• Anza
  • Iliyopita
  • 3 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 3307 / Pakua: 1856
Kiwango Kiwango Kiwango
WAPOKEZI WA KISHIA NDANI YA VITABU VYA KISUNNI

WAPOKEZI WA KISHIA NDANI YA VITABU VYA KISUNNI

Mwandishi:
Swahili

WAPOKEZI WA KISHIA NDANI YA VITABU VYA KISUNNI

RIWAYA ZA WAANDISHI MASHI'A KATIKA VITABU VYA SAHIH NA MUSNAD VYA AHL AS-SUNNA

UTANGULIZI

Makala haya yafuatayo ni barua ambayo Sheikh wa Kisunni, Sheikh Salim al-Bishri, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar, huko Cairo, Misri alimwandikia Sheikh wa Kishi'a katika karne ya ishirini na alianza majadiliano pamoja na Sheikh wa Kishi'a Mwanachuoni mashuhuri wakati huo, Sayyid 'Abd al-Husayn Sharaf al-Din wa Jabal 'Amil (upande wa kusini mwa Lebanon) ambaye aliizuru Misri katika mwaka 1329 - 1330 Hijriyyah muafaka wa 1911 - 1912 A.D. na walikutana pamoja.

Sheikh Bishri hakuamini kuwa Ahl al-Sunnah wanazo riwaya[1] kutoka Mashi'a katika vitabu vyao vitukufu na hivyo alitaka uthibitisho pamoja na majina yao na iwapo kutakuwapo na kukiri kwa Masunni kuwa hao waandishi walikuwa ni Mashi'a.

Barua ya maswala na majibu yametengenezwa kuwa kitabu kimoja mashuhuri sana kijulikanacho kwa jina la al - Muraja'at.

Kwa hakika kitabu hicho kimewaathiri wengi mno waliojaribu kukisoma hasa miongoni mwa wasomi na Mashekhe. Na makala haya ni barua mojawapo tu ya jibu kwa Sheikh Salim kutoka kwa Sheikh Sharaf al-Din.

Ni matumaini kuwa msomaji atafaidika na makala haya. Sheikh Sharraf al-Din anamwandikia majina 100 ya waandishi wa Kishi'a.

Ombi la Majina ya waandishi wa riwaya na ahadith za Ahl al-Sunnah ambao walikuwa ni Mashi'a waliojulikana

'Allamah Sayyid 'Abd al-Husayn Sharaf al-Din,

Assalaam 'Alaykum.

Nimepokea barua yako ya hivi sasa. Yaani ina nguvu huku ikiungwa mkono kwa majibizano yako na maamuzi yaliyokomaa kiasi kwamba sijiwezi illa kukubalia kila neno ulilolisema. Lakini habari isemayo kuwa Ahl al-Sunnah kwa mara nyingi wamekuwa wakizichukua riwaya na Ahadith zao kutoka kwa waandishi wa Kishi'a, ni kiujumla na kwa maneno machache. Hivyo utoe maelezo zaidi juu ya swala hili. Itakuwa vema iwapo ungekuwa umetaja majina ya hao waandishi wa Kishi'a na vile iwapo Ahl al-Sunnah wakikiri kuwa hao ni Mashi'a. Natumai kuwa unaelewa aina ya majibu ninayoyahitaji.

Ifuatayo ni orodha fupi ya waandishi wa Shi'a ambao riwaya na Hadith zao zipo zinapatikana katika vitabu vyenu vya Sahih na Musnad (musnad kutokea sanad, ikimaanisha mamlaka, ukusanyaji wa Hadith, mfano Musnad ya Ahmad ibn Hanbal).

Orodha hii ipo kwa mujibu wa mpangilio wa herufi za Kiarabu.

ISMA'IL IBN ABAN, AL-AZDI AL-KUFI AL-WARRAQ

Yeye alikuwa ni mmoja wa Mashekhe wa Bukhari. 'Allamah Dhahabi anaandika kuwa Bukhari na Tirmidhi wametegengeneza hoja zao kwa riwaya zake na vile vile kuelezea kuwa Yahya na Ahmad wamechukua riwaya kutoka kwake. Bukhari anamwelezea kuwa ni msema mkweli. Waandishi wengine wanasema kuwa yeye alikuwa ni mfuasi wa Madhehebu ya Kishia na alifariki mwaka 286 H. Al-Qaysarani, hata hivyo, anaandika tarhe ya kifo chake kuwa ni 216 H. na vile vile amechukizwa kwa kuwa Bukhari amechukua riwaya za Isma'il moja kwa moja kutoka kwake katika vitabu vyake mbali na Sahih.

'ABAN IBN TAGHLIB, IBN RIYAH

Qari (msomaji wa Qur'an), wa Kufah (Alikuwa mwanafunzi wa Imam Zayn al-'Abedin(a.s) na Imam Muhammad al-Baqir(a.s)

YAFUATAYO YAMENAKILIWA KUTOKA MIZAN CHA DHAHABI

'Aban ibn Taghlib wa Kufah; mfuasi halisi wa Shi'a, lakini hata hivyo alikuwa ni msema ukweli na kusadikiwa, na sisi tunachojihusisha naye ni ukweli wake tu, na swala la yeye kutokufuata dini zetu, basi hilo ni swala lake la kibinafsi. [Dhabahi anaendelea:] Ahmad ibn Hanbal, Ibn Mu'in na Abu Hatim wanamwamini yeye kuwa ni mtu anayeaminiwa na kusadikiwa; na Ibn 'Adi anadokeza kusema kuwa yeye (ibn Taglib) alikuwa ni Mshi'a halisi; na Sa'di anaandika kuwa yeye alikuwa ni mtu mwenye kufarakanisha waziwazi

Miongoni kwa wale ambao wamemtegemea yeye ni Muslim na waandishi wa vitabu vinne (4) vya Sunan, tukiwataja Abu Dawud, Tirmidhi, Nasai na Ibn Majah kwa kidhibiti cha wao kutumia kifupisho cha jina lake. Zaidi ya hayo, unazo riwaya zake katika Sahih Muslim na vitabu vinne vya Sunan kutokea Hakim, Al-A'mash na Fudayl ibn 'Amr kama zilivyo rekodiwa na Muslim, Sufyan ibn 'Uyaynah, Sha'bah na Idris al-Awdi.

Yeye alifariki katika mwaka 141 Hijriyyah. Allah swt amrehemu.

IBRAHIM IBN YAZID, IBN 'AMR IBN ASWAD IBN 'AMR AL-NUKHA'I

Hakimu wa Kufah. Mama yake alikuwa malikah bin Yazid ibn Qays, naye kutokea Nukha'iyah; ndugu zake Al-Aswad, Ibrahim na 'Abd al-Rahman, wana wa Yazid ibn Qays, walikuwa kama wajomba zao 'Alqamah ibn Qays na Ubayya ibn Qays, Waislam thabiti na ushahidi wao ulikuwa daima ukisadikiwa kuwa ni wa ukweli kabisa. Waandishi wa vitabu sita vya Sahih na wengineo wamechukua riwaya nyingi kutoka kwa hawa, wakijua waziwazi kuwa hao walikuwa ni Ma Shi'a.

Ama kuhusu Ibrahim ibn Yazid mwenyewe, Ibn Qutaybah katika Ma'arif anamtambulisha yeye kuwa ni Mshia kamili bila shaka yoyote ile. Pamoja na hayo, Riwaya zake zipo zinapatikana katika katika vitabu vya Sahih i.e Bukhari na Muslim. Yeye vile vile amewaripotia riwaya kutokea kwa mjomba wa mama yake, 'Alqamah ibn Qays, ambaye ameripoti kutoka kwa Himam ibn al-Harith na Abu 'Ubaydah ibn 'Abdullah ibn Mas'ud, or from 'Ubaydah au mjomba wake kwa upande wa mama yake Al-Aswad ibn Yazid.

Riwaya zake zinginezo zilizoko katika Sahih Muslim ni zile ambazo yeye amezichukua kutoka wajomba zake kwa upande wa mama yake, kwa kuwataja majina 'Abd al-Rahman ibn Yazid, na vile vile Sahm ibn Munjab, Abu Mu'ammar na 'Ubaydah ibn Nadlah, na 'Abis. Riwaya zake zipo zimeripotiwa katika Sahih mbili kwa kupitia Mansur, Al-A'mash, Zubayd, Hakam na 'Ibn 'Aun; na katika Sahih Muslim kwa kupitia Fudayl ibn 'Amr, Mughayrah, Ziyad, Ibn Kulayb, Wasil, Hasan ibn 'Ubaydullah, Hamad ibn Abu Sulayman na Simak. Ibrahim ibn Yazid alikuwa amezaliwa katika mwaka 50 Hijriyyah na alifariki mwaka 95 au 96 Hijriyyah, baada ya miezi minne kupita tangia afe Hajjaj ibn Yusuf.

AHMAD IBN MUFADDAL, IBN AL-KUFI AL-HAFRI

Abuy Zar'ah na Abu Hatam wamechukua riwaya kutoka kwake na kuunga mkono hoja zao, huku wakijua na kukiri kuwa huyo alikuwa ni Mshi'a halisi. Hivyo, Abu Hatam anaelezea kwa kusisitiza katika kitabu chake Mizan:

Ahmad ibn Mufaddal alitokana na watukufu wa Kishi'a na alikuwa ni mtu wa kusadikiwa na kuaminiwa.

Dhahabi vile vile amemwelezea katika Mizan na kumpatia vifupisho vya jina lake. Abu Dawud na Nasa'i vile vile wamechukua riwaya kutokea kwake katika vitabu vyao vya Sahih kwa kupitia Al-Thawri naye ameripoti riwaya kutoka kwa Asbat ibn Nasr na Isra'il.

ISMA'IL IBN ABAN, AL-AZDI AL-KUFI AL-WARRAQ

Yeye alikuwa ni mmoja wa Mashekhe wa Bukhari. 'Allamah Dhahabi anaandika kuwa Bukhari na Tirmidhi wametegengeneza hoja zao kwa riwaya zake na vile vile kuelezea kuwa Yahya na Ahmad wamechukua riwaya kutoka kwake. Bukhari anamwelezea kuwa ni msema mkweli. Waandishi wengine wanasema kuwa yeye alikuwa ni mfuasi wa Madhehebu ya Kishia na alifariki mwaka 286 H. Al-Qaysarani, hata hivyo, anaandika tarhe ya kifo chake kuwa ni 216 H. na vile vile amechukizwa kwa kuwa Bukhari amechukua riwaya za Isma'il moja kwa moja kutoka kwake katika vitabu vyake mbali na Sahih.

ISMA'IL IBN KHALIFAH, AL-MALA'I AL-KUFI

Jina la kiukoo ni Abu Isra'il na hili ndilo jina ambalo analotambuliwa kwa kawaida. 'Allamah Dhahabi ameandika katika kitabu chake Mizan al-I'tidal kuwa yeye alikuwa ni Mshia shupavu kabisa na daima akidai kuwa 'Uthman alikuwa kafiri na ameongezea maoni mengi kuhusu yeye. Licha ya hayo, Tirmidhi na waandishi wengine wa Sunan wamezichukua riwaya kutoka kwake na Abu Hatam amezitambulisha riwaya hizi kama nzuri; Abu Zar'ah amemchukulia yeye kama mwandishi mkweli, ingawaje maoni yake yamekuwa yenye juhudi zaidi. Imam Ahmad (ibn Hanbal) anachukulia riwaya zake kuwa ni zenye kuaminiwa Fallas anatoa maoni: yeye si miongoni mwa wale waliosema uongo na uzushi na riwaya zake zipo zinapatikana katika Sahih al-Tirmidhi; na Ibn Qutaybah katika Ma'rif anamhesabu miongoni mwa Mashi'a mashuhuri.

ISMA'IL IBN ZAKARIYA, KHALQANI AL-KUFI

Dhahabi anaandika katika kitabu cha Mizan al I'tidal kuwa yeye ni mwaminifu na ni Mshi'a na kwamba riwaya zake zipo zimeandikwa katika vitabu sita vya Sahih. Riwaya, mapokezi yake ya Ahadith yanapatikana katika Bukhari na Muslim. Yeye amefariki huko Baghdad, mwaka 104 H.

ISMA'IL IBN 'ABBAD, IBN 'ABBAS AL-TALIQANI

(Kwa umashuhuri alijulikana kama Sahib ibn 'Abbad)

Abu Dawud na Tirmidhi wamechukua riwaya kutoka kwake, kama vile ilivyoelezwa na Imam al-Dhahabi katika kitabu chake Mizan kwa kutoa maoni kuwa mtu adhimu kabisa wa uandishi wa mabarua na Mshi'a.

Hapana shaka kuwa kwake Mshi'a, na hayo ni kutokana na imani yake kwamba alikuwa Waziri Mkuu katika Utawala wa Buwayhiya. Yeye alikuwa ni mtu wa kwanza kwa kupewa jina la Sahib, kwa sababu alikuwa mwenzie Mu'ayid al - Dawlah katika ujana wake na huyo ndiye aliyempatia heshima hiyo, na kwamba alikuja kujulikana kwa jina la Sahib na baada yake ilikuwa ni desturi kumwita Waziri Mkuu waliofuatia kwa jina la Sahib. Yeye kwanza alikuwa ni Waziri wa Mu'ayid al-Dawlah, na baada ya kifo chake, ndugu yake Fakhr al-Dawlah, alimbakiza katika cheo hicho. Wakati wa kifo chake (24 Safar, 385 H., akiwa na umri wa miaka 59) wakazi wote wa mji wa Ray (kwa sasa inajulikana kwa jina la Tehran, mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran) walifunga milango ya nyumba zao na walikwenda nyumbani kwa Waziri Mkuu kushiriki katika mazishi yake, na Mfalme akiandamana na watu wote alishiriki kikamilifu katika mazishi yake. Yeye alikuwa Mwanachuoni Mkubwa na mwandishi na mtunzi wa vitabu vingi pamoja na makala mbalimbali.

IBN 'ABD AL-RAHMAN, IBN ABI KARIMAH

Mfasiri mashuhuri, aliyejulikana kama Al-Suddi.

'Allamah al-Dhahabi ameandika katika kumwelezea Al-Suddi kuwa yeye alidaiwa kuwa Mshi'a na Husayn ibn Waqid al-Muruzi ametaja kuwa yeye amemsikia akiwalaumu Abu Bakr na 'Umar, lakini pamoja na kujua ukweli huu, Al-Thawri, Abu Bakr ibn 'Ayyash na wengineo wamezichukua na kuzipokea riwaya zake, na Imama Muslim, Tirmidhi, Abu Dawud, Ibn Majah, na Nasa'i wameziandika katika vitabu vyao vijulikanavyo kwa jina la Sahih kwa kuunga maoni yao. Imam Ahmad (ibn Hanbal) amemchukulia yeye mwaminifu na Ibn 'Adi amemchukulia yeye kama msema ukweli wakati ambapo Yahya ibn Sa'id anasema: "Nilimwona kila mtu akimsema vema Al-Suddi na wao wote wamezichukua na kuzikubalia riwaya kutoka kwake." Yeye alifariki mwaka 127 Hijriyyah.

ISMA'IL IBN MUSA, AL - FAZARI AL-KUFI

'Allamah al-Dhahabi ameandika kuhusu huyu bwana katika kitabu chake Mizan al-I'tidal kuwa Ibn 'Adi alikuwa na mazoea ya kusema kuwa yeye alikuwa akilaumiwa kwa kuwa Mshia shupavu. Abdan anaelezea kuwa "Hannad na Ibn Abi Shaybah walichukizwa mno na kwenda kwetu kwake na daima walikuwa wakituambia sisi tusiende kwa huyo mtu mwovu ambaye anawalaumu vikali viongozi wetu watukufu." Lakini pamoja na hayo, Ibn Khuzaymah, Abu 'Arubah na wengi mno walijifunza Ahadith na riwaya kutoka kwake na yeye alikuwa na wadhifa na elimu ya waalimu kama Abu Dawud, Tirmidhi na wengineo. Wao wote wamechukua Ahadith na riwaya kutoka kwake na kuziingiza katika Sahih zao. Nasa'i amesema kuwa hakuna ubaya katika kuuchukua Ahadith na riwaya kutoka kwake. Yeye alifariki mwaka 245 H. Baadhi ya waandishi wanadai kuwa yeye alikuwa ni mjukuu wa Al-Suddi kwa upande wa mama.

TALID IBN SULEYMAN AL-KUFI

Ibn Mu'in ameandika kuwa yeye alikuwa akimshutumu mno 'Uthman. Hivyo wa-'Uthmani walipoyasikia hayo, walimwua kwa kumpiga mshale uliovunja mguu wake. Abu Dawud amemsema huyo kuwa ni rafidhi (yaani kafiri ilivyokuwa ikitumika kuwataja Mashi'a) na mshutumu mkuu wa Abu Bakr na 'Umar. Lakini pamoja na kujua ukweli huo, Ahmad (ibn Hanbal) na Ibn Namir walijifunza riwaya na Ahadith kutoka kwake na Imam Ahmad alisema: " Ingawaje Talid ni Mshi'a, lakini hakuna madhara kwa kuzipokea riwaya zake." Kitabu kiitwacho Sahih al-Tirmidhi kinacho riwaya zake huyu Bwana.

THABIT IBN DINAR (ALIJULIKANA KAMA ABU HAMZAH AL-THUMALI)

Yeye kuwa Mshi'a haina shaka kabisa. Tirmidhi inayo riwaya zake mbalimbali.

THAWBAR IBN ABI FAKHNAH

Yeye alikuwa ni mtumwa aliyefanywa huru na Umm Hani, binti yake Bwana Abu Talib(a.s) (dada yeke na Amir al-Mu'minin Imam Alia.s ) Dhahabi amemwelezea kwa kusisitiza kuwa huyo ni rafidhi; yeye alikuwa ni mfuasi halisi wa Imam Muhammad al-Baquir(a.s) , riwaya zitokanazo na yeye zinapatikana katika Sahih al-Tirmidhi.

JABIR IBN YAZID, IBN HARITH AL-JU'FI AL-KUFI

Dhahabi anaandika kuhusu huyu katika kitabu chake Mizan kuwa alikuwa ni mmoja wa Mashia waliosoma na anaandika kuwa Sufyan alisema kuwa alimsikia Jabir akisema kuwa ilimu ya Mwenyezi Mungu ilifikishwa na Mtume(s.a.w.w) kwa Imam Ali(a.s) , na kutoka kwake kwa Imam Hasan(a.s) , na kutoka kwake kwa Imam Hussein(a.s) na kuendelea, yaani kutoka kwa Imam mmoja hadi mwingine hadi kufikia kwa Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) na kwamba yeye alijifunza riwaya nyingi kutokea Imam(a.s) Muslim anasema mwanzoni mwa kitabu chake cha Sahih Muslim kutokea Jarrah kuwa Jabir alisema: "Mimi kwa ujumla ninazo riwaya na Ahadith elfu sabini ambazo zote zimenifikia kutoka kwa Abu Ja'afar (yaani Imam Muhammad al-Baqira.s .) kutokea kwa Mtume(s.a.w.w) " Mwandishi huyo huyo anasema kutokea Zuhayr kuwa Jabir alisema: "Mimi ninazo Ahadith elfu hamsini ambazo sijazisimulia chochote," na hapo alisimulia Ahadith moja na kusema: " Hii ni mojawapo ya elfu hamsini." Dhahabi anaendelea kuelezea katika kitabu chake cha Mizan kuwa popote pale Jabir alipokuwa amezoea kusimulia Ahadith ya Imam Mohammad al-Baqir a.s., yeye daima alikuwa akianza kwa kusema: "Hivyo ndivyo mrithi wa warithi (wa Mtume(s.a.w.w) alivyoniambia." Mwandishi huyu huyu anaandika kuwa wengi walimshutumu kwa kuamini katika raj'ah (marudio). Dhahabi anaelezea kwa mara nyingine tena kwa mamlaka ya Za'idah kuwa Jabir alikuwa rafidhi, na alikuwa akiwashutumu wapinzani wote wa Imam 'Ali (a.s) Lakini pamoja na hayo yote, Nasa'i na Abu Dawud wamechukua riwaya zake kama vile riwaya yake kuhusu suju al-sahwa yaani kurekebisha kupitiwa wakati wa sala. Sha'ba na Abu 'Awanah na washiriki wao vile vile wamechukua riwaya zake. Abu Dawud na Tirmidhi wanamchukulia yeye miongoni mwa waandishi wao waaminiwao na kuwategemea kwa usahihi. Sufyan al-Thawri alimwelezea kama mwandishi mwenye imani ya riwaya na alisema: "Mimi kamwe sijamwona mtu yeyote aliye mwangalifu kuliko yeye," na Sha'bah anasema: "Jabir ni mwenyekuripoti aliye mkweli," na yeye pia husema: "Popote pale Jabir aliporipoti Hadith yoyote ile, basi mimi daima nimemwona yeye kuwa mwaminifu kabisa miongoni mwa watu." Waki anasema: "Lipo jambo moja ambalo mimi sina shaka nalo kwa vyovyote vile, nayo ni kwamba Jabir al-Ju'fi ni mtu wa kutegemewa na kusadikiwa." Ibn 'Abd al-Hakam alimsikia Al-Shafi'i akimwambia Sufyan al-Thawri: "Iwapo mimi ningalikuwa nikimshuku Jabir al-Ju'fi basi mimi nisingalitilia shaka yale uyasemayo wewe." Jabir alifariki ama katika mwaka 127 au 128 Hijriyyah; Allah swt amrehemu.

JARIR IBN 'ABD AL-HAMID, AL-DABBI AL-KUFI

Ibn Qutaybah katika kitabu chake Al-Ma'arif, amemhesabu yeye miongoni mwa Mashi'a waliojulikana vyema na Dhahabi amemtambulisha kwa vifupisho vya jina lake popote pale alipomtumia katika riwaya zake katika kitabu chake Mizan, inathibitisha vile alivyo mtu wa kutegemewa katika maoni ya waandishi wa vitabu vya Sahih.

Zaidi ya hayo, Dhahabi anasema katika kumsifu: "Mtu msomi kutoka Ray, msema kweli, aliyechukuliwa na waandishi wa vitabu kuwa ni mtu wa aina yake pekee," naye ameelezea mwungano wa maoni kuhusu kutegemewa kwake. Vile vile, kuna riwaya kutokea kwake katika Sahih al-Bukhari na Sahih al-Muslim ambazo yeye anazielezea kutoka Al-A'mash, Mughayrah, Mansur, Ismail ibn Abu Khalid na Abu Is-haq al-Shaybani na Qutaybah ibn Sa'id, Yahya ibn Yahya na 'Uthman ibn Abu Shaybah ni miongoni mwa watu ambao wamezieleza riwaya kutoka kwake. Yeye amefariki huko Ray katika mwaka 187 H akiwa na umri wa miaka 77, Allah swt amrehemu.

JA'FAR IBN ZIYAD, AL-AHMAR AL-KUFI

Abu Dawud anamwelezea katika maneno yafuatayo: "Mtu msema ukweli na yu Mshi'a." Juzjan anamwelezea yeye kama "anayetoka nje ya njia," yaani yeye ametoka nje ya njia ya Juzjan, na akaelekea katika njia ya Ahl al-Bayt(a.s) Ibn 'Adi anasema kuwa "yeye ni mcha Mungu na ni Mshi'a." Mjukuu wake mwenyewe, yaani Husayn ibn 'Ali ibn Ja'far ibn Ziyad anasema: "Babu yangu, Ja'far, alikuwa miongoni mwa masharifu wa Kishi'a wa Khurasan." Abu Ja'far al-Dawaniqi anamwelezea yeye kama mfungwa aliyefungwa mkanda shingoni na kwa kamba ndefu, pamoja na Mashi'a wengineo. Abu 'Uyaynah, Waki', Abu Ghassan al-Mahdi, Yahya ibn Bushr al-Hariri na Ibn Mahdi wamezieneza riwaya walizojifunza kutoka kwake, yaani ama yeye alikuwa ni mwalimu au mwongozi wao; na Ibn Mu'in na wengineo wanathibitisha ukweli wake, ambapo Ahmad ibn Hanbal anamsema hivi: " Mwandishi mzuri wa riwaya." Dhahabi amemtaja katika kitabu chake cha Mizan na ameandika uhakika uliotajwa hapo awali kuhusu yeye na Tirmidhi na Nasa'i walitengeneza vifupisho vya jina lake, ambavyo inamaanisha kuwa wao walikuwa wakimtumia kwa mara nyingi katika kuziandika riwaya zake. Zaidi ya hayo, zipo riwaya nyingi kutokea kwake katika vitabu vyote vya Sahih kutokea Bayan ibn Bushr, 'Ata' ibn Sa'ib na wengineo. Yeye alifariki katika mwaka 167 Hijriyyah, Allah swt amrehemu.

JA'FAR IBN SULAYMAN, AL - DAB'I AL-BASRI

Ibn Qutaybah amemhesabu yeye miongoni mwa Mashia mashuhuri katika kitabu chake kiitwacho Ma'arif, uk. 206. Ibn Sa'd (kitabu cha Tabaqat).

Riwaya Za Waandishi Mashi'a Katika Vitabu Vya Sahih Na Musnad Vya Ahl as-Sunna

Kimetarjumiwa na

Amiraly M H Datoo

Bukoba - Tanzania

Kimetolewa wavuni na timu ya

Ahlul Bayt Digital Islamic Library Project

SHARTI YA KUCHAPA

Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.

MWISHO WA KITABU

YALIYOMO

WAPOKEZI WA KISHIA NDANI YA VITABU VYA KISUNNI 1

RIWAYA ZA WAANDISHI MASHI'A KATIKA VITABU VYA SAHIH NA MUSNAD VYA AHL AS-SUNNA 1

UTANGULIZI 1

ISMA'IL IBN ABAN, AL-AZDI AL-KUFI AL-WARRAQ 2

'ABAN IBN TAGHLIB, IBN RIYAH 2

YAFUATAYO YAMENAKILIWA KUTOKA MIZAN CHA DHAHABI 2

IBRAHIM IBN YAZID, IBN 'AMR IBN ASWAD IBN 'AMR AL-NUKHA'I 2

AHMAD IBN MUFADDAL, IBN AL-KUFI AL-HAFRI 3

ISMA'IL IBN ABAN, AL-AZDI AL-KUFI AL-WARRAQ 3

ISMA'IL IBN KHALIFAH, AL-MALA'I AL-KUFI 3

ISMA'IL IBN ZAKARIYA, KHALQANI AL-KUFI 4

ISMA'IL IBN 'ABBAD, IBN 'ABBAS AL-TALIQANI 4

IBN 'ABD AL-RAHMAN, IBN ABI KARIMAH 4

ISMA'IL IBN MUSA, AL - FAZARI AL-KUFI 4

TALID IBN SULEYMAN AL-KUFI 5

THABIT IBN DINAR (ALIJULIKANA KAMA ABU HAMZAH AL-THUMALI) 5

THAWBAR IBN ABI FAKHNAH 5

JABIR IBN YAZID, IBN HARITH AL-JU'FI AL-KUFI 5

JARIR IBN 'ABD AL-HAMID, AL-DABBI AL-KUFI 6

JA'FAR IBN ZIYAD, AL-AHMAR AL-KUFI 6

JA'FAR IBN SULAYMAN, AL - DAB'I AL-BASRI 7

SHARTI YA KUCHAPA 7

MWISHO WA KITABU 7

YALIYOMO 8


[1] . Kwa riwaya tutakuwa tukimaanisha mapokezi ya Ahadith na Sunnah za Mtume s.a.w.w. zilizowafikia Mashi'a kwa kupitia Ahl al- Bayt watukufu (a.s)