• Anza
  • Iliyopita
  • 7 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 2561 / Pakua: 1602
Kiwango Kiwango Kiwango
MAMBO YANAYO MUHUSU MAITI

MAMBO YANAYO MUHUSU MAITI

Mwandishi:
Swahili

MAMBO YANAYO MUHUSU MAITI

DIBAJI

Namshukuru Mwenyezi Mungu. Ule waadi niliotoa katika gazeti letu la "Sauti Ya Bilal", la mwezi Sept. 1974, toleo Ia No. 5, nilisema, nitaandika kitabu kizima kuhusu mambo anayofanyiwa Maiti kwa kirefu Inshallah, Alhamdulillah Mwenyezi Mungu kwa baraka ya Muhammad na Aali zake watakatifu [s] kautimiza kwa kunipa tawfiki ya kuchapisha kitabu hiki.

Kwa kuwa wafuasi wa madhehebu ya Ahlul Bait [a] ambayo hujulikana kwa jina la "Shia Ithnaashariya", makao humu Afrika ya Mashariki (East Africa) ambao wanatumia zaidi Lugha ya Kiswahili, na mpaka hivi sasa kitabu chenye kueleza mambo anayofanyiwa Maiti kwa wajibu ya Madbehebu ya Shia Ithnaashariya hakikuwepo, imetubidi kutayarisha kitabu hicho ili Waislamu Shia waweze kufuata wakati wanapohitajia. Wabillahi At-tawfiq Wassalatu Wassalamu Alaa Muhammadin Wa Aa'lihi At-tahirin.

Al Ahqar Muhammad Mahdi Al -Muusawy

Mwezi mosi R. Awwal (mfungo sita, 1396)

MAMBO YANAYO MUHUSU MAITI

KUHUSU MAMBO YA MAITI

Mwenyezi Mungu katika Qur'ani Tukufu, sura ya 'TABARAKA' Aya ya kwanza na ya pili, Amesema hivi "Ametukuka yule Ambaye Mkononi mwake umo ufalme wote; naye ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu. Ambaye Aliumba kifo na uzima ili kukujaribuni (kukufanyieni mtihani); ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi. Naye ni Mwenye nguvu na Mwenye Msamaha. (67:1 na 2).

Kwa kuwa mauti ni haki na lazima, na aendapo huko binadamu atayakuta aliyoyachuma mazuri au mabaya, na kila nafsi ni rehani kwa aliyoyachuma, basi ayatende yale ya kumridhisha Mola kwa kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu, Mtukufu Mtume [s] nauwongozi wa Ahlul Bait [a] watakatifu. Tusiwe miongoni mwa wale ambao Mwenyezi Mungu Ameeleza katika Qur'ani habari zao. "Ni kipi kilichowapelekeni Motoni? Watasema: Hatukuwa miongoni mwa waliokuwa wakisali, wala hatukukuwa tukilisha Maskini na tulikuwa tukipiga porojo na kuzama katika maasi pamoja na waliokuwa wakizama, na tulikuwa tukikadhibisha Siku ya hukumu (Siku ya Qiyama) Mpaka mauti yakatufika". (74:42 hadi 47) Mwenyezi Mungu Atubarikie "Husnul Khatimah" (Amin).

Kwa vile mauti ni lazima kwa kila kiumbe kilicho hai, kwahiyo imekuwa ni lazima kwa kila kiumbe kufariki na kuacha dunia. Basi ni lazima kwa kila Mwislamu anapoona alama za mauti ausie (afanye wasia) kuhusu mali kama anayo, kuhusu madeni, amana za watu, saumu, Hija (kama hakuhiji na hali ilikuwa fardhi kwake kuhiji) na Sala kama ameacha hakuweza kukidhi. Ni Sunna mtu kuandika wasia wake na akaweka chini ya mito yake.

HUKUMU KATIKA HALL YA "IHTIDHAAR" (KUKATA ROHO)

Mambo anayofanyiwa mtu anapokata roho na baadaye: Mwislamu anapofika katika hali ya Ihtidhari (wakati wa ukata roho), mwanamume au mwanamke, mkubwa au mdogo; ni wajibu (ni fardhi) kwake kama anajiweza na anayo fahamu na kama si hivyo basi kwa wale watu waliohudhuria hapo wamlaze huyo mgonjwa chali, miguu na nyayo zake zielekee Qibla, na ikiwa haimkiniki kufanya hivyo kwa ukamilifu basi kadri itakavyomkinika waanye, na ikiwa haimkiniki kabisa basi wamkalishe kuelekea Qibla. Na kama hiyyo pia haimkiniki basi wamlaze mkono wa kulia au wa kushoto kuelekea Qibla.

Ni Sunna: Wakati ule waliohudhuria wamfahamishe na kumtamkia 'Shaadatain' na majina matakatifu ya Maimamu kumi na wawili(a.s) na itikadi zote za haki, akumbushwe (kwa utaratibu na upole si kwa haraka na ukali aweze kufahamu kwa kukaririwa kaririwa).... Na pia asomeshwe dua maarufu iitwayo, "KALIMAA-TUL FARAJ nayo ni hii:

LAA-ILAA-HA, IL-LAL-LAA-HUL HALIMUL KARIM, LAA-ILAA-HA IL-LAL-LAA-HUL ALIYYUL ADHIM, SUB-HAA-NAL-LAA-HI RAB-BIS-SAMAA WAA-TIS-SAB-I, WA RAB-BIL ARA-DHIY-NAS-SABI-WAMAA FIY-HIN-NA, WAMAA BAY-NAHUN-NA, WAMAA TAH-TA-HUN-NA WARAB-BIL AR-SHIL ADHIYM WAL-HAMDU LIL-LAA-HI, RAB-BIL AA LAMIN, WAS SALA'A-TU ALAA MUHAMMADIN WA AALIHIT-TAYYIBEEN.

Ni Sunna: Wakati ule asomewe sura ya YAASIN, WAS-SAAFATI, AHZABI, AYATUL KURSI", na aya tatu za mwisho za sura ya BAQARAH, na pia kama iki Mkinika asomewe sura zaidi. Kwa kufanya haya yule mgonjwa atakata roho kwa raha bila ya taabu.

Mwenye Janaba na mwanamke mwenye hedhi (ujusi) wakati wa kukata roho wasije na wasimsogelee, kwani (Malaika hawatahudhuria ikiwa watu hao wapo hapo).

Hukumu Baada Ya Kufa

Baada ya kufa ni sunna:

(1) Kufumbwa macho yakiwa wazi.

(2) Kuzibwa kinywa kwa utepe utakaopitishwa chini ya taya na kufungwa tanzi juu ya kichwa.

(3) Kunyooshwa mikono, miguu na mapaja yake,

(4) Kufunikwa shuka na kama amekufa usiku, mahala hapo pawashwe taa wasimwache maiti kizani.

(5) wapashwe wenye imani (Waislamu) majira za mazishi ili waweze kuhudhuria mazishi yake, na wafanye haraka upesi kuzikwa. Lakini kama hawana yakini kwa kufa kwake, basi wasubiri hata wayakinishe, na kama maiti mwenye mimba, na mtoto yu hai basi asizikwe mpaka apasuliwe upande wa kushoto na kutolewa mtoto na baadaye ashonwe.

Mtu akishakufa na kupoa mwili wake mtu yoyote atakayemgusa yule maiti kabla hajawoshwa ghusli tatu kwa viungo au mwili wake,, kwa sehemu yoyote ya mwili wake itamlazimu aoge GHUSLU MASSI Al- MAYYIT, yule mwenye kumgusa.

Hukumu Za Kumwosha Maiti

Ni fardhi juu ya kila Mwislamu kumwosha maiti huyo, na kutengeneza mazishi yake yote, lakini wakishajitokeza watu kumshughulikia huyo maiti basi kwa wengine fardhi hiyo huondoka.

Ni haramu mwanamke kuoshwa na mwanamume, au mwanamume kuoshwa na mwanamke, lakini mke ana weza kumwosha mume hata kama wapo wanaume, na mume anaweza kumwosha mke hata ikiwa wapo wanawake wa kumwosha.

Mwanamume anaweza kumwosha mtoto wa kike asiyezidi miaka mitatu, na pia mwanamke anaruhusiwa kumwosha mtoto wa kiume asiyezidi miaka mitatu.

Ikiwa hakuna mwanamume wa kumwosha mwanamume, wanawake walio karibu naye kwa ujamaa na damu wanaweza kumwosha, kama mama, dada, shangazi, mama mdogo (dada wa mama yake). Vivyo hivyo ikiwa maiti mwanamke na hakuna mwanamke wa kumwosha huyo maiti, basi majamaa waliokaribu naye kwa ujamaa na damu wanaweza kumwosha kama baba, ndugu, na mtoto wake na wale ambawo ni haramu kumuoa, kwa kisheria wanaitwa "MAH-RAM".

Mtoto aliyezaliwa kwa kuharibika mimba, ikiwa mimba iko chini ya miezi minne (bado hakukamilishwa umbo lake) huyu hana haja ya kuogeshwa (kumuosha GHUSLI), ni lazima aviringishwe katika kitambaa na akazikwe. Lakini mimba ya miezi minne au zaidi (aliyekamilika umbo lake), lazima aogeshwe na kuvikwa sanda kama desturi.

Mwenye kumwosha maiti lazima awe mwislamu, tena Shia, na awe amebalehe, mwenye akili, na ajue namna ya kumwosha maiti.

Ni fardhi kumwosha Mwislamu hata akiwa wa madhehebu nyingine, lakini utamwosha kwa mujibu ya Madhehebu ya Shia lthnaasharia tu.

Mwosha maiti anapomwosha maiti anuwie kama ninafanya kazi hii Qurbatan llal-Laahi Taala, na vitu vyote avitumiavyo kwa kumwosha maiti viwe vya halali, si vya kunyang'anya au kuiba hata maji na mahala atumiapo wakati wa kumwosha maiti pawe pa halali.

Sunna Za Kumwosha Maiti

Awekwe mahala palipo juu, kama kitanda, au baraza n.k. na mahala pa kuwekea kichwa chake painuke zaidi kuliko miguu.

Alazwe chali, miguu na nyayo zielekee Qibla (kama tulivyotaja katika mambo ya hali ya 'IHTIDHARI'.

Maiti avuliwe nguo zote kwa upande wa chini (miguuni) hata ikibidi itatuliwe (ichanwe) lakini kwa idhini ya warithi wa maiti.

Aoshwe chini ya sakafu, au banda au hema asioshwe chini ya mbingu.

Uchimbwe "UFUO" wa kuingia maji ya kuoshea.

Mwili wake wote uwe wazi isipokuwa utupu wake.

Ufunikwe utupu wake hata ikiwa mkoshaji au watu wanaomuosha ni miongoni mwa wale wanaoruhusiwa kumwangalia.

Mkoshaji apitishe mkono wake juu ya tumbo la maiti kwa taratibu lakini ikiwa maiti mwenye mimba ambaye mtoto pia amekufa tumboni hairuhusiwi kufanya hivyo.

Mkoshaji asimame upande wa kulia wa maiti.

Aanze kuosha upande wa kulia wa kichwa cha maiti.

Mkoshaji aoshe mikono yake mara tatu hadi begani kwa kila 'GHUSLI' tatu.

Mwoshaji anapokuwa anaosha kiwiliwili cha maiti anatakiwa aseme hivi: "Ewe Mola! Hiki ni kiwiliwili cha mja wako mwenye imani (Mumin) na umetoa roho yake kutoka kiwiliwili chake, na umetenga kati yao, basi msamehe kwako." Hasa wakati anapomgeuza.

Asitangaze mwoshaji aibu yoyote aliyoiona mwini mwa maiti.

Utaratibu Wa Kumwosha Malti

(a) Baada ya kusafishwa mwili wake wote kwa sabuni (au kitu kingine) na kuondoshwa uchafu wa aina yo yote kama (madawa, marhamu au mafuta) ndipo huyo mwoshaji Mwislamu atamwosha ghusli tatu (mara tatu kuoshwa). Ni sunna kabla ya kuanza kumwogesha maiti ghusli tatu, atamwosha mikono yake mara tatu, kwa kila ghusli.

(b) Kwa mara ya kwanza, atachanganya katika maji ya kumwoshea maiti kidogo SIDRI (majani ya mkunazi) kwa kutia katika pipa la maji anachochotea maji ya kumwoshea huyo maiti (atayafikicha yale majani yapate kutoa harufu), wala asitie majani mengi hata maji yawe mudhafu. Baada ya kumaliza ghusli ya kwanza atakisuza kile chombo (pipa) kuondoa harufu ya Sidri.

(c) Na kwa mara ya pili atamwosha kwa maji yaliyochanganishwa na 'Kaafuri' (Karafu maiti) kidogo tu, wala asitie nyingi hata maji yakawa mudhafu. Tena atasuza pipa baada ya kumaliza ghusli ya pili ili kuondoa harufu ya Kaafuri.

(d) Na kwa mara ya tatu atamwosha (ghusli) kwa maji haya ya kawaida yaliyo safi bila ya kuchanganywa na cho chote, na hii ndio mara ya mwisho. Ni sunna mwoshaji katika muda anapomwosha maiti awe anasoma, "AFWAN AFWAN".

HADHARI

Taratibu zote za kuosha ni lazima zifuatwe na kama si hivyo GHUSLI ya maiti hubatilika na ni lazima uanze upya kwa utaratibu ule ule tuliyoueleza.

Kwa hivyo huyo maiti wa Ki-Islamu baada ya kuoshwa ghusli tatu hizo kama tulivyoeleza, sasa atakuwa ametaharika, Mwislamu yo yote akimgusa wakati huu, hakuna haja ya kuoga kwa yule mwenye kumgusa, lakini ikiwa baada ya kutoka roho na kupoa mwili, na kabla hajapewa (maiti) hizo ghusli tatu, akimgusa tu kwa mwili (si juu ya nguo) basi kwa kila mwenye kumgusa ni fardhi juu yake aoge "ghusli massul Mayyit", (ghusli ya kumgusa maiti). Na ghusli (kuoga) hiyo ni faradhi kwa mujibu wa Madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s.) tu.

MAMBO YANAYO MUHUSU MAITI

NAMNA YA KUMWOSHA MAITI

Baada ya kusafishwa mwili wote wa yule maiti hapo (yule mwoshaji) atanuia kuwa, namwosha (huyu maiti) ghusli ya kwanza kwa maji yaliyochanganyishwa na majani ya mkunazi kama tulivyoeleza huko nyuma.

(a) Kwanza ataanzia kwa kummwagia maji kichwani (maji yafike hadi utosini kwenye ngozi) masikio, pua, mdomo, macho na shingo pia aoshe. Ahakikishe kilmara anapomwosha, maji yafike sehemu zote za mwili wake.

(b) Tena upande wa mbele wa kulia kutoka begani chini ya shingo na pote kulia hadi kwenye nyayo tena baadaye amlaze ubavu amwoshe sehemu ya nyuma kama alivyomwosha sehemu ya mbele ya kulia.

(c) Baadaye atamwosha upande wa mbele wa kushoto na baadaye upande wa nyuma kama alivyomwosha upande wa kulia.

(d) Utupu wa maiti lazima uoshwe anapokoshwa kila upande (maana yake kwa kila mwosho (ghusli) ataosha utupu mara mbili). Ni haramu kuangalia utupu wa maiti na mwoshaji akiangalia ametenda dhambi, lakini ile ghusli haibatiliki.

(e) Mwoshaji wakati anapoosha utupu wa maiti Iazima aviringe kitambaa au avae mfuko wa kitambaa mkononi, ni haramu kupeleka mkono upekee.

Hii ndio namna ya kumwosha maiti ambayo utaratib huo kwa kisheria unaitwa "ALGHUSL AT-TAR-TIBI" na inambidi kwa kila mwenye Janaba pia akitaka kuondo (kuoga) Janaba au mwanamke mwenye hedhi au nifasi au kuoga ghusli za sunna lazima waoge vivyo hivyo kama tulivyoeleza katika kitabu chetu cha Sala (mlango wa ukurasa wa 33).

Kwa kuoshwa ghusli tatu hizo, tena haina haja kumwogesha, ghusli ya janaba au hedhi au nifas ikiwa maiti alikuwa katika hali ile.

Ikiwa SIDRI (majani ya mkunazi) au KAA-FUR (Kafuri maiti) zote mbili au mojawapo haipatikani, basi maiti ataoshwa kwa maji haya ya kawaida kwa nia ya badala ya Sidri au Kafuri mradi lazima maiti aoshwe Ghusli tatu tu (mara tatu).

(a) Ikiwa maji hayapatikani au maiti ameungua au alikuwa na maradhi fulani na akitiwa maji nyama au ngozi itatoka, basi badala ya maji atafanyiwa Tayamamu mara tatu kwa Ghusli tatu.

(b) Tayamamu ni lazima ifanywe na yule hai, na kumpaka maiti, na kama inamkinika kutayamamu kwa mikono ya maiti pia ifanywe - (Namna ya Tayamamu angalia kitabu chetu cha 'Sala' ukurasa wa 44 Mlango wa 8).

Mambo Ya Faradhi Baada Ya Kuogeshwa Maiti Hadi Kuzikwa Kwake

Haifai wakati anapooshwa maiti kuweko moto au kiteso cha kufukiza wala wakati wa mazishi hadi mwisho.

AL-HUNUUT: Kupakwa maiti kafuri mahali maalum ni faradhi kwa Waislamu baada ya kumwosha na kupanguswa (afutwe vizuri kwa nguo kavu) maiti kabla ya kusaliwa na kuzikwa apakwe 'Kafuri' laini sehemu saba (viongo vya kusujudia) navyo ni kipaji, viganja viwili, magoti mawili, ncha za vidole gumba viwili. Na sunna kupakwa kwenye pua, vile vile sunna kuwekwa pamba kwenye utupu wa maiti na kila penye tundu. Wakati wa kupaka HUNUUT ni baada ya kuogeshwa na kupanguswa na kabla ya kuvikwa sanda au wakati wa kuvikwa sanda.

Ikiwa Kafuuri haikupatikana hatakumwoshea maiti, basi hapo faradhi ya HUNUUT inaondoka, na kama amekogeshwa na Kafuuri lakini haikuzidi kwa ajili ya HUNUUT basi si kitu.

AL-HUNUUT: Kupakwa maiti Kafuri ni faradhi kwa kila maiti mdogo, mkubwa mwanamke, mwanamume, huru au mtumwa isipokuwa maiti yule aliyekufa hali yuko katika Ihramu ni haramu kumpaka Kafuri. Kafuri lazima iwe mpya si kukuu yenye kupotea harufu yake, na pia lazima iwe laini iliosagwa.

Sanda Ya Maiti Iliyo Wajibu

Ni faradhi kuvishwa maiti mwanamume au mwanamke mkubwa au mdogo vipande vitabu vya nguo:

(1) Kanzu (2) Shuka (3) Shuka

(1) Kanzu: Bila kuishona, itobolewe sehemu ya shingo tu halafu kitumbukizwe kichwa. Kuanzia begani hadi nusu ya miguu kupita goti.

(2) Shuka: Kama anavyovaa mwanamume kutoka kitovuni

hadi magotini, na ni bora si wajibu kuanzia kifuani hadi chini ya magoti.

(3) Shuka: Kitambaa kikubwa cha kumfunika mwiIi wake wote mzima mbele na nyuma kwa urefu hata uweze kufunga pande zote mbili (upande wa kichwa na upande wa miguu) na kwa upana, ncha moja iweze kuja juu ya ncha va pili

SUNNA

Si wajibu bali ni sunna:

(a) Kuvishwa mwanamume kiIemba, mwanamke sidiria na ushungi

(b) Nguo nyeupe isiyokuwa na rangi yoyote

(c) Nguo iwe ya pamba

(d) Ni bora kama aliwahi kuhiji basi 'IHRAMU' itumiwe au nguo za kusalia ambazo akisali nazo.

SANDA: Kwa kiasi kilichofaradhi lazima gharama yake na gharama ya vitu vya kumwoshea maiti, maji, Sidri, Kafuri, ardhi pa kuzikiwa na gharama zake zote haya hutoka katika asili ya mali ya maiti kabIa ya kulipwa deni au kufuatwa wasia wake. Na yako mambo ya sunna katika sanda ikiwa ameusia sanda itolewe katika theluthi (1/3) ya mali yake, au ameusia theluthi ya mali atumiliwe yeye basi sanda itatolewa humo, na kama hakuusia theluthi (1/3) basi kiasi kilichowajibu kitatolewa katika asili mali.

Sanda ya mke juu ya mumewe hata ikiwa mke anayo mali ya kutosha, na vivyo hivyo yule mke aliyeachwa kwa mara ya kwanza au ya pili na bado yupo katika eda, mume lazima atoe sanda. Ikiwa mtu mwingine yoyote ametoa sanda ya yule maiti (mwanamke) basi faradhi humuondokea mume.

Ni sunna kwa kila mwislamu kutayarisha SANDA yake na kuiweka nyumbani, pia ni sunna kuiangalia hiyo sanda kila mara. Mtukufu ,Mtume(s.a.w. w ) amesema, "Mwenye kutayarisha sanda yake, huwa kila siku zipitazo kila huandikwa thawabu kila apoiangalia, na kwa kufanya hivyo hatahesabiwa miongoni mwa waliomsahau Mwenyezi Mungu.

Namna Ya Kumkafini (Kumvisha Sanda Maiti)

Baada ya kukatwa mapande hayo, kwanza utatandika ile shuka kubwa ya Namba 3: Na ndio ya kwanza, baadaye utatandika Kanzu Kanzu kwa kuikunjua upande mmoja, (na hii ni ya pili), baadaye utaliweka shuka kwa upana kwa kukunjua. Ukisha tandika yote hayo vipande vitatu vya vitambaa vilivyo wajibu, basi sasa atalazwa maiti juu ya mapande yote ya sanda.

Kwanza utamfunga shuka na kuondoa kile kitambaa ulichotumia wakati wa kumwoshea kuficha utupu wake.

Utaurejesha ule upande wa kanzu ulioukunjua kwa kupitisha kichwa cha maiti kwenye shingo.

Ikiwa umeshafanya mambo ya 'AL-HUNUUT' basi utaikunja hiyo shuka kubwa kwa kuiweka ncha moja juu ya pili, na kama bado hujampaka AL-HUNUUT na mambo yake basi fanya, ndipo umalize kumfunika.

Kumsalia Maiti

Sala Ya Maiti: Lazima iwe baada ya kuvishwa sanda na kutia HUNUUT (KUPAKA KAFURI kwenye VIUNGO VYA KUSUJUDIA). Kuanzia maiti mwenye umri wa miaka sita (6) huwa faradhi kusaliwa sala ya maiti.

Sala ya maiti haina Adhana wala Kukimu na pia hakuna rukuu wala sijda, lakini inakusimama tu, na ina Takbira tano tu (badala ya sala tano za faradhi za kila siku). Hakuna shuruti ya kuwa na wudhuu lakini ni sunna kuwa nao. Ni sunna pia wakati wakutoa kila Takbira, anyanyuwe mikono hadi masikioni mwake yule mwenye kuswali.

Namna Ya Kumsalia Maiti

Mwenye kumsalia lazima asimame nyuma ya jeneza (jeneza liwe mbele yake) asiwe mbali nae, aelekee Qibla, kichwa cha maiti kiwe upande wa kulia wa mwenye kumsalia, na miguu upande wa kushotona awe amesimama. Akiwa maiti mwanamume basi ni sunna kusimama kati-kati na akiwa maiti mwanamke, asimame sawa na kifua cha maiti. Huwezi kumsalia maiti asiyekuwa mbele yako ijapokuwa akiwa mjini humo.

Namna ya Kumsalia Maiti kwa Njia ndefu

(1) Baada ya kupata ruhusa kwa wafiwa ndipo kwanza atatia nia ya kumsalia huyo maiti aliyoko mbele yake. Nia ni moyoni tu, kutamka si lazima katika ibada zote za faradhi (isipokuwa katika mambo ya Hijani sunna kutamka).

(2) Baada ya Takbira ya kwanza atasema hivi:

ASH-HADU AN LAA ILAA-HA IL-LAL LAA-HU WAH-DAHU LAA SHA-RIY-KA LAH, WA ASH-HADU AN-NA MUHAM-MADAN AB-DUHU-WARA-SUU-LUH, AR-SALA-HU BIL-HAK-KI BASHIY-RAN WANA-ZIY-RAN BAY-NA YADA-YIS-SAA-AH.

(3) Baada ya Takbira pili atasema:

AL-LAA-HUMMA SAL-LI ALAA MUHAM-MADIN WA AALI MUHAM-MAD, WAR-HAM MUHAM-MADAN WA AALA MUHAM-MAD, KA-AFDHALI MAA SAL-LAY-TA, WABAA-RAK-TA, WATA-RAH-HAMTA, ALAA IB-RAA-HIMA, WA AALI IB-RAA-HIM- IN-NAKA-HAMIY DUN MAJIYD, WA SAL-LI ALAA JAMIY-IL AN-BIYAA-I WAL MUR-SALIYN".

(4) Baada ya Takbira ya tatu atasema:

"AL-LAA-HUM-MAGH-FIR LIL MU'U-MINIY-NA WAL MU'U-MINAAT WAL MUS-LIMINA WAL MUS-LIMAAT, AL-AHYAA-I, MIN-HUM WAL-AMWAATI, TAA- BIU,BAY-NANAA- WA BAY -NAHUM BIL-KHAY-RAATI, IN-NAKA MUJIY-BUD DA'AWAAT IN-NAKA ALAA KUL-LI SHAY-IN-QA-DEER".

(5) Baada ya Takbira ya nne atasema hivi:

AL-LAA-HUM-MA IN-NA HAA-DHAA, AB-DUKA WAB-NU AB-DIKA,WAB-NU AMA-TIKA, NAZALA BIKA WA-ANTA, KHAY -RU MAN-ZUU-LIN BIH, AL-LAA-HUM-MA, IN-NAA, LAA, NA'ALAMU MIN-HU, IL-LAA KHAY-RAA, WA AN-TA, A'ALAMU, BI-HI MIN-NAA, ALLAA-HUM-MA IN- KAA-NA, MUH-SINAN, FAZID FlY IH-SAA-NIH, WA-IN -KAA-NA, MUSIY-AN, FATA-JAA-WAZ AN-HU-WAGH-FlR LAH, AL-LAA-HUM-MA, AJ-ALHU IN-DAKA FIY, A' ALAA IL-YEEN, WAKH-LUF ALAA AH-LIHI, FIL GHAA-BIRIYN, WARHAM-HU, BIRAH-MATIKA YAA AR-HAMAR-RAA-HIMIYN.

Akiwa Maiti ni Mwanamke baada ya Takbira ya nne atasema hivi :

AL-LAA-HUM-MA IN-NA HAA-DHIHI, AMATUKA WAB-NATU AB-DIKA,WAB-NATU AMA-TIKA, NAZALAT BIKA WA-ANTA, KHAY -RU MAN-ZUU-LIN BIH, AL-LAA-HUM-MA, IN-NAA, LAA, NA'ALAMU MIN-HA, IL-LAA KHAY-RAA, WA AN-TA, A'ALAMU, BI-HA MIN-NAA, ALLAA-HUM-MA IN- KAA-NAT, MUH-SINATA, FAZID FlY IH-SAA-NIHA, WA-IN -KAA-NAT, MUSIY-ATAN, FATA-JAA-WAZ AN-HA WAGH-FlR LAHA, AL-LAA-HUM-MA, AJ-ALHA IN-DAKA FIY, A' ALAA IL-YEEN, WAKH-LUF ALAA AH-LIHA, FIL GHAA-BIRIYN, WARHAM-HA, BIRAH-MATIKA YAA AR-HAMAR-RAA-HIMIYN.

(6) Utatoa Takbira ya tano ni kama salamu ya hiyo Sala.

Pia kuna njia fupi ya kumsalia Maiti huyo, nayo ni na ifuatayo:

(1) Baada ya Takbira ya kwanza atasema "ASH-HADU LAA-ILAA-HA IL-LAL-LAAH WA ASH-HADU ANA-MUHAM-MADAR RASUU-LUL-LAAH."

(2) Baada ya Takbira ya pili atasema: AL-LAA-HUMA SAL-LI ALAA-MUHAMMADIN WA AA-LI MUHAMMAD.

(3) Baada ya Takbira ya tatu:

AL-LAA-HUM-MAGH- FIR LIL MU'U-MINIY-NA WAL MU' MINAA-TI.

(4) Baada ya Takbira ya nne atasema hivi:

AL-LAA-HUM-MAGH-FIR LI-HAA-DHAL, MAY-YIT

(5) Akiwa maiti ni mwanamke baada Takbira ya nne sema hivi:

AL-LAA-HUM-MAGH-FIR LI HAA DHIHIL, MAY-YIT.

(6) Utatoa Takbira ya tano ni kama salamu ya hiyo na, hakuna faradhi ya kusoma kitu baada ya hiyo Takbira tano, ni sunna kusema, "RAB-BANAA AATINAA, FIDUN-YAA, HASA-NA- TAN, WAFIL AA-KHIRATI; HASANATAN, WA QINAA ADHAA-BAN NAAR."

Ukisali namna hiyo pia yatosha.

Ikiwa baada ya kusaliwa maiti, ikajulikana kwamba maiti alipinduka kifudifudi, basi lazima awekwe chali na asaliwe tena. Na kama kwa kusahaulika maiti hakusaliwa hadi akazikwa ni wajibu asaliwe juu ya kaburi, na vivyo hivyo ikiwa baada ya kuzikwa ikajulikana kuwa sala aliyosaliwa si sahihi.

MAMBO YANAYO MUHUSU MAITI

ADABU NA SUNNA ZA KUBEBA JENEZA

Thawabu ya kufuata Jeneza: Imepokewa hadithi kwa Mtukufu Mtume(s.a.w. w ) kwamba amesema: "Habari njema na (bishara) nzuri ya kwanza atakayopewa yule maiti 'MUMIN' ataambiwa, 'Karibu' kwa hakika Mwenyezi Mungu Amemghufuria kila mwenye kufuata Jeneza lako, na Dua zote za wale waliokuombea ughufuriwe Ameyakubali. Imam JAFFER AS- SADIQ(a.s) Amesema, "Kila mwenye kufuatana na Jeneza la mumin (mwenye imani) kwa kila hatua moja aaendayo mpaka arudipo mazishini ataandikwa thawabu elfu mia, na kufutwa madhambi elfu mia na kuongezwa daraja peponi elfu mia kwa kila hatua. Mtukufu Mtume(s.a.w. w ) Amesema:

Ni sunna kila mwenye kuona jeneza alikabili na kulipokea na kusema maneno haya:

Basi mwenye kusoma hayo, Malaika wote wa mbinguni watalia kwa kumhurumia msoma dua hiyo.

Wanatakiwa watu waende na maiti kwa heshima na adabu wasiongee na kuzungumza hasa mambo ya kidunia au habari ya yule maiti, bali waende na huku wanasoma dhikri kama "BIS-MIL-LAA-HI WA BIL-LAA-HI WASAL-AL-LAAHU ALAA MUHAM-MADIN WA AA-LI MUHAM-MAD AL-LAA-HUM-MAGH-FIR LIL MU'U-MINIY-NA WAL-MU'U-MINA-AT." Au dhikri yoyote ya Mwenyezi Mungu. Haifai kucheka wala kuamkiana (kutoa salamu) na kwenda mbele ya jeneza, wala kuendesha jeneza mbio mbio, isipokuwa kama inaogopewa maiti hiyo kuharibika au inanuka. lnafaa kuwa nyuma ya jeneza au pande mbili ya jeneza.

Ni sunna kubeba jeneza kwa mpango ufuatao:

Kwanza beba upande wa kulia wa mbele wa maiti kwa bega lako la kulia (kushoto ya jeneza).

Njoo kwenye mguu wa kulia wa maiti kwa bega lako Ia kulia (kushoto ya jeneza).

Njoo kwenye mguu kushoto wa maiti kwa bega lako la kushoto (kulia ya jeneza).

Nenda kwenye mkono wa kushoto wa maiti kwa bega lako la kushoto. Baadaye utarejea kama awali (Ia kulia mara moja tu ukishafuata sunna hiyo) unaweza kukamata mahali popote pa jeneza au fuata mpango ule ule wa awali.

Namna Ya Kuzika

(1) Ni faradhi kaburi lichimbwe kiasi cha kumfunika huyo maiti asiweze kufukuliwa na wanyama na isiweze kusikilizana harufu yake atakapoharibika.

(2) Ni sunna kuchimba kiasi cha urefu wa binaadamu au uchimbe hadi shingoni.

(3) Alazwe katika ubavu wa kulia iwe sehemu yake yote yote ya uso, kifua, tumbo na miguu (mwili wake mzima umeelekea Qibla).

Na ya Sunna ni haya:

(a) Ardhi ikiwa ngumu inayoweza kujishika, ni lazima ukeketwe ukuta wa Qiblani kiasi cha urefu wake na kwa upana kiasi cha kuweza kukaa huyo maiti, ni lazima aIazwe kwa ubavu wa kulia, hapo kwenye mkeketo huo, unaitwa mwanandani. Na ubao au kitu kingine uwe mgongoni mwake.

(b) Ama ikiwa ardhi laini kama hivi hapa kwetu pwani, na mahala pengine, mwanandani hachimbwi kwenye ukuta; unachimbwa chini upande wa Qibla, achimbwe kiasi cha kuweza kukaa mtu na ubao unamfunika juu: hau mfuniki mgongoni.

(c) Awekewe mawe nyuma ili asipate kupinduka na kulala chali. Ikiwa mtu ametumbukia kisimani na akafa na haikumkinika kumtoa humo, yule maiti basi kizibwe hicho kisima na litakuwa ndilo kaburi lake.

(d) Ni bora wateremke watu wasio jamaa lakini akiwa maiti mwanamke si halali kushuka humo asiyekuwa Mahram (jamaa wa karibu).

(e) Jeneza liwekwe upande utakaokuwa miguu ya maiti anapolazwa kaburini kwani hapo ni mlango wa kaburi.

(f) Jeneza liwekwe kidogo mbali na kaburi kiasi cha mikono miwili au mitatu (3), baadaye iondolewe na ku wekwa mara tatu mpaka kufika kwenye kaburi.

(g) Ni sunna wenye kushuka katika kaburi wawe na (Tahaara) wudhuu, kichwa wazi, miguu wazi na waka wa kutoka watoke upande wa mguu wa maiti.

(h) Atolewe maiti jenezani kwa kichwani, na kuteremshwa kaburini kwa upole bila haraka.

(i) Ikiwa maiti ni mwanamke, jeneza liwekwe upande wa Qibla na maiti atolewe kwa upana, na tangu wakati wa kutolewa maiti (mwanamke) mpaka kwisha funika mwana ndani, kaburi liwe limefunikwa nguo.

(j) Kuna dua wakati wa kuteremsha maiti na kama hawajui basi wataje dhikri yoyote ya Mwenyezi Mungu. Wakati wa kumtoa maiti humo jenezani na kumlaza kaburini ni sunna kusoma hao wanaomtoana kumlaza dua ifuatayo:

BISMILLAHI WA BIL-LAAHI WA 'ALA MILLATI RASULILLAH. ALLAHUMMA ILAA RAHMATIKA LAA ILA 'ADHABIKA. ALLAHUMMA IFTAH LAHU FI QABRIHI WA LAQINHU HUJJATAHU WA THABIT-HU AL-QAWL ATH-THAABIT WA QINA WA IYYAHU 'ADHABAL QABR.

Na wanapoliona kaburi waseme:

ALLAHUMAJ-ALHU RAWDATAN MIN RIYADIL JANNAH WA LA TAJ-ALHU HUFRATAN MIN HUFURIN-NAAR

(k) Afunguliwe vile vitanzi, halafu iregezwe regezwe ile sanda, na kusogeza sanda kwenye shavu la kulia mpaka lilalie mchanga, itakuwa vizuri kama akitengenezewa mto wa mchanga kwenye kichwa chake.

Jariy-Datain

Ni sunna iliohimizwa sana kwa SHIA WA AHLUL-BAIT(a.s) kuwekewa maiti vijiti viwili vibichi vya mti wa mtende, kiasi cha urefu wa kila kijiti kiwe mkono mmoja, ambao huitwa "JARIY-DATAIN". Huandikwa juu ya maiti hayo jina lake na Ia baba yake maiti na Shahadatain, na majina ya Maimamu kumi na wawili(a.s) . Maiti huwa haadhibiwi vijiti vinapokuwa vibichi mpaka kukauka.

Sunna hii ya kuwekewa vijiti viwili vya mtende imeanzia zama za Mtume ADAM(a.s) alipofanya wasia na ikaendelea zama za Mitume wote na ikawachwa zama za JAHILIA na Mtume wetu(s.a.w.w) akaanzisha upya, na inafaida sana kwa maiti. Siku moja Mtukufu Mtume(s.a.w. w ) alipita kwenye kaburi la maiti ambaye alikuwa ana aadhibiwa akaamrisha yaletwe vijiti vya mtende na papo hapo akakata vipande viwili, kimoja akakifukia kwenye kichwa na cha pili kwenye miguu, na akasema, "Sasa atapunguziwa adhabu".

Moja katika vijiti hivyo kiwekwe mkononi ya kulia karibu na shingo la maiti kwa kugusanana maiti na cha pili upande wa kushoto juu ya kanzu chini ya shuka. Vijiti hivi viwe vya mtende au mkomamanga hata ya mnazi yanafaa, na ikiwa yote hayo hayapatikani basi, vijiti vya aina yoyote vinafaa na bora vile vinavyochelewa kukauka.

Namna Ya Kulakiniwa Maiti

Ni Sunna kulakiniwa (kukumbushwa jawabu la kuwajibu hao Malaika). Nako ni kusema huku ameweka mkono wa kulia kwenye bega la kulia la maiti, na mkono wa kushoto kwenye bega la kushoto, na mdomo kwenye masikio ya maiti huku anamtikisa: "IS-MAA IFHAM YAA Fulaan (utaje jina la maiti) mara tatu. Na kama hajui jina lake aseme:

"YA ABDAL-LAA HAL-ANTA ALAL- AHDIL-LADHIY FAA-RAQ-TANAA ALAY-HI MIN SHA-HAA-DATI AN-LAA ILAA-HA-IL-LAL-LAAH, WAH-DAHU-LAA SHARIYKA LAH, WAAN-NA MUHAM-MADAN, SAL-LALLAA-HU, ALY-HI, WA AA-LIHI AB-DU-HU WARA-SUU-LUHU, WA SAY-YIDUN NABIY-YINA WA KHAA-TA-MUL-MUR-SALIY-NA, WA AN-NA ALIY-YAN AMIY RUL-MU'U-UMINIY-NA-WA SAY-YIDUL WASIY-Y1YNA, WA IMAA-MUNIF-TARA-DHAL-LAA-HU, TAA-TA-HU ALAL AA-LAMIY-NA, WA AN-NAL HASANA, WAL HUSAIN, WA ALIY-YABNAL HUSAIN, WA MUHAM-MADA-BNA ALlY-YIN WA JAA-FARABNA MUHAM-MADIN, WA MUU-SAB-NA JAA-FARIN-WA ALIY-YABNA MUU-SA, WA MUHAM-MAD AB-NA AALIY-YIN, WA-ALIY-YAB-NA MUHAM-MADIN, WAL HASA-NABNA ALIY-YIN, WAL QAA-IMAL HUJ-JATAL MAH-DI, SALA-WA-A-TUL LAAHI ALAY-HIM, A-IM-MATUL MU-UMINIY-NA, WA-HUJA-JUL-LAAHI ALAL-KHAL-QI AJ-MA-IYN, WA AIM-MATUKA AIM-MATU-HUDAN AB-RAAR.

YA (Fulan bin fulan) IDHAA, ATAA-KAL-MALA-KAA-NI, AL-MUQAR-RA--BAA-NI, RASUU-LAYNI, MIN INDIL-LAA-HI TABAA-RAKA WA TA-AALA,-WA SAALAA-KA, AN RAB-BIKA, WAAN NA-BIY-YIKA, WA-AN DIY-NIKA, WA-AN KITAA-BIKA, WA-AN QIBLATIKA, WA-AN AlM-MATIKA, FALAA TA-KHAF, WA-QUL FIY JAWAA-BIHlMAA AL-LAA-HU JAL-LA JA-LAA-LU-HUU RAB-BIY, WA-MUHAM-MADUN, SAL-LAL-LAA HU ALAY-HI WA AA' LIHIY-NABIY-YII ,WAL ISLAMU DIY-NIY, WAL-QUR-AA-NU KITAA-BIY, WAL KABATU QIB-LATIY WA AMIY-RULMU-MINIY-NA ALIYYUB-NU ABlY-TAALIBIN IMAA-MIY WAL-HASANUBNU-ALIY-YINIL-MUJTABA IMAAMIY, WAL HUSAl-NUB-NU ALlY-INISH-SHA-HIY-DU BI-KAR-BALAAl-IMAA-MIY, WA ALIY-YUN ZAY-NUL AA-BIDIY-NA, IMAA-MIY WA MUHA-MADUN-BAA-QIRUL-IL-MIN-NABIY-YII-NA IMAA-MIY, WA JA'AFARU-NIS-SAADIQU IMAA-MIY, WA MUU-SAL-KAA-DHIMU IMAA-MIY, WA ALIY-YU-NIR-RIDHAA IMAA-MIY WA MUHAM-MADUL JAWAA-DU, IMAA-MIY WA AllY-ULHAA-DIY IMAA-MIY- WAL HASA-NUL AS-KARIY-YU IMAA-MIY, WAL HUJ-JATUL MUN-TADHARU, IMAA-MIY HAA-ULAA-IY, SALA-WAA-TUL-LAA-HI ALAYHIM AJ-MA-IYN A-IM-MATIY WASAA-DATIY WA-QAA-DATIY WA-SHUFA-AA-IY BIHIM, ATA-WALLAA WAMINA'A-DAA-IHIM A- BAR-RAU FID-DUNYAA WAL AAKHI-RATI.

THUM-MA I'I-LAM YA (Fulaan bin fulaan).

AN-NAL-LAA-HA TA-BAA-RAKA WATA AA-LA NI' A-MAR-RAB, WA AN-NA MUHAM-MADAN SAL-LALLAA-HU ALAY-HI WA-AA-LIH1, NI'MAR-RASUUL WA AN-NA AMIY-RAL-MUMINIY-NA, ALIY-YAB-NA ABlY TAA-LIB WA AW-LAA-DA-HUL AIM-MATA AL-AHA-DA ASHARA, NIA-MAL, AIM-MAH, WA AN-NA MAA JAA-A BIHIY, MUHAM-MADUN SAL-LAL- LAA-HU ALAY-Hl WA-AA-LIHI, HAQ-QUN WA AN-NAL MAW-TA HAQ-UN, WA-SU-AA-LA MUN-KARIN WANA-KIYRIN, FIL-QAB-RI HAQ-QUN, WAL-BA-ATHA-HAQ-QUN WAN-NUSHUU-RA-HAQ-QUN, WAS-SIRAA-TA HAQ-QUN, WAL-MIY-ZAA-NA HAQ-QUN, WATA-TAA-IRUL KUTUBI-HAQ-QUN, WAL JAN-NATU HAQ-QUN, WAN-NAA RA HAQ-QUN, WAAN-NAS-SAA-ATA, AA-TIYA-TUN LAA LAA RAY-BA FIY-HA , WA-AN-NAL-LAAH YAB-ATHU MAN FIL QUBUUR (Tena aseme) AFAHIM-TA (yaa fulaan bin fulaan?) THAB- BATA KAL-LAA-HU BIL-QAW-LITH-THA-BITI, WA HADAA-KAL-LAA-HU

ILAA SIRAA TIN MUS-TAQIYM, AR-RAFAL-LAA-HU BAY-NAKA WA BAY-NA, AW-LIYAA-IKA FlY MUS-TAQAR-RIN MIN RAH-MA-TIH. (Tena aseme) AL-LAA-HUM-MA, JAA-FIL AR-DHA, AN JAN-BAY-HI WAS-AD BIRU HIHI ILAYK, WA LAQ-QIHI, MlNKA BUR-HA-ANAN, AL-LAA-HUMA AF-WAKA AF-WAK." (Baadaye huyo msoma Talkini aseme kwa sauti) "AL-FAA-TIHA" na wote walioko hapo watamsomea pia.

Hadhari Muhimu

Akiwa maiti ni mwanamke, basi katika Talkini pale mwanzo atasema, "IS MA-IY IF-HA-MIY YAA" jina la mwanamke (maiti) huyo na baba yake na kama halijui atasema, "YAA AMATAL-LAAH;" tena ataendelea na hiyo Talkini kwa kusema, "HAL AN-TI ALAL AH-DIL LADHIY FAA-RIQ- TINAA".

Tena ataendelea vivyo hivyo mpaka atakapofika sehemu ya pili baada ya kutaja jina la maiti na baba, au kusema, "YAA AMA-TAL-LAAH". Tena ataendelea kusema: "IDHAA ATAA-KIL MA- LA-KAA-NI AL-MUQAR RABAANI RASUU-LAY-NI MIN INDIL-LAAHI TABAA RAKA WATA-AA-LA, WA SA-A-LAAKI ANRAB BIKI WA ANABIY-YIKI WA AN DIYNI-KI WA AN KITAA-BIKI WA AN QIB LATI-KI WA AN AIM MATIKI FALAA TA-KHAA-FIY-WA QUU-LIY".

Baadaye utaendelea vivyo hivyo hadi kufika kwenye, neno la "THUM-MA" litafuata NA la "IE-LA-MIY YAA" (kutaja jina lake na la baba yake YAA AMATAL-LAAH, tena utaendelea hadi kufika kwenye neno la AFA-HIM-TI (Jina na baba) au YAA AMATAL LAAH; utasema "THAB-BATA-KIL LAA-HU BIL QAWLI-TH THAA BITI WA HADAAKIL-LAA-HU ILAA SIRAA-TIM-MUS- TAQIYM AR-RAFAL-LAA-HU BAY NAKI WA BAY-NA AW LI-YAAIKI"; endelea na baadaye sema, "AL LAA HUMMA JAA-FIL AR DHA AN JAN BAY-HAA, WAS AD BIRUUHI HAA, ILAYK WA LAQ-QIHAA MIN-KA BUR HAA-ALLAA HUMMA AF-WAKA AF-WAKA".

Namna Ya Kufukia Kaburi

(a) KiIa aliyoko hapo atabaruku naye kwa kusukuma mchanga kwenye kaburi kwa mgongo wa mkono wake wa kulia, na mwengine kwa majembe. Hala hala jamaa zake maiti wasitie mchanga, na makruhu na huleta ugumu wa moyo kama ilivyopokewa hadithi Tukufu ya Mtume(s.a.w.w) .

(b) Likishajaa kaburi linyanyuliwe kidogo kiasi cha kipimo cha vidole vinne wazi na kutandazwa kufanya kama mraba.

(c) Liwekwe alama ya kujulisha kuwa kaburi hili ni la nani.

(d) Litiwe maji juu ya kaburi, mtiaji aelekee Qibla na aanzie kumwaga kutoka kichwani hadi miguuni, tena azunguke akirudia rudia hadi kichwani na maji ya faidi yamwagwe kati ya kaburi hilo. Ni sunna kutia maji vivyo hivyo, kila siku hadi siku arobaini au miezi arobaini.

(e) Baada ya kutia maji waliohudhuria watie vidole vyao kwa kuvizamisha kidogo ili ibakie alama za vidole katika kaburi upande wa juu na kusoma sura ya "IN-NAA AN-ZAL-NAAHU" mara saba, na kumwombea maiti kwa Mwenyezi Mungu amghufurie.

(f) Baada ya kuondoka watu kwenye kaburi ni sunna alakiniwe kwa mara nyingine, (mara hii kwa sauti kubwa) ukifanya hivyo yule maiti hataulizwa maswali (ni sunna walie jamaa karibu sana au mtu alioruhusiwa na huyo ndio asome Talikini mara hii).

(g) Hasa ni sunna mara tatu kulakiniwa (i) wakati wa kukata roho (ii) akishalazwa kaburini (iii) Na mwisho baada ya kuondoka watu kwenye kaburi.

(h) Baada ya hayo yote, ni sunna kuwapa mkono wa rambirambi wafiwa, hufuatia matanga uchache wake siku moja na isizidi siku tatu. Ni sunna kuusia mali (Fedha) kwa ajili ya kulisha katika matanga yake.

(i) Ni sunna majirani wawapelekee wafiwa chakula kwa muda wa siku tatu kwa kuwa wao wameshughulika na msiba huo, sio wafiwa wawapikie watu. Ni karaha sana kwenda kula chakula matangani, ipo hadithi kwamba kufanya hivyo (kwenda kula) ni vitendo vya watu wasiokuwa waislamu katika zama za Jaahiliya.

SALAAT UL WAH-SHI

Ni sunna usiku wa kwanza wa kuzikwa maiti kusali sala rakaa mbili kwa ajili ya yule maiti na namna yake ni kama hivi:

Unanuia moyoni kwamba nasali rakaa 2 salaatul-wahshi, katika rakaa ya kwanza baada ya suratul Faatiha (AL-HAMDU) utasoma Aayatul Kursi, na rakaa ya pili baada ya "AL-HAMDU" utasoma sura ya IN-NAA ANZAL-NAA mara kumi, na ukisha toa salamu. Utasema "AL LAA-HUM-MA SAL-LI ALAA-MUHAM MADINI WA AA-LI MUHAM-MAD WAB-ATH THA-WAA BAHAA ILAA QABRI (FULAN jina la maiti) unaweza kusali wakati wowote usiku huo, lakini ni bora baada ya sala ya 'ISHA.

(Tajan) Taja jina la Maiti.

MAMBO YANAYO MUHUSU MAITI

MKE KUKAA EDA YA KUFIWA NA MUMEWE

Mwanamke mwenye kufiwa na mume kama hana mimba eda yake ni miezi minne (4) na siku kumi (10), na kama mwenye mimba eda yake mpaka azae, lakini iki wa amezaa kabla ya kupita miezi minne na siku kumi lazima akae eda hadi zipite, siku hizo.

Mwanamke mwenye eda ya kufiwa na mumewe, ni haramu kuvaa nguo za rangi; kujipamba kwa namna yo yote kwa mwili au kwa nguo kama kujitia manukato, kutia wanja machoni, mapodari, hina na kila jambo la kujipamba ni haramu kwake hata nguo nyeusi ikiwa ina nakshi au mkato wa kujipamba.

Eda huanzia siku ya kufa kwa mume ikiwa yupo hapo, na kama hayupo huanzia siku atakapopata habari hata kama kumepita muda mrefu sana. Katika muda huo wa eda hawezi kuposwa au kuolewa.

Uislamu unaamrisha unadhifu, basi wanaruhusiwa wanawake wenye eda kuoga kujisafisha na kuweka mwili safi, kukata kucha.

Anaruhusiwa kutoka nje kama ipo haja kama kununua mahitaji yake au kumwangalia jamaa au mgonjwa na kadhalika, asitoke nje paisipo na haja.

Tunaomba kwa Mola wetu atupe sote Twafiki ya kufuata maamrisho ya dini na kuepukana na yaliyoharamishwa au kufuata mambo ya Bida'a uzushi, usiona msingi.

Thawabu Ya Kwenda Kuzuru Makaburi Ya Ndugu Zetu Mumineen (Wenye Imani)

Siku moja Mtukufu Mtume(s.a.w.w) aliwaambia Masahaba: "Watuzeni maiti wenu? Wakauliza, "Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu tuwatuze nini maiti?" Akajibu Sadaka na Dua, tena akaendelea kusema, "Hakika roho za wenye imani siku ya Ijumaa kwenye mbingu ya kwanza sawa na mahala walipokuwa wakikaa majumba yao na kila mmoja wao hupiga kelele kwa sauti ya kuhunisha na kulia na husema, Enyi watu wangu, watoto wangu, baba na mama yangu na majamaa zangu, tuonee huruma na Mwenyezi Mungu Atakuoneeni huruma, kwa mali hiyo mliyo nayo ilikuwa mikononi mwetu, sasa haipo mikononi mwetu, mateso na hesabu tunafanyiwa sisi na faida yake wanafaidi wengine". Na kilamoja (roho) humpigia kelele jamaa zake.

Tuonee huruma kwa kutoa sadaka 'dirham' moja (pesa za zama zile) au kwa kutoa mkate kumpa maskini, au kwa nguo kumvisha asiekuwa na nguo, na Mwenyezi Mungu atakuvisheni nguo za "Janah" (Pepo). Baadaye Mtukufu Mtume(s.a.w .w ) akalia na Masahaba pia wakalia, na kilio kilimshika kwa wingi hata hakuweza kusema. Baadaye akasema "Hao ni ndugu zenu katika dini (Imani) sasa wameshageuka udongo na mifupa imesagika baada ya kuishi humu duniani kwa raha na furaha, basi wanapiga kelele na kusema, "Ole juu yetu, laiti katika uhai wetu tungali toa sadaka na kutenda mazuri kwa (pesa zetu) hizo tulizokuwanazo katika njia ya Mwenyezi Mungu leo tusengelikuwa muhutaji wenu". Basi wanarudi wanyonge na huku wanpiga kelele, "Haraka toeni Sadaka kwa maiti wenu".

Inafaa kwa Mwislamu kila wiki kwa uchache hasa siku AIhamisi awakumbuke wafu wake kwa kufika kwenye makaburi yao, hii ni Sunna ya Mtukufu Mtume(s.a.w. w ) akiwaamrisha Masahaba wake kuzuru makaburi.

Amepokea Bi Aisha (r.a) na Abu Hurayrah (r.a) kwamba Mtukufu Mtume(s.a.w.w) amesema: "Amekuja Jibrili kwangu na akaniambia kwamba "Mola wako Anakuamrisha uende kwa watu wa 'AL-BAQEE' makaburini mwa watu wa Madina na uwaombee waghufuriwe ". Nikasema (Aisha), "niseme nini ninapofika makaburini?" Akasema, Sema, "AS-SALAA-MU ALAA AHLID-DIYAAR, MINAL MU'MINEE-NA- WAL MUS-LIMEEN. YARHAM UL-LAA-HUL MUSTAK-DIMEE-NA-MIN-NAA, WAL MUS-TA'A-KHIREEN, WA IN-NAA IN-SHAA-AL-LAAHU Bl-KUM, LAA-HI KUUN.

Licha ya kuwepo wapokezi wa hadithi kuhusu jambo hilo kutokana na wanachuoni, wa Ki-Shia vile vile wamepokea hadith hizo wanachuoni wa Ki-Sunni nao ni: Bwana Muslim katika Saheeh yake, na Bwana Bayhaki katika 'Sunan' yake na pia Bwana Ahmad Bin Hambal, Bwana Abudaud, Bwana Tirmizi, Bwana Nasaina Bwana Baghawi.

Ni sunna unapofika kwenye kaburi uelekee Qibla, weka mkono kwenye hilo kaburi na soma mara saba (7) sura ya Innaa Anzalnahu (5:97) na pia bora usome sura ya AL-FAATlHA (S:1) na sura ya AL-FALAQ (5:113) na WAN-NASI (S:114) na sura ya QUL-HUWL-LAAHU (S:112) na Ayatul-Kursi kila moja mara tatu.

Ni sunna unapoingia makaburini usome:

"BlS-MIL-LAA-HIR-RAH-MAA-NIR RAHEEM, ASSALAA-MU ALAA AHLI LAA-ILAA-HA IL-LAL-LAAH, MIN AH-LI LAA-ILAA-HA IL-LAL LAAHI YAA AH-LA LAA-Llaa-HA, IL-LAL-LAAH, BI-HAK-KI- LAA-ILAA-HA IL-LAL-LAAH, KAY-FA WAJAD-TUM KAULA LAA-ILAA-HA-IL-LAL-LAAH MIN LAA ILAA-HA IL-LAL-LAAH, YAA LAA-ILAA-HA, IL-LAL-LAAH, BI HAK-KI LA-ILAA-HA IL-LAL-LAAH, IGH-FIR LIMAN KAA-LA LAA-ILAA-HA, IL-LAL-LAAH WAH-SHUR NAA, FIY ZUM-RATI MAN KAA-LA, LAA-ILAA HA IL-LAL-LAA-HU, MUHAM-MADUN RASUU-LUL-LAAH ALY-YUN WALIY-YUL-LAAH

Kwa kusoma haya Mwenyezi Mungu atambarikia msomaji thawabu ya kutenda mema ya miaka hamsini na kumsamehe madhambi yake na ya wazazi wake ya miaka hamsini.

Tunaomba kwa Mola Atupe tawfiki ya kuwakumbuka wafu wetu hasa wazazi kwa kuwatendea mambo ya heri kwa thawabu yao na kuwazuru makaburini kwa kuwa somea Fatha Amin. Na kwa kuzuru makaburi tutakumbuka kuwa kuna kufa (mauti), hao walikuwa kama sisi sasa hawajiwezi kujisaidia.

Ruhusa Ya Kulia Ufiwapo

Ni sunna ya Mtukufu Mtume(s.a.w.w) kumlilia maiti wako.

Mtukufu Mtume(s.a.w.w) alimlilia Bwana ZAIDI (r.a) na Bwana JA'AFAR (R.A.) na pia alimlilia Ami yake Sayidna HAMZA(a.s) na mwanawe Sayidna lbrahimu(a.s) Mtume(s.a.w.w) alipomwona ami yake Hamza(a.s) ameuwawa akalia, na alipoona namna Ilivyotendewa kinyama maiti tukufu ya Hamza(a.s) akalia sana kwa kwikwi.

Kwa hivyo haikatazwi kulia bali inakatazwa kusema maneno yasiomridhisha Mwenyezi Mungu kama kusema "Umenionea umenichukulia mpenzi wangu" n.k. Kulia hakuna muda madhali roho inauma, inahuzuni unaruhusiwa kulia n kulia ni dawa.

SHARTI YA KUCHAPA

Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.

MWISHO WA KITABU

YALIYOMO

MAMBO YANAYO MUHUSU MAITI 1

DIBAJI 1

MAMBO YANAYO MUHUSU MAITI 2

KUHUSU MAMBO YA MAITI 2

HUKUMU KATIKA HALL YA "IHTIDHAAR" (KUKATA ROHO) 3

Hukumu Baada Ya Kufa 3

Hukumu Za Kumwosha Maiti 4

Utaratibu Wa Kumwosha Malti 5

HADHARI 5

MAMBO YANAYO MUHUSU MAITI 6

NAMNA YA KUMWOSHA MAITI 6

SUNNA 7

Namna Ya Kumkafini (Kumvisha Sanda Maiti) 7

Kumsalia Maiti 8

Namna Ya Kumsalia Maiti 8

MAMBO YANAYO MUHUSU MAITI 10

ADABU NA SUNNA ZA KUBEBA JENEZA 10

Namna Ya Kuzika 10

Jariy-Datain 11

Namna Ya Kulakiniwa Maiti 12

Hadhari Muhimu 13

Namna Ya Kufukia Kaburi 14

SALAAT UL WAH-SHI 14

MAMBO YANAYO MUHUSU MAITI 15

MKE KUKAA EDA YA KUFIWA NA MUMEWE 15

SHARTI YA KUCHAPA 17

MWISHO WA KITABU 17

YALIYOMO 18