HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.0%

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s. Mwandishi:
Kundi: VITABU VYA HADITHI

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.

Mwandishi: AMIRALY M.H.DATOO
Kundi:

Matembeleo: 10237
Pakua: 1320

Maelezo zaidi:

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 13 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 10237 / Pakua: 1320
Kiwango Kiwango Kiwango
HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.

Mwandishi:
Swahili

2

HADITH ZA MTUME (s.a.w.w) NA MA-IMAMU (a.s)

UTAMBULISHO WA MA'SUMIIN (a.s) KATIKA AHADITH: KUNIYYAT NA ALQAAB

Mara nyingi tunaposoma vitabu vya riwaya tunapata majina mengine yaliyotofauti na majina ya asili. Hivyo tunaona katika Ahadith kuwa Ma'asumiin(a.s) wanatambulishwa kwa majina yanayoitwa Kuniyyat au Iaqab, kwa mfano: Qala Abul Hasan ( yaani amesema Abul Hasan ) au Qala Abu 'Abdillah (yaani amesema Abu 'Abdillah) n.k. na hapo ndipo tunakuwa hatuelewi ni Ma'sum(a.s) yupi ambaye amesema hayo. Waarabu wanayo desturi ya kuwaita wazee wao si kwa majina yao bali kwa majina mengineyo yaan Kuniyyat au Alqaab. Hivyo inatubidi tupate ufafanuzi zaidi kuhusu majina hayo yanayotumiwa kwa ajili ya Ma'sumiin(a.s) zaidi ya mara moja. Na hivyo Maulamaa wetu wametuelewesha ilivyo sahihi kabisa. Wakati wa kujaribu kufafanua juu ya Laqab au Kuniyyat kunatiliwa maanani kuhusu maneno na maana ya Hadith, zama za kusemwa na habari za wale wanaoziripoti, ndipo hapo panapoweza kutambuliwa kwa Alqaab au Kuniyyat katika Hadith hiyo kunatambulishwa Ma'sumiin(a.s) yupi. Hivyo kuelezea hayo na mengineyo, maelezo yafuatayo yatasaidia kutoa mwanga katika swala hili kwa ujumla:

1.ABUL QASIM

Kuniyyat hii inatumika kwa ajili ya Mtume Muhammad(s.a.w.w) na Imam al-Mahdi(a.s) Iwapo kutaripotiwa riwaya kuwa Abul Qasim tu, basi ijulikane kuwa ni Imam al-Mahdi(a.f) .

2.ABU MUHAMMAD

Zipo Hadith chache mno zinazojulikana kuwa Imam Hasan(a.s) Hata hivyo hiyo ndiyo Kuniyyat yake.

3.ABU 'ABDILLAH

Kuniyyat hii inatumika kwa ajili ya Imam Hussein(a.s) na vile vile inatumika kwa ajili ya Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) .

4.ABUL HASAN

Kuniyyat hii inatumika kwa ajili ya Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) , Imam Musa ibn Ja'afer(a.s) , Imam Ali ibn Musa al-Ridha(a.s) na Imam Ali an-Naqi(a.s) Iwapo kutakuwapo na Abul Hasan tu katika riwaya, basi kutatambuliwa Imam Musa ibn Ja'afer(a.s) Na iwapo kutaandikwa Abul Hasan Thani (Abul Hasn wa pili) basi kutakuwa kumefanywa ishara ka Imam Ali ar-Ridha(a.s) na pale panapoandikwa Abul Hasan Thalith (Abul Hasan wa tatu) basi tujue kuwa kunamaanishwa Imam Ali an-Naqi(a.s)

5.ABU MUHAMMAD

Kuniyyat hii inatumika kwa ajili ya Imam Hasan(a.s) , Imam Zaynul Aabediin(a.s) na Imam Hasan al-'Askari(a.s) lakini iwapo kutaandikwa riwaya kwa Abu Muhammad tu tutatambua kuwa riwaya hiyo ni kutoka Imam Hasan al-'Askari kwa sababu riwaya za Imam Zaynul Aabediin(a.s) zinatajwa kwa jina lake tu, bali zipo riwaya chache mno tu kwa Kuniyyat yake.

6.ABU IBRAHIM

Katika Hadith Kuniyyat hii inatumika hasa kwa ajili ya Imam Musa ibn Ja'afer(a.s) .

7.ABU IS-HAQ

Kuniyyat hii inatumika kwa kumtambulisha Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) .

8.ABU JA'AFER

Kuniyyat hii inatumika kwa ajili ya Imam Muhammad al-Baquir(a.s) na Imam Muhammad Taqi(a.s) Lakini iwapo kutakuwapo na Abu Ja'afer tu au Abu Ja'afer Awwal, (Abu Ja'afer wa kwanza) basi ijulikane kunamaanishwa kwa Imam Muhhammad al-Baquir(a.s) Na iwapo kutaandikwa Abu Ja'afer Thani (Abu Ja'afer wa pili) basi kutambuliwe kuwa ni Imam Jawad(a.s) Kwa mara chache mno Abul Hasan inatumika kwa ajili ya Imam Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) lakini mahala pengi mno kunatumika Kuniyyat yake mahsusi ya Abul Hassanain.

ALQAAB

Wakati pale utakapoona riwaya zinanakiliwa kutoka kwa 'Aalim, Sheikh Faqih au 'Abdi Salih, basi mutambue kuwa kunamaanishwa kwa Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) Vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) anajulikana kwa alqaab zifuatazo: Abu 'Abdillah, Faqih na 'Aalim. 'Allamah Majlisi a.r. anasema kuwa mahala pengi mno katika riwaya kunapotajwa Faqih basi kunamaanishwa kwa Imam 'Ali an-Naqi(a.s) na kwa mara chache mno kunatumika kwa ajili ya Imam Hasan al-'Askari(a.s) na Imam al-Mahdi(a.s) Naqi, Mazii, Sahibul 'Askar na Hajjul kunamaanisha Imam Hasna al-'Askari(a.s) Sahib na Sahibuddaar zinatukika makhsusi kwa ajili ya Imam al-Mahdi(a.s) Lakini Sahibun Nahiyah inapokuja, basi kwa mara nyingine hutumika kwa ajili ya Imam 'Ali an-Naqi(a.s) au Imam Hasan al-'Askari(a.s) 'Allamah Majlisi anasema kuwa mara nyingine katika Ahadith hutumika maneno Ghaib, 'Alil au Gharim basi inatubidi kuelewa Imam al-Mahdi(a.s) .

Iwapo kutakuwapo bi ahadihima (kwa mojawapo) basi itatubidi tuelewe kuwa ni ishara kwa Imam Muammad al-Baquir(a.s) au Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s). Na iwapo tutakuwa bi 'Askariyyen, tuelewe kuwa ni Imam Alian-Naqi(a.s) . na Imam Hasan al-'Askari(a.s) . Vile vile iwapo tutaona bi Kadhimain basi kunamaanishwa Imam Musa al-Kadhim(a.s) . na Imam Mahammad at-Taqi(a.s) . Kwa mukhtasari, zipo alqaab nyingi ambazo zinajulikana kimakhsusi kwa ajili ya Ma'sumiin(a.s) . kama vile Amir al-Muuminiin, Mujtaba Shahid, Zaynul Aabediin, Baquir, Sadiq, Kadhim, Ridha, Jawad, Hadi, 'Askari, na Sahibuz Zamaan (salaam ziwe juu yao wote).

MWENYE KURIPOTI AHADITH AWEJE?

Kwa hakika somo hili ni kubwa na lenye kwenda kwa undani zaidi, lakini kwa ajili ya wasomaji, tunawaleteeni habari hizi kwa kifupi ili kuwafaidisha. Katika lugha ya Kiarabu, mtu anayeripoti riwaya huitwa Rawi na sifa zake zimeelezwa na kubainishwa na Ma'ulamaa walio mabingwa wa ilimu ya Ahadith:

1. Rawi lazima awe mtu mwenye akili na fahamu timamu. Riwaya zozote zitakazotolewa katika hali ya kuwehuka au kurukwa na fahamu, basi hazitathaminika au kukubalika.

2. Ni lazima Rawi awe amebaleghe na Mukallaf, yaani shariah za Dini ziwe zimeshakwisha kuwa faradhi juu yake. Hapa inawajumuisha vijana na watoto na wale wote ambao bado hawajabaleghe lakini wanaweza kutofautisha baina ya wema na ubaya. Aina hii ya vijana hao huitwa Mumayyiz na hivyo riwaya zao zinapotimika masharti mengineyo, huweza kukubalika na kusadikika.

3. Ni lazima Rawi awe Mwislamu. Riwaya za mtu asiye Mwislamu haziwezi kuaminiwa au kusadikiwa.

4. Rawi lazima awe ni Mwislamu mfuasi wa Madhehebu ya Sh'iah Ithna-Asheria. Lakini iwapo kutakuwa na riwaya kutokea Mwislamu mfuasi wa Madhehebu mengine, basi kwa uzito wa dalili zinginezo na kufanya uchunguzi iwapo huyo Rawi ni mtu aaminiwaye katika historia.

5. Uadilifu wa Rawi pia ni sharti mojawapo, yaani asiwe akifanya madhambi makuu (ghunah-i-Kabira) na wala asiwe akirudiarudia madhambi madogo madogo (ghunah-i-saghirah).

Sheikh Tusi a.r. ametilia mkazo swala hili kwa kuelezea kuwa kuna tofauti katika uadilifu wa Rawi na mtoa ushahidi. Iwapo Rawi ni fasiki na iwapo itathibitika kuwa yeye katika riwaya yake na habari zake ni mkweli bila ya udanganyifu, basi riwaya yake inaweza kufuatwa.

6. Rawi asiwe msahaulivu, bali awe ni mtu mwenye kukumbuka vyema na udhibiti wake, (yaani haimaanishi kuwa Rawi asiwe akisahau kama mtu wa kawaida) yaani Rawi anapotaka kuelezea riwaya au Hadith, basi asiwe na mushkeli wa kuikumbuka.

AINA ZA AHADITH

Sayyid Ibn Taus (a.r) (amefariki 673 Hijriyyah) na 'Allamaha Hilli (a.r) (amefariki 726 Hijriyyah) kwa juhudi zao, wao wamefanikiwa kutuletea kanuni nne kuu zijulikanazo usul-i-'arbi'ah ambazo ni kama zifuatazo:

1.HADITH SAHIH : Rawi wote lazima wawe waaminifu na Shia Ithna-Asheri na riwaya hizo ziwe zikifika hadi kwa Ma'sumiin(a.s) .

2.HADITH HASAN : Riwaya ambazo Rawi wake ni Mashiah na ambapo hapakufanywa uchunguzi wowote juu ya uadilifu wao.

Hadith kama hizo zinajulikana kama hasan kwa sababu Rawi amepokelewa kwa misingi ya husn-dhan yaani kwa dhana njema.

3.MUWATH-THAQ : Yaani Rawi wote wawe wakiaminiwa lakini miongoni mwao si wote ambao ni Mashiah.

4.DHAIF : Ni riwaya ambazo hazina sifa hata mojawapo za hapo juu. Tanbih lipo jambo moja la kuzingatia, kuwa Ma'ulamaa wanakubaliana na Hadith zilizo Sahih, Hasan na Muwath-thiq. Ama kuhusu Hadith zilizo dhaif ni kwamba iwapo atayamkinika kuwa Rawi hao si watu wa kutegemewa lakini maelezo na maana yake ni sawa na maana ile ya Ma'sumiin(a.s) . na katika sura hii, itaweza kukubalika, na wakati Ma'ulamaa wanaozisimulia basi nia yao huwa juu ya Hadith, bali huwa ni kutoa ushahidi tu.

HADITH ZILIZOTOLEWA

Kwa mujibu wa kanuni hizi nne, mmefahamu kuwa Hadith inapoangukia kuwa dhaifu haimaanishi kuwa ni Hadith ya uongo, yenye mfululizo dhaifu, na kwa dalili zinginezo na kwa nyenzo zinginezo inaweza kuthibitika kuwa Hadith hiyo inaweza kukubalika, Lakini inapokuwa imekosewa kabisa basi huitwa Kidhb (uongo) au Iftira' (tuhuma). Yaani utaratibu uliotumiwa wa kuwanasibisha Ma'sumiin(a.s) . haupo wenye ukweli, bali tunaweza kusema kuwa ni tuhuma. Hadith hizo ni uzushi mtupu. Katika historia ya ilimu ya Hadith, utaratibu huu mmoja ni tatizo kubwa mno kuling'amua iwapo Hadith hii ni uzushi au la.

Sayyid Murtadha 'Alamal Hudaa a.r. anasema: "Zipo baadhi ya sehemu za Hadith katika Mashia na Waislamu wote kwa ujumla ambazo zimejazwa makosa na uzushi ambazo zinatufanya kuzichukulia kuwa ni Hadith za uongo. Katika Hadith hizo kuna mambo fulanifulani ambazo kwa hakika si rahisi kukubalika kiakili na ni pingamizi mtupu. Kwa mfano imani juu ya jabr (ushurutisho) yaani mwanadamu ameshurutishwa na Allah swt katika matendo ya madhambi na uasi, au siku ya Qiyamah Allah swt ataonekana n.k. na hivyo inamaanisha kuwa kunahitajika uchuguzi na utafiti mkubwa katika kuthibitisha ukweli wa usahihi wa Hadith kama hizo." Imam Ali(a.s) . amesema: "Mtume Muhammad(s.a.w.w) alisema: "Enyi watu, kumekithiri mno kuninasibishia mambo ya uzushi, hivyo mutambue kuwa mtu yeyote kwa makusudi ataninasabisha na uongo au uzushi wowote, basi hakuna mahala pale pengine isipokuwa ni Jahannam tu. "

Katika zama hizi ni lazima kufahamu 'Ilmul Hadith na Rijal yaani kujua habari za wale wenye kuleta riwaya. Kazi hii ni ya wale mabingwa katika fani hii na wala si ya wale wenye ilimu kidogo ambao wamejua Kiajemi na Kiarabu kidogo hivyo wakaanza kuwapotosha watu. Sasa tuangalie ni kwa sababu gani kumetokezea haja ya kutaka kuzichuja Ahadith na tuwaangalie watu mbalimbali ambao wamefanya juhudi za kuingiza uongo na uzushi na tuhuma katika Ahadith.

(1). Baada ya kifo cha Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kulizuka mgogoro kuhusu ukhalifa ambapo kulitokezea makundi mawili. Kundi moja likidai kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alikuwa amekwisha elezea ni nani atakaye kuwa Khalifa baada yake na kundi la pili likaanza kuzua Hadith kuwa swala hilo liachiwe 'ummah wa Kiislamu kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alisema kuwa ukhalifa baada yake hautatokana na Bani Hashim (uzushi mtupu).

(2). Wakati Uthman alipouawa, basi Ma'uwiya bin abi Sufiyan kwa hila zake alitupa tuhuma za mauaji yalilengwa kwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . Hapo kuliibuka Hadith za kuzuliwa katika kuwatukuza Bani Umayyah, umadhulumu wa Uthman na hukumu juu ya Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . katika mauaji ya Uthman. Si hayo tu, bali Hadith zile zilizokuwa zikielezea fadhila za Imam Ali(a.s) . pia zilianza kubadilishwa na kupotoshwa. Mfano, ipo ayah ya Qur'an tukufu: 'wa minanaasi manyashrii nafsahubtighaa mardhatillah' Aya hii inatoa shuhuda ya tukio lililotokea katika usiku wa Hijrah ambapo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . alijitolea nafsi yake kwa ajili ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Kwa amri za Mu'awiyah, Hadith hii ikageuzwa kuwa imeteremka kwa ajili ya Ibn Muljim kwa sababu yeye alikuwa ameiweka nafsi yake hatarini katika kumwua Imam Ali(a.s) .

(3). Makhariji walizua Hadith chungumzima kuhusu akida zao na Waislamu kwa ujumla pia walizizua Hadith nyingi mno katika upinzani wao

(4). Ma'ulamaa wa Kiislamu walianza kuzua na kutumia hizo Ahadith katika kuzieleza na kuziendeleza fikra, nadhiri na akida zao. Mu'tazila, Tasawwuf, Gulat na Ash-Ari na wengineo wote wakaanza kuzua Hadith katika kueneza imani zao. Iwapo utabahatika kukisoma kitabu kiitwacho Ihyaul Ulumiddiin basi ndipo utakapokuja kujua hali halisi ya uovu huu wa kuzua Ahadith za kiuongo dhidi ya Ma'sumiin(a.s) . ambazo kwa hakika hazikubaliki kuwa zimesemwa nao. Kwa kutoa mfano, tunawaleteeni chache ili muweze kuziangalia:

(a). Ahmad bin Mansur anasema kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Baina mikono miwili ya Allah swt kuna maandiko fulani ambamo kuna majina ya wale watu ambao wanaitikadi kuhusu kuwapo kwa uso na kuonekana kwa Allah swt siku ya Qiyama. Na Malaika wanaona fakhari kwa majina hayo!

(b). Mamun bin Ahmad Harwi anamnakili Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akisema:

"Kuna mtu mmoja katika 'Ummah wangu ambaye ni hatari hata kuliko Shaytani, na jina lake ni Muhammad bin Idris (yaani Imam Sahfi'i) na vile vile kuna mtu mwingine ambaye yuko sawa na nuru kwa 'Ummah wangu, na jina lake ni Abu Hanifa."

Tanbihi : Mwandishi wa Lisanul Mizaan anaandika kuwa sababu kubwa ya kuizua Hadith hii ni kwamba huko Khurasan, wafuasi wa Imam Shafi'I walikuwa wengi.

(c). Ahmad bin Nasr anasema kuwa siku moja alimwota Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) katika ndoto akimwambia; "Itakuwa wema kwako kumtii Shafi'i kwani anatokana nami na Allah swt yu radhi naye"

(d). Kwa hakika jambo lakusikitisha mno ni kwamba hawa wataalamu wa kuzua (wazushi) ni watu ambao wameilimika vyema katika masomo ya Qur'an na Hadith. Mafunzo ya Qur'an hayakuwa yenye maana kwao bali wametilia mkazo masilahi na ulafi wa dunia hii.

Ayatullah al-Khui r.a. anaandika katika kitabu chake Al-Bayan fi tafsiril Qur'an, Uk. 28 kuwa kuna rundo kubwa kabisa la riwaya za uongo na zilizozuliwa, ambamo hawa wazushi wamechukua tahadhari kuwa kusije kukapunguzwa fadhila za Qur'an, basi wamezua Hadith zao binafsi; na wamezirembesha kwa fadhila mbalimbali kiasi kwamba zinapopimwa kwa kauli za Allah swt zinajulikana kuwa ni za uongo mtupu. Mfano Abu Ismah Faraj bin Abi Maryam al-Maruzi, Muhammad bin Akasha al-Kirmani, Ahmad bin Abdillah Juibarri na wengineo wengi. Wakati mtu mmoja alipomwuliza Abu Ismah kuwa amezitoa wapi Hadith chungu mzima kutokea kwa Ikramah na Ibn 'Abbas kuhusu fadhila za Sura moja moja za Qur'an tukufu ? Alianza kusema: "Mimi niliona kuwa watu wameanza kuipa mgongo hiyo Qur'an na badala yake wanajishughulisha mno na fiqhi ya Abu Hanifa, watu wamejishughulisha kuisoma Maghazi ya Muhammad bin Is-Haq, basi mimi nimezusha Hadith hizo juu ya Qur'an kwa kutaka furaha ya Allah swt .!

(e). Wakati kulikuwapo utawala wa Bani 'Abbas, basi Ma'ulamaa wenye tamaa ya dunia walizizusha Ahadith nyingi mno katika kuelezea fadhila za watawala hao. Katika Tarikhul Khulafa anaandika as-Sayyuti: "Mtume Muhammad(s.a.w.w) amesema kuwa yeye alipoona kuwa Bani Marwan wanachezea Mimbar yangu, basi hapo mimi nilisikitishwa mno. Na hapo baadaye nikaona Bani 'Abbas pia wanachezea, na kwa hayo mimi nilifurahishwa mno."

Abu Hurairah ananakiliwa riwaya moja kuwa siku moja Mtume Muhammad(s.a.w.w) alitoka nje, na hapo alikutana na Baba mkubwa 'Abbas, na alimwambia: "Ewe Abul Fadhl! Je nikupe habari njema? 'Abbas alisema: "Naam, Ewe Mtume wa Allah swt!" Ndipo Mtume Muhammad(s.a.w.w) aliposema: "Allah swt ameitengeneza swala hili (yaani Dini hii ya Islam) kwangu na kuishia kwa 'Ummah wangu." Na akaendelea kusema: "Wakati kizazi chako kitakapoishi Iraq, watakuwa na usukani huu wa Islam kwa muda mpaka atakapodhihiri Mtume Isa (a.s) . na kumkabidhi."

Tanbihi : Ni jambo la kushangaza mno kuwa huyu huyu as-Suyuti ameandika kitabu kimoja juu ya masuala ya uzushi kiitwacho Al-Lulil mansukh (Lulu bandia) na amewatahadharisha Waislamu kujitahadharisha na Hadith kama hizo za uzushi, pamoja na hayo yeye mwenyewe amenakili riwaya nyingi mno zilizo bandia na Ahadith zilizo zuliwa na hivyo ameshiriki kikamilifu katika kuifikishia Islam jeraha kubwa.

(f). Baadhi ya makafiri na maadui wa Islamu wamekuwa wakiishi miongoni mwa Waislamu na kujihusisha katka harakati za kueneza sumu hii miongoni mwa Waislamu kwa hila na njama mbalimbali. Wao ili kutaka kutimiza mikakati yao hiyo ya kueneza upotofu, wamekuwa wakijishughulisha na uzushi wa Ahadith za Mtume Muhammad(s.a.w.w) na Ma'sumiin(a.s) . na walikuwa wakizileta mbele ya watu. Ibn Abil Awjah amekiri mwenyewe kuwa yeye ameingiza kiasi cha Ahadith zipatazo elfu nne zilizozuliwa miongoni mwa Ahadith zilizo za kweli.

(g). Katika kipindi cha mwanzo cha Islam, watu walikuwa na shauku kubwa ya kusikiliza visa na masimulizi mbalimbali na katika hali hii kuliibuka wasimulizi wengi wa masimulizi kama hayo na hivyo wao walikuwa wakifanya kila jitihada za kukusanya habari na porojo za kila aina na walikuwa wakiongezea chumvi na pilipili ili kwamba mazungumzo yao yalete ladha nzuri na kuwavutia watu. Matokeo yakawa ni kwamba Mayahudi walikuwa wamezusha visa na hadithi nyingi kuhusu mitume yao, hivyo mazushi hayo yakapata soko kubwa miongoni mwa Waislamu, na rundo kubwa hili linajulikana kwa jina la Israiliyyaat Hadith zilizozushwa juu ya Mitume(a.s) . inapatikana katika Tarikhul Ambiya' na hususan katika tafisiri za Ayah ambazo zinazungumzia habari za Mitume(a.s) .

Ibn Jawzi anaandika kuwa Imam Ahmad bin Hambal na Yahya bin Mu'in walikuwa wakisali Msikitini na wasimuliaji wakaja wakatandika mikeka yao tayari kuanza masimulizi yao mbele ya halaiki kubwa ya mashabeki wao. Wasimulizi wakiendelea na masimulizi yao, wakasema: "Mimi binafsi nimemsikia Ahmad bin Hambal na Yahya bin Mu'in kuwa wao wamewasikia Rawi fulani fulani kuwa Mtume Muhammad(s.a.w.w) amesema: "Mtu yeyote atakaye sema La ilaha Illallaah basi Allah swt atamwumba ndege mmoja ambaye mdomo wake utakuwa wa dhahabu na macho ya marjaan" Hivyo wao walizielezea habari za ndege huyo, na kama tukianza kuziandika tutaandika kurasa ishirini zinginezo. Kwa hakika watu walipoyasikia haya walianza kuyumba na kwa kutoa shukurani zao walianza kuwatupia mapesa hao wasimulizi, nao walibakia kimya kwa muda zaidi kidogo ili waendelee kupata zawadi zaidi, na hapo ndipo Yahya bin Mu'in alipojitokeza na kumwita aje mbele yake. Msimulizi alikuja mbio mbio hapo mbele kwa kutarajia kupata zawadi nono, ndipo Yahya alipomwuliza: "Je habari zote hizi zisizo na miguu umeyatoa wapi?" Akajibu: "Nimemsikia Yahya bin Mu'in na Ahmad bin Hambal."

Yahya na Ahmad bin Hambal walishikwa na bumbuwazi na walibakia wakitazamana, na hapo ndipo Yahya kwa hasira alimgeukia msimulizi na kumwambia: "Je hauoni aibu? Wewe umethubutuje kuzusha uongo dhidi yetu ilhali tukiwa mbele yako ? Jina langu ni Yahya bin Mu'in na huyu ndiye Ahmad bin Hambal." Yule msimulizi alianza kusema: "Mimi daima nimekuwa nikisikia kuwa Yahya bin Mu'in ni mtu mpumbavu na mjinga kabisa, na kwa hakika nimepata uthibitisho huo leo hii, kwa hakika ni ajabu kubwa !. Je dunia hii nzima ina Yahya bin Mu'in na Ahmad bin Hambal nyie wawili tu na wala haina wengine? Kwa kusema ukweli mimi nimewanakili riwaya mbalimbali Yahya bin Mu'in sabini na Ahmad bin Hanbal sabini." Kwa kusema hayo msimulizi alijiondokea zake.

(h). Kulizuliwa Ahadith nyingi mno katika kutukuza makabila na Miji ya Kiislamu. Tazameni mfano mmoja. Imeripotiwa kuwa al-Imam ar-Ridha(a.s) . amesema kuwa Mji mtukufu wa Qum umeitwa hivyo kwa sababu hapo ndipo Safina ya Mtume Nuh(a.s) . iliposimama baada ya kuisha kwa tufani. (Katika lugha ya Kiarabu neno Qum linamaanisha kusimama).

(i). Katika zama za Makhalifa watu walikuwa wakijishughulisha mno katika kuzusha Hadith za uongo au kuzigeuza maana ili waweze kupata zawadi, hongo au kutukuzwa miongoni mwa watu. Katika zama za Mahdi 'Abbasi ambaye alikuwa khalifa wa Bani 'Abbas, aliijiwa na mtu mmoja aitwaye Ghiyas Bin Ibrahim ambaye aliwakuta njiwa wengi mno katika kasri ya khalifa, na kwa hayo alisema: "Ipo riwaya kutokea Mtume Muhammad(s.a.w.w) kuwa imeruhusiwa mashindano matatu tu yaani ngamia, farasi na njiwa." Kwa hayo, khalifa alimpa zawadi na wakati alipokuwa akiondoka, khalifa alimwambia: "Mimi nashuhudia kuwa huyu aliyetupa mgongo amemnasibishia Mtume Muhammad(s.a.w.w) uongo."

SIFA ZA KUZITAMBUA HADITH

Ili kuweza kuzitambua ni Hadith za aina gani zilizo za uongo, Ma'ulamaa wetu wametupatia dalili ambazo zitakazotujulisha usahihi na ukweli wa Hadith hizo na masharti ni kwamba mtu yeyote asijitumbukize katka kuzieneza na kuzisherehesha Hadith hadi hapo atakapoweza kuthibitisha kuwa zinastahili hivyo. Hapa tunawaleteeni kwa mukhtasari:

(1). Habari zilizoelezwa katika Hadith zisiwe zikipingana na Ayah za Qur'an tukufu, yaani zisipingane na maamrisho ya Allah swt. Angalieni kuwa mara nyingi 'Aam, khaas, mutlaq, muqayyad - kwa kutokujua mambo haya watu wanafikia uamuzi wa kusema kuwa Hadith fulani inakwenda kinyume na Ahadith, kunaleta hatari kubwa ya kupotosha maana sahihi ya Hadith.

(2). Hadith kamwe isiwe kinyume na akili bali iwe kwa mujibu wa akili.

(3). Iwapo Hadith itakuwa ni salama kwa Dini na Madhehebu, basi ipokelewe.

(4). Kwa kuitambua Hadith mambo yafuatayo yanatosha:

(a). Ujue lugha ya Kiarabu na kanuni zake kwa ukamilifu,

(b). Zaidi ya hayo inabidi Lisan-i-Suduur yaani kujua maarifa na ubalagha wa lugha ya Ma'sumiin(a.s) .

(c).Inabidi kuwa mjuzi wa historia ya Kiislamu na sirah za Ma'sumiin(a.s) .

(d). Ni lazima ajue Madhehebu na mwanzo wao na kuzijua itikadi zao kwa vyema.

(e). Itabidi mtu huyo awe amejiepusha na ta'assub yaani chuki za aina yoyote ile kwani hapo ndipo hapo atakapoweza kushughulikia bila ya upendeleo au ushawishi wa aina yoyote ile.

HADITH YA UFUNGUZI

1. Amesema al-Imam as- Zayn al-'Aabidiin(a.s) ., katika Bihar al- Anwar, j. 90, uk 187 na Sahifah as-Sajjadiyyah, uk. 572: "Sifa zote ni za Allah swt, na kusiwa Kwake ni haki Yake: sifa zisizo na kifani ndizo zinazomstahiki Yeye. Na mimi najiepusha kwa msaada wake dhidi ya shari za nafsi yangu: Kwa hakika mwanadamu yupo katika kutenda madhambi isipokuwa wale waliobarikiwa na Mola wao. Naomba msaada wake Allah swt dhidi ya maovu ya Shaytani ambaye daima ananiongezea dhambi moja juu ya lingine. Naomba msaada wake Allah swt dhidi ya watawala waovu, watawala katili, na maadui wa nguvu. " "Ewe Mola! Naomba unifanye mimi kuwa mmoja wa Majeshi yako, kwa sababu kwa hakika Majeshi Yako tu ndiyo yenye kushinda; na unifanye miongoni mwa wanachama Wako, kwani kwa hakika, chama Chako tu ndicho kitakachofanikiwa; na unikubalie kama mmoja wa wapenzi Wako, kwani kwa hakika, wapenzi wa Allah swt hawana hofu na kamwe hawatahuzunika."

Mola! Naomba uniimarishie Dini kwa ajili yangu, kwani hiyo ndiyo hifadhi ya matendo yangu yote; na unitengenezee Aakhera yangu, kwa sababu hakuna shaka kuwa hiyo ndiyo mwisho wangu wa kudumu na kuepukana na watu wenye dharau na dhihaka, na uyafanye maisha yangu yawe ya kuniongezea mema, na mauti yangu yawe ndiyo kujitoa huru kutokana na kila aina ya kasoro za magonjwa." "Ewe Mola! Mbariki Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , Mtume wa mwisho katika jamii ya Mitume yote, na Ahli Bayti(a.s) . tukufu, na vile vile Masahaba wake wema, na naomba unijaalie mahitaji matatu kwa leo: Usinibakizie dhambi lolote lile isipokuwa umenisamehe na wala huzuni yoyote ile isipokuwa umeniondolea, wala kusikwapo na adui isipokuwa wewe umemwondosha kwa jina lako tukufu la Allah ambayo ni jina bora kabisa i.e.Bismillah, Mola wa Mbingu na Ardhi .."

KUMJUA ALLAH SWT, UKUU NA BARAKA ZAKE

2. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Enyi Watu! Kwa hakika hakutakuwapo na Mtume baada yangu, na wala hakutakuwapo na Ummah baada yenu (Waislamu). Hivyo, Muwe waangalifu katika kumwabudu Allah swt, musali sala tano za siku, mufunge saumu katika mwezi uliowekwa (Ramadhaan al-Mubarak), mufanye Hijja ya Nyumba ya Allah swt (Al-Ka'aba huko Makkah al-Mukaramah), mutoe Zaka kutoka mali zenu kwa ajili ya kuitakasisha nafis zenu kwa hayo, na mutii amri za Wale wenye mamlaka, ili muweze kuingia Pepo ya Mola wenu. " [2]

3. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) Amesema: "Kwa kuwa na tasawwuri ya Ukuu wa Mola wako basi itakufanya wewe utambue udogo wa viumbe katika mitazamo yako. "[3]

4. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) Amesema: "Tawba ni kwa ajili ya yule ambaye ametakasisha kwa ajili ya Allah swt matendo, ilimu, mapenzi, bughudha, kuchukua, kutoa, misemo, ukimya, matendo na asemavyo ."[4]

5. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) : "Moyo ni mahala pa takatifu ya Allah swt, hivyo, basi hakikisha hapawi kitu kingine chochote isipokuwa Allah swt tu ."[5]

(Moyo mtukufu ni wa Allah swt tu. Hivyo mapenzi ya dunia isivyo sahihi, lazima iwekwe mbali.)

6. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) : "Wafuasi wetu ni wale ambao wanapokuwa peke yao, wanamkubuka Allah swt kwa kupita kiasi. "[6]

(Kwa hivyo, wao hujiepusha kutenda madhambi wanapokuwa peke yao wakati ambapo kuna hakuna kizuizi cha kuwazuia wao wasitende madhambi na badala yake humkumbuka Allah swt kwa kupita kiasi).

7. Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir(a.s) : "Kwa kiapo cha Allah swt! Yeye, aliyetukuka, huwategemea kwa mawili:wao waungame na kushukuru Kwake kwa neema ili Yeye awaongezee wao; na waungame kwa madhambi yao ili kwamba Yeye awasamehe madhambi yao ."[7]

8. Amesema al-Imam Husayn ibn Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Kwa hakika, Allah swt, aliye Mkuu, hakuwaumba wanadamu isipokuwa kwa kumjua Yeye na baada ya kumjua Yeye kumwabudu kwa kumjua Yeye; na wakati wanapomwabudu basi kusikuwepo na haja tena ya kumwabudu yeyote mwingine isipokuwa Yeye peke yake ."[8]

9. Amesema al-Imam Zayn-al-'Aabediin(a.s) : "Hakuna maangamizo (Jahannam au Motoni ) kwa ajili ya Mumiin aliye na sifa tatu : Kuungama na kukubali kuwa hakuna Allah swt mwingine isipokuwa Allah swt tu peke yake, pekee ambaye hana mshiriki; Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w) ni mtetezi; ukubwa usio na kipimo cha Rehema za Allah swt ."[9] .

SALA NA ATHARI ZAKE

10. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Mtu yeyote aichukuliaye sala pasi na uzito wake, basi si hatokani nami. Hapana, Kwa kiapo cha Allah swt, mtu kama huyo hatafikia chemchemi ya Haudh Kawtha ". [10]

11. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) : "Iwapo kutakuwapo na mto unaopita nyumbani mwa mtu ambamo mtu huyo anaoga mara tano kwa siku, je kutabakiapo aina yoyote ya uchafu mwilini mwake? Kwa hivyo sala ndivyo ilivyo mfano wa mto huo. Mtu ambaye anasali sala zake basi hujiondolea madhambi yake yote isipokuwa kutabakia madhambi yale ambayo yanamtoa katika Imani yake.[11]

12. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Sala iliyofaradhishwa kwa Allah swt ni sawa na kutimiza Hajj elfu moja na 'Umrah elfu moja ambazo ni sahihi na zilizokubalika. " [12]

13. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Kamwe musizipoteze sala zenu, kwa hakika, mtu yeyote anayezipoteza nyakati za sala zake atainuliwa pamoja na Qarun na Hamaan na itamwia haki Allah swt awatumbukize katika moto wa Jahannam pamoja na Munafiqiin (wanafiki) . [13]

14. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Musali sala zenu kama kwamba hiyo ndiyo sala yenu ya mwisho ". [14]

15. Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Iwapo mwenye kusali angalikuwa akifahamu kiasi alichozungukwa na rehema za Allah swt, basi kamwe asingaliinua kichwa chake kutoka hali ya kusujudu "[15] .

16. Amesema Al-Imam Al-Muhammad al-Baqir(a.s) : "Siku ya Qiyama, jambo la kwanza litakalo hisabiwa ni kuhusu sala; kwa hivyo, iwapo itakuwa imkubaliwa, basi matendo mengine pia yatakuwa yamekubaliwa (amasivyo matendo yake mengine mema hayatamnusuru)" .[16]

17. Amesema Al-Imam Al-Sadiq(a.s) : Katika siku za mwishoni mwa maisha yake, Imam As-Sadiq(a.s) . aliwaita Jama'a na wafuasi wake na kuwaambia "Kwa hakika, Uokovu wetu hautamfikia yule aichukuliaye sala kiepesi (bila ya kuichukulia kuwa ndiyo fardhi na lazima)"[17]

18. Amesema Al-Imam Al-Muhammad al-Baqir(a.s) :

"Yapo mambo kumi ambayo mtu atakapokutana na Allah swt siku ya Qiyama ataingia Peponi:

" Kuamini na kukiri kuwa hakuna Allah swt mwingine isipokuwa Allah swt,

" Na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allah swt

" Kukiri na kuamini kuwa kile kilichoteremshwa juu ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kutokea Allah swt ni Qur'an tukufu,

" Kutimiza sala

" Kutoa Zaka

" Kufunga saumu mwezi wa Ramadhani,

" Kuhiji Makkah,

" Kuwatendea mema wale wampendao Allah swt,

" Kujiepusha na maadui wa Allah swt,

" Na kujiepusha mbali na ulevi wa kila aina.[18]

19. Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Kwa kila mwenye kusali, sala ndiyo sababu kubwa ya kumfanya amkaribie Allah swt,; na kwa yule aliye dhaifu, Hajj - kuhijji Makkah - ni sawa kabisa na Jihadi - kupigana katika njia ya Allah swt. Kwa kila jambo kuna zaka yake, na hivyo zaka ya mwili ni saumu. Jihadi ya mwanamke ni kuwa mwenzi mwema wa mume wake. "[19]

20. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Hakuna usiku unaopita isipokuwa Malaika wa Mauti huwaita 'enyi watu wa maqaburi!' na huwauliza kile kinachowasikitisha kwa siku hiyo kwa yale waliyoyaona na maisha yajayo. Kwa hayo wafu husema 'kwa hakika, sisi twasikitika na kuwaonea wivu muminiin wale ambao wapo misikitini mwao ambapo wao wapo wansali wakati sisi hatusali; wao wanatoa zaka wakati sisi hatutoi; wao wanafunga mwezi wa Ramadhan wakati ambapo sisi hatufungi; wao wanatoa misaada kwa kile walichonacho ziada ya familia yao, wakati sisi hatufanyi hivyo. "[20]

21. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Kwa kila wakati uliyofanywa muayyan kwa ajili ya sala , mimi huwa ninamsikia mpiga mbiu ambaye huita na kusema 'Enyi wana wa Adam! Dumisheni sala ili muweze kuuzima moto ambao nyinyi wenyewe muliuwasa kwa ajili yenu (kwa kutenda madhambi) ." [21]

22. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Lazima muwe waangalifu wa Sala, kwani siku ya Qiyama Allah swt atakapomsimamisha mja wake (kwa hisabu) basi jambo la kwanza la kuulizwa litakuwa ni kuhusu Sala. Iwapo mtu atakuwa amekujanayo kamilifu, basi atakuwa miongoni mwa watu waliookoka, ama sivyo, atatupwa Motoni (Jahannam) ." [22]

23. Abu Basir Amesema kuwa yeye alimtembelea Ummi- Hamidah (mama yake Imam Musa ibn Ja'afar(a.s) ., kwa ajili ya kumpa pole kwa kifo cha Ja'afar ibn Muhammad(a.s) . Yeye alilia na hivyo yeye pia alilia kwa sababu ya kilio cha mama huyo. Baadaye, mama yake al-Imam(a.s) . alisema: "Ewe Aba Muhammad! Iwapo ungalikuwa umemwona Ja'afar ibn Muhammad alipokuwa kitandani wakati wa kufariki, basi ungalikuwa umejionea mambo ya ajabu kabisa: Yeye alifumua macho yake na kutaka maJama'a wote wakusanywe.' Na hapo yeye aliendelea kusema kuwa maJama'a wote walikusanyika bila ya kubaki mtu. Hapo al-Imam(a.s) . alisema kwa kuwaangalia wote: "Kwa hakika, Uokovu wetu hautamfikia yule aichukuliaye Sala kiepesi (bila ya kuichukulia kuwa ndiyo fardhi na lazima)"[23]

24. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Ibada ya yule mtu ambaye mapato yake yanatokana na njia zilizo haramu ni sawa na kujenga nyumba juu ya mchanga."[24]