• Anza
  • Iliyopita
  • 3 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 1209 / Pakua: 511
Kiwango Kiwango Kiwango
SAFARI YA BIBI MAASUMA

SAFARI YA BIBI MAASUMA

Mwandishi:
Swahili

UTENZI WA IMAM HUSEN SAFARI YA BIBI MAASUMA

SAFARI YA BIBI MAASUMA

JINA LA KITABU: MAISHA YA BIBI FATUMA MAASUMAH (A.S)

MTUNZI: GHULAM RIDHAA HAIDARY ABHARY

MTARJUMI: KHEIR ABOUKHEIR

WAENEZAJI: MUASSASATUL IMAM ALI (A.S.)

MWAKA WA CHAPA: 2002/1423

KOPI: 3000

Kilikuwa kimepita kipindi cha mwaka mmoja tangu Imamu Ridhaa(a.s) aondoke katika mji mtukufu wa Madina na kuelekea Marw, jambo hili liliwaathiri kwa kiasi kikubwa ndugu na jamaa zake waliokuwa katika mji wa Madina na hasa Ahlulbayti(a.s) waliokuwa wamebaki Madina. Wote walikuwa ni wanyonge kwa kukikosa kipenzi chao ambacho walikuwa bado wakizihisi hisia zake na zile neema alizokuwa nazo pindi walipokuwa karibu naye na ilikuwa ni vigumu kwa hisia ndoto na mapenzi waliyokuwa nayo juu ya Imamu kuwatoka haraka kiasi hichi na sasa walikuwa na hamu na shauku ya kutaka kuonana tena na Imamu(a.s). Fatuma Maasuma(a.s) kama walivyokuwa kaka na dada zake yeye pia alijawa na huzuni na shauku ya kutaka kuonana na kaka yake, kwani kule kumkosa kwake Imamu kulizidi kumhuzunisha kila kulipokucha. Imamu pia huko alikokuwa alikuwa akiwakumbuka sana familia yake na hasa dada yake mpenzi Faatuma(a.s) , na katika hali hiyo ndipo Imamu alipoamua kuandika barua kwa ajili ya dada yake na kumpa mmoja kati ya wasaidizi wake kwenda katika mji mtukufu wa Madina kupeleka barua hiyo lakini kwa masharti ya kwamba asisimame njiani wala sehemu yeyote hadi afike katika mji mtukufu wa Madina haraka iwezekanavyo. Hivyo kabla ya kuondoka huyo bwana, Imamu alimwelekeza hadi katika nyumba aliyokuwa akiishi baba yake na familia yake tukufu na alifanya hivi ili huyu bwana asije akamuuliza mtu mwengine yeyote kuhusu nyumba hiyo. Kwa kutekeleza amri mjumbe aliyetumwa na Imamu Ridhaa(a.s) kupeleka barua alifika mapema katika mji wa Madina na kuukabithisha ujumbe aliotumwa mikononi mwa Fatuma maasumah. Japokuwa haikufahamika juu ya kiwango na uzito wa barua yenyewe lakini la muhimu tuu ni kwamba barua ile ilizidi kuamsha kuchochea na kutia hamasa ile nia ya kutaka kumuona ndugu yao, na kutokana na hali hiyo bibi maasumah hakusita kuwafahamisha ndugu zake kuhusu ujumbe ule na kwamba alilazimika kuondoka Madina kwenda Marw kumfuata kaka yake na ndugu zake waliafiki na haraka wakaandaa mipango ya safari. ilipokamilika walianza safari ya kuelekea Marw msafara ambao uliwajumuisha bibi maasumah na ndugu zake wengine watano ambao walikuwa ni:- (i) Faadhil, (ii) Jaafar, (iii) Haady, (iv) Qaasim na Zaidi. Pia bibi Maasumah na ndugu zake katika msafara huo waliongozana na watoto wa ndugu zake pamoja na watumishi wa kike na kiume. Safari ilianza na kila mmoja kichwani alikuwa akitafakari namna atakavyokutana na Imamu Ridhaa(a.s) Itakuwa ni furaha iliyoje kwao kukutana na kipenzi chao waliyetengana naye zaidi ya mwaka? Hili ni suali ambalo kila mmoja laikuwa akijiuliza wakati msafara wa kuelekea Marw ulipokuwa unaanza harakati. Msafara ulizidi kwenda kwa kasi huku wakipita milima na mabonde na kuhakikisha ya kwamba walikuwa hawasimami sehemu yoyote ile njiani isipokuwa katika mambo ya dharura tuu kama vile ibada na chakula, zaidi ya hayo hakuna jambo lingine ambalo liliweza kuwasimamisha njiani. Walizidi kutembea kwa kasi kadiri walivyoweza na huku wakizidi kupita miji na kuviacha nyuma yao vilima hivi na vile na hatimaye sasa msafara ulikuwa unaupa mgongo mji mtukufu wa Madina na kuzidi kuukaribia mji wa Marw. Kwa kweli safari ya jangwani sii kama safari nyingine kwa hiyo haikuwa ni kazi rahisi kwa bibi maasumah na kundi lake kusafiri katika jangwa. Kwani ilikuwa ni safari ndefu na yakuchosha mno, hata baadhi ya nyakati ngamia zao zilikuwa zinalemewa kutoka na ugumu na uzito wa safari hiyo, lakini pamoja na hayo haikuwa hoja ya kuakhirisha safari au kufanya safari nzima ishindwe kuendelea, lakini kutokana na nuru, shauku, hamasa na mapenzi ya kukutana na kaka yao walijikuta wakipata mori na motisha uliowafanya wasahau taabu matatizo na uchovu wote wa safari hiyo ndefu na yenye matatizo mengi jangwani na kujilazimu kuendelea na safari. Lakini safari ni safari kama zilivyo safari nyingine ndefu za jangwani ama sehemu nyengine yeyote kwani kila safari inakuwa na matatizo yake, na hata katika zama zile safari kama hizo Zilikuwa pia na matatizo yake haswa za Jangwani kama hizi ambazo ziliulikuwa na khatari kubwa ya watekaji nyara ambao waliwavizia wasafiri na hata wafanyabiashara mbalimbali nje na mijini huko majangwani. Waliwavamia na kupora mali zao walizokuwa nazo vito vya thamani na hata vipando vyao. Na kuna nyakati zingine waliwauwa wale wamiliki wa mali hizo ili waweze kupata urahisi wa kuzipora mali hizo, na hili lilikuwa ni tatizo kubwa ambalo liliwakumba wasafiri wengi waliokuwa wakifnya safari ndefu jangwani, Hili lilikuwa ni tatizo lingine lililo msumbua sana bibi maasumah na ndugu zake katika msafara huo, lakini kutokana na shauku ya kuonana na kaka yao hilo halikuwa muhimu tena kwao kwani hasa baada ya kutawakul na kutaraji ulinzi kutoka kwa Mola wao walilisahau kabisa tatizo hilo wakiwa na wazo moja tuu lilokuwa likiwasumbua akili zao nalo ni kuonana na kaka yao mpenzi. Hivyo safari iliendelea na siku baada ya siku walikuwa wakiikaribia sehemu waliyokuwa wameikusudia. Zilipita sekunde, dakika, masaa, na hata masiku huku msafara ukizidi kusonga mbele na kuacha nyuma milima na mabonde na sasa hayakubaki masafa marefu kwa msafara kuingia katika ardhi ya Iran. Lakini kutokana na matatizo na urefu wa safari bibi maasumah(a.s) alikuwa amechoka sana na hata ndugu zake wengine ambao alikuwa ameongozana nao katika safari hiyo. Lakini jambo lililokuwa likiwajasiri ni ile hamu na shauku ya kuonana na kaka yao mpenzi Imamu Ridhaa(a.s) . Marw ni moja ya mji katika nchi ya Iran kwa hiyo kila mmoja alikuwa akijitahidi kwa kadiri ya uwezo wake wote ili angalao wakutane na kaka yao mpenzi Imamu Ridhaa, na walikuwa wakiyakumbuka masiku ambayo yalipita wakiwa pamoja katika mji mtukufu wa Madina, jambo hilo liliwapa matumaini mengi na kuwajaza furaha nyingi sana na hichi ndicho kitu kilichasababisha woga na uchovu ukose nafasi katika nafsi zao tukufu, na sasa kile kipindi kigumu cha shida na matizo ya safari ndefu yenye kutisha na kuchosha safari ya jangwani kilikuwa kimekwisha na sasa walikuwa wanaingia katika arthi ya Irani wakipita kijiji kimoja hadi kingine na mji mmoja hadi mwingine.

HATIMAYE MSAFARA WAINGIA MJI WA SAVEE

Hatimaye msafara uliingia katika mji wa Savee, lakini kutokana na shida na uchovu mwingi na pia kubadilika kwa hali ya hewa safari iliingia dosari pale maradhi yalipomwanza bibi maasumah(a.s) , yalikuwa ni maradhi makali kiasi kwamba sasa hawakuwa na uwezo wa kuweza kuendelea na safari na sasa kutokana na maradhi yaliyo changanyika na uchovu wingi wa safari ulipelekea mwili mtukufu wa bibi maasumah kubadilika rangi. Na sasa walikuwa wakijiuliza maswali kadhaa lakini swali gumu ambalo lilikuwa juu yao ni kwamba hivi kweli bibi maasumah katika hali kama ile angeweza kutekeleza ile nia na azma aliyokuwa nayo na kuendelea na safari ili kuonana na kaka yake mpenzi huko Marw?. Swali hili lilimuumiza hata bibi maasumah mwenyewe na kumsababishia majonzi makubwa. Hivyo basi msafara ulisimama na baada ya kushauriana waliamua ya kwamba waende katika mji wa karibu ili bibi maasumah(a.s) aweze kupata matibabu na kisha waendelee na safari yao kuelekea Marw. Kwa pamoja msafara ulikubaliana kwamba uelekee katika mji wa Qom. Qom ni mji wa pekee ulioonekana kuwa na mashia wengi japo kuwa katika zama hizo dhehebu hilo lilikuwa ni halijaenea katika mji ya Iran, lakini kutokana na kuhama kwa mashia wengi kutoka katika miji ya Kuufe ulioko Iraq na kuja Iran ambako walikusanyika katika mji wa Qom. Mji ambao wakazi wake walikuwa wamejawa sana na mapenzi mazito juu ya Ahlulbayti wa Mtume wetu Mtukufu. Kutokana na uadui wa wazi uliokuwa ukifanywa na watawala waliokuwa madarakani katika enzi hizo dhidi ya Ahlulbayti na hii ilisababisha mashia wengi sana kuhama kutoka katika miji mingine mingi kama vile Kufaa na kuja kuujenga mji wa Qom na hasa ndio waliouanzisha. Na pindi zilipowafikia watu wa Qom khabari za kuwepo kwa bibi maasumah ndani ya Irani katika mji wa Savee na vilevile ni mgonjwa, walikusanyika watu wa Qom ili kupanga na kisha kuongozana hadi katika mji wa Savee ili kumlaki bibi maasumah na kuongea naye uwezekano wa yeye kuja katika mji wa Qom. Hivyo basi waliamua kumteua mjumbe wa kuwawakilisha huko nae ni bwana Mussa bin Khazraj aupeleke ujumbe wao hadi kwa maasumah na kisha amweleze ni kiasi gani watu wa Qom walivyokuwa na shauku ya ziara yake katika mji huo ujumbe ambao aliuafiki bibi maasumah na kuamuru msafara uelekee Qom. Na aliyekuwa akiuongoza msafara huo alikuwa ni bwana Mussa bin Khazraji, aliuongoza msafara huo hadi katika mji ambao wakazi wake walikuwa na mapenzi na shauku kubwa ya kumuona mjukuu huyo wa Mtume wetu mtukufu na dada yake Imamu Ridhaa(a.s) katika mji wa Qom.

KIFO CHA BIBI MAASUMU

Ilikuwa ni tarehe 23 ya mwezi watatu (Rabiul Awal) mwaka wa 201 msafara wa bibi Maasumuah ulifika katika mji wa Qom na waliona fahari sana watu wa Qom na kutokana na ugeni huo uliowajia. Na kwa upande mwingine bwana Mussa bin Khazraj alikuwa ni mtu mwenye nafasi nzuri kimaisha na alikuwa na nyumba ambayo ilikuwa na nafasi nzuri na ya kutosha na hivyo msafara ulipofika tuu Qom ulifikia moja kwa moja nyumbani kwake. Na kwa msafara wa bibi maasumah kufikia katika nyumba ya bwana Mussa ilikuwa ni furaha ya ajabu bahati na utukufu wa kipekee katika familia ya bwana Mussa na hata kwa yeyote yule ambaye angeweza kuipata fursa hiyo hivyo bwana Mussa alijikuta akiwa na furaha isiyosemeka kwa kupata nafasi ya kuwahudumia wageni wake waliotoka katika mji mtukufu wa Mtume wetu Mtukufu(s.a.w.w) mji wa Madina. Na alijitahidi kuwahudumia kwa kadiri alivyoweza kwa kuwatayarishia kila jambo ambalo walilihitaji kwa haraka na uchangamfu wa hali ya juu. Katika muda wote ambao bibi maasumah(a.s) alikuwa katika mji wa Qom alikuwa ni mwingi sana wa ibada na unyenyekevu akiomba kutoka kwa mola mwingi wa rehema na msamehevu aweze kumsahilishia yote aliyokuwa nayo na sehemu ambayo alikuwa akifanyia ibada bibi maasumah ipo hadi leo na huitwa "Nyumba yenye nuru" Wakazi wa mji wa Qom pamoja na msafara mzima aliokuja nao bibi maasumah alikuwa na majonzi mazito kutokana na hali liyokuwa nayo bibi maasumah na japokuwa alikuwa ni mtumiaji wa dawa lakini bado hali yake ilizidi kuwa mbaya siku hadi siku na hii ilitokana na kwamba maradhi yake yalikuwa yameenea mwili wake wote. Na siku ya kumi katika mwezi wa rabiu Thaani (Mwezi wa Kumi) mwaka wa mia mbili na moja 201 baada ya hijra mwezi wa kiarabu ilikuwa ni siku ambayo ilikuwa ni chungu kuliko siku nyingine zozote katika Ahlubayti walio ongozana na bibi maasumah katika msafara wao na watu wa Qom pia ni siku ambayo wapenzi wa Ahlulbayt walipata pigo lingine na pigo kubwa kuliko lile la mwanzoni. Pigo ambalo kwamwe sii la kusahaulika kwani liliandikwa katika vitabu vya historia ili kila mtu alielewe nayo ni siku hiyo ambayo bibi maasumah alifariki duni alifariki dunia bila hata ya kutimiza azma yake ya kutaka kukutana na kaka yake mpenzi Imamu Ridhaa ambaye yeye alikuwa katika mji wa Marw. Hata kabla ya kifo chake bibi maasumah alikuwa akibubujikwa na machozi na moyo wake kugubikwa na wimbi la huzuni kwa kutengana na kaka yake na hata alipoondoka katika mji mtukufu wa Madina kwa lengo moja tuu la kuja kumuona kaka yake mpenzi lakini sasa alikuwa anafariki dunia bila hata kumwona tena kwa mara ya mwisho kaka yake mpenzi, na wakati huo bibi maasumah alikuwa na umri wa miaka 28. Walipigwa na butwaa watu wa Qom kutokana na msiba huo uliowapata na hawakuweza kabisa kuzuia huzuni zao zilizojaa nyoyoni mwao kwa kuondokewa na kipenzi chao, na hivyo basi waliweka vikao vya kuombaoleza msiba huo.

MAZISHI YAKE BIBI MAASUMU.

Kutokana na mapenzi mazito waliyokuwa nayo wanawake wa kishia waliokuwa Qom juu ya bibi Maasumah walijitolea kwa mapenzi makubwa na moyo mkunjufu kuuosha mwili mtukufu wa bibi maasumah na kisha wakaukafini na sasa ulifika wakati wa mazishi. Wakati wa mazishi walionelea ni vema azikwe na kiongozi mwadilifu na mwenye utukufu fulani huyo haswa ndiye auzike mwili mtukufu mahala palipostahili tofauti kabisa na yale maeneo yaliyokuwa yanazikwa watu wengine na hilo alilikusudia kutoakana na mapenzi mazito waliyokuwa nayo juu ya bibi maasumah hawakupenda kabisa azikwe katika makaburi ya pamoja na yaliyozikwa watu wengine. Na ni yule yule Mussa bin Khazraj ambaye kutokana na nafasi aliyokuwa nayo aliweza kumtengea ardhi kubwa katika sehemu iliyojulikana kwa jina la "Babilon" iliyokuwa pembezoni mwa mto Qom. Mahali ilipo haram tukufu kwa hivi sasa. Kila kitu kilikuwa ni tayari lakini jambo moja ni kwamba ni nani haswa ambaye angeshughulika na kuuzika mwili mtukufu wa bibi maasumah? Tendo hilo lilipelekea maelfu ya watu waliokuwa pale kuanza kujadili kuhusu nani hasa anayefaa na kustahiki kuuzika mwili wa bibi maasumah. Baada ya mjadala wa muda waliafikiana kwa pamoja kwamba wamwite sheikh mkubwa na wakuaminika aliyekuwa anakaa maeneo hayo shekhe huyo alijulikana kwa jina la "KAADIR" hivyo walimtuma mtu kumwita sheikh huyo haraka iwezekanavyo lakini kwa bahati mbaya mtu huyo hakumkuta lakini nyumbani kwake, na alipokuwa akirejea toka nyumbani kwa sheikh Kaadir alikuatana na watu wawili waliokuwa wamepanda vipando walitokea pembezoni mwa mto Qom. Na huku wakielekea sehemu ya maziko na walipofika ulipokuwa mwili mtukufu waliuswalia swala ya jeneza na kisha wakaanza kuuzika mwili mtukufu wa bibi maasumah. Na kwa mshangao wa watu wengi pindi watu hao walipomaliza kuuzika mwili mtukufu wa bibi maasumah walipanda vipando vyao na kutokomea kwa haraka. Yalimalizika maziko kwa kila aina ya heshima na taadhima toka kwa mashia waliokuwa wamejaa majonzi na masikitiko na kuanzia kipindi hicho ndipo mji wa Qom ulipoanza kujulikana kama kiota cha familia ya Muhammad rehema na amani za mwenyezi Mungui ziwe juu yake na ahli zake. Na baada ya muda Mussa bin Khazraj aliamua kuitoa sehemu hiyo aliyozikiwa bibi Fatuma wakfu kutokana na heshima aliyokuwa amempa bibi huyo maasumah na kwa kuwa sehemu hiyo alizikwa kiumbe kitukufu na ili pia iwe ni sehemu ya kuzikiwa mashia wa Ally pembezoni mwa kaburi lake tukufu.

KABURI TUKUFU LA BIBI FATUMA MAASUMU (A.S)

THAWABU ZINAZOPATIKANA KWA KUMZURU

Saad bin Abdullah anasema ya kwamba:- " Nilimuuliza babake Hassan Ridhaa kuhusiana na Faatuma mtoto wa Mussa bin Jaafar(a.s) kisha akajibu kwa kusema :-("Amebashiriwa pepo yeyote atakae mzuru") .[1] Na pia amesema mtoto wa Imamu Ridhaa ya kwamba:-("Atakayezuru kaburi la shangazi yangu katika mji wa Qom basi amewajibikiwa na pepo"). [2] Na pia Imam Swaadik amesema:hakika mwenyezi Mungu Mtukufu anayo haram nayo iko Makka, na ya Mtume (s.a.w.w) iko Madina, na na amiirul muuminiina iko Kuufa, na sisi tunayo haram ambayo iko Qom. Na atazikwa hapo msichana katika watoto wangu ambaye atakuwa na jina la Faatuma na atakayemzuru basi amewajibikiwa pepo .[3] Na akaongeza Imamu siku hiyo:- (("Ni jambo ambalo Imam Mussa hakuwahi kulifanya kwa mama yake)) Na akaendelea kusema(a.s) :- ("Malipo ya ziara yake ni pepo")[4]. Na kutoka kwa Saadi anasema ya kwamba amepokea kutoka kwa Ally bin Mussa Ridhaa(a.s) :- [5] ((Ewe Saad kwenu mna kaburi?)) Saad akajibu, "Tafadhali unakusudia kaburi la Fatuma bint Mussa(a.s) ?" Imam akamwambia, "ndiyo atakaye mzuru akiwa anajuwa haki zake basi amewajikiwa pepo, na ufikapo kwenye kaburi lake simama upande wa kichwa chake ukiwa umeelekea kibla, na kisha useme:- Allahu akbaru mara 34, Subhanallah mara 33, Alhamdulilah 33, kisha Imam alisoma ziara yenyewe hadi mwisho kama ifuatavyo.:-5

اَلـسَّلامُ عَـلى آدَمَ صَـفْوَةِ اللّه ِ، اَلسَّلامُ عَلى نوُح نَبِىِّ اللّه ِ ، اَلسَّلامُ عَلى ا ِبْراهیمَ خَلیل اللّه ِ، اَلسَّلامُ عَلى موُسى کَلیم ِاللّه ِ ، اَلسَّلامُ عَلى عیسى روُح ِ اللّه ِ، اَلسَّلامُ عَلَیْکَ یا خَیْرَ خَلْقَ اللّه ِ ، اَلسَّلامُ عَلَیْکَ یا صَفِىَّ اللّه ِ، اَلسَّلامُ عَلَیْکَ یا مُحَمّدَ بْنَ عَبْد ِاللّه خاتَمَ النَّبِیّینَ، اَلسَّلامُ عَلَیْکَ یا اَمیرَالْمُؤْمِنینَ عَلىَّ بْنَ اَبى طالِب وَصِىَّ رَسوُل ِ اللّه، اَلسَّلامُ عَلَیْكِ یا فاطِمَةُ سَیِّدَةَ نِساءِ الْعالَمین، اَلسَّلامُ عَلَیْکُما یا سِبْطَىْ نَبِىِّ الرَّحْمَةِ، وَ سَیِّدَىْ شَباب ِ أَهْل ِ الْجَنَّة، اَلسَّلامُ عَلَیْکَ یا عَلِىَّ بْنَ الْحُسَیْن سَیِّدَ الْعابِدینَ وَ قُرَّةَ عَیْن ِ النّاظِرینَ، اَلسَّلامُ عَلَیْکَ یا مُحَمَّدَ بْنَ عَلِىٍّ، باقِرَ الْعِلْم ِ بَعْدَ النَّبِىِّ ، اَلسَّلامُ عَلَیْکَ یا جَعْفَرَ بْنَ مُحَمَّد الصّادِقَ الْبارَّ الْامینَ ،اَلسَّلامُ عَلَیْکَ یا موُسَى بْنَ جَعْفَر الطّاهِرَ الطُّهْر، اَلسَّلامُ عَلَیْکَ یا عَلِىِّ بْنَ موُ سَى الرِّضَا الْمُرْتَضى، اَالسَّلامُ عَلَیْکَ یا مُحَمَّدَ بْنَ عَلِى التَّقِىَّ، اَلسَّلامُ عَلَیْکَ یا عَلِىِّ بْنَ مُحَمَّد النَّقِىَّ النّاصِحَ الْأَمینَ، اَلسَّلامُ عَلَیْکَ یا حَسَنَ بْنَ عَلِىٍّ، اَلسَّلامُ عَلَى الْوَصِىِّ مِنْ بَعْدِه ِاَللّهُمَّ صَلِّ عَلى نُورِکَ وَ سِراجِکَ، وَ وَلِىِّ وَلِیِّکَ، وَ وَصِیِّکَ، وَ حُجَّتِک عَلى خَلْقِکَ، اَلسَّلامُ عَلَیْکِ یابِنْتَ رَسوُل ِ اللّه ِ، اَلسَّلامُ عَلَیْکِ یابِنْتَ فاطِمَةَ وَ خَدیجَةَ ،اَلسَّلامُ عَلَیْکِ یابِنْتَ اَمیر ِ الْمُؤْمِنینَ ، اَلسَّلامُ عَلَیْکِ یابِنْتَ الْحَسَن ِ وَ الْحُسَیْنِ، اَلسَّلامُ عَلَیْکِ یابِنْتَ وَلِىِّ اللّه، اَلسَّلامُ عَلَیْکِ یا اُخْتَ وَلِىِّ اللّه، اَلسَّلامُ عَلَیْکِ یا عَمَّةَ وَلِىِّ اللّه، اَلسَّلامُ عَلَیْکِ یابِنْتَ موُسَى بْن ِ جَعْفَر، وَ رَحْمَةُ اللّه ِ وَ بَرَکاتُهُ، اَلسَّلامُ عَلَیْک ِ، عَرَّفَ اللّهُ بَیْنَنا وَ بَیْنَکُمْ فِىالْجَنَّة ِ، وَ حَشَرَنا فى زُمْرَتِکُمْ، وَ أَوَرَدْناحَوْضَ نَبِیِّکُمْ، وَ سَقانا بِکَأْس ِ جَدِّ کُمْ مِنْ یَدِ عَلِى ِّ بْن ِ اَبى طالِب ، صَلَواتُ اللّه عَلَیْکُمْ ،أَسْئَلُ اللّه أَنْ یُرِیَنا فیکُمُ السُّروُرَ وَ الْفَرَجَ ،وَ أَنْ یَجْمَعَنا وَ إِیّاکُمْ فى زُمْرَة ِ جَدِّکُمْ مُحَمَّد،صَلَّى اللّهُ عَلَیْه ِ وَ آلِه ِ، وَ أَنْ لا یَسْلُبَنامَعْر ِ فَتَکُمْ، إِنَّهُ وَلِىِّ قَدیر أَتَقَرَّبُ إِلَى اللّه ِ بِحُبِّکُمْ وَ الْبَرإَة ِ مِنأَعْدائِکُمْ، وَ التَّسْلیم ِ إِلَى اللّه ، راضِیاً بِه ِ غَیْرَ مُنْکِر وَ لا مُسْتَکْبِر وَ عَلى یَقین ِ ما أَتى بِه ِمَحَمَّدٌ وَ بِهَ راض، نَطْلُبُ بِذلِکَ وَجْهِکَ یا سَیِّدى ، اَللّهُمَّ وَ رِضاکَ وَ الدّارَ الْآخِرَةِ یا فاطِمَةُ ا ِشْفَعى لى فِى الْجَنَّة فَا ِنَّ لَکَ عِنْدَاللّْه ِ شَأْناً مِنَ الشَّأْن اَللّْهُمّ ا ِنى اَسْئَلُکَ أَنْ تَخْتِمَ لى بِالسَّعادَة ِ، فَلاتَسْلُبْ مِنّى ِ ما أَنَا فیه ِ،وَ لاحُولَ وَ لا قُوَة إِلا بالّله الْعَلِىِّ الْعَظیم اَللّهُمَ اسْتَجِبْ لَنا، وَ تَقَبَّلْهُ بِکَرَمِکَ وَ عِزَّتِکَ ،وَ بِرَحْمَتِکَ وَ عافِیَتَکَ، وَ صَلَّى الّلهُ عَلى مُحَمَّد وَ آلِه ِ أَجْمَعینَ، وَ سَلَّمَ تَسْلیما

Tafsiri ya ziara:- Asalaamu ala Adam sifwati llah. Asalaamu ala Nuuhi nabiyi Llah, Asalaamu ala Ibrahim Khalili Llah, Asalaamu ala Muusa kalimi llah, Asalaamu ala Isa ruuhi llah, Asalaamu alaika ya rasul Allah, Asalaamu alaika yaa khaira lkhalki Allah, Asalaamu alaika yaa safiyu Allah, Asalaamu alaika yaa Muhammad bn Abidillah Khaatamu Annabiyyina, Asalaamu alaika Amirul Muuminiina Ali ibn Aby Twalib wasiya Rasula Allah, Asalaamu alaiki yaa Fatuma sayidati nisaai fil almiina. Asalaamu alaikuma yaa Sibtwai nabiyi rahma wa sayidi ashababu al Janna. Asalaamu alaika yaa Ali ibn Hussaini sayidi al'abidina wa kurata aini nadirina. Asalaamu alaikum yaa Muhammada bn Ali Baqir alilmi baada Annabi. Asalaamu alaika yaa Jaafar bn Muhammad Aswadiq barral-amin. Asalaamu alaika yaa Musa bn Jaafar Twahir-tuhra. Asalaamu alaika yaa Ali bn Mussa Aridhaa Al-Murtadhaa. Asalaamu alaika yaa Muhammad bn Ali Takii. Asalaamu alaika yaa Ali bn Muhammad Nakii naasir Al-amin. Asalaamu alaika yaa Hassan bn Ali. Asalaamu ala waswiyi min baadihi. Allahuma swali ala nurika wasirajika wa waliyika wawaswiyika wahujatika ala khalkika. Asalaamu alaiki yaa bint Rasula Allah. Asalaamu alaiki yaa binti Faatuma wa Khadija. Asalaamu alaiki yaa bint Amirul Muuminiina. Asalaamu alaiki yaa bint l-Hassan wal Hussain. Asalaamu alaiki yaa bint waliyu Allah. Asalaamu alaiki yaa ukhta waliyi Allah. Asalaamu alaiki yaa ammata waliyi Allah. Asalaamu alaiki ya bint Musa bn Jaafar warahmatu-Llahi wabarakatuh. Asalaamu alaiki Arafa Allahu bainana wabainakum fil-jannati wahasharna fi zumratikum. Wa'auradnaa haudhwa nabiyikum wasakaana bika'asi jaddikum min yadi Ali bn Aby Twalib Swalawati Allahi Alaikum. As'alu Allah an yuriina fiikum surura walfaraja wa an yajmaana waiyakum fii zukrati Jaddikum Muhammad(s.a.w.w) wa anlaa yaslubana maarifatakum inahu waliyu kadiru. Atakaraba Ila Allah bihubikum walbaraay'ti man aadaikum warasliim Ila Allah radhiya bihi khairi munkirin wala mustakbirin wa ala yakini maa ataa bihi Muhammadun wa bihi radhwin natlubu bidhaalika wajhaka yaa sayidi Allahumma waidhwaaka waddarul Akhira. Yaa Fatuma Shfaa ly fii jannati fainna laki inda Allah sha'anan min Sha'anin. Allahumma inni As'aluka an takhtima ly bisaadati fala taslubu minni maa anaa fihi wala haula wala kuwata ilaa billahi al-aliyyu al-adhwiimu. Alwahumma stajib lanaa watakabalahu bikaramika waizzatika wabitahmatika wa'aafiyatika. Waswalla Allahu ala Muhammad wa alihi ajmaina wasalama tasliiman ala yaa arhama ar'raahimiin. Wa aakhir da'awana Anilhamdulilah Rabbi al-alamiina.

MAREJEO (REFERENCES)

[1] Biharul Anwar Juzuu 99, uk 265, H.1.

[2] Biharul Anwar juzuu 99, uk 265, H.3.

[3] Biharul Anwar juzuu 99 uk. 267 H 5.

[4] Biharul Anwar juzuu 99 uk 267 H 6.

[5] Biharul Anwar juzuu 99 uk. 102 - 103, H 4.

MWISHO

YALIYOMO

UTENZI WA IMAM HUSEN SAFARI YA BIBI MAASUMA 1

SAFARI YA BIBI MAASUMA 1

JINA LA KITABU: MAISHA YA BIBI FATUMA MAASUMAH (A.S) 1

MTUNZI: GHULAM RIDHAA HAIDARY ABHARY 1

MTARJUMI: KHEIR ABOUKHEIR 1

WAENEZAJI: MUASSASATUL IMAM ALI (A.S.) 1

MWAKA WA CHAPA: 2002/1423 1

HATIMAYE MSAFARA WAINGIA MJI WA SAVEE 3

KIFO CHA BIBI MAASUMU 3

MAZISHI YAKE BIBI MAASUMU 4

KABURI TUKUFU LA BIBI FATUMA MAASUMU (A.S) 5

THAWABU ZINAZOPATIKANA KWA KUMZURU 5

MAREJEO (REFERENCES) 8

MWISHO 8