HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.0%

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s. Mwandishi:
Kundi: VITABU VYA HADITHI

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.

Mwandishi: AMIRALY M.H.DATOO
Kundi:

Matembeleo: 27622
Pakua: 8033

Maelezo zaidi:

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 13 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 27622 / Pakua: 8033
Kiwango Kiwango Kiwango
HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.

Mwandishi:
Swahili

4

HADITH ZA MTUME (s.a.w.w)NA MA-IMAMU (a.s)

WAFUASI HALISI WA AHLUL-BAYT (A.S) NA SIFA ZAO

77. Al Imam Muhammad al Baqir(a.s) . alimwambia, Ja'bir: "Je inatosheleza kwa mtu kujiita Shia na mfuasi wetu ati kwa kudhihirisha mapenzi yetu, Ahlul Bayt? Kamwe sivyo hivyo!, Kwa kiapo cha Allah swt, huyo mtu kamwe hawezi kuwa mfuasi wetu isipokuwa yule ambaye amejawa khofu ya Allah swt na kumtii ipasavyo. Ewe Ja'abir! Wafuasi wetu hawawezi kutambuliwa isipokuwa kwa sifa zifuatazo watakazokuwanazo kama unyenyekevu, kujitolea; uadilifu; kumsifu Allah kupita kiasi; kufunga saumu na kusali; kuwatii wazazi; kuwasaidia masikini, wenye shida, wenye madeni, na mayatima wanaoishi karibu naye; kusema ukweli; kusoma Qur'an; kuuzuia ulimi kusema chochote kuhusu watu isipokuwa kwa mapenzi; na kuwa mwaminifu kwa majama'a kwa maswala yote ."[72]

78. Amesema Sulayman Ibn Mahran kuwa Yeye alimtembelea Imam Ja'afer as-Sadique(a.s) . wakati ambapo baadhi ya wafuasi (Mashiah) walikuwa karibu naye na alimsikia Imam(a.s) . akiwaambia:"(Mujiheshimu) muwe kama vito vya thamani kwa ajili yetu na wala kamwe musiwe wenye kutuaibisha sisi. Waambieni watu kuhusu mema, na muizuie ndimi zenu zisizungumze mneno maovu na mambo yasiyo na maana ."[73] .

79. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) : "Kwa hakika, sisi huwapenda wale walio na busara, wenye kuelewa, wenye elimu, wenye kufanya subira, waaminifu na wenye imani. Kwa hakika Allah swt aliwajaaliwa Mitume(a.s) . kwa tabia njema. Kwa hivyo yeyote yule aliye na sifa hizo basi amshukuru Allah swt, lakini yule ambaye hana hayo basi amlilie Allah swt, Aliye Mkuu na Mwenye uwezo, na amwombe hayo. "Ja'abir kwa unyenyekevu alimwuliza Imam(a.s) . ndiyo yapi hayo", na Imam(a.s) . alimjibu: "Nayo ni: Ucha-Allah swt, kutosheka, subira, kushukuru, kuvumilia, tabia njema, furaha, hima, bidii, shauku, mkarimu, mkweli na mwaminifu katika amana ."[74] .

80. Amesema Al-Imam Muhammad al-Baquir(a.s) : "Yeyote yule anamtii Allah swt basi ni mpenzi wetu, na yeyote yule asiyemtii Allah swt basi ni adui wetu (sisi Ahlul-Bayt) .."[75] .

MADHAMBI NA ATHARI ZAKE

81. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Msitazame udogo wa dhambi, lakini muangalie mliyemuasi (Allah swt) ." [76] .

82. Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Iwapo mtu anapenda kujiona vile alivyo mbele ya Allah swt, basi ajitathmini kwa madhambi na maasi yake mbele ya Allah swt; basi kwa kipimo hicho ndivyo alivyo huyo mtu mbele ya Allah swt ."[77] .

83. Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) . aliwauliza watu ni kwa nini wanamwudhi Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Basi mmoja wa watu alimwuliza Imam(a.s) . vipi, naye Imam(a.s) . aliwaambia: "Je hamujui kuwa matendo yenu yapoyanajulishwa kwa Mtume Mtukufu (s.a.w.w) na pale aanapoona madhambi dhidi ya Allah swt miongoni mwao, basi husikitishwa mno. Kwa hivyo musimuudhi Mtume wa Allah swt na badala yake munatakiwa kumfurahisha (kwa kutenda mema) ."[78] .

84. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Kukosa kusamehe ni kasoro moja kubwa kabisa na kuwa mwepesi katika kulipiza kisasi ni miongoni mwa madhambi makubwa kabisa "[79] .

85. Kutokea Asbaghi bin Nabatah kutokea kwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . Amesema: "Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kuwa:Allah swt anapoukasirikia Ummah na kama hakuiadhibu basi bei za vitu vitapanda juu sana yaani maisha yatakuwa ghali, maisha yao yatakuwa mafupi, biashara zao hazitaingiza faida, mazao yao hayatukuwa mengi, mito yao haitakuwa imejaa maji, watanyimwa mvua (itapungua), na watatawaliwa na waovu miongoni mwao ." [80] .

(Yaani Hadith hiyo juu inatubainishia kuwa iwapo kutakuwa na jumuiya ambayo imejitumbukiza katika madhambi basi wanabashiriwa kupatwa na mambo saba hayo yaliyotajwa.).

86. Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) . Amesema kuwa amekuta katika kitabu cha Al-Amir al-Muminiin Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . akisema kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Amesema: "Wakati zinaa itakapokithiri katika jumuiya basi idadi za mauti za ghafla zitakithiri; na patakapokuwa na uovu basi Allah swt atawatumbukiza katika maisha ya ghali na hasara. Wakati watu watakapoacha kulipa zaka , basi ardhi itazinyakua baraka zake kutokea mazao, matunda, madini na vitu vyote kama hivyo. Wakati watakapotenda bila haki kwa mujibu wa Shariah, basi itakuwa sawa na kumsaidia dhalimu na ugaidi. Na watakapozikiuka ahadi zao, basi Allah swt atawafanya maadui wao kuwasaliti na kuwakandamiza. Wakati watakapoacha uhusiano pamoja na ndugu na Jama'a zao, basi yote yale wayamilikiayo yatakwenda mikononi mwa waovu. Na wakati watakapojiepusha na kutoa nasiha ya mambo mema na kuyakataza maovu na kama hawatawafuata waliochaguliwa Ahl-ul-Bayt(a.s) , basi Allah swt atawasalitisha kwa walio wenye shari miongoni mwao na katika hali hii, wataomba duaa lakini hazitakubalika."[81] .

87. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Machozi hayaishi illa kwa nyoyo kuwa ngumu, na nyoyo haziwi ngumu illa kukithiri kwa madhambi .[82] "

88. Allah swt alimwambia Mtume Dawud(a.s) : "Ewe Dawud! Wabashirie habari njema wale watendao madhambi kuhusu msamaha wangu, ambayo inajumuisha kila kitu kilichopo humu duniani, ili wasikate tamaa ya msamaha wangu; na waonye wale watendao mema kwa adhabu zangu ili wasije wakajifanyia ufakhari kwa utii wao, kwani ufakhari ni dhambi mbaya kabisa."[83] .

ELIMU NA THAMANI YAKE

89. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Waalimu pamoja na wanafunzi wanashirikiana katika kuulipwa mema wakati watu wengine hawabahatiki.."[84] .

90. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Yeyote yule aienezaye Din kwa watu bila ya yeye mwenyewe kuwa na ilimu ya kutosha, basi anaidhuru Din zaidi kuliko vile anavyoitumikia."[85] .

91. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Thamani ya kila kitu ni katika ubora wake." Yaani thamani ya mtu ni katika ilimu yake. Cheo na utukuzo wake utakuwa katika kiwango cha ilimu aliyonayo. Macho yetu hayaangali sura, urefu ukubwa wa mwili wa mtu bali humthamini kwa kufuatana na kiwango cha ilimu aliyonayo. Hivyo inatubidi sisi sote tujitahidi katika kutafuta na kuipata ilimu kwa kiasi tuwezacho.[86] .

92. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Elimu ni amana ya Allah swt juu ya ardhi hii na wanazuoni ndio wenye amana hii. Hivyo yeyote yule atebdaye kwa mujibu wa ilimu yake, basi kwa hakika ameiwakilisha amana vile ipasavyo"[87] .

93. Al-Imam Muhammad Baqir(a.s) . amesema: "Jitafutieni ilimu kwa sababu kujifunza ni matendo mema na kusoma kwenyewe ni 'ibada ."[88] .

94. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) Amesema: "Mtu ambaye anatafuta ilimu, ni sawa na mpiganaji vita katika njia ya Allah swt ."[89]

95. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) : "Uichunge sana ilimu yako na utazame ni kwa nani unaitoa ."[90] .

96. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) : "Muitafute ilimu na kuipamba kwa subira na ukuu ; na uwe mnyenyekevu kwa yule ambaye anaitafuta ilimu kutoka kwako "[91] .

97. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) katika, Al-Kafi, J. 1, Uk. 35: "Yeyote yule ajifunzae ilimu na kutenda vilivyo, na kuifundisha kwa ajili ya Allah swt, basi Malaika watatmukuza mbinguni ."

98. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Wema wa duniani humu pamoja na Aakhera ni pamoja na ilimu ." [92] .

ILIMU NA FADHILA ZA KUJIFUNZA

99. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Yeyote yule atafutaye ilimu ni sawa na mtu anayefunga saumu mchana na akikesha macho usiku kucha akifanya ibada. Iwapo atajifunza ilimu kwa sehemu fulani, basi itakuwa kwake ni afadhali kabisa hata kuliko kuwa na dhahabu ya ukubwa wa mlima Abu Qubais na ambayo itagawiwa sadaqa katika njia ya Allah swt ." [93] .

100. Al-Imam Zaynul 'Aabediin(a.s) . Amesema: "Iwapo watu wangalikuwa wakitambua kile kilichopo ndani ya kutafuta ilimu, basi wao wangaliitafuta hata kama itawabidi kusafiri na hata kuhatarisha maisha yao katika kuipata ."[94] .

101. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . Amesema: "Kutafuta ilimu haitawezakana wakati mwili unastareheshwa ."[95] .

(yaani mtu hataki kutaabika)

102. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) : "Hifadhini maandiko na vitabu vyenu kwa sababu hautapita muda mutakapovihitaji ."[96] .

103. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . Amesema: "Kwa hakika, kukamilika kwa Din ni kule kuitafuta ilimu na kuitekeleza ipasavyo, na muelewe waziwazi kuwa kutafuta ilimu ni faradhi zaidi kwenu nyinyi kuliko kutafuta mali na utajiri. "[97] .

104. Amesema al-Imam al-Hassan ibn Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Wafundisheni watu wengine ilimu muliyonayo na mujaribu kujifunza ilimu waliyonayo wengineo "[98] .

105. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Fadhila za ilimu zinapendwa zaidi na Allah swt hata kuliko fadhila za ibada ." [99] .

ILIMU NA FADHILA ZA KUIFUNDISHA

106. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Mtu yeyote aliyekuwa na ilimu kuhusu swala fulani na akaificha pale atkapoulizwa basi Allah swt atamkasirikia kwa ghadhabu za moto."[100] .

(yaani mtu anapokuwa na habari ambazo zitamsaidia mtu aliyepatwa na shida na ikaweza kumsaidia kuimarisha hali yake, badala ya kumsaidia yeye akaificha, basi hapo kwa hakika ametenda dhambi kubwa.)

107. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Qur'an Tukufu ni chuo kikuu ; hivyo jielimisheni kiasi muwezavyo kutokea chuo hiki ." [101] .

108. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Kwa hakika, kile kitakachoendelea kumfikia mtu hata baada ya kufa kwake, miongoni mwa matendo yake mema ni: ilimu ambayo yeye amewafundisha na kuieneza kwa wengineo, mtoto mwema aliyemwacha, kuacha Qur'an Tukufu ikapatikana ." [102] .

109. Amesema al-Imam Ali ar-Ridha(a.s) : "Rehema za Allah swt ziwe juu ya yule ambaye anazihuisha amri zetu." Na halikuwapo mtu akamwuliza Imam(a.s) . ni vipi wanaweza kuhuisha amri zao, na Imam(a.s) . alimjibu: "Anaweza akijifunza ilimu zetu na akawafundisha watu. Kwa hakika, iwapo watu wangelikuwa wamezijua faida na mema ya semi zetu, basi kwa hakika wangalitufuata sisi ."[103] .

ELIMU - HEKIMA - MA'ARIFA

110. Elimu ni fidia kwa juhudi za akili.

111. Wema ni sababu kuu ya elimu.

112. Kumwogopa Allah swt ni matokeo ya elimu.

113. Jumla ya utukufu wote, ni elimu au ma'arifa.

114. Yeyote afundishaye herusi moja, amenifunganisha nae minyororo.

115. Elimu iliyo bora ni ile inayomfaa mwenye kuwa nayo.

116. Elimu ni hazina na maisha.

117. Unyenyekevu ni matokeo ya elimu na ma'arifa.

118. Mtu mwenye elimu yu hai hata kama amekufa.

119. Dini ni ghala na elimu ni mwongozo wa kuifikia ghala.

120. Ili kupata ufanisi itikia elimu na kupuuzia ujahiliya.

121. Wengi wanaelezea ma'arifa, lakini ni wachache waiingizayo akilini mwao.

122. Bakhshishi iliyo kamili ya Allah swt ni ile maisha iliyotegemea elimu na hekima.

123. Wapumbavu wengi mno wanawafanya wasomi kuwa wachache.

124. Aliyeelimika anamwelewa vyema mjinga kwani yeye binafsi alikuwa mjinga awali.

125. Na mtu aliye jahili hataweza kumwelewa mtu aliyeelimika kwani hajaelimika mwenyewe.

126. Wana elimu wanaishi katika kiwiliwili kilichokufa cha ujahili.

127. Ma'arifa huuwa ujahili.

128. Elimu ndiyo iipatiayo maisha Roho.

129. Ma'arifa chache (ya Allah swt) huharibu mwenendo wa mtu.

130. Hakuna chochote kile pasi na nuru ya kweli tu itakayokutakasisha.

131. Kuwaheshimu waliosoma ni kumheshimu Allah swt.

132. Ma'arifa ni chanzo cha khofu ya Allah swt (--inaletwa na )

133. Kile kikomazacho ma'arifa ni matendo kwa kutumia hekima na ma'arifa hayo.

134. Kufundisha ndiko kujifunza.

UMUHIMU WA MAARIFA

135. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alielekea Msikitini na huko akakuta makundi mawili ya Waislamu. Kikundi cha kwanza kilikuwa kikijifunza ilimu ya Dini, na kikundi cha pili kilikuwa kinafanya 'ibada. Kwa kuona hayo Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Vikundi vyote viko katika kheri, ama hawa wanamwomba Allah swt na hawa wanajifundisha na kuwafundisha wengine wasio na ilimu, kwa hakika hawa ndio bora, nimetumwa kwa watu ili kuwafundisha." Kisha akakaa pamoja nao .

136. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Ewe Kumail ! Hakuna harakati zozote utakazozifanya, ila unahitaji kuwa na maarifa ."

137. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Kukosa macho ni jambo jepesi kuliko kukosa mwanga (maarifa) ".

138. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Usizungumzie usilolifahamu ".

139. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Elimu ni msingi wa kila heri ".

140. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Katika hadith inayotokana na mababa zake, toka kwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . ambae ameipokea toka kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) "Watu wengine walio na thamani (qimmah) kwa watu ni wale walio na elimu nyingi kati yao, na wale wenye thamani duni kati yao ni wale wachache wao wa elimu ".

KUTAFUTA ELIMU

141. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Kutafuta elimu ni faradhi (lazima) kwa kila Mwislamu Mwanamme na Mwislamu Mwanamke ".

142. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Kujitolea nafsi yake mtu kwa ajili ya kutafuta elimu, mfano wake ni kama anaepigana vita kwa ajili ya Allah swt .".

143. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . "Watu ni aina mbili; Aalimu (mwenye elimu) na mwenye kujifundisha, ama watu wengine ni upumbavu na wapumbavu mahala pao ni motoni ".

144. Amesema Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) : "Kuwa mwenye elimu au mwenye kujifundisha elimu, jiepushe kuwa mwenye kupumbazika na kuona ladha ( ya kutojihangaisha kutafuta elimu.)

145. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . "Sikupenda kumwona kijana, kijana kati yenu ila amekuwa kati ya moja ya hali mbili; Ima awe mwenye elimu au mwenye kutafuta elimu, na kama hakufanya hivyo basi amepoteza nafasi yake, na aliye poteza nafsi yake amefanya dhambi na anayefanya dhambi ndio amekaa motoni. "

AKILI. 146. Mtukufu Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema "Hakika heri yote hupatikana kwa akili ".

147. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Akili ni jahazi ya elimu. "

148. Mtukufu Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema: "Hakugawa Allah swt kwa waja wake kitu kilicho bora kuliko akili, usingizi wa mwenye akili ni bora kuliko kukesha kwa mtu mjinga, kufuturu (kutofunga) kwa mtu mwenye akili ni bora kuliko Saumu ya mtu mjinga, na kutosafiri kwa mtu mwenye akili ni bora kuliko safari ya mtu mjinga ".

149. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema "Ubinadamu wa mtu hutokana na akili yake ."

150. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : Kumwambia mtoto wake Al Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Ewe Mwanangu! Hakika ya utajiri ni utajiri wa akili na ufakiri mkubwa ni kuwa mtu mpumbavu ."

151. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Akili ndio mjumbe wa haki. "

152. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Rafiki wa kila mtu ni akili yake, na adui ni ujinga wake ".

153. Mtukufu Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema: "Mwenye kutekeleza (vitendo) kutokana na kile anachojua, Allah swt humrithisha (humjalia) elimu ambayo haijui ."

154. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Akili ni kitu cha maumbile, huzidi kwa elimu na majaribio ."

155. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Asiejaribu mambo hudanganyika ."

156. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Na majaribio ya muda mrefu ni nyongeza ya akili ."

157. Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) . amesema: "Ewe Hisham! Hakika kwa Allah swt juu ya watu kuna dalili (burhani) mbili: Dalili ya wazi, na dalili ya ndani. Na ama ile ya wazi ni Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w) , Manabii na Maimamu (a.s). na ama ya ndani ni akili ."

158. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema "Mwenye kuwa nayo akili, amekuwa na dini. "

159. Mtukufu Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema: "Mwenye kuijua nafsi yake, hakika amemjua Allah swt ."

160. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Huzijua mtu aibu za nafsi yake, ni maarifa yenye kunufaisha zaidi ."

161. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Na akili ni ngao (ngome) ya majaribu ."

162. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema "Na kila ujuzi unahitaji majaribio ."

163. Mtukufu Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema: "Kutafuta elimu ni bora kuliko kufanya ibada. Amesema Allah swt, Hakika wanaomwogopa Allah swt miongoni mwa waja wake ni wanachuoni .

164. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema "Hakuna zaka iliyo bora katika elimu kuliko kuifanyia kazi ."

165. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Mweney kuwa na yakini (uhakika wa Jambo) hufanya amali (kazi) hali ya kuwa yeye ni mwenye kupigania Jihadi. "

166. Mtukufu Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema: "Lau (mtihani wa Allah swt) husubiri, na asiyefahamu hakanushi ."

167. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Hasubiri mtu yeyote katika uchungu wa haki ila yule anae kuwa na yakini (uhakika) wa matokeo yake. "

168. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema: "Hakuna kitu chochote kile ila kina upeo wake," akaulizwa" Ni nini upeo wa Yaqini (kuwa na uhakika)?. Akasema "Usiogope kitu chochote ."

169. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema: "Kutoa majabali kutoka mahali pake ni rahisi kuliko kuutoa moyo kutoka katika chochote ."

170. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Haisafiki kazi mpaka isihi (iwe sahihi) elimu ."

171. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema: "Mwanachuoni katika zama zake, hayamhujumu matatizo. "

172. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Aliye kamilika kiakili hayawi mazito kwake matatizo ."

173. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Akili iliyokamilika, ndiyo yenye kuvunja mabaya ."

174. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Lengo la elimu ni kufanya kazi vizuri ".

MAELEZO

1. Katika nadharia za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na Mawasii wake, elimu ni kitu bora kuliko kitu kingine chochote kile, kiasi kwamba jambo hili limeweza kuwastajaabisha watu wengi kutokana na hadithi nyingi zilizo pokewa zinazo sifa ubora wa elimu, hadithi kadhaa zimesikiwa toka kwenye ulimi wake Mtukufu Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na Maimamu (a.s) . Lakini je! Mshangao huo utabaki mpaka lini? Mshangao mbele ya uhakika wa mambo yalivyo hausaidii kitu. Je hatuamini kwamba maendeleo ya Dunia na Akhera hupatikana kwa elimu?. Jibu liko wazi kwamba kwa elimu hupatikana na maendeleo. Kwahiyo tunajionea wazi kuwa thamani ya elimu iko juu sana.

MAELEZO

2. Mwanadamu hutokea akajifunza elimu, lakini elimu yake ikawa ni upuuzi mtupu na balaa kwa watu, kutokana na kule kuvuka mpaka kwake na kuitumia elimu yake isivyo ndivyo na kinyume cha mtu mwenye akili, matokeo ya mtu wa ina hii ni kugundua mambo ambayo hayana faida yoyote kwa wengine, elimu kama hii humpoteza yeye mwenyewe na ummah pia katika dunia na akhera, hatimaye mtu huyu hugunduwa utengenezaji wa pombe na mabomu.

175. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Inamtosha mtu kuwa mjinga kwa kutokuzijua aibu zake ."

176. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Enyi watu! Hakuna heri katika dini isiyo na mafunzo ndani yake ."

177. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Mfanya ibada bila ya mafunzo ni kama punda mwenye kuzunguka, anazunguka na wala hachoki .''

178. Mtukufu Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema: "Mwenye kueneza elimu basi anao ujira mfano wa mwenye kutekeleza kwa hiyo (kutokana na elimu hiyo) ."

179. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Upingeni ujinga kwa elimu ."

180. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Katika kuwasifu waja wa Allah swt: Nawakasimamisha masikio yao (kwakusikiliza ) elimu yenye manufaa kwao ."

181. Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) . amesema: "Nimekuta elimu ya watu iko katika mambo manne: Kwanza kati ya hayo manne ni kumjua Mola wako, Pili kujuwa alicho kiumba, Tatu kujuwa anacho taka kwako, Nne kujuwa chenye kukutoa katika dini yako ."

182. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema: "Lau ningeijiwa na kijana miongoni mwa vijana wa ki-Shi'a hajifunzi (elimu ya dini) ninge mtia adabu. "

183. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema: "Rafiki wa kila mtu ni akili yake na adui wake ni ule ujinga wake. "

184. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Mwenye akili ni kufikiri ataona (kuona muongozo)

185. Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) . amesema: "Kila kitu kina dalili, dalili ya mwenye akili ni kufikiri na dalili ya kufikiri ni kunyamaza ."

186. Mtume Mtukufu Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema: "Kufikiri kwa muda wa saa moja ni bora kuliko ibada ya mwaka ."

187. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Kufikiri ni kioo kilicho safi. "

188. Al Imam Hassan al-'Askari(a.s) . amesema: "Haikuwa ibada kwa uwingi wa kufunga na kusali, hakika ya ibada ni kufikiri (na kuzingatia) kuhusu Allah swt ."

189. Mtukufu Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema: "Elimu ndio kichwa cha kila heri na ujinga ndio kichwa cha kila shari ."

190. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . amesema: "Ujinga ni Umauti ."