JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA28%

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA Mwandishi:
: HEMEDI LUBUMBA SELEMANI
Kundi: Vitabu mbali mbali

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA
  • Anza
  • Iliyopita
  • 11 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 16049 / Pakua: 4431
Kiwango Kiwango Kiwango
JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA

Mwandishi:
Swahili

1

2

3

5

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA

MADHARA YA KIELIMU NA KISIASA

WAJIBU WA KUJIKINGA DHIDI YA MADHARA YA KIELIMU

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Wahadharisheni watoto wenu na maghu- lati ili wasiwaharibu, kwani hakika maghulati ni viumbe wabaya mno kati ya viunbe vya Mwenyezi Mungu. Wanadharau utukufu wa Mwenyezi Mungu na wanadai uungu kwa waja wa Mwenyezi Mungu ."[411]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Harakisheni kuwafunza wanenu hadithi kabla murjiina hawajawatangulia kwao ."[412]

Tahadhari dhidi ya kuwafuata mbumbumbu: Mwenyezi Mungu amesema: "Wala usifuate usiyo na elimu nayo, hakika masikio na macho na moyo, hivyo vyote vitaulizwa ." (Surat Banii Israil: 36).

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Msiwe mabubusa, mnasema: 'Watu wakifanya wema nasi tunafanya, wakidhulumu nasi tunadhulumu. Lakini zipeni mamlaka nafsi zenu, watu wakifanya wema nanyi fanyeni wema, wakifanya ubaya basi nyinyi msidhulumu ." [413]

Kumayl bin Ziyad amesema: "Jemedari wa waumini Ali bin Abu Talib alinishika mkono akanitoa hadi jangwani, basi alipoligusa tu jangwa alivuta pumzi kidogo na kisha akasema:'Ewe Kumayl bin Ziyad! Hizi nyoyo ni vyombo na kilicho bora zaidi ni kile chenye kuzingatia. Basi hifadhi kutoka kwangu yale nikwambiayo: Watu ni wa aina tatu: Yupo alimu mtiifu kwa Mola, mwenye kujifunza katika njia ya uokovu. Na mawimbi wafuata upepo wenye kumfuata kila mpiga kelele, wanafuata kila upepo, hawajaangaziwa kwa nuru ya elimu na wala hawajakimbilia kwenye nguzo imara. "[414]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Msiwe mabubusa, mnasema: Mimi niko pamoja na watu nami ni kama mmoja kati ya watu ."[415]

Abu Hamza Thumali amesema: Abu Abdillah(a.s) aliniambia: 'Jiepushe na uraisi na jiepushe usiwe mfuata nyayo za watu." Nikamwambia: 'Mimi ni fidia kwako. Ama urais tunaujua, ama kufuata nyayo za watu ni kuwa theluthi ya niliyonayo ni kutokana na kufuata nyayo za watu.' Akaniambia:'Si kama unavyodhani, ni kuwa jiepushe kumpa mtu utawala bila kuwa na hoja, ukaja kumsadikisha kwa kila alisemalo ."[416]

Imam Al-Kadhim(a.s) alimwambia Fadhlu bin Yunus: "Fikisha kheri na sema kheri na wala usiwe bubusa." Nikamwambia: 'Bubusa ni nani?' akasema: 'Usiseme: Mimi ni kama mmoja miongoni mwa watu, kwani hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: 'Enyi watu! Hakika njia ni mbili: Njia ya kheri na njia ya shari. Hivyo njia ya shari isiwe ipendwayo kwenu kuliko njia ya kheri ." [417]

WAJIBU WA KUWAKHALIFU VIONGOZI WAOVU

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Enyi kundi la vijana mcheni Mwenyezi Mungu na wala msiwafuate viongozi, waacheni mpaka wawe wafuasi. Msiwafanye watu marafiki wa moyo mkamwacha [418] Mwenyezi Mungu. Hakika sisi wallahi ni bora kwenu kuliko wao.' Kisha akapiga mkono wake juu ya kifua chake ."[419]

MAAFA YA KITABIA NA KIMATENDO

KUTOTIMIZA HAKI ZA WAZAZI WAWILI

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Lau kama Mwenyezi Mungu angefahamu kilicho chini zaidi ya (kusema kumwambia mzazi) Akh! katika kutotimiza haki za wazazi wawili basi angekiharamisha. Mwenye kushindwa kutimiza haki za wazazi afanye afanyavyo hatoingia Peponi ." [420]

Imam Al-Baqir(a.s) amesema: "Baba yangu alimwona mwanaume akiwa na mwanaye akitembea kwa miguu huku mtoto akiwa kaegemea kwenye dhiraa ya baba. Akasema: Basi baba yangu hakumsemesha kwa ajili ya kuchukizwa naye mpaka anaiacha dunia ."[421]

Imam Al-Baqir(a.s) amesema: "Baba mbaya ni yule ambaye wema unam- peleka kwenye uvukaji mipaka. Na mtoto mbaya ni yule ambaye kupuuzia humpelekea kutotimiza haki za wazazi ."[422]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Kiwango cha chini kabisa cha kutotimiza haki za wazazi ni neno Akh. Na lau kama Mwenyezi Mungu angejua kitu chepesi zaidi ya hilo basi angekikataza ."[423]

Imam Al-Askar(a.s) amesema: "Ujasiri wa mtoto dhidi ya baba yake utotoni mwake hupelekea kumnyima haki zake ukubwani mwake ."[424]

TABIA MBAYA

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Tabia mbaya ni dham- bi isiyoghufiriwa ." [425]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alipoambiwa: "Fulani anafunga mchana na kuswali usiku lakini yeye ana tabia mbaya anamuudhi jirani yake kwa ulimi wake.'Akasema: 'Hana kheri, naye ni miongoni mwa watu wa motoni ." [426]

Imam Ali(a.s) amesema: "Ambaye tabia zake zitakuwa mbaya basi riziki yake itabana ."[427]

Imam Ali(a.s) amesema: "Ambaye tabia yake itakuwa mbaya atatengwa na rafiki ."[428]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Ambaye tabia yake itakuwa mbaya basi ameiadhibu nafsi yake ."[429]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Luqman(a.s) alisema:'Ewe mwanangu mpendwa! Jiepushe na ghadhabu, tabia mbaya na uchache wa subira, haku- na mtu anayekuwa sawa juu ya sifa hizi. Ilazimishe nafsi yako ridhaa kati- ka mambo yako, na ivumilishe nafsi yako katika matumizi ya jamaa na wafanyie watu wote tabia njema ."[430]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Ambaye ulimi wake utaogopwa na watu basi huyo ni mtu wa motoni ."[431]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Maafa ya uzuri ni mawazo hewa (yatokanayo na kiburi) ." [432]

KUJIONA/ KUJIKWEZA

Imam Ali(a.s) amesema: "Lililo baya mno kati ya mambo ni mtu kujikweza mwenyewe ."[433]

Imam Ali(a.s) amesema: "Atakayejiona adhimu ndani ya nafsi yake basi mbele ya Mwenyezi Mungu atakuwa duni ."[434]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Mcheni Mwenyezi Mungu wala msihusudiane nyinyi kwa nyinyi, hakika miongoni mwa sheria za Isa bin Maryam ilikuwa ni kutembea mjini, ndipo siku moja akatoka katika

matembezi yake akiwa na mwanaume mbilikimo miongoni mwa sahaba zake, naye alikuwa ni mwandama mno wa Isa bin Maryam(a.s) .

Isa(a.s) alipofika baharini alisema: 'Bismillahi' kwa usahihi akiwa na yakini nayo, akatembea juu ya maji. Basi mtu yule mbilikimo alipomtazama Isa(a.s) alimuiga kwa usahihi akiwa na yakini nayo, naye akapita juu ya maji na kuungana na Isa(a.s) . Hilo likamfanya ajikweze, akasema: 'Huyu Isa(a.s) Ruhullah anatembea juu ya maji nami pia natembea juu ya maji, basi ana ubora gani juu yangu.' Hapo hapo akazamishwa ndani ya maji na ndipo akaanza kuomba msaada toka kwa Isa(a.s) , akamshika mkono na kumwopoa toka ndani ya maji, kisha akamwambia: 'Ulisema nini ewe mbilikimo?' Akasema: 'Nilisema: Anatembea juu ya maji nami natembea juu ya maji, basi hilo likanifanya nijione.' Isa(a.s) akamwambia: 'Umeiweka nafsi yako sehemu isiyokuwa ile aliyokuweka Mwenyezi Mungu, ndipo Mwenyezi Mungu akakuchukia kwa uliyosema, hivyo tubu kwa Mwenyezi Mungu kutokana na uliyose- ma.' Basi mbilikimo yule akatubu na akarejea kwenye daraja lake ambalo Mwenyezi Mungu alimweka. Mcheni Mwenyezi Mungu msihusudiane nyinyi kwa nyinyi."[435]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Jiepusheni na kiburi, kwani hakika kiburi huwa kwa mtu hata kama ana joho ." [436]

PUPA

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Hakika mwanaadamu ni mwenye pupa juu ya yale aliyonyimwa ." [437]

Imam Ali(a.s) amesema: "Mwenye pupa ni fakiri hata kama ataimiliki dunia kwa mikono yake ."[438]

HUSUDA

Imam Ali(a.s) amesema: "Husuda ni matokeo ya kuchoka ."[439]

Imam Ali(a.s) amesema: "Husuda huzuia raha ."[440]

Imam Ali(a.s) amesema: "Husuda haileti ila madhara na hasira. Hudhoofisha moyo wako na kuuguza mwili wako. Na shari ambayo inayohisiwa na moyo wa mtu ni husuda ."[441]

Imam Ali(a.s) amesema: "Hasidi milele ni mgonjwa (alilu) ."[442]

Imam Ali(a.s) amesema: "Hasidi daima ni mgonjwa hata kama ni mwenye mwili wenye siha ."[443]

Imam Ali(a.s) amesema: "Hasidi hafanikiwi ."[444]

Imam Ali(a.s) amesema: "La ajabu ni mghafiliko wa mahasidi kunako usalama wa miili ."[445]

Imam Ali(a.s) amesema: "Hasidi hudhihirisha mapenzi yake kwenye kauli zake na huficha chuki yake kwenye vitendo vyake. Ana jina la rafiki na sifa ya adui ."[446]

Imam Ali(a.s) amesema: "Matunda ya husuda ni mahangaiko ya dunia na akhera. "[447]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Luqman(a.s) alimwambia mwanae:'Hasidi ana alama tatu: Anasengenya anapokuwa hayupo. Huonesha mapenzi ya uongo anaposhuhudia na hufurahia msiba ."[448]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Hasidi ni mwenye kujidhuru yeye mwenyewe kabla hajamdhuru mhusudiwa, kama ambavyo Ibilisi kwa husuda yake alirithisha laana ndani ya nafsi yake, na akarithisha kwa Adam (a.s) kujielekeza (kwa Mola wake) ."[449]

CHUKI YA NDANI (HIKDI)

Imam Ali(a.s) amesema: "Hikdi huumiza nafsi na huongeza maumivu ya moyo ."[450]

Imam Ali(a.s) amesema: "Atakayetoa chuki basi moyo wake na akili yake hustarehe .''[451]

HASIRA

Imam Ali(a.s) amesema: "Hasira ni sehemu ya uwendawazimu kwa sababu mwenye nayo hujuta, na ikiwa hajuti basi uwendawazimu wake huendelea ."[452]

UBISHI

Imam Ali(a.s) amesema: "Ubishi hunyakua rai ."[453]

Imam Ali(a.s) amesema: "Ubishi huharibu rai ."[454]

Imam Ali(a.s) amesema: "Matunda ya ubishi ni kuangamia ."[455]

Imam Ali(a.s) amesema: "Mbishi hukumbana na balaa. "[456]

Imam Zainul-Abidiin(a.s) amesema: "Ubishi huambatana na ujinga, na ushabiki huletwa na msiba, na sababu ya heshima ni unyenyekevu. "[457]

UVIVU

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alimwambia Ali(a.s) : "Jiepushe na sifa mbili: Hasira na uvivu, kwani hakika wewe ukikasirika hutosubiri juu ya haki, na ukifanya uvivu hutotekeleza haki ."[458]

Imam Al-Baqir(a.s) amesema: "Hakika mimi nachukia sana mtu kufanya uvivu kunako jambo la dunia yake. Na atakayefanya uvivu juu ya jambo la dunia yake basi ni mvivu kunako jambo la akhera yake ."[459]

Imam Ali(a.s) amesema: "Hakika mambo yalipochanganyikana, uvivu na kushindwa vilijichanganya pamoja na hatimaye vikazaa ufakiri ."[460]

Imam Ali(a.s) amesema katika sifa za muumini: "Utamuona uvivu wake uko mbali; na uchangamfu wake ni wa daima ."[461]

Imam Zainul-Abidiin(a.s) amesema katika dua zake: "Ewe Mola wetu Mlezi tupe neema ya uchangamfu na utukinge na kufeli na uvivu ."[462]

KUVUKA MIPAKA KATIKA IBADA

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Jiepusheni kuifanya nzito dini, kwani hakika Mwenyezi Mungu ameifanya nyepesi, ichukueni kadri muwezavyo, kwani hakika Mwenyezi Mungu hupenda maadamu tu ni katika amali njema hata kama ni ndogo. " [463]

Imam Ali(a.s) amesema: "Atakayeifanya nzito dini basi hatafika kwenye haki ."[464]

Imam Ali(a.s) amesema: "Hutomuona mjinga ila ni mwenye kupuuza au mwenye kupituka ."[465]

KUJIPAMBA KULIKOKEMEWA

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Si miongoni mwetu wale wanawake wenye kujishabihisha na wanaume. Na wala wanaume wenye kujishabihisha na wanawake ." [466]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Makundi ya aina mbili ni ya motoni na sitoyaona: Kaumu wenye mijeledi kama mikia ya ng'ombe wanaitumia kuwapiga watu. Na wanawake wenye kujiachia wenye kubaki uchi, wenye kushawishi wenye kuringa.hawatoingia peponi na wala hawatoipata harufu yake ."[467]

Imam Ali(a.s) amesema: "Mwenye kushabihiana na kaumu hukaribia kuwa miongoni mwao ."[468]

KUENDEKEZA KUFIKIRIA STAREHE

Imam Ali(a.s) amesema: "Ambaye fikara zake zitazama kwenye starehe basi zitamshinda ."[469]

Imam Ali(a.s) amesema: "Ambaye fikara zake zitazama kwenye maasi yatamwita ayaendee ."[470]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Wanafunzi wa Isa(a.s) walijikusanya kwake na kumwambia: 'Ewe mwalimu wa kheri tuongoze.' Akawaambia: 'Hakika Musa Kalimullah aliwaamuru msiape kwa Mwenyezi Mungu ilihali ni waongo. Na mimi nawaamuru kuwa msiape kwa Mwenyezi Mungu ilihali ni waongo na si wakweli.' Wakasema: 'Ewe Ruhullah tuzidishie.' Akasema:'Musa Nabii wa Mwenyezi Mungu aliwaamuru msizini nami nawaamuru msizisimulie nafsi zenu zinaa achia mbali kuitekeleza. Kwani hakika mwenye kuisimulia nafsi yake zinaa anakuwa kama mtu aliyewasha moto ndani ya nyumba iliyorembwa, na hatimaye moshi ukaharibu marembo hata kama nyumba haikuungua ."[471]

KUNYWA POMBE

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Pombe ni mama wa maovu na maasi ." [472]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Pombe ni mama wa mabaya. " [473]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Shari yote imekusany- wa ndani ya nyumba, na kunywa pombe kukafanywa ndio ufunguo wake ." [474]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Atakaelala amelewa basi huwa amelala akiwa biharusi wa shetani ." [475]

Imam Ali(a.s) amesema: "Mwenyezi Mungu alifaradhisha kuacha pombe ili kuilinda akili ."[476]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Hakika maasi akiyatenda mja kwa siri hayamdhuru ila mtendaji wake. Na akiyatenda waziwazi bila kukemewa hudhuru jamii nzima ." [477]

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA

SEHEMU YA NNE

HAKI ZA VIJANA

HAKI ZA VIJANA JUU YA WAZAZI WAO

UMUHIMU WA HAKI ZA MTOTO

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Mzazi hupatwa kutokana na haki za mtoto wake yale ambayo humpata mtoto kutokana na haki za mzazi wake ." [478]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Wazazi hupatwa kutokana na kutomtimizia haki mtoto wao yale ambayo humpata mtoto wao kutokana na kutowatimizia haki zao ." [479]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Wazazi hupatwa kutokana na kutomtimizia haki mtoto wao iwapo ni mwema yale ambayo humpata mtoto ." [480]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Mtoto ni bwana miaka saba, ni mtumwa miaka saba na ni waziri miaka saba ." [481]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Mwache mwanao acheze miaka saba, na huadabishwa miaka saba na mfuatilie miaka saba ."[482]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Ambaye mwanae atafikia umri wa kuoa na akawa ana mali anayoweza kumuozesha lakini hakumuozesha kisha (mtoto) akizua la kuzua madhambi ni juu yake (mzazi) ." [483]

UADILIFU

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Fanyeni uadilifu baina ya wanenu. Fanyeni uadilifu baina ya wanenu ." [484]

Nu'man Bin Bashir amesema: "Baba yangu alinipa kipawa basi Amrat bint Rawaha akasema: 'Siridhii mpaka umshuhudishe Mtume wa Mwenyezi Mungu.' Akamjia Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) na kumwambia: 'Hakika mimi nimempa mwanangu toka kwa Amrat binti Rawaha kipawa, akaniamuru (Amrat) nikushuhudishe wewe ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.' Akamuuliza: 'Je umewapa wanao wengine kama hivyo?' akasema 'La.' Akamwambia: 'Mcheni Mwenyezi Mungu na fanyeni uadilifu baina ya wanenu.' Anasema: Basi akarejea na kumnyang'anya kipawa kile."[485]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Uadilifu ni mtamu kuliko maji ayanywayo mwenye kiu. Ni upana ulioje wa uadilifu pindi mtu akifanyiwa hata kama ni mdogo ."[486]

DUA

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Dua njema ya mzazi kwa mwanae ni sawa na dua njema ya Nabii kwa umma wake ." [487]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Dua njema ya mzazi kwa mwanae ni sawa na maji kwenye mmea kwa manufaa yake ." [488]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Mwenyezi Mungu humrehemu anayemsaidia mwanae kumfanyia mema, nako ni kumsamehe makosa yake na kumuombea mema katika yale yaliyopo kati yake na Mwenyezi Mungu ." [489]

KUACHA KUMUOMBEA MABAYA

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Msiwaombee mabaya wanenu ikaja kuwa mwafaka kwa jibu kutoka kwa Mwenyezi Mungu ." [490]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Msijiombee mabaya na wala msiwaombee mabaya wanenu, wala msiiombee mabaya mali yenu, msifanye iwe mwafaka na saa ambayo humo huombwa kipawa kutoka kwa Mwenyezi Mungu na hatimaye akawajibu ." [491]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Msitamani kuhiliki kwa vijana wenu hata kama wana madhara, kwani hakika wao pamoja na hivyo walivyo bado wana vipindi (vya manufaa): Ima watubu na Mwenyezi Mungu awakubalie toba yao, na ima madhara yawapate. Na ima adui aje wamuue, ima janga la moto walizime, na ima maji wayazuie ." [492]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Mtu yeyote atakayemuombea mwanae mabaya basi Mwenyezi Mungu humrithisha ufakiri (mtu huyo) ."[493]

Alama ya kuvuka mipaka katika kumlaumu: Imam Ali(a.s) amesema: "Utakapomkemea kijana basi mwachie nafasi katika kosa lake ili kumkemea kusimpelekee kuwa na jeuri ."[494]

Imam Ali(a.s) amesema: "Kuzidisha kukemea huwasha moto wa ubishi (upinzani) ."[495]

Imam Ali(a.s) amesema: "Unapokemea kemea kwa wastani ."[496]

HAKI ZA KIJANA KIJAMII

KUWAKIRIMU

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Wapeni nafasi vijana katika mabaraza, waelewesheni hadithi, kwani hakika wao ni warithi na watu wa hadithi ." [497]

Sahlu bin Sa'ad amesema: "Mtume(s.a.w.w) aliletewa bilauri akanywa kilichomo, kuliani mwake kulikuwa na kijana mdogo kuliko wote waliokuwepo, na kushotoni mwake(s.a.w.w) kulikuwa na wazee, basi akamwambia: 'Ewe kijana unaniridhia niwape wazee kilichomo?' akasema:'Siwezi kumrithisha yeyote fadhila yangu kutoka kwako ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.' Basi akawa amempa ." [498]

Kuwaomba ushauri

Imam Ali(a.s) amesema: "Ukihitaji ushauri wa jambo lililokutokea basi lidhihirishe kwa kuwaanza vijana kwani hakika wao ni moja ya akili na wepesi wa kutafakari, kisha baada ya hapo lirejeshe kwenye rai ya wazee na vikongwe ili walipitie tena, na wafanye uteuzi wa maamuzi mazuri, kwani hakika uzoefu wao ni mwingi ."[499]

Kutilia umuhimu mahitaji yao maalumu

Ima Al-Baqir(a.s) amesema: "Hakika Ali(a.s) aliwaendea mabazazi na kumwambia aliye mtu mzima: 'Niuzie nguo mbili.' Mwanaume yule akasema: 'Ewe Jemedari wa waumini, kwangu kuna haja yako.' Alipojua kusudio lake akamwacha na akaenda kwa kijana, akachukua nguo mbili, moja kwa dirhamu tatu na nyingine kwa dirhamu mbili, akasema: 'Ewe Qanbar chukua ya dirhamu tatu.' Akasema:'Wewe ndiye aula kwayo kwani unapanda mimbari na kuhutubia watu.' Akamjibu: 'Nawe ni kijana na bado una mvuto wa ujana, nami naona haya mbele ya Mola wangu Mlezi kuwa mbora juu yako ."[500]

Na mwisho wa dua yetu ni kumshukuru Allah Bwana Mlezi wa walimwengu.

SHARTI YA KUCHAPA

Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.

MWISHO WA KITABU

YALIYOMO

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA 1

UDONDOZI KUTOKA KITABU: JAWAAHIRU AL-HIKMAH LI 'SH-SHABAAB 1

KIMEANDIKWA NA: MUHAMMAD REYSHAHRI 1

KIMETARJUMIWA: HEMEDI LUBUMBA SELEMANI 1

NENO LA MCHAPISHAJI 1

DIBAJI 2

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA 4

SEHEMU YA KWANZA 4

NAFASI YA KIPINDI CHA UJANA KATIKA USTAWI 4

1- KIPINDI CHA USTAWI WA MAISHA 4

KUNUFAIKA NA FURSA YA UJANA 4

HAZINA YA SIKU 6

JUHUDI ZA DHATI KATIKA NJIA YA MAENDELEO 6

2- USTAWI KATIKA KUJIJENGA 7

NAFASI YA VIJANA KATIKA KUJIELIMISHA 8

MAFUNZO YA KIROHO 9

MANABII(A.S) WALITUMWA WAKIWA VIJANA 9

3 - NAFASI YA VIJANA KATIKA SERIKALI YA 10

BALOZI WA KWANZA WA MTUME (s.a.w.w) NI KIJANA 10

GAVANA WA KWANZA WA MAKKA NI KIJANA WA MIAKA ISHIRINI NA MOJA 11

NAFASI YA VIJANA KATIKA SERIKALI YA IMAM WA ZAMA ZETU 12

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA 13

SEHEMU YA PILI 13

SABABU ZINAZOPELEKEA USTAWI WA VIJANA 13

1- MAARIFA 13

KUJIELIMISHA 13

KUJITAMBUA 13

KUIJUA QUR'ANI TUKUFU 14

KUJIFUNZA DINI 15

UMUHIMU WA UDADISI 16

2 - AZMA 17

KUJITUMA 17

MALENGO YA JUU 18

KUJIHESHIMU 18

MSIMAMO 19

KUMTAWAKALI MWENYEZI MUNGU 19

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA 20

3 - UHUSIANO NA MWENYEZI MUNGU 20

THAMANI YA IBADA KATIKA KIPINDI CHA UJANA 20

BARAKA ZA IBADA YA UJANANI 21

MAANA YA IBADA 21

WASTANI KATIKA IBADA 22

4 - RAFIKI MWEMA 22

NAFASI YA RAFIKI MAISHANI 22

KUMJARIBU RAFIKI 22

AINA ZA MARAFIKI 23

MARAFIKI BORA 23

HAKI YA MWENZI WAKO 25

5 - MAHITAJI YA HALALI NA NGUVU ZA MWILI 25

NGUVU ZA MWILI ZASIFIWA 25

SABABU ZA MVUTO 26

BURUDANI 26

MATEMBEZI 27

MIZAHA 27

KUOGELEA NA KUTUPA MSHALE 28

MIELEKA 29

MASHINDANO 29

6 - THAMANI YA TABIA NJEMA NA MATENDO MEMA 30

KUACHA MAASI 30

TOBA 31

NIDHAMU 34

KUHESHIMU HAKI ZA WAZAZI WAWILI 34

KAZI 35

KUWAHUDUMIA WATU 36

UAMINIFU 37

KUJIPAMBA 38

MAADILI MEMA 39

UTAWA 40

KUANGUSHA MACHO 41

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA 43

UDONDOZI KUTOKA KITABU: JAWAAHIRU AL-HIKMAH LI 'SH-SHABAAB 43

3 - HIJABU 43

NDOA 44

A: MKAZO WA KUOA UJANANI 44

B: MUME MARIDHAWA 44

C: MKE MARIDHAWA 44

D: KUOA AKRABA 45

HAYA 45

HAYA 46

UNYENYEKEVU 46

MTAZAMO WA MBALI 46

UHURU 47

KUKUBALI UDHURU 47

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA 49

3 - SEHEMU YA TATU 49

VIZUIZI VINAVYOZUWIA USTAWI WA VIJANA 49

KUTOKUJISHUGHULISHA KWAKEMEWA 49

MADHARA YA KUTOJISHUGHULISHA 50

ULEVI 50

KILA KILEVI KIMEHARAMISHWA 50

TAHADHARI DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA 51

RAFIKI MBAYA 51

MADHARA YA RAFIKI MBAYA 51

ULEVI WA UJANA 53

MATAMANIO YA KIJINSIA 53

MTEGO WA SHETANI 53

MALIPO YA UTAWA WA JINSIA 56

MALIPO YA MWENYE ASHKI ALIYE MTAWA 57

MITEGO YA SHETANI 57

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA 59

MADHARA YA KIELIMU NA KISIASA 59

WAJIBU WA KUJIKINGA DHIDI YA MADHARA YA KIELIMU 59

WAJIBU WA KUWAKHALIFU VIONGOZI WAOVU 60

MAAFA YA KITABIA NA KIMATENDO 60

KUTOTIMIZA HAKI ZA WAZAZI WAWILI 60

TABIA MBAYA 60

KUJIONA/ KUJIKWEZA 61

PUPA 62

HUSUDA 62

CHUKI YA NDANI (HIKDI) 63

HASIRA 63

UBISHI 63

UVIVU 63

KUVUKA MIPAKA KATIKA IBADA 64

KUJIPAMBA KULIKOKEMEWA 64

KUENDEKEZA KUFIKIRIA STAREHE 64

KUNYWA POMBE 65

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA 66

SEHEMU YA NNE 66

HAKI ZA VIJANA 66

UMUHIMU WA HAKI ZA MTOTO 66

UADILIFU 66

DUA 67

KUACHA KUMUOMBEA MABAYA 67

HAKI ZA KIJANA KIJAMII 68

KUWAKIRIMU 68

SHARTI YA KUCHAPA 68

MWISHO WA KITABU 68

YALIYOMO 69

4

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA

3 - SEHEMU YA TATU

VIZUIZI VINAVYOZUWIA USTAWI WA VIJANA

KUTOJISHUGHULISHA

KUTOKUJISHUGHULISHA KWAKEMEWA

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu anamchukia mwenye siha asiyejishughulisha, hayupo katika kujishughulisha na dunia wala katika kujishughulisha na akhera ." [336] 335

Imam Ali(a.s) amesema: "Ikiwa kujishughulisha ni taabu basi kuendelea na kutojishughulisha ni uharibifu ."[337]

Imam Ali(a.s) amesema: "Moyo usiyojishughulisha hutafuta mabaya. Na mkono usiojishughulisha hupelekea kwenye ubaya ."[338]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Atakayefanya uvivu kwenye tohara yake na Swala yake basi hana kheri na jamabo la akhera yake. Na atakayefanya uvivu kwenye jambo litakalotengeneza maisha yake basi hana kheri na jambo la dunia yake ."[339]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Mwenyezi Mungu anachukia kuendekeza kulala na kuendekeza kukaa bila kujishughulisha ."[340]

Imepokewa kutoka kwa Umar bin Yazid amesema: "Nilimwambia Abu Abdillah(a.s) : Mtu anayesema: 'Nitakaa nyumbani kwangu, nitaswali, nitafunga na kumwabudu Mola wangu Mlezi. Ama riziki yangu itaniijia yenyewe.' Abu Abdillah(a.s) akasema:'Huyu ni mmoja kati ya watu watatu ambao dua zao hazijibiwi ."[341]

Asbatu bin Salim amesema: "Niliingia kwa Abu Abdillah(a.s) akatuuliza kuhusu Umar bin Muslim amefanya nini? Nikasema: Ni mwema lakini yeye ameacha biashara. Abu Abdillah(a.s) akasema: 'Kazi ya shetani.' Mara tatu. Kisha akasema:'Hivi hajui kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) alinunua bidhaa kutoka Shamu ndipo akajipatia riziki ambayo alilipia deni lake na kuwagawia karaba zake ."[342]

Zararah amesema: "Mtu mmoja alimjia Abu Abdillah(a.s) na kumwambia: 'Mimi siwezi kufanya kazi vizuri kwa mkono wangu, na wala siwezi kufanya vizuri biashara, nami ni muhitaji mwenye haja.' Akamwambia:'Fanya kazi, beba juu ya kichwa chako, na usiwahitajie watu ."[343]

Imepokewa kutoka kwa Al-Mufadhal bin Umar amesema: "Tafuteni msaada kupitia sehemu ya dunia kwa ajili ya akhera, kwani hakika mimi nimemsikia Abu Abdillah(a.s) akisema:'Tafuteni msaaada kupitia sehe- mu ya hii ili mpate hii. Na wala msiwe wategemezi kwa watu ."[344]

Imam Al-Kadhim(a.s) amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anamchukia mja mwenye kulalalala asiyejishughulisha ."[345]

MADHARA YA KUTOJISHUGHULISHA

Ibnu Abbas amesema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa amuonapo mtu na akavutiwa naye husema: 'Je ana kazi?' Wakimwambia hana, basi husema: 'Hana nafasi tena kwangu.' Huambiwa: Vipi hilo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Husema:'Kwa sababu muumini akiwa hana kazi ataishi kwa dini yake ."[346]

Imam Ali(a.s) amesema: "Ujinga hutokana na kutojishughulisha ."[347]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Huko Madina kulikuwa na mtu asiyejishughulisha ambaye watu walikuwa wakimcheka. Akasema: 'Huyu mtu -Yaani Ali bin Husein - amenishinda kumchekesha. Basi akapita Ali(a.s) akiwa na vijana wake wawili, ndipo mtu yule akaja na kumnyang'anya joho lake toka shingoni, kisha akaondoka na wala Ali(a.s) hakumgeukia. Wakamwendea na kumnyanganya joho, wakalileta kwake na kumtupia. Umam(a.s) akawauliza ni nani huyu? Wakamwambia: Huyu ni mwanaume asiyejishughulisha huwa anawachekesha watu wa Madina. Basi akasema: 'Mwambieni:Hakika Mwenyezi Mungu ana siku ambayo wasiyojishughulisha watapa hasara humo ."[348]

Luqman(a.s) alisema: "Wenye hesabu kali siku ya Kiyama ni aliyetoshelezwa asiyejishughulisha, kwani ikiwa kujishughulisha ni taabu basi kutokujishughulisha ni uharibifu ."[349]

ULEVI

KILA KILEVI KIMEHARAMISHWA

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Fahamuni kila kilevi ni haramu, na kila kilegezacho ni haramu. Kila kileweshacho kwa wingi ni haramu hata kwa uchache. Na kila kichanganyacho akili ni haramu ." [350]

Ummnu Salamah amesema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) alikataza kila kilevi na kila kilegezacho nguvu ."[351]

Imam Al-Kadhim(a.s) amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu hajakataza pombe kwa ajili ya jina lake, lakini aliikataza kutokana na matokeo yake. Basi kila ambacho matokeo yake ni sawa na pombe nacho ni haramu ."[352]

TAHADHARI DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Umma wangu utafikiwa na zama watakuwa wanakula kitu jina lake ni Banji [353] .Mimi najitenga nao na wao wako mbali na mimi ."[354]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Mtoleeni salamu Myahudi na Mnasara, lakini msimtolee salamu mlaji wa Banji ." [355]

(Nasema: Huenda kwa sasa ni aina moja ya madawa ya kuilevya ya kisasa. Na huenda ikawa ni jamii fulani ya milungi, japo maumbile yanatofautiana, kwani hata hii huliwa kama iliwavyo milungi.) - Mfasiri.

RAFIKI MBAYA

MADHARA YA RAFIKI MBAYA

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Mfano wa mwenza aliye mwema ni mfano wa muuza manukato, ikiwa hatakupa manukato yake basi harufu yake itakupata. Na mfano wa mwenza muovu ni mfano wa muhunzi, ikiwa hatakuunguza nguo yako basi harufu yake itakusibu ." [356]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika mimi najikinga kwako na sahiba mwenye mghafala na rafiki mbaya ." [357]

Imam Ali(a.s) amesema: "Kuandamana na watu waovu kunaleta uovu, ni kama upepo upitapo kwenye harufu mbaya huleta harufu mbaya ."[358]

Musa(a.s) amesema: "Atakayejiepusha na rafiki mbaya ni kana kwamba ameifanyia kazi Taurati ."[359]

Luqman(a.s) alimwambia mwanawe: "Anayefanya urafiki na mtu mbaya basi hatosalimika ."[360]

Ali bin Asbati amepokea kutoka kwa Maimamu(a.s) kuwa: "Miongoni mwa mawaidha ya Mwenyezi Mungu kwa Isa (a.s) ni: Ewe Isa! Jua kuwa rafiki mbaya ananifanyia uadui, na rafiki mbaya ananipinga. Na jua ni nani unayefanya naye urafiki. Na jichagulie ndugu miongoni mwa Waumini ."[361]

Imepokewa kutoka kwa Sufyan At-Thawriy amesema: "Nilikutana na mkweli mwana wa mkweli Jafar bin Muhammad(a.s) , nikamwambia: Ewe mwana wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, naomba uniusie. Akaniambia: 'Ewe Sufyan! Mzazi wangu aliniamuru mambo matatu na akanikataza mambo matatu, na miongoni mwa hayo aliyoniambia ni:'Ewe mwanangu mpendwa! Atakayeandamana na rafiki mbaya hatosalimika ."[362]

Alama za rafiki mbaya: Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya mwisho basi asifanye undugu na kafiri na wala asiandamane na muovu. Atakayefanya undugu na kafiri au akaan- damana na muovu atakuwa kafiri au muovu ." [363]

Imam Ali(a.s) amesema: "Atakayekusitiri aibu yako na akakuaibisha uwapo haupo basi ni adui, jihadhari naye ."[364]

Imam Ali(a.s) amesema: "Jiepusheni na wale ambao nyoyo zenu zinawachukia ."[365]

Imam Ali(a.s) amesema: "Ambaye mapenzi yake si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu basi jihadhari naye. Kwani hakika mapenzi yake ni mabaya na usuhuba wake ni hatari ."[366]

Imam Ali(a.s) amesema: "Inafaa kwa anayetaka kuitengeneza nafsi yake na kuihifadhi dini yake ajiepushe kuandamana na watu wa dunia ."[367]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Tazama kila asiyekuwa na manufaa na wewe katika dini yako basi usiwe na mazoea naye, na wala usiwe na ragh- ba ya kusuhubiana naye, kwani hakika kila asiyekuwa katika njia ya Mwenyezi Mungu matokeo yake ni mabaya yenye kudhuru ."[368]

Adam(a.s) alimuusia mwanae Shi'ithi: "Nyoyo zenu zikikataa kitu basi jiepusheni nacho, kwani hakika mimi niliposogea kwenye mti ili nichume moyo wangu ulikataa, hivyo lau kama ningelijizuia kula basi yasingelinis- ibu yaliyonisibu ."[369]

Marafiki wabaya

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Msiandamane na waovu ." [370]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Msifanye urafiki na mlevi wa pombe, kwani kufanya naye urafiki huleta majuto ." [371]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Jizuieni kufanya urafiki na kila mwenye kheri ndogo, mwenye shari nyingi, khabithi wa nafsi. Anapokhofu hujikunyata na anapopata amani hufanya ujabari ." [372]

Imam Ali(a.s) amesema: "Aliye mbaya kati ya ndugu zako ni yule anayekuridhisha kwa batili ."[373]

Imam Ali(a.s) amesema: "Aliye mbaya kati ya ndugu zako ni anayekupaka mafuta ndani ya nafsi yako na kukuficha aibu zako ."[374]

Imam Ali(a.s) amesema: "Jiepushe kuwapenda maadui wa Mwenyezi Mungu, au kuonyesha mapenzi yako ya dhati kwa wasiokuwa mawalii wa Mwenyezi Mungu, kwani hakika atakayeipenda kaumu fulani atafufuliwa pamoja nao ."[375]

Imam Ali(a.s) amesema: "Mwenye kusuhubiana na watu wabaya ni sawa na alierakibu merkebu baharini ."[376]

Imam Jawad(a.s) amesema: "Jiepushe kusuhubiana na mtu muovu, kwani hakika yeye ni sawa na upanga wenye sumu, ukiutazama wavutia lakini athari zake ni mbaya ."[377]

ULEVI WA UJANA

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Ujana ni matawi ya uendawazimu ." [378]

Imam Ali(a.s) amesema: "Aina za ulevi ni nne: Ulevi wa ujana, ulevi wa mali, ulevu wa kulala na ulevi wa ufalme ."[379]

Imam Ali(a.s) amesema: "Inapasa kwa mwenye akili ajiepushe na ulevi wa mali, ulevi wa uwezo, ulevi wa elimu, ulevi wa sifa, na ulevi wa ujana,kwani hakika hayo yote yana riha mbaya inayoondoa akili na kupunguza unyenyekevu ."[380]

Imepokewa kuwa Imam Ali na Maimamu(a.s) walikuwa wakiomba ndani ya mwezi wa Shabani: "Ewe Mungu wangu nimemaliza umri wangu kwenye shari ya kukusahau Wewe. Na nimeumaliza ujana wangu katika ulevi wa kujitenga na Wewe. Ewe Mungu wangu ni siku nyingi sijaamka kwa ajili ya kukufanyia ujeuri, na kurakibu nikielekea njia ya ghadhabu Yako ."[381]

MATAMANIO YA KIJINSIA

MTEGO WA SHETANI

Mwenyezi Mungu amesema: "Waambie waumini wanaume wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, hili ni takaso kwao, bila shaka Mwenyezi Mungu anazo khabari za yale wanayoyafanya. Na waambie waumini wanawake wainamishe macho yao na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipokuwa unaodhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, na wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba za waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au watoto wa kaka zao, au watoto wa dada zao, au wanawake wenzao, au wale waliomilikiwa na mikono yao au wafuasi wanaume wasio na matamanio (kwa wanawake), au watoto ambao hawajajua siri za wanawake. Wala wasipige chini miguu yao ili yajulikane mapambo waliyoyaficha. Na tubieni nyote kwa Mwenyezi Mungu enyi wenye kuamini ili mpate kufaulu ." (Surat Nuur: 30 -31).

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Mtazamo wa kwanza ni bahati mbaya, wa pili ni makusudi na wa tatu huangamiza ." [382]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Ghadhabu ya Mwenyezi Mungu imeongezeka juu ya mwanamke mwenye mume aliejipodoa macho yake kwa ajili ya asiyekuwa mumewe au asiyekuwa maharimu wake. Kwani hakika yeye iwapo atafanya hivyo Mwenyezi Mungu humporomoshea kila amali aliyoitenda ." [383]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Jiepusheni na mitazamo ya ziada, kwani yenyewe hupanda matamanio, na huzalisha mghafiliko ." [384]

Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Abbas amesema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu alimuweka Fadhlu bin Abbas nyuma ya kipando chake

siku ya kuchinja (Siku ya Iddi kubwa), na Fadhlu alikuwa ni mwanaume mwenye mvuto, basi Mtume akasimama mbele ya watu akiwapa fatwa, ndipo akatokea mwanamke kutoka Khath'am naye akawa anamuuliza maswali Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) , basi Fadhlu akawa akimkodolea macho mwanamke yule na akapendezwa na uzuri wake. Mtume akageuka ilihali Fadhlu akiwa bado anamkodolea macho, ndipo(s.a.w.w) akakishika kidevu cha Fadhlu na kuuondoa uso wake kwa mwanamke yule." [385]

Imam Ali(a.s) amesema: "Macho ni mitego ya shetani ."[386]

Imam Ali(a.s) amesema: "Jicho lionapo tamanio basi moyo hufumbia ambacho ni matokeo ya baadaye ."[387]

Imam Ali(a.s) amesema: "Ni dhambi ngapi hupatikana kwa kufumba na kufumbua? "[388]

Imam Al-Baqir(a.s) amesema: "Mwanamke malaya alitoka kuwafuata vijana wa kibani Israil na akawafanyia fitina. Baadhi yao wakasema: Mfanya ibada fulani angemuona angemfitini. Basi akasikia kauli zao, akasema: 'Wallahi siendi nyumbani kwangu mpaka nimfitini. Ndipo akamwendea usiku akamgongea mlango, akasema: 'Nimekimbilia kwako.' Akamkatalia. Akasema: 'Baadhi ya vijana wa kibani Israil wamenitamani wao wenyewe hivyo niingize kwako la sivyo watanikuta hapa na kunifedhehesha.' Basi aliposikia kauli yake hiyo akamfungulia mlango. Alipoingia akavua nguo zake, basi alipoona uzuri wake na umbile lake akamtamani, na hatimaye akaweka mkono wake juu yake, kisha nafsi yake ikarejea, wakati huo alikuwa amewasha moto ambao ametenga chungu, basi akaweka mkono wake juu ya moto. Mwanamke akasema: 'Unafanya nini?' Akasema: "Nauunguza kwa sababu wenyewe umefanya kitendo." Basi mwanamke akatoka akaliendea kundi la kibani Israil, akawaambia: 'Muokoeni fulani ameweka mkono wake juu ya moto.' Basi wakamwen- dea wakamkuta mkono wake umeshaungua ."[389]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Mtazamo ni mshale miongoni mwa mishale ya Ibilisi wenye sumu, ni mitizamo mingapi ya muda mfupi imeleta hasara ya muda mrefu ."[390]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akiwasalimu wanawake na wanamjibu. Na jemedari wa waumini alikuwa akiwasalimu wanawake na alikuwa hapendi kuwasalimu mabinti miongoni mwao, na akisema: Nahofia sauti yake isinivutie nikaingiwa na mengi kuliko malipo niyatafutayo ."[391]

Masihi(a.s) amesema: "Usiwe na macho makali ya kukodolea kisicho cha kwako, kwani utupu wako hautazini madamu macho yako umeyahifadhi. Ukiweza kutoitazama nguo ya mwanamke ambaye si halali kwako fanya hivyo ."[392]

Masihi aliwaambia wanafunzi wake: "Jiepusheni kuwatazama wanawake ajnabiya (asiye maharim wako), kwani kwenyewe ni kupanda matamanio na ni miche ya ufuska ."[393]

Imam Ali(a.s) amesema: "Ashki huenda ikapatikana kwa sekunde chache ."[394]

Imam As-Sadiq(a.s) alipoulizwa kuhusu ashki alisema: "Nyoyo zilizojie- pusha na utajo wa Mwenyezi Mungu basi Mwenyezi Mungu akazionjesha mapenzi ya kumpenda asiyekuwa Yeye ."[395]

Maangamio ya wafuata matamanio:

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Ambaye hima yake kubwa ni kupata matamanio basi moyo wake hunyang'anywa utamu wa imani ." [396]

Imam Ali(a.s) amesema: "Ni mara ngapi starehe za muda mfupi hurithisha huzuni ya muda mrefu? "[397]

Imam Ali(a.s) amesema: "Jiepusheni matamanio yasizishinde nyoyo zenu, kwani hakika mwanzo wake ni nguvu na mwisho wake ni maangamizi ."[398]

Imam Ali(a.s) amesema: "Mwanzo wa matamanio ni burudani na mwisho wake ni karaha ."[399]

Madhara ya kujichanganya na wasiokuwa maharimu: Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho halali sehemu ambayo mwanamke asiyekuwa maharimu wake anaisikia nafsi yake ." [400]

Imam Al-Baqir(a.s) amesema: "Nuh (a.s) alipomuomba Mola wake Mlezi kuwaombea kaumu yake, Ibilisi aliyelaaniwa na Mwenyezi Mungu alimjia na kumwambia: 'Ewe Nuh! Nikumbuke sehemu tatu, sehemu niwapo karibu mno na mja na awapo moja ya sehemu hizo: Nikumbuke unapoghadhibika. Nikumbuke uhukumupo kati ya watu wawili. Na nikumbuke uwapo pamoja na mwanamke faraghani mkiwa hamna yeyote pamoja nanyi ."[401]

Muhammad Tayar amesema: "Niliingia Madina na nikatafuta nyumba nikodishe, basi nikaingia nyumba ambayo ndani yake mna nyumba mbili, kati yake kuna mlango na humo mna mwanamke, akasema: 'Unakodi nyumba hii?' Nikasema: Kati yake kuna mlango nami ni kijana. Akasema: 'Mimi nitafunga mlango kati yangu na wewe.' Basi nikahamishia mizigo yangu humo na nikamwambia: Funga mlango. Akaniambia: 'Uache upepo unaingia kwangu kupitia hapo.' Nikamwambia: Hapana, mimi ni kijana na wewe ni binti, mimi naufunga. Akasema: 'Kaa wewe nyumbani kwako mimi sikuijii na wala sikukaribii.' Basi akakataa kufunga mlango, ndipo nikamwendea Abu Abdillah(a.s) nikamuuliza kuhusu hilo. Akasema:'Hama humo, kwani hakika mwanamke na mwanaume wanapokuwa faraghani ndani ya nyumba moja shetani huwa wa tatu wao ."[402]

MALIPO YA UTAWA WA JINSIA

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Atakayekuwa na uwezo juu ya kitendo cha haramu juu ya mwanamke au kijakazi lakini akamwacha kwa ajili ya kumuogopa Mwenyezi Mungu basi Mwenyezi Mungu ataharamisha moto juu yake na Mwenyezi Mungu Mtukufu atam- pa amani dhidi ya mshituko mkubwa (Kiyama) ." [403]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Atakayetokewa na ufuska au matamanio kisha akajiepusha kwa ajili ya kumuogopa Mwenyezi Mungu basi Mwenyezi Mungu atamuharamishia moto na atampa amani dhidi ya mshituko mkubwa na atamtimizia alichomwahidi ndani ya Kitabu chake katika kauli yake: 'Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake atapata Bustani mbili ." [404]

Imam Zainul-Abidina(a.s) amesema: "Mwanaume mmoja alirakibu baharini akiwa na mkewe basi jahazi likawapasukia, hakuna aliyeokoka miongoni mwa waliokuwa ndani ya jahazi ila mke wa mwanaume yule. Yeye aliokoka kwa kutumia mbao za jahazi ambazo zilimpeleka hadi kwenye kisiwa miongoni mwa visiwa vya bahari. Ndani ya kisiwa hicho kulikuwa na mwanaume mmoja ambaye alikuwa akisafiri na hakuacha heshima yoyote kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ila aliivunja. Basi hakujua lolote ila mwanamke aliyekuwa amesimama juu ya kichwa chake, akainua kichwa chake kumtazama, akasema: 'Ni binadamu au jini?' mwanamke akajibu: 'Mwanadamu.' Basi hakumzungumzisha neno lingine mpaka akawa amekaa kwake mkao wa mwanaume kwa mkewe. Alipoanza kumkusudia yule mwanamke akatetemeka, akamwambia: 'Kitu gani kinakutetemesha?' Akajibu: 'Namkimbia huyu.' Akaashiria mkono wake mbinguni. Akasema: 'Umemfanya huyu chochote?' Akasema: 'Hapana bali nguvu zake.'Akasema: 'Wewe unamkimbia huyu mbio zote hizi ilihali hujamfanya huyu chochote, basi mimi nakuchukia mno, wallahi mimi ndiye ninayefaa zaidi kukimbia huku na kukhofu kuliko wewe.' Basi mwanaume akasimama bila ya kufanya chochote, ndipo akarudi kwa mkewe akiwa hana hima yoyote ila kutubu na kurejea Kwake. Alipokuwa akitembea njiani ghafla akasadifiana na padri, basi jua likawa kali juu yao, ndipo padri akamwambia kijana: 'Muombe Mwenyezi Mungu atufunike kwa kivuli cha mawingu kwani hakika jua limekuwa kali juu yetu.' Kijana akasema: 'Mimi sijui kama nina jema mbele ya Mola wangu Mlezi hata nipate ujasiri wa kumuomba chochote.' Akamwambia: 'Mimi nitakuwa naomba nawe unaitikia.' Akasema: 'Ndio.' Basi padri akaanza kuomba na kijana akiitikia, basi haraka sana kivuli cha wingu kikawa kimewafunika. Wakatembea chini yake mchana kidogo, kisha wakaachana njiani. Kijana akachukua njia yake na padri njia yake, ndipo ghafla mawingu yakawa pamoja na kijana. Padri akasema: 'Wewe ni bora kuliko mimi, kwa ajili yako dua imejibiwa na wala haijajibiwa kwa ajili yangu. Nipe habari ni kipi kisa chako?' Ndipo akampa habari za yule mwanamke. Akasema: 'Umesamehewa yaliyopita kutokana na kuingiwa na khofu, na angalia mustakbali wako jinsi gani utakuwa."[405]

MALIPO YA MWENYE ASHKI ALIYE MTAWA

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Atakayekuwa na ashki akaficha na akajizuia na hatimaye akafariki basi yeye ni shahidi ." [406]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Ashki pasipo na matamanio ni kafara ya dhambi ." [407]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Atakayekuwa na ashki akaficha na akavuta subira, Mwenyezi Mungu atamghufiria na kumwingiza Peponi. " [408]

Imepokewa kutoka kwa Ibnu Abbas kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) kuwa amesema: "Watu bora katika umma wangu ni wale ambao hufanya utawa pindi Mwenyezi Mungu anapowapelekea balaa ya kitu." Wakamwambia: Ni balaa ipi? Akasema: 'Ashki ." [409]

MITEGO YA SHETANI

Imam Ridhaa(a.s) amepokea kutoka kwa baba zake kuwa: "Hakika Ibilisi alikuwa akiwajia Manabii(a.s) kuanzia kwa Adam(a.s) mpaka Mwenyezi Mungu alipomleta Masih(a.s) , alikuwa akiongea nao na kuwadadisi, na hakuna aliyekuwa akizungumza naye mara kwa mara kama Yahya bin Zakariya(a.s) . Yahya akamwambia: 'Ewe Abu Marah mimi nina haja kwako.' Akamwambia: 'Wewe una uwezo zaidi siwezi kukukatalia ombi basi niulize ulitakalo, hakika mimi si mwenye kukukhalifu katika jambo ulitakalo.' Yahya akasema: 'Ewe Abu Marah napenda unionyeshe mitego yako na mbinu zako ambazo kwazo huwanasa wanaadamu.' Ibilisi akasema: 'Kwa ukarimu wako na mapenzi yako, ninakuahidi hadi kesho.' Yahya alipoamka alikaa nyumbani kwake akisubiri ahadi na akamfungia mlango kabisa, ghafla akamhisi yuko usawa wake kutokana na mtego uliokuwa ndani ya nyumba yake, na hatimaye akaona sura ya uso wa kima na mwili wake ukiwa katika sura ya nguruwe, na macho yake yamepasuka kwa urefu. Kinywa chake kimepasuka kwa urefu na meno yake na kinywa chake ni mfupa mmoja bila kidevu wala ndevu, akiwa na mikono minne: Mikono miwili ikiwa kifuani mwake na miwili kwenye mabega yake. Mshipa wa kisigino ukiwa mbele na vidole vyake vikiwa nyuma na juu yake kukiwa na kuba na katikati yake kuna eneo lenye nyuzi zilizo kati ya rangi nyekundu, kijani njano na rangi zote, na mkononi mwake akiwa na kengele kubwa na juu ya kichwa chake kukiwa na yai na ndani ya yai kuna chuma kilichotungikwa kinashabihiana na koleo. Yahya alipotaamali akamwambia: 'Ni eneo gani hili ambalo liko katikati yako?' akajibu: 'Huu ni umajusi, mimi ndiye niliyeuanzisha na kuupamba kwa ajili yao.' Akamuuliza: 'Vipi hizi nyuzi zenye rangi?' akajibu: 'Hizi zote ni rangi za wanawake, mwanamke anaendelea kupaka rangi mpaka ananasa kwa rangi zake na kwazo nawatia watu kwenye fitina.' Akamuuliza: 'Vipi hii kengele iliyoko mikononi mwako?' Akasema: 'Huu ni mjumuiko wa ladha zote, kuanzia ngoma, zumali, gita, filimbi na ala. Na watu wanakaa kwenye vinywaji vyao wakiwa hawaburudiki kwa ladha basi hapo ndipo naitikisa kengele kati yao na hatimaye wanapoisikia basi mvuto wake huwavuta na hapo hupatikana anaecheza, mwenye kutikisa vidole vyake na hadi mwenye kuchana nguo yake.' Akamuuliza: 'Ni mambo gani ambayo yanakuridhisha sana?' Akasema: 'Wanawake, wao ndio mtego wangu, na kwa hakika wanapokusanyika walinganizi wema na watoa laana basi huenda kwa wanawake na wao huniridhisha.' Yahya akamwambia: 'Vipi hili yai lililopo juu ya kichwa chako?' Akasema: 'Kwalo najikinga na dua ya waumini.' Akamuuliza: 'Vipi hiki chuma nikionacho ndani yake?' Akajibu: 'Kwacho nazigeuza nyoyo za waumini.' Yahya akasema: 'Je kuna wakati wowote ulinishinda hata kido- go?' Akasema: 'Hapana, lakini kwako kuna sifa inivutiayo.' Yahya akamwambia: 'Ni ipi hiyo?' Akasema: 'Wewe ni mtu mlaji mno, unapofu- turu huendelea kula na kuvimbiwa na hilo hukukataza kutekeleza baadhi ya Swala na kisimamo chako cha usiku.' Yahya akamwambia: 'Hakika mimi nampa Mwenyezi Mungu ahadi kuwa sintoshiba chakula mpaka nitakapokutana naye.' Ibilisi akasema: 'Nami nampa Mwenyezi Mungu ahadi kuwa mimi sintomnasihi mwislamu mpaka nitakapokutana naye.' Kisha akatoka na hakurudi tena kwake baada ya hapo."[410]


6

7