• Anza
  • Iliyopita
  • 21 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 18902 / Pakua: 2144
Kiwango Kiwango Kiwango
MAISHA YA ABU DHARR

MAISHA YA ABU DHARR

Mwandishi:
Swahili

7

MAISHAYA ABU DHARR

"Sasa sikilizeni! Maisha yenu yamegawanyika katika hatua mbili. Mojawapo ya hatua hizo imepita na nyingine inakuja. Fanyeni amali njema na jiepusheni na kutenda dhambi wakati huu uliopo kwa ajili ya hatua ijayo. Sikilizeni! Kama hamtafuata ushauri huu, bila shaka mtaangamia na mtalaaniwa huko Peponi."

Mtu mmoja akamuuliza, "Vema! Tujulishe kwa nini hatupendi kifo?" akasema, "Kwa sababu mmeangamiza maisha yenu ya baada ya hapa duniani kwa sababu ya kupenda mambo ya kidunia. Mnajua kwamba hamkufanya lolote kwa ajili ya Pepo na mtapata matatizo huko. Kwa hiyo inawezekanaje mtu apende kuondoka kwenda mahali, ambapo anajua kwamba haitakuwa vizuri yeye kufanya hivyo."

Halafu akauliza, "Ni jinsi gani tutafikishwa mbele ya Mwenyezi Mungu?" Abu Dharr akajibu, "Wale waliofanya amali njema watakwenda Kwake kama msafiri ambaye amerudi nyumbani kwake, na wala waovu watafika huko kama mtoro aliyefikishwa hapo baada ya kukamatwa."

Halafu, akauliza tena, "Hali yetu itakuwaje mbele ya Mwenyezi Mungu?" Abu Dharr alijibu, "Unaweza kuamua wewe mwenyewe. Yafanyie hukumu matendo yako kwa kuzingatia Kitabu cha Dini. Mwenyezi Mungu anasema: "Watu waadilifu watakwenda Peponi na waovu watakwenda Jahanamu." Akauliza, "kama ndiyo hivyo, huruma Yake itatusaidiaje?" Abu Dharr alisema; "Mwenyezi Mungu tayari amekwisha sema kwamba, huruma Yake ni kwa ajili ya watu waadilifu."

Mtu mmoja alimwandikia Abu Dharr, "Andika vitu vya ujuzi kwa ajili yangu." Alijibu, "Mambo ya ujuzi ni mengi wala hayana mwisho. Ninaweza kukuandikia hadi wapi kuhusu ujuzi huo? Jambo moja tu la kuzingatia usimfanyie ubaya rafiki yako." Halafu aliandika, "Yupo mtu yeyote ambaye humfanyia ubaya rafiki

yake?" Abu Dharr akaandika, "Ujipende wewe zaidi na usiwe na mtu mwingine yeyote ambaye utampenda kuliko unavyojipenda wewe mwenyewe. Kwa hali yoyote ile, ukimkosea Mwenyezi Mungu kwa kutenda dhambi, hakika utakuwa umejifanyia ubaya wewe mwenyewe."

Pia, mahali pengine amesema, "Enyi watu! Mwenyezi Mungu amekuumbeni kama mwanadamu. Usijiteremshe daraja na kuwa hayawani na kuwa mnyama katili kwa kumkosea Yeye kwa kutenda dhambi."

Allamah Shaykh Mufid ameandika; "Siku moja Abu Dharr alisema katika hotuba: "Utalipwa kufuatana na matendo yako. Utavuna kile ulichokipanda, yaani utapata thawabu kulingana na amali zako.Ukifanya amali njema hapa duniani utapata thawabu nzuri Peponi na endapo unafanya matendo maovu utapata adhabu kulingana na hayo Ulimi wako ni ufunguo wa matendo mema na maovu. Unatakiwa kuuziba moyo wako kama unavyofunga pochi yako. Ni kwamba, kama unavyolinda utajiri wako, unatakiwa kuulinda moyo wako vivyo hivyo na jaribu kufanya kila uwezavyo usiruhusu uovu wowote usiingie humo.

Mawazo yanayojikusanya humo lazima yawe safi." (Amali, Shaykh Mufid)

Allamah Majlis ameandika: "Abu Dharr alikuwa na desturi ya kusema mihadhara yake na hotuba zake. Ewe mtafutaji wa ujuzi! Vitu vyote vya hapa duniani vinavyo hali moja katika hizi mbili. Uzuri wao unakunufaisha wewe au uovu wao unakudhuru wewe. Unatakiwa ukipende kitu chenye matarajio ya kukunufaisha. Ewe mtafutaji wa ujuzi! Upo uwezekano isije familia yako na utajiri wako vikufanye wewe usiwe mwangalifu wa maisha yako, kwa sababu ipo siku ambapo kwa hakika utatenganishwa na familia yako na rasilimali yako

na utakapokaribia kuondoka, utakuwa kama mgeni ambaye ameishi na kundi la watu kwa usiku moja na kuondoka kesho yake asubuhi. Sikiliza! Umbali uliopo baina ya kifo na Ufufuo ni kama kuwa katika hali ya ndoto na kuamka haraka sana."

"Ewe mtafutaji wa ujuzi! Peleka amali zako njema mapema kwa ajili ya siku hiyo ambapo utasimamishwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuhojiwa na kujieleza. Mnamo siku hiyo utapata thawabu za amali zako njema na utalipwa fidia kwa tendo lolote jema ambalo umelifanya hapa duniani."[13]

SURA YA NANE

Masimulizi ya hadithi ni kitu chenye muhimu mkubwa. Wala si kila mtu anaruhusiwa kusimulia, ama kusikiliza simulizi zao. Ujuzi wa wahadithi ndio kipimo chake. Abu Dharr ni mmojawapo wa wasimulizi wa kuaminika, kutegemewa na wakweli ambao simulizi zao hazitiliwi shaka au kukataliwa. Amekuwa na Mtukufu Mtume kwa muda mrefu sana wa uhai wake. Kwa maelezo yake ni mengi sana miongoni mwa hayo, machache yameandikwa hapa.

Kuhusu Aya za Qurani Tukufu! Enyi mliamini! Mtiini Mwenyezi Mungu, Mjumbe wake na "Ulil amr-i minkum," Imamu Fakuddin Razi ametoa maelezo kwenye Tafsirul Kabir kwamba Aya hiyo inawazungumzia wale wasiokosea na Saiyid Ali Hamadani ameitaja katika Mawaddatul Kubra kwamba inawahusu wenye utakaso kumi na wawili.

Lakini inahitaji kuthibitishwa na masahaba wa Mtume wenye kuheshimika kwamba Mtume mwenyewe alisimulia hadithi hiyo. Abu Dharr anasimulia kutoka kwa Mtume kwamba aya iliyotajwa hapo juu ilipo funuliwa, alimwomba Mtukufu Mtume amwambie majina ya Waku wa mambo 'Ulil Amr. Aliwataja maimamu kumi na mbili. Baada ya kuwataja majina, Abu Dharr anatoa maelezo kwa ufupi kwamba mteule wa kwanza ni Ali na wa mwisho ni Imamu Mahdi. (Yanabiul Mawaddah, Shaykh Sulayman Qandozy al-Hanafi na Riuzatul Ahbab).

Abu Ishaq Thalabi ameandika kwenye maelezo yake: "Siku moja Bin Abbas alikuwa anasimulia hadithi za Mtukufu Mtume(s.a.w.w) alipokuwa ameketi karibu na kisima cha Zamzam ambapo mtu mmoja aliyefunika uso wake alikuja hapo. Bin Abbas alinyamaza kwa muda. Mtu huyo alianza kusimulia hadithi ya Mtume Bin Abbas akasema, "Ewe mtu! Nina kuuliza katika jina la Mwenyezi Mungu uniambie kwa kweli wewe ni nani?" Alifunua uso wake na akasema, "Enyi watu! Yule anaye nijua mimi ananijua mimi, lakini yule asiyenijua mimi, anatakiwa anitambue kwamba mimi ni Abu Dharr Ghifari. Nimesikia kutoka kwa Mtukufu Mtume kwa masikio haya mawili ambayo yanaweza kupata maradhi na kuwa kiziwi kama sikukosea, na nimeona kwa macho haya mawili ambayo yanaweza kupofuka endapo mtasema uwongo kwamba Mtume alisema kuhusu Ali kwamba ni kiongozi wa watu waadilifu na muuaji wa watenda maovu. Mtu aliye msaidia yeye alipata ushindi na yule aliye mtelekeza yeye naye alitupwa."

Kufuatana na simulizi ya Abu Dharr Ghifari, Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: "Ali ni lango la ujuzi wangu mwongozo wa wafuasi wangu wa lengo lililosababisha nitumwe. Kumpenda yeye ni imani na kumfanyia uadui yeye ni unafiki na kuwa rafiki yake ni ibada."[14]

Kwa mujibu wa simulizi ya Abu Dharr, Mtume alisema: "Mtu akiniheshimu mimi, anamheshimu Mwenyezi Mungu. Asiye iheshimu mimi, hamheshimu Mwenyezi mungu. Mtu anayemheshimu Ali, ananiheshimu mimi, na yule asiyemheshimu Ali haniheshimu Mimi."[15]

Abu Dharr anasema; "Tulikuwa tunawatambua wanafiki kwa vitu vitatu: Kwanza kwa kumkana Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, mbili kwa kuacha kusali, na tatu kwa chuki yake dhidi ya Ali." (Arjahul Matalib uk. 608 kwa mamlaka ya bin Shazan).

Ipo hadith ambayo imesimuliwa na Abu Dharr, kwamba Mtume alisema, "Ali ni lango la ujuzi wangu. Yeye ni msimulizi wa mambo hayo ambayo yamesababisha niteuliwe. Ku mpenda Ali ni imani na kumchukia ni unafiki, na kumwangalia yeye ni ibada." Bin Abd al-Barr ameandika kwenye Istiab kwamba masahaba wengi wamesimulia hadithi hii ya Mtume: "Ewe Ali! Hapana yeyote atakaye kuwa rafiki yako isipokuwa muumini, na hapana yeyote atakayekuwa adui yako isipokuwa mnafiki."[16]

Abu Dharr amemnukuu Ummu Salamah kwa kusema kwamba alimsikia Mtukufu anasema; "Ali yu mkweli na ukweli umo kwa Ali na Ali na ukweli hawatatengana hadi watakapofika kwenye Haudhi ya Neema.[17]

Allamah Subaiti ameandika: "Abu Dharr amesema kwamba Mtume alimwambia yeye "Mtu anaye kubali imani kwa uaminifu huuweka moyo wake katika hali safi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, husema ukweli, huwa makini, anakuwa na tabia njema, hutumia masikio yake kusikiliza mambo mazuri, na hutumia macho yake kuona vitu vinavyostahili, atapata ukombozi."

Abu Dharr anasema kwamba Mtume amesema: "Wafuasi wangu hawata neemeshwa endapo watafuturu kabla ya muda na kuchelewa kula daku kabla ya alfajiri (muda wa kuanza kufunga wakati wa mwezi wa ramadhani)."Abu Dharr anasema kwamba Mtukufu Mtume anasema: "Furaha yangu ni kwamba dhahabu igawiwe kama sadaka hata kama ingekuwa kubwa kama Mlima Uhud."[18]

Abu Dharr anasema kwamba Mtukufu Mtume amesema: "Ewe Ali! Mwenyezi Mungu ametufanya mimi na wewe kuwa mti mmoja. Mimi ni mizizi ya mti huo na wewe ni tawi lake. Mwenyezi Mungu atamtupa mtu Jahananu kwa kutanguliza uso wake, kama akikata Tawi Lake." Aliendelea kusema, "Ali ni kiongozi wa Waislamu na Imamu wa wacha Mungu. Atawaua watakaovunja ahadi ya utiiifu kwake (watu wa Jamal), walio tengwa na jamii (makhawariji) na wakanushaji."[19]

Abu Dharr anasema kwamba Mtukufu Mtume amesema; "Ali kwangu ni kama Harun alivyokuwa kwa Musa isipokuwa tofauti moja tu kwamba hapatakuwepo na Mtume badala yangu."

Hadithi hii imenukuliwa na masahaba wengine wengi, miongoni mwao wakiwemo Umar bin Khatab, Sa'd bin Abi Waqqas, Abu Hurayrah, Abdullah bin Mas'oud, Abdallah bin Abbas, Jabir bin Abdullah, Abu Said Khidri, Jabir bin Samrah, Malik bin Harith, Bara bin Azib, Zayd bin Arqam, Anas bin Malik, Abu Ayyub Al-Ansari, Aqil bin Abi Talib na kadhalika (Arjahul Matalib).

Allamah Abdul Mu'min Shablanji ameandika kwenye kitabu chake 'Nurul Absar' kwamba, Abu Dharr, ananukuu kutoka kwa Mtume ambaye alisema: "Kitendo kizuri kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni kumpenda yeye na kutofanya chochote kinyume na Ridhaa Yake.."

Abu Dharr anamnukuu Mtukufu Mtume(s.a.w.w) akisema: "Unapokuwa na urafiki na mtu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mfahamishe ."

Abu Dharr anasimulia kwamba Mtukufu Mtume anasema; "Mtu anapokasirika, kama amesImamua, ni vema aketi chini na endapo hasira haipungui, alale chini. "[20]

Abu Dharr ananukuu hadithi ya Mtume kwamba Mwenyezi Mungu humpenda mtu anaye vumilia anapotendewa mabaya na jirani yake. (Nurul Absar, uk. 32).

Abu Dharr anasema kwamba Mtume(s.a.w.w) ameagiza uchaji Mungu na kujinyima na alituomba tulinde dhamana, tusipite tunaomba kwa mtu yeyote, tusivunje uhusiano wa kimapenzi uliopo baina ya watu wawili, kumtendea wema mtu anayekutendea ubaya, na kumuogopa Mwenyezi Mungu kila mara katika jambo la wazi na siri (Nurul Absar, uk. 33).

Abu Dharr anasimulia hadith ya Mtume hivi: "Mwenyezi Mungu alifananisha Ahlul Bait na Safina ya Nuhu (Safinatu Nuh) kwa wafuasi wangu. Yeyote aliyepanda humo, aliokoka na yeyote ambaye hakupanda alikufa maji, yaani kwa usemi mwingine alikengeuka.

Pia Ahlul Bait wangu, wapo kama mlango wa kwendea toba (Hittab) kwa wafuasi wangu. Kuhusu wana wa Uyahudi ambao Mwenyezi Mungu aliwaambia kwamba mtu aliyeingia kupitia mlangoni, ataokoka kutokana na mateso ya dunia na Akhera. Vivyo hivyo,

yeyote yule kutoka miongoni mwa wafuasi wangu akifuata njia ya Ahlul-Bait wangu na anaendelea kuwa imara katika kuwafuata, ataokolewa katika Siku ya Hesabu."

(Ainul Hayat).

Ali bin Shahab Hamadani anamnukuu Abu Dharr ambaye anasema kwamba alimsikia Mtukufu Mtume anasema; "Ewe Abu Dharr! Ali ni yeye ndiye atakayezigawanya Pepo na Jahanamu. Ewe Abu Dharr! Hakuna hata malaika moja aliyeweza kupata heshima ya kugawa Pepo kutoka kwenye Jahamanu. Tazama! Pepo ipo pale kwa ajili ya wanao muunga mkono yeye na amepewa ndugu kama mimi ambapo hakuna ndugu ya mtu yeyote yupo kama mimi."

Abu Dharr anamnuku Mtukufu Mtume akisema; "Mwenyezi Mungu ameimarisha Uislamu kupitia kwa Ali Ali anatokana na mimi na mimi ninatokana na Ali, na Aya hii,

"Basi mtu aliye na dalili wazi itokayo kwa Mola wake Mlezi, inayofuatwa na shahidi anaye toka kwake na kabla yake kilikuwa Kitabu cha Musa kilicho kuwa mwongozi na rehema ......" (11:17).

Imeteremshwa kuhusu yeye (Ali) mimi ninao uthibitisho katika Aya hii na Ali ni shahidi yangu" (Muwaddatul Qurba, uk. 78)

Kwa mujibu wa Abu Dharr, Mtume alimwambia Ali, "Ewe Ali! Mtu anayenitii mimi, anamtii Mwenyezi Mungu na mtu anayekutii wewe,

ananitii mimi, na mtu asiyenitii mimi hamtii Mwenyezi na mtu asiyekutii wewe, hanitii mimi." (Muwaddatul Qurba uk. 78 na Yanabiul Mawaddah, Shaykh Sulayman Qandozy).

8

MAISHA YA ABU DHARR

Abu Dharr anasema kwamba siku moja alipokuwa kwenye Uwanja wa makaburi wa Baqi' (Madina) na Mtume(s.a.w.w) , ambapo alisema, "Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu ambaye anaoudhibiti wa maisha yangu kwamba yupo mtu miongoni mwenu ambaye atapigana kwa ajili ya fasiri iliyo sahihi ya Quran Tukufu, kwa namna ile ile niliyopigana mimi na wanao abudu miungu wengi wakati wa ufunuo wa Qurani, ingawa watakuwa wanakariri mfumo ya imani (Hapana Mungu ila Mwenyezi Mungu). Ambapo yeye (Ali) atapigana nao watu wataona si sahihi na watamkosoa rafiki ya Mwenyezi Mungu (yaani Ali) na watamkasirikia kwa sababu ya vita hii kama Mtume Musa alivyomkasirikia Khidhr kwa sababu ya kutoboa mashua, kumuua mtoto na kujenga ukuta, ingawa kutoboa mashua, kumuua mtoto na kujenga ukuta ni matukio yaliyotekelezwa kufuatana na amri ya Mwenyezi Mungu."[21]

Muhammad bin Yusuf Kanji Shafii amemnukuu Abu Dharr akisema kwamba Mtume alisema, Bendera ya Ali bin Abi Talib, kiongozi wa waumini, kiongozi mkuu wa wenye nyuso zing'arazo na mrithi wangu itanifikia mimi kwenye Haudhi ya Neema (kifay tut Talib).

Abu Dharr anasema kwamba alimuuliza Mtume, "Ni msikiti gani wa kwanza kujengwa hapa duniani? " Akajibu, "Msikiti wa al-Haram " Akasema, "Na baada ya huo?" Akajibu, "Msikiti wa Bayt al-Maqdis (Yerusalemu)" Halafu aklasema, "Palikuwepo urefu gani wa kipindi?" Mtume alijibu, "Miaka arobaini." (Tajrid Bukhari).

Imamu Bukhari amemnukuu Abu Dharr anasema kwamba Mtukufu Mtume alisema, "Endapo kwa makusudi mtu anajihusisha na mtu mwingine kwamba ni baba yake ambapo sivyo, mtu huyo si muumini, na mtu, ambaye anajionesha kwamba yeye ni mtu wa jamii ambamo hana wazazi. Lazima ajitayarishe kufanya Jahanamu kuwa masikani yake." (Tajrid Bukhari).

SURA YA TISA

Wataalamu wa historia na wahadithi wa madhehebu yote mawili (Shia na Sunni) wanakubaliana kwamba pale ambapo Mtume(s.a.w.w) alitaka kuanza safari yake ya kwenda kwenye hija yake ya mwisho, alitangaza waziwazi kwamba masahaba wote lazima wafuatane naye kwenye safari hiyo. Baada ya tangazo hili, masahaba wa Mtume walianza kufika Madina kutoka sehemu zote. Pia aliwataarifu watu kwamba wale ambao hawangeweza kufika Madina, waende Makkah moja kwa moja ili wahiji pamoja naye.

Mtume aliondoka Madina tarehe 25 ya mwezi wa Zilqadah, mwaka wa 10 Hijiriya (Tarikh bin Alward). Masahaba wengi sana walianza safari naye tangu madina, pamoja na Salman, Miqdad, Abu Dharr na Ammar.

Alipofika Makkah, Mtume alitekeleza ibada zote za Hijja. Ahlul-Bait wake wote, wake zake na masahaba wote walikuwa naye katika Hijja. Alitoa hotuba wakati wa Hijja na akaorodhesha mambo yenye kuendeleza matumaini kwa wafuasi wake na akaeleza njia ambazo umma ungepita ili upate kukombolewa.

Alipomaliza Hijja Mtume aliondoka Makkah kwenda Madina. Kufuatana na masimulizi ya Muhadithi Dehlavi walikuwepo masahaba 124,000 au kwa mujibu wa taarifa ya Khawand Shah 125,000.[22]

Alipofika sehemu iitwayo Ghadir Khum akiwa na masahaba wake, malaika Jibril aliteremsha ujumbe wa Mungu usemao: "Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Na ikiwa hukufanya hayo basi hukufikisha ujumbe wake. Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu ." (5:67).

Baada ya amri hii ya wazi hapakuwepo na chaguo lingine sipokuwa yeye (Mtume) alifikisha ujumbe kwa watu.

Aliagiza mimbari itengenezwe kufuatana na hali halisi kwa kutumia mito ya kukalia kwenye ngamia! Baada ya hapo alimwambia Bilal wa Afrika, "Ewe Bilal! Waite watu na waambie masahaba wangu kwamba wale walioko mbele warudi na wale ambao bado wapo nyuma, wafanye haraka kuja mbele." Bilal aliita, Hayya ala Khairil Amal (Kimbilieni kwenye kitendo kilicho bora). Kundi lilikusanyika kuzunguka mimbari ya Mtume. Alipanda kwenye mimbari na baada ya hotuba ndefu sana alimwita Ali aende aliposimama. Halafu, akiwa ameshika mikono miwili ya Ali kwa mikono yake mwenyewe, alinyanyua mikono hiyo juu sana hivyo kwamba weupe wa kwapa za Ali ulionekana wazi. Halafu akasema; "Yeyote anayefikiria mimi kuwa mtawala na mlezi wake lazima pia amfikirie Ali kuwa mtawala na mlezi wake. Ee Mwenyezi Mungu! Uwe rafiki ya mtu ambaye ni rafiki yake Ali na uwe adui ya mtu ambaye ni adui yake Ali."

Mara watu waliposikia taarifa hii walitamka kwa sauti kubwa kuonesha kumuuunga mkono. Mtukufu Mtume aliondoka kwenye mimbari na akamwamuru Ali kupokea hongera kutoka kwa masahaba kwenye hema la kijani. Ali alipokea pongezi za kumrithi Mtume na

aliwashukuru watu kwa kumpongeza. Imeandikwa kwenye Maarijun Nubuwwah kwamba, licha ya masahaba, wake zake Mtume pia walimpongeza Ali kwa kuwa mtawala na kiongozi wa umma wa Waislamu.

Kwa mujibu wa Tarikh bin Khalqami Mtume katika ho tuba yake ya Ghadir iliweka wazi kuhuzu kuwa na sifa, fahari na kukubalika kwa Ali akasema kwamba Ali alikuwa na uhusiano sawa na yeye kama Harun alivyokuwa na Musa.

Ukifuatana na Mustadrak al-Hakim alisema, "Ninawaachieni vitu viwili vya thamani sana miongoni mwenu, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Ahlul Bait wangu.

Hamtapotoka mkivishikilia vitu hivyo." Maneno kama hayo yameandikwa kwenye Khasais an-Nasai. Kwa mujibu wa Rauzatul Ahbab, Mtukufu Mtume pia alisema, "Ee Mwenyezi Mungu! Mfanye rafiki yako yule anayempenda Ali na uwe adui wa yule ambaye ni adui wa Ali na pia ielekeze kweli upande huo ambako Ali huelekeza uso wake."

Imeandikwa kwenye Asbab al-Nuzul Tafsir Durrul Manthur, kwenye Tafsir Fatahul Bayan kilichoandikwa na Siddiq Hasan, kwamba Aya hii 'Balligh' imeteremshwa kuhusu Ali tu. Imeandikwa kwenye Sharh Bukhari Aini, Tafsir Gharaibul Qurani of Naishapuni, Tarikh bin Wazih, Kanzul Ummal na kadhalika, kwamba Aya ya 'Balligh' imeteremshwa kuhusu hadhi na ubora wa Ali.

Imeandikwa kwenye Tarikh Abul Fida kwamba baada ya kurudi kutoka Ghadir al-Khum, Mtukufu Mtume aliugua mwishoni mwa siku za Safar (Machi), 11, Hijiriya. Kwa mujibu wa Mishkat Sharif, sababu ya ugonjwa ilikuwa sumu ile ile iliyopelekwa huko Khaybar

na ambayo ilionesha athari yake nyakati fulani. Imetaarifiwa kwenye Tarikh bin Alward kwamba aliwaomba masahaba wake wote kwenda na jeshi la Usmah bi Zayd na akasema kwamba alimteua Usamah kuwa ndiye kamanda wa jeshi.

Muhadithi Dehavi ameandika kwenye Madarij kwamba siku iliyofuata Mtukufu Mtume akiwa mahututi, alimkabidhi Usamah bendera ya vita na akamwomba aondoke aende kupigana na makafiri kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Usamah alimpa bendera hiyo Buradah bin Khazib nje ya jiji na akamteua kuwa mbeba bendera ya jeshi. Akaanza safari yake kutoka Madina na akasimama 'Jaraf' sehemu ambayo ipo karibu na Madina hadi jeshi lilipokusanyika. Pia Mtume aliagiza kwamba Muhajirina na Ansar isipokuwa Ali lazima wajiunge na jeshi la Usamah na kwenda naye. Baadhi ya masahaba walianza kulaumu kwamba Mtukufu Mtume alimteua mtumwa na kumweka juu ya Muhajirina na Ansari wenye vyeo vya juu. Kwa hiyo walijiingiza katika ukosoaji wa wazi kuhusu suala hili. Taarifa hii ilipomfikia Mtukufu Mtume alihuzunika sana, na licha ya homa, alitoka nje ya nyumba yake akiwa amekasirika sana na alipanda kwenye mimbari. Hapo, aliwahutubia watu, "Enyi watu! Haya ni mazungumzo gani ambayo mmejiingiza kuhusu kuteuliwa kwa Usamah kama kamanda wa jeshi, kama mlivyofanya wakati wa Vita ya Motah ambapo baba yake Usamah aliteuliwa kuwa kamanda wa jeshi. Kwa jina la Mwenyezi Mungu Usamah anastahili kuwa kamanda kama alivyokuwa baba yake."

Ni kwenye al-Milal wan Nahl kilichoandikwa na Shahristan na Hujajul Karamah kilichoandikwa na Sidiq kwamba Mtukufu Mtume aliwaambia masahaba kufanya matayarisho ya haraka kwa ajili ya jeshi la Usamah. Alaaniwe mtu anaye pinga jeshi la Usamah! Kwa mujibu wa Madarijun Nubuwwah, Abu Bakr na Umar walibaki

Madina na Usamah akaondoka na jeshi. Alipokaribia kuondoka mama yake alimwambia kwamba hali ya Mtume haikuwa nzuri. Alimshauri asiendelee na safari na hakwenda. Kwa mujibu wa Tarikhut Tabari, katika hali hiyo, Mtume aliagiza Ali aende kwake. Aishah alimshauri amwite baba yake (Abu Bakr) badala ya Ali, na Hafsa alishauri jina la baba yake (Umar) badala ya jina la Ali. Wakati huo watu hawa walikusanyika hapo. Lakini Mtume alisema, "Rudini makwenu. Nitawaiteni mimi endapo nitawahitaji." Waliposikia hivyo watu hao waliondoka.

Kwenye Sahih Muslim imetaarifiwa kutoka kwa Bin Abbas kwamba Mtukufu Mtume alikaribia kutawafu akiwa kitandani kwake, Umar bin Khatab na masahaba wengine walikuwepo hapo nyumbani kwake Mtume. Mtukufu Mtume akasema, "Niletee kipande cha karatasi na kalamu ili kwamba niweze kuandika kitu (kama wosia wangu) kwa ajili yenu msije mkapotoka baada yangu." Umar akasema, "Mtume haya kwa sababu ya weweseko. Tunayo Quran Tukufu na hiyo inatosha." Hapo hapo palitokea mzozo miongoni mwa watu waliokuwepo hapo.

Baadhi yao walisema, "Ni wajibu wetu kutii maagizo yake ili kwamba aweze kuandika chochote apendacho kutuandikia." Baadhi yao walimuunga mkono Umar. Ilipotokea kelele kubwa kuhusu suala hili, Mtume alisema, "ondokeni hapa kwangu." Ilikuwa kwa sababu hii kwamba Bin Abbas alikuwa akisema, "Ulikuwa msiba mkubwa na maafa kwamba Mtume hangeweza kuandika chochote kwa sababu ya kelele na mfarakano miongoni mwa watu."

Abdullah bin Abbas amenukuliwa na anasema kupitia kwa simulizi ya Said bin Jubayr alieleza kwenye Sahih Bukhari. "Ni siku ya janga iliyoje siku hii ya Alhamisi!" Baada ya kusema hivi, alilia na halafu akasema, "Siku hiyo ya Alhamisi, ugonjwa wa Mtume ulizidi sana,

akasema nileteeni kitu cha kuandikia ili niweze kuandika kitu kwa namna ya wosia wangu ambao mkiufuata hamtakengeuka baada yangu." Baada ya kusikia haya watu walianza kubishana na kupingana Mtume akasema: "Haifai kugombana mbele ya Mtume." Watu wakasema, Mtume anasema katika hali ya kuweweseka. Mtume akasema, "Ondokeni hapa kwangu. Hali yangu ni njema hata iwe vyopvyote vile. Si sahihi vyovyote vile mtakavyo sema. Niacheni peke yangu. Ondokeni hapa." Baada ya hapo Mtukufu Mtume alitamka wosia zake tatu kwanza kuwa fukuza kwa nguvu washirikina wote waliopo kwenye Rasi ya Uarabuni na pili, kuridhia ujumbe uliotoka sehemu za mbali. Msimulizi hakusimulia wosia wa tatu au alisahau."

Imesimuliwa kutoka kwa Said bin Jubayr kwenye Musnad Ahmad Bin Hanbal na Sahih Muslim kwamba Abdullah bin Abbas alisema, "Ni siku iliyoje siku hii ya Alhamisi, akalia sana hivyo kwamba machozi yalitiririka kwenye mashavu yake kama nyuzi za lulu. Baada ya hapo alielezea kwamba Alhamisi ni siku ambapo Mtukufu Mtume alisema, "Nipeni vitu vya kuandikia ili kwamba niweze kuandika kitu kwa ajili yenu ambacho kwa njia ya wosia wangu msije mkapotoka kwamwe baada yangu." Lakini, pamoja na yote hayo, watu walisema, "Anasema akiwa katika kuweweseka."

Shahabuddin Khafaji ameandika kwenye Nasimur Riyaz Sharah Shafa Qadhi Ayaz kwamba kufuatana na maelezo ya hadith zingine kuhusu tukio hili, Umar alisema, "Mtume anasema akiwa katika kuweweseka." Shahristani ameandika katika kitabu chake al-Milal wan Nihal kwamba mabishano na tofauti ya kwanza wakati Mtume anaugua ni pale ambapo Muhammad Ismail bukhari amesimulia kutoka kwa Abdallah bin Abbas kwa mamlaka ya kwake kwenye kitabu chake- Sahih Bukhari kwamba wakati maradhi yaliyo sababisha kifo cha Mtume yalipozidi, alisema, "Nipeni kidau cha

wino na karatasi ili niweze kuandika kwa ajili yenu hati kwa njia ya uthibitisho msije mkapotoka baada yangu." Aliposikia hivi, Umar alisema, "Mtume anasema hivyo kwa sababu ya ukali wa maumivu ya ugonjwa. Kitabu cha Mungu kitafanya kazi hiyo." Hivyo, palitokea mzozo, Mtume alisema, "Ondokeni niacheni mimi na msibishane na kuhojiana mbele yangu." Hii ndio sababu iliyomfanya Abdullah bin Abbas aseme baadae, "Ni balaa iliyoje iliyo sababishwa na mabishano hayo! Ilikuwa baina yetu na kuandika kwa Mtume na ilisababisha asiandike."

Allamah, Shibli Nomani ameandika, "Lipo neno la Hayr kwenye hadith lenye maana ya kuweweseka. Umar aliifasiri hotuba ya Mtukufu Mtume kama kuweweseka." (Al-Faruq, ul. 61) kwenye kamusi maana ya neno 'Hizyan' imeoneshwa kama mazungumzo ya upuuzi.[23]

Nazir Ahmad Dehlavi ameandika, "Wale waliokuwa na njozi za Ukhalifa katika akili zao walitangua mpango huo kwa kutumia ugomvi wa kuhalalisha upinzani wao kwa kusema kwamba Qurani ilitosha kufanya yote na kwa kuwa Mtume alikwishapoteza fahamu hapakuwepo na haja ya kumpa karatasi na kidau cha wino au vinginevyo angetoa imla ya mambo yasio na umuhimu."[24]

Imamu Ghazali ameandika kwamba kabla ya kifo chake Mtume wa Mwenyezi Mungu aliwaambia masahaba wake wampe kalamu, karatasi na wino ili aandike ni nani aliye stahili na kuwa Imamu na Khalifa wao. Lakini wakati huo Umar, aliwaambia watu kumwacha mtu huyo kwani alikuwa anasema upuuzi.[25]

Kwa ufupi, Mtume aliponyimwa kalamu na wino palitokea mzozo miongoni mwa wale waliokuwepo hapo. Ufahamu wangu wa kihistoria umesema kwamba wakati huo Abu Dharr, Salman, Miqdadi na bin Abbas na kadhalika walipinga kitendo cha kukataa na wanawake wakawaasa kutoka nyuma, "Nini kimewatokea! Kwa nini hamsikilizi kile anachosema Mtukufu Mtume? Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, mpeni anachotaka." Waliposikia hivyo Umar akasema, "Nyamazeni! Nyini ni sawa na wanawake wa Yusuf. Mnalia wakati Mtume mgonjwa na mnamghasi wakati anayo afya njema." Mtume aliposikia sauti yake akasema, "Usiwakaripie kwani wao ni bora zaidi kuliko nyinyi." (Tabrani).

9

MAISHA YA ABU DHARR

Kwa mujibu wa Rauzatul Ahbab, wakati wa kifo chake, Mtume alimwambia mwanawe Fatimah Zahra awaite wanawe wa kiume. Aliwapeleka mbele yake. Wajukuuu hao wawili, waliketi karibu na babu yao baada ya kumpa heshima yake na walipomwona yupo katika maumivu makubwa ya ugonjwa, walilia sana hivyo kwamba watu waliowaona nao pia wakaanza kulia. Hasan aliweka uso wake kwenye uso wa Mtume na Husein aliweka kichwa chake kwenye kifua chake. Mtume alifungua macho na akawatazama kwa huba, akawapapasa kwa mahaba, na akaonesha utashi wake kwa watu kwamba wanastahili kuheshimiwa na kunyenyekewa. Pia ipo Hadith kwamba baada ya kumsikia Husain analia, wote wale waliokuwa hapo walianza kulia na alipowasikia Mtume pia alianza kulia. Halafu akaagiza ndugu yake mpendwa, Ali aende kwake, Ali alikwenda na akaketi kuelekea kichwa cha Mtume. Aliponyanyua kichwa chake, Ali alikuwa anasogea karibu naye, alikiweka kichwa cha Mtume kwenye mkono wake. Mtume akasema, "Ali! Nimekopa kiasi hiki cha deni kutoka kwa Myahudi fulani kwa ajili ya vifaa vya jeshi la Usamah. Mlipe kiasi hicho cha fedha. Ewe Ali! Utakuwa mtu wa kwanza kuja kwangu kwenye Haudhi ya Neema na utapata matatizo makubwa baada yangu. Yakabili matatizo hayo kwa uvumilivu na utakapoona kwamba watu wamechagua dunia, wewe shughulikia mambo ya akhera."[26]

Pia imeandikwa kwenye Madarijun Nubuwah kwamba Fatimah Zahra lipata mshituko mkubwa kwa sababu ya kifo cha Mtume na alilia sana kwa uchungu. Muhadithi Dehlavi ameandika kwenye kitabu 'Ma thabatabis Sunnah" kwamba matukio mengi ya hatari yalitokea baada ya kifo cha Mtume. Ameyataja kwenye shairi akisema kwamba endapo matatizo ambayo yalimpata, yangeipata mchana ungegeuka kuwa usiku wa giza. Mwandishi wa Rauzatul Ahbah anasema kwamba baada ya kifo cha Mtume hakuna mtu aliyemwona anacheka.

Tabaqatcha bin Sad ameandika kwamba kichwa cha Mtume kilikuwa kwenye paja la Ali wakati wa mwisho wa uhai wake. Hakim anasema kwenye Mustadirak kwamba Mtume kabla hajakata roho alipitisha siri kwa Ali na alitatua matatizo yake ya kimuujiza.

Abdul Barr kwenye kitabu chake, Istiab amemnukuu Abdullah bin Abbas akisema, "Ali anazo sifa nne za aina hiyo na hakuna miongoni mwenu aliye nazo. Kwanza, Alikuwa mtu wa kwanza kupata heshima ya kuswali na Mtukufu Mtume. Pili, alikuwa ndiye mshika bendera pekee wa Mtume katika kila vita. Tatu, ambapo wakati wa vita vitakatifu wakati mwingine watu walikuwa wanakimbia kutoka kwenye uwanja wa vita na kumwacha Mtume nyuma, Ali alikuwa imara kuwa pamoja na Mtume. Nne, Ali ni mtu aliyeiosha maiti ya Mtume na kuizika kaburini."

Kwa mujibu wa imani ya Waislamu wa madhehebu ya Shia, Mtukufu Mtume alifariki siku ya Jumatatu terehe 28 ya mwenzi wa Safar (machi), 11A.H. (Muwaddatul Qurba), uk. 49 kimechapishwa

Bombay, 1310 A.H). Baada ya kifo chake palikuwepo na masikitiko na kilio miongoni mwa watu wa nyumba yake na masahaba walioheshimiwa. Abu Dharr, Salman, Miqdad, Ammar na masahaba wengine waaminifu walikuwa wanalia sana. Kwa ufupi alikuwa kama rafiki mpenzi aliyekuwa na masikitiko kando yake. Historia inaonyesha kwamba Abu Dharr Ghifari alikuwa na maono ya kudumu kuhusu msiba huu. Manazir Aksan Gilan ameandika, "Kwenye maelezo mengi ya maisha ya Abu Dharr japokuwa dalili za wazi zinaonekana za maumivu hayo ambayo bila ya kuwepo muumini anakuwa si muumini, hata hivyo yapo matukio kadhaa ya kutia moyo ambayo yanadhihirisha taswira nzuri ya uhusiano wa wote wawili yaani anayependa na anayependwa katika macho ya akili zetu."[27]

Wakati Mtukufu Mtume anakata roho, Abu Bakr alikuwa nyumbani kwake, Sakh, umbali wa maili moja kutoka Madina. Umar alizuia taarifa ya kifo isienee na Abu Bakr alipofika wote wawili walikwenda Saqifah Banni Saidah iliyopo maili tatu kutoka Madina, na pamoja nao pia alikuwa Abu Ubaydah bin Jarrah ambaye kazi yake ilikuwa mwosha. Vyovyote vile, masahaba wakuu wa Mtume walikwenda kuungana na kugombea Ukhalifa na kuacha maiti yake, na Ali alifanya mpango na akamudu mambo ya kuosha maiti ya Mtume na maziko. Ali aliosha maiti, Fazal bin Abas alinyanyua kaptura yake, Abbas na Qathm walimgeuza na Usamah na Shaqran walimwagia maiti maji. Baada ya maiti ya Mtume kuoshwa, ilivishwa sanda. Abu Talhah alichimba kaburi. Ali, aliongoza Swala ya kumsalia maiti na yeye ndiye aliyeingia kaburini na kuilaza maiti inavyo stahili mahali pake. Baadda ya hayo, alifukia kaburi kwa masikitiko makubwa. Abu Bakr na Umar na wengineo hawakushiriki matayarisho ya maziko yaani kuosha maiti, kuvesha sanda kusalia hadi kushusha maiti ndani ya kaburi, na kufukia kaburi la Mtukufu Mtume. Kwa sababu waliporudi kutoka Saqifah, Mtume alikwisha zikwa.[28]

Mtukufu Mtume alikuwa na umri wa miaka 63 alipotawafu.[29]

SURA YA KUMI

Baada ya kifo cha Mtume, wale masahaba ambao hawakuridhika kwa kitendo chake cha Ghadir Khum ambao walimpinga Ali, haraka sana walikusanyika Saqifah Bani Sadah mahali ambapo palitayarishwa maalumu kwa mashauriano yasiyofaa (Ghayathul Lughaat) na watu wachache wapatao 200 ambao walikuwemo Muhajirina na Ansar waliokubali na wasikubali walikuwemo, walianzisha msingi wa serikali ya mtu binafsi. Aliporudi Madina kutoka Saqifa, baada ya maziko ya Mtume, walianza kudai kiapo cha utii kutoka kwa watu kwa lengo la kupatia serikali hiyo ya kibinafsi sura ya pamoja na aina ya kidemokrasia. Ili kukamilisha lengo hili walionesha tabia ambayo katika ubinadamu wa kawaida inatetemesha si tu kwa masahaba wa kuheshimiwa lakini pia kwa Ahlul-Bait.

Kiini hasa cha hadithi hiii inayoumiza ya kipindi hiki ni kwamba, Ali alilazimishwa kutoa kiapo cha utii (Rauzatul Ahbab) na alipokataa, jeshi la Khalifa lilimpeleka mahakamani, huku shingo yake ikiwa imefungwa kwa kwamba (Bin Abil Hadid Motazali). Nyumba ya Fatimah ilichomwa moto (Tarikh Tabari, Tarikh al-Imamuah wa as-Siyasah Miratul Uqul) Mlango wa nyumba ulimwangukia Fatimah na kusababisha kuharibika kwa mimba ya mtoto wake wa kiume.(al-Milal wan Nahl of Shahristani). Allamah Mukkah Muin Kashifi ameandika kwamba Fatimah aliugua kwa sababu ya mshtuko wa tukio hili, na hatimaye alifariki.[30]

Halafu wale watu ambao walikataa kula kiapo cha uaminifu kwa Abu Bakr walilazimishwa kwa ukali, na wengine walipigwa sana. Salman Farsi ambaye Mtume alikwisha mjumuisha kwenye Ahlul Bait wake, pia alikuwa mmoja wapo wa majeruhi wa udikteta wao. Alipigwa sana hivyo kwamba shingo yake ilitenguka na hali hiyo ilidumu hadi kifo chake.

Majina ya wale waliokuwepo Madina na ambao walikataa kula kiapo cha uaminifu kwa Abu Bakr yameorodheshwa chini: Imamu Ali, Abu Dharr, Salman Farsi, Ammar bin Yasir, Miqdadi bin al-Aswad Khalid bin Said, Burayda Aslami, Ubay bin Kab, Huzayma bin Thabit, Suhayl bin Harrif, Uthman bin Hanif, Abu Ayyub Al-Ansari, Hudhayfa bin al-Yamani, Sad bin Ubaydah, Qays bin Sad Abdullah bin Abbas, Abbas bin Abdul Muttalib, Abdul Haytham bin Tayhan, Jabir bin Abdullah, Abdullah bin Thamit, Ubaydah bin Thamit, Abu Said Khidri. [31]

Imeandikwa kwenye ukurasa wa 43 wa kitabu hicho hicho (Tabsaratul Awam) kwamba baada ya siku chache Sad bin Ubaydah alipigwa mshale na akafa kwa sababu ya kukataa kwake kutoa kiapo cha utii.

Vyovyote vile uhuni huu wa kisiasa uliendelea baada ya kifo cha Mtukufu Mtume. Waandishi wa historia wameandika kwamba kiunga cha Fadak, rasilimali ya Ahlul bait kilinyang'anywa kwa sababu tu ya kukataa kutoa kiapo cha utii. Watu hawa walisema kwamba Ukhalifa ni haki isioondolewa kwa Ali na lazima apate. Maelezo marefu ya madai haya bado yapo kwenye hotuba ya Ali ya Shiqthiyyah iliyopo kwenye Nahjul Balaghah. Ali amesema wazi kwamba Ukhalifa ilikuwa haki yake ambayo iliporwa kutoka

kwake. Pia amesema jaribio lake la kuanzisha madai yake kama inavyoonekana kwenye ukurasa wa 231 katika kitabu cha an-Nihayah cha bin Athir. Sasa tunanukulu kutoka kwenye Tarikhi Ahmadi kuhusu msiba wa tukio hili la maangamizi ambalo liliwatokea Ahlul-Bait na masahaba waaminifu baada ya kifo cha Mtukufu Mtume, hivyo kwamba msomaji aweze kujua nini kilitokea baada ya yote kwa uzao wa Mtume na masahaba wake waaminifu majuma mawili tu baada ya kifo cha Mtume na Abu Dharr aliwajibika vipi kwa hali mambo yalivyokuwa.

Kwa mujibu wa Tarikh bin Jasir, Umar alikuwepo wakati wa kifo cha Mtukufu Mtume lakini Abu Bakr hakuwepo. Alikuwa kwenye kijiji kiitwacho Sakh. Mtume alipokufa, Umar alisema, "Kufuatana na dhana ya wanafiki, Mtume ametawafu, lakini ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba yu hai."

Kwa mujibu wa al-Milal wan Nihal cha Shahristani, Umar alitishia kumuua kwa upanga wake endapo mtu anasema Mtume ametawafu. Tukio hili pia limeandikwa kwenye vitabu vingine.[32]

Kwa mujibu wa Rauzatul Alhbab watu walianza kuwa na shaka kuhusu kifo cha Mtume waliposikia tishio hili la Umar. Wakati huo, Abu bakr alikuwa nyumbani kwake Sakh. Alipopewa taarifa ya kifo cha Mtume haraka sana alikwenda Madina na alipofika kwenye msikiti wa an-Nabi aliona kwamba watu walikuwa katika ghasia nyingi.

Kwa mujibu wa Tarikh Abul Fida, Abu Bakr alipoona hali hii ya watu, akakariri Aya ifuatayo: "Na Muhammad hakuwa ila ni Mtume tu. Wamekwisha pita kabla yake Mitume. Je, akifa au akauawa ndiyo mtageuka mrudi nyuma? (Qurani 3:144).

Waliposikia hivi watu wakasadiki kuhusu kifo cha Mtukufu Mtume. Baada ya hapo watu wote waliondoka kwenda Saqifah Bani Sadah.

Kwa mujibu wa Tarikh Bin Khaldun, baada ya kufika Saqifah Abu Bakr alisema, "Sisi ni sahaba na ndugu wa Mtume na kwa hiyo tunastahili zaidi kudai Ukhalifa wa Mtume kuliko mtu mwingine yeyote."

Kwa mujibu wa Tarikh Tabari cha Bin Jarir, Umar alimwambia Abu Bakr; "Nyoosha mkono wako ili niweze kutoa kiapo cha uaminifu kwako" Abu Bakr alisema, "Hapana; wewe ndiye unyooshe mkono kwa sababu katika kila hali wewe ni mwenye uwezo zaidi kuliko mimi." Pambano hili liliendelea kwa kipindi fulani. Hatimaye Umar aliunyoosha mkono wa Abu Bakr na akatoa kiapo cha uaminifu kwake na pia alisema, "Pia uelewe kwamba nguvu zangu zimeunganishwa."

Kwa mujibu wa Tarikh Kamil cha Bin Athir, Umar na watu wengine waliapa kuwa waaminifu kwa Abu Bakr, lakini Ansar wote au baadhi miongoni mwao walisema, "Hatutatoa kiapo cha uaminifu kwa yeyote isipokuwa Ali."

Kufuatana na Tarikg Khamis, wakati Abu Bakr alipomaliza kazi ya kupokea viapo, aliondoka Saqifa na kwenda Msikiti wa Nabi na akaketi kwenye mimbari. Hapa, pia, aliendelea kupokea viapo hadi mwisho wa siku na watu walishindwa kuhudhuria mazishi ya Mtukufu Mtume. Ilikuwa siku ya Jumanne usiku.

Kwa mujibu wa Kanzul Ummal imesimuliwa na Urwa kwamba Abu Bakr na Umar hawakuwepo kwenye mazishi ya Mtukufu Mtume, lakini walikuwepo kwenye kundi la Ansari (huko Saqifa bani Sadah) na Mtume alizikwa kabla ya kurudi kutoka huko.

Kwa mujibu wa Nihayah cha Bin Athir Jazari, Majma al-Bidar cha Mulla Tahir Qutni na al- Milal wa Nihal cha Shahristani, baadaye Umar alisema kwamba kutoa kiapo cha uaminifu kwa Abu Bakr ni jambo lililotegemewa lakini Mwenyezi Mungu alitunusuru kutoka kwenye uovu wake.

Kufuatana na Tarikh Abu Fida kundi la Bani Hashim na pia Zubayr bin al-Awam, Miqdadi bin Amr, Salman Farsi, Abu Dharr, Ammar al-Yasir, Bara bin Azib na wengine waliokuwa upande wa Ali, walikaa pembeni wakati wa kutoa kiapo cha uaminifu kwa Abu Bakr.

Imeandikwa kwenye Istiab cha Abdul Barr kwamba wakati kiapo cha uaminifu kilikuwa kinatolewa kwa Abu Bakr, Ali hakuapa uaminifu kwake na alikaa nyumbani kwake.

Kwa mujibu wa Muruj uz-Zahab cha Masudi, ambapo mnamo siku ya Saqifah kiapo cha uaminifu kilitolewa kwa Abu Bakr, Ali alimwambia Abu Bakr; "Umeharibu mambo yetu, ulituona kwa ushauri na hukufikiria haki yetu." Abu Bakr akasdma, "Lalamiko lako ni halali lakini nimefanya hivyo kwa kuhofia maasi."

Kwa mujibu wa Rauzatul Ahbab, Abu Bakr alipomaliza kazi ya kutafuta kiapo cha uaminifu kwake, alimwita Ali kupitia kwa Wahajirina na Ansari kadhaa. Ali alikwenda na akauliza kwa nini nimeitwa? Umar akasema, "Umeitwa ili kutoa kiapo cha uaminifu kama ambavyo wengine wamekwisha fanya". Ali akasema, "Ninaiweka mbele yako hoja ile ile, ambayo umewaambia Ansari kupata Ukhalifa. Niambie kwa uaminifu mtu ambaye yu karibu zaidi na Mtume."

Umar alisema, "Hatutakuachia hadi hapo utakapotoa kiapo cha uaminifu." Ali alisema, "Jibu swali langu kwanza halafu niambie suala la kutoa kiapo cha uaminifu." Abu Ubaydah bin Jarrah akasema, "Ewe Abul Hasan! Ni wewe tu ndiye unayestahili Ukhalifa na utawala kwa sababu ya kutangulia katika Uislamu na ukaribu wako kwa Mtume, lakini kwa kuwa masahaba wamemkubali Abu Bakr, ni vema wewe pia uungane nao," Ali akasema Abu Ubaydah! Unataka kuhamisha neema kubwa ambayo Mwenyezi Mungu ameipatia familia ya Mtume na kupeleka kwingineko. Tazama! Sisi ni mahali palipoteremshwa Wahyi, mahali ambapo ziliwasili amri na makatazo, chanzo cha uadilifu na maarifa, na mgodi wa akili na ustahamilivu.

"Aliposikia hivi, Bashir bin Said akasema, "Ewe Abu Hasan! Tulidhania kwamba kukaa kwako nyumbani ulikuwa tayari kujitoa katika kinyang'anyiro cha Ukhalifa." Ali akasema, "Hivi nyinyi watu mnaona ni sawa kuacha maiti ya Mtume bila kukafiniwa, kuvishwa sanda na kuzikwa, na kwa hiyo ningejiingiza kwenye kugombania na kukirimu watu kwa kutafuta Ukhalifa?"

Imeandikwa kwenye Usudul ul-Ghibah kwamba Ali alimnukuu Mtukufu Mtume akisema, "Ewe Ali! Wewe ni kama Ka'abah ambapo

kila mtu huenda kuzulu, ambapo yenyewe haiendi kuzulu mtu yeyote. Kwa hiyo, endapo watu wa kundi lako wanakuja kwako kutoa kiapo cha uaminifu kwako kubali. Usiende kwao hadi wao waje kwako."

Kwa mujibu wa Rauzatul Ahbah, Abu Bakr aliposikia mambo haya na kuona kwamba kila sababu na hoja ya Ali, Ilikuwa haipingiki, thabiti na dhahiri kama hoja elfu moja, alisema kwa upole, "Ewe Abul Hasan! Nilidhani kwamba hungekataa kutoa kiapo cha uaminifu kwangu. Kama ningejua kwamba ungekataa, nisingekubali kuwa Khalifa. Sasa, kwa kuwa watu wametoa kiapo cha utii kwangu, nafikiri ni vema uungane nao, kama utapenda. Lakini, kama unasita kwa sababu hii, sitakulaumu." Baada ya Ali kusikia haya alinyanyuka na kwenda nyumbani kwake.

Kwa mujibu wa Iqdul Farid, cha Shahabuddin bin Abd Rabbihi Undlusi, watu waliokataa kutoa kiapo cha uaminifu kwa Abu Bakr walikuwa; Ali, Abu Dharr, Zubayr na Sad bin Ubadah. Miongoni mwao, Ali Abbas na Zubayr walikaa nyumbani kwa Bibi Fatimah hadi Abu Bakr alipomtuma Umar aende kuwatoa nje watu hao na kutumia upanga endapo wangekataa. Kwa hiyo, Umar alifika hapo akiwa na moto kwa lengo la kuchoma nyumba hiyo. Fatimah alipotambua nini kinachoendelea, alisema; "Ewe mwana wa Khattab! Umekuja kuchoma moto nyumba yangu!?" Umar alisema, Bila shaka nimekuja kwa nia ya hiyo, au vinginevyo, watu waliomo ndani ya nyumba hii watoke na watoe kiapo cha uaminifu kwa Abu Bakr."

Kwa mujibu wa Tarikh Abul Fida, Umar alikwenda na moto kwa nia ya kuchoma moto nyumba ya Fatimah. Fatimah alipotambua, alisema, "Ewe mwana wa Khatab! Umekuja kuchoma moto nyumba

yangu!?" Umar akajibu, "Ndio, vinginevyo watu waliopo ndani watoe kiapo cha uaminifu kwa Abu Bakr."

Kufuatana na Tarikhut Tabari cha bin Jarir, Umar alikwenda nyumbani kwa Murtaza (Imamu Ali) ambamo walikuwemo Talha, Zubayr na muhajirina kadhaa na akasema, "Kwa jina la Mwenyezi Mungu! Nitachoma moto nyumba hii vinginevyo mtoke nje kwa ajili ya kutoa kiapo cha uaminifu."

Imeandikwa kwenye Al-Imamah wa as-Siyasah cha bin Qutaybah Dinuri kwamba Abu Bakr alipogundua kwamba wale waliokuwa na Ali hawakuwepo wakati kiapo cha auaminifu kilipokuwa kinatolewa, alimtuma Umar awaite. Watu hao walikuwa ndani ya nyumba ya Ali. Walikataa kutoka nje. Umar aliagiza apewe kitita cha kuni zilizowashwa moto na akasema, "Tokeni nje au vinginevyo kwa jina la Mwenyezi Mungu nitawachoma watu waliomo ndani kwa moto!" Watu wakasema, "Fatimah, binti yake Mtukufu Mtume na yeye pia yupo ndani ya nyumba hii."

Umar akajibu, "Haidhuru kitu," Waliposikia hivi watu wote waliokuwa ndani ya nyumba walitoka nje isipokuwa Ali aliyekuwa anawapa maelezo watu ambao walitumwa wamwite, akasema; "Enyi kundi la Muhajirina! Ninayo haki zaidi ya kuchukua Ukhalifa kuliko nyinyi katika hali zote.

Sitatoa kiapo cha uaminifu kwenu. Kwa usahihi zaidi, nyinyi mnatakiwa kutoa kiapo cha uaminifu kwangu.

Tazama! Mmepata Ukhalifa kwa hoja mliyowapa Ansari kwamba nyinyi ni ndugu wa Mtume na jambo la kushangaza ni kwamba sasa mnajaribu kuchukua isivyo halali Ukhalifa kutoka kwa Ahlul-Bait wa Mtume.

Hamweki madai yenu katika msingi kwamba nyinyi ni bora zaidi kuzidi Ansari kwa kisingizio kwamba Mtume alikuwa wa kabila lenu? Sasa nakupeni hoja hiyo hiyo ambayo mliwapa Ansari kwamba, uhusiano wetu na Mtume ni mkubwa na karibu zaidi kuliko wenu wakati wa uhai wake na baada ya kifo chake.

Sasa mnatakiwa kutenda haki bila upendeleo endapo nyinyi mnamwanini Mwenyezi Mungu na kumwogopa Yeye.

Kuhusu kundi la wahajirina! Mkumbukeni Mwenyezi Mungu na msichukue uongozi wa Mtume kutoka kwenye nyumba yake na kupeleka nyumbani kwenu." Baadhi ya hapo, Fatimah alisema akiwa kwenye ngazi za mlango wake, "Enyi watu! Mlituachia maiti ya Mtume, mkatatua jambo la Ukhalifa kwa kujipendelea nyinyi na hamkuzingatia haki yetu."

Kwa mujibu wa Tarikh bin Qataybah Umar alipokwenda kwa Abu Bakr alisema, kwa nini hutoi amri ya kukamatwa Ali ambapo anapinga kutoa kiapo cha utii kwako?

Kwa mara nyingine Abu Bakr alimtuma mtumwa wake Qanfaz amwite Ali. Qanfaz alimwambia Ali, "Khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu anakuita wewe." Ali akasema, 'Mmemkashifu Mtume haraka kiasi hicho nyie watu."

Qanfaz alirudi kwa Abu Bakr na akarudia maneno aliyoambiwa na Ali. Baada ya kusikia Abu Bakr aliendelea kulia kwa kipindi fulani. Umar akamwambia Abu Bakr kwa mara ya pili, "Usimpe muda Ali ambaye hataki kutoa kiapo cha utii kwako." Abubakr akamuagiza tena Qunfaz kwenda kwa Ali na kusema, Amiri wa Waumini anakuita ili utoe kiapo cha uaminifu. Qanfaz aliwasilisha ujumbe wa Abubakr kwa Ali. Ali akasema kwa sauti kubwa "Mwenyezi Mungu na

asifiwe! Bwana wako amedai uhusiano huo ambao hana uwiano nao." Qafaz akaenda kwa Abu Bakr na kurudia maneno ya Ali. baada ya kusikia hivi, Abu Bakr alianza kulia tena. Halafu Umar akasimama na akifuatana na kundi la watu, alikwenda nyumbani kwa Fatimah na akagonga mlango. Aliposikia kelele za watu, Fatimah alianza kulia kwa sauti kubwa, "Ewe Baba! Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni tatizo gani hili lenye uzito mkubwa ambao limeletwa kwetu na mwana wa Khattab na Abu Quhafah!" Watu waliposikia kilio cha Fatimah, wengi wao walirudi huku wanalia na wachache tu ndio waliobaki nyuma na Umar. Halafu Ali akatoka nje ya nyumba na akaenda nao kwa Abu Bakr. Ali aliambiwa atoe kiapo cha uaminifu kwa Abu bakr. Alisema, "Endapo sitatoa kiapo cha utii itakuwaje?" Akasema, "Endapo hutatoa kiapo cha uaminifu, kwa jina la Mwenyezi Mungu tutakuua."