• Anza
  • Iliyopita
  • 21 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 20691 / Pakua: 3997
Kiwango Kiwango Kiwango
MAISHA YA ABU DHARR

MAISHA YA ABU DHARR

Mwandishi:
Swahili

MAISHA YA ABU DHARR

KIMEANDIKWA NA: KIKUNDI CHA WANACHUONI ISLAMIC SEMINARY PUBLICATIONS

KIMETARJUMIWA NA: AL-AKH SALMAN SHOU

KIMEHARIRIWA NA: USTADH ABDALLAH MOHAMED

NENO LA MCHAPISHAJI

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza, kwa jina la: "Abu Dharr"

Kitabu hiki kinahusu maisha ya Sahaba mkubwa na mashuhuri; Abu Dharr (Jundab bin Junadah). Abu Dharr alikuwa mtu wa tano kuingia kwenye Uislamu na upanga wake ulikuwa unafaa sana katika kuendeleza Uislamu. Aliona mikengeuko mingi katika Uislamu tangu kuanza kwake, na baada ya kifo cha Mtukufu Mtume mambo hayakuwa mazuri. Alishuhudia mitafaruku mingi wakati wa makhalifa watatu wa mwanzo kiasi kwamba hakuweza kuvumilia, na alianza kukemea maovu yanayofanywa na makhalifa wazi wazi na kwa ujasiri mkubwa sana mpaka ikafikia Khalifa wa tatu kuchukua hatua za kumhamisha na kumpeleka jangwani ambako aliishi maisha ya dhiki mpaka kifo kikamkuta huko.

Kwa bahati mbaya sana wanahistoria wengi wa Kiislamu na wasio wa Kiislamu hawakuzungumza habari zake kwa kina na kama inavyostahiki kuwa. Kwa hakika Abu Dharr pamoja na Masahaba wengine kama vile Amar bin Yasir, Mikidadi, Salman Farsy, halikadhalika na ami yake Mtukufu Mtume, mzee Abu Twalib na mke wa Mtume Bibi Khadija, alikuwa ni madhulumu wa historia.

Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huo,

Taasisi yetu ya 'Al-Itrah Foundation' imeona ikitoe kitabu hiki kwa luhga ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yale yale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.

Tunamshukuru ndugu yetu, Salman Shou kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vile vile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.

Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni mwanga kwa wasomaji wetu na kuzidisha upeo wao wa elimu katika dini.

KUHUSU WACHAPISHAJI

Leo hii akili yenye hadhari inaona kiakili mabadiliko ya maisha ya mwanadamu. Sayansi na teknolojia na mafanikio yao ya kushangaza yanaonekana yamefika kwenye kilele chao. Mahitaji ya kidunia hisia kali za matamanio ya mamlaka na ukubwa, ni mambo ambayo yamemwelekeza mwanadamu kwenye muflisi wa maadili mema. Katika hali hii ya kukatisha tamaa, mtu analazimika kutulia na kukadiria upya hatari zinazoweza kuwa tishio kwa mwanadamu kwa ujumla. Mwanadamu kwa mara nyingine tena ameelekeza macho yake kwa Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu kwani sasa ametambua kwamba ufumbuzi wa matatizo yake na hatima ya ukombozi wake ni mambo yaliyomo katika kufuata na kutekeleza.

Kuhama huku kutoka kwenye fikra ya mambo ya kidunia na kwenda kwenye mambo ya kiroho ni hali inayoafikiana kikamilifu na malengo na madhumuni ya seminari ya Kiislamu. Miongozo ya kidini, iliyo sambamba na maendeleo ya wakati uliopo, yanatoa kimbilio linalohi-tajiwa sana na akili inayosumbuliwa na yenye wasi wasi. ni matokeo ya ongezeko la utambuzi, kwamba imeeleweka kwamba siri ya kuishi maisha ya uadilifu hapa duniani kuelekeza kwenye furaha kamili ya milele ya maisha ya Peponi. Huu ni ujumbe wa Uislamu kwa ulimwengu wote.

Jumuiya yetu ya Kiislamu inataka kunyanyua juu mwenge wa mwongozo wa kiroho na kusaidia kwa moyo wote kutangaza urithi wa kiroho wa mwanadamu. Inaonyesha njia ya maisha kwa mujibu wa Quran katika utukufu wake ulio safi kabisa. Inaonyesha hayo tu yenye mamlaka na yaliyothabiti. Uenezi wake umebuniwa kwa jinsi inayoweza kukidhi mahitaji ya kiroho katika wakati uliopo.

Itahudumia kama chemchem ya kudumu kwa wale wenye kiu ya ujuzi. Seminari ya Kiislamu ni taasisi ya kimataifa ambayo inajaribu kuleta udugu wa Kislamu. Inapata mchango mzuri sana kutoka kwa wanachuo, kama nyongeza ya kuwa na msaada wa kimataifa kwa ajili ya kutimiza lengo lake kubwa. Inayo vituo; Asia, Afrika, Ulaya, Amerika, Canada na Mashariki ya mbali.

MPENDWA MSOMAJI

Kitabu hiki kimechapishwa na Seminari ya Kiislamu. Uenezi wake umebuniwa kwa ajili ya kuhudumia mahitaji ya kiroho katika kipindi hiki ukiwa na msisitizo mahsusi kusafisha akili na fikra ya Muislamu. Juhudi kubwa sana zimefanywa na Seminari kuweka katika machapisho yake yale ambayo yanaaminika na thabiti kweli katika Uislamu.

Unaombwa kwa ukarimu kukisoma kitabu hiki kwa moyo ambao umekusudiwa. Pia unaombwa uwe huru kuwasilisha kwetu maoni yako ambayo yatathaminiwa sana kuhusu uenezi wetu.

Kutangaza ujumbe wa Uislamu ni kazi inayotaka ushirikiano wa watu wote. Seminari inakukaribisha katika kazi hii ikikubaliana kwa furaha na Aya ya Quran Tukufu.

"Sema; Mimi ninakunasihini kwa jambo moja tu ya kwamba msimame kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wawili wawili na mmoja mmoja. " (34:46).

Mwenyezi Mungu na akurehemu. Wako katika Uislamu.

UTANGULIZI

Baada ya miaka kumi na tatu ya mfululizo wa mateso na mapambano, Mtume wa Uislamu aliondoka Makkah na kwenda Madina. Alihisi kwamba kipindi cha uvunjaji sheria na kutangazwa kwa siri kwa Uislamu kilikwisha na kwa msaada wa masahaba wake waaminifu na jasiri angeweza kujenga jumba kubwa la dola ya Kiislamu na kuweka msingi wa serikali ya kisiyasa kama anavyotaka Mwenyezi Mungu.

Mara tu baada ya kufika Madina, Mtukufu Mtume alijenga msikiti hapo. Alijenga nyumba yake iliyotazamana na msikiti, na alifanya mlango wake wa kuingia moja kwa moja msikitini. Hapakuwepo na mabadiliko ya maisha yake tangu mwanzo hadi mwisho. Tabia, mwenendo na maadili mema yalikuwa hivyo hata baada ya kuanzisha serikali ya Kiislamu katika Arabia yote.

Mfumo wa utawala mpya na dola mpya vilitokeza na kuanza kuwepo katikati ya dola mbili za wakati huo. Kwenye Serikali hii ya Kiislamu hapakuwepo na mtawala na mtawaliwa, hapakuwepo afisa na wa chini yake, na hapakuwepo na bwana na mtumwa. Wote walikuwa sawa mbele ya Mwenyezi Mungu.

Mwasisi wa mfumo huu mpaya wa utawala alitawafu na baada ya kunyang'anywa Ali urithi na kuundwa kwa vikundi vya kisiasa, mkengeuko wa kwanza ambao ulitikisa msingi wa Kiislamu ulitokeza kwenye jambo la Ukhalifa.

Mmojawapo wa masahaba waaminifu sana na jasiri sana wa Mtukufu Mtume alikuwa Abu Dharr. Alikuwa mtu wa tano kuingia kwenye Uislamu na upanga wake ulikuwa unafaa sana katika kuendeleza Uislamu. Aliona mikengeuko yote hii. Ali ambaye alikuwa mfano halisi wa wema na ukweli, alilazimika kuishi maisha ya upweke na

maadui wa Uislamu walipe na kwenye mfumo wa Ukhalifa na walikuwa wanauharibu Uislamu kwama mchwa.

Abu Dharr alisumbuliwa sana na kushtuka na aliona kwamba hali ya Uislamu ya siku za usoni ilikuwa ya wasi wasi na kuogopesha. Hata hivyo pia aliona kwamba kwa hali yoyote ile msafara wa Uislamu ulikuwa unaendelea kwenye njia yake, ingawa haki kuu ilikuwa, mpangilio wa Kiislamu hakuvunjika kabisa. Kwa hivyo, ingawa alihuzunika na kufadhaika, alinyamaza kimya!

Mfumo wa utawala wa Uthman ulipopata uwezo kamili wa serikali ya Kiislamu, haki za wafanya kazi na Waislamu wasio jiweza zilikiuka na wala riba, wanao shughulika na watumwa, matajiri na makabaila, ambao walifika kwenye baraza la Uthman na Muawiyah. Tofauti za matabaka na kuhodhi utajiri ni tabia zilizoanzishwa tena na Uislamu uliotishiwa na hatari kubwa. Njia na tabia za Mtukufu Mtume ziliachwa. Maelfu ya dinari zilitumika kujenga Ikulu ya Muawiyah iliyoitwa (Green Palace) ya mtawala wa Kiislamu na utaratibu wa mabaraza ya Kifalme ulianzishwa. Umari aliendesha maisha yake kama mtu wa kawaida na Abu Bakr naye aliishi hivyo hivyo, ili kuendesha maisha yake, alikuwa anafanya kazi ya kukamua mbuzi wa Myahudi ambapo kidani cha mke wa Uthman, Khalifa wa tatu kiligharimu thuluthi moja (1/3) ya pato la lililoletwa kutoka Afrika.

Akichukua nafuu isiyostahili ya kazi anayofanya baba yake, mtoto wa kiume wa mmojawapo wa maofisa wa ngazi ya juu sana katika utawala wa Umari alichukua farasi wa mtu kwa lazima. Kwa upande mwingine Uthman alimteua Marwan bin Hakam kama mshauri wake mtu ambaye alipewa adhabu ya uhamisho na Mtukufu Mtume na akampa zawadi ya kiunga cha Kheybar pamoja na malipo kutoka Afrika!

Abu Dharr alipochunguza shughuli hizi za kuaibisha hakuweza kuvumilia yote haya, aliamua kufanya upinzani dhidi ya mfumo huo wa kidikteta. Yalikuwa maasi ya kijasiri na ukakamavu ambayo yalisababisha nchi zote za Kiislamu kufanya uasi dhidi ya Uthman; mawimbi yake yanayo rindima bado yanaweza kuonekana kwenye jamii nyingi za binadamu.

1

MAISHA YA ABU DHARR

Abu Dharr alikuwa na shauku ya kuanzisha mfumo wa maadili ya Kiislamu, ambapo utawala wa Uthman ulikuwa unakiuka kwa kuhuisha utawala wa kitabaka. Abu Dharr aliona Uislamu kuwa ndio kimbilio la wasiojiweza, na mafakiri waliokuwa wanakandamizwa, na Uthman aliufanya utawala wake kuwa njia ya kuwafadhili jamii ya watu wakuu na wala riba.

Ugomvi huu baina ya Abu Dharr na Uthman uliendelea, hatimaye Abu Dharr alipoteza maisha yake kwa sababu hii.

Abu Dharr alimtambua Mwenyezi Mungu Mweza wa yote; kwa hiyo kamwe hakutetereka katika njia Yake hata kwa nukta moja. Aligeuka kuwa mtu bora katika kundi la Uislamu na ndio jambo ambalo linatosha kuonyesha umashuhuri wake.

Abu Dharr ni mmojawapo wa wale viongozi na wakombozi wa uhuru ambapo mwanadamu anautaka leo hii. Hususan kwa vile utaratibu wa muda umefanyiza hali ya wasiwasi mkubwa katika ulimwengu wa uchumi na matatizo ya kiuchumi yanashughulikiwa kuwa ndio matatizo ya msingi zaidi ya maisha, maoni yake yamepata umuhimu mkubwa. Hali hiyo hiyo iliyoanzisha huko Syria na Madina kwa kuwakusanya mafakiri na wasiojiweza na kuwashawishi waasi dhidi ya wala riba na wanaohodhi utajiri, pia leo hii imejitokeza. Waislamu hapa duniani wanakumbuka maneno yake ya kuvutia, maoni sahihi na ho tuba kali. Inawezekana kwamba wanaweza kuona kwenye sehemu za mbali sana historia kwamba amewakusanya wanaokandamizwa na

wasiojiweza kwenye msikiti na ana chokonowa hisia zao dhidi ya wale waishio kwenye ikulu (majumba ya maraisi wa mataifa mbali mbali duniani) na utaratibu mchafu wa Uthman na kutangaza hadharani: "Watu hao wanao hodhi dhahabu na fedha na hawatumii katika njia ya Mwenyezi Mungu, wanapaswa kujua kwamba adhabu yao itakuwa mateso makali ." (Quran 9:34).

"Ewe Muawiyah! Endapo unajenga Ikulu hii kwa fedha yako mwenyewe ni ubadhilifu, na kama unajenga kwa kutumia hazina ya taifa, huko ni kuitwalia ."

"Ewe Uthman! Masikini wamekuwa masikini zaidi na matajiri wamekuwa matajiri zaidi. Yote haya yanasababishwa na wewe."

SURA YA KWANZA

Abu Dharr alikuwa mmojawapo wa hao masahaba wa Mtume wa Uislamu, Muhammad(s.a.w.w) ambao walikuwa wachaji Mungu na wapenda uhuru na walikuwa na tabia bora kwa mujibu wa maneno ya Mtukufu Mtume: Pepo na wakazi wa huko wanawataka haraka sana. Alifaidika kuwa na Mtume katima uhalisi wake.

Abu Dharr mwenyewe anasema: "Jina langu halisi ni Jundab bin Junadah, lakini baada ya kuingia kwenye Uislamu, Mtume alinipatia jina la 'Abdullah' na hili ndilo jina ninalolipenda hasa ."

Abu Dharr ilikuwa Kuniyah yake (kutokana na mtoto wake wa kwanza aliyeitwa Dhar).

Wanavyuoni wanakubaliana kwamba Abu Dharr alikuwa mtoto wa kiume wa Junadah bin Qays bin Saghir bin Hazam bin Ghafir na mama yake alikuwa Ramlah binti Wafiah Ghifariah. Alikuwa wa jamii ya Kiarabu na alikuwa wa kabila la Ghifar. Ndio sababu ya neno 'Ghifar; limeandikwa na jina lake.

Abdullah al-Subaiti ameandika: "Tunapoangalia wasifu wa Abu Dharr inaonekana kama vile ni nuru iliyopewa umbo la Binadamu. Alikuwa mfano halisi wa sifa za mtu mashuhuri. Alikuwa na sifa pekee ya akili, uelewa, busara na werevu." Kwa maneno ya Imamu Jafar Sadiq: "Wakati wote alikuwa katika tafakuri na Swala zake ziliegemezwa kwenye mawazo kuhusu Mungu ." (Sahih Muslim).

Mwandishi maarufu wa Misri Abdul Hamid Jaudatus Sahar, kwenye kitabu 'Al-Ishtiraki az-Zahid, ameandika: Wakati fulani ilitokea njaa kali. Watemi wa kabila la Ghifar walikusanyika kwa ajili ya kushauriana ili wapate ufumbuzi wa tatizo hilo kwa sababu ya ukame wa muda mrefu. Kwa hiyo hicho kilikuwa kipindi cha mateso makubwa. Wanyama walikonda na akiba kwenye maghala ilikwisha. Waliambizana wao kwa wao, 'Hatujui kwa nini Mungu wetu (Sanamu Manat) amekasirishwa na nini kutoka kwetu, ingawa tumeomba mvua, tumetoa sadaka ya ngamia na tumefanya kila linalowezekana ili atupendelee.

Msimu wa mvua sasa umekwisha. Hakuna hata dalili ya wingu angani. Hapajatokea mngurumo na rasha rasha ya mvua kipindi hiki, hakuna hata tone la mvua au manyunyu. Unafikiria nini? Tumekuwa wapotevu hivyo kwamba ghadhabu ya mungu wetu imetuangukia? Kwa nini ahisi amekosewa na sisi ambapo tumetoa sadaka nyingi kwa ajili ya kumfurahisha yeye?"

Watu walianza kutafakari juu ya jambo hili na kubadilishana mawazo. 'Binadamu hawezi kuingilia mipango ya Mbinguni. Hakuna

mtu yeyote anayeweza kuleta mawingu ya mvua kutoka angani. Anayeweza kufanya hivyo ni 'Manat' tu. Kwa hiyo hatuna njia nyingine isipokuwa sisi, wanaume na wanawake, twende Hija huku tunalia kwa huzuni na kusali na kumwombea kwa huzuni na kusali na kumwomba Manat atusamehe. Labda inawezekana akatusamehe na mvua ikaanza kunyesha na kuifanya ardhi kuwa kijani kibichi baada ya ukame, ili umasikini wetu ubadilike kuwa mafanikio, uchungu kuwa furaha na matatizo kuwa raha na starehe."

Kwa hiyo, kabila lote lilianza matayarisho ya safari ya kwenda kumuona Manat. Wale waliokuwa wamelala waliamka na kuweza kuweka mito ya kukalia juu ya migongo ya ngamia wao. Unais (ndugu yake Abu Dharr) naye pia alipanda ngamia wake na kumwendesha, ili aungane na msafara, karibu na Pwani ya bahari, Mushalsal na Qadid sehemu zilizomo kati ya Makkah na Madina, ambapo ndipo Manat alipo.

Unais alitazama huku na kule lakini hakumuona kaka yake. Alimbembeleza ngamia akakaa chini. alikimbia kuelekea nyumbani. Aliingia ndani huku akiita 'Jundab!

Mara tu Unais aliposikia hivyo, alikimbia kwenda huko. Alipofika hapo, alimuona mtu anasema, "Sifa zote zinastahiki kwake Mwenyezi Mungu. Ninamsifu Yeye na ninahitaji msaada Wake. Ninamwamini Yeye, ninamtegemea Yeye na ninashahidilia kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu na Hana mshirika."

Katika nukuu ya Subaiti, Unais alimsikia mtu huyo akitangaza, "Enyi watu! Nimekuleteeni neema ya dunia hii na baada ya maisha haya. Semeni kwamba hapana mungu isipokuwa Allah ili muweze kupata ukombozi. Mimi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na nimekuja kwenu. Ninawaonya kuhusu adhabu ya siku ya Hukumu. Kumbukeni kwamba hakuna mtu atakayepata kuokolewa isipokuwa yule anayekuja mbele ya Mwenyezi Mungu kwa moyo wa unyenyekevu. Wala utajiri hautakuwa na manufaa kwake, ama watoto hawatawasaidieni. Mwogopeni Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atakuwa mwema kwenu. Enyi watu! Nisikilizeni! Ninasema wazi kabisa kwamba mababu zetu walifanya upotovu kwa kuacha njia iliyonyooka na kuanza kuabudu masanamu haya na nyinyi mnafuata nyayo zao. Kumbukeni kwamba masanamu wala hayawezi kuwaumizeni ama kuwanufaisheni. Wala hayawezi kuwazuieni ama kuwaongozeni."

Unais aliposikia hotuba hii yenye ushawishi mkubwa alishangaa. Lakini katika kustajabu kwake aliona kwamba watu walikuwa wanasema mambo tofauti dhidi yake.

Aliposikia Mtume alisema, "Mitume hawasemi uongo. Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu mbali na Yeye, kwamba nimetumwa kwenu kama mjumbe. Kwa jina la Mwenyezi Mungu mtakufa kama mnavyolala na mtafufuka kama mnavyoamka. mtaitwa kuhesabiwa matendo yenu. Halafu mtapewa Pepo au Jahanamu ya milele!"

Aliposema hivi watu walimuuliza Mtume, watafufukaje baada ya kuwa vumbi?

Wakati huu huu Mwenyezi Mungu aliteremsha Aya zifuatazo: "Sema: Kuweni hata mawe, na chuma. au umbo lolote mnaloliona kubwa katika vifua. Watasema: Nani atakayeturudisha tena? Sema: Yule aliye kuumbeni mara ya kwanza! Watakutikisia vichwa vyao, na watasema: Lini hayo? Sema: Asaa yakawa karibu! " (17:50-51).

Mara tu Mtume alipomaliza hotuba yake watu walinyanyuka. Wakati walipokuwa wanasambaa, mmoja wao alisema: "Huyu ni mtabiri?" Mwingine akasema, "Huyu ni mchawi."

Unais alimsikiliza Mtume na watu. Aliinamisha kichwa chake kwa muda fulani na akanong'ona: "Kwa jina la Mwenyezi Mungu maneno yake ni matamu. Hayo aliyoyasema ni kweli na watu wanaompinga ni wapumbavu."

Halafu akapanda ngamia wake akaanza safari ya kuelekea kwao. Aliendelea kufikiria kuhusu Muhammad, Mtume wa Mwenyezi Mungu wakati wote wa safari yake, na alikuwa anashangaa kuhusu mazungumzo yake, hadi alipoonana na Abu Dharr.

Abu Dharr alipomuona Unais, alimuuliza kwa shauku kubwa, "Kuna taarifa gani? Uliona nini Makkah?"

Unais: "Wanasema kwamba mtu huyu ni mshairi, mchawi na mtabiri. Lakini nilipochunguza mazungumzo yake kulingana na wale wanaosema kuwa ni mshairi, niliona kwamba maneno yake si mashairi wala si utabiri kwani nimewahi kukutana na watabiri wengi, na mazungumzo yake si sawa na yale ya watabiri.

Abu Dharr: "Hufanya nini na husema nini?"

Unais: "Husema mambo ya ajabu."

Abu Dharr: "Huwezi kukumbuka chochote katika yale aliyosema."

Unais: "Kwa jina la Mwenyezi Mungu! Hotuba yake ilikuwa tamu sana lakini sikumbuki chochote zaidi ya yale ambayo nimekwisha kwambia, lakini nimemuona anasali karibu na Al-Ka'abah, na pia nimemuona kijana moja mwenye sura ya kupendeza ambaye haja-balekhe, akisali pamoja naye. Watu wanasema kwamba huyo ni binamu yake Ali. Pia niliona mwanamke anasali nyuma ya mtu huyu. Watu waliniambia huyo ni mke wake, Khadijah.

SURA YA PILI

Baada ya kumsikiliza kaka yake, Abu Dharr alisema, "Sijaridhishwa na ripoti yako. Nitakwenda huko mimi mwenyewe, nimuone na nimsikilize mimi binafsi."

Abu Dharr alifika Makkah, aliingia kwenye eneo la Ka'abah na akaanza kumtafuta Mtume, lakini wala hakumuona pale, ama kusikia akitajwa. Alikaa hapo hadi machweo ya jua. Ali aliwasili hapo na akapita karibu na pale alipoketi Abu Dharr. Alimuuliza, "Unaonekana kuwa msafiri. Ni kweli?"

Abu Dharr: "Ndio." Ali: "Njoo nifuate."

Ali alimchukua nyumbani kwake. Wote wawili walikuwa kimya wakati wanakwenda nyumbani kwa Ali. Abu Dharr hakumuuliza Ali kitu chochote hadi walipofika nyumbani. Ali alitayarisha mahali pa kulala na Abu Dharr akalala. Kesho yake asubuhi alikwenda tena Ka'abah kumtafuta Mtume. Wala hakumuuliza mtu yeyote ama mtu

yeyote kumwambia chochote. Abu Dharr aliendelea kungoja kwa hamu kubwa hadi mwisho wa siku. Ali alikwenda tena kwenye Al-Ka'abah kama kawaida yake na alipita mbele ya Abu Dharr: mara alipomuona Abu Dharr, alimuuliza: "Kwa nini hujaenda nyumbani hadi sasa?"

Abu Dharr: "Hapana."

Ali: "Vema! Sasa twende nifuate Mimi."

Wote walili walikuwa wanakwenda kimya Ali alipouliza, "kwa nini!

Umekuja hapa kwa sababu gani?"

Abu Dharr: "Ninaweza kukuambia sababu endapo hutamwambia mtu

mwingine."

Ali: "Sema wazi chochote unachotaka kusema. Sitamwambia mtu yeyote."

Abu Dharr: Nimekuja kumuona mtu baada ya kupata taarifa kwamba mtu huyu anajiita yeye Mtume. Nilimtuma kaka yangu azungumze naye. Aliporudi hakunipa taarifa ya kuridhisha. Sasa, nimeamua kumuona mtu huyu mimi mwenyewe."

Ali: Umefika. Sasa ninakwenda pale alipo. Nifuate. Ingia popote nitakapoingia. Endapo nitaona hatari yoyote nitaanza kukiweka sawa kiatu changu, nikiwa nimesimama karibu na ukuta, na nikianza kufanya hivyo, wewe rudi."

2

MAISHA YA ABU DHARR

Abu Dharr anasema, "Ali alinipeleka hadi ndani ya nyumba. Niliona nuru katika umbo la mtu inaonekana hapo. Mara tu nilipo muona, nilivutiwa kwake na nikahisi ninataka kubusu miguu yake. Kwa hiyo, nilimsalimia Assalamu Alaykum." (Alikuwa mtu wa kwanza kumsalimia Mtume wa Uislamu kwa desturi ya Kiislamu, kabla ya kusilimu).

Alijibu salamu, akasema, "Waa Aliakum as Salam, wa rahmatullah

wa Barakatuh. Ndio Unataka nini?"

Nilijibu; "Nimekuja kuwako kwa moyo na imani."

Alinielekeza mambo fulani muhimu na akanitaka nikariri Kalimah

(Shahada) yaani (La ilaha illalah Muhammadun Rasulul lah) nilisoma

hivyo, na kwa hiyo nikaingia kwenye Uislamu.

Baada ya hapo, aliondoka kwenda Ka'abah. Alipofika hapo alipoona kundi kubwa la makafiri wa kabila la Quraishi, alisema kwa sauti kubwa, "Sikilizeni enyi Waquraishi nina shahidilia kwamba Mwenyezi Mungu ni Mmoja na Muhammad ni Mtume Wake."

Sauti hii iliwaogofya Quraishi na kuvunja sanamu lao la Lat na Uzza. Hisia za Quraishi kwamba heshima ya masanamu yao imeshushwa iliwatia wasiwasi sana.

Hatimaye watu walimzunguka Abu Dharr wakaanza kumpiga sana hadi akazirai. Ilibakia kidogo afe lakini Abbas bin Abd al-Mutalib alifika hapo ghafla. Alipoona kwamba mfuasi wa Muhammad alikaribia kufa, alilazimika kumlalia Abu Dharr.

Akasema: "Enyi watu! Nini kimewatokea ninyi? Munataka kumuua mtu mkubwa wa kabila la Bani Ghifar. Mmesahau kwamba nyinyi hufanya biashara na Bani Ghifar na huwa mnatembelea huko mara kwa mara. Hamliogopi kabila lake kabisa!"

Baada ya kusikia hayo, watu hao waliondoka hapo na Abu Dharr ambaye alikuwa anatoka damu, alinyanyuka na kwenda kwenye kisima cha zam zam.

Alihisi kiu sana kwa sababu ya majeraha makubwa na kutoka damu nyingi. kwa hiyo, kwanza alikunywa maji halafu akasafisha mwili

wake. Baada ya hapo alikwenda kwa Mtukufu Mtume huku akigumia. Mara tu Mtume alipomuona katika hali ile, alisikitika sana na akasema, "Abu Dharr! Umekula au kunywa chochote?"

Abu Dharr: "Bwana wangu! Nimeona nafuu kidogo baada ya kunywa

maji ya Zam zam."

Mtume: "Bila shaka maji hayo hutoa nafuu."

Baada ya hapo alimliwaza Abu Dharr na akampa chakula. Ingawa

Abu Dharr aliumia sana kwa sababu ya hotuba yake, bado hamasa ya

dini haikumruhusu aondoke kwenda kwao kimya kimya. Imani yake

ilimtaka awafanye Maquraishii waamini kwamba akili ya

mwanadamu hudharau ushirikina wa uchaji masanamu.

Aliondoka hapo akaenda kwenye eneo la Al-Ka'abah tena. Alisimama sehemu iliyoinuka na akaita kwa sauti ya ushupavu imara. "Enyi watu wa Quraishii! Nisikilizeni! Ninashahidilia kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu na ninashahidilia kwamba Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu."

Waliposikia hivyo wale wapotovu ambao waliona misingi ya miungu yao inatikiswa na ambao walikasirishwa sana na hotuba yake ya mwanzo, kwa mara nyingine waligutushwa na wakawa katika hali ya wasiwasi na wakageuka kuelekea upande inakotoka sauti na haraka sana walikusanyika na kumzunguka yeye. Walikuwa wanapiga kelele "Muueni huyu Ghifari haraka iwezekanavyo kwani yeye nia yake ni kuwatukana miungu wetu."

Mkusanyiko wote ulisema kwa sauti moja, Mueni Abu Dharr." Kwa hiyo walimpiga Abu Dharr hadi akazirai.

Abbas bin Abdul Muttalib alipoona hivi alijitokeza mbele na kumlalia Abu Dharr kama ilivyofanya jana yake, na akasema; "Enyi Quraishi!

Nini kimewatokeeni kwamba mnamuua mtu wa kabila la Ghifari ingawa mnao uhusiano mzuri na kabila lake na biashara yenu inaendelea vizuri kwa msaada wa kabila lake. Msiendelee kumpiga."

Baada ya kusikia haya, watu wote waliondoka na kumwacha Abu Dharr akiwa amepoteza fahamu. Alipopata fahamu, alikwenda kwenye kisima cha Zam zam! na baada ya kunywa maji alisafisha mwili wake uliokuwa umetapakaa damu.

Abdullah Subaiti ameandika kwamba ingawa Abu Dharr aliteseka sana kwa majeraha lakini hata hivyo aliwalazimisha Quraishi kuwa na maoni kwa mujibu wa ho tuba zake kwamba Uislamu ulikwisha enea kwa watu na uliwavutia sana.

Kwa ufupi Abu Dharr alinyanyuka kutoka kwenye kisima cha Zamzam na kwenda kwa Mtukufu Mtume. Mtume alipomuona Abu Dharr katika hali hiyo alisema, "Ewe Abu Dharr! Ulikwenda wapi na kwa nini umekuwa katika hali hii?" Abu Dharr alijibu, "Nilekwenda kwenye Ka'abah tena. Nilitoa ho tuba tena na nikatapakaa damu kwa kipigo. Sasa nimekuja kwako baada ya kuoga maji ya Zam zam." Mtume akasema; "Ewe Abu Dharr! Sasa ninakuamuru urudi nchini kwako mara moja. Nisikilize! Utakapofika nyumbani kwako, mjomba wako tayari atakuwa amekufa. Kwani hana mrithi mwingine isipokuwa wewe, wewe utakuwa mrithi wake na kuwa mmiliki wa rasilimali yake. Nenda ukatumie mali hiyo kwa kutangaza Uislamu. Baada ya muda mfupi nitakwenda na kuhamia Madina mji wa mitende. Wewe endelea kufanya kazi huko hadi nitakapohamia huko." Abu Dharr alisema, "Ndio! Bwana wangu vyema sana. Nitaondoka hivi karibuni na kuendelea kutangaza Uislamu." Sahih Bukhari, Sura ya Uislamu na Abu Dharr, chapa ya Misri, 1312 Hijiriya.

SURA YA TATU

Baada ya kuingia kwenye Uislamu, Abu Dharr aliondoka Makkah kwenda nchini kwake. Abdullah Subaiti ameandika kwamba Abu Dharr alipoondoka, alikuwa anabubujika imani, kamili, na alikuwa na furaha sana. Alifurahia sana kwamba Mwenyezi Mungu, alimwongoza kwenye imani ambayo imekubaliwa na waliotakasika na dhamira imeridhika nayo na akili inakaribisha kwa ukamilifu.

Aliendelea na safari hadi nchini kwake. Mtu wa kwanza kumsalimia alikuwa kaka yake Unais na pia alikuwa mtu wa kwanza kupata mwamko wa imani yake. Unais alikwenda kubusu miguu ya kaka yake na kusema, "Ewe ndugu yangu! Umepitisha siku nyingi sana Makkah sasa niambie ulichopata huko."

Abu Dharr alisema, "Unais! Nimefanya uamuzi wenye busara. Niliamua baada ya kutafakari sana kwamba lazima nikubali imani ya Muhammad! Ewe Unais! siwezi kukuambia kwamba nilipokutana na Muhammad na kumtazama uso wake, nilihisi kama vile kifua changu kilikuwa kinaongezeka. Moyo wangu ulijaa furaha na akili yangu ililewa imani. Mara nikakariri kalimah-shahada na kukubali Utume wake nilimwomba alifundishe vipengele vya imani. Kwa hiyo alinieleza kanuni za Uislamu. Ewe Unais ninakuomba kwa kweli na kwa moyo safi na nia njema uinamishe kichwa chako kwa unyenyekevu mbele ya Mwenyezi Mungu na uache kuabudu miungu hii iliyotengenezwa na mikono ya watu yenye asili ya mawe."

Aliposikia hivi, Unais alikaa chini huku akiwa ameinamisha kichwa chake na kuanza kufikiri. Alipatwa na hali kama vile umelewa. Unais alikumbuka mambo hayo yote aliyo yaona huko Makkah. Baada ya muda fulani alisema, "Ewe Ndugu! Akili yangu imethibitisha ukweli

wako na mantiki yangu inanieleza nikutii wewe. kwa hiyo sikiliza! Ninashahidilia kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu na ninakiri kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu."

Abu Dharr alifurahi sana kuona Unais anaikubali imani. Alimwambia: "Sasa twende kwa mama yetu." Wote wawili walikwenda kwa mama yao. Baada ya kumuamkia mama yao, Abu Dharr akasema, "Mama yangu mpendwa! Nakuomba unisamehe! Nimekuwa mbali na wewe kwa kipindi kirefu sana. Lakini, nimepata kitu cha nadra ambacho hakuna mtu aliye nacho hapa."

Mama Akamuuliza, "Kitu hicho ni kipi ambacho kinakubainisha wewe?" Abu Dharr alisema, "Hii ni tunu ya imani mama. Nilikutana na mtu huko Makkah ambaye uso wake uling'aa nuru ya uadilifu, hana wa kumlinganisha kwa uzuri wa tabia yake na ukarimu wake. "Yeye husema kweli tupu. Yeye husema kilicho sahihi. Hutenda haki. Maneno yake yanayo busara. Mama! Maadui zake pia humwita mkweli na mwaminifu. Huwaita watu wamwelekee Mwenyezi Mungu ambaye ni muumba wa mbinguni na ardhi na mpangiliaji wa kuweza kudumu kwa ulimwengu huu.

"Nimekubali kumuamini mtu huyu kwa kuvutiwa na mwelekeo wake, maneno yake na semi zake, na Unais pia amekuwa Muislamu. Tumekubali Upweke wa Mwenyezi Mungu na Utume wa Muhammad."

Mama yake Abu Dharr akasema: "Mwanangu, endapo ndio hivyo, mimi pia nina shahidilia kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu, na kukiri kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu."

Abu Dharr alitiwa moyo baada ya kaka yake na mama yake kuingia kwenye Uislamu na sasa alianza kutafakari jinsi ya kuwashawishi

watu wa kabila lake na kuwavuta waelekee kwenye njia iliyonyooka. Baada ya kufikiri sana Abu Dharr alitoka nje ya nyumba yake. Mama na kaka yake pia walikuwa naye. Baada ya kusafiri mwendo mfupi walipiga hema lao karibu na mahema ya watu wa kabila lao.

Usiku uliingia. Wasafiri hawa waliochoka walikuwa wamelala kwenye mahema yao walipohisi kwamba watu wengi wa kabila hilo waliokuwa pale walikuwa wanasimuliana hadithi wao kwa wao na kuelezea matukio mbali mbali. Walikuwa katika mazungumzo mfululizo.

Abu Dharr alipojaribu kusikiliza kwa siri walikuwa wanasema nini, alisikia kwamba walikuwa wanamsema yeye. Baada ya hapo watu waliondoka kutoka kwenye mahema yao na kwenda kwenye hema la Abu Dharr, akamwambia kaka yake, Unais, "Watu wa kabila letu wamekuja karibu na hema letu. Nenda nje ukawaone."

Unais alitoka nje mara moja. Aliwaona vijana wa kabila hilo walikuwa karibu na hema. Walikwenda karibu na hema ili wajue endapo Unais na Abu Dharr walikuwa hapo. Walimsalimia. Baada ya Unais kujibu salamu yao, aliwauliza sababu ya wao kutembelea hapo. Wakasema, "Tumekuja tu kukuona wewe na Abu Dharr."

Unais alirudi ndani na akamwambia Abu Dharr, "Vijana wa kabila letu wamekuja kutaka kujua hali ya safari."

Abu Dharr alisema, "Waambie waingie ndani. Nitazungumza nao. Inawezekana labda nikawasilimisha waanze kumuabudu Mwenyezi Mungu, Aliye Pekee."

Unais alitoka nje na akawaambia, "Ingieni ndani kwani kaka Abu Dharr anawaiteni."

Wote walikwenda kwa Abu Dharr. Mmojawao akasema, "Ewe Abu Dharr! Hatujakuona kwa kipindi kirefu na matokeo yake ni kwamba tunasikitika sana."

Abu Dharr akasema, "Wapendwa wangu vijana! Moyo wangu unayo mapenzi makubwa sana kwenu, na ninawahurumieni."

Mtu mmoja: "Abu Dharr! Ulikuwa wapi kwa muda mrefu hivi? Tumeshindwa kukuona kwa kipindi kirefu."

Abu Dharr: "Nilikwenda Makkah. Nilirudi siku chache zilizopita." Mtu wa pili: "Tunafurahi kwamba ulikwenda Makkah."

Abu Dharr: "Kama mambo yalivyo, nilikwenda Makkah, lakini sikutoa sadaka kwa Hubal wala sikuwasujudia Lat na Uzza. Vijana wangu! Kwa nini nifanye yote haya ambapo ninafahamu kwamba masanamu haya wala hayana uhai, ama kuweza kuumiza au kumnufaisha yeyote? Wala hayawezi kuona ama kusikia, ama kuzuia janga linaloweza kuwapata.

"Sikilizeni! Mimi nimekimbilia kwa Mwenyezi Mungu katika matendo yangu na mambo yangu yote. hakika Yeye ni Peke yake, hana mfano wala mshirika, na ninakiri kwa Mwenyezi Mungu ambaye ni Yeye peke yake anapaswa kuabudiwa, Yeye ni Muumbaji wa kila kitu na mwezeshaji wa kila kiumbe.

Ninawaomba njooni kwangu tuwe pamoja katika mpango wetu wa utekelezaji na mshahidilie Upweke wa Mwenyezi Mungu kama sisi" Waliposikia hivi, watu wote walianza kutetemeka. Mmoja wao

alisema kwa mshangao, "Ewe Abu Dharr! Unasema nini?" Abu Dharr: "Sikilizeni kwa yale ninayowaambieni ingawa siwezi kumuona Mwenyezi Mungu kwa macho yangu bado ninaweza kumuona Yeye kwa jicho langu la kiroho na sikilizeni! Inawezekanaje kitu chochote kinachotengenezwa na mikono ya mwanadamu kiwe na thamani ya kuabudiwa na binadamu? Si busara kuabudu masanamu yaliyotengenezwa kwa mawe na miti, na kuyaomba ili yatutimizie haja zetu.

"Watu wa kabila langu! mnajua kwamba masanamu haya hayana uwezo wowote. Wala hayawezi kuzuia uovu, ama kuwa na nguvu ya kupata manufaa?"

Baada ya kusikia ushawishi huu wa Abu Dharr, watu walianza kunong'onezana wao kwa wao.

Mmoja wao alisema; "Nimekwisha waambieni kwamba huko Makkah, mtu amejitokeza, anajiita yeye ni Mtume na anawaita watu kumwabudu Mwenyezi Mungu Mmoja. Abu Dharr amekutana na mtu huyu, na mahubiri ya mtu huyu yamesisimua sana hivyo kwamba fikra zozote anazozitoa Abu Dharr ni za mtu huyo."

Mtu mwingine akasema; "Hali ni mbaya sana. Sasa tupo hatarini ambayo inatujia kupitia kwa Abu Dharr na mahubiri yake. Tunadhani kwamba endapo ataendelea kuhubiri namna hii, tofauti zitajitokeza kwenye kabila letu na maisha yetu yataharibika. Ni vema twende kwa mtemi wetu Khafaf, tumwelekeze hatari zote zinazoweza kujitokeza, na tumsisitizie na alipatie jambo hili kipaumbele ili tuweze kukabiliana nalo."

Vijana wa kabila la Ghifari waliondoka nyumbani kwa Abu Dharr na walikwenda kumwona Khafaf. Wakati wapo njiani walibadilishana

mawazo wao kwa wao. Mmoja wao alisema, "Abu Dharr ameanzisha ghasia kubwa."

Mwingine akasema, "Itakuwa aibu kubwa sana kwetu kama tutaifumbia macho dhambi hii kubwa ya Abu Dharr. Anaifanyia ufisadi dini yetu waziwazi na kukebehi miungu yetu." Mtu wa tatu akasema, "Ni wajibu wetu kumfukuza kutoka kwenye kabila letu bila kuchelewa hata kidogo, kwa sababu kama tukichelewa kumtenga katika kipindi kifupi tu, atawaelemea vijana wetu, wanawake zetu, watumwa wetu na kuwatia mawazo yake maovu akilini mwao. Endapo inatokea hivyo, tutapata hasara kubwa sana."

Mtu wa nne akasema, "Maoni yako ni sahihi. Lakini, nani atamfunga paka kengele? Huyu ni mtu mashuhuri wa kabila na ni mzee wa kaya. Ninaona kwamba hata Unais anayo mawazo haya haya, na yeye pia ni mtu mwenye kuheshimiwa."

Mtu wa tano akasema, "Hakuna haja ya wasi wasi. Njooni tukamtaarifu Khafaf. Tunao uhakika kwamba Khafaf na watu wengine waungwana wa kabila ndio watakao mfukuza kutoka kwenye kabila."

Mtu wa sita akasema, "Ninatafakari kuhusu mawazo yao. Sina uhakika kama wataweza kuwabadili. Inawezekana kwamba wao ndio watakao badilika na kwenda kwenye njia iliyo nyooka tusijisumbue, lakini na tutafakari kuhusu dini yao. Nisikilizeni! Ninaona kuna ukweli kwenye imani yao. Hata hivyo karibu tutafika kwa mtemi Khafaf. Baada ya mazungumzo yetu na yeye, tunategemea kufikia uamuzi wenye msimamo."

Kwa ufupi, wakizungumza pamoja, watu hawa walifika nyumbani kwa mtemi wa kabila la Ghifar na wakamwambia, "Tumetoka kwa Abu Dharr kuja kwako."

Khafaf: "Abu Dharr amerudi kutoka safari yake ya kutoka Makkah?" Mtu mmoja akasema, "Bwana, Abu Dharr ameasi. Aliwabeza miungu wetu. Anasema kwamba yupo mtu ameteuliwa kuwa Mtume. Kazi yake ni kuwaita watu waende kumuabudu Mungu Mmoja na pia kufundisha mambo mazuri. Abu Dharr haridhiki bila kukubali utume wa mtu huyu na kuendelea na msimamo huo, lakini wakati wote anahubiri kwa watu na kuwaita wote wengine waende kwa Mtume huyo na Mungu wake.

Khafaf aliposikia, alisema, "inasikitisha kuona kwamba Abu Dharr, anawaacha miungu wote, na kutangaza kumuabudu Mungu Mmoja. Ni uovu mkubwa sana na kutia kinyaa.

Ninaona kwamba jambo hili litachochea vurugu kubwa katika kabila letu, na matokeo yake kabila litaangamia. Enyi vijana wangu! Msifanye haraka lakini nipeni, muda wa kutafakari kuhusu jambo hili la Abu Dharr."

Baada ya vijana hao kuondoka na kurudi makwao, Khafaf mtemi wa kabila, alianza kufikiri kwa nini wote walikuwa wanasema kwa kumpinga Abu Dharr. Aliendelea kutafakari usiku wote akiwa kitandani kwake. Hali ilimkanganya sana na hakuweza kufanya msimamo hasa. Lakini akili yake ilikuwa na fikra nzito kuhusu maneno yaliyosemwa na Abu Dharr. Saa nyingi zilipita bila kupata usingizi, na alikuwa anafumba macho yake.

Mtemi Khafaf pia alikumbuka hotuba ya mwanafalsafa wa Kiarabu, Qays bin Saidah, pale sokoni. Alisema kwamba Muumbaji wa ulimwengu bila shaka ni Mmoja na ni Yeye tu ndiye anaye stahiki kuabudiwa. Aliunga mkono kikamilifu maoni ya Abu Dharr kwenye hayo mahubri yake ya kusifika na pia alitamka kwamba fikra za Warqa bin Naufal, Zayd binAmr, Uthman bin Hoverath na Abdallah bin Hajash kuelekea kwenye imani ya Abu Dharr.

Alikuwa katika hali hii ya kustaajabisha ambapo akili yake ilimuongoza na akajisemea mwenyewe, 'Naam! Abu Dharr yu sahihi kwa sababu Qays bin Saida amemuunga mkono na ninao uhakika kwamba Qays hawezi akashindwa kuelewa wala kukubali itikadi yoyote ya uongo. Bila shaka, lazima atakuwepo muongozaji wa dunia hii, na lazima pawepo na nguvu yenye uwezo wa kuendesha mpangilio wote wa ulimwengu na ni dhahiri kwamba miungu wetu wa mawe na miti hawana kabisa uwezo kama huu. Ee Mungu wa Abu Dharr! Tuongoze na utukomboe kutoka kwenye uovu huu na utuweke kwenye njia ya haki."

Wakati ambapo Khafaf alikuwa anafanya uamuzi wake muhimu, siku ilipambazuka hadi jua lilionekana angani pamoja na kuenea kwa mwanga wa jua, pia habari zilizidi kuenea kwamba Abu Dharr, kaka yake na mama yake wote wamerudi kutoka Makkah na wamemuabudu Mungu Mmoja tu.

Pamoja na kuenea habari hizi hasira ilichochewa. Watu walianza kumlaani Abu Dharr na kusema, 'Amepata kichaa na hawezi kuelewa kwamba haya masanamu yetu hutuponya maradhi, yanatupatia riziki na kutulinda. Abu Dharr ni mtu wa ajabu ambaye anatuita twende kwa mungu asiyeonekana! Inaonyesha kama vile Abu Dharr anataka kuanzisha vurumai na matatizo miongoni mwa vijana wetu na kuwapotosha watoto wetu na wanawake wetu. Hakika mtu huyu ni muongo na madai yake si sahihi. Lazima afukuzwe kutoka kwenye kabila."

Mmojawao akasema, "Kwa nini! Unawezaje kuelezea wazo la kumfukuza mtu huyu? Itafanyikaje? Hapana , kamwe! Haiwezekani kutokea. Huyu ni mtu jasiri katika kabila letu."

Baada ya mazungumzo haya watu hao waliamua kutaka wasikilizwe na wazee kuhusu suala hili. Kufuatana na uamuzi wao, waliwaendea

wazee wao kushughulikia jambo hili. Wazee wao waliamua kulipeleka jambo hili la Abu Dharr kwa mtemi. Kwa hiyo, wote walikwenda kwa Khafaf.

Mtemi wa kabila alimtuma mtumwa wake haraka aende kumwita Abu Dharr. Mtumwa huyo alipofika nyumbani kwa Abu Dharr alisema, "Abu Dharr! Wewe na Unais mnaitwa na Mtemi."

Abu Dharr akajibu kwamba alikuwa tayari kwenda kwa mtemi. Mtumwa alipoondoka, Abu Dharr alichukua upanga wake na kuhifadhi kwenye mkanda na alimwambia kaka yake, Unais, "Njoo; twende kwa Khafaf!"

Unais: "Ewe kaka! Nimesikia mambo mabaya yanazungumzwa na watu kuhusu wewe. Nina hofu huu mkutano wetu unaweza usiwe na manufaa, jambo lisilotegemewa linaweza kutokea badala ya mategemeo yetu."

Abu Dharr: "Hapana, siyo. Namjua Khafaf vizuri sana. Ni mtu mwenye hekima. Mwenyezi Mungu amempa hekima. Ni mtu mwenye akili sana miongoni mwa kabila letu."

Ndugu hawa wawili waliendelea kuzungumza hadi wakafika kwa Khafaf. Hapo waliona kwamba watu maarufu wa kabila hilo walikuwa wamekaa kumzunguka Khafaf. Akawaamkia wote Abu Dharr akasema, "Salaamu Alaykum " (Amani iwe kwenu).

Waliposikia maamkizi ya Abu Dharr kwa jinsi ya Kiislamu, wazee wa kabila hilo walikasirika na walisema kwa hasira; "Salamu gani hii ambayo hatujawahi kuisikia kamwe." Halafu mmojawao akasema "Inasikitisha. Hatujui Abu Dharr anakoelekea."

Mtu mwingine akasema, "Hebu mtazame. Amekaa na upanga wake, na hana heshima kwa mtemi." Mtu wa tatu akasema, maneno yako ni sahihi. Lakini, huyu ni mpanda farasi wa kabila letu na watu jasiri wakati wote huwa tayari kwa lolote."

Abu Dharr akasema, "Silikizeni! Ninawaheshimu nyinyi kwa sababu ni watu maarufu wa kabila letu, ambao mnastahili kujivuniwa na kuwaenzi. Salaamu niliyo wapeni ni Salamu ya Kiislamu."

4

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA TISA

وَوَاعَدْنَا مُوسَىٰ ثَلَاثِينَ لَيْلَةً وَأَتْمَمْنَاهَا بِعَشْرٍ فَتَمَّ مِيقَاتُ رَبِّهِ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً وَقَالَ مُوسَىٰ لِأَخِيهِ هَارُونَ اخْلُفْنِي فِي قَوْمِي وَأَصْلِحْ وَلَا تَتَّبِعْ سَبِيلَ الْمُفْسِدِينَ ﴿١٤٢﴾

142. Na tulimwahidi Musa masiku thalathini na tukayazitimiza kwa kumi; ndipo ikatimia miadi ya Mola wake siku arubaini. Na Nabii Musa akamwambia ndugu yake Harun: Shika mahali pangu katika watu wangu na utengeneze wala usifu- ate njia ya waharibifu.

وَلَمَّا جَاءَ مُوسَىٰ لِمِيقَاتِنَا وَكَلَّمَهُ رَبُّهُ قَالَ رَبِّ أَرِنِي أَنظُرْ إِلَيْكَ قَالَ لَن تَرَانِي وَلَـٰكِنِ انظُرْ إِلَى الْجَبَلِ فَإِنِ اسْتَقَرَّ مَكَانَهُ فَسَوْفَ تَرَانِي فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُ لِلْجَبَلِ جَعَلَهُ دَكًّا وَخَرَّ مُوسَىٰ صَعِقًا فَلَمَّا أَفَاقَ قَالَ سُبْحَانَكَ تُبْتُ إِلَيْكَ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٤٣﴾

143. Na alipofika Musa kwenye miadi yetu Na Mola wake akamsemeza, alisema: Mola wangu nionyeshe nikutazame. Akasema: Hutaniona, lakini tazama jabali, kama litakaa pahali pake ndipo utaniona. Basi Mola wake alipojionyesha kwa jabali alilifanya lenye kuvunjika vunjika, na Musa akaanguka hali amezimia. Alipozinduka alisema: kutakasika ni kwako! Natubu kwako na mimi ni wa kwanza wa wanaoamini.

قَالَ يَا مُوسَىٰ إِنِّي اصْطَفَيْتُكَ عَلَى النَّاسِ بِرِسَالَاتِي وَبِكَلَامِي فَخُذْ مَا آتَيْتُكَ وَكُن مِّنَ الشَّاكِرِينَ ﴿١٤٤﴾

144. Akasema: Ewe Musa! Mimi nimekuteua kwa watu kwa ujumbe wangu na kwa kusema nawe kwangu; basi yashike ninayokupa, na uwe miongoni mwa wanaoshukuru.

وَكَتَبْنَا لَهُ فِي الْأَلْوَاحِ مِن كُلِّ شَيْءٍ مَّوْعِظَةً وَتَفْصِيلًا لِّكُلِّ شَيْءٍ فَخُذْهَا بِقُوَّةٍ وَأْمُرْ قَوْمَكَ يَأْخُذُوا بِأَحْسَنِهَا سَأُرِيكُمْ دَارَ الْفَاسِقِينَ ﴿١٤٥﴾

145. Na tukamwandikia katika mbao kila kitu mawaidha na ufafanuzi wa kila jambo. Basi yashike kwa imara na uwaamrishe watu wako washike mazuri yake zaidi, Nitawaonyesha makao ya wafasiki.

Aya 142 – 145

MAANA

Na tulimwahidi Musa masiku thalathini na tukayazitimiza kwa kumi; ndipo ikatimia miadi ya Mola wake siku arubaini.

Nabii Musa(a.s) alimtaka Mola wake amteremshie Kitab atakachowaongozea watu kwenye yale wanayoyahitajia katika mambo ya dini yao. Ndipo Mwenyezi Mungu (s.w.t) akamwahidi kuteremshia Kitab baada ya siku thalathini, na utaendelea ushukaji wake kwa siku kumi. Kwa ujumla itakuwa muda wa miadi na wa kushuka ni siku arubaini.

Hapa tumefafanua baada ya kueleza kwa ujumla kwenye Juz. 1 (2:51).

Na Musa akamwambia ndugu yake Harun: Shika mahali pangu katika watu wangu na utengeneze wala usifuate njia ya waharibifu.

Nabii Musa alipoondoka alimwachia mahali pake ndugu yake Harun kwa Wana wa Israel; akampa nasaha kusimamia mambo yao na kuyatengeneza. Akamhadharisha na tabia zao zinazopondokea zaidi kwenye ufisadi. Ni jana tu walipokodolea macho ibada ya masanamu mpaka Nabii Musa akawaambia kuwa ni watu wajinga.

Harun akakubali nasaha kwa moyo mkunjufu, kama anavyokubali nasaha kaimu kiongozi mwenye ikhlasi kutoka kwa kiongozi wake mwaminifu.

Na alipofika Nabii Musa kwenye miadi yetu ambayo aliiweka Mwenyezi Mungu (s.w.t) kumpa Tawrat,

Na Mola wake akamsemeza bila ya kumwona kwa sababu:

وَمَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُكَلِّمَهُ اللَّـهُ إِلَّا وَحْيًا أَوْ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ أَوْ يُرْسِلَ رَسُولًا ﴿٥١﴾

“Haikuwa kwa mtu aseme na Mwenyezi Mungu ila kwa wahyi au kwa nyuma ya pazia au kumtuma mjumbe” (42:51)

Nabii Musa alisema:Mola wangu nionyeshe nikutazame.

Baadhi ya maulamaa wanasema kuwa Nabii Musa hakumwomba Mola wake kumwona kwa ajili yake isipokuwa ni kwa ajili ya watu wake. Lakini hii inapingwa na kauli yake Nabii Musa pale aliposema:

Kutakasika ni kwako, na natubu kwako.

Vyovyote iwavyo ni kwamba Nabii Musa alitaka kuona, ni sawa iwe ni kwa ajili yake au kwa ajili ya wengine, sisi hatuoni ubaya wowote katika ombi hili, kwa sababu nafsi ya mtu ina hamu ya kutaka kujua yanayokuwa na yasiyokuwa hasa kuona kile ambacho kitazidisha utulivu wa nafsi.

Ibrahim(a.s) alitaka mfano wa hayo. Angalia Juz.3 (2:260).

Akasema: Hutaniona.

Kwa sababu kumwona Mwenyezi Mungu ni muhali. Tumeyazungumza hayo kwa ufafanuzi katika kufasiri Juz. 1(2:51).

Lakini tazama jabali, kama litakaa mahali pake utaniona.

Nabii Musa aligeuka kwenye jabali ili amwone Mwenyezi Mungu, mara akaanguka chini na hakuona chochote. Mwenyezi Mungu (s.w.t) alifanya hivi ili kumfahamisha Nabii Musa(a.s) kwamba kumwona Mwenyezi Mungu hakuwezekani kwake wala kwa mwingine.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliuwekea sharti uwezekano wa kuonekana kwake kwa kutulia mahali jabali na jabali halikutulia, Kwa hiyo kumwona Mwenyezi Mungu hakuwezekani.

Mfumo huu alioutumia Mwenyezi Mungu hapa ni kama ule wa kusema: Nitafanya hivi kunguru akiota mvi, Au akipita ngamia kwenye tundu ya sindano.

Basi Mola wake alipojionyesha kwenye jabali alilifanya lenye kuvunjika vunjika.

Yaani ilipodhihiri amri ya Mola wake; sawa na kauli yake Mwenyezi Mungu:

وَجَاءَ رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا ﴿٢٢﴾

“Akaja Mola wako na Malaika (wamejipanga) safu kwa safu.” (89:22).

Yaani ikaja amri ya Mola wako.

Na Musa akaanguka chini amezimia.

Akawa hana fahamu kwa kishindo cha ghafla, Mwenyezi Mungu akamhurumia akazinduka.

Alipozinduka alisema: Kutakasika ni kwako! Natubu kwako. Kwa kukuomba kukuonana mimi ni wa kwanza wa wanaoamini.

Kwa sababu wewe ni mtukufu zaidi ya kuonekana kwa jicho.

Makusudio ya wa mwanzo sio kulingana na hisabu ya wakati; isipokuwa makusudio yake ni uthabiti na kutilia mkazo.

Akasema: Ewe Musa! Mimi nimekuteua kwa watu kwa ujumbe wangu na kwa kusema nawe kwangu; basi yashike ninayokupa, na uwe miongoni mwa wanaoshukuru.”

Baada ya Nabii Musa kunyenyekea kwa muumba wake, Mwenyezi Mungu alimkumbusha neema yake, kubwa zaidi ni Utume na kuzungumza na Mwenyezi Mungu. Makusudio ya watu ni watu wa zama zake, kwa dalili ya kauli yake: Kwa ujumbe wangu. Kwani Mwenyezi Mungu aliwachagua Mitume wengi kabla ya Nabii Musa na baada yake.

Ama kuhusika kwake na kuzungumza naye hakuna dalili ya ubora zaidi. Ikiwa kunafahamisha ubora wowote basi kupelekewa roho mwaminifu kwa mwisho wa Mitume na bwana wa Mitume ndio daraja ya juu na bora zaidi.

Na tukamwandikia katika mbao kila kitu mawaidaha na ufafanuzi wa kila jambo.

Makusudio ya mbao ni Tawrat kwa sababu ndiyo aliyoteremshiwa Nabii Musa, ndani yake mna mawaidha na upambanuzi wa hukumu.

“Kila jambo ni neno la kiujumla, lakini limekusudia mahsusi; yaani kila linalofungamana na maudhui ya risala miongoni mwa mawaidha, hukumu, misingi ya itikadi, kama vile kumwamini Mwenyezi Mungu, Mitume yake na siku ya mwisho, na hukumu za sharia, kama halali na haramu. Kwa hiyo kauli yake: Mawaidha na maelezo ni ubainifu wa tafsiri ya kauli yake kila jambo. Kwa sababu makusudio ya maelezo ni kubainisha hukumu za kisharia.

Basi yashike kwa imara.

Yaani ichunge Tawrat na uitumie kwa ukweli wa nia.

Na uwaamrishe watu wako washike mazuri yake zaidi.

Kila aliloliteremsha Mwenyezi Mungu ni zuri, lakini kuna yaliyo mazuri zaidi. Mwenyezi Mungu mtukufu anasema: “Na fanyeni wema, Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema.”

Nitawaonyesha makao ya wafasiki.

Yaani fasiki na dhalimu atafikwa na majanga. Haya ndiyo niliyoyafahamu kutokana na jumla hii kabla ya kupitia tafsir, Baada ya kuzipita nikakuta kauli kadhaa. Miongoni mwazo ni kwamba Mwenyezi Mungu atawaonyesha makao ya Firauni na watu wake baada ya kuangamizwa kwao. Nyingine inasema kuwa atawaonyesha ardhi ya Sham iliyokuwa mikononi mwa waabudu mizimu wakati huo.

سَأَصْرِفُ عَنْ آيَاتِيَ الَّذِينَ يَتَكَبَّرُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَإِن يَرَوْا كُلَّ آيَةٍ لَّا يُؤْمِنُوا بِهَا وَإِن يَرَوْا سَبِيلَ الرُّشْدِ لَا يَتَّخِذُوهُ سَبِيلًا وَإِن يَرَوْا سَبِيلَ الْغَيِّ يَتَّخِذُوهُ سَبِيلًا ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَكَانُوا عَنْهَا غَافِلِينَ ﴿١٤٦﴾

146. Nitawatenga na ishara zangu wale wanaofanya kiburi katika ardhi pasipo haki. Na wakiona kila ishara hawaiamini; na wakiona njia ya uongofu hawaishiki kuwa ndiyo njia; lakini wakiona njia ya upotofu wanaishika kuwa ndiyo njia. Hayo ni kwa sababu wao wamezikadhibisha ishara zetu na wameghafilika nazo.

وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَلِقَاءِ الْآخِرَةِ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ هَلْ يُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٤٧﴾

147. Na wale waliozikadhibisha ishara zetu na mkutano wa akhera, amali zao zime- poromoka. Kwani watalipwa isipokuwa yale waliyokuwa wakiyatenda?

وَاتَّخَذَ قَوْمُ مُوسَىٰ مِن بَعْدِهِ مِنْ حُلِيِّهِمْ عِجْلًا جَسَدًا لَّهُ خُوَارٌ أَلَمْ يَرَوْا أَنَّهُ لَا يُكَلِّمُهُمْ وَلَا يَهْدِيهِمْ سَبِيلًا اتَّخَذُوهُ وَكَانُوا ظَالِمِينَ ﴿١٤٨﴾

148. Na baada yake watu wa Musa walimfanya ndama kutokana na mapambo yao, kiwiliwili kilichokuwa na sauti, Je, hawakuona kwamba huyo hasemi nao wala hawaongozi njia? Walimfanya na wakawa wenye kudhulumu.

وَلَمَّا سُقِطَ فِي أَيْدِيهِمْ وَرَأَوْا أَنَّهُمْ قَدْ ضَلُّوا قَالُوا لَئِن لَّمْ يَرْحَمْنَا رَبُّنَا وَيَغْفِرْ لَنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿١٤٩﴾

149. Na walipojuta na wakaona kwamba wamekwishapotea walisema: Kama Mola wetu hataturehemu na kutusamehe bila shaka tutakuwa miongoni mwa waliopata hasara.

NITAWAEPUSHIA AYA ZANGU

Aya 146 – 149

MAANA

Nitawatenga na ishara zangu wale wanaofanya kiburi katika ardhi pasipo haki.

Wenye kufanya kiburi katika ardhi ni wale wanaopinga haki na wasiotaka kutawaliwa nayo. Kusema kwake bila ya haki ni kwa ufafanuzi, sio kwa kuvua; sawa na kusema: “Na wakiwaua mitume bila ya haki.”

Neno Aya katika Qur’an mara nyingine hutumia kuwa ni Aya zenye misingi ya itikadi na hukumu ya sharia na mfano wake. Mara nyingine hutumi- ka kuwa ishara yaani hoja na dalili zenye kuthibitisha uungu na utume.

Ikiwa makusudio ni maana ya kwanza katika Aya hii tunayoifasiri, basi maana yatakuwa kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) anazihifadhi Aya na kuzilinda zisipotolewe; sawa na kauli yake: “Hakika sisi ndio tuliouteremsha ukumbusho huu na hakika ndio tutakaoulinda”

Na ikiwa makusudio ni maana ya pili, yaani ishara kwa maana ya dalili na hoja, basi maana ni kwamba baada ya wapinzani kujiepusha nazo na kuacha kuzisikiliza, basi Mwenyezi Mungu ataachana nao, wala hatawategemeza kwenye imani. Tumekwisha elezea hilo mara kadhaa; kama vile katika kufasiri Juz.5 (4:88).

Na wakiona kila ishara hawaiamini; na wakiona njia ya uongofu hawaishiki kuwa ndiyo njia; lakini wakiona njia ya upotofu wanaishika kuwa ndiyo njia. Hayo ni kwa sababu wao wamezikadhibisha ishara zetu na wameghafilika nazo.

Huu ni ubainifu wa hakika ya wenye kiburi na sababu inayowajibisha kiburi chao vilevile. Ama hakika yao ni kuwa wao hawajizuilii na uovu wala hawapondokei kwenye uongofu.

Sababu inayowajibisha hilo ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewaletea hoja na dalili; akawataka wazichunguze, wazizingatie na wazitumie vile inavyotakikana, wakakataa na wakaendelea kuzipinga tena bila ya kuzichunguza. Lau kwamba wao wangeliziitikia na kuzichunguza dalili hizo kungeliwapelekea kuamini na kuikubali haki; wala wasingelikua na kiburi na kufanya ufisadi katika nchi.

Na wale waliozikadhibisha ishara zetu na mkutano wa akhera, amali zao zimeporomoka. Kwani watalipwa isipokuwa yale waliyokuwa wakiyatenda?

Kila asiyemwamini Mwenyezi Mungu na kukutana na Mola wake, basi yeye ni katika wale watakaoangamia kesho na yote yale aliyokuwa akijifaharisha nayo yatakuwa si lolote. Hayo ni malipo ya ukafiri wake na inadi yake.

Yamenipendeza yale aliyoyasema mfasiri mmoja Mwenyezi Mungu amughufirie na amrehemu, namnukuu: “Kuporomoka amali kunachukuliwa kama wanavyosema: ‘Ameporomokaa ngamia.’ ikiwa amekula mmea wenye sumu na tumbo lake likafura kisha akafa.

Hiyo ndiyo sifa ilivyo kwa batili inayowatokea wenye kukadhibisha ishara za Mwenyezi Mungu na kukutana na akhera, Mwongo hufura mpaka watu wanamdhania kuwa ni mkubwa mwenye nguvu, kisha huporomoka, kama alivyoporomoka yule ngamia, aliyekula mmea wa sumu.”

Na baada yake watu wa Musa walimfanya ndama kutokana na mapambo yao, kiwiliwili kilichokuwa na sauti.

Imetangulia kuelezwa katika Aya 142 kuwa Nabii Musa(a.s) alikwenda kwa miadi ya Mola wake, na kwamba yeye alimpa ukaimu nduguye Harun kwa watu wake. Vilevile imeelezwa katika Aya 138 kwamba Wana wa Israel baada ya kupita bahari walimtaka Nabii Musa awafanyie sanamu watakayoiabudu; si kwa lolote isipokuwa tu wameona ni vizuri waabudu masanamu.

Kwa hivyo mara tu Nabii Musa alipokuwa mbali nao waliitumia nafasi hiyo; Msamaria (Samiri): akakusanya mapambo ya wanawake akaten- geneza ndama; akatengeneza katika umbo ambalo liliweza kutoa sauti ya ndama.

Akawaambia huyu ni Mola wenu na Mola wa Musa; wakaingilia kumwabudu. Harun aliwakataza, lakini hakuweza kuwazuia, na hawakum- sikiliza isipokuwa wachache, Yametangulia kudokezwa hayo katika kufasiri Juz, 1 (2: 51), Pia yatakuja tena maelezo.

Aya hii tuliyo nayo, inatilia nguvu yale tuliyoyakariri katika Juzuu ya kwanza na ya pili, kuwa Israeli haithibiti ila kwenye misingi ya matamanio na hawaa; ikiwa ni kweli kuwa matamanio ni misingi.

Je, hawakuona kwamba huyo hasemi nao wala hawaongozi njia? Walimfanya na wakawa wenye kudhulumu.

Haya ndiyo mantiki ya kimaumbile na akili ambayo inakataa mtu amwabudu Mungu aliyemtengeneza kwa mkono wake, lakini waisraili hawana akili wala maumbile au dini.

Na walipojuta na wakaona kwamba wamekwishapotoea walisema: Kama Mola wetu hataturehemu na kutusamehe bila shaka tutakuwa miongoni mwa waliopata hasara.

Hii ndiyo sifa nzuri pekee na ndiyo ya kwanza na ya mwisho, iliyosajiliwa na Qur’an kwa waisrael kwa ujumla, bila ya kuangalia uchache wa wachache waliomwamini Nabii Musa hadi mwisho.

Baadhi ya Wafasiri wamechukulia dhahiri toba ya Bani Israel kwamba wakati huo ilikuwa ni masalia ya maandalizi ya wema, kisha masalia hayo yakaenda; wala haikubaki athari yoyote kwao ya kuonyesha kujiandaa kwa kheri. Kuchukulia huku hakuko mbali na ukweli na kunaashiriwa na Aya isemayo:

ثُمَّ قَسَتْ قُلُوبُكُم مِّن بَعْدِ ذَٰلِكَ فَهِيَ كَالْحِجَارَةِ أَوْ أَشَدُّ قَسْوَةً ﴿٧٤﴾

“Kisha nyoyo zenu zikawa ngumu baada ya hayo, zikawa kama mawe au ngumu zaidi” Juz.1(2: 74)

Aya hii ni baada ya kisa cha ng’ombe ambacho kilitokea baada ya kuabudu ndama.

5

وَلَمَّا رَجَعَ مُوسَىٰ إِلَىٰ قَوْمِهِ غَضْبَانَ أَسِفًا قَالَ بِئْسَمَا خَلَفْتُمُونِي مِن بَعْدِي أَعَجِلْتُمْ أَمْرَ رَبِّكُمْ وَأَلْقَى الْأَلْوَاحَ وَأَخَذَ بِرَأْسِ أَخِيهِ يَجُرُّهُ إِلَيْهِ قَالَ ابْنَ أُمَّ إِنَّ الْقَوْمَ اسْتَضْعَفُونِي وَكَادُوا يَقْتُلُونَنِي فَلَا تُشْمِتْ بِيَ الْأَعْدَاءَ وَلَا تَجْعَلْنِي مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿١٥٠﴾

150. Aliporudi Musa kwa watu wake naye ameghadhibika na kuhuzunika. Akasema: Ni uovu ulioje mlionifanyia nyuma yangu! Je, mmeitangulia amri ya Mola wenu na akazitupa mbao na akamkata kichwa ndugu yake akimvuta kwake. Akasema: Ewe mtoto wa mama yangu! Hakika watu hawa wamenidharau na wakakaribia kuniua. Basi usiwafurahishe maadui juu yangu wala usinifanye pamoja na watu madhalimu.

قَالَ رَبِّ اغْفِرْ لِي وَلِأَخِي وَأَدْخِلْنَا فِي رَحْمَتِكَ وَأَنتَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ ﴿١٥١﴾

151. Akasema: Mola wangu! Nisamehe mimi na ndugu yangu na utuingize katika rehema yako na wewe ni mwenye kurehemu kushinda wote wenye kurehemu.

إِنَّ الَّذِينَ اتَّخَذُوا الْعِجْلَ سَيَنَالُهُمْ غَضَبٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَذِلَّةٌ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُفْتَرِينَ ﴿١٥٢﴾

152. Hakika wale walioabudu ndama, itawapata ghadhabu kutoka kwa Mola wao na madhila katika maisha ya dunia, Na hivyo ndivyo tunavyowalipa wazushi.

وَالَّذِينَ عَمِلُوا السَّيِّئَاتِ ثُمَّ تَابُوا مِن بَعْدِهَا وَآمَنُوا إِنَّ رَبَّكَ مِن بَعْدِهَا لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٥٣﴾

153. Na wale waliotenda maovu, kisha wakatubia baada yake na wakaamini, hakika Mola wako baada ya hayo ni mwenye kusamehe mwenye kurehemu.

وَلَمَّا سَكَتَ عَن مُّوسَى الْغَضَبُ أَخَذَ الْأَلْوَاحَ وَفِي نُسْخَتِهَا هُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلَّذِينَ هُمْ لِرَبِّهِمْ يَرْهَبُونَ ﴿١٥٤﴾

154. Na ilipomtulia ghadhabu Musa, aliziokota zile mbao na katika maandiko yake mna uongozi na rehema kwa wanaomwogopa Mola wao.

ALIPORUDI MUSA KWA WATU WAKE

Aya 150-154

MAANA

Aliporudi Musa kwa watu wake naye ameghadhibika na kuhuzunika.

Nabii Musa(a.s) alipokuwa mlimani akizungumza na Mola wake mtuku- fu, alipewa habari na Mola wake kuwa watu wake wameabudu ndama baada yako; kama inavyofahamisha Aya isemayo:

قَالَ فَإِنَّا قَدْ فَتَنَّا قَوْمَكَ مِن بَعْدِكَ وَأَضَلَّهُمُ السَّامِرِيُّ ﴿٨٥﴾ فَرَجَعَ مُوسَىٰ إِلَىٰ قَوْمِهِ غَضْبَانَ أَسِفًا ﴿٨٦﴾

“Akasema: Sisi tumewatia mtihani watu wako bada yako na Msamaria amewapoteza. Nabii Musa akarudi kwa watu wake kwa ghadhabu na kusikitika.” (20:85-86).

Ghadhabu ilidhihiri kwa kusema:Ni uovu ulioje mlionifanyia nyuma yangu! Je, mmeitangulia amri ya Mola wenu.

Aliwaacha kwenye Tawhid, lakini aliporudi aliwakuta kwenye shirk.

Ama amri ya Mola wao ambayo hawakuingoja ni kumngoja Nabii Musa siku arubaini.

Hii inafahamishwa na Aya isemayo:

أَفَطَالَ عَلَيْكُمُ ﴿٨٦﴾

“Je, umekuwa muda mrefu kwenu?” (20:86).

Kama ambavyo ghadhabu yake ilidhihiri kwa kauli, Vilevile ilidhihiri kwa vitendo:

Na akazitupa mbao na akamkamata kichwa ndugu yake akimvuta kwake.

Wamesema baadhi ya maulama kuwa Nabii Musa alitupa Tawrat nayo ina jina la Mwenyezi Mungu na akamvuta nduguye Harun naye ni mja mwema. Imekuwaje na Nabii Musa ni ma’sum? Baada ya kujiuliza huku wakaanza kuleta taawili na kutafuta sababu.

Ama sisi hatu hatuleti taawili wala kutafuta sababu, bali tunayaacha maneno na dhahiri yake. Kwa sababu isma haibadilishi tabia ya maumbile ya binadamu na kumfanya ni kitu kingine wala haimuondolei sifa ya kuridhia na kukasirika hasa ikiwa ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu; tena ikiwa ni ghafla kama ilivyomjia Nabii Musa(a.s) .

Amekaa na watu siku nyingi akiwafundisha tawhid na dini ya Mwenyezi Mungu, kiasi cha kutulia imani yao; halafu ghafla tu waache yote na waingie kwenye shirki bila ya sababu yoyote ya maana.

Wengine wamesema kuwa Nabii Musa alikuwa mkali na Haruna alikuwa mpole. Sisi tunasemaNabii Musa alikuwa mwenye azma kubwa, mwenye nguvu ya alitakalo na mwenye kujiamini; na Haruna naye alikuwa chini kidogo ya Nabii Musa kulingana na masilahi.

Akasema: Ewe mtoto wa mama yangu! Hakika watu hawa wamenidharau na wakakaribia kuniua. Basi usiwafurahishe maadui juu yangu wala usinifanye pamoja na watu madhalimu.

Anakusudia madui ni wale walioabudu ndama; kama kwamba anamwambia nduguye: unachinganya mimi na maadui zangu na maadui zako, tena unanivuta mbele yao wanicheke. Vipi unanichanganya nao kwenye hasira zako na mimi niko mbali nao na vitendo vyao? Tena nimewapinga na wala sikuzembea kuwapa nasaha na tahadhari!

Hapo Nabii Musa akarudi chini na kumuonea huruma nduguye, akasema: Mola wangu! Nisamehe mimi na ndugu yangu na utuingize katika rehema yako na wewe ni mwenye kurehemu kushinda wote wenye kurehemu.

Alijiombea maghufira yeye mwenyewe kwa ukali wake kwa nduguye, kisha akamuombea maghufira nduguye kwa kuhofia kuwa hakufanya bidii ya kuwazuia na shirk. Bila shaka Mwenyezi Mungu, aliitikia maombi ya Nabii Musa kwa sababu yeye ni mwenye kurehemu kushinda wenye kurehemu; na pia kujua kwake ikhlasi ya Nabii Musa na nduguye Harun.

Hakiaka wale walioabudu ndama, itawapata ghadhabu kutoka kwa Mola wao na madhila katika maisha ya dunia. Na hivyo ndivyo tunavyowalipa wazushi

Unaweza kuuliza kuwa : dhahiri ya Aya hii nikuwa wale walioabudu ndama wamekasirikiwa na Mwenyezi Mungu na hali wao walitubia na kuomba maghufira; kama ilivyoeleza Aya ya 149 ya Sura hii na Aya nyingine inasema:

ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ عَمِلُوا السُّوءَ بِجَهَالَةٍ ثُمَّ تَابُوا مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ وَأَصْلَحُوا إِنَّ رَبَّكَ مِن بَعْدِهَا لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١١٩﴾

“Kisha hakika Mola wako kwa waliotenda uovu kwa ujinga; kisha wakatubia baada ya hayo na wakatenda mema; bila shaka Mola wako ni mwingi wa maghufira mwenye kurehemu” (16:119).

Kwa hiyo vipi walazimiane na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu ya milele na laana ya daima?

Baadhi wamejibu kuwa : waabudu ndama waligawanyika mafungu mawili baada ya kurudi Nabii Musa, Kundi moja lilitubia toba sahihi. Hao ndio waliosamhewa na Mwenyezi Mungu. Na wengine waling’ang’ania ushirikina; kama vile Msamaria na wafuasi wake. Hawa ndio waliokasirikiwa na Mwenyezi Mungu na akawadhalilisha katika maisha ya duniani.

Ilivyo ni kwamba kwenye Aya hakuna ufahamisho wowote wa makundi haya. Jibu linalonasibu zaidi ni kuwa Mwenyezi Mungu alijua kuwa Mayahudi milele hawatubii wala hawatatubia toba ya kiuhakika ambayo hawatarudia. Hakia hii inafahamishwa na tabia yao na sera yao. Kwani wao walikuwa na wanaendelea kuwa ni watu wasiokatazika wala kukanyika na ufisadi na upotevu ila kwa kutumia nguvu peke yake.

Swali la pili : Mayahudi leo wanayo dola inayoitwa Israil, kwa hiyo hawana udhalili; je hili si jambo linalopingana na dhahiri ya Aya?

Jibu : Hapana! Tena hapana! Hakuna dola wala haitakuwa dola ya Mayahudi milele; kama kilivyosajili kitabu cha Mwenyezi Mungu. Israil sio dola, kama dola nyingine; isipokuwa ni kambi ya jeshi; kama vile askari wa kukodiwa waliowekwa na wakoloni kulinda masilahi yao na kuvunja nguvu za wazalendo. Tumeyathibitisha hayo katika kufasiri Juz.4 (3:112) na Juzuu nyenginezo.

Vilevile katika kitabu Min huna wa hunaka (Huku na huko) mlango wa man baa’ dinahu li shaitan (Mwenye kumuuzia dini yake shetani)

Na wale waliotenda maovu, kisha wakatubia baada yake na wakaami- ni, hakika Mola wako baada ya hayo ni mwenye kusamehe mwenye kurehemu.

Maana ya Aya yako wazi, na mfano wake umekwishapita mara nyingi. Lengo la kutajwa kwake baada ya Aya iliyotangulia ni kutilia mkazo kwamba mwenye kutubia na akarudi kwa Mola wake kwa ikhlasi na asirudie maasi, kama walivyofanya waisrail, basi Mwenyezi Mungu (s.w.t) atamrehemu, awe ni mwisraili au Mkuraysh n.k.

Na ilipomtulia ghadhabu Musa, aliziokota zile mbao na katika maandiko yake mna uongozi na rehema kwa wanaomwogopa Mola wao.

Nabii Musa ni Mtume aliye ma’sum, hilo halina shaka, lakini yeye ni binadamu, anahuzunika na kufurahi, anridhia na kukasirika. Hasira zilimpanda alipoona watu wake wamertadi dini ya Mwenyezi Mungu. Hasira aliiacha alipombwa na ndugu yake, Harun; na Mungu akamwahidi kuwaadhibu walortadi.

Baada ya Nabii Musa kurudia hali yake ya kawaida, alizirudia zile mbao alizokuwa amezitupa alipokuwa amekasirika na akatulizana kutokana na yaliyomo ndani yake katika uongofu kwa yule ambaye moyo wake utaifungukia kheri na rehema zilizomo kwa yule anayeogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu. Hekima ya Mwenyezi Mungu imepitisha kumpa radhi na rehema kila mwenye kumtii kwa kuogopa adhabu yake, na kumletea adhabu na mateso kila mwenye kuasi kwa kubweteka na rehema yake.

وَاخْتَارَ مُوسَىٰ قَوْمَهُ سَبْعِينَ رَجُلًا لِّمِيقَاتِنَا فَلَمَّا أَخَذَتْهُمُ الرَّجْفَةُ قَالَ رَبِّ لَوْ شِئْتَ أَهْلَكْتَهُم مِّن قَبْلُ وَإِيَّايَ أَتُهْلِكُنَا بِمَا فَعَلَ السُّفَهَاءُ مِنَّا إِنْ هِيَ إِلَّا فِتْنَتُكَ تُضِلُّ بِهَا مَن تَشَاءُ وَتَهْدِي مَن تَشَاءُ أَنتَ وَلِيُّنَا فَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا وَأَنتَ خَيْرُ الْغَافِرِينَ ﴿١٥٥﴾

155. Na Musa akachagua watu sabini katika kaumu yake kwa miadi yetu. Lilipowashika tetemeko alisema: Mola wangu! Lau ungetaka ungeliwaangamiza wao na mimi zamani. Unatuangamiza kwa sababu ya yale waliyoyafanya wajinga katika sisi? Halikuwa hilo ila ni adhabu yako, humpoteza kwayo umtakaye na kumwongoza umtakaye, Wewe ndiye mlinzi wetu. Basi tughufurie na uturehemu nawe ndiye bora wa kughufiria.

وَاكْتُبْ لَنَا فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ إِنَّا هُدْنَا إِلَيْكَ قَالَ عَذَابِي أُصِيبُ بِهِ مَنْ أَشَاءُ وَرَحْمَتِي وَسِعَتْ كُلَّ شَيْءٍ فَسَأَكْتُبُهَا لِلَّذِينَ يَتَّقُونَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَالَّذِينَ هُم بِآيَاتِنَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٥٦﴾

156. Na utuandikie mema katika dunia hii na katika akhera, Sisi tunarejea kwako. Akasema: Adhabu yangu nitamsibu nayo nimtakaye; na rehema yangu imekienea kila kitu. Nitaiandika kwa ajili ya wale wanaoogopa, na wanaotoa Zaka na wanaoziamini ishara zetu.

الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الرَّسُولَ النَّبِيَّ الْأُمِّيَّ الَّذِي يَجِدُونَهُ مَكْتُوبًا عِندَهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ يَأْمُرُهُم بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَاهُمْ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُحِلُّ لَهُمُ الطَّيِّبَاتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمُ الْخَبَائِثَ وَيَضَعُ عَنْهُمْ إِصْرَهُمْ وَالْأَغْلَالَ الَّتِي كَانَتْ عَلَيْهِمْ فَالَّذِينَ آمَنُوا بِهِ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَاتَّبَعُوا النُّورَ الَّذِي أُنزِلَ مَعَهُ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿١٥٧﴾

157. Ambao wanamfuata Nabii asiyesoma wala kuandika ambaye wanamkuta ameandikwa kwao katika Tawrat na Injili ambaye anawaamrisha mema na anawakataza maovu, na anawaahalalishia vizuri na kuwaharamishia vibaya, na kuwaondolea mizigo yao na minyororo iliyokuwa juu yao. Basi wale walioamini na wakamheshimu na wakamsaidia na wakafuata nuru iliyoteremshwa pamoja naye, Hao ndio wenye kufaulu.

HAIKUWA ILA NI ADHABU YAKO

Aya 155 – 157

MAANA

Na Musa akawachagua watu sabini katika kaumu yake kwa miadi yetu.

Wafasiri wamerefusha maneno kuhusu Aya hii na zikagongana kauli zao katika kuifasiri. Wakatofautiana katika kubainisha miadi, kuwa je, ni miadi ya kuteremshwa Tawrat au mingine?

Vilevile wametofautiana kuwa ni kwa nini Nabii Musa aliwachagua watu sabini katika watu wake, Je, ni kwa kuwa wao walimtuhumu Nabii Musa na kumwambia hatutakuamini mpaka tusikie maneno ya Mwenyezi Mungu kama unavyosikia wewe; ndipo akasuhubiana nao ili asikie, kama alivyosikia; au ni kwa sababu nyingine?

Vilevile wametofautiana wafasiri katika sababu ambayo aliwaadhibu Mwenyezi Mungu, Hatimae wakahitalifiana kuwa je, mtetemeko uliwaua au ulikurubia tu kuvunja migongo yao, lakini hawakufa?

Katika Aya hakuna kidokezo chochote cha yale waliyoyachagua kikundi katika wafasiri. Linalofahamika ni kuwa tu, Nabii Musa aliwachagua watu sabini ili aende nao kwa miadi ya Mola wake. Kwa hali ilivyo ni kuwa uchaguzi huo ulikuwa ni kwa amri ya Mwenyezi Mungu, kwa sababu Nabii Musa hafanyi ila aliloamrishwa; na kwamba Mwenyezi Mungu ali- wateremshia hao sabini aina ya adhabu kulingana na hekima ilivyoka.

Basi hatuna cha kuthibitisha miadi ilivyo kuwa wala sababu ya kuchagua au ya adhabu.

Ni kweli kwamba kauli ya Nabii Musa kumwambia Mwenyezi Mungu:Unatuangamiza kwa sababu ya yale waliyoyafanya wapumbavu katika sisi? inafahamisha kwamba wao walifanya yaliyowajibisha maangamizi, lakini halikubainishwa walilolifanya; nasi hatuna haki ya kusema tusiyoyajua.

Lilipowashika tetemeko alisema: Mola wangu! Lau ungetaka ungeli- waangamiza wao na mimi zamani!

Nabii Musa alichagua watu sabini walio bora katika watu wake akaenda nao kwenye miadi ya Mola wake, walipofika huko wakaangamia wote akabakia, peke yake. Hilo ni tatizo la kukatisha tamaa hakuna la kufanya tena. Je, arudi peke yake kwa wa Israel? Atawajibu nini wakimuuliza watu wao?

Hakuna kimbilio kabisa isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Basi akanyenyekea kwa Mwenyezi Mungu amwondolee tatizo hilo na akatamani lau Mwenyezi Mungu angelimwangamiza pamoja nao kabla ya kuja nao hapa.

Kisha akasema kumwambia mtukufu aliye zaidi:

Unatuangamiza kwa sababu ya yale waliyoyafanya wajinga katika sisi?

Yaani wewe ni mtukufu na mkuu kuliko kufanya hivyo. Kwa sababu wewe ni Mpole na Mkarimu.

Halikuwa hilo ila ni adhabu yako, humpoteza kwayo umtakaye na humwongoza umtakaye.”

Neno Fitna lililofasiriwa adhabu hapa, lina maana nyingi; ikiwemo upote- vu na ufisadi; kama ilivyo katika Aya ya 26 ya Sura hii. Maana nyingine ni kupigana na majaribu, mara nyingi hutumiwa kwa maana ya adhabu; kama anavyosema Mwenyezi Mungu:

وَاتَّقُوا فِتْنَةً لَّا تُصِيبَنَّ الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنكُمْ خَاصَّةً ﴿٢٥﴾

“Na jikingeni na adhabu ambayo haitawasibu waliodhulumu peke yao” (8:25).

Haya ndiyo makusudio yake katika Aya hii tuliyonayo, Dhamir ya hilo inarudia tetemeko ambalo limekwishatajwa. Maana ya kumpoteza amtakaye, ni kuwa Mwenyezi Mungu humpelekea tetemeko, ambalo ndio adhabu, yule amtakaye katika waja wake, na maana ya kumwongoza ni kumwepushia tetemeko amtakaye.

Maana ya kijumla ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) huteremsha adhabu kwa amtakaye anayestahiki na kumwondolea asiyestahiki. Kwa hiyo inatubainikia kuwa kauli yake halikuwa hilo ila ni adhabu yako, maana yake yanafungamana na yaliyotangulia na yaliyo baada yake; na kwamba haijuzu kuitolea dalili kuwa upotevu unatokana na Mwenyezi Mungu.

Vipi Mwenyezi Mungu ampoteze mtu kisha amwaadhibu kwa upotevu huo? Na hakuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kutaka kuwadhulumu waja. Hakika Shetani ni adui mwenye kupoteza na inatosha kuwa Mola wako ni mwongozi na mwenye kunusuru.

Kwa maelezo zaidi rudia Juz.1 (2:26).

Wewe ndiye mlinzi wetu, Basi tughufurie na uturehemu nawe ndiwe bora wa kughufuria. Na utuandikie mema katika dunia hii na katika akhera. Sisi tunarejea kwako”

Hakuna tafsir bora ya Munajat huu, kama kauli ya bwana wa mashahidi, Imam Husein bin Ali(a.s) wakati alipozungukwa na maelfu kila upande akiwa peke yake. Akakimbilia kwa Mola wake na kumtaka hifadhi dhidi ya maadui zake akisema:

“Ewe Mola wangu wewe ndiye matarajio yangu katika kila shida, Kila jambo lililonishukia wewe ni tegemeo, Ni matatizo mangapi ya kukatisha tamaa, ya kuondokewa na marafiki na kufuatwa na maadui, uliyoniteremshia, kisha nikakushitakia wewe, kwa kuwa sina mwingine zaidi yako, nawe ukanitatulia na kunifariji! Basi wewe ndiye mtawalia kila neema,mwenye kila hisani na mwisho wa matakwa yote!”

Akasema: Adhabu yangu nitamsibu nayo nimtakaye katika wananostahiki adhabu.

Kwa sababu matakwa ya Mwenyezi Mungu yanapitia kwenye haki na uadilifu tu, hakuna mchezo wala dhulma mbele ya Mwenyezi Mungu.

Razi anasema: “Amesoma Hasan: Usibu bihi man Asaa kwa sin (nitam- sibu nayo mwenyewe kufanya uovu), na Shafii amechagua kisomo hiki.”

REHMA YA MWENYEZI MUNGU INAMFIKIA IBLISII

Qur’an hutumia neno Rehma ya Mwenyezi Mungu kwa maana ya msaada wake na kwa thawabu zake. Maana ya usaidizi kutoka kwake Mwenyezi Mungu ni kwamba vitu vyote vilivyoko, hata Iblisi, vinamhitajia Mwenyezi Mungu katika kubakia kwake na kuendelea kwake; kama ambavyo vinamhitajia yeye katika asili ya kupatikana kwake, na kwamba yeye ndiye anayevisaidia kubaki wakati wote, kiasi ambacho lau msaada wake huo utakiepuka kitu kitambo kidogo cha mpepeso wa jicho, basi kitu hicho hakitakuwako tena.

Ufafanuzi zaidi wa rehma hii ni kauli yake Mwenyezi Mungu mtukufu:

وَلَوْ يُؤَاخِذُ اللَّـهُ النَّاسَ بِمَا كَسَبُوا مَا تَرَكَ عَلَىٰ ظَهْرِهَا مِن دَابَّةٍ وَلَـٰكِن يُؤَخِّرُهُمْ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ﴿٤٥﴾

“Lau Mwenyezi Mungu angeliwachukulia watu kwa waliyoyachuma, asin- geliacha juu ya ardhi hata mnyama mmoja” (35:45).

Rehma hiyo ndiyo iliyokusudiwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu:Na rehma yangu imekienea kila kitu hata Iblisi aliyelaaniwa. Ama rehma kwa maana ya thawabu, Mwenyezi Mungu (s.w.t) humpa anayemwamini na kumcha. Ndiyo aliyoiashiria kwa kusema kwake. Nitaiandika kwa ajili ya wale wanaoogopa maasi na wakafuata amri ya Mwenyezi Mungu na kuacha makatazo yake.

Na wanaotoa Zaka.

Ametaja Zaka badala ya Swala. Kwa sababu mtu hupituka mpaka kwa kujiona amejitoshea.

Na wanaoziamini ishara zetu ambao wanamfuata Nabii asiyesoma wala kuandika.

Rehma ya Mwenyezi Mungu ambayo ni kwa maana ya thawabu haipati isipokuwa mwenye kumwogopa Mwenyezi Mungu, akatoa mali kwa kupenda kwake na akauamini utume wa Nabii Muhammad(s.a.w.w) kama utamfikia ujumbe wake.

Amehusisha kutaja mali kutokana na tulivyoyadokezea, na pia kuwa mazungumzo ni ya Mayahudi ambao mali ndio Mola wao hakuna mwingine isipokuwa yeye. Mwenyezi Mungu amemsifu Nabii Muhammad(s.a.w.w) , katika Aya hii kwa sifa hizi zifuatazo:-

1.Nabii Asiyesoma Wala Kuandika.

Hiyo ni sifa inayomhusu yeye tu, kinyume cha Mitume wengine, kutambulisha kuwa licha ya kuwa hivyo lakini amewatoa watu kutoka katika giza mpaka kwenye mwangaza, akaathiri maisha ya umma wote wakati wote na mahali kote.

2.Ambaye Wanamkuta Ameandikwa Kwao Katika Tawrat Na Injil.

Rudia Juz.1 (2:136) na Juz.6 (4:163).

3.Ambaye Anawaamrisha Mema Na Anawakataza Maovu.

Rudia Juz, 4 (3:104 - 110).

4.Na Anawahalalishia Vizuri Na Kuwaharamishia Vibaya.

5.Na Kuwaondolea Mizigo Na Minyororo Iliyokuwa Juu Yao.

Makusudio ya minyororo ni mashaka. Mwenyezi Mungu aliwaharamishia waisrail baadhi ya vitu vizuri, vilivyodokezwa kwenye Juz.8 (6:146); kama ambavyo sharia ya Nabii Musa ilikuwa ngumu na yenye mashaka; kiasi kwamba mwenye kutubia katika waisrael hakubaliwi toba yake ila kwa kujiua:

فَتُوبُوا إِلَىٰ بَارِئِكُمْ فَاقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ ﴿٥٤﴾

“Basi tubuni kwa Muumba wenu na jiueni” Juz.1 (2:54).

Kwa hiyo Mwenyezi Mungu amewaambia waisrael ambao wamemkuta Nabii Muhammad(s.a.w.w) kwamba wao wakisilimu watahalalishiwa vizuri vilivyokuwa haramu, na atawaondolea mashaka katika taklifa. Kwa sababu Nabii Muhammad ametumwa na sharia nyepesi isiyo na mikazo.

Basi wale waliomwamini.

Makusudio ni waliomwamini Nabii Muhammad(s.a.w.w) miongoni mwa Mayahudi na wengine.

Na wakamheshimu.

Yaani kumsaidia katika mwito wake na kumheshimu kwa cheo chake.

Na wakamsaidia juu ya maadui zake.

Na wakafuata nuru iliyoteremshwa pamoja naye.

Yaani wakafanya matendo kwa mujibu wa Qur’an.Hao ndio wenye kufaulu duniani na akhera.

6

7

8

9

10

11