HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.27%

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s. Mwandishi:
Kundi: VITABU VYA HADITHI

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.
  • Anza
  • Iliyopita
  • 13 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 30829 / Pakua: 10404
Kiwango Kiwango Kiwango
HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.

Mwandishi:
Swahili

1

1

HADITH ZA MTUME (s.a.w.w) NA MA-IMAMU (a.s)

3. HISTORIA YA UANDISHI WA HADITH KWA MASUNNI

Kazi zote zilizopo hadi leo zinazohusu Hadith zilikuwa zimekusanywa katika kipindi cha karne 2 A.H./8 A.D. au katika karne ya 3 A.H./9 A.D. Historia inatuonyesha kuwa katika kukaribia karne ya 2 A.H. kulitokezea idadi ndogo ya Muhaddithun ambao walianza kuziandika Hadith, ingawaje hazikuwa na mpangilio. Baadaye mkusanyiko huu mdogo ulikuwa kiini cha kazi zote kubwa. Hata hivyo wingi wa Hadith zilizopo sasa kwa kukusanywa, zilienezwa kwa desturi ya kutamkwa (kusemwa), na wakati zilipokuja kuandikwa vitabuni, zilikuwa hazikuwahi kuandikwa popote kabla yake. Ucheleweshwaji katika kuandikwa kwa Hadith ni swala mojawapo muhimu katika historia ya Hadith. Umuhimu wake ni wa ukweli kwamba kucheleweshwa huu kuliathiri hasa kuhusu utunzi na idadi ya Hadith pamoja na uwepesi wao wa kuzushwa (zikaongezwa na kupunguzwa na hatimaye zikawa ni zile zilizo na uongo) na matatizo mengi mengineyo yanayohusiana. Jambo la umuhimu huu katika swala hili linawahusu wale ambao ndio waliokuwa wamesababisha ucheleweshwaji huo wa kuandikwa kwa Hadith. Mwelekeo wao ulikuja kama ni mfano kwa ajili ya wengine katika kutoziandika Hadith. Katika sehemu yetu hii, tutaweza kuchambua makusudio yao na athari za mwenendo wao wa aina hiyo juu ya Hadith.

Kila kinachoweza kukusanywa kwa shida katika Historia ni kwamba baadhi ya Makhalifa walizuia uandikaji wa Hadith kwa sababu fulani fulani. Baada yao kikundi cha Sahaba na Tabiun waliwafuata katika swala hili. Kwa mujibu wa msemo "Watu hufuata dini ya wafalme wao," wao walijiepusha na uandikaji wa Hadith kwa kukubali na kuridhia kwa kuharamishwa hivyo. Wao walizihifadhi Hadith za Mtume(s.a.w.w) kwa kuzikariri tu (kwa kuzihifadhi akilini mwao tu). Kama vile tutakavyoona hapo mbeleni, wao nyakati zinginezo walijaribu kurejea katika kuziandika, ili kuyateketeza maandishi yao katika kipindi cha mwisho wa maisha yao, kama kwamba maandishi hayo yaliwasaidia wao tu katika kuhifadhi kwao. Kumbukumbu hizo za Hadith zilizokuwa zimeandikwa hazikutumiwa kwa kutaka kuzihifadhi kwa ajili ya vizazi vijavyo. Ni jambo la kuvutia sana kuona kuwa kupigwa marufuku wa uandikaji wa Hadith katika Sunni ulitolewa na watawala wao; na vile vile ile amri ya kuziandika Hadith pia zilitolewa na watawala wao.

Al-Zuhri anasema: "Sisi tulikuwa tukichukia mno uandishi wa elimu, hadi hapo wakuu wetu walipotulazimisha kuyaandika hayo. Hapo baadaye tulikuja kugundua kuwa hapakuwapo na yeyote miongoni mwa Waislam waliopinga." Al-Zuhri anaendelea kusema: "Wafalme waliniambia kuandika elimu ('ilm, i.e. Hadith) kwa ajili yao. Baada ya kuwaandikia kwa muda fulani, mimi nilishikwa na aibu mbele ya Allah swt; (mimi nilijiuliza): Je, kwa nini nimejitayarisha kwa ajili ya kuwaandikia wafalme na wala si kwa ajili ya watu wengineo!?".

Ni dhahiri, kama vile itakavyokuja kuonekana kwamba Hadith hazikuwa ni kweli kwa ajili ya Sahaba na Tabiun wote. Wengi wao na akiwemo Ali ibn Abi Talib(a.s) waliziandika Hadith na vile vile waliwaambia wengine kufanya hivyo. Wengine walianza kuziandika Hadith wakati sheria zilizowekwa na Makhalifa juu ya kutoziandika Hadith zilipobadilishwa na amri ya Kikhalifa kutoka kuziandika Hadith. 'Umar ibn Abd al-Aziz (101 A.H./719 A.D.) ndiye aliyekuwa Khalifa wa kwanza kuamrisha wanazuoni wa miji mbalimbali kuziandika Hadith na kumpelekea huyo Khalifa maandishi yote. Imeripotiwa kuwa Khalifa alimwandikia Muraah ibn Kathir akimwomba amwandikie Hadith za Mtume(s.a.w.w) Vile vile yeye alimwandikia Abu Bakr ibn Muhammad Hazm: "Andika Hadith yoyote ile ya mtume(s.a.w.w) uliyonayo na kunitumia na chochote kile kilichonakiliwa kutoka kwa Umar, kwa sababu ninayo hofu kuwa utafika wakati ambapo Hadith zitakuwa zimetoweka." Yeye pia aliwaandikia watu wa Madinah akiwataka wamwandikie chochote kile kilichobakia cha Hadith za Mtume(s.a.w.w) Ripoti hizi zinaonyesha wazi wazi kuwa uandikaji wa Hadith haukuwa jambo lenye umuhimu hadi wakati huo, hata hivyo, haimaanishi kuwa hapakuwepo na Hadith zilizokuwa zimeandikwa hadi wakati huo.

Pamoja na kifo cha Umar ibn Abd al-Aziz kazi hii haikufuatiliwa na Makhalifa waliofuata, na kwa mara nyingine tena uandikaji wa Hadith uliangukia katika kusahauliwa. Kukariri (kuhifadhi katika akili) ndiyo iliyokuwa njia iliyobakia. Hadith za kusemwa mdomoni tu (bila ya maandiko) ndiyo iliyokuwa njia ya uenezaji wakati ambao Sunni walirithi kutoka vizazi vyao vilivyowatangulia, ilisababisha upinzani mkubwa mno katika kuziandika Hadith. Sisi twaweza kuelewa vyema hali hii wakati tutakapokuja kujua kuwa baadhi ya Muhaddithun walichukizwa mno na uandishi wa Hadith hadi kufikia mwishoni mwa karne ya 2 A.H./8 A.D. Kauli za wanahistoria kuhusiana na ukusanyaji wa Hadith hapo mwanzoni zinaelezea hayo hayo. Abd al- Razzaq anaelezea kuwa mtu wa kwanza kuzikusanya Hadith alikuwa Abd al-Malik ibn Jurayj, aliyejulikana kama Ibn Jurayj (150 A.H./767 A.D.) Vile vile Abd al-Rahman Al-Awzai (88-157 A.H./707-773 A.D.) alikuwa ni miongoni mwa wale walioanza kuzikusanya Hadith.

Al-Dhahabi anaandika kuwa, katika kipindi hiki ndipo Wanazuoni wa Kiislamu walianza kuandika Hadith, Fiqh na tafsiri katika mwaka 143 A.H./760 A.D. Wafuatao ndio waliokuwa wakiongoza katika kazi hizo nao ni Ibn Jurayj katika mji wa Makkah, Malik (179 A.H./795 A.D.) huko Madinah, al-Anzai katika Syria, Said ibn Abi Urwah (156 A.H./783 A.D.) huko Basrah, Muammar huko Yemen, Sufyan al-Thawri (156 A.H./783 A.D.) huko Kufah. Kabla ya kipindi hicho, hata hivyo, Muhaddithun waliongoza wakiripoti Hadith kutokea kukariri au kutokea kwa waliotegemewa lakini zilikuwa ni mikusanyo isiyokuwa na mipangilio.

Mahali pengine yeye ni mbainifu zaidi wakati asemapo: "Ibn Jurayj na Ibn Abi Urwah walikuwa ni miongoni mwa watu wa kwanza katika ukusanyaji wa Hadith na Muammar ibn Rashid alikuwa ni wa kwanza miongoni mwao huko Yemen." Ipo habari iliyoripotiwa na Abd al-Aziz ibn Muhammad al-Darwardi kuwa mtu wa kwanza kukusanya elimu alikuwa Ibn Shihab al-Zuhri. Ibn Shihab al-Zuhr (124 A.H./742 A.D.) mwenyewe anaripotiwa akiwa amesema: "Umar ibn Abd al-Aziz alituamrisha kuzikusanya Hadith za Mtume(s.a.w.w) Kufuatiwa hayo sisi tuliandika katika sura ya kitabu, na kupeleka nakala ya kitabu hicho katika sehemu zote za utawala wake." Ni dhahiri, ingawaje Hadith zilikuwa zikikusanywa kwa kiasi fulani katika siku hizo, kazi ya ukusanyaji ilianza kuzorota kwa sababu ya upingamizi uliofuatia kifo cha Umar ibn Abd al-Aziz, na vile anavyosema al-Dhahabi, kazi hiyo ya ukusanyaji wa Hadith uliahirishwa au kuachwa kwa kipindi cha nusu karne.

Ibin Hajar anasema: "Kazi ya ukusanyaji na upangaji (tabwib) wa Hadith ulianza katika miaka ya mwishoni mwa kipindi cha tabi'un, yaani ni kwamba, wakati ambapo Wanazuoni wa Kiislam walipokuwa wameenea katika miji. Wa kwanza katika ukusanyaji wa Hadith walikuwa ni Rabi ibn Subayh na Sa'id ibn Abi Urwah......hadi wakuu miongoni mwa Wanazuoni wa tabaka la tatu walipokusanya ahkam. Al-Dhahabi pia anaelezea kitu kama hicho. Kutokana na taarifa hizo inaweza kudadisiwa kuwa ukusanyaji wa Hadith uliotokezea katika sehemu mbili: Sehemu ya kwanza ni mkusanyiko usio kamilifu mwanzoni mwa karne ya 2 A.H./8 A.D. na sehemu ya pili ni ukusanyaji uangalifu katika sehemu yake ya pili. Hajji Khalifah anakubaliana na haya pale asemapo: "Wakati Islam ilipoenea katika sehemu mbalimbali, na miji ya Islam ilipopanuka, tabi'un walisambaa mote humo. Baada ya muda, mkuu wao alipofariki dunia na hivyo ndivyo ilivyokuwa imekuja kuathiri ukusanyaji wa Hadith. Wanazuoni walianza kuhisi haja ya kuziandika Hadith na kuzihifadhi kwa njia ya kuziandika. Katika maisha yangu, lilikuwa ni jambo la maana la kuziandika Hadith, kwa sababu kukariri tu kuna uwezekano mkubwa wa kuweza kuja kupoteza fahamu au kuzipotoa. Baada yao, kulitokezea kipindi cha wataalamu wa Hadith kama Ibn Jurayj na Malik ibn Anas. Inasemekana kuwa mtu wa kwanza katika kukusanya Hadith alikuwa Rabi ibn Subay wa Basrah. Baada yahuyo, zoezi kama hili lilikuwa ni la kawaida. Kutokana na taarifa hizo, tunaweza kumalizia kuwa, kotekote, kulikuwapo na vipindi vitatu katika mpitilio wa Hadith za kutamkwa. Kipindi cha kwanza kilichukua/kilidumu mwanzoni hadi mwishoni mwa karne ya 1 A.H. /7 A.D. katika kipindi hiki uandishi wa Hadith haukuwapo wala haukujaribiwa isipokuwa tu katika hali chache ambapo Sahaba walijaribu kuziandika kwa kwenda kinyume na amri ya Makhalifa. Katika kipindi cha pili, kuanzia mwanzoni mwa karne ya 2 A.H./8 A.D. hadi kwa kufikia katikati, kulitokezea uandishi na ukusanyaji wa Hadith katika hali isiyokuwa kamilifu na pia mambo yaliyoandikwa yaliweza kukusanywa. Katika kipindi cha tatu, kilichoanzia katikati ya karne ya 2 A.H./8 A.D., uangalifu mkubwa ulielekezwa katika ukusanyaji na uandikaji wa Hadith ikiwa ni shughuli muhimu kimsingi. Vitabu vichache mno vilivyoandikwa katika kipindi hiki vinaweza kupatikana na baadhi ya mikusanyiko ya zamani sana pia vinaweza kupatikana na baadhi ya mikusanyiko ya zamani sana pia vinaweza kupatikana- kama vile musannaf Ibn Abi Shaybah, musannaf ya Abd al-Razzaq na Muwatta ya Malik ibn Anas yalikuwa yameanzishwa katika sehemu ya pili ya karne ya 2 A.H./8 A.D. Kwa mujibu wa ripoti ya al-Dhahab, musnad ya kwanza ilikusanywa na Nu'aym ibn Hammad. Yahya al-Hamani huko Kufah na al-Musd huko Basrah nao ndio waliokuwa wa kwanza miongoni mwa Wanazuoni wa miji hii katika kukusanya musnad.

4.SABABU ZA KUCHELEWA KUANDIKA HADITH

Inafahamika vyema kabisa kuwa Mtume(s.a.w.w) , kuanzia mwanzoni kabisa mwa Utume wake, aliupatia umuhimu zaidi kuhusu uandishi wa Qurani. Kimatokeo Qurani ikawa ipo mbali na makosa au mabadiliko (tahrif). Hata hivyo, katika hali ya Hadith kwa mujibu wa imani yetu mbali na ruhusa au amri ya Mtume(s.a.w.w) kwa kuhusiana na uandishi wa Hadith na mbali na ukweli kwamba Hadith zilikuwa zimeandikwa katika zama za uhai wa Mtume(s.a.w.w) , sio kwamba tu kuwa haukupewa umuhimu kwa kazi, pia iliweza hata kupingwa. Upingamizi huo ulisababisha matatizo mengi kuhusiana na Hadith, ambayo tutayaona hapo mbeleni. Uchelewesho huo wa kuziandika Hadith na matokeo yenye hatari yalifanya kikundi kimoja kumtupia lawama na 'udhubillah Mtume(s.a.w.w) Wao walitambua wazi kuwa upingamizi wa uandishi wa Hadith iwapo itatokea kwa Mtume(s.a.w.w) , basi haitaweza kulaumiwa, kwani Mtume(s.a.w.w) hawezi kulaumiwa; hata hivyo, iwapo wataielezea kwa wengine basi itatoboa udhaifu wao. Kwa hivyo, walimwelekezea Mtume(s.a.w.w) kuwa ndiye aliyekataza kuandikwa kwa Hadith.

HADITH NI NINI?

Mawaidha na Nasiha maneno aliyoyazungumza Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ni Hadith kwa kifupi, maneno yoyote yaliyotoka mdomoni kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) mbali na ayah za Qur'an Tukufu, ama yale aliyoyatenda kuonyesha, hayo yote ni Hadith. Vile vile maneno na matendo yote ya Ma'asumin (a.s) pia ni Hadith yaani yataingizwa katika Hadith. Kutokana na Hadith sisi tunaweza tukajua na kufuatilia na kutekeleza mambo ambayo ni usuli - Furu', Sunnah na faradhi. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) kwa maisha yake yote alikuwa pamoja na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Hivyo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) popote pale alipokuwa akiwapa watu nasiha na mawaidha katika mambo mbalimbali na kuwaongoza katika masuala mbalimbali basi Al Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s) daima alikuwa akinufaika na hayo yaliyokuwa yakisemwa na kutendwa na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na ndivyo alivyosema "Sisi ndio dalili za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na vile vile ndio Sahaba wake halisi, na sisi ndio ufunguo wa hazina yake ya ilimu na mlango wa mji wake wa ilimu alioutangaza Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na mtu yeyote hawezi kuingia katika nyumba au mji isipokuwa kwa kupitia mlango wake." Kwa kiapo cha Allah swt! Mimi nina ilimu na ma'arifa ya Utume na maneno ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Sisi Ahlul Bayt (a.s) ni milango ya hekima na kwa hakika sisi ndio tunayo nuru ya hukumu za Allah swt. (Nahjul Balagha).

Katika historia tunapata habari kuwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) ndio aliyekuwa mtu ambaye amekusanya na kuwa na hazina kubwa ya Hadith za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Tumepata kuona kuwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) yeye daima alikuwa akiziandika Hadith za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na kuzielewa na kuzikariri vyema kabisa. Na kwa amri ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ndipo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s) alitayarisha kitabu kimoja ambamo kumeandikwa Hadith za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na Sunnah zake, na kitabu hicho kinaitwa Sahifat Jami'a na kitabu kingine kinaitwa Kitabul Faraidh, ambamo katika vitabu hivyo vyote viwili kumeandikwa Ahkam za Sharia. Vitabu hivyo vimenakiliwa katika vitabu vingine mfano Sahih Buhari amenakili kwenye kitabu chake ambao ni upande wa Masunni. Na upande wa Mashi'ah Ma'ulamaa wa Kishi'ah Sheikh Sadduq (a.r) amenakili katika kitabu kinachoitwa Manla yahdharulfaqih na Sheikh Tusi (a.r) kinachoitwa Tahdhib na Thiqqatul Islam Quleyni r.a amenakili katika Al Kafi.

SHIA NA HADITHI

Kwa hakika Mashiah wana mchango mkubwa sana katika uandishi wa Hadith na katika hali ambayo ni sahihi. Na wa kwanza kabisa ni mchango Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) ambao hauna kifani wala usioelezeka, je litakuwa ni kosa gani iwapo wafuasi wake watamfuata yeye katika kuzidumisha na kuzihifadhi sirat na sunnah za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ? Katika historia vile vile tunapata mambo yaliyowazi kabisa kuwa kulikuwa na baadhi ya Ma-sahaba wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ambao walikuwa wakikataa kabisa kusiandikwe Hadith kwa sababu ya visingizio kuwa vilikuwa vikigongana na ayah za Qur'an Tukufu. Na wapo Ma-Sahaba wengine pia wameadhibiwa vifungo na adhabu mbalimbali kwa ajili ya kunakili na kusambaza Hadith za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Kwa hakika Ibn Hajar anaandika katika Futuh al-Bari utangulizi wake jambo moja la kustaajabisha, kuwa yeye anasema, "Mwanzoni mwa Waislam kulikuwa na utata katika uandishi wa Hadith, kwa sababu baadhi yao walikuwa wanasema kuwa ni karaha kuziandika. Na katika wale waliokuwa wakisema kuwa ni makuruh alikuwepo 'Umar bin Al Khattab, Ibn Masoud na Abu Sai'd Al Khudhri. Na katika upande wa pili ambao walikuwa wakieneza Hadith kwa usahihi walikuwa ni Al Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s) , mtoto wake Al Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) na vile vile Anas alikuwapo. Na kwa hakika Mashi'ah wamekuwa mbele katika kueneza Hadith zilizokuwa sahihi na miongoni mwao nawaletea majina yao:

1. Mtumwa wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) aliyekuwa akiitwa Abu Rafi', na ambaye alikuwa miongoni mwa wale Waislam wa mwanzoni kabisa. Bwana 'Abbas mjomba wake Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ndiye aliyekuwa amempa zawadi huyo, na wakati huyo mtumwa alipompa habari Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kuwa mjomba wake huyo Bwana 'Abbas ameukubalia Uislam, basi Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kwa kusikia hiyo habari njema alimfanya huru huyo mtumwa kwa sababu ya kuleta habari hizo njema. Katika fadhila zake tunaona kuwa yeye alifanya Hijra mara mbili, na amesali katika Qibla zote mbili na amefanya Bay'a ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) mara mbili.

Na vile vile ameshiriki katika vita vya Jihad vingi sana pamoja na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , na baada ya kifo cha Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) yeye hakumwacha Al Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s) na daima alikuwa naye pamoja. Alikwenda na Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) hadi Kufa, Nchini Iraq na alishiriki naye katika vita vitukufu vyote vilivyotokea na alikuwa ni mtu mmoja aliyekuwa akiaminiwa sana na Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) kiasi kwamba yeye alikuwa akitunza Baitul Maal pia. Yeye alifariki akiwa na umri wa miaka themanini na tano. Na yeye ni miongoni mwa Rawi wa Kishi'ah wanaoaminiwa na kusadikiwa, naye ameandika kitabu kimoja ambamo ameandika riwaya za Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) kinachoitwa Kitabu Sunan Wal-ahkam Wal-Qadhaya. Katika vitabu vya 'ilmul Rijal kitabu hiki ni muhimu sana na chenye faida kubwa sana.

2. Bwana Salman Muhammad (Al Farsi) ambaye baada ya kifo cha Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) aliandika habari za Jasliq kwa niaba ya Mfalme wa Roma

3. Asbagh bin Nabata, aliandika usia wa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) alioumfanyia Bwana Malik Ashtar, vile vile aliandika Nasiha alizomfanyia mtoto wake Muhammad. Asbagh bin Nabata alikuwa ni mmoja wa Ma-Sahaba wa karibu sana wa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s)

4. Suleim bin Kais Al Hilali yeye ameandika kitabu chenye Ahadith ambacho kinatumika mpaka sasa hivi na kwa mara ya mwisho kilikuwa kimechapwa huko Najaf Al Ashraf, nchini Iraq. Hadith zake zimetokana na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) mwenyewe na vile vile Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) ; Miqdad, Salman, Abudhar na wapenzi wa Ahlul Bayt(a.s)

5. Mitham al-Tammaar yeye alikuwa mmoja wa Ma-Sahaba mashuhuri na mshupavu wa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) yeye naye ameandika kitabu ambacho Sheikh Sadduq amekitumia katika 'Aamali na vile vile Tabari ametumia katika Basharatul Mustafa.

6. Zaid bin Wahab Aljahni ambaye ametunga kitabu kimoja ambamo ameandika hotuba zote za Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) alizokuwa akizitoa siku za Ijumaa na Idi, kwa hakika ameufanyia 'umma huu ihsani kubwa sana. Ibn Hajar na Ma'ulamaa wengine wanasema kuwa huyu bwana Zaid bin Wahab Thiqqah na wanampa Ukuu. Yeye amefariki katika mwaka takribani 96 Hijriyyah.

7. Mkusanyiko mkubwa kabisa wa semi na Dua za Ma'sumin(a.s) yanayojulikana kama Sahifa al-Kamila na vile vile inajulikana kama Zaburi Al Muhammad. Kitabu hicho kimekuwa tangia uhai wa Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) na humo kumeandikwa semi zao n.k. ambayo yalikuwa yamesimamiwa kikamilifu na Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) ndiye aliyefanya mpango huo.

8. Jabir bin Yazid bin Al Harith Al Jaufi, yeye ameziandika yaani yeye katika nuru ya ahadith za Masumin(a.s) ameandika Tafsiri, vita vya Jamal, Siffin, na Naherwaan, na vile vile ameandika kuuawa kwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) na Al Imam Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) Yeye amefariki katika mwaka 128 Hijriyyah.

9. Bwana Abu Hamza Thumali (aliyefariki mwaka 150 Hijriyyah) alikuwa mmoja Sahabi mashuhuri mwaminifu kabisa wa Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) na Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) na ameweza kutunga kitabu kiitwacho Annawadir Wa-Dhuhud. Vile vile amefanya tafsiri ya Qur'an Tukufu pia.

10. Vile vile miongoni ma Ma-Sahaba wa Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) na Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) alikuwa akiitwa Muhammad bin Keis Al Bijalli ambaye ameandika kitabu kiitwacho Qadhaya Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s)

11. Aban bin Taghlib (aliyefariki mwaka 141 Hijriyyah) ni kwamba wote wanaafikiana kuwa yeye ameishi katika zama za Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) , Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) na Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) , na Hadith zao alizozileta huyu Aban bin Taghlib zinasemwa kuwa ni Asili. Yaani inamaanisha kuwa Hadith zake hizo yeye alizoziandika zimetoka moja kwa moja kutoka kwa Maimamu(a.s) na si kwa kupitia watu wengine walizozisikia inamaanisha kuwa ni yeye mwenye amezisikia hizo.

12. Takriban waliosomea ilimu ya Hadith ilifikia elfu nne au na zaidi kuanzia katika zama za Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) na Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) Siku moja Hassan bin Ali Alwashakhi yeye alikutana na wale watu waliokuwa wakizoea kuzisema Hadith si chini ya mia tisa katika Masji Al-Kufa, na wengi wa wale waliokuwa wakizisema hizo Hadith walikuwa wakisema tumeambiwa Hadith hii na Ja'afar bin Muhammad yaani zilikuwa ni Hadith asili ambazo huyo mtu amezisikia moja kwa moja kutoka kwa Maimamu(a.s) .

13. Ibn Nadhir katika kitabu chake Fahrist amemwandikia yule Yunusu bin 'Abdul Rahman na habari zake kuwa ni mtu mmoja mwaminifu na mwenye kutegemewa kabisa ambaye miongoni mwa Ma-Sahaba wa Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) na Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) Kwa hakika kitabu hiki ni chenye manufaa sana kiitwacho Jawamiul Aasar.

14. Ibn Nadiim katika kitabu chake Fahrist amewaandika watoto wawili wa Sa'id bin Himad ambao ni Hussein na Hassan na vile vile ameandika habari zao pia, kuwa hawa watu walikuwa ni hodari kabisa katika 'ilimu ya Hadith,Fiq-h na Manaqib. Hao wote walikuwa wana kitabu walichokitunga juu ya Hadith na walikuwa ni miongoni mwa Ma-Sahaba wa Al Imam Muhammad Taqi Al Jawad(a.s) na Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) .

15. Fadhl Bin Shaazan Nishapouri (aliyefariki 260 Hijriyyah) yeye amewahi kuwa Sahaba wa Maimam watatu(a.s) ambao ni, Al Imam Muhammad at-Taqi(a.s) , Al Imam 'Ali an-Naqi(a.s) na Al Imam Hassan al-'Askari(a.s) Naye ameandika vitabu vitatu: " Cha kwanza Kitabul Faraidh Al Akbar, " cha pili Kitabu Faraidh Al Awsat, " cha tatu Kitabu Faraidh Al-Asghar ambacho ni mashuhuri.

16. Na baada ya hapo hii kazi ya ukusanyaji na uandishi wa Hadith ulikuwa umeendelezwa na Ma-Sahaba na wazee na wameweza kuleta kazi nne zilizo kubwa kabisa. Kazi hizo nne ambazo mpaka leo zinajulikana kwa jina la mashuhuri Kutub Al-'Arbi'a yaani inajulikana kwa jina la vitabu vinne. Kitabu Cha kwanza kabisa ni Al Kafi, ambacho kimetayarishwa na kuandikwa na Thiqqatul Islam Al Quleyni a.r. (amefariki mwaka 329 Hijriyyah) katika kitabu hiki zipo Hadith takribani elfu kumi na sita. Vile vile kuna kitabu kingine kinachoitwa Man la haydharul faqih ambacho kimeandikwa na Bwana Abu Ja'afer As-Sadduq humo takribani Hadith elfu sita zinapatikana. Vile vile kulikuwa na kitabu chake kingine kijulikanacho kwa jina Madinatul 'Ilm ambacho Shahid a.r. amekizungumzia. Na kwa kutokana na fitina za zama hizi kitabu hiki hakipo yaani hakipatikani Na Sheikh Sadduq a.r. katika mwaka 381 Hijriyyah. Vile vile tunapata vitabu viwili mashuhuri na vyenye faida sana ambavyo vinavyoitwa Tahdhibul Ahkam na kingine Al-Istibsaar vyote vikiwa vya Sheikh Taifah Bwana Ja'afer Muhammad bin Hassan Tusi (aliyefariki mwaka 460 Hijriyyah). Kwa kuunganisha vitabu vyote viwili zipo Ahadith elfu kumi na nane zilizo andikwa. Kwa hakika katika zama zote hizi ilimu hii ya Hadith na katika nuru ya Ayah za Qur'an Tukufu na Sunnah ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) 'ummah umeweza kuwatambua na kuwafuata Ahlul Bayt(a.s) na kuweza kujipatia ma'arifa yao na Ma-Sahaba. Katika kila zama kazi zilikuwa zikifanyika kwa kiwango fulani katika kuendeleza jitihada hizi za Hadith lakini katika mwaka wa 11 Hijriyyah kulifanywa kazi moja kwa kiasi kikubwa sana cha kutungwa kwa kitabu kiitwacho Bihar Al Anwar ambacho kilitungwa na Muhaqqiq 'Allama Majlisi (a.r) (aliyefariki 1111 Hijriyyah), kitabu hicho ambacho kilikusanya Hadith kwa wingi. Kwa hakika kitabu hiki kimoja yaani Bihar Al Anwar sisi hatujakipa heshima kiasi inavyotakiwa na wala sisi hatujafaidika nacho kiasi tunachotakiwa kufaidika nacho. Bihar Al Anwar ni kitabu ambacho Hadith ambazo hazikuandikwa katika Kutub Al-'Arbi'a basi hizo Hadith zinapatikana katika kitabu hiki cha Bihar Al Anwar. Kwa hakika kitabu hiki kina Juzuu ishirini na sita lakini katika Jamhuri ya Kiislam ya Iran na Beirut wamejaribu kukipanga katika vitabu vidogo zaidi ambavyo vimefikia Juzuu mia moja na kumi, ambavyo hata mimi ninavyo. Katika zama hizi vitabu hivyo na vingine vingi vinapatikana kwa urahisi katika CD za compyuta ambavyo mtu hana haja ya kujitwisha vitabu hivyo na inakuwa rhisi kutafuta masuala atakayo.

Kwa hakika Maulamaa wamefaidika sana na Hadith zilizo andikwa katika Bihar Al Anwar na vile vile inadhihirisha vile wanavyoonyesha kuisifu na kuiheshimu kazi hiyo na hapa nimejaribu kuwaletea baadhi ya majina yao ambao wamekuwa katika zama zake hizo na mmoja miongoni mwao kama Marhum 'Allamah Majilisi alipewa ruhusa ya kunakili yaani 'ijaza ya riwaya.

1. Muhammad bin Hassan Hurri 'Aamili aliyefariki mwaka 1104 na mwandishi wa kitabu kinachoitwa Wasa'il as-Shi'ah, nacho kimechapwa si chini ya Juzuu ishirini.

2. Mullah Muhsin Faiz Khashani aliyefariki 1091 na ambaye ni mwandishi wa Al-wafi Kitabu hiki kina Juzuu kumi na nne kinazungumzia juu ya Usul, Furu', Sunan, na Ahkam.

3. Mulam 'Abdullah bin Nurullah Bahrani mwandishi wa kitibu kiitwacho Al Awalim kitabu hiki kiko katika Juzuu mia moja.

4. Sheikh Muhammad Ridha bin Abdul Latif Tabrizi, aliyefariki mwaka 1158 na ni mwandishi wa kitabu kiitwacho As-Shifa'. Sote kwa pamoja tunaomba kwa Allah swt nguvu zetu na jitihada zetu hizi azikubalie. Iwapo kumetokezea au kumebakia kasoro zozote katika kutarjumu basi tunamwomba Allah swt atusamehe na ninawaomba Wanazuoni na wenye Ilimu wajaribu kusaidia turekebishe kwa sababu katika kukitarjumu kitabu hiki hapakuwapo na matayarisho kamili kuanzia awali.

Na kazi hii imefanywa kwa nia njema kwa matarajio kuwa itatumika kwa nia njema na itafaa kutukupeleka mahala pema. Inshallah. Naomba kazi yangu hii niiweke mbele kwa idhini ya Allah swt. Na kuiweka mbele ya Al Imam Muhammad Sahibuz-Zamaan(a.s) iwe ni kama zawadi kwake.

3

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA SABA

﴿جَعَلَ اللَّـهُ الْكَعْبَةَ الْبَيْتَ الْحَرَامَ قِيَامًا لِّلنَّاسِ وَالشَّهْرَ الْحَرَامَ وَالْهَدْيَ وَالْقَلَائِدَ ذَٰلِكَ لِتَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَأَنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ﴾

97.Mwenyezi Mungu amefanya Al-Kaaba nyumba tukufu, kuwa ni kisimamo cha watu na miezi mitukufu na wanyama wa kuchinja na vigwe; hayo ni kwa sababu mjue kuwa Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo mbinguni na yaliyomo ardhini na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.

﴿اعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ وَأَنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴾

98. Jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu na kwamba Mwenyezi Mungu ni mwingi wa maghufira, Mwingi wa kurehemu.

﴿مَّا عَلَى الرَّسُولِ إِلَّا الْبَلَاغُ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا تُبْدُونَ وَمَا تَكْتُمُونَ﴾

99.Haimlazimu Mtume ila kufikisha tu, na Mwenyezi Mungu anajua mnayo yadhihirisha na mnayoyaficha.

NYUMBA TAKATIFU

Aya 97-99

MAANA

Mwenyezi Mungu ameifanya Al-Kaaba, nyumba takatifu, kuwa ni kisimamo cha watu na miezi mitakatifu na wanyama wa kuchinja na vigwe.

Kisimamo cha watu; yaani mahali pa ibada na ibada za Hijja. Miezi mitakatifu ni ile minne Rajab, Dhul-qa'da, Dhul-Hijja na Muharram[5] Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameharamisha kupigana huko na katika miezi hiyo; ispokuwa kutetea nafsi au mali. Anasema:

﴿وَلَا تُقَاتِلُوهُمْ عِندَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ حَتَّىٰ يُقَاتِلُوكُمْ فِيهِ﴾

"Wala msipigane nao karibu na Msikiti Mtakatifu mpaka wakupigeni huko" (2:191) Na akasema tena:

﴿الشَّهْرُ الْحَرَامُ بِالشَّهْرِ الْحَرَامِ وَالْحُرُمَاتُ قِصَاصٌ فَمَنِ اعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ فَاعْتَدُوا عَلَيْهِ بِمِثْلِ مَا اعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ ﴾

"Mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu; na vitu vitakatifu vina kisasi. Basi wanaowachokoza, pia nanyi wachokozeni kwa kadiri walivyowachokoza" (2:194)

Mnyama wa kuchinja, ni wale wanaochinjwa Makka. Na kigwe ni ukambaa anaofungwa nao mnyama wa kuchinja kuwa ni alama ya kufahamisha kuwa ni wa Al-Kaaba ili asitaradhiwe na yeyote. Kwa hiyo kuunganisha vigwe kwa wanyama ni kuunganisha maalum katika ujumla.

Makusudio ya kutaja chinjo pamoja na Nyumba takatifu na miezi mitakatifu ni kwamba mnyama wa kuchinja inapasa awe salama yeye na anayemchunga, kwa sababu yeye anakusudia Haram tukufu.

Bali ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewapa amani ndege na wanyama walio katika haramu yake; isipokuwa mwewe, kipanga, kunguru, panya, nge, mbwa anayeuma watu na kila tunayemuona anaudhi.

Hayo ni kwa sababu mjue kuwa Mwenyezi Mungu anayajua yaliomo mbinguni na yaliyomo ardhini na kwamba Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila kitu.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kubainisha miko ya Al-Kaaba, miezi mitukufu na wanyama wa kuchinja, anaashiria kwamba hekima ya sharia hii ni kuwa watu wajue kwamba Mwenyezi Mungu anajua ufafanuzi wa mambo katika ardhi na katika mbingu; na ambayo yana masilahi kwa watu katika dini yao na dunia yao.

Kuna masilahi gani makubwa zaidi ya usalama wa maisha ya mtu na mali yake ijapokuwa ni kwa kipindi fulani. Tumeyaona mataifa makubwa yanayotwangana, wakati huu, yakiafikiana kuwa baadhi ya miji iwe ni maeneo maalumu ya amani, haijuzu kwa taifa linalopigana kuishirikisha katika vita wala kuweka vituo vya kijeshi katika ardhi hiyo au kupita wanajeshi wake.

Jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu na kwamba Mwenyezi Mungu ni mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) amekutanisha adhabu na rehema na maghufira ili mja awe anahofia adhabu yake na kutaraji rehema yake. Kwa sababu mja, akiwa na hofu atajiepusha na maasi na akiwa na matarajio atajitahidi katika twaa.

Razi anasema: "Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametaja kuwa yeye ni mkali wa kuadhibu, kisha akafuatishia kwa wasifu wa rehema na maghufira. Na huu ni uzinduzi juu ya undani kuwa kupatikana kiumbe ni kwa ajili ya rehema. Na kwa dhahiri ni kuwa mwisho hauwi ila kwa rehema" Hiyo ni kweli kabisa.

Haimlazimu Mtume ila kufikisha tu.

Hatakiwi jingine zaidi ya hilo, ambapo hapana udhuru baada ya kufikisha kwa anayepuuza na kupetuka mpaka. Ama hisabu na adhabu hiyo ni juu ya Mwenyezi Mungu pekee Yake. Mwenyezi Mungu anasema:

"Hakika ni juu yako kufikisha tu, na ni juu yetu hisabu." (13:40)

Mwenyezi Mungu anayajua mnayoyadhihirisha katika kauli na vitendo na mnayoyaficha. Haya ni makemeo kwa anayeinyamazia haki, na hasa yule anayeifanyia biashara kwa kujipanua na jina la dini na la nchi.

﴿قُل لَّا يَسْتَوِي الْخَبِيثُ وَالطَّيِّبُ وَلَوْ أَعْجَبَكَ كَثْرَةُ الْخَبِيثِ فَاتَّقُوا اللَّـهَ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ﴾

100.Sema: Hawi sawa habithi na mwema, hata ukikupendeza wingi wa habith, Basi mcheni Mwenyezi Mungu enyi wenye akili ili mpate kufaulu.

WINGI WA MWOVU

Aya 100

MAANA

Aya hii inarudufu Aya ile isemayo:

﴿لَا يَسْتَوِي أَصْحَابُ النَّارِ وَأَصْحَابُ الْجَنَّةِ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ هُمُ الْفَائِزُونَ﴾

"Hawawi sawa watu wa Motoni na watu wa Peponi, watu wa Peponi ndio wenye kufuzu" (59:20)

Wingi wa habithi ni anayoyamiliki miongoni mwa jaha na mali. Mwenye akili hawezi kumweka sawa habithi, na mwema hata kama ana mali nyingi na jaha kubwa. Kwa sababu jaha na mali hazimfanyi mwovu kuwa mwema; wala ufakiri na udhaifu haumfanyi mwema kuwa mwovu.

Mtu habith katika kipimo cha dini ni yule anayeasi hukumu za Mwenyezi Mungu katika kitabu chake na Sunna za Mtume wake. Na katika desturi ya watu ni yule wanayemhofia kwa shari yake na wasiyemwamini kwa jambo lolote na kutomsadiki katika kauli au vitendo vyake. Kimsingi ni kwamba mwenye sifa hizi, ni mbaya pia mbele ya Mwenyezi Mungu. Mtume wa Mwenyezi Mungu anasema:"Utukufu zaidi wa imani ni kuaminiwa na watu." Ama mtu mwema ni yule aliye kinyume cha mtu habithi katika sifa zake zote.

JE RIZIKI NI BAHATI AU MAJAALIWA?

Unaweza kuuliza : Ikiwa habithi anachukiwa na Mwenyezi Mungu na mwema anaridhiwa na Mwenyezi Mungu, kwa nini basi habithi anafaulu katika maisha haya na kuneemeshwa kwa jaha na utajiri, na mwema anaanguka na wala hapati matakwa yake?

Jibu : Maisha yana desturi na kanuni zinazokwenda nayo, na hazigeuki kwa hali yoyote ile. Kwa sababu hisia na uoni unakataa mkorogano katika ulimwengu. Desturi na kanuni hizi ni katika matengenezo ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kwa sababu yeye ni muumbaji wa asili na vilivyomo katika asili.

Kimsingi ni kuwa desturi ya kawaida ya tabia inakataa kuwa mali, afya na ilimu, vishuke tu kutoka mbinguni. Isipokuwa vitu hivi na mfano wake vinakuja kwa njia zake na sababu zake za kimaumbile. Elimu inatokana na kujifundisha, afya inatokana na lishe na kinga, na mali inatokana na kazi. Kwa hiyo mwenye kujifunza hujua, mwenye kujiepusha na visababishi vya maradhi husalimika, mwenye kujinyonga atakufa tu; awe mwema au mwovu, mumin au kafiri.

Kwa hiyo wema au imani hauoteshi ngano wala hauponeshi ugonjwa wala haumfanyi asiyejua kuwa mjuzi, Yote haya na mfano wake yanakwenda kwa desturi ya tabia na desturi ya tabia inakwenda kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu, hilo halina shaka.

Kwa sababu yeye ndiye aliyejaalia kujifundisha ndio sababu ya elimu na kujikinga ndio sababu ya afya na kupanda kuwa ndio sababu ya kuvuna. Yeye ni Muumba wa kila kitu na kwake yeye ni mwishilio wa kila jambo.

Ndiyo! kuchuma mali kuna njia nyingi, na milango mingi, nyingine Mwenyezi Mungu amezihalalisha na nyingine akaziharamisha. Mwenyezi Mungu (s.w.t) amehalalisha biashara, kilimo na viwanda; na akaharamisha riba, utapeli, rushwa, kupora na ulanguzi.

Mwenye kuchuma mali kwa njia ya halali hunasibishwa chumo lake kwake, kwa sababu yeye amejitahidi na kufanya bidii kuitafuta, na vilevile hunasabishwa kwa Mwenyezi Mungu. Kwa sababu yeye ndiye aliyepitisha sababu hizi na kuzihalalisha kwa kila azitakaye, awe mwema au mwovu.

Ama mwenye kuchuma mali kwa njia za haramu; kama vile riba na unyang'anyi; chumo lake litanasibishwa kwake na kwa hali aliyoitumia, wala halinasibishwi kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu ameharamisha njia hizi kwa mwema na mwovu.

Utasema : Haya yote ni kweli, lakini hayajibu swali wala hayatatui mushkeli. Tumewahi kumuona mwema na mwovu wote wakifuata njia za sharia za riziki, na kuzitafuta riziki kwa njia zile alizozihalalisha Mwenyezi Mungu na kuziharamisha, lakini pamoja na hayo, riziki inakuwa zaidi kwa mwovu aliye habith na kuwa dhiki kwa mwema, pengine huyu mwema ametoa juhudi maradufu ya yule mwovu, bali mara nyingine riziki humjia mwovu bila ya kutazamia wala maandalizi au juhudi, na inazuilika kumwendea mwema anapoitazamia na kuifanyia maandalizi na juhudi?

Jibu : Baadhi ya watu wanakimbilia kulifasiri hilo kwa kusema ni sadfa au bahati. Hakuna kinachofahamika kutokana na maelezo hayo zaidi ya kushindwa kwao kutoa tafsiri sahihi. Vinginevyo wasingelikimbilia kwenye maelezo ya kubahatisha tu.

Kwa hiyo sisi tunapinga Sadfa na bahati na tunaamini kwa imani ya mkato kwamba kuna chaguo la juu linajiingiza kwa sababu tusizozijua. kwa vile elimu katika masuala hayo na mfano wake, bado ni changa. Na kushindwa kwa elimu hakumaanishi kuwa kitu hakiko. Imani yetu hii inatiliwa mkazo na kauli zake Mwenyezi Mungu zifuatazo:

﴿وَاللَّـهُ فَضَّلَ بَعْضَكُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ فِي الرِّزْقِ﴾

"Na Mwenyezi Mungu amewafadhilisha baadhi yenu kuliko wengine katika riziki" (16:71)

﴿اللَّـهُ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ وَيَقْدِرُ﴾

"Mwenyezi Mungu hukunjua riziki kwa amtakaye na huidhikisha (13:26) Ay a hii imekuja kwa herufi zake katika 17:30, 28:82, 29:62, 30:37, 34: 36, 34: 39, 39:52, 42:12.

Kwa hiyo basi aliyesema au anayesema: Mwenyezi Mungu amemtajirisha fulani kwa kuwa yeye ni mwema basi atakuwa anazungumza mantiki ya Firaun na kupima kwa kipimo cha Shetani. Hekima yake Mwenyezi Mungu Mtukufu imetaka kumlipa mwema malipo mazuri na kumwadhibu mwovu katika akhera inayobakia sio katika hii dunia inayokwisha. Hii ni Nyumba ya matendo na ile ni Nyumba ya Hisabu. Zaidi ya haya ni kuwa wingi wa mali wa mwovu huenda ukawa ni balaa kwake na sababu ya kuadhibiwa kwake. Mwenyezi Mungu anasema:

﴿ذَرْهُمْ يَأْكُلُوا وَيَتَمَتَّعُوا وَيُلْهِهِمُ الْأَمَلُ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ﴾

"Waache wale na wafurahi na iwazuge tamaa, watakuja jua." (15:3)

﴿يَتَمَتَّعُونَ وَيَأْكُلُونَ كَمَا تَأْكُلُ الْأَنْعَامُ وَالنَّارُ مَثْوًى لَّهُمْ﴾

"Hujistarehesha na hula kama walivyo wanyama, na moto ndio makazi yao." (47:12)

Kwa ufupi ni kwamba riziki inategemea mambo mawili. Kuhangaika na matakwa ya Mwenyezi Mungu. Asiyehangaika ataishi omba omba; na mwenye kuhangaika Mwenyezi Mungu humruzuku kutokana na bidii yake, akitaka humpa nyingi na akitaka humpa chache.

Uhakika huu umo katika maumbile ya binadamu na anaufanya bila ya kujitambua. Mfanya biashara humwomba Mwenyezi Mungu (s.w.t) amruzuku kupata soko zuri la bidhaa zake na watu wazikubali. Mkulima anamwomba Mungu aiteremshie mimea yake mvua; wala hamuombi kumwoteshea mimea bila ya mvua.

Mimi hapa namwomba Mwenyezi Mungu ampe tawfiq mwanangu katika masomo yake na kufaulu mtihani; wala si mwombi akipe mawazo chuo kikuu kimpatie shahada bila ya kusoma na kufanya mtihani. Iko methali isemayo: Mgaagaa na upwa hali wali mkavu.

Pengine inawezekana mahangaiko yasiambulie kitu, lakini pamoja na hayo inatakikana kupanga mipango na kuongeza juhudi. Kwa sababu kuongeza juhudi, kutumia mipango, na kuvumilia tabu ni sababu ya matakwa ya kufaulu kutoka kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu.

﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَسْأَلُوا عَنْ أَشْيَاءَ إِن تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ وَإِن تَسْأَلُوا عَنْهَا حِينَ يُنَزَّلُ الْقُرْآنُ تُبْدَ لَكُمْ عَفَا اللَّـهُ عَنْهَا وَاللَّـهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ﴾

101.Enyi Mlioamini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatawachukiza. Na mnapoyauliza inapoteremshwa Qur'an mtabainishiwa. Mwenyezi Mungu ameyasamehe hayo. Na Mwenyezi Mungu ni mwingi wa maghufira Mpole.

﴿قَدْ سَأَلَهَا قَوْمٌ مِّن قَبْلِكُمْ ثُمَّ أَصْبَحُوا بِهَا كَافِرِينَ﴾

102.Waliyauliza watu waliokuwa kabla yenu kisha wakawa makafiri kwayo.

MSIULIZEULIZE MAMBO

Aya 101-102

MAANA

Enyi Mlioamini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatawachukiza.

Kauli yake Mwenyezi Mungu 'Msiulize' inaishiria kuwa baadhi ya Masahaba walikuwa waking'ang'ania kuuliza mambo yasiyokuwa na dharura yoyote kuyajua na huenda jibu lake likawaudhi waulizaji. Kuna riwaya isemayo kuwa mtu mmoja alimuuliza Mtume(s.a.w.w) : "Ni nani baba yangu?" Mtume akamwambia, "baba yako ni Fulani" Mwingine akauliza "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Baba yangu yuko wapi? Mtume akajibu: "Yuko motoni," ndipo ikashuka Aya hiyo.

Riwaya nyingine inasema kuwa Mtume alisema: "Mwenyezi Mungu amewafaradhishia kuhiji, basi hijini." Wakauliza: "Kila mwaka ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?" Mtume akanyamaza. Wakarudia kuuliza, akasema La; lau ningelisema naam, ingelikuwa wajib." Ndipo ikashuku Aya hii. Riwaya hii ndiyo yenye nguvu kuliko ile ya kwanza.

Na mnapoyauliza inapoteremshwa Qur'an mtabainishiwa.

Yaani msijikalifishe kuuliza mambo ila baada ya kuteremshwa Qur'an. Mtakapoanza kuuliza Mtume(s.a.w.w) atawadhirishia mliyokuwa mkiyauliza.

Kwa hali hii, inatubainikia kuwa riwaya ya Hija ndiyo yenye nguvu katika sababu ya kushuka Aya, kuliko riwaya ya kuuliza mababa na wahenga wa Masahaba. Kwa sababu Qur'an inaanza kuleta itikadi na sharia na wala sio kuanzia kwa mababa na mababu wa Masahaba. Katika Hadith imeelezwa:"Hakika Mwenyezi Mungu ameweka mipaka msiikiuke; amewafaradhishia faradhi msizipoteze; ameharamishia vitu msivifanye; na ameacha vitu vingine si kwa kusahau, lakini ni kwa kuwahurumia, basi vikubalini wala msivifanyie utafiti".

Mwenyezi Mungu amesamehe hayo

Yaani maswali yenu yaliyotangulia, kwa hiyo msiyarudie. Imesemekana kuwa maana yake ni amezuia kutaja vitu mlivyoviulizia, basi nanyi jizuieni wala msijikalifu kuviulizia. Tafsir zote mbili zina uwezekano hazikataliwi na dhahiri ya tamko.

Na Mwenyezi Mungu ni mwingi wa maghufira, Mpole.

Humsamehe mkosaji akikosea tena.

Waliyauliza watu waliokuwa kabla yenu kisha wakawa makafiri kwayo.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuwakataza kuuliza mambo wasiyokuwa na haja nayo, anawapigia mfano wa watu waliokuwa kabla yao, waliuliza wakang'ang'ania kuuliza. Walipobainishiwa na Mwenyezi Mungu walichukia wakaasi na wakastahiki adhabu. Lau wangeliacha kuuliza ingelikuwa bora kwao.

Wafasiri wamerefusha maneno katika kubainisha makusudio ya watu waliouliza, kisha wakawa makafiri kwa sababu ya kuuliza, lakini Aya haikubainisha. Pamoja na hivyo, tunaweza kusema kuwa watu waliouliza wakawa makafiri kwa sababu ya kuuliza ni wana wa Israil, kwa sababu ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu akiwasimulia:

﴿فَقَدْ سَأَلُوا مُوسَىٰ أَكْبَرَ مِن ذَٰلِكَ فَقَالُوا أَرِنَا اللَّـهَ جَهْرَةً ﴾

"Hakika walimtaka Musa makubwa kuliko hayo, Walisema: Tuonyeshe Mwenyezi Mungu waziwazi" (4:153)

﴿مَا جَعَلَ اللَّـهُ مِن بَحِيرَةٍ وَلَا سَائِبَةٍ وَلَا وَصِيلَةٍ وَلَا حَامٍ وَلَـٰكِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ وَأَكْثَرُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ﴾

103.Mwenyezi Mungu hakujaalia Bahira wala Saiba wala Waswila wala Hami; Lakini waliokufuru wanamzulia Mwenyezi Mungu uwongo na wengi wao hawafahamu.

﴿وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا إِلَىٰ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَإِلَى الرَّسُولِ قَالُوا حَسْبُنَا مَا وَجَدْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا أَوَلَوْ كَانَ آبَاؤُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ شَيْئًا وَلَا يَهْتَدُونَ﴾

104.Wakiambiwa njooni katika yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu na kwa Mtume, husema: Yanatutosha yale tuliyowakuta nayo babu zetu. Je hata kama baba zao walikuwa hawajui kitu wala hawakuongoka?

﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَيْكُمْ أَنفُسَكُمْ لَا يَضُرُّكُم مَّن ضَلَّ إِذَا اهْتَدَيْتُمْ إِلَى اللَّـهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴾

105.Enyi mlioamini! Jiangalie nafsi zenu. Hawawadhuru waliopotea ikiwa mmeongoka. Marejeo yenu nyote ni kwa Mwenyezi Mungu. Atawaambia yale mliyokuwa mkiyatenda.

HAKUNA BAHIRAWALA SAIBA

Aya 103-105

MAANA

Mwenyezi Mungu hakujaalia Bahira wala Saiba wala Waswila wala Hami.

Bahira, ni ngamia aliyetobolewa masikio, watu wa wakati wa Jahilia walikuwa wakifanya hivyo, ikiwa ngamia atazaa mimba kumi ; na inasemekana ni mimba tano. Wanamwacha bila ya kutumiwa na mtu yoyote. Saiba ni ngamia waliyemwekea nadhiri kwa waungu, na wana mwacha akijilisha mwenyewe popote bila ya kufungwa wala kuwa na mchungaji sawa na Bahira.

Wasila ni mbuzi anayezaa mtoto wa kiume na wa kike pamoja. Desturi yao ilikuwa kama akizaa mume wanamfanya ni wa waungu na akizaa mke ni wao. Iwapo atazaa mume na mke pamoja, hawamchinji mume wakisema kuwa ameunganishwa na dada yake. Hami ni dume aliyezalisha mimba kumi, wanamwacha hazuiliwi na maji wala malisho, wakisema ameuhami mgongo wake.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) anabainisha kwamba yote hayo hayamo katika dini, na kwamba dume, jike na mbuzi, vyovyote wanavyofanyiwa, wanabakia na uhalali wake kama walivyokuwa mwanzo na wala hawaharamishwi na porojo hizo.

Lakini waliokufuru wanamzulia Mwenyezi Mungu uwongo na wengi wao hawafahamu.

Watu wa kijahilia walikuwa wakikubali kuweko kwa muumba kwa dalili kwamba wao wamenasibishia uharamu wa Hami, Saiba, Bahira na Waswila, lakini pamoja na hayo Mwenyezi Mungu amewanasibishia ukafiri.

Kwa sababu wao wamemnasibishia uharamu kwa uwongo na uzushi. Kwa hiyo, basi kila anayemnasibishia Mwenyezi Mungu na yasiyokuwa na dalili ya Kitab wala Hadith ya Mtume wake basi huyo ni kafir kwa sharti ya kutegemea kumnasibishia Mungu, huku akijua kutokuwepo dalili.

Hii, kwa lugha ya watu wa sharia, huitwa Bid'a (uzushi). Kuna Hadithi isemayo: "Kila bid'a ni upotevu na kila upotevu ni motoni".

Ilivyo ni kuwa kufaradhia huko kuko mbali na hali halisi ilivyo, Ni nani anayemnasibishia hukumu Mwenyezi Mungu huku akijua kuwa hakuna dalili. Pengine anaweza akadhani ni dalili, lakini kumbe sio dalili.

Wakiambiwa njooni katika yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu na kwa Mtume, husema: "Yanatutosha yale tuliyowakuta nayo babu zetu. Je hata kama babu zao walikuwa hawajui kitu wala hawakuongoka?

Razi anasema: "Maana yanajulikana, nayo ni jibu la kuwapinga watu wa Taqlid (kufuata)". Tumezungumzia kuhusu Taqlid katika Juz.2 (2:170)

Enyi mlioamini! Jiangalieni nafsi zenu, Hawawadhuru waliopotea ikiwa mmeongoka, Marejeo yenu nyote ni kwa Mwenyezi Mungu.

Razi ametaja njia nane za kufasiri Aya hii. Mmoja wa wafasiri wapya ameandika kurasa 33. Lililowafanya wawili hawa na wengineo kurefusha mambo hivi ni kuwa kuamrisha mema ni wajibu na dhahiri ya Aya inafahamisha kutokuwa wajib na kwamba ni juu ya mtu kujishughulikia mwenyewe. Ama wengine wana majukumu yao juu ya nafsi zao wala si wajibu kwa yoyote kuiongoza au kuikanya nafsi ya mwingine.

Ilivyo tafsir ya Aya hii ni kwamba, ni juu ya mtu kuamrisha mema. Kuamrisha kwake kukinufaisha basi hayo ndiyo yanayotakikana. Vinginevyo basi atakuwa ametekeleza lile aliloamrishwa wala hautamdhuru upotevu wa aliyepotea.

Mwenye jukumu baada ya kuamrisha ni yule aliyepotea na wala sio mwamrishaji. Tafsir hii imetilia mkazo wajibu wa kuamrisha mema na sio kupinga.

5

6

7

8

9

10

11