• Anza
  • Iliyopita
  • 21 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 18835 / Pakua: 2096
Kiwango Kiwango Kiwango
MAISHA YA ABU DHARR

MAISHA YA ABU DHARR

Mwandishi:
Swahili

26

MAISHA YA ABU DHARR

Ali alisema, Mtamuua mtu ambaye ni mja wa Mwenyezi Mungu na ndugu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu?" Umar akasema, "Tunakiri kwamba wewe ni mja wa Mwenyezi Mungu, lakini hatujui kama pia wewe ni ndugu yake Mtume." Abu Bakr alikuwa kimya wakati huo. Umar akamwambia, "Kwa nini hutoi amri, umekaaa tu?" Abu Bakr akasema, "Sitamlazimisha Ali wakati Fatimah bado hai." Halafu Ali alinyanyuka na alikwenda kwenye kaburi la Mtume ambapo alilia, kwa uchungu na akasema, "Ewe ndugu! Watu wa kabila wamenitukana sana na walikaribia kuniua."

Abu Dharr alikuwa anayaona mambo haya kwa macho yake.

Alikuwa na kumbukumbu ya yele aliyoyaona humo Ghadir al- Khum. Alishangaa sana kuona yaliyokuwa yanatokea.

Akiwa bado yupo katika mshangao, ghafla imani yake ilitikisa hisia zake na alikimbia hadi kwenye Msikiti wa Nabi. Akili yake ilipatwa

na fadhaa na kusumbuliwa na damu yake ilichemka kwa shauku. Alikuwa anangoja apate fursa ili atoe mawazo bila woga. Alipofika msikitini aliona kundi la masahaba wakiwemo Abu Bakr na Umar miongoni mwao.

Ujasiri wake wa kiume ulisisimuka na akaanza kutoa hotuba akiwa amesimama kwenye sehemu iliyoinuka.

Alisema: "Enyi watu wa Qurayshi! Nini kimetokea? Mmekuwa wazembe kiasi gani! Mmedharau kabisa ndugu wa karibu zaidi wa Mtume! Kwa jina la Mwenyezi Mungu kundi la Waarabu limeamua kuasi, na kutengeneza nyufa za mashaka katika imani. Nisikilizeni! Ukhalifa ni haki ya Ahlul Bait. Vurugu hii na ugomvi wa kelele ni mambo yasiyo na maana. Nini kimewapateni? Mnawaita wenye uwezo hawana uwezo na mnawasifu wasio na uwezo. kwa jina la Mwenyezi Mungu wote nyinyi mnatambua kwamba Mtume ametangaza tena na tena, 'Baada yangu Ukhalifa na uongozi ni wa Ali, halafu Hasan halafu Husein na halafu uzao wangu ambao ni maasum ndio watakao shika nafasi hii.'

Hamjali neno la Mwenyezi Mungu! Mlisahau mkataba ule na amri ile ambayo inawapa masharti. Mnaisujudia dunia hii ambayo inaandamia na mnauza Pepo ambayo inadumu milele, na ambamo vijana hawatazeeka na neema hazitapungua, na wakazi wake na neema hazitapungua, na wakazi wake hawatapata huzuni au kufadhaika na ambamo malaika wa kifo hatafika. Mmeuza kitu cha thawabu kubwa sana kwa bei ndigo sana. Mmefanya kitu kile kile walichofanya watu wa Mitume wa zamani. Walivunja kiapo chao cha uaminifu na waliasi pindi Mtume wao alipokufa!

Walitangua mikataba yao, walibadilisha amri na kugeuza imani. Sasa mnathibitisha kwamba mpo sawa na wao. Kundi la Quraishii! Baada

ya muda mfupi sana mtapata malipo ya makosa yenu na adhabu kwa maovu yenu. Kile mlichokituma kupitia na tabia yenu kitakuja kwenu kumbukeni! Vyovyote itakavyotokea itakuwa haki, kwa sababu Mwenyezi Mungu hawadhulumu waja Wake.[33]

Ujasiri wa kiume wa Abu Dharr unaweza kudhihirishwa na hotuba iliyojaa ushawishi. Ni wazi kwamba alikuwa na moyo ulio mwepesi kuhisi na alijaalia kuwa shupavu na jasiri.

Abu Dharr alitoa hotuba hii wakati ambapo hakuna hata mtu mmoja ambaye angeweza kusema neno. Jeshi la Khalifa lilikuwa linawasonga masahaba wa Mtukufu Mtume. Yeyote aliyeonesha dalili za kukataa kutoa kiapo cha uaminifu aliuawa. Yeyote aliyesita kutoa kiapo cha Uaminifu alisongwa. Mtu jasiri kama Ali alifungwa kwamba shingoni na sahaba kama Salman alikabwa koo na kupigwa sana hivyo kwamba maumivu yake yalisababisha kifo chake.

Shaykh Abbas Qummi ameandika kwamba Fatimah binti yake Mtume baada ya kupata maumivu kwa kuangukiwa na mlango, aliugua kwa kipindi fulani na alifariki dunia. Kwa mujibu wa wosia wake, Ali hakutangaza kifo chake kwa watu walioshiriki katika kusababisha usumbufu wake. Baada ya kumaliza kuosha maiti, Ali alimtuma Imamu Hasan kumwita Abu Dharr ili aisalie maiti, na alikwenda akamwambia.[34]

Hafidh Muhammad bin Ali bin Shahr Ashob (alifariki dunia mwaka 588 A.H) ameandika kwamba, maiti ya Fatimah ilisaliwa na Ali, Hasan na Husein, Aqil, Salman, Abu Dharr, Miqdad, Ammar na Buraydah. Hadith nyingine imejumuisha majina ya Abbas bin Abdul Muttalib, Fazal, Huzayfah na bin Masud pia.[35] .

SURA YA KUMI NA MOJA

Abu Dharr, kwa sababu ya desturi yake, mwenendo wake, tabia na amri ya Mtume, alishindwa kunyamaza inapobidi alisema kweli na aliishi maisha ya kimya. Kazi kubwa zaidi ya kumuabudu Mwenyezi Mungu ilikuwa kukaa karibu na kaburi la Mtume na kuwasifu Aali Muhammad (Uzao wa Mtume). Inaonekana na kwenye vitabu vingine vya historia kwamba Ali alimshauri afuate sera ya upole.[36]

Baada ya muda kupita hadi mwaka wa 13. A.H., Abu Bakr alifariki dunia. Kwa mujibu wa Tarikh Tabari na Mujam Kabir ya Tabarani, Abu Bakr alisema kwa majuto na masikitoko; "Endapo nisinge fungua nyumba ya Fatimah hata kama ilifungwa kwa nia ya kupigana, na kama nisingekubali Ofisi ya Ukhalifa, lakini ni kwamba niliweka mkufu wa Ukhalifa kwenye shingo la Umar au Abu Ubaydah."

Imeandika kwenye Tarikhi bin al-Wardi kwamba baada ya hapo alimteua Umar kuwa Mrithi wake. Kwa mujibu wa al-milal wan nahl cha Shahristani, Abu Bakr alipomteua Umar kuwa Khalifa muda mfupi kabla ya kifo chake, watu walipiga kelele, "Umemteua mtu mwenye hasira na moyo mgumu kama kiongozi wetu."

Kwa mujibu wa Tarikh Abul Fida, Abu Bakr alikufa mwezi wa Jamadiul ukhra tarehe 22, mwaka wa 13 A.H, kati ya muda wa Swala ya magharibi na Isha (usiku) na siku hiyo hiyo kiapo cha utii kilitolewa kwa Umar. Abu Dharr hakushiriki Swala ya kumsalia maiti au taratibu zingine za mazishi ya Abu Bakr kwa sababu hakuna kitabu cha historia kinachotaja jina lake katika tukio hili.

Wimbi la ushindi lilijitokeza bada ya kifo cha Abu Bakr. Chini ya hali iliyojitokeza wakati huo, Abu Dharr aliamua kuondoka Madina na kwenda Syria na kuishi huko kwa kipindi chote cha uhai wake. Kwenye kitabu cha Musnad cha Ahmad, anasema kwamba Abu Dharr alipendelea kuishi Syria kwa sababu ya wasia wa Mtume ambapo unasema ifuatavyo; "Ewe Abu Dharr! Ondoka Madina uende Syria wakati idadi ya watu itaongezeka na kuenea hadi Mlima Sala."

Kwa vyovyote vile, kwa mujibu wa wosia wa Mtume, Abu Dharr aliondoka kwenda Syria akiwa na mke wake na mtoto wa kike mmoja. Shah Walyullah Dehlavi, ameandika kwamba Abu Dharr aliondoka kwenda Syria baada ya kifo cha Abu Bakr na akaloea huko.[37]

Abu Dharr alikuwa mkali sana kuhusu kweli. Kwa hali hii, kamwe hakujali ukali wa mtu yeyote, wala hakuogopa serikali ya mtu yeyote au uwezo wa mtu yeyote.

Baada ya Abu Dharr kuondoka kwenda Syria, Umar alikwenda huko kwa madhumuni mengine alipokutana na Abu Dharr ambaye alimsimulia hadith moja ya Mtume. Abu Dharr alisema; "Nina shahidilia kweli kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema; "Mtu ambaye anafanywa kuwa mtawala au kiongozi wa mtu, ataamuriwa kusImamua kwenye daraja la Jahanamu. Atapata ukombozi kama yeye ni muadilifu, lakini kama ni mwovu, daraja litavunjika na kuanguka na mtu huyo ataanguka ndani ya Jahanamu."

Abu Dharr alikuwa anampenda sana Mtume(s.a.w.w) . Mapenzi haya yaliongezeka zaidi baada ya kufa Mtume na alikuwa akilia sana. Wakati alipokuwa anaishi Syria, watu walimshinikiza Bilal aadhini Adhana kwa ajili ya Swala.

Bilal akasema, "Nimeacha kuadhini Adhana baada ya kifo cha Mtume(s.a.w.w) . Wala sewezi kukariri Adhana sasa na siwezi kuivumilia." Kwa hali yoyote Bilal alishindwa na kwa shida sana alilazimishwa kukubali. Bilal alisimama ili adhini Adhana na akaanza kuadhini kwa sauti yake kubwa ambayo kipindi fulani ilisikika kwenye mitaa ya Madina wakati wa uahi wa Mtume(s.a.w.w) . Abu Dharr aliinamisha kichwa chake kuelekea mbele. Machozi yalianza kutiririka kwenye machavu yake. Fikra zake zilimkumbusha Madina na akamuona Mtume kwa macho yake ya kiroho, akiwa amezungukwa na masahaba wake. Akakumbuka mambo yaliyopita akaanza kulia kwa sauti kubwa huku machozi yakimtoka machoni pake." (al-Ishtiraki az-Zahid).

Abu Dharr aliishi nje ya Madina kwa muda wa miaka kumi huko Syria na alirudi Madina baada ya kupata taarifa kwamba Umar ameuawa.

Abdul Fida ameandika kwenye historia yake kwamba mtu aliyeitwa Abu Lulu alimshambulia Umar mnano mwezi wa Dhil Hijjah tarehe 24, mwaka wa 23 A.H Tarikh Kamil bin Athir ameonesha kwamba Umar alipojeruhiwa, mganga wa kabila la Bani Harith aliagizwa. Alimpa Umar divai ya tende. Uliotoka bila mabadiliko. Halafu akampa maziwa anywe, pia yalitoka bila ya kuona hali hiyo; "Ewe Amiri wa Waumini! Tayarisha wosia wowote unaotaka."

Imesimuliwa kutoka kwa Abu Wajiz kwenye Kanzul Ummal kwamba Umar aliuliza watu, "Mnataka nani awe Khalifa baada yangu?" Mmoja wao alisema, :"Zubayr bin al-Awam."

Umar akasema, "Mtamfanya mtu huyo kuwa Khalifa wenu ambaye ni bahili na hana staha." Mtu mwingine akasema; "Tutamfanya Talha awe khalifa wetu," Umar akasema; "Mtapenda kumpa Ukhalifa mtu ambaye aliweka rehani kwa mwanamke wa Kiyahudi

aridhi iliyotolewa wakfu na Mtume wa Mwenyezi Mungu?" Baada ya kusikia hivi, bado mtu mwingine akasema, "Tutamfanya Ali kuwa Khalifa wetu." Umar akasema, "Kwa niaba ya uhai wangu! Hamtamfanya Ali kuwa khalifa na endapo kwa jina la Mwenyezi Mungu, mtamfanya Ali kuwa Khalifa wenu, hatajizuia kuwawekeni katika njia iliyonyoka hata kama nyinyi ham-pendi." Walid bin Uqbah aliposikia hivyo, akasema, "Namjua mtu atakayekuwa khalifa baada yako," Umar alinyanyuka na akamuuliza, "Nani?" Walid akasema; "Uthman". Huzayfa bin al-Yaman anasimulia kwamba Umar aliulizwa, alipokuwa na afya njema, kama nani angekuwa khalifa baada yake. Akajibu, "Uthman bin Affan." Mulla Ali Qari ameandika kwenye ' Sharah I-iaqh Akbar' kwamba wakati wa muda wa kifo cha Umar ulipokaribia shughuli za Ukhalifa zilianza kufanywa na Uthman, Ali, Talha, Zubayr, Abdul Rahman bin Auf na Sad bin Abi Waqqas, na akasema kwamba Ukhalifa usivuke hawa watu sita.

Imeandikwa kwenye Tarikh Kamil kwamba Baada ya hapo Umar alimlaumu Suhayb, "Waongoze watu kwenye Swala kwa kipindi cha siku tatu wafungie ndani ya nyumba hawa watu sita ambao wengine miongoni mwao wanatekeleza kazi za ukhalifa halafu uwaangalie. Kama watano miongoni mwa watu hawa wanamkubali mtu mmoja na mtu mmoja anapinga, auawe endapo watu wanne wanakubaliana na wawili hawakubaliani, wawili wanakataa wauawe na kama watatu wanakubaliana na watatu wengine wanakataa, Abdullah bin Umar ateuliwe kuwa mwamuzi wa kuamua, na kama watu hawa wanamkataa Abdullah bin Umar kuwa mwamuzi, kundi ambalo Abdullah Rahman yupo lishinde na kundi lingine la watu liuawe."

Kwa mujibu wa Tarikh Abul Fida, Umar alikufa siku ya Jumamosi tarehe 30 mwezi wa Zil Hajjah. Kwa mujibu wa 'Sharah Fiqh Akbar,'

Ambapo baada ya kifo cha Umar, na kufuatana na maagizo yake, kikao cha baraza la ushauri kilifanyika ndani ya nyumba ya Fatimah, dada yake na Ashath bin Qays. "Kwa mujibu wa Tarikh Aathama, uk. 112, watu wa kundi hilo la watu sita lilimpa Abdul Rahman bin Auf, haki ya kumteua khalifa.

Abdul Rahman akiwa amenyanyua mkono wa Ali aliuliza mara tatu, "Endapo tunakuteua wewe Walyyul Amir na Imamu upo tayari kufuata Kitabu cha Mungu, Hadith za Mtume na hadith za Shaykhain (Abu Bakr na Umar)?" Ali alijibu, "Nitafanya hivyo, vyovyote vile itakavyokuwa, nitafuata Quran Tukufu na Suna ya Mtukufu Mtume(s.a.w.w) lakini (kuhusu suna za (shaikhain), nitapitia amri za kidini kufuatana na ujuzi wangu." Baada ya kusikia hivi Abdul Rahman alimuuliza Uthman mara tatu, "Utafuata Kitabu cha Mungu, Suna za Mtume na Suna za Abu Bakr na Umar, endapo tunakuteua wewe kuwa Imamu?" Uthman alisema, "Ndio vyovyote vile itakavyokuwa, nitafanya." Halafu Abdul Rahman alitoa kiapo cha uaminifu kwake na wengine wakafuata hivyo.

Imetamkwa kwenye Tarikh Kamil na Tarikh Abul Fida kwamba kiapo cha uaminifu kilipokuwa kinatolewa kwa Uthman, Ali alipoona hila katika jambo hili la kutoa kiapo cha uaminifu alisema, "Leo si mara ya kwanza kwamba mmepata ushindi kwa kutumia hila. Vema! Ni bora zaidi kuwa mvumilivu. Ewe Abdul Rahman! Kwa jina la Mwenyezi Mungu! Umetoa kiapo cha uaminifu kwa Uthman ili ukhalifa ukuelekee wewe," Abdul Rahman alisema; "ewe Ali! Usijali hili." Halafu akatoka nje ya nyumba huku akisema; Ilitakiwa iwe hivyo. Miqdad akasema; "Ewe Abdul Rahman! Ulimwacha Ali pamoja na kwamba, kwa jina la Mwenyezi Mungu, yeye ni miongoni mwa watu wasio achana na kweli na hutoa hukumu zenye haki."

Tarikh Kamil na Tarikh Tabari ni maandishi yanayosema kwamba, Miqdad iliendelea kusema., 'nilikuwa sijaona kitendo cha ukorofi kama hiki wanafanyiwa watu wa Nyumba ya Mtume baada ya kifo chake. Ninashangaa kuona kwamba Qurayshi wamemwacha mtu ambaye ninamfikiria kuwa mwanachuoni bora kuliko wote (Alim-i Rabbani) na jaji muadilifu kuliko wote (Adil). Kwa jina la Mwenyezi Mungu, endapo ningepata wa kuniunga mkono na msaidizi!" Miqdadi alisema hivi tu ambapo Abdul Rahman aliingilia kati, "Ewe Miqdadi! Muogope Mwenyezi Mungu. Ninahofu vinginevyo waweza ukajikuta upo kwenye matatizo."

Imeandikwa kwenye Murujuz Zahab cha Musudi kwamba Ammar Yasir alisimama kwenye Msikiti wa Nabi na akasema; "Enyi kundi la Waquraishi! Mlipopora Ukhalifa kutoka kwa Ahlul Bait wa Mtume wenu na mkauondosha na kuupeleka mara hapa mara kule, pia lazima tuwe na matumaini kwamba Mwenyezi Mungu atauchukua ukhalifa kutoka kwenu na kumpatia mtu mwingine kama ambavyo mmechukua kutoka kwa anayestahili." Halafu Miqdadi akasimama na kusema, Sijapata kuona kamwe aina hii ya mateso na maudhi ambayo Ahlul Bait wanapewa baadda ya kifo cha Mtume." Abdul Rahman akasema, "Ewe Miqdadi! Unafanya nini?" Miqdad akasema, "Kwa nini nisiseme?

Mimi ni rafiki wa Ahlul Bait wa Mtume kwa sababu mapenzi niliyonayo kwa Mtume na hakika wao hawaachani na kweli na ipo kwao peke yao. Ewe Abdul Rahman! Ninawashangaa Waquraishi ambao unajaribu kuwasaidia wapate kuwazidi wengine na ambao wamekula nyama kutaka kupora upendo na ukuu wa Mtume(s.a.w.w) kutoka kwa Ahlul Bait wake baada yake. Ewe Abdul Rahman! Tambua! Kwa jina la Mwenyezi Mungu! Kama ningekuwa na watu wa kuniunga mkono na marafiki, ningepigana na Quraishii kama ambavyo nilivyofanya kwenye vita ya Badr."

8

MAISHA YA ABU DHARR

Tambueni kwamba kuweza kukalia kiti cha Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na kuendesha ukhalifa ni kazi ngumu sana. Pia cheo cha Ukhalifa kipo nje ya uwezo wenu wa kuelewa. Mwenyezi Mungu amewapa utawala Mawalii na Maamiri ili waweze kuamua ugomvi baina ya wanyonge na wenye uwezo na kuwazuia wenye uwezo wasiwakandamize wanyonge.

Mjue kwamba ni amri ya Mwenyezi Mungu kumtii mtawala. Muwe na hofu kwa Mwenyezi Mungu. Mfuate maagizo Yake. Mjiepushe na upinzani na dhambi.

Wapo wengi miongoni mwenu ambao wameona siku za Mtukufu Mtume, wamesikia mazungumzo yake matakatifu na wameshuhudia matendo yake. Zaidi ya hayo, Kitabu cha Mwenyezi Mungu kipo mikononi mwenu. Lazima mmezisoma amri zote na makatazo yote na matendo mema na maovu. Mwenyezi Mungu amekupeni tangazo Lake la mwisho, Ameahidi kuwazidishia neema wale watakao mshukuru Yeye kwa neema hizo. Watu waadilifu watapata thawabu na adhabu watapewa waovu. Tayari

nimesikia ufahari na maonyesho na utukufu na uwezo wa wafalme na watawala. Wao walikuwa na uwezo zaidi kuzidi sisi na walikuwa na majeshi makubwa zaidi. Walikuwa na majiji makubwa na walikuwa wanaishi kwenye raha na starehe. lakini, kwa kuwa hawakutekeleza amri za Mwenyezi Mungu, walipenda zaidi dunia kuliko pepo, walipenda zaidi ugomvi na vurugu, na hawakutaka kumshukuru Yeye kwa ajili ya neema Zake. Aliwaweka kwenye uoza, na akawapeni nyinyi miji yao, nyumba zao na malisho yao wakawapeni neema zao zote. Neema zitabaki kwenu kama mkiendelea kumshukuru Mwenyezi Mungu kwazo, au vinginevyo zitapunguzwa kwa sababu ya dhambi zako na kutokuwa mtiifu na hatimaye utaangamia.

Mwenyezi Mungu amenipa mimi Ukhalifa wa Mtume. Nina uwezo wa kufanya kazi hii leo. Nimechukua ofisi hii mkononi mwangu na ninafanya kazi muhimu na nzito.

Mwenyezi Mungu huyu huyu ambaye amenipa Ukhalifa, hunipa uwezo unaolingana na ridhaa Yake, na pia nilitambua siri ya sentenso; Wote nyinyi ni walinzi na wote mtaitwa kuhesabu masuala yenu, na mmeelewa ukweli ulio wazi kwamba mtu ambaye amefanywa kuwa kamanda, amepewa dhamana kueleza kila tendo la watu wake na kuhesabu kila chembe na atomi. Watu wameniambia kwamba baadhi yenu waneweka pingamizi kuhusu fedha ninayotumia na wanaambizana kwamba ingelikuwa vizuri kama Uthman angeliwapa fedha hizi wapiganaji na watoto wao. Kwa vyovyote vile lingekuwa jambo la manufaa na lingekubaliwa na Mwenyezi Mungu. Ninakubali na nitaebndelea kukubali siku zijazo. Nimewatuma watu wa kuaminika katika kila jiji na kuwagawia wapiganaji na watoto wao fedha nyingi kadiri watakavyokusanya na kuweka akiba zitakazobaki kwa matumizi wakati zitakapohitajika.

Inshallah, nitakuwa ninawalipia haki zao wazee, fakiri, mayatima na wajane, nitataka ushauri wenu ninapokuwa na muda, kuhusu mambo yanayojitokeza na kuhitaji kufikiriwa na nitatekeleza kufuatana na ushauri wenu. Njooni kwangu mara kwa mara, zungumzeni na mimi matatizo na manufaa na nielezeni yale mnayoona yanastahili. Nitafanikisha kazi kama mnavyotaka na kufuatana na dharura itakayo kuwepo muda huo. Sina mlinzi mlangoni kwangu wa kuwakagua nyinyi. Mtu yeyote anaweza kuja wakati wowote na kuniambia lolote atakalo. Amani iwe kwenu!"

Baada ya kumsikia Uthman Waislamu wote walifurahi na walirudi kwao wakimsifu na kumwombea. Uthman alifuata njia ya haki, akazingatia usawa baina ya wapiganaji na raia, aliwafanya wema watu wote na aliwatimizia masikini na mayatima. Mwaka mmoja ulikwisha katika hali hii.

Kwa mara nyingine tabia yake ilibadilika kufuata taratibu ambazo zilikuwa kinyume na Sunna na uadilifu. Masahaba wa Mtume walikasirika sana. Walifanya mkutano na wakaamua kumuona Khalifa na wawasilishe kwake orodha ya maandishi ya mambo hayo ambayo yanachukiza katika Uislamu na ambayo yametokea tangu alipochukua cheo cha ukhalifa, kwa sababu mazungumzo ya mdomo yangeweza kusahaulika na hata kama wangekumbuka baadhi ya mambo muhimu lakini wangeshindwa kuyabainisha wazi wazi. Kwa hiyo ilionekena ni busara kuyaandika mambo hayo. Baada ya hayo, waloandika mambo yote matatu yanayo pingana na dini ambayo yalitokea tangu mwanzo wa Ukhalifa wa Uthman hadi muda huo, na walitaka waende wote kwa pamoja kukabidhi Khalifa waraka huo.

Halafu, watu hawa walionana na Ammar bin Yasir, wakamwambia walichoandika na wakamwomba awasilishe waraka huo kwa Uthman.

Ammar akajibu kwamba alikuwa tayari kufanya hivyo. Halafu akaemda kwa Uthman na waraka ule. Wakati ambapo khalifa alikuwa anatoka nje ya nyumba yake, Ammar alikuwa amefika mlangoni na akamuuliza, "Ewe Abul Yaqzan! Unataka kuniona?" Ammar akajibu, "Sina jambo lolote la kibinafsi na wewe lakini masahaba wa Mtume kwa pamoja wameandika orodha ya matendo yako ambayo umeyafanya kinyume na sharia ya dini , ili ufafanue maoni yako."

Uthman alichukua waraka huo akiwa amekasirika, alisoma mistari michache halafu akazitupa. Ammar akamwambia, "Usitupe kwa kuwa makaratasi haya yameandikwa na masahaba wa Mtume(s.a.w.w) . Badala yake, soma kwa uangalifu na utoe jibu ipasavyo, nina kwambia mambo haya kwa maslahi yako." Uthman akasema, "Ewe mwana wa Sumayyah! Unasema uwongo!" Akajibu, "Bila shaka mimi mtoto wa Sumayyah bin Yasir."

Khalifa akakasirika. Akaamuru watumishi wake wampige Ammar, sahaba wa Mtume(s.a.w.w) . Alipigwa sana hivyo kwamba alianguka chini na kupoteza fahamu. Halafu yeye mwenyewe Uthman alimpiga Ammar mateke kadhaa tumboni na sehemu za siri. Ammar akapoteza fahamu tena. Alipata mpasuko tumboni na kusababisha ngiri. Watu wa bani Makhzum ambao walikwua ndugu zake Ammar, walikwenda na Hashim bin Walid bin Mughirah waliposikia habari hizo. Wakamchukua Ammar na kumlaza kitandani. Ammar alikuwa bado amepoteza fahamu ambapo watu wote waliapa kiapo kwamba endapo angekufa, kwa sababu ya kipigo wangemuua Uthman. Wakati Ammar bado hana fahamu, vipindi vya Swala vya adhuhuri na jioni vilipita. Alipopata fahamu wakati wa usiku aliamka, akatawadha na kusali Swala zake za vipindi vilivyopita.

Jambo hili la Ammar pia ni mojawapo ya matendo mabaya ya Uthman ambayo yalisababisha masahaba wa Mtukufu Mtume(s.a.w.w) kuvunja kiapo cha uaminifu kwa hasira[38] . Hili ni tukio moja tu ambalo limeandikwa kwenye vitabu vya historia. Ifuatayo ni mifano michache kutoka kwenye vitabu vya kuaminika na mashuhuri vya historia, ili ijulikane ni matendo gani aliyoyafanya wakati wa Ukhalifa wake na alifanya kwa umma na masahaba wa Mtukufu Mtume(s.a.w.w) .

Imeandikwa kwenye Tarikh khulafa cha Suyuti, kwamba Uthmani alikuwa mtu wa kwana kuanzisha Adhan ya kwanza kabla ya Sala ya Ijumaa. Kufuatana na 'al-Wasail Fi Marifatul A wail' Uthman alikuwa mtu wa kwanza kufanya hotuba itangulie Swala ya Idd. Kamwe haikufanyika wakati wa uhai wa Mtume(s.a.w.w) na wakati wa utawaka wa khalifa wa kwanza na wa pili. Kwa mujibu wa taarifa ya Masoud iliyopo kwenye, Murujuz Dhahab, Uthman alipopata Ukhalifa, mjomba wake Hakam bin al-Aas, Marwan bin Hakam na wengineo kutoka Bani Umayyah (ambao walifukuzwa Madina kwa amri ya Mtume) walikusanyika kwa Uthman. Marwan alikuwa ni yule yule aliyetengwa na kutolewa Madina na Mtume na alikatazwa kusogea karibu na Madina. Pia magavana walioteuliwa na Uthman, alijumuishwa kaka yake upande wa kikeni, Walid bin Uqbah ambaye Mtume alikwisha sema habari zake kwamba angekwenda Jahanamu. Walid bin Uqbah alikuwa na tabia ya kunywa kilevi na marafiki zake wapiga muziki na Malaya usiku kucha, na muadhini (anayewaita watu kwenye Swala) alikuwa akimwamsha kwa ajili ya Swala, naye (akiwa amelewa) alikwenda msikitini kuongoza Swala ya alfajiri, na baada ya Swala kusalisha rakaa nne badala ya mbili, alionesha kutaka kuendelea na rakaa zingine endapo watu walitaka kuendelea. Pia imeandikwa kwamba Walid akiwa kwenye rukuu ya Swala alikawia kunyanyuka na kusema; kunyweni na mnifanye mimi ninywe. Kwa hiyo, mara mmoja ilitokea watu waliokuwa mstari wa

mbele nyuma yake walisema, 'Hatukushangai wewe lakini tunamshangaa yule aliyekuleta wewe hapa ili uwe kamanda wetu." Taarifa ya ufisadi wa Walid na kulewa kwake ilipoenea kwa watu wote, kundi la Waislamu, akiwemo Abu Jundab na Abu Zaynab, walimzonga Walid msikitini. Wakamuona amelala na hana fahamu.

Watu walijaribu kumwamsha, lakini aliposhindwa kupata fahamu, walichukua pete yake ya alama kutoka kwenye kidole chake na haraka walikwenda Madina na kutoa taarifa ya ulevi wa Walid kwa Uthman. Uthman alimuuliza Abu Jundab ba Abu Zaynab walijuaje kama Walid alilewa mvinyo. Walisema huku wanampa pete yake kama ushahidi wa ulevi wake. Alikunywa mvinyo huo huo tuliokuwa tunakunywa wakati wa siku za ujahiliya (kabla ya Uislamu). "Badala ya Uthman kusikiliza mazungumzo yao yote, alianza kuwa laumu na kuwasukuma huku akisema, "Ondokeni hapa." Waliposikia hivi wote wawili walirudi haraka.

Kwa mujibu wa Tarikh Abul Fida Uthman alimfukuza Amr bin al-Aas kwenye ugavana wa Misri na badala yake akamteua kaka yake wa kuchangia ziwa Sad bin Ali Sarh na ni mtu huyu huyu ambaye Mtume alikwisha toa ruhusa ya kuuawa siku Makah ilipotekwa na Waislamu. Kwa mujibu wa Tarikh Kamil, Uthman alikwenda Hija na watu mwaka 26 A.H. Marwan bin Hakim anasimulia kwenye Musnad Abu Daud Tialisi. Nilimuona Uthman na Ali wakati wa Hija. Uthman alikuwa anawakataza watu kufanya Hija ya Mut'a (kutekeleza Hija na Umra). Ali alipoona hivi alikariri Tahlil (La ilaha illallah) ya Hija na Umra kwa pamoja na akasema; "Nipo hapa kwa Hija na Umra pamoja," Uthman akasema, "Ewe Ali! Unafanya jambo lile ambalo nimekataza watu wasifanye," Ali akajibu, 'Sitaacha Sunna ya Mtume kwa ombi la mtu." (Hadith hii inaweza kuonekana kwenye Sahih Bukhari pia).

SURA YA KUMI NA MBILI

Abdul Hamid wa Misri na Allamah Abdullah Subaiti wameandika kwamba Abu Dharr alikaa Madina baada ya kifo cha Umar. Aliona kwamba Uthman alikuwa anawapendelea Bani Umayyah ambao mvuto wao ulipenya kwa kina kirefu katika serikali ya Kiislamu ambapo ilikwisha pata utukufu wa himaya. Watu waliendekeza ufahari na maonesho na waliishi maisha ya anasa sana. Watu walipendelea zaidi pato la dunia. Aliona kwamba masahaba wengi walibadilika kabisa. Zubayr, Talha na Abdul Rahman bin Auf (wakawa wamepatana na serikali) walinunua ardhi na nyumba! Sad bin Abi Waqqas alikuwa na mawe magumu yaliyo kongomewa kwenye ikulu yake, aliinyanyua sana, akapanua na akajenga minara juu yake. Kwa hiyo, Abu Dharr alisimama na akajitokeza wazi wazi. Hangevunjwa moyo na kamanda au Khalifa yeyote. Alianza kuwaita watu kwenye kushikilia maadili na kumshambulia Uthman katika ho tuba zake.

Siku moja alitambua kwamba Uthman alimpa moja ya tano ya ushuru kutoka Afrika Marwan bin Hakam, dinari 300,000 alimpa Harith bin al-As, Zayd bin Thabit alimpa dinari 100, 000, Abdullah bin Ali Sarah kaka yeke wa kuchangia ziwa, alimpa sehemu kubwa sana isiyo na idadi ngawira kutoka Afrika, na ardhi ya Fadak iliyoporwa kwa Fatimah alimpa Marwan alianza kukariri aya hii msikitini; "Na wanaokusanya dhahabu na fedha, wala hawazitumii katika Njia za Mwenyezi Mungu ." (Quran Tukufu, 9:34).

Marwan akatambua kwamba Abu Dharr alimshambulia yeye na Uthman, akalalamika kwa Uthman ambaye alimuagiza mtumishi wake amwite Abu Dharr aende kwake. Abu Dharr alikwenda kwake. Uthman alipomuona akasema, "Abu Dharr! Acha hayo ambayo yanasikia, vinginevyo hutamuona mtu yeyote aliye na madhara kwako isipokuwa mimi." Abu Dharr akasema, "Ewe kamanda! Umesikia ninasema nini?" Uthman akasema, "Nimetambua kwamba unawachochea watu dhidi yangu." Abu Dharr aliuliza, "Kwa vipi?" Uthman alisema, "Unakariri aya 'Tangaza . mateso machungu . ndani ya msikiti." Abu Dharr akasema, "Ewe kamanda! Unanikataza mimi nisikariri kitabu cha Mwenyezi Mungu na nisifichue dosari za wale ambao wameacha amri za Mwenyezi Mungu! Kwa jina la Mwenyezi Mungu, siwezi kumkosea Mwenyezi Mungu kwa ajili ya Uthman. Hasira ya Uthman ni bora zaidi kwangu kuliko hasira ya Mwenyezi Mungu."

Aliposikia hivi Uthman alimkunjia uso Abu Dharr lakini hakuweza kuamua ajibu vipi maneno ya Abu Dharr. Kwa hiyo, hakusema kitu na akanyamaza kwa muda fulani. Abu Dharr alisimama na akaondoka hapo, akiwa na azimio madhubuti la kuwakosoa wale ambao walikuwa wanafanya kinyume na amri za Mwenyezi Mungu kuliko kipindi chochote kile.

Abu Dharr alimshambulia Uthman mara nyingi zaidi. Kwa hiyo alikasirika sana na alingojea fursa ijitokeze amfukuze Abu Dharr aende uhamishoni. Siku moja alipata nafasi na akaitumia.

Kwa mujibu wa Bin Wazir mwandishi wa Tarikh Yaqubi, watu walimwambia Uthman kwamba Abu Dharr Ghifari alimdhihaki yeye msikiti na alitoa ho tuba kwenye lango la msikiti ifuatayo: "Enyi watu! Yule anayenijua mimi ananijua mimi, lakini yule ambaye hanijui mimi, ambaye hanitambui ajue kwamba mimi ni Abu Dharr Ghifari. Jina langu ni Jundab bin Junadah Rabazi. Mwenyezi Mungu alimnyanyua Adam, Nuh, uzao wa Ibrahim na watoto wa Imrani, miongoni mwa watu wa duniani. Mtume Muhammad ni mrithi wa ujuzi wa Adam na maadili yote ambayo yaliwabainisha Mitume, na Ali bin Abi Twalib ni mrithi wa Mtume na mrithi wa ujuzi wake.

Enyi watu mliokanganyikiwa! Endapo baada ya Mtume wenu mlimpenda yule ambaye Mwenyezi Mungu amempenda na alimweka nyuma yule ambaye Mwenyezi Mungu alimweka nyuma na amaeuwekea mipaka utawala na urithi miongoni mwa Ahlul -Bait, mungepata neema zisizo na hesabu kutoka juu ya vichwa vyenu na kutoka chini ya miguu yenu na hakuna rafiki yake Mwenyezi Mungu angekuwa masikini na fukara, na hakuna sehemu ya wajibu wa Dini ingepotezwa, na hakuna watu wawili ambao wangepambana kwa sababu ya amri ya Mungu kwa sababu wangepata taarifa kuhusu amri hiyo kwenye Kitabu cha Mungu na Sunna za Mtume, kwa mujibu wa Ahlul-Bait kuhusu Mtume wao. Lakini kwa kuwa amekusudia kufanya yale ambayo hungefanya, lazima utapata adhabu kwa sababu ya maovu yako, na haikuchukua muda mrefu kabla ya hao ambao wamefanya uovu watajua watarudi kwa nani."

Pia imeandikwa kwenye kitabu hicho hicho kwamba Uthman pia alipata taarifa kwamba alifanya mabadiliko ya Sunna za Mtukufu Mtume na Sunna za Abu Bakr na Umar kwenye msingi ambapo ndoto ya Ukhalifa wake ulitokeza, na kwamba Abu Dharr aliweka lalamiko hilo mbele ya Umma.

Uthman aliposikia mambo haya, alimpeleka kwa Muawiyah, gavana wa Syria. Kwa mujibu wa Tarikh Abul Fida, tukio hili lilitokea mwaka wa 30. A.H.

Wasomi wanasema kwamba kwa kuwa Abu Dharr aliendelea kumkosoa Uthman kwa matendo yake ambayo yalikiuka sheria za dini, Uthman alimwekea mipaka mikali. Uthman aliagiza kwamba hakuna mtu aliyeruhusiwa kuzungumza na Abu Dharr au kwenda naye au kukaa naye. Mikutano iliitishwa mara kwa mara kutangaza agizo hili.

Kwa mujibu wa maelezo ya Allamah Majlis na Allamah Subaiti, Ahnaf bin Qays mara nyingi alikuwa na mazoea ya kwenda msikitini na kuketi humo siku moja aliomba kwa Mwenyezi Mungu; "Ee Mola! Nibadilishie kutokuchangamana kwangu na watu niwe na upendo na upweke wangu na watu wa kuwa nao na nipe rafiki anayefaa asiye na mfano."

Baada ya kumaliza Swala hii alimuona mtu amekaa na kufanya ibada kwenye pembe ya msikiti. Alinyanyuka kutoka alipoketi na akamwendea mtu huyo na kuketi karibu naye. Halafu akasema, "Wewe ni nani na jina lako ni nani?" Akajibu, "Jundab bin Junadah." Aliposikia hivi akasema, Mwenyezi Mungu mkubwa! Mwenyezi Mungu Mkubwa."

Abu Dharr akasema, "Kwa nini ulikariri Takbira?" Akajibu, "Nilipoingia msikitini leo nilimwomba Mwenyezi Mungu anipe rafiki mzuri sana. Ametimiza matakwa yangu haraka sana na amenipa mimi heshima ya kukutana na wewe."

Abu Dharr akasema, "Ninamwita Mwenyezi Mungu, zaidi yako, kumtukuza Yeye kwa sababu niliamuriwa kuwa sababu anayefaa. Ewe binadamu! Nisikilize mimi. Mtukufu Mtume ameniambia kwamba wewe na mimi tutakuwa sehemu ya juu sana na tutabaki hapo hadi watu wote wamefanyiwa hesabu." Abu Dharr aliendelea kusema; "Ewe mja wa Mwenyezi Mungu! Kaa mbali na mimi vinginevyo utapata matatizo." Akauliza, "Vipi hivyo rafiki?" Abu Dharr alimjibu, "Uthman bin Affan amenikataza nisikae na watu na ameagiza kwamba yeyote atakayekutana na mimi na kuzungumza na kaka na mimi ataadhibiwa." (Hayatul Qulub, cha Allamah Majlis Juzu ya 2, na Abu Dharr bin Al-Ghifari, cha Allamah Subaiti).

Kwa ufupi, Uthman alikasirishwa na ukweli wa Abu Dharr. Aliendelea na kazi yake licha ya kuwekewa mipaka na Uthman alipata taarifa kama kawaida. Hatimaye, alipochoshwa na Abu Dharr aliamua kumpeleka uhamishoni Syria.

SURA YAKUMI NA TATU

Waandishi wa historia wanasema kwamba Uthman alipochoshwa na kilio cha kutetea ukweli cha Abu Dharr alimfanyia kila aina ya ugandamizaji huko Madina. Amri yake ilikuwa hakuna ruhusa mtu yeyote kusema na kukaa naye. Alilazimishwa kunyamaza, lakini kilio chake cha kutetea ukweli kiliendelea. Alipotoa hotuba kwenye msikiti wa Mtume, watu waliyasikia maneno yake. Alipozungumza kuhusu masuala yanayohusiana na makatazo ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hotuba yake ilisisimua nyoyo za watu wa kawaida. Watu walizidi kuudhika kwa sababu ya matendo maovu na shughuli za Uthman zilikuwa kinyume na Uislamu. Kwa hiyo, kisiasa aliona inafaa kumtoa nje ya mji. Kisiasa aliona inafaa kumtoa nje ya mji. Katika kutekeleza lengo hili alimpeleka Syria. Labda alidhani kwamba kwa kuwa Muawiyah alikuwa Gavana wa Syria na pia mwerevu sana, Abu Dharr angepooza kabisa huko.

Kufuatana na uamuzi wake, Uthman alimlazimisha Abu Dharr kwenda Syria.

Abu Dharr aliondoka na kuacha maskani yake akiwa na familia yake na akafika Syria. Kufika kwake Syria ni tukio liliolothibitisha utabiri wa Mtume(s.a.w.w) ambao alitamka mbele ya Abu Dharr walipokuwa katika mazungumzo siku za nyuma. Kufuatana na ushawishi wa

Mtume alioonesha uvumilivu na alikubali uhamisho wake bila ubishi[39] .