• Anza
  • Iliyopita
  • 21 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 10410 / Pakua: 967
Kiwango Kiwango Kiwango
MAISHA YA ABU DHARR

MAISHA YA ABU DHARR

Mwandishi:
Swahili

13

MAISHA YA ABU DHARR

Watu hao walikwenda kwa Abu Dharr usiku wakiwa na huo mfuko wa fedha. Wakati huo alikuwa anasali msikitini. Labda alikuwa anakaa kwenye msikiti wa Mtume wakati huo kwa sababu Uthman alimuita kwa lazima kutoka Syria ambapo familia yake ilikuwa bado huko.

Akiwatazama wageni, Abu Dharr aliwauliza wao walikuwa nani na walikuwa na madhumuni gani? Wakampa mfuko wa fedha na wakasema, "Khalifa Uthman amekupa salamu zake na anakuomba ukubali kuchukua hizi dinari mia mbili kwa ajili ya matumizi yako." (Kashkol Bahai).

Abu Dharr akasema, "Je! Amegawa kiasi kama hiki kwa Muislamu mwingine pia?" Wakajibu, "Hapana, hajampa yeyote. Huu ni ukarimu wa Khalifa kwako peke yako.

Tafadhali chukua."Abu Dharr akasema, "Mimi pia ni mmojawapo wa Waislamu ambapo Khalifa hajampa Muislamu yeyote, mimi peke yangu siwezi kukubali kuchukua. Mimi sihitaji fedha ambapo Waislamu wengine masikini hawakupata. Nendeni, mrudishieni na mwambieni kwamba mimi ninatosheka na ngano kidogo tu, mimi hupata ujira wa riziki yangu. Nifanye nini na dinari hizi?"[122]

Marwan alikosea kufanya uamuzi huo kuhusu Abu Dharr. Yeye alidhani kwamba kama vile watafutaji wengine wa dunia hawakujali imani na itikadi kwa ajili ya utajiri, Abu Dharr naye angefanya hivyo. Hakujua kwamba Abu Dharr alikuwa kwenye daraja la juu zaidi kulinganishwa na watafutaji wa dunia.

Tukiliangalia tukio huli kwa uangalifu, Abu Dharr alifuata kwa karibu sana nyayo za Mtukufu Mtume na Ali kwa kurudisha fedha na kwa kusema, "Maana yake nini kunipelekea fedha peke yangu na

kutowajali Waislamu wengine?" Hawa (Mtume na Ali) ni watu ambao walijali kuwatumikia Waislamu zaidi kuliko kutumikia nafsi zao. Wao hawakutaka wawe wanabilingika kwenye utajiri ambapo masikini waendelee kuwa masikini. Wao hawakupenda kuwepo na hata ile tofauti ndogo baina yao na watu masikini. Kwa uthibitisho tunaweza kutoa mfano wa tukio la kufuturu kwa Ali kama ilivyosimuliwa na Ahnaf bin Qays mbele ya Muawiyah barazani kwake.

Kwa mujibu wa Mansur bin Husein Abi alikufa 422 A.H) kwenye kitabu chake Nass ud-Duras, kama ilivyo nukuliwa na Shaykh Muhammad husayn Ale Kashiful Ghita; Ahnaf bin Qays alisema, "Wakati fulani nilikwenda kwa Muawiyah.

Aliweka mbele yangu vyakula vya aina nyingi mno. Nilikuwa bado ninashangaa ambapo aliweka mbele yangu chakula maalum ambacho sikuweza kukitambua. Nikamuuliza hicho kilikuwa chakula gani. Akajibu kwamba huo ulikuwa utumbo wa bata uliojazwa ubongo na kukaangwa kwenye mafuta na kunyunyiuzia viungo.

Niliposikia hivi nilianza kulia. Muawiyah akaniuliza sababu ya kulia, nikamwambia kwamba nilimkumbuka Ali wakati huo.

"Siku moja nilikuwa na Ali ambapo muda wa kufturu ulifika. Aliniomba nisiondoke. Wakati huo huo mfuko ulio zibwa vizuri uliletwa. Nikamuuliza mfuko ulikuwa na nini. Akajibu kwamba huo ulikuwa unga wa shayiri iliyokaushwa Nikamuuliza kwa nini mfuko huo ulizibwa kwa uangalifu kiasi hicho, ilikuwa ni sababu ya kuzuia usiibwe au matatizo ya kiuchumi. Akajibu kwamba haikuwa sababu yoyote kati ya hizo mbili zilizotajwa. tahadhari hiyo ilikuwa kuwazuia wanawe wasije wakachanganya unga huo na mafuta ya samli au michikichi.

"Niliendelea kuuliza endapo mafuta ya samli au mchikichi yaliharamishwa. Akajibu kwamba hayakuharamishwa. Bado, ilikuwa muhimu kwa viongozi wa umma kujiweka katika hali iliyo sawa na ile ya watu masikini, ili kwamba ukosefu wa njia za kujikimu isije ikawa sababu ya tabaka la watu masikini kugeuka kuwa waasi. Muawiyah akaniambia kwamba nilimkumbuka mtu ambaye uadilifu wake si rahisi kukanusha."

Hata hivyo, wale waliopeleka mfuko wa dhahabu kwa Abu Dharr walirudi kwa Uthmani na wakamwambia alivyowaambia Abu Dharr. Uthman akamwambia Marwan, "Nilijua kabla kwamba Abu Dharr hangekubali kuchukua fedha hiyo."

Abu Dharr aliendelea na shughuli yake ya kuhubiri kama kawaida. Kila alichosema haikuwa upinzani ulioelekezwa kwa mtu fulani pekee. Hakika, alitaka watu wasimsahau Mwenyezi Mungu kwa sababu ya kuhodhi fedha lakini kuimarisha kanuni za Uislamu kwa kuwahurumia masikini. Abu Dharr hakuweza kuvumilia kuona utajiri wa Hazina ya Taifa unatumika kwa kupewa watu wasiostahili bila sababu yoyote ambapo watu wanaohitaji wanateseka njaa.

Hakuvumilia hata kupasuliwa na kuchomwa Quran. Hakuchoka kuwashutumu wale ambao walikuwa na hatia kwa kufanya uhalifu kama hao. Alikuwa nazo amri za Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Alikuwa anazingatia kanuni za Uislamu. Alitaka watawala Waislamu kufuata njia ya Uislamu.

Kwa ufupi, kwa upande moja Abu Dharr alikuwa anashughulika na kazi yake ya kuhubiri na kwa upande mwingine, Uthman alikuwa na shauku ya kupata njia ya kumnyamazisha. katika kutimiza lengo hili alijaribu kushauri kila aina ya mpango lakini hakuweza kufaulu. Hatimaye alitoa amri katika tangazo la jumla, "Hakuna ruhusa mtu yeyote kukaa na Abu Dharr, wala kusema naye." (al-Masud).

Agizo la mtawala lilitakiwa kutekelezwa bila masharti. Mara tu tangazo hili lilipofanywa watu waliacha kuwasiliana naye na wakaacha kusema naye. Watu waliondoka popote pale Abu Dharr alipopita kuepuka wasije wakashtakiwa kwa khalifa. Hakuna mtu aliyemsikiliza Abu Dharr wala kufika mahali alipokuwa. Lakini Ahuzar alikuwa mtu jasiri aliyoje. Hakujali mambo haya. Alikuwa anasadiki kwamba lolote alilofanya ilikuwa inalingana na Radhi ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo, alikuwa anaridhika kabisa na yale aliyokuwa anayafanya na hakuna sharti lolote ambalo lingefaulu.

Subaiti anasema kwamba licha ya tangazo, Abu Dharr aliendelea kuwapa nasaha watu kama kawaida. Kwa bidii sana hivyo kwamba humo Madina watu wa ukoo wa Umayyah ambao walikuwa waunga mkono wa Uthman, walichoshwa naye na wakalalamika kwa Uthman, kwamba Abu Dharr alikuwa hajaacha kuhubiri. "Sasa ametuchosha sana. kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na ufanywe mpango mwingine."

Aliposikia hivi, Uthman aliamuru Abu Dharr apelekwe kwenye baraza lake.

Kwa amri ya Uthman watu wakamkamata Abu Dharr na kumpeleka kwa Uthman ambaye alisema, "Ewe Abu Dharr! Nimekuonya kwa kila njia lakini hutaki kuzingatia ushauri wangu. Nini kimekutokea?" Abu Dharr akajibu, "Laana iwe juu yako, ewe Uthman! Mwenendo wako ni sawa na ule wa Mtukufu Mtume, au sawa na ule wa Abu Bakr bin Quhafa na Umar bin Khatab? Wewe unafanya mambo miongoni mwetu yale ambayo madhalimu hufanya." Uthman akasema, "Sijui lolote. Toka nje ya jiji langu!"

Abu Dharr, "Mimi pia sitaki kukaa karibu na wewe. Sawa, niambie niondoke nielekee wapi?"

Uthman, "Nenda popote unapotaka lakini ondoka hapa!" Abu Dharr, "Naweza kwenda Syria?"

Uthman, "Hapana, nimeagiza na ukaburuzwa kutoka huko. umewafanya watu wa Syria wanione mimi ni mkosaji kwao. Ninaweza kukupeleka huko tena?" Abu Dharr, "Labda niende Iraq?"

Uthman; "Hapana, unataka kwenda ambako watu hawashutumu

watawala wao?"

Abu Dharr, "Kama hivyo, niende Misri?"

Uthman, "Hapana!"

Abu Dharr; "Niende Kufah?"

Uthman, "Hapana."

Abu Dharr, "Sasa niende wapi? Niende Makkah?"

Uthman, "Hapana!"

Abu Dharr; "Ewe uthman! Hutaki mimi niende kwenye nyumba ya

Mwenyezi Mungu! Kuna tatizo gani kwako endapo mimi ninakwenda

huko na kumuabudu Mwenyezi Mungu hadi kifo changu?"

Uthman, "Hapana, kwa jina la Mwenyezi Mungu, kamwe!" Abu Dharr, "Basi niambie niondoke niende wapi. Niende porini."

Uthman, "Hapana"

Abu Dharr; "Basi nirudi kwenye siku zangu kabla ya Uislamu na

niende kuishi Najd. Kwa vyovyote vile niambie mahali pa kwenda."

Uthman, "Ewe Abu Dharr! Niambie ni sehemu gani unapenda zaidi

zaidi."

Abu Dharr, "Madina au Makkah au Jerusalem.

Uthman, "Huwezi kuishi huko kwa vyovyote vile. Sasa niambie sehemu unayo ichukia kuliko zote."

Abu Dharr, "Rabzah"

Uthman, "Vema, ninakuamuru uondoke uende Rabzah!" Aliposikia hivi, Abu Dharr akasema; "Mwenyezi Mungu Mkubwa! Mtukufu Mtume alisema kweli kwamba yote haya yatatokea." Uthman, "Mtume alisema nini?"

Abu Dharr, "Alisema Mtume Kwamba, ningehamishwa kutoka Madina, ningezuiwa kwenda Makkah ningelazimishwa kuishi sehemu mbaya sana Rabzah ambapo ningeuawa na ningezikwa na kundi la watu wa Iraq ambao wangekuwa wanakwenda Hijaz."

Aliposikia hivi Khalifa Uthman kwa mujibu wa Athan kufi, alisema, "Nyanyuka ondoka kwenda Rabzah. Kaa huko na usiende popote." Kwa mujibu wa Damah Sakibah Juz. 1, uk 194, aliteswa na kujeruhiwa sana. Halafu Khalifa akamuagiza Marwan ampeleke Rabzah akiwa amepanda ngamia asiye na tandiko la kukalia, na atangaze kwamba hakuna mtu atakaye ruhusiwa kumuona wakati anaondoka![123]

Haiwezekani kukanushwa kwamba huhamishwa kwa lazima ni sawa na kuuawa. Wale wanaofukuzwa kutoka nchini kwao hupendelea zaidi kuuawa kuliko kuhamishwa. Matukio yanajieleza yenyewe kwamba watu waliofukuzwa kutoka kwenye nchi ya uzalendo wao kila mara walilia sana. Uzalendo ni zawadi ya viumbe vyote. Hadith zimeiita hali hiyo ni sehemu ya imani. Mtume Yusufu alikuwa na kawaida ya kulilia kwao alikozaliwa wakati ameketi kwenye kiti cha ufalme wa Misri.

Bila kutaja Mitume wengine, na tutafakari matukio ya Mtume Muhammad(s.aw.w) . Alilazimika kuhama Makkah na kwenda Madina. Lakini kila alipokumbuka Makkah au alipowaona wakazi wa jiji hilo, macho yake yalijaa machozi. Loo! Abu Dharr alikuwa anafukuzwa kutoka kwenye mji wa nyumbani. Fikiria jinsi ambavyo alijihisi hususan alipokuwa anaondoka na kuacha kaburi la Mtume. Lakini hapakuwepo na uchaguzi wowote kwa sababu aliondolewa na kuhamishwa kwa mujibu wa mwandishi wa historia Tabari, ilikuwa ni utendaji wa Uthman kwamba alimfarikisha mtu kutoka watu, aliye kuwa kero kwake na alikuwa na kawaida ya kusema kwamba hakuna adhabu iliyokuwa kali kama hiyo.[124]

Amri zilitolewa kwa ajili ya kuhamishwa kwa Abu Dharr na pia kwamba hakuna mtu aliyeruhusiwa kumuaga au hata kusema naye au kumtembelea.

Abdullah bin Abbas anasema kwamba Abu Dharr alipohamishwa Madina kwenda Rabzah tangazo lilitoka kwamba hakuna mtu aliyeruhusiwa kusema na Abu Dharr au kumuona anaondoka.[125]

Hili ni agizo ambalo lilifadhaisha watu na kuwazuia makwao. Hakuna mtu aliyeweza kuwa jasiri kutoka nje ya nyumba yake kwa madhumuni ya kumuona sahaba wa Mtukufu Mtume(s.a.w.w) mwenye kuheshimiwa kama Abu Dharr isipokuwa Imamu Ali, Hasan, Husein, Aqil, Abdullah bin Jafar, Abdulah bin Abbas na Miqdadi bin al-Aswad.

Ingawa masahaba wa Mtukufu Mtume(s.a.w.w) hawakuweza kutoa maoni yao dhidi ya agizo la Uthman kuhusu uhamisho wa Abu Dharr, bado walipata wasi wasi sana. Si tu masahaba waliokuwa pale ambao walisumbuliwa na tukio hili lakini pia wale ambao walikuwa nje ya Madina lakini walisikia habari ya kufukuzwa kwa Abu Dharr Madina.

Mathalan Abdullah bin Masud ambaye alikuwa Kufah na pia watu wa kabila lake walipatwa na fadhaa.

Abdullah bin Masud aliposikia habari hizi akiwa Kufah, alipata wasi wasi na akahutubia kundi la watu ndani ya msikiti wa Kufah, "Enyi watu! Mmewahi kuisikia Ayah hii? "Bado, ni nyinyi ndio mnao waua watu wenu, na mnawafukuza baadhi yao nje ya makazi yao." Alipinga khalifa kwa kukariri ayah hii. Walid, gavana wa Kufah alimtaarifu Khalifa Uthman kuhusu tukio hili. Khalifa alimjibu barua yake kwa kumuagiza ampeleke bin Masud kwake. Abdullah bin Masud alipofika Madina, Uthman alikuwa na hutubia. Alipomuona, Uthman alimuamuru mtumishi wake Aswad ampige bin Masud. Alimvuta na kumtoa nje ya msikiti na kumtupa chini na akamcharaza sana, akamzuia nyumbani mwake na akasitisha ruzuku yake kwa maisha yake yote.[126]

Lazima ieleweke kwamba Ali pia ameonesha masikitiko yake kuhusu kufukuzwa kwa Abu Dharr kwa maombi ya 'Zammul Quraysh." (Sahifah Alawiyah).

Kwa ufupi, kufuatana na agizo la Uthman, Marwan alimpeleka ngamia ambaye hakuwekewa tandiko la kukalia kwa lengo la kumsafirisha Abu Dharr kusiko julikana ambapo ghafla Ali, Hasan, Husein, Aqil, Ammar, Abdullah bin Jafar, Miqdadi bin al-Aswad na Abdullah bin Abbbad walifika hapo na kusema; "Wewe Marwan uliye laaniwa! Acha! Usimkalishe kwenye ngamia. Lazima tumpe kwa heri."

2. Allamah Subaiti anasema kwamba masahaba wa Mtume walionesha kukasirika kwao kwa sababu ya kufukuzwa Abu Dharr kutoka Madina na kupelekwa Rabzah. Kwa mujibu wa Mustadirak wa Hakim, Abu Darda aliposikia habari za kufukuzwa kwake alisema kwa mshangao, "Inna Lillahi wa inna illahe rajiun!" (Sisi tumetoka kwa Mwenyezi Mungu na tutarudi Kwake) Alirudia maneno haya mara kumi

Ali akasema; "Ewe Abu Dharr! Usiwe na wasi wasi. Watu walikuogopa kwa sababu ya tamaa ya mambo ya dunia, na wewe hukuwaogopa kwa sababu ya imani yako hadi wakati walipofukuza. Abu Dharr! Mchamungu hupatwa na kila aina ya matatizo, lakini kumbuka kwamba Mwenyezi Mungu ni stadi wa kutengeneza njia za ajabu za ukombozi kwa wacha mungu. Hakuna kitu kinachoweza kukupatia maliwazo isipokuwa 'ukweli'. Ukweli' ndio utakao kuwa sahaba wako huko kwenye upweke. Najua kwamba wewe unaweza kupata mshtuko wa hofu kutokana na uwongo na hali hiyo haiwezi kuja karibu na wewe.

Halafu Imamu Ali akawaambia wanawe waagane na mjomba wao. Baada ya kusikia hivyo, Imamu Hassan akasema, "Ewe mpendwa wangu mjomba Abu Dharr! Mwenyezi Mungu na akuhurumie. Nyoyo zetu zinateseka. Usiwe na wasi wasi. Mwenyezi Mungu ndiye kiongozi wako na ni Yeye unatakiwa umweke mbele yako. Ewe Mjomba! Hakuna kitu kizuri kama uvumilivu. Mwamini Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye mpangaji wa mambo yako."

Ammar alisema kwa hasira, "Mwenyezi Mungu na asimhurumie mtu ambaye amekupa taabu kubwa sana na ampe wasi wasi mtu ambaye anakusumbua. Ewe Abu Dharr, kwa jina la Mwenyezi Mungu, endapo ungeikumbatia dunia ya watafutaji wa dunia, hawangekufukuza na endapo angekuwa umekubali tabia yao, wangekufanya wewe rafiki yao. Uliposimama kidete kwenye imani yako, wapenda mambo ya dunia wamechoshwa na wewe. Usiwe na wasi wasi kwa sababu Mwenyezi Mungu yupo pamoja na wewe.

Watu hawa ni wale wenye bahati mbaya ambao mawazo yao yanatamani dunia na wamo kwenye hasara kubwa sana.

Vivyo hivyo, watu wengine pia walisema na kumliwaza Abu Dharr kwa maneno tofauti.

Baada ya kusikia hotuba hizi Abu Dharr akalia sana na akasema, "Enyi Watu wa familia ya Mtukufu Mtume mlio neemeshwa! Nilipo waoneni, nilimkumbuka Mtukufu Mtume(s.a.w.w) na neema zikanizunguka. Enyi watu ninao waenzi! Ni nyinyi peke yenu mlikuwa njia ya kupita faraja hapa Madina! Wakati wowote nilipowaoneni nilipata hali ya kuridhisha moyo wangu na utulivu wa akili yangu.

Enyi wazee wangu! Kama ambavyo nilikuwa mzigo kwa Uthman hapa Hijaz, nilikuwa mzigo kwa Muawiyah huko Syria, kwa sababu anaye kaka yake wa kuchangia ziwa Abdallah bin Sarah kama gavana wa Misri, na mtoto wa kiume wa mama yake mdogo, Abdullah bin Amir kama Gavana wa Basra.

Sasa mnanipeleka mahali ambapo ni jangwa ambapo sina anayeniunga mkono mwingine isipokuwa Mwenyezi Mungu. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, natambua kwamba ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye msaidizi wangu na kwa ajili Yake peke Yake sitajali upweke wa nyika."

Kwa mujibu wa Allamah Subaiti, baada ya haya, Abu Dharr ambaye alikwisha kuwa mzee na dhaifu, alinyanyua mikono yake kuelekea mbinguni na akasema, "Ee Mwenyezi Mungu! uwe shahidi kwamba mimi ni rafiki yao Ahlul Bait na kila mara nitakuwa rafiki yao kwa ajili yako na kwa ajili ya Akhera, hata kama nitakatwa vipande kwa ajili ya mapenzi yangu kwa vitu hivi viwili." Baada ya haya Ali(a.s) akasema, "Ewe Abu Dharr! Mwenyezi Mungu na akuhurumie.

Tunatambua sana kwamba sababu pekee ya wewe kufukuzwa kutoka sehemu moja na kupelekwa nyingine ni mapenzi yako kwetu, wazao wa Mtukufu Mtume(s.a.w.w) .

Hata hivyo, watu hawa mashuhuri waliporudi Madina baada ya kuagana na Abu Dharr kwa huzuni, Uthman alikasirika sana.

Atham Kufi ameandika, Abu Dharr alianza safari ya kwenda Rabzah na masahaba wengine na Ali wakarudi. Khalifa akaagiza Ali aende kwake na akamuuliza sababu ya kutoka nje ya Madina na kumuaga Abu Dharr na kwa nini alichukua kundi la masahaba kwenda naye, bila kujali amri yake. Ali alimuuliza Khalifa endapo ilikuwa wajibu kwake kufuata amri za Uthman hata pale ambapo zilipingana na utii kwa Mwenyezi Mungu na ukweli. Halafu akaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba kamwe hangefanya hivyo."[127]

Allamah Majlis akimnukuu Shaykh Mufid anasimulia kutoka kwa Abu Ammah Bahili kwamba Abu Dharr baada ya kufika

4. Jina lake alikuwa Sadi bin Ajlan Zaidi hujulikana jina lake la utani, Bahilah ni jina la kabila lake. Hadith nyingi zimesimuliwa na yeye. Aliishi Homs (Syria) ambako alikufa akiwa na miaka 91. Watu wengine husema kwamba huko Syria alikuwa sahaba wa mwisho wa Mtume(s.a.w.w) kufia huko. Lakini ukweli ni kwamba huko Syria sahaba wa mwisho kufa alikuwa Abdallah bin Bashir[128] .

Rabzah alimuandikia mambo ya hatari yaliyo mpata Huzayfah bin al-Yaman, sahaba wa Mtukufu Mtume ambaye labda alikuwa Kufah. Kwenye barua hiyo, ametoa, ushauri wa aina mbali mbali na akaeleza kuhusu shida zake na matatizo yake. Ameandika' Neorullah Shustari ameandika kwamba wakati moja Huzayfah alimtembelea Abdullah bin Umar ambaye hakumheshimu. Wakati huo Huzayfah alimwambia kwamba wale ambao walikuwa bora zaidi yeye (binUmar) walihesabiwa kama wanafiki. Tukio la Uqbah lilitokea wakati watu wanarudi kutoka Vita ya Tabuk. Ali hakuwa na Mtume. Hatamu ya ngamia wa Mtume ilishikwa na Huzayfah na Ammar alikuwa anamwendesha ngamia. Ngamia alipofika kwenye mpasuko wa hatari baadhi ya wanafiki walijaribu kumuua Mtume kwa kumuogofya ngamia. Lakini aliokolewea na ujanja wa Ammar na Huzayfah. Huzayfah alikwenda kuishi Kufah siku arobaini baada ya kutoa kiapo cha uaminifu kwa Ali. Alikuwa anamuunga mkono kwa uaminifu. (Majalisul Monimi).

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu. Mpendwa Huzaifah, Ninakuandikia kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu kwamba kilio chako kimechupa mipaka. Ewe ndugu! Ikatae dunia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Usilale usiku kucha ukeshe unamuabudu Mwenyezi Mungu na uweke mwili

5. Huyu alikuwa sahaba aliye heshimiwa. Jina halisi la baba yake, Yaman lilikuwa Asal au Umail. Alikufa shahidi kwenye vita ya Uhud. Hudhayfah aliambiwa majina ya wanafiki na Mtume wa Uislamu. Kila mara Umar alikuwa akimuuliza Hudhayfah majina ya wanafiki. Hudhayfah pia alikuwa mtawala katika Madain wakati wa khalifa wa pili[129] .

Tabarsi anasema kwamba wanafiki walitayarisha njama ya kumuua Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenye bonde la Uqbah, lakini mpango huo ulivurugwa na Ammar yasir na wengineo. Mara tu baada ya tukio hilo, Mtukufu Mtume akafichua majina ya wanafiki kwa Hudhayfa. . Kwa mujibu wa maandishi ya Abu Dharr orodha ya majina yaliyofichuliwa kwa Hudhayfa pia ilijulikana Ashrah Mubashirah (Masahaba kumi wa Mtume ambao walijulikana kwa cheo hiki baada ya kifo cha Mtume.[130]

wako na roho yako katika taabu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Haya ni mambo yafaayo kufanya. ewe Ndugu! Ni muhimu kwa mtu ambaye anatambua kwamba mtu ambaye amekasirikiwa na Mwenyezi Mungu atadumu Jahanamu, ili uondokane na starehe za dunia, kesho usiku kucha katika kumuabudu Yeye na uteseke kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Ewe Ndugu! Ni muhimu kwa mtu anaye tambua kwamba furaha ya Mwenyezi Mungu ni ujumbe kuishi Peponi, kujaribu kutafuta radhi Yake mfululizo ili upatikane ukombozi na kufuzu. Ewe Ndugu! Mtu asijali kufarakana na familia yake kwa ajili ya radhi ya Mwenyezi Mungu. Ni radhi ya Mwenyezi Mungu tu ndio usalama wa Peponi. Endapo Mwenyezi Mungu anaridhika mambo yetu yote yatatimia na Pepo itakubalika. Lakini, endapo Mwenyezi Mungu haridhiki ni vigumu sisi kuwa na mwisho wenye furaha. Ewe Ndugu yangu! Mtu anayetaka kuwa pamoja na Mtume na watakatifu huko Peponi, lazima abadili maisha kama ambavyo nimefanya na kama ambavyo nimesema hapo juu. Ewe Hudhayfah! Wewe ni mmojawapo wa watu ambao ninao furaha kuwaelezea kuhusu machungu na mateso yangu. Kwa kweli mimi ninajiliwaza kwa kukutaarifu wewe yale yanayonipata au yaliyonipata.

"Ewe Hudhayfah! Nimeona dhuluma ya madhalimu kwa macho yangu, na nimesikia maneno yao ya kuchukiza kwa masikio yangu. Kwa hiyo, ninalazimika kutoa maoni yangu kuhusu mazungumzo hayo karaha na kuwaambia wao kwamba vyovyote walivyo kuwa wanafanya haikuwa sahihi kabisa. Nilifanya kwa kutimiza wajibu na kwa hiyo watu hao dhalimu wakaninyang'anya haki zangu zote. Wakanifukuza kutoka jiji hadi jiji na kuniswaga kutoka sehemu hadi sehemu na wakaniweka mbali na ndugu na jamaa zangu. Ewe Hudhayfa! Walisababisha vurugu kubwa na baya zaidi kuliko yote, walinizuia hata kwenda kutembelea kaburi la Mtume.

"Ewe Hudhayfa! Ninakuelezea kuhusu mateso yangu, lakini nina hofu isije maelezo yangu haya yakageuka kuwa malalamiko dhidi ya Mwenyezi Mungu. Hudhayfah! Ninakubali kwamba uamuzi wowote wa Mola wangu Mlezi na Muumbaji atakao ufanya kuhusu mimi ni sawa. Ninainamisha kichwa changu mbele ya amri Yake. Maisha yangu na yawe mhanga katika njia Yake. Ninatamani kupata radhi Yake. Nionaandika yote haya kwako ili uniombee na Waislamu wanaojitolea kwa Mwenyezi Mungu.

Amani iwe kwako." Abu Dharr.

Haijulikani Abu Dharr alipelekaje barua hii kwa Huzayfah bin al-Yamah. Huzayfah aliposoma barua hii macho yake yalijaa machozi. Akazikumbuka hadith za Mtume(s.a.w.w) kuhusu Abu Dharr. Kilichomshangaza yeye zaidi ni kufukuzwa kwa Abu Dharr na kupelekwa kwenye upweke. Alishika kalamu kwa uchungu mwingi na akaandika jibu la barua hii:

"Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye kuneemesha.

Mpendwa wangu Abu Dharr! Niliipokea barua yako na nikajua yanayokusibu. Umeniogofya kuhusu kurudi kwangu siku ya Hukumu na umeshawishi nifanye mambo fulani, kwa ajili ya kujitengeneza na kujiboresha mimi mwenyewe.

Ewe ndugu! Wewe umekuwa ukinitakia mema mimi na Waislamu wote kila mara na umekuwa na huruma na mwema ka wote. Kila mara ulikuwa na shauku ya ustawi wa wote. Kila mara uliwaonesha watu

njia ya uadilifu na ukakataza wasifanye uovu. Mambo kama yalivyo, uongozi ni haki ya pekee ya Mwenyezi Mungu. Humwokoa amtakaye na ukombozi unategemea radhi Yake. Ninamuomba Mwenyezi Mungu Atoe msamaha kwa jumla na neema nyingi kwangu, kwa wateule na watu wa kawaida wa umma wote.

Nimafahamu hayo mambo ya kushangaza, ambayo umeyataja kwenye barua yako, ni kwamba, ule uhamisho wako wa kufukuzwa kutoka mji wa nyumbani kwako na kuachwa kwenye nchi ya kigeni bila marafiki na wanao kuunga mkono, na kule kutupwa nje ya nyumba yako.

Ewe Abu Dharr! habari kuhusu mateso yako zimevunja moyo wangu kabisa kabisa na mateso ambayo unayapata sasa yanasikitisha sana. Lakini ninasikitika kusema kwamba siwezi kufanya lolote nikiwa hapa. Kama ingekuwa inawezekana kununua mabalaa yako yote kwa fedha yangu yote, ningefanya hivyo. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, kama ingewezekana ningejitolea kila kitu changu kwa ajili yako. Ewe Abu Dharr! Umo katika dhiki na siwezi kufanya lolote.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu kama ingekuwa inawezekana mimi na wewe kugawana matatizo yako hakika ningefanya hivyo. Nina hisi uchungu ulioje kwamba siwezi kukutana na wewe. Ni vigumu kufika pale ulipo. Endapo watu hawa katili wakinifanya mimi mshirika sawa na wewe katika matatizoa yako, nipo tayari kuchukua matatizo yako. Lakini, loo, haiwezekani iwe hivyo.

Ewe Abu Dharr! Usiwe na wasi wasi. Mwenyezi Mungu ndiye anayekuunga mkono. Anayaona mambo haya yote. Ndugu! Ni muhimu kwetu sisi, mimi na wewe, kumwomba Mwenyezi Mungu na tumsihi Yeye ili atuzawadie thawabu nyingi na atuokoe kutoka kwenye adhabu. Ewe ndugu! Muda unakaribia sana ambapo mimi na

wewe tutaitwa mbele ya Mwenyezi Mungu na tutaondoka kuelekea huko hivi karibuni. Ewe Ndugu! Usiwe na wasi wasi kwa matatizo ambayo umekuwa unayapata na usistaajabu. Mwombe Mwenyezi Mungu akupatie malipo yake.

Ewe ndugu! Ninafikiria kifo ni bora zaidi kwetu sisi kuliko kuishi hapa. Sasa ni muhimu sisi kuiacha dunia hii ya kupita kwa sababu baada ya muda si mrefu ghasia6 zitatokea kwa mfuatano moja baada ya nyingine. Ghasia hizi zitaendelea kuongezeka na zitawa-gandamiza watu waadilifu wa dunia. Panga zitachomolewa kwenye vurugu hizi na kifo kitawazunguka watu pande zote. Yeyote ambaye atanyanyua kichwa chake kwenye vurugu hizi hakika atauawa.

Ewe Abu Dharr! Ninakuombea wewe wakati wote. Mwenyezi Mungu na atuweke chini ya huruma Yake na atulinde tusiwe na kiburi wakati wa ibada. Mpangaji mkubwa wa mambo yetu. Siku zote sisi hutegemea ukarimu Wake. Amani iwe kwako Hudhayfah."[131]

Wasomi wanasema kwamba Abu Dharr aliishi na familia yake huko Rabzah ambapo ghafla mtoto wake wa kiume, Dhar aliugua. Hapakuwepo na daktari wa kumwendea huko jangwani kwa ajili ya tiba isipokuwa kumwamini Mwenyezi Mungu. Hatimaye maradhi yalizidi hadi wakati wake wa kufa ulikaribia. Mama mwenye huzuni

6. Labda anataja rejea ya utawala wa Bani Umayyah na Bani Abbas. Hakuna Kabila la makabila yote ya miji na majangwa ya Arabuni ambalo halitaathiriwa. Wakati huo, watu katili watafikiriwa kuwa ndio wa kuheshimiwa, na wachamungu watadharauliwa. Mwenyezi Mungu na atunusuru kutokana na uovu a kipindi hicho.

alinyanyua kichwa cha mwanae kutoka kwenye mchanga na kukiweka juu ya goti lake. Dhar alifariki. Mama na dada yake Dhar walianza kulia. Abu Dharr alishtuka sana lakini imani yake kwa Mwenyezi Mungu ilimliwaza. Alijizuia na hakulia. Kwa kuwa ilikuwa jangwa hapakuwepo na matayarisho kwa ajili ya mazishi. Historia haisemi haituambii Abu Dharr alivyomzika mwanae, lakini inajulikana kutoka kwa chanzo cha kuaminika alichofanya baada ya hisia zake kwa maneno muhadithi Yaqubi Kulayni ameandika; "Wakati mtoto wa kiume wa Abu Dharr, Dhar alipokufa Abu Dharr aliweka mkono wake juu ya kaburi lake na akasema; "Ewe mwanangu! Mwenyezi Mungu na akuhurumie. Ulikuwa mtoto anaye jiweza sana. Umekufa wakati mimi nina furaha na wewe. Utambue kwamba, kwa jina la Mwenyezi Mungu, sikupata hasara yoyote kutokana na kifo chako na simhitaji mwingine yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu. Ewe mwanangu! Endapo hapangekuwepo na kufikiria mshtuko baada ya kifo ningefurahi kutamani kuchukua nafasi yako kaburini. Lakini sasa kwa kuwa mimi nina omboleza kifo chako, hutaomboleza kifo changu. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sikulia kwa ajili ya kifo chako lakini mateso yako ndio yamenifanya nilie. Natamani ningejua nini ulichoulizwa na majibu yako. Ee Mwenyezi Mungu! Nimesamehe haki zangu ambazo nilikuwa ninamdai. Ee mstawishaji wangu! Ninakuomba umsamehe haki zozote ambazo ulikuwa unamdai. Mola wangu Mlezi! Wewe ni msamehevu zaidi kuliko mimi." (Usudul Kafi).

Shaykh Abbas Qummi ameandika kwenye kitabu chake Safinatul Bahar Juzuu ya 1, ukurasa wa 438 kwamba maneno yaliyotamkwa na Abu Dharr juu ya kaburi la mwanae Dhar, pia yalitamkwa na Imamu Jafar Sadiq juu ya kaburi la mwanane Ismail.

Abu Dharr alikuwa hajasahau kifo cha mwanae kijana ambapo mke wake pia alipatwa na mauti na hakumuona tena hadi milele.

Kwa mujibu wa Allamah Abdul Hamid, Abu Dharr na watu wa familia yake walikuwa wanaishi katika hali ambayo haikuwa na mpango unaostahili kuhusu chakula isipokuwa walikuwa wanapata kipande kidogo cha nyama ya ngamia aliyechinjwa kwa ajili ya maafisa wa serikali.[132]

Kwa kawaida walikula majani kama chakula chao kikuu au vitu vingine kipindi hicho. Siku moja mke wa Abu Dharr alikula majani yenye sumu ambayo yalisababisha apate maradhi ya hatari na alifariki dunia.[133]

Baada ya kifo cha mke wake, Abu Dharr alihisi kuwa mpweke mno. Alibaki yeye na mwanae wa kike. Watu waliokuwa wanaishi Rabzah walipojua kuugua kwa Abu Dharr, baadhi yao walimtembelea na kumtaka hali. Kwa mujibu wa usemi wa mtoto wa kike wa Abu Dharr, watu hao walimwambia; "Ewe Abu Dharr!Unaumwa na nini na unalalamika kuhusu nini?" Abu Dharr akajibu; "Nina malalamiko kuhusu dhambi zangu." Watu hao wakasema, "Unatamani kitu chochote?" Akasema, "Ndio natamani huruma za Mwenyezi Mungu" Wakasema, "Kama unataka tunaweza kumwita daktari wa tiba." Akasema, "Mwenyezi Mungu ndiye mganga wa uhakika. Maradhi na tiba yake vyote vimo kwenye uwezo Wake. Mimi sihitaji mganga wa tiba." (Hayatul Qulubi) Alikuwa na uhakika wa kifo chake.

Majlis, kwa mamlaka ya Sayyid bin Taus, amemnukuu Muawiyah bin Thalabah anasema: Hali ya Abu Dharr ilipozidi kuwa mbaya huko Rabzah na tukapata taarifa, tuliondoka Madina kwenda Rabzah kwa lengo la kumuona yeye. Baada ya kuulizia kuhusu hali yake tulimsihi atengeneze wasia wake. Akasema kwamba alikwisha tayarisha wasia wake, vyovyote itakavyo kuwa, mbele ya Amiri wa Waumini. Tukauliza, "Kwa Amiri wa Waumini unamaanisha Khalifa Uthman?" Akasema, "Kamwe! Kwa Amiri wa Waumini maana yake ni kwamba yule ambaye ndiye anayestahili kuwa Amiri wa Waumini. Ewe bin

Thalabah! Nisikilize! Abi Turab, (Baba wa Ardhi) Ali ndiye yeye ambaye ni maua ya dunia. Yeye ni msomi wa dini wa umma huu. Sikiliza! Utaona mambo mengi ya kuchukiza sana hapa duniani baada ya kifo chake." Nikasema; "Ewe Abuzah! Tunaona kwamba unafanya urafiki na watu ambao Mtume aliwapenda."

Sasa tunataka kusema kitu kuhusu mahali, Rabzar ambapo Abu Dharr alizuiliwa na hakuruhusiwa kuvuka mipaka yake.

Wasomi na waandishi wa historia wanakubaliana kwamba Rabzah ipo umbali wa maili tatu kutoka Madina karibu na Zate Araq kufuata njia ya kuelekea Hijaz na wakati huo huo haikuwa zaidi ya sehemu iliyotekelezwa na pweke maoni ukurasa wa 17 wa Juz. 2, ya Nahjul Balagha kwamba Rabzah ni sehemu iliopo karibu na Madina ambapo kaburi la Abu Dharr lipo. Bin Abil Hadid anasema kwamba Kufukuzwa kwa Abu Dharr na kupelekwa Rabzah ilikuwa sababu moja wapo ambayo iliwachochea Waislamu kumuasi Uthman.