kiongozi, enyi Maquraish. Basi ugomvi ukawa mkubwa na makelele yakawa mengi mpaka nikatoka na kuacha ikhtilafu[126] .”

Na katika Masahaba kuna Abu Huraira - ambaye tumetenga nafasi yake maalumu katika sehemu ya nne - vile vile kuna Mu’awiyah bin Abi Sufian hivyo rejea tuliyoyataja kuhusiana naye katika sehemu ya kwanza kwa kuongezea hadith nne zifuatazo:-

Kutoka kwa baba yake amesema: Nabii alimtuma Khalid bin Al-Walid kwenda kwa Bani Jadhima akawalinganie Uislamu, basi hawakuweza kusema kwa ufasaha: “Aslamna (tumesilimu) wakawa wanasema: “Sabaana Sabaana” Khalidi akawa anawaua baadhi yao na kuwateka, na kutupa kila mmoja wetu mateka ilipopita siku Khalidi akaturuhusu kila mtu auwe mateka wake: “Nikasema Wallahi sitouwa mateka wangu na wala hatouwa mtu katika wafuasi wangu mateka wake, mpaka tukafika kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) tukamweleza Nabii(s.a.w.w) akanyanyua mikono yake akasema: Ewe Allah, mimi najikinga kwako na aliyoyafanya Khalidi mara mbili[127] .”

Tumeona katika siku ya Hudaibiyyah yaani suluhu ambayo ilikuwa baina ya Nabii na washirikina, na kama tungeona vita basi tungepigana, akaja ‘Umar akasema, je hatuko katika haki? Na wao wako katika batili? Je, watu wetu si wataingia Jannat na watu wao wataingia Jahannam? Akasema: “Ndiyo”, akasema kwa nini tuwe wanyonge katika dini yetu na tunarudi, na Allah bado haja hukumu baina yetu?” Akasema: “Ewe mtoto wa Khattab! Mimi ni Mtume wa Allah (s.w.t) na Allah (s.w.t) hawezi kunipoteza kamwe.”

Akarejea akiwa na hasira, hakusubiri akamwendea Abubakr akasema: “Ewe Abubakr je, hatuko katika haki na wao wako katika batil?” Akasema: “Ewe mtoto wa Khattab, hakika yeye ni Mtume wa Allah, na allah hatampoteza kamwe[128] .”

Hivyo ‘Umar bin Al-Khattab hakuridhika na kupata tumaini kwa majibu ya Mtume akaenda kwa Abubakr na akaeleza upinzani wake pamoja na kwamba haijuzu Nabii kupingwa na yeyote katu.

Kutoka kwa ‘Urwah kutoka kwa ‘Aisha (r.a) amesema Mtume wa Allah(s.a.w.w ) aliingia kwangu nikiwa na wasichana wawili wakiimba wimbo wa jeshi, akajilaza kitandani na akageuza uso wake, akaingia Abubakr akanikemea na akasema zumari za Shetani mbele ya Mtume wa Allah(s.a. w.w) , Mtume wa Allah(s.a.w.w ) akamjia akamwambia waache, alipolala nikawafanyia ishara, wakatoka[129] .”

Habari hii haisihi kwa hali yeyote, kwa sababu Mtume haiwezekani akasikiliza zumari na muziki ukiachilia mbali hayo kutendeka ndani ya nyumba yake, wakati ambapo Abubakr anajizuia kutokana na hayo na kuyaita zumari za Shetani. Je Abubakr ni mchamungu zaidi ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) ? Na habari hii imepokewa kutoka kwa Sahaba; namna gani tutaafiki uadilifu wao na ukweli wao? Kutoka kwa Mulaikah amesema: “Ilikaribia Wema wawili kuangamia: Abubakr na Umar walinyanyua sauti zao mbele ya Nabii ulipowasili msafara wa Bani Tamim”[130] .

Hakika kuwa rafiki wa Nabii sio sifa kubwa kuliko utukufu wa kuoa kwa Nabii. Amesema Allah (s.w.t) kuhusu wanawake:

يَا نِسَاءَ النَّبِيِّ مَن يَأْتِ مِنكُنَّ بِفَاحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍ يُضَاعَفْ لَهَا الْعَذَابُ ضِعْفَيْنِ و َكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرًا ﴿٣٠﴾

Enyi wake wa Nabii atakayefanya miongoni mwenu uovu ulio wazi basi ataongezewa adhabu mara mbili .” (Al-Azhaab 33:30).

ن تَتُوبَا إِلَى اللَّـهِ فَقَدْ صَغَتْ قُلُوبُكُمَا وَإِن تَظَاهَرَا عَلَيْهِ فَإِنَّ اللَّـهَ هُوَ مَوْلَاهُ وَجِبْرِيلُ وَصَالِحُ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمَلَائِكَةُ بَعْدَ ذَٰلِكَ ظَهِيرٌ ﴿٤﴾

Tubuni kwa Mwenyezi mungu kwani nyoyo zenu zimeasi na kama mtasaidiana dhidi yake basi Allah (s.w.t) ni mlinzi wake.” (At-Tahriim 66:04)

ضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا لِّلَّذِينَ كَفَرُوا امْرَأَتَ نُوحٍ وَامْرَأَتَ لُوطٍ كَانَتَا تَحْتَ عَبْدَيْنِ مِنْ عِبَادِنَا صَالِحَيْنِ فَخَانَتَاهُمَا فَلَمْ يُغْنِيَا عَنْهُمَا مِنَ اللَّـهِ شَيْئًا وَقِيلَ ادْخُلَا النَّارَ مَعَ الدَّاخِلِينَ ﴿١٠﴾

Hadi kauli yake “Allah (s.w.t) amepiga mfano kwa wale walio kufuru, mke wa Mtume Nuh(a.s ) na mke wa Mtume Lut(a.s ) walikuwa chini ya waja wawili miongoni mwa waja wetu wema, basi wakafanya hiyana hivyo haikuwasaidia chochote mbele ya Allah (s.w.t) na ikasemwa ingieni motoni pamoja na wenye kuingia.” (At-Tahriim 66:10).

Tazama Hadith zifuatazo zinazoweka wazi baadhi ya maana ya Ayah zilizotangulia: Kutoka kwa ‘Ubaid bin Hunain kutoka kwa Ibn ‘Abbas amesema: “Nilikaa mwaka na mimi nataka kumwuliza ‘Umar juu ya wanawake wawili ambao wamemuasi Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) basi nikawa namwogopa siku moja aliteremka sehemu akaingia katika mti wa miiba alipotoka nikamwuliza, akasema:

‘Aisha na Hafsa, kisha akasema tulikuwa katika ujahili hatuwahesabu wanawake kuwa ni chochote, ulipokuja Uislamu na Allah (s.w.t) akawataja tukaona kuwa wana haki kwetu bila ya kuwaingiza kwa chochote katika mambo yetu na kulikuwa na maneno baina yangu na mke wangu akanikasirikia, nikamwambia: hakika wewe uko huko, akasema unaniambia mimi hayo ilihali binti yako anamwudhi Mtume wa Allah (s.a.w.w.)? Basi nikamwendea Hafsa nikamwambia na kumtahadharisha juu ya kumuasi Allah (s.w.t) na Mtume wake[131] .

Kutoka kwa ‘Aisha amesema: Mtume wa Allah(s.a.w.w ) alikuwa anakunywa asali kwa Zainab binti Jahshi na kukaa kwake nikaafikiana mimi na Hafsa yeyote kati yetu akiingia kwake basi amwambie, umekula maghaafiir hakika mimi nanusa kutoka kwako harufu ya maghafir, akasema hapana isipokua nilikuwa na kunywa asali kwa Zainab binti Jahshi basi sitokunywa, nimeapa na usimwambie hayo yeyote[132] .

Kutoka kwa ‘Aisha (r.a): hakika wake wa Mtume wa Allah(s.a.w.w ) walikuwa makundi mawili kundi ambalo yumo ‘Aisha, Hafswa, Swafiyyah na Sauda na kundi jingine yumo Umm Salamah na wake wengine wa Mtume wa Allah(s.a.w.w ) [133] .

Kutoka kwa ‘Aisha (r.a) amesema: “nilikuwa nawaonea gherah wake ambao wametoa nafsi zao hiba kwa Mtume(s.a.w.w) na nasema: ‘Mwanamke ametoa nafsi yake?’ Basi Allah (s.w.t) alipoteremsha Ayah isemayo (umuahirishe umtakaye miongoni mwao na umsogeze umtakae.

Na kama ukimtaka yule uliyemtenga basi si vibaya kwako) nikasema naona Mola wako anafanya haraka katika matamanio yako[134] . “

Kutoka kwa ‘Aisha amesema: “Sikumwonea gherah mwanamke yeyote kama nilivyomfanyia gherah Khadija, na alikwishakufa kabla ya kunioa mimi kwa miaka mitatu, kwa yale niliyokuwa namsikia akimtaja na Mola wake alikwisha mwamuru ambashirie nyumba ya marumaru Jannat na alikuwa anachinja mbuzi kisha anatoa zawadi kwa marafiki zake[135] .

Kutoka kwa ‘Aisha amesema: “Halah binti Khuwailid dada wa Khadija alitaka idhini kwa Mtume wa Allah(s.a.w.w ) basi akajua kubisha hodi kwa Khadija akafanya haraka kwa hilo. Akasema (Mtume): “Ee Allah! Ni Halah huyo.” Akasema (‘Aisha): “Nikaona gherah na kusema: “Nini unamtaja kikongwe katika vikongwe wa Kiquraish mwekundu wa mashavu ameshakufa na Allah (s.w.t) amekubadilishia aliye bora kuliko yeye?”[136]

Kutoka kwa Hisham kutoka kwa Baba yake kutoka kwa ‘Aisha amesema: “Sikufanya gherah kwa yeyote kati ya wake wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) kama nilivyofanya gherah kwa Khadija na wala sikumwona, lakini Nabii alikuwa akimtaja kwa wingi na huenda alichinja mbuzi kisha anawagawa na kuwapelekea rafiki zake Khadija, na huenda nilimwambia: “Kana kwamba hapakuwa na mwanamke duniani isipokuwa Khadija.” Akasema: “Hakika alikuwa; na nimepata watoto kutoka kwake[137] .”

Amesema: “Nabii alisimama alihutubia akaashiria upande wa makazi ya ‘Aisha akasema: ‘Hapa kuna fitina mara tatu, ambapo utatokea upembe wa Shetani[138] .”

Hakika Hadith ya mwisho ya juu inaashiria fitina ambayo ameelekezewa ‘Aisha kwa kutoka kwake kuongoza jeshi ili kumpiga vita Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) Khalifa wa Waislamu katika vita vya Jamal - rejea maelezo zaidi katika sehemu ya kwanza.

Na ambacho wanakitegemea wanaoitakidi uadilifu wa Masahaba wote ni madai yao kuwa Mtume wa Allah(s.a.w.w ) amesema: “Masahaba wangu ni kama nyota yeyote mtakaye mfuata mtaongoka” na katika Hadith nyingine: “Kwa yeyote utakayechukua kauli yake...”.

Tukiachilia kuwa Hadith hii ni sahihi, na kwa kuchukulia Hadith zilizotangulia hiyo itamaanisha kuwa atakayemfuata aliyeondoka msikitini kwa ajili ya maslahi ya kidunia yenye kupita na Mtume(s.a.w.w ) amesimama akihutubia, basi atakuwa ameongoka na kwamba atakayewafuata walioacha sehemu zao ambazo Mtume aliwaamuru wasiziache kwa ajili ya kuchukua baadhi ya ngawira atakuwa ameongoka!

Na kwamba anayemfuata anaye tuhumu uongozi aliouweka Mtume(s.a.w.w ) kwa Usamah basi atakuwa ameongoka! Na kwamba anayemfuata anayepinga na kumuasi Nabii(s.a.w.w ) atakuwa ameongoka!

Hakuna shaka kwamba katika hilo kuna mgongano unao kataliwa na tabia ya kibinadamu na fitra sahihi, tukiachilia mbali kwamba kuitakidi kwetu usahihi wa Hadith hiyo ina maana ya Uma’asum wa Masahaba vile vile, kwa sababu kauli yao hiyo ni dhamana ya amri kutoka kwa Mtume(s.a.w.w ) kwa Waislamu kufuata Masahaba wote bila ya sharti au pingamizi kulingana na mafhum ya Hadith. Lakini haiwezekani Mtume kuamuru kufuatwa ambaye anaweza kufanya maasi, na kwa sababu hiyo Hadith hizo hazikubaliwi kwa yale yaliyo julikana na ni dhahiri kwamba sahaba sio ma’asum.

Hakika Hadith hizo zimezuliwa ili ziwe badala ya Hadith tukufu za Nabii(s.a.w.w ) ambazo amezitoa Al-Hakim katika Mustadark As-Sahihain kwa Sanad yake kutoka kwa Ibn ‘Abbas: “Amesema Mtume wa Allah(s.a.w.w ) nyota ni tumaini kwa watu wa ardhini kutokana na kughariki na Ahlul-Bayt (a.s.) ni tumaini kwa ‘Ummah wangu kutokana na ikhtilafu, basi kama kabila (lolote) la Kiarabu litawakhalifu, watakhitalifiana na kuwa makundi ya Ibilisi[139] .”

Na miongoni mwa athari mbaya ambazo ni matokeo ya kuitakidi uadilifu wa Masahaba wote ni kupatikana idadi kubwa ya Hadith hizo potovu katika vitabu vya Hadith kama vile Israiliyyaat, Masihiyyaat *na nyinginezo katika upotovu ambazo ndiyo mianya ya tuhuma katika dini ya Kiislamu, hiyo ni kwa sababu Hadith zimechukuliwa na kuaminiwa kwa kuwa tu zimepokewa kutoka kwa Sahaba pamoja na kuwa kuna uwezekano wa kufanya ambayo tumeyabainisha katika Hadith zilizotangulia.

UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYA

SEHEMU YA TATU

SHI'A NA QUR'AN TUKUFU

Shi'a wanaitakidi kuwa (Qur'an ni wahyi wa kimungu ulioteremshwa kutoka kwa Allah (s.w.t) katika ulimi wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) kwa kubainisha kila kitu, nayo-Qur'an hiyo-ni muujiza wa milele ambao wanadamu wameshindwa kupambana nao katika balagha, fasaha na katika ukweli na maarifa ya hali ya juu, haiguswi na mabadiliko, mageuzi wala upotovu, na hii ambayo iko mikononi mwetu tunayoisoma ndiyo ile ile Qur'an iliyo teremshwa kwa Nabii(s.a.w.w ) na atakaye dai yasiyokuwa hayo basi ni mwongo au ni mwenye kukosea au amechanganyikiwa na wote -hao- hawako katika uongofu, hakika hayo ni maneno ya Allah (s.w.t) ambayo hayapatwi na upotovu kwa hali yoyote)[140] .

Na amesema Sheikhul Muhadith Muhammad Al-Qummi ambaye amepewa lakabu ya As-Swaduuq: "Itikadi yetu katika Qur'an ambayo ameiteremsha Allah (s.w.t) kwa Nabii wake Muhammad(s.a.w.w) ni ambayo iko baina ya majalada mawili na ambayo iko kwa watu na sio zaidi ya hayo na anayetunasibishia kuwa tunasema zaidi ya haya basi ni muongo[141]

Na hayo yanatiliwa nguvu na aliyoyasema Al-Bahansawiy naye ni mmoja wa wanafikra wa Ikhwanul-Muslimin: "... hakika Shi'at al-Ja'afariyyah Al- Ithna-'Ashariyyah wanaona kuwa ni ukafiri kwa anayepotosha Qur'an ambayo 'Ummah umekubaliana tangu mwanzo wa Uislam. na kwamba msahafu uliopo baina ya Ahl as-Sunnah ndiyo ule ule uliopo katika misikiti na nyumba za Mashi'a." Na anaendelea katika kumjibu (Dhahir na Khatib) kwa kunukuu rai ya As-Sayyid Al-Khui ambaye ni mmoja wa maraaj'i wakubwa wa Kishi'a katika zama hizi*:

"Iliyo mashuhuri baina ya Waislamu ni kutokuwepo upotoshaji katika Qur'an na iliyopo mikononi mwetu ni Qur'an yote iliyoteremshwa kwa Mtume(s.a.w.w.) "[142] .

Ama Sheikh Muhammad Al-Ghazali anasema katika Kitabu chake Difau anil-'Aqidati wash-shariah dhidu mata'inil-mustash'riqina "Nimesikia kutoka kwa hawa miongoni mwa ambaye anasema katika majlisi za hadhara: "Hakika Shi'a wana Qur'an nyingine ambayo ni zaidi na inapunguza Qur'an yetu iliyo maarufu."

Nikamwambia: "Iko wapi hii Qur'an? na kwa nini majini na wanadamu hawakuona nakala yake kwa muda wote huu mrefu? Huu uongo ni wa nini? Kwa nini kuwasingizia watu na (kuusingizia) wahyi[143] ."

Ama Hadith ambazo sio Sahih ambazo baadhi wanaweza kuzitegemea ambazo zinaeleza kupotoshwa kwa Qur'an na ambazo zipo katika vitabu vya Hadith katika Shi'a, hakika ni dhaifu na hazikubaliwi na mfano wake ni nyingi katika vitabu Sahih vya Ahl as-Sunnah na tutaonyesha mifano ya hayo katika Sahih Bukhari, tunatanguliza Hadith walizozipokea kuhusu kusahau Mtume(s.a.w.w) katika baadhi ya Ayah:-

Kutoka kwa baba yake kutoka kwa 'Aisha amesema: "Mtume wa Allah(s.a.w.w) alimsikia mtu (mmoja) anasoma Surah usiku akasema: 'Allah (s.w.t) amrehemu kwani amenikumbusha Ayah kadha wa kadha nilikuwa nimezisahau katika sura kadha wa kadha[144] ."

Vile vile katika Sahih Bukhari ni kwamba, walipokuwa wanakusanya Qur'an hawakupata sehemu ya Surah al-Ahzab isipokuwa kwa Khuzaimah Al-Ansar na hii inapingana na ukweli unaosema kuwa Qur'an imepokewa kwa Tawaatur (na watu wengi sana) na wala sio kwa riwayah za ahad (mtu mmoja).

"Tulipokuwa tunanakili karatasi katika misahafu, niliikosa Ayah katika sura ya Ahzaab niliyokuwa namsikia Mtume wa Allah(s.a.w.w) anaisoma (na ambayo) sikuikuta kwa yeyote isipokuwa kwa Khuzaimah Al-Ansariy, Khuzaima Al-Ansariy ambaye Mtume wa Allah(s.a.w.w) amejaalia ushahidi wake kuwa ni sawa na ushahidi wa waumini wawili"[145] .

Na katika riwayah nyingine kutoka kwa Zayd bin Thaabit alisema: "…Niliifuatilia Qur'an yote kutoka kwenye vipande vya nguo, mifupa, magome na kwa watu waliohifadhi hadi nikakuta Ayah mbili za sura ya Tawbah kwa Khuzaimah Al-Ansariy ambazo sikuzipata kwa yeyote mwengine [146] ".

Na miongoni mwa Hadith ambazo zinasema wazi wazi kupotoshwa kwa Qur'an ni ambayo ameipokea Bukhari, vile vile katika Sahih yake katika Hadith kutoka kwa 'Umar Al-Khattab: Alitoka 'Umar bin Al-Khattab, nilipomwona anakuja nilimwambia Sa'idi bin Zaid bin Amr bin Naufail: "Hakika leo atasema maneno ambayo hajawahi kuyasema tangu akalie ukhalifa ."

Akanipinga na akasema: "Ni kipi kimekufanya udhanie kuwa atasema ambayo hajawahi kuyasema kabla yake?" 'Umar alikaa juu ya mimbari, muadh-dhin alipomaliza, alisimama akamshukuru Allah (s.w.t) kama inavyostahiki kisha akasema: "Ammaa ba'd, hakika mimi nitawaambia maneno nimejaaliwa kuyasema na sijui huenda kifo changu kiko karibu, atakayeyaelewa na kuyafahamu basi ayasimulie pale atakapoishia na ambaye anaogopa kutoyafahamu simruhusu anisingizie.

Hakika Allah (s.w.t) alimtuma Muhammad(s.a.w.w) kwa haki na akamteremshia Kitabu na miongoni mwa aliyo yateremsha Allah (s.w.t) ni Ayah ya Rajm, tulisoma na tukaifahamu.

Mtume alifanya rajm na sisi tuliifanya baada yake, naogopa watu watakapopitiwa na muda mrefu atakuja sema msemaji wao Wallahi hatupati Ayah ya rajm katika Kitabu cha Allah (s.w.t) basi wakapotea kwa kuacha faradhi aliyo iteremsha Allah (s.w.t), na rajm katika Kitabu cha Allah (s.w.t) ni haki kwa mwenye kuzini ambaye ameoa kwa wanaume na wanawake kama ushahidi ukithibiti au akiwa mja mzito au akikiri (mwenyewe)[147] ."

Na katika Hadith nyingine: "'Umar anatamani kuongeza Ayah hiyo ambayo ameidai kuwa imeondolewa katika Kitabu cha Allah (s.w.t) yeye binafsi. "'Umar amesema lau kama watu wasingesema 'Umar amezidisha katika Kitabu cha Allah (s.w.t) basi ningeiandika Ayah ya rajm kwa mkono wangu, alikiri Maa'iz mara nne mbele ya Nabii(s.a.w.w) kuwa amezini basi akaamuru apigwe mawe[148] .

Na Ayah iliyodaiwa ni kama ilivyo katika riwayah ya Ibn Majah: "As-shaikhu wa-sh- Shaikha Idha Zanayaa farjumuhumal-battah[149] ".

Na ukweli katika kukaganyikiwa ni kwamba Ayah ya rajm ipo katika Tawrati ya Ahlul-kitab na wala sio katika Qur'an tukufu kama alivyo kanganyikiwa 'Umar ibn al-Khattab.

'Umar amesema: "Mtume aliletewa mwanamume na mwanamke wa kiyahudi wakiwa wamezini akawaambia (wale) wayahudi, Mtawafanyaje?" Wakasema: "(hawa) tunazipaka nyuso zao masizi na tunawafedhehesha", akasema: " Nileteeni Taurati na muisome kama nyinyi ni wakweli.”Walikuja wakamwambia mwanamme katika wanaowaridhia Aa'wari (aliyekuwa na makengeza) soma, akasoma hadi akaishia katika sehemu akaweka mkono wake juu ya sehemu hiyo. Akasema(s.a.w.w) : 'Nyanyua mkono wako', akanyanyua mkono wake basi ikadhihirika Ayah ya rajm. Akasema: “Ewe Muhammad hakika ni juu yake kurujumiwa, lakini sisi tunaficha baina yetu basi akaamuru warujumiwe, basi nilimwona akiwapiga mawe[150] ."

Na kuchanganya kati ya Kitabu cha Allah (s.w.t) na Taurati ambako 'Umar alitumbukia humo.

Mtume alimtanabahisha 'Umar alipomuona akiwa na karatasi ya Taurati mkononi mwake, Mtume alikasirika sana na akamwamuru 'Umar kutokuisoma na akasema: "Kama Mtume Musa(a.s) angekuwepo angenifuata?"[151] .

Pia imepokelewa kauli ya kutoka kwa 'Umar kuwa: "Kisha tulikuwa tunasoma katika Kitabu cha Allah (s.w.t), msiwachukie baba zenu kwani ni ukafiri kwenu kuwachukia baba zenu au hakika ukafiri wenu ni kuwachukia baba zenu[152] ." (Yaani kuoa wake walio olewa na baba zenu). Na haifichikani kwa yeyote kuwa Ayah hii ni kama ile iliyotangulia haipatikani katika Kitabu cha Allah (s.w.t).

Tunahamia kwa Sahaba Abdallah ibn Masu'ud ambaye imepokewa kutoka kwake kuwa alikuwa anasoma Ayah ya (Wallaili idha yaghsha...) kwa kuongeza wa dhakar wal-untha, kama ambavyo inajulikana vile vile kuwa Ayah hii iliyozidi haipo katika Kitabu cha Allah (s.w.t).

Kisha akasema: "Namna gani Abdallah anasoma Wallaili idha yakh'sha, basi nikamsomea - Wallaili idha yakh'sha wannahaari idha tajallaa wadhakari wal-unthaa - akasema Wallahi alinisomea Mtume wa Allah(s.a.w.w) kutoka katika kinywa chake hadi kwenye kinywa changu"[153] . Na hiyo bila shaka inapingana na yaliyo pokewa kwa Mtume wa Allah(s.a.w.w) kwamba amesema katika Hadith mbili zifuatazo chini ambapo haingii akilini, Mtume(s.a.w.w) kutuamrisha kujifunza Qur'an kwa mtu asiye na hifdhi nzuri.

Kutoka kwa Abdillahi ibn 'Umar amesema:"Huyo mtu sikuacha kuwa nampenda baada ya kumsikia Mtume wa Allah(s.a.w.w) anasema: 'Jifunzeni Qur'an kwa watu wanne: kwa Abdillahi ibn Mas'ud …(akaanza kwaye)’[154] .

Na amesema: "Hakika anaye pendeza kwangu sana miongoni mwenu ni mbora wenu wa tabia na akasema: Jifunzeni Qur'an kwa watu wanne: Abdallah bin Mas'ud, Salim mtumwa wa Abu Hudhaifah, Ubay bin Ka'ab na Ma'adhi bin Jabal."

Na Muslim amepokea katika Sahih yake kutoka kwa 'Aisha kwamba amesema: Ilikuwa katika yaliyo teremshwa katika Qur'an ('Ashara ridha'atim-ma'alumaatin) na Mtume amefariki ingali inasomwa katika Qur'an[155] .

Pia katika Muslim ni kwamba (Abu Musa Al-Ash'ari aliwatumia wasomaji wa Basra, na walikuwa wanaume mia tatu na akasema katika aliowaambia: hakika tulikuwa tunasoma Surah tuliyokuwa tunaifananisha kwa urefu na ukali na Surahal-Baraat, isipokuwa nimehifadhi baadhi yake "Lau kaana libni aadama waadiyaani min-malin labtaghaa waadiyan thaalithan, wa laa yamla'u jaufa-bni-aadama illa-t-turaab[156] ."

Na katika Kitabu Al-Itiqan fi ulumil Qur'an cha Suyuti anataja baadhi ya riwayah kwamba Qur'an ina sura mia moja kumi na mbili tu au kwa kuongeza sura mbili Al-Hafd na Al-Khal'i...! [157] 18

Na Waislamu wote hawajui kitu kinachoitwa Suratul-hafdi wala Al-khal'i, na mengineyo yasiyo kuwa hayo mfano wa riwayah hizo dhaifu zilizopo kwa Ahl as-Sunnah na ambazo tunatosheka kwa kiasi tulichokinukuu.

Na baada ya hayo je, inajuzu kwa Shi'a kusema kuwa Qur'an ya Masunni imepungua au imezidi kwa kuwepo riwayah zinazosema hivyo katika vitabu vyao vya Hadith? Bila shaka laa! Kwa sababu kongamano la Ahl as-Sunnah ni kauli inayosema kutopotoshwa Qur'an.

Na maadamu hali ni hii, basi ni kwa nini tunaona tuhuma kali kutoka katika baadhi ya waandishi wa siku hizi katika kuwatuhumu Shi'a kwa kupotosha Qur'an kwa kupatikana tu baadhi ya riwayah dhaifu zinazosema hayo, ambazo hazikubaliwi kwao na kuna mifano ya riwayah nyingi katika vitabu sahihi vya Hadith vya Ahl as-Sunnah. Basi ambaye nyumba yake ni ya vioo asitupie mawe nyumba za wengine!


5

6

7