BIBI FATIMA (A.S) KIIGIZO CHEMA KWA WANAWAKE

BIBI FATIMA (A.S) KIIGIZO CHEMA KWA WANAWAKE60%

BIBI FATIMA (A.S) KIIGIZO CHEMA KWA WANAWAKE Mwandishi:
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi: Faatima (a.s)

BIBI FATIMA (A.S) KIIGIZO CHEMA KWA WANAWAKE
  • Anza
  • Iliyopita
  • 11 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 12109 / Pakua: 3167
Kiwango Kiwango Kiwango
BIBI FATIMA (A.S) KIIGIZO CHEMA KWA WANAWAKE

BIBI FATIMA (A.S) KIIGIZO CHEMA KWA WANAWAKE

Mwandishi:
Swahili

1

BIBI FATIMA (A.S) KIIGIZO CHEMA KWA WANAWAKE

KIMEANDIKWA NA: MUHAMMAD IBRAHIM EL-QAZWINIY

Ewe Mume Mwema

Jukumu lako ewe mume kuhusu suala la ndoa ni muhimu sana mbele ya Mwenyezi Mungu, kwani unawajibika kutengeneza na kurekebisha mwenendo na tabia ya mkeo.

Mwenyezi Mungu amekufanya uwe msimamizi wa mkeo na kiongozi wake. Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema:

الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنْفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ.

"Wanaume ni walinzi juu ya wanawake kwa sababu Allah amewafadhilisha baadhi yao kuliko wengine na kwa sababu ya mali zao walizozitoa ." 4:34.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنْفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ.

Na Mwenyezi Mungu anasema: "Enyi mlioamini jiokoeni nafsi zenu na watu wenu kutokana na moto ambao kuni zake ni watu na mawe " 66:6.

Na ili uweze kutekeleza wajibu wako kisheria na majukumu yako ya dini kama alivyoamuru Allah s.w.t na Mtume Wake, ni lazima uambatanishe mafunzo na maelekezo ya Kiislamu kwa vitendo kama ifuatavyo.

Hijabu liwe ni jambola mwanzo : Unalazimika kumuamuru mkeo avae Hijabu kama alikuwa havai, na pia umuoneshe dalili za kutosheleza na kukinaisha kuhusu Hijabu. Hii ni kwa sababu atakapovaa awe anafahamu na kuelewa umuhimu wa kanuni hii ya Kiislamu. Endapo utashindwa kumkinaisha kimaelezo basi fuatana naye hadi kwa Sheikh ambaye ataweza kumfahamisha kwa maelezo yatakayoonesha umuhimu wa falsafa inayopatikana katika Hijabu. Na ikiwa kuna njia nyignine ya kumfahamisha kama vile kumtafutia vitabu ajisomee yeye mwenyewe ni bora kumpatia.

Imam Ali(a.s) anasema kumuusia mwanawe Muhammad AlHanafiyya: "Umuhimu wa Hijabu ni kitu bora kwako na kwao wanawake, ili muondokane na shaka. Kutoka nje (kwa matembezi ya kawaida) na wanawake siyo jambo baya kuliko wewe kuja na mgeni mwanaume asiyeaminika nyumbani mwako kisha ukamtambulisha kwao (wanawake) na iwapo utaweza kutowatambulisha wake zako kwa yeyote basi fanya hivyo ."[30]

Imam Ali anamaanisha kwamba, mume asimtambulishe mkewe kwa wanaume wasiomuhusu mkewe, kwa kuwa jambo hili husababisha fitna.

Jambo la pili : Tahadhari na sherehe zenye mchanganyiko: Ewe mume mwema, epukana na mahafali na sherehe zenye mchanganyiko wa wanaume na wanawake. Usimpeleke mkeo sehemu hizo, muepushe mbali kabisa na mikesha ya nyimbo na magoma. Kumpeleka mkeo, katika majumba ya sinema kunachangia kwa kiasi kikubwa kuharibu mwenendo wa mkeo na pia hali hii itasaidia kumfanya asiwe na aibu na heshima yake itatoweka.

Mume anayempeleka mkewe sehemu zenye sherehe zenye mchanganyiko wa wanawake na wanaume, au anayemuingiza mkewe katika majumba ya sinema, mume huyu ni haini wa kwanza dhidi ya mkewe. Yeye ndiye dhalimu atakayekuwa mfundishaji wa mwelekeo mbaya wa mkewe.

Dhoruba la uovu atakalolianzisha mume huyu dhidi ya mkewe, bila shaka litaanza kumpiga yeye mwenyewe, ili ayaone matunda ya kazi yake hiyo mbaya. Dhoruba hili si jingine, bali ni pale mkewe atakapofanya hiyana ya kuanzisha uhusiano na watu wengine. Hivyo ni wajibu wako wewe mume kumuepusha mkeo kutokana na maeneo ya uovu na mengineyo machafu. Asiyakaribie maeneo hayo licha ya kwenda ili uishi kwa amani na nafsi iliyotulia.

Jambo la tatu : Usimtii mkeo: Inakulazimu uishi maisha ya muongozo wa dini ya Mwenyezi Mungu na hukumu zake na utahadhari na kila mwelekeo mbaya na wa kupotosha. Kwa kuwa utulivu wa nafsi yako hupatikana toka kwa mkeo, basi huenda akataka umfanyie jambo ambalo Mwenyezi Mungu kaliharamisha. Iwapo hali hii itajitokeaza kwa mkeo, jaribu kumuleza kwa upana hukmu ya Mwenyezi Mungu kuhusu ombi lake hilo ili atambue ubaya wa jambo hilo. Haifai kabisa kumtii mkeo (hata mtu mwingine) katika mambo ya kumuasi Mwenyezi Mungu s.w.t kwani hapana twaa ya kumtii kiumbe katika kumuasi Muumba.

Hivi sasa soma hadithi ifuatayo: Mtume(s.a.w.w) anasema: "Mwenye kumtii mkewe Mwenyezi Mungu atamuingiza motoni mtu huyo. Mtume(s.a.w.w) akaulizwa huko kumtii mke ni namna gani? Mtume akasema: Mke kuomba ruhusa kwa mumewe kwenda kwenye starehe na michezo hali ya kuwa kavaa nguo nyepesi (na mume akatoa ruhusa).[31] "

Kwa hiyo basi, usimruhusu mkeo kuhudhuria sherehe au harusi zenye mchanganyiko na usimkubalie kuvaa mavazi mepesi mbele ya wanaume wengine kwa kuwa yote haya hayamridhishi Mwenyezi Mungu.

Jambo la nne : Kuwa na wivu kwa mkeo: Huna budi ewe mume kuwa na wivu kwa mkeo, kwani imekuja hadithi kutoka kwa Imam Jaafar Sadiq(a.s) kwamba: "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ana wivu na anampenda kila mwenye wivu, na kwa wivu wake Allah (s.w.t) amekataza maovu yafanywayo dhahiri na yale yafanywayo kwa siri.”[32] Kwa ajili hiyo basi ni lazima umuhifadhi mkeo na binti zako kitabia, pia mavazi ili msijefikwa na balaa na ghadhabu za Allah (s.w.t). Amesema Imam Jaafar(a.s) kwamba: "Pepo imeharamishwa kwa mtu duyuuth (asiye na wivu)." Na amesema tena Imam Jaafar(a.s) "Watu wa aina tatu Mwenyezi Mungu hatawasemesha siku ya kiama wala hatawatakasa

1. Sheikh (mwanachuoni) mzinifu .

2. Duyuuth (asiye na wivu)

3. Mwanamke anayemlaza mwanamume mwingine kwenye kitanda cha mumewe ."[33]

Na katika kuonesha kuwa una wivu, ni kutomwacha mkeo au mmoja kati ya watu wa nyumba yako, wakiwemo mabinti zako wakatoka nje hali ya kuwa wamejitia manukato na madawa ya kujirembesha na mapambo mengine. Hapana shaka kwamba jambo hilo huwa linatishia heshima yako na yao ndani ya jamii, na matokeo ya hali hiyo ni mabaya mno. Mtume(s.a.w.w) amesema: "Mwanaume yeyote atakayemwacha mkewe ajipambe na kisha mwanamke huyo akatoka nyumbani mwake akiwa katika hali hiyo, basi mume huyo atakuwa ni duyuuth (hana wivu) .

Na ikiwa mke huyu atatoka nyumbani mwake hali kajipamba na kutia manukato na mumewe akawa radhi, mumewe atajengewe nyumba ndani ya moto kwa kila hatua moja atakayotembea mkewe[34] . Bwana Mtume(s.a.w.w) anasema kuwa: "Aina kumi za watu hawataingia peponi mpaka kwanza watubie:…. Miongoni mwa hao kumi Bwana Mtume alimtaja Duyuth, na akaulizwa, ni nani huyo Duyuth? Akasema ni yule mwanaume asiyekuwa na wivu kwa mkewe[35] .

Imetokea zaidi ya mara moja, kwangu mimi kumuona mtu anakula chakula ndani ya mgahawa au hoteli hali ya kuwa na mkewe na watu wengine wakiwa wanamuangalia mtu huyo na mkewe. Cha ajabu ni kwamba bwana huyo anapokuwa katka mazingira hayo anakuwa yuko huru bila wasiwasi kabisa. Hajali kama kuna sitara yoyote au hapana, na wala hana hata habari juu ya kuwa mkewe kavaa Hijabu au hapana. Kama ambavyo sasa hivi iko wazi kabisa kule kuwako kwa mabustani na maeneo ya matembezi yanayotembelewa na watu wengi wake kwa waume. Kwa hakika jambo hili bila kificho ni jambo baya mno linalohatarisha usalama wa jamii. Kuna Mkurugenzi wa mgahawa mmoja aliniambia kuwa: "Wako baadhi ya watu wanakataa kula chakula ndani ya vyumba maalum vilivyotengwa kwa ajili ya watu wenye familia, na wanaona ni bora wale chakula mahali pa wazi hali ya kuwa wamefuatana na familia zao!" Kama hali ni hii, uko wapi basi wivu wa wanaume kwa wake zao enyi Waislamu?

Mfundishe mkeo Surat An-Nur. Inapendekezwa kwako ewe mume kumfundisha mkeo surat Annur na tafsiri yake, kwa kuwa ndani yake mna Aya nyingi zinazozungumzia mas'ala ya wanawake.

Aya hizo zimedhibiti mambo mengi ambayo yanamlazimu mwanamke ayafahamu ili aishi maisha bora ya Kiislamu na awe mbali na maovu. Mtume wa Mwenyezi Mungu anasema: "Wafundisheni wanawake surat An-nur kwani ndani yake mna mawaidha mengi (kwa wanawake).[36]

Usimuweke mkeo katika chumba cha barabarani. Bwana Mtume(s.a.w.w) amekataza kuwaweka wawnawake katika vyumba vya barabarani akasema: "Musiwaweke wanawake katika vyumba vya barabarani." Makusudio halisi ya hadithi hii ya Bwana Mtume(s.a.w.w) ni kuwaonya wanaume juu ya kuwaweka wake zao katika vyumba vinavyotazamana na barabara.

Zaidi ya hapo ni lazima tufahamu hata vyumba vinavyotazamana na masoko na maeneo mengine yenye msongamano wa watu ni hatari kuwaweka wanawake ndani ya vyumba hivyo. Imekuja katika hadithi kwamba, miongoni mwa hatua ambazo Imam Mahdi(a.s) atazichukua katika kurekebisha hali ya Umma pindi dola yake itakaposimama, ni kuondosha madirisha yanayoelekea barabarani.[37]

Pengine utajiuliza kwamba ni ipi hekima ya jambo hilo? Jawabu lake ni hili lifuatalo: Hapana shaka kwamba madirisha yanayotazama barabarani ni kichocheo kikubwa katika kuleta uharibifu ndani ya ndoa za watu na pia kuvuruga familia. Na sababu yake ni kwamba dirisha hilo huwa ni nyenzo ya kumfanya mtu aone ni kitu gani kilichomo ndani ya chumba na hasa katika majengo ya ghorofa kadhaa. Majengo haya huwa yanaonesha kila kilichomo ndani ya chumba hicho kwa wapita njia na hata watu wanaoshi mkabala na majengo hayo.

Sasa basi uharibifu wa familia na ndoa za watu unaweza kuja kutoka katika moja ya pande mbili, yaani upande wa mwanamke aliyemo ndani ya jengo hilo au yule mwanaume mpita njia. Kwa mfano mwanamke ikitokezea akachungulia njiani kwa kupitia dirishani na kwa bahati mbaya mmoja kati ya wapita njia akimuona na moyo wake ukaingia namna fulani ya kumpenda huyo mwanamke, basi hapo ndipo unapoanzia ule msiba wa maovu. Na pengine mwanaume naye anaweza kuwa amesimama dirishani na mara akamuona mwanamke kwenye ghorofa lililoko mkabala na ghorofa analoishi yeye, basi kutokana na mazingira ambayo hayapingiki ni kuwa bila ya shaka mwanamke huyo atakuwa hakujisitri kwa kutambua kuwa yumo ndani mwake. Katika hali kama hii tunataraji matokeo gani baina ya wawili hawa ikiwa hawatamuogopa Mwenyezi Mungu? Hapana shaka kwamba Bwana Mtume(s.a.w.w) amesema kuwa:

"Yeyote atakayechungulia ndani ya nyumba ya jirani yake kisha akaona tupu ya mwanaume au nywele za mwanamke au akaona sehemu yoyote ya mwili wa mwanamke, basi Mwenyezi Mungu atakuwa na haki ya kumuingiza motoni mtu huyo pamoja na wanafiki ambao walikuwa wakifuatilia tupu za wanawake hapa duniani na wala Mwenyezi Mungu hatamtoa ulimwenguni mpaka kwanza amfedheheshe na audhihrishe wazi utupu wake huko akhera.[38]

Hekima inatwambia kwamba: "Kinga ni bora kuliko tiba." Hali inajieleza wazi kwamba, ni mara nyingi tiba imekuwa ni jambo lisilo na mafanikio, wakati ambapo kinga imekuwa ni dhamana yenye nguvu. Kwa hakika miongoni mwa mambo yanayohuzunisha ni kuona kwamba jamii kwa jumla inaishi nje ya mafunzo haya ya Kiislamu yenye ulinzi madhubuti.

Utamuona mwanamke anatoka barazani hali ya kuwa kavaa nguo zinazostahili kuvaliwa ndani, kisha katika hali kama hiyo anaanika nguo kwenye kamba. Au utamkuta mwanamke anachungulia njiani katika hali ile ile huku akiwa amejisahau kwamba kwa kufanya hivyo anajiletea msiba na huzuni yeye binafsi na familia yake. Basi ni juu yako ewe mume mwema uzindukane na ushikamane na mafunzo bora ya Kiislamu, na pia uyatumie ndani ya maisha yako ya ndoa na familia yako kwa jumla mpaka ifikie hali ya maisha yako na familia yako kuwa maisha mema yenye kuepukana na fedheha za duniani na udhalili wa huko akhera.

Mafunzo ya Kiislamu. Ndugu Mwislamu pokea baadhi ya mafundisho ya Kiislamu ambayo Mwenyezi Mungu ametuamrisha kuyatumia katika maisha yetu ya kijamii. Mafunzo haya yanalenga kumhifadhi mtu kutokana na uovu pia kumlinda asiteleze na kuingia makosani.

Kwanza: Usimuangalie mke asiyekuhusu.[39] Kumtazama mwanamke asiyekuhusu ndiyo hatua ya kwanza kuelekea kwenye uharibifu wa tabia na ndiyo ufunguo wa shari na kutelezesha watu. Katika kumtazama mara moja hutokea ukavutika na kuongeza mtizamo wa pili, na hatimaye watatu na mwisho husababisha nia mbaya katika nafsi.

Mshairi mmoja anasema: Kutazama ndiyo hatua ya mwanzo, tabasamu hufuatia, kisha salamu. Kinachofuata ni mazungumzo, na hatimaye ahadi hufungwa na mwisho wa yote kitendo hutimia.

Kwa sababu kama hizi, Uislamu kwa kutaka kukata mizizi ya fitina umekataza jambo hili.

Mwenyezi Mungu Mtukufu ameharamisha kumtazama mke asiyekuhusu, na akaonya kwa onyo kali. Isitoshe Mwenyezi Mungu amewaamuru Waumini wa kiume wainamishe macho yao wasiwatazame wanawake wasiowahusu Akasema:

قُلْ لِلْمُؤْمِنِينَ يَغُضُّوا مِنْ أَبْصَارِهِمْ وَيَحْفَظُوا فُرُوجَهُمْ ۚ ذَٰلِكَ أَزْكَىٰ لَهُمْ ۗ إِنَّ اللَّهَ خَبِيرٌ بِمَا يَصْنَعُونَ

"Waambie Waumini wanaume wainamishe (chini) macho yao na wazilinde tupu zao, kwani kufanya hivyo kuna utakaso kwa ajili yao. Na hakika Mwenyezi Mungu anafahamu wanayotenda .[40] "

Hapana shaka kwamba tabia ya kibinaadamu ni tabia inayopelekea mvuto baina ya jinsiya mbili hizi , yaani ya kiume na ile ya kike kwa sababu tu ya kila mmoja kumtazama mwenzake. Kwa hiyo basi, ni lazima tabia hii iwekewe mipaka kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu, vinginevyo matokeo ya maisha ya jamii ya wanaadamu yataingia ndani ya ufisadi na matokeo ya ufisadi huo ni mabaya. Imam Jaafar As-sadiq(a.s) amesema: "Kuangalia kwa kukazaia macho kunapanda mbegu ya matamanio ndani ya moyo, na kwa hakika inatosha kuwa ni fitna kwa mwenye kuangalia namna hiyo." Hapana41 shaka kwamba kuangalia huko kulikoharamishwa na sheria, ndiko kunakoandaa maovu hapa duniani, na kwa ajili hii kumekuja maonyo ndani ya hadithi kama ifuatavyo: "Kuangalia ni mjumbe wa uzinifu.

"Hadithi hii inatufunza kwamba, mwanzo wa uzinifu hupatikana kwa njia ya kuangalia kulikoharamishwa na sheria. Jambo hili liko wazi kwa kuwa, uzinifu haupatikani ila baada ya mwanaume kumkazia macho mwanamke, na ndiyo maana tukaambiwa ndani ya ile hadithi iliyotangulia hapo kabla kwamba:

"Kuangalia kulikoharamishwa ni mjumbe wa uzinifu." Kwa maelezo haya ndugu msomaji, wala hakuna haja ya kuuliza juu ya athari mbaya zinazojitokeza kutokana na uzinifu ikiwemo maradhi mabaya yanayosababishwa na tendo hilo chafu. Isitoshe hali hiyo, bali kuna uharibifu mkubwa mno ndani ya jamii. Na kila ukichunguza utakuta kuwa uzinifu ndiyo chanzo cha misiba hii, na ambayo chimbuko lake ni kumuangalia mwanamke asiyekuhusu kwa mujibu wa sheria. Nabii Yahya ibn Zakariyya(a.s) aliulizwa kuhusu chanzo cha uzinifu akasema: "Ni kumuangalia (mwanamke asiyekuhusu) na nyimbo." Siyo jambo la ajabu kuwa, sheria imekuja kuyakataza kwa mkazo sana mambo haya, na wala siyo jambo la kushangaza kuwa, huko akhera kutakuwa na adhabu kali na ngumu kwa watendao matendo haya. Imekuja ndani ya hadithi tukufu ya Mtume(s.a.w.w) kwamba: "Mtu yeyote atakayeyajaza macho yake kwa kumuangalia mwanamke ambaye ni haramu kwake, Mwenyezi Mungu atayajaza macho yake siku ya kiama kwa misumari ya moto na ataendelea kuyajaza moto macho hayo mpaka watu wote waishe kuhukumiwa ndipo naye aamuriwe kuingia motoni.[41] "

Hadithi nyingine nayo inasema kuwa: "Yeyote mwenye kuyajaza macho yake kwa kuanglia vitu vilivyoharamishwa, Mwenyezi Mungu atayajaza macho yake siku ya kiyama kwa misumari ya moto, isipokuwa kama atatubia.[42] "

Miongoni mwa athari za kuwaangalia wanawake wasiyokuhusu ni kujiadhibu wewe mwenyewe nafsi yako na kujisababishia mawazo mengi bila sababu ya msingi.

Imam Ali(a.s) anasema:

"Yeyote mwenye kuliachilia jicho lake (likawaangalia wanawake wasiomhusu) mtu huyo hujisababishia majonzi mengi ."[43]

Na kasema tena Imam Ali(a.s) :

"Mtu yeyote ambaye macho yake ni yenye kuangalia kwa kufuatilia (wanawake wasiomhusu au mambo ya haramu) mtu kama huyu majuto yake huwa ni ya kudumu ."[44] Mtu anayeishi maisha yanayoruhusu macho yake kuangalia kila anayemtaka na anachokitaka, hapana shaka kwamba mtu huyu huishi maisha yenye majonzi mengi na huiadhibu nafsi yake mwenyewe, na huwa mwenye mawazo yasiyo na kikomo. Yote haya yatampata kwa sababu moyo wake utakuwa umefungwa kwa huyo aliyemuona na akamtamani kisha asimpate. Akili yake ataishughulisha akifikiria namna ya kumpata, na huwenda akakosa raha na hata usingizi.

Hadithi hii iliyotaja hatari za kuangalia, na kisha kumsababishia taabu na majuto mwenye tabia hiyo, inahusisha mambo mengi ambayo haipaswi kuyaangalia, lakini moja wapo na muhimu ni hili la kuwaangalia wanawake wasiokuhusu, bali tunaweza kusema kuwa hilo ndilo makusudio. Na kwa ajili hiyo basi Imam Jaafar(a.s) akibainisha hatari za kumuangalia mwanamke asiyekuhusu anasema: "Kumtazama mwanamke asiyekuhusu ni mshale wenye sumu miongoni mwa mishale ya iblisi, na ni mara nyingi kumtazama mwanamke asiyekuhsu limekuwa ni jambo lenye kuleta majuto ya muda mrefu[45] ."

Ewe ndugu yangu bila shaka unafahamu jinsi mshale unavyoweza kuingia mwilini na kupasua mishipa iliyoko mwilini. Hebu fikiria namna mshale usiokuwa na sumu unavyoweza kuleta madhara pindi uingiapo mwilini, sasa je itakuwaje hali ya mshale wenye sumu ukiingia mwilini?

Bila shaka madhara yake ni makubwa zaidi ambayo yanaweza kupelekea mauaji kwa mtu. Hali ni kama hiyo kwa mtu mwenye tabia ya kuangalia wanawake wasiomhusu, kwani kuangalia huko ni sawa na mshale wenye sumu, mshale huo hujitengenezea njia mpaka ndani ya moyo ili kumnyima mtu huyo raha na utulivu na kumuachia majuto ya muda mrefu. Ewe ndugu yangu mpendwa! Ili uweze kujitakasa na kuwa mbali na mawindo ya shetani, napenda kukufahamisha pia kwamba Uislamu unachukizwa na tabia ya kuwaangalia wanawake. Mimi naamini kwama kuna baadhi ya watu wasiofuata mafundisho ya dini wanapokutana na wanawake, wakishakupishana nao basi huwaangalia nyuma hali ya kuwa wanatizama kwa mtazamo wa kutaka kufahamu namna wanawake hao walivyo au wanavyotembea, pia maumbo yao. Kwa hakika hii ni tabia mbaya mno haifai kabisa. Inasimuliwa kwamba Abu Basir alimuuliza Imam Jaafar(a.s) "Ni vipi mtu anapomwangalia mwanamke kwa nyuma? "Imam a.s. akajibu kwa kusema: "Hivi mmoja wenu anapenda mkewe au jamaa yake wa kike aangaliwe namna hiyo?" Abu Basir akajibu: "Hapana." Imam akasema: "Basi waridhie watu kwa kile unachokiridhia kwa ajili ya nafsi yako .[46] "

Kuna kisa kimoja kinamuhusu Mtume Musa(a.s) katika tafsiri ya neno la Mwenyezi Mungu akimnukuu Binti ya Mtume Shuaibu(a.s) aliposema:

قَالَتْ إِحْدَاهُمَا يَا أَبَتِ اسْتَأْجِرْهُ ۖ إِنَّ خَيْرَ مَنِ اسْتَأْجَرْتَ الْقَوِيُّ الْأَمِينُ

"Ewe Baba muajiri huyu, hakika mbora uwezaye kumuajiri ni mtu mwenye nguvu tena mwaminifu [47] .

Nabii Shuaibu alipoyasikia maneno ya Binti yake alimuuliza akasema: "Huyu Musa ni mwenye nguvu na hii ni kwa sababu umemuona akilinyanyua jiwe kwenye kisima, sasa je, huu uaminifu wake umeufahamu vipi?" Yule Binti akajibu kwa kusema: "Ewe Baba mimi nilikuwa natembea mbele yake, mara Musa akaniambia, tembea nyuma yangu na iwapo nitapotea njia basi wewe utanielekeza, kwani sisi ni watu tusiyowaangalia wanawake kwa nyuma[48] .

Katika tafsiri ya neno la Mwenyezi Mungu lisemalo kuwa: "Waambie Waumini wanaume wainamimshe macho yao." Imamu Muhammad Al Baqir(a.s) anasema: "Kijana mmoja wa Kiansari alikutana na mwanamke fulani katika vichochoro ya mji wa Madina, na huyu kijana akamkazia macho yule mwanamke. Walipopishana kijana huyu akageuza shingo yake na akaendelea kumuangalia yule mwanamke huku anakwenda hali ya kuwa kageuza shingo yake akimuangalia. Basi ghafla alijikuta amejigonga ukutani na damu zikaanza kumchuruzika. Kijana yule kuona hivyo akasema: Ni lazima niende kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu nikamueleze juu ya kisa hiki. Kijana yule alipofika mbele ya Mtume(s.a.w.w) hali damu zikiendelea kumtoka, Mtume alimuuliza umepatwa na nini? Yule kijana akasimulia yaliyomfika, na mara Malaika Jibril(a.s) alishuka akiwa na Aya inayowaamuru Waumini wanaume wainamishe macho yao.[49] "

Kipo kisa kingine kinasimuliwa kuhusu hali kama hizi na kinasema kuwa: "Kuna mtu mmoja ambaye kazi yake ilikuwa kuteka maji na kupeleka ndani ya nyumba ya Sonara fulani kwa muda wa miaka thelathini.

Bila shaka kuna wakati yule hakuwako nyumbani kwa mke wa sonara alikuwa akija kumfungulia mlango yule mchota maji ili apate kumimina maji mahala panapostahili. Kipindi chote hiki yule mchota maji hakuwahi kufanya hiyana yoyote dhidi ya mke wa sonara japo kumuangalia kwa jicho la hiyana.

Siku moja wakati yule mama anamfumngulia mlango yule mchota maji, mara ghafla aliunyoosha mkono wake na kumvuta yule mama na akambusu!! Kwa bahati nzuri mwanamke huyu aliuvuta mkono wake kwa nguvu kisha akapiga makelele na hapo hapo akamfukuza yule mchota maji kutoka mule ndani. Baadaye huyu mama alianza kufikiria huku akishangazwa na hali ile iliyojitokeza. Imekuwaje mchota maji yule kufanya hiyana ile baada ya kuwa muaminifu kwa muda wa miaka thelathini?!! Mumewe aliporudi nyumbani mkewe akamuuliza: 'Je leo kuna jambo gani limetokea huko dukani kwako?' Yule mume akajibu kwa kusema: 'Leo kuna mwanamke alikuja dukani kwangu kununua bangili, basi nilipomfunua mikono yake ili apate kuvaa bangili zile, nilimshika mkono wake kisha nikambusu.'! Basi pale pale mkewe alipiga makelele akasema: 'Allahu Akbaru!'[50] Baada ya hapo alimsimulia mumewe mambo yaliyotendwa na yule mchota maji."

Naam chochote atakachokifanya mtu kuwafanyia wenziwe na wake wa wenzake, basi na yeye yatamfika hivyo kwa mkewe, mama yake, dada yake na binti yake. Ndani ya hadithul Qudsi inasemwa kuwa: "Vile uwatendeavyo wenzako, basi na wewe utatendewa hivyo hivyo." Maana yake ni kwamba: Iwapo utawatendea wema wenzako basi na wewe utatendewa wema, na iwapo wewe utawatendea ubaya wenzako fahamu wazi kuwa na wewe utatendewa ubaya[51] .

Ewe msomaji mpendwa: Narudia tena kuzungumzia suala la kumuangalia mwanamke asiyekuhusu na ninasema: Hapana shaka kwamba Uislamu ni dini yenye mafunzo yanayokuhamasisha kutenda mema, na wakati huo huo inayo mafunzo ya kukuonya usiyaendee maovu. Ndiyo maana utaiona Qur'an Tukufu pindi Mwenyezi Mungu anapoitaja pepo na neema zake, hapo hapo hufuatisha kuelezea habari za moto na adhabu zake. Yote haya lengo lake ni kumfanya mtu awe katika mazingira ya kutumainia neema na thawabu, na pia awe na khofu ya moto na adhabu kwa upande wa pili. Hivi punde tu umesoma baadhi ya hadithi tukufu zilizosimulia kuhusu adhabu za kumuangalia mwanamke asiyekuhusu na pia matokeo mabaya yanayoletwa na tabia hiyo mbaya.

Hivi sasa umefika wakati wa kuzungumzia hadithi zinazoelezea malipo mema aliyoyaandaa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ajili ya wale watakaojiepusha na mambo ya haramu. Kadhalika hadithi hizo zitaelezea athari njema zinazopatikana kutokana na tabia njema za kujiepusha na mambo aliyoyakataza Mwenyezi Mungu.

Bwana Mtume(s.a.w.w) anasema: "Kuyatazama mapambo ya wanawake wasiokuhusu ni mshale miongoni mwa mishale ya ibilisi iliyo na sumu, atakayeliacha jambo hilo kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu (s.w.t) basi Mwenyezi Mungu atamuonjesha ladha ya ibada itakayomfurahisha [52] .

"Katika hadithi nyingine Mtume(s.a.w.w) anasema: "Kumtazama mwanamke asiyekuhusu ni mshale miongoni mwa mishale ya ibilisi iliyo na sumu, atakaye acha jambo hilo kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu (s.w.t) basi Mwenyezi Mungu atampa mtu huyo imani ambayo furaha ya imani hiyo ataihisi moyoni mwake .[53] "

Bwana Mtume anaendelea kutufunza anasema kwamba: "Yainamisheni macho yenu, kwa kufanya hivyo mtaona maajabu (makubwa)[54] .

Hapana shaka kwamba Mwenyezi Mungu humfunika mtu huyo kwa wingi wa baraka kutokana na kitendo chake cha kuinamisha macho na kutowaangalia wanawake wasiomhusu. Imam Ja'far Sadiq(a.s) anasema: "Mwenye kumuangalia mwanamke asiyemhusu kisha akanyanyua macho yake juu au akayafumba (ili tu asimuone mwanamke huyo), Mwenyezi Mungu humuozesha mtu huyo mwanamke wa peponi kabla hajarudisha macho yake chini.[55] " Anasema tena Imam Ja'far(a.s) : "Hawezi mtu yeyote kujihifadhi isipokuwa kwa kuyainamisha macho yake, kwani macho hayatainamishwa kutokana na mambo aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu, isipokuwa ndani ya moyo wa mtu huyo huwa kumetangulia kuuona utukufu wa Mwenyezi Mungu.[56] " Sasa hivi kumebakia kitu cha mwisho ambacho ni: Je! Ni namna gani basi mtu anaweza kuepukana na jambo hili la haramu, wakati sote tunafahamu kwamba, gonjwa hili la kansa ya wanawake kuvaa nusu Hijabu na kutokujisitiri kwa mujibu wa sheria limeenea? Na kwa bahati mbaya sana hata katika nchi zetu za Kiislamu gonjwa hili limo. Hivi kweli kwa hali tuliyonayo mtu anaweza tena kuinamisha macho yake na ni vipi ataiona njia?

Jawabu la suali hili ni kama ifuatavyo: Sina shaka umesoma baadhi ya Aya na hadithi tulizozitaja. Kinachotakiwa ni kuinamisha macho siyo kuyafumba, na hii ndiyo maana iliyokusudiwa, yaani uangalie chini.

Anachopaswa mtu kukifanya wakati anapomuona mwanamke asiyemhusu, haraka sana ateremshe macho yake chini au aangalie upande mwingine. Kwa hakika Mwenyezi Mungu hawezi kupoteza malipo yake.

1. Usimpe mkono mwanamke asiyekuhusu: Ndugu Mwislamu, Mwenyezi Mungu ameharamisha kumpa mkono mwanamke asiyekuhusu. Mtume Muhammad(s.a.w.w) amesema: "Yeyote atakayepeana mkono na mwanamke asiyemhusu mtu huyo hujiingiza katika ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, na anayedumisha uhusiano (wa kimapenzi) na mwanamke asiyekuwa mkewe, atafungwa kwa mnyororo wa moto pamoja na shetani kisha wasukumizwe motoni [57] .

2. Usimtanie mwanamke asiyekuwa mkeo: Miongoni mwa mambo ambayo Mwenyezi Mungu amekukataza na kukuharamishia ewe ndugu Mwislamu, ni kufanya utani na mwanamke asiyekuhusu kisheria, kwani jambo hili mara nyingi hukaribisha uovu na pia husaidia kwa kiasi kikubwa kuamsha hisia za maumbile zilizokuwa zimejificha katika pande mbili hizi. Bwana Mtume(s.a.w.w) anasema: "Yeyote anayemtani mwanamke asiye na milki naye (asiyekuwa mkewe) Mwenyezi Mungu atamfunga mtu huyo miaka alfu moja (huko akhera) kwa kila neno moja alilomsemesha mwanamke huyo ."

3. Usichelewe kuoa: Ndugu yangu Mwislamu, kuoa ni jambo la lazima kwa Mwislamu anapofikia umri wa kubalehe.

a. Ni lazima Mwislamu aoe ili ailinde dini yake, na ndiyo jambo la kwanza apasalo kufahamu.

b. Jambo la pili: Pindi atakapooa atapata radhi za Mwenye Mungu Mtukufu.

c. Na jambo la tatu: Atakuwa amehifadhi nafsi yake kutokana na mambo ya haramu. Kwa hakika Mwenyezi Mungu amemuumba mtu na akamuwekea matamanio ya kijinsiya, na akayafanya kuwa ndiyo matamanio yenye nguvu kuliko mengine yote. Kwa matamanio hayo Mwenyezi Mungu akafanya kuwa ndiyo njia ya kukidumisha kizazi cha wanaadamu, na akafanya kuoa ndiyo njia ya pekee kuyatosheleza matamanio haya. Kwa hiyo kuoa ndiyo njia nzuri na tukufu na ndiyo ufumbuzi wa pekee uliopo kisheria kuhusu tatizo hili la kijinsiya.

Ukweli ulivyo ni kwamba, kuchelewa kuoa kunamfanya mtu akumbwe na mambo mawili.

1. Kwanza: Katika kushindana na matamanio yake kutamfanya aiumize nafsi yake na kupata taabu kubwa ya kuvumilia katika muda huo.

2. Pili: Huenda hatimaye akaingia katika haramu ikiwa ni pamoja na njia isiyo ya kawaida katika kuyatosheleza matamanio yake, au akajikuta anafanya mambo machafu zaidi ambayo ni kinyume na maumbile. Au huenda akafanya uzinifu na matokeo yake ni kuvunja heshima yake au heshima za watu wengine. Na kutokana na hali halisi ilivyo, kila jambo moja katika hayo lina hatari kubwa kwa mtu yeye mwenyewe na heshima yake na utu wake. Kwani kuzuia matamanio na kuyadhibiti kunasababisha kuiadhibu roho na matokeo yake huleta athari mbaya mwilini na hasa katika akili.

Hali hii husababisha kuingia katika dhambi na hatimaye mtu ndipo hujikuta akifanya ambalo hakulitarajia, hapo utu wake huporomoka na mwisho hupata akahukumiwa kwa kosa la jinai na kuingia gerezani na kuishi humo sawa na wezi na wanyang'anyi.

BIBI FATIMA (A.S) KIIGIZO CHEMA KWA WANAWAKE

KIMEANDIKWA NA: MUHAMMAD IBRAHIM EL-QAZWINIY

Basi Nini Ufumbuzi Wa Tatizo Hili?

Ufumbuzi wa tatizo hili ni kuoa, kitu ambacho Uislamu unakitanguliza mbele na hata akili inakubaliana kabisa na ukweli huu, kwa kuwa kuoa ndiyo dawa pekee ya kutibu maumbile haya. Kuoa kunatimiza furaha ya kiroho kwa mtu na kuiliwaza nafsi na kuyapamba mazingira na tabia ya mtu. Kwa jumla ladha ya maisha na starehe vimo ndani ya ndoa, na kwa upande mwingine kuoa kunazuia mtu kuyaingia maovu na madhambi. Zaidi ya hapo ni kwamba, Mwenyezi Mungu hakumuumba mtu ili aishi maisha ya ujane na upweke, bali amemuumba aishi na mkewe aliye Muumini bega kwa bega ili wajenge familia na jamii bora hasa katika malezi ya watoto. Kwa hakika ujane ni miongoni mwa mambo yanayomchukiza Mwenyezi Mungu, pia Uislamu unapinga kwa nguvu zake zote jambo hili na hata Mawalii wa Mwenyezi Mungu wanachukizwa na ujane. Bwana Mtume(s.a.w.w) anasema: "Waovu miongoni mwenu ni wajane, (wasiyooa au kuolewe) nao ni ndugu wa shetani."[58] Na akasema tena: "Watu wengi wa motoni ni wale wajane (wasiyooa au kuolewa).[59] "

Imesimuliwa kutoka kwa al-Ukaaf al-Hilali anasema: "Nilikwenda kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) akaniambia 'ewe U'kaafu unaye mke?' Nikamwambia, Hapana sina mke. Mtume akaniambia: 'Je unaye mjakazi?' Nikasema: Hapana sina. Bwana Mtume akasema: 'Je wewe ni mzima na mwenye uwezo (yaani unao uwezo wa mali na unalimudu tendo la ndoa)?

'Nikamjibu: Ndiyo tena namshukuru Mwenyezi Mungu. Bwana, Mtume akasema: 'Ikiwa unayamudu hayo na hujaowa, basi kwa kweli wewe ni miongoni mwa ndugu wa mashetani, au basi utakuwa miongoni mwa mapadri wa Kikristo na kama si hivyo, fanya kama wanavyofanya Waislamu kwani miongoni mwa mila zetu ni kuowa.' Mtume aliendelea kunionya na kusisitiza suala la kuowa mpaka akafikia hatua ya kuniambia: 'Ole wako ewe U'kaafu, owa hakika wewe ni miongoni mwa waovu ( ikiwa hukuowa).' Nikamwambia Bwana Mtume: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu niozeshe kabla sijaondoka hapa." Bwana Mtume akamuozesha Bwana huyo kabla hajaondoka[60] .

Na katika kulitilia mkazo suala la kuoa na kuhimiza watu waowe, Bwana Mtume(s.a.w.w) anasema: "Hakuna jengo bora lililojengwa katika Uislamu na likawa linapendeza mbele ya Mwenyezi Mungu na likapata utukufu kuliko kuoana."

Na akasema tena: "Kijana yeyote anayeowa katika umri wake wa mwanzo katika ujana, shetani huchukia na kusema: Lo nimepata hasara theluthi mbili za dini yake kijana huyu amezikinga kutokana na uovu wangu." Kisha Mtume akamuusia kijana wa aina hii akasema: Na amuogope Mola wake kijana huyu katika theluthi iliyobaki.[61] "

Makusudio ya maelezo haya ni kuonesha kwamba kuoa kunahifadhi theluthi mbili ya dini, kwa hiyo mtu anatakiwa awe mchamungu katika theluthi iliyobakia. Na kama hali ni hii, umuhimu wa kuoa katika maisha ya mtu ni jambo ambalo linayo nafasi ya pekee na tukufu, na pia mwanaadamu anatakiwa alipatie nafasi kubwa ya kulitekeleza katika mipango yake.

Tukamilishe mazungumzo juu ya kuowa kwa hadithi ya Mtume(s.a.w.w) inayosema kuwa: "Rakaa mbili anazoswali mtu aliyeowa, ni bora zaidi kuliko rakaa sabini anazoswali mtu asiyeowa[62] ."

Makazi Ya Mwanamke Asiyejisitiri.

Ni yapi makazi ya mwanamke asiyevaa Hijabu wala hajisitiri Kiislamu huko akhera?

Sote tunafahamu kwamba, Mwenyezi Mungu ameweka adhabu kali kwa wale wanaokiuka maamrisho yake na wanaamua kuyaingia mambo ya haramu. Je ni adhabu gani atakayoadhibiwa mwanamke asiyejisitiri kwa vazi la Kiislamu na akaona ni bora kuutembeza mwili wake wazi kinyume na sheria inavyomtaka avae? Jawabu lake ni kama ifuatavyo: Kwa mwanamke asiyejsitiri hujisababishia laana na kujiweka mbali na rehma na radhi za Muumba wake. Pia hujiingiza mwenyewe katika unyonge na adhabu za Mwenyezi Mungu. Bwana Mtume(s.a.w.w) anasema: "Katika zama za mwisho watakuja watu katika umati wangu ambao wanawake zao nusu wamevaa na nusu wako uchi. vichwani watasuka mafundo ya nywele na kuyaacha wazi bila kuyafunika.

Basi sikilizeni (niwaambieni) kuweni wenye kuwalaani wanawake hao kwa kuwa wamekwisha kulaaniwa, wala hawataipata harufu ya pepo na iko mbali nao kwa masafa ya mwendo wa miaka mitano[63] ."

Naye Imam Ali(a.s) amesema: "Katika zama za mwisho kitapokuwa kiama kimekaribia, watatokea wanawake watakaokuwa wakitembea uchi bila kujisitiri kisheria.

Wanawake wa aina hii watakuwa wametoka katika dini na wataingia katika fitna, watapenda starehe na mambo ya fahari na watahalalisha mambo ya haramu. Wanawake hawa malipo yao ni kuingia motoni, basi angalieni sana kipindi hicho ni kibaya kuliko vyote."

Kuna hadithi nyingine kutoka kwa Bwana Mtume(s.a.w.w) inayoelezea adhabu za wanawake wasiojisitiri kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu. Hadithi hii tunainakili kwa kifupi. Imam Ali(a.s) anasema: "Mimi na Fatma(a.s) tuliingia nyumbani kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu tukamkuta analia sana. Nikamwambia ni kitu gani kinakuliza? Mtume akasema: 'Ewe Ali, usiku niliopelekwa mbinguni niliwaona wanawake katika umati wangu wakiadhibiwa vikali. Nilihuzunishwa na hali yao hiyo na nikalia kutokana na adhabu kali wanayoadhibiwa.' Kisha Bwana Mtume(s.a.w.w) akaanza kueleza aliyoyaona katika usiku huo wa Miraji akasema

'Nilimuona mwanamke amefungwa kwa nywele zake kwenye moto na ubongo wake unatokota. Na nikamuona mwanamke mwingine amening'inizwa kwa ulimi wake huku moto ukimiminwa kooni mwake. Pia nikamuona mwanamke anakula nyama ya mwili wake hali yakuwa chini yake panawaka moto mkali, na mwingine amefungwa mikono yake na miguu kwa pamoja, kisha amezungukwa na mojoka mengi na nge wanamuuma. Pia nilimuona mwanamke kiziwi tena kipofu halafu hawezi kusema akiwa ndani ya moto ubongo wake unavuja kupitia puani, mwili umeenea vidonda mithili ya mgonjwa wa ukoma. Na kuna mwanamke mwingine anakatwa nyama za mwili wake kwa mikasi.

Bibi Fatma(a.s) akasema kumwambia baba yake: 'Baba hebu nifahamishe ni matendo gani waliyoyatenda wanawake hao hapa duniyani?' Mtume(s.a.w.w) akajibu: 'Ewe Binti yangu, ama yule aliyekuwa amefungwa kwa nywele zake, yeye alikuwa hafuniki kichwa chake mbele ya wanaume wasiomhusu. Na yule aliyening'inizwa kwa ulimi wake alikuwa akimkera na kumuudhi mumewe. Ama aliyekuwa akila nyama ya mwili wake, huyo alikuwa akiupamba mwili wake kwa ajili ya watu wamuone. Na yule mwanamke aliyefungwa mikono na miguu kwa pamoja na akawa anaumwa na majoka na nge, huyu alikuwa mchafu hana udhu nguo zake chafu na alikuwa hakogi janaba wala hedhi na alikuwa akipuuza kuswali. Ama yule kipofu, kiziwi na hawezi kusema alikuwa akizaa watoto wa zinaa (nje ya ndoa) na kisha humpachikia mumewe na kudai kwamba ni watoto wa mumewe. Na huyu wa mwisho ambaye alikuwa akikatwa nyama za mwili wake kwa mikasi, alikuwa Malaya, akiitoa nafsi yake kwa kila mwanaume.[64] ” Kwa hiyo imetudhihirikia wazi katika hadithi hii aina mbali mbali za mateso na adhabu alizoziandaa Mwenyezi Mungu kwa wanawake wasiozingatia kanuni ya Hijabu kwa maana zake zote.

Miongoni mwa adhabu hizo ni kufungwa kwa nywele zake nwanamke na kutokota ubongo baada ya kupata adhabu ya moto unaowaka pande zake zote. Kwa hivyo basi, ina maana kila mwanamke atakayeshindwa kusitiri mwili wake na akauacha wazi kwa kila mtu, hapana budi ataadhibiwa kwa adhabu kali inayoumiza, kama zilizotajwa ndani ya hadithi.

Lakini ikiwa mwanamke mwenye sifa hizi zilizotajwa katika hadithi atatubia kwa Mwenyezi Mungu na kuacha kabisa makosa hayo aliyokuwa akiyatenda, kisha akavaa kama sheria ya Kiislamu inavyomtaka avae kwa ukamilifu, bila shaka Mwenyezi Mungu atakubali toba yake na atamsamehe. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anasema:

وَهُوَ الَّذِي يَقْبَلُ التَّوْبَةَ عَنْ عِبَادِهِ وَيَعْفُو عَنِ السَّيِّئَاتِ وَيَعْلَمُ مَا تَفْعَلُونَ.

"Ni yeye Mwenyezi Mungu ambaye anakubali toba za waja wake (wanapotubia) na anasamehe makosa na anafahamu mnayoyatenda [65] ".

وَإِنِّي لَغَفَّارٌ لِمَنْ تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا ثُمَّ اهْتَدَىٰ.

Na anasema tena Mwenyezi Mungu (s.w.t.): "Nami kwa hakika ni mwingi wa kusamehe kwa yule anayetubia na akaamini na kutenda mema kisha akaoongoka [66] ’.

Hijabu Isiyokamilika: Kuna baadhi ya dada zetu ambao utwaona wamavaa Hijabu, lakini Hijabu yao hiyo siyo kamilifu kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu. Kina dada hao utawaona wamejistiri sehemu fulani tu ya kichwa, na au sehemu fulani ya mwili na halafu sehemu nyingine za mwili ziko wazi mbele ya kila mtu. Wakati mwingine wanaweza kujisitiri vizuri kichwa chote, lakini utaona mikono au miundi iko wazi au ikawa haikusitiriwa ipasavyo.

Kwa hakika Hijabu kama hi moja kwa moja ni Hijabu isiyokamilika ni Hijabu pungufu isiyoweza kutimiza lengo la Hijabu linalokusudiwa. Wakati huo huo, uvaaji kama huo si uvaaji ulioko juu ya msingi wa kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu.

Hali kama hii ya uvaaji usiokamili iliwahi kutokea katika zama za Bwana Mtume(s.a.w.w) , ambapo walikuwako wanawake ambao hujistiri sehemu ya kichwa na kuacha sehemu nyingine bila kuisitiri ikiwa ni pamoja na masikio. Tendo kama hili Mtume(s.a.w.w) alilikemea na akawaamuru wanawake wajisitiri kikamilifu kwa mujibu wa sheria. Kumbuka ndugu msomaji ile hadithi ya Mtume aliposema: "Nusu wamevaa na nusu wako uchi." Hadithi hii inamaanisha kwamba, wanawake watakuwa wanajisitri sehemu ya maungo yao na sehemu nyingine hawajisitiri. Kama hali ndiyo hii tuliyonayo, lengo la Mtume(s.a.w.w) ni kuwafahamisha wanawake wanaovaa hivyo kwamba wasidhani kuwa wamevaa Hijabu, bali inawapasa watambue kwamba uvaaji huo siyo kamili na haukubaliki kisheria.

Neno La Mwisho

Wasomaji wapendwa imetudhihirikia katika yale tuliyoyataja ndani ya kitabu hiki kwamba, Hijabu ni vazi la Kiislamu na siyo fashion[67] , na ni kanuni iliyojaa hekima nyingi. Hijabu inalinda heshima ya mwanamke na inaitakasa familia na jamii nzima.

Zaidi ya hapo ni amri ya kidini na hukumu ya sheria za Kiislamu, Mwenyezi Mungu ameithibitisha na kuitaja ndani ya Qur'an Tukufu. Naye Bwana Mtume(s.a.w.w) na watu wa nyumba yake wamesisitiza na kuitilia mkazo sheria hii. Kinyume cha maagizo haya na faida zilizomo ndani ya Hijabu, tayari tumekwishakuona wazi kwamba jamii huwa inaharibika na mwanamke kuangamia na ndipo familia inapotengana.

Zaidi ya hapo kutokuchunga mipaka ya mavazi, hasa Hijabu kwa wanawake ni uasi wa amri ya Mwenyezi Mungu, na maamuzi yake pia ni kinyume na maslahi ya wengi. Kwa hiyo ni wajibu wetu sote kufanya kila linalowezekana ili kuona sheria hii inafanya kazi na kuieneza baina ya wanawake waliomo katika jamii zetu, majumbani, mashuleni, maofisini na kila mahali. Kwa kufanya hivyo, tutapata radhi za Mwenyezi Mungu, pia huu utakuwa ni wema kwa ajili ya nafsi zetu hapa duniani na kesho akhera.

Habari Motomoto

1. AlAzhar Yasema: Wanawake Wa Kiislamu Walioko Ufaransa Wanaweza Kuvua Hijab Kama Wakilazimishwa

Cairo, Desemba 30, 2003 (IslamOnline, net):

Imamu Mkuu wa Al-Azhar Sheikh Mohammad Sayed Tantawi siku ya jumanne, Desemba 30, 2003 alisema kwamba: Wanawake wa kiislamu wanaoishi Ufaransa wanaweza kuvua Hijab zao kama wakilazimishwa kwa shida, alikuwa akirejea kusudio la sheria ya kupiga marufuku Hijab katika shule za serikali.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari na waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy (aliyekuwa anaizuru Misir), Tantawi alisisitiza kwamba Hijab "ni sharti la kiMungu kwa mwanamke wa kiislamu… Hakuna Mwislamu yeyote, awe yeye ni mtawala au mtawaliwa, awezaye kulipinga hilo."

Lakini alihoji kwamba Ufaransa wana haki ya kupiga marufuku Hijab katika shule za serikali, akaongeza kwamba chombo chochote cha kiislamu au nchi ya kiislamu haina haki ya kulipinga hilo, kwa sababu Ufaransa sio nchi ya kiislamu.

"Hijab ni wajibu kama mwanamke anayeishi katika nchi ya kiIslamu. Kama anaishi katika nchi isiyo ya kiislamu, kama Ufaransa, ambayo watawala wake wanataka kufuata sheria inayopinga Hijab, ni haki yao," alisema Imamu mkuu huyu wa AlAzhar, mwachuoni aliyeteuliwa na serikali.

Alisema kwamba iwapo mwanamke wa kiislamu atafuata sheria za nchi isiyo ya kiislamu (kwa kuvua Hijab yake), basi Uislamu humchukulia kama aliyelazimishwa kwa shida.

Sheikh Tantawi alitetea maoni yake hayo kwa kusoma Aya Tukufu, ambayo inasema:

"Mmeharamishwa (kula) nyama mfu na damu na nyama ya nguruwe, na kilichosomewa jina lisilo la Mwenyezi Mungu…Lakini mwenye kusongeka kwa njaa, pasipo kuelekea kwenye dhambi, wala kupituka mipaka basi Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kusamehe mwenye kurehemu."

"Nasisitiza na kukazia: Ni haki yao na siwezi kuipinga… sisi, kama nchi ya kiislamu, hatuwezi kumruhusu mtu yeyote kuingilia katika mambo yetu ya ndani," alisema akisherehesha juu ya upigaji marufuku wa Ufaransa ulio na majadala.

"Mimi mwenyewe, katika wadhifa wangu kama Imamu Mkuu wa Al-Azhar, siwaruhusu watu wasio Waislamu kuingilia katika mambo yetu ya ndani, na kwa mantiki hiyo hiyo, siwezi nikaruhusu nafsi yangu kuingilia katika mambo ya ndani ya nchi isiyo ya kiislamu," aliongeza Sheikh Tantawi.

Rais wa Ufaransa Jacques Chirac siku ya jumatano, 17 Desemba, 2003 aliunga mkono kusudio juu ya utungaji mpya wa sheria ya kupiga marufuku uvaaji wa Hijab katika shule za serikali.

Waziri wa sheria wa zamani wa Ufaransa, Bernard Stasi, ambaye aliongoza kamati ya serikali juu ya mazingira ya kilimwengu na dini, alipendekeza mapema katika mwezi huo kuwekwa sheria ya kupiga marufuku Hijab, misalaba mikubwa na vikofia vya kiYahudi.

Hatua hiyo iliyopendekezwa, imepangwa kuwakilishwa mbele ya Bunge la Ufaransa mwezi Februari 2004, na inatarajiwa kuanza kutumika katika mwezi wa Septemba 2004.

{Kwa mujibu wa fatwa za wanachuoni wengi pamoja na Mkuu wa Mamlaka kubwa ya ulimwengu wa Waislamu-Mashi'a, Ayatollah Mkuu Sayyid Seestani (HA): hairuhusiwi kwa msichana wa kiIslamu kuvua Hijab yake Shuleni, na kama akilazimishwa kuvua, basi asihudhurie Shuleni hapo[68] .

ORODHA YA WAPOKEZI WA UONGO WA SABA’100

MZUSHI WAKE NI SEIF BIN ‘AMRU AT-TAMIMIY ALIYEFARIKI MWAKA WA 170 HIJRIYYAH. WAPOKEZI WAKE:-

JINA MWAKA ALIOFIA

Tabari 310 Hijriyyah

Ibn-Asaakir 571 Hijriyyah

Adh-Dhahabi 748 Hijriyyah

Ibnul-Athir 630 Hijriyyah

Abul-Fidai 733 Hijriyyah

Abi Bakar 741 Hijriyyah

Fan Fulton Nikison

Ibn-Kathir 774 Hijriyyah

Ibn-Khaldun 808 Hijriyyah

Ghiyathu-d-din 940 Hijriyyah

Mir Akhawandi 903 Hijriyyah

Ibn Badaran 1346 Hijriyyah

Rashid Ridhaa 1356 Hijriyyah

Sa’ad Afghani

Farid Wajidi

Ahmad Amini

Saba: Vita Vya Siffin Na Uasi Wa Mu’awiyah Bin Abi Sufian.

Baada ya kutimia nusura kwa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) katika vita vya Jamal, Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) na jeshi lake aliondoka kwenda kuondoa upinzani ambao aliuongoza Mu’awiyah bin Abi Sufian huko Sham, na majeshi mawili yalikutana katika mto Furat. Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) alijaribu kusuluhisha jambo hili kwa njia ya mazungumzo, isipokuwa majibu ya Mu’awiyah bin Abi Sufian kwa ujumbe ambao Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) aliutuma kwake yalikuwa: “Ondokeni kwangu mimi sina njia nyingine isipokuwa vita tu[101] .

Hivi ndivyo yalivyokutana majeshi mawili. Na zilipo dhihiri ishara za ushindi kwa jeshi la Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) na kundi ovu likakaribia kushindwa, waliandaa hila (`hadaa ya misahafu`), kwani walinyanyua misahafu juu ya ncha za mikuki na panga. Hila hiyo ya udanganyifu ikabadilisha msimamo wa jumla kwa wengi, pamoja na kwamba Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) alijitahidi kufichua hadaa ya kunyanyua misahafu kwamba huo ni udanganyifu wa kupoteza ushindi ambao umekaribia kwa jeshi la Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) , isipokuwa wale waliotaka vita visimamishwe hawakukubali wito wake wa mara kwa mara, na wakamlazimisha kukubali suluhu pamoja na kuwa Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) alipinga sana, na pia akapinga kuchaguliwa Abu Musa Al-Ash’ari kuwa mjumbe anayewakilisha jeshi lake katika suluhu, kwa sababu ya udhaifu wake na wepesi wa rai yake pale alipowaambia: “Sikubali mumchague Abu Musa kuwa hakimu kwa sababu yeye ni dhaifu kwa ‘Amr na hila zake[102] .

Na hasa baada ya kumwondoa ugavana wa Kufah, ni katika yanayomfanya aone kuwa uaminifu wake kwake ni dhaifu, pamoja na hayo kundi katika jeshi la Imam lilimng’ang’ania Abu Musa tu.

Na kuonyesha kuwepo hila na njama ni utangulizi wa lengo la kunyanyua misahafu, na kutumia utukufu wa Qur’an kwa waumini dhaifu sambamba na hilo, ni pamoja na kuwepo kundi lililomuunga mkono Mu’awiyah bin Abi Sufian lilijipenyeza katika jeshi la Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) na wakaeneza nguvu zao katika safu ya jeshi la Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) , mpaka wakamlazimisha suluhu na uteuzi wa mjumbe wake, katika suluhu baadaye ambapo ilifanya matokeo yawe kama alivyo sema Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) kwa maslahi ya Mu’awiyah bin Abi Sufian ambapo mambo yalianza kumnyookea kidogo kidogo, baada ya kufanya uasi wake mkubwa ambapo alitoka katika utii wa Amirul-Muuminina na Khalifa wa Waislamu ambaye ni wajib kumtii, kwa uasi wake na tamaa ya utajiri wa kidunia ambao ni ndoto yake ya muda mrefu.

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) alitoa habari za uovu wa Mu’awiyah bin Abi Sufian, alimwambia ‘Ammar: “Litakuuwa kundi ovu” na yalitokea aliyoyasema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) alipokufa shahidi ‘Ammar akiwa anapigana chini ya uongozi wa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) huko Siffin. Amesema: “Tulikuwa tunasomba matofali na ‘Ammar alikuwa anasomba matofali mawili mawili, Mtume(s.a.w.w ) akapitia karibu yake na akagusa vumbi kichwani kwake na akasema: “Namhurumia ‘Ammar litamuuwa kundi ovu, ‘Ammar anawalingania kwa Allah (s.w.t) na wao wanamwita kwenda kwenye moto[103] .

Na katika Mustadrak Sahihain kwa sanad ya Khalid Al-’Arabi amesema: “Niliingia mimi na Abu Said Al-Khudhri kwa Hudhaifah tukasema: “Ewe Abu ‘Abdillah! Tusimulie uliyoyasikia kutoka kwa Mtume wa Allah(s.a.w.w ) miongoni mwa fitina”.

Hudhaifah akasema: “Mtume wa Allah(s.a.w.w ) amesema: “Zungukeni pamoja na Kitabu cha Allah (s.w.t).” Tukasema watu wakihitalifiana tutakuwa pamoja na nani? Akasema angalieni kundi ambalo lina mtoto wa Sumayyah, liandameni kwani yeye anazunguka pamoja na Kitabu cha Allah (s.w.t), nimemsikia Mtume wa Allah(s.a.w.w ) anamwambia ‘Ammar: ‘Ewe Abul-Yaqidhan! Hutokufa mpaka likuue kundi lililo potoka njia[104] .

Na uovu wa Mu’awiyah bin Abi Sufian ulikuwa ni jambo lenye kutarajiwa kutokea, kwa sababu ya kuchukua ugavana wa Sham tangu wakati wa ‘Umar na akapata mali, jaha na majumba ya fahari aliyo yajenga.

Na akajijenga wakati wa ‘Uthman, haikuwa rahisi kuyaacha na alikuwa na yakini kuwa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) kama hatomuuzulu basi atamnyang’anya yote aliyo yamiliki kutoka katika hazina ya Waislamu, na atamfanya awe sawa na watu wengine miongoni mwa Waislamu.

Na kisa chake pamoja na Abudhar wakati wa ‘Uthman kinaonyesha tunayoyasema kupenda kwake dunia na ufujaji wake katika mali za dola kwa ujumla, na upinzani wa Abudhar kwa Mu’awiyah bin Abi Sufian ulisababisha aamuru kufukuzwa Abudhar kwenda Rabadhah baada ya kuwa alimwita arejee Madina.

“Kutoka kwa Wahhab amesema: “Nilimkuta Abudhar Rabadhah nikamwambia:”Ni kipi kilichokuleta katika ardhi hii?” Akasema: “Tulikuwa Sham, basi nikasoma Ayah: ‘Na wale ambao wanalimbikiza dhahabu na fedha na wala hawazitoi katika njia ya Allah (s.w.t), basi wabashirie adhabu iumizayo.’ Mu’awiyah bin Abi Sufian akasema hii haikuteremka kwetu, hii haikuteremka isipokuwa kwa Ahlul-Kitab, akasema; na nikasema: Hakika imeshuka kwetu na kwao[105] .

Na Abudhar aliadhibiwa kwa kufukuzwa pamoja na kwamba kuna ushahidi wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) juu ya ukweli wake aliposema: “Haikumfunika mbingu wala hakutembea ardhini (mtu) mkweli wa kauli kuliko Abudhar [106] .”

Na tabia ya Mu’awiyah bin Abi Sufian katika ugavana na utawala inadhihirika wazi katika kauli ya baba yake Abu Sufian kwa ‘Uthman baada ya kupewa Bai’a: “Enyi Bani Umayyah udakeni kama mnavyodaka mpira, (naapa) kwa ambaye Abu Sufian anaapa kwake sikuacha kuwa nalitamani liwe kwenu na mlirithishe kwa watoto wenu[107] .” Na katika mapokezi mengine kuna ziada: “Huko Akherah hakuna Jannat (pepo) wala Jahannam (moto)[108] .” Na hii inathibitisha ni aina gani ya Uislamu ulioingia katika nyoyo zao hali wao wanauchukia.

“Abu Sufian amesema: “Wallahi sikuacha kuwa dhalili hali ya kuwa na yakini kuwa jambo lake litadhihiri, hadi Allah (s.w.t.) akauingiza moyo wangu katika Uislamu na mimi ni mwenye kuchukia[109] .”

Na miongoni mwa kauli za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) kwa Mu’awiyah bin Abi Sufian ni ambayo ameipokea Muslim katika Sahih yake. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) siku moja alimtuma ‘Abbas kwenda kwa Mu’awiyah bin Abi Sufian ili aje amwandikie Ibn ‘Abbas akamkuta anakula, Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) alimrejesha tena kwenda kumwita akamkuta anakula hadi mara ya tatu, Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) akasema Allah (s.w.t) asilishibishe tumbo lake”[110] . Pia katika Sahih Muslim, amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) ; “Amma Mu’awiyah bin Abi Sufian ni fakiri hana mali yoyote[111] .

Na katika Musnad Ahmad, amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) kwa Mu’awiyah bin Abi Sufian na ‘Amr bin ‘Aas: “Ewe Allah (s.w.t) watie katika fitina kuwatia na waingize motoni kuwaingiza[112] .”

Na zipo Hadith nyingi zisizokuwa hizo miongoni mwa Hadith zinazo bainisha ukweli wa Mu’awiyah bin Abi Sufian huyu ambaye amehitimisha vitendo vyake katika dunia hii kwa kumtawalisha mwanae Yazid mlevi, fasiki kuwa khalifa wa Waislaam baada yake.

Nane-Kufa Shahid Kwa Al-Imam ‘Ali Ibn Abi Talib(A.S )

Vita vya mwisho alivyopigana Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) ni vita vya Nahrawan ambapo alipigana dhidi ya kundi lililo lazimisha suluhu Siffin, lakini likajuta baada ya siku chache, hivyo likatengua ahadi yao na wakatoka katika Bai’a ya Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) na ambalo baadaye likajulikana kwa jina la Khawarji au Al-Maariqina (waasi). Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) aliwashinda na akawa anajiandaa kurudia mapambano na wapinzani wa Sham baada ya suluhu kushindwa walipokutana wajumbe wawili, lakini Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) akawa ameuliwa shahidi na

‘Abdurahman bin Muljim naye ni mmoja wa Makhawariji ambaye alimpiga Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) kwa dharuba ya upanga huku akiwa katika sala ya Al-fajiri katika msikiti wa Kufah asubuhi ya kuamkia siku ya kumi na tisa katika Mwezi mtukufu wa Ramadhan Mwaka wa 40 Hijriyyah baada ya kuongoza kwa muda wa miaka mitano.

Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) alibakia siku tatu akiumwa kutokana na pigo, ambapo alimwita mtoto wake Al Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) mjukuu wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) kuja kushika majukumu yake ya Uimamu katika kuongoza ‘Ummah baada yake.

Al Imam Hasan Ibn ‘Ali Ibn Abi Talib(a.s) Na Suluhu Ya Mu’awiyah Bin Abi Sufian

Baada ya Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) kufa shahid, Al Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) alipanda Mimbar na watu wa Kufah walinyanyuka na kumbay’i Khalifa wa Nabii na Imam wa Ummah. Lakini hilo halikudumu isipokuwa kwa muda wa miezi sita ambapo habari za Kufah Shahid Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) zilifika Sham, na Mu’awiyah bin Abi Sufian aliondoka na jeshi kubwa kuelekea Kufah kwenda kuchukua hatamu za uongozi wa Waislamu na kumlazimisha Al Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) kufanya suluhu. Imam Hassan hakuwa na njia nyingine isipokuwa kukubali. Na hapa baadhi ya watu wanatia shaka juu ya suluhu ya Al-Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) , wakati ambapo ndugu yake Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) alichagua njia ya vita na kupigana.

Hakika Al-Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) hakufanya mkataba wa suluhu pamoja na Mu’awiyah bin Abi Sufian bali amelazimishwa. Kulikuwa na mgawanyiko katika jeshi lake na hali ya Iraq kwa ndani haikuwa ni muafaka kwa vita, na ufalme wa Roma ulikuwa unangojea fursa ya kuupiga Uislam, na ulikuwa umejiandaa kwa jeshi kubwa tayari kuwapiga vita Waislamu.

Na kama vingetokea vita baina ya Mu’awiyah bin Abi Sufian na Al-Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) , basi ushindi ungekuwa ni wa ufalme wa Roma na sio kwa Al Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) wala kwa Mu’awiyah bin Abi Sufian.

Na hivyo kukubali kwa Al Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) kumeondoa hatari kubwa iliyokuwa ikitishia Uislamu. Kwa ujumla hali iliyo kuwepo wakati wa Al-Imam Hassan ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) , sio hali iliyo kuwepo wakati wa Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) , ambaye baadaye alichagua njia ya Thawrah na vita ambavyo ndugu yake Al-Imam Hassan ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) alivitayarisha kwa udadisi wake kwa kudhihirisha ukweli wa wafalme wa Bani Umayyah katika wakati wake.

Ama misingi ya makubaliano ya suluhu ilikuwa kama ifuatavyo:-

1. Al-Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) asalimishe utawala na hatamu za uongozi kwa Mu’awiyah bin Abi Sufian kwa sharti, Mu’awiyah bin Abi Sufian ahukumu kulingana na misingi ya Qur’an na Sunnah za Mtume wa Allah(s.a.w.w ) .

2. Baada ya kufa Mu’awiyah bin Abi Sufian Ukhalifa utakuwa ni haki ya Al-Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) na kama akifariki basi Ukhalifa utakuwa kwa Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) .

3. Shutuma zote na uovu dhidi ya Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) uzuiwe, iwe ni kwenye Mimbar au popote (Mu’awiyah bin Abi Sufian alikuwa ana amuru makhatibu katika wilaya zote kumtukana Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) , Hassan na Ibn ‘Abbas, katika kila hutuba ya Ijumaa na Iddi, na Mu’awiyah bin Abi Sufian hakutekeleza ahadi yake hii wala nyinginezo ambazo zilikubaliwa).

4. Kutoa kiasi cha dirham milioni tano zilizopo katika hazina ya Kufah ziwe chini ya usimamizi wa Al-Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) na ni wajibu kwa Mu’awiyah bin Abi Sufian kutuma kwa kila mwaka dirham milioni moja za pato kwa Al-Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) ili azigawe kwa familia za wale ambao walikufa shahid katika vita mbili, Jamal na Siffin, katika upande wa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) .

4. Mu’awiyah bin Abi Sufian anaahidi kuwaacha watu wote wa aina yeyote kutokana na kusumbuliwa na anaahidi vile vile kuwa atatekeleza misingi ya suluhu hii kwa umakini na anaifanya dini iwe ni shahidi juu yake.

Tisa: Kufa Shahid Kwa Al-Imam Hasan Ibn ‘Ali Ibn Abi Talib(a.s)

Mu’awiyah bin Abi Sufian alimshawishi (Ju’udatu binti Al-Ash’ath bin Qais) mke wa Al-Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) ambaye alikuwa ni wa ukoo wa familia zinazo wapinga Ahlul-Bayt(a.s ) , kwa kumtumia dirham laki moja akamwahidi kuwa atamwozesha kwa mtoto wake Yazid kama atampa sumu Al-Imam Hasan bin Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) . Mke mwovu alidanganyika na ahadi za uongo za Mu’awiyah bin Abi Sufian na akampa Imam sumu, na hiyo ilikuwa Mwaka wa 50 Hijriyyah. Mu’awiyah bin Abi Sufian alifurahi sana alipojua kufa shahid kwa Al-Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) kwa kuwa alikuwa anaona kuwa ni kipingamizi kikubwa katika matakwa yake na hasa katika kuimarisha utawala katika familia ya Mu’awiyah bin Abi Sufian kimekwisha kuondoka.

Kumi: Thawrah (Mapambano) Ya Karbala Na Kufa Shahid Kwa Al Imam Hussein Ibn ‘Ali Ibn Abi Talib(a.s)

Al-Imam Hussein bin ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) ni Imam wa tatu wa Ahlul- Bayt(a.s ) , na tukio muhimu katika historia lilikuwa ni kujitoa muhanga na kufa kwake shahid pamoja na watoto wake Ahlul-Bayt(a.s ) na wafuasi wake pale Karbala. Katika tukio lililotingisha akili na fikira na kuandikwa katika kurasa za historia na litaendelea kuthibiti na kubaki daima.

Hakika sababu zilizowazi za Thawrah ya Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) , ni upotovu ambao ulidhihiri wakati huo katika watawala wa Bani Umayyah na ukandamizaji wao kwa watu.

Mu’awiyah bin Abi Sufian kwa muda wa miaka ishirini alikuwa anaimarisha kumtawalisha mwanae mwovu Yazid na kumpa nguvu ili kumfanya kuwa Amirul-Muuminina na Khalifa wa Mtume wa Allah(s.a.w.w ) kwa Waislamu, na kwa hivyo akakhalifu ahadi zake kwa Al- Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) na kutengua ahadi zote alizomwahidi Allah (s.w.t).

Yazid kwa mtazamo wa makundi yote ya Kiislam, alikuwa anakunywa pombe wazi wazi na anakunywa hata makapi na kukesha, na kuimba mashairi ya kipuuzi tunataja baadhi yake:- “Muziki wa didan umenishughulisha kutosikia adhana, na mwanamke kikongwe asiyejiweza amekuwa ni badala ya hurulain”.

Hakuna ajabu katika hili kwani Yazid bin Mu’awiyah bin Abi Sufian amelelewa na yaya wa Kikristo, na alikuwa ni kijana mjinga mwovu, tegemezi, mfujaji, hana haya, asiyeona mbali na asiye na maarifa kama walivyosema wanahistoria.

Baada ya kufariki Al-Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) katika Mwaka wa 50 Hijriyyah, Mashi’a wa Iraq walijaribu kujikomboa na walimwandikia Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) wakitaka amuuzulu Mu’awiyah bin Abi Sufian katika uongozi wa Waislamu. Lakini Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) akawaambia katika jibu lake kuwa ana ahadi na makubaliano na Mu’awiyah bin Abi Sufian hawezi kuyavunja.

Baada ya kufa Mu’awiyah bin Abi Sufian Mwaka wa 60 Hijriyyah, Yazid alichukua utawala, basi utawala wake ukawa ni mwanzo wa upuuzi na madhambi. Katika hali hii Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) aliona sio kwamba wakati ni mwafaka tu, bali ni wajibu kufanya harakati na Thawrah kwa ajili ya kuunusuru Uislamu na misingi ya dini, na sio kwa ajili ya kuchukua Ukhalifa na utawala ambao ndiyo ulikuwa matamanio ya Bani Umayyah, ambapo walipania mno katika kuupata na hasa baada ya watu wa Iraq kukataa kumnusuru Al Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) na hofu yao kwa Bani Umayyah.

Na anabainisha wazi Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) katika moja ya hotuba zake alipokuwa karibu na Karbala kuhusu sababu ya Thawrah yake, kwa kusema:

“Enyi watu atakayemwona kiongozi mwovu anahalalisha aliyoharamisha Allah (s.w.t) baada ya kumwahidi, anakhalifu Sunnah za Nabii wake, na anahukumu baina ya waja wa Allah (s.w.t) kwa ufisadi na ujeuri; na asimpinge kwa ulimi wake na vitendo vyake; basi ni haki kwa Allah (s.w.t) kumtupa Jahannam.” Vile vile amesema: “Enyi watu, na hakika wao wamemtii Shetani na wamemwasi Allah (s.w.t) na wamefanya ufisadi katika ardhi, wamevunja Sunnah na wamefuja hazina ya mali ya Waislamu, na wamehalalisha aliyoyaharamisha Allah (s.w.t), na wakaharamisha aliyoyahalalisha Allah (s.w.t), na mimi nina haki zaidi kumpinga kuliko watu wengine.” Akakusanya wafuasi wake na Ahlul Bayt wake waliokuwa pamoja naye na akawaeleza wazi kukataa na kusitasita kwa watu wa Kufah, kisha akawaambia: “Wafuasi wetu wametufedhehesha hivyo anayependa kuondoka basi na aondoke na wala hatakuwa na dhima yetu.”

Pamoja na hivyo Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.) alibaki na msimamo wake na azma ile ile aliyotoka nayo Makkah na hakuwa na yeyote isipokuwa wafuasi, ndugu, watoto na watoto wa Ami zake, na idadi yao haizidi sabini na nane na hapo alitamka tamko lake lenye kudumu; “Kama dini ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w ) haiwezi kusimama isipokuwa kwa kuuliwa kwangu, basi enyi mapanga niuweni.”

Na alikutana na jeshi la Yazid bin Mu’awiyah bin Abi Sufian, ambalo idadi yake ilikuwa ni elfu thelathini na mbili, chini ya uongozi wa Hur bin Yazid Ar-Riyaahi. Kwa kawaida kulikuwa na uwezekano mkubwa wa jeshi la Banu Umayyah kuuwa kundi hili lenye idadi ndogo, na hiyo ni kweli. Katika siku hiyo yalitokea mauaji hayo kwa Ahlul-Bayt(a.s ) na kudhulumiwa kwao kunasikitisha, kana kwamba Yazid bin Mu’awiyah bin Abi Sufian alikuwa analipa malipo ambayo Mtume wa Allah(s.a.w.w ) alimuomba: “Sema siwaombi juu yake malipo isipokuwa kuwapenda jamaa zangu”.

Tarekh imesimulia matukio na mauaji ambayo ni vigumu mno kwa mtu yeyote kuyaelezea. Kati ya hayo ni ya mtoto mchanga, naye ni ‘Abadallah bin Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) , ambaye Imam Hussein alimbeba kwenda kumwombea maji baada ya wao kuweka kizuizi baina ya watu wa kambi ya Al Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) , na mto Furati na kiu ikawabana sana. Alimbeba kwenda kumwombea maji na ili kuzitikisa dhamiri zao na kuathiri hisia zao za kibinadamu, hawakumjibu isipokuwa kwa kumlenga mshale mtoto mchanga na wakamwua, na mashahidi katika wafuasi wa Hussein na Ahlul-Bayt(a.s ) waliendelea kuuawa mmoja baada ya mwingine. Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) alikuwa ni wa mwisho kufa shahid katika vita hivyo vibaya.

Hawakutosheka kwa kumuuwa Bwana wa vijana wa watu wa Jannat (pepo) bali walikata kichwa chake na wakakitenganisha na mwili wake, kichwa cha Al Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) na vichwa vya wafuasi wake vilichukuliwa na kuwa zawadi, wauaji walivigawa na wakavinyanyua huku wakielekea kwa Yazid bin Mu’awiyah bin Abi Sufian huko Sham ambaye, baadhi ya Waislamu wamempa sifa ya Amirul-Muuminin basi hakuna nguvu wala hila isipokuwa kutoka kwa Allah (s.w.t)...!

Hakika matukio, mambo na misimamo ambayo tumeieleza na ambayo wameafikiana wapokezi wote wa Kiislamu Sunni na Shi’a, yanabainisha wazi malengo matukufu na ambayo kwa ajili yake Al Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s ) alifanya Thawrah, pamoja na hayo, ingawa ufisadi, uasherati na upotovu, na uovu ulioenea ambao ni wajibu kuuondoa kwa mkono, ulimi na kuchukia kwa moyo kumepatikana, wanaokosoa Thawrah hii tukufu kwa sababu ya kutumbukia kwao katika propaganda wa upotoshaji wa Bani Umayyah ambao umejaribu kupotosha historia, na vile vile kwa sababu ya kutumbukia kwao katika ta’asub (ushabiki) mbaya za kimadhehebu.

Hivyo zikadhihiri hukumu zenye kutia kasoro na kauli zenye kutuhumu juu ya Thawrah ya ambaye Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema juu yake kwa mapokezi ya Waislamu wote, kwamba yeye ni Bwana wa vijana wa watu wa Jannat; kwa mfano kauli ya Ibn Taymiyyah: “Hakika Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) kwa Thawrah yake amekwisha toka katika utii wa kiongozi wa Waislamu na kwamba vile vile amechochea fitina katika ‘Ummah wa Kiislamu!!” Na kama tutamwuliza huyu juu ya kutoka Mu’awiyah bin Abi Sufian katika utii wa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) jibu lake lingekuwa hiyo ni fitina iliyotokea baina yao na wala wao hawana dhambi katika hilo.

Na hili si lingine isipokuwa ni hali miongoni mwa hali za kujaribu kupotosha na udanganyifu ambao uko wazi katika historia ya Kiislamu, vinginevyo itatafsiriwaje hali ya baadhi ya Waislamu ya kujifanya kutojua mauaji haya ya kihistoria, ambayo humo wameuliwa watoto wa Mtume wa Allah(s.a.w.w) katika hali mbaya kabisa ya mauaji na adhabu?

Sio hayo tu, bali watawala wengine wa Bani Umayyah walifuata mwendo wa Mu’awiyah bin Abi Sufian na mtoto wake Yazid; watawala wengine katika kuzima harakati za wapinzani wa utawala wao, na hasa Ahlul-Bayt(a.s) wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , walihahikisha kwamba, daima wanakandamizwa, wanafukuzwa, wanaadhibiwa na kuuliwa.

Na udhalimu wao ulikuwa kwa Ahlul-Bayt(a.s) na wasiokuwa Ahlul-Bayt(a.s) , walikuwa ni shabaha katika kila nyanja ambazo kuna dhana ya kuleta ushindani katika utawala wao wa kidunia na ufalme wa Kisra.

Historia imeandika kwa mfano - tukio la mauaji ambalo alichinjwa ‘Abadallah bin Zubeir, na akachunwa katika eneo takatifu la Makkah ambalo hata makafiri walikuwa wanalitukuza na kuliheshimu, wala hawakuhalalisha kumwagwa humo damu ya mnyama tukiachilia mbali ya binadamu. Al-Ka’abah Tukufu haikumsaidia kitu chochote Ibn Zubeir ambapo aligandamana na pazia yake kwa watawala wa Bani Umayyah.

Vipi nyumba ya Allah (s.w.t) itakuwa na utukufu kwao na wao ndio ambao waliipiga Al-Ka’abah Tukufu kwa manjanikh (makombeo ya moto), wakati wa utawala wa Abdul-Malik bin Marwan ambaye alitoa mamlaka katika mkono wa mwovu wake Hajjaj ya kuuwa, anauwa na kuchinja watu bila ya haki, na ambao Hassan Al-Basri amesema juu yao: “Kama ‘Abdul-Malik asingekuwa na kosa isipokuwa Hajjaj basi lingemtosha”. Na amesema ‘Umar Abdul-Aziz: “Kama kila ‘Ummah ungekuja na mwovu wao na sisi tukaja na Hajjaj basi tungewashinda”, tukiachilia mbali kisa mashuhuri cha ‘Abdul-Malik cha kuchana Kitabu cha Allah (s.w.t.).

Je, vitendo hivi vinamfanya mwenye kuvitenda kuwa Mwislamu? Tukiachilia mbali kumuuwa kwake Khalifa wa Waislamu na Amirul- Muuminin?

Hapana shaka kwamba sisi leo tuna haja ya kuangalia historia ya Kiisalmu, na kudadisi katika mengi ya matukio na kuchunguza kwa yale yaliyopo miongoni mwa uhusiano mkubwa na maisha yetu ya kila siku na yawe ndiyo hukumu yetu katika kundi hili au lile, mbali na dhuluma au makosa kwa sababu ya matukio hayo Waislamu wamegawanyika madhehebu na makundi yenye kuzozana, kila moja linadai kuwa ndilo kundi lenye kunusurika na sio kwa yeyote kusubiri wahyi kutoka mbinguni umteremkie na kumwambia jina la kundi hili lenye kunusurika.

Na Allah (s.w.t) ametujaalia akili ili tutofautishe ovu na jema na akatukataza kuiga kwa upofu na akatutanabahisha: “Bali aliwajia kwa haki na wengi wao ni wenye kuchukia haki.” Na akatuhadharisha kuchukua kutoka kwa kila mtu, “kama akikujieni fasiki kwa habari basi chunguzeni msije mkawadhuru watu kwa ujinga na mkaja juta kwa mliyoyafanya.”

Shura Baina Ya Misingi Na Utekelezaji

Baadhi ya wenye kukhalifu wanajaribu kupinga Ayah za Uimamu wa Ahlul Bayt(a.s) kwa madai kuwa Uimamu wa Waislamu umefanywa kuwa Shura na wametoa ushahidi wa Ayah mbili kutoka katika Kitabu cha Allah (s.w.t). Ya kwanza ni:

Na jambo lao ni Shura baina yao .” (Asy Syuura 42:38).

Ayah hii haionyeshi Shura katika mambo yote ya Waislamu, hiyo ni kwa sababu kushauriana hakusihi katika jambo ambalo kuna Ayah ya Allah (s.w.t) na kauli ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) :

وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ ۗ وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا ﴿٣٦ ﴾

Haikuwa kwa Muumini mwanamme wala Muumini mwanamke anapohukumu Allah (s.w.t) na Mtume wake wawe na hiari katika jambo lao na atakae muasi Allah (s.w.t) na Mtume wake basi amepotea upotevu ulio wazi .” (Al-Azhaab 33:36).

Vinginevyo, je inajuzu kushauriana katika idadi ya raka’a za sala kwa mfano, au mengineyo katika hukumu ambazo kumeteremka Ayah, na tumebainisha yaliyo pokewa kutoka kwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) miongoni mwa hadith za Uimamu, hivyo haibaki nafasi ya kushauriana. Ama Ayah ya pili ambayo ni:

Washauri katika jambo ” (Ali-Imran 3:159)

Bali anamwambia: “ukiazimia mtegemee Allah (s.w.t).” Na fanya kulingana na unavyoona na inadhihiri kuwa nafasi ya kushauriana inayo pendekezwa ni katika vita, na utapata mfano katika ushauriano huu katika sehemu ya nne ya kitabu hiki wakati Mtume lipowashauri Masahaba wake katika vita vya Badr. Na kama tutajaalia uwa hukumu ya Khalifa wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ni Shura hakika tutajiuliza. Hii Shura ni ya namna gani?

Na ni ipi njia ya kuitekeleza? Na namna gani makhalifa walitekeleza Shura hii? Na nini hukumu ya khalifa ambaye anafikia katika utawala hali amekwishavunja misingi ya Shura?

Na namna gani makhalifa walitekeleza Shura hii kisha tuangalie namna gani kila mmoja katika makhalifa wa mwanzo alivyofika katika utawala.

1. Ukhalifa Wa Abubakr Ibn Abu Quhafa

Hakika njia ambayo ilitimia katika kumtawalisha Abubakr na kupewa Bai’a, amekwisha ieleza ‘Umar ibn Al-Khattab - kama ilivyotangulia - ilikuwa ghafla, lakini Allah (s.w.t) ameepusha shari yake. Na tumeona kutukanana kwa Muhajirin na Ansar juu ya Ukhalifa, na Ansar walitoa hoja ya kustahiki kwao ukhalifa, tukizingatia asili na nafasi yao katika uongozi wa Madina na kunusuru kwao kukubwa katika Uislamu, na hoja za Muhajirin zilikuwa kwamba wao wanastahiki zaidi, na Abubakr alipendekeza uongozi uwe wa Muhajirin na wasaidizi wawe ni Ansar. Ansar wakamjibu kutokana na mapendekezo yake kuwa kila kundi katika makundi mawili yawe na kiongozi kwa kauli yao: “Kwetu kuwe na kiongozi na kwenu kuwe na kiongozi.”

Na tumeona namna gani ‘Umar aliokoa msimamo huu kwa kuuchukua kwa nguvu na kumpa Abubakr bay’a. Wakati ambapo Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) pamoja na jamaa wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) hawakuwepo, hivyo Ahlul- Bayt(a.s) wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) hawakupata fursa katika kuchagua au hata kutoa maoni, iko wapi Shura katika hayo yote?

2. Zama Za ‘Umar

Njia ambayo amefikia ‘Umar katika utawala ni kutokana na wosia aliyo ulioandikwa na Abubakr akiwa katika maradhi yake ya mwisho mbele ya ‘Uthman bin ‘‘Affan tu! Na ‘Umar akachukua wosia huo na kutoa ushahidi kwa watu na akachukua Bai’a kwao kwa sababu hiyo. Je, iko wapi Shura katika hili?

3. Zama Za ‘Uthman Bin ‘‘Affan

Njia ambayo amefikia ‘Uthman bin ‘‘Affan katika utawala, ilitegemea kikao cha Shura na ‘Umar bin Al-Khattab peke yake aliteua wajumbe wake sita, na akajaalia rai ya mwisho mikononi mwa Abdur-Rahman bin ‘Auf katika hali ya kugawanyika wajumbe sita sehemu mbili kama ilivyotokea. Shura iko wapi hapo?

4. Zama Za Mu’awiyah Bin Abi Sufian

Njia ambayo Mu’awiyah bin Abi Sufian alifikia katika utawala, ilikuwa ni kwa kunyanyua upanga dhidi ya Khalifa wa Waislamu na Imam wao aliyepewa Bai’a na wao, baada ya watu kumkimbilia na kumbay’i baada ya kuuliwa ‘Uthman bin ‘Affan kisha, baada ya kumlazimisha Al-Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) kufanya suluhu.

5. Zama Za Yazid Bin Mu’awiyah Bin Abi Sufian

Njia ambayo Yazid bin Mu’awiyah bin Abi Sufian amefikia katika utawala ilikuwa ni wosia kutoka kwa baba yake, ambaye alileta njia mpya katika ukhalifa na kuufanya kuwa ni wa kurithiana. Shura iko wapi hapa?

Na Yazid bin Mu’awiyah bin Abi Sufian alizatiti utawala wake kwa kumwua Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) , na watoto wengine wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) pale Karbala. Vivyo hivyo ndivyo watawala wengine wa Waislamu walifikia katika utawala tangu siku hiyo hadi leo hii.

Hivyo njia ambayo ilitumika kuwatawalisha makhalifa katika maelezo tuliyoyataja tunailinganisha na njia ambayo inatumiwa kuwateua watawala wa dola za kimagharibi katika njia ambayo inaitwa Demokrasia.

Basi ni ipi kati ya njia mbili hizi ambayo ni bora kwa mtazamo wa akili sahihi ambayo imeepukana na ta’asub ya dini na madhehebu?

Jamhuri ya Waislamu katika Ahl as-Sunnah wamekataa Hadith zilizopokelewa kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kuteua Maimamu wa Ahlul-Bayt(a.s) kuwa ni Makhalifa wake katika ‘Ummah wa Kiislamu, hivyo wakapinga Hadith katika hilo na wakawapinga wale wanaoziitakidi kwa kusema kwamba jambo hili ni Shura, wakati ambapo Shura haikuwa na athari yoyote katika kutawalisha makhalifa ambao wanawakubali. Wamepinga Hadith za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kuhusu ukhalifa na wakaukubali kutoka kwa asiyekuwa Mtume, na hawakuweka sharti la Shura katika nassi (pokezi) nyingine zisizokuwa hizo bali wamekubali uteuzi wa waliye mchagua.

Wamehukumu uhalali wa Yazid bin Mu’awiyah bin Abi Sufian, ingawa kulikuwa na Thawrah ya Bwana wa mashahidi, na wakahukumu uhalali wa Mu’awiyah bin Abi Sufian ingawa alimuasi Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) na akatoka katika utii wake.

Hakika kosa la wazi ambalo Jamhuri ya Waislamu wanatumbukia kwalo, ni kuchukua Hadith za Nabii katika madhehebu ambayo wanayaamini - yaani wengi wao wanakataa Hadith kwa sababu tu ina khalifu madhehebu yao hata kama Hadith hii imetoka katika vitabu vyao ambavyo wanaamini usahihi wake - pamoja na kwamba hukumu ya akili inawajibisha kuchukua madhehebu kutoka katika nassi na wala si kinyume.

Mwisho Wa Utafiti Wa Uimamu

Tumebainisha katika yaliyotangulia Hadith za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) katika Uimamu ambao unapatikana katika Maimamu wa Ahlul-Bayt(a.s) wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , na ambao ni maalumu kwa Maimamu kumi na wawili(a.s) , ambao wa kwanza ni Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) . Na tukaweka wazi baadhi ya (mambo) yasiyo eleweka vizuri katika Hadith hizo miongoni mwa dalili, na tukatengua shaka zinazoizunguka. Kisha tukabainisha jinsi Jamhuri ya Masahaba walivyo amiliana na Hadith hizo, kisha Jamhuri ya Waislamu ikaufuata mwendo wao huo hadi leo hii.

Hakika mafhumu ya Uimamu ndiyo ambayo yamewafarakisha Waislamu punde tu baada ya kufariki kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , isipokuwa Mashi’a ndio wamejulikana kwa kuchukua kwao Sunnah hizi kutoka katika njia ya Ahlul-Bayt(a.s) na Maimamu wao kumi na wawili; ambapo Ahl as-Sunnah wanachukua Sunnah za Nabii kutoka kwa sahaba yeyote. Aidha wameongezea katika Sunnah ya Nabii, Sunnah ya Makhalifa wawili Abubakr na ‘Umar (na utaona katika sehemu zinazofuatia mengi miongoni mwa ushahidi juu ya ukweli huu).

Na tumebainisha namna gani Jamhuri ya Masahaba walivyofanya ijtihad kati ya Waislamu waliotangulia (na waliosifika zaidi kwa hilo miongoni mwao ni Abubakr, ‘Umar, ‘Aisha na Mu’awiyah bin Abi Sufian); mbele ya Hadith za Mtume kuhusu Uimamu. Jambo ambalo limewaweka mbali Maimamu wa Ahlul Bayt(a.s) katika uongozi wa mambo ya ‘Ummah wa Kiislamu, na hasa baada ya kufa shahidi Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) na wakawa ni wenye kupokonywa haki.

Moja kwa moja wamekuwa ni kundi la upinzani ambao hawaoni uhalali wa watawala ambao wameshika uongozi wa Waislamu bila ya haki. Basi wafuasi wa Ahlul Bayt(a.s) wakawa ni kundi lenye kuchukiwa na watawala wa Waislamu; na hasa Bani ‘Umayyah na Bani ‘Abbas.

Na mgawanyiko wa Waislamu ulikuwa ni makundi mawili yaliyo dhihiri baada ya matukio mawili ya Vita vya Jamal na Siffin, na kufa shahidi kwa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) . Baada ya kuwa kundi la Ahlul Bayt(a.s) ni lenye kufichikana katika zama za Makhalifa watatu wa mwanzo kufuatana na siasa ya hekima aliyoifuata Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) , kila kundi likawa linadhihirisha dalili na ushahidi walio nao katika haki ya madai yao na kundi lao.

Wakati ambapo wafuasi wa Mu’awiyah bin Abi Sufian, Yazid bin Mu’awiyah bin Abi Sufian na watawala wengine wa Bani ‘Umayyah walikosa hoja na ushahidi wa kupinga Hadith zenye nguvu za Uimamu wa Ahlul-Bayt(a.s) , mmoja wao ambaye ni Seif bin ‘Umar At-Tamimiy ambaye amejulikana kwa uongo na uzindiki kwa maulamaa wa Hadith walio tangulia, akazua kwa msaada wa mabwana zake ambao kwayo amejengea Ushi’a kwa huyu mtu wa bandia; na tumebainisha ubatili wa njama hii ya uongo wa ‘Abdillah bin Saba,’ na hata kama ikadhaniwa kuwa alikuwepo kweli, basi hakika yeye siye ambaye alitangaza uwasii wa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib(a.s) na kumfanya kuwa Khalifa, bali ni Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kutokana na Hadith tulizozieleza katika sehemu ya kwanza.

5