• Anza
  • Iliyopita
  • 21 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 20689 / Pakua: 3997
Kiwango Kiwango Kiwango
MAISHA YA ABU DHARR

MAISHA YA ABU DHARR

Mwandishi:
Swahili

3

MAISHA YA ABU DHARR

Baada ya haya, Abu Dharr na Unais waliketi kwenye nafasi zao wakitazamana uso kwa uso na mtemi, Khafaf. Khafaf alisema kwa sauti ya upole lakini kali, "Ewe Abu Dharr! Ninayo Taarifa kwamba wewe umekuwa na msimamo wa kumuabudu Mwenyezi Mungu Ambaye haonekani. Watu mashuhuri wa kabila letu wamekasirika na msimamo wako huu. Wanasema kwamba Abu Dharr amewatukana miungu yao na anawaita hawana hekima yoyote.

Ewe Abu Dharr! Tunakuheshimu lakini haimaanishi kwamba tupo tayari kustahamili miungu yetu kubezwa. Ninakuomba uache hoja ya mawazo yako ya sasa na urudi kwenye imani ya wahenga wako, au vinginevyo unatakiwa uieleze imani yako kwangu ili niweze kuelewa ukweli wa imani yako. Pia, ninakuhakikishia kwamba nitafikiria kuingia kwenye imani hiyo endapo utathibitisha kwamba imani yako haina shaka zaidi kuliko ya kwetu.

Abu Dharr naye alijibu, "Ewe mtemi wa kabila! Tunakuheshimu na kustahi chochote unacho sema. Lakini, wakati huo huo tunataka kueleza kwamba Mwenyezi Mungu, wa Pekee Ambaye tumeamua kumuabudu na Ambaye tunamwamini, ni huyu huyu ambaye ameumba dunia na mbingu, Ambaye huruzuku viumbe vyote, Ambaye kudhibiti maisha ya viumbe vyote vyenye uhai na Ambaye uwezo wake hauna mipaka.

Masanamu ambayo tumekuwa tunayaabudu hadi sasa, yametengenezwa na mikono yetu kwa kutumia patasi na nyundo. Akili inaweza kuamrisha kwamba yule ambaye ametengenezwa na mikono yetu anaweza kuwa muumbaji wetu, anaweza kuruzuku na tusikiliza dua zetu?

Mwanadamu ni kiumbe bora zaidi kuliko viumbe vya muumbo wote. Inawezekana yeye na heshima yake astahili kuinamisha kichwa chake mbele ya jiwe? Mtemi wangu! Tafadhali tafakari bila upendeleo kuhusu haya ninayosema. Masanamu hayana hata uwezo wa kufukuza adui yao.

Nisikilize, ewe mtemi! Wakati fulani nilikwenda kwa Manat na nikampa sadaka ya kikombe cha maziwa. Nilikuwa bado nipo eneo hilo ambapo mbweha alifika hapo na akanywa maziwa hayo yote na akamkojolea Manat. Tukio hili liliniathiri sana na nilifikiri kwa nini mungu anashindwa kujilinda mwenyewe?

Jambo hili lilinidhihirishia kwamba sanamu haliwezi kuwa mungu. Nina uhakika na kila mtu mwenye akili ataamini kwamba Muumbaji wa mbingu ni bora zaidi kuliko mbingu na muumbaji wa dunia ni bora zaidi kuliko ardhi. Kwa mujibu wa kanuni hii yenye mantiki, masanamu hayawezi kuwa ni bora kuzidi sisi, haina maana sisi kuyaabudu.

Ewe mtemi wangu! Nimekuja kwenye kweli kwamba Mwenyezi Mungu ni Peke Yake Ambaye ni Mumbaji na mwenye kuruzuku ulimwengu, na Muhammad Mustafa ambaye alipelekwa Makkah ni Mjumbe Wake.

"Anazo sifa nzuri kama hizo hivyo kwamba hakuna afananaye Naye hapa duniani. Quraishi ambao ni maadui zake wabaya wanakubali

ukweli wake na uwezo wake. hata wanapojua kuwa Muhammad ni mpinzani mkubwa wa miungu yao na dini yao, wamempatia jina la Sadiq na Amin, kama ambavyo, nimetambua hivi karibuni tu. Sikiliza! Uso wake unang'aa nuru na hekima inatiririka kutoka kwenye maneno yake."

Mara tu Abu Dharr alipomaliza hotuba yake, kelele kubwa ilitoka sehemu zote, "Jinsi gani maneno ya Abu Dharr yalivyo matamu! Kwa hiyo, miungu yetu haisikii na haisemi! Abu Dharr ameidhalilisha imani yetu na anaitukana miungu yetu!"

Kundi moja lilisema kwa pamoja, "Rafiki zangu! Msizungumze mambo yasiyo na mantiki. Kwa uaminifu tunasema kwamba lolote alilosema Abu Dharr linaonekana kuwa sahihi na akili inataka kwamba lazima tukubali ukweli. Tunao uhakika kwamba hatuwezi kupata mwongozo mzuri zaidi kuzidi yale ambayo Abu Dharr ametuletea."

Sauti nyingine ilitokeza: "Nchi ya Arabuni inahitaji muongozaji na inaonyesha kama vile hakuna mwongoaji bora zaidi kuliko huyu ambaye amedhihirishwa na Abu Dharr."

Halafu sauti nyingine ilitokeza, "Hotuba ya Abu Dharr ni ya maana sana." na baada ya hii sauti ya juu sana ilitokeza; kama vile ingetoboa masikio, Ewe Abu Dharr! Ninashahidilia kwamba hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu na ninakiri kuamba Muhammad ni Mtume Wake!"

Alipoona hivi, Khafaf, mtemi wa kabila, baada ya kufikiri sana alinyanyua kichwa chake na akawaambia watu wake: "Wapendwa watu wa kabila langu! Nisikilizeni kwa makini. Mmesikia yote hayo aliyoyasema Abu Dharr. Ni wajibu wetu kutafakari kuhusu hotuba

yake kwa uangalifu sana na kwa makini sana na tuweze kuona inayo kiasi gani cha ukweli.

Uamuzi wa haraka haufai. Si busara kutupilia mbali ushauri wa mtu bila kuchunguza. Rafiki zangu! Mnatambua kiasi cha machafuko yaliopo miongoni mwetu na jinsi uhalifu ulivyo zidi ambao sisi tunahusika. Matajiri wanawanyonya masikini na hakuna mipaka katika kufanya dhambi na maovu.

"Mimi nimeamua kwamba lazima nikubali na kuunga mkono yale anayoyasema Abu Dharr. Sasa ni juu yenu nyinyi kujiamulia wenyewe. Sikilizeni nyinyi nyote. Ninashahidilia kwamba hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wake!"

Mara tu Khafaf alipotamka Kalimah (la ila ha illalah Muhammadan Rasulillah) palitokea kelele kubwa ndani ya kabila, Khafaf amekuwa Muislamu. Khafah ameingia Uislamu!"

Haikupita muda mrefu baada ya Khafaf kuingia kwenye Uislamu, hali ya kabila ilibadilika kabisa. Watu walio wengi walisilimu na kuwa Waislamu hapo hapo, ambapo wengine walingojea kukubali kuwa Waislamu mbele ya Mtukufu Mtume baada ya kuwasili huko Madina.

Kwa ufupi, kwa juhudi kubwa ya Abu Dharr watu wengi wa kabila la Ghifar walikubali kuwa Waislamu na palitokeza ukelele wa "Mungu Mkubwa! na "Mungu ndiye Mwenye Kusifiwa!" na jina la Mtukufu Mtume likaanza kutangazwa mchana na usiku.

Baada ya kujaza moyo wa Uislamu kwenye kabila la Ghifari na kuwasilimisha watu na kuingia kwenye Uislamu, Abu Dharr alielekeza umakini wake Asfan. Alipofika huko alianza kuhubiri Uislamu miongoni mwa watu. Kwa kuwa sehemu hii ilikuwa kwenye njia kuu iliyotumiwa mara nyingi na Quraishi na alijenga hisia dhidi yao kwa sababu ya mateso aliyofanyiwa nao alifanya zoezi la nidhamu kali katika kuwafanya kuwa Waislamu. Kundi la Quraishi lilipopita hapo, aliwaeleza habari ya Uislamu na kwa hiyo idadi kubwa ya Quraishi walikubali kuwa Waislamu.

SURA YA NNE

Abdul Hamid Jaudatus Sahar wa Misri ameandika, Uislamu ulienea Madina kama moto wa mbuga ya majani makavu." Kabila la Ghifar lilifurahishwa sana na hali hiyo. Waislamu walipongezana wao kwa wao kwamba makabila mawili ya Aus na Khazraj, ambao walikuwa wasemaji sana, wapiganaji wazuri sana na waunga mkono wazuri sana walikubali kuingia kwenye Uislamu, na pia kwa kuwa Mwenyezi Mungu alikwisha ridhika kuinyanyua dini Yake na alinuia kumsaidia Mtukufu Mtume na kutimiza ahadi yake.

Unais alikwenda kwa kaka yake Abu Dharr akiwa na habari za kufurahisha na akasema "Uislamu umeenea Madina na Aus na Khazraj wamekubali Uislamu!"

Abu Dharr akasema, "Mtume wa Mwenyezi Mungu atakwenda na kuhamia huko baada ya kipindi kifupi."

Unais alimwangalia kaka yake kwa mshangao na alisema, "Umepokea habari zozote za aina hiyo?"

Abu Dharr, "Hapana, wala sina taarifa yoyote kuhusu habari hizi, ama kujua kwamba watu wa Yathrib wamekuwa waumini."

Unais, "Vipi sasa ulijua kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu atahamia Yathrib?"

Abu Dharr, "Aliniambia siku hiyo hiyo nilipokutana naye, kwamba alitarajia kwenda kwenye mji wa mitende na nadhani sehemu hiyo ya Yathrib, Mtume alisema kweli."

Unais, "Inawezekana kwamba kabila lake litamruhusu aondoke hapo akiwa na Waislamu, ili kwamba baada ya matayarisho kamili awashambulie?"

Abu Dharr, "Wanaweza wakamruhusu au wasimruhusu, lakini baada ya kipindi kifupi atahamia huko. Kama mambo yalivyo, ni Mwenyezi Mungu tu ndiye anaye jua ni vipi na lini itatokea."

Abu Dharr alisilimisha kabila lake na kuingia kwenye Uislamu baada ya yeye kuwa muumini. Halafu akaelekeza shughuli hiyo Madina. tangu aliporudi kutoka Makkah hadi kuhama kwa Mtukufu Mtume, Abu Dharr alikuwa anashughulika na kuhubiri Uislamu na aliendelea kufanya juhudi kuipeleka dini ya Mungu kwa umma Mtukufu Mtume aliendelea kufanya kazi yake ya kuhubiri Uislamu na Quraishi waliendelea kufanya kazi yao ya kumtesa Mtume. Walimpa mateso makubwa sana hivyo kwamba hakuwa na uchaguzi mwingine isipokuwa kuondoka nyumbani kwake. Kwa ufupi, kwa amri ya Mwenyezi Mungu Jibril alimwambia aondoke Makkah baada ya kumwambia Ali alale kwenye kitanda cha Mtume.

Alifanya alivyoagizwa. Alimwambia alale kitandani pake na akaondoka, hivyo kwamba Quraishi hawangejua kama hayupo kitandani pake. Baada ya kukaa siku tatu kwenye pango la Hira aliondoka kwenda Madina.

Abu Dharr alikuwa anangojea uhamiaji Madina. Watu wa kabila lake pia walikuwa wanangojea na walikuwa wanauliza mara kwa mara habari za Mtukufu Mtume kwa mtu yeyote aliyetokea sehemu hiyo.

Kuanzia Makkah na baada ya kukaa kwa muda wa siku chache pangoni, Mtume aliondoka kwenda Madina. Kabila la Ghifar lilipopata taarifa kwamba alikuwa kati ya Makkah na Madina walifurahi sana. Abu Dharr alihisi wimbi la neema lilikuwa linakuja. Aliungana na kabila kungoja.

Watu walikusanyika na kumzunguka na walimuuliza kuhusu Mtume wa Mwenyezi Mungu, mwenendo wake na umbile lake alijibu, "Mtamuona baada ya muda si mrefu.

Yeye ni bora kuliko wote na anamzidi kila mtu kwa sifa." Watu walipongojea kwa kipindi kirefu, Abu Dharr alikuwa anaangalia njia, ili awe mtu wa kwanza kuwataarifu watu atakapo wasili Mtume na kutuliza nyoyo za watu na kuondoa hofu iliyokuwa inawaelemea kwa kungojea kwa kipindi kirefu hivyo.

Muda uliendelea kupita. Watu wa kabila la Ghifar walikuwa na shauku kubwa ya kumpokea Mtume. Abu Dharr alipotupa jicho aliona ngamia anakwenda hapo. Watu wote walikuwa wanaangalia macho ya Abu Dharr. Baada ya muda mfupi, Abu Dharr akasema kwa sauti ya kushangaa, "Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mtume anawasili!"

Allamah Subaiti ameandika, "Uso wa Mtukufu Mtume ulikuwa unatoa nuru. Kwa ufupi watu wote walimfuata Abu Dharr, huku wakisema kwa sauti moja, "Mtume wa Mwenyezi Mungu amekuja! Mtume wa Mwenyezi Mungu amekuja!" Abu Dharr alikwenda mbele haraka na akashika hatamu ya ngamia wake.

Watu walianza kusema, "Allahu Akbar." (Mwenyezi Mungu Mkubwa) huku wakimzunguka Mtume kwa hamu kubwa. Wanawake wote, vijana na vikongwe, wavulana na wasichana walikuwa wanashangilia kwa furaha kubwa. Mtume wa Mwenyezi Mungu amewasili! Mtume wa Mwenyezi Mungu amewasili!"

Baada ya hapo watu wa kabila la Aslam walisema, "Pia na sisi tumekuwa Waislamu kama walivyo fanya ndugu zetu wa kabila la Ghifar." Mtume wa Mwenyezi Mungu alifurahi sana na alinyanyua mikono yake kuelekea mbinguni aliomba, "Ee Mola wa ulimwengu! Wasamehe kabila la Ghifari na uwaweke kabila la Aslam salama."

Baada ya hapo Mtukufu Mtume aliteremka kwenye ngamia na akaanza kukariri Quran. Sauti yake iliingia kwenye nyoyo za watu. Halafu akaanza kuhubiri. Watu walikwenda mbele kwa makundi na kutoa kiapo cha utii kwake. Abu Dharr alisimama kwa maringo karibu na Mtume akiwa amefurahi kupita kiasi.

Watu wa kabila la Ghifari walijitokeza mbele na wakasema, "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Abu Dharr alitufundisha yote yale uliyomwambia. Tukasilimu na kuwa Waislamu na tukakiri kwamba wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu."

Baada ya hapo watu walifurahi sana na walikuwa wanaangalia uso wa Mtume mara kwa mara. Abdul Hamid Jaudatus Sahar ameandika, "Watu walianza kuangalia uso wa Mtume kwa makini, waliona kwamba alikuwa mtu mwenye uso unao ng'aa midomo inayo tabasamu na tabia njema kuhusu umbo lake, hakuwa mwembamba au aliye konda ama mnene. Alikuwa na sura nzuri ya kupendeza.

Macho yalikuwa makubwa na meusi, kope za macho zilikuwa ndefu, nyusi zake nyeusi zilizojikunja mfano wa tao, nywele nyeusi, shingo

ndefu na ndevu nyingi. Alikuwa Mtukufu wakati ametulia na alikuwa anatia moyo kwa heshima wakati anasema. Mazungumzo yake yalikuwa matamu. Wala hakuwa mkimya au msemaji. Alikuwa na sura ya kupendeza sana akiwa mbali na mzuri sana akiwa karibu.

Saizi ya umbile lake ilikuwa ya kati, wala hakuwa mrefu sana kiasi cha kutokupendeza kumwangalia, ama mfupi sana kiasi cha kufikiriwa kuwa mtu duni.

Baada ya hapo Mtukufu Mtume aliondoka kwenda Madina na Abu Dharr aliendela kuishi na kabila lake."

Kutoka hapo, Mtukufu Mtume aliondoka kuelekea Madina. Alipofika Madina, watu walimkaribisha kwa moyo mkunjufu. Mara tu baada ya kufika, alianza kuhubiri ujumbe wa Uislamu. Abu Dharr ambaye hakuweza kumsindikiza Mtukufu Mtume huko Madina aliishi mjini kwake kwa kipindi kirefu sana hivyo, vita kuu tatu za Kiislamu (Ghazawat) vita vya Badr, mwaka wa 2, Hijiriya, Uhud mwaka wa 3 Hijiriya, na Ahzab mwaka wa 5 Hijiriya zilipiganwa hadi mwisho.

Baada ya vita ya Ahzab, aya ya Quran Tukufu ilimlazimisha Abu Dharr kuondoka kwenda Madina. Siku moja alikuwa anashughulika na dua baada ya Swala ya jioni kwenye msikiti wa mjini kwake, ambapo alisikia mtu anasoma kwa sauti Aya (61:10)

"Enyi mlio amini! Nikuonyesheni biashara itakayokuokoeni na adhabu iliyo chungu ."(61:10)

Baada ya kutafakari maana ya Aya hii alipata shauku ya Jihadi na akamwambia Unais, "Nitaondoka kwenda Yathrib kesho."

Unais: "Sawa! Nenda. Mwenyezi Mungu na akufikishe huko Salama!"

Abu Dharr, "Sitarudi. Nitatumia maisha yangu yote katika kumtu-mikia Mtukufu Mtume."

Unais, "Ewe ndugu yangu! Umekuwa muumini wa kweli na imani imepenya kwenye moyo na roho yako. Kabila lako na watu wako hapa wanakutaka sana. Patakuwepo pengo kubwa sana ukiondoka hapa. Nadhani ungeacha mpango wa kwenda Madina na uishi hapa hadi mwisho wa uhai wako."

Abu Dharr; "Mtukufu Mtume ni bora zaidi kuliko watu hawa. Chochote ambacho kimetekelezwa kinatosha. Mtukufu Mtume alipigana Badr, Mimi sikuwa naye. Akapigana huko Uhud Mimi si kuwepo. Hadi lini nitaendelea kulitumikia kabila langu na nikose baraka za kufa shahidi. Yote hayo ambayo yamefanyika mpaka sasa yanatosha. Sasa sitakata tama hata kwa dakika moja kuhusu uamuzi wangu wa kwenda Yathrib."

Unais, "Pendekezo langu ni kwamba wewe uendelee kuishi hapa nyumbani kama kawaida. Mtukufu Mtume atakuita yeye mwenyewe atakapokuhitaji. Wewe angalia walikuwepo watu wengi waliokuwa katika miji ya kwao na waliondoka kwenda Madina baada ya kuitwa na Mtukufu Mtume."

Abu Dharr akasema: "muda wa kungojea umepita. Endapo Mtume hajaniita mimi pia nina wajibu. Sitaendelea kungoja, nitakwenda huko bila kuitwa."

Unais: "Vema! Lakini usifanye haraka. Chukua mahitaji ya muhimu kwa safari."

Abu Dharr; "Sihitaji chochote. Vipande vya mikate mikavu vinanitosha."

Abu Dharr aliondoka nyumbani kwake na kuelekea Madina. Alipofika huko alipata heshima ya kukutana na Mtume na akawa naye.

Alikuwa na desturi ya kulala kwenye msikiti wa Mtume usiku na wakati wa mchana alikutana na watu. Alikula chakula pamoja na Mtume na akaiga maisha yake ya kidunia kwa uchaji Mungu na uadilifu. Alifanya bidii sana kujifunza hadithi za Mtume na kuzihifadhi katika kumbu kumbu.

Baada ya kuifika Madina Abu Dharr aliugua kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa. Mtume alipata taarifa ya ugonjwa wake. Akaenda kumuona Abu Dharr na akamwambia; "Abu Dharr! Unatakiwa uishi nje ya Madina kwa muda fulani sehemu ambayo ngamia, kondoo na mbuzi wa taifa huchungwa na uzingatie kwamba usile chochote isipokuwa maziwa wakati wote utakapo kuwa kule."

Mara tu baada ya kupokea amri ya Mtume, Abu Dharr aliondoka kwenda mahali hapo alipoambiwa akiwa na mkewe.

Ugonjwa ulikuwa mkali sana kwa kipindi cha siku kadhaa lakini, ulipungua pole pole akapata afya nzuri hadi akaweza kutimiza tendo la ndoa na mke wake. Sasa, palijitokeza tatizo la upatikanaji wa maji kwa ajili ya josho kubwa la kuondoa janaba kabla ya Swala. Hadi hapo alikuwa hajajua Tayamamu. Kwa hiyo alikuwa hajui la kufanya kwa muda fulani. Hatimaye akili yake ilimwongoza na akaenda kumuona Mtume kwa mwendo wa haraka sana wa ngamia. Mara tu

Mtume alipomuona Abu Dharr alitabasamu na alisema kabla Abu Dharr hajasema, "Abu Dharr! Usiwe na wasiwasi. Maji yametayarishwa kwa ajili yako hapa na sasa hivi. kwa hiyo, msichana aliyekuwa mtumishi wa Mtume alitayarisha maji na Abu Dharr akaoga. Baadaye alikwenda kwa Mtukufu Mtume na aka fundishwa jinsi ya kutumia udongo kwa ajili ya kuchukua Wudhu (Tayamamu)- (Musnad Ahmad bin Hanbal).

Abu Dharr alikuwa anaendesha maisha yake ambapo Vita ya Tabuk ilitokea mnamo mwaka wa 9 Hijiriya. Waandishi wa historia wanasema kwamba Mtume alijua kwamba Wakristo wa Syria walifanya uamuzi thabiti wa kushambulia Madina na wapiganaji elfu arobaini kutoka kwa Harcules, Mfalme wa Roma. Kwa hiyo, Mtume aliamua kuondoka kwenda Syria kama hatua ya tahadhari akiwa na wapiganaji kati ya elfu thelathini hadi arobaini. Alimteua Ali kuwa mbadala wake Madina. Baada ya kutayarisha jeshi lake aliondoka Madina.

Baada ya kuondoka Mtume wanafiki walianza kumdhihaki Ali kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu alimwacha ili kupunguza mzigo wake mwenyewe. Katika kuwathibitishia kwamba wanafiki ni waongo aliamua kwenda kwa Mtume.

Kwa kufuatana na Mtume mahali paitwapo Jaraf na akamtaarifu kuhusu dhihaka ya wanafiki.

Mtume akasema, "Wanafiki ni waongo. Nimekuja hapa baada ya kukufanya wewe kuwa kaimu wangu. Ewe Ali hufurahikii cheo chako cha juu zaidi. Uhusiano wako na mimi ni sawa na uhusiano aliokuwa nao Harun na Musa ila tofauti moja tu ni kwamba hapatakuwepo na Mtume baada yangu. Maana yake ni kwamba Musa alipokwenda kwenye Mlima wa Tur alimteua Harun kuwa kaimu (wakili) wake na yeye (Mtukufu Mtume) alifanya namna hiyo hiyo."

Aliposikia hivi Ali alirudi Madina na Mtume aliendelea na safari ya kwenda Tabuk sehemu iliyokuwa kwenye mpaka wa iliyokuwa Falme ya Roma katika urefu wa vituo kumi kutoka Madina na Dameski. Alipofika Tabuk, alikaa hapo kwa muda wa siku kumi. Wakati wa kuwepo yeye hapo, alimtuma Sariys (jeshi la Uislamu linaloongozwa na mtu mwingine na si Mtume) sehemu zote, na alisisitiza kuwaita watu waingie kwenye Uislamu. Hakuna jeshi lililofika hapo kutoka Roma kwa madhumuni ya vita. Kwa hiyo, alilazimika kurudi Madina.

Wakati wa safari hiyo, siku moja usiku wanafiki walitaka kumuua wakati anapita kwenye bonde la Aqaba Zi Fata, kwa kumuogofya ngamia wake, ambaye angeweza kumwangusha chini, lakini Hudhayfah bin Yaman na Ammar bin Yasir walimwokoa. Baada ya Mtukufu Mtume kuvuka bonde, alimwambia Huzayfah bin Yaman majina ya wanafiki waliotaka kumuua kwenye giza, na akamuamuru kuwa majina hayo iwe siri yake. Masahaba maarufu walikuwemo kwenye orodha hiyo.[1] Kwa mujibu wa Tahzibut Tahzib, watu hao walijaribu kupata majina hayo kutoka kwa Hudhayfah lakini hakufichua.

Hatimaye mmoja wapo wa masahaba hao alikiri mwenyewe, "Uniambie ama usiniambie, kwa jina la Mwenyezi Mungu, mimi nilikuwa miongoni mwa wanafiki hao!" Kwa ufupi, Mtume alirudi Madina wakati wa mwezi wa Ramadhani.

Wakati wa kuondoka kutoka Madina kwa madhumuni ya Vita ya Tabuk, Abu Dharr alikuwa naye. Lakini kwa kuwa ngamia wake alikuwa dhaifu na kukonda, hakuweza kuwa katika msafara. Abu Dharr, hata hivyo, alibaki nyuma ya msafara kwa umbali wa muda wa safari ya siku tatu.

Alijitahidi sana kuwa karibu na Mtume lakini alishindwa. Alihuzunika sana alipotambua kwamba haingewezekana yeye kuwa ndani ya msafara.

Kwa mujibu wa maelezo mengine, alipobaki nyuma, watu fulani walimwambia Mtume kwamba ilikuwa vigumu sana Abu Dharr kuwa naye. Aliposikia hivi, Mtume akasema, "Mwacheni huyo hivyo alivyo. Atafika Inshallah. Kwa hiyo msafara uliendelea na Abu Dharr alizidi kubaki nyuma akiwa amefadhaika na wasi wasi.

4

MAISHA YA ABU DHARR

Wakati mwingine alifikiria kurudi Madina na halafu tena alishawishika kuendelea na safari hadi Tabuk kwa jinsi yoyote ile kwa sababu kuwa nyuma ya Mtume ni hali ambayo ilimtesa sana.

Aliendesha ngamia wake kwa msisimko mkubwa lakini hakuweza kwenda haraka kwa sababu ya udhaifu wake.

Alipogundua hivi, aliteremka kutoka kwenye ngamia na akachukua mzigo wake wote na kubeba mgongoni mwake na akaendelea na safari kwa mguu. Ulikua msimu wa joto kali. Kwa hiyo, ni jambo linalojulikana kwa wasafiri kiasi cha ukali wa kiu ambayo ingempata.

Alikuwa anatembea na mzigo mgongoni mwake wakati ambapo kiu ilikaribia kumwelemea. Tayari alikwisha choka na wakati huo kiu ilifanya hali yake kua mbaya zaidi. Abu Dharr akiwa na kiu kali, alitafuta maji huku na kule akaona maji ya mvua yaliyokuwa kwenye dimbwi. Akafika kwenye dimbwi la maji ambapo alikuwa na kiu sana, na alitaka kunywa maji yaliyojaa kwenye kiganja chake, ambapo ghafla, aliwaza kwamba maji hayo yalikuwa baridi sana na haikuwa vema yeye kunywa maji hayo kabla ya Mtukufu Mtume. kwa hiyo, baada ya fikra hii kuingia akilini mwake akayamwaga maji hayo na akajaza maji hayo kwenye gudulia.

Abu Dharr alikuwa peke yake huku akiwa na kiu kali sana na gudulia lililojaa maji hadi akafika kwenye mipaka ya Tabuk.

Mara tu alipofika kwenye mipaka ya Tabuk, Waislamu walimuona na wakamtaarifu Mtume kuhusu kuwasili kwa msafiri aliyedhikika. Mara moja alisema, huyu ni sahaba wangu, Abu Dharr. Kimbieni, enyi masahaba wangu, na mleteni kwangu. Waliposikia hivyo, masahaba walikwenda haraka kwa Abu Dharr na wakamfikisha kwa Mtume.

Baada ya Mtume kuuliza kuhusu afya yake, akasema, "Ewe Abu Dharr, unayo maji. Kwa nini basi unakiu kali namna hii?"

Abu Dharr; "Bwana wangu, kama unavyoona, maji yapo, lakini siwezi kunywa."

Mtume; "Kwa sababu gani?"

Abu Dharr; "Bwana wangu! Nilipokuwa njiani. Kuja hapa niliona maji karibu na kilima, lakini dhamiri yangu haikuniruhusu kunywa maji haya kwa ajili yako. Mimi nitayaonja baada ya wewe kunywa."

Aliposikia hivi Mtume alisema; "Ewe Abu Dharr! Mwenyezi Mungu Atakuhurumia. Utaishi peke yako na utaondoka hapa duniani peke yako. Utafufuka peke yako mnamo Siku ya Hukumu. Utaingia Peponi peke yako na kundi la watu wa Iraq watapata furaha kamili kwa sababu yako, ni kwamba watakuosha watakuvika sanda na kusalia maiti yako."

Tukio hili si tu linaonyesha mapenzi makubwa ya Abu Dharr kwa Mtume lakini kupitia kwenye tukio hili Mtukufu Mtume kwa wazi kabisa alitabiri matatizo na majanga ambayo yangemfika Abu Dharr katika maisha yake. Ni dhahiri kutoka katika maneno ya mwanachuo wa madhehebu ya Shia yangemtokea Abu Dharr. Amenukuu tukio kutoka kwa Bin Babway kutoka kwa Abbas kwamba siku moja Mtume(s.a.w.w) alikuwa ameketi ndani ya msikiti wa Quba na masahaba wake wengi walikuwa wamemzunguka.

Alisema, "Mtu ambaye atakuwa wa kwanza kuingia kwenye lango la Msikiti huu, atakuwa ametoka kwenye kundi la watu wa Peponi." Baada ya muda mfupi Abu Dharr aliingia kupitia kwenye lango hilo. Alikuwa wa kwanza ambaye alitoka nje akiwa peke yake. Mtukufu Mtume akasema hapo hapo, "Ewe Abu Dharr! Wewe unatoka kwenye watu wa Peponi." Aliendelea kusema, wewe utafukuzwa Makkah kwa sababu ya kuwapenda watu wa Nyumba yangu. Utaishi ugenini na utakufa katika hali ya upweke. Kundi la watu wa Iraq wataneemeka kwa kushughulikia maziko yako na utakuwa pamoja na mimi Peponi."

SURA YA TANO

Historia inashuhudia kwamba Abu Dharr alielimika sana baada ya kuwa Muislam hivyo kwamba hapakuwepo wa kumlinganisha naye miongoni mwa masahaba. Alipata utakaso ulio bora wa imani na unyofu wa moyo hivyo kwamba alihakikisha kwamba yeye ni nguzo ya nuru kwa watu wenye utambuzi. Alizirutubisha akili za watu kwa ushauri, baada ya kuja kwa Uislamu, aliwafundisha watu masomo ya usawa na upendo na aliwafundisha jinsi ya kumtii Mwenyezi Mungu na Mtukufu Mtume.

Maisha yake ya Kiislamu yaliheshimika sana hivyo kwamba hapakuwepo na mtu wa kulingana naye miongoni mwa waumini. Abdulah Subaiti ameandika kwamba Abu Dharr alijipatia sifa sana miongoni mwa masahaba hao ambao walifanya vizuri kuzidi wengine katika uchaji Mungu, kujihini, kumuabudu Mwenyezi Mungu, ukweli,

uimara wa imani na hakuna wa kumfananisha katika kujisalimisha kwa Radhi ya Mwenyezi Mungu. Wakati wa uhai wa Mtume(s.a.w.w) chakula chake cha kila siku kilikuwa kilo tatu za tende na aliendelea hivyo hadi mwisho wa maisha yake.

Anaendelea kuandika Abdullah Subaiti kwamba Abu Dharr alinyanyuliwa juu sana katika maadili na tabia yake hiyo kwamba Mtukufu Mtume alimjumuisha kwenye kundi la Ahlul-bait (watu wa Nyumba ya Mtume) kama alivyo mjumuisha Salman Farsi. Hafiz Abu Naim anasema kwamba Abu Dharr alikuwa msalihina, mtu mchaji Mungu, na alikuwa na moyo ulioridhika. Alikuwa mtu wa nne katika msululu wa kukubali Uislamu. Aliacha maovu yote hata kabla ya kuanza kutekeleza sharia ya Kiislamu. Hili lilikuwa lengo lake alilolihifadhi, kukataa kuwatii watawala dhalimu. Alikuwa imara katika kuvumilia maumivu na huzuni. Alijipatia sifa ya juu katika kuhifadhi hadithi na nasaha za Mtukufu Mtume.

Abu Naim ameandika kwamba Abu Dharr alitoa huduma kubwa kwa Mtukufu Mtume na alipata ujuzi wa vipengele vya imani na utekelezaji akiwa naye, na alijiepusha na maovu. Sifa yake maalum ilikuwa kuuliza maswali kwa Mtukufu Mtume. Alijifunza kuhifadhi maana na fahamu zilizotolewa na yeye (Mtume) na alikuwa na shauku sana kuhusu jambo hili. Kwa ufupi, kwa kadiri alivyoweza, hakuridhika na kuuliza maswali tu lakini pia alikusanya hazina kubwa ya ujuzi wa Kiislamu kwa ajili ya wafuasi wa Uislamu.

Kitendo kingine maarufu cha maisha yake ni kwamba alifuata nyayo za Mtukufu Mtume alizozitilia maanani na kuzithibitisha, na ambazo aliziamuru zifuatwe.

Akaambatana na Imamu Ali baada ya Mtukufu Mtume na hakumkana hata kidogo. Alimfuata na alipata manufaa kutokana na ujuzi mkubwa

wa Imamu Ali. Abu Dharr alihifadhi akilini anasa za mwili, ukarimu, maadili mema na tabia njema za Imamu Ali. Ndio sababu Mtume(s.a.w.w) alisema, "Abu Dharr ni Mtu mkweli zaidi katika taifa hili."

Mahali pengine alisema, "Abu Dharr yu kama Mtume Isa katika ibada ya kujinyima anasa za mwili." Kwa mujibu wa hadithi alisema, "Mtu anayetaka kuona mfano wa maisha na staha ya Isa amwangalie Abu Dharr."

Ni dhahiri kwamba ibada ya dini kama alivyofanya Abu Dharr, haikuwekewa mpaka kwenye Swala peke yake. Alikuwa hodari kiutendaji katika aina zote za ibada. Ni jambo lisilo na upinzani kwamba, kutafakari kuwepo kwa Mwenyezi Mungu na muumbo wake, pia ni ibada kubwa. Abu Dharr alifanikiwa katika ibada hii pia.

Waandishi wa historia na hadithi wanakubaliana kwa pamoja kwamba Abu Dharr alipata kiwango kikubwa cha ujuzi na hii ilikuwa kwa sababu alipata ujuzi kwa moyo ulio nyooka wakati anafuatana na Mtukufu Mtume. Alimuuliza maswali Mtume kila wakati na alijifunza na kuhifadhi majibu yake. Alikuwa na uzoefu mkubwa wa ujuzi wakati anafuatana na Mtume. Mwandishi wa Kitabu Darayatus Rafiah anasema kwamba Abu Dharr alihesabiwa katika safu ya wanachuo wakubwa na washikilia maadili na alikuwa na daraja la pekee la kitaalam. Alikuwa sahaba mwandamizi wa Mtume alikuwa miongoni mwa watu hao waliotimiza agano lao na Mwenyezi Mungu yaani, watu hao walitimiza ahadi ambayo waliahidiana Naye kuhusu wao kuwa wafuasi wa imani iliyokamilika, na alikuwa mmojawapo wa wale watu wanne ambao waumini wote wanawajibika kuwapenda.

Allamah Manazir Ahsan Gilani ametoa maelezo mafupi kuhusu utaalamu wa juu wa Abu Dharr, ameandika, Soma tamko la Ali,

mbora wa majaji miongoni mwa masahaba, na lango la Ujuzi na uhitimishe mwenyewe kwamba anaposema, "Abu Dharr alikuwa na shauku na hamu kubwa ya kupata ujuzi;" anasema jambo lililo sahihi.

Je! Hivi ushahidi huu wa Iman Ali, hauhalalishi madai ya Abu Dharr? Wakati mwingine Abu Dharr mwenyewe alikuwa akisema kwa shauku kubwa, "Tumetenganishwa na Mtukufu Mtume wakati ambapo hakuna hata mmoja wetu ambaye anaweza kujitegemea mwenyewe, kwa sababu bado hatujajua mambo fulani maalum."[2]

Allamah Gilani ameandika kuhusu ujuzi wa Abu Dharr, "Mtu mmoja alimuuliza Imamu Ali, alimfikiriaje Abu Dharr. Akamjibu kwamba wa'aa ilman ajaza fike, yaani 'Yeye, Abu Dharr alihifadhi ujuzi ambao ulimuemea.'

Umesoma na kuona jinsi alivyo kuwa mwepesi kukubali fikira, na wewe mwenyewe unaweza kukisia kutokana na matukio. Ndio maana kila mara alikuwa tayari kutekeleza kwa mujibu wa vile alivyosikia kutoka kwa Mtukufu Mtume. Kama vile alivyo jaribu kusikia kutoka kwa Mtukufu Mtume, kutoka kwa Mtukufu Mtume alitaka kutekeleza kwa vitendo bila kusita hata kidogo. Ilikuwa utashi wa dhati kuona kwamba tendo lake liliendana kwa ukamilifu na ujuzi.

Abu Dharr alinuia sana na alikuwa imara kuhusu kipengele hiki hivyo kwamba hakujali kamwe mamlaka yenye uwezo mkubwa kuliko zote hapa duniani kama ingekuwa kipingamizi chake. Hotuba na ushawishi hazikuweza kumtikisa kutokana na msimamo wake aliokuwa nao.

Akajivunia sifa hii wakati mwingine alisema, "Enyi watu! Mnaona siku ya Hukumu, mimi nitakuwa karibu sana na Mtume(s.a.w.w) na

kundi lake, kwa sababu nimemsikia akisema kwamba atakayekuwa karibu sana naye mnamo siku ya Hukumu atakuwa mtu ambaye ataondoka katika dunia hii katika hali ile ile ambayo alimwacha. Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba sasa hapana yeyote aliye achwa miongoni mwenu ambaye yumo katika hali ile ya wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume isipokuwa mimi na sijanajisiwa na kitu chochote kipya. (Tabaqat bin Sad na Musnad ya Ahmad bin Hanbal).

Hili halikuwa dai la haki peke yake tu, lakini pia kiongozi wa dunia na Mtume wa mwisho alishuhudia hivyo.

Allamah Subaiti amesema kwamba mifano ya uadilifu iliyowekwa na Abu Dharr inastahili pongezi. Msimulizi anasema, "Nilipomuona Abu Dharr amejifunika blanketi na amekaa kwenye kona ya msikiti, nilimuuliza kwa nini alikuwa amekaa peke yake hapo? Alisema kwamba alimsikia Mtukufu Mtume anasema, "Ni vizuri kukaa kwenye kona peke yako kuliko kuketi katikati ya kundi la watu wabaya na ni vema kuketi na watu wenye maadili mema kuliko kuketi peke yako. Kimya ni kizuri kuliko kusema jambo baya na kusema jambo zuri ni vema kuliko kunyamaza kimya."

Abu Dharr alisema kwamba Mtukufu Mtume amemwambia mengi kuhusu maelekezo ya maadili mema. Yapo Saba:

Fanya urafiki na watu masikini na jaribu kuwa nao karibu.

Ili uweze kuboresha hali yako waangalie watu wenye hali ya chini

kuzidi wewe na usijilinganishe na watu wenye hali nzuri kuzidi yako.

Usimwombe mtu yeyote msaada wa mambo ya kidunia na ujenge tabia ya kuridhika.

Wahurumie ndugu zako na wasaidie wanapohitaji msaada. Usisite kusema kweli hata kama dunia itakugeukia wewe.

Usijali shutuma za Kafiri kuhusu Mwenyezi Mungu.

Kila mara sema. "La hawla wa la quwwata illa billah." (Hapana mweza isipokuwa Mwenyezi Mungu). Kwa maneno mengine, 'Mwenyezi Mungu ni Uwezo Usiowezwa.

Abu Dharr anasema, baada ya kusema mambo haya, Mtume alisema huku anashika kifua changu, "Ewe Abu Dharr hakuna busara nzuri zaidi kama kupanga mambo vizuri, hakuna uchaji Mungu ulio bora zaidi kama kujizuia na hapana kitu kizuri zaidi kama maadili mema."

Allamah Gihani alikinukuu Musnad ya Ahmad bin Hanbal anataja madili mawili tu miongoni mwa maadili haya yaliyotajwa hapo juu, ambayo yanaendana na kufanya urafiki na watu maskini na kuwatazama watu wenye hali ya chini kuzidi ya kwako, na halafu ameandika: "Kwa kweli, haya ndio marekebisho mazuri kuliko yote dhidi ya maradhi ya kupenda utajiri na kupenda anasa za dunia. idhaniwe kwamba yupo mtu ambaye analo shati la Muislamu na suruali ndefu kuvaa, mkate wa ngano na nyama ya kondoo kwa ajili ya chakula, na nyumba ya udongo wa mfinyazi iliyo pangwa vizuri na safi kuishi humo. Sasa, endapo mtu huyu anajilinganisha na mtu ambaye hana kitu isipokuwa nguo iliyo duni. Mkate wa shayiri nyumba iliyoezekwa kwa mabua, atamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hali yake nzuri zaidi na hatateseka kisaikolojia, mateso ambayo angeyapata endapo angejilinganisha na mtu tajiri mwenye nguo za gharama zadi na chakula kizuri. Njia hii ndio bora zaidi kupata kujitosheleza kidunia na manufaa mengineyo ya kidunia.

Lakini wangapi miongoni mwetu wanatekeleza hivi leo? Hata ninaweza kwamba mtu hatapata matatizo yoyote endapo anafuata kanuni hii. Hii peke yake ndio kanuni ya muhimu kwa ajili ya dunia hii na kwa ajili ya Peponi, ambayo imeelezewa katika sentenso ifuatayo" ya Sheikh Sa'd, bingwa wa mashairi wa Iran.

"Nilikuwa nalilia jozi ya viatu hadi nilipo muona mtu asiyekuwa na miguu." Baada ya kupenda utajiri sehemu nyingine ya kupenda dunia ni kupenda daraja na uwezo. Hii inayo hatari zaidi na ni sababu ya uovu wa mpangilio wa dunia. Uharibifu unaendelezwa duniani na watumwa wa utajiri ni pungufu zaid kuliko ule unaosababishwa na watu wenye uroho wa cheo na uwezo.

Sababu halisi ya maradhi haya ni kwamba mtu anapohisi ubora wake katika fani fulani, husahau uwezo wa yule ambaye amemboresha, na hujifikiria yeye ni matokeo ya hivi hivi tu. Halafu hajaribu kuwafanya watu wengine, wako karibu naye, watambue umuhimu wake ambao amejipachika mwenyewe. Akiwa na hitimisho la fikra hii, hutayarisha mipango kwa mujibu wa uwezo wa akili yake. Ni mara chache sana kuonekana kwamba mtumwa wa ulafi na uchoyo ashindwe kufanya kila awezalo kwa lengo la kutimiza kusudio lake. Hujaza akili yake unafiki na wakati wote hubakia kuwepo kwake kupitia njia za halali na mbaya sana. Ubora ambao Abu Dharr alipata au alikaribia kupata, ulikuwa ule wa uchaji Mungu. Palikuwepo hofu kwamba hali ile ingemfanya kuwa na majivuno na kupenda makuu, ambayo baadaye tamaa ya hadhi na heshima huvuruga amani ya hapa duniani na Peponi. Kwa hiyo Mtume alizuia hiyo mapema na akamwambia Abu Dharr, siku moja kwa maneno ya wazi.

Mwenyezi Mungu alisema: "Enyi waja wangu! Wote nyinyi mnazo dhambi isipokuwa hao ambao nimewapa kinga. Kwa hiyo wote lazima msali mkiomba msamaha kwa utaratibu unaokubalika. Nitawasameheni.

Nitasamehe dhambi za mtu anayeniona Mimi kuwa ninao uwezo wa kutosha kumkomboa kutoka kwenye dhambi zake na kwamba ninawaokoa, na kwa mtu aliyeomba msamaha wa dhambi zake kupitia kwenye uwezo Wangu.

Enyi waja wangu! Nyote nyinyi ni wapotovu isipokuwa hao Ninawaonyesha njia iliyonyooka. kwa hiyo lazima mniombe Mimi ili niwaongoze. Wote nyinyi ni masikini na wahitaji isipokuwa wale Ninao wafanya matajiri.

Niombeni Mimi kwa ajili ya riziki yenu na kumbukeni kwamba endapo nyinyi wote walio hai na wafu, wazee na vijana, waovu na waadilifu, muungwana na kujizuia msiombe chochote kutoka kwangu hapataongezeka chochote kwenye milki Yangu. Na endapo wote nyinyi wafu na walio hai, wazee na vijana, waovu na waadilifu mnakusanyika pamoja na kuniomba Mimi niwatimizie mahitaji yenu na kuwatosheleza mahitaji yenu, hapatatokea upinzani wowote kwenye himaya yangu usiolingana hata na wingi wa maji yaliyochukuliwa na ncha ya sindano mtu anapoitumbukiza baharini. Hii ni kwa sababu Mimi ni Mkarimu, msamehevu, Mkuu, Anayetukuzwa na Aliyeko kila mahali.

Mtu yeyote anaweza kujivunia kuwepo kwake au mafanikio yake na utulivu wake baada ya kuamini ukweli wa Utulivu wa Mungu na Ufahari ambao unauona katika hali hii? Hivi mtu yeyote anaweza kuwa na kiburi hata kwa sekunde moja baada ya hapa? Mtu yeyote anayemwamini Mwenyezi Mungu anaweza kuchochea uhaini hapa duniani kwa ajili ya kituo chake cha maisha, heshima, kujionyesha na hudumu baada ya hao? Nani mwenye wazimu anayeweza kujivunia uchaji Mungu wake ambapo kila mmoja wetu ana dhambi?

Pale ambapo utajiri wa watu matajiri upo kwenye udhabiti na mamlaka ya Mwenyezi Mungu; yeyoye huyo anayeonyesha pesa si mpumbavu huyu? Endapo ni sahihi kwamba makubwa na madogo yetu hayawezi hata kwa kuungana kuongeza hata nukta moja upana wa himaya ya Mungu, mtu ambaye ni vumbi la kujaa kiganja tu atajivunia nini? Inapokuwa hii ni hali ya uhuru wake kutokana na utashi hata katika mambo ya mwongozo na ukomavu wa akili anafikiria upendeleo na uwezo a Mwenyezi Mungu kuwa ndio wakala halisi, ni katika misingi gani mhudumu wa dini au mrekebishaji atafikia juhudi zake zitastahili kuthaminiwa?

Ambapo kila kitu ni mali yake na sisi ni masikini na wahitaji, kwa nini basi kiburi hiki na kwa nini ufidhuli huu na majigambo haya?

Hizi zilikuwa amri na hotuba ambazo ziliiingiza maadili ya Mtume Isa kwenye moyo wa Abu Dharr. Hata hivyo, hali ilikuwa hiyo na hata zaidi ya Mtume alivyokuwa na desturi ya kuchokonoa tabia ya kujinyima ya Abu Dharr.

Lakini tunatakiwa kutazamna kwa makini zaidi wa upande huo wa mafundisho yake na nasaha ambamo humo ndimo Uislamu umesimama na kutofautiana na dini zingine zote.

Lazima utajihisi unataka kujaribu kufikiria kwamba kama haya yalikuwa mafundisho ya Mtukufu Mtume, kwa nini Uislamu ulipinga maisha ya utawa na kuyafikiria kuwa ni bidaa zilizoendakezwa na watawa na wahudumu wa kanisa? Nitajaribu kuelekeza usikivu wako kwenye jibu la swali hili. kwa ujumla kujizuia na uchaji mungu maana yake ni kuondoka mijini na kwenda milimani na misituni kuabudu Mwenyezi Mungu katika hali ya upweke. Abu Dharr anaeleza ifuatavyo:

Mtukufu Mtume alimwabia kwamba pia ni jambo zuri kuondoa mawe njiani, kuwasaidia wasiojiweza pia ni hisani na hata lendo la ndoa na mkeo ni kitendo cha fadhila. (Musnad Ahmad bin Hanbal)

Nilimuuliza Mtukufu Mtume kwa mshangao, pia ni sadaka kufanya tendo la ndoa na mke wa mtu, ingawa anatosheleza tamaa yake kwa tendo hili? Endapo mwanamume anatosheleza tamaa yake, pia atapata fidia kwa tendo hilo? Mtume alisema, "Vema, niambie, haitakuwa dhambi endapo ungetosheleza tamaa kwa kufanya kitendo kisicho halali na kilicho haramishwa?" Nilijibu, "Bila shaka."

Akasema, "Nyinyi watu mnafikiria kuhusu dhambi lakini si matendo mema. Kwa kawaida watu wanaoishi maisha ya kushikilia maadili kuacha kufanya kazi ili wajipatie riziki na baadaye pale ambapo mahitaji ya kidunia yanapowabana sana wanaanza kuomba."

"Siku moja Mtume(s.a.w.w) aliniita na akasema, "Unaweza kutoa kiapo cha uaminifu kwamba baada ya hapo patakuwepo Pepo tu inakungojea wewe." Nikajibu, "Ndio" Halafu nikanyosha mkono wangu. Mtukufu Mtume akasema, Ninataka useme kwamba hutaomba kitu chochote kutoka kwa mtu yeyote?" Nikajibu "Sawa" akasema, "hata ule mjeledi unaoanguka kutoka kwenye farasi wako. unatakiwa uteremke chini na kuchukua wewe mwenyewe."

Abu Dharr anasema kwamba Mtukufu Mtume alimwambia, "Usifikirie wema wowote na upendeleo kuwa ni kitu kisichokuwa na thamani na kidogo. Endapo hunacho kitu cha kumpa ndugu yako Muisilamu, angalau ni muhimu ukutane naye huku unatabasamau."

Abu Dharr anasema, "Mpendwa wangu (yaani Mtume) ameniusia kwamba niendelee kuonyesha wema kwa ndugu zangu, hata kama siwezi kutimiza kikamilifu, (Musnad Ahmad bin Hanbal) kwa sababu

ni vigumu sana. Hata hivyo mtu anatakiwa kuwafanyia wema watu wote kadiri iwezekanavyo."

Tabia ya Abu Dharr inadhihiri ambapo tunaona kwamba kila mara yupo na watu fukara na wenye kuhitaji. Alikuwa makini sana kuhusu mafundisho ya Mtume na hakuna miongoni mwa masahaba wenye mioyo migumu ambao hawakuathiriwa na maadili ya Mtume. Alikuwa muungaji mkono madhubuti wa Imamu Ali hivyo kwamba alichota tabia ya kiwango cha juu cha desturi njema za Mtume.

Agizo la Mtume lilikuwa: "Wape watumwa wako na watumishi wako chakula unachokula wewe, na wape nguo unazovaa wewe." (Musnad ya Ahmad bin Hanbal) Na Abu Dharr alifuata utaratibu huo huo. Kila siku aliwapa watumwa wake na watumwa wasichana chakula alichokula yeye na aliwapa nguo alizovaa yeye.

9

HADITH ZA MTUME (s.a.w.w) NA MA-IMAMU (a.s)

KUSEMA UONGO

498. Anas Ibn Maliki Khisal-i-Sadduq, Uk. 321: Anaelezea kutoka Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema: "Chukueni mambo sita kutoka kwangu, na mimi nakubalia, na kutoa dhamana (Ya wewe kuingizwa Jannat)

1. Usiseme uongo

2.Unapo toa ahadi, usivunje

3. Unapo pewa amana na wengine, basi uwemuaminifu

4. Tazama chini ( usitende dhambi ).

5. Chunga heshima yako

6. Idhibiti mikono yako na ulimi wako.

499. Amesema Imam Al Hassan al-'Askari(a.s) : "Iwapo maovu yote yatawekwa katika nyunba moja, basi ufunguo ( wa milango yake ) itakuwa ni uongo ."[213] .

500. Amesema Al Imam Zaynul 'Abediin(a.s) : "Jiepusheni na kusema uongo hata kama ni uongo mgogo au mkubwa, kama kwa wadilifu au unasema kwa kdhihaki, kwasababu mtu anapo sema uongo mdogo basi anaweza kudiriki kusema uongo mkubwa pia.[214] .

501. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : Wakati mmoja Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . aliulizwa kuhusu umbali baina ya ukweli na uongo naye akiwa akionyesha umbali huo baina ya macho yake na maskio yake kwa vidole vinne katika kutoa jibu hilo, "Kile majo yako yanayooonani ukweli na mengi na yale yanayo sikilizwa na maskio yako ni sehemu kubwa ni uongo."[215] .

502. Amesema Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) : "Kwa hakika Allah swt ameyawekea maufuli maovu fulani, na ufunguo wake Allah swt ameweka katika pombe, lakinimaovu yatokanayo na kusema uongo ni zaidi hata kuliko pombe yenyewe ."[216]

503. Amesema Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) : "Muwe wasema ukweli na mujiepushe na usemaji uongo ."[217]

504. Amesema Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) : "Kwa hakika Allah swt ameya wekea maufuli maovu fulani, na ufunguo wake Allah swt ameweka katika pombe, lakinimaovu yatokanayo na kusema uongo ni zaidi hata kuliko pombe yenyewe ."[218] .

505. Amesema Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) : "Muwe wa sema ukweli na mujiepushe na usemaji uongo ."[219] .

MARAFIKI NA URAFIKI

506. Mtume Muhammad(s.a.w.w) Amesema: "Mtu anaathirika kwa imani ya marafiki zake. Kwa hivyo, muwe waangalifu kabisa katika urafiki wenu pamoja nao . " [220]

507. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) , Amesema: "Uwe rafiki wa yule ambaye atakuwa ndio heshima yako, si wewe uwe heshima yake. (Ufanye urafiki na wale walio juu yako ili wewe uweze kupata maendeleo kutokana na urafiki huo).[221] .

508. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . Amesema: "Ndugu yangu mpenzi ni yule (anayenitambulisha) makosa na kasoro zangu.[222]

509. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . Amesema: "Kwa hakika kuna marafiki wa aina tatu kwa ajili ya Muislam:

1. Rafiki anayesema mimi niko pamoja nawe iwapo upo hai au umekufa: Na hili ndio matendo yake.

2. Rafiki anayesema mimi nipo rafiki wako hadi ukingoni mwa kaburi na nitakuacha:hawa ni watoto wake.

3. Rafiki anayesema mimi nitakuwa nawe hadi pale utakapo kufa:hii ni mali ambayo ataiacha humu duniani kwa warithi wake baada ya kifo chake.[223]

Tanbih Kutokana na riwaya hii, na kama hizi sisi tunaelewa kuwa kitu ambacho kitakuwa pamoja na huyo mtu aliye kufa na kuaga dunia hii katika siku ya Qiyamah imani na matendo yake mema. Na suala hili limezungumziwa katika ahadithi nyingi sana za Kiislam na vile vile katika ayah za Qur'an tukufu, kwa mfano:

510. Allah swt anatuambia: Wale walio amini na wakatenda mema watakuwa na raha na marejeo mazuri. (Qur'an, 13:29).

511. Allah swt anatuambia: Hakika wale walio amini na wakatenda mema - hakika Sisi hatupotezi ujira wa anaye tenda mema. (Qur'an,18: 30).

512. Allah swt anatuambi: Hakika wale walio amini na wakatenda mema mashukio yao yatakuwa kwenye Pepo za Firdausi. (Qur'an, 18: 107).

513. Allah swt anatuambia:" Hakika walio amini na wakatenda mema Arrahmani Mwingi wa Rehema atawajaalia mapenzi. (Qur'an,19: 96).

514. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Muwe waangalifu katika kutafuta marafiki wa kweli na mujaribu kuwafanyia majaribio, kwa sababu wao watakuwa ndio msaada wenu pale mnapokuwa katika hali nzuri na watetezi wenu pale mtapokuwa katika shida na matatizo."[224]

515. Amesema Al Imam Zaynul 'Abediin(a.s) : "Kukutana pamoja na wacha Mungut kunawaleteeni mema ."[225]

516. Al Imam Zaynul 'Abediin(a.s) . Amesema: "Jitahadharisheni na urafiki wa watendao madhambi, na kuwasaidia madhalimu ."[226]

MARAFIKI WASIO WEMA

517. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Anayetafuta uhusiano na marafiki wa wale wanao wadhalilisha wapenzi wa Allah swt basi watambue kuwa wao wamemuasi Allah swt ."[227]

518. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . Amesema: "Mnapojulishwa kuhusu marafiki zenu wanapotenda maovu, nendeni mumwambie: Ewe fulani bin fulani ! Ama acha kutenda madhambi au ukae mbali nasi: Na hapo utengane naye hadi atakapo acha kutenda maovu.[228]

519. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amenakili kutoka baba yake Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) . ambaye Amesema kuwa baba yake Al Imam Hussein ibn Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . Amesema: "Ewe mwanangu! Jichunge na makundi matano na kamwe usifanye urafiki nao, wala usiongee nao na wala usifanye urafiki pamoja nao. Kwa hayo Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) . alimuuliza baba yake Je ni makundi gani hayo matano. Imam(a.s) . alimujibu: Jitahadharishe na wala usifanye urafiki pamoja na yule msema uongo kwa sababu yeye ni kama mazua mazua anaye kufanyia vitu vya mbali vikawa karibu, na anakifanya kiwe mbali kile ambacho kiko karibu nawe.[229]

Jihadhari na usifanye uhusiano pamoja na mtu ambaye hana tabia njema, kwa sababu atakuuza kwa thamani kwa tonge moja au hata chini ya hiyo. Jihadhari na wala usifanye uhusiano na bahili kwa sababu yeye atakunyima kutoka mali yake pale wewe utakapo hitaji hasa. Jihadhari na usifanye urafiki pamoja na mpumbavu, kwa sababu yeye atataka kukufaidisha wewe lakini kwa uhakika anakudhuru zaidi. Jihadhari na usifanye uhusiano pamoja na yule ambaye hawajali ndugu na maJama'a zake, kwa sababu mimi nimemona mtu kama huyo akilaaniwa katika kitabu cha Allah swt (yaani Qur'an Tukufu) katika sehemu tatu.

Nayo ni: Sura Al Baqarah, 2, Ayah ya 27; Wanao vunja ahadi ya Allah swt baada ya kwisha ifunga, na wakayakata aliyo amrisha Allah swt kuungwa, na wakafanya uharibifu katika nchi; hao ndio wenye Khasara. Sura Al-Raa'd, 13, ayah ya 25 Na wale wano vunja ahadi ya Allah swt baada ya kuzifunga, na wanakata aliy amrisha Allah swt yaungwe, na wanafanya fisadi katika nchi: Hao ndio watakao pata laana, na watapata Nyumba mbaya. Sura Muh'ammad, 47, ayah 22 Basi yanayo tarajiwa kwenu mkitawala ndio mfisidi katika nchi na mwatupe Jama'a zenu ?

520. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Ewe Kumail ! sema kile kilichopo katika hali yoyote ile. Uwe marafiki pamoja na wacha Allah swt na jiepushe na watendao maovu, jiweke mbali na wanafiki na usiwe pamoja na wadanganyifu na wahalifu na wahaini ."[230]

KUWAHUDUMIA WATU

521. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) : "Yeyote yule atakaye mpuuzia ndugu yake Muislam mwenzake matatizo na shida za dunia hizi, basi Allah swt atampunguzia shida na matatizo yake huko Akhera ." [231]

522. Amesema Al Imam Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Kwa hakika, maombi ya shida za watu zinazokuijia wewe ni miongoni mwa neema na baraka za Allah swt juu yako. Hivyo usisikitike kwa sababu ya neema na baraka hizi ."[232]

523. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Popote pale utakapoona ndugu yako Muislam ana shida, jaribu kuangalia kama utaweza kumusaidia. (Usimpuuze mpaka akutamkie shida zake.) "[233]

524. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . kuwa amenakili kutoka mababu zake(a.s) . ambao wamemnakili Mtume Muhammad(s.a.w.w) akisema: "Yeyote yule anayemlisha muumin aliye na njaa akashiba basi Allah swt atamlisha mpaka ashibe kutoka matunda ya Jannah; Na yeyote yule atakaye mvisha nguo yule aliye na shida za nguo, Allah swt atamvisha nguo zilizofumwa na za hariri, na yeyote yule atakaye mumalizia kiu muumin basi Allah swt atamjaalia kinywaji kilichopigwa lakiri; Na yeyote atakaye msaidia muumin kupunguza shida yake, basi Allah swt atamweka chini ya Arshi yake siku ya Qiyama siku ambayo hakutakuwa na kivuli chochote isipokuwa kivuli cha Arshi yake."[234]

525. Mtume Muhammad(s.a.w.w) Amesema: "Watu wanamtegemea Allah swt kwa ajili ya riziki, kwa hiyo mpenzi miongoni mwa watu kwake Allah swt ni yule ambaye anawasaidia wale watu wanaomtegemea Allah swt na kuwafanya watu wa familia ya nyumbani wakawa na furaha."[235] .

526. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) : "Yeyote yule atakaye wasaidia Waislam ndugu zake wakati wa shida, Allah swt atamwondolea shida na matatizo sabini na tatu, moja ambayo ni ambayo iko humu duniani na sabini na mbili zingine zitakazo kuwa wakati wa shida kubwa, ambapo watu watakuwa mashughuli katika mambo yao ya binafsi (katika Akhera) ." [236]

KUTOA MIKOPO

527. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) : "Yeyote yule anayeijiwa na ndugu yake Muislam kwa ajili ya kukopa na kama yeye hampi mkopo, basi Allah swt atamharamishia kuingia Jannat siku ambayo waja mema watakuwa wakilipwa na kufidiwa ." [237]

528. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) : "Yeyote yule anayetakiwa na ndugu yake Muislam kwa kukopeshwa na kama yeye hamkopeshi mkopo, Allah swt atamzuia kuingia Jannat siku ambayo waja wema watakuwa wakilipwa mema yao ." [238]

KUWASAIDIA WENYE SHIDA

529. Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) : "Waulizeni maswali walio elimika, muongee pamoja na wale wenye hekima, na mujihusishe pamoja na masikini."[239]

530. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Sababu mojawapo ya kuteketea na kupotea kwa mali na utajiri wa mtu ni kule kutowajali na kutowasaidia wale wenye shida."[240]

531. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Mtume Muhammad (s.a.w.w) amemnakili Allah swt kwa kuameambiwa usiku wa Mi'raj: Ewe Ahamad! Mapenzi yangu ni kule kuwapenda masikini. Wafanye masikini wawe karibu nawe na uwaweke karibu nawe ili mimi niweze kukufikia wewe .."[241]

532. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Yeyote yule anayemmalizia muumin njaa yake kiasi kwamba akaridhika kikamilifu, basi hakuna binadamu yeyote miongoni mwetu au miongoni mwa Malaika wanaojua kiasi cha thawabu yake siku ya Qiyamah isipokuwa Allah swt mmiliki wa Malimwengu yote. Na aliongezea: Kumlisha Muislam aliye na njaa ni njia moja kubwa sana ya kuomba Tawba( usamehevu)."[242]

Baada ya hapo alisoma ayah ya Qur'an Tukufu Sura Al-Balad, 90, ayah 14 - 16. Au kumlisha siku ya njaa Yatima aliye Jama'a, Au masikini aliye vumbini.

ZAWADI NA KUWAFURAHISHA MUUMIN

533. Mtume Muhammad(s.a.w.w) Amesema: "Wakati sadaka inapotolewa na mtu kutoka mikononi mwake, basi hiyo sadaka inasema: Mimi nilikuwa kitu cha kwisha, lakini wewe umenipa maisha; Mimi nilikuwa sina thamani sasa wewe umenifanya niwe na thamani kubwa; mimi nilikuwa ni adui nawe umenifanya mie kuwa rafiki; Wewe ulikuwa daima ukinilinda na kunihifadhi lakini sasa mimi nitakulinda na kukuhifadhi hadi siku ya Qiyamah ." [243]

534. Amesema Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) : "Yeyote yule atakaye mfurahisha Muumin, basi kwa hakika kwanza kabisa amemfurahisha Allah swt, na pili amemfurahisha Mtume Muhammad (s.a.w.w) na tatu ametufurahisha sisi Ahlul Bayt (a.s) "[244]

535. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Allah swt ameweka mahitaji ya wale wasio na uwezo katika mali ya matajiri. Kwa hivyo atakapokuwa mtu asiye na uwezo akabakia katika hali ya njaa basi ni kwa sababu matajiri wamemnyima haki yake ."[245] .

536. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . Amesema: "Kwa kiapo cha Allah swt! Yeyote yule anayeizuia mali yake isiwasaidie Mumin wenye shida basi siku ya Qiyamah kamwe hawataonja chakula cha Jannat wala Kinywaji kilichopigwa Lakiri."[246]

SADAKA NA MISAADA

537. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Sadaka inalipia madeni na inaongezea katika barakah ."

538. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amenakili riwayah kutoka Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kuwa: "Sadaka inamwepusha mtu na ajali mbaya ."

539. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . anasema kuwa: "Mtu yeyote yule aliye mja wa Allah swt akiwa Mumin akatoa Sadaka, basi Allah swt baada ya kifo chake huyo mtu huwaweka vyema na kuwasaidia wananyumba yake katika hali njema." Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akaendelea kusema: "Faida ya kutoa Sadaka ni kwamba inamsaidia kulipia madeni na viile vile kuongezea katika barak a."

540. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Kusaidia na kutoa sadaka vyote hivyo vinaondoa umasikini na hurefusha umri wa mtu. Na yule anayetoa huweza kuepukana na aina sabini za ajali mbaya .

541. Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) . katika kuelezea tafsiri ya aya, ya Qur'an Tukufu, Sura Al-Layl, 92, Ayah ya 5 na 6: Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali Ama mwenye kutoa na akamcha Mungu. Ndipo amesema kuwa; Allah swt ndivyo anavyo walipa wale watendao mema, kwa mema yao mara kumi, au hata mara laki moja na hata zaidi ya hapo. Na vile vile amesema kuwa: anayetoa katika njia ya Allah swt basi Allah swt humjaalia kila aina ya tawfiqi katika kazi hiyo ya khairi."

542. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amemnakili Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kuwa "Mtu yeyote yule ambaye anamwamimi Allah swt kuwa atamlipa na atamwongezea zaidi ya kile anacho kitoa basi huyo mtu kwa moyo mkunjufu na bila aina ya ubakhili wowote atatoa sadaka na misaada kwa wingi kabisa."

543. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amemnakili Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kuwa: "Siku ya Qiyama ardhi itakuwa imepata moto kupita kiasi na mumin watakuwa katika kivuli na kivuli hicho itakuwa ni kile alicho kuwa akitoa Sadaka ."

544. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amenakili riwayah moja kutoka Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akisema kuwa: "Enyi watu! Toeni sadaka bila shaka sadaka inaongezea katika mali yenu, na hivyo mtoe sadaka na Allah swt atawarehemu ."

545. Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) . amesema kuwa: "Toeni sadaka mjipatie riziki ."

546. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Toeni sadaka mjiongezee riziki yenu. Bila shaka anayeamini kuwa Allah swt hulipa mambo yote. Basi yeye huwapa sadaka masikini kwa kupita kiasi. Allah swt humjaalia riziki kwa njia mbalimbali kwa kile huyu mtu akitoacho katika mali yake ."

547. Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) . amenakili riwayah kutoka Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akisema kuwa: "Kuwa na akida ya Tawhid ni nusu ya sehemu ya dini, enyi watu! Toeni Sadaka ili mpate riziki zaidi ".

548. Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) . ametoa riwayah kutoka Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kuwa: "Kuwa mali halisi ya mtu ni ile ambayo yeye ametolea sadaka ."

549. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema kuwa: "Toeni Sadaka asubuhi na mapema ili balaa zisiwafikieni katika siku nzima ."

550. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amenakili riwayah kutoka Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . kuwa: "Sadaka ni kinga dhidi ya moto wa Jahannam ."

551. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alikuwa akisema: "Enyi watu muwatibu wagonjwa wenu kwa kutoa Sadaka ."

552. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . katika Nahjul Balagha amesema kuwa: "Mnapoona riziki yenu inapungua na kuwa finyo basi muwe mkitoa sadaka ndivyo mtakuwa mkifanya biashara na Allah swt ."

553. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Imani ya muumini inakuwa na sifa nne za lazima, "Awe na tabia njema, "Awe mkarimu na mwepesi wa kutoa "Asizungumze zaidi ya yale yanayo takikana (hazungumzi mambo ovyo ovyo) " Hutumia kile kiasi kinacho takiwa ,siyo mfujaji (anaotoa katika njia ya Allah swt ).

554. Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) . amesema kuwa: "Iwapo mimi nitakwenda Hijja moja basi afadhali niwafanye huru watumwa kumi, lakini iwapo mimi nitajichukulia jukumu la kuwalisha familia ya Waislamu ambao wanashida ya chakula na ambao wanaishi kwa njaa nikawamalizia shida zao, nikawavalisha nguo wale ambao hawana nguo, na nikawarudishia heshima yao miongoni mwa watu, basi mimi ninaona jambo hili ni afadhali na bora zaidi kuliko hata kwenda kuhiji Hijja sabini. "

555. Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) . aliijiwa na mtu mmoja na aliyeuliza, "Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w)! Mimi ninazo pesa na utajiri je ni jambo gani afadhali nitoe sadaka au nimnunue mtumwa na kumfanya huru ?"

556. Kwa hayo Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) . alimjibu kuwa: "Kuwa mimi ninaonelea kuwa kutoa Sadaka ni afadhali zaidi."

557. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Siku moja Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimwuliza Maimuna binti Harun, Je Kijakazi wako amekuwaje? Akasema Maimuna kwa hayo alimjibu Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , 'Ewe Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ! Mimi nimemfanya huru.' Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimwambia "Iwapo kama wewe ungelichukua jukumu la kumlisha, kumtunza, kumsaidia na kumwonea huruma basi ingekuwa afadhali zaidi."

558. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Muwatibu wagonjwa wenu kwa Sadaka, na muzuie maafa kwa kuomba dua na kutoa sadaka muongezee riziki zenu zipanuke, na kwamba Sadaka inawaepusheni na mitego ya mashetani sabini ."

559. Siku moja walikuja wagonjwa wakilalamikia magonjwa yao mbele ya Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) ., naye akawaambia; "Nendeni mtoe Sadaka kwa ajili ya magonjwa yenu na mtapona, iwapo mtu atatoa Sadaka kwa kile akitumiacho kwa siku dharura wake, basi Allah swt huahirisha hata kifo chake na vile vile humwepusha na ajali mbaya ."

560. Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) . aliulizwa na Sahaba mmoja: "Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ! Mimi watoto wangu wawili wamefariki na amebakia mtoto wangu mdogo." Kwa hayo Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) . kamwambia: "Basi toa Sadaka kwa niaba ya mtoto wako huyo." Na siku moja Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) . alipomtembelea huyo mtu akamwambia, "Mwambie mtoto wako huyo atoe Sadaka kwa mkono wake walau kiasi kidogo chochote kile au hata kama kitakuwa ni kipande kidogo tu. Utambue wazi kuwa kiasi chochote kile hata kikiwa kiasi gani kama kitatolewa kwa roho safi basi mbele ya Allah huwa ni kipenzi, kwani Allah swt ameelezea kuwa: Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona! Na anaye tenda chembe ya uovu atauona! (Qur'an,99: 7 – 8).

561. Vile viel Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) . alimwelezea kuwa: "Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu, Surah Al-Balad,90, Ayah11 - 16 Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani. Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani? Kumkomboa mtumwa; Au kumlisha siku ya njaa Yatima aliye jamaa, Au masikini aliye vumbini

"Hivyo ewe Sahabi uelewe kuwa Allah swt anaelewa wazi wazi kuwa si watu wote wenye uwezo wa kuwanunua na wenye kufanya huru watumwa hivyo yeye ameweka thawabu hizo hizo kwa wale watakao toa Sadaka au watakao walisha yatima na masikini."

562. Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) . alijiwa mtu mmoja mbele yake na kuelezea habari za mtoto wake, na kwa hayo Al Imam akamjibu: "Toa Sadaka kwa niaba yake." Na mtu huyo akajibu kuwa "Sasa mtoto wake amekuwa na umri yaani amekuwa kijana." Basi Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) . alimwambia kuwa "Mtoto wako atoe Sadaka kwa mkono wake, hata kama itakuwa ni kipande cha mkate, na hapo ndipo Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) . alisema riwayah ya Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) . kuwa: "Katika Israil alikuwa mtu mmoja aliyekuwa akimpenda mno mtoto wake, na akaona katika ndoto yake anaanmbiwa kuwa, mtoto wako huyo umpendaye mno atakufa usiku wa ndoa yake. Kulipowadia usiku wa arusi baba mzazi wa mtoto huyo, usiku kucha akawa katika wasiwasi na hakupata usingizi na kamwe hakupata raha usiku huo. Na kulipo pambazuka asubuhi na mtoto alipotoka chumbani mwake akiwa hai basi baba yeke alimwuliza 'Ewe mwanangu! Je katika usiku huu wako wa kuamukia leo umefanya mema yoyote?' Kwa hayo mtoto akajibu "Ewe baba yangu! hakuna jambo la maana sana lililotendeka, bali alitokezea masikini mmoja akaja mlangoni kuomba chakula, alikuwa na njaa na kile chakula walichokuwa wameniwekea, mimi nikampa chakula chote huyo mtu aliyekuja kuomba.' Kwa hayo baba yake akasema "Kwa sababu hii tu ndiyo Allah swt amekuondoshea balaa kubwa iliyokuwa ikupate wewe usiku huo."

563. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . anasema kuwa: "Kwa kutoa Sadaka kwa mkono wako mwenyewe basi unajiepusha na ajali mbaya, unajiepusha na balaa na maafa sabini na mitego ya mashetani sabini na ambamo kila shetani yuko anakwambia 'ewe fulani! Usitoe Sadaka kamwe."

564. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Mgonjwa atoe Sadaka kwa mkono wake mwenyewe na anayempa amwambie amwombee dua ".

565. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) katika hadith zake amesema kuwa: "Mkono uliye juu yaani mtoaji ni afahali kuliko mkono ule ulio chini yake, yaani mpokeaji ."

566. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema kuwa: "Kuna aina tatu ya mikono wa " kwanza ni mkono ule wa Allah swt ambao uko juu kabisa na kwa hakika neema zote ni za Allah swt, " mkono wa pili ni ule mkono wa yule mtu anaye toa, ambaye anatoa katika njia ya Allah swt na " mkono wa tatu ni wa yule anaye pokea ambao mkono uliochini wa yule anayetoa. Kwa hivyo enyi watu chochote kile kinachobakia miongoni mwenu mtoe katika njia ya Allah swt na musikalifishe nafisi zenu".

567. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alikuwa amemfanyia usia Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) ; Ewe Ali! Ninakufanyia usia wa mambo mema machache na uyakumbuke vyema.

Ewe Allah swt umsaidie Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . Baada ya hapo wakati akifanya usia, Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alisema: Ama kuhusiana na sadaka tafadhali usiwe na mnunguniko wowote. Utoe kiasi kwamba mpaka uhisi kwamba wewe umefuja mali yako, lakini utambue wazi kuwa hiyo sio ufujaji bali hiyo umetoa katika njia ya Allah swt."

568. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . anasema kuwa kuna riwayah kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kuwa "Toeni Sadaka, angalau hata kwa sa' ya tende, na kama sa' moja hiyo hamnayo basi mtoe tende kwa kiganja kimoja na hata kama hivyo haitawezekana basi mtoe tende kiasi chochote kile na kama hivyo haitawezekana basi mtoe angalau kokwa moja ya tende, na kama hivyo pia haitawezekana basi yule masikini aliyekuja kuwaomba mumwambie maneno mazuri na matamu na maneno matakatifu katika kumwelezea kuwa hakuna chochote, na hayo pia ni sadaka. Kwa sababu isitokee Siku ya Qiyama kwamba Allah swt atakapo kuuliza hesabu ya neema alizokujaalia akakuambia 'Ewe mja! Mimi nilikupa mambo chungu nzima, sasa hebu angalia nafsini mwako je kwa kutumia neema hizo wewe umejiandalia nini?' Na hapo wewe utaangalia sehemu zote nne za dunia na utajawa na masikitiko, na utakuta hakuna jambo lolote lile litakalo kuokoa dhidi ya adhabu za Allah swt."

569. Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) . amesema kuwa: "Mtoe tende kiasi fulani kwani itawaokoa na moto wa Jahannam , mpanue riziki zenu na mteremshiwe riziki nyingi kwa kutoa Sadaka na kupitia dua mziondoe balaa na shida zenu." Mkumbuke kuwa kwa kutoa Sadaka hamtapungukiwa katika mali yenu. Na miongoni mwa jamaa zenu wanapokuwa na shida muwasaidiapo hiyo siyo Sadaka bali hiyo ni wajibu wenu."

570. Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) . amesema kuwa: "Kulikuwa na mja mmoja aliyekuwa akifanya ibada ya Allah swt kwa umri wake wa miaka themanini. Siku moja alimwona mwanamuke mmoja mzuri aliyekuwa akipendeza naye akawa ameingia katika mtego wake. Yeye alitimiza matamanio yake visivyo halali na mara akatokezea Malakul mauti (malaika anayetoa roho). Ulimi wake ulifunga kuongea na jasho lilianza kumtoka na kutokwa kwa roho na mara hapo alipita masikini akiomba. Basi mtu huyu ambaye alikuwa katika hali ya kukata roho alimwambia yule masikini kwa ishara kuwa mahala fulani kuna mkate hivyo auchukue hivyo aweze kula huyo masikini, na masikini huyo alivyoelekezwa akauchukua mkate akaondoka zake. Kwa hiyo ikatokea kwamba Allah swt aliibatilisha ibada zake za miaka themanini kwa sababu ya kuzini na ikatokea kwamba Allah swt akamsamehe madhambi yake yote kwa sababu ya kutoa Sadaka kwa moyo mkunjufu."

571. Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) . amesema kuwa; " Katika zama za Bani Israil kuliwahi kutokea baa la njaa ambao uliendelea kwa muda wa miaka mingi. Katika wakati huo ikatokezea kwamba bibi kizee mmoja akiwa amekabwa na njaa hali ya juu alikuwa ameketi akiwa na kipande kidogo cha mkate huku akitaka kukila kipande hicho, mara akasikia mlangoni sauti ikisema ya masikini aliyekuwa amekuja kuomba: 'Ewe mja wa Allah swt! Mimi nakufa kwa njaa naomba unisaidie, bibi kizee huyo akajiambia kwa hakika Sadaka ndiyo wakati huu muafaka wa kutoa, na kile alichokuwa akila akakitoa haraka akampa huyo aliyekuwa akiomba.

Bibi kizee huyo alikuwa na mtoto mmoja aliyekuwa amekwenda porini na ghafla kule alishambuliwa na mnyama. Kwa kusikia sauti ya mtoto wake huyo bibi kizee ikimwita, alikimbia kumfukuza mnyama huyo na kwa muujiza wa Allah swt ni kwamba, Allah swt alimtuma Malaika Jibrail(a.s) kwenda kumwokoa mtoto huyo katika mdomo na mabano ya mnyama wa huyo muuwaji, na Malaika Jibraili(a.s) . akamwambia 'Ewe bibi kizee! Je umefurahi sasa? Kwa kile ulichokitoa sadaka basi Allah swt naye amekulipa mema yake."

572. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema kuwa: " Mfanye mema katika hali ya shida na ufakiri, na wema huo ni Sadaka. Toeni Sadaka kama itakuwa ni kiasi gani kwa udogo wake. Mnaweza kutoa kiasi cha tende mkajiokoa na Jahannam. Kwa hakika udogo huo siyo hoja na Allah swt ataulea udogo huo kama kwamba nyie mnavyo walea watoto wadogo wanaonyonya maziwa, na siku ya Qiyama wakati mema yenu hayo (mliyokuwa mkisema ni madogo) yatakapoletwa mbele yenu mtaona kuwa ni sawasawa na ukubwa wa milima mikubwa sana."

573. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . ameseama kuwa Allah swt anasema kuwa : "Hakuna kitu kingine mbali na Sadaka ambacho mtu anaweza kumpatia mtu mwingine kidhahiri, na kwa hakika mimi ndiye wakili wake musitahiki, na mimi ninayepokea kwa mikono Sadaka hiyo halafu hata ikiwa kama ni tende kidogo haidhuru mimi ndiye ninaitunza, kama vile mwanadamu anavyowatunza watoto wake.

Siku ya Qiyama huyo mtoa Sadaka atastaajabishwa mno kwa Sadaka zake ndogo alizokuwa akitoa zimekuwa kubwa kama milima ya Uhud, milima mikubwa sana."

574. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amenakili riwayah kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kuwa: "Toeni Sadaka asubuhi na mapema kwa sababu kunaondoa balaa kwa siku nzima ."

575. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Kwa kutoa Sadaka asubuhi na mapema basi mtoa Sadaka huepukana na kila aina ya matatizo na mabaya yote kwa siku nzima ."

576. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema kuwa: "Toeni Sadaka asubuhi, na kwa mapenzi kabisa, mwenyewe kutoa Sadaka amebahatika. Basi humwomba Allah swt amani kutokana na balaa zote zilizoko ardhini na mbinguni, na kwa hakika Allah swt humjaalia hivyo kwa sababu ya kutoa Sadaka ."

577. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . anaelezea kuwa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w) alimwusia Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . kuwa: "Ewe Al Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s).! Sadaka huondoa balaa ambazo lazima zitatokezea, na kwa kutenda mema pamoja na ndugu na majamaa kunarefusha umri .

Ya Ali! Iwapo jamaa na ndugu ni watu wenye shida, basi kuwapa Sadaka hao haitakuwa ni Sadaka. Ya Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) .!Kusema maneno bila vitendo ni ya bure hayana maana, na Sadaka bila kuwa na nia nayo haiwi Sadaka ."

578. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . anasema kuwa: Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimwuliza mtu mmoja "Je leo umefunga Saumu?" Mtu huyo alijibu "La hapana! Ewe Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) " Tena Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimwuliza: "Je leo umeshawahi kumtembelea aliye mgonjwa?" Naye akajibu: "Hapana! Ewe Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) " Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) aliendelea kumwuliza naye aliendelea kumjibu hapana hakufanya hivyo.

579. Mwishoni Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) aliendelea kumwuliza: "Je umemlisha masikini yeyote?" Naye akajibu: "Hapana Ewe Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) !" Na hapo ndipo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alipomwambia huyo mtu: "Nenda kwa wananyumba wako, nenda ukawatendee na uwe nao kwa mema na uwawie wema, basi hayo ndiyo yatakuwa Sadaka yako kwao."

580. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . ameripoti riwayah kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ambaye ameseama: "kwa baraka za Sadaka Allah swt humwondolea mwenye kutoa Sadaka balaa sabini, ambamo kuna magonjwa, madhara yatokanayo na moto, kuzama maji, kufunikwa na majumba mpaka kufa na atamwepusha ili asiwehuke au asiwe mwehu."

581. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . ameripoti riwayah kutoka Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . kuwa: "Ili kutaka kuepukana na shari za madhalimu basi toeni Sadaka ."

582. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . anaelezea kuwa: Siku moja Myaudi mmoja likuwa akienda kukata miti porini na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimwangalia na kuwaambia Ma-Sahaba wake : "Myahudi huyu leo ataumwa na nyoka na kifo chake kitasababishwa na sumu ya nyoka. Myahudi huyo kama kawaida yake alikata kuni na alijitwisha kichwani mwake na akarud akiwa salama. Na tena Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alipomwona Myahudi huyo akamwambia ateremshe mzigo wa kuni huo na auweke chini. Na Myahudi akafanya hivyo alivyoambiwa, na katika mzigo huo wa kuni wakaona kuna nyoka mweusi mwenye sumu kali sana huku akiuma kuni. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimwuliza Myahudi yule,'Je wewe leo umefanya jambo gani?' Myaudi huyo akasema: Mimi nimekata kuni na kuzifunga tu, lakini wakati nilivyokuwa nikirudi nilibakiwa na vipande viwili vya mkate na kipande kimoja mimi nikala na kipande kimoja nikampa masikini Sadaka. Hapo ndipo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akasema kwa kiapo cha Allah swt ni kwa sababu ya Sadaka ndiko balaa hii imekuondokea, kwa hakika Sadaka humwepusha mtu na ajali mbaya."

583. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . siku moja alikuwa pamoja na Ma-sahaba wake katika Masjid Nabawi, na upande mmoja wa ukuta ukaanguka chini. Kulikuwa na mtu mmoja hapo ambaye aliponea chupu chupu tu, kulianguka kizingiti kizito karibu na muguu wake. Lakini yeye bahati nzuri hakupata udhuru wowote. Hapo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . aliwaambia Ma-sahaba wake, hebu mwulizeni huyu mtu leo amefanya matendo gani? Na wakati alipoulizwa huyo mtu akasema: "Mimi nilipotoka nyumbani mwangu leo nilikuwa na kokwa chache za tende. Na kukatokezea na masikini mmoja akaniomba basi mimi nikampa kama Sadaka Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . akajibu "Basi kwa sababu hiyo tu leo, Allah swt amekuepusha na balaa hii ambayo ingekumaliza."

584. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . siku mmoja alimwambia Sahabi wake Mayassari kuwa: "Ewe Mayassari je wajua kuwa wewe umeisha fikiwa na mauti mara nyingi, lakini Allah swt amekuongezea umri wako zaidi kwa sababu ya wewe kuwa mkarimu na kuwajali jamaa na ndugu zako umewawia wema ndio maanake umri wako umezidi."

585. Al Imam Hasan al-'Askary(a.s) . anasema kuwa: " Wakati mmoja Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akiwa pamoja na wenzake walikuwa safari na wenzake hao walikuwa na mali nyingi sana. Na njiani wakapata habari kuwa wako majambazi wanaowapora matajiri mali zao. Kwa kusikia hayo hao matajiri walianza kutetemeka na wakaingiwa na hofu na wakaanza kumwuuliza Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . je tufanyeje sasa? Na kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akawajibu: 'Mkabidhini mali yenu yule ambaye ataweza kuifadhi mali yenu, na kwa kweli ataitunza sana na baada la kupungua hata itazidi pia, sio hayo tu na pale mutakapokuingiwa na shida ya mali yenu basi yeye kila siku atawarudishia pamoja na nyongeza yake. ' Kwa kusikia hayo hao wenzake aliokuwa nao katika safari wakamwuliza : "Je ni nani huyo?" Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akawajibu: "Yeye ni miliki wa malimwengu zote Allah swt." Basi hao wenzake wakamwuliza je tunaweza kumkabidhi vipi mali zetu hizi? Hapo Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akawaambia: Toeni Sadaka muwape wale wanaostahiki. Kwa kusikia hayo wakauliza ewe mjukuu wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ! Hapa tulipo tutawatoa wapi hawa masikini na mafakiri tutawatafuta wapi? Basi Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . aliwajibu: munuie kuwa sehemu moja ya mali yenu mtatoa Sadaka basi na msiwe na wasiwasi Allah swt atailinda mali yenu yote.

"Wale waliokuwa naye pamoja safarini walinuia hivyo kama vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . alivyowaambi,a na Imam(a.s) . akawaambia sasa nyie mko katika amani ya Allah swt, na wakiwa wanaendelea na safari majambazi hao walikumbana nao na kwa kudura za Allah swt wao wakawapita salama usalimini bila ya kudhurika na kusumbuliwa, hadi wakafika mwisho wa safari yao. Waliopofika tu mwisho wa safari yao wao wakatoa sehemu moja walizokuwa wamenuia kama Sadaka na sehemu iliyo bakia walifanyia biashara yao, na Allah swt akawajaalia baraka kiasi kwamba wakapata faida hata zaidi ya mara kumi."

586. Siku moja Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . alikuwa Mina pamoja na Ma-sahaba wake wakila zabibu. Mara akatokezea mtu mmoja na akaomba. Basi Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . kwa mkono wake akachukua fungu moja la zabibu akampa basi huyo akakataa kupokea, akisema "mimi sitaki zabibu hizi bali ninataka pesa tasilimu kama zipo ndio nichukue". Basi kwa kusikia hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akamwambia "Allah swt atakuzidishia" na Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . hakumpa chochote, baada ya muda si muda huyo mwombaji tena akarudi kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . na akamwambia Imam(a.s) . "Nipe zile zabibu ulizokuwa ukitaka kunipa." Na Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akamwambia Allah swt atakutafutia njia yake, pamoja na hayo Imam(a.s) . hakumpa chochote.

Wakati bado wakiwa wamekaa akatokezea mtu mwingine kuja kuomba, na Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . alitoa mbegu tatu tu za zabibu akampa huyo mwombaji. Mwombaji huyo alianza kumshukuru Allah swt kwa kumjaalia riziki hiyo na akaonyesha shukurani kwa ujumla. Kwa kusikia hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . alichota mikono ya zabibu miwili akampa na hapo tena huyo mwombaji akaendelea kumshukuru Allah swt zaidi na zaidi. Kwa kusikia hayo tena Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . akamwambia mtumwa wake kama tuna pesa zozote zile tulizo nazo kwetu mpe huyo. Na huyo mfanyakazi wa Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . kwa amri yake alimpa Dirham Ishirini alizokuwa nazo. Mwombaji akiwa anachukua Dirham akasema: 'Ewe Allah swt! Nakushukuru mno sana na hakuna mwingine wa kushirkishwa nawe. Kwa kusikia hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . nguo aliyokuwa amejifunika akampa huyo mwombaji na huyo mwombaji baada ya kuivaa na kujifunika na hiyo nguo akamshukuru Allah swt ambaye amemjaalia nguo ya kujifunika. 'Ewe Aba 'Abdillah! Allah swt akulipe kila la heri. Na baada ya kusema hayo akaondoka zake. Kwa kuona haya Ma-sahaba wakamwambia Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . kuwa kila alivyoendelea yeye kumsifu Allah swt ndivyo wewe ulivyoendelea kumpa na kama asinge omba kwa kutaja jina la Al Imam(a.s) . lazima angeendelea kumpa chochote zaidi ya hayo."

5

6

7

8

9

10

11