BIBI FATIMA (A.S) KIIGIZO CHEMA KWA WANAWAKE

BIBI FATIMA (A.S) KIIGIZO CHEMA KWA WANAWAKE0%

BIBI FATIMA (A.S) KIIGIZO CHEMA KWA WANAWAKE Mwandishi:
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi: Faatima (a.s)

BIBI FATIMA (A.S) KIIGIZO CHEMA KWA WANAWAKE

Mwandishi: Sheikh Muhammad Ibrahim El-Qazwini.
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi:

Matembeleo: 8257
Pakua: 1656

Maelezo zaidi:

BIBI FATIMA (A.S) KIIGIZO CHEMA KWA WANAWAKE
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 11 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 8257 / Pakua: 1656
Kiwango Kiwango Kiwango
BIBI FATIMA (A.S) KIIGIZO CHEMA KWA WANAWAKE

BIBI FATIMA (A.S) KIIGIZO CHEMA KWA WANAWAKE

Mwandishi:
Swahili

BIBI FATIMA (A.S) KIIGIZO CHEMA KWA WANAWAKE

KIMEANDIKWA NA: MUHAMMAD IBRAHIM EL-QAZWINIY

KIMETARJUMIWA NA: MSABAH S. MAPINDA

UTANGULIZI

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni sehemu ya tarjuma ya kitabu cha Kiarabu, kwa jina la: Al-Hijab Saa'datun laa shiqaaun, kilichoandikwa na, Sheikh Muhammad Ibrahim El-Qazwiniy

Kitabu hiki kinahusu vazi la Hijabu: vazi ambalo ni rasimi kwa wanawake wa kiislamu kwa ajili ya kustiri maungo yao.

Katika kitabu hicho tumechukua kipengele kimoja tu, kinacho husiana na bibi Fatima(s.a) ambacho nia: Bibi Fatima(a.s) Kiigizo Chema Kwa Wanawake.

Kipengele hicho tumekinyambua kutoka katika kitabu hicho kwa mnasaba wa masiku ya Shahada ya Bibi huyo mtukufu, kwa lengo la kumuenzi Mama huyo Adhimu.

Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni chenye manufaa kwa wasomaji wetu, hususan wanawake wa kiislamu na kuiokoa jamii yetu kutokana na maovu.

Pia Tunamshukuru ndugu yetu, Sheikh Msabah S. Mapinda kwa kukubali kwake kuchukuwa jukumu hili la kutarjum kitabu hiki, kutoka lugha yake ya asili ya Kiarabu kwenda lugha ya Kiswahili. Halikadhalika tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.

BIBI FATIMA (A.S) KIIGIZO CHEMA KWA WANAWAKE

KIMEANDIKWA NA: MUHAMMAD IBRAHIM EL-QAZWINIY

KIMETARJUMIWA NA: MSABAH S. MAPINDA

Bibi Fatimah(a.s) ni mwanamke anayezingatiwa kuwa ni mwanamke wa kutolea mfano katika dini ya kiislamu, na pia ni kiigizo chema kwa kila mwanamke anayetafuta mafanikio katika maisha yake. Bibi Fatimah binti Muhammad(s.a.w.w) ndiye mwanamke bora ulimwenguni aliyezaliwa na kupata malezi katika nyumba iliyokuwa ikishuka ndani yake Wahyi kutoka mbinguni.

Si hivyo tu bali Bibi Fatimah alihitimu mafunzo ya Uislamu katika madrasa ya Utume, na kutokana na mafunzo hayo aliweza kufikia daraja ya juu na tukufu. Katika kuthibitisha ubora wa Bibi Fatimah, Mtume(s.a.w.w) amepata kusema, "Hakika Mwenyezi Mungu huwa radhi kwa radhi ya Fatimah, na huchukia kutokana na kuchukia kwa Fatimah.[1] "

Kwa ajili ya daraja kubwa aliyonayo Bibi Fatimah katika Umma wa Nabii Muhammad(s.a.w.w) imekuwa ni wajibu kwa kila mwanamke duniani kuiga mwenendo wa Bibi huyu katika maisha yake, ajing'arishe kwa nuru yake nzuri na afuate nyayo zake ambazo zitamuelekeza kwenye mafanikio na utukufu. Hakika Bibi Fatimah(a.s) , ni mfano wa kila utukufu na kila jema. Mwanamke yeyote atafanikiwa iwapo ataamua kufuata mwenendo wa Bibi Fatmah(a.s) , na kinyume chake ni kuwa, kila mwanamke ataangamia iwapo ataamua kujichagulia mwenendo wake au kuiga usiyokuwa mwenendo wa Bibi Fatimah. Pia Fatimah(a.s) alikuwa Mchaji Mungu na mwenye kutekeleza vilivyo maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Pia ile maana nzima ya Hijabu aliifahamu vema na kuitekeleza kama ilivyoamriwa na Mwenyezi Mungu.

Hivyo utekelezaji wake katika maamrisho ya Mwenyezi Mungu ulikuwa wa hali ya juu, kwani hakupata kutoka nje ila huwa amevaa vazi la kumsitiri mwili wake wote tangu kichwani hadi miguuni. Isitoshe alikuwa akiichukia mno tabia ya wanawake kutoka majumbani mwao bila kujisitiri kisheria. Bibi Fatimah alichukizwa na tabia hiyo kwa sababu Mwenyezi Mungu pia anaichukia tabia ya kutokujisitiri na hasa kwa kuwa kukosa sitara ya kishera kwa wanawake ni ufunguo wa kuyaendea maovu na ni miongoni mwa vitangulizi vinavyosababisha watu kuteleza, bali wanaaanguka kabisa.

Sasa hivi tunawaletea baadhi ya mafundisho kuhusu Hijabu na tutaona pia utukufu wa Bibi Fatimah katika mafunzo hayo.

Ni Kitu Gani Kilicho Bora Kwa Mwanamke?

Inasimuliwa katika historia kwamba, Mtume(s.a.w.w) siku moja aliwauliza Masahaba suali lifuatalo: "Je! ni kitu gani kilicho bora kwa mwanamke?" Masahaba walinyamaza kwa kuwa jibu la mkato na sahihi hawakulifahamu, ikawa kama kwamba akili zao zinahangaika baina ya kuwa kilicho bora kwa mwanamke ni mali, uzuri wake, kuolewa au kitu gani? Kipindi chote hiki Bibi Fatimah alikwisha lisikia swali hilo, na baada ya kimya cha kukosekana jibu, Bibi Fatimah alimtuma mtu aende kwa Mtume(s.a.w.w) akatoe jibu sahihi la swali hili nalo ilikuwa: "Kilicho bora kwa mwanamke ni yeye mwanamke asimuone mwanaume na mwanaume naye asimuone mwanamke.[2] "

Baada ya jibu la bibi Fatimah Masahaba walikuwa wakisubiri jibu la Mtume atasema nini kuhusu jawabu alilotoa Binti yake. Mtume(s.a.w.w) akasema "Amesema kweli Fatimah." Na akaongeza kusema, "Fatimah ni sehemu iliyotokana na mwili wangu." Maana ya maneno ya Mtume yalimaanisha kwamba hilo ndilo jawabu sahihi na hiyo ndiyo imani.

Kutokana na jawabu hili, Bwana Mtume(s.a.w.w) akawa ameitangazia dunia nzima kwamba: Utu, heshima, utukufu, na wema wa mwanamke unapatikana ndani ya Hijabu, na kinyume chake ni uovu na shari, isitoshe hasara humfika mwanamke anapoitupa Hijabu.

Mazungumzo Ya Kustaajabisha

Historia inaendelea kutufahamisha kwamba Bibi Fatimah(a.s) alikuwa amekaa na baba yake ambaye ndiye Mtume(s.a.w.w) , mara alibisha hodi Sahaba Abdalla ibn Ummi Maktum ambaye alikuwa kipofu. Kabla Sahaba huyu hajaingia Bibi Fatimah(a.s) alisimama akaondoka mahali hapo. Baada ya kwisha mazungumzo baina ya Mtume na Sahaba huyu, Sahaba Abdallah ibn Ummi Maktum aliondoka. Bibi Fatima alirudi na akaendelea kuzungumza na Mtume(s.a.w.w) Bwana Mtume(s.a.w.w) .wakamuuliza Binti yake sababu ya kuondoka wakati alipoingia Sahaba Abdallah ibn Ummi Maktum hali kuwa anafahamu kabisa kwamba yule ni kipofu haoni[3] .

Bibi Fatimah alijibu kama ifuatavyo."Ikiwa yeye hanioni basi mimi namuona na yeye ananusa harufu ya wanawake.

"Mtume(s.a.w.w) alifurahishwa mno na jawabu la Binti yake ambalo linaonyesha kipimo cha Uchamungu na utukufu unaotoka kwa Binti yake Mwenye hekima. Isitoshe kwa jawabu hilo, Bwana Mtume hakumlaumu binti yake kutokana na mkazo huu mkali unaohusu Hijabu, bali furaha ya Mtume iliendelea kwa upeo mkubwa na akaunga mkono kwa dhati kabisa kisha akasema: "Nashuhudia kwamba wewe ni sehemu iliyotokana nami[4] "

Tukio Muhimu Ndani Ya Msikiti Wa Mtume (s.a.w.w)

Siku moja Bibi Fatimah(a.s) alitaka kutoa mhadhara ndani ya msikiti wa Mtume(s.a.w.w) . Kabla ya kuanza kuhadhiri alitengenezewa sitara humo Msikitini, akakaa yeye na Waumini wengine wakike upande mmoja na Waumini wanaume wa Kiansari na Muhajirina nao wakakaa upande wa pili. Sitara hii aliyotengenezewa Bibi Fatimah(a.s) ilikuwa ina maana nyingi ndani yake.

Kwanza ilikuwa ni kutekeleza sheria inayohusu Hijabu katika sura ya kuweka kizuizi, ambapo pande mbili hizo zilitenganishwa. Pili, hali hiyo ilikuwa ni kuonesha kutokuukubali kwa vitendo mchanganyiko wa wanaume na wanawake, jambo ambalo maadui wa Uislamu wanatumia kila mbinu kulihalalisha kwa kulitolea hoja batili.

Sasa nakutazama ewe dada yangu wa kiislamu, nikitarajia umeiona mifano hii mitatu inayohusu maisha ya Bibi Fatimah(a.s) ambaye ni mwanamke bora kuliko wanawake wote duniani, na ni mwanamke anayestahiki kuigwa katika Uislamu. Inafaa uige na ujifunze kwake ili upate kupambika kwa umbile la kike ( yaani kuwa na haya) na utukufu, kadhalika ifanye nafsi yako iwe ya mwanamke Mchamungu mwenye kushika mafunzo ya kiislamu na hukmu za Qur'an. Ewe dada wa kiislamu hebu shikamana na mafunzo ya kiislamu ambayo Mwenyezi Mungu amekupa ili ufanikiwe duniani na akhera. Mafunzo haya yatakupandisha kwenye daraja tukufu la wenye imani na mafanikio. Fahamu kwamba hutafanikiwa isipokuwa uwe umeshikamana na kuyatumia mafunzo hayo kwa kuyatekeleza maishani mwako.

Kujiheshimu Ndiyo Pambo La Mwanamke.

Bwana Mtume(s.a.w.w) amesema, "Kujiheshimu ndiyo pambo la Mwanamke.[5] "

Hapana shaka kwamba pambo limegawanyika sehemu mbili: Pambo lisilo halisi na pambo halisi. Ama pambo lisilo halisi ni lile ambalo linaloonekana wazi, na ni lenye kubakia kwa muda maalum, kisha hutoweka bila hata ya kumuongezea kitu muhusika katika utu wake. Ama lile pambo halisi, ni lile ambalo hubakia muda wote na pia humfanya mwanamke aupate ule utu wake kamili na kumfikisha kwenye daraja ya ukamilifu. Ukweli usiokuwa na shaka ni kuwa, pambo halisi ndilo lenye umuhimu mno kuliko lile jingine, bali ndilo lengo analopaswa kulishughulikia kila mtu. Endapo mtu atakosa kuwa na fungu fulani katika pambo hili halisi, basi pia huwa hana faida yoyote ndani ya lile pambo la dhahiri.

Hapana shaka kwamba kujiheshimu ndilo pambo pekee linalomfaa mwanamke kama alivyosema Bwana Mtume(s.a.w.w) . Pambo hilo humjengea mwanamke utu, heshima na utukufu hapa duniani na kesho akhera. Ama madawa ya kujirembesha, manukato na mengineyo miongoni mwa mapambo, yote hayo ni mapambo ya nje tu na hayana maana yoyote khususan mwanamke mwenyewe atakapokuwa si Mchajimungu: Mwenyezi Mungu apishe mbali.

Hijabu ndiyo alama pekee inayoweza kutambulisha Uchaji Mungu wa mwanamke na pia heshima yake na utu wake. Wakati huo huo tabia ya kutokuwa na Hijabu huchafua heshima ya mwanamke na kuacha maswali chungu nzima kuhusu Uchaji Mungu wake na kujiheshimu kwake kwa jumla.

Yote haya yanakuja kwa sababu yeye mwenyewe kauweka mwili wake kuwa maonesho mbele ya maelfu ya watu siku zote. Kutokana na hali kama hiyo, hata huwezi kutambua ni mikono mingapi iliyowahi kuushika mwili wake kwa kuuacha wazi na kutokujisitiri kwa mujibu wa sheria!.

Hivi unadhani watu wa kale na hata wa leo hii, nyoyo zao zitasal imika vipi katika mazingira hayo ya wanawake kuicha wazi miili yao? Kamwe hawatasalimika kabisa, kwani wanawake wanapoiacha wazi miili yao ni jambo linalopelekea tuhuma mbaya kwa wanawake. Imam Ali(a.s) anasema : "Yeyote mwenye kuiweka nafsi yake mahala penye tuhuma mbaya, basi asimlaumu mtu atakaye mdhania vibaya.[6] "

Hapana shaka kwamba, mwanamke asiyekuwa na Hijabu huwa anaidhuru nafsi yake mwenyewe kwa sababu. Kwanza, huwa anapata hasara mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Pili, heshima yake ndani ya jamii huwa inaporomoka.

Hasara anayoipata mwanamke huyo mbele ya Mwenyezi Mungu inakuja kwa sababu mwanamke huyo huwa amekwenda kinyume na kanuni za mbinguni na kukosa utiifu kwa Mwenyezi Mungu. Baadaye tutaeleza adhabu za huko akhera atakazozipata mwanamke asiyejali kujisitiri kwa mujibu wa sheria ya KiIslamu.

Ama hasara atakayoipata mwanamke kutoka na na heshima yake kuporomoka ndani ya jamii, hali hiyo inasababishwa na yeye mwenyewe kutokana na tabia yake ya kuyaacha wazi maungo yake yaonekane kwa kila mtu, hali ambayo humuingiza ndani ya kila aina ya uovu na ufisadi na hatimaye akadhalilika vibaya.

Na tukirejea kwa mwanamke mwenye kujisitiri kwa mujibu wa sheria ya kiislamu, huyu hupata faida za aina mbili kwa pamoja:

Faida aipatayo mbele ya Mwenyezi Mungu ni kwamba, yeye huwa ni mwanamke mtukufu mbele ya Mwenyezi Mungu na Malaika wake pamoja na Mawalii wa Mwenyezi Mungu. Utukufu huu anaupata kwa kuwa amemtii Mola wake, ametekeleza maamrisho yake na ameyasitri maungo ambayo Mwenyezi Mungu ameamrishsa yasitiriwe. Na kwa ajili hii basi, mwanamke kama huyu kamwe hatonyanyua unyayo wake bali rehma za Mwenyezi Mungu huwa ziko pamoja naye, pia radhi za Mwenyezi Mungu humbatana naye, na wakati huo huo Malaika wa Mwenyezi Mungu wanamuombea msamaha. Mwenyezi Mungu anasema: "Kilichoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora na ni chenye kubakia .[7] "

Ama faida atakayoipata ndani ya jamii, ni pale mwanamke huyo anapokuwa ni mwenye kuheshimiwa na kutukuzwa, yote haya anayapata kwa kuwa yeye amejipamba kwa pambo la kujiheshimu na kuuhifadhi utu wake, kisha akausitiri uzuri huo aliopewa na Mwenyezi Mungu.

Majadiliano Na Msichana Wa Kikristo.

Msichana mmoja wa Kikristo alikwenda kwa mwanachuoni wa kiIslamu na kumwambia. "Mimi nimefahamu mambo mengi kuhusu Uislamu na kwa hakika dini hii imenishangaza sana kwa kanuni zake na miongozo yake, na nimeupenda Uislamu kwa mapenzi ya kweli.

Lakini kanuni moja tu kwangu mimi imekuwa ni kikwazo kuingia katika Uislamu. Nimewauliza watu wengi kuhusu kanuni hiyo, mpaka sasa sijapata jawabu la kunitosheleza.

Iwapo wewe Sheikh utaweza kunibainishia hekima iliyomo ndani ya kanuni hii, basi nakuthibitishia kuwa nitaingia katika Uislamu."

Yule Mwanachuoni akasema, "Ni ipi kanuni hiyo?" Msichana akajibu. "Kanuni ya kuvaa Hijabu, ni kwa nini Uislamu haumuachi mwanamke akatoka nje apendavyo kama ilivyo kwa wanaume?" Mwanachuoni yule wa kiislamu akasema, "Je umepata kumuona sonara ameweka dhahabu na johari nyinginezo katika sanduku la kioo, kisha akalifunga sanduku hilo kwa kufuli? Msichana akajibu, "Ndiyo." Sheikh huyu akamwambia tena yule msichana, "Je, ni kwanini sonara hakuziacha johari hizo zikawa zinashikwa na kila mtu ajaye kutaka kununua? Kwa nini amezihifadhi ndani ya sanduku la kioo lililofungwa?" Msichana akasema: "Amefanya hivyo ili azilinde johari zake kutokana na wezi na mikono yenye khiyana." Yule Mwanachuoni akamwambia msichana: "Hii ndiyo hekima ya Hijabu, fahamu kwamba mwanamke ni johari ya thamani ambayo ni lazima kuilinda kutokana na waovu na wahaini.

Pia ni wajibu kumhifadhi mwanamke kutokana na macho ya watu waovu ndani ya kitu ambacho kitamsitiri barabara kama inavyolindwa lulu katika kola lake, ili asije akaangukia mikononi mwa watu hao na kumgeuza kuwa ngawira yao." Hakuna njia bora isipokuwa Hijabu, hicho ndiyo kizuwizi na ni mlinzi wa mwanamke. Kwa hakika mwanamke mwenye Hijabu huwa salama kutokana na shari. kwa kuwa mwili wake umesitirika, na mapambo yake nayo hayaonekani mbele ya kila mtu.

Hali ya kuvaa Hijabu inawafanya watu wasimtamani mwanamke huyo kwa kuwa hakuna wakionacho cha kuwafanya wamtamani. Kutokana na hali hiyo huwa wanamuepuka, wala hakiwageuzi kitu chochote cha kuwafanya wamuangalie mwanamke huyo, bali humuogopa na kumuheshimu. Mwisho wa yote watu humuogopa na kumpa heshima yake kama anavyostahiki. Yote hayo yatapatikana kwa ajili ya kuvaa Hijabu, na hali hii inamaanisha kwamba, Hijabu ndiyo mlinzi wako na ni hifadhi ya heshima, na utukufu wako. Ewe msichana huu ndio upande mmoja wa falsafa ya Hijabu."

Baada ya maelezo hayo ya Sheikh, msichana yule wa Kikristo alionesha furaha na akaridhishwa na maelezo ya Sheikh kisha akasema, "Sasa nimetosheka na falsafa iliyomo ndani ya kanuni hii ya kiislamu, na pia nimefahamu hekima iliyomo na ninapendezwa kuingia katika Uislamu." Baada ya hapo msichana akatoa Shahada mbili na akawa Muislamu. Majadiliano haya mazuri ya kidini yanatubainishia kwamba Uislamu unakusudia kuihifadhi hehsima na utukufu wa mwanamke, pia Uislamu unataka kuilinda jamii. Na kwa sababu hizo basi, Uislamu umewajibisha Hijabu kama sharti la msingi kuweza kutimiza malengo hayo.

BIBI FATIMA (A.S) KIIGIZO CHEMA KWA WANAWAKE

KIMEANDIKWA NA: MUHAMMAD IBRAHIM EL-QAZWINIY

Tofauti Ya Mwanamke Mwenye Hijabu Na Asiye Na Hijabu.

Mmoja wa marafiki zangu alinisimulia tukio la kufurahisha lililomtokea Muumini mmoja wa kiislamu. Tukio hili lilikuwa kama ifuatavyo. Siku moja Muumini huyo alikuwa akitembea pamoja na mkewe aliyekuwa kavaa Hijabu. Matembezi hayo yalimfikisha katika moja ya bustani zinazotembelewa na watu wa aina tofauti.

Ghafla Muumini huyo alijiwa na mtu fulani ambaye naye alikuwa na mkewe. Mke wa mtu huyu hakuwa amevaa vazi la Hijabu na hivyo basi kwa dharau na kejeli alimwambia yule Muumini. "Kwa nini umemvalisha mkeo Hijabu, kwa nini hukumuacha akatoka bila Hijabu kama jinsi alivyo mke wangu? Hijabu ina faida gani?" Jawabu alilotoa Muumini yule lilikuwa la kushangaza na la kishujaa. Alimwambia. "Je unafahamu tofauti ya mwanamke mwenye Hijabu na asiyekuwa na Hijabu? Bwana yule mwenye kejeli akasema "Nini tofauti yake?" Yule Muumini akajibu kwa njia ya kuuliza, je, kuna tofauti gani baina ya taxi na gari ambalo mtu hulitumia yeye binafsi? Yaani kwa matumizi yake pekee yake." Bwana yule akajibu akasema, "Taxi hutumiwa na kila mtu, wakati ambapo gari maalum linamuhusu mwenyewe peke yake. Hii ndiyo tofauti iliyopo." Basi yule Muumini akasema, "Hali hiyo ndio iliyopo baina ya mwanamke aliyevaa Hijabu na yule asiye na Hijabu.

Mwanamke asiye na Hijabu ni sawa na taxi ambayo kila mtu anaweza kuikodisha na kuitumia. Mwili wa mwanamke huyo huwa wazi na kuonesha mapambo yake na uzuri wake, na kuwafanya watu wavutike kutokana naye, jambo ambalo linaweza kusababisha kutendewa maovu, kama ambavyo mara kwa mara hali hii inavyowapata wanawake wa aina hii. Ama mwanamke aliyevaa Hijabu yeye ni bibi aliyemtukufu, ni maalum kwa ajili ya mumewe, mapambo yake na uzuri wake havionekani kwa kila mtu. Pia watu wenye nyoyo chafu na dhaifu hawamuangalii, na uso wake na mapambo yake havikutani na macho yenye khiana, kwa kuwa amehifadhiwa ndani ya Hijabu. Kwa hiyo utukufu wa mwanamke huyu na mwili wake vimo ndani ya hifadhi bora, pia bibi huyu hupendwa na kupendeza mbele ya mumewe na kumfanya mume kuwa na imani na mkewe, kwa sababu ya hifadhi hiyo inayomkinga kuwa na mahusiano na watu wengine kwa njia mbaya." Baada ya maelezo yaliyotolewa na yule Muumini wa kiIslamu, bwana yule mwenye kejeli aliona haya na akaanza kumwambia yule Muumini, "Najuta kwa kukuudhi, kwani maneno yako ni ukweli mtupu, na mifano uliyonipa ni sawa kabisa naomba samahani kwa haya niliyokutamkia na pia natubia kwa Mwenyezi Mungu kwa kitendo nilichokitenda na sasa. Kabla bwana huyu hajamaliza kujieleza mkewe alimkatiza na kusema. "Naam, naapa maneno haya aliyosema bwana huyu ni sawa na mfano aliotoa ni mzuri sana, kwani kabla ya leo nilikuwa sijasikia mawaidha kama haya. Mfano huu umeniingia moyoni nami pia natubia kwa Mwenyezi Mungu."

Baadaye yule mume akarudia kukamilisha usemi wake akasema, "Na mimi sasa naiamini Hijabu na kuanzia leo mke wangu ataingia katika uwanja mtukufu kwa kuvaa Hijabu. Kamwe sikubali mke wangu atoke bila Hijabu, kwani ndiyo vazi la amani na imani. Nafsi yangu haipendi kabisa kumuona mke wangu akidhihiri mbele za watu kama kwamba yeye ni kwa ajili ya kila mtu."

Ni Lipi Lengo La Wanaopinga Hijabu?

Baada ya kuusoma Uislamu kwa undani, maadui wa Uislamu wameandaa mikakati ya kuuangamiza Uislamu na Waislamu kidogo kidogo, bila Waislamu kuigundua hali hii isipokuwa wachache. Na miongoni mwa mikakati yao ya kishetani katika kutilia mkazo kuiondoa Hijabu, wametumia na bado wanatumia kila njia za kuvutia na madai batili kutimiza lengo lao hilo. Kuna mambo mengi machafu wanayoyaeneza katika jamii ya Waislamu, chini ya kiza kinene chenye ibara zinazovutia na kampeni ambazo matokeo yake ni mabaya. Kwa kutumia mbinu za kimaendeleo na utaalamu, wamefaulu kuwapotosha Waislamu, na wakasambaza uovu mwingi. Kwa madai hayo hayo ya maendeleo na kupigania uhuru na haki za binadamu, uchafu wao umeenea ndani ya jamii zetu za kiislamu. Kwa hakika wamefaulu kuzinyang'anya jamii zetu maumbile ya kuwa na haya na heshima. Ibara hizi zimewahadaa Waislamu wengi, wake kwa waume.

Masikini Waislamu hawa wamekuwa wafuasi wa itikadi hizi zenye sumu kali inayovuja kuelekea kwenye maovu na maangamio. Wanawake wa kiislamu na mabinti wa kiislamu wanafanya upinzani hadharani dhidi ya vazi hili la kiislamu. Wametoka katika nyumba ya utukufu na imani na kuingia katika nyumba ya kiza na upotovu. Wanawake wetu na wasichana wetu wameathiriwa na mavazi ya Kiyahudi na Kikristo yatokayo kwa wapinzani wa kimagharibi na makafiri wa mashariki. Maadui na wavamizi hawa wamefanikisha kwa kiasi kikubwa lengo lao, kwa kuwa sasa hivi jamii ya kiislamu imekwisha tumbukia na kuzama katika dimbwi la matendo machafu. Jamiii ya kiislamu ambayo asili yake ni adilifu na yenye muruwa, leo imegeuka na kushika bendera ya maovu ya kila aina.

Matukio ya kubaka,[8] kupora, udanganyifu, dhulma, kutoa mimba na mengineyo, yameivamia jamii yetu tukufu. Watu hawa wa Ulaya magharibi na mashariki yake, hawali wakashiba wala hawalali wakapata usingizi, ila mpaka watimize lengo lao la kutuachisha utamaduni wetu wa kiislamu.

Ni wazi kabisa kwamba watu hao wanaomtaka mwanamke wa kiislamu avue Hijabu lengo lao wanataka wamuone mwanamke huyu anafanya ufisadi kwa kumlazimisha akae uchi. Nia yao ni kumuangamiza na kuipotosha jamii kwa jumla. Kumtaka mwanamke asivae Hijabu ni kumuondolea heshima yake na uchamungu wake.

Ewe msomaji wangu, iwapo utataka kuyafahamu vizuri maneno yangu, muulize mzee yeyote katika wazee wa makamo na mababu ambao bado wanayo kumbukumbu ya hali ya mambo ilivyokuwa hapo zamani. Waulize kwa kusema, "Hivi maovu haya yaliyopo sasa hivi ya kuwavunjia heshima wanawake na kuwabaka, na watu kudhulumia, mambo haya yakulikuwepo hapo zamani kabla ya miaka ishirini au thelathini iliyopita?" Watakujibu kwa nguvu zao zote, kwa kusema, Hapana kabisa hayakuwako."

Sasa yametoka wapi mambo haya maovu na matukio ya kuhuzunisha? Watakuambia, "Hali hii imetokana na mambo mengi, miongoni mwake ni wanawake wenyewe kutembea mabarabarani bila sitara ya kisheria."

Hili ndilo jibu sahihi kwa matatizo kama haya ya ubakaji ambayo takwimu zake zinaongezeka kila siku. Iwapo utataka uhakika zaidi, waulize wakazi wa miji michache ambayo wakazi wake bado wanashikamana na sheria za kiislamu na imani zao zingali hai na uwaambie, "Hivi katika miji yenu kuna matukio maovu ya kubaka na unyang'anyi kama inavyotokea katika miji mikubwa?" Bila shaka watakujibu hapana. Sababu kubwa ya kutokuwepo maovu kwa wingi katika sehemu hizo, ni kwa kuwa jamii bado inauheshimu na kuulinda Uislamu na kanuni zake zenye hekima.

Maovu mengi zaidi yanajitokeza katika miji au sehemu ambazo zinadai kuwa zimeendelea. Miji hiyo imehusika kwa kiwango kikubwa na ongezeko la maovu ambayo yanakithiri kwa kasi ya kutisha, licha ya serikali zao kutoa adhabu kali kwa wanaohusika kila wanapobainika na kukamatwa[9] .

Hali hii inaonyesha wazi kwamba kanuni peke yake hazitoshelezi, wala hazinufaishi katika kuirekebisha jamii, bali kinachotakiwa ni kuing'oa mizizi ya maovu kwanza, ili maovu hayo yapate kunyauka yenyewe. Kwa kawaida kila kitu kina asili yake, na asili ya maovu yaliyozikumba jamii zetu sasa hivi, ni hizi picha za video wanazooneshwa vijana wetu, picha ambazo huwa zinaonesha hali ya maumbile ya siri, isitoshe huonesha pia matendo ya jinsiya baina ya mke na mume bila kuona aibu wala huzuni kuuchezea na kuudhalilisha uanadamu ambao ni kitu cha thamani, kutokana na kuwa na uwezo wa kutambua nini cha kufanya na nini si cha kufanya. Kitu kingine kinachochangia ni nchi zetu zinaporuhusu uingizaji wa magazeti na majarida yanayochapisha picha zinazoonesha sehemu za siri na kisha magazeti hayo na majarida yanasambazwa katika jamii. Maadam asili ya maovu bado ipo kama mifano ya picha za video na majarida tuliyoyataja hapo kabla, basi maovu na matukio machafu yataendelea kutokea siku hadi siku, na kamwe hayataondoka kwa kutegemea kanuni hizi za kidunia.

Ni Yupi Mwanamke Bora

Sasa napenda kutoa mifano miwili ya wanawake wawili ambao kila mmoja anao mwelekeo wake na mwenendo tofauti na mwenzake, lakini wote wanaishi katika jamii moja. Wa kwanza ni yule mwanamke mwenye kuvaa Hijabu ambayo ni sitara ya imani na ni vazi la kiislamu, tena ni vazi la heshima na humpa utukufu mvaji.

Kwa kuvaa Hijabu, mwanamke huyu atakuwa amepata radhi za Mola wake na kupata utukufu wa watu wa peponi. Kwa vazi hili mwanamke huyu huvutia mvuto wa ucha Mungu na heshima. Pia dalili za utulivu hujitokeza kwa mwanamke huyu na dhana njema kwake hutawala fikra za kila amuonaye. Amtazamapo mwenye kumtazama, huwa ni shida kutambua, je, mwanamke huyu ni msichana au ni mtu mzima? Sura yake ikoje nzuri au la? Hutatizika wanaomuangalia. Matokeo yake watu humuangalia kwa jicho la heshima, hakuna awezaye kumkabili kwa maneno chafu au maudhi, kwani anafahamu wazi kwamba mwanamke huyo ameshikamana na dini yake na anaheshimu utu wake. Isitoshe mwanamke kama huyu huwa amejitenga na matendo ya aibu na kujiepusha na wanawake wasio na sitara, na kwa ajili hiyo hayuko tayari kuidhalilisha nafsi yake.

Huo ndiyo mfano wa mwanamke mmoja na namna alivyojiweka katika jamii yake. Kwa upande wa yule mwanamke wa pili, ni yule asiyejali kujisitiri uso wake amevua vazi la la stara, hana aibu wala haya. Kwa maana hiyo ameing'oa imani yake, kwa sababu Mtume anasema: "Mtu kuwa na haya ni sehemu ya imani, na mtu asiye na haya hana imani." Kwa mwenendo wake mwanamke huyu, huwa ni mpinzani mkubwa wa muongozo wa Qur'an na huwa anajidhalilisha kwa kuonesha mapambo yakem, kama walivyokuwa wakionesha mapambo yao wanawake wa zama za kijahiliya kabla ya kuja Uislamu. Isitoshe kwa mwanamke huyu, hali aliyo nayo huwa amejifananisha na wanawake wa Kiyahudi na Kikristo, na huwa yuko mbali na heshima yake na utu wake. Kutokana na kuudhihirisha mwili wake na uso wke na mikono yake, pia kifua chake na sehemu nyingine katika maumbile ya kike. Watu waovu na wenye tamaa huyaona wazi wazi maumbile yake na hapo tayari anakuwa mfano wa bidhaa zilizotandazwa sokoni, kwani kila mtu ana uhuru wa kuziangalia bila mipaka.

Matokeo ya uovu wa mwanamke huyu, ni kupata usumbufu toka kwa wahuni ambapo hatimaye wanaweza kumtendea matendo machafu yanayoweza kumharibia tohara yake. Na iwapo itafikia hali ya kuharibiwa tohara yake, basi atakuwa amepoteza heshima yake na utu wake katika jamii. Hii ni kwa sababu ameacha kuulinda mwili wake ndani ya vazi la kisheria.

Baada ya kuwa mmefahamu namna za wanawake hawa wawili sasa tuwe pamoja kaitka kulinganisha hali zao kati yao na tujiulize masuali yafuatayo.

1.Je ni yupi mwanamke bora baina yao?

2.Yupi kati yao ni mtulivu na anayevutia,

3.Mwenye kujilinda au yule anayeuacha wazi mwili wake?

4.Ni yupi mwenye kuheshimika kati yao, mwenye Hijabu au yule asiye na Hijabu?

Bila shaka, mwanamke mwenye Hijabu na ucha Mungu ni bora na ni mtukufu tena ni mwenye thamani kuliko yule mwingine.

Kipindupindu Ndani Ya Jamii

Miongoni mwa maradhi yanayoua haraka ni kipindupindu kwa mujibu wa taarifa ambazo huwa zinatolewa baada ya maradhi hayo kuingia katika kijiji au mji. Kila yanapodhihiri maradhi haya, hutangazwa hali ya hatari katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na kuwekwa karantini. Kama ilivyo katika kuzuia kipindupindu kisienee katika mji au kijiji, na fisadi nyingine ni hivyo hivyo. Sasa basi mtazamo wa Uislamu katika kuitazama jamii ni mtazamo wenye hekima kubwa, na ni mtazamo ambao lengo lake ni kujenga jamii nzuri na safi isiyokuwa na maovu ndani yake. Miongoni mwa mambo yanayoweza kudhibiti amani na ubora wa jamii ni mavazi. Siyo kweli kwamba kila vazi linaweza kukidhi haja hii, bali Hijabu pekee ndiyo jawabu, kwa sharti ya kuwa mvaaji aivae kwa kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu na siyo kinyume chake[10] .

Hijabu humlinda mwanamke kutokana na ufasiki na inamzuia kukhalifu maumbile yake aliyopangiwa kuishi ndani yake. Kwa kanuni hii ya Hijabu, Uislamu unakuwa umeisalimisha jamii na kuilinda isije ikajikuta imeteleza na kuvamiwa na maovu. Hali halisi inayojitokeza katika malengo ya msingi kuhusu kanuni hii ya Hijabu, ni kuitakasa jamii na kuisafisha, pindi wanawake watakapofuata sheria ya kuvaa Hijabu. Kinyume chake haitawezekana kabisa kudai kwamba jamii yetu ni safi, wakati wanawake zetu wanatembea bila kujali ni nguo gani wamevaa, kwa kuwa suala la mavazi kwa wanawake linataka litazamwe kwa mapana na marefu isiwe mradi kuvaa tu. Ni mara ngapi tunashuhudia mambo ya aibu na ya kuhuzunisha wanafanyiwa wanawake? Hivyo uchafu unasambaa haraka na kuleta madhara kwa wingi, kama kipindupindu kilichoingia mjini au kijijini. Na kwa ajili hiyo karantini inahitajika kuwekwa na kufuatwa kwa mujibu wa maelekezo ya wataalamu.

Uislamu kwa upande wake unataka kukata na kung'oa mizizi ya fitina na maovu kwa kutumia njia mbali mbali ikiwemo kusisitiza vazi la Hijabu. Pia Uislamu kwa nafsi yake unapinga kwa nguvu uovu na kila jambo linalokuwa ni sababu ya kueneza uchafu ndani ya jamii, miongoni mwa sababu hizo ni mwanamke kutokuwa na Hijabu ambayo ni vazi la kisheria.

Kukosekana Sitara Kunaleta Maovu.

Miongoni mwa maovu na athari mbaya katika jamii, ni wanawake kuacha kuisitiri miili yao ipasavyo, kitu ambacho kimesababisha vijana wetu wa kiume kuteleza na kujikuta wanafanya mambo machafu bila kukusudia. Imam Ali ibn Musa Ar-ridha anasema, "…….Imeharamishwa kuangalia nywele za wanawake, kwani katika kuziangalia nywele hizo kunasababisha kuamsha hisia za wanaume ambazo huwafanya waingie katika maovu na mambo yasiyo halali na yasiyopendeza."[11] Hapana shaka kwamba, mwanamke anayetoka nyumbani mwake na kwenda sokoni bila kujali ni vazi gani alilovaa, hajali kama limemsitiri vizuri au hapana, ni wazi kabisa huko njiani ataonekana kwa watu wa aina mbali mbali wakiwemo vijana ambao ndiyo kwanza wanaingia katika rika la ujana na nafsi zao bado hazijaweza kujimiliki kuhusu suala la kijinsiya. Hali kama hii ni lazima itaamsha hisia za kimaumbile za vijana hao kutokana na jinsi mwanamke huyo atakavyokuwa amevaa na umbile lake linavyoonekana kwa jumla pindi atakapopita mbele yao. Hisia hizi za kimaumbile ni lazima ziamke kwa kuwa ndivyo ilivyo hali halisi. Kwa hali hii basi nafsi za vijana hawa kwa tabia ya maumbile ya mwanaadamu huanza kuhangaika kutafuta njia za kuyatosheleza maumbile yao.

Suala la kujiuliza hapa ni je, vijana hawa watafanya nini? Ikiwa wao sio watu walioshikamana na mafunzo ya dini wala hawafuati miongozo ya kiislamu, basi watajaribu kutosheleza hamu zao kwa njia ya siri ambayo ni kujitoa manii jambo ambalo ni hasara na aibu. Ama wengine hufanya baya zaidi ambalo ni kinyume cha utaratibu aliotuwekea Mwenyezi Mungu, hawa hufanya liwati. Kundi jingine wao huamua kuzini na katika huko kuzini huwa wanatumia kila njia kufanikisha azma yao hiyo, ikiwa ni kwa hila au hata kwa nguvu ambayo ni kubaka wanawake mitaani. Matokeo ya ubakaji ni kuvunja heshima za watu na kuwadhalilisha wanawake.

Pamoja na matendo haya kwenda kinyume na maamrisho ya Mwenyezi Mungu, pia yanasababisha maradhi hatari na vifo vya ghafla[12] .

Inakadiriwa kwamba idadi ya hospitali zinazo shughulikia maradhi ya uasherati peke yake inafikia hospitali mia sita hamsini.

Hesabu hii ni kwa nchi ya Marekani peke yake. Chanzo cha balaa lote hili ni kwa wale wanawake wasiojali kutenganisha maumbile yao na ya wanaume mpaka wakawa wanaona miili yao haistahiki kulindwa na kupewa hadhi ya pekee. Lakini kila mwanamke asiyezingatia suala la mavazi kisheria ni lazima atambue kwamba, yeye ni mshiriki mkubwa anayesababisha madhambi na misiba hii, na anayo sehemu yake ya adhabu mbele ya Mwenyezi Mungu.

Yote yaliyotajwa hapa sasa hivi, yanatokana na vijana ambao wao siyo watu wa dini wala hawashikamani na Uislamu. Kwa upande wa pili inawezekana vijana hao wakawa ni watu wa dini na wanaambatana na mafunzo ya kiislamu na sheria zake, basi vijana hao huzuia hisia zao zisivuke mipaka ya Mwenyezi Mungu na hupambana na matamanio ya nafsi zao na kumlaani shetani asije akawahadaa. Vijana hawa huvumilia kero ya maumbile na kubeba mzigo mzito ambao hawakutarajia kuubeba. Kwa mara nyingine tena mwanamke au wanawake wasiojali sheria ya mavazi kama Mwenyezi Mungu alivyoamrisha, wanabeba uzito wa taabu na maudhi yanayowapata watu hawa wa dini.