• Anza
  • Iliyopita
  • 21 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 10404 / Pakua: 967
Kiwango Kiwango Kiwango
MAISHA YA ABU DHARR

MAISHA YA ABU DHARR

Mwandishi:
Swahili

14

MAISHA YA ABU DHARR

Hapana shaka kwamba Abu Dharr alipata daraja la juu zaidi la imani. Alizingatia hadi dakika za mwisho za uhai wake kwamba aliapa kwa Mtume kusema kweli na bila kujali shutuma yoyote kwa ajili ya ukweli. Shah Walyullah Dehlavi ameandika kwamba katika utekelezaji kwa Mtume(s.a.w.w) ni kwamba alichukua viapo vya uaminifu vya aina mbali mbali kutoka kwa watu mbali mbali yaani kwenda Jihad, kukataa bidaa, kuanzisha sheria za Kiislamu, na kusema kweli. (Shifau alil).

Kiapo alichochukua kutoka kwa Abu Dharr ni kusema kweli. Abu Dharr alifanya kwa mujibu wa kiapo cha uaminifu baada ya kutambua vema maana yake na kwamba asingefanya hivyo, ambapo alikwisha sadiki sana hali ambayo iliondoa shaka kwake, kwamba chochote alichofanya kililingana na Ridhaa ya Mwenyezi Mungu na nia ya Mtukufu Mtume(s.a.w.w) [134] .

Kuhusiana na hilo, kamwe hakujali nguvu za serikali wala kuogopa kupata matatizo. Alistahamili kila aina ya ukandamizaji na alibeba kila aina ya usumbufu lakini hakuacha kusema kweli, hadi akafukuzwa na kupelekwa uhamishoni mara mbili. Uhamisho wa Abu Dharr wa mara ya mwisho hauna mfano wake.

Alijitolea mhanga kwa kuzuiliwa kwenye jangwa ambalo ni pweke. Bila kuzungumzia habari za nyumba ya kuishi, alifanya kivuli cha mti kuwa makazi yake. Hakuwa na mpango wowote wa chakula na makazi ambapo angepumzika au kulala. Lakini kwa ujasiri wake wa hali ya juu na azima aliokuwa nayo, Abu Dharr aliyachukua matatizo yote kwa uchangamfu kwa sababu ya kumridhisha Mwenyezi Mungu. Mke na mtoto wake wa kiume walipokufa sasa muda ulikaribia ambapo alikuwa anangojea kifo chake mwenye we akiwa kwenye sehemu pweke kama hiyo akiwa na mtoto wake wa kike tu.

Loo! Siku ya mwisho ya uhai wa Abu Dharr kwenye sehemu hiyo pweke ilikaribia. Alikuwa anasali mara nyingi na binti yake alikuwa na wasi wasi na shauku kuhusu hali ya baba yake na mwisho wake uliokuwa unakaribia. Hapakuwepo na mtu. Hapakuwepo na hata mnyama. Muda wa kuwasili malaika wa kifo ulikaribia. Muda ambao binadamu hulia na mtoto wa kike kunyang'anywa mapenzi ya baba yake.

Si tu kwamba alikuwa anaangalia kwa makini kwa kutokuwa na msaada kwa baba yake ambaye mapenzi yake yalisababisha mshtuko mara kwa mara7

7. Waandishi wengi wa historia wamehusisha tukio la kifo cha Abu Dharr kwa mke wake Umm Dhar, lakini haioneshi kuwa sahihi kwa sababu waandishi wa historia kama vile Masudi na Yaqubi, wameandika kwamba mke na binti yake Abu Dharr walikwisha fika huko Rabzah. Majilisi ametoa maelezo ya kifo cha mke wake huko Rabza kama alivyoeleza bint yake. Tabari amesema kwamba mtoto wa kike alipelekwa Madina baada ya kifo cha Abu Dharr. Bin Athir pia amekiri kuwepo kwa mtoto wa kike [135] na hakuna hata mwandishi yeyote wa historia mwenye kuaminika ambaye ametamka kuhusu kuwasili kwa mke wa Abu Dharr Madina.

Hapa tunatoa maelezo ya historia ya hatari ya kifo cha Abu Dharr kama ilivyosimuliwa na binti yake kama ilivyoandikwa na Majlisi. Binti huyu anasema; "Siku zetu zilipita katika mateso yasiyo elezeka kwenye upweke. "Siku moja ilitokea kwamba hatukuweza kupata chochote chakula. Tulijitahidi kutafuta lakini hatukufanikiwa. Baba yangu aliyekuwa taabani akaniambia, "Binti yangu kwa nini una wasi wasi sana leo?" Nikasema, "Baba, mimi nina njaa sana na wewe unazidi kudhoofika pia kwa sababu ya njaa. Nimejaribu kujitahidi kila nilivyoweza kupata chakula ili niweze kuhisi ninaheshimika kwako lakini sikufanikiwa." Abu Dharr akasema, "Usiwe na wasi wasi.

Mwenyezi Mungu ndiye mpangaji mkuu wa mambo yetu." Mimi nikasema, "Baba! Ni sawa lakini hakuna kitu chochote sasa ambacho kinaweza kukidhi mahitaji yetu."

Akasema; "Binti yangu! Nishike bega langu na unipeleke hapa na pale. Labda tunaweza tukapata chochote huko." Nilimshika mkono wake na tukaanza kwenda kuelekea upande alikonielekeza. Wakati tupo njiani baba yangu aliniambia nimkalishe chini. Nikamketisha kwenye mchanga wenye joto. Akakusanya mchanga na akalaza kichwa chake juu ya mchanga huo.

Mara tu alipolala chini, macho yakaanza kuzunguka na akahisi uchungu wa kifo. Nilipoona hivi nikaanza kulia kwa sauti kubwa sana. Akajikaza kidogo na akasema, "Kwa nini unalia, binti yangu?" Nikasema, "Nitafanya nini baba yangu? Hapa ni jangwa na hakuna mtu yeyote. Sina sanda ya kukuvesha na pia hakuna mtu wa kuchimba kaburi hapa. Nitafanya nini mauti yakikufika hapa kwenye sehemu hii pweke."

Akalia baada ya kuona jinsi nilivyokuwa sina jinsi ya kuwa na msaada wowote na akasema, "Binti yangu! Usiwe na wasi wasi. Huyo rafiki yangu ambaye kwa ajili ya kumpenda yeye na watoto wake ninavumilia matatizo yote haya, aliniambia kuhusu tukio hili mapema, Sikiliza, Ewe bint yangu mpendwa Alisema mbele ya kundi la masahaba wake wakati wa Vita ya Tabuk kwamba mmojawao angekufa lakini jangwani na kundi la masahaba wangekwenda kwenye maziko na mazishi yake. Sasa hakuna hata mmoja wao aliyehai isipokuwa mimi. Wote wamekufa wakiwa kwenye sehemu zenye watu. Ni mimi tu niliye baki na pia nipo kwenye upweke wa pekee. Kamwe sijapata kuona jangwa la aina hii ambapo nimelala sasa na mwenye uchungu wa kifo. Binti yangu mpendwa! Nikifa nifunike joho langu na ukae kwenye njia inayoelekea Iraq. Kundi la watu waumini watapita hapo. Waambie kwamba Abu Dharr sahaba wa Mtume(s.a.w.w) amekufa. Kwa hiyo tafadhalini tayarisheni mazishi yake."

Alikuwa anazungumza na mimi wakati malaika wa kifo alipofika na kumtazama uso wake. Baba yangu alipomtazama uso wake ukawa mwekundu na akasema, "Ewe Malaika wa Kifo! Umekuwa wapi hadi sasa? Nimekuwa ninakungojea wewe. Ewe rafiki yangu! Umekuja wakati ambapo mimi ninakuhitaji sana. Ewe Malaika wa kifo! Na asiokolewe mtu asiyefurahi kuonana na wewe. Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu nichukue haraka sana na unipeleke kwa Mwenyezi Mungu mwenye Huruma sana ili niweze kupumzika na matatizo ya dunia hii."

Baada ya hapo alimwambia Mwenyezi Mungu, "Ee Msitawishaji wangu! Ninaapa Kwako Wewe, na Unajua kwamba ninasema kweli kwamba kamwe sikuchukia kifo na kila mara nilitamani kukutana na wewe."

Baada ya hapo jasho la kifo likatoka kwenye uso wa baba yangu na aliponitazama, aligeuza uso wake na kuiaga dunia daima milele. Sisi tunatoka kwa Mwenyezi Mungu na Kwake tutarejea."8

Binti yake Abu Dharr aliendelea, "Baba yangu alipokufa nilianza kulia huku ninakimbia kuelekea kwenye njia inayoelekea Iraq. Nilikuwa nimeketi pale nikangojea kundi la watu linalokuja. Ghafla nilikumbuka kwamba maiti ya baba yangu ilikuwa haina mtu wa kuiangalia. Kwa hiyo, nilikimbia hadi ilipokuwa maiti. Tena nikarudi kwenye njia isije kundi likapita bila kulitaarifu. Kwa hiyo, ikawa ninakwenda kwenye maiti na kurudi njiani, mara kadhaa.

Sasa, ghafla nikawaona watu wanakuja wakiwa wamepanda ngamia. Walipokaribia, nikawaendea huku nikilia na kutokwa na machozi na nikawaambia; "Enyi masahaba wa Mtume! Sahaba wa Mtume amekufa." Wakaniuliza sahaba huyo ni nani?" Nikajibu; "Baba yangu, Abu Dharr Ghifari."

Mara waliposikia waliteremka kutoka kwenye ngamia na wakafuatana na mimi huku wakilia. Walipofika hapo wakalia sana kuhusu kifo chake cha kuhuzunisha na wakashughulikia ibada ya mazishi yake.

Mwandishi wa historia Atham Kufi, amesema kwamba kundi la watu waliokuwa wanakwenda Iraq, alikuwepo; Ahnaf bin Qays, Tamimi,

8. Imetamkwa kwenye masimulizi ya kwamba Abu Dharr hakuhisi uchungu wowote wa kifo, na uhalali wake ulithibitika kwa sababu uchungu wa kifo anauhisi yule tu ambaye matendo yake yalikuwa ya kuchukiza au ambaye amefanya kitu ambacho kumbukumbu yake katika maisha husababisha kizuizi kwa roho kutoka. Mathalani Aishah alipohisi mateso makubwa alipokuwa kwenye uchungu wa kukata roho na alianza kupumua kwa nguvu sana watu wakamuuliza, Ewe Mama wa Waumini! Kwa nini imekuwa hivi? Nini kinachokusumbua" Akajibu, Vita vya Ngamia vinasonga roho (Rauzatul Akhyar anasimulia kutoka kwenye Rabiul Abrar).

Sasaah bin Sauhan al-Abdi, Kharijah bin Salat Tamimi, Abdulah bin Muslimah Tamimi, Halal bin Malik Nazle, Jarir bin Abdullah bajali, Malik bin Ashtar bin Harith na wengineo. Watu hawa walimkosha Abu Dharr na wakafanya mpango wa kumvisha sanda. Baada ya mazishi Malik bin Ashtar alisimama pembeni mwa kaburi na akatoa hutuba ambapo ilirejea mambo ya Abu Dharr na kumwombea yeye. Baada ya kumsifu Mwenyezi Mungu Mweza wa yote akasema"

"Ee Mwenyezi Mungu! Abu Dharr alikuwa sahaba wa Mtume Wako na muumini wa Vitabu Vyako na Mitume Wako. Alipigana kishujaa sana katika njia Yako, alikuwa, mfuasi imara wa sheria Zako za Kiislamu na kamwe hakubadilisha au kugeuza amri yoyote miongoni mwa amri Zako.

Ee Mola wangu Mlezi! Alipoona ukinzani unafanywa dhidi ya Kitabu na Sunna akapiga kelele na kuwa tahadharisha wahusika kwa umma ili wajirekebishe, matokeo yake wakamtesa, wakamhamisha kutoka sehemu moja hadi nyingine, wakamfedhehesha, wakamhamisha kutoka katika nchi ya Mtume Wako mpendwa na kumweka kwenye matatizo makubwa sana. hatimaye amekufa akiwa katika hali ya upweke kabisa sehemu ambayo hawaishi watu.

Ee Mwenyezi Mungu! Mpe Abu Dharr sehemu kubwa ya hizo neema za mbinguni ambazo Umewaahidi waaminio na umlipe kisasi yule ambaye amemfukuza kutoka Madina na umpe adhabu kamili anayostahiki."

9. Upo uwezekano kwamba matokeo ya laana hiyo Uthman aliuawa baadaye kwa mfano wake. Historia inasema kwamba mwili wake ulilala juu ya lundo la kinyesi kwa muda wa siku tatu na mbwa walikula mguu wake mmoja. (Tarikh Atham Kufi).

Baada ya mazishi ya Abu Dharr watu waliondoka Rabzah lakini mwanae wa kike aliendelea kukaa hapo kufuatana na wasia wake. Baada ya siku kadhaa, khalifa Uthman alimwita na akampeleka kwao.[136]

Malik Ashtar alimwombea Abu Dharr kwenye hotuba yake na wote wale ambao walikuwepo hapo na akasema, "Amini" (Na iwe hiyo). Hata hivyo, walipokamilisha ibada ya mazishi ilikuwa jioni na wakawa hapo hadi asubuhi. Wakaondoka asubuhi siku iliyofuata."[137]

Hata hivyo bint yake Abu Dharr ambaye aliendelea kukaa hapo Rabzah kwa muda wa siku chache zaidi. Siku moja usiku alimuona Abu Dharr kwenye ndoto ameketi na anakariri Qurani Tukufu. Akasema, Baba! Nini kimekutokea na umerehemewa kwa kiwango gani na Mwenyezi Mungu ambaye ni Mwingi wa Rehma? Akasema, Ewe binti yangu! Mwenyezi Mungu amenizawadia upendeleo usio na mipaka, amenipa starehe zote na amenipa kila kitu. Ninafurahia sana ukarimu Wake. Ni wajibu wako kujishughulisha na kumuabudu Mwenyezi Mungu kama kawaida na usiruhusu aina yoyote ya maringo na kiburi kuja kwako."[138]

Wasomi na waandishi wa historia wanakubaliana kwamba Abu Dharr alikufa tarehe 8, Zilhajjah, 32 A.H, Rabzah. Alikuwa na umri wa miaka 85.

SURA YA ISHIRINI NA MOJA

Baada ya kupata mateso ya kugandamizwa na matatizo mfululizo na mfuatano wa kuhamishwa kutoka kwa watu wenye fikra za kidunia, Abu Dharr aliiacha dunia hii ya muda mfupi akiwa Rabzah. Lakini hadith ya mapenzi yake kwa Mwenyezi Mungu bado inaendelea kuishi hadi daima milele. Historia imejaa mifano, ukweli na hotuba zake zilizowazi na kuaminika zitaendelea kusikika kwenye nyoyo za waumini. Abu Dharr bado yu hai kupitia kwa tabia yake hata baada ya kifo chake; na ataendelea kuwa hai kupitia kwa kanuni alizozishikilia sana.

Dunia inatambua kwamba Abu Dharr alikufa katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Aliteseka kwa matatizo na dhiki kwa ajili ya kutetea ukweli na kuanzisha na kutangaza kanuni za Uislamu katika Nchi za Kiislamu. Lakini inasikitisha kuona kwamba dhalimu hataki kutubu kwa udhalimu wake. Tunatoa maelezo ya tukio hili hapa kwa maneno ya mfasiri wa 'Hitoria' yaliyoandikwa na Muhammad bin Ali bin Atham Kufi, mwandishi wa historia wa karne ya 3 Hijiriya. Ameandika;

Habari za kifo cha Abu Dharr zilipomfikia Uthman, Ammar bin Yasir alikuwepo hapo. Ammar akasema; "Mwenyezi Mungu amhurumie Abu Dharr. Mwenyezi Mungu! Uwe shahidi kwamba tunaomba kwa nyoyo na roho zetu umhurumie yeye. Ee Mwenyezi Mungu umsamehe."

Mara tu khalifa aliposikia akakasirika na akasema, "Ewe mpumbavu! Na wee utakutana na hatima ya aina hii hii. Nisikilize! Sioni aibu kwa sababu ya kumhamisha Abu Dharr na kifo chake cha upwekeni." Ammar akasema, "Kwa jina la Mwenyezi Mungu, hii haitakuwa sababu ya mwisho wangu."

Khalifa aliposikia hivi akaagiza wafanya kazi wake wa baraza, "Msukumeni nje, mhamisheni hapa Madina na mpelekeni sehemu hiyo hiyo ambako Abu Dharr alipelekwa Yeye pia aendeshe maisha ya aina ile ile na msimruhusu arudi Madina almradi bado nipo hai."

Ammar akasema, "Kwa jina la Mwenyezi Mungu! Napenda zaidi kuwa jirani na mbwa mwitu na mbwa kuliko kuwa karibu na wewe." Baada ya kusema hivyo alinyanyuka na kuondoka hapo na akaenda kwake.

Khalifa alipoamua kumpeleka Ammar huko Rabzah na taarifa ikalifikia kabila lake la Bani Makhzum, wakakasirika. Wakasemezana wao kwa wao kwamba Uthman alikwisha chupa mipaka ya uadilifu. Baada ya hapo walikaa kikao cha baraza na wakafikiria kwamba ingekuwa bora endapo kabla ya kuchukua hatua yoyote jambo hili lisuluhishwe kwa maelewano. Wakiwa na lengo hili katika maoni yao, walikwenda kumuona Ali. Ali akawauliza, kwa nini nyinyi wote mmenijia wakati kama huu? Wakasema, "Lipo tatizo kubwa linatukabili, khalifa ameamua kumfukuza Ammar kutoka Madina kwenda Rabzah. Uwe mwema kiasi cha kutosha, uende kwa khalifa na umsihi kwa maneno yenye busara amwache Ammar kama alivyo na asimfukuze kutoka jijini, vinginevyo ghasia ya aina hiyo inaweza kuanzisha vurugu ambayo itakuwa si rahisi kuizima."

Imamu Ali aliwasikiliza, akawaliwaza na akawaomba wasifanye haraka. Akawaambia, "Nitakwenda nijaribu kusuluhisha jambo hili. Ninao uhakika litasuluhishwa kwa makubaliano. Ninatambua vema hali hii. Nitamfikisha pale kwenye fikra yenu."

Baada ya mazungumzo haya, Ali alikwenda kwa khalifa Uthman na akasema, " Ewe Uthman! Kuna mambo mengine unayafanya haraka na unadharau ushauri wa marafiki na washauri. Wakati fulani ulimfukuza Abu Dharr Madina. Alikuwa Muislamu Muadilifu sana, sahaba mashuhuri wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na muhajirina bora sana. ulimpeleka Rabzah ambako alifariki katika hali ya upweke. Kwa sababu ya tukio hili, Waislamu sasa tayari wamekugeuka, hawako na wewe. Sasa ninasikia kwamba umeamua kumfukuza Ammar kutoka Madina. Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu usiwape usumbufu wa aina hii masahaba wa Mtume(s.a.w.w) na waache waishi kwa amani." Uthman aliposikia hivi akamjibu Ali kwa hasira; "Wewe ndiye unayetakiwa kufukuzwa kwanza kutoka hapa jijini kwa sababu ni wewe ndiye unayemharibu Ammar na wengine."

Ali aliposikia maneno haya yasiyofaa, akassema; "Ewe Uthman! Unawezaje kudiriki kunifikiria mimi namna hii? Hutaweza kufanya jambo hili hata kama unatamani kulifanya na kama unatilia mashaka maneno yangu, jaribu kufanya hivyo. Hapo ndipo utakapotambua hali halisi ya mambo na ndipo utakapotambua ni nani hasa unaokabiliana nao. Na sasa unasema kwamba mimi ninamharibu Ammar na wengine. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, vurugu hii inatoka upande wako. Sioni kama watu hawa wana dosari yoyote. Unafanya matendo ambayo ni kinyume cha dini na maadili mema. Watu hawatayavumilia, na sasa wanaanza kukupa kisogo, na wewe huwezi kuvumilia mambo haya. Unahisi unakosewa na kila mtu na halafu unawasababishia matatizo. MsImamuo huu upo mbali sana na vile walivyofanya wazee wetu." Baada ya maneno haya akanyanyuka na kuondoka hapo.

Watu wa Bani Makhzum walipokwenda kwa Ali kutaka kujua khalifa alimwambia nini kuhusu suala lao, Ali aliwaambia, "Mwambieni Ammar asitoke nje ya nyumba yake.

Mwenyezi Mungu atamkomboa kutoka kwenye mbinu za hila." Khalifa pia alipata taarifa ya mazungumzo haya kupitia kwa mtu mwingine na akaacha kumfukuza Ammar. Zayd bin Thabit akamwambia Uthman, "Endapo khalifa anataka hivyo tunaweza kwenda kwa Ali na kubadilishana mawazo naye kwa lengo la kuondoa hali ya kutoelewana ambayo imejitokeza na uelewano uendelee kama kawaida." Khalifa akasema; "mnao uhuru wa kufanya hivyo."

Zayd bin Thabit na Mughyrah bin Ahnas Thaqafi walikwenda kwa Ali, wakamsalimia na wakaketi. halafu Zayd bin Thabit alianza kumsifu Ali na akasema, "Hapana mtu yeyote hapa duniani ambaye anao ukaribu huo, undugu, daraja na heshima kwa Mtukufu Mtume

kama wewe ulivyo. Hapana mtu yeyote anaweza kulingana na wewe katika kuunga mkono Uislamu na kuwa mtu wa kwanza kuwa Muislamu. Wewe ni chemchem ya uadilifu na chanzo cha ukarimu."

Baada ya wasifu huu Zayd bin Thabit akasema lengo lake hasa lililompeleka kwake na akasema; "Ewe Ali bin Abi Talib! Tulikwenda kwa khalifa Uthman. Ametoa aina fulani ya malalamiko dhidi yako, na amesema kwamba wakati mwingine unapinga matendo yake na unaingilia mambo anayotaka kuyafanya. Kwa hiyo, ili maudhi na kero zilizopo kati yenu ziondolewe kwani hiyo itakuwa ni furaha na shangwe kwa Waislamu wote."

Ali akasema, "Kwa jina la Mwenyezi Mungu, kwa kadiri nilivyoweza. Sikupinga kitu chochote wala sikuingilia jambo lolote. Lakini, sasa, mambo yamekuja kwenye kiwango ambacho haiwezekani kuonesha uvumilivu au kunyamaza. Nilimwambia ukweli kuhusu Ammar jambo ambalo lilimaanisha ustawi wake Uthman, uswalama na manufaa yake mwenyewe. Nilifanya kazi yangu na sasa shauri yake kufanya apendavyo."

Aliposikia hivi Mughyrah bin Ahmad akasema; "Ewe Ali! Unatakiwa kukubaliana na hayo anayoyasema au anayoyataka kufanya Khalifa hata kama unasadiki moyoni mwako au hapana. Unatakiwa kufikiria kwamba utiifu kwa amri zake ni muhimu kwa sababu yeye anaoudhabiti juu yako na wewe huna udhibiti juu yake. Ametutuma kwako kwa sababu anataka tu tushuhudie yale unayoyasema na baada ya hapo, anaweza akasema lolote kuwa kosa."

Aliposikia maneno ya Mughyrah, Ali alikasirika na akasema, "Kwa jina la Mwenyezi Mungu, yule nnaye muunga mkono, kamwe hataheshimiwa na yule ambaye mna mfukuza kamwe hatapumzika. Ondoka nenda zako."

Mughyrah alipatwa na bumbuwazi kwa yale aliyoyasema Ali na hakuweza kusema, "Ewe Ali! Mughyrah amesema upuuzi. Amesema mambo haya kufuatana na anavyotaka mwenyewe. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, hatukuja kwako kwa ajili ya kushuhudia wala si nia yetu kukukosoa wewe au kupinga yale unayoyasema. Tulitaka tufungue mlango wa maelewano na mapatano na kwamba hiyo ndio sababu iliyotuleta hapa. Tunakuomba ufikirie jambo hili." Ali akaonesha ridhaa yake na Zayd bin Thabit akarudi.

Imesimuliwa hapo juu jinsi Ali alivyopinga mwenendo wa Uthman. Bila shaka kuchupa mipaka kwa Uthman, iliwafanya masahaba wa Mtume(s.a.w.w) kuwa na wasi wasi na kusumbuka sana. Tayari walikwisha mkasirikia Uthman waliposikia mateso ya Abu Dharr. Mkasa huu ulisababisha hasira kubwa miongoni mwa Waislamu wa matabaka yote. Kwa hiyo, watu walianza kumkosoa Khalifa kibinafsi na kwa makundi.

Kuhusu suala hili, Zubayr bin al-Awam, sahaba wa Mtume alikwenda kwake na akasema, "Hivi Umar alichukua ahadi kwako kwamba hungewapachika watoto wa Abi Muit kwa watu?" Khalifa akasema, "Ndio, alichukua ahadi hiyo kutoka kwangu." Zubayr akasema, "Kwa nini ulimteua Walid bin Uqbah Gavana wa Kufah?" Khalifa akasema, "Nimefanya hivyo kama Umar alivyompa Ugavana wa Kufah Mughayrah bin Shubah. Kama mambo yalivyo, nilikwisha mteua kuwa gavana wa kufah lakini tabia yake ilipogeuka na kuwa kinyume na Uislamu, yaani akaanza kunywa mvinyo na kuzini, nilimwondoa na kumweka mtu mwingine kushika nafasi yake." Halafu Zubayr akasema, kwa nini ulimteua Muawiyah kuwa Gavana wa Syria kwa mujibu wa maoni ya Umar bin Khatab kwa sababu kabla yangu ni yeye ndiye aliyemteua Muawiyah kuwa Gavana wa Syria." Tena akauliza, "Kwa nini uliwakemea masahaba wa Mtume, ingawa wewe si bora kuliko wao kwa namna yoyote ile?" Uthman akasema,

Sikukusema wewe kwa ubaya. Kwani unajali nini ikiwa niliwakaripia wengine?"

Halafu akauliza, Kwa nini ulisema kwamba kukariri nakala ya Quran Tukufu ya Abdullah bin Masud ni vibaya, ambavyo alijifunza kukariri Qurani Tuklufu kutoka kwa Mtume Zaidi ya hayo, kwa nini ulimgandamiza? Ukaagiza apigwe hadi akapoteza fahamu." Khalifa akasema, "Alikuwa na desturi ya kusema maneno ambayo hayangevumiliwa." Akauliza tena, "Kwa nini ulimpiga mateke Ammar bin Yasir na kwa agizo lako akapigwa sana hadi akapata maradhi ya henia?" Uthman akasema, "Kwa sababu alikuwa na desturi ya kuwachochea watu waniasi mimi."

Zubayr akamuuliza tena, kwa nini ulimhamisha Abu Dharr na ukamtupa mahali ambapo penye upweke na hakuna hata mti. Mtu alikufa katika hali ya kukata tamaa kwa kutokuwa na msaada. Ewe Uthman! Hukuwa unatambua kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu alimfanya kuwa rafiki yake mkubwa, na akasema kwamba hapana mtu aliye mkweli zaidi ya Abu Dharr kati ya mbingu na dunia? Hukuwa unajua kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu hakuwa anastahamili kuwa mbali naye na wakati wowote walipokuwa hamuoni alitoka kwenda kumtafuta Abu Dharr?" Uthman bin Affan akajibu, "Alikuwa anawachochea watu wa Syria waniasi, alikuwa ananikashifu na alikuwa anafichua mapungufu yangu kwa watu." Halafu Zubayr akauliza, "Kwa nini ulimfukuza Malik Ashtar na masahaba wake kutoka Kufah na kwa nini uliwatenganisha na familia zao?" Uthman akasema, "Walikuwa wanasababisha vuruga Kufah na hawakumtii Gavana wangu Said bin Aas." Zubayr bin Awam akasema, Ewe Uthman matendo yako si halali. Hukuwa unafikiri na kujua ni nani hao uliokuwa unawachukulia hatua kama hizo. Mambo uliyoyataja hayakuwa sababu ya kuwafanyia mateso kama hayo masahaba wa Mtume walio heshimiwa sana.

Ewe Uthman! Endapo utaniruhusu, nitakutajia matendo yako yaliyokiuka mafundisho ya imani. Ninasisitiza kwamba umuogope Mwenyezi Mungu na usijitenge kwa sababu ya serikali ya Kiislamu ambayo wewe ni kiongozi, vinginevyo siku utakapopata malipo ya matendo yako hapa duniani, wala haipo mbali. Adhabu hii itakuwa nyongeza ya adhabu utakayopata Akhera."

15

MAISHA YA ABU DHARR

Baada ya kifo cha kutisha cha Abu Dharr ambapo watu mashuhuri wa Misri walikwenda Madina kutafuta marekebisho ya malalamiko yao na wakaingia kwenye msikiti wa Mtukufu Mtume , humo waliona mkusanyiko wa Muhajirina na Ansar. Wakawasalimia na wao wakaitikia. Waislamu waliokusanyika hapo wakawauliza watu wa Misri, "Kwa nini mmekuja hapa kutoka Misri," Wakawaelezea sababu ya safari yao ndefu kama hiyo. Walisema kwamba Gavana wa Misri aliyeteuliwa hakuwa na uwezo wa kazi kabisa na katili.

Hata hivyo watu wa Misri walikwenda mlangoni kwa khalifa Uthman na wakaomba wamuone. Wakapata ruhusa na wakaingia bada ya kupeana salamu, wakasema, "Ewe Uthman! Tumeteswa na Gavana wako. Mtendo anayoyafanya yanararua moyo, yanatia uchungu na kusikitisha. Ewe khalifa! Mwenyezi Mungu amekupatia utajiri mwingi.

Umshukuru Mwenyezi Mungu, uwe mchunguzi na mkali kwa watendaji wako na lengo lako liwe kusitawisha umma. Si tu kwamba tumeleta malalamiko dhidi ya Gavana wako, lakini pia mambo ambayo unayafanya wewe yana udhia."

Uthman akasema, "Niambieni mambo hayo ni yepi." Wakasema; "Ulimwita Hakam bin Aas arudi Madina tena, ingawa Mtume alikwisha mfukuza kutoka Madina na akampeleka Taif milele na Abu Bakr na Umar waliheshimu uamuzi wake wakati wa uongozi katika

serikali zao. Ulipasua Qurani na kuichoma. umewapa udhibiti wa maji ya mvua ndugu zako ambapo yanatakiwa yatumiwe na watu wote na watu wamenyang'anywa manufaa yake. Umewafukuza baadhi ya masahaba wa Mtukufu Mtume kutoka Madina. unataka watu wakufuate wewe kwa hali yoyote ile hata kama yale unayoyafanya yanaendana na sheria za imani au vinginevyo. Ewe Uthman! Sikiliza; tunakwambia wazi wazi kwamba tutakufuata wewe endapo utafuata njia iliyo sahihi na kama uking'ang'ania kuendeleza mwenendo ulio nao sasa, tutawajibika kutupilia mbali kiapo cha uaminifu kwako na kwa hiyo pande zote mbili kwa hakika zitaharibika.

Ewe Uthman! Mwenyezi Mungu anatambua hali ya kila mtu. Kila Muislamu lazima amuogope yeye, sikiliza Uhusiano baina ya mtawala na mtawaliwa ni dhaifu sana. Mtawala lazima amuogope Mwenyezi Mungu na aache kufanya vitu ambavyo ni kinyume na amri ya Mwenyezi Mungu na mtawaliwa lazima wamtii yeye. Mtu ataitwa kuhesabu hata matendo madogo kiasi chochote kile mbele ya Mwenyezi Mungu. Tumesema tulichotaka kusema. Sasa ni shauri lako kufanya unavyotaka."

Baada ya kusikia haya Uthman aliinamisha kichwa chake kuelekea mbele na baada ya kuwa kimya kwa muda fulani akasema, kwa hali ilivyo sasa sitatoa maelezo yoyote kuhusu upinzani wenu kwa sababu mojawapo ya haya ni mengi sana, lakini ninachosema kuhusu Hakam bin Aas kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu hakukosewa naye kwa sababu ya matendo yake mabaya na yasiyo stahili na ndio sababu alimfukuza kutoka hapa jijini. Sasa, niliposhika kazi ya Ukhalifa nilimwita arudi kwa sababu ya kuzingatia undugu wetu. Niambieni ikiwa watu wa Madina wanayo malalamiko yoyote yake, kwa hakika nitamwita ili ajieleze.

Waandishi wa historia wanasema kwamba watu walipompelekea Uthman mfululizo wa kipingamizi kuhusu mambo kadhaa, aliamua kuyafikiria mambo hayo na kuhusiana na hilo aliwaandikia barua magavana wote wa utawala wake kuwaambia watu waende Madina na kulalamika moja kwa moja kwake dhidi ya magavana. Mara tu barua hizi zilipowafikia magavana, malalamiko kutoka kila sehemu ya utawala yalianza kupelekwa Madina mfululizo.

Malalamiko ya kwanza kuasili yalikota Kufah, Basrana Misri. Kutoka Kufah, Malik bin Ashtar Nakhai akifuatana na watu mia moja. Kutoka Basra Hakam bin Heil akifuatiwa na watu mia moja hamsini. Kutoka Misri watu mia nne wakifuatiwa na Abu Umar bin Badil, Wahhab bin Waraqa Khuzai, Kanana bin Shir al-Hamni na Saidi bin Hamran Muradi walifika Madina.

Baada ya watu hawa kufika Madina, Muhajirina na Ansari waliokasirishwa na tabia ya Uthman na walikuwa wamehuzunika sana kwa sababu ya matendo yake mabaya, waliungana nao na wote wakaamua kukubaliana endapo Uthman atafikiria kuhusu mambo hayo ambayo walimpa na akatoa majibu sahihi na ya kuridhisha, walikuwa tayari kumfuata lakini kama hakutoa majibu yaliyo sahihi na ya kuridhisha, wangempindua na kumpa Ukhalifa mtu mwingine aliye bora badala yake.

Mjumbe alipo wasilisha habari hizi kwa Uthman, alitubu na kukiri kwamba alifanya kosa kubwa la kipumbavu kwa kuwaita watu hao Madina. baada ya kutafakari kwa kina sana kuhusu jambo hili, hata hivyo, alifanya uamuzi kwamba hatakutana nao. Huu ulikuwa uamuzi wake usio sahihi, lakini aliamua hivyo. Akajificha ndani ya nyumba yake na milango mikubwa yote ilifungwa kwa ndani.

Watu walipofika kwenye lango la ikulu ya Uthman, alianza kufanya mazungumo nao kutoka kwenye paa la nyumba. Akasema, Ni jambo gani ambalo nimelifanya linalowakera? Kuweni na uhakika kwamba nitakubali madai yenu yote na nitafanya kama mnavyotaka. Msiwe na wasi wasi. Sitawakasirisha kwa namna yoyote ile."

Watu hao wakassema, "umeyafanya maji ya mvua kwamba si sheria watu wote kuyatumia isipokwua ndugu zako." Khalifa akasema, Msiwe na wasi wasi. Nisikilizeni kwa makini, nimesitisha matumizi ya maji kwa sababu nimeyahifadhi kwa ajili ya ngamia ambao nimewapokea kwa njia ya sadaka lakini endapo mnataka niruhusu yatumiwe na watu wote sina kipingamizi kwa hilo."

Watu wakasema, "Umepasua nakala nyingi zisizohesabika za Qurani na ukazichoma moto. Huu ni ukiukaji wa sheria ya Kiislamu." Khalifa akajibu, "Kwa kuwa palikuwepo na matokeo mengi ya Qurani moja, nilikusanya maandishi kwenye nakala zingine zote kwenye ardhi badala ya kuzichoma?" Kwa nini hukufuatana na Mtume kwenye Vita ya Badr na kwa nini hukushiriki?" Akajibu, "Wakati huo mke wangu alikuwa mgonjwa kwa hiyo nilishughulika kumtunza." Wakasema, "Kwa nini hukushiriki kwenye Bayatus Rizwan (Kiapo cha ahadi kwa Mtume kilichofanyika Rizwan)?" Akajibu, "Nilikuwa nimetoka nje wakati huo," Wakauliza, "Kwa nini ulikimbia na kumwacha Mtume peke yake kwenye Vita ya Uhud?" Akajibu, "Nilikimbia kama mambo yalivyotokea, lakini hii ni dhambi yangu ambayo nilisamehewa. Kwa hiyo hakuna haja ya kuhoji jambo hili sasa."

Wakasema, "Umewafukuza masahaba wengi wa Mtume ambao waliteseka kwa matatizo mengi huko uhamishoni. Baadhi yao walikuwa wanaheshimiwa sana na wenye hadhi. Uliwafukuza kutoka nyumbani kwao na ukawaweka kwenye dhamana ya vijana wasio na uzoefu na watu waovu ambao alijihalalishia umwagaji damu na utajiri ulikatazwa. Ewe Uthman! Miongoni mwa wale waliofukuzwa alikuwepo pia sahaba ambaye alikuwa kipenzi cha Mtume na Mwenyezi Mungu alimuamuru Mtume ampende.

Unatambua kwamba Abu Dharr alipokwenda mahali Mtume mwenye alikuwa anatoka kwenda kumtafuta. Ulimpeleka kwenye jangwa lililo na upweke huko alikufa kwa njaa na kiu. Unayo maelezo gani kuhusu kitendo chako hiki kiovu."

Uthman akasema, "Niliwafukuza watu hawa kutoka kwenye miji ya masikini walipoanza kuwashawishi watu kutoniamini. Nilihofu kwamba wangesababisha mgogoro na kutokuelewana. Mwachieni Mwenyezi Mungu kama mnafikiria kuwa ni dhambi yangu. Sasa, kuhusu wale watu ambao bado wapo kwenye uhamisho ninasema kwamba kuanzia sasa mnaweza kuwaita kupitia kwa mtu mwingine kama mnataka hivyo. Sina kipingamizi."

Wakasema, "Dhuluma uliyomfanyia Ammar haisameheki. Kwa nini uliagiza apigwe sana hivyo kwamba akapata maradhi ya henia na bado mgonjwa hadi sasa." Khalifa akasema, "Alinikosoa mimi na akatangaza mapungufu yangu hadharani."

Wakasema, Kwa nini uligawa fedha ya Hazina ya Taifa kwa ndugu zako na kuwafanya kuwa matajiri? Masikini wanateseka na njaa na ndugu zako wanaishi maisha ya anasa.?"

Akajibu; "Umar bin Khatab pia alitumia mtindo huu.

Alikuwa anampa zaidi mwenye kujiweza." Wakasema, "Hakufanya upendeleo kama unavyofanya wewe. Uligawa fedha yote kwa ndugu zako. Hivi sifa zimewekewa mipaka kwa nduguzo tu? Salman,

Miqdad, Ammar, Abu Dharr hawakuwa na sifa hadi wakanyang'-anywa mgao wa ruzuku na msaada? Umetumia fedha yote kwa ubadhilifu na kupoteza utajiri wa Waislamu." Uthman akasema, "Kama mnadhani hivyo, fanyeni hesabu fedha ninazolipwa. Nitalipa fedha hiyo polepole na kuziweka kwenye Hazina ya Taifa."

Baada ya hapo khalifa alizungumza kwa maneno laini na kunyenyekea mbele yao, na wakati huo watu hao walikwenda zao. Khalifa hakuridhika hata walipokwisha ondoka. Alitambua kwamba watu hao wangemshambulia baada ya muda mfupi. Kwa hiyo akamwita Abdullah bin Umar na akataka ushauri wake. Alimshauri amwite Ali ili amwombe aende kuwapooza watu hao. Alikuwa na uhakika kwamba wangefuata ushauri wa Ali.

Khalifa akamwita Ali kupitia kwa mjumbe maalum na akamweleza jambo lote na jinsi alivyotakiwa kuwatuliza watu hao. Ali akamuahidi kufanya kufuatana na ombi la Khalifa na alipokwenda kwa watu akawaambia, "Ni bora zaidi kuwa na moyo mtulivu." Walikasirika sana; wakasema; "Tunakuchukulia katika heshima ya juu, lakini hatuwezi kuvumilia jeuri na kujiachia hadi kuchupa mipaka kwa Uthman." Kwa mujibu wa Athan Kufi, Ali aliwahakikishia na akasema, "Msiwe na wasi wasi, maelewano ni bora zaidi kuliko ugomvi." Baada ya hapo Ali akaenda kwa Uthman akifuatana na viongozi wa makundi hayo. Baada ya mabishano marefu walihitimisha kwa kukubaliana na Uthman aliandika mkataba wa makubaliano ambao tunaunukuu hapa kwa maneno ya mfasiri wa Tarikh Atham Kufi:

Kwa niaba ya Uthman, waraka huu umetolewa kwa maandishi kwa watu wa Basra, Kufah na Misri ambao amepinga vitendo vyangu, na ninategemea kwamba kuanzia sasa na kuendelea nitafanya kazi yangu kwa kufuata Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Suna za Mtume. Sitadharau ridhaa ya watu na nitaepuka ugomvi. Nitawaita watu

niliowafukuza warudi makwao na nitawarudishia watu misaada ya fedha walio nyang'anywa. Nitamwondosha Abdullah bin Sad bin Abi Sarah kwenye Ugavana wa Misri na nitamteua mtu ambaye angependwa na watu wa Misri."

Watu wa Misri wakasema; "Tunamtaka huyo Muhammad bin Abi Bakr bin Abi Quhafah ateuliwe kuwa mtawala wetu." Uthman akasema; "Ndio, hilo litafanyika." Kwa ufupi, Ali ndiye aliyekuwa dhamana katika mambo yote haya na ushahidi wa Zubayr bin al-Awam, Talha bin Abdullah bin Umar, Zayd bin Thabit Suhayl bin Hanif na Abu Ayyub bin Zayd, waliandikwa na alama zao zilibandikwa. Maneno ya mwisho yalikuwa, "Waraka huu uliandikwa mwezi wa Ziqadah 35 A.H." Baada ya hapo Ali na watu wote waliondoka hapo.

Waandishi wa historia wanasema kwamba Uthman alitoa waraka wa maandishi kuhusu Ugavana wa watu wa Misri, wakaondoka Madina wakiwa wamefurahi na kuridhika. Wakiwa amefuatana na Muhammad bin Abi Bakr (mtoto wa kiume wa Khalifa wa kwanza), walikuwa wamesafiri hatua kwa hatua hadi walipokuwa wamesafiri hatua tatu au walikuwa wamekwenda umbali wa siku tatu, kwa mujibu wa bin Qutaybah na Atham Kufi, wakamuona mtu amepanda ngamia akienda mwendo wa haraka kuelekea Misri.

Muhammad bin Abi Bakr aliamuru mtu huyo wakamatwe na apelekwe kwake. Watu walimwendea mtu huyo haraka na akamkamata na kumfikisha kwa Muhammad. Muhammad akamuuliza; "Unatoka wapi na unakwenda wapio?" Akajibu; "Ninatoka Madina na ninakwenda Misri." Wakamuuliza kwa nini alikuwa anakwenda Misri? Akajibu kwamba alikuwa na shughuli zake binafsi. Kwa kuwa wakikwisha mtilia shaka walimuuliza kama alikuwa na barua yoyote.

Akakataa. Muhammad bin Abi Bakr aliamuru apekuliwe. Alipopekulia, hakuna barua yoyoite iliyoonekana.

Muhammad akasema, "Pekueni kiriba chake cha maji." Maji yaliyokua kwenye chupa yalipomwagwa, waliona barua ambayo ilihifadhiwa kwa kuzungushia nta. Walipoifungua, waligundua kwamba barua hiyo iliandikwa na Uthman na ikagongwa muhuri wake na ilikuwa inapelekwa kwa Gavana wa Misri, Abdullah bin Sad bin Abi Sarah:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma Mwenye Kurehemu.

Mimi, mtumishi wa Mwenyezi Mungu, Uthman ninakuagiza wewe (Abdullah bin Sarah) kwamba mara tu Umar bin Badil Khuzai akifika kwako umkate kichwa na ikate miguu ya Alqamah bin Adis, kananah bin Bashir na Urwaisi ili wafe wakiwa wanabilingika na kugaragara kwenye damu yao. Halafu itundike miili yao kwenye miti karibu na njia panda. Utekeleze amri zilizoandikwa kwa mkono wangu, ambazo Muhammad bin Abi Bakr anazo anakuletea wewe, na ikiwezekana muue kwa kutumia mbinu zozote. Endelea kuwa gavana bila wasi wasi. Usiogope kitu chochote na uitawale Misri."

Muhammad bin Abi Bakr na watu wengine mashuhuri wa Misri walishtuka baada ya kusoma barua hiyo na wakasema, "Mkataba mzuri ulioje ambao ameuhitimisha! Kwa uaminifu wa jinsi gani kiapo kimetolewa na kwa uaminifu kiasi gani ahadi imetimizwa! Ingekuwaje kama tungefika Misri baada ya kuwasili mtumwa wa Uthman!!"

Kwa ufupi walimshukuru Mwenyezi Mungu kwamba waliikwepa hatari, na wakarudi Madina waliwakusanya masahaba wote wa Mtume na wakaisoma barua ya Uthman bin Affan mbele yao.

Baada ya kusikia yaliyokuwa kwenye barua hiyo na kugundua ukweli halisi, hakuna hata mkazi moja wa Madina aliyekuwa na huruma kwa Khalifa. Msisimko wa uasi mkubwa ulikuwa unatokeza pole pole na watu wote wakaanza kuzungumza wazi wazi shutuma dhidi ya khalifa. Nyoyo zilijaa shauku na kwa sababu ya hila hii kila mtu alikasirikia utawala wa Khalifa. Watu hao -kwa mujibu wa al-Fakhri ambao waliwahi kusikia sentenso ya Aishah 'Muueni yahudi huyu Uthman" na watu hao ambao kwa mujibu wa Atham Kufi walikirahishwa na kuhuzunishwa ssana, kwa sababu wazee wao waliteswa, walikuwa tayari kupigana.

Bani Salim walikasirishwa kwa sababu ya Abdullah bin Masud, BaniMakhzum walikwua na wasi wasi kwa sababu ya tukio la hatari lililomtokea Ammar bin Yasir na Bani Ghifar walikasirishwa kwa sababu ya yale aliyofanyiwa Abu Dharr Ghifari. Kwa maneno mengine, makabila haya yaliasi kwa sababu ya tabia ya Uthman kuhusiana na viongozi wao na walikasirika sana hivyo kwamba hawakuwa wanafikiria jambo lingine isipokuwa kumuua Uthman.

Katika hali hi makala yote pamoja na watu wa Misri waliazimia kumuona Ali Kwanza, kwa sababu yeye alikuwa dhamana yao katika mkataba wao na walitia sahihi hati ya mkataba kwa cheo hicho. Kwa hiyo watu wote walikwenda kwa Ali na wakampa barua hiyo ya Khalifa iliyozuiwa njiani. Ali alipoisoma barua ile na kufahamu yaliyoandikwa humo, alishtuka sana. Alisema kwa mshangao mkubwa, "Mimi nimeshangaa sana. Uthman amefanya nini?" Baada ya hapo Ali alikwenda kwa Uthamn akiwa na barua hiyo na akaiionesha mbele yake, alisema, "Soma barua hii!" Uthman aliposoma hadi mwisho, Ali akasema, "Mimi sijui nifanye nini kuhusu wewe. Umecheza mchezo wa uharibifu. Niliwafanya watu hawa wakubaliane na wewe. Sasa umefanya yasiyofikiriwa kufanywa na Muislamu. Ninasikitika kwamba hata hukutambua ugumu niliopata katika kuondoa uadui wao kwako. Unatambua kwamba, watu hawa walikwishaondoka kwenda kwao wakiwa wameridhika na kufurahi kikamilifu kwa sababu ya imani yao kwangu. Ewe Uthman! Nilidhani jambo hili lilikwisha suluhishwa moja kwa moja. Nilidhani kwamba uadui uliondolewa na Waislamu walikwisha maliza ugomvi huu. Lakini loo! Niambie hii ni barua ya aina gani? Nani mwandishi wa barua hii? Hiki ni kitendo cha aina gani? Kutumia itakuwa maoni gani kuhusu udanganyifu hu na njama hii?"

Uthman akasema, "Ewe Abul Hasan! Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sikuandika barua hii, wala sikumwambia mtu yeyote kuandika, wala sikumwambia mtumishi wangu kwenda Misri. Mimi sijui lolote kuhusu tatizo hili!" Ali akauliza; "Huyu ni ngamia wako?" Akajibu; "Ndio." Ali akauliza tena, "Muhuri wako?" Akajibu, "ndio" Ali akasema; "Mwandiko huu unafanana na ule wa mwandishi wako. Muhuri wa kwako. Mtumwa wa kwako na ngamia ni wa kwako; hata hivyo unasema kwamba hujui lolote!" Khalifa akasema; "Inawezekana kwamba sikutaarifiwa, na barua ikaandikwa na kusafirishwa." Hata hivyo, Ali aliondoka hapo baada ya mazungumzo haya.

Hatimaye, Khalifa alihutubia kwenye Msikiti wa kati na alijaribu kutoa mmaelezo kuhusu msimamo wake kuhusu barua Watu wakasema, "Sawa! Tunadhani kwamba hukuandika barua hii. Lakini imethibitishwa kwamba imeandikwa na mkono wa mwandishi wako, Marwan. Muhuri ni wako. Ngamia ni wako. Mtumwa ni wako. Sasa tunakuomba urudi kwenye ikulu yako na utuletee Marwan."

Khalifa akasema, "Hapana, kamwe haitawezekana!"

Ghasia kubwa zilitokea baada ya mazungumzo haya. Kwa mujibu wa Tham Kufi mapigano yalianza na msikiti ukageuka kuwa uwanja wa

vita, hali hiyo iliendelea kuwa mbaya zaidi hivyo kwamba Uthman alipoteza fahamu kwa sababu ya kupigwa mawe. Halafu akaondoshwa hapo na kupelekwa kwake.

Sasa muda ulikaribia ambapo wale watu ambao waliagizwa na Uthman kuwa huko Misri waliamua kutekeleza amri ya Ummul Muminina, mfululizo wa maneno, "Muueni Yahudi huyu! Amekua asi!" Kwa hiyo watu wakaizunguka nyumba ya Khalifa. Al-Fakhi ameandika kwamba mara tu nyumba ilipozungukwa na waasi, Aishah aliondoka Madina na akaelekea Makkah na khalifa Uthman akauawa na watu, chini ya uongozi wa Muhammad bin Abi Bakr:

Kwa mujibu wa Tarikh Abul Fida, Uthman aliuawa tarehe 18, Zilhajjah 35 A.H.Ukhalifa wake ulidumu kwa muda wa miaka kumi na tatu. Mwili wake ulidumu siku tatu bila kuzikwa kwa sababu maadui zake walizuia asizikwe. Kwa mujibu wa bin Jarir Tabari, maiti ya Uthman ilidumu siku mbili na hakuna mtu aliyediriki kuuzika. Mwandishi wa historia, Atham Kufi, ameandika kwamba maiti ya Uthman haikuzikwa mpaka baada ya siku tatu na haukupata ulinzi hadi mbwa walinyofoa mguu wake mmoja. Baada ya hapo, Hubayr bin Mutia Taujeer bin Mutim na Hakim bin Hizam walikwenda kwa Ali na wakasema, "Tafadhali jaribu kupata maiti hiyo izikwe." Kufuatana na vitisho vya Ali, mpango ulifanywa kuzika maiti hiyo. Lakini watu hawakukubali maiti hiyo izikwe kwenye uwanja wa makaburi ya Waislamu! Hatimaye mwili wake ulizikwa Hash Kaukab uwanja wa makaburi ya Wayahudi.

Baada ya hapo mwandishi wa historia huyo huyo ameandika kwamba tukio hili lilitokea tarehe 17, Zilhajjah, 35, A.H. siku ya Ijumaa baada ya Sala ya Alasiri. Uthman alikuwa na umri wa miaka 82. Taarifa ya tukio hili ilipomfikia Aishah, mama wa Waumini huko Makkah alipojua kwamba Uthman aliuawa na masahaba mashuhuri wa Mtume, alifurahi sana na akasema, "Mwenyezi Mungu amempa

malipo kwa ajili ya matendo yake. Ninamshukuru Mwenyezi Mungu, Amemwadhibu kama ilivyo stahili."[139]

Kwa ufupi, Uthman aliuawa miaka mitatu tu ya kifo cha kutisha cha Abu Dharr. Ukitafakari kwa uangalifu, mauaji yake yalihusiana na matendo hayo ambayo Abu Dharr alimwambia aache kufanya. Kama Uthman angekubali ushauri wa mheshimiwa Abu Dharr, hangekutana na siku kama hii, na mabalaa kama hayo hayangemfika na Abu Dharr pia hangetupwa huko upwekeni Rabzah ambako alikufa kifo cha kutisha.

SURA YA ISHIRINI NA MBILI

Jaun bin Huwi alikuwa mtumwa wa Abu Dharr ambaye historia ya maisha yake yanaonekana jinsi alivyofundishwa na Abu Dharr. Kwa mujibu wa Mama qani, nasaba ya Jaun ni kama ifuatavyo: Jaun bin Huwi bin Qatadah bin Awar bin Saidah bin Awf bin Kab bin Huwi Habashi[140]

Imeandikwa kuhusu mtu huyu kwamba alikuwa wa jami ya Kiafrika na alikuwa anamilikiwa na Fadhl bin Abbas bin Abdul Muttalib, ambako Ali alimnunua kwa sarafu za dhahabu 150 na akamtoa kama zawadi kwa Abu Dharr. Ali alitaka Jaun amtumikie Abu Dharr.

Kama ilivyotarajiwa, Jaun alifanya kazi inayostahili sifa kwa Abu Dharr ambaye alikuwa akifurahi sana kuwa anaye. Jaun alimtumikia Abu Dharr na pia alipata faida ya kuwa naye. Alichunguza kila kipengele cha tabia ya Abu Dharr kwa uangalifu mkubwa na alipendezwa sana nayo.

16

MAISHA YA ABU DHARR

Kwa mambo yalivyokuwa, Jaun alimtumikia Abu Dharr kwa kila jinsi alivyoweza. Pia hakuna mahali ambapo alikosa heshima ya kuwa na Abu Dharr isipokuwa huko Rabzah ambako kuwepo kwake huko hapatajwi na mwandishi yeyote wa kuaminika wa historia. hata hivyo, Jaun alimtumikia Abu Dharr kwa ufanisi kwa kadiri alivyoweza. baada ya Abu Dharr kuondoka kwenda Rabzah yeye alibaki na kuendelea kumtumikia Ali. Baada ya Ali kufa kishahidi aliendelea kumtumikia Imamu Hasan naye alipokufa kishahidi mwaka wa 50 A.H alianza kumtumikia Imamu Husein.

Kwa ufupi, aliwatumikia kwa uaminifu watu waadilifu maisha yake yote. Imamu Husein alipoondoka Madina na kwenda kwanza Makkah na halafu Karbalah wakati wa mwezi wa Rajabu, mwaka wa 60 A.H. Jaun alikuwa naye kwenye safari hii.

Allamah Majlisi na Allamah Samawi wameandika kupitia kwa mamlaka ya Sayyid Razi daudi kwamba mapigano yalipoanza Karbala tarehe 10, Muharram, mwaka wa 61, A.H. Jaun alikwenda kwa Imamu Husain na akaomba ruhusa apigane. Imamu Husain akasema unaruhusiwa.

Lakini ewe jaun! Umeishi na mimi kwa kipindi kirefu katika amani na sasa unataka kuuawa!" Aliposikia maneno haya, Jaun alianguka miguuni mwa Imamu Husain na akasema, "Ewe bwana wangu, mimi si mmojawapo wa wale wanaokudanganya wakati wa amani na na furaha, na kukuacha wakati wa dhiki. Ewe bwana wangu! Hapana shaka kwamba jasho langu hunuka harufu mbaya, nasaba yangu si ya watu bora na rangi yangu nyeusi, lakini ukiniruhusu, jasho langu litanukia harufu nzuri, nasaba yangu itakuwa bora na rangi yangu itakuwa nyeupe huko peponi. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sitakuacha hadi hapo damu yangu itakapo changanyika na damu yako."

Hatimaye Imamu Husain alimpa ruhusa. Jaun akaingia kwenye uwanja wa vita, akaanza kupigana na akakariri rajaza ifuatayo: "Enyi mliolaaniwa! Mliwahi kuona mtumwa Mwafrika anavyopigana? Angalieni anavyopigana akiwaunga mkono uzao wa Mtukufu Mtume!"

Baada ya kukariri 'rajaz' Jaun alifanya shambulizi kali kwa adui na aliendelea kupigana mfululizo hadi akawaua maadui ishirini na tano na yeye mwenyewe alikufa kishahidi (Muntahul Amal).

Muhammad bin Abi Talib Makki ameandika kwamba Jaun alikufa kishahidi, Imamu Husain alikwenda kwenye maiti yake, akaweka kichwa chake kwenye maiti yake, akaweka kichwa chake kwenye paja lake na akamwombea Mwenyezi Mumgu; "Ee Mwenyezi Mungu! Tia nuru uso wa Jaun, fanya jasho lake liwe na harufu ya kupendeza na mpe mahali awe na waadilifu wa huko Peponi, ili aweze kuwa na Muhammad na uzao wake (Ahlul-Bait)."

Wasomi humnukuu Imamu Muhammad Baqir ambaye humnukulu baba yake Imamu Zaynul Abidin akisema kwamba siku chache baada ya Bani Asad kuzika maiti ya mashahidi na kuondoka, waliona maiti ya Jaun ambayo uso wake ulikuwa unang'ara na maiti yake ilitoa harufu nzuri ya manukato.[141]

Kwa ufupi, mtumwa huyu mwaminifu wa Abu Dharr aliyeweka mhanga maisha yake kwa ajili ya bwana wake, Imamu Husain, aliyekuwa anapigana na Yazid bin Muawiyah Dikteta wa Umayyad, kwa ujasiri ushujaa na ushupavu na akafa shahidi.

Ni ukweli uliothibitishwa kwamba mara tu baada ya kutawafu Mtukufu Mtume, mafundisho yake yote na maonyo hayakutiliwa

maanani na wanafiki, ambao lengo lao moja tu lilikuwa kupata manufaa ya kidunia na wakayadharau mafundisho ya Mtume.

Baadhi ya masahaba wa Mtukufu Mtume walikuwa waumini imara wa Uislamu na mapenzi yao kwake na Ahlul Bait wake yalijaa kwenye mioyo yao, walinyanyuka kupigana kufa na kupona na hizo nguvu za uovu. Walikuwa wafuasi wa kweli wa Mtume Muhammad na Ahlul-Bait wake na walichukua mwongozo kutokana na yale waliyoyasema na kuyatenda. Pia walipata masahaba wengine ambao walipata uwezo na mamlaka kwa jina la Uislamu. Lakini badala ya kutumikia njia ya Uislamu, wakalitumia vibaya jina la Uislamu na utajiri kwa maslahi yao binafsi na kujiongezea kifamilia. Walifuja utajiri wa taifa kama vile ulikuwa rasilimali yao. Miongoni mwa masahaba alikuwepo mmoja ambaye aliweza hata kutamka; "Kwa jina la Mwenyezi Mungu hadi hapo nitakapolifuta jina la Mtume Muhammad kutoka kwenye uso wa ardhi sitapata amani". (Murujuz Zahab Andalus Press) Matokeo yake ni kwamba mfumo mpya wa utawala ulijitokeza yaani ufalme ambao ulisababisha matisho miaka iliyofuata. Kupotoshwa kwa Uislamu kwa namna hiyo haikuvumiliwa na masahaba wa kweli ambao hawakujizuia kusema kweli hata kama ilimanisha kupoteza maisha.

Abu Dharr ni mfano wa wazi wa kubeba dhiki za kila aina na uimara na ujasiri ambazo ni sifa alizozionesha alipokuwa anateswa na mateso hayo yalikuwa makali kiasi cha kusababisha kifo chake kama ambavyo ilikwisha tabiriwa na Mtukufu Mtume(s.a.w.w) . Mfano wake ulifuatwa na mtumwa wake Jaun ambaye naye pia alijitoa mhanga kwenye mchanga wa Karbala ambapo aliamua kuutetea Uislamu bega kwa bega na mjukuu wa Mtukufu Mtume, Husein(a.s) .

SHARTI YA KUCHAPA

Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.

MWISHO WA KITABU