HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.0%

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s. Mwandishi:
Kundi: VITABU VYA HADITHI

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.

Mwandishi: AMIRALY M.H.DATOO
Kundi:

Matembeleo: 27685
Pakua: 8091

Maelezo zaidi:

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 13 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 27685 / Pakua: 8091
Kiwango Kiwango Kiwango
HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.

Mwandishi:
Swahili

3

HADITH ZA MTUME (s.a.w.w)NA MA-IMAMU (a.s)

SALA ZA USIKU WA MANANE

25. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Heshima ya Mumiin ipo katika kukesha kwake usiku na utukufu wake upo katika kujitawala mwenyewe miongoni mwa watu ." [25]

26. Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Yeyote yule alale zaidi wakati wa usiku, lazima atapoteza kitu mujimu kabisa katika matendo yake (i.e. sala ya usiku) ambayo hataweza kuipata wakati wa mchana ."[26]

27. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) : Allah swt katika ufunuo wake kwa Mtume Musa(a.s) ., mwana wa 'Imran(a.s) . alisema: "Ewe Mwana wa 'Imran! Wale tu ambao wanadai kunipenda mimi, wasema uongo, kwani usiku unapoingia wao hulala huku wakiniacha mimi ."[27]

28. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) : "Kamwe usiikose Sala ya usiku wa manane! Kwa sababu, ukweli ni kwamba, mpotezaji ni yule anayeikosa (faida zake) Sala za usiku wa manane. "[28]

29. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) : Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . alimwambia Jibrail amwambie chochote, naye alimwambia: "Ishi utakavyo huku ukitambua kuwa utakuja kufa; penda chochote kile utakacho lakini utatengana nacho; tenda utakavyo lakini utakutana nacho ( na kulipwa malipo yake). Heshima ya Mumin ni Sala yake ya Layl (usiku wa manane), na utukufu wake upo katika kujiepusha (na kuangamiza) sifa za watu. " [29] .

30. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) : "Vipo vitu vitatu ambavyo ndivyo sifa za Muumin na ndivyo vito vya thamani kwake humu duniani na Aakhera. Navyo ni: Sala katika sehemu ya mwisho wa usiku (Salat ul-Layl), kutotamani au kuwa na wivu kwa kile kidogo kilicho mikononi mwa watu, na mapenzi (na uongozi ) wa Imam kutokana na kizazi cha Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w) "[30] .

31. Amesema al-Imam Muhammad ibn Ali al-Jawad ul- 'A'immah(a.s) : "Yeyote yule aliye na imani kamili juu ya Allah swt, anaona furaha; na yeyote amwaminiaye, basi anatosheleza matendo yake ."[31] .

KUMWAMINI ALLAH NA KUIPATA FURAHA YAKE

32. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) : "Baba yangu aliniambia kuhusu baba yake kuwa mtu mmoja kutoka mji wa Kufa alimwandikia baba yake viz. Al-Husayn ibn Ali(a.s) ., akimwuliza(a.s) . kumjulisha yeye kuhusu mema ya dunia hii na mema ya Akhera. Kwa hayo Imam(a.s) . alimwandikia (katika majibu): "Kwa jina la Allah,aliye Rahmaan na Rahiim'. Baadaye akiendelea 'Kwa hakika yeyote yule atakaye furaha ya Allah swt hata wakati wa kutokuwafurahisha watu, Yeye humtosheleza katika masuala ya watu. Lakini, yule ambaye hutaka furaha za watu wakati anamuudhi Allah swt, basi Allah swt humwachia watu ( na yeye atakuwa mbali na baraka za Allah swt), Wassalaam' ."[32]

33. Amesema Al-Imam Zayn Al-Abedin(a.s) : "Yeyote yule atendaye matendo yake kwa mujibu wa vile alivyoamrisha Allah swt, ni miongoni mwa watu bora ."[33] .

34. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) : "Yeyote yule aliye na mapenzi ya Allah swt,anachukia kwa ajili yake Allah swt, na anatoa msaada kwa ajili ya Allah swt, basi huyo ni miongoni mwa wale ambao Imani yao imekamilika ."[34]

35. Amesema Al-Imam Al-Hasaan Al-Askari, Imam wa Kumi na Moja,(a.s) : "Hakuna sifa zaidi ya hizi mbili: Kuwa na Imani kwa Allah swt na kuwa mwenye manufaa kwa Waislamu ."[35] .

TAQWA NA UMUHIMU WAKE KWA WAISLAMU

36. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Miongoni mwa kitu kilicho muhimu kabisa kwa kuwafikisha watu hadi kufikia Peponi ni taqwa na tabia njema ." [36] .

37. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Wakati wa kutoa uamuzi wa kitu, fikiria matokeo yake. Iwapo ni nzuri kwako wewe kuendelea na maendeleo, fuata hivyo, lakini iwapo inakupotosha, uiachilie mbali ."[37] .

38. Aliulizwa Al-Imam As - Sadique(a.s) . kuhusu maana ya Taqwa, na alijibu: "Allah swt hakukosi mahala pale alipokuamrisha wewe uwepo, na hakuoni pale ambapo amekuharamishia wewe kuwepo ."[38]

39. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Onyesha heshima zako kwa ajili ya Allah swt kama vile utakavyoonyesha heshima zako mbele ya mtu mwema miongoni mwa ukoo wako ." [39]

40. Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Al Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s): "Kwa mtu kuinamisha macho yake kutamwia kama kizuizi dhidi ya matamanio (shahwa) yake ."[40]

41. Al-Imam Amir-ul-Muminiin Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amewaambia wana wake Al Imam Hassan ibn Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . na Al Imam Hussein ibn Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . wakati 'Abdur Rahman ibn Muljim (Allah amla'ani) alipokuwa amempiga dharuba ya upanga kichwani mwake, katka Nahjul Balagha, Barua no. 47: "Ninawasihini nyote mumwogope Allah swt na nyinyi wala musiwe na uchu wa starehe za dunia hii hata kama itawakimbilia nyinyi. Wala musikisikitikie kitu chochote cha dunia hii ambacho mumekikosa. Semeni ukweli na mutende (kwa kutumai) malipo. Muwe adui wa mdhalimu na msaidizi wa mdhulumiwa ."

42. Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Ninawauusieni kumwogopa Allah swt, Ewe mwana wangu, kubakia katika Amri Zake, kuujaza moyo wako kwa ukumbusho Wake na kubakia katika kumtegemea Yeye tu. Hakuna Hakuna ushikamano unaotegemewa kuwa madhubuti baina yako na Allah isipokuwa wewe iwapo utaishikilia menyewe .[41]

43. Abi Osama Amesema kuwa alimsikia Al Imam Ja'afer as- Sadiq(a.s) . alisema: "Muwe nakhofu za Allah, taqwa, ijtihadi, kusema ukweli, uaminifu katika amana, tabia njema na ujirani mwema. Muwaite wengine kwenu (kwa tabia zenu njema), wala si kwa maneno tu. Muwe watu wenye kupendeza na kamwe musiwe watu wa kutuaibisha. Ninawausieni murefushe rukuu' na sujuda zenu. Kwani kila mmoja wenu anaporefusha rukuu' na sujuda basi Shaytani hulia nyuma yenu kwa kusea 'Ole wako! yeye ametii; amesujudu na mimi nilikataa ."[42]

44. Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein bin Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . Amesema: "Kwa hakika marafiki wa Allah hawatakuwa na khofu yoyote juu yao wala hawatakuwa watu wenye kuhuzunika) iwapo watadumisha yaliyofaradhishwa na Allah swt, wakafuata Sunnah za Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w)wakajiepusha na yale yaliyoharamishwa na Allah swt, wakawa wacha Allah swt wema katika kile walichonacho katika utajiri na wadhifa wa humu duniani, wakajitahidi kujitafutia kile kilicho halali, wakaamua kutojifakharisha wala kutojilimbikia katika mali na utajiri isipokuwa katika kutoa misaada na kutoa malipo ya kulipa yaliyofaradhishwa kwake. Basi kwa hakika hao ndio waliobarikiwa katika mapato yao na watalipwa mema kwa yale waliyoyatanguliza huko Aakhera. "[43]

45. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Kwa hakika Wana wa Adam wapo sawa na meno ya kitana kuanzia zama za Mtume Adam (a.s) . hadi leo, na wala hakuna utukufu wa Mwarabu juu ya asiye Mwarabu, wala Mwekundu juu ya Mweusi isipokuwa kwa Taqwa ."[44]

46. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) : "Kwa hakika, tendo dogo kabisa lifanywalo pamoja na Taqwa ni bora kabisa kuliko tendo kubwa (au matendo mengi) lifanywalo bila Taqwa. "[45]

KUOMBA DUA

47. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) : "Dua yoyote inayoombwa kwa Allah swt, inakuwa imezuiwa na mbingu hadi hapo iwe imeshirikishwa na Salawat i.e. kumsaliwa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w)pamoja na Ahlil Bayt (a.s) . "[46]

48. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) : "Muminiin waombao Dua zao hazikukubaliwa humu duniani watatmani kuwa dua zao hata moja zisingelikubaliwa pale watakapoonyeshwa hapo Aakhera, mema kupita kiasi ya thawabu (akipewa yeye kwa kutokujibiwa Dua zake na kwa mateso na shida alizozipata akiwa humu duniani) ."[47]

49. Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Tendo lipendwalo sana mbele ya Allah swt humu duniani ni Dua na ibada iliyo bora kabisa mbele Yake ni unyenyekevu na ucha-Allah swt. "[48]

50. Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Milango ya Peponi ipo wazi kwa nyakati tano: wakati mvua inyeshapo; wakati wa Vita vitukufu; wakati wito wa Sala utolewapo (wanapotoa Adhaan) ; wakati wa kusoma Qur'an Tukufu wakati ambapo jua linazama na linachomoza alfajiri ."[49]

51. Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Mujiweke tayari kuomba Dua katika nyakati tano: Wakati usomwapwo Qur'an; Wakati utolewapwo Aadhaan; Wakati unaponyesha mvua; Wakati wa kwenda kupigana katika vita vitakatifu kwa ajili ya kuwa shahidi; Wakati madhulumu anapoomba dua, kwa sababu yeye hana kizuizi cha aina yoyote chini ya mbingu ."[50]

52. Amesema Al Imam Hussain ibn 'Ali bin Abi Talib(a.s) . , katika Dua 'Arafah: "Ewe Mola Wangu! Wewe U karibu kabisa wa kuombwa; Na mwepesi wa kujibu; na Wewe Mkarimu wa kutoa; na unamtosheleza umpaye; unamsikia vyema akuulizae; Ewe Uliye Rahmaan wa dunia na Aakhera na Mremehevu kote !"

53. Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Anayejaaliwa vitu vinne hanyimwi vinne: Anayejaaliwa kuomba Dua hanyimwi kukubalika kwake; anayejaaliwa kufanya Tawba hanyimwi kukubalika kwake; anayejaaliwa kuomba msamaha hanyimwi kusamehewa kwake; anayejaaliwa kutoa shukuurani zake hanyimwi kuongezewa kwake ."[51]

54. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) : "Siku ya Qiyama, Allah swt atazihesabu Dua zote alizokuwa akiziomba Mja wake na kuuzibadilisha katika matendo mema na kwa hayo atawapandisha daraja katika Jannat (Peponi) ."[52]

55. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) : "Ponyesheni magonjwa yenu kwa kutoa Sadaka na mujiepushe na balaa za kila aina kwa Dua "[53]

56. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) .

60: "Mwombe Allah swt maombi yako na daima uwe ukisisitiza katika kumwomba kwani Allah swt mwenyewe anapenda mno kubakia kwa kumsisitiza miongoni mwa waja wake Muminiin ."[54]

57. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) : "Ninakuusieni muombe Dua', kwa sababu hamtaweza kumkaribia Allah swt kwa vinginevyo kama hivyo ."[55]

58. Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Inawezekana kuwa wewe umemwomba Allah swt Dua ya kitu fulani ambacho yeye hakukujaalia kwa sababu yeye anataka kukupa kitu kilicho bora zaidi ya kile ulichokuwa umekiomba, hapo mbeleni(unatakiwa kufanya subira - mtarjum) ."[56]

AHLUL BAYT (A.S)

59. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Mfano wa Ahlul-Bayt yangu kwa Ummah wangu ni sawa na Safina ya Mtume Nuh (a.s). Wote wale watakaoipanda ndani yake basi wameokolewa na wote wale waupingao, basi wamezama na kupotea ."[57]

60. Amesema Al-Imam Muhammad al-Baqir(a.s) ., Imam wa tano: "Ahadith zetu (za Alhul Bayt) zinahuisha nyoyo ."[58]

61. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Muhuishe mikutano na mikusanyiko yenu kwa makumbusho ya Ali ibn Abi Talib (a.s) ." [59]

62. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : na yenye maana yakaribiayo katika Yanabi-ul- Muwaddah, uk. 117: Ipo riwaya kupitia Jabir-il-Ju'fi iliyopokelewa kutoka Jabir-ibn-Abdillah isemayo: Mimi nilisema: Ewe Mtume wa Allah swt, sisi tunamwelewa Allah swt na Mtume wake(s.a.w.w) Sasa jee hawa 'Ulul-Amr ni wakina nani ambao utiifu wao umefardhishwa sawa na wako?

Hapo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . alisema: "Ewe Ja'abir! Wao ni, baada yangu, Makhalifa wangu na Ai'mmah wa Waisilamu; wa kwanza miongoni mwao ni Ali ibn Abi Talib(a.s) ; atafuatia (Imam) Hassan, na (Imam) Husayn; atafuatia Ali ibn il Husayn; atafuatia Muhammad ibn Ali; ajulikanaye katika Tawrati kama Baqir, ambaye utakutana naye, Ewe Ja'abir! Pale utakapomtembelea, umpe salaam zangu. Baada yake Musa ibn Ja'afar; atafuatia Ali ibn Musa, atafuatia Muhammad ibn Ali; atafuatia Ali ibn Muhammad, atafuatia Hassan ibn Ali; na baada yake (atakuja) Al-Qaim, ambaye jina lake ni sawa na jina langu. Yeye ndiye atakaye kuwa Mamlaka Ya Allah swt juu ya ardhi hii na Aliyebakia miongoni mwa Waja wake. Yeye ndiye mwana wa (Al-Imam) Hassan ibn Ali ( al-'Askari). Huyu ndiye shakhsiyyah ambaye Allah swt atafungua Dhikiri zake Mashariki na Magharibi na huyu ndiye Shakhsiyyah ambaye atakuwa ghaibu kwa wafuasi na wapenzi wake ambavyo hakuna nyoyo zozote zile zinazoweza kukubali isipokuwa nyoyo za wale tu ambao Allah swt ameshakwishakuzijaribu kwa ajili ya Imani."[60]

Ja'abir alisema: "Mimi nilimwuliza 'Ewe Mtume wa Allah swt! Je wafuasi wake watafaidika naye wakati akiwa ghaibu? Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . alijibu: 'Naam. Kwa kiapo cha Yule aliyenichagua kuwa Mtume, wao watafaidika kwa nuru yake na watafaidika kwa ibada akiwa ghaibu kama vile kufaidika kwa watu kutokana na (nuru ya ) jua hata pale linapofunikwa kwa mawingu.'"

63. Amesema Malik ibn Anas kuhusu mema ya Imam As-Sadique(a.s) : "Hakuna macho yaliyowahi kuona, hakuna masikio yaliyokwisha kusikia, na wala hakuna moyo uliyokwisha shtushwa kwamba kunaweza kuwapo na mtu yeyote aliye bora zaidi kuliko (Imam) Ja'afar as- Sadique(a.s) . katika Taqwa, elimu, ibada na Ucha-Allah swt."[61]

64. Amesema Al Imam Hussain ibn 'Ali bin Abi Talib(a.s) ., Al-Irshaad, Uk. 204: "Kwa roho yangu, hakuna Imam isipokuwa ni Hakimu kwa Kitabu, anaimarisha uadilifu, anaamini katika Dini ya Ukweli, na anajizuia nafsi yake pamoja na njia ya Allah swt ."

MAPENZI YA AHLUL-BAYT (A.S).

65. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , Al-Jami'- ul-Saghir, J. 1 Uk. 14: "Wafunzeni watoto wenu vitu vitatu: Mapenzi ya Mtume wenu, Mapenzi ya Ahlul-Bayt, usomaji wa Qur'an ."

66. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) : "Mtu yeyote ambaye hawezi kutufanyia wema wowote sisi Ahlul-Bayt basi wawafanyie mema wafuasi wetu walio wema; na yeyote yule asiyeweza kutuzuru, basi wanaweza kuwazuru wafuasi wetu walio wema ambavyo thawabu za kutuzuru sisi zitaandikiwa yeye ."[62]

67. Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir(a.s) : "Kwa kile kilicho bora kabisa kwa mja kumkaribia Allah swt ni utiifu kwake Allah swt, utiifu kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . na utiifu kwa ulil Amr." Aliendelea kusema: "Mapenzi yetu (ya Ahlul-Bayt) ni Imani na chuki dhidi yetu ni kufr." [63]

68. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) : "Kwa hakika zipo daraja za ibada, lakini mapenzi yetu , Ahlul-Bayt, ni ibada iliyo bora kabisa ."[64]

SIFA NA TABIA ZINAZOKUBALIKA

69. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Je niwatambulisheni Mu'miin ni nani? Muumin ni yule ambaye waumini wengine wanamwamini kwa nyoyo zao na mali pia. Je niwatambulisheni Mwislamu ni nani ? Mwislamu ni yule ambaye Waislamu wengine wanakuwa wamehifadhika kwa ulimi na mikono yake.. Ni haramu kwa Mumiin kumfanyia ubaya mumin mwenzake, au kumwacha katika hali ya shida, au kumsengenya au kumkataa kwa ghafla ."[65]

70. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) : "Haimpasi Mwislamu kuhudhuria au kushiriki katika mikutano au mikusanyiko ambapo Sharia za Allah swt zinavunjwa na kwamba yeye (huyo Mwislamu) hana uwezo wa kuyazuia hayo ."[66] .

71. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) : "Yeyote yule kwa tabia yake husema ukweli, basi matendo yake yametakasika; Na allah swt humwongezea riziki yule aliye na nia njema; na yeyote yule awatendeaye mema familia yake, Allah swt humwongezea umri mrefu ."[67]

72. Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . alijiwa na mtu mmoja aliyeomba kufundishwa tendo kwayo ataweza kupendwa na Allah swt pamoja na watu, utajiri wake utaongezeka, mwili wake utakuwa na siha nzuri, umri wake utaongezeka na atainuliwa Siku ya Qiyama pamoja na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . alimjibu: 'Hizi ndizo njia sita zinazohitaji sifa sita: Iwapo wataka Allah swt akupende, lazima umwogope na ujiepushe na madhambi,Iwapo wataka watu wakupende, lazima uwe mkarimu kwao na ukatae walichonacho mikononi mwao, Iwapo wataka Allah swt akuongezee utajiri wako, hunabudi kutoa malipo yaliyofaradhishwa kwako i.e. Zaka, Khums, na zinginezo.

Iwapo wataka Allah swt aupatie mwili wako afya njema, basi uwe ukitoa sadaqa kila mara iwezekanavyo, Iwapo wataka Allah swt aurefushe umri wako, basi uwe ukiwajali maJama'a zako, Iwapo wataka Allah swt akuinue pamoja nami Siku ya Qiyama, basi ni lazima urefushe sujuda zako mbele ya Allah swt, aliye Pekee na Mmiliki."[68]

73. Amesema Al-Imam Ar-Ridhaa(a.s) . Imam wa Nane: "Mumin hawezi kuwa mumin kamili hadi hapo atakapokuwa na mambo matatu: Sunna za Allah swt, Sunna za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . na Sunna za Imam(a.s) . wake. Ama Sunna za Allah swt ni kuzificha siri zake; kama vile Allah swt anavyosema katika Sura Al-Jinn, 72, Ayah 26 & 27. Yeye ndiye mwenye kujua ya siri, wala hamdhihirishii yeyote siri yake, Usipo kuwa Mtume wake aliye mridhia. Naye huyo humwekea walinzi mbele yake na nyumba yake.[69]

Na ama Sunnah za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ni kule kupatana na kuelewana na watu, wakati ambapo Allah swt alimtuma Mtume wake kuwapenda watu na Amesema: 'Uzoee usamehevu na uwafundishe mema na ujiondoe kutoka majaheli Ama kuhusu Sunnah za Imam(a.s) . (kuwa imara na) mwenye subira katika siku nzuri na siku mbaya na nzito, ambavyo Allah swt anatuambia katika Sura Al-Baqara, 2, Ayah 177. Sio wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi. Bali wema ni wa anaye muamini Allah swt na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii, na anawapa mali, kwa kupenda kwake, Jama'a na mayatima na masikini na wasafiri, na akawa anashika Sala, na akatoa Zaka, na wanao timiza ahadi yao wanapo ahidi, na wanao vumilia katika shida na dhara na wakati wa vita; hao ndio walio sadikisha, na hao ndio wajilindao.

74. Amesema Al Imam Muhammad al-Taqi(a.s) . (al-Jawad Imam wa Tisa), Muntah al-'Amal, Uk.229: "Mumin anahitaji mambo matatu: mafanikio yatokayo kwa Allah swt, mwenye kujipa mawaidha, kukubaliwa na yule ampaye nasiha. "

75. Al Imam Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . Imam wa Nne, aliulizwa "Ewe mwana wa Mtume! Huanzaje siku yako?" Na Imam(a.s) . alijibu: "Mimi huanza siku yangu huku nikitakiwa kutimiza mambo manane (8): Allah swt ananitaka nitimize yaliyafaradhiwa juu yangu; Na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . ananitaka nitimize yale yaliyo Sunna yake; Familia yangu inanitaka mimi niwatimizie mahitaji yao kama chakula n.k.; Nafsi yangu inanitaka niitimizie matamanio yangu; Shaytani aninitaka mimi nitende madhambi; Malaika wawili wanaonihifadhi wananitaka mimi nitende matendo kwa moyo halisi, Malaika wa Mauti anataka roho yangu na Kaburi inautaka mwili wangu. Basi mimi ndivyo nilivyo baina ya mzunguko wa matakwa hayo."[70]

76. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Kwa hakika kila kitu kinashawishiwa na Mumin kwa sababu Dini ya Allah swt inamfanya yeye awe ni mtu mwenye nguvu, na wala yeye kamwe hashawishiwi na kitu chochote kile, na kwa hakika hii ndiyo dalili ya kila Mumin ." [71]